Published By Said Al Habsy  UCHAMBUZI KUHUSU HADITHI ZA KUINUA NA KUFUNGA MIKONO
SEHEMU YA KWANZA:
HADITHI ZA KUINUA MIKONO
1-عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : " كَانَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ رَفَعَ يَدَيْهِ مُدًّا " .
رواه الخمسة إلا ابن ماجة ، ويقصد بالخمسة إلا ابن ماجة ، أحمد- أبو داود-الترمذي و النسائي[19]
TAFSIRI
(1)Kutoka kwa Abi Hurayrah (r.a) amesema: “Mjumbe wa Allah rehma na amani ziwe juu yake alikuwa akisimama kusali huinua mikono yakejuu”.
Wamepokea wapokezi watano isipokuwa Ibnu Maajah, na inakusudiwa watano isipokuwa Ibnu Maajah, ni Ahmad, Abu Daud, Attirmidhy na Annasaaiy, kwa istilahi ya mtunzi wa kitabu Muntaqaa Al-akhbaar.
[19]- Ahmad 2/375 hadithi ya : 8862. (مكتبة الشاملة)
- Abu Daud 1/255 hadithi ya: 738 . (مكتبة الشاملة)
-Attirmidhiy 2/5-6 hadithi ya: 239 : (مكتبة الشاملة)
239 - حدثنا قتيبة و أبو سعيد الأشج قالا حدثنا يحيى بن اليمان عن ابن أبي ذئب عن سعيد بن سمعان عن أبي هريرة قال : كان رسول الله صلى الله عليه و سلم إذا كبر نشر أصابعه
قال أبو عيسى حديث أبي هريرة [ حسن ]
[ و ] قد روى غير واحد هذا الحديث عن ابن أبي ذئب عن سعيد بن سمعان عن أبي هريرة أن النبي صلى اله عليه وسلم كان إذا دخل في الصلاة رفع يديه مدا
وهذا أصح من رواية يحيى بن اليمان وأخطأ يحيى بن اليمان في هذا الحديث
قال الشيخ الألباني : ضعيف.
240 -[ قال و ] حدثنا عبد الله بن عبد الرحمن أخبرنا عبيد الله بن عبد المجيد الحنفي حدثنا ابن أبي ذئب عن سعيد بن سمعان قال سمعت أبا هريرة يقول : كان رسول الله صلى الله عيه وسلم إذا قام إلى الصلاة رفع يديه مدا
قال [ [ أبو عيسى قال ] عبد الله [ بن عبد الرحمن ] وهذا أصح من حديث يحيى ابن اليمان وحديث يحيى بن اليمان خطأ
قال الشيخ الألباني : صحيح . (مكتبة الشاملة)
-Vipi iwe sahihi na ndani yake yumo Said bnu Sam’aan na Ubaydullah Alhanafiy nao wote wana udhaifu, angalia katika uchambuzi wa hadithi hii utaona.
-Annasaaiy 1/124 hadithi ya:883.(مكتبة الشاملة)
UCHAMBUZI WA HADITHI:
Na kasema Ashshawkaaniy katika kitabu cha Naylul-Awtwaar[20] :“Na ameipokea Addaaramiy kwa njia ya Ibni Abi dhi’ib kutoka kwa Muhammad bni Umar bni A’twaai kutoka kwa Muhammad bni Abdurrahman bni Thuwban kutoka kwa Abi Hurayrah”.[21]Hadithi hii katika sanad ya upokezi wa Ahmad na Abi Daud na Attirmidhiy na Annasaaiy yumo Said bni Sam-a’an, amesema Al-hafidh Adhdhahabiy kuhusu mtu huyo kwenye kitabu chake kiitwacho Miizanul-I-itidal: “Kuna ujahala juu ya mtu huyo, na Al-Azdiy amemdhoofisha”.[22]
Na kwenyeupokezi wa Addaaramiy[23] katika sanadi yake yumo Ubaydillahi bni Abdulmajiid Alhanafiy, amepokea Adhdhahabiy kutoka kwa Uthman bni Said kutoka kwaYahya kwamba mtu huyo si chochote si lolote (katika upokezi wa hadithi[24].(na misingi ya sheria katikahadithi inasema (إن الجرح مقدّم على التعديل)
Tafsiri yake: hakika illa au tuhuma hutangulizwa juu ya uadilifu.[25]
Hayo yote ni kwa ajili ya kuzilinda sunna tukufu za Bwana Mtume (s.a.w) kutokana na mchezo wa wachezaji na utunzi wa watungaji (yaani hadithi za uongo), kwa sababu hiyo hakika hadithi hii ni dhaifu.
2-وعن وائل بن حجر ( أَنَّهُ رَأَى رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَرْفَعُ يَدَيْهِ مَعَ التَّكْبِيرَةِ) رواه أحمد - وأبو داود، قال الشوكاني وأخرجه البيهقي أيضا :
TAFSIRI:
(2) Imepokewa kutoka kwa Wail bnu Hujri (amemuona Mjumbe wa Allah rehma na amani ziwe juu yake huinua mokono yake miwili pamoja na takbira(.
Ameipokea Ahmad - Abu Daud, amesema Imam Ashshawkaniy ameielezea hadithi hii AlBayhaqiy vilevile. [26]
UCHAMBUZI WA HADITHI:
Na hadithi hii ni dhaifu kwa njia mbili:
a-Ameipokea Ahmad na Abu Daud kwa njia ya Abduljabbaar bni Wail, amesema ( yaani Abduljabbaar ): “Wamenihadithia watu wa nyumbani kwangu kutoka kwa baba yangu kwamba amemuona Mjumbe wa Allah rehma na amani ziwe juu yake anainua mikono pamoja na takbira”. Amesema Ashshawkaniy: “Amesema Almandhiry kuwa Abduljabbaar hakusikia hadithi hiyo kutoka kwa baba yake na watu wa nyumbani kwake hawatambuliki ni kina nani[27],kwa hivyo sanadi yake imekatika, na kukatika kwa sanadi katika hadithi ni daliliyaudhaifuwake” .
b-Kwenye upokezi wa Al-bayhaqiy katika sanadi yake yumo Abul-Bukhtury Said bni Fayruz Attwaiy, na amenukuu Adhdhahabiy kutoka kwa Salamata bnu Suhayl amesema kuhusu Abul-Bukhtury “kuwa ni mwenye kukithirisha na hadithi zake ni mursalna hupokea kutoka kwa maswahaba, na wala hakupokea kutoka kwa hata mmoja katika maswahaba wakubwa, na katika hadithi zake zilizopokewakwa kusikia (سماعا)basi hizo ni katika hadithi hasan((حسن nazilizokuja kwa upokeziwa(عن) hizo ni hadithi dhaifu, na katikaupokezi wa Al-Bayhaqiy imekuja kwa njia ya ( عن) kwa maana hiyo hadithi hii ni dhaifu.
3-Imepokewa kutoka kwa Ibni Umar ya kuwa:
3-((كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ رَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّى يَكُوْنَا بِحَذْوِ مَنْكِبَيْهِ ثُمَّ يُكَبِّرُ , فَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَرْكَعَ رَفَعَهُمَا مِثْل ذَلِكَ , وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرُّكُوْعِ رَفَعَهُمَا كَذَلِكَ أَيْضًا , وَقَالَ سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ)) متفق عليه ,
قال الشوكاني أخرجه البيهقي بزيادة؛ " فَمَا زَالَتْ تِلْكَ صَلاَتُهُ حَتَّى لَقِيَ اللهَ تَعَالَى "
TAFSIRI:
3-“Alikuwa mjumbe wa Allah rehma na amani ziwe juu yake akisimama kwa ajili ya kusali huinua mikono yake mpaka inakuwa karibu na mabega kisha huleta takbira, na akitaka kurukuu huinua mikono hiyo vile vile,na akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu huinua vile vile nahusema“سمع الله لمن حمده ربنا ولك الحمد” muttafaqun-alayhi.
Amesema Ashshawkaniy hadithi hii ameitoa Al-Bayhaqiy mna ziada ndani yake “Haikuacha kuwa hiyo ndiyo swala yake hadi kufa kwake”.
[20]--Naylul Awtwaar Mujallad 1/ j2/181, Chapa 1 mwaka 1415H / 1995M. Daarul-Kutubil-ilmiyyah , Beirut-Lebnon
[21] - Sunani Addaaramiy 1/308 hadithi ya : 1237.
[22]-3206 - سعيد بن سمعان [ د، س، ت ].
عن أبى هريرة. فيه جهالة. ضعفه الازدي، وقواه غيره. وقال النسائي: ثقة . 2/143 (مكتبة الشاملة).
[23] --1237 - أخبرنا عبيد الله بن عبد المجيد الحنفي ثنا بن أبي ذئب عن محمد بن عمرو بن عطاء عن محمد بن عبد الرحمن بن ثوبان عن أبي هريرة : أن رسول الله صلى الله عليه و سلم لم يكن يقوم إلى الصلاة إلا رفع يديه مدا .(1/308)
قال حسين سليم أسد : إسناده صحيح.(مكتبة الشاملة)
[24]- 5381 - عبيد الله بن عبدالمجيد [ ع ]، أبو على الحنفي.عن قرة بن خالد، وطبقته وعنه الدارمي، والذهلى، وخلق. قال أبو حاتم، وغيره: ليس به بأس وروى عثمان بن سعيد، عن يحيى: ليس بشئ . - ميزان الإعتدال3/ 13
(مكتبة الشاملة).
[25] - Maana yake ni kuwa akitokea mtu katika wapokezi wa hadithi akawa anasifiwa kwa sifa aina mbili tofauti za uadilifu na udhaifu basi hutangulizwa sifa mbaya na zile nzuri hutupwa wala hazitizamwi, yote hayo ni kwa sababu ya kuzilinda hadithi tukufu na mikono ya wenyekuzichezea hadithi hizo au wenye kuzua hadithi za uongo, kwa hivyo hadithi hii ni dhaifu.
[26] - Nimeangalia musnad ya Imam Ahmad sijaiona hadithi hiyo.
- Sunanu Abu Daud 1/250 hadithi ya 725 (مكتبة الشاملة)
– Sunanul kubra lilBayhaqiy: 2/26 hadithi ya 2144.. (مكتبة الشاملة)
[27]-Naylul Awtwaar Mujallad 1/ j2/184, Chapa 1 mwaka 1415H / 1995M. Daarul-Kutubil-ilmiyyah , Beirut-Lebnon.
UCHAMBUZI WA HADITHI:
a-Hadithi hii katika sanadi yake kwenye upokezi wa Al-Bukhariy na Muslim kuna mtu anaitwa Muhammad bnu Muslim bnu Shihab Azzuhriy.
Amesema Alhafidh Adhdhahabiy (amekufa 748 H) kuhusu mtu huyo kwenye kitabu chake cha (mizaanul-iitidaal) “Kwa hakika alikuwa anafanya tadliis”.[28]
Na ametiwa aibu Azzuhriy kwa sababu ya kuchanganyika kwake na wafalme madhalimu katika Baniy Umayya, na akafungua mlango wa kuingia kwa wafalme hao “Wakamfanya (yaani Azzuhriy) ndiye mwega mkubwa wa kupitishia batili zao, na daraja la kuvukia katika kufikia balaa zao, wanawaingizia shaka maulamaa wengine na nyoyo za majahil zinafuata” kama alivyomuandikia juu ya hilo mmoja wa ndugu zake katika dini na kwa kweli jambo hilo ni katika mambo yanayoshusha na kuangusha cheo na heshima ya wanachuoni hasa kwa wapokezi wa sunna na maulamaa wa hadithi, amesema Imam Abu Ya-aquub Alwarjilaaniy kwenye kitabu chake Addaliil walburhaan “Na wakamuandikia yeye (yaani Azzuhriy) mafaqihi wapatao 120 wakimsimanga na kumtia aibu juu ya alilolifanya, miongoni mwa hao ni Jabir bni Zayd na Wahbu bni Munabbih na Abu Hazimil-faqiih, mwanachuoni wa Madina na mfano wa hao na kwa hakika nimeziona barua za hao watatu walizompelekea yeye”, na vile vile amenukuu Ibnu Qutaybah katika kitabu chakeAl-imamatu wassiyaasatu maneno ya Abi Haazimil mwanachuoni wa Madina aliyomwambia Azzuhriy mbele ya Sulayman bni Abdulmalik.
b-Vile vile hadithi hiyo kwenye sanadi yake katika upokezi wa Muslim na Albayhaqiy yumo Abdulmalik bni Abdul-aziz bni Jurayj, na Abdurrazzaaq bni Himam, ama Ibnu Jurayj amesema Adhdhahabiy kuwa alikuwa anadallis يُدَلِّسُ, na imenukuliwa kutoka kwa Abdillahi bni Ahmad bni Hanbal “ Amesema baba yangu baadhi ya hadithi hizi ambazo Ibnu Jurayj akiziunganisha (hadi kwa Bwana Mtume) ni hadithi zilizozuliwa”[29], na ama Abdurrazzaaq bni Himam wamemzungumza maulamaa wa hadithi baina ya kumkubali na kumdhoofisha[30] na kanuni za elimu ya hadithi zinasema ((أََنَّ الجَرْحَ مُقَدَّمٌ عَلَى التَّعْدِيلِ )) .
c-Vile vile katika hadithi hii kuna makosa ya kilugha kwenye lafdhi zake kwani kimekuja kitendo katika sigha (mfumo) wa sifa ya kiume na ambayo inatakiwa iwe ya kike[31], hadithi inasema ( حَتَى يَكُوْنَا ) na inavyotakikana iwe (حََى تَكُوْنَا) kwa sababu inayozungumzwa hapo ni mikono na maulamaa wanakataza kuwepo makosa ya kilugha katika hadithi, anasema Dr Subhi Ssaalih kwenye kitabu chake:“علوم الحديث ومصطلحه” Anashurutiza mpokezi wa hadithi awe “mwenye uwezo wa kuifikisha hadithi ufikishaji ambao hautakuwa na makosa ya kilugha”, na tuyatizame hayo maneno amenasibishiwa nani? Amenasibishiwa Abdillahi bni Umar na yeye anajulikana ni nani, ni Sahaba tena katika wenye elimu, naye ni miongoni mwa Maquraysh wenye akili sana na mwenye fasaha na ujuzi wa kuzungumza, tena Qur-ani imeteremshwa kwa lugha yao, na kwa kweli iko mbali sana kuwa Abdillahi bni Umar aweke lafdhi ya kiume kwenye lafdhi ya kike, tena bila ya sababu yoyote ya kimsingi inayohitaji kufanya hivyo na hapa haikupokewa hadithi hii kwa njia ya maana رِوَايَةُ الحَدِيْثِ بِالمَعْنَى, kwani riwaya za namna hizo ni kuwekwa neno badala ya neno tena liwe na maana hiyo hiyo bila ya kutoka nje ya kanuni za lugha ya kiarabu, na hao walioruhusu riwaya za aina hizo wameshurutisha mpokezi wa hadithi awe ni mjuzi wa misingi ya lugha ya kiarabu kama Sarfu –Nahaw na mfano wake, basi kutokana na vipimo hivi inamdhihirikia wazi msomaji kuwa hadithi hii ni dhaifu na udalili wake unaporomoka.
4-Imepokewa kutoka kwa Nafi-i :
4-أَنَّ ابنَ عُمَرَ كَانَ إِذاَ دَخَلَ فِي الصَّلاَةِ كَبَّرَ وَرَفَعَ يَدَيْهِ ، وَإِذَا رَكَعَ رَفَعَ يَدَيْهِ، وَإِذَا قَالَ سَمِعَ اللّهُ لِمَنْ حَمِدَه رَفَعَ يَدَيْهِ ، وَإِذَا قَامَ مِنَ الرَّكعَتَيْنِ رَفَعَ يَدَيْهِ ،وَرَفَعَ ذَالِكَ ابن عمر إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم . رواه البخاري والنَّسَائي وأبو داود.
TAFSIRI:
Kutoka kwa Nafi’i:
“Alikuwa Ibnu Umar akiingia ndani ya swala husoma takbira na kuinua mikono yake, na akirukuu huinua mikono yake, na akisemaسَمِعَ اللّهُ لِمَنْ حَمِدَه huinua mikono yake, na akiinuka kutoka kwenye rakaaya pili huinua mikono yake, na Ibnu Umar akaiinua hadithi hii hadi kwa Bwana Mtume (s.a.w).
Ameipokea Albukhariy –Annasaaiy- Abu Daud.
UCHAMBUZI WA HADITHI
Hadithi hii ni dhaifu kwa sababu mbili zifuatazo:-
)1(-Hadithi hii imetiwa illa kwa sababu ya ikhtilafu iliyopo katika kuiinua hadi kwa Bwana Mtume (s.a.w) na kutokuiinua, amesema mwanachuoni Ashshawkaniy katika kitabu chake Naylul-Awtwaar:[32]
“Na ameelezea Addaaraqutniy katika Al-ilal -العلل-ikhtilafu katika kuifikisha kwa Bwana Mtume (s.a.w) na kutoifikisha”[33].
Na hadithi iliyo sahihi ni ile iliyosalimika na shudhuudh na illa (شُذُوْذٌ وَ عِلَّةٌ ) .
)2(-Na katika sanadi yake kwenye upokezi wa Albukhary na Abi Daud, yumo Abdul-A-ala bin Abdul-A-ala Ashshamiy, amesema Ibnu Sa-ad mtu huyo hakuwa na uzito katika hadithi, na akasema Imam Ahmad alikuwa na aqida ya Alqadriyya, na amesema Bundaar ninaapa kwa jina la Allah alikuwa haujui mguu wake upi mrefu, tizama mizaanul-I-iitidaal cha Adhdhahabiy[34], na wala sikuiona hadithi hii kwa lafdhi hii kutoka kwa Naafii kwenye upokezi wa Annasaaiy, bali amepokea Annasaaiy hadithi za Anaafii kutoka kwa Ibnu Umar (r.a) kwa njia ya Salim bni Abdillahi. Na huenda ikawa imo katika kitabu cha Almujtabaa cha Annasaaiy. Na Almujtabaa ni kitabu kilichozikusanya hadithi zilizo sahihi kwa rai ya Annasaaiy kutoka katika kitabu chake cha Assunan. Na Allah ndie mjuzi zaidi kwa hilo.
5- Imepokewa kutoka kwa Imaam Aliy (k.w):
5-" عَنْرسول الله صلى الله عليه وسلم أَنَّهُإِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ الْمَكْتُوْبَةِ كَبَّرَ وَرَفَعَ يَدَيْهِ حَذْوَ الْمَنْكِبَيْهِ ، وَيَصْنَعُ مِثْلَ ذَلِكَ إِذَا قَضَى قِرَاءَتَهُ وَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَرْكَعَ، وَيَصْنَعُهُ إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرُّكُوْعِ ، وَلاَ يَرْفَعُ فِي شَيْءٍ مِنْ صَلاَتِهِ وَهُوَ قَاعِدٌ ، وَإِذَا قَامَ مِنَ السَّجْدَتَيْنِ رَفَعَ يَدَيْهِ كَذَلِكَ وَكَبَّرَ"
رواه أحمد وأبو داود والترمذي وصححه ، قال الشوكاني وأخرجه أيضا النسائي وابن ماجة.
TAFSIRI:
5-Amesema Imaam Aliy (k.w) kuwa: “Bwana Mtume (s.a.w.) alipokuwa akisimama kusali swala za Fardhi huleta takbiira na hunyanyua mikono yake kukaribia (sawa na) mabega yake, na hufanya hivyo akimaliza kisomo chake na pindi akitaka kurukuu, na huinyanyua pindi akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu, na wala hainui kitu katika swala ikiwa amekaa, na anapoinuka kutoka kwenye sijda mbili huinua mikono yake vilevile na huleta takbiira”. Imepokewa na Ahmad na Abu Daud na Attirmidhiy na kuisahihisha, na kasema Ashshawkaaniy (hadithi hii) vilevile ameipokea Annasaaiy na Ibnu Maajah.
UCHAMBUZI WA HADITHI
1-Hadithi hii kwenye upokezi wa Abu Daud na Ibnu Maajah katika sanadi zao yumo Mussa bni U’qbah, amesema Imaam Adhdhahabiy katika kitabu cha Almiizaan:( Na hakika mara nyengine amesema Ibnu Mai’in kuwa mtu huyo ana baadhi ya udhaifu[35], na ndani yake vile vile yumo Abdurrahman bniAbi Zzinaad, na amepokea Alhaafidh Ibnu Hajar katika kitabu cha Attahdhiib[36]udhaifu wa mtu huyo kutoka kwa wanavyuoni wengi miongoni mwao Ibni Mai’in na Aliy bni Mudiiniy na Saleh bni Muhammad na Ya’aquub bni Shaybah na A’mru bni Aliy na Annasaaiy na Abi Zar’a na Assaajiy na vile vile Malik naye kamzungumza na akaashiria kuhusu hadithi ya Attirmidhiy pale aliposema ( na katika mlango huu .. kutoka .. Aliy) na sikuiona katika Sunani- Nnasaaiy.
6-عن أبي قلابة (( أَنَّهُ رَأَى مَالِكَ بنَ الْحُوَيْرِثِ إِذَا صَلَّى كَبَّرَ وَرَفَعَ يَدَيْهِ وَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَرْكَعَ رَفَعَ يَدَيْهِ ، وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ رَفَعَ يَدَيْهِ ، وَحَدَّثَ أَنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَنَعَ هَكَذَا )) متفق عليه وعند أحمدومسلم(( أَنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، كَانَ إِذَا كَبَّرَ رَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّى يُحَاذِي بِهِمَا أُذُنَيْهِ، وَإِذَا رَكَعَ رَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّىيُحَاذِي بِهِمَا أُذُنَيْهِ، وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرُّكُوْعِ فَقَالَ سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ فَعَلَ مِثْلَ ذَلِكَ ))
TAFSIRI
6-Kutoka kwa Abi Qilaabah yeye ((Amemuona Malik bnal Huwayrith anaposali husoma takbira na kuinua mikono na anapotaka kurukuu huinua mikono yake, na akiinua kichwa chake huinua mikono yake, na akaelezea kuwa Bwana Mtume (s.a.w) alifanya hivi)) muttafaqun alayhi na katika upokezi wa Ahmad na Muslim (( kuwa Bwana Mtume (s.a.w) alikuwa akisoma takbira huinua mikono yake hadi kukaribia masikio yake, na akirukuu huinua mikono yake hadi kuwa sawa na masikio, na anapoinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu na kusema: سمع الله من حمدهhufanya kama hivyo)).
UCHAMBUZI WA HADITHI
1-Hadithi hii imepokewa kwa njia ya Abi Qilaabah nae ni dhaifu, kasema Ibnu Hajar katika kitabu cha Attah-dhiib[37]amemdhoofisha Ibnu Ttiin katika sherhe yake ya Albukhariy, وقال إنه معدود في البلهyaani yeye ni katika wanaohesabiwa kwa kuwa ni mwenye kupitilia mpaka katika kughafilikana kasema Adhdhahabiy katika Almizaan[38]((anajiamini nafsi yake isipokuwa anadallis kwa wale aliokutana nao na wale asiowahi kukutana nao, na alikuwa na suhuf (kurasa) akihadithia hadithi ndani yake na anadallis)).
8- وعن أَبِي حُمَيْدٍ السَّاعدِيِّ (( أَنَّهُ قَالَ وَهُوَ فِي عَشَرَةِ مِنْ أَصْحَابِ رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَحَدُهُمْ أَبُوْ قَتَادَةِ ، أَنَا أَعْلَمُكُمْ بِصَلاَةِ رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، قَالُوْا مَا كُنْتَ أَقْدَمَ مِنَّا لَهُ صُحْبَةً ، وَلاَ أَكْثَرَنَا لَهُ إِتْيَانًا ، قَالَ بَلَى، قَالُوْا فَاعْرِضْ , فَقَالَ كَانَ رَسُوْلُ اللهِ صَلىَّ اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ اعْتَدَلَ قَاِئمًا وَرَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّى يُحَاذِي بِهِمَا مَنْكِبَيْهِ ثُمَّ يُكَبِّرْ .. إلى آخر الحديث)) رواه الخمسة إلا النسائي ورواه البخاري مختصرا .
TAFSIRI
7-Kutoka kwa Abi Humayd Assa’adiy amesema ((Naye yu pamoja na Masahaba 10 wa Bwana Mtume (s.a.w) mmoja wapo akiwa ni Abu Qataadah): “Mimi ninaijua zaidi swala ya Bwana Mtume (s.a.w) kuliko nyinyi” , wakwambia: “Wewe hujatutangulia sisi kwa usuhuba naye, wala kuwa naye zaidi kuliko sisi, akasema: Ndio, wakasema haya tuonyeshe (tuelezee), Akasema: Alikuwa Bwana Mtume (s.a.w) akitaka kusali husimama sawa sawa hali amenyooka na huinua mikono yake juu hadi kufikia mabega yake kisha huleta takbira … hadi mwisho wa hadithi”.
Wamepokea wapokezi watano isipokuwa Annasaaiy na ameipokea Albukhariy kwa ufupi.
UCHAMBUZI WA HADITHI
Hadithi hii inayo ya kuzungumziwa katika matni na sanad:
1-Kuhusu matni inaonyesha lugha yake ni nyepesi mno kupita kiasi katika maana yake, na wepesi wa maana ya kilugha unahisabiwa ni alama za hadithi ya kutungwa, kwa maana vipi wakhitilafiane 10 miongoni mwa maswahaba wakubwa ndani yake akiwemo Abu Humayd na Abu Qataadah, Abu Usayd na Abu Hurayrah juu ya usahihi wa namna ya kuisali swala? Hali wao walikuwa daima wapo na Bwana Mtume (s.a.w) wakati wote takriban, na walikuwa wakisali naye swala zote, basi inayumkinika kufichika swala ya Bwana Mtume (s.a.w) juu yao? Au inawezekana Bwana Mtume wa Allah awaache Maswahaba zake bila ya kuwafundisha swala! -Hasha haiwezekani kabisa- Bwana Mtume ambaye alikuwa akiwafundisha attahiyyatu kama alivyokuwa akiwafundisha sura miongoni mwa Qur-ani, na mwisho wa hadithi hiyo wakasema: “Umesema kweli hivi ndivyo alivyokuwa akisali Mjumbe wa Allah rehma na amani iwe juu yake na ali zake”.
Jee hivi inaingia akilini wakubali kirahisi kama hivyo na hali walikuwa wanakumbushana swala ya Bwana Mtume (s.a.w) huku wakiwa wamekhitilafiana namna ya kuisali, pamoja na hayo hadithi hii haikutaja kufunga mikono ndani yake na hao wanaojuzisha kufunga mikono wanaling’ang’ania sana jambo hilo kupita kiasi.
Na ninasema: Maneno kama haya hayawezi kutoka kwa Maswahaba, hayo maneno yote ni ya kutunga tu.
2-Ama kwa upande wa sanad katika upokezi wa Abu Daud na Ibnu Maajah yumo Muhammad bnu Amru bnu A’twa na vile vile Abdul-Humayd bnu Jaafar:
)a(-Wakakhitilafiana kuhusu Muhammad bnu Amru bnu A’twaa khitilafu kubwa sana wapo waliosema hakumdiriki Aba Qataadah wengine wamesema amemdiriki, wengine wakasema alifariki katika utawala wa Alwaliid bnu Yazid, baadhi yao wakasema kifo chake kilitokea katika utawala wa Hisham, pamoja na kuwa wengi miongoni mwa wachambuzi wa hadithi wanasema alifariki baada ya mwaka 120 Hijria, na amesema mwanachuoni Mahmoud Muhammad Khatwaab Assubkiy kwenye kitabu المنهل العذب المورود شرح سنن أبي داود “ Na imesemwa kuwa amefariki mwaka wa 154 Hijria”.
Vile vile wamekhitilafiana katika umri wake alipofariki, wapo waliosema amefariki akiwa na umri wa miaka 80 na ziada, wengine wakasema amefariki akiwa na miaka 90, kwa maana hiyo kwa tarehe aliyoitaja Assubkiy itakuwa hakumdiriki Aba Qataadah wala Aba Humayd, kwani Aba Qataadah inasemekana amefariki mwaka 54 Hijria na kauli nyengine amefariki katika ukhalifa wa Sayyidna Ali (k.w), na ama Abu Humayd amefariki mwaka 60 Hijria, kwa hivyo hakuwadiriki na Yahya amemdhoofisha katika baadhi ya riwaya zake.[39]
)b(- Na kuhusu Abdul-Humayd bnu Jaafar amesema Adhdhahabiy kwenye kitabu chake Almiizaan[40]: “Amesema Abu-Haatim si mtu wa kujengea hoja, na imesemwa kuwa alikuwa na rai ya Qadria, amesema Ali bnul-Mudiiniy alikuwa anaongelea imani ya Alqadria na alikuwa kwetu ni Thiqah na akasema alikuwa Sufiyan akimdhoofisha” .
Na amesema Assubkiy katika sherhe ya Sunani Abi Daud: “Amemdhoofisha Yahya bnu Said na Aththawriy na kasema Ibnu Hibban huenda ikawa mwenye kukosea”.
(c)- Na ameipokea Abu Daud kwa njia ya Abbaas bnu Suhl, lakini katika sanadi yake yumo Issa bni Abdillahi bni Malik amesema Assubkiy: “Amesema Ali bnul-Mudiiniy kuhusu (Issa bnu Abdillah) kuwa ni majhuul na wala hakuna mwengine aliyepokea hadithi kwake isipokuwa Muhammad bnu Is-haaq.[41]
(d)-Vile vile ameipokea Ibnu Maajah kwa ufupi na Attirmidhiy kwa njia ya Abbaas bnu Suhl, isipokuwa katika sanadi yake yumo Fulayh bnu Sulayman.
Amesema Adhdhahabiy:“Na hakika amesema Ibnu Mai’in na Abu Haatim na Annasaaiy huyo (Fulayh) si madhubuti, na kasema Abu Haatim nimemsikia Muawiya bnu Salih nimemsikia Yahya bnu Maiin amesema Fulayh bnu Sulayman si thiqah na wala mtoto wake si thiqah, na amepokea Abbaas bnu Yahya kuwa Fulayh si mtu wa kutolewa hoja, na amesema Abdullah bnu Ahmad nimemsikia Ibnu Mai’in anasema watu watatu wanaepukwa hadithi zao, Muhammad bnu Twalha bnu Musraf – Ayub bnu U’tba na Fulayh bnu Sulayman. Na amesema Abu Daud haitolewi hoja kwa njia ya Fulayh”.[42]
Na amenukuu Assubkiy katika sherhe yake ya Abi Daud kutoka kwa Alhakim kuwa amemdhoofisha, na amenukuu Alhafidh Ibnu Hajar Al-Asqalaaniy katika Attahdhiib kudhoofishwa kwake na idadi yawanavyuoni kati yao ni Ali bnu Mudiiniy.[43]
(e)-Na Albukhariy vile vile ameipokea hadithi hii kwa ufupi na bila ya sanadi.
Kwa hivyo hapana shaka yoyote kuwa hadithi hii ipo mbali na usahihi, na ina udhaifu katika matni na sanad, na kusimamisha hoja kwa hadithi yenye sifa kama hizi ni jambo lisilokubalika, na katika kitabu cha Subulu-ssalaam zimetajwa hadithi 4 zinazohusiana na kuinua mikono katika swala:
1-Hadithi ya Abu Humaiyd Assaadiy.
2-Hadithi ya Ibnu Umar kuwa Bwana Mtume (s.a.w) alikuwa anainua mikono yake ….
3-Hadithi ya Malik bnu Huwayrith.
4-Hadithi ya Wail bnu Hujr.
Na hadithi hizo tumeshazielezea na kubainisha udhaifu wake kwa namna yenye kutosheleza in shaa Allah, na zimekuja hadithi nyengine katika suala la kuinua mikono katika swala lakini ni dhaifu kama alivyoweka wazi Ibnu Hajar katika Fat-hul-Baary pale aliposema: “Na katika mlango huu –yaani wa kuinua mikono- zimepokewa hadithi nyingi kutoka kwa Maswahaba lakini zote hazikosi na ya kusemwa (upungufu na illa)”.[44]
[28] - محمد بن مسلم الزهري الحافظ الحجة-رقم: 8171- كان يدلس في النادر.( ميزان الإعتدال 4/40)
-Tadliis maana yake ni kumficha mpokezi usimtaje kabisa au ukamtaja kwa kun-ya au kabila ili asijulikane nani, kutokana na illa mbaya aliyonayo huyo aliyefichwa au kumtaja mtu kuwa kapokea kwake na hali hajapokea hadithi hiyo kutoka kwa huyo mtu .
[29]-ميزان الإعتدال2/659 mtu wa: 5227. Vile vile angalia Attahdhiib 3/476-8. (مكتبة الشاملة)
[30] -Angalia ميزان الإعتدال 2/ 609-14 , katajwa katika nambari 5044. (مكتبة الشاملة)
[31]- Kwani viungo vyote vilivyokuwa viwili viwili katika mwili wa mwanaadamu vinahesabiwa vina sifa ya kike.
[32] -Naylul Awtwaar Mujallad 1/ j2/188, Chapa 1 mwaka 1415H / 1995M. Daarul-Kutubil-ilmiyyah , Beirut-Lebnon.
- Vile vile amesema katika ukurasa huo: “Amesema Abu Daud:Ameipokea Aththaqafiy yaani Abdulwahhaab kutoka kwa Ubaydillah yaani Ibnu Umar ibn Hafswi wala hakuifikisha kwa Bwana Mtume (s.a.w) na hiyo ndio sahihi. Na vile vile ameipokea Allayth bni Saa’d na Ibnu Jurayj na Malik yaani Hawakuifikisha kwa Bwana mtume (s.a.w) –Mawquuf-.
[33]-Yaani hayo ayafanyayo ni kutoka kwa Mtume (s.a.w) au yanatokana na yeye mwenyewe Ibnu Umar (r.a)?
[34]-Juzuu 2/531 mtu wa 4728 المكتبة الشاملة .
- Vile vile Angalia Attahdhiib 10/321-2. Mtu wa:638 المكتبة الشاملة.
[35]-Miizaanul-i-itidaal 2/214, mtu wa :8897.المكتبة الشاملة
[36]-Attahdhiib 6/155 mtu : 356 .المكتبة الشاملة
-Angalia hadithi hiyo Imam Ali (k.w) anasema katika swala za fardhi kwa hivyo ina maana kwenye swala za sunna alikuwa hainui mikono.
[37] - Attahdhiib 5/197-8. Mtu wa:388 المكتبة الشاملة.
[38] -Mizaanul- i-itidaal 2/425-6 mtu wa: 4334. المكتبة الشاملة
[39] - Attahdhiib 9/332. Mtu wa :618 المكتبة الشاملة.
[40] - Miizanul-I-itidaal 2/539 mtu wa : 4767.المكتبة الشاملة.
[41]- Attahdhiib 8/194. Mtu wa :402. المكتبة الشاملة.
[42]-Miizanul –I-itidaal 3/365 Mtu wa : 6782.المكتبة الشاملة.
[43] - Attahdhiib 8/272. Mtu wa :553 المكتبة الشاملة.
[44] - J2/261- Chapa 1407H/1986ADدار الريان للتراث- القاهرة -
* Amesema Sh Assiyabiy:Na labda baadhi ya watu wamemevutiwa na kuathirika na kitabu –صفة صلاة النبي صلى الله عليه وسلم – cha Sheikh Albaaniy, ambaye ameweka ndani yake vipande vipande miongoni mwa hadithi hizi na hadithi nyengine, na katika jambo la kushangaza ni kuwa Sheikh Albaaniy ambaye anajulikana katika ufatiliaji wa kukosoa hadithi (zisizo sahihi) utamwona anajikalifisha – analazimisha – kwenye hadithi za kuinua na kufunga (mikono katika swala) kuzitafutia usahihi.
قال أبو عيسى حديث أبي هريرة [ حسن ]
|