Ibadhi.com

WATU WA HAKI NA MSIMAMO

WATU WA HAKI NA MSIMAMO - AHLU L HAQQI WAL ISTIQAAMA (( IBADHI ))

Wao Ibadhi ni wenye pupa zaidi ya kushikamana na njia ya Allah mtukufu na kumfuata Nabii wa Uongofu Muhammad s.a.w. yeye ndiye imam wao na wao wapo katika mwenendo wake.

Anasema mwanachuoni mkubwa Sayyid Abdul haafidh Abdurabbihi, mmoja wa wanachuoni wa Azhar katika kitabu cha “Al ibadhiyya: madh habun wa Sulukuun” (( IBADHI: Madhehebu na mwenendo )): “Hakika hawa ndio Ahlu l istiqama, au wao kwa uhalisia na uhakika ndio KUNDI LILILO OKOKA ambalo alitueleza Mkweli aliyekingwa na maasi, na ambalo Allah mtukufu alimuamrisha Mtume wake alichague na alifanye kuwa ndiyo njia yenye kufikisha katika ibada zake na radhi zake”[1]

Zimeendelea kuwa hatua za Mchaguliwa – Sallallahu alayhi wasallam- ndio hatua zao Nafsi na sheitan havikuweza kuondosha azma yao.[2]

------------------------------------------------------------------------

[1] Alsayyid Abdulhaafidh Abdurabbih, Alibadhiyya Madh habu wasuulukun uk 624

[2] - Alrawahi Abuu Muslim Naasir bin Salim, Aldiiwan uk 206

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment