Ibadhi.com

MLANGO WA KWANZA - 1.RAI YA MAIBADHI KATIKA KUNYANYUA NA KUFUNGA MIKONO

 

RAI YA MAIBADHI KATIKA KUNYANYUA NA KUFUNGA MIKONO

Maibadhi wanaona kuinua na kufunga mikono katika swala hakusihi kwa sababu hivyo ni vitendo vilivyozidi katika swala, na wakahesabu kufanya hivyo ni mchezo katika swala na hoja zao juu ya hayo ni:-

 

 

KWANZA


Hadithi iliyopokewa na Imam Arrabii katika Musnad yake kutoka kwa Abi Ubayda kutoka kwa Jabir bin zayd kutoka kwa Ibnu Abbas (r.a) kutoka kwa Bwana Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) amesema:

"كَأَنِّي بِقَوْمٍ يَأْتُوْنَ مِنْ بَعْدِي يَرْفَعُوْنَ أَيْدِيَهُمْ فِي الصَّلاَةِ كَأَنَّهَا أَذْنَابُ خَيْلٍ شُمُسٍ" .

TAFSIRI:

(Kama kwamba kuna watu watakuja baada yangu wanainua mikono yao katika swala kama mikia ya farasi walioasi). 1

Kwa hivyo hadithi hii inaonyesha kuwa suala la kuinua mikono limezuka baada ya kufa Bwana Mtume (s.a.w). Kutokana na maneno yake (Kama kwamba kuna watu watakuja baada yangu).

Kwa maana hiyo Maibadhi wanasema kuwa hadithi za kufunga mikono zitakuwa ni dhaifu au zimetugwa, amesema Al-Imam Alqutb Muhammad bni Yussuf Atfayyish: "Na jambo lilokuwa wazi na lilonidhihirikia mimi kuwa madhehebu nyengine –wenye madhehebu manne - wameweka hadithi za kuitikia amin na kuinua mikono na (kudai) kuwa Bwana Mtume (s.a.w) alifanya hivyo hadi kufa kwake na wakawaekea maswahaba baada yake katika njia inayokubalika kwao wao".

Na mimi ninasema kuwa hata kwao wao hadithi hizo haziwezi kukubalika lau kama zitafanyiwa uchambuzi wa kina wa kielimu kwa kutumia misingi ya elimu ya hadithi ambayo imewekwa kwa ajili ya kuzitambua hadithi zilizo sahihi na dhaifu.

______________________

1 - الجامع الصحيح مسند الإمام الربيع بن حبيب ابن عمر الأزدي البصري ، إعداد سعود بن عبدالله الوهيبي ، مكتبة مسقط ،1414هـ 1994م، ج1/58 ،الحديث 213

 

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment