Published By Said Al Habsy
Mtu akimuingilia mkewe na hakushusha manii hata kidogo je wanapaswa kuoga?
“Pakikutana pawili panapotahiriwa, kuoga huwajibika sawa ikiwa mtu ameshusha manii au hajashusha”. Hivi ndivyo ilivyothibiti katika hadithi. Na hadithi isemayo “Maji huwajibika kwa maji” imefutwa hukumu yake kwa maafikiano ya Umma. Na Allah anajua zaidi.
Published By Said Al Habsy
Mtu akimuingilia mkewe na hakushusha manii hata kidogo je wanapaswa kuoga?
“Pakikutana pawili panapotahiriwa, kuoga huwajibika sawa ikiwa mtu ameshusha manii au hajashusha”. Hivi ndivyo ilivyothibiti katika hadithi. Na hadithi isemayo “Maji huwajibika kwa maji” imefutwa hukumu yake kwa maafikiano ya Umma. Na Allah anajua zaidi.
Published By Said Al Habsy
Je inajuzu kutamka Bismillahi na nia wakati wa kuoga janaba ? Na je inamjuzia mtu kuoga akiwa utupu katika mahala pa stara, sawa ikiwa kuoga huko ni wajibu au sunna ?
Hakuna haja ya kutamka Bismillahi wakati wa kuoga, na nia ya moyoni inatosha, wala haikatazwi kuoga utupu katika mahala pa stara. Na Allah anajua zaidi.
Published By Said Al Habsy
Mwenye janaba akitayamamu kwa ajili ya kusali, je inamjuzia kusoma Qur’ani na kugusa msahafu mtukufu ? Kumekuwapo hitilafu kuhusu kutayamamu: je kunaiondoa hadathi kabisa au kunaruhusu kusali tu ?
Rai yenye nguvu ni ya pili. Lakini aula akunuilie kutayamamu kwake kupata ruhusa ya kusali, kusoma Qur’ani na kugusa msahafu. Na Allah anajua zaidi.
Published By Said Al Habsy
Mtu amepatwa na janaba, alipotaka kuoga aliyakuta maji yabaridi sana, akasahau kuyapasha moto, bali akajiosha mahala pa najsi na kuoga kuanzia kitovuni hadi magotini kisha akatayamamu akasali hivo hivo. Nini hukumu ya hilo?
Akiogopa dhara ikiwa ataoga kwa maji haikatazwi kutayamamu mpaka aweze kuyatumia. Na Allah anajua zaidi.
Published By Said Al Habsy
Nini kauli yenu kuhusu mwenye kuacha kuoga janaba kwasababu ya ubaridi wa maji akasali bila kuoga? Nini analazimika kufanya ?
Sala haijuzu bila kuoga janaba; isipowezekana kuoga kwa ubaridi wa maji itapasa yapashwe moto ikiwezekana; isipowezekana kuyapasha moto pamoja kutowezekana kuyatumia hivo hivo yalivo itapasa kuelekea kwenye kutayamamu. Na mwenye kusali bila kuoga wala kutayamamu, sala yake ni batili, haisihi. Na Allah anajua zaidi.
Published By Said Al Habsy
Nini kauli yenu kuhusu mwenye kutoa dalili kwa kauli ya Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- “Hedhi yako haimo mkononi mwako” juu ya utohara wa mwili wa mwenye hedhi na mwenye janaba akawa anasali na kufunga bila kuoga mpaka ikambainikia hukumu ya suala hilo ? Nini analazimika kufanya kwa sala na saumu zilizopita ?
Anawajibika kulipa sala alizosali na siku alizofunga katika hali ya janaba kwa kuwa ni sharti hadathi kubwa iondolewe ili sala na saumu ziwe sahihi. Na Allah anajua zaidi.
Published By Said Al Habsy
Nini kauli yenu kuhusu mwanamke ameota anayoyaota mwanamme usingizini na hakuoga kwa kutolijua hilo, na ikampitia siku nzima hata ikambainikia hukumu, nini anapaswa afanye ?
Anawajibika kuoga, kutubu na kurudia sala na saumu ikiwa alifunga siku hiyo, na hayo ikiwa aliona ametokwa na maji. Na Allah anajua zaidi.
Published By Said Al Habsy
Nini kauli yenu kuhusu mwanamke hakuwa akioga janaba kwa kutokuijua hukumu yake, na alikuwa akisali na muda mrefu umepita tangu kaolewa hadi sasa, nini analazimika kufanya?
Anawajibika kuzilipa sala zote alizozisali na janaba. Ikiwa hajui sala gani na ngapi basi naalipe sala zote tangu siku aliyoolewa mpaka siku aliyoanza kuoga janaba. Na Allah anajua zaidi.