Home Projects

Projects

UTANGULIZI:

Kutenda wema ni miongoni mwa mambo ya wajibu ambayo yanamlazimu kila Muislamu kwa mujibu wa uwezo wake, na bila ya shaka wema huo atakaoufanya mtu kuwafanyia waja na viumbe wengine ni hakiba njema, na ni hazina ya pekee atakayonufaika nayo yeye kabla ya wengine ndani ya maisha haya ya duniani, huku akisubiria ujira maradaufu katika maisha ya akhera; kwani katu Allah hapotezi ujira wa wanao fanya wema. Anasema Allah mtukufu:

{لِّلَّذِینَ أَحۡسَنُوا۟ ٱلۡحُسۡنَىٰ وَزِیَادَةࣱۖ}

{Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi}.

Na pia anasema:

{وَأَنفِقُوا۟ فِی سَبِیلِ ٱللَّهِ وَلَا تُلۡقُوا۟ بِأَیۡدِیكُمۡ إِلَى ٱلتَّهۡلُكَةِ وَأَحۡسِنُوۤا۟ۚ إِنَّ ٱللَّهَ یُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِینَ}.

{Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema}.

Miongoni mwa mambo ambayo kuyafanya kwake ni katika wema ni mtu kutoa mali yake kwaajili ya kuwasaidia wasio jiweza, wakiwemo masikini, mafukara, mayatima, n.k.

Anasema Allah mtukufu:

{ یَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَا یُنفِقُونَۖ قُلۡ مَاۤ أَنفَقۡتُم مِّنۡ خَیۡرࣲ فَلِلۡوَ ٰ⁠لِدَیۡنِ وَٱلۡأَقۡرَبِینَ وَٱلۡیَتَـٰمَىٰ وَٱلۡمَسَـٰكِینِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِیلِۗ وَمَا تَفۡعَلُوا۟ مِنۡ خَیۡرࣲ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِیمࣱ }.

{Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua}.

Bila ya kusahau kua bora ya sadaka ni ile iliyotolewa katika njia ya Allah, tena athari yake ikawa inaurudia umma mzima, au wanaonufaika nayo ni idadi kubwa ya watu. Na miongoni mwa sadaka hizo ni kujenga nyumba za Allah, madrasa, vituo vya kuwatunza mayatima, visima, pamoja na kuvindeleza vitu kama hivyo kwa kuvishuhulikia ili visianguke. Kufanya hivyo ni katika sadaka yenye kuendelea, tena ujira wake ni kama mtu aliepanda chembe moja, ikisha ikachipua mashuke saba, ndani ya kila shuke zikawemo chembe mia moja, tena ujiri huo hausitii katika idadi hiyo, bali Allah anamuongeza maradufu amtakae, kama alivyoeleza kwa kusema:

{مَّثَلُ ٱلَّذِینَ یُنفِقُونَ أَمۡوَ ٰ⁠لَهُمۡ فِی سَبِیلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتۡ سَبۡعَ سَنَابِلَ فِی كُلِّ سُنۢبُلَةࣲ مِّا۟ئَةُ حَبَّةࣲۗ وَٱللَّهُ یُضَـٰعِفُ لِمَن یَشَاۤءُۚ وَٱللَّهُ وَ ٰ⁠سِعٌ عَلِیمٌ}

{Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua}.

Na kwaajili ya kuonyesha uzito wa ujira wa sadaka ndiyo Allah ameeleza kua mtu anapokufa akafunguliwa kuyaona yale aliyokua hayaoni kabla basi jambo la mwanzo atakalo tamani kurejeshwa duniani kwaajili ya kilifanya ni kutoa sadaka. Anasema Allah mtukufu:

{وَأَنفِقُوا۟ مِن مَّا رَزَقۡنَـٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن یَأۡتِیَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَیَقُولَ رَبِّ لَوۡلَاۤ أَخَّرۡتَنِیۤ إِلَىٰۤ أَجَلࣲ قَرِیبࣲ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِینَ}

{Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema?}.

Na ikiwa kutoa sadaka ni katika wema ambao mtu atatamani lau arudishwe duniani ili aufanye, basi pia kuwahamasiha wengine katika kuufanya wema huo pia ni jambo jema, bali ni moja kati ya sifa za Waumini wa kweli ambao wataokoka kutokana na khasara kubwa siku ya Qiyama. Kama alivyosema Allah mtukufu:

{إِلَّا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَتَوَاصَوۡا۟ بِٱلۡحَقِّ وَتَوَاصَوۡا۟ بِٱلصَّبۡرِ}.

{Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri}.

Na pia akasema:

{وَتَعَاوَنُوا۟ عَلَى ٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُوا۟ عَلَى ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَ ٰ⁠نِۚ}.

{Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui}.

Na bila ya shaka taasisi hii inakusaidia wewe na kukuwepesishia njia ya kuwafikia hao wanaostahiki kufanyiwa wema, na mchango wako ukafika katika hali ya usalama na uaminifu. Basi ni jambo jema kusimama nayo na kuiunga mkono kwa hali na mali.

 

MAMBO TUNAYO HUSIKA NAYO:

(i) Tunajenga na kuendesha na kusimamia vituo vya watoto mayatima.

(ii) Tunajenga Misikiti, Madrasa, pamoja na kufungua vituo vyenginevyo vinavyo hudumia Uislamu.

(iii) Ujenzi wa visima.

BISMILLAH RAHMAN RAHIM

Miradi iliyotekelezwa na Taasisi ya Al Rawdha Association Nchini Tanzania chini ya usimamizi wa Sheikh Said Al habsi.

  1. Ujenzi wa Msikiti
  2. Ujenzi wa Madrasa
  3. Uchimbaji wa Visima vya Maji safi
  4. Ugawaji wa Iftar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani
  5. Ugawaji wa Nyama kwa wahitaji Eid a dha

1. Ujenzi wa Msikiti

Masjid Al Firdaus Nakafuru Ifakara.

Taasisi ya Al rawdha association imejenga msikiti Afrika katika nchi ya Tanzania Mkoa wa Morogoro wilaya ya Kilombero-Ifakara. Msikiti huu umejengwa katika kata ya kibaoni kitongoji cha Nakafuru. Kutokana na hitajio la Msikiti katika eneo hilo Taasisi ilipokea maombi toka kwa waumini wa eneo hilo na Kuanza utekelezaji wa Ujenzi wa Msikiti huu Mnamo 25/05/2020na Kukamilika 04/02/2021

Eneo la Kiwanja cha Msikiti ni mita za Mraba 2450. Msikiti una ukubwa wa Mita 10 upana na urefu Mita 20. Pia msikiti una vyoo 9 ambapo 7 kwa waunaume na viwili kwa wanawake Pia kuna choo kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum (disabled people) Pamoja na chumba kimoja cha stoo.

Msikiti unauwezo wa kuingia waumini 400 kwa eneo la ndani na veranda za nje waumini 50 jumla msikiti unauwezo wa kuswaliwa na waumini 450.

Siku ya kwanza ya Ujenzi wa Masjid Al Firdaus Nakafuru. Uzinduzi ulifanyika kwa Dua

2. Ujenzi wa Madrasa.

Madrasatul Aisha Khair

Taasisi ya Al Rawdhwa pia ilipokea maombi ya Ujenzi wa Madrasa katika Mji wa Ifakara Morogoro Tanzania. Waumini wa Eneo la Kapolo lililopo katika Mji wa Ifakara Morogoro walituma ombi lao la uhitaji wa chumba cha Madrasa kwani katia eneo hilo hapakuwa kabisa na madrasa hivyo vijana na watu wazima walikua wamekosa kabisa kupata elimu ya dini kutokana na changamoto ya madrasa Hivyo Taasisi ya Al Rawdha ilipokea ombi hilo na kuanza ujenzi wa Madrasa ya vyumba viwili na ofisi ya sheikh sambamba  na vyoo viwili na mnara wa maji.

Vyumba vya madrasa viwili kila kimoja kina ukubwa wa mita 7 kwa 4.5 na ofisi ya sheikh ina ukubwa wa Mita 2.5 kwa mita 4.5. Madrasa hii ina uwezo wa kuchukua vijana 150 wanaosomea katika vyumba viwili. Ujenzi ulianza tarehe 04/11/2021 na kukamilika tarhe 04/03/2022.

3. Uchimbaji wa visima vya Maji safi

Taasisi ya Al Rawdha Association kupitia tawi lake la Thuraiya wells foundation imekua ikifanya shughuli za kuwapatia maji safi na salama wananchi wa Africa na kwengineko. Kwa sasa Thuraiya wells foundation imekua ikichimba visima katika Wilaya ya Kilombero Ifakara  Morogoro Tanzania.

4. Ugawaji wa Futari Mwezi Mtuklufu wa Ramadhan

@Instagram