Home Sh.Humoud Al-Rawahy

Sh.Humoud Al-Rawahy

Published By Said Al Habsy

SWALI

Sheikh nina suala “Nini maana ya Ramadhani” ❓

JAWABU

✏️ Ramadhani (رمضان) ni neno la kiarabu latokana na neno la asli lenye harfu 3 za asili ( mujrrad), nalo ni ramadha (رمض) .

✏️ Neno ramadhani limetajwa ktk qur-ani surat baqarah aya 185 aliposema allah taalaa

“شهر رمضان الذي أنزل فيه القرءان “
Mwezi wa ramadhani ambao umeteremshwa ndani yake (ktk laylatu qadri) qur-an.

Na hakuna mwezi uliotajwa kwa jina lake ila mwezi huu kwa utukufu mkubwa uliopo ndani yake na fadhila zake.

wametofautiana maulamaa neno la (ramadhan) nini hassa maana yake, ufupisho wake ni kama hivi 

1⃣ – Amesema alkhalili kuwa maana yake ni mvua Huja kusafisha ktk ardhi na mavumbi.., yaani mwezi huu ukija husafisha miili ya binaadamu na maovu .

2⃣- na wako waliosema kuwA ramadha ni jiwe lilokuwa moto sanaa baada ya kupigwa na juwa kisawa sawa.

3⃣ – na wako waliosema kuwa ramadha ni unguzaji uliomkali .. Yaani kumainisha kuwa mwezi huu unaunguza madhambi ya waja wake Allah.

4⃣ – Amesema Mujaahid kuwa ramadha ni jina katika Majina yake Allah

Kwa ufupi ramadhani inamainisha kuwa kusafisha, kufuta, kuunguza, kutoharisha kila kichafu kiovu ktk mwili na roho

 والله أعلم. 

Published By Said Al Habsy

SWALI

Sheikh nina suala “Nini maana ya Ramadhani” ❓

JAWABU

✏️ Ramadhani (رمضان) ni neno la kiarabu latokana na neno la asli lenye harfu 3 za asili ( mujrrad), nalo ni ramadha (رمض) .

✏️ Neno ramadhani limetajwa ktk qur-ani surat baqarah aya 185 aliposema allah taalaa

“شهر رمضان الذي أنزل فيه القرءان “
Mwezi wa ramadhani ambao umeteremshwa ndani yake (ktk laylatu qadri) qur-an.

Na hakuna mwezi uliotajwa kwa jina lake ila mwezi huu kwa utukufu mkubwa uliopo ndani yake na fadhila zake.

wametofautiana maulamaa neno la (ramadhan) nini hassa maana yake, ufupisho wake ni kama hivi 

1⃣ – Amesema alkhalili kuwa maana yake ni mvua Huja kusafisha ktk ardhi na mavumbi.., yaani mwezi huu ukija husafisha miili ya binaadamu na maovu .

2⃣- na wako waliosema kuwA ramadha ni jiwe lilokuwa moto sanaa baada ya kupigwa na juwa kisawa sawa.

3⃣ – na wako waliosema kuwa ramadha ni unguzaji uliomkali .. Yaani kumainisha kuwa mwezi huu unaunguza madhambi ya waja wake Allah.

4⃣ – Amesema Mujaahid kuwa ramadha ni jina katika Majina yake Allah

Kwa ufupi ramadhani inamainisha kuwa kusafisha, kufuta, kuunguza, kutoharisha kila kichafu kiovu ktk mwili na roho

 والله أعلم. 

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Sheikh,  Nini maana ya saumu ( funga )❓

JAWABU:

✏️ Saumu ni neno la kiarabu lenye harufu 3 za asili nazo ni ص/ و/م Saad/waaw/ mimu.

✏️ Neno hili kwa upande wa maana yake kilugha lina maana zifuatazo :–

1⃣- Kujizuiya na kitu na ukakiacha (kukinyamazia), yaani kunyamaza kimyaaa.

Allah anasema ktk Surat Maryam, Aya 26.  ” إني نذرت للرحمن صوما”

Hakika yangu mimi nimeweka nadhiri kwa Rahmaan ( Allah) kuwa sitoongea ( na mtu yoyote yule).

2 –  Kutulia na kusimama; Kwa mfano unaweza kusema hivi , “صامت الريح”

Umetulia upeo na kunyamaza Au .. صام الفرس ” Farasi Ametulia “

Hizi ni maana za kilungha yaani saumu ina maana ya ( kunyamaza, kujizuiya, kusimama.)

Ama neno hili kwa upande wa kisheria ni kujizuiya kila kina chofuturisha tangu kuchomoza kwa alfajiri ya kweli mpaka kuzama kwa juwa (loote) pamoja na kutia nia tangu usiku .

kujuzuiya na vinavo futurisha yaani kila vinavo haribu funga yako, kwa mfano maasi yoyote, kuywa au kula kwa maksudi, kuingiza kitu katika tundu zenye kufisha mpaka ndani , kufanya tendo la ndowa . Nk…

Unapaswa kujizuiya tangu adhana ya pili haijaadhiniwa mpaka juwa lizame lolote usiku hapo tena yafaa kula na kunywa na nk…..

Kutia nia tangu usiku ni sharti katika masharti ya funga sahihi bila ya kutia nia itakuwa funga yako baatili.

Kwa ufupi “funga imekuja ili itufunze uchamungu na kutupa afya na kuacha maasi maovu na kula na kunywa hata tendo la ndoa la halali.

 والله أعلم 

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Sheikh :- Nielezee funga za umma zilizopita; walikuwa wakifunga vipi❓

JAWABU 

Naam ❗
Qur-an tukufu imethibitisha kuwa umma zilizotutangulia walikuwa wakifunga … funga zao.. ..

Fungua Surat Baqarah. Aya 183

” ياأيها الذين ءامنوا كتب عليكم
الصيام كما كتب على الذين من قبلكم “

“Enyi mulioamini mumefaradhishiwa kufunga kama vile walivo faradhishiwa umma zilizotangulia “

– Namna na watu gani na idadi ndio tumetafautia na umma zilizopita na ktk hili kuna khilaafu baina maulamaa.

– Baadhi ya mapokezi yanasema kuwa mayahudi na manasara ndio waliofaradhishiwa kufunga, na mapokezi mengine yanasema ni umma zoote zilizopita.

– Walikuwa wakifunga siku 3 tu kwa mwezi na wa mwanzo kufunga Ramadhani ni Nabii Nuhi A. S.

Mapokezi mengine yanathibitisha kwamba kuwa manasaara walikuwa wakifunga Ramadhani lakini wakati wa juwa kali sana walikuwa hawaifungi Ramadhani bali walikuwa wakiichelewesha mpaka siku za usoni kisha huongeza siku 20 kwasababu ya kuchelewesha kwao huko .

– Na kabla kidogo ya kufaradhishwa funga hii ya Ramadhani … Walikuwa wakifunga sunna tu sio funga ya faradhi.

– Na wako waliosema kuwa walikuwa wakifunga saumu nyengine ya fardhi kisha ikafutwa funga Yao hio kwa Kuja funga ya ramadhani .

Ufupisho

– Umma zilizopita walikuwa wakifunga kwa uthibitisho wa Qur-an .

– Idadi na jinsi walivokuwa wakifunga ndio kuna khilaafu baina ya maulamaa

 والله أعلم 

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Sheikh :- Naomba unielezee funga imefaradhishwa lini❓

JAWABU: 

– Funga imefaradhishwa mwaka 2 baada ya kuhama Mtume wetu S.A.W. kutoka Makka kwenda Madinat Munawwara na baada ya kubadilishwa kibla kuelekea Al-Qabas.

– Na ilikuwa kufaradhishwa huko ni haramu kukutana kindoa na mkeo usiku wa Ramadhani.

Kisha hukmu hii ikafutwa pale Allah aliposema katika Surat Baqarah, Aya 187

” أحل لكم ليلة الصيام الرفث إلى نساءكم هن لباس لكم وأنتم لباس لهن”

” Mumehalalishiwa kwenu usiku wa funga (ya Ramadhani au nyengineo) kuingiliana na wake zenu kwani wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao.”

– Kufaradhishwa funga hii ni siku 30 au 29 nazo Allah amezitaje kuwa ni zenye kuhisabika pale aliposema
Katika Surat Baqarah, Aya ya 184 

“أياما معدودات ”  Ni siku zenye kuhisabika”

– Na Allah ametufurashia funga hii ktk mwezi wa Ramadhani tu na kutusaameh ktk miezi 11 iliyobakia.

– Na wengine akawatowa katika hukmu ya faradhi; Kama vile msafiri, mgonjwa, mpumbavu, mwenye kupata hedhi na nifasi na wengineo pamoja kuwa wanalipa wengine na Kutowa fidya katika hao ,,

والله أعلم 

 

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Sheikh mimi nauliza hivi ni nini hikma ya kufaradhishwa funga ❓

JAWABU 

– Bila Shaka funga ni ibada pekee yenye siri kubwa baina ya mja na mola wake, hebu njooni tuziangalie hizo hekma na utukufu wa kufunga.

1 – Kuitakasa nafsi na kuipa khofu na ulinzi mbele ya mola wake ili apate kuwa mcha mungu ..

Allahu Anasema katika Kitabu Chake kitukufu Surat Baqarah, Aya 183.

“. لعلكم تتقون “

” Ili tuweze kumuogopa Allah (kumcha Allah).”

2 – Funga ni Kinga ya maradhi na maovu ..

Naam❗ Funga iliyo kamilika Inamlinda na maradhi mbali mbali katika mwili wake na maradhi ya nafsi yake.

Amesema mtume wetu S.A.W. kuwa:

“” Yoyote yule Kama hakuacha kusema uongo basi Allah hana haja na kujihangaisha kwake na kukaa bila ya kula na kunywa “”

3 – Ni nusu ya subra ..

Naam funga iliyokuwa kuwa sahihi Inakujenga kuwa nasubra kama vile

– Kujizuiya na kula na kunywa na hata kukutana na mke wako wa halali.

– Kujizuiya na maovu na machafu kama, (uongo, kusengenya, kujibizana na maneno maaovu).

Amesema mtume wetu S.A.W.

 “الصِّيَام نصف الصبر” “Funga ni nusu ya subra “

4 – Funga ni Chuo pekee cha kuhurumiana, kusaidiana , kusamehana baina yetu ..

Naam ❗

Katika mwezi huu jinsi ya utukufu wake ni fursa ya pekee kwa waliokhasimiana kukaa wakasuluhisha na kusamehana yaliyopita na ni fursa vile vile ya kuwasaidia kihali na mali maskini na mafakiri..ili nawao wajisikie kuwa na furaha na upendo mbele ya wenzao wenye uwezo..

5⃣ – Funga ina kufundisha uwe Mwenye nidhaamu na kuwa sawa na wenzako ..

 – Ukiangalia wakati wa kufunga na kula ikiwa nchi ziko sawa pamoja katika ufungaji na kula basi utawaona woote wanakula na kufunga kwa muda maalum ..

– woote wanafunga mwezi wa Ramadhani kwa kuona mwezi na kula siku kuu kwa kuona mwezi…

– wooote wanaanza kufunga kwa kuanza alfajiri ya kweli na wanakula kwa kuzama kwa jua.

Hizi ndizo nidhamu za funga hii.

والله أعلم 

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Sheikh :- Mimi nauliza hivi.. ❓ ” Naomba nitajiwe Fadhila za funga Ramadhan ❗

JAWABU: 

✏️ Funga ya Ramadhani Ina fadhila kubwa sanaa jinsi ya utukufu wake na cheo chake.

Mtume wetu S.A.W. Amesema :-

” Lau mungekuwa munajuwa fadhila na utukufu uliopo katika mwezi huu basi mungetamani Ramadhini iwe mwaka “

– Na Allah kausifu mwezi huu kuwa ndani yake kumeteremshwa Qur-an na katika usiku wa laylatu qadri ambao ni bora kuliko miezi 1000 . Allah anasema ktk Surat Qadri, Aya ya 1

” إنَّا أنزلناه في ليلة القدر ” ..

“Halika ya sisi tume iteremsha (hio Qur-an) katika usiku wenye cheo kikubwa”..

– Funga na Qur-an zitakuja siku ya qiyama ili kumuombea aliyefunga na kuisoma Qur-an.

Imethibiti hadithi sahihi ambayo kaipokea Abdillah bin Amri kuwa Mtume S.A.W.

قال
 “الصيام والقران يشفعان للعبد يقول الصيام : أي رب منعته الطعام والشهوات بالنهار فشفعني فيه، ويقول القران :
⭐ منعته النوم بالليل فشفعني فيه فيشفعان”

” Funga na Qur-an zitamuombea (siku ya qiyama) mja, funga itasema kumuambia mola wake:

Hakika yangu nimemzuiya na kula na matamanio wakati wa mchana basi namuombea kwa hilo,

Na Qur-an nayo itasema:

Nimemnyima usingizi usiku basi namuombea kwa Hilo .. Hapo basi ataombewa ( atakubaliwa uombezi huo).

Na katika pepo kuna mlango maalum wa waliofunga unaitwa “Rayyan”

Kama ilivothibiti katika hadithi sahihi ambayo kaipokea Suhayl bin Saad:

” في الجنة ثمانية أبواب ، منها باب يسمى الريان لا يدخله إلا الصائمون “

” katika pepo kuna milango minane , katika hio minane kuna mlango mmoja unaitwa Rayyan ambao hawataingia humo ila waliofunga ( lillaah taalaa)

– Na mfungaji aliyekuwa na iman na kutaraji malipo yake basi Allah Taalaa Atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia nyuma.

Imethibiti hadithi sahihi kutoka kwa abuu huraira r.a kuwa mtume S.A.W. amesema:-

” من صام رمضان إيمانا واحتسابا غفر ما تقدم من ذنبه “

” Atakae funga Ramadhani kwa Imani safi (mbele ya Allah) na kutaraji kwake malipo basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia “

– Na mwezi huu unapoingia tu basi kwanza milango ya moto hufungwa na ikafunguliwa ya peponi na mashetani wakadhibitiwa kwa Kutiwa mbaroni ( vitimbi vyao )

Imethibiti hadithi sahihi ambayo kaipokea Abuu Hurayra R.A. kuwa Mtume wetu S.A.W. Amesema :-

” إذا دخل رمضان فتحت أبواب الجنة وغلّقت أبواب جهنم وسلسلت الشياطين “

“Unapoingia mwezi wa Ramadhani basi milango ya pepo hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na wakapigwa minyororo mashetani”

Naam ❗ Hizi ni miongoni tu za Fadhila za mwezi wa Ramadhani .

Allah atufikishe salama na kuifunga Ramadhan kwa iman na matarajio.

Amin yaa Rabiynaa..

والله أعلم 

 

Published By Said Al Habsy

007: Naomba unielezee aina za funga za ulazima ❓

SWALI:

Sheikh – Naomba unielezee aina za funga za ulazima ❓ 

JAWABU:

– Funga ziko aina nyingi kwa kuja kwa matokeo tofauti na huja kwa hukmu tofouti. Nazo ni kama hizi:~

1⃣ – (“funga ya nadhiri”)

Hii ni ile anayojilazima binaadamu mwenyewe,

Kwa mfano atakaposema :- ” Naweka nadhiri nikifanikiwa kupata kitu flani basi nitafunga mwezi au mwezi flani”

– Hukmu ya nadhiri hii kuwa atalazimika kuitekeleza funga hii

– Dalili yake :-

Imethibiti kuwa mwanamke alisema kumwambia mtume wetu S.A.W. :~

” Ewe mjumbe wa allah hakika ya mama yangu kafa na anadaiwa funga ya nadhiri, je nimfungie❓

Mtume S.A.W. akasema:~ ” Je waonaje ingekuwa mama yako anadeni si ungelilipa lile deni lake❓

Akasema Yule mwanamke ” ndio ” basi mtume S.A.W. akamwambia aifunge saumu ile (ya nadhiri).

2 – ( funga ya tamatui)

Funga hii ni kwa Yule aliye fanya kuinganisha Hija yake na umra kisha asiweze kutekeleza ibada ya kuchinja mtu huyu atapaswa kufunga siku 10; 3 atazifunga akiwa ktk ibada ya Hija na 7 atazifunga pindi akirudi nyumbani kwake.

– Dalili yake, Allah Anasema katika Surat Baqarah, Aya 196.

” فصيام ثلاثة أيام في الحج وسبعة إذا رجعتم ”   Atafunga siku 3 akiwa katika ibada za hija na 7 atazifunga atakaporudi (nyumbani)

3 – (Funga ya kafara)

Hii ni funga ya kulipa kafara pindi ikitokezea kauwa au kumsema mkewe ( kuwa Kama mgongo wa mama yangu, dhihaari) au kafara ya kuaapa kisha asitekeleze kiapo chake .

Na hii huja baada ya kushindikana kutekeleza kuacha mtumwa huru.

Allah Anasema katika Surat An – Nisaai, Aya 92, katika kafara ya kuuwa kwa bahati mbaya tu.

” فمن لم يجد فصيام شهرين متتابعين توبة من الله “

Na katika kafara ya kumrejea mke baada ya kumwita (dhihaar), kama mgongo wa mama yangu, katika Surat Mujaadala, Aya ya 4

” فمن لم يجد فصيام شهرين متتابعين من قبل أن يتماسا “

“Basi asiyeweza kuacha huru mtumwa basi atapaswa kufunga miezi 2 mfufulizo kabla ya kumgusa (kumuingilia mkewe)

Kwa ufupi 

– Funga za ulazima ni funga ya Ramadhani, funga ya kuweka nadhiri, funga ya kutowa kafara na funga ya tamatui.

و الله اعلم

Published By Said Al Habsy

SWALI:

بسم الله الرحمن الرحيم

السلام عليكم ورحمة الله و بركاته

Sheikh – Afanye nini alikuwa kaacha funga ramadhani hali ya kuwa mjamzito na akachelewa kufunga mpaka ikamfikia ramadhani nyingne❓

JAWABU 

Ikiwa ameacha kufunga ramadhani kwa hali ngumu ya ujauzito na ikamchelewesha mpaka kumfikia ramadhani nyingne basi hakuna tatizo muhimu azilipe funga zake zote alizoziacha nyuma.

Lakini ikiwa amechelewesha bila ya sababu yoyote ya msingi mpaka kumfikia ramadhani nyingine basi yampasa atoe kafara.

و الله اعلم 

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shekh :- ” Naomba unielezee aina za funga za sunna.”

JAWABU: 

Naam!.

Kuna funga ambazo zimekuja kutuhimiza na kuturaghibisha na kujipendekesha kwa allah wala hakuna ulazima wa kufunga ila kuna Fadhila kubwa zinapatika kwa mwenye kufunga.
Nazo ni :-

1 )-( ayyamu baydhi)

– funga hii maana yake ni masiku matatatu meupee kwani mwezi wakati huo unakuwa unangaaza zaid nazo ni mwezi 13,14 na 15 kila mwezi wa kiislamu.

– Dalili yake:- kutoka kwa abiy hurayra r.a amesema: ” ameniusia alkhaliliyli ( mtume s.a.w) juu ya mambo matatu kufunga siku 3 kila mwezi, na rakaa mbili za dhuhaa na kusali witri kabla sijalala “

Na funga hii fadhila zake Kama umefunga mwezi mzimaa.

2 – ( A’shuraa)
-funga hii asili yake ilikuwa mayahudi ndio walikuwa wakiifunga wakati wa jaahiliya alipokwenda mtume wetu s.a.w Madina akawamrisha masahaba wake waifunge funga hii .

– na utaratibu wa kufunga hii kiusahihi zaid kuwa mayahudi wao walikuwa wakiifunga mwezi 9 mtume s.a.w akaturisha tuwakhaalifu ( twende nao kinyuma) yaani tufunge siku moja kabla ya 9 yaani tufunge 8na 9. Au tufunge siku moja mbele yake yaani 9na 10 ili tuonyeshe kuwa sisi tumetafautiana nao.

– Dalili ya maneno hayo ni aliposema mtume wetu s.a.w  ” صوموا يوم عاشوراء وخالفوا اليهود وصوموا يوما قبله أو يوما بعده “
” fungeni siku ya a’shuraa ,na kuwenikinyume nao ,na fungeni siku moja kabla ya hio funga Yao ( mwezi 9) au fungeni siku moja baada ya funga Yao ” 

– fadhila zake
Amesema mtume wetu s.a.w kuwa
“من صام عاشوراء كان كفارة لستين شهرا وعتق عشر رقبات مؤمنات من ولد إسماعيل”
” atakae funga ya A’shuraa itakuwa ndio kafara yake (ya kufutiwa madhambi ) yake miezi 60 na kama kawaacha huru watumwa waumini kumi ktk kizazi cha nabii ismaili a.s””

3 – ( Arafa)

–  Siku ya Afara ni nguzo kubwa ambayo mahujaaj woote wanamiminika ktk mlima huo wa arafa.

–  Na funga ya arafa ambyo ni mwezi 9 imethibiti uhakika wa funga hio kwa wale tu walikuwa hawapo ktk Kiwanja hicho Ama kwa mahujaaj sio vzr kufunga siku hio kwa vile watadhaufika ktk ibada zao
Na ktk hili kuna khilaafu.

– Fadhila ya funga hii kuwa imethibiti dalili sahihi kuwa mtume s.a.w anasema:-
” صوم يوم عرفة كفارة سنتين.”
” funga ya siku ya arafa ni kafara( ya kusamehewa) miaka mwili( mmoja uliopita na wapili ujao)”

Tanbihi muhimu

Siku ya Arafa Kama ilivothibiti kuwa ni mwezi 9 na sisi tunafunga kwaajili ya kupata fadhila hizo inshaallah ..hatufungi kwasababu wao mahujaj ndio siku ile wamesimama kwasababu tarehe za miandamo zinatafautiana wako wengine siku hio kwao ni mwezi 8 kwa mujibu wa muandamo wao, kwa hivyo wao watapaswa waifunge siku ya pili yake.

Na wako wengine wakati huo mahujaaj wamesimama wao ni usiku vp watafunga??na hakuna funga usiku kwa hivyo moja kwa moja kila nchi itaangalia kwa mujibu wa muandamo wake Kama vile ungiaji wa sala na kutoka kila mji unawakati wake Allah anasema ktk Surat baqarah aya 189

” يسؤلونك عن الأهلة قل هي مواقيت للناس والحج”
“Wanakuuliza kuhusu miezi ( mabadiliko yake ) sema hio ndio nyakati za watu na ( nyakati) za hija”

– Na ktk hili kuna khilaafu kwa wenzetu na isiwe ndio uwanja wa kudharauliyana na kukufurishana na kutuhimiyana baina yetu.. Bali iwe ni uwanja wa kuelimishana kihoja tu.

والله أعلم

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shekh: – nakuomba unimalizie funga za sunna ?

JAWABU:

Naam – Ni muendelezo wa kutaja Sunna za kufunga na tunamaliza kutaja sunna hizo za kufunga.

4 – ( sifa za shawaal)
Funga 6 za shawali ni zile zinazokuja baada ya funga ya ramadhani kumalizika na sikukuu ya kwanza.. Hapa tena unakhiyari kwako kufunga mwanzo wake au katikati au mwishoni .

– Dalili ya kuthibiti funga hii ni :-
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:” من صام رمضان ثم أتبعه ستا من شوال فذالك صيام الدهر “
” atakae funga ramadhani Kisha akafuatiza na kufunga siku 6 za shawaal basi hio nikama kafunga mwaka “

5 – (siku 9 dhiyl-hija)
Funga hii huwa inakuja pindi Tu inapiingia dhul-hija ila siku ya sikuu ni haramu kufunga na Fadhila zake ni kubwa Kama ilivothibiti ktk hadithi sahihi

” ما من أيام العمل الصالح أحب إلى الله فيها من هذه الايام ، قالوا ولا الجهاد في سبيل الله ؟
قال إلا من خرج بنفسه وماله ثم لم يرجع”

” hakuna masiku matendo memo yakawayanapendwa zaid mbele ya allah Kama masiku haya, masahaba wakamuulizA mtume s.a.w hata jihaadi ktk njia ya allah? Mtume s.a.w akasema rabda mtu katoka yeye na nafsi yake na mali yake kisha asirejee tena “

والله أعلم

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shekh :- “nitajiwe sababu za kuthibiti kufunga mwezi wa ramadhani “

– huwezi kujitia kufunga kivyako vyako tu ila kuna sababu moja katika hizo zikikuthibitikia basi hapo sheria inakutaka ufunge sababu wenyewe ni :-

1⃣)- kuonekana kwa mwezi
2⃣)- kuenea kwa khabari.
3⃣)- kukamilisha siku 30 za mwezi wa shaabani.

UFAFANUZI:-

Kuonekana kwamwezi

Imethibiti ktk Surat baqarah aya ” فمن شهد منكم الشهر فليصمه ”  “atakaeushuhudiya mwezi katiyenu ( na akawepo ktk mji wake) basi na aufunge”
Na ktk hadithi sahihi mtume s.a.w anasema ;-  ” لا تصوموا حتى تروا الهلال ولا تفطروا حتى تروه فإن غم عليكم فأكملوا العدة ثلاثين يوما ” 
” musifunge mpaka muuone mwezi na musile (skukuu) mpaka muuone huo ( mwezi) , nakama mukizibiwa na mawingu (mukautafuta musiuwonee) basi kamilisheni idadi ya siku 30 za ( shaabani)

Naam!
Dalili hizi ziko wazi kabisa kuwa funga inaambatana na kuonekana kwa mwezi na usichokore chokore ukatafuta mwezi wa nchi nyengine na Hali hadithi mwisho iko wazi kabiza

فإن غم عليكم”   “mukizingwa na mawingu kwenu” hii yaonesha wazi ima tutauona au tusiuwone bila kudapiya miezi ya watu na kama ilivothibiti ktkhadithi ya ibni abaas r.a kuwa amesema mtume s.a.w anasema :-
“” أن لكل قوم هلالهم ”  “Kila watu ( wa miji) wana mwezi wao””

Kukamilisha siku 30.

Pindi ikishindikana baada ya kuuwangaliya mwezi vzr na mwisho wa mambo tukaambiwa kuwa mwezi haujaonekana hapo basi utapaswa kukamilisha siku 30 za mwezi wa shaabani usiwe naharaka na kudapiya miezi ya watu. Imethibiti ktk hadithi ya nyuma kwamba “فإن غم عليكم فأكملوا العدة ثلاثين من شعبان”  “Mukizingwa na mawingu basi kamilisheni siku 30 za shaabani”

Kupata khabari.

Haiwezekani ikawa sooooote ndio tumeuona mwezi … Inaweza kutokezea baada ya muda flani tukapata khabari kwa mtu flani au watu flani kuwa wao wameuona mwezi ktk kijiji flani mudaa kadhaa

Na ktk hili kuna shuruuti ili tumkubali huyo Jamaa aliyeuona mwezi :-nazo ni
1)- mwenye akili
2)- kabaleghe
3)- mwanamme
4)- muaminifu ktk Dini yake
5)- na shahada yake hio isijekuwa kinyume na anayosema.

Imethibiti ktk hadithi sahihi iliyopokewa na ibni abaas r.a kuwa “” alikuja bedwi mmoja huku akisema ewe mjumbe wa allah hakika yangu Mimi nimeuona mwezi mtume s.a.w akamuuliza jee unashihudiya kuwepo kwa Allah kuwa yeye ni mmoja ?? Na mm ni mjumbe wake ?? Akasema ndio
Basi hapo mtume s.a.w akamuamrisha bilaal awatangazie watu kesho wafunge”
Hii kuonesha sababu Kama hii unaweza kuitumia kwa kuthibiti kwa kuingiza kwa mwezi lkn kwa masharti.

والله أعلم

Published By Said Al Habsy

SWALI:

shekh, ” naomba ufafanuzi wa “Muandamo wa mwezi wa ramadhani”

JAWABU:

Naam!..
– tuelewe kuwa “kufunga na kula “kunaambatana moja kwa moja na kuonekana kwa mwezi Mtume wetu s.a.w. Ametuelekeza nini tufanye anasema:

”  صموا لرؤيته وأفطروا لرؤيته “..
“Fungeni kwa kuona kwake huo ( mwezi) na kuleni kwa kuonekana kwake huo( mwezi).
Na hadithi zimekuja kwa njia tofauti na matamshi mingi lkn yoote yanalenga kuwa tuuwangalie mwezi ktk Hali mbili hizi..

– na kuonekana kwa mwezi kunatafautiana kwa mujibu ya utafauti wa miji yetu ktk kuchomoza kwa juwa na kuzama kwake..

Kutokana na namantiqi hio huwezi kabisa kulinganisha kuonekana pahala flani ikaweza kuathiri mji mwengine wa mbali .kama vile ibada ya sala
Sala ya adhuhuri inathibiti kwa kutenguka kidogo juwa au sala ya maghrib inaingia na kuthibiti kwa kuzama kwa juwa lote.
Kwa hivyo huwezi kulinganisha kabisa ukasema kuwa ikiingia adhuhuri zanzibari kwa mfano ndio walioko marekanani au india au suidia na wao wasali sala ya adhuhuri !! 
Hii haingii akilini kabisa kwani wao wanamuda wao wa machomozo ya juwa na kuzama kwake ..
Pesa ya oman huwezi kabisa ukaitumia vile vile ilivo ukanunuwa nazi soko la Chake pemba lazima utaichenji kwanza ndio uitumie kwa pesa iliyopo pale tanzania.

–  na madai ya baadhi ya watu kusema kuwa nchi flani kwa mfano suudia ndio inafuatwa kwa vile inazingatiwa ndio chimbuko la uislamu pindi ukionekana mwezi suudia ndio dunia nzima wafunge madai haya sio sahihi kabisa .
Uislamu unafuatwa popote utakapukuwepo wewe sheria hazikubatanishwa na nchi ya suudia.

Kitu cha kujiiliza sasa ni hichi:-
Wale waliopo katika nchi zao mchana na wale waliopo usiku vp watafunga
Na funga inaanza kwa kuchoma alfajiri na mwisho wake ni kuzama kwa juwa ?

–  dalili tosha ya kuonyesha kuwa kila mji una muandamo wake ni ile hadithi mashhuri kwetu sote. ( hadithi ya kureybu)

Ambapo ABDALLAH ibni abbasi r.a ali ukatakataa kata mwezi aliouona kureyb pindi alipokuwa shamu kikazi na

Kureyb akashaangaa huku akimuiza
” أو ما تكتفي برؤية معاوية وصيامه “
” Jee hutosheki wewe na mwezi aliyouwona muaawiya na kufunga kwake ” !!?

Abdallah bin abaas r.a akamjibu :-
” لا هكذا أمرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم “
” laa (sitotosheka na hayo) hivi ndivo alivotuamrisha mtume wetu s.a.w )

Hii hadithi iko wazi kabisa kuwa ibni abaas kaukataa mwezi ulioindama sham na Hali yakuwa madina na shamu ni karibu vip iwe miji ya mbali Sanaa isende Kama alivokwenda abdallah ibni abaas . Na kwanini abdallah ibni abaas r.a asifuate mwezi wa muaawiya??

Na ktk fani za hadithi pindi sahaba akisema
“أمرنا / نهيناعن كذا /كنّا نعمل.
” ametuamrisha /ametukataza na kitu flani/ tulikuwa tukifanya.
Hizi huzingatiwa kuwa hukmu yake ni inapandishwa moja kwa moja kwa mtume s.a.w .

والله أعلم 

Tanbihi muhimu:-
1 – Nas-ala haya kuna khilaafu baina ya ndungu zetu nawawo kwetu wana nia safi kwetu kwa ufahamu wao mwengine wa hizi hoja.

2 – Tofauti zetu hizi isiwe ndio firimbi ya kutangaza uaduwi na chuki na ukhasama baina yetu Bali iwe ni uwanja wa kupeana hoja kwa hoja .

3 – Wako wenzetu -allah atuongoze sisi na wao- wanaufarikisha umma na kutukanana na kudharau wenzao kwa sababu hii Tu ya ” kutafautiana kufunga”

4 – Hii isiwe ndio sababu ya kuwa hivo bali tuzidi kupendana na kushikamanana japo tumetafautiana.

والله أعلم

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shekh, Naomba unitatajie aina ya makundi walioruhusiwa kula mchana! ?.

JAWABU:

Naam hakika miongoni mwa rehma zake Allah na uepesi wa Dini Hii ni kuwa Allah hawakuwalazimisha waja waje wake woote kufunga ,kwani wako wenye dhuruugu nzito au wengine itawasababishia funga kuwapa matatizo katika afya zao .

Allah anasema ktk surat baqarah aya 185

“يريد الله بكم اليسر ولا يريد بكم العسر ” “Anakutakieni Allah kwenu uwepesi wala hakutakieni uzito “

Naam❗
Maulamaa wamewagawa watu hawa ktk makundi manne makuu nayo :–

1⃣- Wanaolazimika kulipa tu ( funga)

2 – Wanaolazimika Kutowa kafara bila kulipa au kufunga

3 – Wanaolazimika Kutowa kafara na kulipa

4 – Wasiolazimika kulipa na Kutowa kafara wala kufunga

– Inshaallah tutataja kila kundi mifano yake na ikiwezekana kutoka dalilis 


والله أعلم

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shekh :- Nakuomba unitajie shuruti za funga❗❓

JAWABU:

Ibada yoyote bila kutambuwa masharti yake huwezi kuifanya kiusahihi daima utakuwa wadapiya gari tu bila kujuwa wapi unakwenda..

Na leo biidhnilaah tutamalizia na sharti la pili :-

2 – KUJIZUIYA NA VIFUTURUSHAJ TANGU KUCHOMOZA KWA AlFAJIRI MPAKA KUZAMA KWA JUA KWA NIA

-Kujizuiya na vifuturishaji ambazo vinaharibu funga yako

Navo viko aina 4 kuu

1 – kuingiza kitu kutoka njee kuiingia ndani

Kama vile kuingiza chakula au kinywaji au kupitia ktk tundu za macho au mdomo au kupigwa sindano yenye chakula.

2 – Kutowa kitu kutoka ndani kwenda injee.

Kama matapishi kwa maksudi au kujitowa manii.

3 – Tendo la ndowa mchana wa ramadhani.

4 -Kutenda maasi

Kama vile kusengenya, kusema uongo na mfano wake .

Amesema mtume wetu s.aw. ” ولا صوم إلا بالكف عن محارم الله “

” wala hakuna funga mpaka ujizuiye na Yale aliyeyaharamisha Allah “

Tangu kuchomoza kwa juwa mpaka kuzama :-

– na hii ili tuwe mbali na mayahudi na manasara Kwani wao wanafunga baada ya sala ya isha .

– Sisi Allah katutaka tufunge tangu juwa la kweli lachomoza (kabla ya adhana ya pili )

Allah anasema ktk Surat baqarah aya 187

” وكُلُوا واشربوا حتى يتبين لكم الخيط الأبيض من الخيط الأسود من الفجر “

” kuleni na kunyweni mpaka ikubainikien kwenu uweupe wa alfajiri ktk weusi wa usiku “

Pamoja na kutia nia.
Naam ibada yoyote ile inasimamiwa na nia kabla yake.

Amesema mtume wetu s.aw. :-

“إنما الاعمال بالنيات “

” hakika ya matendo hutanguliwa na nia “

والله أعلم

 

Published By Said Al Habsy

SWALI.

Shekh, ” naomba unitajiye watu ambao wanaolazimika kula na kulisha maskini ❗”


JAWABU.


بِسْم الله الرحمن الرحيم


– Watu ambao wanao lazimika kula mchana na Kisha kulipa ni :-


– Mgonjwa ambae ugonjwa wake ni wenye kuendelea –  yaani mgonjwa ambaye hawezi kabisa kufunga wala hakuna matarajio ya kupona ugonjwa wake ❗

– Mtu mzima sanaa – Amekusudiwa hapa ni babu ambaye ni mtu mzima sanaa na hajiwezi au Bibi ambaye ni mtu mzima Sanaa na hajiwezi ..

Hukmu ya watu hawa wawili :-

– Watalazimika kula mchana na kulisha kila siku nusu pishi au watamlisha kila siku maskini mmoja kwa mlo mmoja basi ( mlo wa mchana)

– Dalili yake
Fungua Surat baqarah aya 184 …

” وعلى الذين يطيقونه فدية طعام مسكين “

Neno “” يطيقونه”
Ibni Abaasi r.a amelitafsiri kuwa “” wanapata shida na dhiki “”

– Maana ya aya :-
” Nawale wanaopata shida ( ktk kufunga huko) basi watatowa fidya ya kulisha maskini “

– Qauli hii ndio yenye kutegemewa ktk fatwa za mashekhe wawili watukufu ( Shekh Khalili na Sheikh Qannubi) Allah awahifadhi ..

Tanbihaat

– Hukmu ya kupewa wao (Hao wawili mgonjwa wenye kudumu na mtu mzima) ni vile kuenekana kwao na aghlab ya dhanna ,
Lakini watakapopata na afya njema siku za usoni hukmu hio itaondoka .

– Utaratibu au jinsi ya kutowa fidya ni hivi Kama ifuatavo ;:-

Unaweza kumlisha maskini mmoja Tu huyo huyo kwa kila siku 29 au 30.

Na vile inajuzu kwako kulisha maskini 29 au 30 kwa mpigo.

Huwezi kulisha maskini kabla ya ramadhani kuingia, asli ni kumlisha kwa kumpa chakula lakini hakuna tatizo kama ukampa thamani yaani pesa ikiwa hakuna wa kuku ali chakula.

Nusu pishi imeqadiriwa kuwa ni kilo mmoja na gram 20 na atakae ongeza zaid ya hapo Allah atamuongezea .

والله أعلم

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shekh , ” Naomba unitajiye watu ambao wanaolazimika kulipa na kutowa kaffara “❓

JAWABU. 

بِسْم الله الرحمن الرحيم

Naam❗.

– Watu ambao watakaopaswa kulipa na kutowa kaffara ni :-

 1. Mpuzaji wakutokulipa ramadhani iliyopita bila sababu.

Hukmu yake :-
Mtu Kama huyu ambaye imeingia ramadhani nyengine bila kulipa deni la nyuma hukmu yake ni:-

Atatubia kwa kupuuza kwake wajibu wa kufunga

– atalipa funga alizoziacha zoote.

– atalisha kila siku maskini siku aliyeipoteza.

2 – Mwenye kuasi na kuvuka mipaka.

– mwenye kuasi hapa amekusudiwa Yule ambaye aliyekwenda kinyume na sheria za funga au akavunja nguzo au shart la funga❗

– Kwa mfano :-

❗Mwenye kula au kunywa maksudi.

❗Mwenye kufanya tendo la ndowa mchana.

❗ Mwenye kujitowa Nanii kwa njia yoyote ile .

Hukmu Yao :-
– Kutubia na kuomba msamaha.

– Kulipa funga ya siku hio aliyofanya kosa hilo.

– Atatowa kafara nzito (kaffara mughaladha) nayo ni hivi :-

Kuacha mtumwa huru, kama hakumpata basi atafunga miezi 2 mfufulizo. 

Kama ha kuweza basi..

– Atalisha maskini 60
..
والله أعلم

 

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Shekh , Naomba unitajiye watu ambao hawalazimiki kufunga wala kulipa wala kutowa kaffara”❓

JAWABU. 
بِسْم الله الرحمن الرحيم

Naam❗.

✒Watu ambao watakaopaswa kulipa na kutowa kaffara ni :-

1. “Mpuzaji wakutokulipa ramadhani iliyopita bila sababu”

-Hukmu yake, Mtu Kama huyu ambaye imeingia ramadhani nyengine bila kulipa deni la nyuma hukmu yake ni atatubia kwa kupuuza kwake wajibu wa kufunga

– Atalipa funga alizoziacha zoote.

– Atalisha kila siku maskini siku aliyeipoteza

2 – Mwenye kuasi na kuvuka mipaka “

✏️ mwenye kuasi hapa amekusudiwa Yule ambaye aliyekwenda kinyume na sheria za funga au akavunja nguzo au shart la funga❗

Kwa mfano :-

❗Mwenye kula au kunywa maksudi.

❗Mwenye kufanya tendo la ndowa mchana.

❗ Mwenye kujitowa Nanii kwa njia yoyote ile .

Hukmu Yao ni – KUtubia na kuomba msamaha.

 

Published By Said Al Habsy

SWALI

Shekh, naomba unitajiye mambo yasiyoharibu au kutengua funga❓

JAWABU

بِسْم الله الرحمن الرحيم

Naam❗..

Utangulizi.

– Kutokana na uepesi wa dini yetu kuna mambo unaweza kuyafanya bila kuharibika funga yako Kama vile :-

1 – “” kuoga “”

Inajuzu kuoga kwa mwenye kufunga ikiwa asubuhi au mchana au jioni muhimu tu Achukuwe hadhari kutoingia kitu ndani .

2 – “kutia wanja na manukato “”
 Kuunusa harufu za udi au mafuta mazuri haiharibu funga Ila unapaswa usiwe karibu sana na huo udi ili isijekuingia harufu tumboni.

3 – “” kumeza mate””