Ibadhi.com

Hekima Za Khotuba Ya Iddi

Hizi ni miongoni mwa hekima za mafundisho ya Uislamu alizozitoa Sheikh Falaah Hamed Sulleiman Al-Wihebi -Allah amuhifadhi- katika hotuba yake ya Iddi ya Al-udhhiyah ya mwaka huu 1436 HJ.

Hapo chini ni video fupi ya hotuba yake na maandishi ni tafsiri ya hotuba hiyo kwa Kiswahili.

((Tunaona umma unahalalisha damu za watu wake.

((na wala musiuwe nafsi zenu))

Huu ni wasia wa Allah mtukufu ulioenea kuanzia kwa wana wa Israili (Mtume Yaaqoob) mpaka kwa wana wa Islamil (alitokea Mtume wetu Muhammad (s.a.w)).

Na wala musiuwe nafsi zenu, wala musiuwe nafsi zenu.

Kuiuwa nafsi ni kurejea na kuwahukumu wengine kuuliwa, kwa kumwaga damu, kwa kuwakufurisha (ukafiri wa ushirikina) kwa kuwatoa katika mila.

Hii ni adhabu ya wazi enyi waumini watukufu.
Hakuna tatizo kwa mtu kubakia katika madhehebu yake, na kubakia katika aliyoyakinai, lakini asiyajaalie hayo tena ndiyo msitari wa haki, huku akiyajaalia ya wengine kuwa ndiyo msitari wa batili, kwa kumkurifisha huyu, na kumtia katika upotevu yule, na kumtia katika ubidaa mwengine, mwisho anamalizia katika uhalalishaji wa umwagaji damu kama tunavyoona leo.

Enyi waumini wakarimu.
Allahu akbar,, Allahu akbar,, Allahu akbar, laa ilaaha illallahu wa Allahu akbar kabiiraa.
Alisimama Nabii -rehma na amani ziwe kwake- katika siku ya Hija kubwa mbele ya Nyuma ya Alqaabah, kisha akanyanyua kidole chake akiiashiria huku akisema: "utukufu ulioje wako, na ukutufu ulioje wa heshima yako, na lau utabomolewa jiwe jiwe ni bora kuliko kumwagwa damu ya mtu muislamu".

Enyi waumini wakarimu.
Leo hii, watu wanaapa kwa cheo cha Alqaabah kwa ajili ya kumwaga damu za waislamu, wamefikia kuchukuwa kiapo kwa cheo cha Alqaabah dhidi ya heshima zao na mali zao, nao wameingia katika kuwauwa na kuwangamiza.

Enyi waumini wakarimu.
Wallahi, kama mimi naziona damu hizo siku ya kiama, nao hawana viatu wako uchi kama walivyozaliwa wanasimamishwa mbele ya hukumu ya Allah mtukufu, tunahesabiwa kwa kila tone la damu lililomwagwa kwa njia isiyokuwa ya haki.
Na hiyo siasa chafu ambayo imeifanya hii dini kuwa ni kipando cha uuaji na ubomoaji na umwagaji damu.
Wallahi kisha Wallahi kisha Wallahi.
Watajerea wote hao kwa Allah mtukufu, kisha watahesabiwa na Allah mtukufu, na watahesabiwa kwa pamoja, na watahesabiwa mmoja mmoja, na juu ya yote hayo watalengwa katika moto kwa kuchukuwa katika shingo zao haki za damu za waislamu.
Allahu akbar,, Allahu akbar,, Allahu akbar, Allahu akbar kwa haki na ukweli na kwa kumuabudu yeye peke yake na kujiokoa kwake yeye peke yake.))

Media

Hekima Za Khotuba Ya IDDI Sh Falaah Hamed Al Wihebi 1:30 / 3:00
Last modified onIjumaa, 02 Septemba 2016 14:40

Add comment


Security code
Refresh