Home SH.SHAABAN AL- BATAASHY

SH.SHAABAN AL- BATAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI : Asalaam alaykum shekh! Kuna jambo linanitatiza mwanamke ukiwa kwenye ada yako inaswihi kusoma na kuishika quraan? Madrasa ninayo soma ukiwa kwenye ada yako wanakwambia tunakukamatia  msahafu halafu unasoma.

mimi inanichanganya wanasema kwa dharura unasoma.

 JAWABU

➡ qurani ni kitabu cha allaah s.w kilicho safi,  na hakikamatwi wala kuguswa isipokuwa na watu waliotwaharika.

➡ Na muisilamu japokuwa  mwili wake hauwi najisi kama unajisi wa mnyama alieharamishwa . 

➡ Lakini ziko baadhi ya hali zinamfika muisilamu wa kiume na wa kike,  zikamzuia kufanya baadhi ya ibada ambazo zinahitaji twahara. 

➡ Na katika hali hizo ni : 

-Janaba :

Kwa mwanaume na mwanamke sawasawa . 

-Hedhi  -Nifasi :

Na hizi ni maalumu kwa wanawake tu peke yao. 

➡ Katika lugha ya kifiqhi :

Vyote hivyo vinaitwa hadathi kubwa. 

➡ Na vyote hivyo vinamlazimu muisilamu kujitwaharisha kwa kukoga mwili mzima kwa maji. 

➡  Na vyote hivyo vinamzuia muisilamu kutekeleza ibada zinalolazimu twahara,  k.v 

Sala  – saumu  – kutufu alkaaba – na kusoma qurani. 

➡ Amesema Allaahu s.w katika surati l waaqia : aya 77 – 79

“Hakika hiyo ni qurani kariim,  iko katika kitabu kilichohifadhiwa,  hawakigusi ila walikuwa wametwaharishwa” 

 ➡ Na katika hadithi ya imaamu rabii bin habiib r.a,  amesema mtume s.a.w kuhusu wenye janaba na wenye hedhi na waliokuwa hawana twahara :

“Wasisome qurani,  wala wasiguse mus’ hafu kwa mikono yao,  mpaka wawe wasafi “

 ➡ Na baadhi ya maulamaa wanasema kuwa :

Hata mwenye hedhi haruhusiwi kuswali,  kwa sababu ndani ya sala kuna qurani inasomwa katika rakaa zake. 

➡ Na Kauli hii ndio yenye nguvu zaidi kwa mujibu wa qurani na sunna na Kauli za maulamaa wa kiswahaba na wengineo waliowafuatia. 

➡ Na hiyo ndio Kauli inayolingana na maumbile sahihi ya kila muisilamu. 

➡ Hakuna tofauti kati ya hadathi hizo tatu kubwa tulizozitaja juu 

➡ Japokuwa iko Kauli katika madhehebu nyingine za ahli sunna,  zinajusisha kusoma qurani mwanamke mwenye hedhi au nifasi. ..

➡ Na ndio Kauli mashuhuri kwa ibni uthaimiin na al nawawy na wengine.

➡ kwa hoja kuwa :

Hakuna hadithi sahihi inayokataza mwanamke kusoma qurani kwa mwenye hedhi.

➡ kisha masiku ya hedhi yanaweza kuwa mengi,  kumfanya mwanamke akose kusoma qurani kwa muda mrefu.  Na huenda akasahau baadhi ya sura au aya.

➡ Kila penye khilafu ukiweza kuiepuka ni salama zaidi kwa dini yako.

Allaahu aalamu.

U / SHAABAN ALBATTAASHY NA UKHTI ZAKE.

Published By Said Al Habsy

SWALI : Asalaam alaykum shekh! Kuna jambo linanitatiza mwanamke ukiwa kwenye ada yako inaswihi kusoma na kuishika quraan? Madrasa ninayo soma ukiwa kwenye ada yako wanakwambia tunakukamatia  msahafu halafu unasoma.

mimi inanichanganya wanasema kwa dharura unasoma.

 JAWABU

➡ qurani ni kitabu cha allaah s.w kilicho safi,  na hakikamatwi wala kuguswa isipokuwa na watu waliotwaharika.

➡ Na muisilamu japokuwa  mwili wake hauwi najisi kama unajisi wa mnyama alieharamishwa . 

➡ Lakini ziko baadhi ya hali zinamfika muisilamu wa kiume na wa kike,  zikamzuia kufanya baadhi ya ibada ambazo zinahitaji twahara. 

➡ Na katika hali hizo ni : 

-Janaba :

Kwa mwanaume na mwanamke sawasawa . 

-Hedhi  -Nifasi :

Na hizi ni maalumu kwa wanawake tu peke yao. 

➡ Katika lugha ya kifiqhi :

Vyote hivyo vinaitwa hadathi kubwa. 

➡ Na vyote hivyo vinamlazimu muisilamu kujitwaharisha kwa kukoga mwili mzima kwa maji. 

➡  Na vyote hivyo vinamzuia muisilamu kutekeleza ibada zinalolazimu twahara,  k.v 

Sala  – saumu  – kutufu alkaaba – na kusoma qurani. 

➡ Amesema Allaahu s.w katika surati l waaqia : aya 77 – 79

“Hakika hiyo ni qurani kariim,  iko katika kitabu kilichohifadhiwa,  hawakigusi ila walikuwa wametwaharishwa” 

 ➡ Na katika hadithi ya imaamu rabii bin habiib r.a,  amesema mtume s.a.w kuhusu wenye janaba na wenye hedhi na waliokuwa hawana twahara :

“Wasisome qurani,  wala wasiguse mus’ hafu kwa mikono yao,  mpaka wawe wasafi “

 ➡ Na baadhi ya maulamaa wanasema kuwa :

Hata mwenye hedhi haruhusiwi kuswali,  kwa sababu ndani ya sala kuna qurani inasomwa katika rakaa zake. 

➡ Na Kauli hii ndio yenye nguvu zaidi kwa mujibu wa qurani na sunna na Kauli za maulamaa wa kiswahaba na wengineo waliowafuatia. 

➡ Na hiyo ndio Kauli inayolingana na maumbile sahihi ya kila muisilamu. 

➡ Hakuna tofauti kati ya hadathi hizo tatu kubwa tulizozitaja juu 

➡ Japokuwa iko Kauli katika madhehebu nyingine za ahli sunna,  zinajusisha kusoma qurani mwanamke mwenye hedhi au nifasi. ..

➡ Na ndio Kauli mashuhuri kwa ibni uthaimiin na al nawawy na wengine.

➡ kwa hoja kuwa :

Hakuna hadithi sahihi inayokataza mwanamke kusoma qurani kwa mwenye hedhi.

➡ kisha masiku ya hedhi yanaweza kuwa mengi,  kumfanya mwanamke akose kusoma qurani kwa muda mrefu.  Na huenda akasahau baadhi ya sura au aya.

➡ Kila penye khilafu ukiweza kuiepuka ni salama zaidi kwa dini yako.

Allaahu aalamu.

U / SHAABAN ALBATTAASHY NA UKHTI ZAKE.

Published By Said Al Habsy

SWALI :

SHEIKH NINI HUKUMU YA MWENYE KUWEKA PICHA YA MWANAMKE  KICHWA WAZI AU PIA KAVAA MTANDIO KATIKA PROFILE YA WHATSAPP ?


JAWABU: 

➡ Mwanamke ni kiumbe bora ambae allaah s.w  amemuhifadhi na kumuwekea sheria bora kabisa zenye kuhifadhi utu wake.

➡ Kutokana na hayo;

Hata qurani haikutaja majina ya wanawake waziwazi,  ila tu katika kuzungumza jambo zito la muujiza wa bi maryam mama yake nabii iisa a.s  katika kumzaa mwanae bila ya kuwa na mume.

➡ Wanawake wengine wote hawakutajwa kwa majina yao.

Isipokuwa wametajwa kwa jinsia zao au Sifa zao,  au kwa kunasibishwa kwa waume zao.

Kama vile :

1 “Na mke wake…”
Katika surati l masad – tabbat yadaa…

2 Mke wa nuuhu na mke wa luut.

3 Mke wa fir’aun.

4 “Ummi muusaa ” Katika surati l qaswas.

5 “Ukhtihi “
Dada yake nabii Musa.

6 Imra’ataini “
Wanawake wawili katika kisa cha nabii Musa akiwa katika mji wa madyana

➡ Vipi Leo ikafikia wanawake wanatembea wamevaa lakini sawa na hawakuvaa.

➡ Wanakaa nywele wazi na vifua vyao pia,  hali ya kuwa wameamrishwa wahifadhi hata sauti zao.

➡ Haifai kwa mwanamke kuweka picha yake katika profile ambayo wanaiona  watu mbalimbali,  wakiwemo wanaume wasiofaa kumuona mapambo yake.

➡ Nywele za mwanamke ni sehemu katika aibu kubwa kudhihirisha kwa watu.

➡ Na Hakuna dharura yoyote katika kufanya hivyo.

➡ Ila katika hali moja tu ambayo inawezekana kuweka picha hiyo katika profile,  nayo ni :

• na ikiwa profile hiyo hatuiona isipokuwa mtu wake wa karibu tu ambae ana nambari zake.

• Ikiwa picha hiyo iko katika stara ya kisheria

Allaahu aalamu.

SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je picha ya mtu aliekufa inafaa kutumiana ?


JAWABU:

➡ Suala la kupiga picha bila ya kuwepo haja muhimu au dharura ya kufanya hivyo,  lina mtazamo wa Kauli mbili katika maulamaa.

1 Kujuzu kufanya hivyo ikiwa ni picha ya photograph kwa kuzingatia pia adabu na stara ya anaechukuliwa picha hiyo.

2 Kauli ya pili ni
Hakuna ruhusa ya kupiga picha ila katika hali ya dharura ,  kama kutoa paspot au kitambulisho cha uraia na mfano wake.

➡ Na Kauli ya mwanzo ndio ya wengi zaidi katika maulamaa.

➡ Amma kumpiga picha mtu mwingine bila ya ruhusa yake,  jambo hilo halifai kisheria.

➡ Anasema sheikh Dk kahlaan bin Nabhaan al kharuusy – Naibu wa mufti  wa Oman allaah awahifadhi :

➡ Si haki ya muisilamu kuingilia mambo ya mtu mwingine na utu wao – au hali maalumu ya mtu mwingine.

➡ Ikiwa muisilamu katika sheria ya KIISILAMU   amekatazwa kutazama ndani ya nyumba ya mwingine bila ruhusa yake, Vipi itafaa kwake kuuchukua picha na kuieneza kwa wengine

➡ Haifai kuchukua muisilamu picha ya mtu,  ikiwa yu hai au ameshakufa,  mgonjwa au mzima,  au majeruhi, ila kwa kupata ruhusa yake mwenyewe kuchukuliwa picha yake,
Na ruhusa yake kutangaza picha yake.

➡ Amma ikiwa mwenyewe hakuruhusu,  basi asili ya hukmu katika hilo ni kuwa linakatazwa.

➡ Mara ngapi imeonekana kutokea matatizo na mishituko mikubwa sana,  kwa kutokea ajali pahala fulani,  kisha kwa haraka watu wakaeneza picha za waliosibiwa na ajali,  na zikawafika jamaa zao kwa ghafla, na kuwasababishia mfadhaiko mkubwa.

➡ Na kama ikiwa lengo la picha mathalan ni :
Kuwazindua wengine mfano hatari ya kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kubwa,  ili kuwatahadharisha na hilo,  inajuzu kuchukua picha za wenye mwendo kasi kama huo kwa kuonyesha ule mwendo tu na chombo Chao,  bila kuonyesha picha za watu wenyewe wanaohusika na mwendo huo.

➡ Amma kuchukua picha ya mtu au watu waliokufa na kueneza kwa wengine,  haisihi ila kwa kupata ruhusa kutoka kwa jamaa wa maiti huyo au hao.

➡ Na haifai kuchukua picha ya mtu kwa ajili ya kumfanyia maskhara na dhihaki tu katika vikao na mazungumzo na wengine.

➡ Amma kuchukua picha za watu waliokuwa ni mashuhuri katika jamii zao,  kama vile watu wema  – au maulamaa – au watu wenye vyeo vya juu.

 

LIMEJIBIWA NA

SH. SHAABAN AL-BATAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI :

NAOMBA KUKUULIZA ETI KUMFUNGA MVUJE MTOTO  MCHANGA NA KUMUEKEA KISU NA NDIMU PAHALI ANAPOLALA INAFAA ?


JAWABU:

➡ Hayo yote yalioulizwa ni miongoni mwa bid’aa katika itiqaadi.

➡ Na ni katika mambo ambayo walikuwa wazee wa zamani wakiyatumia kwa ajili ya kuwakinga watoto wao na shari za viumbe vyenye shari.

➡ Na wengine huwa wanawafunga vikamba vyeusi mkono wa kulia.

➡ Wengine wanafunga  mvuje na ubani wa dua na mfano wake,  kwa kuitakidi kuwa ni kinga kutokana na shari.

➡ Wengine wana wakakaa jivu la moto wa mafia au majifya yaliyobakia baada ya kupika kwa moto wa kuni.

➡ Wengine huwapakaa masizi ya vyombo katika nywele za  tosi za  vichwa vyao.

➡ Haya yote kuyafanya kwa nia ya kuwa vinaondoa shari au vinamkinga na shari,
Au vinamuhifadhi,
Hiyo ni shirki katika itiqaadi,  na analazimika mtu kutubia na kuacha mara moja shirki hiyo,  na badala yake anatakiwa :

➡ Arudi kwa allaah s.w.

➡ Amtegemee allaah s.w.

➡ Atafute kinga kwake kupitia ibada na dhikri mbalimbali katika qurani na sunna.

➡ Kumbuka kuwa :
Kujitibu tiba ya kawaida kwa kutumia vitu kama;
Ndimu  – mvuje kwa kunywa au kupakaa,  inajuzu kutumia,

➡ Kinachoharamika ni kuvifunga na kuvining’iniza na kuitakidi kuwa vina uwezo wa kuondoa shari.

➡ Na katika hadithi ya mtume s.a.w amesema :
” yoyote mwenye kuning’iniza kitu,  basi allaah atamuacha awe tegemeo lake hicho kitu ” na hakitomsaidia kitu.

Allaahu aalamu.
LIMEJIBIWA NA 

SH.SHAABAN ALBATTAASHY.

 

Published By Said Al Habsy

SWALI :

Asalam alaykum me natak kuuliza ni sura gani unasoma unaposwali sala ya usiku? Na ni dua gani unaisoma?


JAWABU :

➡ sala ya usiku  (qiyaamu llaili), inaswaliwa kwa rakaa 11 au 13.

➡ Na inaswaliwa rakaa mbili mbili kisha salaam,  mbili kisha salaam ,  hadi kutimia rakaa nane.

➡ kisha baada ya nane hizo,  ataswali witri rakaa tatu kama anavyosali magharibi,
Au anaweza kuswali rakaa mbili kisha salaam,  kisha anyanyuke tena kwa ajili ya rakaa moja.

➡ Na sura za kusomwa katika sala hiyo ni :

1 Alhamdu na sura nyingine yoyote baada yake.
Kama alivyosema allaah s.w katika surati l muzammil
“فاقرؤوا ما تيسر من القرآن “
“Someni kilicho wepesi katika qurani “

➡ amma katika rakaa tatu za witri, utasoma kama ifuatavyo:

1. Rakaa ya kwanza :
Alhamdu na sabbihi sma rabbika l a’alaa”

2. Rakaa ya pili :
Alhamdu na qul yaa ayyuha l kaafiruun”

3 Rakaa ya tatu :
Alhamdu na qul huwa llaahu ahad.

➡ Na dua za kuomba wakati wa usiku baada ya sala Inshaallaah nitazituma baada ya muda Inshaallaah.

Allaahu aalamu

LIMEJIBIWA NA
sH.sHAABANI AL-BATASHI

Published By Said Al Habsy

SWALI :

KUJITOLEA MUISILAMU SEHEMU YA VIUNGO VYAKE VYA MWILI KUMSAIDIA MGONJWA ANAEHITAJIA ?

JAWABU :

➡Mwili wa binaadamu katika mtazamo wa sheria ya KIISILAMU si haki yake mwenyewe kamili.

➡ mwili huo ni haki ya Allaah s.w alieuumba.

Na haijuzu kuudhuru kwa chochote.

➡ Kwa hiyo haijuzu kutoa kiungo ambacho kikitolewa kitasababisha kuharibika maumbile ya mtoaji au kuharmtarisha maisha yake.

➡ Kutokana na kuwa binaadamu anafikwa na mengi,  na huenda akahitajia kusaidiwa kitu kutoka mwili wa mwingine ili kuokoa maisha yake,  na katika hilo kuna ujira mkubwa sana.

➡ Kutokana na hilo maulamaa wameweka masharti ili jambo hilo kukualika,  nayo ni :

1 Kujitolea huko kusipelekee kifo kwa mwenye kujitolea huyo.

➡ Haifai kutoa kitu kama ini,  moyo .

2 Haifai kumpa mtu viungo vya mwili ambavyo vitasababisha kuchanganyika nasabu.

Kama korodani za mwanaume,  au yai la uzazi la mwanamke.

3 Uwe mwili wa mtoaji hauhitajii kiungo hicho,  na mwili haupati madhara kwa kutolewa kiungo hicho.

4 Jambo hilo kufanyika liwe ni kutokana na dharura kubwa,  kiasi ambacho Hakuna tiba badala ya hiyo.

5 Jambo hilo lifanywe na madaktari bingwa wenye uzoefu,  kiasi ambacho hawatomsababishia madhara kwa mtoaji wala mpewaji.

6 Mafanikio ya jambo hilo yawe ni uhakika kuwa yatawezekana kufanikisha,  na hii inakuwa kwa makadirio ya madaktari hao.

7 Kuruhusika kujitolea viungo hivyo kusiwe ni sababu ya watu kufanya Biashara ya kuuza viungo vyao,  Kama wanavyofanya wengi katika nchi masikini ulimwenguni.

➡ Na viungo hivyo ikiwa atatoa mtu kwa masharti tuliyoyasema,  haifai kuuza kwa Gharama yoyote.
Kwa sababu binaadamu hamiliki mwili wake.

➡ Na pia haifai mtu kuusia kuwa akifa atolewe viungo vyake.
Usia huo utakuwa ni batili.

➡ Na maiti ana haki na utukufu wake sawa na aliekuwa hai.


➡ Rejea kitabu cha fataawa twibiyya cha mufti shaikhinaa alkhaliily allaah s.w amuhifadhi.

 

LIMEJIBIWA NA

SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

 

Published By Said Al Habsy

SWALI :

JE INAFAA KUSALI BILA YA NGUO YA NDANI?

 

JAWABU :

➡Katika masharti ya sala ni kusitiri mwili katika sala.

➡ Na mwili unaositiriwa ni mwili ambao unahalesabika kuwa ni aibu kudhihirisha kama uchi na mipaka yake kwa mwanamke na mwanaume.

➡ Na mwanamke mwili wake wote ni uchi – yaani una hukmu kama sehemu za siri,  na ni aibu kudhihirisha katika sala,  ila sehemu mbili tu kwa mwanamke,  ambazo ni uso na viganja viwili vya mikono,  hivyo vinafaa kuwa wazi katika sala,  Bali ni lazima kuviacha wazi ila kwa dharura tu.

➡ Kwa hiyo mwanamke anatakiwa Kuvaa guo refu linalofunika mpaka nyayo za miguu,  au avae soksi miguuni ili kufunika miguu yake.

➡ Na hiyo ndio Kauli sahihi inayotegemewa hata kwa masheikh wawili :
1 – Sh. Ahmad bin Hamad Al- Khaliily

2 – Sh. Said bin Mabruuk Al – Qannuuby.


Allaah awahifadhi.

 

➡ Amma kusali bila nguo ndogo ya ndani,  Inshaallaah Hakuna tatizo katika hilo,  midhali mwili wake wote umesitiriwa,  na sisi tumeamrishwa kusitiri miili inayodhihirika, na sio iliyofichikana kwa chini.

➡ Na imaamu nuuru ddiini assaalimy R.a akiulizwa kuhusu mwanaume anaeswali huku amevaa kikoi bila nguo nyingine kwa ndani,  yaani uume wake ukawa wazi kwa upande wa chini ya kikoi,  Akasema haina tatizo katika hili Inshaallaah midhali amemsitiri mwili wake katika pande zote hizo.

Allaahu aalamu.

LIMEJIBIWA NA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

 SWALI :

 

Assalam aleykum warahma tullahi wabarakatuh!! Sheikh kuna swali: Eti kuna Hadith iliyosahihi inayosema kua mwanamke akimruhusu mumewe kwa hiari yake kuoa mke wa pili ni kwamba  mwanamke hy akifa ataingia peponi moja kwa moja kwa kua kumruhusu Mume kuoa mke wa pili ni km kapigana jihad je ni Kweli sheikh? Naomba majibu ukijaaliwa in shaa Allah!


JAWABU :

➡ Hadithi hiyo ina uzushi mtupu na wala Hakuna kitabu chochote nilichokuta habari kama hii.

➡ Na hata maelezo yaliyomo ndani ya hiyo inayosemwa kuwa ni hadithi yanaonyesha uongo uliomo ndani yake.

➡ Na katika alama za kuwa Hadithi  ni ya kutungwa tu :


1.  Kutoa malipo makubwa sana kwa sababu ya amali ndogo sana.
 
➡ mume akiwa ana uwezo wa kutekeleza uadilifu kati wake zake,  inajuzu kwake kuoa hata bila ruhusa ya mkewe.

➡ Na Hakuna malipo maalumu kwa mwanamke mwenye kumruhusu mumewe kuoa kwa hiyari yake.

Ila atapata malipo ya kawaida tu kwa kuwa amefanya jambo la kheri,  na hakuwa na chuki na mwenzake,  na amesubiri katika jambo ambalo nafsi huwa ina uzito kulisubiria.
 
Allaahu aalamu.
 

 
LIMEJIBIWA NA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI :


Kuna swali sheikh limeulizwa kuna mtu kaolewa na mume mzee lakini mumewe alipofika mwaka 2012 nguvu hana tena za tendo la ndoa – Nini afanye?
Anaomba ushauri .JAWABU :

➡ Katika misingi mikuu  ya kuchagua mke au mume ni :
Kuwepo ” kafaa’a” “الكفاءة “

➡ Na maana yake ni
“Usawa au ulingano ” kati ya mke na mume katika baadhi ya sifa.

➡ Na ulingano mkubwa unaotakikana kisheria ni ulingano wa kidini,  wakawa wote wawili ni waisilamu na wema.

➡ Amma  ukabila huo si sharti katika usawa kati yao.

Na ndio Kauli sahihi katika fatwa za maulamaa wengi,  na katika hao masamaaha wawili wakuu katika fatwa,
1. Sh. Ahmad bin Hamad Al – Khaliily

2. Sh. Said bin Mabruuk Al- Qannuuby.

Allaah awahifadhi.

➡ Pia usawa wa kipato na maisha si lazima wawe sawa katika hilo.

➡ Pia katika aina ya kazi si lazima wawe sawa,  kama wanavyodhani wengi kuwa kuna baadhi ya kazi zinaweza kumkosesha mtu sifa za kuowa baadhi ya aina fulani za wanawake,  kama vile mume ikiwa kazi yake ni :

* Muuza mboga.

* Kinyozi

* Mpiga chuku. Nk

➡ Haya yote si sahihi,  kwa kuwa Hadithi iliyotaja kazi kama hizo kuwa zina athari katika kukualika mume,  ni hadithi dhaifu,  na zinapingana na dalili zilizokuwa wazi kabisa katika qurani na sunna na vitendo vya maswahaba r.a.

➡ Na hukmu ya udhaifu wa hadithi hiyo imeelezwa  na maulamaa wakubwa wa fani ya hadithi ambao ni :

1- Sh. Nuuru ddiini assaalimy R.A

2- Sh. Said bin Mabruuk Al -Qannuuby – allaah amuhifadhi.

➡ Amma kuhusu umri kati ya mume na mke;
Hapo inategemea jinsi gani wametofautiana katika umri wao;

1⃣ ikiwa tofauti ni kubwa sana,  mfano :
Mume ana umri wa miaka 50 au 60, na mwanamke hajatimiza hata miaka 20,
Hapo Itabidi umri uzingatiwe katika suala la usawa au ulingano,  kwa kuwa kumuozesha mtu kama huyo itakuwa ni kumdhulumu mtoto wa kike haki yake,  na kumkosesha haki zake nyingi za kimsingi katika sheria.

2 Amma ikiwa tofauti ya kiumri ni ndogo na ya kawaida,  hiyo haina athari yoyote katika ndoa au kukualika mume.

➡ Na dalili ya hilo,  ni mtume s.a.w alipomuoa bi khadija ulikuwa umri wa mtume s.a.w ni miaka 25.

Wakati huo bi khadija akiwa na miaka 40.

Na Hakuna athari yoyote iliyokezea kwa sababu ya kutofulautiana umri kati yao.

➡  Amma kiafya,  ikiwa mume ana maradhi ya kuwa amekosa tena nguvu za kiume,  akawa hawezi kumuingilia mkewe,  hapo kuna hali mbili :

1 Imma hali hiyo haitibiki tena kabisa,  hapo mke ataomba ruhusa ya kuachwa na mumewe;  kwa kuwa atakuwa katika hali ngumu na kuvumilia hakuwezekani,  na dharura hiyo si ya kumalizika.

2 Au itakuwa ugonjwa huo unatibika :
Na hapo kadhi atakarldiria muda maalumu wa kushulikia mume matibabu ya ugonjwa huo.

Na muda huo ni muda ambao kikawaida mwanamke anaweza kusubiri bila kuingiliwa na mume.

➡ Na maulamaa wanaukadiria muda huo kuwa ni mwaka mmoja tu kamili.

➡ ikiwa atapona na kuweza kumuingilia mkewe itakuwa vizuri,  na kama itakua bado,  basi mwanamke ana haki ya kudai kuvunjwa ndoa kati yake na mumewe.
Na huenda ikawa kupata mwingine ni kheri kwake.

Rejea kitabu cha
Almuutamad katika fiqhi nnikaah – UK 389 – 390.

Allaahu aalamu.

Nuurun alaa nuur.

LIMEJIBIWA NA

SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI :
Salaa ya Ijumaa kwa sisi wanawake tunasali nyumbani. Tukisali Salaa ya Ijumaa Rakaa mbili za mwanzoni tunasoma Alhamdu na sura ?
Au tunasali kama kawaida Salaa ya Dhuhur Alhamdu tu bila kuisoma sura nyingine ?

JAWABU :

➡ sala ya ijumaa Inaswaliwa rakaa mbili tu katika muda ambao ni wa sala ya adhuhuri.

➡ Na sala ya ijumaa ni badala ya sala ya adhuhuri kwa siku hiyo.

➡ mwenye kusali sala ya ijumaa,  inamtosheleza yeye sala hiyo,  wala haifai kusali tena adhuhuri baada ya kumalizika sala ya ijumaa.

➡ Na katika masharti ya kuswaliwa ijumaa,  ni lazima sala hiyo itanguliwe na khutba ya ijumaa.

➡ Na sala hii ya ijumaa ni wajibu kama zinavyowajibika sala nyingine tano kwa siku.

➡ Na sala ya ijumaa ni wajibu kwa wanaume tu,  kwa kuwa wao ndio inawawajibikia sala ya jamaa.
➡ Na dalili ya kuwajibika sala hiyo ni aya 9 ya qurani katika surati l jumuaa .

➡ Na sala hiyo ni wajibu kwa watu wafuatao :

1 Mwanaume :
Kwa hiyo kwa mwanamke si wajibu kuswali ijumaa.
Abakie nyumbani na kuswali adhuhuri tu.

2 Baaleghe :
Sala hiyo haimuwajibikii mtoto ambae haja baaleghe bado.

3 Mkaazi :
Kwa hiyo haimuwajibikii aliekuwa ni msafiri akiwa njiani au katika mji ambao si wake na hajakusudia kuwa mkaazi wa hapo.

4 Huru :
Haimuwajibikii mtumwa ambae amemilikiwa na bwana wake na hajawa huru bado.

5 Mwenye uwezo:
Haimuwajibikii ambae hawezi,  imma kwa uzee au maradhi.

➡ Na ikiwa mwana ataswali sala ya ijumaa nyumbani kwake,  sala hiyo itakuwa ni batili Haikubaliki.

➡ Lakini ikiwa kutakuwa katika mji kuna amani,
Na Hakuna kuhofia fitna,  na mwanamke akaswali msikitini sala hiyo ya ijumaa,  sala yake itasihi bila tatizo lolote,  midhali masharti ya kutimia na kusihi sala hiyo yametimia.

➡ Sala adhuhuri Inaswaliwa kwa kusomwa Alhamdu katika rakaa zake zote nne,  na hii ni Kauli ya madhehebu ya ibadhi wote bila tofauti yoyote kati yao.

Amma katika sunni wao ni sunna kusoma sura nyingine baada ya alhamdu katika rakaa mbili tu za mwanzo,  Ijapokuwa kuna Kauli pia ya kusoma sura katika rakaa zote nne,  lakini mashuhuri na sahihi kwao ni ile ya mwanzo.


➡ Na hao wote wamekubaliana kuwa :
Mwenye kusoma alhamdu tu katika sala sala yake itakuwa imetimia.


Allaahu aalamu.

ELIMU KWA ELIMU HADI MAARIFA.

LIMEJIBIWA NA

SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:


Kama itatokea kwa upande wa mke akawa mzinifu na akamuomba radhi mumewe kuwa hatofanya tena uzinifu ndoa yao inaweza kuendelea kama mume akimsamehe?

 

JAWABU :

➡ Jambo la zinaa  ni zito na lina hatari mbaya sana,  kwa mke au mume,  Bali hata family na jamii nzima.
 
➡ Ikitokea kuwa mke aliwahi kuzini kabla ya kuolewa na mume huyo alienae, basi mke huyo anatakiwa afanye yafuatayo :

1. Atubie kwa mola wake toba ya kweli,  na ajute sana kwa dhambi hilo.

2. Afiche siri na kujisitiri kama ilivyokuwa allaah amemsitiri kwa kuwa hakumfedhehesha kwa dhambi hilo,  na wala asilitaje kwa watu kulihadithia, hata mumewe asimtajie dhambi kama hilo.

➡ Na hii haina maana kuwa anaruhusiwa kuasi kisha ayafiche maasi yake…
Laa haashaa!

Bali hiyo ni katika kuhifadhi maslahi makubwa yafuatayo :


1 Kuhifadhi dini ya mwanamke na uisilamu wake.

2 Kuhifadhi utu na heshima yake,  kwa kuwa kujitangazia zinaa ni kuvunja heshima na utu wake .

3 Kuhifadhi ndoa ya wawili hao,  kwa sababu Ikitokea mmoja wao kujisema kuwa aliwahi kufanya uovu wa aina hiyo,  kunavunja mapenzi kati yao.

➡ Na kunaondoa uaminifu baina yao.

➡ Kunaondoa utulivu wa nafsi katika nafsi zao.

➡ Pamoja na hayo ikiwa mtu ametubia maasi yake hayo,  kwa kufuata taratibu zote za toba,  Inshaallaah allaah s.w atamsamehe makosa yake,  na atambalishia maovu yake kuwa mema, kama alivyosema allaah katika aya za mwisho mwisho katika surati l furqaan.

➡ Na haya yote tuliyoyataja hapa yanamuhusu kila muisilamu wa kiume na wa kike.

➡ Tumuombe allaah atusitiri duniani na akhera.

Allaahu aalamu.

ELIMU KWA ELIMU HADI MAARIFA.

 

 

LIMEJIBIWA NA

SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI  :

Juzi nikiwa Dar es salaam na mmoja katika dada zetu kuwa :

Nini humu ya mwanamke anaevua nguo zake zote mbele ya wanawake wenzake?

JAWABU :

➡ Uisilamu ni dini ya usafi na kuhifadhi maumbile ya mwana adamu.

➡ Ni haramu kisheria kwa yoyote kufunua na kukashifu mwili wake mbele ya mwingine,  ila ikiwa ni sehemu za mwili ambazo ni kawaida kuonekana,  kama viganja vya mikono,  na uso na sehemu za mwili mwingine ambazo si kati ya kitovu na magoti.

➡ mwanamke haifai kudhihirisha mapaja yake mbele ya wanawake wenzake.

➡ Na mwenye kufanya hivyo analaaniwa na allaah s.w yeye na kila mwenye kutazama kwa makusudi.

➡ Mtume s.a.w alimuusia swahabi wake Ally bin abii twaalib r.a kwa kumwambia :


“Ewe Ally;
“Usifunue paja lako kwa watu,  na wala usitazame paja la aliekuwa hai wala aliekufa”

➡ Ni ajabu katika zama hizi kuona na kusikia wanawake Leo wanafanya haya yafuatayo :

1. Wanatoka majiani vichwa wazi na nywele zikionekana kwa watu.

2. Wengine wanavaa mashungi mafupi kiasi ambacho vifua vyao huonekana hata maumbile ya maziwa ya vifua vyao.

3. Na wengine wanakata nguo zao mpasuo sehemu ya kifua, na wanatembea hivyo mbele za wanaume wala hawajali.

4. Kuna wenye Kuvaa visketi  vivupi na vya kubana na vya mpira,  tena wanavaa viguo hivyo mbele za watu.

5. Na kuna mashule mengi yenye hostel za wanawake, hazina maadili ya kidini kabisa wala malezi.

➡ wanafunzi wanawake wakubwa wanakoga pamoja na kuvua nguo mbele za wenzao na kukoga pamoja.

Na hili ni kosa kubwa sana.

➡ wanavua nguo zote na Kuvaa nyingine mbele za wenzao hali ya kuwa wako miili mitupu haina kitu kinachiloifunika.

6. Wanachukuana picha wakiwa wamevaa nguo za ndani tu,  na kutumiana katika simu kupitia mitandao ya kijamii, na wengine kuweka profile picha hizi.

7. Kupewa uhuru wa kutumia simu kwa uhuru bila nidhamu yoyote wala mipaka maalumu.

➡ je nini kinatarajiwa katika mazingira haya kwa wanawake hawa

➡ lini watapata tabia ya kuwa na haya

➡ lini watajifunza kuwa wema na wenye kuuhifadhi utu wao 

➡ Ndugu zangu tukumbuke kuwa :

Watoto ni dhamana,  na wazazi ni wadhamini.

Allaahu aalamu.

 

 

LIMEJIBIWA NA

SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI :
Jamani  Eti kama wewe mwanaume umesafiri ukamuacha mkewako na mdogo wako wakiume ukakaa sana huko uliko kwenda kwa bahati mbaya mke wako akashkika akashindwa kujizuwiya na wewe madamu anakupenda akaamuwa asiende mbali akaona bora afanye mapenzi na ndugu yako kwa bahati mbaya amapata uja uzito na wewe uliporudi akaona asikufiche akwambiye ukweli.

Je ? Kama wewe ndio kaka utachukuwa uwamuzi gani ?
Utamuacha mke au utamfukuza nduguyako au utaficha siri ule maisha yako? Nahitaji jibu jamani lakueleweka!

JAWABU 

➡Zinaa ni moja ya madhambi makubwa ambayo yana hukmu zake kutekelezewa duniani kabla ya akhera.

➡ Kutokana na hatari kubwa ya jambo hili:
Uisilamu umeweka mipaka maalumu ili kumkinga muisilamu asifikie kuwa mzinifu.

1. Kukatazwa mchanganyiko kati ya wanawake na wanaume,  ambao kisheria wanaweza kuoana,  japokuwa kujuzu huko ni kwa siku za baadae.

➡ watu wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mahram na ajnabiy katika Wanawake na wanaume.

➡ MAHRAM ni “Kila ambae anaharamika kuoana nae mpaka qiyaama “

Yaani haitotokea hali yoyote ikafaa kuoana nae.

Mfano :

* Baba hawezi kumuoa binti yake maisha.

* Kaka hawezi kumuoa dada yake maisha.

* Mtoto wa kiume hawezi kumuoa mama yake daima.

Na mfano wa hayo.

➡ Kuna wengine wanadhani kuwa :
Mke wa kaka yake anafaa kukaa nae faragha wao wawili tu,  au kusafiri nae n.k

Au wanaume wengine wanadhani kuwa dada wa mkewe anafaa kuchanganyika nae katika faragha, na kugusana nae mikono n.k.

➡ Naam :
Uharamu wa kuoana kati ya hao upo, lakini ni wa muda maalumu ambao unaweza kumalizika kwa hali moja kati ya mbili :

1. Mume akimuacha mkewe talaka ambayo hawezi kumrejea tena,  au talaka ya kuweza kumrejea, lakini akawa hakumrejea  hata muda wa eda ukamaliza,  hapo inajuzu kumposa dada wa aliekuwa mkewe.  N.k

➡ Kwa hiyo shemeji kubakia na shemeji yake ni hatari kama kifo. Haifai.

2. Hali ya kutokea kifo cha mkewe.
Inajuzu kwa mume huyo kumuoa dada wa aliekuwa mumewe wakati wowote baada ya kifo hicho,  kwa sababu mume hana eda ya kusubiri.

➡ Na mke wa mtu akizini na mwanaume zinaa ya hakika ya kuingiliana kwa tupu zao, kama yanavyokuwa  maingiliano kati ya mke na mume;  Mke huyo kuhusu ndoa yake kuna hali hizi  :

1. ikiwa mumewe atamsadikisha katika hilo, Itakuwa ndoa yao imeharibika. ..NA wala haifai kwa mwanaume msafi wa tabia kuishi na mwanamke mchafu  mzinifu.

➡  Na ikiwa madai yake yana aina ya kuwa hayana ukweli,  basi haitokubalika mpaka akiri mara nne katika nyakati tofauti kuwa kweli amezini.

Akikiri mara hizo ni ikathibitishwa  hilo,  ndoa inavunjwa, na mwanamke huyo hatopata haki yoyote kwa mumewe.

Na ni kauli ya maulamaa wengi wa kiibaadhi allaah awahifadhi maulamaa wote wa kiisilaamu.

➡Tahadhari kubwa sana napenda kunabahisha 

1. Kuna hatari kubwa katika kuchanganyika watoto wa kiume na wa kike hasa  katika zao za kulala.

2.Pia kuchanganyika wafanyakazi wa ndani wa kiume na wa kike bila kuwa na mipaka maalumu ya kisheria.

3. Hatari ya ushemeji unaovuka mipaka ya dini ya kiisilaamu.

4. Hatari ya watoto wa kiume waliofikia umri wa kutambua mambo mbalimbali,  kulala pamoja katika kitanda kimoja na kujifunika shuka moja.

Zimekuja hadithi mbalimbali za mtume s.a.w  kutahadharisha mengi katika haya,  na hata kwa wanawake kwa wanawake pia kuna mipaka yao maalumu.

Allaahu aalamu.
ELIMU KWA ELIMU HADI MAARIFA.


 

LIMEJIBIWA NA

SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI :

Asalam Aleykum !

Kuna mafuta ya nywele hayo mafuta ndani yake yamechangaywa na mkojo wa ngamia bikri sasa haya mafuta ukipaka itafaa kusali au itakua najisi?

Je na kama mtu akipaka halafu aoshe nywele ndipo asali itafaa?JAWABU

➡ Mkojo wa wanyama katika asili ni najisi.

➡ Na hasa wanyama ambao asili yao ni haramu kuliwa.

➡ Amma mkojo wa wanyama ambao asili yao ni halali kuliwa,  hukmu ya mkojo wa wanyama hao ina maelezo kama ifuatavyo :

1 Katika madhehebu ya maaliky na hanbaly  wanasema :

” mkojo wa wanyama ambao asili yao ni halali kuliwa,  ni twahiri wala si najisi.

Kama mkojo wa –  Ngamia – Ng’ombe  – Mbuzi – Kondoo – Kuku – Njiwa na jamii ya wengineo wanaoliwa.

➡ Na macheuzi ya wanyama hao na haja zao kubwa si najisi.

➡ Isipokuwa madhehebu ya maaliky wanabagua hali moja ambayo inasababisha kuwa mkojo wa wanyama hao unaweza kuwa najisi,  nayo ni :


“Ikiwa wanyama hao wanakula au kunywa vitu ambavyo ni najisi,  hapo vitokavyo katika njia mbili hizo navyo vitakuwa ni najisi.

➡ Na hali kadhalika hukmu ya mkojo wao na kinyesi Chao inatokana na asili ya hukmu ya nyama yake, ,,

➡ Mnyama anaehalalika nyama yake,  vinyesi vyake pia si najisi.

➡ Na aliekuwa makruuh kuliwa pia vinyesi vyake huwa makruuh kutumika.

➡ Na asiekuwa haramu kuliwa pia huwa haramu vinyesi vyake vyote.

➡ Na hoja ya hawa wa Kauli hii ni kuwa :
Imepokewa hadithi katika sahiihi – bukhaary na Muslim na musnadi  imaam ahmad,  kutoka kwa swahabiyi anas bin maalik r.a amesema :
” Watu kutoka ukli au uraina,  waliingia mji wa madina,  na wakachukia kukaa katika mji huo,  kwa kuumwa kwao –  Mtume s.a.w  akawaamrisha watoke nje ya mji, kisha wakanywe  mkojo wa ngamia na maziwa yake “

2 Kauli ya pili ni madhehebu ya shaafy na hanafy wanasema :
” mkojo , matapishi na kinyesi cha wanyama  na binaadamu vyote ni najisi.

➡ Na hoja zao ni :


1 Hadithi aliyoamrisha mtume s.a.w kumwagia maji katika sehemu ambayo alikojoa bedui.

2 Na hadithi ya wanaoadhibiwa katika makaburi mawili,  mmoja wao alikuwa hajisafishi  mkojo.

3 Na ziko hadithi nyingine nyingi zinaamrisha kujisafisha na kujisafisha kutokana na mkojo.

3 Kauli ya tatu ni Kauli ya hanafii, ni kuwa :


➡Mkojo wa mnyama anaeliwa  nyama yake ni najisi na najisi yake ni hafiifu haiathiri katika sala ikiwa itaingia katika nguo kiasi cha robo ya nguo tu,  ikizidi hapo itakuwa haifai kuswalia.

➡ Amma kinyesi cha wanyama kama farasi ambae nyama yake hailiwi,  inakuwa ni najisi nzito.

➡ Na Kauli katika madhehebu ya ibaadhi pia ni kuwa :

“Mkojo wa wanyama wanaoliwa asili yake unakuwa ni najisi.

➡ Kutokana na hayo;

1 Haifai kutumia mafuta yalichanganyishwa na kitu chenye najisi kama mkojo wa ngamia n.k

2 Na ikiwa atapakaa mafuta yenye mchanganyiko huo baada ya udhu itakuwa udhu haisihi.

3 Na haifai kutumia vitu vyenye najisi kwa ajili ya tiba.

Allaahu aalamu.

 

LIMEJIBIWA NA

SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Kuna mtu anaomba musaidie anauliza: Yeye  hakujaliwa kusoma utotoni mwake,  sasa ndio anasoma, Je  akipata ada yake ya hedhi aendelee kusoma tu? maana bado yuko kwenye alifu huko ?

JAWABU 

 ➡ Mwanamke mwenye hedhi au nifasi,  na pia mwanaume au mwanamke  mwenye janaba,  hao wote hawaruhusiwi kusoma qurani wakiwa katika hali ya kukosa twahara mpaka wat’ahirike.

 ➡ Na hii ndio Kauli yenye nguvu zaidi katika Kauli zote zilizotajwa katika suala hili.

 ➡ Lakini ikhtilafu ipo katika kuhusu mwanamke mwenye hedhi au nifasi,  ambapo Kauli za maulamaa wa madhehebu za ahli sunna wengi wao wanaona kuwa inafaa kusoma qurani katika hali hizo mbili za hedhi na nifasi,  japokuwa wametofautiana katika masharti ya kujuzu huko.

➡ Amma katika madhehebu ya ibaadhi ni kuwa : ” Ni haramu kwa mwenye janaba au hedhi au nifasi kusoma qurani “

 ➡ Na katika fatwa za sheikh Swaaleh bin fauzaan al fauzaan,  Amenukuu kuwa kauli ya maulamaa wengi ni kuwa inaharamika kusoma qurani kwa wenye hali hizo.

Japokuwa yeye ametoa Ruhsa ya kujuzu kuisoma katika hali ya dharura kama akiwa mwanamke huyo mwenye hedhi au nifasi ni mwanafunzi,  na anatakiwa kufanya mtihani wa qurani.

 ➡ Na katika madhehebu ya ibaadhi inajuzu kwa dharura tu kwa kiasi cha dharura hiyo,  kama akiwa ana hali ya wasiwasi au khofu ya kitu fulani.

 ➡ Amma katika suala la kusoma zile herufi za kujifunza kuunganisha maneno ya kiarabu tu,  kama alif –  baa –  taa n.k hizo haziitwi qurani,  kwa sababu ni herufi ambazo ziko mbalimbali na wala hazileti maana mpaka ziunganishwe na kusomeka kama aya kamili.

 ➡ Kwa hiyo hizo anaweza kuzisoma wakati wowote bila kizuizi Inshaallaah taalaa.

 ➡ Isipokuwa zikiwa zimo katika juzuu amma kwa mfano,  na juzuu amma hiyo ina sura kamili ambazo zinahesabika kuwa ni Qur’ani,  hapo anatakiwa asisome hizo herufi kwa kukamata juzuu , kwa kulinda utukufu wa qurani.

 ➡ Japokuwa wako maulamaa wanaona kuwa ikiwa Qur’ani ni nyingi zaidi kuliko kisichokuwa  qurani ndio inazuiliwa kuikamata,  amma ikiwa yaliyokuwa si qurani ndio mengi zaidi kuliko qurani inafaa kukamata, yaani kama Kauli kuhusu kusoma Tafsiri ya Qur’ani kwa kukamata kwa aliekuwa hana twahara,  ikiwa tafsiri hiyo imekusanya baadhi ya sura za qurani.

 ➡NAMUOMBA ALLAAH ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA.

 ALLAAHU AALAMU.

Sh.Shaabani Al -Bataashi

Published By Said Al Habsy

SWALI

Kwa kuongezea Je wale ahlu kitabu wa zama za Nabii Issa pia wao hawataingia peponi? maana wao waliamini na kumfuata Nabii Issa

JAWABU

➡ Subhaana LLAAH :

Ndugu zangu jawabu hizi ziko wazi sijui pahala gani panaposhindwa kufahamika kwa baadhi ya ndugu zetu.

➡ Hatujakataa kuwepo watu wa kitabu ambao wana imani ya kuamini sahihi,  kwa sababu Qur’ani imewataja wazi kabisa bayana,  aliposema ALLAAH S.W :

(لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ)

[Surat Aal-E-Imran 113]

(يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ)

[Surat Aal-E-Imran 114]

Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanakimbilia katika mambo ya kheri. Na hao ndio miongoni mwa watenda mema.

➡ Hao wenye sifa hizo ziliizotajwa katika aya hizo na mfano wake ikiwa wapo katika zama zetu kwa Sifa hizo hakuna anaekanusha kuwa watapata malipo mazuri kwa mola wao.

➡ Na wale waliomuamini Nabii Isa a.s,  hata wakaitwa kuwa ni :

Al hawaariyyiin “

“الحواريين”

Hao walikuwa ni wakweli katika Imani zao,  na wasafi katika nyoyo zao,  na waliinusuru dini ya ALLAAH S.W.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ)

[Surat Al-Maeda 111]

Na nilipo wafunulia Wanafunzi – yaani wa Nabii isa a.s , kwamba waniamini Mimi na Mtume wangu, wakasema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu.

➡ Hao hakuna shaka katika kuwa ni katika wema kwa mujibu wa qurani,  na hata mwisho wa aya imetaja kuwa ni waisilamu.

➡ Kwa hiyo  hii ni sifa wanayo baadhi ya watu wa kitabu wana sifa kama hizo,  na kwa hiyo wanakuwa ni katika miongoni mwa waumini na waisilamu.

➡ Tatizo ni ufahamu mbaya wa baadhi watu na kudai kuwa watu wa  kitabu wote ni wote wa pempmbeni.

➡ Na masharti yako wazi katika aya zote nilizozitaja katika jaawabu.

➡ YAA ALLAH TUFAHAMISHE  YALIYO NA KHERI NA TONGOZE KWA KUYANYIA KAZI.

➡ ALLAAHU AALAMU.

Sh.Shaabani Al -Bataashi

Published By Said Al Habsy

SWALI

Nimepewa pesa za zakaa inafika mwezi sasa ila sijazituma nimependa nije mwenyewe zanzibar nizitowe na mimi nina nia ya kuja mwezi wa kwanza. Je inajuzu hizo pesa niwe nazo mimi mpaka nikija huko au haijuzu?

 

JAWABU

 

➡ Zaka ni moja katika nguzo kuu tano ambazo uisilamu umejengeka juu ya nguzo hizo.

➡ Na zaka ya mali na mazao ya chakula na wanyama,  ina masharti yake na viwango vyake maalumu vimewekwa na Sheria za dini yetu.

➡ Na ni lazima kuitekeleza zaka hiyo kwa kuwapa wanao stahiki katika muda uliopangwa na sheria bila kuchelewesha.

➡ Amesema ALLAAHU S.W katika zaka ya nafaka  :

(وَهُوَ الَّذِي أَنْشَأَ جَنَّاتٍ مَعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِنْ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ)

[Surat Al-Anaam 141]

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

➡ Ameamrisha kutoa haki ya zaka ya mazao siku ya kuvuna , na hii inaonyesha umuhimu wa kuwahisha kutoa haki hiyo bila ya kuchelewesha.

➡ Ikiwa aliekupa zaka hiyo uilete zanzibar amekuwakilisha wewe uilete mwenyewe na kusimamia ugawaji wake,  basi inakulazimu wewe mwenyewe ndie uisimamie kama mulivyokubaliana.

➡ Na katika hali hii,

Ikiwa utachelelewa kuja kwa dharura ya kuandaa safari yako kwa muda wa kiasi hicho,  Inshaallaah hakuna tatizo katika hilo.

➡ Lakini pia ni lazima umjulishe mtoaji zaka wa asili aliekutuma wewe kuwa utachelelewa kusafiri hadi siku hiyo uliyoikusudia.

➡ Pia inakulazimu kuandika wasia / maelezo kuhusu amana za watu ulizonazo,  kwa sababu binaadamu hufikwa  na umauti wakati wowote na pahala popote.

➡ Na wako baadhi ya maulamaa wanaruhusu kuchelewa hata mwezi mmoja tu baada ya kuingia muda wa kuwajibika kutoa zaka,  na wako walioruhusu hata muda zaidi ya huo,  midhali hakuchelewa mpaka kuingia mwaka wa pili.

➡ Na asili ya zaka inatakiwa kutolewa kwa kuwapa wanaostahiki zaka,  miongoni mwa wakaazi wa nchi au mji anaoishi mtoaji zaka huyo mwenyewe.

➡ Na wala haihamishwi zaka kutoka mji kwenda mji mwingine ila ikiwa watu wa mji wa mwanzo wametosheka na hawahitajii kupewa zaka tena.

➡ Au ikawa watoaji zaka hatika mji ni wengi,  na itakuwa kuna mali nyingi ambazo zitazidi katika mji huo,  na wakati mji mwingine unahitajia zaidi zaka.

➡ Na ni vizuri zaidi kwa mwenye kutaka kutoa zaka atoe mwenyewe bila kumuakilisha mtu,  ili kupata ladha ya kutekeleza nguzo hiyo,  na kupata mazingatio kwa kuona hali za masikini anaowapa zaka hiyo.

➡ Na Ikithibiti kuwa zaka hiyo imegaiwa kupewa wasiostahiki zaka,  itamlazimu mtoaji zaka kurejea kutoa upya tena,

Kwa sababu atakuwa hakufikisha wajibu katika pahala pake husika.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUPE TAWFIQ KATIKA KUTEKELEZA AMRI ZAKE,  NA KUSIMAMIA AMANA TULIZOPEWA.

Published By Said Al Habsy

SWALI

Ust: Shaaban Al-batwashi: Kama nimekuelewa vizuri, umekataa kwamba: Ahlu kitabi hawataingia peponi ktk hali ya Umum , je! Hizo aya zinazowataja Ahlu kitabi walioamini , au wale waaminifu nk . zinawataja hivo mwisho wao jazaa yao itakuwa nini?

JAWABU

➡ Ndugu yangu alueuliza suala hili mara nyingine tena inawezekana jawabu hakuisoma kwa utulivu hadi mwisho.

➡ Katika jawabu yangu nimetaja masharti ya kufaulu katika hesabu ya akhera kwa uwazi,  ambayo ni :

1- Imani sahihi.

2 – Matendo mema.

➡ Sasa hao watu wa kitabu kwanza katika zama zetu hizi hakuna tena wenye sifa ya kustahiki wasfu huo,  na wala hakuna kitabu sahihi wanachokifuata wao kwa sasa kikawa sawasawa kama kilivyokuwa zama za mtume wao.

➡ Amesema ALLAAHU S.W kuhusu ubadilishaji wao wa sheria katika maneno ya ALLAAH katika vitabu vyao :

(أَفَتَطْمَعُونَ أَنْ يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِنْ بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ)

[Surat Al-Baqara 75]

Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua?

➡ Na akasema pia :

(مِنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَنْ مَوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَاسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَاعِنَا لَيًّا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِي الدِّينِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَاسْمَعْ وَانْظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَٰكِنْ لَعَنَهُمُ اللَّهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا)

[Surat An-Nisa 46]

Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na husema: “Raai’naa”, kwa kuzipotoa ndimi zao ili kuitukana Dini. Na lau kama wangeli sema: Tumesikia na tumet’ii, na usikie na “Undhurna” (Utuangalie), ingeli kuwa ni kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini ila wachache tu.

➡ Pia akasema :

(وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا ۖ وَقَالَ اللَّهُ إِنِّي مَعَكُمْ ۖ لَئِنْ أَقَمْتُمُ الصَّلَاةَ وَآتَيْتُمُ الزَّكَاةَ وَآمَنْتُمْ بِرُسُلِي وَعَزَّرْتُمُوهُمْ وَأَقْرَضْتُمُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا لَأُكَفِّرَنَّ عَنْكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَلَأُدْخِلَنَّكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ فَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ مِنْكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ)

[Surat Al-Maeda 12]

Na Mwenyezi Mungu alifanya agano na Wana wa Israili. Na tukawateulia kutokana nao wakuu kumi na mbili. Na Mwenyezi Mungu akasema: Kwa yakini Mimi ni pamoja nanyi. Mkisali, na mkatoa Zaka, na mkawaamini Mitume wangu, na mkawasaidia, na mkamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, hapana shaka nitakufutieni maovu yenu na nitakuingizeni katika mabustani yapitayo mito kati yake. Lakini atakaye kufuru miongoni mwenu baada ya hayo bila ya shaka atakuwa amepotea njia iliyo sawa.

(فَبِمَا نَقْضِهِمْ مِيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَنْ مَوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ)

[Surat Al-Maeda 13]

Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

➡ Aya zote hizo ziko wazi kuonyesha hali zao watu wa kitabu , na juu ya hayo hazikusema kuwa watu wa kitabu wote ni makafiri au waovu,  Laaa;  bali zimetaja baadhi yao.

➡ Na katika jawabu yangu sikusema kuwa watu wa kitabu wote hawatopata malipo, ,  abadan. ..

Ni kama aya za qurani ziluvyotaja hali zao hao watu wa kitabu,  na kila mwenye kutimiza sharti la Imani sahihi na amali njema na kufuata sheria ya KIISILAMU,  huyo atakuwa ni katika kundi la waisilamu.

➡ Inshaallaah soma jawabu kwa utulivu unazidi kufahamu bi idhini llaah taalaa.

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUFUNGULIE MILANGO YA ELIMU NA HIKMA.

ALLAAHU AALAMU.

SH.Shaaban Al Bataashi

Published By Said Al Habsy

SWALI

Mume akimuambia mumewe kuwa: “Ukitoka tu kwenda kwa fulani hiyo ndio talaka yako ” au ukinyanyua tu mguu kutoka kwenda kwa fulani ndio talaka yako ” Je hiyo inakuwa ni talaka?

JAWABU 

➡ Talaka ndugu zangu ni moja katika mambo ambayo yameruhusika kisheria panapolazimu kufanya hivyo.

➡ Na wala haipendezi kwa mume kuwa ni mwenye kumtishia mkewe kwa talaka kila mara kwa sababu ya ikhtilafu ndogo ndogo tu katika maisha yao.

➡ Na Talaka ina vigawanyo vingi katika aina zake.

 

➡ Miongoni mwa aina hizo ni talaka ya iliyoning’inizwa,  kwa lugha ya kiarabu inaitwa ” Al ttwalaaq l muallaq ” “الطلاق المعلق “

➡ Na hii inakuwa kama ifuatavyo :

“Ni mume kumuambia mkewe : ukifanya siku fulani ndio talaka yako “

“Au Ikitokea kadhaa hiyo ndio talaka yako “

➡ Hiyo ni aina ya talaka ambayo imefungamanishwa na sharti maalumu kwa wakati ujao.

➡ Na hukmu yake ni kuwa :

” itahesabika kuwa ni talaka mara tu ikitimia sharti lililotajwa katika maneno ya mume.

➡ Mfano :

Akisema mume kumuambia mkewe : ukiingia nyumba ya mama  yako hiyo ndio talaka yako “

Ikitokea siku yoyote mke akiingia nyumba hiyo kuanzia hapo alipoingia tu itahesabika tayari mke ameachika.

➡ Na idadi ya talaka itakuwa ni moja kama ametamka kuwa ni moja.

➡ Na kama hakutaja idadi ya talaka pia itahesabika ni moja,  kwa kuwa asili asili ya talaka huwa ni moja.

➡ Na ikiwa atamuambia:

Kila  ukienda kwa mama yako ndio talaka yako “

Itakuwa idadi ya talaka ni kwa mujibu wa mara alizotoka kwenda kwa mama yake.

Na ikitimia kwenda kwake mara tatu, itakuwa mume amekwishamaliza nafasi tena ya kuendelea kuishi na mkewe,  kwa sababu hakuna kumrejea tena baada ya Talaka tatu.

➡ Na jambo hili halina ikhtilafu yoyote katika madhehebu za kiisilaamu.

➡ Kwa nini mume anakuwa hana subra wala uvumilivu mpaka inafikia kuitundika ndoa yake na ikabaki kuwa inasubiri tu kutokea jambo fulani na ikatike ndoa hiyo? ?

➡ Na kwa nini mke anafanya mambo ambayo yatamsabibishia mume kufanya kama hivyo? ??

➡Hayo ndio malipo ya wenye kuchezea sheria za ALLAAH S.W  na kushindwa kuiheshimu mipaka ya dini,  na kutothamini ndoa kati yao,  ambayo ALLAAH S.W ameiita kuwa ni ahadi nzito.

➡ Na ninakumbusha kuwa : ”  Talaka kama hii inakuwa haifutiki kwa sababu ya kupita muda fulani,  au mume Kubadili maamuzi katika sharti alilokuwa amelitoa mwanzo.

➡ Mathalan akamwambia mkewe : “basi mke wangu,  ile talaka nimeshaifuta tena hakuna tatizo nenda tu “

Bado kule kusamehe kwake kutakuwa hakubadilishi sharti la talaka hiyo.

➡ Innaa lillaahi wa Innaa ilaihi raajiuun,  hakika huu ni msiba umeingia katika umma wa kiisilaamu kama ikuvyokuwa zama za ujinga.

➡ Kwa mwenye kufanya hivyo basi anatakiwa kumrejea mkewe ikiwa atataka kumrejea,  na itakuwa talaka imeshahesabika moja katika hali hiyo.

➡ Na katika kumrejea ni sharti ashuhudishe mashahidi wawili kuwa amemrejea mkewe,  na hii ndio Kauli ya maulamaa wa madhehebu ya Ibaadhi,  na ni rai katika madhehebu ya imamu Ahmad bin hanbal r.a.

➡ Amma maulamaa wengine wa madhehebu za ahli sunna,  wao wanaona kuwa si sharti kushuhudisha mashahidi katika kumrejea.

➡ REJEA VITABU VIFUAVYO :

1- Fataawa shaikhinaa alkhaliily.

2 – Al mulakhasw l fiqhy cha shaikhinaa Swaaleh bin fauzaan al fauzaan

3 – Fataawa l mar’ati l muslimah,  cha fatawa za maulamaa wakubwa wanane katika maulamaa wa Makka na wengine

4 – Al fiqhu shaamil cha

sh Saalim bin said Al buusaidy.

Na vingine vingi tu miongoni mwa vitabu vinavyotegemewa katika ulimwengu wa kiisilaamu.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUNUSURU NA HAYA NA MFANO WAKE,  NA ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA.

ALLAAHU AALAMU.

Sh. Shaaban Al Baatashi

Published By Said Al Habsy

SWALI

Nini hukmu ya sadaka anayotoa mtu mwenye kampuni ya pombe?

JAWABU 

➡ Sadaka ni :

” Muisilamu kutoa sehemu katika mali yake,  kuwapa wanao stahiki miongoni mwa mafakiri na masikini,  kwa kutaka Radhi za ALLAAH S.W “

➡ Na sadaka ni ibada miongoni mwa ibada katika uisilamu,  ni lazima mwenye kutoa atoe kwa nia na kufanya ikhlaasw katika kutoa huko.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ)

[Surat Al-Bayyina 5]

Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.

➡ Na amesema ALLAAH s.w kuwasifu waja wema wenye kutoa na kulisha kwa ajili yake :

(وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا)

[Surat Al-Insan 8]

Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.

(إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنْكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا)

[Surat Al-Insan 9]

Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.

(إِنَّا نَخَافُ مِنْ رَبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا)

[Surat Al-Insan 10]

Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu.

➡ Subhaana LLAAH :

Hao ni waja wa ALLAAH S.W,  wametoa mali zao za halali,  tena katika njia za halali,  tena  kwa kuwapa wanao stahiki kupewa,  na juu ya kufanya hivyo bado wanatoa kwa kuwa wanaogopa uzito wa siku hiyo ya malipo!

Huyu mwenye kampuni ya pombe anafañya biashara ya haramu,  na anatoa haramu,  eti kwa nia nzuri!  Vipi iwe nia nzuri katika aliyoharamisha ALLAAH S.W? ?

➡ALLAAHU S.W hakubali amali mbaya ya mja,  wala sadaka ya haramu haikubaliki na wala haina malipo yoyote akhera.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنْفِقُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنْفِقُونَ وَلَسْتُمْ بِآخِذِيهِ إِلَّا أَنْ تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ)

[Surat Al-Baqara 267]

Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

➡ Na bila shaka pombe si katika vizuri vilivyochumwa katika chuma la mja.

➡ Bali pombe ni katika njia za shetani,  na imeharamishwa na ALLAAH S.W katika QURANI,  pia katika sunna na makubaliano ya maulamaa wote bila ikhtilafu yoyote.

➡ Na katika hadithi ya mtume s.a.w anasema :

أيها الناسُ ! إنَّ اللهَ طيِّبٌ لا يقبلُ إلا طيِّبًا . وإنَّ اللهَ أمر المؤمنين بما أمر به المرسلين . فقال : يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ . [ 23 / المؤمنون / الآية 51 ] وقال : يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ [ 2 / البقرة / الآية 172 ] . ثم ذكر الرجلَ يطيلُ السَّفرَ . أشعثَ أغبَرَ . يمدُّ يدَيه إلى السماءِ . يا ربِّ ! يا ربِّ ! ومطعمُه حرامٌ ، ومشربُه حرامٌ ، وملبَسُه حرامٌ ، وغُذِيَ بالحرام . فأَنَّى يُستجابُ لذلك ؟

الراوي: أبو هريرة المحدث: مسلم  – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 1015

خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡Maana ya hadithi ni :

“Hakika ALLAAH ni mzuri na hakubali ila yaliyo mazuri,  na hakika ALLAAH S.W amewaamrisha waumini yale ambayo amewaamrisha mitume,

Akasema ALLAAH S.W :

” Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda”.

Na akasema :

Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.

Kisha mtume s.a.w akamtaja mtu mmoja ambae,  amekwenda safari ndefu,  amekuwa na nywele timu timu kwa mavumbi,  ananyanyua mikono yake upande wa mbinguni na kusema :

Yaa Rabbi – yaa Rabbi,

Na chakula chake cha haramu,  na kinywaji chake cha haramu,  na kivazi chake cha haramu,  na amekulia kwa kula haramu,  vipi atakubaliwa mtu huyo?

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATURUZUKU VYA HALALI,  NA TUWEZE KUVITOA KATIKA NJIA ZA HALALI.

ALLAAHU AALAMU.

SH. Shaabani Al Bataashi

Published By Said Al Habsy

SWALI

Je madereva kulingana na kazi zao, wao Kila siku husafiri Je,  wanaudhuru wa kutokufunga saumu ya Ramadhani  ?

Na vipi pia  kuhusu swala zake, hukum ya swala ya msafir inaswih kwake kupunguza rakaa??

JAWABU 

 

➡ Uisilamu ni dini ya wepesi katika sheria zake,  na wala hakuna kulazimishana katika dini.

➡ Ibada kama saumu kisheria ikiwa mtu yuko safarini,  na kazi yake ni hiyo,  na safari yake ni ndefu na Inafikia kiwango cha kuzingatiwa kuwa ni safari,  anawajibikiwa Dereva huyo kuswali sala ya msafiri.

➡ Na sala ya safari ni :

Kuswali kwa kupunguza Rakaa za sala zote zenye Rakaa nne nne na kuziswali Rakaa mbili mbili.

➡ Na jambo hili la kupunguza Rakaa kwa msafiri ni lazima kwa kila msafiri,  na hii ndio Kauli sahihi ya jamhuri ya maulamaa,  ila katika baadhi ya maulamaa wengine wao wanaona kuwa ni sunna ya khiyari,  Mwenye kutaka apunguze na mwenye kutaka aswali kamili aswali.

➡ Isipokuwa katika hali moja hii haruhusiwi kupunguza Rakaa,  nayo ni :

Ikiwa  ataswali nyuma ya imaamu ambae yeye ni mkaazi pahala hapo,  hapo ni lazima amfuate imamu kwa kuwa sala yake inafungamana na sala ya imaamu.

➡ Kwa hiyo Dereva huyo mfano anaondoka Dar wakati adhuhuri imeshaingia muda wake,  basi anaweza kuswali adhuhuri hapo Dar rakaa mbili,  kisha anatoa salaam,  kisha anakimu sala tena na kuswali alasiri rakaa mbili.

➡ Au anaweza kuswalia njiani pia sala zote mbili katika muda wa alasiri.

➡ Kwa sababu :

Msafiri inajuzu kwake kutanguliza sala ya alasiri katika wakati wa alasiri kwa kuchanganya na adhuhuri,  na inajuzu pia inajuzu kuchelewesha adhuhuri na kuiswali katika muda wa alasiri kwa kuichanganya pia.

➡ Na kuhusu saumu ya Ramadhani ikiwa ni vigumu kwake kufunga safarini inajuzu kuacha kufunga katika siku ambazo atakuwa safarini,  kisha atakuja kulipa siku nyingine atakapokuwa ametulia.

Lakini akiweza kufunga bila mashaka yoyote basi kufunga kwake ni bora zaidi.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(فَمَنْ خَافَ مِنْ مُوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ)

[Surat Al-Baqara 182]

(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.

➡ Hii ndio rehma ya ALLAAH S.W kwa waja wake katika sheria hakuwafanyia ugumu.

➡ Wa l hamdu lillaahi Rabbi l aalamiin.

➡ NAMUOMBA ALLAAH AWAHIFADHI WASAFIRI WOTE,  NA AWAPONYE WAGONJWA WETU.

ALLAAHU AALAMU.

Sh. Shaabani Al Bataashi

Published By Said Al Habsy

SWALI

Amesema ALLAAHU S.W :

[10/1,  2: {إِنَّ الَّذِينَ آمَنُواْ وَالَّذِينَ هَادُواْ وَالنَّصَارَى وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحاً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ }البقرة62

 Masheikh kuna mtu anataka kupotosha watu kupitia aya hiyo ya kwamba hadi wakristo na mayahudi wanaofanya mema wataingia peponi.

 JAWABU

➡ Qur’ani ni kitabu ambacho kinaongoza katika njia ya haki iliyo sawa.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(إِنَّ هَٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا)

[Surat Al-Isra 9]

 

Hakika hii Qur’ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa.

➡ Sasa Hebu tazama aya hiyo iliyotangulia hapo juu

Published By Said Al Habsy

SWALI LA 893 :mimi nilikua nimefunga Saumu hadi  siku ya 6,siku ya 7 niliamka na saumu mpaka mchana ndio nikapata dharura  ya kufungua.

SWALI

mimi nilikua nimefunga Saumu hadi  siku ya 6,siku ya 7 niliamka na saumu mpaka mchana ndio nikapata dharura  ya kufungua.

sasa  nikitaka kulipa nitalipa hiyo siku moja tu au ni zote ambazo sikukamilisha?

 JAWABU 

➡ Saumu muda wake ni kuanzia kuingia kwa Alfajiri ya kweli na inamalizika kwa kuzama jua jioni upande wa magharibi.

➡ Na mwanamke akiwa katika ada yake ya mwezi,  yaani hedhi,  au akiwa katika nifasi,  haruhusiwi kufunga saumu ya aina yoyote ile,  ikiwa ni saumu ya Faradhi au sunna.

➡ Na ikiwa imetokea hali kama hiyo mchana wakati yeye amefunga,  saumu yake itakuwa imeharibika hapo hapo baada tu ya kutokea udhuru huo.

➡ Kwa hiyo baada ya kumaliza mwanamke huyo ada yake,  atajitwaharisha kamili na kuanza kufunga saumu yake kwa kuendeleza idadi ambayo wameifikia watu wafungao ikiwa bado siku zinaruhusu kufunga na waliotangulia.

➡ Kisha baada ya kumaliza mwezi wa Ramadhani na sikukuu yake,  atatakiwa kulipa saumu zile tu ambazo alifungua kutokana na dharura hiyo.

➡ Kwa hiyo atalipa tu idadi ambayo anadaiwa kwa kuwa hakuzifunga.

➡ Na hukmu hiyo pia inakuwa hata kwa mgonjwa ambae hakuweza kufunga saumu ya Ramadhani,  anatakiwa kulipa masiku anayodaiwa wakati wa kuumwa kwake.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ ۚ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَنْ تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ ۚ وَأَنْ تَصُومُوا خَيْرٌ لَكُمْ ۖ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ)

[Surat Al-Baqara 184]

(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUWEZESHE KUFUNGA NA KUTEKELEZA IBADA ZAKE.

ALLAAHU AALAMU.

Sh. Shaabani Al Bataashi

Published By Said Al Habsy

SWALI

Nauliza hivi ustadh kwa upande wa dini hii ni ya ukweli na dini yetu. Inatufundisha vipi kuhusu jimai kwa wiki tunatakiwa tufanye ?

JAWABU 

➡ Suala la maingiliano ya kindoa kati ya mume na mke  ni suala ambalo limebainishwa katika qurani na sunna na Kauli za maulamaa wa kiisilaamu.

➡ Kwa kuwa sheria za dini ya kiisilaamu hazina kumpa uzito mja  wala ugumu ndani yake,  ALLAAH S.W hakuweka idadi maalumu ya kuingiliana kati ya mume na mke kwa wiki iwe mara ngapi.

➡ Na kama ingelikuwa  imewekwa  idadi maalumu,  basi kuna watu wangefanya makosa katika hilo,  imma kwa kupitiliza kuliko idadi iliyopangwa,  au kwa kupuguza chini ya kiwango kiwango kilichowekwa.

➡ Na ingekuwa kuna ugumu katika kutekeleza sheria katika hili kama lingekuwa hivyo.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(وَجَاهِدُوا فِي اللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِنْ قَبْلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ)

[Surat Al-Hajj 78]

Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur’ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa.

➡ Kwa hiyo jambo hili linarudi katika makubaliano ya mume na mke wenyewe,  kwa mujibu wa makubaliano kati yao,  na uwezo wa kila mmoja,  muhimu ni kufanya mambo kati na kati bila ya kuvuka mipaka katika kiwango.

➡ Kupanga idadi ya kuingiliana kati ya mume na mke ni kuleta ugumu katika dini.

➡ Na suala hili haudhibitiki kwa idadi kwa kila mmoja,  kwa kuwa watu wanatofautiana katika uwezo wa kufanya tendo hilo kwa waume na wake pia.

➡ Lakini ziko baadhi ya kauli za maulamaa zinaonyesha kuwa :

” Jimai ambayo inakuwa ni wajibu kwa mume kumuingilia mkewe inakuwa ni mara mara mbili katika wiki “

Na wengine wakasema :  Ni mara moja katika wiki.

➡ Na wako waliosema kuwa :

” ni mara moja katika kila mwezi baada ya kutwaharika mwanamke kutokana na hedhi “

 

Kwa maana ya undani wa Kauli ya ALLAAH S.W isemayo :

(وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ)

[Surat Al-Baqara 222]

Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat’ahirike. Wakisha t’ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.

➡ Lakini suala hili pia ni muhimu kupata ushauri wa Daktari mwenye ujuzi,  ikiwa kuna madhara yanamsibu mmoja kati ya wanandoa wawili kutokanana jimai.

➡ Hili ni kwa sababu :

1. Kuna baadhi ya wanaume wamepewa nguvu zaidi za jimai ikawa wanasababisha madhara kwa wake zao kwa sababuya kuwaingilia sana mara kwa mara.

2. Na wako waliojaaliwa maumbile makubwa sana,  ima kwa unene au urefu,  pia ikawa na athari kwa wake zao.

3. Na wengine kinyume cha hayo,  wana maumbile mafupi sana yakawa hayawafikishi wake zao katika kilele cha utamu wa kuingiliwa.

4. Na wengine hufikwa na maradhi ya kukosa hisia na hamu ya tendo la ndoa kabisa, ikawa pia ni madhara kwa upande mwingine.

➡ Muhimu suala hili ni kwa mujibu wa wanandoa wenyewe,  al muhimu wasivuke mipaka tu na kusababishiana madhara.

➡ Na kufanya jimai sana kunaleta baadhi ya madhara,  na hasa akifikia mtu katika umri wa uzee,  na miongoni mwa hayo ni kupinda mgongo,  na kukosa nguvu za miguu na hasa magotini.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUHIFADHI NA ATUPE AFYA NJEMA.

ALLAAHU AALAMU.

Sh. Shaabani Al Bataashi

Published By Said Al Habsy

SWALI
KUNA MTU KANIPA OMR 500 KASEMA WEKA KTK MASJID,NA HAPO KWENYE MSIKITI TUMEWEZA KUMALIZA TAYARI, LAKINI PEMBENI MWAKE PANA MADARASA HAIJAMALIZIKA.

JE TUNAWEZA KUCHUKUA PESA HIZO ILI  KUMALIZIA HIYO MADARASA AU LAZIMA TUMUARIFU ALIYETOA ???

JAWABU

➡ Muamala huu ndio ambao unaitwa katika sheria kuwa ni : ” Wakfu ” lakini kutoa pesa tu kwa ajili ya msikiti inakuwa si katika  maana sahihi ya wakfu.

➡ Yaani  wakfu unaokusudiwa katika maana sahihi ni: 
” Kuweka asili ya mali kwa kuifunganisha kwa ajili ya manufaa maalumu,  kwa pahala maalumu au watu maalumu  , kwa kutaka Radhi za ALLAAH S.W “

➡ Japokuwa asili ya wakfu ni kuweka asili ya mali,  kama vile : 

Nyumba – shamba – duka  na mfano wake,  lakini pia ikiwa mtu atatoa kitu ambacho ni manufaa yenye kuendelea, pamoja na kubakia asili ya mali katika milki ya ALLAAH S.W. 

➡ Kwa hiyo katika suali hili,  naona alietoa pesa hizo hakuweka wazi makusudio ya pesa hizo alizozitoa kuwa zifanyiwe nini katika msikiti?

➡Na  Ikiwa amekusudia kuwa pesa hizo zishughulikie msikiti na huduma za msikiti huo,  katika hali hii haifai kuhamisha pesa hizo kwa kufanyia kazi nyingine zisizokuwa za msikiti huo. 

➡ Amma ingelikuwa kazi inayotaka kufanyika badala ya msikiti ni kazi ambayo inahusika moja kwa moja na msikiti wenyewe,  kama kumlipa mshahara mwalimu anaesomesha katika msikiti, au kununua vitabu kwa ajili ya msikiti,  Naam katika hali hiyo inajuzu kutumia mali hiyo kwa kazi nyingine, ikiwa kuna dharura iliyokuwa muhimu kuliko lengo la asili lililowekewa mali hiyo. 

Na fatwa kama hii katika suala la wakfu,  nimeikuta katika fatwa za imaamu al ssaalimy r.a. 

➡ Pia kwa mfano ingekuwa mali imewekwa wakfu kwa ajili ya sanda ya kuzikia maiti wa kiisilaamu sehemu fulani,  lakini ikawa mahitaji ya sanda tena yameshatimia na kuzidi,  kiasi ambacho hawahitajii tena kwa muda huo sanda nyingine,  na pesa zake zimebakia bila kazi ya wakati huo,  katika fatwa ya samaahati shaikhinaa alkhaliily  kitabu cha nne ukurasa wa 303 anasema : 
” Ikiwa imeshindikana kutekeleza wakfu katika njia iliyotolewa katika muqtadha wa wakfu,  Hakuna kizuizi katika kutumia wakfu katika kuchimbia makaburi mfano,  kwa sababu katika kila hali mbili hizi kunapatikana kusitiri maiti…”

➡ Kwa maana hiyo inaonekana pesa hizo ni sadaka tu ya msikiti huo,  na sio wakfu,  kwa sababu wakfu unakuwa kwa kuweka asili ya mali kwa ajili ya manufaa yenye kuendelea. 

➡ Kwa suali hili nashauri kwanza : 
1 –  Mwenye kutoa pesa hizo afahamishwe mambo  muhimu yanayohitaji kuchangiwa msaada wa mali, ili kukubaliana kuweka mali hiyo pahala panapostahiki,  na hasa ikiwa madrasa hiyo ikiwa katika msikiti huo. 

2 – la pili ni kuwa : 
Suala hili lirejeshwe kwa Mufti au mmoja katika wanazuoni wa mji ambao muko huko,  ili kupata fatwa kwa mujibu wa hali ilivyo. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI
Kama kuna mtu nimemsaidia kwa kupata kazi au kupata kitu chochote ambacho kitamuingizia pesa, Kisha akanipa zawadi ya pesa. Je hiyo pesa aliyonizawadia inafaa kuichukua? .
 
JAWABU

➡ Kusaidia mtu katika jambo lolote la kheri, au kumuondoshea lenye shari, ni katika mambo ambayo uisilamu umehimiza sana. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(… ۘ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ)

Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
[Surat Al-Maeda 2]

➡Na ukimsaidia mwenye shida bila kuchukua malipo kwake hivyo ni bora zaidi .
➡ Na amesema mtume s.a.w : 
من نفَّسَ عن مؤمنٍ كُربةً من كُرَبِ الدنيا ، نفَّسَ اللهُ عنه كُربةً من كُرَبِ يومِ القيامةِ . ومن يسّرَ على معسرٍ ، يسّرَ اللهُ عليه في الدنيا والآخرةِ .
ومن سترَ مسلمًا ، ستره اللهُ في الدنيا والآخرةِ . 
واللهُ في عونِ العبدِ ما كان العبدُ في عونِ أخيه…
الراوي: أبو هريرة المحدث: مسلم – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 2699
خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Amesema s.a.w katika hadithi hiyo kuwa : 
” Mwenye kumuondoshea muisilamu shida miongoni mwa shida za duniani, Allaahu atamuondoshea shida miongoni mwa shida za siku ya qiyaama , 
Na na mwenye kumfanyia wepesi mwenye uzito , ALLAAH S.W humfanyia nae wepesi katika dunia na Akhera, 
Na mwenye kumstiri muisilamu , basi ALLAAH atamsitiri duniani na akhera, 
Na ALLAAH huwa katika kumsaidia mja midhali mja huyo yuko katika kumsaidia ndugu yake – muisilamu – mwenzake. 

➡ Lakini hii haina maana kupokea zawadi kutoka kwa uliemsaidia haifai. …

Hapana :
“Ikiwa mtu uliemsaidia ameamua mwenyewe kukupa zawadi ya kitu chochote, unaruhusika kuchukua, midhali kitu hicho kinafaa kuwa zawadi “

➡ Zawadi ambayo imekatazwa katika sunna kuichukua ni : ” Zawadi ambayo anaitoa mtu aliekopeshwa, kumpa aliemkopesha, baada ya kumpa mkopo wa pesa au mfano wake katika mali “

➡ Hiyo tu ndio imekatazwa katika sunna, kwa sababu kila mkopo ambao unavutia manufaa kwa mkopeshaji huwa ni haramu. 

➡ Lakini ikiwa wenye kukopeshana hao huwa wana kawaida ya kupeaana zawadi, na wala hawakuekeana sharti la kutoa zawadi kwa ajili ya mkopo, hapo hakuna tatizo katika kuchukua zawadi hiyo. 

➡ Kwa hiyo jawabu yako katika suala hili ni kuwa : 
” inafaa kuchukua zawadi hiyo kutoka kwa huyo mtu uliemsaidia , midhali yeye mwenyewe amekupa kwa khiyari yake. 

➡ Bali hata kama angekuwa amekutuma umtafutie kazi fulani, na ikiwa utampatia kazi hiyo atakulipa kitu fulani, pia inajuzu kuchukua ujira huo atakaokupa, midhali kazi hiyo haikuwa na udanganyifu ndani yake.

Na hii wanaiita maulamaa wa fani ya fiqhi kuwa :
” ju’ulu ” au ” Jaalah” …

Kama ilivyokuja katika kisa cha nabii Yusufu a.s alipokuwa akitafuta kifaa cha Mfalme, na akaahidi zawadi kwa mwenye kukileta. 
Amesema ALLAAHU S.W : 
(قَالُوا نَفْقِدُ صُوَاعَ الْمَلِكِ وَلِمَنْ جَاءَ بِهِ حِمْلُ بَعِيرٍ وَأَنَا بِهِ زَعِيمٌ)
[Surat Yusuf 72]

Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na ataye lileta atapewa shehena nzima ya ngamia. Nami ni dhaamini wa hayo.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATURUZUKU HALALI, NA ATUWEZESHE KUMSHUKURU KWA NEEMA ZAKE. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

SWALI

Jee ikiwa mtu hana pa kukaa wala hana uwezo wa kujenga wala kukodi nyumba akitokea mtu au watu wakimjengea pa kukaa itakuwa ni Sadaka tu au Inaingia katika Sadakatun Jaariya?

 

JAWABU 

Neno swadakatun jaariya maana yake ni: ” Sadaka yenye kuendelea “

➡ Na sadaka ni :” Muisilamu kutoa sehemu katika mali yake bila ya kulipwa kitu mubadala kutoka kwa aliempa sadaka hiyo “

➡ Na sadaka katika uisilamu haina kiwango wala muda maalumu uliowekwa,  bali kila mtu ana khiyari ya kutoa awezacho kwa kadri ya alivyowezeshwa na ALLAAH S.W. 

➡ Na sadaka yenye kuendelea ni sadaka ambayo :

1- Manufaa yake ni yenye kudumu kwa muda mrefu zaidi bila ya kumalizika. 

2 – Sadaka ambayo manufaa yake yanafika kwa watu wengi zaidi katika kukidhi mahitaji yao ya lazima. 

➡ Na hadithi ya mtume s.a.w imetaja mifano ya sadaka zenye kuendelea kama alivyosema mtume s.a.w : 
إذا مات الإنسانُ انقطع عنه عملُه إلا من ثلاثةٍ : إلا من صدقةٍ جاريةٍ . أو علمٍ ينتفعُ به . أو ولدٍ صالحٍ يدعو له
الراوي: أبو هريرة المحدث: مسلم  – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 1631
خلاصة حكم المحدث: صحيح

Amepokea imamu muslimu,  kutoka kwa Abii huraira r.a amesema : 
Amesema mtume s.a.w : 
” Akifa mwanadamu,  amali zake hukatika isipokuwa kutokana na mambo matatu : 
Isipokuwa Kutokana na sadaka yenye kuendelea,  au elimu inayopatiwa manufaa,  au mtoto mwema anaewaombea dua “

➡ Kila jambo la kheri katika yenye kuafaidisha mtu au watu,  na lenye kudumu. 

➡ Mfano : 
Kujenga mashule.

Kujenga madrasa za Qurani. 

Kujenga misikiti. 

Kumjengea masikini nyumba na kadhalika mengine yaliyokuwa mfano wa hayo. 

➡ Kwa hiyo ikiwa ulimjengea mtu anaestahiki hiyo sadaka inafaa , na nyumba ni moja katika sadaka yenye kuendelea. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W AWAPE TAWFIQ KATIKA  KHERI

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI

Je Sadaqat Jaria inafaa pia kupewa mayatima kwa ajili ya mahitaji yao ?

JAWABU:

➡ Suala la sadaka katika uisilamu,  linakubalika katika njia yoyote miongoni mwa njia za halali na zenye kheri. 

➡ Na sadaka yenye kuendelea vinaingia katika maana hiyo vifungu vingi vya mambo ya kheri :

➡Miongoni mwa mambo hayo ni : 

1⃣Kutoa mali katika njia aina  zote za ALLAAH S.W,  kama ikilazimika kupigana jihadi kwa ajili ya kutetea uisilamu,  ikiwa uisilamu umedhalilishwa kiasi hata waisilamu wanashindwa kutekeleza ibada zao za lazima. 
Amesema ALLAAHU S.W : 
                          (أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ)
[Surat Al-Hajj 39]

Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa – na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia –

2⃣Kutoa mali kwa ajili ya kuokoa nafsi ya muisilamu mgonjwa ambae ameshindwa kupata uwezo wa  matibabu. 

Kuokoa nafsi moja ya muisilamu ni sawa na kuokoa na nafsi za watu wote.
Na mwenye kuua nafsi moja ni sawa na kuuwa nafsi za watu wote. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَنْ قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِنْهُمْ بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ)
[Surat Al-Maeda 32]

Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

3⃣Pia kusomesha mtu elimu yenye manufaa,  na yeye baada ya kusoma akasomesha wengine,  hiyo elimu itaendelea kuenea kwa watu kila sehemu,  na inakuwa elimu hiyo ni sadaka yenye kuendelea kwa kadri inavyozidi kuenea 
➡Na yatima ana haki zaidi ya kutazamwa katika yote hayo yalivyotajwa na mengine. 

➡ Na Zimekuja aya mbalimbali katika QURANI zinaonyesha ulazima wa kusimamia haki za yatima,  na kuwalisha na kuwatimizia mahitaji yao yote. 

➡ Na bila shaka malipo ya mwenye kufanya hayo kwa yatima ni makubwa sana,  kama ilivyokuja kutoka mtume s.a.w amesema : 
                                                                                                 – أنا و كافلُ اليتيمِ في الجنةِ هكذا و قال بإصبعيْهِ السبابةِ و الوسطى
الراوي: سهل بن سعد الساعدي المحدث: الألباني     – المصدر: صحيح الأدب المفرد – الصفحة أو الرقم: 101
خلاصة حكم المحدث: صحيح

” Mimi – yaani yeye mtume s.a.w – na mwenye kulea yatima,  tutakuwa pamoja katika pepo kama hivi;  akaashiria kwa vidole viwili kuwa – atakuwa karibu nae kama ukaribu wa vidole viwili vya mkono – kidole cha shahada na cha kati  “

➡ Kwa hiyo kila sadaka ambayo manufaa yake ni yenye kuendelea na kudumu inaingia katika maana hiyo ya sadaqatin jaariya. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUPE UWEZO WA KUTEKELEZA IBADA ZAKE KWA UKAMILIFU. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH.SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

SWALI

Mume ameoa mke wa pili kwa siri,  na sasa ana watoto huku na kule,  na anakwenda zamu  kwa mke wa siri  mchana tu,  na usiku kwa mke wa mwanzo kama kawaida.  Je hivi ni sawa? 

JAWABU
➡ Ndugu zangu : 
Jambo la ndoa ni jambo la ibada ambayo inapelekea kuungana pande mbili za walioowana. 

➡ Na katika ndoa kuna mambo ambayo ni haki kwa upande na upande mwingine unakuwa ni wajibu kutekeleza. 

➡ Na katika ndoa kuna kuunga udugu,  na kupatikana nasabu ,  vipi inakuwa mtu anaoa kwa siri bila kutangaza ndoa yake ikajulikana kwa watu wengine ila wawili watatu? 

➡ Katika kuoa pia kuna hukmu za kisheria  ambazo zinafanyiwa kazi kwa sababu ya kutokea ndoa hiyo; 

1- Kama kuharamika kumposa mke wa mtu. 

2 – Kuhalalika baadhi ya jamaa wa kiume  wa mume kuchanganyika nae kwa sababu ya kuwa anakuwa ni mke kwa upande wa baba wa mume. 

3 – Kisha kuna kizazi kwa upande wa mke wa kwanza na wa pili,  ikiwa watoto hawajkujuana tokea udogo inaweza kuja tokea makosa ya kuja kuoana pengine katika mustaqbal,  japokuwa baadaya miaka mingi, kwa sababu ya kutokujuana. 

4 – Pia kuna haki za mke mwenyewe ambazo kama mke hakujulikana inawezekana haki zake zikapotea katika masiku ya baadae,  kama vile haki ya kurithi mali ya mume baada ya kufariki. 

➡ Na mara nyingi katika ndoa za siri hutokea mapungufu mengi katika kutekeleza uadilifu kati ya wake wawili hao,  au katika malezi ya watoto wao. 

➡ uadilifu ni :  ” kukipa kila kitu haki yake kama kinavyo stahiki “

➡ Na mume kuwa muadilifu baina yake na wakeze ni jambo la wajibu. 

➡ Na mume anatakiwa kugawa siku za zamu sawasawa kwa wake zake wote wawili,  hata kama atakuwa mke mmoja ni mgonjwa ni lazima akitaka kwenda kwa mke ambae si zamu yake amuombe ruhusa mke mwenye zamu. 

➡ Ikiwa atakwenda bila ruhusa ya mke mwenye zamu atakuwa mume huyo amedhulumu na amefanya dhambi. 

➡ Na akitaka kusafiri ni lazima apige kura na wakeze wote,  na anatakiwa kugawa zamu za kusafiri na wakeze kwa mujibu wa inavyostahiki, ila ikiwa watarirdhiana wenyewe kati yao kwa kuacha mmoja wao zamu yake kwa mwenzake,  hapo hakuna tatizo. 

➡ Mfano ikiwa ana safari mbili kwa mwaka,  basi agawe kwa kila mke safari moja. 

➡ Na mambo ya lazima kufanya uadilifu kwa wake zaidi ya mmoja ni : 

1 – Matumizi ya lazima ya kila siku,  kama vile : Chakula , Malazi : Yaani sehemu za kulala. Kipando. 

Zamu za kulala. 

➡Hayo ndiyo mambo muhimu ambayo ni lazima kwa mume kuyatekeleza,  na kinyume cha hapo atakuwa ni dhwaalimu hata kama anaswali sana na kufunga. …  hana faida ya saumu zake na ibada zake. 

➡ Amma mume kuwa anakwenda zamu mchana tu kwa mke mmoja,  na huku kwa mke wa mwanzo anakwenda usiku tu,  hapo mara nyingi hawezi kufikia uadilifu unaotakiwa kisheria, ila kwa rehma za ALLAAH S.W. 

➡ Na sababu kubwa ya hilo ni kuwa : 
” ALLAAH S.W amejaalia wakati wa mchana ni wa kutafuta maisha,  tofauti na wakati wa usiku ambao utulivu mkubwa unapatikana zaidi. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ)
[Surat Al-Anaam 96]

Ndiye anaye pambazua mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko na utulivu, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hayo ndiyo makadirio ya Aliye tukuka Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi.

➡ Na katika aya nyingine akasema : 
(وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِبَاسًا وَالنَّوْمَ سُبَاتًا وَجَعَلَ النَّهَارَ نُشُورًا)
[Surat Al-Furqan 47]

Naye ndiye aliye kufanyieni usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa mapumziko, na akakufanyieni mchana ni kufufuka.

➡ Na wakati wa mchana bila shaka hauna utulivu kama usiku. 

➡ Pamoja na hivyo; 
Ikiwa mke wa pili ameolewa kwa ndoa hiyo ya siri,  ndoa ikiwa imetimiza masharti yake yote kamili ya kusihi,  na Mashahidi wanapatikana,  na ridhaa,  na mke na mume wakakubaliana masharti ambayo hayapingani na qurani na sunna,  ndoa hiyo inasihi kisheria. 

➡ Lakini mume lazima atekeleze yote yaliyokuwa ni wajibu juu yake katika kuhudumia family zote mbili bila kumili upande mmoja. 

➡ Na lazima agawe muda wake katika kusimamia malezi ya watoto wa pande mbili zote ikiwa amejaaliwa kupata watoto. 

➡ Namuomba ALLAAH S.W ATUPE TAWFIQ KATIKA KUTEKELEZA AMRI ZAKE NA KUACHA MAKATAZO YAKE,  NA KUMFUATA MTUME WAKE.

 

ALLAAHU AALAMU.
SH. SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

 SWALI

Jee mwanamke ni akae na asubiri mume aje amuowe ama pia anaruhusa ya kujitafutia mume Wa kumuoa ?

JAWABU 

 

➡ Kila jambo katika dini lina asili yake na misingi yake na adabu zake.

 ➡ Na kila mmoja katika jinsia mbili hizi,  ya kiume na kike,  imeumbwa na tabia ambazo zinatofautiana,  mwanaume si kama mwanamke.

 ➡ Asili ni kuwa :

” mwanaume ndie anamposa mwanamke,  na sio mwanamke ampose mwanaume “

 ➡ Imekuja katika hadithi mbalimbali za mtume s.a.w zina onyesha kuhusu suala hili.

  إذا خطب إليكم من ترضوْن دينَه وخُلقَه فزوِّجوه ، إلَّا تفعلوا تكنْ فتنةٌ في الأرضِ وفسادٌ عريضٌ

الراوي: أبو هريرة المحدث: البخاري             – المصدر: العلل الكبير – الصفحة أو الرقم: 154

 Maana yake ni kuwa :

Amepokea Abuu huraira r.a kutoka kwa mtume s.a.w amesema :

” akiposa kwenu mtu ambae munamridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, ikiwa hamkufanya basi itakuwa katika ardhi    fitna na ufisadi wenye kuenea “

 ➡ Hadithi inaonyesha mambo mengi muhimu :

 1- Asili ya mwenye kuanzisha maombi ya kuoa ni mwanaume.

 2 – Inaonyesha ubaya mkubwa kwa kumkataa na kumrejesha  mposaji ambae anakubalika kwa dini yake na tabia zake.

 3 – Inaonyesha kuwa :

Kinachozinfatiwa hasa katika kuchagua mume bora ni dini yake na uzuri wa tabia zake,  na wala si wingi wa mali wala ukubwa wa cheo.

 4 – Inaonyesha kuweza kutokea maharibiko makubwa ikiwa wazazi watawazuia watoto wao kuolewa ikiwa wameposwa na watu wema,  na haya ndiyo ambayo yanaonekana katika jamii nyingi za kiisilaamu.

 ➡ Pamoja na hilo pia;

Uisilamu haukumnyima mwanamke haki ya kuchagua mume ampendae ➡Wala haukumnyima haki ya kusema maoni yake kuhusu mume mwema anaemuona kuwa atamfaa katika maisha yake ya ndoa ➡Lakini mwanamke huyo anatakiwa kuchunga mipaka ya sheria katika kubainisha hilo jambo kwa walii wake.

 ➡ Bali anatakiwa kutumia lugha ya ishara tu ikiwa amesikia kuna mume mwenye sifa nzuri za kidini.

 ➡ Tazama binti wa Nabii Shuaibu a.s,  alipokuwa amemuoa mtu ambae amewasaidia kuwanyweshea maji wanyama wao baada ya kuwa wameshindwa kufanya hivyo wao wenyewe kutokana na kuwepo wanaume wengi katika wachungaji wa wanyama.

 

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنْزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ) [Surat Al-Qasas 24]

 Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayo niteremshia.

 

(فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ) [Surat Al-Qasas 25]

 Basi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema: Baba yangu anakwita akulipe ujira wa kutunyweshea. Basi alipo mjia na akamsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwisha okoka kwenye watu madhaalimu.

 (قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ) [Surat Al-Qasas 26]

 Akasema mmoja katika wale wanawake: Ewe baba yetu! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu.

 ➡ Bint huyo hakumuambia baba yake moja kwa moja kuwa : ” Niozeshe huyu , Bali alimtaja kwa Sifa nzuri tu alizoziona kwake katika kuwasaidia katika kuwanyesha maji wanyama wao,  na wingi wa haya zake,  na kutotaka kusema nao ila maneno kidogo tu kwa mujibu wa haja,  na katika kutembea kuelekea kwa mzazi wao hakutembea nyuma yao,  bali alikuwa mbele yao.

 ➡ Kwa hiyo ikiwa mwanamke amemuoa mtu ambae anafaa kumuoa,  ni vizuri atumie hikma na adabu katika kufikisha wasfu wa mume huyo kwa wazee wake.

 ➡ Na ni bora zaidi ikiwa atamuwakilisha mtu katika jamaa zake anaowaamini ili wao wafikishe ombi hilo la kuoa katika family hiyo.

 ➡ Amma kutafutana watu na kupendana kwa sababu ya kuona picha tu katika mitandao mbalimbali,  hiyo si njia sahihi ya kuchagua mume wala mke.

➡ Wala face book hawezi kuwa ndio walii wa mkmwanamke katika kuposa.

 ➡ NAMUOMBA ALLAAH AWAJAALIE AMBAO HAWAJAOA BASI WAPATE WAKE BORA,  NA WALIKUWA HAWAJAOLEWA NAO WAPATE WAUME BORA .

ALLAAHU AALAMU.

  1. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI 

Nini hukmu ya muisilamu kumkodisha nyumba au duka mtu anaeuza sigara ?

JAWABU 

➡ Sigara ni moja katika miti yenye laana kutokana na madhara makubwa yatokanayo na mti huo. 

➡ Na sigara ina madhara makubwa sana kwa mtumiaji,  na pia inasababisha madhara hata kwa wengine ambao hawatumii ikiwa atachanganika mvutaji pamoja nao. 

➡ Na imethibiti kuwa sigara inauwa,  na ni sawa na sumu  inayouwa taratibu 
➡ Na ALLAAH s.w ameharamisha kujidhuru wala kujisababishia maangamivu kwa nguvu zetu wenyewe. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَأَنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ)
[Surat Al-Baqara 195]

Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

➡ Na mwenye kuuza sigara anafañya kueneza ufisadi katika ardhi,  na kueneza madhara katika jamii. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ اللَّهِ قَرِيبٌ مِنَ الْمُحْسِنِينَ)
[Surat Al-Araf 56]

Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema.

➡ Na amekataza ALLAAH S.W kusaidiana watu katika dhambi na uadui. 

➡ Ni haramu kwa muisilamu yoyote kuvuta sigara yeye mwenyewe. 

➡ Pia ni haramu kwa muisilamu kumnunulia mtu mwingine sigara,  hata kama atakuwa mvutaji ni Baba yake mzazi au mfano wake. 

➡ Ni haramu kwa muisilamu  kumuwashia sigara mtu yoyote,  kwa sababu ni kusaidia katika uovu. 

➡ Ni haramu pia kuuza sigara,  ikiwa katika duka au kutembeza mikononi,  au kwa njia za magari mitaani. 

➡ Pia ikiwa mtu ana milango ya maduka anakodisha kwa watu,  ni haramu kumkodisha muuza sigara duka lako hilo. 

➡ Na kama una gari la kuchukua mizigo basi pia inaharamika kuchukua bidhaa mbaya na ovu kama sigara. 

➡ Hata mchoraji anaechora matangazo ya sigara au kuandika maandishi na ibara za kuwavutia watu ili wanunue sigara,  kazi hiyo pia kisheria haikubaliki,  na ni chumo la haramu. 

➡ Na sigara ndugu zangu ina madhara mengi sana na makubwa,  hata baadhi ya wataalamu wamefikia kutaja maradhi yanayotokana na sigara,  na yanafikia hata maradhi aina “Mia moja na ishirini “” 120 “

➡ Je ikiwa utamuona mtu anafañya kazi,  kisha akapewa malipo ya kazi yake hiyo pesa maalumu,  alipochukua pesa hizo tu akachukua kibiriti na kuzichoma moto. 

Je mtu huyo atakuwa na akili mgojwa wa akili huyo? 

Bila shaka jawabu tunasema mtu huyo hana akili sawa. 

Hali kadhalika mfano huo uko sawa na mvutaji sigara kwa kuwa ananunua sigara kwa  pesa kisha sigara hiyo anaunguza kwa moto yeye anaambulia moshi tu wenye sumu. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUNUSURU NA TAMADUNI OVU ZA KI MAGHARIBI NA NYINGINE PIA .

ALLAAHU AALAMU

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

mke kamwambia mume wake: niache”mume akasema: ” mimi na wewe hatuna talaka twakaa tuu”.hebu nipe ufafanuzi wa habari hiyoo ?

JAWABU

 

➡ Ndugu zangu : 
Jambo la talaka si jambo jepesi tu la kuchezewa katika ndimi za watu watakavyo. 

➡ Na si kila ibara yenye maelezo kama hayo huwa ni talaka. 

➡ Talaka ni lazima iwe ni kwa ibara yenye maelezo ya wazi,  yanayo onyesha kutokwa mume tena na lengo la kuendelea kuishi na mumewe. 

➡ Pia inaweza kuwa ni kwa ibara yenye ishara tu ya kuonyesha kumuacha mkewe,  lakini ibara hiyo ikawa ni fumbo ambalo haliko wazi katika kubainisha talaka. 

➡ Katika aina hiyo ya fumbo,  talaka huwa haihesabiki mpaka aulizwe mume kuhusu maneno yake hayo anakusudia nini? 

Ikiwa atasema anakusudia kwa fumbo hilo Talaka basi itakuwa talaka hiyo itahesabika talaka kwa mujibu wa makusudio yake. 
➡ Amma mke pia kumuomba Talaka mumewe pasi na sababu zenye kupelekea kuachika,  basi mke huyo atakosa rehma za ALLAAH S.W. 
Na wala hatonusa hata harufu ya pepo. 

➡ Amesema mtume s.a.w kuhusu maana ya maelezo hayo katika hadithi hii ifuatayo :
: أيما امرأةٍ سألت زوجها طلاقًا من غير
بأسٍ، فحرامٌ عليها رائحةُ الجنة”
الراوي: ثوبان مولى رسول الله صلى الله عليه وسلم
المحدث: الترمذي – المصدر: سنن الترمذي – الصفحة أو الرقم: 1187
خلاصة حكم المحدث: حسن

➡Kwa hiyo maneno hayo hatuwezi kuyatolea tafsiri yoyote sisi ila baada ya kurudi kwa huyo mume na kumuuliza nini anakusudia kwa maneno hayo? 

➡ Ikiwa anakusudia kuwa : 
” amesha muacha mkewe talaka zote tatu na ameshamaliza nafasi yake ya kumrejea,  hapo itakuwa hakuna ndoa tena ikiwa maana ya maneno yake ni  hiyo. 

➡ Amma akiwa hajakusudia talaka yoyote,  isipokuwa anakusudia maana nyingine,  basi Kauli ni Kauli ya mume kwa mujibu wa makusudio yake. 
➡ Lakini napenda kutahadharisha sana kutokana na matumizi mabaya na yenye kuwaweka wake roho zao juu kwa juu na kuwatishia talaka kila mara. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W AJAALIE MAPENZI NA HURUMA BAINA YA KILA MUME NA MKEWE NA VIZAZI VYAO PIA. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH.SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

SWALI

Ikiwa mume anasema ataoa lakini ukamkuta ana wapenzi anachati nao kwenye simu na kurushiana picha zao, na akisafiri hukutana nao wakawa kama boy friends Na girl friend.. Hapo mwanamke hata posa hajapeleka, Jee nini hukmu ya watu hao. Na nini afanye mke wa huyo?

JAWABU

➡ Subhaana LLAAH : 
Mambo ya mitandao sasa yamekuwa ni tishio kubwa la ndoa za asilimia kubwa katika waisilamu,  wadogo na wakubwa. 

➡ Ikiwa mume huyo ameamua kuoa mke wa halali basi na aoe  mke mwingine kwa sharti awe ni muadilifu kwa wake zake wote. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانْكِحُوا مَا طَابَ لَكُمْ مِنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا)

[Surat An-Nisa 3]

Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana.

➡ Amma ikiwa anafañya uhusiano wa haramu na wanawake hao wa nje na kuvuka mipaka ya ALLAAH S.W,  huyo atakuwa anafañya makosa katika hilo.

➡ Na wala haifai kutumiana picha ila ikiwa kuna ukweli wa makusudio ya kumuoa mwanamke huyo,  na hilo lifanywe na walii wa mwanamke kwa kadri ya dharura. 

➡ Kwa mfano ikiwa mchumba huyo yuko mbali na hawezi kumuoa kwa wepesi, na yeye ana hima ya kweli ya kumuoa,  inawezekana walii wake kumtumia picha ili amuone kwa nia nzuri. 

➡ Na katika zama hizi ni zama za fitna kubwa sana katika suala la kutuma picha za wachumba. 

➡ Wako baadhi ya watu hawajui kutunza siri na amana za watu,  mara huanza kuituma picha kila pahala na kuieneza. 

➡ Na kufanya hivyo ni makosa makubwa na mtu atabeba jukumu zito siku ya qiyaama. 

➡ Na huyo mume anafañya makosa pia kwenda kukutana na wanawake hao na kufanya urafiki wakati hajawaoa bado. 

➡ Na wakiwa peke yao kama hivyo ni kufungua njia ya shetani. 

➡ Amesema mtume s.a.w : “لا يخلون أحدكم بامرأة فإن الشيطا ثالثهما

الراوي: عبدالله بن عمر المحدث: أحمد شاكر        – المصدر: مسند أحمد – الصفحة أو الرقم: 1/73
خلاصة حكم المحدث: إسناده صحيح

➡Amepokea Abdullah bin Omar r.a,  amesema mtume s.a.w : 
” asibakie mwanaume na mwanamke peke yao usipokuwa wa tatu yao ni shetani “

➡ Mke anatakiwa kumnasihi mumewe kwa hikma na maneno mazuri mpaka mumewe aache tabia hiyo mbaya. 

➡ Pia azidishe kufanya mambo mazuri yatakayomfanya mume avutike moyo wake zaidi kwake kuliko hao wanawake wa nje. 

➡ Ikiwa hakuacha bado basi mke ana haki ya kushitaki kwa wazazi wa mume,  na ikibidi basi ni muhimu kuita wazazi wa pande mbili zote ili kuweka sulhu baina yao. 

➡ Ikiwa bado tena zaidi ya hapo basi mke akashitaki uovu wa mumewe kwa kadhi wa kiisilaamu ili aweze kumuonya tabia zake hizo. 

➡ Na Ikithibiti kuwa hakuacha tabia hizo za uhuni, baada ya kupita njia hizo,  basi mwanamke ana haki ya kudai Talaka. 

➡ Na hii ni kwa sababu : 
Mume mchafu hafai kukaa na mke mwema msafi. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(الْخَبِيثَاتُ لِلْخَبِيثِينَ وَالْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثَاتِ ۖ وَالطَّيِّبَاتُ لِلطَّيِّبِينَ وَالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَاتِ ۚ أُولَٰئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ)
[Surat An-Noor 26]

Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Hao wameepushwa na hayo wanayo yasema; wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUNUSURU NA FITNA HIZI ZILIZOENEA KATIKA JAMII ZETU. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

SWALI

Nimechinja mbuzi kwajili ya kutoa sadaqa je niigawie vipi ?

JAWABU.

➡ Sadaka ni : ” Muisilamu kutoa sehemu katika mali yake bila ya kulipwa kitu chochote badala ya alichokitoa kutoka kwa mtu aliempa sadaka hiyo ” 

➡ Na sadaka haina kiwango maalumu kilichowekwa katika sheria ya dini yetu hii ya kiisilaamu. 

➡ Kila mmoja ana uhuru wa kutoa sadaka kwa mujibu wa uwezo wake, lakini ni muhimu kuzingatia katika kutoa huko mambo yafuatayo : 

1⃣Kinachotolewa sadaka kiwe ni katika vizuri vilivyo halalishwa na ALLAAH S.W. 
➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنْفِقُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنْفِقُونَ وَلَسْتُمْ بِآخِذِيهِ إِلَّا أَنْ تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ)
[Surat Al-Baqara 267]

Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

2⃣Atoe mtoaji kuwapa wanao stahiki kupewa. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا)
[Surat Al-Isra 26]

Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo.

Na akasema pia : 
(وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا)
[Surat Al-Insan 8]

Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.

3⃣Na afanye yote hayo kwa kutafuta Radhi za ALLAAH S.W. 

Amesema ALLAAHU S.W kuwasifu watu wema  : 

(إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنْكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا)
[Surat Al-Insan 9]

Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.

➡Lakini tukumbuke kuwa : anachokitoa mtu katika mali yake kwa ajili ya wajibu wa kuwahudimia watu wake wa karibu kabla ya watu wa mbali,  hicho ndio muhimu zaidi kwa kuwa ni miongoni mwa wajibu. 

➡ Amesema mtume s.a.w : أربعةُ دنانيرَ : دينارٌ أعطيتَه مسكينًا ، دينارٌ أعطيتَه في رقبةٍ ، دينارٌ أنفقتَه في سبيلِ اللهِ ، و دينارٌ أنفقتَه على أهلِك ؛ أفضلُها الذي أنفقتَه على أهلِك

الراوي: أبو هريرة المحدث: الألباني      – المصدر: صحيح الأدب المفرد – الصفحة أو الرقم: 578
خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Maana yake ni kuwa : 
” Dinari nne :
Dinari umempa masikini, 
Dinari umekombolea mtumwa, 
Dinari umeitoa katika njia ya ALLAAH, 
Dinari umeitoa kwa watu wako wa nyumbani, 
Basi iliyo na fadhila zaidi ni ile uliyoitoa kwa watu wako wa nyumbani “

➡ Kwa hiyo nyama hiyo ikiwa inatosheleza kupata mafungu mengi zaidi,  basi ni bora upate malipo makubwa kwa kugawa katika mafungu ya wengi zaidi kama ifuatavyo : 

1⃣Gawa fungu kwa ajili ya nyumbani kwako. 

2⃣Fungu jingine kwa ajili ya jamaa zako wa karibu kwa nia na lengo la kuunga udugu. 

3⃣Gawa fungu kwa jirani zako wa karibu na hasa waliokuwa ni masikini zaidi katika hao. 

➡ Na mtumes.a.w alikuwa akiwahimiza maswahaba kuzidisha mchuzi wanapopika majumbani mwao ili jirani nao wapate sehemu katika mchuzi au chakula hicho. 

➡ Amesema Abuu dharri kuwa mtume s.a.w alimuusia Abaa dharri kwa kumwambia  : 
إنَّ خليلي صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ أوصاني ” إذا طبخْتَ مرَقًا فأَكثِرْ ماءَه . ثم انظُر أهلَ بيتٍ من جيرانِك ، فأَصِبْهم منها بمعروفٍ ” .
الراوي: أبو ذر الغفاري المحدث: مسلم     – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 2625
خلاصة حكم المحدث: صحيح

“Ewe Abaa dharri; 
Ukipika mchuzi basi ongeza maji yake, kisha tazama nyumba ya jirani yako , na uwapatie  katika sehemu hiyo ya mchuzi huo kwa wema “

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUJAALIE NYOYO ZENYE KUTOA KWA AJILI YAKE. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI: 

Naomba unisaidie kuhusu kula udongo je ni haramu ?

JAWABU

➡ Asili ya vitu huwa ni uhalali mpaka ithibi dalili ya kisheria kwa kutoa hukmu nyingine isiyokuwa hiyo. 


➡ ➡ Amesema ALLAAHU S.W kuhusu uhalali wa asili wa vitu kuwa : 
(هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُمْ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ)
[Surat Al-Baqara 29]

Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu.

➡ Pia inawezekana kitu kikawa ni cha halali katika asili yake,  lakini ikabadilika hukmu kutokana na kuwepo madhara ndani yake. 

➡ Na ALLAAH s.w ameharamisha kwa mtu kujidhuru nafsi yake na kuipelekea katika kuangamia. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَأَنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ)
[Surat Al-Baqara 195]

Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

➡ Na amesema pia kuhusu kula vilivyokuwa ni vya halali na vizuri :

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ)
[Surat Al-Baqara 172]

Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.

➡ Na kwa hakika udongo si katika aina ya chakula kwa mujibu wa ada na kawaida ya watu katika jamii zao. 

➡ Na kwa kuwa hakuna dalili ya kuharamisha kula mchanga moja kwa moja,  lakini kama tulivyosema kuwa : 
” Kuna vitu huwa vinabadilika hukmu kwa mujibu wa madhara yake au manufaa yake “

➡ Na kwa mujibu wa utafiti niliopata kuusikia kwa baadhi ya madaktari, ni kuwa : 

1⃣Udongo unakuwa na aina ya chenga chenga ambazo zikiingia katika tumbo huwa hazisagiki wala kuyayuka. 

2⃣Pia udongo unapojikusanya katika chango tumboni unaweza kuganda na kusababisha uvimbe katika baadhi ya chango,  na kupelekea  kupata maradhi ( pendex ) yanayopelekea kufanyiwa oparesheni ndogo. 

3⃣Pia husababisha kutoa haja kubwa kwa ugumu,  na hii inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi kutokana na kutumia nguvu katika kukidhi haja. 

➡ Kwa jumla muisilamu anatakiwa kujiepusha na kila lenye kumtia shaka au kumletea madhara. 

➡ Amesema mtume s.a.w :
  ” دَع ما يَريبُكَ إلى ما لا يَريبُك…”

الراوي: – المحدث: الهيتمي المكي – المصدر: الزواجر – الصفحة أو الرقم: 1/232
خلاصة حكم المحدث: صحيح

Maana yake ni kuwa : 
” Acha lenye kukutia shaka na ufuate lisilokutia shaka “

➡ Jizoeshe kuacha kula mchanga kama ulivyojizoesha kuula. 

➡ Tumia vitu vingine ambavyo havina madhara kama vile : 
Biskuti – chokleti na mfano wake. 

Nafsi ukiizoesha kitu kuacha inaweza kuacha bi idhini llaah taalaa. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA KUTEKELEZA. 

Published By Said Al Habsy

SWALI

Je adhana mbili kwa siku ya ijumaa ilianza zama za Khalifa gani? 

JAWABU

 

➡ adhana ni :  ” wito kwa ajili ya sala za faradhi,  kwa matamshi maalumu,  baada ya kuingia muda wa sala “

➡ Asili ni kuwa wito huu unakuwa katika mwanzo wa wakati wa sala ya faradhi,  lakini pia ziko baadhi ya sala zimeongezewa adhana nyingine mwanzo kabla ya kuingia muda wa sala yenyewe,  ili kuwakumbusha waliokuwa wamesahau,  au kuwasogeza waliokuwa mbali. 

➡ Na miongoni mwa sala ambazo zimewekewa adhana mbili ni : 

1⃣Sala ya Alfajiri. 
Na mtume s.a.w alikuwa ameweka waadhini wawili,  mmoja ana adhini kabla ya kuingia Alfajiri,  na mwingine baada ya kuingia Alfajiri. 

➡ Alikuwa  mtume s.a.w akisema :
كان النبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يقولُ إنَّ ابنَ أمِّ مكتومٍ ينادي بلَيْلٍ فكلُوا واشربوا حتى ينادِيَ بلالُ أوْ إنَّ بلالًا ينادي بِلَيْلٍ فكلُوا واشرَبُوا حتَّى ينادِيَ ابنُ أمِّ مكتومٍ…

الراوي: أنيسة بنت خبيب بن يساف المحدث: الهيثمي  – المصدر: مجمع الزوائد – الصفحة أو الرقم: 3/156
خلاصة حكم المحدث: رجاله رجال الصحيح‏‏

Maana yake ni kuwa : 
” Hakika ibnu ummi maktuumi ananadi wakati wa usiku,  basi Kuleni na kunyweni,  na kunyweni hadi ataponadi Bilali,  
Au alikuwa akisema kuwa : 
” Hakika Bilali ananadi wakati wa usiku,  basi Kuleni na kunyweni hadi ataponadi ibnu ummi maktuumi…”

➡ Na hiyo adhana imethibiti katika sunna sahihi za mtume wetu muhammad s.a.w. 

2⃣Sala ya pili ni : 
Sala ya ijumaa :
Imethibiti pia adhana ya kwanza kabla ya kuingia muda wa sala ya adhuhuri kwa siku ya ijumaa.

➡ Na adhana hii kwanza alianzisha swahahabiy Uthmaan bin Affaan r.a katika zama za ukhlalifa wake. 

➡ Na hii ilikuja baada ya kuona watu wengi wameshughulika na kuwa wanachelewa kuja msikitini. 
➡ Kawaida ilikuwa ni adhana moja tu katika siku ya ijumaa. 

➡ Alikuwa mtume s.a.w akishapanda katika minbari ndipo anasimama Bilali r.a na kuadhini katika mlango wa msikiti. 

➡ Na alilofanya Uthmaan lilikuwa ni jambo zuri ambalo linakubaliana na makusudio ya asili katika dini. 

➡ Kutokana na hilo, 
Hata maswahaba wengine hawakupinga alilofanya Uthmaan r.a,  bali waliafiki na kulifanyia kazi hata likawa ni kama makubaliano ya wote hadi leo hii. 

➡ Na iko Kauli kuwa : Omar bin l khatwaab r.a alikuwa akiamrisha mtu kunadi  kabla ya muda ili kuzindua watu,  na inaonekana kuwa ilikuwa si adhana kamili,  bali ni wito tu kwa ajili ya kuukumbusha watu. 

➡ Na baadhi ya maulamaa wameita kitendo cha uthmaan kuwa ni bid’aa nzuri,  kwa kuwa ni jambo ambalo mtume s.a.w hakulifanya ,  lakini lina msingi wake katika dini. 

➡ Juu ya hilo tukumbuke kuwa : ”  Kufuata makubaliano ya maswahaba katika hukmu mbalimbali ni sehemu katika kufuata sunna “

➡ Amesema mtume s.a.w :
” … فعليكُم بسُنَّتِي ، و سُنَّةِ الخلفاءِ الرَّاشدين المهديِّين ، عَضُّوا علَيها بالنَّواجذِ …”

الراوي: العرباض بن سارية المحدث: الألباني       – المصدر: صحيح الترغيب – الصفحة أو الرقم: 37
خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Maana yake ni kuwa :
” …Basi ni juu yenu kufuata sunna zangu na sunna za makhalifa baada yangu. ..”

➡ Japokuwa wako baadhi ya maulamaa wanaona kuwa : ” Hakuna haja ya kufanya adhana ya kwanza kwa siku ya ijumaa,  kwa kuwa jitihada ya uthmaan bin affaan amefanya vile kwa kuwa kilikuwa na haja ya kufanya hivyo. 

Amma ikiwa Hakuna dharura wala ulazima wa kukumbusha watu kwa adhana ya kwanza basi kufanya adhana moja ni bora zaidi kuliko mbili. 

➡ Lakini hii Kauli ya baadhi ya maulamaa wa salafi. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA NANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO. 

Published By Said Al Habsy

SWALI

Nina shamba la wakfu kutoka babu yangu mzaa baba.Mie nimesha staafu kazi yangu kwa sasa, 
Sasa sina uwezo wa kulitizama hilo shamba sasa limekua kama mzigo na halina msaada bali linazidi kuharibika .Je naweza kuliuza nabadala yake kununua kitu kitakacho tusaidia na kukifanya Wakfu?

 

JAWABU

➡ Asili ya wakfu ni : ” Muisilamu kutoa sehemu katika mali yake ambayo ni asili ya mali,  na kuifunganisha kwa ajili ya njia za ALLAAH S.W “

➡ Na mali ikishakuwa ni wakfu basi inakuwa na hukmu zake maalumu tofauti na sadaka nyingine za kawaida. 

➡ Imepokewa kuwa : 
أصاب عمرُ أرضًا بخيبرَ . فأتى النبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ يستأمرُه فيها . فقال : يا رسولَ اللهِ ! إني أَصبتُ أرضًا بخيبرَ . لم أُصِبْ مالًا قطُّ هو أَنفسُ عندي منه . فما تأمرُني به ؟ قال ( إن شئتَ حبستَ أصلَها وتصدقتَ بها ) . قال : فتصدَّق بها عمرُ ؛ أنه لا يباعُ أصلُها . ولا يبتاعُ . ولا يورثُ . ولا يوهبُ . قال : فتصدَّق عمرُ في الفقراءِ . وفي القُربى . وفي الرِّقابِ . وفي سبيلِ اللهِ . وابنِ السبيلِ . والضَّيفِ . لا جناح على مَن وَلِيها أن لا يأكل منها بالمعروفِ…
الراوي: عبدالله بن عمر المحدث: مسلم     – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 1632
خلاصة حكم المحدث: صحيح

Maana yake ni kuwa : 
” alipata Omar bin l khatwaab r.a ardhi katika mji wa khaibara,  akamuendea mtume s.a.w kumshauri kuhusu ardhi hiyo,  akasema : 
” Yaa rasuula llaah; 
Hakika mimi nimepata ardhi huko khaibara,  sijapatapo  mali yenye thamani kuliko hiyo katu, nini unaniamrusha niifanyie mali hiyo ?

Akasema mtume s.a.w : 
” Ukitaka ; 
Izuie asili yake na uitoe sadaka”
Anasema ibnu umar r.a : 
” Akaitoa sadaka ” ila haiuzwi asili yake,  wala hainunuliwi, wala hairithiwi wala haitolewi zawadi”
Akaitoa Omar kwa ajili ya watu wa karibu na kukomboa watumwa,  na  wageni,  na wasafiri walioharibikiwa, na hakuna tatizo kwa anaeisimamia kutumia – katika wakfu huo kwa wema -, .

Ameipokea imaamu muslimu. 

➡ Japokuwa wakfu asili yake haiuzwi,  kwa kuwa wakfu ni sawa na wasia,  na wakfu pia ni sawa na yatima,  lakini katika hali ya dharura hukmu yake hubadilika kwa mujibu wa dharura. 

➡ Ikiwa wakfu huo wa shamba sasa umekuwa hauna manufaa yaliyokusudiwa hapo ulipo,  na ukawa wakfu huo unaharibika ,  na maslahi ya asili hayapatikani,  katika hali hiyo inajuzu kuuzwa wakfu huo,  na kununua badala yake kitu kingine ambacho kitakuwa pia ni wakfu kama ulivyokuwa wakfu wa mwanzo,  na kwa malengo na maslahi yale yale ya wakfu wa asili . 

➡ Muhimu ni lazima pia kuwashauri watu waaminifu na wenye ujuzi katika wasimamizi wa wakfu huo,  ili lifanyike hilo kwa rai zao pia kwa mujibu wa lilikuwa ni lenye maslahi zaidi katika wakfu huo. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA.

Published By Said Al Habsy

SWALI

ikiwa nimepeleka msaada kwa mtu ambae msaada huo nimetumia mtu mwengine kuupeleka,
lakini nikagundua kwamba ule msaada haukufika kwa muhusika, yule mplekaji katumia yeye; Je hapo mimi nitapata thawabu kama nilivokusudia au inakuwaje hapo ? naomba ufafanuzi.

 

JAWABU

➡ Kuhifadhi mali ni moja katika miongoni mwa makusudio ya lazima katika dini. 

➡ Na unapotaka kumtuma mtu amana yoyote ni lazima uzingatie yafuatayo : 

1⃣Dini yake kwanza. 
Kwa kuwa wako watu huwa hawatunzi amana hata kama itakuwa ni ndogo sana,  na wengine wanatunza hata kama itakuwa ni kubwa sana. 

➡ Tazama aya hii kuhusu watu wa kitabu. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِنْ تَأْمَنْهُ بِقِنْطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُمْ مَنْ إِنْ تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 75]

Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurudishia, na miongoni mwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari moja hakurudishii isipo kuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi Mungu, hali nao wanajua.

2⃣Uaminifu wake katika mambo mbalimbali tokea asili yake. 

Si kila muisilamu muaminifu,  kuna baadhi ya waisilamu hawajasalimika bado katika uisilamu wao. 

➡Amesema mtume s.a.w katika hadithi alivyoipokea Abdullah bin Amruu r.a  : 
تدرونَ مَنِ المسلمُ ؟ قالوا: اللهُ ورسولُهُ أعلمُ قالَ: مَن سلِمَ المُسلِمونَ من لِسَانِهِ ويدِهِ قالَ: تدرونَ مَن المؤمنُ ؟ قالوا: اللهُ يعنِي ورسولُهُ أعلَمُ قال: مَن أَمِنَهُ المؤمنونَ علَى أنفسِهِم وأموالِهِم …”
الراوي: عبدالله بن عمرو المحدث: أحمد شاكر       – المصدر: مسند أحمد – 
الصفحة أو الرقم: 11/190
خلاصة حكم المحدث: إسناده صحيح

” Munamjua nani muisilamu? Wakasema maswahaba r.a :  “ALLAAH na Mtume wake ndie wajuzi zaidi.  Akasema mtume s.a.w : “Muisilamu wa kweli ni yule ambae waisilamu wengine wamesalimika kutokana na ulimi wake na mkono wake ” 

Kisha akasema : 
” Munamjua nani muumini? 
Wakasema maswahaba r.a : ALLAAHU na mtume wake ndio wajuzi zaidi,  
Akasema mtume s.a.w : 
” Muumini wa kweli ni yule ambae wameaminisha watu katika damu zao – sisimwagwe – na mali zao “

➡ Ikiwa mali hiyo iliyokuwa unakusudia kumpa mtu huyo ni msaada wa kawaida tu,  Inshaallaah hutokuwa na dhamana ya kurejea kumlipa tena kwa kuwa haikufika,  ikiwa huo ni msaada ambao haukuwajibikii katika asili. 

➡ Amma ikiwa ni katika wajibu wa lazima juu yako,  kama mfano ilikuwa ni zaka ya mali yako unampa masikini huyo,  kisha ikapotea njiani na haikumfika mkusudiwa,  hapo inakulazimu kuitoa tena kwa mara nyingine,  na inabakia deni juu yako mpaka imfike. 

➡ Pia kama ulikuwa umeweka nadhiri ya kutoa mali hiyo kwa mtu huyo,  inakulazimu kuilipa kwa kuwa haitenguki mpaka utekeleze ulichokiwekea nadhiri. 

➡ Pia nakushauri kuwa mfuatiliaji zaidi wa misaada hiyo unapoitoa kwa watu. 

➡ Kwa nia yako nzuri Inshaallaah utapata ujira wako na thawabu zako kamili japokuwa sadaka hiyo haikufika,  kwa sababu hujadababisha wewe sadaka hiyo ipotee. 

➡ Na huyo uliyempa amana hiyo kama atakuwa hakutubia kutokana na dhulma hiyo,  mbashirie kuwa anakula mali kwa njia ya haramu,  na huenda akawa anakula moto na atauingia moto siku ya qiyaama,  ila akitubia  toba ya kweli,  na akarejesha amana ya mali hiyo kwa mwenyewe au kuifikisha kwa mwenye kuistahiki. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUEPUSHE NA TAMAA KATIKA HAKI ZA WATU. 

ALLAAHU AALAMU. 


SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI 

Mimi ni muislamu,Je nikienda kanisani  kuombewa kwa matatizo yangu ya mashet’ani  na nikapona nitakuwa nimefanya makosa au nipo sahihi? na kama ni kosa je hilo kosa lipo katika kiwango gani cha makosa ? 

JAWABU

➡ Maombi yote ya waja lazima wamkusudie yeye peke ALLAAH S.W. 

➡ Na Hakuna anaeweza kumuondoshea mwingine shida zake isipokuwa ALLAAH S.W peke yake mola wa kweli .

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(أَمَّنْ يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَٰهٌ مَعَ اللَّهِ ۚ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ)
[Surat An-Naml 62]

Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.

➡ Na yeye ALLAAH S.W ndie ameamrisha Tumuombe yeye tu kwa majina yake mazuri, na amekataza kufuata njia za wenye kwenda kinyume katika maombi yao. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَلِلَّهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ)
[Surat Al-Araf 180]

Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda.

➡ Bila shaka waliokuwa si waisilamu wanaharibu utukufu wa ALLAAH S.W, 

1 – Kwa kuwa ALLAAH S.W wanamuita Baba. 

2 – Wanaamini kuwa yuko mbinguni. 

3 – Wanaamini kuwa ana mwana. 

4 – Wanaamini kuwepo nafsi katika Mungu Mmoja. 

Haya yote ni katika kukanusha itiqaadi sahihi katika kumsimfu ALLAAH S.W. 

➡ Bali pia wako baadhi ya waisilamu nao pia hukosea kumuomba ALLAAH S.W,  na hatimae humuomba kupitia majina si yake Yeye ALLAAH S.W,  na hili ni kinyume na Qur’ani na mafundisho sahihi ya ALLAAH S.W. 

➡ Mifano ya makosa watafanyayo baadhi ya waisilamu katika dua ni : 

1 – Kumuomba kupitia majina ya mitume au haki ya mtume fulani. 

2 – Kutumia majina ya maswahaba,  kama ikivyokuwa imeenea kwa watu kusoma majina ya maswahaba walipigana vita vya Al badri,  maarufu kinaitwa na watu kuwa : 
“AHLUL BADRI ” Pia ni makosa kutumia kitabu hicho. 

3 – Kutaja majina ya maulamaa maalumu katika maombi,  kama vile kumtaja Sh Abdul Qaadir al jiilaany na mfano wake,  pia hili ni makosa. 

4 – Na hili haliko mbali kuingia hatarini katika itiqaadi kama lilivyowapeleka mayahudi na manasara katika kuwatikuza wanazuoni wao hata wajawafanya kama miungu. 

➡ Kwa hiyo:
1-  kwenda kuombewa Dua na aliekuwa si muisilamu ni kwenda kinyume na mafundisho sahihi ya dini ya kiisilaamu.  

2 – Ikiwa utaitaqidi usahihi wa wansyoyafanya na kutaraji kuwa manufaa yako katika maombi yao,  hilo ni jambo la hatari sana,  na linamtoa mtu katika Kundi la waumini na kumtupa katika kundi la makafiri,  na ikiwa atakufa katika hali hiyo atakuwa amekufa hali ya kuwa si katika miongoni mwa wafuasi wa mtume s.a.w. 

➡ Na wala hatofantiwa haki za uisilamu ikiwa atakufa bila kutubia na kurudi katika itiqaadi sahihi. 
➡ Na muisilamu lazima awe na yaqini  na dhana nzuri kwa mola wake s.w. 

➡ Na ajue kuwa : 
” Huenda analolidhania ni kheri kwake kumbe ni shari kwake,  na kinyume chake pia. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَنْ تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَكُمْ ۗ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ)
[Surat Al-Baqara 216]

Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI

SWALI LA 920:
Ktk sura za Qur’an ambazo zinazungumzia ahlil kitabu. Je ahlil kitab wamekusudiwa kina nani ?

Suala la pili :
Je inafaa kula Chakula halali kama wali nyama au wali wa kuku ktk restaurants ya myahudi au manasara ? Na kama kuna dalili ya hayo itakuwa vizuri. 

 

JAWABU

 

➡ Neno “Ahlu l kitaabi ” limetajwa katika qurani katika aya nyingi sana.

➡ Na maana ya neno hilo ni : “Watu wa kitabu “

➡ Na wameitwa watu wa kitabu, kwa kunasibishwa wao kwa kitabu ili kuwaonyesha mambo yafuatayo : 

1 –  Umuhimu wa vitabu walivyoletewa na mitume wao. 

2 – Kuonyesha ubora wa mitume wao juu yao. 

3 – Kuonyesha ulazima wa kufuata mafundisho ya vitabu vyao na kuwatii mitume yao. 

➡ Na watu hao wa kitabu hasa wamekusudiwa watu wa Nabii Musa na Isa a.s.

➡ Na hao walijiita mayahudi na manaswara ,  kama alivyosema ALLAAH s.w katika QURANI tukufu. 

➡ Na hawa watu wanatofautiana hali zao katika kufuata mafundisho sahihi ya vitabu na mitume yao. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 113]
Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama baraabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu.

(يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ)
[Surat Aal-E-Imran 114]

Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanakimbilia katika mambo ya kheri. Na hao ndio miongoni mwa watenda mema.

(وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَنْ يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ)
[Surat Aal-E-Imran 115]

Na kheri yoyote wanayo ifanya hawatanyimwa malipwa yake. Na Mwenyezi Mungu anawajua wachamngu.

➡ Hao ndio watu wa kitabu wenye sifa sahihi za kustahiki kuwa pamoja nao katika miamala yetu ambayo inahitaji twahara na ni sehemu katika ibada au itiqaadi. 

➡ Ikiwa wapo wenye sifa hizo katika watu wa kitabu,  basi hao ndio halali kula wanyama waliochinja wao,  kwa kuwa watachinja kama alivyo amrisha ALLAAH S.W,  lakini je wapi wapo wenye sifa kama hizi? 

➡Na pia haitoshi kuwa hivyo tu,  bali ni lazima wao pia wafuate sheria za mtume wetu muhammad s.a.w,  na wamuamini mtume s.a.w ambae ni mtume aietajwa katika vitabu vyao pia. 

Na wao hawamuamini yeye wala kitabu chake katika zama hizi. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِنْ بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَٰذَا سِحْرٌ مُبِينٌ)
[Surat As-Saff 6]

Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!

➡Bali ALLAAH S.W mwenyewe amewataja kuwa wamekufuru hao,  

Amesema ALLAAHU S.W : 
(لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قُلْ فَمَنْ يَمْلِكُ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ أَنْ يُهْلِكَ الْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ وَمَنْ فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ۗ وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)
[Surat Al-Maeda 17]

Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu. Sema: Ni nani mwenye kumiliki cho chote mbele ya Mwenyezi Mungu ikiwa Yeye angetaka kumuangamiza Masihi mwana wa Maryamu, na mama yake, na wote waliomo katika ardhi? Na mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ni vya Mwenyezi Mungu. Huumba apendavyo. Na Mwenyezi Mungu anao uweza juu ya kila kitu.

Na manaswara wanasema hilo. 

➡ Na kuhusu mayahudi nao pia wamekufuru. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُمْ بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ)
[Surat At-Tawba 30]

Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!

➡ Na akawafundisha  kuhusu haki juu ya Masihi mwana wa Maryamu, na kumuamini ALLAAH S.W na mitume yake,  na wasiseme kuwa miungu wako watatu. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انْتَهُوا خَيْرًا لَكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّهُ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ سُبْحَانَهُ أَنْ يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ وَكِيلًا)
[Surat An-Nisa 171]

Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.

➡ Hizi ni baadhi ya dalili kuonyesha hali za hawa watu waliopotea katika kila kitu katika dini na mila wafuatazo .

➡ Amma kuhusu kula chakula Chao ,  hapa kuna hali mbili kwa mujibu wa sifa zao hizo zilizo tangulia :

1⃣Kujuzu kula nyama waliochinja :
Ikiwa watu wa kitabu hao ni wenye sifa za imani na kufuata vitabu vyao na kuwatii mitume wao na mtume s.a.w. 

Na hao ndio aliowataja ALLAAH S.W katika Kauli yake aliposema :
(الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَنْ يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ)
[Surat Al-Maeda 5]

Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a’mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.

➡Kinyume na hao ni haramu  kula vitu vyao walivyochinja. 

2⃣Amma vyakula ambavyo wao wamepika tu kwa kuwa ni wapishi ,  hukmu ni katika hali zifuatazo : 

1 – Ikiwa hawa kuchanganya na vilivyo haramishwa itafaa kula. 

2 – Lakini pia ikiwa vimepikwa katika moto au njia ambayo itakuwa wao hawa kuvikamata moja kwa moja kwa miili yao baada ya kuwa vimeshakuwa tayari kuliwa. 

Akiwa amekikamata kabla ya kupikwa kisha kikapikwa Inshaallaah hakuna tatizo katika kula chakula hicho. 

➡ Kwa hiyo yakitimia masharti hayo,  na ikawa kuna dharura ya kuelekea kula katika mikahawa yao,  Hakuna kizuizi Inshaallaah pamoja na kuchunga hayo.

➡ Pia kumbuka kuwa : 
” Acha lenye kukutia shaka na ufuate lisilokutia shaka ” 

Huu mukhtasari wa jawabu kuhusu hili  Inshaallaah. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI


1. Ikiwa mtu kamuota maiti wake nini afanye?

2. Ikiwa mtu anaijiwa katika fikra zake saa zote na maiti wake nini afanye?

 

JAWABU

Namuomba ALLAAH S.W atujaalie kheri ya ndoto uliyoiona,  na akuondoshee shari yake ikiwa kuna shari. 


➡ Elimu ya kuagua ndoto sina,  na hiyo ni Elimu maalumu ambayo ALLAAH S.W humpa amtakae katika waja wake. 

➡ Na napenda kukumbusha jambo ambalo watu wengi huwa wanachukulia kuwa ni jambo la kawaida sana kumbe ni hatari sana kwao. 

Nalo ni suala la kuagua ndoto kwa mujibu wa akili ya mtu inavyomtuma tu au anabyofikiria yeye anaona hivyo ndio maana yake. 

➡ Ndoto na Kutoa Fatwa vyote viwili hivyo viko daraja sawa katika dhambi ikiwa atajitia mtu kusema ndani yake hali ya kuwa hana ujuzi nayo,  kisha akakosea au akapatia kwa kubahatisha bila ya kuwa na hakika ya kujua haki. 

➡ Amesema mtume s.a.w : 35) … أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ أَفْتَى مَسْأَلَة أَوْ فَسَّرَ رُؤْيًا بِغَيْرِ عِلْمٍ كَمَنْ وَقَعَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الأَرْضِ فَصَادَفَ بِئْرًا لاَ قَعْرَ لَهُ وَلَوْ أَنَّهُ أَصَابَ الْحَقَّ».

➡ Maana ya hadithi ni : 
” mwenye kufutu mas’ala au kufasiri ndoto bila ya elimu,  atakuwa kama alieporomoka kutoka mbinguni mpaka ardhini,  kisha akakuta kisima ambacho hakina kina,  japokuwa yeye atapatia haki “.

➡ Tazama hatari hiyo ya kufasiri ndoto au kutoa fatwa bila ya kuwa na ujuzi wa kujua sheria za ALLAAH na kuchimbua hukmu zake kutoka katika dalili zake. 

➡ Ndio maana ALLAAH S.W amesema kuhusu kujua nabii yuusuf a.s maana ya ndoto za watu kuwa : 
(وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِنْ تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ آلِ يَعْقُوبَ كَمَا أَتَمَّهَا عَلَىٰ أَبَوَيْكَ مِنْ قَبْلُ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ)
[Surat Yusuf 6]

Na kadhaalika Mola wako Mlezi atakuteuwa na atakufundisha tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa’qub, kama alivyo watimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni Mjuzi Mwenye hikima.

➡ Amma kuhusu mawazo ysnsyokujia katika kukumbuka mtu aliekufa tayari,  Jitahidi kufanya yafuatayo Inshaallaah : 

1 – Ikikujia fikra kama hiyo sema :  Audhubillahi mina sshaitwaani rrajiim “

2 – Kisha Jitahidi kujilazimisha kuweka mbali fikra hizo. 

3 – Changanyika na watu usipendelee kukaa peke yako kila mara. 

4 – Badilisha baadhi ya maeneo baadhi ya wakati,  usikae sehemu moja muda mrefu. 

5 – Fanya harakati mbalimbali ambazo zitakufanya muda wako uwe umeshughulika ,  lakini yasikushughulishe ambayo yatakuwa ni yenye kumuudhi ALLAAH S.W. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W AKUFANYIE WEPESI KATIKA HILO NA MENGINE. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI

Mimi nimetumwa pesa za masjid  kumalizia ujenzi wa msikiti,lakini kuna kazi za kupaka rangi au kuweka singboad sikuzifanya nikauacha vile vile lakini watu wakaanza kusali. Sasa yule alietoa pesa hizo  akauona msikiti hauna singboad na rangi,  nikamjibu kuwa:
“pesa hizi nimezitia katika matengenezo ya msikiti mwengine”jee hapo  nimekosea kufanya hivyo ?

JAWABU

 

➡ Subhaana LLAAH : 
Mali yoyote ambayo ameitoa muisilamu kwa ajili ya kufanyia jambo maalumu katika dini,  ni lazima ichukuliwe kuwa hiyo ni Amana kubwa ameibeba mtu huyo. 

➡ Haifai kwa mtu yoyote kubadilisha asili ya lengo la pesa alizoaminiwa katika kazi inayohusu haki za ALLAAH S.W kama vile wakfu. 

➡ Kwa kuwa pesa hizo alizopewa aliambiwa kuwa azipeleke katika kusimamia kukamilisha ujenzi wa msikiti maalumu,  basi ilikuwa yeye haifai kisheria kuacha kumalizia kazi aliyotumwa,  na badala yake kuanzisha kazi nyingine ambayo si asili kutumika pesa hizo kwa msikiti huo. 

➡ Kwa nini watu wamekuwa wanachezea hukmu za dini kwa kiasi hichi zama hizi? ??!!

➡ Hebu Tazama nini wanasema maulamaa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu wakfu :

1.Kuhusu mali ya msikiti iliyo bakia baada ya kutumiwa :

Amesema Sh Isa bin swaaleh al haarithy r.a : 
” Wakili msimamizi wa mali hiyo aiweke katika mahitaji mengine ya msikiti huo huo,  kama kujenga kuta za ngome yake,  au dari au kuoteshea miti,  au kumwagilia miti ya msikiti,  na mengine ambayo wanahitajia watumiaji wa msikiti huo “

Na katika suali jingine aliulizwa kuhusu matumizi yaliyobakia katika kinachofutarishwa watu katika msikiti,  – yaani : mali iliyobakia katika mali ya kufutarisha msikiti huo ikiwa ni wakfu wa msikiti huo;  akasema : 
” Kilichobakia kihifadhiwe kwa ajili ya lengo la kuwafutarisha watu wa msikiti huo kwa mwaka ujao “

2⃣Pia katika Fataawa za samaahati shaikhinaa alkhaliily katika wakfu ya mali ya futarisho kuhaimishiwa msikiti mwingine amesema kuwa : 
” Ikiwa hilo kwa Makubaliano ya wahusika wote wa Wakfu miongoni mwa wahusika wa wa msikiti”.

➡ Huyo mtu kwa hakika amefanya kosa kubwa kubadilisha malengo yaliyokusudiwa katika mali hiyo. 

➡ Na kosa kubwa ni kuhamisha pesa hizo kutoka msikiti huo aliotumwa kusimamia na kupeleke msikiti mwingine wakati msikiti huo haujakamilika matengenezo yake. 

➡ Amefanya khiyana kubwa katika Amana alizopewa.

➡ Anatakiwa Atubie kwa ALLAAH S.W kutokana na khiyana hiyo,  na arejeshe pesa hizo kutoka katika msikiti aliohamishia pesa hizo kwa rai yake mwenyewe. 

➡ Ikiwa haikuwezekana kuzirejesha tena kwa sababu yoyote ile ya kisheria basi,  basi msimamizi huyo atatakiwa kuzirejesha amana za watu katika kazi hiyo ya asili. 

➡ Ikiwa atauwa Mathalan hana uwezo wa kulipa,  basi arudi kwa mtoaji mali wa asili, na amjulishe mwenye haki hiyo kosa lake. 

Na amtake radhi kwa hilo,  na Asaa akaonshosha Dhimma juu ya nafsi yake.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA NANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO. 

ALLAAHU AALAMU. 

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

”Ustadh kama mtu kapata msiba wakawa wameshazika,ikapita muda kama mwezi mmoja halaf aliefiwa akatuma salam kwa majirani kama nnafanya dua kumuombea marehem naomba mje,je inajuzu kwenda au?

na kama kuna chakula inafaa kula?

JAWABU:

➡Hakika maneno ya kweli kuliko yote ni kitabu cha ALLAAH s.w, na hakika muongozo bora ni muongozo wa Nabii s.a.w , na shari ya mambo ni yale yaliyozushwa, ni kila chenye kuzushwa ni bid’aa – uzushi -, na kila uzushi unapelekea katika moto “

➡Muongozo wa mtume wetu muhammad s.a.w ulikuwa ni kumuombea maghfira yule aliekufa baada ya kumzika tu.

➡Ndio maana mtume s.a.w alikuwa aliwaambia maswahaba r.a baada ya kuzika kuwa :
كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا فرغ من دفن الميت وقف عليه فقال استغفروا لأخيكم وسلوا له التثبيت فإنه الآن يسأل
الراوي: عثمان بن عفان المحدث: أبو داود – المصدر: سنن أبي داود – الصفحة أو الرقم: 3221

” muombeeni – maghfira – msamaha ndugu yenu, na muombeeni kupewa thabati, kwa sababu muda huu ataulizwa “

➡ Huu ndio muongozo sahihi katika kuwaombea dua maiti wetu baada ya kuwazika.

➡ Na wala hakuna katika uisilamu siku maalumu za kuwaombea dua maiti wa kiisilaamu, wakati wowote muisilamu yoyote anaweza kuwaombea waisilamu waliotangulia katika haki bila kuweka muda maalumu
➡Hakuna katika uisilamu kitu kinaitwa arobaini wala matanga.

➡ Wala haifai kwa mtu yoyote kumkalia msiba mtu aliekufa zaidi ya siku tatu, isipokuwa mke tu kumkalia eda mumewe miezi minne na siku kumi.

Na hii imethibiti katika hadithi sahihi ya mtume s.a.w ambayo imetaja hasa mwanamke ambae mwenye imani ya kumuamini ALLAAH S.W na siku ya mwisho, si halali kufanya hivyo ila kwa kufiliwa mumewe.

➡ Na wala haifai kuweka matanga katika misikiti baada ya kumzika maiti.

➡ Na wala haifai kwa mtu kusafiri masafa marefu kwa ajili tu ya kumpa pole ya kufiliwa mfiwa, ila ikiwa kuna haki ya udugu baina yao.

➡ Na katika sunna ni :
” Jamaa na majirani kupeleka chakula na sadaka mbalimbali kwa wafiwa, ili kuwapunguzia uzito wa msiba na mambo mengine.

➡ Lakini ni ajabu leo kuona baadhi ya jamii za kiisilaamu zinaacha muongozo wa mtume wetu muhammad s.a.w na kuzusha mambo mengine kabisa katika dini.

➡ Wanafanya misiba kama sherehe za furaha badala ya kufanya kuwa ni mazingatio kwa waliokuwa hai.

➡ Na wengine kugawa vinywaji na vyakula kwa waliohudhuria mazishi katika makaburi, wengine wanazika na wengine wanakula na kunywa na kuzungumza pembeni.

➡ Na wengine pia hurudia nyumbani kwa wafiwa na kubakia hapo msibani siku nzima au mbili au tatu, kwa hoja kuwa anataka kuwalizawa wafiwa, anakula vyakula wafiwa na mengine mengi, tena bila ya haki .

➡ Na huenda miongoni mwa mali ambazo zimetumika kuandaa chakula cha matanga ni fungu katika urithi wa warithi, na huenda ikawa ni katika fungu la watoto yatima.

➡ Na mwenye kula mali ya yatima kwa dhulma , basi hao waanakula moto katika matumbo yao moto, na watauingia moto wa saiir.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا)
[Surat An-Nisa 10]

Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni.

➡ Na wala haifai kwa muislamu kula chakula cha msibani au matangani.

➡ Na mwenye kuwalisha watu msibani kwa mali ambayo ni haki ya warithi baada ya kufa ndugo yao atakuwa amefanya dhulma, na wala hapati thawabu kwa kufanya hivyo.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA NANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI
ustadh kuna mama mmoja analea watoto yatima,
na katika dini nimeskia wanasema kuwa : haifai kuwakusanya watoto yatima sehem moja na kuwalea, kinachotakiwa anaeweza achukue mtoto amlee nyumbani.
je ni sawa?

Na kama ikiwa haifai je nini hukmu ya kumsaidia huyo mama msaada kwa kazi hiyo ? 

JAWABU 

➡ Yatima katika binaadamu kisheria ni : ” Kilamtoto ambae amefiwa na baba yake, nae akiwa na umri chini ya baaleghe “

➡ Na Zimekuja katika qurani na sunna dalili nyingi za kisheria zinazo onyesha ulazima wa kuchunga haki za mayatima, na fadhila za kuwalea yatima.

➡ Na wala haifai kuwatenza nguvu wala kuwanyanyasa katika hali yoyote.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ)
[Surat Ad-Dhuha 9]

Basi yatima usimwonee!

➡ Na mwenye kumlea yatima, basi siku ya qiyaama atakuwa pamoja na mtume wetu muhammad s.a.w katika pepo.

➡ Ndugu zangu :
Hii dini yetu ya kiisilaamu haikuleta ugumu wowote katika sheria zake zote.

➡ Ndio maana utakuta kuna aya za qurani nyingi zimeweka baadhi ya sheria bila kuwalazimisha watu kufuata mtindo mmoja tu katika kuitekeleza.

➡ Mfano wa hayo ni suala la waisilamu kushauriana katika mambo yao.

Amesema ALLAAHU S.W :
(وَالَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ)
[Surat Ash-Shura 38]

Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulicho waruzuku wakawa wanatoa,

➡Aya hiyo imetuwekea hukmu ya kisheria katika kufanya waisilamu ushauri katika mambo yao.

Lakini ALLAAHU S.W hakulazimisha watu njia maalumu ya kukaa na kushauriana.

➡ Kutokana na hayo ni kuwa :
Wakikaa watu shura msikitini inasihi.

Wakiwa katika ukumbi maalumu wa shura au mikutano pia inajuzu.

Ikiwa watakutana katika majlisi moja pia ni sawa.

Ikiwa itakuwa shura kwa njia ya simu na mfano wake pia itakuwa ni shura.

➡Hiyo ndiyo raha na wepesi katika sheria za dini yetu, kila jambo tumewekewa wepesi wa kulitekeleza.

➡ Sasa kuhusu yatima kuwaweka sehemu moja kwa ajili ya kuwalea nini hukmu yake?

➡Jambo katika dini halikatazwi , bali huenda ikawa ni bora zaidi katika baadhi ya hali.

➡ Ikiwa wako watu wanaweza kuwalea yatima hao kwa kuchukua kila mtu mfano yatima mmoja nyumbani kwake Inshaallaah hilo ni jambo zuri kabisa.

Lakini kwa sharti :
Ahakikishe anamsimamia na kumtendea haki zake zote kama ipasavyo.

➡ Na kwa kuwa katika karne yetu hii ya sasa kuna sababu nyingi zinasababisha ugumu wa kulea yatima mmoja mmoja katika family , miongoni mwazo ni :

1.Imekuwa si rahisi kupatikana uadilifu wakiwa majumbani tu mwa Watu wanalelewa.

2.Pia kutokana na baadhi ya walezi kuwa na hali ngumu za kimaisha.

3.Kuwepo watu wenye uwezo wa kujitolea mali zao kwa ajili ya kuwalea, lakini kujitolea kwa mikono yao hawawezi kutokana na majukumu yao, au umbali wa sehemu waliyopo.

➡ Hizi zote ni sababu za kukubalika kuwalea mayatima wakiwa katika sehemu moja, kwa lengo la urahisi wa kuwahudumia kwa pamoja, na kupatikana walezi wao na huduma zao nyingine kwa wepesi zaidi.

➡ Pia hata kuwapatia masomo na huduma nyingi wakiwa pamoja ni rahisi kuliko wakiwa mbalimbali, na hii ni kwa mujibu wa kila jamii na mazigira yake.

➡Kwa hiyo sioni hikma yoyote katika kukataza hili wakati uisilamu wenyewe haukukataza na wala hakuna madhara yoyote.

➡ Kwa hiyo kumsaidia huyo mama kwa ajili ya kulea mayatima hao ni jambo muhimu na zuri sana.

➡ Jambo muhimu tu ni kuhahikisha huyo mama amefundishwa na awe na ujuzi wa kujua kila chenye haki na haki yake.

➡ TUSIFANYE DINI KUWA NGUMU.

ALLAAHU AALAMU.

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI: 
Ustadh ntachangia hilo suali kuhusu kukusanywa mayatima, nilisikia kuna watu hukusanya kama hivo ili wasaidiwe wao, lakini wanachopewa wanatumia wao binafsi sio kwa mayatima ?

JAWABU: 

➡ Kuwalea mayatima ni moja miongoni mwa ibada katika uisilamu.

➡ Kwa yoyote mwenye kumlea yatima basi ni lazima afanye ulezi huo kwa nia na ikhlaasw.

➡ Na wala asifanye kazi hiyo ni kama biashara ya kupatia faida yeye za kidunia , au kitega uchumi chake yeye.

➡ Ikiwa jambo hilo ni kama lisemwavyo kwa baadhi ya watu wanadai kukusanya mayatima hao lakini kwa maslahi yao wenyewe, na wala hawatekelezi amana hizo kwa wahusika kama ipasavyo, basi wajue kuwa wao wanakula moto katika matumbo yao.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا)
[Surat An-Nisa 10]

Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni.

➡ Amma akiwa msimamizi wa mayatima hao yeye mwenyewe ni masikini mwenye kuhitajia, na akawa yeye ametoa muda wake mkubwa kwa ajili ya kuwashughulikia yatima hao kwa amana na uadilifu, basi inajuzu kwake Yeye kutumia sehemu katika mali aliyopewa kwa ajili ya mayatima, lakini atumie kwa uadilifu na wala asivue mila Inshaallaah.

➡ Na kama atakuwa yeye mwenye ana uwezo, basi asichukue chochote katika mali za mayatima hao.

➡ Na hayo Amesema ALLAAHU S.W katika QURANI tukufu :

(وَابْتَلُوا الْيَتَامَىٰ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغُوا النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُمْ مِنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُوا إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَأْكُلُوهَا إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَنْ يَكْبَرُوا ۚ وَمَنْ كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَنْ كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ فَأَشْهِدُوا عَلَيْهِمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ حَسِيبًا)
[Surat An-Nisa 6]
Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliye kuwa tajiri naajizuilie, na aliye fakiri basi naale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao washuhudizieni. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu.

➡ Na ni vizuri kwa mwenye kutaka kusaidia yatima ahakikishe kwanza hali ya msimamizihuyo na uaminifu wake kwanza kabla ya kumuamini kumpa mali .

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA NANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:
Tunahitaji darsa kuhusu ihlaswi.


JAWABU

➡ Ikhlaasw ni neno la kiarabu na lina maana kubwa katika makusudio yake.

➡ Miongoni mwa maana zake ni :

1.Usaf na uhalisi:
Amesema ALLAAHU S.W kuhusu uumbaji wa maziwa ambayo rangi yaje ni nyeupe. ..:
(وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُسْقِيكُمْ مِمَّا فِي بُطُونِهِ مِنْ بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَبَنًا خَالِصًا سَائِغًا لِلشَّارِبِينَ)
[Surat An-Nahl 66]

Na hakika katika nyama hoa nyinyi mna mazingatio. Tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, vikatoka baina ya mavi na damu, maziwa safi mazuri kwa wanywao.

➡ Hebu tazama maziwa yalivyotajwa katika uumbaji wake yametokana na kitu gani? Na baada ya kuumbwa yamekuwa vipi?

Tuseme Subhaana llaah ✋

➡Kwa hiyo neno ikhlaasw na khaaliswan yanarudi maneno hayo katika asili moja.

2. Wamesema baadhi ya maulamaa kuwa ikhlaasw ni :
” kumkusudia ALLAAH S.W kwa matendo yote “

3. Na wamesema wengine kuwa :
” ikhlaasw ni : ” Kuacha kutazama waja katika matendo yako, na mtazamo wako uwe kwa muumba peke yake “

4.Na amesema Mtu mwema aitwae Yaa’qub al nakfuuf kuwa :
Mtu mwenye ikhlaasw ni yule ambae, anaficha mema yake kama anavyoficha mabaya yake “

➡ Mara nyingi moyo wa mja huwa unatamani sana kusifiwa kwa mazuri ambayo ameyafanya.

➡ Na miongoni mwa alama za mtu kukosa ikhlaasw ni kama ifuatavyo :

1 – Kupenda kusifiwa na watu.

2 – Kupenda mtu kutangaza amali zake bila ya sababu maalumu za lazima.

3 – Kujiona yeye ndie yuko sawa na wengine wote ni wakosa.

4 – Kujiona kuwa ana amali nyingi sana kuliko wengi katika waja wa ALLAAH S.W.

5 – Kujiona yeye ndie mwenye haki ya kuwakosoa wengine lakini yeye hana haki ya kukosolewa.

6 – Kupenda kujisifu yeye mwenyewe hata kama hakusifiwa na mtu mwingine.

7 – Kuchukia ikiwa atafanya jambo la kheri kisha watu hawakumsifu.

➡ Ziko alama nyingi sana kwa hakika ambazo zinaonyesha kukosa ikhlaasw katika matendo ya waja.

➡ Nakumbusha pia kuwa : ziko amali nyingine za kheri ambazo mtu anaweza kuzifanya kwa siri zikawa baina yake na mola wake tu, basi asitangaze kwa watu amali hizo.

➡ Na pia ikhlaasw hii iko katika sehemu mbili, japokuwa watu wengi wamezoea kuwa ikhlaasw iko katika kufanya matendo mema tu kwa ajili ya ALLAAH S.W.

Sehemu hizo ni :

1.Ikhlaasw katika kufanya matendo mema.
Yaani afanye mema yote kwa ajili ya kutafuta Radhi za ALLAAH S.W.

Amesema ALLAAHU S.W :

(قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَنْ كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا)
[Surat Al-Kahf 110]

Sema: Mimi ni mwanaadamu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.

2.Ikhlaasw katika kuacha maovu.

Yaani mja aache kufanya maasi wakati ana uwezo wa kuyafanya, lakini anaacha kwa ajili ya ALLAAH S.W.

➡ Na hili wengi sana huwa hawalitazami kuwa ni katika ikhlaasw.

➡ Watu wangapi leo wanaogopa na kuacha zinaa kwa sababu ya kuogopa ukimwi? ???

➡Wangapi wameacha wizi kwa sababu ya kuona aibu kwa watu kutokana na umaarufu wao? ???

➡Wangapi leo hii wameacha kusoma elimu za dini kwa sababu mishahara ya walimu wa dini ni midogo? ??

➡Imekuwa dunia kwa watu ni bora kuliko akhera, wakati ALLAAH S.W anasema :
(بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا)
[Surat Al-Ala 16]

Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!

(وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ)
[Surat Al-Ala 17]

Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.

➡ Kumbuka kuwa :
Amali yoyote anayoifanya mja kwa ajili ya watu, basi hatokipwa chochote siku ya qiyaama kutoka kwa ALLAAH S.W.

➡ Na amali hiyo itakuwa sawa na mzoga wa mnyama unukao hata nzi wanaukimbia kwa harufu mbaya.

➡ TUNAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE IKHLAASW KATIKA KAULI VITENDO NA NIA ZETU.

ALLAAHU AALAMU.

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Ibadhi administrator

SWALI: 
Mtu ameowa kakaa muda wa miezi 3 akapata kazi nje ya nchi, akakaa huko muda wa miaka miwili kisha akarudi. ..
je hii ndoa itavunjika ?

JAWABU:

➡ Ndoa katika uisilamu imewekewa nguzo na masharti yake, kwa mujibu wa qurani na sunna.

➡ Na kilichojengeka kupitia qurani na sunna hakuna wa kuweza kukivunja ila kwa mujibu wa qurani na sunna.

➡ ALLAAHU S.W ameweka njia mbalimbali ambazo zinaweza kupelekea kuvunjika kwa ndoa baina ya mume na mke.

➡ Na miongoni mwa njia hizo ni :

1.Talaka :
” Nayo inakuwa ni matamshi kutoka kwa mume au Wakili wa mume, yanayoonyesha kukata ndoa baina yao “

2.Khul’uu :
Nayo ni : ” Mke kutoa fidya kwa kurejesha mahari kwa mumewe ili mume amuache, ikuwa kuna jambo ambalo mke anaona kuwa yeye hawezi kuendelea kuishi tena na mumewe “

3.Faskhu:
“Na hii inakuwa ni kuvunja ndoa baada ya kuwepo au kutokea jambo ambalo linapekekea ndoa kuwa ni batili.

4.iilaa:
” Nayo ni : ” mume kula kiapo kwa ajili ya kumuharamisha mkewe juu ya nafsi yake, kwa kuacha kumuingilia muda maalumu ambao ni miezi minne kwa nia ya kumuharamisha mke “

➡ Ni jambo la ajabu sana kusikia suala kama hili la kuharibika ndoa eti kwa sababu tu mume amesafiri mbali na mkewe Muda mrefu.

➡ Mume kuwa mbali na mkewe muda mrefu haipelekei kuharibika wala kuvunjika ndoa baina yao.

➡ Bali wala haihitajiki kuoana upya tena ikiwa mume atarejea kwa mkewe baada ya muda huo.

➡ Jambo ambalo linapelekea kumuoa upya ni kuwa : Ikiwa alimuacha mume huyo mkewe talaka ya kumrejea, kisha akawa hakumrejea mpaka eda ikamaliza muda wake “
Hapo ndipo atatakiwa kumuoa upya ikuwa atakuwa na haja nae tena.

➡ Kinyume na hivyo ndoa haihitajiki kufanywa upya tena ndoa.

➡ Lakini pia tukumbuke kuwa :
” Ikiwa mume amepotea na hajulikani aliko , au kuna chombo kimezama baharini nae alikuwemo lakini hajulikani uhai wake au umauti wake, katika hali hii atatakiwa mke kupeleka taarifa kwa kadhi au hakimu wa kiisilaamu.

➡ Na taarifa hiyo utamsaidia mje huyo kuweza kuhifadhi haki zake na za mumewe aliepotea.

➡NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUHIFADHI NA ATUONGOZE KATIKA NJIA ILIYO NYOOKA.

ALLAAHU AALAMU.

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI 
Mwanamke anasoma nje masomo ya dini muda wa miaka 4, lakini anarudi kila baada ya miezi 6,
je ukimuowa halafu akarudi kusoma muda kama huo je ndoa itakuepo?

JAWABU.

➡ Naam :
Ndoa itakuwepo kama kawaida, japokuwa mke huyo atakuwa mbali na mumewe.

➡ Na jawabu ya suala hili ni kama suala nililojibu kwa upande wa mume kuwa mbali na mkewe kwa muda mrefu, na tumesema kuwa : ” hili halina athari yoyote katika kuvunja ndoa baina yao “

➡ Isipokuwa kuna mambo muhimu sana hapa yafuatayo :

1.Mwanamke wa kiisilaamu haruhusiwi kisheria kusafiri peke yake safari ndefu, ambazo zinapita umbali wa kuwa mtu yuko katika hukmu ya msafiri ila mwanamke huyo awe na mumewe au mahramu yake.

➡ Na kama itakuwa ni dharura kubwa kwenda kuchukua elimu hiyo, basi wako maulamaa wamejuzisha kusafiri wanawake peke yao lakini kwa sharti wawe ni kundi la wanawake waisilamu wanaoaminika.

2.Kusafiri mwanamke katika nchi ambazo si za kiisilaamu akiwa peke yake kuna khofu kubwa kuharibiwa dini yake na kuvunjiwa heshma yake.

3.Ikiwa mume ana uwezo wa kusafiri na mkewe, na kusoma katika nchi hiyo yeye na mkewe, basi hivyo ni bora zaidi kuliko kuwa peke yake.

4.Pia ni muhimu sana kwa mume au mzazi kujua mazingira anayokwenda kuishi mkewe au binti yake katika siku hizo za masomo.

5.Na ikuwa kutakuwa hakuna haja ya kuchukua elimu kutoka nchi ya mbali, basi ni bora mwanamke asome katika nchi ambazo ziko karibu na mji wake, ili kutunza na kuhifadhi utukufu wake na dini yake.

Pia hiyo iramsaidia kuweza kutekeleza haki za mumewe kwa wepesi zaidi, na pia yeye kupata haki zake kutoka kwa mumewe.

➡ Na miongoni mwa mambo ambayo ni muhimu pia kukumbuka ni kuwa :

Muda wa mume kuwa mbali na mkewe, au mke kuwa mbali na mume, unatakiwa usizidi miezi minne hadi sita tu katika hali ya dharura.

➡ Kuna baadhi ya hali za kinafsi zinaweza kumfika mmoja wao, akajikuta amefanya kitendo cha kinyama wakati yeye ni binaadamu.

➡ Watu wangapi wameingia katika kufanya maasi kama ya zinaa na liwati na ubakaji katika vipindi ambavyo utakuta wako mbali na wake zao???

➡Na wanawake wangapi ambao wana waume zao, lakini kwa kuwa mbali na waume zao wamejikuta wakifanyiwa kuingiliwa na wanaume wa haramu katika njia za nyuma ili kukidhi matamanio hayo ya kujinsia? ??

➡Na wanawake wangapi wameamua kukidhi matamanio yao ya kujinsia wao kwa wao, kwa kusagana tupu zao, au kutumia vidole na kuchezeana tupu zao mpaka kila mmoja atoe shahwa zake? ???

➡Na vijana wangapi wa kiume leo wamekuwa na matamanio, na wakawa hawajaoa bado, nao wakaamua kujitoa manii yao kwa kutumia mikono yao kusugua tupu zao? ??

➡Haya yote ni katika madhambi makubwa na madhara pia kidini, afya na kijamii.

➡ Ili kuondoa yote hayo ni lazima kwa kila mwenye kutimiza uwezo wa kuoa na aowe.

➡ Na kila mwenye kuwa na mke au mume basi ajitahidi kuwa karibu na mwenzake, ili kuweza kusitiriana, kwa sababu kila mmoja ni stara kwa mwenzake.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَكُمْ وَأَنْتُمْ لِبَاسٌ لَهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَخْتَانُونَ أَنْفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنْكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنْتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ)
[Surat Al-Baqara 187]

Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate kumcha.

➡ Ikiwa hao wameambiwa kuwa walikuwa wakizikhini nafsi kwa sababu tu ya kuzuiliwa kustarehe na wake usiku mmoja katika mwezi wa Ramadhani, vipi itakuwa kwa hao wanakaa mbali na wake zao miaka minne na mfano wake? ??

➡NAMUOMBA ALLAAH S.W AJAALIE MAPENZI NA HURUMA BAINA YA WANA NDOA WOTE.

NA AMBAO BADO BASI ALLAAH AWAJALIE WAPATE NA WAO YALIYOKUWA MAZURI KWAO.

ALLAAHU AALAMU.

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI.
Ustaadh naomba ufafanuzi kuhusu Kuvaa mwanamke ma jeans.
Wako masheikh wanasema inafaa vipi inakuwa hili suala ?

JAWABU.

➡ Asili ya kitu kuharamika au kuhalalika ni kwa mujibu wa dalili za kisheria, au kuwepo madhara ambayo yansingia katika jumla ya kukatazwa katika sheria.

➡ Asili ya mavazi amesema ALLAAH s.w :
(يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنْزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ)
[Surat Al-Araf 26]

Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za uchamngu ndio bora. Hayo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu mpate kukumbuka.

➡ Na akasema baada ya hapo :
(قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ)
[Surat Al-Araf 32]

Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.

➡ Vazi la suruali tumeshawahi kubainisha hukmu yake kwa upande wa mwanamke kisheria katika zilizotangulia, Khulaswa yake ni kuwa :

1. Ikiwa mwanamke atavaa suruali ya kike ndani ya nguo nyingine, Inshaallaah hakuna tatizo katika hilo.

2. Anatakiwa katika hali hiyo mwanamke kuacha suruali ambayo itamsababishia kuonekana mipaka ya mwili wake na uzuri wake wa maumbile ya mwili.

3.Kisha suruali isiwe na mapambo ambayo yanaonekana na nje.

➡ Kwa hiyo ikiwa jinzi hiyo itakuwa haina moja katika mambo ambayo tumeyataja hapo, basi hakuna tatizo kuvaa mwanamke kwa ajili ya stara ya mwili wake maumbile yake.

➡ juu ya hilo nakumbusha kuwa : ” Ni lazima afunike na kusitiri suruali yake hiyo anapotembea au kukaa, na wala asiache wazi kwa watu inaonekana, kwa sababu hiyo ni katika nguo zake za mapambo.

➡ Amma kuharamika moja kwa moja ni jambo hatuwezi kusema, lakini hukmu itakuwa kwa namna ya hali ya nguo ilivyo na mvaaji na uvaaji wake.

➡ Na kuacha kuvaa jinzi ni bora kuliko kuvaa.

➡ Na hasa jinzi ni vazi lenye athari kubwa hata kiafya.

Ni bora kuvaa suruaki nyingine ambazo hazina shubha yoyote ndani yake.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUNUSURU NA MADHAMBI AINA MBALIMBALI.

ALLAAHU AALAMU.

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI
Naomba kuuliza, Yule kondoo alie mchinja mtume badala ya mwanae alfanywa nini? Alitolewa sadaka au Aliliwa?
na kama Aliliwa walio Kula Akina nani?naomba kujua ?

JAWABU

➡ Kwa mujibu wa suali hili inaonyesha anakusudia muulizaji kuhusu Nabii Ibraahiim a.s alipoamrishwa kumchinja mwanae Ismail.

➡ Kuchinja ni moja ya ibada ambazo mja anajikurubisha kwa ALLAAH S.W ikiwa atachinja kwa ajili yake s.w

➡Amesema ALLAAHU S.W kumwambia mtume wake s.a.w :
(قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ)
[Surat Al-Anaam 161]

Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

(قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ)
[Surat Al-Anaam 162]

Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.

➡ Nabii Ibraahiim a.s alikuwa ameshakuwa tayari kutekeleza amri hiyo ya ALLAAH kwa mwanae, na mwanae pia alikuwa tayari kutekelezewa amri hiyo, baada ya hapo ALLAAH S.W akampa fidya kwa kumletea kondoo badala ya kumchinja mwanae.

➡ Muhimu katika suali hili, jawabu ni kuwa :

1.Hakuna dalili yoyote niliyoikuta inaonyesha jinsi gani Nabii Ibraahiim a.s aligawa nyama hiyo baada ya kumchinja kondoo huyo.

2.Wala hakuna dalili yoyote ya kuonyesha kondoo huyo alikuwa ana rangi gani, wala uzito wa kilo ngapi, wala kuonyesha kuwa alikuwa ni dume au jike .

➡ Ndio maana ALLAAH S.W ametaja mnyama kwa Sifa maalumu tu kwa kusema :
(وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ)
[Surat As-Saaffat 107]
Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.

3.Kisha Nabii Ibraahiim a.s alikuwa ni mkarimu kwa watu wote, na mfano mwema katika umma na kaumu yake pia.

Bila shaka atakuwa aligawa sehemu katika nyama hiyo baada ya kuchinja, na fungu la watu wake pia hakuwasahau.

➡ Na hivyo ndivyo alivyokuwa pia mkewe Nabii Ibraahiim a.s.

➡ Tazama aya zifuatazo :

(وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَنْ جَاءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ)
[Surat Hud 69]
Na wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema: Salama! Naye akasema: Salama! Hakukaa ila mara akaleta ndama wa kuchoma.

➡ Na nyama hiyo iliyochomwa alikuwa ameiandaa mje wa Nabii Ibraahiim a.s, jana ilivyokuja katika aya nyingine :

(فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ)
[Surat Adh-Dhariyat 26]
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.

(فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ)
[Surat Adh-Dhariyat 27]

Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?

➡ Ukaribu kwa watu ndiyo ilikuwa sunna ya mitume yote a.s, kinyume na waisilamu wengi wa zama hizi.

4.Pia tunakuta katika qurani kuwa ALLAAH S.W amemuamrisha mtume Muhammad s.a.w kufuata mila ya Nabii Ibraahiim a.s katika mambo mengi sana.

Amesema ALLAAHU S.W :
(ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ)
[Surat An-Nahl 123]

Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

➡ Na tunakuta katika qurani tumeamrishwa baada ya kuchinja basi nyama hiyo tuwalishe watu maalumu ambao wenye sifa ambazo amezutaja ALLAAH S.W kwa kusema :

(لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُمْ مِنْ بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ)
[Surat Al-Hajj 28]

Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri.

➡ Na akasema pia :
(وَالْبُدْنَ جَعَلْنَاهَا لَكُمْ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ ۖ فَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهَا صَوَافَّ ۖ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرْنَاهَا لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ)
[Surat Al-Hajj 36]

Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni kudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu; kwa hao mna kheri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanapo simama kwa safu. Na waangukapo ubavu kuleni katika hao na walisheni walio kinai na wanao lazimika kuomba. Ndio kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru.

➡ Amma kuwaju watu waliokula kondoo huyo kwa majina yao hao watu, au walikuwa ni wanaume au wanawake, au wanaume wangapi na wanawake wangapi, au mengine katika undani wake, hilo jambo halina umuhimu kuijua, na wana hakuna dalili wala faida katika kulijua hilo.

➡ Lengo ni kutekeleza yale ambayo yamekusudiwa katika kisa miongoni mwa mazingatio na mafundisho.

➡ TUNAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE SIFA YA UKARIMU NA KUPENDA KHERI KWA NDUGU ZETU PIA.

ALLAAHU AALAMU.

SHEIKH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habs

SWALI: 
Napenda kuliza, Mtu Akifanya kazi kama hoteli Au seheemu ina ulevi nini hukmu yake ? 

JAWABU: 

➡ Ndugu zangu : 
ALLAAHU S.W ameamrisha watu wote  kuwa wale katika vilivyo kuwa vimechumwa kwa njia za halali.

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 

  (يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ)
[Surat Al-Baqara 168]

Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za Shet’ani. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhaahiri.

➡ Na bila shaka kufanya biashara ya kuuza pombe au katika kitengo ambacho kinauza yaliyokuwa ni haramu pia kazi hiyo ina haramu katika kwa mujibu wa kitengo hicho.

➡ Haifai kufanya kazi katika kiwanda cha pombe wala sigara na mfano wake. 
➡ Wala mwanamke kufanya kazi za kuhudumia wanaume katika mahotel na kuchanganyika na wanaume waliokuwa Haramu kuchanganyika nao. 

➡ Wala haifai kwa mwanamke kuvaa viguo vifupi eti kwa kisingizio kuwa ndio nguo za kazi walio amrisha na wakuu wao wa kazi au sheria za nchi zao. 

➡ Na mwenye kumcha ALLAAH S.W basi ALLAAH S.W atampa riziki kwa njia ambazo hakuzidhania kabisa. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W 
…وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا)
[Surat At-Talaq 2]

..  Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea.

(وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا)
[Surat At-Talaq 3]
Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.

➡ Na kwa nini iwe kwa mwanamke wa kiisilaamu kufanya kazi kama hizo wakati wanawake hasa wametakiwa kukaa majumbani mwao na wala si kutoka toka kila mara. ?!

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 

(وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا)
[Surat Al-Ahzab 33]

Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt’iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara.

➡ Na mwenye kuacha kitu kwa ajili ya ALLAAH S.W,  basi ALLAAH humjalia mtu huyo kitu kingine kilichokuwa ni bora kuliko hicho alichokiacha. 

➡ Mwenye kuwa alifanya kazi kama hivo au hadi sasa anafanya kazi hizo,  basi ni lazima  watubie kwa ALLAAH S.W. 

➡ Na wale wenye Magari yanayokodishwa kubeba pombe au sigara pia ni lazima kazi hiyo waiche mara moja. 

➡ Na pia wanaokodisha Magari yao kwa ajili ya kutangazia wanamuziki au michezo iliyoharamishwa na ALLAAH S.W ni lazima watubie na kuacha haraka. 

➡ Na pia wenye kukodisha majumba yao kwa wenye bank za riba nao watubie kwa ALLAAH S.W. 

➡ Na wanaofanya kazi za ulinzi wa kulinda maduka ya pombe au mambo ya haramu pia lazima watubie haraka kabla ya kufikia siku ambayo amesema ALLAAH s.w. ….:
(هَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا أَنْ تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنْفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِنْ قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ انْتَظِرُوا إِنَّا مُنْتَظِرُونَ)
[Surat Al-Anaam 158]

Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATURUZUKU TOBA KABLA YA KUPITA MUDA WAKE. 

ALLAAHU AALAMU. 


SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Mume wangu tokea  anioe hajalala hata siku moja kwa mke yeyote, mimi kwake  ni mkewe wa tatu.. 
Yupo kwangu tu mimi. nikimwambia ananiona sijui sheria na mimi nilitaka kuolewa na yy kwa vile nitapata zamu kupumzika matokeo nimemchoka becouse kaniganda kwa mambo yote, wake zake wananitishia amani nikimwambia ananimbia yngu yaache shughulika na yako. 
Istoshe wananitumia msg za kashfa kwa kweli sina Amani ya mume.

JAWABU

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Huyo mume anaebakia zamu kwa mke wa tatu na kuwaacha zamu ni kuwa : 
Huyu wa kwanza ambae alizaa nae watoto alihama chumba eti kwa sababu mumewe  kaoa. 

Na wapili anaishi pemba. anasema hana pesa hana kazi kwahilo hawezi kuenda zamu huko. 
kubwa zaid alifiwa na mwanawe aliezaa na mume mwengine pia hajaenda mpaka leo ni mwezi watatu 

JAWABU 

➡ Subhaana LLAAH : 
Ndugu zangu ikiwa mume anataka kuongeza mke wa pili au wa tatu au wa nne,  ni lazima azingatie mambo muhimu yafuatayo : 

1⃣Uwezo wa kumiliki kuidhibiti nafsi isielekee kupenda  upande mmoja mapenzi ya kuzidi mpaka ikawa ni jambo la wazi kabisa. 

Amma ndani ya nafsi tu inawezekana kuwa mume nafsi yake ikawa inampenda zaidi kindani kuliko mwingine,  lakini hiyo ni mapenzi ya ndani ya nafsi tu bila kudhihirisha wala kudhulumu upande mwingine. 

➡ Na hili jambo ni la kimaumbile ya nafsi ya kila mmoja,  hata mzazi kwa wanae hutokea hili ndani ya nafsi ikawa mmoja katika watoto wake anaona ni bora zaidi kuliko mwengine. 
➡ Na hili ndilo jambo ambalo ALLAAH S.W amesema kuwa uadilifu huo kwa wake zetu hatutouweza – Yaani kuifanya nafsi iwe sawasawa katika kiwango cha mapenzi ya ndani ya nafsi,  hilo hakuna anaeliweza. 

➡ Lakini linatakiwa hilo libakie ndani ya nafsi wala lusidhihirishwe,  na wala lisiwe sababu ya kudhulumu wengine. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَلَنْ تَسْتَطِيعُوا أَنْ تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِنْ تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا)

[Surat An-Nisa 129]
Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamngu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu.

➡ Kuhusu kuwa mke mmoja yuko pemba na yeye hana uwezo wa kwenda huko,  hiyo si sababu wala hoja ya kumfanya asiende huko kwa mkewe wala kutimiza zamu kwa mwenye haki yake. 

➡ Yeye anajua uwezo wake wa ki uchumi ulivyo kwa nini awaweke wake zake katika umbali huo ambao hawezi kuwaendea katika zamu kwa urahisi? 

➡Ni lazima afanye mbinu yoyote ili kuwaweka wote katika maeneo ya karibu,  kwa namna ambayo ataweza kufanya zamu kwa wote kwa wepesi. 

➡ Na amma kuwa hakwenda msibani baada ya kufiliwa na mtoto ambae ni wa mkewe kwa mume mwingine wa mwanzo,  hilo si kosa kubwa ikiwa alikuwa hana uwezo wa nauli kuja katika mazishi. 

➡ Na kuhudhuria mazishi ni faradhi ya kifaya :
” yaani wakihudhuria baadhi ya waisilamu tu inatosheleza,  na wala ambao watakuwa hawakuhudhuria hawatokuwa na kuwa na dhambi yoyote. 

➡ Lakini kuhudhuria yeye kwa mkewe kwa kutekeleza zamu yake katika haki ya mkewe :
Hilo jambo ni wajibu juu yake kulifanya. 

Na wala hakuna mtu mwingine wa kufanya jambo hili badala yake. 

➡ Na huyu mume alikuwa hakutumia hikma wala busara katika kuongeza idadi ya wake hao wakati hana uwezo,  kisha anawaweka mbali kiasi hicho wakati yeye ni masikini hana uwezo wa kwenda huko. 

➡ Huyo mume amedhulumu nafsi yake na amedhulumu wake zake ambao haendi katika zamu zao. 

➡ Na ikiwa hakujirekebisha katika uhai wake atakufa hali ya kuwa ana madhambi juu yake. 

➡ Na hii ndio natija  ya mtu kufanya mambo bila ya kumuomba ALLAAH uchaguzi wa lililokuwa na kheri,  wala hakuwashauri wenye kuwa na ujuzi katika hili ili wamshauri ushauri wenye faida na maslahi kwake na wengine. 

➡ Sasa ni wajibu kwa huyo mume atafute mbinu zote za kufanya ili aweze kufika katika zamu za wake wengine. 

➡ Na ni wajibu afanye kazi ili kupata uwezo wa kumiliki kutekeleza hayo,  asikae tu na kusema yeye masikini hana uwezo,  wakati ana nguvu za kufanya kazi. 

➡ Pia namshauri amuhamishe mke alie mbali nae amuweke karibu nae ,  hata ikiwezekana katika nyumba moja akawaweka wote wawili na kuishi nao. 

➡ Na kama itakuwa hakuweza yote hayo,  basi ni bora agawe zamu kwa idadi ya wiki moja moja kila mke,  ili ndani ya wiki moja aweze kutafuta cha kumuwezesha kwenda kwa mke mwingine huko aliko. 

➡ Kwa hakika huu ni mtihani mkubwa sana kwa baadhi ya waume wasiofifikiria kabla ya kufanya jambo. 

➡ Hatua ya mwisho kabisa ni kuwa : 
” Ikiwa ameshindwa kuwatekelezea haki zao wake zake hao au baadhi yao,  wake waliokuwa hawapati haki zao wanao uwezo wa kumshitaki kwa kadhi,  na kadhi ana haki ya kumtenganisha baina yake na wake zake au baadhi yao kwa kushindwa kutekeleza haki zao. 

➡ Na mara nyingi wanaume wengi hudanganyika na baadhi ya visa ambavyo watu huvieneza na kudhania kuwa ni hadithi sahihi,  Kumbe ni hadithi za kutunga tu. 

➡ Na miongoni mwazo ni : 
” Inahadithiwa kuwa : ”  swahaba mmoja aliekwenda kwa mtume s.a.w kumshitakia kuwa ana mke mmoja lakini maisha ni magumu saba,  mtume s.a.w akamwambia :
“Ongeza mke mwingine “
Akaongeza wa pili,  maisha yakazidi kuwa magumu, : akashitaki tena kwa mtume s.a.w,  akamwambia:
” Ongeza wa tatu ” hivo hivo mpaka akatimiza wanne na maisha yake yakawa mazuri “

➡ Hii habari ni uongo na uzushi mtupu wala hakuna ukweli wowote katika hili. 

➡ Wala haiwi kwa mtume s.a.w kumshauri mtu huyo ushauri kama huo,  wakati Qur’an imeweka sharti la mtu kuwa na uwezo. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA TUWEZE KUTAFUATA. 

ALLAAHU AALAMU. 

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI


Nauliza:
niko safarini imenikuta sala, lakini sikuweza kusali kwa vile niko njiani,  mpaka ikanikuta sala nyengine. sasa je ipi iloniwajibikia zaidi ilonipita au ya wakati ule niisali  mwazo???  

JAWABU 

➡ Sala za faradhi zimewekewa muda wake maalumu na ALLAAH S.W katikaQURANI tukufu,  na pia katika sunna za mtume s.a.w. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنْتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَوْقُوتًا)
[Surat An-Nisa 103]

Mkisha sali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala. Na mtapo tulia basi shikeni Sala kama dasturi. Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu.

➡ Na wala haifai kwa muisilamu yoyote kuchelewesha sala hata muda wake ukapita,  ila katika moja ya hali zifuatazo : 

1.Ikiwa muislamu amesahau sala kabisa katika muda wake hakukumbuka. 

Huyo anakuwa hana dhambi kwa kuchelewa kwake kwa sababu kusahau ni udhuru ambao uko juu ya uwezo wake. 

2.Ikiwa amelala na usingizi ukamchukua wala hakuzindukana ila baada ya kupita muda wa sala. 

Huyo anakuwa hana dhambi kwa kuchelewa kwake kwa sababu usingizi wake wakati amelala ulikuwa  ni udhuru ambao uko juu ya uwezo wake. 

3.Msafiri ambae yuko safarini njiani,  au msafiri ambae yuko yuko katika mji tayari,  lakini mji huo si mji wake. 

➡ Amma kinyume na hali hizo hakuna ruhusa kwa muisilamu kuchelewesha sala yake,  ila ikiwa kuna hali ambayo inakubalika kisheria zaidi ya hizo nilizozitaja mwanzo, 
Kama vile : 
Kutokwa na akili kwa wazimu au maradhi .

➡ Msafiri anatakiwa kuswali sala zote tano kama ilivyokuwa kwa aliekuwa msafiri. 

➡ Lakini juu ya hivyo,  msafiri anaruhusiwa kuchanganya sala mbili katika muda mmoja kati ya mida miwili ya sala hizi katika njia mbili hizi :

1.Anaweza kuchelewesha adhuhuri mpaka muda wa alasiri,  kisha akaziswali pamoja katika muda wa alasiri. 

2.Au anaweza pia kutanguliza alasiri katika muda wa alasiri,  akiswali adhuhuri na alasiri kwa pamoja katika muda wa adhuhuri. 

➡ Kwa hiyo wewe msafiri katika safari yako umefanya makosa makubwa kwa kuchelewesha sala ya adhuhuri na alasiri mpaka ukaingia muda wa magharibi. 

➡Unatakiwa utubie kwa ALLAAH S.W kwa kosa hilo.

➡ Kisha uzilipe sala zote hizo kwa mpangilio wake kama zilivyo,  kwa sababu sala zote hizo ni wajibu kwako,  Hakuna iliyokuwa wajibu na nyingine wajibu zaidi,  bali zote ni wajibu. 

➡ Na kwa kuwa uliacha kuziswali bila udhuru wa kisheria,  utatakiwa kuzilipa kama kwa idadi ya rakaa kama  unavyoswali ukiwa mkaazi katika mji wako. 

Hii ni katika hali ambayo ukiwa tayari umefika katika mji ambao unsishi.

➡ Amma ukiwa uko katika safari bado,  au uko katika mji ambao wewe hapo ni mgeni si mkaazi,  utatakiwa kulipa sala ya adhuhuri na alasiri kila moja kwa rakaa mbili mbili. 

Kisha baada ya hapo utaswali sala ya magharibi ambayo ndio wewe katika muda wake wakati huo. 

➡ Ikiwa uko safarini na umeshindwa kuswali kwa kawaida,  basi unatakiwa uswali kwa kadri utakavyoweza,  muhimu uswali ndani ya wakati ambao unaruhusika kuswali. 

➡ Hata ukiswali kwa kukaa au kwa kusimama  pia yote ni kwa mujibu wa hali ikiyokufika. 

Muhimu usicheleweshe sala tu hata muda ukatoka. 

➡ Ndio maana ALLAAH S.W ameamrisha hata katika hali ya hofu za kivita,  basi watu hata kama kwa kutembea  au juu ya vipando vyao. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّهِ قَانِتِينَ)
[Surat Al-Baqara 238]

Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea).

(فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنْتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُمْ مَا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ)
[Surat Al-Baqara 239]
Ikiwa mnakhofu (Salini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapo kuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu kama alivyo kufunzeni yale mliyo kuwa hamyajui.

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUFANYIE WEPESI KATIKA KUMUABUDU,  NA ATUSAMEHE MAKOSA YETU. 

ALLAAHU AALAMU. 

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

SWALI
NENO INSHAALLAH  LIKO MARA  NGAPI  KTK QURUAN?NA KWA NINI TUNAAMBIWA KILA MARA TUSEME INSHAALLAH ?

JAWABU 

➡ Neno Inshaallaah katika qurani limetajwa katika matamshi ya miundo ya tofauti katika aya nyingi. 

➡ Ziko aya zilizotaja kwa kusema ” illaa an yashaa’a Llaah “

Na ziko zioutaja
” Maashaallaah “

Na ziko pia zilitaja 
“Maashaallaah “

➡ Ama kutajwa kwa neno
”  Inshaallaah” utakuta katika sehemu nne tu katika qurani,  kwa kiasi kinacho nihudhuria katika kumbukumbu ya qurani,  unaweza kurejea na kuhskikisha zaidi hata kwa njia ya compute au mfano wake Inshaallaah,  kwa sababu hifdhi ya binaadamu inaweza ikafikwa na kusahau. 

1.ya kwanza : 

(قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّنْ لَنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّهُ لَمُهْتَدُونَ)
[Surat Al-Baqara 70]

Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni yupi? Hakika tunaona ng’ombe wamefanana. Na kwa yakini, Inshaallah, Mwenyezi Mungu akipenda, tutaongoka.

➡ Hiyo ni katika munasaba wa Banii israa ila kuchinja ng’ombe walieamrishwa,  wao wakaleta maswali mengi na mwisho ikawa ng’ombe wa aina ile wakawa  hawampati ndio maana wakakumbuka kusema ” Inshaallaah “

➡ Na kama wasingefanya hivyo basi wasingempata. 

2.Ya pili ni : 
(فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَبَوَيْهِ وَقَالَ ادْخُلُوا مِصْرَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ آمِنِينَ)
[Surat Yusuf 99]
Na walipo ingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, Inshallah, mmo katika amani.

3.Ya tatu ni : 

(قَالَ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ صَابِرًا وَلَا أَعْصِي لَكَ أَمْرًا)
[Surat Al-Kahf 69]
Akasema: Inshaallah, Mwenyezi Mungu akipenda, utaniona mvumilivu, wala sitoasi amri yako.

Nabii Musa alisema hivyo katika kutafuta Elimu kutoka kwa mja wa ALLAAH. 

4.Ya nne ni : 
(قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنْكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَنْ تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ ۖ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِنْدِكَ ۖ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ ۚ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّالِحِينَ)
[Surat Al-Qasas 27]

Akasema: Mimi nataka kukuoza mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane. Ukitimiza kumi, khiari yako; lakini mimi sitaki kukutaabisha. Inshallah utanikuta miongoni mwa watu wema.

Alisema mja mwema ambae alimuozesha binti yake kwa Nabii Musa baada ya kufanya kazi kwake katika mji wa Madyana. 

5.Ya tano ni : 
(فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانْظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّابِرِينَ)
[Surat As-Saaffat 102]

Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.

Hayo alisema Nabii Ismail baada ya kuambiwa na  baba yake kuwa ameamrisha na ALLAAH S.W amchinje. 

6.Ya sita ni : 
(لَقَدْ صَدَقَ اللَّهُ رَسُولَهُ الرُّؤْيَا بِالْحَقِّ ۖ لَتَدْخُلُنَّ الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ آمِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَ ۖ فَعَلِمَ مَا لَمْ تَعْلَمُوا فَجَعَلَ مِنْ دُونِ ذَٰلِكَ فَتْحًا قَرِيبًا)
[Surat Al-Fath 27]


Hakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah, kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele. Hamtakuwa na khofu. Yeye anajua msiyo yajua. Basi atakupeni kabla ya haya Ushindi karibuni.

➡ Hizo ndio idadi ambazo nimejaaliwa na ALLAAH S.W  kuzikumbuka kwa muda huu kuhusu neno ” Inshaallaah ”  insahaah. . 

➡ Na hikma katika kuamrishwa kusema ” Inshaallaah ”  ni nyingi sana. 

Miongoni mwa hikma hizo ni : 

1.Kumtaja ALLAAH S.W kila wakati na hiyo ni moja miongoni mwa njia za kumtaja. 

2.kudhihirisha utukufu wa ALLAAH S.W juu ya waja,  na kudhihisha  udhaifu wa mja kwa mola wake. 

3.Kukiri kuwa sisi hatuna uwezo wa kufanya lolote ila idhini llaa ya ALLAAH S.W. 

4.Ushindi katika mambo yote ni katika kumtaja ALLAAH S.W kwa kumtaja ALLAAH S.W. 

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUJAALIE KUMTEGEMEA YEYE KWA TAWFIQ yaje. 

➡ ALLAAHU AALAMU. 

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Aslkum warahmatullah wabarakatuh suali langu nini hukmu ya muajiriwa ktk kuuza duka ambalo lina fanaka mbali mbali ikiwemo na ulevi ndani yake.

JAWABU 

➡ Kwanza kabisa neno
” fanaka ” katika suali hili nadhani muulizaji anakusudia “nafaka ” yaani aina fulani za mazao au bidhaa .

➡ Biashara yoyote ambayo imekusanya vitu ambayo vimehalalishwa kisheria hiyo ni biashara halali na inakubalika kisheria. 

➡ Amma ikiwa atatia bidhaa ya haramu katika duka lenye bidhaa za halali,  na ikawa kila kimoja kimejitenga na kingine,  yaani kiko sehemu yake,  kikichokuwa haramu kutakuwa haramu kwa nafsi yake chenyewe,  na kikichokuwa halali kutakua halali kwa nafsi yake chenyewe. 

➡ Amma vikichanganyikana vikawa katika kitu kimoja,  mfano chupa ya juice ya matunda,  nusu yake ni juice na nusu yake ni pombe,  hapo itakuwa inaharamika  yote kamili,  wala huwezi kusema kuwa hapa haramu ni pombe tu peke yake. 

➡ Au katika gari la abiria mfano,  Dereva amepakia abiria,  na amepakia pia mzigo wa chupa za pombe au ulevi wa aina nyingine,  itakuwa amechanganya mambo mawili pamoja,  kwa hiyo malipo anayolipwa kwa ajili ya pombe ni haramu,  na malipo kwa ajili ya abiria ni halali. 

➡ Na ikiwa mali yake atachanganya yote pamoja ya halali na haramu,  atakuwa katika aina ya utata mkubwa katika uhalali wa mali yake au Uharamu wake. 

➡ Mwenye kutaka malipo ya Akhera basi asichanganye halali na haramu katika miamala yake. 

➡ Na anatakiwa Atubie kwa ALLAAH S.W na wala asifanye kazi katika sehemu kama hizo zenye mchanganyiko wa halali na haramu. 

➡ Na mara nyingi sana utakuta mali za watu kama hao mali zao za haramu ni nyingi zaidi kuliko halali,  au zina changanyika na kusababisha kuharamika yote , au kuwa katika hali ya shaka katika uhalali wa mali yote. 

➡ Na miongoni mwa malizenye mchanganyiko wa haramu miongoni mwa jamii nyingi ni kama ifuatavyo:

1.Kukodisha nyumba kwa benk zenye kutoa Riba. 

2.Gari la abiria au mizigo  kubeba ulevi au vikundi vya Ngoma na mfano wake. 

3.Mafundi wa nguo kuwashonea wanawake nguo za kuwabana wanawake ambao wanakwenda kuvaa nguo hizo nje kwa wanaume wasiofaa kuona miili yao. 

4.Duka la bidhaa za kawaida kuchanganya na bidhaa haramu kana pombe au ulevi wa aina nyingine. 

5.Kuuza cd au dvd za qurani na mihadhara hali ya kuwa zimechanganyika na za nyimbo au sinema  chafu. 


6.Kufanya kazi ya ulinzi katika mahotel yenye baa na madanguro ya maasi. 


7.Kutia miziki na mfano wake katika simu za watu kwa kutumia kompyuta 
(Computer ) .

8.Kuwapamba maharusi kwa kuwachonga  nyusi na kuwaunga nywele.

9.Mpinga picha au video kuwachukua picha wanawake katika hali ya kuwa stara hawana ,  au wakiwa katika maharusi na sherehe mbalimbali wanacheza na kukata viuno. 

10.Kuuza masanamu yaliyochongwa kwa miti au mawe au kunakishiwa. 

➡ Yote hayo ni miongoni mwa mambo ambayo jamii inayachukulia kama ni ya kawaida tu,  Kumbe yana athari mbaya katika amali zao,  na kuwa na Uharamu ndani yake. 

➡ Kazi yoyote iliyochanganyika na haramu haifai kuifanya,  hata kama kama itakuwa asili yake ni halali. 

➡ Ndio maana hadithi ametuambia mtume s.a.w : 

  لعنَ اللَّهُ الخمرَ وشاربَها وساقيَها وبائعَها ومبتاعَها وعاصرَها ومعتصرَها وحاملَها والمحمولةَ إليهِ
الراوي: عبدالله بن عمر المحدث: ابن الملقن       – المصدر: خلاصة البدر المنير – الصفحة أو الرقم: 2/319
خلاصة حكم المحدث: إسناده جيد

” Ameilani ALLAAH pombe,  na mwenye kuinywa,  na mwenye kunywesha, na mwenye kuuza,  na mwenye kununua,  na mwenye kutengeneza,  na mwenye kutengenezewa, na mwenye kubeba na mwenye kubebewa “

➡ Na pia amesema : 

لعنَ اللهُ الربا ، وآكلَهُ ، وموكِلَهُ ، وكاتِبَهُ ، و شاهِدَهُ ، وهم يعلمونَ ، والواصِلَةَ ، والمسْتَوْصِلَةَ ، و الواشِمَةَ ، والمستوشِمَةَ ، والنامِصَةَ ، والمتنمِّصَةَ
الراوي: عبدالله بن مسعود – المصدر: صحيح الجامع – الصفحة أو الرقم: 5094
خلاصة حكم المحدث: صحيح

Ameilani ALLAAH S.W Riba,  na mwenye kuila,  na mwenye kumlisha mwingine,  na mwenye kuandika – mkataba wa riba – na mwenye kushuhudia hali ya kuwa wanajua,  na mwenye kuunga nywele zake kwa nyingine,  na mwenye kuungwa nywele,  na mwenye kuchora kwa moto, na wenye kuchorwa,  na wenye kuchonga nyusi “.

➡ Hizi ni miongoni mwa kazi za haramu ambazo jamii ndio zimefanya kuwa ni chumo la maisha yao,  Kumbe ni chumo la haramu,  na ni njia za kupatia laana. 

➡ Baraka zitatoka wapi wakati laana zimejaa kila upande? !

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE KUTAFUATA YA HALALI NA ATUBARIKIE NDANI YAKE. 

ALLAAHU AALAMU. 

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

SWALI 


Mume ameoa mke wa pili kwa siri bila mke wa mwanzo  kujua,  na makubaliano ya mume na mke wa pili ni kuwa atakuwa anakwenda zamu mchana tu usiku atakuwa kwa mke wa mwanzo. 

Sasa hivi  mume anakwenda kulala zamu kwa mke huyo wa pili,  na ambae ana mtoto mmoja je hivyo ni sawa? 

JAWABU

➡ Ndugu zangu : 
Ndoa ni katika moja ya ibada muhimu sana katika uisilamu,  na ndio siri ya kupata utulivu na amani katika nafsi,  miili na jamii nzima. 

➡ Na ndoa inatakiwa itangazwe na watu wajue kuwa fulani ameoa,  na kutangaza ndoa ni katika sunna muhimu sana. 

➡ Amesema mtume s.a.w : 
أعلِنوا النِّكاحَ
الراوي: عبد الله بن الزبير المحدث: ابن حبان     – المصدر: صحيح ابن حبان – الصفحة أو الرقم: 4066
خلاصة حكم المحدث: أخرجه في صحيحه

➡ Amepokea Abdullah bin zubair r.a,  kutoka kwa mtume s.a.w amesema : 
” Tangazeni ndoa. ..”

➡ Na hiyo ni hadithi sahihi Ameipokea imaamu Ibnu hibbaan na wengine. 

➡ Na kutangaza ndoa si katika ndoa ya kwanza anayoowa mtu kwa mara ya kwanza katika uhai wake, 
Bali hata kama mtu anaoa mke wa pili au wa tatu au wa nne ni sunna kutangaza ndoa yake. 

➡ Na kuna faida kubwa katika kutangaza ndoa,  na ikiwa itafichwa pia kuna madhara yake makubwa. 

➡ Huyo mume alieowa kwa siri na kumficha mkewe kwa hakika hakufanya jambo zuri,  japokuwa ndoa yake ni sahihi na imetimia na wala haina kasoro yoyote katika kusihi kwake,  midhali walii na mashahidi na mahari na ridhaa ya mke pia vimetimia. 

➡ Na kugawa zamu kwa mke wa wa pili mchana tu ikiwa mke mwenyewe amekubali hilo hakuna tatizo lolote Inshaallaah. 

➡ Na midhali wamekubaliana hivyo ni lazima kutimiza makubaliano hayo kama walivyokubaliana, midhali masharti hayo hayavunji misingi mikuu sahihikatika dini yetu. 

➡ Amesema mtume s.a.w katika hadithi aliyopokea Abuu huraira r.a  :

” المسلمونَ على شروطهِم”

الراوي: أبو هريرة المحدث: النووي        – المصدر: المجموع – الصفحة أو الرقم: 9/376
خلاصة حكم المحدث: إسناده حسن أو صحيح
“Waisilamu wanakuwa juu ya masharti yao “

➡ Mume akianza kugawa zamu za usiku bila kumjulisha mke wa kwanza suala hilo atakuwa mume anadhulumu haki ya mke huyo wa kwanza. 

➡ Kwa sababu mke huyo ana haki kwa mumewe kuwa nae karibu kwa yote ila ikiwa kuna dharura ya kisheria. 

➡ Pia mume huyo kwenda usiku kwa mke wa pili ni jambo ambalo linaweza kusababisha dhana mbaya kwa mkewe juu yake,  na linaweza kumsababisha aseme uongo kila mara ili kumficha mkewe. 

➡ Na pia mume asipoweka nafsi yake sawa katika hili atajikuta hana raha ya ndoa zote mbili,  na huenda akawa ana dhulumu haki za wakeze wawili hao au mmoja wao.

➡ Na pia huenda akadhulumu hata haki za wanae katika usimamizi wao na ulezi wao. 

➡ Na hakika zamu hasa kwa wake wawili au zaidi ni zamu ya kulala kwa mke wakati wa usiku hadi asubuhi yake au zaidi yake,  kwa mujibu wa atakavyogawa zamu mwenyewe. 

➡ Na ikiwa atagawa zamu kwa kila mke siku moja kuanzia magharibi ya leo mpaka magharibi ya kesho hiyo ni bora zaidi,  kisha inaingia zamu ya mke wa pili kama hivyo nae. 

➡ Na hii ni kwa sababu muda wa mchana kwa hakika si muda wa kutulia katika majumba,  huo huwa ni muda wa kufanya kazi na kutafuta RIZKI za ALLAAH katika ardhi. 

➡Na hata utulivu wa nafsi na kutekelezeana haki za ndoa kwa muda huo huwa haziwi sawa na wakati wa usiku ambao unakuwa na utulivu mkubwa kwa viumbe vyote. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَسْمَعُونَ)
[Surat Yunus 67]

Yeye ndiye aliye kujaalieni usiku mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea. Hakika katika haya zipo Ishara kwa watu wanao sikia.

➡ Na ndio maana hata katika mwezi wa Ramadhani tumehalalishiwa kuwaingilia wake zetu wakati wa usiku. 

Je huyo mwenye kufanya zamu mchana kwa siri atafanya vipi zamu wakati wa mwezi wa Ramadhani? 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَكُمْ وَأَنْتُمْ لِبَاسٌ لَهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَخْتَانُونَ أَنْفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنْكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ ….َ)
[Surat Al-Baqara 187]

Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku…”

➡ Sharti hilo ni lazima alibadikishe,  na aweke zamu sawa kwa wake zake wote wawili. 

➡ Na atumie mbinu sahihi na hikma kumwambia mkewe wa kwanza kuwa ana mke mwingine. 

Kwa sababu kuwa wake wawili haina maana ya kuleta magomvi katika familia,  bali ni kuongeza ukubwa wa familia na kuunga udugu baina ya familia hizo. 

➡ Bali pia hata watoto wa mke wa kwanza na wa pili ni lazima wajuane kwa sababu watakuwa ni ndugu moja kwa upande wa baba yao. 

➡ Kwa nini ufiche ndoa yako wakati ni halali? ??

➡NAMUOMBA ALLAAH ATUJAALIE KUWA WAKWELI NA WAADILIFU KWA WAKE ZETU. 
ALLAAHU AALAMU. 

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:
nauliza salati Istikhara inasaliwa wakati gani? 
na muda gani- Yaani mara ngapi?  Na inashuruti yoyote kama ndio ni zipi. Wa shukran.

JAWABU 

➡ Sala ya istikhaara ni : 
” Ni sala ya sunna ambayo huswaliwa kwa ajili ya kumuomba ALLAAH uchaguzi wa lililokuwa na kheri zaidi katika mambo ambayo yamekukabili”

➡ Na hii ni sala muhimu sana katika hali ya kutaka kufanya moja katika mambo mawili tofauti,  unaswali rakaa mbili ambazo si katika sala ya faradhi,  kisha ukuitoa salamu unamuomba ALLAAH akufanyie wepesi katika lenye kheri nawe. 

➡ Na sala hii inaswaliwa kwa rakaa mbili tu katika Kauli sahihi ambayo imethibiti kwa mujibu wa hadithi ya mtume s.a.w. 

➡ Amepokea swahaba Jaabir bin Abdillaah Al answaary amesema :  : 

كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يُعَلِّمُ أصحابَه الاستخارةَ في الأمورِ كلِّها، كما يُعَلِّمُ السورةَ من القرآنِ، يقولُ : ( إذا همَّ أحدُكم بالأمرِ فليركَعْ ركعتينِ من غيرِ الفريضةِ، ثم لْيقُلْ : اللهم إني أَستخيرُك بعِلمِك، وأستقدِرُك بقُدرتِك، وأسألُك من فضلِك، فإنك تَقدِرُ ولا أقدِرُ، وتَعلَمُ ولا أَعلَمُ، وأنت علَّامُ الغُيوبِ، اللهم فإن كنتَُ تَعلَمُ هذا الأمرَ – ثم تُسمِّيه بعينِه – خيرًا لي في عاجلِ أمري وآجلِه – قال : أو في دِيني ومَعاشي وعاقبةِ أمري – فاقدُرْه لي ويسِّرْه لي، ثم بارِكْ لي فيه، اللهم وإن كنتَُ تَعلَمُ أنه شرٌّ لي في دِيني ومَعاشي وعاقبةِ أمري – أو قال : في عاجلِ أمري وآجلِه – فاصرِفْني عنه، واقدُرْ ليَ الخيرَ حيثُ كان ثم رَضِّني به ) .
الراوي: جابر بن عبدالله السلمي المحدث: البخاري  – المصدر: صحيح البخاري – 

Alikuwa mtume s.a.w akiwafundisha maswahaba zake sala ya istikhaara kama alivyokuwa akiwafundisha sura miongoni mwa Qur’an,  anawaambia :
“Akitaka mmoja wenu kukusudia jambo,  basi aswali rakaa mbili ambazo si katika faradhi. ….”

➡ Amma kuswali mara nyingi katika siku moja ni suala lenye ikhtilafu katika maulamaa. 

➡ Na sala hii inaswaliwa muda wowote ule ambao unafaa ndani yake kuswali. 

➡ Na inakatazwa kuswali sala yoyote katika nyakati kuu zifuatazo katika hadithi hii hapa

ublished By Said Al Habsy

SWALI:


Tunashukuru kwa jawabu kuhusu ugawaji zamu kwa wake zaidi ya mmoja. 

Kuhusu watoto Vipi anagawa mume  muda? Malezi si kitu rahisi hasa watoto wanapokuwa umri zaidi Ya miaka 12.
Kuwepo wazazi wote wawili na kuwasimamia ni jukumu kubwa. Dini inawapa haki gani ya muda  watoto wa zaidi Ya mke mmoja? Majukumu Ya mume si zamu za wake tu na watoto bila Shaka ni jukumu lake.

JAWABU

➡ Naam : 
Bila shaka haki ziko katika pande nyingi sana kwa mujibu wa kila mmoja na jamii yake ya karibu na ya mbali pia. 

➡ Tumetaja haki za kugawa zamu kwa wake wawili au zaidi kwa sababu suali lilikuwa limehusika zaidi upande huo kuliko upande mwingine. 

➡ Kisha utulivu katika ndoa chanzo kikuu ni utulivu kati ya mke na mume kwa kuishi kwa mapenzi na huruma. 

➡ Na mapenzi na huruma yanajengwa kwa itikadi sahihi na matendo mema kupitia Elimu sahihi ya kitabu na sunna. 

➡ Na katika lugha ya Qur’ani na sunna tukitaja mke na mume basi na wanaofuatia wataingia katika jumla ya wanaostahiki kutekelezewa haki zao wakiwemo watoto. 
➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ)
[Surat At-Tahrim 6]

Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.

➡ Neno ” Ahli ” katika aya hiyo limechukua maana pana zaidi,  kuliko lingetajwa neno jingine lolote. 

➡ Kwa sababu hata mke katika lugha ya Qur’ani anaitwa “ahli , kama alivyosema ALLAAH s.w katika kuelezea Nabii Musaa.s alipomaliza muda wake wa ajira,  aliondoka pamoja na mkewe,  na alikuwa wakati huo bado hajazaa na mkewe,  lakini ametajwa kwa Sifa ya “ahli “
(فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِنْ جَانِبِ الطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَعَلِّي آتِيكُمْ مِنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ)
[Surat Al-Qasas 29]

Basi alipo timiza muda wake na akasafiri na ahali zake, aliona moto upande wa Mlima T’uri. Akawaambia ahali zake: Ngojeni! Mimi nimeona moto, labda nitakuleteeni kutoka huko khabari au kijinga cha moto ili mpate kuota moto.

➡ Ni lazima kwa mume kuwa na muda wa kukaa na watoto wake na kufurahi pamoja nao. 

➡ Pia kuwatazama tabia na mienendo yao ya masomo ibada na mengineyo. 

➡ Watoto ni neema na amana juu yetu sote wazazi,  wa kiume na wa kike kwa kushirikiana. 

➡ Lakini juu ya hilo ni kuwa : 
Mama katika nyumba amepewa uwezo zaidi wa kuweza kuwatazama watoto kuliko baba. 

➡ Ndio maana ALLAAH S.W kwa ujuzi wake na hikma zake ameamrisha wanaume kuwahudumia wake zao majumbani,  ili wanawake washughulikie malezi ya ndani zaidi. 

➡ Na mume kwa maumbile yake ni kuwa : 
Afanye kazi na kutafuta RIZKI kwa ajili ya nafsi yake na watu wake wa nyumbani. 

➡ Yote hayo ni muhimu katika maisha kuyatazama kwa sababu ni majukumu na amana juu yetu sote. 

➡ Na  haki ziko aina nyingi  katika ndoa :

1.Haki za kimwili :
” kama vile kutimiziana matamanio ya kijinsia baina ya mume na mke,  kupitia maumbile sahihi aliyoumbiwa kila mmoja. 

Na hii ni haki ambayo ni lazima iwe baina yao wawili tu,  Hakuna kumuwakilisha mwingine. 

2.Haki za kiroho :
” Kama mapenzi ya nafsi na maneno mazuri baina ya mume na mke. 

Pia kuwa pamoja wakionana kila mmoja kuwa ni kitulizo cha macho kwa mwingine. 

Hii ni haki baina yao wawili tu hakuna wa kuitekeleza kwa niaba. 

3.Haki za kidhahiri :
Kama mambo ya matumizi na mahitaji ya vitu vya ndani,  miongoni mwa vyakula vinywaji na sehemu za kulala na vipando,  hivi ni katika haki ambazo inawezekana kufanyika kwa niaba katika baadhi ya hali. 

➡ Ndio maana tukataja zaidi upande wa zamu kwa wake wawili kabla ya kutaja upande wa watoto. 

➡ Sehemu ya malezi ya baba kwa wanae si kubwa sana kama nafasi ya mama kwa watoto hao. 

➡ Hii haina maana kuwa mke ndie aachiwe jukumu lote la kulea bila kusaudiwa. 
➡ Mtoto anaweza kuwa muda mwingi yuko katika malezi nje ya nyumba ya wazazi wake. 

➡ Muda mwingi atakuwa katika kusoma nje ya nyumbani. 

➡ Muda mwingine anaweza kuwa anafañya kazi zake za shule au madrasa. 

➡ Muda mwingine pia anafañya usafi wa nyumbani au mfano wa hayo. 

➡ Lakini ni wajibu kwa baba kuweka muda kwa kadri ya uwezo ili kukaa pamoja na wanae na kuwashauri na kujua mienendo yao. 

➡ Mapenzi ya wazazi kwa watoto ni dawa kubwa ya kuwafanya wawe bora zaidi 
➡Kuwa bize na kazi hakumaanishi kuacha majukumu ya familia yako. 

➡ Kazi zako utakufa na kuziacha , lakini matendo yako ukifa utakwenda nayo.


➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE VIZAZI VYEMA,  NA ATUWEZESHE KUVILEA KWA WEMA. 

ALLAAHU AALAMU. 

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:
Mdogo wangu alie jiuwa kwa kula dawa Je naweza kumuombea duwa au vipi?

na hilo lilikuwa ni mwezi waramadhani, na  je siku alizo bakisha hakufunga naweza kumlipia .? Naomba jawabu shukran

JAWABU

➡ Namuomba ALLAAH atukinge na shari za vifo vibaya. 

➡ Nafsi ya mtu si haki yake wala milki yake Yeye mwenyewe,  bali ni milki yake ALLAAH S.W. 

➡ Na ALLAAH s.w ameharamisha kujiua mtu mwenyewe nafsi yake kwa kuwa yeye ni mwenye huruma kwa waja wake. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ بَيْنَكُمْ بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَنْ تَكُونَ تِجَارَةً عَنْ تَرَاضٍ مِنْكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنْفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا)
[Surat An-Nisa 29]

Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni.

➡ Pia katika aya nyingine akasema : 
(وَأَنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ)
[Surat Al-Baqara 195]

Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

➡ Na ameharamisha pia kuua nafsi ya mtu mtu mwingine bila ya haki. 

Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَنْ قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِفْ فِي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنْصُورًا)
[Surat Al-Isra 33]
Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.

➡ Na mwenye kumuuwa muumini bila ya haki atawajibika kuingia motoni,  ila akitubia kabla ya umauti na anatekeleleza haki za warithi wa aliemuuwa ,  hakika ALLAAH ni mwenye kukubali toba. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا)
[Surat An-Nisa 93]

Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.

➡ Ni haramu kwa muisilamu kujiua mwenyewe au kumuuwa binaadamu mwingine ila kwa haki ambayo sheria ya KIISILAMU imeidhinisha kuuliwa mtu huyo. 

➡ Hayo ndiyo malipo ya mwenye kufanya dhulma ya kujiua mwenyewe. 

➡ Na sisi waisilamu tumetakiwa kuishi na watu na kufanya miamala nao kwa mujibu wa dhaahiri ya walivyo,  amma undani wao hiyo ni siri ya ALLAAH S.W. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 
(وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ)
[Surat Al-Qasas 69]

Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza.

➡ Na huyo ndugu yako katika hukmu ya dhwaahir ni kuwa amekufa hali ya kuwa amejidhulumu nafsi yake,  na kudhulumu haki ya Mola wake na jamaa zake waliobakia hai. 

➡ Na mtu mwenye kujiua katika hali kama hiyo huwa ni miongoni mwa waovu waliokufa katika dhambi kubwa,  na amevuka mipaka ya ALLAAH S.W 

➡Na wala haijuzu kisheria kumuombea dua ya kheri mtu huyo baada ya kufa kwake kabisa,  kwa kuwa amekufa si mwema,  na amevuka mipaka ya ALLAAH S.W. 

➡ Na ALLAAH s.w amesema : 

“…وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ ۚ وَمَنْ يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ…)
[Surat At-Talaq 1]

Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake.

➡ Na amekataza kuwapenda hao wenye kuvuka mipaka yake hata kama watakuwa ni ndugu wa damu au jamaa wa karibu. 

➡ Amesema ALLAAHU S.W : 

(لَا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُمْ بِرُوحٍ مِنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَٰئِكَ حِزْبُ اللَّهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ)
[Surat Al-Mujadala 22]

Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.

➡ Kwa mujibu wa dalili hizo za kisheria katika QURANI,  na nyingine nyingi ambazo hatukuzitaja hapa,  huna ruhusa ya kumuombea dua za kheri huyo mtu. 

➡ Wala huna jukumu la kumfungia siku ambazo hakufunga baada ya kufa kwake mtu huyo. 

Kwa sababu mtu mwenye kufa anakuwa hana jukumu katika masiku ambayo yatakuja mbele wakati yeye hayuko hai. 

➡ Maiti ambae anafungiwa saumu baada ya kufa ni yule ambae amekufa hali ya kuwa ana daiwa saumu ya siku za nyuma ,  huyo ndie anafungiwa saumu zake na jamaa zake wa karibu. 

➡ Amesema mtume s.a.w :
– “من مات وعليه صيامٌ, صام عنه وليُّه.”

الراوي: عائشة أم المؤمنين المحدث: البخاري       – المصدر: صحيح البخاري – الصفحة أو الرقم: 1952
خلاصة حكم المحدث: [صحيح]

➡ Imepokewa kupitia kwa Bi Aisha r.a anasema : 
Amesema mtume s.a.w : 
” Mwenye kufa na ana deni la saumu,  atamfungia walii wake “
Ameipokea imaamu al bukhaary na wengineo. 

➡ Uisilamu umetukataza hata kuyatamani mauti vipi mtu huyo anajiua kabisa hali ya kuwa ana akili timamu? 

➡Haya yote hutokea kwa sababu ya udhaifu wa imani na ujinga uliopo katika kuiga tabia za ki magharibi na kizungu. 

➡ Vijana wangapi zama hizi wamejiua kwa sababu ya kukosa kazi au pesa au uraia wa nchi fulani au mume au mke? ??

➡Na wako wanaojiuwa kwa sababu tu ya kugombana na hawara katika mambo ya uhuni? ??

➡Wengine wamejiua kwa sababu ya madeni mengi yamewazidia wanaona bora kufa kuliko kuishi? ??

➡Hawa wote wanaokufa katika hali hizi wanakufa ni waovu na wala hawafai kuombewa Dua za kheri na rehma. 

➡ Wala haifai kuwapenda hao mapenzi ya imani. 

➡ Na haya yote ikiwa mtu amejiuwa hali ya kuwa ana akili zake kamili na ufahamu wake. 

➡ TUNAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE MWISHO MWEMA. 

ALLAAHU AALAMU. 

SHEIKH SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shk mimi ninalo suali yupo mtu na binaami yake wameona na wamepata wtt Sita , na huyu mme anae dada yake yeye kaolewa na mume wa familia ya mbali na anao wtt 4. Mara huyu dada akamuhisi yule wifi yake (ambae ni cousin wake )anatembea  na mume wake ,na wamekiri kuwa wamefanya tendo hilo.
Suali : je hapa ndoa bado ipo Kwa huyu kaka na huyu dada mtu ?

JAWABU

➡ Namuomba ALLAAH atukinge na madhambi yote yaliodhihiri na yaliyojisitiri .

➡ Zinaa ni moja katika mambo yaliyoamrishwa na ALLAAH S.W katika QURANI tukufu na pia katika sunna za mtume s.a.w.

➡ Na zinaa ni miongoni mwa madhambi makubwa yanayopelekea kuingia mja katika moto na kubakia humo dhalili maisha yake.

➡ Amesema ALLAAHU S.W katika kubainisha sifa za waja wema ambao ni katika miongoni mwa waja wake kuwa ni :
(وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا)
[Surat Al-Furqan 68]

Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini – na atakaye fanya hayo atapata madhara,

(يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا)
[Surat Al-Furqan 69]

Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka.

(إِلَّا مَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا)
[Surat Al-Furqan 70]
Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

➡ Na ikiwa huo ndio ubaya wa zinaa katika jumla yake,  basi zinaa ya kumzini mke wa mtu,  au mke wa mtu kukubali kuutoa mwili wake kwa mwanamume asiekuwa mumewe,  hilo ni baya zaidi katika makubwa hayo.

➡ Amesema mtume s.a.w katika kubainisha watu ambao hawatopata rehma za ALLAAH siku ya qiyaama ni mwenye kuzini na mke wa jirani yake  :
الإشراكُ باللهِ وقتلُ الولدِ والزِّنا بحَليلةِ الجارِ [ أيْ من الكبائرِ ]
الراوي: عبدالله بن مسعود المحدث: ابن العربي     – المصدر: عارضة الأحوذي – الصفحة أو الرقم: 6/127
خلاصة حكم المحدث: ثابت

Maana yake ni kuwa :
” Kumshirikisha ALLAAH,  na kuuwa mtoto – yaani kwa kuhofia kupungua riziki kwa kumzaa – na kuzini na mke wa mtu  mwingine “

➡ ALLAAHU S.W ameharamisha maasi ya aina zote hata kama itakuwa maasi hayo ni kwa siri na kujificha sana.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَنْ تُشْرِكُوا بِاللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَنْ تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ)
[Surat Al-Araf 33]

Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua.

➡ Ikiwa yametokea hayo hayo yaliyotokea kwa ujinga na kughilibiwa kisha wakajua ubaya wa kosa lao hilo,  na ikawa halikutangazika, na wala halijafika kwa hakimu au kadhi wa kiisilaamu,   basi wanatakiwa wafanye toba ya siri baina yao na mola wao,  huenda wakasamehewa makosa yao.

➡ Na Kauli wamesema maulamaa kwa sababu ya ile hadithi ya yule mwanamke aliezini na akapata ujauzito,  kisha alikwenda kwa mtume s.a.w Kukiri ili afanyiwe hukmu ya mzinifu, akasema :
” Nitakase yaa rasuula llaah – yaani kutokana na dhambi ya zinaa kwa kunihukumu “

Mtume s.a.w akamrejesha mara ya  kwanza na akamwambia :
 “Mpaka utakapozaa “

Alipozaa akaenda tena mara ya pili na kumwambia mtume s.a.w : nimezaa tayari “

Mtume s.a.w akamrejesha na akamuambia : “mpaka aache kunyonya ”  

Akarudi tena mpaka alipomuachisha  kunyonya akaenda tena mara ya tatu na kumuambia : “ameacha kunyonya, na sasa anakula chakula   “
Aksamrisha mtume s.a.w mtoto yule apewe mmoja katika waisilamu,  kisha akaamrisha mtume s.a.w achimbiwe mwanamke huyo shimo hadi kifuani kwake,  kisha akaamrisha apigwe nawe na akapigwa mawe hadi kufa. ..”

“… قال : فجاءتِ الغامديةُ فقالت : يا رسولَ اللهِ ! إني قد زنيتُ فطهِّرْني . وإنَّهُ ردَّها . فلما كان الغدُ قالت : يا رسولَ اللهِ ! لم تردَّني ؟ لعلك أن تردَّني كما رددتَ ماعزًا . فواللهِ ! إني لحبلى . قال ( إما لا ، فاذهبي حتى تَلِدِي ) فلما ولدت أتتْهُ بالصبيِّ في خرقةٍ . قالت : هذا قد ولدتُه . قال ( اذهبي فأرضعِيهِ حتى تفطُمِيهِ ) . فلما فطمَتْهُ أتتْهُ بالصبيِّ في يدِه كسرةُ خبزٍ . فقالت : هذا ، يا نبيَّ اللهِ ! قد فطمتُه ، وقد أكل الطعامَ . فدفع الصبيَّ إلى رجلٍ من المسلمين . ثم أمر بها فحُفِرَ لها إلى صدرها . وأمر الناسَ فرجمُوها…”

الراوي: بريدة بن الحصيب الأسلمي المحدث: مسلم     – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 1695
خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Mtume s.a.w alimrejesha mwanamke huyo mara tatu,  kama alivyomrejesha Maazin alipozini na kwenda Kukiri kwa mtume s.a.w.

➡ Na hii inaonyesha mtume s.a.w alimpa fursa ya kutubia kwa siri,  ndio maana akawa akimrudisha mara tatu zote,  alipokuja ya nne ikawa tayari ni sawa na kupatikana mashahidi wanne,  ndio akahukumiwa kuuliwa,  na kama asingerudi basi mtume s.a.w asingemtafuta tena ili arudi.

➡ Kwa hiyo hadithi wakaona kuwa :
” Ikiwa watatubia kwa siri toba ya kweli ndoa yao itakuwa ipo na itaendelea.

➡ Na wengine wamesema pia kuwa :  ” ikifikia mume  Kukiri kwa mkewe  kuwa yeye  amezini,  au mke Kukiri mbele ya mumewe kuwa ameziniwa,  hapo ndoa itakuwa hakuna tena baina yao.

➡ Na wengine wakasema kuwa :  ” Ikiwa mume amesema kumuambia mkewe kuwa amezini lakini kusema huko ni kwa ajili ya kujuta kutokana makosa hayo,  ndoa hiyo itaendelea,

➡Amma akiwa anasema hivyo kwa kujifakharisha kwa maovu yake na wala hajuti, basi huyo atakuwa hafai tena kuendelea katika ndoa.

➡ Na nilimuuliza mmoja katika maulamaa kuhusu mke huyo alieziniwa nini afanye baada ya kutubia?  Kwa sababu huenda alipozini siku alibeba ujauzito kupitia mwanaume huyo aliezini nae ,  na inaweza kupelekea kuchanganyika mtoto wa zinaa katika nasabu ya mumewe …

➡ Akasema :
Ikiwa hali hiyo,  ni lazima mwanamke huyo ajizuie kuingiliana na mumewe mpaka apate hedhi mara moja,  kwa sababu hedhi inaonyesha usalama wa tumbo kuwa halina ujauzito.

➡ Kwa hakika hili ni kosa kubwa sana,  na wala haifai kuchukuliwa wepesi katika hukmu ikiwa ni jambo ambalo limeshakuwa na madhara kiasi hicho.

➡ Ndoa itakuwa baina yao kama tulivyosema kwa masharti hayo.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUHIFADHI NA MAASI YOTE MAKUBWA NA MADOGO NA ATURUZUKU TOBA.

➡ REJEA KITABU CHA
AL MUHAMMAD HII FIQHI TTWALAAQ.

ALLAAHU AALAMU.

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Nini hukmu ya kuamkia na kutoa mkono kwa asokuwa maharim wako? Shukran

JAWABU

➡ Salamu ni moja miongoni mwa haki za muisilamu kwa muisilamu mwenzake.

➡ Na salamu inatakiwa iwe kwa maamkizi ya kiisilaamu, na jawabu ya salamu pia iwe hivyo hivyo.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَإِذَا حُيِّيتُمْ بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَسِيبًا)
[Surat An-Nisa 86]

Na mnapo amkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila kitu.

➡ Na salamu hiyo inatakiwa iwe kwa sauti, ili mwenye kusalimiwa apate kuisikia na kuitikia salamu hiyo.

➡ Na ni sunna kwa waisilamu kupeaana mikono katika kusalimiana ikiwa hakuna kizuizi cha kisheria au cha kawaida baina yao.

➡ Amesema mtume s.a.w :

➡Lakini hukmu ya kupeaana mikono katika salamu ina hukmu zake tofauti kwa mujibu wa wanao salimiana hao kama ifuatavyo :

➡ Inajuzu kupeaana mikono katika hali zifuatazo

1⃣Ikiwa wanao salimiana ni wanaume kwa wanaume, au wanawake kwa wanawake.

2⃣Ikiwa ni wanaume kuwasalimia wanawake ambao wao ni haramu kuwaoa kisheria Uharamu wa maisha yao mpaka kufa.
K.v :
# Baba kwa binti yake au mjukuu wake wa kike .

#mama kwa mwanae wa kiume au mjukuu wake wa kiume.

# Na mfano wa hao miongoni mwa wanaoharamika miongoni mwa ndugu wa mama wanawake na ndugu wa kike wa baba. ..

3⃣Ikiwa mwanaume au mwanamke atasalimiwa na mtoto mdogo wa jinsia tofauti na yake kwa mikono, lakini mtoto huyo hajafikia umri wa kubaleghe, wala hatamaniwi matamanio ya nafsi.

Na bora zaidi ni kutowazoesha watoto tokea wadogo kutopeana mikono na watu wasiofaa kupeana nao mikono.

➡ Na iko kauli kuwa :
Inajuzu kupeana mkono na mwanamke aliekuwa ni mzee sana ki umri kiasi ameshakuwa hatamani tena au hatamaniwi kutokana na uzee wake.

Lakini hii ni Kauli ambayo haina hoja zenye nguvu.

➡ Mtume s.a.w amesema :

” ما مَسَّت يدُ رسولِ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ علَيهِ وسلَّمَ يدَ امرأةٍ إلَّا امرَأةً يملِكُها
الراوي: عائشة أم المؤمنين
– المصدر: صحيح الترمذي –
الصفحة أو الرقم: 3306
خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Maana yake ni kuwa :
” Haujapatapo kukamata mkono wa mtume s.a.w mkono wa mwanamke isipokuwa mwanamke ambae anaemiliki “

Ameipokea imaamu Al ttirmidhy.

➡ Na akasema pia katika hadithi kuwa :
لأن يطعن في رأس أحدكم بمخيط من حديد خير له من أن يمس امرأة لا تحل له
الراوي: معقل بن يسار المحدث: الهيثمي – المصدر: مجمع الزوائد – الصفحة أو الرقم: 4/329
خلاصة حكم المحدث: رجاله رجال الصحيح

Maana yake ni kuwa :
” Kutogwa mmoja wenu kwa sindano ya chuma katika kichwa chake ni bora kuliko kumgusa mwanamke ambae si halali kwake “

Ameipokea imaamu Al haithamy kutoka kwa miiqal bin yasaar r.a.

➡ Ni ajabu kuona wengi waisilamu wamechukulia wepesi jambo la kupeana mikono wanaume na wanawake hali ya kuwa lina hatari kubwa sana.

➡ Pia wanawake na shemeji zao wa kiume wengi wao hawajui kuwa ni haramu wao kupeana mikono katika hali hizo zote.

➡ Kadhalika binaamu na bint aamy na watoto wa wajomba na shangazi na mfano wao, pia haifai hivyo.

➡ Mwenye kuwa aliwahi kufanya hivyo anatakiwa afanye toba kwa ALLAAH S.W na aache tena kufanya hivyo.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA NANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

 

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je kwa sheria ya dini inafaa kuwaowa wanawake wawili ndugu ? Na Je, km ukioa siku moja wanawake wawili lkn ni tofauti inafaa?

 

JAWABU 

➡ Katika ndoa ALLAAH S.W amebainisha katika qurani wanawake ambao wanaharamika kuolewa na wanaume kwa upande wa udugu wa nasabu au ukwe au kunyonya katika ziwa la mama mmoja.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ مِنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُمْ مِنْ نِسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُمْ بِهِنَّ فَإِنْ لَمْ تَكُونُوا دَخَلْتُمْ بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَنْ تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا)
[Surat An-Nisa 23]

Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

➡ Na baada ya aya hiyo ametaja pia walioharamika kuwa ni : ” wanawake waliokuwa na waume zao “

➡ Katika aya niliyoitaja juu imtatajwa kuharamika ni :
” …Na kuwaoa pamoja dada wawili…”

➡Kwa hiyo :
Ikiwa unakusudia ndugu wa damu katika nasabu zao, au ndugu walionyonya ziwa la baba mmoja, au mama mmoja, hiyo haifai.

➡ Na kuna jambo moja muhimu sana napenda kuzindua kuhusu suala la kuitana kaka na dada kwa waliokuwa si ndugu wa nikiowataja katika ambao wanaoharamika kuoana.

➡ Mfano :
Kijana wa kiume kumuita binti wa shangazi yake dada. ..

Au mtu kumuita binti ammi dada.

➡ Kuitana huku ni kwa mujibu wa mazoea ya watu walivyozoea kuitana, lakini kuitana huku hakuna athari yoyote wala kizuizi katika kuoana kati yao kisheria.

➡Kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa mtoto wa shangazi au mtoto wa ammi au mtoto wa mjomba kwa kuwa wanaitana dada ndio hawafai kuoana.
Na hili si sahihi kabisa.

➡ Bali hata ikiwa mtu ataoa wake wawili ambao mmoja wao ni mtoto wa ammi na mwingine mtoto wa mjomba mfano, ndoa yake itakuwa ni sahihi wakiwa pamoja katika ndoa moja.

➡ Amma kuhusu kuoa mtu wake wawili kwa pamoja mara moja kwa siku moja, ikiwa hakuna kizuizi cha kisheria, wala mume hahofii kufanya uadilifu baina yao, Inshallah hakuna tatizo lolote kufanya hivyo.

➡ Amma kwa kuchunga na kuepusha kutokea mapungufu katika kudhibiti mambo yake ya harusi kwa siku hiyo ya kwanza.

➡ Mke siku ya kwanza katika ndoa yake ni vizuri awe na mumewe kwa muda mrefu zaidi, ili kumtuliza moyo wake na kumuondoshea ugeni wa siku hiyo ya ndoa.

➡ Na kuoa kwa siku tofauti huenda ikawa ni njia ya kumpa wasaa mzuri mume huyo wa kujiweka sawa kwa kuwapa nafasi wake zake wawili hao na yeye mwenyewe pia.

➡ Lakini juu ya nasaha hiyo hakuna Uharamu wa kuoa wake wawili kwa wakati mmoja, ikiwa wake hao kisheria hawaharamiki kuwa pamoja katika ndoa moja kwa pamoja.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ABARIKI NDOA ZETU, NA AWAJAALIE AMBAO HAWAJAPATA WAKE AU WAUME, WAPATE WALIOKUWA NA KHERI.

ALLAAHU AALAMU.

“Jambo kwa kadri ya uwezo

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Kuna lugha tofauti katika majina 99 ya ALLAAH S.W kwa kiarabu. Je kwa kiswahili kumuita ALLAAH Mungu inafaa ? ama haifai ?

JAWABU 

➡ Ndugu zangu :
ALLAAHU S.W ametaja katika qurani kuwa yeye ana majina mazuri na Tumuombe kupitia majina hayo.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَلِلَّهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ)
[Surat Al-Araf 180]

Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda.

➡ Na akasema pia :
(قُلِ ادْعُوا اللَّهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَٰنَ ۖ أَيًّا مَا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا)
[Surat Al-Isra 110]

Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo.

➡ Na amesema pia :
(اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ)
[Surat Ta-Ha 8]
Mwenyezi Mungu! Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri kabisa.

➡ Na yako majina na sifa zake ALLAAH S.W amezitaja katika qurani na nyingine pia zimetajwa katika sunna za mtume wetu muhammad s.a.w.

➡ Na hapana shaka yoyote kuwa : Allaahu s.w ndie ambae ameumba watu na amewajaalia kuwa wakatofautiana katika mataifa yao na makabila pia rangi na lugha zao.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ)
[Surat Al-Hujraat 13]

Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.

➡ Na bila shaka watu hawawezi kumjua ALLAAH kwa ukamilifu wa kumjua ila kupitia kusomeshwa elimu ya kumjua ALLAAH S.W.

➡ Na ili wafahamu suala hili ni lazima wasomeshwe kwa kufasiriwa kupitia lugha ambazo wanazitumia watu hao ili waweze kufahamu.

➡ Na ndio maana hata mitume walikuwa wakitumwa katika kaumu zao kwa lugha za kaumu zao ili waweze kuwabainishia kile ambacho wametumwa kuwafikishia.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ رَسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ فَيُضِلُّ اللَّهُ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ)
[Surat Ibrahim 4]

Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

➡ Kutokana na hayo yote,
Hakuna kizuizi chochote katika kutamka majina ya ALLAAH S.W kwa lugha nyingine katika kufikisha elimu ya kumjua ALLAAH S.W, au katika kuelimisha watu kwa mujibu wa lugha zao.

➡ Na maulamaa wamejuzisha hili ni kutokana na dharura ambazo hapana budi baadhi ya wakati kutumia lugha hizo, lakini inajuzu hilo kwa sharti :

1 – Ikiwa maana itakayotumika haitopelekea kuharibu maana ya asili ya jina hilo la ALLAAH S.W au sifa yake.

2 – Iwe ni kwa kiasi cha haja tu, isiwe ndio kawaida yenye kudumu mpaka wakachukulia watu wepesi katika jambo na kuacha asili ya lugha ambayo majina hayo yameteremshwa kwayo.

➡ Kwa hiyo ikiwa mtu atatumia jina la
” ALLAAHU ” kwa kiswahili akasema ” (Mwenyezi Mungu) , Hakuna tatizo katika kusema hivyo, kwa sababu ni neno ambalo katika matumizi ya lugha ya kiswahili neno hilo hutumika katika maana sahihi ya kujulisha utukufu na ukubwa wa ALLAAH S.W kwa mujibu wa lugha hiyo.

➡ Na niliwahi kuuliza baadhi ya wajuzi zaidi wa lugha ya kiswahili kuhusu nene (Mwenyezi Mungu) asili gani?

Nilipata jawabu ya neno la mwanzo kuwa ni :
” Mwenye enzi : na maana yake ni : ” Mwenye sifa ya kuwa yeye ni wa zamani, ni wa tangu, wa enzi ambae hakutanguliwa na kitu chochote kabla yake.

➡ Na bila shaka maana hiyo ni nzuri.

➡ Kwa hakika ni makosa kukataza watu kutumia majina kama hayo katika kuifikisha maana kwa wasiojua hasa maana nyingine ila kwa lugha hiyo.

➡ Pia ni jambo ambalo halipendenzi kwa muisilamu anaejua kutumia neno ALLAAH au mfano wa hilo katika majina ya ALLAAH S.W.

➡ Neno ALLAAH ni rahisi kulitumia kila muisilamu bila taabu yoyote, na ndio ambalo tunalitumia sana katika ibada ya sala hasa katika vipengele vingi vya sala.

➡ Tujizoeshe kutumia lugha ya Qur’ani zaidi kuliko lugha nyingine ila panapokuwa hapana budi.

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUFUNGULIE MILANGO YA KHERI NA BARAKA NA HIKMA.

ALLAAHU AALAMU.

“Hikma kabla ya hukmu “

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Nauliza kuhusu kufanya kunuti katika swala ya ijumaa je inafaa ?

JAWABU 

➡ Qunuuti ni neno lenye asili ya kiarabu na lina maana nyingi sana katika matumizi ya lugha hiyo kiarabu kwa mujibu wa makusudio ya mtamkaji.

➡ Miongoni mwa maana zake ni :

1⃣Kudumisha utiifu kwa unyenyekevu kwa ALLAAH S.W .
Amesema ALLAAHU S.W kuhusu Bi Maryamu mama yake Nabii Issa a.s :
(يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ)
[Surat Aal-E-Imran 43]

Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola Mlezi wako na usujudu na uiname pamoja na wainamao.

2⃣Kunyenyekea na kuwa watulivu katika sala.

Au kuwa kimya na kuacha maneno yaliyokuwa nje ya sala.

Amesema ALLAAHU S.W :
(حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّهِ قَانِتِينَ)
[Surat Al-Baqara 238]

Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea).

3⃣Utiifu kamili.
Amesema ALLAAHU S.W kuhusu sifa za waja wema.
(الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنْفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ)
[Surat Aal-E-Imran 17]

Wanao subiri, wanao sema kweli, na wat’iifu, na wanao toa sadaka, na wanao omba maghafira kabla ya alfajiri.

4⃣Pia kisimamo kirefu cha sala za usiku huitwa Qunuuti.

Amesema ALLAAHU S.W :
(أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ ۗ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ)
[Surat Az-Zumar 9]

Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi… Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili.

➡ Na ziko aya nyingine nyingi na hadithi pia zimetaja Qunuuti kwa maana mbalimbali.

➡ Lakini je imethibiti Qunuuti kwa maana ya dua inayosomwa katika sala za faradhi au za sunna ndani ya sala au laa?

➡ Suala hili lina ikhtilafu katika maulamaa kwa Kauli nyingi kupitia hadithi zilizotaja suala hili kama ifuatavyo :

1⃣Madhehebu ya ibaadhi ni kuwa : Qunuuti kwa maana ya dua isomwayo ndani ya sala jambo hili halikuthibiti.

Amepokea Abuu Ghaanim al khuraasaany kuwa alimuuliza Abaa l muarrij : je katika sala kuna Qunuuti?
Akamjibu kuwa :
” Amenihadithia Abuu ubaida kutoka kutoka kwa jaabir bin zaid aliulizwa suala hili akasema :
” Sala yote ni Qunuuti “
Amesema ALLAAHU S.W :

(أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا… )

Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama …).

Nikasema:
Si hili nauliza mimi,
Lakini nakuuliza hili walifanyalo baadhi ya watu baada ya kurukuu wanasimama na kuomba dua na tahlili hali ya kuwa wamesimama!

Akasema Imaamu Jaabir bin zaid r.a :
” Jambo hili limezushwa, hatulijui wala hatukulipokea kutoka waliotangulia katika wabora wa umma huu.

2⃣Imaamu maalik anasema kuwa :
Qunuuti katika sala ya Asubuhi – Alfajiri – ni kitu kinapendekezwa (mustahabu).

Na akasema Abuu umar ibnu abdi l Barri kuwa :
” Na kufanya Qunuuti kwa ajili ya kuwalaani makafiri katika Ramadhani ni jambo mashuhuri hakika karne ya mwanzo iliyotangulia, kwa kumfuata mtume s.a.w alipokuwa akiwaombea watu wa kabila la “Raali na dhakwaan “.

3⃣Na amesema Imaamu laithu bin saad r.a :
” sijafanya Qunuuti tokea miaka 40 nyuma au 45 isipokuwa nikiswali nyuma ya imaamu anae qunuti .

Na anasema hili nimelichukua katika hadithi ya mtume s.a.w iliyotaja kuwa mtume s.a.w alifanya Qunuuti mwezi mmoja tu au siku arobaini, mpaka ilipoteremka Kauli ya ALLAAH S.W isemayo :
(لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 128]

Wewe huna lako jambo katika haya – ama atawahurumia au atawaadhibu, kwani wao ni madhaalimu.

Akaacha mtume s.a.w kufanya Qunuuti baada ya kuteremshiwa aya hiyo mpaka kukutana kwake na ALLAAH (yaani hadi kufa kwake ).

➡ Na hii ndio Kauli yenye nguvu zaidi kuwa Qunuti ilifutwa kuanzia kuteremshwa aya hiyo.

➡ Na Imaamu Muslim katika kitabu chake cha hadithi sahihi amepokea hadithi kutoka kwa Abuu huraira r.a kuwa mtume s.a.w aliacha Qunuuti baada ya aya hiyo.

➡ Na ziko baadhi ya hadithi zinaonyesha kujuzu kufanya Qunuuti katika matukio na majanga mbalimbali.

Na hii ndio Kauli mashuhuri katika madhehebu ya shaafy.

➡ Na pia ni sunna katika sala ya Al fajiri kwa madhehebu ya shaafy.

➡ Na wako waliosema pia kufaa Qunuuti katika shida yoyote iliyofika kwa watu katika miji yao katika sala yoyote ile.

➡ Khulaswa ni kuwa :

Suala hili lina ikhtilafu baina ya maulamaa kwa sababu ya ikhtilafu ya hadithi zikizopokewa kuhusu suala hili.

➡ Kila jambo lenye ikhtilafu na ikawezekana kuitoka ikhtilafu hiyo basi kuitoka ikhtilafu ni bora kuliko kuinguia .

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA.

 ALLAAHU AALAMU.

“Acha lenye shaka na fuata lisilo shaka “

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Hivi mfano amekufa baba yangu na mwalimu wangu” halafu mimi nina uwezo wa sanda moja tu, je nimzikie nani hiyo sanda ?, je nianze kumzika yupi kati ya hawo wawili ?

JAWABU: 

➡ Ndugu zangu :
Mtu yoyote anapokufa, basi asili ya sanda na maziko yake yote gharama zake zinachukuliwa kutoka katika mali zake ambazo alikuwa akimiliki mwenyewe katika uhai wake.

➡ Kwa hiyo ikiwa kumetokea vifo vya watu wawili hao katika wakati mmoja, na sanda ni moja tu anayoimiliki mtu huyo mwenye kutaka kujitolea sanda hiyo kwa ajili ya kuzikia maiti mmoja katika hao wawili, hukmu itakuwa kama ifuatavyo :

1⃣Ikiwa mzazi aliekufa atakuwa hana uwezo wowote wa kumiliki mali yake mwenyewe katika uhai wake, itamlazimu sanda hiyo itumike kumzikia baba yake mzazi.

Kwa sababu :
Haki ya mzazi ni kubwa zaidi kabla ya mwingine yoyote.

2⃣Na Ikiwa yule mwalimu wake hakupata sanda, na mzazi yule hakupata sanda, itabidi sanda ya mwalimu itoke katika nyumba ya mali ya waisilamu (baiti maali l muslimiin ).

➡ Amesema ALLAAHU S.W kuhusu haki za jamaa wa karibu. ..
(وَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا)
[Surat Al-Isra 26]

Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo.

➡ Na ikiwa patakosekana kabisa sanda ya kumzikia mwalimu huyo basi azikwe ndani ya kanzu yake aliyokuwa akiivaa katika uhai wake, ambayo inamsitiri mwili wake.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W AWAREHEMU MAITI WOTE WA KIISILAMU NA ATUJALIE MWISHO MWEMA.

ALLAAHU AALAMU.

“Jiandae na mauti kabla hayakufkufika “

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

A,alaykum
1- Ustaadh : ni ipi hukmu ya kumuoa mwanamke aliyechukua mimba kabla kuolewa ?

2-hivi inafaa kwa kijana aliyekuwa hajaowa kumuowa huyo msichana? 

JAWABU 

➡ Ndugu zangu :
Tumetaja katika jawabu zikizotangulia kuhusu zinaa hukmu yake na madhara yake kidini na kijamii.

➡ Na muisilamu yoyote aliyekuwa anamuogopa mola wake, na kufuata amri zake, na kutaraji maisha mazuri duniani na akhera, basi aowe kwa mujibu wa alivyoamrisha ALLAAH S.W.

➡ ALLAAHU S.W hakuruhusu waisilamu kuoana baada ya kumuasi yeye kwa uchafu wa zinaa.

➡ Wala kuhuruhusu watu wachague wanawake waliokuwa ni wachafu na wazinifu.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ مِنْكُمْ طَوْلًا أَنْ يَنْكِحَ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ فَمِنْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ مِنْ فَتَيَاتِكُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ۚ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِكُمْ ۚ بَعْضُكُمْ مِنْ بَعْضٍ ۚ فَانْكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ فَإِذَا أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَاحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى الْمُحْصَنَاتِ مِنَ الْعَذَابِ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ الْعَنَتَ مِنْكُمْ ۚ وَأَنْ تَصْبِرُوا خَيْرٌ لَكُمْ ۗ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ)
[Surat An-Nisa 25]

Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara. Na wanapo olewa kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu waliyo wekewa waungwana. Hayo ni kwa yule miongoni mwenu anaye ogopa kuingia katika zina. Na mkisubiri ndio bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.

➡ Ameamrisha kuoa wanawake wema na wala si wahuni wala makahaba au malaya kwa lugha nyingine iliyozoeleka kwa watu.

➡ Na pia ALLAAHS.W amekataza kulazimisha watoto wa kike kufanyishwa ukahaba au kaolewa na wanaume wahuni wazinifu.

Na ameamrisha wale ambao hawajawa na uwezo wa kuoa basi wajulizuie nafsi zao na maasi ya uzinifu.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ ۗ وَالَّذِينَ يَبْتَغُونَ الْكِتَابَ مِمَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ فَكَاتِبُوهُمْ إِنْ عَلِمْتُمْ فِيهِمْ خَيْرًا ۖ وَآتُوهُمْ مِنْ مَالِ اللَّهِ الَّذِي آتَاكُمْ ۚ وَلَا تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَمَنْ يُكْرِهْهُنَّ فَإِنَّ اللَّهَ مِنْ بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَحِيمٌ)
[Surat An-Noor 33]

Na wajizuilie na machafu wale wasio pata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhila yake. Na wanao taka kuandikiwa uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni. Wala msiwashurutishe vijakazi vyenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta pato la maisha ya dunia, ilhali wao wanataka kujihishimu. Na atakaye walazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

➡ Mwanamke yoyote mwenye mimba hafai kaolewa mpaka arakapozaa mimba yake hiyo.

Ikiwa mimba hiyo ni ya mume aliekuwa nae katika ndoa kisha akafariki, au kumuacha talaka, na pia hata ikiwa ni mimba katika njia ya zinaa.

➡ Uisilamu umeweka sheria na mipaka yake ili kuhifadhi kizazi nasabu na haki mbalimbali.

➡ Na pia kuhifadhi utu wa watu na heshima zao na mali zao, yote hayo ni miongoni makusudio ya sheria ya dini yetu hii ya kiisilaamu.

➡ Na mwenye kwenda kinyume na sheria za dini atakuwa anakwenda kinyume na makusudio yake, na hatimae ni kumsababisha ufisadi katika ardhi hii na kueneza madhara kwa nafsi yake na wengine pia.

➡ Amma ikiwa mwanamke huyo alikuwa mzinifu zamani lakini akatubia toba ya kweli, na akashika dini na kufuata njia ya wema, Allaahu s.w ameahidi kuyabadilisha maovu yao na kuwa ni mema.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(إِلَّا مَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا)
[Surat Al-Furqan 70]

Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

➡ Kwa aya hiyo juu

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Nina swali la nyongeza hapo mwalimu , umesema sunna ya magharibi iswaliwe msikitini ukaweka na sababu.Sasa mbona katika hadithi ya Ibni Umar inasema ni sunna kuswali baadiya ya ijumaa, magharibi na kabliya ya asubuhi nyumbani ? Yani imetaja kabliya ya magharibi sunna kuswaliwa nyumbani nasio msikitini?

JAWABU:

➡Naam,
imepokewa kutoka Kwa Abdillaahi bin Omar r.a amesema:

أنَّ رسولَ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ كان يُصلِّي قبل الظهرِ ركعتينِ وبعدها ركعتينِ وبعد المغربِ ركعتينِ في بيتِهِ وبعد العشاءِ ركعتينِ وبعد الجمعةِ ركعتينِ في بيتِهِ”

الراوي: عبدالله بن عمر المحدث: أحمد شاكر – المصدر: مسند أحمد – الصفحة أو الرقم: 7/171
خلاصة حكم المحدث: إسناده صحيح

” Alikuwa mtume s.a.w akiswali rakaa mbili kabla ya adhuhuri, na rakaa mbili baada ya adhuhuri, na baada ya magharibi rakaa mbili nyumbani kwake, na baada ya Isha rakaa mbili,
na baada ya ijumaa rakaa mbili nyumbani kwake “

➡Hiyo ni hadithi yenye isnaadi sahihi, Kwa mujibu wa hukmu ya mpokezi alieitoa katika kutabu chake.

➡Na asili ya sunna wanasena maulamaa kuwa:”ni bora kuziswalia nyumbani “

➡Na hii kauli ambayo imetajwa katika kitabu cha Al muurltamad fii fiqhi sswalaat.

➡Lakini juu ya hivyo, kauli niliyoitaja katika jawabu iliyotangulia, haipingani na hadithi ya Ibni Omar r.a, aliyoitaja muuluzaji, Kwa sababu zifuatazo :

1 – Mtume s.a.w Alikuwa akifanya hivyo yeye, Lakini hakuamrisha umna wote wafanye hivyo.

Na kwa kuwa hakuamrisha kuswalia nyumbani , wala hakuamrisha kuswalia msikitini , na wala hakukataza kuswalia sunna hiyo sehemu moja Kati ya hizo, basi jambo Hilo linajuzu kulifanya katika Hali yoyote katika hizo mbili, bila kulazimisha moja wapo.

2 – Ziko Hadithi nyingi zinaonyesha ubora katika kuswalia sunna nyumbani zaidi, bila kutaja aina ya Sala zenyewe.

3- Pia kuhusu mtume s.a.w kuwa alikuwa akiswali sunna baada ya magharibi nyumbani, naam, hiyo imepokewa katika hadithi ya Abdillaah bin omar r.a.

➡lakini hakuamrisha Hilo, kwa hiyo ni kurudi katika asili, nayo ni kuwa sunna zote ziswaliwe nyumbani.

➡Lakini nini sababu kuu ya kuswalia nyumbani Sala za sunna? ??

hikma kubwa ni tusizifanye nyumba zetu kuwa kama makabùri.

➡Je wakiswalia watu wote sunna majumbani, nini kitakuwa baada ya hapo?

➡Kisha nyumba ya mtune s. a.w ilikuwa karibu Sana na msikiti, na Muda baina ya magharibi na ishaa ni mfupi.

➡Na ziko hadithi ambazo zinsonyesha kuwa, malipo mukubwa yatakuwa ni kwa watu ambao wameswali sunna hiyo , ni wale walioswali maghafini kisha wakawa hawakuzungumza chochote baina ya faradhi ya maghriib na sunna yake.

➡Na ndio maulana wengine wakapendekeza baadhi ya sunna kuziswali msikitini hapo hapo, ili kuchunga Muda Pia wa faradhi , kama sunna ya maghribi .

lengo ni kupata fadhila za Allah a.w katika Sala, na wakati , Pia sehemu hiyo ya
ibada.

➡Kumbuka kuwa, ziko baadhi ya sunna zimesunniwa kuswaliwa katika misikitii kwa ajili ya sehemu magharibi, akiingia msikitini Haruhusiwi kukaa ila kwanza aswali rakaa mbilini.

➡Na sunna hiyo ni lazima kuifanya akiingia msikitini na akataka kukaa kitako, hata kama atakuwa aliswali sunna nyingine nyumbani kwake.

➡Huo ni mukhtasari wa jawabu katika suala hilo.


ALLLAAHU AALAMU.

” Sunna zisizowekewa pahala maalumu katika sheria, inajuzu kuzifanya pahala popote panapostahiki kufanyiwa ibada “

JAWABU KUTOKA KWA
SH. SHAABANI AL BATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

A aleykum,
Kufuatia maendeleo ya sayansi wale ambao wana matatizo ya kushika ujauzito imepatikana njia mbadala. Linachukuliwa yai la mwanamke na mbegu za mume na kupandikizwa kwa mwanamke mwingine ambaye huyu atailea mimba mpaka kujifungua mtoto na kukabidhi kwa wahusika (mwenye yai na mbegu). Mfano wa hili watu wengi wanafanya na hivi karibuni mwanamitindo wa kimarekani Tayra Banks amepata mtoto kwa njia hiyo. Swali, je uislamu unasemaje kuhusu jambo hilo.

JAWABU:

➡ALLAAHU sw anetuwekea njia sahihi na yenye manufaa na kukidhi natamanio na mahitaji yote ya nafsi na mwili kwa mume na mke.

➡ Amesema ALLAAHU sw
(إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا)
[Surat Al-Insan 2]

Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.

➡Na mchanganyiko katika aya hiyo ni mchanganyiko wa maji ya uzazi ya mume na mke wakati wa kuingiliana.

➡Na hayo ndio makusudio sahihi ya ndoa na raha yake.

➡ Kwa mujibu wa Swali lako hili, ni jambo ambalo linafanywa katika baadhi ya nchi, lakini jambo hili hukmu yake iko katika Hali tofauti zifuatazo :

1- Ikiwa mume na mke wanaweza kuzaa kwa njia ya asili ya kawaida, basi hakuna ruhusa kusheria kutumia njia hiyo katika Swali hili.

2- Ikiwa inethibiti kuwa mume na mke hawawezi kuzaa ila kwa njia ya kupandikizwa mbegu ya uzazi katika yai la mke, hapo inaruhusiwa kwa sababu ya dharura hiyo, pamoja na hivyo ni lazima pazingatiwe mambo muhimu yafuatayo:

1- Ithibiti kuwa haiwezekani kuzaa kwa njia ya kawaida.

2 – iwe kupandikizwa mbegu hizo chini ya usimamizi wa madaktari wanao aminika.

3 – Iwe kutoa mbegu hizo ni kwa njia ambayo haina madhara wala kudhihishwa yasiyofaa kudhihirishwa , ila Ikiwa ni kwa dharura kwa makadirio ya dharura yenyewe.

4- Yatumike maji ya mume mwenyewe kuwekwa katika yai la mke wake mwenyewe, Amma Ikiwa ni maji ya mwanaume mwingine kuwekwa katika yai la aliekuwa si mkewe , au maji ya mume lakini kuwekwa katika yai ambalo si la mkewe , hiyo haikubaliki kisheria, na inapelekea kuchanyika nasabu, na inapelekea kupatikana watoto wasiokuwa na nasabu sahihi.

5- Na pia mwanamke ashughulikiwe na mwanamke mwenzake, na mwanaume na mwanaume mwenzake.

6 – Na baada ya kupndikiza mbegu hiyo ya mume kwa mkewe, basi ni lazima kuhakikisha kuwa, mbegu nyingine zote za mume zilizobakia ziuliwe kwa njia yoyote ile, ili kuepusha kuja kutumia mbegu hizo kwa kumpandishia mwanamke mwingine.

7- Ithibiti kuwa hakuna madhara yoyote kutokana na kuzalisha kwa njia hiyo.

➡Kutumia njia hii kwa Hakika ni suala lenye ikhtikaafu kubwa baina ya maulamaa, hata katika kikao cha maulamaa wa kiisilamu kilicho fanyika Saudi Arabia , maulamaa walitofatiana katika hukmu ya suala hili kwa kauli tatu:

1- Wako waliokataza moja kwa moja.

2 – Na wengine wakajuzisha kwa masharti mbalimbali, miongoni mwayo ni hayo niliyotaja juu hapo.

3 – Na wengine walikuwa katika msimamo wa kusimama tu Bila ya kutoa kauli yoyote.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW ATURUZUKU VIZAZI VYEMA .

ALLAAHU AALAMU.

” Mfumo wa kiisilamu ndio msingi sahihi unao endana na maumbile sahihi “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Wanasema kila nafsi itaonja umauti na adhabu ya kabur je! Wale wanaochomwa moto adhabu ya kaburi hawaipati au ??

JAWABU

➡Kifo ni haki hakika kipo, kwa uthibiti wa maneno ya ALLAAH SW mwenyewe, na wala si wanasema tu watu.

➡Amesema ALLAAH SW:
(كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَنْ زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ)
[Surat Aal-E-Imran 185]

Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kaamili Siku ya Kiyama. Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu.

➡ Na ALLAAH SW ameweka katika Quran jawabu iliyo wazi kabisa , pale alipoteremsha aya kumjbu yule aliekuwa ana Shaka kuhusu kufufuliwa watu siku ya Qiyaama :

(وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَنْ يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ)
[Surat Ya-Seen 78]

Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung’unyika?

(قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنْشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ)
[Surat Ya-Seen 79]

Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.

➡ Ikiwa ALLAAH SW ana uwezo wa kuumba kitu bila kuwepo mfano wa kitu kabla, je atashindwa kukirejesha kilichokuwa kimekufa tu wakati yeye ndie alikiumba mwanzo?

➡Na hali kadhaalika kwa wale waliokufa duniani kwa kuchomwa moto, au wamekufa Kisha ndio wakachomwa moto, ALLAAH SW atawarejeshea uhai tena na wataadhibiwa kwa moto hata kabla ya siku ya Qiyaama.

➡Na hivyo ndivyo alivyofanya ALLAAH SW kwa Fir’auna na watu wake.

➡Amesema ALLAAHU SW : (فَوَقَاهُ اللَّهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا ۖ وَحَاقَ بِآلِ فِرْعَوْنَ سُوءُ الْعَذَابِ)
[Surat Ghafir 45]

Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizo zifanya. Na adhabu mbaya itawazunguka watu wa Firauni.

(النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ)
[Surat Ghafir 46]


Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!

➡Adhabu ya kaburi ni haki, na itamfika kila mwenye kustahiki popote alipo, na katika hali yoyote aliyo nayo.

➡Na ALLAAH SW hashindiwi na jambo lolote akilitaka basi huamrisha tu na likawa.

➡Amesema Allaahu sw :
(إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَنْ يَقُولَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ)
[Surat Ya-Seen 82]

Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.

(فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ)
[Surat Ya-Seen 83]

Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa.

➡ NAMUOMBA ALLAAH SW ATUJAALIE KIFO CHA KATIKA SHAHADA.

ALLAAHU AALAMU.

” Mambo ya ghaibu yanachukuliwa kwa dalili, na wala si kwa akili “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Naomba kujuulishwa hukmu ya mtu mwenye mumewe akatoka nje ya nyumba ? (ndoa, na mumewe hajui maana ni jirani yangu. nataka nimfuate nimueleze nataka ushahidi nisije kuganda.

JAWABU 

➡Jambo la zinaa ni jambo baya na uchafu uliopita mipaka.

➡Na jambo hilo linataka kuthibitishwa kwa ushahidi kamili kama ilivyotibiti katika qurani tukufu.

➡Ushahidi wa kuthibiti zinaa ni lazima mashahidi wanne.

➡Amesema Allaahu sw :
(وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ فَاجْلِدُوهُمْ ثَمَانِينَ جَلْدَةً وَلَا تَقْبَلُوا لَهُمْ شَهَادَةً أَبَدًا ۚ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)
[Surat An-Noor 4]

Na wanao wasingizia wanawake mahashumu, kisha wasilete mashahidi wane, basi watandikeni bakora thamanini, na msiwakubalie ushahidi wao tena. Na hao ndio wapotovu.

➡Na mashahidi Hao ni lazima wawe wameshuhudia wenyewe kwa macho yao kitendo cha zinaa.

➡Na ikiwa mtu wa kawaida tu anamsema mtu kuwa ni mzinifu, lakini hana ushahidi wowote wa kuthibitisha madai hayo, basi yakifika malalamiko hayo kwa kadhi wa kiisilamu na akatakiwa kuthibitisha hilo na akawa ushahidi hana, hapo atatakiwa kupigwa mijeledi themanini (80 ).

➡Na kama akiwa mwenye kushuku na kutuhumu ni mume wenyewe , basi kama hana ushahidi juu ya hilo itabidi ipite hukmu ya kiapo cha kulaaniana baina yao , kama ilivyokuja katika aya zifuatazo :

➡Amesema Allaahu sw :
(وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنْفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ)
[Surat An-Noor 6]

Na wale wanao wasingizia wake zao na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli.

(وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَتَ اللَّهِ عَلَيْهِ إِنْ كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ)
[Surat An-Noor 7]

Na mara ya tano kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.

(وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَنْ تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ)
[Surat An-Noor 8]

Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba huyu mume ni miongoni mwa waongo.

(وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّهِ عَلَيْهَا إِنْ كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ)
[Surat An-Noor 9]

Na mara ya tano ya kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake kama mumewe yu miongoni mwa wanao sema kweli.

➡ Ikiwa umeona Kuna mambo yanayovunja heshma ya ndoa yake, basi wajibu wako wewe ni kumnasihi huyo mwanamke, na kumkumbusha adhabu ya Allaah sw, na wajibu wa mke kwa mumewe.

➡Na ikiwa bado Kuna kuendelea tatizo hilo, basi ni bora kuwaambia wazazi wake mwanamke huyo ili wamuonye kwa siri.

➡Na wao au mtu mwingine wanaweza kutumia njia ya hikma zaidi ili kuvunja ndoa baina yao.

➡Kwa sababu mume mwema haifai kuishi na mke muovu, na mke mwema pia haifai kuishi na mume muovu.

➡ Amesema Allaahu sw :
(الْخَبِيثَاتُ لِلْخَبِيثِينَ وَالْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثَاتِ ۖ وَالطَّيِّبَاتُ لِلطَّيِّبِينَ وَالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَاتِ ۚ أُولَٰئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ)
[Surat An-Noor 26]

Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Hao wameepushwa na hayo wanayo yasema; wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.

➡Kwa hiyo usiende kumuambia mume moja kwa moja suala kama hilo wakati ushahidi wa kufanyika zinaa kwa yakini haupo bado.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW AWAHIFADHI WANANDOA NA VIZAZI VYAO.

ALLAAHU AALAMU.

” Allaah anamrehemu mja mwenye kusema kheri akafaidika, akakaa kimya akasalimika “

AWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

kulikuwa na mke na mume wameowana, wakapata mtoto mmoja na kwa bahati mbaya wakaachana,sasa yule mtoto akawa analelewa na mama yake kwao, siku moja yule mume akaenda kumuangalia mwanawe pamoja na kumchukuwa ili atembee nae lakini, bibi wa mtoto akamkatalia yule baba. je bibi anayo haki hiyo ya kumzuwia mjukuu wake asichukuliwe na baba yake ? na nini hukmu ya huyu bibi ?

JAWABU 

➡Kisheria haki ya kulea mototo baada ya kuwa ndoa imevunjika baina ya mume na mke, inakuwa ni haki ya mama kwa daraja la kwanza.

➡Lakini pamoja na kuwa mama ana haki zaidi ya kumlea mtoto wakati mtoto hajafikia umri wa kubaaleghe, ila mama huyo hana haki ya kumzuia baba wa mtoto kumuona mtoto huyo, au kuwa nae kwa Muda mfupi.

➡ Kwa hiyo bibi hana haki ya kumzuia baba wa mtoto kumchukuwa mwanae kwa Muda, Kisha kumrejesha kwa mama yake tena kwa ajili ya kuendelea kulelewa.

➡Na mtoto tunae mzungumzia hapa ni mtoto ambae hajafikia umri wa kubaaleghe bado.

➡Katika Muda huo mama ndie mwenye haki ya kumlea mtoto huyo.

➡Na Katika fatwa aliulizwa samaahatu shaikh Ahmad bin Hamad AL khaliily h.f :

ما هي مدة حضانة الأم لأولادها ذكورًا وإناثًا؟

Ni upi Muda wa mama kumlea wanae , wakiume au wakike?

تراعي في ذلك مصلحة المحضون ذكرًا كان أو أنثى، ومع التشاجر يجب أن يجتهد القاضي في رعاية مصلحة الطفل، والله أعلم.

➡Jawabu ni kuwa :
Katika Hali hiyo yanachungwa maslaha ya mwenye kulelewa, ikiwa ni wa kiume au wa kike, na ikiwa Kuna magomvi – baina Yao – basi kadhi anatakiwa kuchunga maslahi ya mtoto.

➡Mtume saw alimuambia mwanamke alieshitakia kuhusu mwanae baada ya ikhitifu baina yake na mumewe :

جاء في الحديث عن الرسول ـ صلى الله عليه وسلم ـ: »أنتِ أحق به ما لم تنكحي«

” wewe una haki zaidi kwa huyu – mtoto – midhali hujaolewa – na mume mwingine”

➡Kwa hiyo hukmu ni kuwa :

“Bibi huyo amefanya makosa kumzuia mjukuu wake kuwa na baba yake kwa Muda huo.

➡Baba ana haki ya kumuona mwanae, na hata kutoka nae kwa badhi ya wakati, kwa kuwa mwanae ni sehemu Katika mwili wake.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW AZULIUNGANISHE NYOYO NA AJAALIE MAPENZI NA HURUMA BAINA YA FAMILY ZETU.

ALLAAHU AALAMU.

“Kuachana kwa mume na mke si sababu ya kuvunjika udugu “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

nauliza kuhusu: mwanaume alie muacha mkewe bila ya kumpa talaka si moja,mbili wala tatu, je kisheria ni Muda gani wakikaa mbali kati ya huyu mume na mke inakuwa si ndoa tena?
au hata wakikaa miaka nenda rudi bado wana rukhsa ya kuwa pamoja kama mke na mme?

JAWABU 

➡Ndoa baina ya mume na mke haivunjiki ila kwa kuivunja ndoa hiyo wao wenyewe.

➡Na miongoni mwa mambo ambayo yanavunja ndoa ni :

1- Talaka : “mume kutamka maneno yanayojulisha kukata uhusiano / mafungamano ya ndoa baina ndoa “

➡Amesema Allaahu sw :
(الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ …َ)

[Surat Al-Baqara 229]

T’alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri.


2 – Au kwa njia ya mke kutaka kujivua ndoa kwa mumewe, kwa kurejesha mke mahari aliyopewa na mumewe kwa mumewe.
(Inaitwa khul’uu ).

وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَنْ تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَنْ يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَنْ يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّهِ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ)

[Surat Al-Baqara 229]

Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlicho wapa wake zenu, ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu hapo itakuwa hapana lawama ikiwa mwanamke atajikomboa. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiikiuke. Na watakao ikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhaalimu.

3- Kulaaniana mume na mke kwa sababu ya kuwepo tuhma ya uzinifu, lakini bila kuwepo ushahidi wa watu wanne.

Amesema Allaahu sw :
(وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنْفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ)
[Surat An-Noor 6]

Na wale wanao wasingizia wake zao na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli.

(وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَتَ اللَّهِ عَلَيْهِ إِنْ كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ)
[Surat An-Noor 7]

Na mara ya tano kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.

➡Hicho juu ni kiapo atakachoapa mume.

➡Kisha baada ya hapo mke nae ataapa mara tano, ili kuweka ushahidi wa Allaah sw katika tuhma hiyo, ikiwa ni kweli au si kweli, muhimu dhamana ya Hilo anaachiwa Allaahu sw mwenyewe.

➡Amesema Allaahu sw :
(وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَنْ تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ)
[Surat An-Noor 8]

Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba huyu mume ni miongoni mwa waongo.

(وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّهِ عَلَيْهَا إِنْ كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ)
[Surat An-Noor 9]

Na mara ya tano ya kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake kama mumewe yu miongoni mwa wanao sema kweli.

4 – Hali nyingine ni mume kula yamini / kiapo kuwa hatomuingilia mkewe maingiliano ya kindoa.

Hii inaitwa ( iilaa ).

➡Amesema Allaahu sw :

(لِلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِنْ نِسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِنْ فَاءُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ)
[Surat Al-Baqara 226]

Kwa wanao apa kuwa watajitenga na wake zao, wangojee miezi mine. Wakirejea basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.

(وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ)
[Surat Al-Baqara 227]

Na wakiazimia kuwapa talaka basi, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mjuzi.

➡Kwa hiyo ikiwa halifanyika moja miongoni mwa mambo hayo, basi ndoa baina ya mke na mume itakuwa ipo kama kawaida, hata ukipita Muda mrefu baina Yao.

➡ Lakini mume anatakiwa asimfanyie madhara mkewe kwa kumuacha mbali nae Muda mrefu.

➡Ndio maana Khalifa Omar bin l khattwaaby r.a aliweka Muda wa kusafiri mume mbali na mkewe usizidi miezi Sita tu, ila awe amerudi kwa mkewe.

➡Ikiwa mke hawezi kuvumilia kuwa mbali na mumewe kwa Muda huo, na mume hataki kurudi au hajulikani aliko, basi mke akashitaki kwa Kadhi wa kiisilamu.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW AWAFANYIE WEPESI KATIKA NDOA NA MAISHA KWA JUMLA.


ALLAAHU AALAMU.

” katika uisilamu hakuna kujidhuru wala kumdhuru mwingine “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABABN AL BATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Hivi mwanamke akimpa mume sharti la kutomuingilia hadi amtimizie jambo fulani ambalo huyo mke anahitaji je hiyo ni halali ?

JAWABU 

➡Mume ana haki kisheria kumuingilia mkewe katika Muda wowote atakao kuhitajia, ila ikiwa yuko katika Hali ambazo kisheria imekatazwa kumuingilia.

➡Ikiwa sharti Hilo ni haki ya wajibu ya mke, na mke ameweka sharti Hilo tokea siku ya ndoa, sharti Hilo linazingatiwa ikiwa Mume atakubali tokea siku hiyo.

➡Mfano,
Mume amemuoa kwa deni la mahari, na mke akaweka sharti kuwa amekubali deni Hilo Lakini kwa sharti asimuingilie mpaka amtangulizie kiasi kadhaa cha mahari.

➡Mahari ni haki ya mke, na ni wajibu juu Mume.

➡Amma kinyume na yaliyokuwa hayo, au hayakuwekwa masharti hayo tokea siku ya ndoa, hukmu inaweza kutofautiana kwa mujibu wa haja ya huyo mke, na aina ya Hilo sharti lenyewe.

➡Amesema mtume saw katika hadithi ya Amruu bin Auf AL muzany :

…المسلمونَ على شروطِهمْ إلَّا شرطًا حرَّمَ حلالَا أوْ أحلَّ حرامًا”

الراوي: عمرو بن عوف المزني المحدث: الترمذي – المصدر: سنن الترمذي – الصفحة أو الرقم: 1352
خلاصة حكم المحدث: حسن صحيح


“Waisilamu – wanalazimika kwa mujibu wa – masharti Yao, isipokuwa Sharti litakalo halalisha haramu, au kuharamisha halali “

➡Asiweke mwanamke sharti Hilo bila ya haki za kisheria.

➡Na mume kwa nini asimtimizie mkewe mahitaji yake ya lazima mpaka awekewe masharti?

➡Kaeni kwa wema na ihsaani, na mapenzi na huruma .

➡NAMUOMBA ALLAAH SW AJAALIE MAPENZI NA HURUMA BAINA YA WAUME NA WAKE ZAO.

ALLAAHU ALLAAHU.

“kwa mapenzi na huruma ndipo ndoa hudumu daima “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Wanamke wa kiislamu kwenda saloon, je ni kweli ? na kama ni kweli ni kwa sababu gani ikiwa wote ni wanawake saloon.

JAWABU 

➡Mwanamke wa kiislamu anatakiwa kujiepusha na kila yenye kuwa kinyume na sharia za Allaah sw, na kuvunja utukufu na heshima Aliyopewa

➡Mwili wa mwanamke haifai kuonwa na mwanaume asiestahiki kuuona, Bali hata mwanamke muovu haifai kuuona Mwili wa mwanamke aliekuwa mwema.

➡Amesema ALLAAH SW :
(وَقُلْ لِلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِنْ زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ)
[Surat An-Noor 31]

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.

➡Katika hao wanaofaa kuonekana mapambo yao kwao wametajwa wanawake kwa sifa ya kuwa ni : ” أَوْ نِسَائِهِنَّ” , – Yaani “au wanawake wenzao”.

➡Na baadhi ya wafasiri wa Qurani wanaona kuwa, Nemo Hilo Katika Aya linaonyesha kuwa, “wawe wanawake hao ni waumini wa kweli mfano wao.

➡Na hii inaonyesha ubaya kwa muisilamu mwanamke kuonyesha mapambo yake kwa mwanamke aliekuwa si muisilamu.

➡Pia ubaya wa kuonyesha mapambo kwa mwanamke muisilamu Lakini si mwema, na wala hawezi kutunza siri za mapambo ya wanawake wenzake na uzuri wao.

➡Kwa hiyo hakuna uharamu wa moja kwa moja kuhusu mwanamke kwenda saloon.

➡Lakini ili kujuzu kwenda saloon mwanamke ni lazima kuzingatiwe yafuatayo :

1 – Iwe ni sehemu yenye stara na hishma.

2 – Kusiwe Kuna mchanganyiko baina ya wanaume na wanawake.

3 – Isiwe Kuna kutumia vitu vya najisi au Kubadilisha maumbile ya asili ya kiungo au Mwili.

4 – Iwe ni kwa Nia ya kujipamba kwa ajili ya mumewe au kwa wanaostahiki kumuona Lakini pasipokuwa na fitna na matamanio.

5 – Asitoke Peke yake kwenda saloon wala sehemu yoyote ya mbali ila awe na mumewe au mmoja Katika jamaa Zake wa kiume, ambao kwao ni haramu kumuoa uharamu wa kudumu. (mahramu ).

6 – As if hi hi rise mapambo hayo kwa yoyote asiestahiki kuona mapambo yake.

➡Yakitimia hayo inshaallaah sw hakuna kizuizi kwa mke kwenda kujipamba kwa ajili ya mumewe.

➡Na pambo Katika asili yake linajuzu, ila tu Yale ambayo yameharamishwa Katika uisilamu.

➡Amesema ALLAAHU SW :
(قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ)
[Surat Al-Araf 32]

Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW ATUBARIKIE NDOA NA VIZAZI VYETU.

ALLAAHU AALAMU.

“Allaah ni mzuri na anapenda uzuri na mazuri “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

JE Mwanamke akiwa katika ada yake afaa kuweka dawa ya nyewele ?


JAWABU 

➡Mwanamke anapokuwa katika siku Zake za ada ya mwezi, panaharamishwa maingiliano ya kindoa baina Yao.

➡Amesema Allaahu sw :
(وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ)
[Surat Al-Baqara 222]

Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat’ahirike. Wakisha t’ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.

➡Alikuwa sheikh wetu Dk Muhammad Abdu sshaafy Ismail AL misry – Allaahu amuhifadhi – akituambia Kuwa:

Kitendo ” فَاعْتَزِلُوا” yaani maana Yake ni ” Basi jitengeni” , Kitendo hiki kinaonyesha hatari ya Kuwa karibu na jambo lilotajwa hapo katika aya.

➡Bila Shaka mke akiwa katika siku Zake za ada ya mwezi Kisha akajipamba kwa mapambo mbali mbali, hiyo inaweza kupelekea kumpa mume matamanio, na huenda akashindwa kuvumilia ila akidhi matamanio yake kwa mkewe.

➡Na kwa Kuwa mke atakuwa yuko katika Hali hiyo, mume akiwa hana uchamungu anaweza kujikuta anamuingilia mkewe katika sehemu hiyo iliyoharamishwa katika wakati wa ada hiyo.

➡Na huenda akafanya lililokuwa kubwa zaidi – Allaahu atunusuru – huenda akamuingilia katika utupu wake wa nyuma, na hivyo ni dhambi kubwa Sana.

➡Kutokana na hayo , maulamaa wametoa fatwa Kuwa :” Mwanamke wakati wa ada yake , haruhusiwi kujipamba kwa mapambo ya aina yoyote yenye kumvutia mume “

➡Na wengine wanaona hata kukata kucha na kutana / kuchana nywele kwa Mwanamke mwenye Kuwa katika hedhi au nifasi haipendezi – yaani ni makruuhu.

➡Kwa hiyo JAWABU ni Kuwa : ” asiweke dawa ya nywele wala mapambo yoyote wakati wa ada ya mwezi, hiyo ni salama kwake na mumewe.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW ATUWEZESHE KUHIFADHI MIPAKA YA SHERIA ZAKE.

ALLAAHU AALAMU.

” usikaribie penye hatari, tahadhari kujikuta umeangukia katika hatari “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTWAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je inajuuzu kufungisha ndoa mwanamke akiwa na mimba ?

JAWABU 

➡Mwanamke mwenye mimba hakosi kuwa ni mmoja katika Hali zifuatazo:

1- Imma ni mke wa mtu, na huyo ni haramu kumuoa kwa mujibu wa dalili sahihi katika Qurani na sunna na makubaliano ya maulamaa wote.

➡Amesema Allaahu sw kuhusu wanawake walio haramika kuwaowa :

(وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُمْ مَا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَنْ تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُمْ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُمْ بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُمْ بِهِ مِنْ بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا)
[Surat An-Nisa 24]

NA WANAWAKE wenye waume, isipo kuwa walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sharia ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalilishiwa wasio kuwa hao, mtafute kwa mali yenu kwa kuowa pasina kuzini. Kama mnavyo starehe nao, basi wapeni mahari yao kwa kuwa ni waajibu. Wala hapana lawama juu yenu kwa mtakacho kubaliana baada ya kutimiza waajibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua na Mwenye hikima.

2 – Imma atakuwa ni mtalaka wa mume aliekuwa amemuacha, au ni mke ambae amefiliwa na mumewe.

Huyo pia haifai kumuoa kwa kuwa atakuwa yuko katika eda, au atakuwa katika hukmu ya ndoa ikiwa ameachwa na mumewe aliekuwa Hai.

➡Amesema Allaahu sw :

(وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُمْ بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنْتُمْ فِي أَنْفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَٰكِنْ لَا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَنْ تَقُولُوا قَوْلًا مَعْرُوفًا ۚ وَلَا تَعْزِمُوا عُقْدَةَ النِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْكِتَابُ أَجَلَهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنْفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ)
[Surat Al-Baqara 235]

Wala si vibaya kwenu katika kupeleka posa kwa ishara tu kwa wanawake waliomo edani au mkadhamiria katika nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msiwaahidi kwa siri, ila mnene maneno mema. Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka eda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo katika nafsi zenu. Basi tahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole.

3 – Na Imma atakuwa mwanamke huyo ana ujauzito wa zinaa tu, na Wala Hana mume Wala Hana ndoa katika asili,

Huyo hukmu yake kuolewa akiwa na mimba Kuna ikhtilaafu baina ya maulamaa.

➡Tazama ufafanuzi huu ufuatao hapa :

1⃣Madhehebu ya hanafy:
” Imekuja katika kitabu cha Al fataawaa l hindiya fii fiqhi l hanafiya juzuu ya 1 / 526 :
“Inajuzu kumuoa mwanamke aliezini, hata bila ya kukaa eda, na hata akiwa ana ujauzito wa zinaa inafaa kumuoa kabla hajazaa, lakini mume asimuingilie kabla hajazaa “

Hiyo ni Kauli ya abuu Hanifa na Muhammad mwanafunzi wake.

➡ Amma zafru – nae ni mwanafunzi wa abuu hanifa pia, yeye amesema :
” Haijuzu kumuoa – mwenye mimba “

Na hoja ya Zafru ni kuwa :
” Ikiwa ujauzito huo wa zinaa unamzuia mume uhalali wa kumuingilia , basi pia ujauzito huo unazuia ndoa , kwa sababu makusudio ya ndoa pia ni mume kumuingilia mkewe, sasa ikiwa haifai kumuingilia itakuwa ndoa hiyo haina faida, na ndio maana hata mimba ya ndani ya ndoa inazuia kumuoa mke huyo “

➡ Na kwa madhehebuya Hanafy wanasema wote kuwa;
” Ikiwa mwanamke mjamzito ni ujauzito wa mwanaume huyo huyo aliezini nae, inajuzu kumuoa na mimba yake…”

2⃣Madhehebu ya Shaafy :
“Ni makruuhu kumuoa mwanamke mzinifu mwenye ujauzito wa zinaa…

3⃣Madhehebu ya Maaliky :
” Ikiwa mwanamke amezini, si halali kwa mwanaume yoyote mwenye kujua hivyo kumuoa mwanamke huyo, ila kwa masharti mawili kutimia :

1- Akae eda na hadi umalize muda wa eda, na eda yake ni kupata hedhi tatu kamili.

2 – Mpaka azae mimba yake.

4⃣Madhehebu ya Al dwaahiry :
” Akibeba ujauzito mwanamke katika njia ya zinaa, inajuzu kuolewa kabla ya kuzaa mimba yake, isipokuwa si halali kwa mumewe kumuingilia mpaka atakapo zaa mimba yake “

5⃣Madhehebu ya Hanbaly :
” Ni wajibu kwa mwanamke aliezini akae eda kwanza, mpaka imalize eda yake kwa kuzaa mimba yake ,

6⃣Madhehebu ya Al jaafariya – katika Shia :
” Akizini mwanamke haiharamiki kumuoa mwanaume aliezini nae au mwanaume mwingine, na inajuzu kwa aliemuoa kumuingilia mwanamke huyo “

7⃣Madhehebu ya ibaadhi:
” Mwanamke mzinifu au alieziniwa ni wajibu kukaa eda, na eda yake ni hedhi tatu ikiwa anapata hedhi, au miezi mitatu ikiwa ambae hapati hedhi, na akiwa mjamzito ni mpaka azae mimba yake “

➡ Utaona kuwa kuna ikhtilafu baina ya maulamaa kama ilivyitangulia, lakini kumbuka na kuzingatia kuwa :

1 – Ndoa yenye baraka ni iliyojengeka kwa misingi halali.

2 – Utulivu wa nafsi na uaminifu baina ya wazinifu haupatikani baada ya kuoana.

3 – Kuruhusu hayo ni kinyume na makusudio ya sheria katika kuhifadhi kizazi na nasabu zao.

4 – Hii pia inafungua milango ya watu kuziniana bila kujali mipaka ya ALLAAH S.W.

5 – Yote hayo ni kinyume na adabu za kiisilaamu kwa mujibu wa Qurani na sunna.
➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA.

ALLAAHU AALAMU.

” Usivuke mipaka ya ALLAAH S.W utaangamia “

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Misikiti mingi imekuwa ikifungua maduka kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa misikiti hiyo, sasa kuna baadhi ya misikiti huwa inapangisha watu wanaouza vitu ambavyo havifai katika uislamu, mfano mawigi, kucha za bandia, suruali za kubana n.k , je inafaa au inakuwa ni njia moja wapo ya kueneza maasi?

JAWABU

➡Misikiti ni nyumba za ALLAAH sw, na nyumba hizo ni kwa ajili ya kufanyia ibada za ALLAAH SW.

➡Amesema ALLAAH SW:
(فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّهُ أَنْ تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ)
[Surat An-Noor 36]

Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni

➡Hiyo ni hukmu kuhusu misikiti kwa upande wa ndani yake .

➡Amma kuhusu eneo la msikiti ambalo limeuzunguka misikiti huo, au pembezoni mwake, Hilo pia ni lazima liheshimiwe na kuhifadhiwa.

➡ Inajuzu kutumia sehemu ya ardhi kwa kuifanyia Lopate ambacho kitasaidia katika kuingiza pato la kuhudumia msikiti huo.

➡Inajuzu kufanyia kilimo na kutumika pato Hilo kwa maslahi ya msikiti huo huo, au kukodisha maduka kwa utaratibu huo tulio utaja hapo juu.

➡Na ili jambo Hilo likubalike kisheria, ni lazima yazingatiwe mambo yafuatayo :

1- Iwe kazi itakayofanyika pahala hapo ni kazi ya halali kisheria .

Kin yum na hapo haikubaliki abadan; k v;
Kuuza sigara, pombe, mavazi yasiyo ya stara, au au mapambo yaliyoharamishwa katika uisilamu, au ukumbi wa kamari, na mfano wa hayo.

2 – Isiwe sehemu hiyo inapelekea kuchanganyika wanaume wanaokuja msikitini na wanawake wanaokuwa katika maduka hayo

3 – Pato linalopatikana liwe ni haki ya msikiti, na lifanyiwe kazi inayohusu msikiti huo.

➡Maduka katika ardhi ya msikiti ni lazima yawe na heshima na kuchungwa mipaka ya sharia za Allaah sw katika kila upande.

➡Na wala haifai kukodisha kwa mwenye biashara ya haramu au shubha katika uharamu wake.

➡Na kuuza mawigi na madude yote ya bandia wanayo tumia baadhi ya wanawake katika milli Yao ni haramu kuyauza wala kuyavaa kwa muisilamu yoyote yule.

➡Na hayo yote ni haramu kwa kuwa Yana peeked katika haramu, na mwenye kutumia hayo basi anelaaniwa na Allaah sw.

➡Na ikiwa anauza minywele hiyo ya bandia basi ajue kuwa anauza yaliyoharamishwa na Allaah sw.

➡Na ajue kuwa anachsngia katika kueneza madhambi katika miji na waja.

➡Na atakuwa amekanusha amri ya Allaah sw aliposema:

(… ۘ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ)
[Surat Al-Maeda 2]

Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

➡Bali hata katika fatwa za maulamaa ni kuwa : “haijuzu kukodisha kiwanja cha mpira ikiwa wachezaji watakuwa wamevaa mavazi ambayo hayana stara kwa mujibu wa sharia za kiisilamu “.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW ATUJAALIE PATO LA HALALI NA ATUEPUSHE NA YA HARAMU.

ALLAAHU AALAMU.

“Kilicho karibu na kingine basi huwa hukmu Zake sawasawa “

AWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Naomba jawabu Ustaadh: Nina ndege nafuga nyumbani. Je inajuzu kuwa nae au nimrejeshe dukani au nimgawe ?

JAWABU

➡Ndege na wanyama na mfano wa hivyo vyote ni miongoni mwa neema za ALLAAH s.w .

➡Nabii suleimaan a.s alipewa ufalme wa kumiliki kila aina za wanyama na Ndege na hata kujua maana ya maneno kupitia sauti zao

➡ Na hiyo kwake ilikuwa ni miongoni mwa miujuza aliyopewa na ALLAAH S.W

➡Amesema ALLAAH S.W
(وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ ۖ وَقَالَ يَا أَيُّهَا النَّاسُ عُلِّمْنَا مَنْطِقَ الطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِنْ كُلِّ شَيْءٍ ۖ إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ الْفَضْلُ الْمُبِينُ)
[Surat An-Naml 16]

Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri.

➡Hakuna kizuizi kufuga ndege nyumbani kwako inshaallaah, kakini unatakiwa kuzingatia yafuatayo :

1- Awe ndege huyo Hana madhara kwa watu na Mali zao ikiwa utamfuga karibu na nyumba zao.

2 – Uwe na uwezo wa kumpatia mahitaji yake ya lazima ambayo ni katika kuhifadhi uhai wake.

3 – Asiwe mwenye kukushughulisha hata ukashindwa kufanya ya wajibu juu yako kwa ajili yake.

4 – Isiwe kumfuga kwako ni sababu ya kufa au kupata shida Zaidi kwa kiumbe huyo.

➡Ukitimiza masharti hayo basi Hakuna tatizo wala kizuizi chochote, kwa kuwa anaingia katika jumla ya tulivyo halalishiwa na ALLAAH SW.

➡Hiyo Nido kauli sahihi ya maulamaa wengi katika madhehebu yote ya kiisilamu.

➡Amma tofauti za baadhi ya maulamaa kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo :

1 – Inajuzu kufuga ndege na mfano wake kwa ajili ya pambo na furahisho katika nyumba.

Na hii ni kauli ya Hanafy, maaliky, shaafy, na imaamu Ahmad bin hanbal katika moja ya mapokezi kutoka kwake.

➡Na hoja ya kauli hii hadithi ya swahaabiyy Anas bin maalik r.a , anasema:

– إن كان النبي صلى الله عليه وسلم ليخالطنا ، حتى يقول لأخ لي صغير : ( يا أبا عمير ، ما فعل النغير ) .

الراوي: أنس بن مالك المحدث: البخاري المصدر: صحيح البخاري الصفحة أو الرقم: 6129 خلاصة حكم المحدث: [صحيح]

” Alikuwa mtume (saw) akiwa pamoja na sisi kila Mara, hata akawa akimuambia ndugu yangu mdogo, ambae alikuwa akiitwa abaa umeir, “nini amefanya nugheir ?”

➡Na nugheir ni aina ya ndege wadogo wadogo, alikuwa ndugu yake Anas akimfuga ndege Huyo, Kisha akafariki, siku hiyo akawa ndugu yake Anas Ana huzuni Sana.

➡Mtume (saw ) hakumkataza kufuga ndege na alikuwa akimuondoshea huzuni kwa maneno hayo , baada ya kumuona Ana huzuni.

2 – Baadhi ya maalikiya wanaona ni makruuhu kufuga ndege au wadudu.

3 – Na Ibnu uqail nae ni katika madhehebu ya Hanbaly, anaona kuwa ni haramu kufuga wadudu na mfano wake.

➡Kauli ya kwanza ya kusihi kufuga ndege au aina za wadudu kwa masharti niliyoyataja juu hapo ndio Kauli sahihi.

➡Kwa hiyo ikiwa unaona huna uwezo wa kumuhudumia , na unahofia kupatikana madhara kuendelea kukaa nae, basi ni bora kumpa mtu mwingine mwenye uwezo wa kumtazama kikamilifu.

➡Na hata ikilazimu kuwauzia wenye it a Alamo au sehemu za maonyesho basi ni bora Zaidi, hii ni katika Hali ambayo hukuweza kumsimamia ndege huyo.

➡ NAMUOMBA ALLAAH SW ATUPE KHERI ZA DUNIA NA AKHERA

ALLAAHU AALAMU.

“uisilamu umehalalisha mapambo kwa mipaka ya kisheria “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Mfano mtu kaja kwako akamkuta mume hayupo akaita mama khamis mathalan khamis ni jina la mume ukaja ukaitikia inakuwa mwanamke kashaachika ? maana kuna watu wanasema hivyo ushaachika ni kweli?

JAWABU

➡Katika sharia ya kiisilaamu tumekatazwa kuwafananisha wake zetu na kuwafanya kama mama zetu.

➡Amesema ALLAAHU S.W :
(الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنْكُمْ مِنْ نِسَائِهِمْ مَا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنْكَرًا مِنَ الْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ اللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ)
[Surat Al-Mujadala 2]

Wale miongoni mwenu wanao watenga wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale walio wazaa. Na hakika hao wanasema neno linalo chusha, na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria, Mwenye kusamehe.

➡ Hiyo ni kwako wale ambao wanajitenga na wake zao na kujiharamishia kuwaingilia kama walivyo haramika mama zao juu yao.

➡Miongoni mwa makosa ambayo baadhi ya waisilamu huyafanya ni : mke kujiita jina la kuwa kama yeye ni mama wa mumewe “

➡Hili ni kosa Miongoni mwa makosa wayafanyayo baadhi ya watu kwa kutaka umaarufu na umashuhuri tu.

➡Lakini kufanya hivyo hakupelekei kuharamika ndoa baina ya mke na mume, ikiwa haikukusudiwa kumuharamisha mke kwa mume au mume kwa mke.

➡ Na Katika suali Hili inaonyesha wazi kuwa huyo mwanamke aliitika tu kwa kuwa ameitwa na mtu mwingine kwa jina ambalo kana kwamba yeye ni mama wa mumewe.

➡Kutokana na Hilo hakuna tatizo lolote Katika ndoa Hiyo inshaallaah kwa Hilo lililotokea.

➡Lakini anatakiwa kuwakataza wenye tabia Hiyo, ili wasiendelee kueneza kumuita kama hivyo, na awajulishe kuwa kufanya hivyo ni makosa na uzushi, na ALLAAHU s.w hapendi Hilo.

➡NAMUOMBA ALLAAH
S.W ATUONGOZE KATIKA YENYE KHERI.

ALLAAHU AALAMU.

” Mume asifamye mkewe kuwa kama mama, wala mke asimfanye mumewe kuwa kama baba”

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN AL BATTAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je inafaa mwanamke kusafiri kwenda africa kuona ndugu na jamaa zake bila kuwa na mahram? lakini mumewe kampa ruhusa aende ?  

JAWABU 

➡ Uisilamu ni dini ambayo sheria zake zinahukumu kwa kuhifadhi maslahi ya dini na maadili na utu na mipaka ya kila jambo.

➡ Mwanamke katika sheria ya KIISILAMU haruhusiwi kusafiri safari yoyote kubwa yenye umbali isipokuwa awe pamoja na mumewe au mmoja katika ndugu zake wa kiume, ambao wao kisheria wanaharamika kumuoa uharamu wa kudumu.

➡ Na hao ndio wanaita “mahramu ” katika lugha ya sheria ya KIISILAMU.

➡ Amesema mtume s.a.w Katika hadithi ya Abii huraira r.a, aliyopokea imaamu al bukhaary :

لا يحل لأمرأة ، تؤمن بالله واليوم الآخر ، أن تسافر مسيرة يوم وليلة ليس معها حرمة .
الراوي: أبو هريرة المحدث: البخاري – المصدر: صحيح البخاري – الصفحة أو الرقم: 1088
خلاصة حكم المحدث: [صحيح]

” Si halali kwa mwanamke mwenye kumuamini ALLAAH S.W na siku ya mwisho, akasafiri mwendo wa usiku na mchana, isipokuwa pawe na mahram “

➡ Na hii haimaanishi kuwa safari ikiwa ni ndefu lakini usafiri wake ni wa kufika haraka kuwa inafaa kusafiri peke yake, bali hata kama itakuwa ni usafiri wa ndege, kwa kuwa safari ni safari tu.

➡ Ikiwa kuna dharura na mume hayuko, na Mahramu yake pia hakuna, basi mwanamke huyo asafiri pamoja na wanawake wenzake wengine – kwa kuwa hii ni vyepesi zaidi.

➡ Mume hana haki ya kutoa ruhusa hiyo kwa mkewe , kwa kuwa yeye hatakiwi kumpa ruhusa ambayo ALLAAH S.W amemnyima kwa hikma.

➡ Kwa hivo mwanamke huyo mipaka ya kutoka kwake aifuate kama ilivyo banishwa.

➡NAMUOMBA ALLAAH S.W ALLAH ATUJAALIE KHERI NA KUFUATA QURANI TUKUFU NA SUNNA ZA MTUME S.A.W:

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je kama mume alimpa mkewe talaka moja kisha akamrejea, wakaishi salama, ila baada ya muda ukatokea mtafaruku mume akamuongeza mkewe talaka mbili ilihali mkewe mjamzito , jumla zitakuwa tatu.
sasa swali langu ni ‘hivi: ” zile talaka mbili za mwisho zimesihi ? naombeni fatwa

JAWABU

➡ Talaka katika sheria ya KIISILAMU inasihi kuwa ni talaka ikiwa mume amemuacha hali ya kuwa yuko katika ndoa kihakika au kihukmu.

➡ Mke ambae yumo ndani ya eda ya talaka ya kurejewa, anahesabika kuwa ni mke, kwa kuwa mume ana haki ya kumrejea wakati wowote bila kizuizi cha aina yoyote.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنْفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَنْ يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِنْ كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ)
[Surat Al-Baqara 228]

Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka t’ahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuzii kuficha alicho umba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu. Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

➡ Kwa hiyo talaka hizo mbili alizomuacha mkewe wakati yuko ndani ya eda na mjamzito, talaka zinasihi na kuhesabika tayari.

➡ Ujauzito si kizuizi katika kusihi talaka.

➡ Isipokuwa kuna ikhtilafu baina ya maulamaa kuhusu talaka za bid’aa, je zinahesabika au hazihesabiki??

Hii ni suala lenye ikhtilafu baina ya maulamaa wa madhehebu za maimamu mbalimbali wa kiisilaamu.

➡ Na Kauli ya waliosema kuwa inahesabika kuwa mbili ni mbili na tatu ni tatu, ni Kauli yenye nguvu kwa upande wake.

➡ Na Kauli hiyo inasaidia katika fatwa za maulamaa kuzuia kuenea kwa talaka bila kuchunga mipaka ya ALLAAH S.W.

➡ Kwa hiyo hiyo ndio hukmu ilivyo, na jambo hili la Talaka halina mzaha .

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.


” Hifadhi ndoa yako muisilamu, na chunga kizazi chako “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Mtu akitubia lakini kishafanya zinaa muda mwiñgi mpka kishapta mtoto wa zinaa, yeye anasema ameshakata tamaa , Je Allaah atanisamehe?

 JAWABU 

➡ ALLAAHU S.W ni Mwingi wa kusamehe na Mwenye huruma kuliko yoyote wala chochote.

➡ Anasamehe waja wenye kutubia, na ni Mkali wa kuadhibu kwa wenye kukaidi na kuacha kurudi kwake.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ)
[Surat Al-Hijr 49]

Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

(وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الْأَلِيمُ)
[Surat Al-Hijr 50]

Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu!

➡ Yeye amewaumba waja wake na yeye ndie mjuzi kwao, anawajua undani wao na udhaahiri wao.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ)
[Surat Al-Mulk 14]

Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?

➡ Muisilamu aliefanya makosa au madhambi, ametakiwa na ALLAAH S.W asikate tamaa kutokana na Rehma za ALLAAH S.W.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنْفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ)
[Surat Az-Zumar 53]

Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

➡ Katika aya hiyo amekata ALLAAH S.W kukata tamaa, kwa hiyo ikiwa mwenye kuasi atakata tamaa na kuacha kutubia kwa ALLAAH S.W, hapo atakuwa anaongeza kosa jingine tena juu ya kosa la mwanzo.

➡ Kwa hiyo asikate tamaa kabisa kukubaliwa toba yake kwa sababu ya zinaa hadi kupata mtoto, wakati fursa ya kutubia iko wazi muda huu.

➡ Jambo muhimu tu ni kutubia toba ya kweli safi isiyokuwa na uongo ndani yake.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَنْ يُكَفِّرَ عَنْكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)
[Surat At-Tahrim 8]

Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

➡ Na baada ya toba muisilamu anatakiwa kuzidisha amali njema.

➡ Amesema ALLAAHU S.W baada ya kukataza kukata tamaa na rehma zake :

(وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ)
[Surat Az-Zumar 54]

Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake, kabla ya kukujieni adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa.

(وَاتَّبِعُوا أَحْسَنَ مَا أُنْزِلَ إِلَيْكُمْ مِنْ رَبِّكُمْ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ بَغْتَةً وَأَنْتُمْ لَا تَشْعُرُونَ)
[Surat Az-Zumar 55]


(وَاتَّبِعُوا أَحْسَنَ مَا أُنْزِلَ إِلَيْكُمْ مِنْ رَبِّكُمْ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ بَغْتَةً وَأَنْتُمْ لَا تَشْعُرُونَ)
[Surat Az-Zumar 55]

Na fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyo teremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, kabla haijakujieni adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui.

➡ Hakuna dhambi kubwa kuliko ukafiri, lakini ALLAAHU S.W ameahidi kusamehe hata walio kufuru, lakini kwa sharti waache ukafiri wao, vipi ashindwe kumsamehe huyo aliefanya zinaa na akajutia hali ya kuwa ni muisilamu?

➡Amesema ALLAAHU S.W :
(قُلْ لِلَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ يَنْتَهُوا يُغْفَرْ لَهُمْ مَا قَدْ سَلَفَ وَإِنْ يَعُودُوا فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ الْأَوَّلِينَ)
[Surat Al-Anfal 38]

Waambie wale walio kufuru: Wakikoma watasamehewa yaliyo kwisha pita. Na wakiyarudia basi imekwisha pita mifano ya wa zamani.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUHIFADHI NA MAASI, NA ATUJAALIE TOBA KABLA YA KUFA.


ALLAAHU AALAMU.

“Tubia haraka kabla ya mlango wa toba haujafungwa “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Kuhusu kufanya tendo la ndoa chooni, kuna vyoo vingine ni vizuri kuliko hata chumba cha kulala, je na humo pia haifai ?

JAWABU

➡ Watu wengi wamekuwa wakizidi kurejea suala hili kwa maswali ya kila aina.

➡ Na wengine wanafasiri kuwa nimesema kuwa ni haramu kufanya tendo la ndoa chooni, wakati mimi sikusema kuwa ni haramu.

➡ Jambo kuwa halifai kulifanya haina maana kuwa kila ambalo halifai ni haramu.

➡ Kuna mambo yanakuwa hayafai kuyafanya lakini ni katika hukmu ya kuwa ni makruuhu tu, na sio uharamu wa kuwa akifanya mtu jambo hilo atapata dhambi.

➡ Katika Fataawa za samaahati shaikhinaa Ahmad bin hamad alkhaliily ALLAAH amuhifadhi, aliulizwa kuhusu mume kumuingilia mkewe katika mas’baha – Yaani sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kukoga “

➡ Na jawabu ilikuwa ni kuwa : ” Hakuna kizuizi kufanya hilo “

➡ Rejea kitabu cha ” Al mar’atu tas alu juzuu ya pili , ukurasa wa 129.

➡ Na zimekuja dalili nyingi katika sunna kukataza mume na mke kuingiliana wakiwa bila ya nguo kama wanyama wawili – au ngamia wawili “

➡ Kuna tofauti kati ya choo na bafu katika matumizi ya lugha kati ya maneno hayo, na katika suala hili lililo ulizwa maana ya iliyo karibu ni chooni kwa maana inayojulikana kwa mujibu wa matumizi ya neno hilo.

➡ Kwa hiyo ikiwa ni sehemu ya kukogea na yenye usafi na nafasi, kwa mwenye kufanya tendo la ndoa humo hakuna tatizo lolote kama walivyotoa fatwa maulamaa.

➡ Amma ikiwa ni sehemu maalumu kwa ajili ya kuendea haja tu, kama nilivyotanguliza mwanzo ni kuwa si bora kufanya hivyo, na hasa miongoni mwa adabu za kuingiliana ni kusema ” Bismillaah, allaahuma jannibnaa sshaitwaana maa razaqtanaa “

➡ Ikiwa atasema hayo wakati wa kutaka kuingiliana kisha wakakadiriwa na ALLAAH S.W kupata mtoto, basi hatomdhuru shetani – mtoto huyo “

➡ Fadhila na ubora ni kufuata yaliyokuwa bora zaidi katika dini.

➡ Na kwa kuwa hakuna dalili yoyote ya kuharamisha wala kuamrisha jambo hilo, kwa hivyo inabakia hukmu ni moja ya hali zifuatazo :

1 – Imma ni halali moja kwa moja, kwa kuwa hakuna dalili ya kuharamisha.

2 – Na imma itakuwa ni makruuhu, kwa kuwa kuna mambo mengi ya sunna za jimai atayakosa ikiwa atafanya jimai humo.

Na sunna hizo zimethibiti katika hadithi mbalimbali.

➡ Jambo lenye ikhtilafu halaumiki mja kufuata kauli moja miongoni mwa kauli.

➡ Kwa hivyo kusema kuwa haifai haina maana kuwa ni haramu, bali ni kwa kauli moja miongoni mwa hizo mbili nilizokutajia juu hapo.

➡ Zaidi unaweza kurejea kwa Mufti katika nchi ambayo wewe unaishi, kwa kuwa fatwa zinazofautiana kwa mujibu wa mazingira na zama Katika baadhi ya mambo.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJALIE KUWA NA HAYA NA HIKMA KATIKA KUFUATA MUONGOZO WA DINI.

ALLAAHU AALAMU.

” Ukamilifu wa muumini ni kuwa na waraa: “Nayo ni muisilamu kuacha lililokuwa si tatizo kulifanya, kwa ajili ya kuhofia kulifanya lenye tatizo :

 JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Eti nini ubaya wa mwanamke kuvaa mkufu miguuni ?

JAWABU 

➡ Mapambo kwa wanaadamu yamehalalishwa na ALLAAH S.W, isipokuwa tu yamewekewa masharti maalumu katika kuvaa mapambo hayo.

➡ Hata wanawake wema katika maswahaba r.a na wengine walikuwa wakitubia mapambo hayo, ikiwa ni ya kuvaa masikioni , mikononi au miguuni.

➡ Na katika QURANI tukufu ALLAAH S.W amewakataza wanawake kupiga miguu chini kwa nguvu wakati wa kutembea, ili mapambo yao yaliyo fichikana yasije yakasikikana wakati kaa watu wasiokuwa mahramu zao.

Na katika aya ifuatayo ALLAAH S.W amebainisha mapambo hayo na hukmu zake.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَقُلْ لِلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِنْ زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ)
[Surat An-Noor 31]

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.

➡ Kutokana na dalili hiyo na nyingine katika sunna, Hakuna ubaya kwa mwanamke kutia pambo hilo miguuni, lakini azingatie yafuatayo kwa mukhtasari:

1- Asifanye israafu katika mapambo kupita ada (kawaida ).

2 – Asivae kwa watu wasio stahiki kuona mapambo yake.

3 – Avae nguo ndefu inayofunika mapambo yake.
➡NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU

(Uisilamu ni dini ya wepesi katika sheria zake )


JAWABU KUTOKA KWA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Ustaadh :Akitaka muisilamu katia udhu, je ni lazina aanze duwa hii au si lazima sukran ?
نيتي واعتقادي إنى أتوضأ لصلاتي أداء للفرض طاعة لله ولرسوله محمد صلى الله عليه وسلم

JAWABU 

➡ Kutia udhu ni moja katika miongonimwa ibada za usafi kwa ajili ya ibada.

➡ Na kwa kuwa ibada yoyote katika uisilamu huwa malipo yake hayawi ila kwa nia, udhu pia ni lazima ufanyike kwa nia.

➡ Lakini nia ni nini?
Nia ni : ” Makusudio katika nafsi kwa Ajili ya kufanya amali fulani kwa kutaka radhi za ALLAAH S.W”.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ “َ)
[Surat Al-Maeda 6]

Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni.

➡ Kwa mujibu wa swali lako jawabu ni kuwa :
” Kutamka nia kwa maneno na sauti kuipandisha hiyo ni miongoni mwa uzushi katika Dini ya kiisilaamu.

➡ Wajibu ni kukusudia tu ndani ya moyo, na hiyo ndio nia sahihi kwa mujibu wa sunna iliyothibiti.

➡ Usihangaishe nafsi kuhifadhi maneno ya nia, nia haisomwi wala haitamkwi , makini nia inakusudiwa kwa ndani ya moyo tu.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

“Uisilamu ni kufuata na wala si kuzusha “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je inafaa kwa wanandoa kuingiliana wakiwa chooni ?

JAWABU

➡ Jambo la maingiliano ya kindoa ni jambo ambalo limewekewa utaratibu maalumu katika uisilamu.

➡ Na kwa kuwa miongoni mwa malengo makuu ya ndoa ni kujenga mapenzi na huruma ili kupata utulivu, basi ni lazima kuandaa mazingira ya kuleta utulivu huo.

➡ Vipi utapatikana utulivu ikiwa wanafanya jambo hilo katika sehemu ambayo ni sehemu ya kukidhia haja mbalimbali?

➡Na vipi iwe sehemu hiyo ambayo ni makaazi ya shetani?

➡Vipi ataweza kutimiza lengo la jambo hilo hali ya kuwa hata sehemu ya utulivu wa mwili na nafsi hakuna?

➡Jambo hili halifai kwa muisilamu kulifanya, na hali ya kuwa ALLAAH S.W ameweka utulivu ni kuwa katika nyumba.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَاللَّهُ جَعَلَ لَكُمْ مِنْ بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُمْ مِنْ جُلُودِ الْأَنْعَامِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَا أَثَاثًا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ)
[Surat An-Nahl 80]

Na Mwenyezi Mungu amekujaalieni majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama nyumba mnazo ziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao na manyoya yao na nywele zao mnafanya matandiko na mapambo ya kutumia kwa muda.

➡ Vitu vyote hivyo vimetajwa kuwa ni miongoni mwa alivyojaalia ALLAAH S.W kwetu sisi.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUWEZESHE KUFUATA MIONGOZO WA DINI YETU YA KIISILAAMU.

ALLAAHU AALAMU.

” Uisilamu ndio dini yenye mfumo sahihi “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Mama amefariki afrika, kaacha bangili za fedha na mikufu,vitu vingi nikapewa mimi nikae navyo, bibi alipokuja huku oman nikaona nimpe avilete vitu hivyo oman, achukua, ila sikumbuki nilimwambia achukue au akae navo nikaja oman nimemkuta kafariki. Je niwalipe pesa? Na mimi sijui thaman yake.naomba jibu.

JAWABU

➡ Mali yoyote kisheria, ambayo imerhusika kisheria kuwa ni mali, basi ni lazima ihifadhiwe.

➡ Na mali maana yake ni :
” Kila ambacho inawezekana kukimiliki na kunufaika nacho kisheria na kimazoea.

➡ kwa maana hiyo;
Hizo bangili na mapambo yote ya marehemu huyo – ALLAAH ampe rehma zake – zilikuwa ni mali yake wakati wa uhai wake.

➡ Kwa hiyo baada ya kufa kwake marehemu huyo, mali hiyo inarudi kuwa ni haki ya warithi wote wenye haki ya kumrithi kisheria.

➡ Ilitakiwa wewe dhamana wa kusimamia mali hiyo na kuihifadhi uipeleke mali hiyo kwa warithi wanao husika nayo, ili ifanyiwe tathmini kwa pesa ili kila mwenye haki apwe haki yake mwenyewe

➡Kwa kuwa mali imepotea sasa, na wewe ulibeba dhamana hiyo, lakini hukuisimami na
Kuilinda ipasavyo, na umempa usimamizi mtu mwingine, utabeba dhamana ya mali hizo, na utalipa wewe au yule mwenye kukosea hata haki kuwa zinapotea .

➡ Na wala hakuna haja ya kumpa mtu maalumu kuwa asafiri na mali hizo kwenda oman, wakati hizo mali ni haki ya watu wengine.

➡ Na kuhusu makadirio ya kuwalipa vitu hiyo ni :
” kukadiria kwa mujibu wa aghlabu ya dhana yake tu mwenyewe “

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

SH. SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je mwanamke aliesuka nywele (minyoosho) akitaka kuoga janaba, ni lazima afumue nywele zote ama zikisha roa imetosha ?

JAWABU

➡ Mwanamke mwenye janaba akitaka kukoga twahara ya jana si lazima kufumua nywele zake alizosuka.

➡ Nywele ni lazima kuzifumua ikiwa mwanamke huyo anataka kukoga josho la hedhi au nifasi tu.

➡ Na fatwa hii ni kwa kuwa dini yetu ya kiisilaamu sheria zake hazimkalifishi mtu sheria iliyokuwa ina uzito kuitekeleza.

➡ Na jambo la janaba ni jambo linaweza kuwa linatokea kila siku mara moja au zaidi, tofauti na hedhi au nifasi.

➡ Hedhi na nifasi inakuwa ni jambo la muda maalumu tu na kwa muda mfupi tu, imma kila mwezi mara moja kama ilivyokuwa katika hedhi, au mara moja baada ya kuzaa.

➡ Imepokewa kutoka kwa
Mtume s.a.w kuhusu ulazima wa kukosha nywele mpaka maji yafike katika asili ya nywele zake mwanamke huyo.

ثبت في الحديث عن النبي ـ صلى الله عليه وسلم ـ أنه قال: (( إن تحت كل شعرة جنابة فبلوا الشعر ونقوا البشر ))،

” Hakika chini ya kila unyweleunywele kuna janaba, basi rowesheni nywele na takaseni ngozi – za miili “

وهو يدل على وجوب تعميم الشعر بالغسل، فمن أضاعت ذلك فعليها التوبة مع إعادة ما صلت من الصلوات بهذه الحالة، وما صامته من الصيام الواجب. والله أعلم.

➡ Hadithi hiyo inaonyesha ulazima wa kufikisha maji katika kichwa chote katika kujitwaharisha wakati wa kukoga.

➡ Na mwanamke yoyote atakaekuwa hafanyi hivyo katika kukoga kwake basi ni lazima Atubie kwa ALLAAH S.W.

➡ Na pia ni lazima arejee sala zake zote alizokuwa ameswali bila ya kuwa amekoga kwa namna hiyo tulio itaja hapo kuhusu hukmu ya nywele.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

” twahara ni sharti katika masharti ya kusihi ibada nyingi katika uisilamu “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Naomba kujua majina ya as-habul kahfi .majina yao hasa ni yepi ?

JAWABU 

➡ Watu wa pangoni ambao maarufu kwa jina la – as’haabu l kahfi, ni:
“Vijana ambao walikuwa na imani kwa mola wao, kisha Mfalme wa mji ule akawatafuta kuwafanyia uadui kwa sababu ya imani yao “

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(أَمْ حَسِبْتَ أَنَّ أَصْحَابَ الْكَهْفِ وَالرَّقِيمِ كَانُوا مِنْ آيَاتِنَا عَجَبًا)
[Surat Al-Kahf 9]

Bali unadhani ya kwamba wale Watu wa Pangoni na Maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu?

➡ (إِذْ أَوَى الْفِتْيَةُ إِلَى الْكَهْفِ فَقَالُوا رَبَّنَا آتِنَا مِنْ لَدُنْكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا)
[Surat Al-Kahf 10]

Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu.

➡ Hao vijana wametajwa kwa sifa zao tu katika Qurani, na idadi yao anaijua mwenyewe ALLAAH S.W, kwa yakini zaidi.

➡ Na kuhusu majina yao pia hakuna dalili yoyote katika Qurani tukufu wala katika sunna imetaja majina yao.

➡ Lakini wako baadhi ya wafasiri wa Qurani wametaja baadhi ya majina kuwa ndio majina ya vijana hao, lakini hii ni ijitihada tu ya maulamaa kwa mujibu wa kuwepo baadhi ya nukuu kutoka katika baadhi ya vitabu.

➡ Lakini haikuthibiti hiyo, kwa kuwa hakuna dalili yoyote inaonyesha kuthibiti majina hayo.

➡ Wametajwa baadhi yao kuwa walikuwa ni :

1- Yamliikhaa.

2 – Mithliinaa.

3 – Kamithliinaa.

4 – Marnuush

5 – Dabarnuush.

6 – Kafash tatyuush

7 – Qitmiir.

➡ Lakini kama nilivyotanguliza kuwa :
” majina haya hakuna dalili yoyote inaonyesha usahihi.

➡ Na mambo haya hayadhuru kutoyajua, wala la hainufaishi kitu kuyajua.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

 ALLAAHU AALAMU.

” Qur’ani ni muongozo wa kila kitu “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Nini hukmu ya muisilamu kujibadili jina lake halisi na kujiita mathalan ronaldo au mfano wa hilo ili hali ana jina lake halisi ?

 JAWABU

➡ Muisilamu anatakiwa kufuata nidhamu ya dini yetu ya kiisilaamu katika mambo yake yote.

➡ Na ndio maana anaitwa muisilamu, kwa sababu uisilamu ni : ” Unyenyekevu na utiifu, na kuwa chini ya sheria za ALLAAH S.W “

➡ Na ndio maana Nabii Ibraahiim a.s alisifiwa kuwa yeye alikuwa ni mnyoofu na muisilamu, na wala hakuwa yahudi wala naswara.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَٰكِنْ كَانَ حَنِيفًا مُسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ)
[Surat Aal-E-Imran 67]

Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.

➡ Na akawasifu watu walio kuwa ni muhimu zaidi na bora kwa Nabii Ibraahiim a.s kuwa ni :

(إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ)
[Surat Aal-E-Imran 68]

Watu wanao mkaribia zaidi Ibrahim ni wale walio mfuata yeye na Nabii huyu na walio amini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa Waumini.

➡ Kwa nini muisilamu afuate majina yaliyokuwa si ya kiisilaamu wakati uisilamu umetuwekea majina mengi tena yenye maana nzuri.

➡ Na tumekatazwa sisi katika uisilamu kuwaiga waliokuwa si waisilamu, na makatazo haya yanahusu kuwaiga katika mambo yote ambayo hayalingani na maadili ya asili ya dini yetu ya kiisilaamu.

➡ Amesema mtume s.a.w katika hadithi ya swahahabiy Abdillaah bin Omar r.a, :
– من تشبَّهَ بقومٍ فَهوَ مِنهم
الراوي: عبدالله بن عمر المحدث: ابن حبان – المصدر: بلوغ المرام – الصفحة أو الرقم: 437
خلاصة حكم المحدث: صحيح

” Mwenye kujifananisha na watu basi huwa ni miongoni mwao “

➡ Amepokea imaamu ibnu Hibbaan, na ni hadithi sahihi.

➡ Anatakiwa muisilamu huyo arudi katika jina lake la asili ambalo linajulikana kwa watu na linaafiki misingi ns adabu za dini yetu ya kiisilaamu.

➡ Na hii kubadili jina kama hivyo inaweza kuleta madhara makubwa sana kinafsi na ki mali bali hata kijamii.

➡ Miongoni mwa athari zake ni :

1 – Huenda wakafahamu baadhi ya watu kuwa muislamu huyo amebadili jina na dini yake pia, akawa si muislamu.

Anaweza akapita za haki zake kama anazopewa muisilamu kikawaida.

2 – Inawezekana kupoteza haki ya nasabu kwa watoto aliokuwa amewajaalia kwa jina la mwanzo kabla ya kubadikisha jina.

3 – Kukosa utulivu na amani na mapenzi na uaminifu katika jamii yake ya kiisilaamu anayoishi.

4 – Kuvunja heshima na hadhi ya dini ya kiisilaamu, kwa kuwa uisilamu unafuatwa si uisilamu ufuate mila nyingine.

➡ Aombe msamaha kwa ALLAAH S.W, na arudi katika jina lake la mwanzo, na wala hakuna haja ya kusilimu upya tena kwa kuwa yeye hakubadili dini yake.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE KUIFUATA MIONGOZO YA DINI YETU KWA UKAMILIFU.

ALLAAHU AALAMU.

” Uisilamu ni kufuata na wala si kuzusha “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY 

Published By Said Al Habsy

SWALI: 

Nini hukmu ya mtu aliyefungulia funga ya Ramadhan kwa kuzini? je inampasa kutoa kafara ?

JAWABU 

➡ Ni ubaya ulioje kwa mja muovu mwenye kukosa haya na heshima kwa mola wake s.w.

➡ Vipi afungue saumu ya siku yake nzima hiyo kwa maasi makubwa na machafu kama hayo?

➡Nini faida na malengo ya funga yake ikiwa amefanya jambo hilo?

➡Ikiwa amefanya jambo hilo atapata dhambi kubwa, na atakuwa ameharibu amali yake hiyo ya saumu ya siku hiyo.

➡ Na ikiwa amefanya zinaa hiyo baada ya kuwa muda wa saumu unemaliza kwa kuingia tayari wakati wa magharibi, hapo kuna ikhtilafu baina ya maulamaa kuhusu kuharibika saumu yake kwa maasi hayo.

➡ Na kuharibika saumu ya siku hiyo ni Kauli yenye nguvu zaidi, kwa kuwa ALLAAH S.W amekataza kuharibu amali zetu kwa maasi ya aina yoyote.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ)
[Surat Muhammad 33]

Enyi mlio amini! Mt’iini Mwenyezi Mungu, na mt’iini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu.

➡ Na hata maneno ya kusimbulia pia yanaharibu malipo ya sadaka ya mja.

Amesema ALLAAHU S.W :
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُمْ بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنْفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ)
[Surat Al-Baqara 264]

Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.

➡ Ikiwa kauli inaharibu sadaka, vipi itakuwa hali katika jambo chafu zaidi kulikoni yote hayo? !!

➡Na ALLAAH s.w akakubali matendo ya waja wema tu wenye uchamungu.

➡ Amesema ALLAAHU S.W baada ya kutaja kisa cha watoto wawili wa Nabii Adam a.s, ambao mmoja wao alimuua mwenzake :

(وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ)
[Surat Al-Maeda 27]

Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu.

➡ Anatakiwa kwa wajibu mtu huyo afanye yafuatayo:

1- Atubie kwa ALLAAH S.W toba ya kweli.

2 – Arudie kufunga siku hiyo kwa salama ya dini yake.

3 – Hakuna kafara yoyote ya kutoa ikiwa amefanya zinaa hiyo baada ya kuzama jua na kuwa ni wakati wa halali kula kwa aliekuwa amefunga.

➡ Na Nakumbusha pia kuwa : ” Ni haramu kisheria kwa muisilamu yoyote kufungulia saumu yake kwa kutumia kitu chochote kilicho haramishwa na ALLAAH S.W “

➡ Hata ikiwa atafungua kwa Kuvuta sigara au kunywa pombe / ulevi, au kumbusu mwanamke alie haramu kwake kumbusu, au kutazama picha za Uchi, au kutukana na mfano wa hayo.

➡ TUNAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

“Ukikosa haya kwa mola basi fanya utakayo uone atakayo kufanyia mola “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je mwanamke baada ya kuzaa, ni lazima aache sala mpaka baada ya siku arobaini ?

JAWABU 

➡ Muda wa nifasi kwa mwanamke, wingi wake huwa ni siku arobaini.

➡ Na hii ndio Kauli ya maulamaa wengi zaidi katika madhehebu yote .

➡ Hata imaamu Shaafy nae amesema kuwa :
” aghlabu ya wingi wa nifasi ni siku arobaini “

➡ Lakini imaamu Maalik bin Anas na Imaamu Shaafy wanaona kuwa :
” Wingi wa damu ya nifasi ni siku sitini.

➡ Amma kuhusu siku arobaini kuwa ndio wingi wa damu ya nifasi, hii ni Kauli ambayo imeafikiwa na sunna za mtume s.a.w.

➡ Amesema Ummu salama r.a, kumjibu yule aliekuwa akimuuliza kuhusu muda wa nifasi :

كانت النفساءُ تَجْلِسُ على عهدِ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم أربعين يومًا ،…ِ

الراوي: أم سلمة هند بنت أبي أمية المحدث: الترمذي – المصدر: سنن الترمذي – الصفحة أو الرقم: 139

” alikuwa mwanamke mwenye nifasi anakaa – katika zama za mtume s.a.w siku arobaini,

➡Na hadithi hiyo ameisifu hata Muhammad bin ismaiil – yaani Imaamu al bukhaary, kama alivyosema imaamu al khattwaaby r.a.

➡ Kwa maana hiyo;
Hadithi hii inaonyesha masiku ambayo ni wingi wa masiku ambayo mwanamke aliezaa itahesabika damu inayomtoka ndani ya masiku hayo kuwa ni damu ya nifasi.

➡ Na wala haina maana kuwa aache sala na ibada kwa aliji ya kusubiri siku arobaini zitimie, bali anatakiwa kukoga na kufanya ibada zake katika muda wowote atakaokuwa ametwaharika, hata kama arobaini itakuwa bado kutimia.

➡ Na katika hadithi nyingine ya mtume s.a.w:
imetaja idadi ya masiku ya nifasi kuwa ni arobaini, kisha akasema kuwa :

” … إلا أن تَرَى الطُّهْرَ قبلَ ذلكَ”

الراوي: أنس بن مالك المحدث: الدارقطني – المصدر: سنن الدارقطني – الصفحة أو الرقم: 1/488

➡ “Isipokuwa akiona twahara kabla ya hapo “

➡ Ni makosa mwanamke kucha sala wakati damu yake ya nifasi imeshakata kutoka tena.

➡ Na ikiwa ataacha sala
Kadhaa kwa kudhania kuwa udhuru kama huo wa kutokujua ni udhuru, basi anatakiwa kulipa sala zote alizokuwa ameziacha kwa ajili ya kusubiri kutimia siku arobaini wakati mwanamke tayari ametwaharika.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

” Sheria za ALLAAH S.W hazina shida kwa waja “

JAWABU KUTOKA KWA :
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je mwanamke akijifungua mtoto ambaye hakutimia miezi Tisa tumboni, je anatakiwa akae hadi 40 ?

JAWABU 

➡ Mwanamke baada ya kuzaa, kikawaida anapata damu ya nifasi.

➡ Kwa hiyo :
Ikiwa mwanamke hiyo amezaa mtoto kabla ya miezi tisa, na ikafuatia kutokwa na damu ya nifasi, basi ni lazima asubiri mpaka atwaharike.

➡ Na kama atakuwa hakutokwa na damu hiyo basi si lazima kwake kusubiri chochote.

➡ Na hii ni kwa sababu :
Damu ikiwa hakuna basi hakuna haja ya kusubiri twahara, wakati sababu haikuwepo.

➡ Pia ikiwa mwanamke atazaa kwa oparesheni / kupasuliwa, na ikawa hakupata nifasi, pia huyo hana ulazima kusubiri.

➡ Amma kuhusu hukmu ikiwa ametoa kitu tumboni ambacho ni pande la damu, Samaahatu shaikhinaa Ahmad bin hamad alkhaliily aliulizwa kuhusu hukmu ya mwanamke ambae ameharibu ujauzito kwa kuzaa pande la damu tu…. na Akajibu kama ifuatavyo :
اختلف العلماء فيما تكون به المرأة نفساء إن وضعت، فقيل:
1- تكون بالعلقة نفساء،
2 – وقيل: حتى تكون لا يذوبها الماء الحار لو ألقيت فيه،
3 – وقيل: حتى يكون ما وضعته مضغة،
4- وقيل: بل مضغة مخلقة،
5 – وقيل: حتى يكون كامل الخلقة،
6- وقيل: حتى يميز أذكر أم أنثى،
7 – وقيل: لكل مرحلة قدرها من أيام النفاس، وإذا اعتمدت قولا من هذه الأقوال عذرت لأن المجال مجال اجتهاد. والله أعلم.

➡ Maana yake ni kuwa :
” wametofautiana maulamaa kuhusu ambacho kitamfanya mwanamke ahesabike kuwa katika nifasi ikiwa atakitoa tumboni :
Wakasema baadhi yao :

1- Kwa kutoa pande la damu tu anahesabika yuko katika nifasi.

2 – wengine wakasema : mpaka liwe pande hilo la damu – lina ugumu – kama likitiwa katika maji ya moto haliwezi kuyayayuka.

3 – Na Imesemwa mpaka kiwe alichokitoa – tumboni – ni pande la nyama.

4 – Wengine wamesema : pande la nyama lililo umbika tayari.

5 – Wakasema wengine :
Mpaka kiwe kiumbe kimekamilika kuumbwa kwake.

6 – Imesemwa pia kuwa :
Mpaka – alichokitoa tumboni – ki bainika – maumbile yake – ni cha kike au cha kiume.

7 – Na Imesemwa pia kuwa : Kwa kila moja katika hatua hizo akae kusubiri kwa kiasi cha siku, kama kile ambacho kawaida anasubiri akiwa katika nifasi “

Na kauli yoyote akichukua mwanamke miongoni mwa kauli hizo itamfaa, kwa kuwa suala hili ni ijitihada za maulamaa tu, – hakuna dalili yoyote.

➡ Na imaamu ibnu Qudaama al hanbaly amesema katika kitabu l mughny, juzuu ya “1” 395 :
” Ikiwa ataona – mwanamke – damu baada ya kuzaa kitu kinabainika maumbile yake basi hiyo ni nifasi.

Na ikiwa ataiona baada ya kutoa mkusanyiko wa manii tu au pande la damu basi hiyo si nifasi.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W AWAHIFADHI WAISILAMU WOTE NA AWAJALIE WEPESI KATIKA KUTEKELEZA SHERIA ZAKE.

 ALLAAHU AALAMU.

” Uisilamu ni dini ya wepesi katika sheria zake “

JAWABU KUTOKA KWA :
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Ustaadh kuna swali nimeulizwa na dada mmoja. Kuwa: “anapo simama kufanya Ibada huwa anatokewa na Qur’ani ikiwa imefunuliwa, wakati mwingine hutokewa na msikiti ikiwa watu wamo wakifanya ibada.
Sasa anauliza nini maana ya hivyo vitu ??

JAWABU 

➡ ALLAAHU AALAMU kuhusu hakika ya suala hili.
➡ Ikiwa Mwanamke huyo ni mwema huenda akawa anaonyeshwa na ALLAAH S.W njia sahihi ya watu wema, njia ambayo anatakiwa ashikamane nayo sana.

➡ Na Qur’ani pia ndio njia sahihi ya kuongoza Umma na kujenga imani.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(إِنَّ هَٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا)
[Surat Al-Isra 9]

Hakika hii Qur’ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa.

➡ Na Qur’ani pia ni Nuuru, kupitia Qurani hiyo ALLAAH S.W anaongoza waja wake.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمْ بُرْهَانٌ مِنْ رَبِّكُمْ وَأَنْزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُبِينًا)
[Surat An-Nisa 174]
Enyi watu! Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni Nuru iliyo wazi.

➡ Jambo muhimu ni kuwa : ” azidishe ibada zaidi, na kusoma Qur’anitukufu kwa wingi, na awe na marafiki wema “.

➡ Na pia asihadithie jambo hilo kila mtu, ili kuepusha kufikwa na hasadi za wenye chuki na wenye kujaliwa kheri kama hizi.

➡ Pia akiwa katika sala asiweke mawazo ya aina yoyote ile kuhusu yeye na sala zake na kadhalika.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUONDOSHEE MAPAZIA YAZUIAYO KUIONA HAKI NA KUFUATA.

ALLAAHU AALAMU.

” ALLAAH akimpenda mja wake humfungulia elimu ya dini yake “

 JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Kwa hiyo mwalimu wale ahlul kitabu enzi za mtume waliokuwa hawafuati vitabu kiusahihi wake je walikuwa hawaitwi ahlul kitabu ??

JAWABU

➡ Jina la ahli l kitaabi linatumika kwa makundi mawili mashuhuri katika mila miongoni mwa mila sita silizotajwa katika QURANI tukufu.

➡ Na makundi mawili hayo ni :

1 – wakristo.

2 – Mayahudi.

➡ Lakini kuitwa jina hili kwa watu hao haina maana kuwa wamehalalika kuwaoa wote katika makundi hayo mawili.

➡ Na hii ni kwa sababu :
ALLAAHU S.W mwenyewe, amewataja watu wa kitabu kuwa wamekufuru, na kafiri hafai kuolewa na muisilamu, wala yeye kumuoa muisilamu.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنْفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ)
[Surat Al-Bayyina 1]

Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,

➡Pia watu hao amewataja pamoja na kundi la washirikina wa kiarabu kwa kuwaahidi adhabu kutokana na kukufuru kwao.

(إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ أُولَٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ)
[Surat Al-Bayyina 6]

Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.

➡ Jina hilo walikuwa wakiitwa hivyo, kwa sababu mitume wao walikuwa wamepewa vitabu, na wao ndio wamepelekewa mitume wengi sana kuliko kaumu zote zilizo tangulia.

➡ Amesema ALLAAHU S.W kuhusu mayahudi alio watoa mtume s.a.w katika mji wa Madina :

(هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِنْ دِيَارِهِمْ لِأَوَّلِ الْحَشْرِ ۚ مَا ظَنَنْتُمْ أَنْ يَخْرُجُوا ۖ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ مَانِعَتُهُمْ حُصُونُهُمْ مِنَ اللَّهِ فَأَتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا ۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ ۚ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُمْ بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الْأَبْصَارِ)
[Surat Al-Hashr 2]

Yeye ndiye aliye watoa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu katika nyumba zao wakati wa uhamisho wa kwanza. Hamkudhani kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyezi Mungu. Lakini Mwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipo patazamia, na akatia woga katika nyoyo zao. Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini. Basi zingatieni enyi wenye macho!

➡ Na watu wa kitabu hao walikuwa wakimuhoji mtume s.a.w baadhi ya mambo katika njia ya kumkana na kumkejeli, lakini juu ya hivyo amewataja kwa jina la ahli l kitaabi.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(يَسْأَلُكَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَنْ تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَابًا مِنَ السَّمَاءِ ۚ فَقَدْ سَأَلُوا مُوسَىٰ أَكْبَرَ مِنْ ذَٰلِكَ فَقَالُوا أَرِنَا اللَّهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ۚ ثُمَّ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ فَعَفَوْنَا عَنْ ذَٰلِكَ ۚ وَآتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَانًا مُبِينًا)
[Surat An-Nisa 153]

Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshia kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi kwa hiyo dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumuabudu, baada ya kwisha wajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa nguvu zilizo dhaahiri.

➡ Kwa hiyo sifa hiyo haina maana kuwa wote ndio wako hivyo kwa uovu au kwa wema, bali ni jina la jumla, lakini ndani yake wanatofautiana.

➡ Na ndio maana waliokuwa wana itakidi kuwa Nabii Issa bin Mariamu a.s ni mungu au mtoto wa Mungu, hao hawafai kuwaoa kwa kuwa wamekufuru hao, wakawa sawa na wengine wenye sifa hiyo.

➡ Na aya ziko wazi kuhusu wenye kusema Utatu wa Mwenyezi Mungu, na wao wanasema hivyo.

➡ Kuna tofauti baina ya kuitwa jina na kusifika kwa sifa za jina lenyewe.

➡ Watu hao hawana sifa ya kufuata kitabu au vitabu vya manabii walio tangulia.

➡ Bali wao ni wajibu kumfuata mtume Muhammad s.a.w kwa kuwa yeye ndie mtume wa mwisho na wa ulimwengu mzima.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

” Uisilamu ndio dini yenye kuridhiwa na ALLAAH S.W”

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Suali la pili juu ya mada yako ya leo, naona masheikh mwatuchanganya, Wasema wa kiristo wa zama hizi sio ahlu lkitab, Je ahlul kitab wa zama za za mtume walikuwa wana sifa gani ambazo nitofauti na.hizi? 

JAWABU

➡ Swali lako zuri sana kwa hakika, na wala hakuna jambo lolote la kuwachanganya waisilamu kuhusu sifa za Ahli l kitaabi.
➡ Qur’ani tukufu iko wazi katika kubainisha jawabu ya swala hili kama ifuatavyo :

1 – Amesema ALLAAHU S.W
(لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 113]

Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama baraabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu.

(يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ)
[Surat Aal-E-Imran 114]

Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanakimbilia katika mambo ya kheri. Na hao ndio miongoni mwa watenda mema.

➡ Sifa hizo hawana watu hao, na hili liko wazi kabisa.

2 – Pia amesema ALLAAHU S.W :
(مَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَنْ يُنَزَّلَ عَلَيْكُمْ مِنْ خَيْرٍ مِنْ رَبِّكُمْ ۗ وَاللَّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَنْ يَشَاءُ ۚ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ)
[Surat Al-Baqara 105]

Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.

➡ Na hiyo ndio hali yao hadi sasa.

3 – Na amesema pia :
(وَدَّ كَثِيرٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُمْ مِنْ بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِنْ عِنْدِ أَنْفُسِهِمْ مِنْ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ ۖ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّهُ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)
[Surat Al-Baqara 109]

Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Na hao ndio lengo leo kufanya hivyo, na kuwahadaa baadhi ya vijana kupitia hata njia za kuwaoa au kuwa na uhawara baina yao.

4 – Amesema ALLAAHU S.W :
(وَدَّتْ طَائِفَةٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنْفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 69]

Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu wanao penda kukupotezeni; lakini hawapotezi ila nafsi zao, nao wenyewe hawatambui.

5 – Na wao wanakana baadhi ya aya za ALLAAH S.W, kama alivyosema ALLAAH s.w katika aya nyingine :

(يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَأَنْتُمْ تَشْهَدُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 70]

Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu ilhali nyinyi mnashuhudia?

6 – Na walikuwa watu wa kitabu baadhi yao wana shuku katika mambo ya ghaibu, na kutia shaka katika yale waliyo amini waisilamu.

Amesema ALLAAHU S.W :

(وَقَالَتْ طَائِفَةٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنْزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 72]

Na kikundi katika Watu wa Kitabu walisema: Yaaminini yale waliyo teremshiwa wenye kuamini mwanzo wa mchana, na yakataeni mwisho wake; huenda wakarejea.

➡ Kwa hakika, wakristo na mayahudi itiqaadi zao ni kinyume kabisa na vitabu vya asili vilivyo teremshwa kwa mitume a.s wa zama hizo.

➡ Kwa nini Waseme kuwa kuna miunngu watatu au kuna Mungu mtoto?

Jee kusema hivyo si kukufuru?

Amesema ALLAAHU S.W :

(لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَٰهٍ إِلَّا إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِنْ لَمْ يَنْتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ)
[Surat Al-Maeda 73]

Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru.

➡ Ndio mtume s.a.w alikuwa akiwalingania katika dini sahihi na kalima yenye usawa baina yetu na wao, nalo ni :

(قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ ۚ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 64]

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.

➡ Maneno haya machache yanaonyesha wazi utofaoti baina ya Ahli l kitaabi sahihi na waliokuwa si ahli l kitaabi.

➡ Qur’ani ndio muongozo wa kila kitu.

ALLAAHU AALAMU.

“Hakuna mkweli kushinda ALLAAH S.W.

JAWABU KUTOKA KWA :
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je inafaa mali ya marehemu kuijengea msikiti? Na hii baada ni maamuzi ya ndugu zake ?

JAWABU

➡ Mali ya muisilamu baada ya kufa kwake inakuwa ni mirathi katika sheria ya KIISILAMU.

➡ Na mirathi ni : ” Mali aliyo iacha mtu baada ya kufa kwake “

➡ Kwa hiyo mali hiyo ni haki ambayo inaondoka katika hukmu ya kumilikuliwa na yule marehemu, na inakuwa ni haki ya warithi wake baada yake.

➡ Na hii ni hukmu ya ALLAAH S.W katika QURANI tukufu.

➡ Ikiwa maiti huyo kabla ya kufa kwake aliusia sehemu katika mali yake itumiwe kwa kujengea msikiti fulani Mathalan, hiyo itakuwa ni sahihi, na itakuwa ni wasia.

➡ Na wasia katika sheria unatakiwa usizidi zaidi ya theluthi ya jumla ya mali zote za maiti huyo.

➡ Na theluthi ni fungu moja katika jumla ya mafungu matatu.

➡ Na wasia huo unachukuliwa hesabu yake katika jumla ya mali yote ya maiti kabla ya kugaiwa mali hiyo kwa warithi, kisha kinachobakia ni haki ya warithi, kila mmoja kwa mujibu wa fungu lake kwa mujibu wa sheria.

➡ Imepokewa kuhusu suala hili kutoka kwa mtume s.a.w, alipokuwa swahahabiy Saad bin Abii waqqaasw amekaribia kufikwa na kifo, anasema :

مرضتُ، فعادني النبيُّ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ،…. قلتُ : أريد أن أوصيَ، وإنما لي ابنةٌ، قلت : أوصي بالنصفِ ؟ قال : ( النصفُ كثيرٌ ) . قلت : فالثلثُ ؟ قال : ( الثلثُ، والثلثُ كثيرٌ، أو كبيرٌ ) . قال : فأوصى الناسَ بالثلثِ، فجاز ذلك لهم .

الراوي: سعد بن أبي وقاص المحدث: البخاري – المصدر: صحيح البخاري – الصفحة أو الرقم: 2744
خلاصة حكم المحدث: [صحيح]

” Niliumwa; akanitembelea mtume s.a.w, nikamuambia: “Ninataka kuusia , na mimi nina mtoto wa kike mmoja tu, niusie kwa nusu ya mali yangu” ?
Akasema mtume s.a.w :
” Nusu nyingi “

Akasema : ” Theluthi “
Akasema mtume s.a.w :
” Theluthi, au kubwa” akawausia watu kwa theluthi na ikajuzu kwao hivyo “

➡ Na katika hadithi nyingine ya imamu muslimu kutoka kwa mtume s.a.w alimuambia swahahabiy Saad bin Abii waqqaasw kuwa :

“…إنك إن تذَرَ ورثتكَ أغنياءَ ، خيرٌ من أن تذَرَهم عالةً يتكففون الناسَ …”

الراوي: سعد بن أبي وقاص المحدث: مسلم – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 1628
خلاصة حكم المحدث: صحيح

” Hakika Wewe kuwaacha warithi wako wanacho cha kuwatosheleza ni bora kuliko kuwaacha masikini wakinyoosha mikono kuomba watu “

➡ Kwa hiyo haifai kutoa mali ya marehemu huyo yote kwa ajili ya kujengea msikiti.

➡ Na kama aliusia basi litolewe fungu kiwango cha theluthi tu ya mali yote kwa ajili ya kutekeleza wasia huo ikiwa aliusia.

➡ Na wala haifai kubadilisha wasia ila ikiwa kupunguza tu kilichozidi ikiwa aliusia zaidi ya theluthi ya mali zote.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(فَمَنْ بَدَّلَهُ بَعْدَمَا سَمِعَهُ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى الَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ)
[Surat Al-Baqara 181]

Na atakaye ubadilisha wasia baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakao ubadilisha; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

➡ Kumbuka kuwa :
Ikiwa warithi wataamuwa wenyewe kutoa kila mmoja fungu lake wote la urithi kwa ajili ya kujenga msikiti, inajuzu kufanya hivyo kwao wote, lakini hiyo ni baada ya kugaiwa kila fungu lake.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W AWAREHEMU NDUGU ZETU, NA ATUFUNGULIE MILANGO YA KHERI NA BARAKA.

ALLAAHU AALAMU.

” Urithi ni haki ya warithi, kila mmoja kwa ukaribu wake na daraja lake “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Mimi ni muislamu nimeowa mkristo, na tumezaa naye watoto wote waislamu, je ndoa hii ni halali ? Na kama ndoa sio halali; watoto ni wa baba au mama ?

JAWABU 

➡ Muisilamu mwanaume ameamrishwa kuoa mwanamke muisilamu, na muisilamu mwanamke pia aolewe na mume muisilamu.

➡ Haifai kuoana wenye dini tofauti baina ya muisilamu na yoyote ambae si muislamu muumini.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَلَا تَنْكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِنْ مُشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنْكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُؤْمِنٌ خَيْرٌ مِنْ مُشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ)
[Surat Al-Baqara 221]

Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake. Naye huzibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka.

➡ Aya hiyo iko wazi kabisa kuonyesha kuwa : ” Sharti la kusihi ndoa kwa waliokuwa katika mila zisizokuwa za kiisilaamu ni kuwa mpaka wawe Waumini “

➡ Kwa dalili hii ya wazi ni kuwa : ” Ndoa hiyo ni ndoa batili haikubaliki kisheria kwa mujibu wa Qurani “

➡ Amma kuhusu wanawake katika waliopewa kitabu – Ahli l kitaabi – Ikiwa wapo kwa sifa kamili za kustahiki kuitwa ni watu wa kitabu, wao ni sawa na waumini katika waisilamu.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَنْ يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ)
[Surat Al-Maeda 5]

Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a’mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.

➡ Aya hiyo iko wazi kuonyesha kufaa kuwaoa watu wa kitabu, na wenye sifa za kufuata kitabu.

➡ Na aya hiyo pia imeonyesha makatazo ya zinaa na kuwaoa wanawake kwa kuwaweka kinyumba – uhawara.

➡ Wakristo wa zama hizi kwa mujibu wa Qurani na uhalisia wa itiqaadi zao zilivyo si sawa na watu wa kitabu, kwa hiyo haifai kuwaoa, wala wao kuoa wanawake wa kiislamu.

➡ Wao itikadi yao ni kuwa :

1 – Mungu ana mwana, na sisi tunasema kuwa : ” ALLAAH S.W hakuzaa wala hakuzaliwa.

Amesema ALLAAHU S.W :
(وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُمْ بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ)
[Surat At-Tawba 30]

Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!

2 – Wao wanamkataa mtume Muhammad s.a.w, wakati ALLAAH S.W amewataka mitume a.s wamkubali mtume huyu, na pia watu wote wamfuate na kumuamini.

(الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِنْدَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ يَأْمُرُهُمْ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنْزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ)
[Surat Al-Araf 157]

Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye – hao ndio wenye kufanikiwa.

➡ Ndoa hiyo iliyofungwa ni ndoa batili na ivunjwe haraka.

➡ Na watoto wote watakuwa ni watoto wa kiisilaamu, kwa kuwa mtoto yoyote anazaliwa na asili ya uisilamu, mpaka afikie umri wa kubaleghe mwenyewe akafuata dini nyingine, hapo jukumu lake litakuwa kwake mwenyewe.

➡ Usidanganike na fikra za ki magharibi na kudai usawa baina ya dini zote abadan.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

” Dini ya kiisilaamu ndio dini pekee yenye kulingana katika sheria na maumbile sahihi ya kila kitu “

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je kufanya kazi ya masaji katika dini yaruhusiwa ?

JAWABU

➡ Mwili wa muisilamu bali kilakila kila binaadamu, unatakiwa kusitiriwa, kwa mujibu wa mipaka ya sheria za ALLAAH S.W.

➡ Kazi ya kuchua miili ya watu kwa kutumia mafuta na mikono katika mwili wa mtu mwingine, ni lazima vitazamwe vidhibiti vya kisheria katika kila upande kama ifuatavyo :

1⃣Asifanye mtu kuchuliwa mwili wake wa sehemu ambazo ni za ndani zaidi ila kwa dharura ambayo hapana budi.

2⃣Ikiwa mwenye kuchuliwa mwili huo ni mwanamke, basi lazima mchuaji pia awe ni mwanamke mwenzake, na ikiwa mchuliwaji ni mwanaume basi pia mchuaji awe ni mwanaume.

3⃣Pia asiache wazi sehemu ambazo kisheria huzingatiwa kuwa ni utupu kuzionyesha kwa mtu mwingine ila kwa udhuru mkubwa.

4⃣Izingatiwe pia kuwa : ” pasiwe pahala hapo pana mchanyiko baina ya wanaume na wanawake, au wanawake waovu na wema, kisha wakawa wanaonana miili yao.

➡ Kwa sababu mwanamke kwa mwanamke pia kuna mipaka ya sheria katika sehemu ambazo zinafaa kuonekana, na ambazo hazifai kuonekana, kama ilivyokuwa hukmu hiyo iko kwa wanaume pia.

5⃣Kitengo kama hicho ikiwa kitakuwepo , basi ni lazima kiwe makini sana katika kushughulikia watu wanao kuja pahala hapo kushughulikiwa.

➡ Huenda wakawa wanakuja baadhi ya watu kwa ajili ya kufanyiwa kwa kuwa wanaona ni kama starehe fulani tu miili yao kufanyiwa hivyo.

6⃣Na katika sharti muhimu pia kuzingatiwa ni kuwa :
” Ikiwa kufanya hivyo au kufanyiwa hivyo kunamsababishia mmoja wao au wote kuamsha hisia za kutamani au kutamaniwa, basi hiyo inaharamika mara moja, hata kama itakuwa baina ya mwanaume kwa mwanaume, au mwanamke kwa mwanamke.

➡ Na hii ni katika kanuni iitwayo : “سد الذرائع “

” saddu ddharaai’i “
Yaani : ” kufungamana milango inayo pelekea katika yaliyo katazwa.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

” Tahadhari kabla ya hatari”

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Kuna dada anauliza hivi: Katokea mume yupo dar es salaam, nae anaishi zanzibar.Amekubali kuolewa lakini hakutaka kwenda dar, Je haitokuwa vibaya kwa mume kuja zamu kila baada ya wiki mbili nae yupo dar? 

JAWABU 

➡ Ndoa ni mafungamano sahihi na masafi kati ya mume na mke.

➡ Na mke na walii wake pamoja na mume nae wanatakiwa kuwa radhi kuoana, ikiwa wameamua kuoana kweli.

➡ Na kutokana na swali hili jawabu ni kuwa : ” Hakuna tatizo wala kosa lolote ikiwa mke ametoa sharti hilo na mume amelikubali “

➡ Sharti hilo linakubalika kabla ya kufunga ndoa.

➡ Na mume anatakiwa kufahamu kuwa :
” Akikubali sharti hilo basi ni lazima alitekeleze kama walivyokubaliana katika ahadi ya kuoana kwao.

➡ Amesema mtume s.a.w katika hadithi iliyopokewa na Amruu bin auf al muzany r.a :
الصلحُ جائِزٌ بينَ المسلمينَ إلَّا صلحًا حرَّمَ حلالًا أوْ أحلَّ حرامًا والمسلمونَ على شروطِهمْ إلَّا شرطًا حرَّمَ حلالَا أوْ أحلَّ حرامًا”

الراوي: عمرو بن عوف المزني المحدث: الترمذي – المصدر: سنن الترمذي – الصفحة أو الرقم: 1352
خلاصة حكم المحدث: حسن صحيح

“Sulhu inajuzu baina ya waisilamu, isipokuwa sulhu inayo haramisha halali au kuhalalisha haramu, na waisilamu kwa mujibu wa masharti yao, isipokuwa sharti linalo halalisha haramu, au kuharamisha halali “

➡ Mume anatakiwa kutazama uwezo wake kabla ya kukubali tu sharti hilo kwa haraka.

➡ Atazame uwezo wake kwanza wa mali na afya kama vinaweza kumruhusu kusafiri kuja zanzibar kwa kila muda huo.

➡ Na mke anatakiwa kujua pia muda ambao atakaa mumewe pamoja nae baada ya kuja kwake huku zanzibar, ili kuondoa ikhtilafu baina yao katika mustaqbali.

➡ Raha ya ndoa hasa ni mume na mke kuwa pamoja na karibu kwa muda mwingi.

➡ Na kuna baadhi ya huduma mume atazikosa kwa mkewe, na mke kwake itakuwa ni uzito kuzifanya akiwa mbali na mumewe.

➡ Mfano wa hayo ni :

1 – Maandalizi ya chakula cha mume.

2 – Nguo za mumewe na usafi wa nyumba na mazingira ya ndani na nje.

3 – ukaribu na mapenzi na huruma baina yao, yote haya yatakuwa mbali kupatikana kutokana na umbali uliopo baina ya mume na mke.

➡ Ikiwa hakuna tatizo katika kuhamia katika mji wa mume, basi kuhamia huko inaweza kuwa ni bora zaidi hata kwa mazingira ya kazi za mumewe.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

ndoa ina jengwa kwa mapenzi huruma “

” Ndoa ni muhimu kwa kila muisilamu “

JAWABU KUTOKA.

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Kila mtindo,hali ya kuwa sjui kama wavaaji watavaa kwa stara sasa je hukmu ya hilo ipoje ?

 JAWABU 

➡ Nguo za kiisilaamu ni lazima ziwe ni zenye kusitiri mwili kwa mujibu wa sheria kwa wanaume na wanawake.

➡ Na juu ya hili ni kuwa :
Uisilamu haukumnyima muisilamu yoyote haki ya kujipamba, lakini uisilamu umeweka tu vidhibiti na mipaka ya kisheria katika kujipamba huko.

➡ Tazama kuhusu nguo tulizoumbiwa na ALLAAH S.W, nini amesema ALLAAH S.W?

(يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنْزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ)
[Surat Al-Araf 26]

Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za uchamngu ndio bora. Hayo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu mpate kukumbuka.

➡ Nguo za pambo hazijakatazwa katika aya hiyo, bali imetajwa miongoni mwa alivyo viteremsha ALLAAH S.W kwa wanaadamu.

➡ Kwa kuwa wewe ni fungi tu wa kushona nguo hizo, na binaadamu hawezi kujua ghaibu wala mambo ambayo yatatokea katika mustaqbali , wala kujua yaliyomo ndani nyoyo za watu, basi juu yako wewe ni kuwanasihi wanao kuja kununua nguo hizo tu kwa wema na maneno mazuri.

➡ Usimtuhumu mtu yoyote pasipo ushahidi wenye yakini juu ya kununua vazi hilo, lakini mkumbushe tu sheria ya KIISILAMU imetusmrisha kuvaa nguo zenye stara.

➡ Pia mwambie kuwa nguo hizi za mapambo ninazo tengeneza hizi ni maalumu tu kwa watu maalumu na pahala maalumu.

➡ Ikiwa yeye ananunua kwa ajili ya kumvalia mumewe ndani ya nyumba yake, si tatizo kwake kufanya hivyo.

➡ Na ikiwa ni nguo zenye mapambo ya kawaida tu, ambayo yanafaa kuvaliwa hata kwa watu wengine -wasiokuwa waume – lakini ni watu ambao inawaharamikia wao kumuoa mwanamke huyo uharamu wa daima, pia mfahamishe adabu zake nguo hizo.

➡ Kuna baadhi ya nguo za mapambo haiwezi kuvaliwa ila baina ya mke tu mumewe.

➡ Na ziko nguo nyingine za mapambo, lakini inawezekana kisheria kuzivaa mwanamke kwa baba yake, au kaka yake na mfano wa hao, wakati nguo hiyo hiyo haifai kuivaa mbele ya wanaume wengine wa kawaida.

➡ Jiondoshee jukumu hilo kwa kuwakumbusha
wateja wa kike mapema, ikiwa watakwenda kinyume na sheria baada ya kuwaambia, basi wewe hauna kosa wala dhambi yoyote juu ya hilo.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W AWASITIRI WANAWAKE WA KIISLAMU KUTOKA NA FITNA ZA KUVUNJIWA HESHINA ZAO NA TAMADUNI ZA KIMAGHARIBI.

ALLAAHU AALAMU.

” Jisitiri usitirike”

JAWABU KUTOKA KWA:
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Eti mfano mimi nina nyumba yangu au biashara, nataka nimchukue shekhe ili aje anisomee kisomo ili kujikingi na watu wabaya, mfano wazi nk, je nitakuwa nimekosea au nayo ni shirki ?

JAWABU

➡ Dua bora zaidi unayotakiwa kuifanya katika nyumba yako na biashara zako na mengine yote ni : “Kudumu katika kumcha ALLAAH S.W”

➡ Mwenye kumcha ALLAAH S.W na kufanya mema basi ALLAAH S.W atakuwa pamoja nae.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(إِنَّ اللَّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوْا وَالَّذِينَ هُمْ مُحْسِنُونَ)
[Surat An-Nahl 128]

Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema.

➡ Na amesema pia :
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ)
[Surat Muhammad 7]

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.

➡ Na Hakuna wa kunusuru isipokuwa ALLAAH S.W mwenyewe peke yake, vitu vingine vyote ni sababu tu.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(إِنْ يَنْصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ ۖ وَإِنْ يَخْذُلْكُمْ فَمَنْ ذَا الَّذِي يَنْصُرُكُمْ مِنْ بَعْدِهِ ۗ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ)
[Surat Aal-E-Imran 160]

Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.

➡ Kumuita sheikh kwa ajili ya kusoma dua au kumuombea dua, ikiwa unaitakidi kuwa : ” Anaeombwa ni ALLAAH S.W, na wa kutegemewa ni ALLAAH S.W mwenyewe, Hakuna kosa wala shirki katika kufanya hivyo “

➡ Lakini bora zaidi ikiwa utataka kufanya hivyo, basi mkaribishe kwa Niya ya kumkaribisha tu nyumbani na kumfanyia ikramu, na kumtaka nasaha zake, na baada ya hapo yeye mwenyewe atakuombea dua ya kheri Inshaallaah.

➡ Pia nyumba ya muisilamu inatakiwa idumishwe kwa kusomwa ndani yake Qur’ani tukufu, na hasa kusoma surati l Baqara.

➡ Nakumbusha kuwa : ” kuna watu wamefanya dua za ufunguzi wa nyumba mpya kuwa ni biashara , anawalipa mwenye nyumba pesa za usomaji dua kwa mujibu wa hedhi ya nyumba yake ilivyo “

➡ Huu ni mtihani umewafika wengi katika wafanyaji wa dua, hata wamepanga baadhi yao bei ya kila dua au sura za qurani atakazo msomea mtu au mgonjwa.

➡ Anawambia : “kusomewa yaasin tatu ni elfu kadhaaa, ukitaka dua ya kinga ni kiasi kadhaa. ..
Hii ni sunna ya nani na wameipata wapi hawa?

➡NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

” Dua yako kwa ikhlaasw ni bora kwa rabbi nnaasi

 JAWABU KUTOKA KWA

SH.  SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Nauliza kuhusu mnyama wa kuwinda, tunaambiwa ni halali kula nyama ya kuwinda suala, Je kama alie winda mnyama huyo si muislamu itafaa kwa muislamu kula mnyama huyo ?

JAWABU

➡ Mnyama aliewindwa kwa kutumia jina la ALLAAH S.W ndie mnyama anaefaa kuliwa.

➡ Na Inajulikana wazi kuwa waliokuwa si waisilamu hawamtaji ALLAAH S.W katika mambo yao yote, na wala hawaamimi kuwepo kwa ALLAAH S.W au baadhi ya sifa zake.

➡ Amesema ALLAAHU S.W kuhusu kula wanyama wa kuwindwa :

(يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُمْ مِنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ)
[Surat Al-Maeda 4]

Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyo kufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni walicho kukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

➡ Na kutokana na hayo, mtume s.a.w alikuwa akimuambia swahahabiy Adiiyy bin haatimii kuwa :

إذا أرسلتَ كلبَكَ المُكلَّبَ وذكرتَ وسمَّيْتَ فكُلْ ما أمسَكَ عليْكَ كلبُكَ المكَلَّبُ ، وإنْ قتَلَ …َ”

الراوي: أبو ثعلبة الخشني
خلاصة حكم المحدث: صحيح

” “Ukimuachia mbwa wako kumtuma – Mbwa aliefunzwa, kisha ukataja na kusema ” Bismillaah ” , basi kula alichokikamata mbwa wako aliefunzwa, hata kama ukikuta kiwindwa hakina uhai tena… “

➡ Amma kilichowindwa na waliokuwa si waisilamu na wala hawamtaji ALLAAH S.W katika kuwinda kwao, hiyo haifai kuliwa kusheria.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ)
[Surat Al-Anaam 121]

Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu. Na kwa yakini mashet’ani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na mkiwafuata basi hapana shaka nyinyi mtakuwa washirikina.

➡ Amma akiwa ambae si muislamu anauza tu yeye nyama ambayo imewindwa na muisilamu, na limetajwa jina la ALLAAH S.W wakati wa kutuma mbwa yule, hapo hakuna tatizo kununua kwa mtu huyo midhali haku mchinja yeye.

➡ Na baadhi ya maulamaa wanaona kuwa : ” Ikiwa nchi hiyo inajulikana kuwa wanyama wote huchinjwa katika ya kiisilaamu, basi yeye anunue nyama hiyo na aseme “Bismillaah ” wakati wa kuipika kwake au kula kwake.

➡ Na kama ikiwa haijulikani namna ya au jinsi ya kuchinja kwao, na dini hawana wala imani sahihi, basi asile nyama hiyo ila kwa yakini .

➡ Namuomba ALLAAH atukinge na shari za viumbe vyake.

ALLAAHU AALAMU.

” UISILAMU NI DINI YA WEPESI katika sheria zake “

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Umri wa kuishi kwa mwanadamu kwa mujibu wa Quran ni miaka mingapi ?

JAWABU 

➡ Umri wa kila kitu chochote katika ulimwengu huu, Hakuna yoyote anaejua hilo isipokuwa ALLAAH S.W peke yake.

➡ Na hili limethibiti katika aya nyingi za Qurani tukufu kama ifuatavyo :

1 – (هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُسَمًّى عِنْدَهُ ۖ ثُمَّ أَنْتُمْ تَمْتَرُونَ)
[Surat Al-Anaam 2]

Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha akakuhukumieni ajali, na muda maalumu uko kwake tu. Tena baada ya haya nyinyi mnatia shaka.

2 – (هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا شُيُوخًا ۚ وَمِنْكُمْ مَنْ يُتَوَفَّىٰ مِنْ قَبْلُ ۖ وَلِتَبْلُغُوا أَجَلًا مُسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ)
[Surat Ghafir 67]

Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu, kisha akakutoeni katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanao kufa kabla, na ili mfikie muda ulio kwisha wekwa, na ili mpate kufahamu.

3 – (أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَنْ يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى الظَّالِمُونَ إِلَّا كُفُورًا)
[Surat Al-Isra 99]

Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhaalimu hawataki ila ukafiri.

4 – (وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُمْ بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُمْ بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ)
[Surat Al-Anaam 60]

Naye ndiye anaye kufisheni usiku, na anakijua mlicho fanya mchana. Kisha Yeye hukufufueni humo mchana ili muda ulio wekwa utimizwe. Kisha kwake Yeye ndiyo marejeo yenu, na tena akwambieni mliyo kuwa mkiyafanya.

5 – (قُلْ لَا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۚ إِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ)
[Surat Yunus 49]

Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao walio wekewa. Ukifika muda wao hawakawii hata saa moja wala hawatangulii.

6 – (وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِنْ قَبْلِكَ وَجَعَلْنَا لَهُمْ أَزْوَاجًا وَذُرِّيَّةً ۚ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَنْ يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ ۗ لِكُلِّ أَجَلٍ كِتَابٌ)
[Surat Ar-Rad 38]

Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukajaalia wawe na wake na dhuriya. Na haiwi kwa Mtume kuleta miujiza isipo kuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake.

➡ Hizi ni baadhi ya aya tu na wala si zote miongoni mwa aya za qurani tukufu.

➡ Na wala hakuna anaejua umri wa hii dunia kutokea imeumbwa hadi sasa isipokuwa ni ALLAAHU S.W tu.

➡ Takwimu zote hazina hata nusu wala robo ya ya uhakika wa Takwimu wazitajazo.

➡ Na ndio maana hadi sasa na itakuwa hivyo hivyo mpaka Kiyama, binaadamu hata wakiwa katika teknolojia ya aina gani, hawatoweza kujua tarehe wala muda wa kufa mtu yoyote.

➡ Kwa hiyo huo ndio umri wa kila kitu kwa mujibu wa Qurani tukufu.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUBARIKIE UMRI WETU.

ALLAAHU AALAMU.

” Mambo ya ghaibu hayadirikiwi kwa akili “

JAWABU KUTOKA KWA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Adamu na Eva baada ya kujuwa wamekuwa MKE na MUME: je Adam alilipa mahari kwa Eva? Kama alilipa alimlipa nani? Kama hakulipa wanaolipa wanamuiga nan?

JAWABU 

➡ Katika historia ya kiisilaamu, mke wa Nabii Adam a.s hajulikani kwa jina hilo lilitojwa katika suali.

➡Jina la mke wa Adam a.s alikuwa akiitwa hawaa, kama ilivyotajwa katika vitabu vingi vya Tafsiri ya Qur’ani tukufu.

➡ Na pia vitabu vya hadithi vimetaja jina hilo katika baadhi ya mapokezi, na miongoni mwa hadithi hizo zimepokewa na kutajwa na imaamu al sakhawy, na swan’aany na wengine wengi.

➡ Adam a.s ameambiwa mke na ALLAAH S.W mwenyewe, na mkewe anatokana na yeye mwenyewe Adam a.s.

➡ AmesemaALLAAHU S.W :

(خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنْزَلَ لَكُمْ مِنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِنْ بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ)
[Surat Az-Zumar 6]

Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile. Na akakuleteeni wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyu ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?

➡ Na huu ni muujuza mkubwa wa kuthibitisha uwezo wa ALLAAH S.W juu ya kila kitu.

➡ Adam a.s hakuzaliwa, bali ameambwa kwa udongo.

➡ Mkewe ameumbwa kutoka ndani ya mwili wa Adam bila ya kuzaliwa .

➡ Nabii Issa bin Mariamu a.s amezaliwa kutokana na mama tu bila ya baba.

➡ Baada ya hapo binaadamu wote wanazaliwa kwa kutokana na baba na mama.

➡ Hakuna dalili yoyote inayo onyesha kuwa : Nabii Adam a.s alioa mwa kutoa mahari “

➡ Mke hiyo ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Mola wake s.w.

➡ Na wala hakuna dalili yoyote inaonyesha khutba ya ndoa yake wala sherehe ya ndoa hiyo ilikuwa vipi.

➡ Wala hakuna dalili kuonyesha kuwa kuna nguo maalumu walivaa siku hiyo kwa ajili ya harusi.

➡ Kisha ndugu zangu Nakumbusha kitu kimoja muhimu sana :
“Sheria za mitume zinatofautiana kutoka mtume hadi mtume mwingine, na hii ni katika baadhi ya sheria tu.

➡ Mahari katika umma wetu sisi ni sheria katika umma wetu kwa mujibu wa Qurani na sunna.

➡ Kwa hiyo mahari katika uisilamu ni amri ya ALLAAH S.W na mtume wetu muhammad s.a.w.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً ۚ فَإِنْ طِبْنَ لَكُمْ عَنْ شَيْءٍ مِنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَرِيئًا)
[Surat An-Nisa 4]

Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni kipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha.

➡ Na amesema pia baada ya kutaja aina za wanawake wanao haramika kuwaoa, kisha akataja miongoni mwa wanaoharamika hao kuwa ni :

(وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُمْ مَا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَنْ تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُمْ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُمْ بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُمْ بِهِ مِنْ بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا)
[Surat An-Nisa 24]


NA WANAWAKE wenye waume, isipo kuwa walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sharia ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalilishiwa wasio kuwa hao, mtafute kwa mali yenu kwa kuowa pasina kuzini. Kama mnavyo starehe nao, basi wapeni mahari yao kwa kuwa ni waajibu. Wala hapana lawama juu yenu kwa mtakacho kubaliana baada ya kutimiza waajibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua na Mwenye hikima.

➡ Kwa hiyo hoja si kutazama sheria za mtume wa zamani wakati sheria yake na yetu iko tofauti.

➡Je huoni hata hukmu ya kuoana watu ndugu katika ummati wetu limekatazwa , wakati zamani walikuwa wanaoana ndugu wa huyu kwa ndugu wa yule?

➡NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNGULIE MILANGO YA HIKMA NA ELIMU.

ALLAAHU AALAMU.

” Asili katika uisilamu ni kufuata muongozo wa kitabu cha ALLAAH s.w, na sunna za mtume s.a.w.”

JAWABU KUTOKA KWA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Uadilifu ni upi kishariah? Je,kwa mume mwenye mke zaidi ya mmoja uadilifu ni kuwagawia sawa katika matumizi hata japo kila mmoja ana mahitaji tofauti ?

JAWABU

➡ Uadilifu ni : ” Kukipa kila kitu haki yake “

➡ Na usawa ni : ” Kulinganisha baina ya vitu viwili bila kutofautisha “

➡Kutokana na hayo, uadilifu si lazima kuwa vitu viwili kuvipa hukmu sawa.

➡ Mume anaweza kufanya usawa wa matumizi baina ya wake wawili, lakini juu hivyo akawa amefanya dhulma.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانْكِحُوا مَا طَابَ لَكُمْ مِنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا)
[Surat An-Nisa 3]
Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana.

➡ Kwa hiyo uadilifu ni mume kumpa kila mke mahitaji yake ya lazima, kwa mujibu wa uwezo wa mume alio jaaliwa na ALLAAH S.W, na kwa mujibu wa mahitaji ya mke mwenyewe.

➡ Mke wa Abii Sufyaan r.a Alikuja kwa mtume s.a.w kushitakia kuwa mumewe ni mzuiaji wa kutoa matumizi kwake.

➡ جاءت هندٌ امرأةُ أبي سفيانَ إلى النَّبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فقالت: إنَّ أبا سفيانَ رجلٌ شحيحٌ فهل عليَّ جُناحٌ أنْ أُصيبَ مِن مالِه فأُنفِقَ علَيَّ وعلى ولَدي ؟ فقال لها نبيُّ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم:
( لا حرَجَ عليكِ أنْ تأخُذي مِن مالِ أبي سُفيانَ فتُنفِقيه عليكِ وعلى ولَدِكِ بالمعروفِ )
الراوي: عائشة المحدث: ابن حبان – المصدر: صحيح ابن حبان – الصفحة أو الرقم: 4258
خلاصة حكم المحدث: أخرجه في صحيحه

➡ Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha r.a, Alikuja Hindu mke wa Abii Sufyaan r.a kwa mtume s.a.w, akasema : ” Yaa rasuula llaah; Hakika Abaa Sufyaan ni mtu bakhili, je kuna tatizo lolote nikichukua katika mali yake kisha nikaitumia mimi na watoto wangu?

Akasema mtume s.a.w :
” Hakuna tatizo lolote ukichukua katika mali ya abii Sufyaan na kutumia wewe mwenyewe na watoto wako – kwa kawaida “

➡ Na hii inaonyesha kuwa alikuwa abuu Sufyaan anatoa lakini kitu kidogo ambacho hakikidhi mahitaji ya mkewe na wanae, na hali ya kuwa ana uwezo.

➡ Nakumbusha kuwa : ” uadilifu huu ni katika mambo ambayo binaadamu tumepewa uwezo wa kuyadhibiti mambo hayo, ambayo ni mambo ya dhaahiri yanayo onekana wazi.

➡ Amma yaliyomo ndani ya nafsi na haya kudhihirishwa nje kutoka kwa mume, wala hakubagua baina ya wake zake wawili, wala kushuhudisha mapenzi juu mmoja wao kuliko mwingine, hilo halina ulazima kwa kuwa liko nje ya uwezo wa mja.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

” uadilifu ni sifa miongoni mwa sifa za ALLAAH S.W na mja aneamrishwa kuwa na uadilifu “

JAWABU KUTOKA KWA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Vipi inafaa mtu na mke wake wakaweka kanda zakuonesha watu wanafanya tendo la jimai, je inafaa ?

 

JAWABU

➡ Dini ya kiisilaamu ni dini inayo fundisha adabu stara.

➡ Si katika adabu wala murua kwa mtu kuweka utupu wake hadharani wala kwa mtu kutazama utupu wa mwenzake.

➡ Na hii hukmu ni kwa watu wote isipokuwa mke na mume tu wao kutazama na wao kwa wakiwa Katika sehemu ambayo hawaonwi na mtu mwingine.

➡ Na juu ya hivyo bado pia sunna zimetaja kuwa :

إذا أتى أحدُكم أهلَه فلْيستَتِرْ ، ولا يتجرَّدانِ تجرُّدَ العِيرَينِ
الراوي: عبدالله بن مسعود المحدث: البوصيري – المصدر: إتحاف الخيرة المهرة – الصفحة أو الرقم: 4/ 57
خلاصة حكم المحدث: له شاهد

➡Kutoka kwa Abdillaah bin masoud r.a, amesema mtume s.a.w : ” Atakapo muingilia mmoja wenu mkewe, basi na ajisitiri, na wala wasijiache wazi kama wanyama wawili “

➡ Bali hata Nabii Adam a.s alipofanya kosa yeye na mkewe, kisha wakaondoshewa ile stara waliyo kuwa wamepewa na ALLAAH S.W, walikimbilia haraka majani ya miti na kuanza kufunika tupu zao.

➡ Tazama aya zifuatazo :
(فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ ۚ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِنْ وَرَقِ الْجَنَّةِ ۖ وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَنْ تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُلْ لَكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُبِينٌ)
[Surat Al-Araf 22]

Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet’ani ni adui yenu wa dhaahiri?

➡ Na ziko hadithi mbalimbali zimekataza hata mwanaume kutazama hata hata paja la mwanaume mwenzake.

➡Hilo jambo halifai na ni haramu kwa mtu yoyote kufanya hivyo.

➡Na amelaaniwa mwenye kutazama Utupu wa mtu mwingine.

➡Na hukmu hii haina tofauti yoyote kwa maulamaa.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUEPUSHE NA MAOVU YOTE.

ALLAAHU AALAMU.

” UISILAMU NI DINI YA HESHINA NA STARA “

JAWABU KUTOKA KWA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shukran allah akulipe kwa juhudi zako albattaashy, Ila njoo na dalili dhidi ya kauli yako hii Na kuangalia wanazuoni wamesemaje kuhusu hili, Yaani kuhusu kuifuatisha adhana kwa kuisikia katika Radio. 

JAWABU

➡ Katika suala hilo la kufuatisha adhana kwa kuisikia katika njia ya Radio, tumebainisha hukmu, na kutaja dalili katika sunna kuhusu amri inayohusu kuitikia wito wa adhana.

➡ Amma kuhusu dalili dhidi ya kauli yangu, hapo hakuna kauli dhidi yangu kwa kuwa sikutoka nje na mafhuumu ya hadithi iliyopokewa kuhusu kuitikia adhana.

➡ Na wala haikutoka nje ya kauli za maulamaa ambao fataawa zao nimezisoma na nikakuta wamesema hivyo.

➡ Na misingi mikuu ya dini ambayo hukmu za uisilamu zimejengeka kwayo nimetaja baadhi yake katika jawabu ikiuotangulia .

➡ Kwa mujibu wa hadithi hii ifuatayo maulamaa wametoa fatwa ya kujuzu kuitika na kufuatisha adhana katika njia ya Radio.

➡ Katika hadithi iliyopokewa Jatika sahihi l bukhaary na Muslim r.a , Amesema mtume s.a.w : :

إذا سمعتُمُ المؤذِّنَ فقولوا مثلَ ما يقولُ ..

الراوي: عبدالله بن عمرو المحدث: مسلم – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 384
خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Maana yake ni kuwa :
” Mutakapimsikia muadhini basi semeni kama anavyosema. ..”

➡ Kwa mujibu wa tamko la hadithi hapo ” إذا ” ” Idhaa ” ; maulamaa wanasema kuwa : ” Tamko hilo linaonyesha ujumla wa wakati wowote mtakapomsikia muadhini, au popote mtakapo msikia muadhini, au kwa njia yoyote.

➡ Na miongoni mwa maulamaa waliotoa fatwa hii ni :

1 – Sh Abdu l Aziiz bin Abdi llaah bin Baaz r.a.

Rejea fataawa ibni Baaz ukurasa wa 259 – 260.

2 – Pia sheikh Muhammad bin Muhammad bin mukhtaar al shanqiitwy

Tena yeye amesema :
” Kauli hiyo ina nguvu zaidi kutokana na ujumla wa tamko lililokuja katika hadithi hizo.

3 – Sh muhammad bin swaaleh al uthaimiin r.a pia amesema : ” Naam, unaifuatisha adhana katika ikiwa inaadhiniwa ndani ya wakati wa sala “

4 – Na Dk ubeid al jaabiry amesema hivyo pia, isipokuwa yeye amesema afuatishe adhana ya chanel au Idhaa ya mji aliopo yeye.

Kama mtu wa makka ya makka na wa Madina ya madina.

ALLAAHU AALAMU.

” Uisilamu ni dini ya wepesi katika sheria zake “

SH.  SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Zipo hadithi zasema tufatishe kuitikia muadhini anapoadhini. Je! Inafaa kufuatisha adhana ya kwenye redio ambayo huwa inarekodiwa?

هل يجوز اتباع كلمات الأذان من تسجيل الأذان عن طريق المذياع؟

JAWABU الجواب = 

➡ Naam :
Ziko hadithi mbalimbali zimetaja amri ya kufuatisha adhana anapo adhini mwenye kuadhini.

نعم : هناك أحاديث كثيرة وردت في فضل اتباع المؤذِّنَ في كلمات الأذان.

➡ Amesema mtume s.a.w katika hadithi aliyo ipokea Swahahabiy Abdullaah bin Amruu r.a :

إذا سمعتُمُ المؤذِّنَ فقولوا مثلَ ما يقولُ . ثمَّ صلُّوا عليَّ . فإنَّهُ مَن صلَّى عليَّ صلاةً صلَّى اللَّهُ عليه بِها عشْرًا . ثمَّ سلوا اللَّهَ ليَ الوسيلَةَ . فإنَّها منزِلةٌ في الجنَّةِ لا تنبغي إلَّا لعبدٍ من عبادِ اللَّهِ . وأرجو أن أكونَ أنا هو . فمن سأل ليَ الوسيلةَ حلَّتْ لهُ الشَّفَاعةُ”

الراوي: عبدالله بن عمرو المحدث: مسلم – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 384
خلاصة حكم المحدث: صحيح

” Mutakapo msikia muadhini, basi semeni kama anavyosema, kisha muniswalie mimi, kwani hakika mwenye kuniswalia mimi sala moja basi ALLAAH S.W atamswalia mara kumi, kisha niombeeni wasila – kiunganishi / kiwasilishi/ njia, kwani wasila hiyo ni daraja katika Pepo, haimstahikii ila mja miongoni mwa waja wa ALLAAH, na ninataraji kuwa mimi ndie mwenyewe, basi mwenye kumuombea mimi wasila hiyo atahalalakiwa na utetezi / uombezi wangu- siku ya qiyaama “

➡ Na adhana ambayo tume amrishwa kuifuatisha ni ile ambayo inaadhiniwa na sisi tuko karibu nayo kwa kuisikia .

و الأذان الذي أمرنا بمتابعته هو الذي يكون أقرب إلينا، ونحن أقرب إليه من حيث السماع.

➡ Amma ambayo iko mbali na sisi, au na sehemu tulizoko, au katika maeneo yaliyokaribiana sana misikiti yake, au katika radio, hizo sisi hatukulazimswa kuzifuatisha zote kila tunapozisikia.

أما الذي يكون بعيدا عنا، أو في مكان غير المكان الذي نحن فيه، أو في أماكن ومساجد متقاربة، أو في الإذاعة، فإننا لسنا مأمورين وجوبا بمتابعته.

➡ Na ndio maana hata hadithi hiyo mtume s.a.w amesema :” Al mu’addhin” ” المؤذن ” Na hakusema :
“Muaddhin” “مؤذنا ” , kwa kuwa hiyo lafdhi ambayo haikuanziwa na herufi za ” ال” ” Al ” ina kuwa inamaanisha mu’addhin yoyote yule utakae msikia.

ولذلك نجد أن اللفظ الذي ورد في الحديث هو لفظ معرف بالألف و اللام ( ال) في قوله : “المؤذن “، ﻷنه لو جاء منكرا لكان لفظا عاما يشمل لزوم متابعة جميع المؤذنين، بخلاف هذا المعرف الذي يدل على العهد والتخصيص .

➡ Lakini hiyo yenye “Al – ال” inaonyesha muadhini maalumu kwa maana ya ukaribu, na wala si ujumla kwa kila muadhini utakae msikia.

➡ Na iko wazi kufahamika hata kwa mujibu wa misingi ambayo dini imejengeka juu ya misingi hiyo.

وهذا واضح حتى من حيث الأسس التي بني عليها هذا الدين.

➡ Na moja ya misingi hiyo ni : ” Kutokuwepo uzito / mashaka katika hii dini “

و أحد هذه الأسس التي بني عليها الدين:
“عدم الحرج في أحكام هذا الدين “

➡ Amesema ALLAAHU S.W: قال الله تعالى

(وَجَاهِدُوا فِي اللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِنْ قَبْلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ. ..ُ)
[Surat Al-Hajj 78]

Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur’ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu.

➡ Ingekuwa ni wajibu Kuitika na kufuatisha kila adhana basi ingekuwa sheria hii ni nzito kutekeleza kwa watu.

فلو وجب متابعة كل مؤذن لكان ذلك مما يشق على الناس أداؤه، وذلك ﻷسباب :

➡ Kwa sababu :

1- Misikiti inaweza kuwa mingi katika mji mmoja, na adhana zote anaweza kusikia kupitia vipaza sauti.

تقارب المساجد في بلد واحد حيث يمكن سماع جميع الأذانات عن طريق مكبرات الصوت.

2 – Pia nyakati za adhana katika mji zinatofautiana kwa muda mfupi baina ya msikiti na msikiti mwingine, kwa hiyo itakuwa ni uzito na mashaka kufuatisha adhana za misikiti yote.

أيضا تفاوت مواقيت رفع الأذان ولو بمدة قصيرة بين مسجد و آخر، وهذا يجلب مشقة على المسلم لو أمر بمتابعة كل أذان يسمعه.

➡ Amma kufuatisha adhana katika radio hiyo ni bora na vizuri kusikiliza , na hasa ikiwa adhana hiyo iko karibu yako zaidi.

أما متابعة الأذان في المذياع، والمذياع قريب منه فهذا فيه فضل، وهو المستحب، و خاصة إذا كان المذياع أقرب إليه.

➡ Lakini ulazima wa kufuatisha adhana ya radio si sawa na kusikia adhana kutoka kwa muadhini mwenyewe ambae ni mtu muadhini moja kwa moja.

ولكن تأكيد هذه المتابعة عن طريق المذياع ليس كتأيد من يسمع المؤذن مباشرة .

➡ Na hii pia ni kwa sababu, adhana ni ibada, na ni lazima aiadhini mtu moja kwa moja msikitini.

وذلك ﻷن الأصل هو أن الأذان عبادة، ولا بد أن يقوم به شخص مباشرة – في المسجدِ.

➡ Na ikiwa watu wa msikiti watakubaliana kuwa :”waweke radio tu iadhini katika kila sala badala ya kuadhini mtu, basi haisihi adhana yao hiyo katika msikiti huo, hata kama radio hiyo iko ndani ya msikiti bila ya ikhtilafu.

ولو أن أهل مسجد اتفقوا على أن يضعوا تسجيل الأذان في مسجدهم ليؤذن بالتسجيل بدلا من الإنسان، فإن أذانهم باطل بلا خلاف.

➡ Kutokana na hayo yote, adhana ya wajibu kufuatisha ni ile ambayo imeadhiniwa na muadhini moja kwa moja, na si ile ya kurekodiwa katika radio na mfano wake, pamoja na kuwa pia kuna fadhila kufuatisha adhana uliyo isikia kwa njia ya Radio.

من هذا المنطلق؛
الأذان الذي يجب متابعته في الأصل هو الذي يسمع مباشرة من المؤذِّن، وليس الذي يسمع من المذياع.

مع أنه هناك فضل في المتابعة في الإذاعة

➡ ALLAAHU AALAMU.

” Uisilamu ni dini ya wepesi katika sheria zake “

SH. SHAABAN ALBATTAASHY
المجيب : الأستاذ / شعبان بن سالم بن حمود بن محمد بن عدي بن شامس البطاشي.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Je maibadhi wameshikamana na sunna za mtume s.a.w ? 

هل الإباضية متمسكون بسنة رسول الله صلى الله عليه وسلم؟ 

 JAWABU= الجواب 

➡ Ibaadhi ni dhehebu miongoni mwa madhehebu sahihi ya kiisilaamu kama yalivyokuwa madhehebu mengine ya sunni kwa jumla.

الإباضية مذهب إسلامي صحيح مثل المذاهب السنية الأخرى من حيث الجملة.

➡ Madhehebu yote hayo yanafuata misingi ya qurani na sunna za mtume s.a.w.

هذه المذاهب كلها تتبع أصول القرآن والكريم وسنة نبينا محمد صلى الله عليه وسلم.

➡ Pamoja na kuwa madhehebu yote hayo yamepewa majina kwa mujibu wa maimaamu walikuwa wakiweka njia za kuweza kuifahamu dini kupitia njia hizo, lakini jina la madhehebu halina maana ya kuwa ndio sifa ya kila mfuasi wa dhehebu hilo.

ومع كون كل مذهب سمي باسم الإمام الذي كان يضع أسسا ومناهج لتيسير فهم الدين على الناس، وفقا لتلك الأسس، ولكن اسم المذهب لا يعني صفة كل تابع لذلك المذهب.

➡ Na ukiangalia madhehebu yote ya kiisilaamu basi utakuta ziko tofauti baina yao katika kuchukulia umuhimu sunna za mtume s.a.w.

و إذا نظرت إلى المذاهب كلها ستجد فرقا كبيرا من حيث قوة الاتباع والتمسك بالسنة
➡Mizani ya kujua ubora wa kila mtu si madhehebu fulani, bali ni kuwa mcha Mungu, kwa kufuata muongozo wa ALLAAH S.W na mtume wake Muhammad s.a.w.

الميزان الصحيح للخيرية والفضل ليس مذهبا فلانيا، بل كون أحدنا تقيا متبعا لهدي الله تعالى ورسوله محمد صلى الله عليه وسلم.

➡ Tukianza kulinganisha idadi ya watu wema katika kila madhehebu, basi hii itapelekea kudharauliana na kufakharishana watu kwa madhehebu yao, na mwisho wa yote ni kuonyeshana watu kwa amali zao.

فإذا بدأنا في المقارنة بين الصالحين من كل مذهب، فسوف يؤدي هذا إلى التفاخر والسخرية بالآخرين، واغترار الناس بمذاهبهم، وفي المآل إلى الرياء بإظهار عمل بعضهم على بعض.

➡ Je hakiwatoshi kitabu cha ALLAAH s.w katika kuhukumu juu ya suala hili?
أما كفاكم كتاب الله تعالى في الحكم على مثل هذه المسألة؟


➡ Amesema ALLAAHU S.W : قال الله تعالى :

(الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنْشَأَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنْتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنْفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ)
[Surat An-Najm 32]

Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.

➡ Kwa hiyo yoyote atakaekuwa anafañya mambo kinyume cha sheria za ALLAAH S.W na mtume wetu muhammad s.a.w, basi huyo si mfuasi wa sunna, hata kama madhehebu yake itakuwa ni ibadhi au ash’ary au salafy, au madhehebu yoyote.

من هذا المنطلق؛
فإن كل من كان يعمل على خلاف شرع الله تعالى، ورسوله محمد صلى الله عليه وسلم، فهو ليس من أتباع السنة حتى لو كان لو كان مذهبه يسمى إباضيا، أو أشعريا، أو سلفيا، أو أي مذهب آخر.

➡ Na ikhtilafu yoyote baina yetu basi turejeshe kwa ALLAAH S.W na mtume wetu muhammad s.a.w.

وأي خلاف وقع فعلينا إرجاع الحكم إلى الله تعالى ورسوله محمد صلى الله عليه وسلم.

➡ Amesema ALLAAHU S.W : قال الله تعالى

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنْكُمْ ۖ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا)
[Surat An-Nisa 59]

Enyi mlio amini! Mt’iini Mwenyezi Mungu, na mt’iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.

➡ Na hukmu ya mwisho ni kwa ALLAAH S.W mwenyewe.

والحكم النهائي لكل شيئ إلى الله تعالى وحده دون غيره.

➡ Amesema ALLAAHU S.W : قال الله تعالى

(وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِنْ شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ)
[Surat Ash-Shura 10]

Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, ninaye mtegemea na kwake Yeye narejea.

➡ Na wasia wa Nabii Ibraahiim a.s kwa umma wote alisema kama alivyosema ALLAAH s.w :

(شَرَعَ لَكُمْ مِنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ ۚ اللَّهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَنْ يُنِيبُ)
[Surat Ash-Shura 13]

Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUPE HIDAYA NA UMOJA BAINA YETU.

“أسأل الله تعالى أن يرزقنا الهداية والوحدة بيننا “

ALLAAHU AALAMU
” الله أعلم “

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Naomba kuuliza swali: ” Khutba moja inaweza kufunga ndoa mbili ?

السؤال : هل تكفي خطبة النكاح واحدة في الزواج الجماعي؟ “

JAWABU الجواب 

➡ينبغي أن تكون خطبة النكاح مشتملة على الحمد والثناء على الله تعالى، والصلاة والسلام على رسول الله صلى الله عليه وسلم.

Khutba katika ndoa inatakiwa iwe imekusanya ndani yake utangulizi katika kumshukuru ALLAAH S.W na kumsalia mtume wetu muhammad s.a.w.

➡ و أن تشتمل على بعض الآيات التي تذكر بتقوى الله تعالى، و أهمية الزواج وبعض آدابه و فضائله.

Na pia iwe ina baadhi ya aya zinazokumbusha kumcha ALLAAH S.W, na umuhimu wa ndoa na baadhi ya adabu na fadhila zake.

➡ أما الاكتفاء بخطبة واحدة في الترويج الاثنين أو أكثر، فإنه لا مانع من ذلك إذا كان المتزوجون كلهم في مكان واحد، مع مراعاة الشروط التالية :

Amma kuhusu khutba moja kwa kuwaozesha watu wawili au zaidi ikiwa wako pamoja wote, Naam inajuzu kufanya hivyo lakini kwa masharti yafuatayo :

1 – تعيين النساء المتزوجات ليكون قبول كل منهم لزوجه التي خطبها.

Kuainishwa wanawake hao wanao olewa, ili kila mume atakapiulizwa kuhusu kukubali kwake kumuoa mwanamke alie mposa, akubali kuwa amemkubali.

2 – أن يكون هناك شهود على ذلك الزواج الجماعي، ويتم الإعلان.

Kuwepo mashahidi walioshuhudia kukubali kwa walii na mwanamke mwenyewe pia alieolewa.

Baada ya hapo itakuja kutangaziwa katika ndoa ya pamoja.


فلا مانع إن شاء الله تعالى من هذا الزواج ما دام كل زوج يعرف قريته، وكذلك هي تعرفه، وقد شهد على ذلك الشهود.

Hakuna kizuizi Inshaallaah katika hilo, midhali kila mume anamjua mke aliemuoa, kila mke anamjua mume aliemuoa, na mashahidi wameshuhudia hilo Inshaallaah.

3 – عدم خلط بين الرجال والنساء في الحفل، لما في ذلك من الفتنة التي لا تخفى.

Kusiwepo kuchanganya baina ya wanaume na wanawake katika hafla hiyo, kutokana na fitna kubwa ambayo haifichikani.

➡ ALLAAHU AALAMU
“الله أعلم “

“الإسلام دين يسر في أحكامه “
” Uisilamu ni dini ya wepesi katika sheria zake “

SH.  SHAABAN ALBATTAASHY
المجيب : الأستاذ / شعبان بن سالم بن حمود بن محمد بن عدي بن شامس البطاشي “

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Ustaadh;  Je kwa mujibu wa maandiko, ni halali mwanamke wa kiislam kukeketwa ?

JAWABU

➡ Kukeketwa maana yake ni : ” Kutahiriwa “

➡ Na hii inakuwa ni wajibu kufanyiwa wanaume, wale ambao wamezaliwa na hali ya kuwa kuna ugozi unafunika kichwa cha sehemu yake ya siri ya mbele “

➡ Na haya ni maumbile ambayo kawaida kila mtoto wa kiume anazaliwa katika hali hiyo, kisha anafañyiwa twahara kwa kukatwa ugozi huo.

➡ Na hukmu ya suala hili ni :
” wajibu kwa kila mwanaume kufanyiwa twahara hiyo na hasa wakiwa katika umri mdogo bado ni bora zaidi kuliko kuchelewesha “

➡ Na muda wa kuanza kufanyiwa khitani mtoto wa kiume kuna ikhtilafu, baadhi ya maulamaa wanaona kuwa :

1 – bora ni kumfanyia siku ya saba tokea kuzaliwa kwake.

2 – Wengine wanaona bora kuanzia miaka saba hadi kumi na mbili, kama ilivyokuja katika ” Al fataawa l hindiyya ” katika fiqhi ya hanafy.

➡ Amma kuhusu wanawake kufanyiwa twahara ya kukatwa vigozi vinavyo dhihirika katika sehemu zao za siri, wao si wajibu kufanyiwa hivyo.

➡ Maulamaa wengi wanaona kuwa ni vizuri kutahiriwa mtoto wa kike, na hasa wa kuwa umri kabla ya kubaleghe “

➡ Na hii imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik r.a, amesema :

➡ – أنَّ النبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ قال لأمِّ عطيةَ ختانةٌ كانت بالمدينةِ إذا خفضتِ فأشِمِّي ولا تنهكي فإنَّهُ أسرى للوجهِ وأحظى عند الزوجِ”

الراوي: أنس بن مالك المحدث: الهيثمي – المصدر: مجمع الزوائد
” Hakika Mtume s.a.w alimwambia ummu Atwiyya r.a, ambae alikuwa ndie mwenye kuwafanyia khitani wanawake katika mji wa Madina, ” Ukikata basi – kata juu juu wala usizamishe sana kikatio chako, kwa sababu hiyo inamfanya awe na uzuri wa uso na raha ya tendo la ndoa kwa mumewe “

➡ Na katika fatwa za sh Ahmad bin hamad alkhaliily anasema kuwa : ” Kuwafanyia kitabu -:kuwatahiri wanawake ni makrama” kitu kizuri kwao lakini si wajibu kufanyiwa twahara hiyo.

➡ Kwa hiyo suala hili hukmu yake iko baina hukmu mbili zifuatazo :

1 – Ni sunna tu.

2 – Ni jambo zuri tu.

➡ Hakuna kauli ya kuharamishwa jambo hili kwa mujibu wa fatwa za maulamaa wa madhehebu za ahli sunna na madhehebu ya ibaadhi.

➡ Muhimu ni:

1- kuchunga mipaka ya kisheria ikiwa kutakuwa na mwanamke mwenye ujuzi wa kuwatahiri wanawake.

2 – Na iwe kwa kusitiri na kutotoa aibu au siri ya mwenye kutahiriwa.

3 – Isiwe kwa kumlazimisha bint bila khiyari yake mwenyewe, kwa sababu jambo hili si lazima kwake.

4 – Iwe hakuna madhara ya aina yoyote katika kufanyiwa twahara hiyo.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

 ALLAAHU AALAMU.

” Uisilamu ni dini ya usafi na maumbile sahihi “

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Mimi wakati wa kwenda haja ndogo mwishoni hutoka majimaji mazito mfano wa manii. je hapo nitalazimika kukoga ?

JAWABU

➡ Kukoga hakulazimiki kwa sababu tu ya kutokwa na maji maji baada ya haja ndogo.

➡ Mambo ambayo yanayo wajibisha kukoga ni :

1 – Kutokwa na manii kwa njia ya kuingiliana baina mke na mume.

2 – Au kutokwa manii kwa kuota usingizini.

3 – Au ikiwa atajitoa mtu mwenyewe manii kwa njia yoyote, atakuwa twahara muda huo hana mpaka akoge twahara ya mwili mzima.

4 – Pia baada ya kumaliza hedhi au nifasi ni lazima ajitwaharishe twahara kubwa kwa kukoga mwili mzima.

➡ Maji maji hayo yanayotoka baada ya mkono kwa mujibu wa lugha ya sheria huitwa
” wadii “

➡ Na haya ni maji ambayo hayawajibishi kukoga , bali ni wajibu kutwaharisha tu kama anavyojitaharisha mtu aliekidhi haja za kawaida.

➡Namuomba ALLAAH s.w atukinge na shari za viumbe vyake.

ALLAAHU AALAMU.

” UISILAMU NI DINI YA WEPESI “

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI: 

Nini hukumu ya mwanamke kuswali na kucha refu ?

JAWABU

➡ Kukata kucha ni miongoni mwa sunna za lazima za kimaumbile katika uisilamu.

➡ Na uisilamu umeme isha sana swala la usafi wa kila aina, hasa usafi wa mwili wa muisilamu.

➡ Kukata kucha ni moja miongoni mwa mambo yaliyoamrishwa na mtume s.a.w katika hadithi mbalimbali.

➡ Amepokea imaamu ibnu Hibbaan, kutoka kwa Abii huraira r.a, amesema mtume s.a.w :

الفطرةُ خمسٌ: تقليمُ الأظفارِ وقصُّ الشَّاربِ والاستحدادُ والختانُ ونَتْفُ الإِبْطِ”

الراوي: أبو هريرة المحدث: ابن حبان – المصدر: صحيح ابن حبان – الصفحة أو الرقم: 5481

“Fitra / maumbile sahihi ni mambo matano : Kukata kucha, kukata masharubu, kunyoa nywele za kibofu , na kutahiriwa , na kuchomoa nywele za makwapa “

➡ Na muda wa kukata kucha na kujisafisha maeneo hayo ya ndani ya mwili ni kama ifuatavyo :

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik r.a kuwa :

“وقت لنا رسول الله صلى الله عليه وسلم : حلق العانة وتقليم الأظفار ، وقص الشارب ، ونتف الابط ، أربعين يوما مرة”

الراوي: أنس بن مالك المحدث: الألباني – المصدر: صحيح أبي داود – الصفحة أو الرقم: 4200
خلاصة حكم المحدث: صحيح

” Alituwekea muda mtume s.a.w wa kunyoa nywele za kibofu, na kukata kucha, na kukata masharubu, na kung’oa nywele za kwapa , kila siku arobaini mara moja “

➡ Mwanamke huyo ikiwa udhu wake umefika sehemu za lazima kufika maji ya udhu, sala yake itakuwa ni sahihi, lakini atakuwa amefanya jambo la makruuhu.

➡ Na kurefucha kucha ni kuiga mila za waliokuwa si waisilamu.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE KUIFUATA MUONGOZO WA QURANI NA SUNNA.

ALLAAHU AALAMU.

” Kufaulu ni katika kufuata muongozo wa Qurani na sunna “

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Ikiwa mke kaachwa na mumewe, lakini hajamaliza eda, kisha akaolewa na mume mwengine nini hukmu yake ?

JAWABU 

➡ Mke yoyote alieachwa na mumewe ni lazima akae eda ya kuachwa, kwa kiasi cha muda aliopanga ALLAAH S.W mwenyewe.

➡ Na eda ya kuachwa mwanamke ni hedhi tatu, au miezi mitatu kwa wanawake ambao hawapati hedhi.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنْفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَنْ يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِنْ كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ٌ)
[Surat Al-Baqara 228]

Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka t’ahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuzii kuficha alicho umba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu.

➡ Na amesema pia kuhusu waliokuwa hawapati hedhi :

(وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِنْ نِسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ ۚ …)
[Surat At-Talaq 4]

Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi.

➡ Ni haramu kumuoa mwanamke ambae yuko ndani ya muda wake wa eda ya kuachwa au kufiliwa na mumewe.

➡ Bali ni haramu hata kumposa mwanamke ambae yuko katika eda.

➡ Amesema ALLAAHU S.W kuhusu mke aliekuwa katika eda ya kufiliwa kuwa :
(وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُمْ بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنْتُمْ فِي أَنْفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَٰكِنْ لَا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَنْ تَقُولُوا قَوْلًا مَعْرُوفًا ۚ وَلَا تَعْزِمُوا عُقْدَةَ النِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْكِتَابُ أَجَلَهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنْفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ)
[Surat Al-Baqara 235]

Wala si vibaya kwenu katika kupeleka posa kwa ishara tu kwa wanawake waliomo edani au mkadhamiria katika nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msiwaahidi kwa siri, ila mnene maneno mema. Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka eda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo katika nafsi zenu. Basi tahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole.

➡Mke ambae yuko katika eda ya kuachwa, mumewe ndie mwenye haki nae, kwa kuwa mke wakati wa eda anakuwa ana hukmu kama mke wakati wa ndoa.

➡ Ikiwa mke aliefiwa na mumewe ni haramu kumuoa, vipi itakuwa hukmu kwa huyu ambae yuko katika eda na mumewe yuko hai? ???

➡Bila shaka hili ni kosa kubwa zaidi bila ikhtilafu yoyote.

➡ Ndoa hiyo iliyofungwa ni ndoa batili haikubaliki kusheria .

➡ Inatakiwa haraka sana watenganishwe hao walio owana katika eda.

➡ Kisha mwanamke huyo anatakiwa arudiwe na mumewe ikiwa mume aliemuacha atataka mwenyewe kumrudia.

➡ Na kama mume huyo atakuwa hataki kumrejea tena basi si tatizo, lakini mke huyo anatakiwa asubiri bila ya kuolewa mpaka amalize Muda wa eda uliobakia, ambao ni haki ya mumewe.

➡ Kisha baada ya hapo atasubiri tena mwanamke huyo bila ya kuolewa mipaka apate hedhi mara moja, ili kuhakikisha kuwa tumbo lake halina ujauzito kutokana na mwanaume huyo wa pili aliemuoa kinyume na haki.

➡ Na huyo mume akitaka kumrejea pia anaweza kumrejea wakati wowote kabla ya kumaliza eda ile ambayo yeye ndie alimuacha.

➡ Na atatakiwa kujizuia asimuingilie kwanza baada ya kumrejea mpaka apate hedhi moja.

➡Hili jambo walilofanya hawa watu ni baya sana, na ilikuwa kama kuna kadhi wa kiisilaamu basi wapelekwe kwa kadhi wakatiwe bakora ili kutiwa adabu.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA.

 ALLAAHU AALAMU.

” Kuvuka mipaka ya ALLAAH S.W ni kufanya uadui katika sheria “

SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Ni zipi sifa za mume bora ?  Mwanamke akija mwanamume kumposa aangalie sifa gani ?

JAWABU

➡ Sifa bora za kutazamwa katika kuchagua mume au mke ni sifa ya uchamungu.

1⃣”Dini “: Nayo ni kuwa muislamu kwa Imani na vitendo vyema pamoja na Kauli “

➡ Na hili ni jambo muhimu sana kwa pande mbili zote kutazamwa, na tatizo kubwa mara nyingi hutokea ni kuwa :
” Wazazi wa mwanamke baadhi yao huwa wanachunguza sana upande wa mume tu, lakini wao huwa hawajitazami wako katika kiwango kipi katika sifa hizo.

➡ Amesema mtume s.a.w :
إذا جاءكم من ترضَونَ دينَهُ وخلُقَهُ فأنكِحوهُ”

الراوي: – المحدث: الترمذي – المصدر: تهذيب التهذيب – الصفحة أو الرقم: 6/62
خلاصة حكم المحدث: حسن

Amepokea imaamu al Tirmidhy , amesema mtume s.a.w : ” Atakapokujieni munae mridhia dini yake na tabia zake, basi muozesheni”.

➡ Na kwa upande wa mwanamke pia tumeambiwa na mtume s.a.w katika hadithi ya Abii huraira r.a, kuwa :

تُنكَحُ المرأةُ لأربَعٍ : لمالِها ولحَسَبِها وجَمالِها ولدينها، فاظفَرْ بذاتِ الدِّينِ تَرِبَتْ يَداكَ
الراوي: أبو هريرة المحدث: البخاري – المصدر: صحيح البخاري – الصفحة أو الرقم: 5090
خلاصة حكم المحدث: [صحيح]

➡ ” Mwanamke huolewa – kikawaida – kwa ajili ya mambo manne;
Kwa mali yake, na kwa koo lake, na kwa uzuri wake, na kwa dini yake, chagua mwenye dini utanusurika na udhalili “

Hadithi hiyo Ameipokea imaamu al bukhaary.

2⃣Pia awe ni muaminifu katika ndoa yake na mambo yote yanayohusu ndoa yake na kuteketeza sheria za ALLAAH S.W.

3⃣Awe Mpole kwa mkewe kwa kiasi kinachotakikana.

4⃣Awe ni mwenye uwezo wa kufikiri na kutoa maamuzi sahihi katika mambo ambayo yeye ni msimamizi juu yake.

5⃣Mwenye kuwa na sifa ya huruma katika Muamala na mfano wa hayo.

6⃣Asiwe na kasoro za kimaumbile ambazo zitasababisha mwanaume kuwa mandhari yake si nzuri kwa mkewe, au kuwa na maradhi ya hatari, au kuwa hawezi kumuingilia mkewe.

➡ Hayo ndio mambo muhimu ya kuzingatia, na hayo ndio siri ya Mafanikio ya kila kitu katika uhai na baada ya umauti inshaaaallaah.

➡ Sifa zote hizo zinajumuishwa na neno “uchamungu “

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

” Mke na mume mwema 
ni zake ALLAAH neema “

JAWABU KUTOKA KWA SH. SHAABAN ALBATTAASHY