Home MASWALI YALIOULIZWA KUHUSU IBADHI.COM

MASWALI YALIOULIZWA KUHUSU IBADHI.COM

Published By Said Al Habsy

1. Ni Nani Mdhamini / Mwanzilishi Wa IBADHI.com
IBADHI.com ni tovuti huru unaofundisha uislam kupitia chuo cha madhehebu ya kiibadhi kilichojengeka katika msingi wa haki kwa dalili, hata hivyo tunapokea maoni na ushauri kutoka kwa watu mbali mbali bila kuangalia madhehebu zao, au nchi zao.

Madhumuni yetu ni kufundisha dini kwa misingi ya elimu na makubaliano ya haki na dalili, nayo ndiyo njia ya wazi kwa kila anaetaka kuufahamu uibadhi.

Published By Said Al Habsy

1. Ni Nani Mdhamini / Mwanzilishi Wa IBADHI.com
IBADHI.com ni tovuti huru unaofundisha uislam kupitia chuo cha madhehebu ya kiibadhi kilichojengeka katika msingi wa haki kwa dalili, hata hivyo tunapokea maoni na ushauri kutoka kwa watu mbali mbali bila kuangalia madhehebu zao, au nchi zao.

Madhumuni yetu ni kufundisha dini kwa misingi ya elimu na makubaliano ya haki na dalili, nayo ndiyo njia ya wazi kwa kila anaetaka kuufahamu uibadhi.

Published By Said Al Habsy

2. Je! IBADHI.com imefadhiliwa za shirika lolote?
Suali.

Je! IBADHI.com imefadhiliwa za shirika lolote?

Jawabu.

Hapana, bali kazi zote zilizomo katika IBADHI.com ni za hiari za kujitolea, gharama zote ni zakujitolea wenyewe.

Published By Said Al Habsy

3. Vipi nitaweza kujitolea na Kuuendeleza IBADHI.com ?
Kama utapenda kusaidia basi tuandikie kwa email hii info@ibadhi.com tutawasiliana na wewe.

Published By Said Al Habsy

4. Je IBADHI.com unaweza ukaiona kwa njia ya SIMU ?
IBADHI.com ina support na kufanya kazi vizuri kabisa na aina zote za telephone kama iPhone, Android, Windows and BlackBerry using their default browsers.

Published By Said Al Habsy

5. Je! Makala na Maandishi yalioandikwa katika IBADHI.com ni ya uhakika/Ukweli?
Naam bila ya wasiwasi wowote, maandiko na makala ni uhakika kutoka kwa wahusika wake nao ni waandishi na wahadhiri waliojitolea na kuweka makala zao hapa katika IBADHI.com, unaweza kutembelea Wajue Masheikh Wetu kwa kuwajua zaidi.

Published By Said Al Habsy

6. Nina Swali Kuhusu Uislam. Wapi nitapata Jibu ?
Sehemu ya Maswali Na Majibu ina maswali ya watu mbali mbali yaliyojibiwa. Kama hujapata unachotaka tafadhali jaza form katika Maoni Yenu na uliza swali lako , utajibiwa haraka na Masheikh wetu.

Vile vile kuna sehemu ya maswali yaliojibiwa kwa sauti na Sh.Muneer Al Masroori, tembelea hapa

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

7. WENGI WANAPOONA IBADHI.COM WANAHISI TUNAJIENGUA.
Tumepokea ujumbe unaosema:

Wengi wanapoona ibadhi.com wanahisi tunajimegua.

Asalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh.

Tunawashauri waanzilishi/wanaotumia ibadhi.com wabadilishe jina na kuwa Istiqama.com au linalokaribiana.

Tusameheni ila tunajaribu tulete umoja wa ummah badala ya makundi ya madhahid.

JAWABU:

Kwanza: Tunafurahi kupata ujumbe wenu na sisi tunaupokea kwa furaha na ukunjufu na tunasema haihitaji samahani, Allah mtukufu awalipe kwa juhudi zenu kila la kheri.

Pili: Ushauri wenu tunaupokea kwa mikono miwili, nao upo katika meza yetu na tunashukuru sana kwa ushauri nzuri.

Tatu: Sisi hatuoni ubaya wowote wa kutumia jina la Ibadhi.com kwa sababu jina ni kiwakilishi tu, kwa hiyo mazingatio ni katika yale yaliyowakilishwa na lile jina.

Nne: Kuwepo madhehebu tofauti ni dharura ya kuhifadhi mafundisho ya vyuo tofauti na athari zake na kuhusika kila upande na mafundisho yake; kwa hiyo hatuoni ubaya wa kuwepo Ibadhi.com ikiwa tu itakuwa mbali na mafundisho ya kuusambaratisha umma na kuujengea uhasama baina ya wafuasi wake.

Tano: Sisi tunaamini kuwa ibadhi.com ni chuo cha kufikisha mafundisho ya Uislamu kupitia kwa wanavyuoni wa Madhehebu ya Ibadhi na kutegemea msingi ya ibadhi katika utoleaji wa dalili.

Sita: Ama kuhusu suala la umoja, kwa hakika Ibadhi.com haipingi umoja wa umma wala haina siasa ya kuvunja umoja wa umma, bali ibadhi.com inahimiza umoja wa umma kwa misingi ya kushikamana katika tuliyokubaliana na katika yenye tofauti kila upande uhusike na majukumu yake.

Saba: Ibadhi.com msingi wake ni Haki kwa dalili mkono kwa mkono hadi peponi.

Kwa hiyo hisia za kujimegua ni hisia batili, na hisia sahihi ziwe za kujenga umma kwa kueneza mafundisho sahihi na ya haki kwa mujibu wa dalili.

Asante sana.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

8. JEE! IBADHI.COM IMETAYARISHWA KWA KUPIGA VITA MADHEHEBU NYENGINE ZA KIISLAMU?
IBADHI.com haijaanzishwa kupiga vita Madhehebu yoyote ya Kiislamu wala kuleta himizo la chuki na kasumba katika Jamii, hayo si mafundisho ya chuo hichi cha Kiislamu wala malengo yake.

IBADHI.com imeanzishwa kwa kuelimisha Jamii inayozungumza Kiswahili kupitia chuo cha Madhehebu ya Ibadhi, na msingi wake ni HAKI KWA DALILI, basi hatuna kinyongo kukubali haki kutokea Madhehebu yoyote yale.

Na hayo ni baada ya kupata maombi ya Waumini kutoka mataifa mbali mbali hususan mataifa ya Afrika na Ulaya.

Asanteni.