Home JAWABU LA SWALI LAKO

JAWABU LA SWALI LAKO

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Ndugu yetu Said Moh’d Abdallah Al Harthy kutoka Oman anauliza

Swali:

Je, kusoma khitma baada ya kufiwa na mzazi wako,ndugu yako au mwanao ni suna kiislam au fardhi?

JAWABU:

Kusoma Khitima baada ya kufiwa na mzazi au ndugu au mwana au yoyote katika jamaa, hilo si katika Sunna wala si Fardhi, hilo la Khitima ni jambo walilolipitisha baadhi ya watu tu na likazoeleka katika jamii kwa muda mrefu.

Kwa hiyo hilo si Sunna wala Faradhi.

Basi mwenye kutaka kumfanyia wema maiti wake, anatakiwa apite mlango wa sadaka, au kumuombea dua ya pekee si dua ya kukusanyika.

Imekuja katika athari za Mtume wetu (s.a.w) kuwa alikuwa akichinja na kugawa sadaka ya kichinjwa hicho kwa ajili ya Mama wa Waumini Bibi Khadija bint Khuweilid (r.a) mke wake (s.a.w) wa mwanzo.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Ndugu yetu Said Moh’d Abdallah Al Harthy kutoka Oman anauliza

Swali:

Je, kusoma khitma baada ya kufiwa na mzazi wako,ndugu yako au mwanao ni suna kiislam au fardhi?

JAWABU:

Kusoma Khitima baada ya kufiwa na mzazi au ndugu au mwana au yoyote katika jamaa, hilo si katika Sunna wala si Fardhi, hilo la Khitima ni jambo walilolipitisha baadhi ya watu tu na likazoeleka katika jamii kwa muda mrefu.

Kwa hiyo hilo si Sunna wala Faradhi.

Basi mwenye kutaka kumfanyia wema maiti wake, anatakiwa apite mlango wa sadaka, au kumuombea dua ya pekee si dua ya kukusanyika.

Imekuja katika athari za Mtume wetu (s.a.w) kuwa alikuwa akichinja na kugawa sadaka ya kichinjwa hicho kwa ajili ya Mama wa Waumini Bibi Khadija bint Khuweilid (r.a) mke wake (s.a.w) wa mwanzo.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Ndugu Massoud Ali Massoud kutoka Tanzania anauliza

Swali:

ASSALAAM ALAYKUM, SHEIKH NILIKUA NAULIZA KWA MFANO MTU KAENDA MSIKITINI SALA YA ALFAJIRI NA ALIPOFIKA ALIWAHI KUSWALI JAMAA LAKINI HAKUWAHI KUSWALI SUNA YA KABLIA JE BAADA YA KUMALIZA JAMAA YA FARADHI ANAWEZA KUSWALI SALA YA SUNNA YA KABLIA?

JAWABU:

Waalaykum salam warahmatullahi wabarakatuh.

Ndio anatakiwa baada ya kumaliza sala ya Jamaa asali ile Sunna ya Alfajiri, na kuitwa hii sunna kuwa ni kablia ni kwa kuzingatia asili ya hukumu yake, kuwa husaliwa kabla ya Faridha ya Alfajiri, kwa hiyo unaposimama kuisali nia yako ni kuwa unasali Sunna ya Alifajiri.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Mr Massoud Ali Massoud kutoka

Tanzania

Swali:

ASSALAAM ALAYKUM SHEIKH SWALI LANGU NI: JE INAFAA KUFANYA AZLU (KUMWAGA NJE MBEGU ZA UZAZI) KWA MUJIBU WA SHERIA?

JAWABU:

Waalaykum salam wa rahmatullahi wabarakatuh.

Hili ni suala linalorejea baina ya wana ndoa wawili, yakipita makubaliano baina yao hakuna tatizo ndani yake, la sivyo haitofaa.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Mr Massoud Ali Massoud kutoka

Tanzania

Swali:

ASSALAAM ALAYKUM SHEIKH NAULIZA: ETI KUMFANYIA DUA MTOTO ANAPOTIMIZA MWAKA INAFAA?

JAWABU:

Haki ya mtoto ni kumlea vizuri kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, na Allah mtukufu kwenye kitabu chake ametueleza kuhusu Waja wake wema, na miongoni mwa sifa zao ni kuwa wao humuomba Allah kwa dua hii:

((وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا))

((Na wale wenye kusema: Mola wetu tupe sisi kwa wake zetu na vizazi vyetu kichombezo cha macho na utujaalie kuwa ni ruwaza njema kwa Wachamungu))

[Furqaan 74]

Amesema Imamu Qutub Al-Aimah (r.a) katika kubainisha Aya hii:

أى هب لنا قرة أعين هى أزواجنا وذرياتنا ، بأن يؤمنوا فتقربهم أعيننا ، لأنا نحب لهم الخير بالطبع ، ولأنهم يعينوننا وينفعوننا فى حياتنا ، وبعد موتنا ان متنا قبلهم ، ويكونون معنا فى الجنة ان كنا سعداء ، وكانوا سعداء

((Yaani tupe sisi kichombezo cha macho nacho ni wake zetu na vizazi vyetu, kwa kuwa wao ni wenye kuamini basi yakafurahika kwa sababu yao macho yetu, kwa sababu sisi tunawapendea wao kheri kitabia, na kwa sababu wao watatusaidia na kutufaa katika maisha yetu, na baada ya kufa kwetu tukifa kabla yao, na watakuwa pamoja na sisi katika Pepo ikiwa sisi ni wenye kufaulu na wakawa wao ni wenye kufaulu))

Kwa hiyo dua ya kuwaombea watoto isihusishwe siku maalumu bali inatakiwa kila wakati mzee awaombee wema watoto wake.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Published By Said Al Habsy

SWALI

Ninapo safiri kiutalii katika nchi nyengine, moja kati ya vivutio vya kitalii hupangiwa kutembelea nyumba za ibada za dini nyengine kama Buddism, Hindu, NK. Jee kuna ubaya wowote kufanya hivyo, hata ikiwa itikadi yangu ni kielimu tuu na kujuwa wengine waabuduvyo katika itikadi zao ?

JAWABU

Kutembea katika ardhi na kutazama tamaduni za watu na nchi zao, na kuchukua mazingatio kutokana na kutebea huko, ni jambo ambalo uisilamu umeruhusu na kuhimiza.

Amesema ALLAAHU S.W :
(قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ)
[Surat An-Naml 69]

Sema: Nendeni katika ardhi, na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu.

Na katika aya nyingine :
(قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلُ ۚ كَانَ أَكْثَرُهُمْ مُشْرِكِينَ)
[Surat Ar-Room 42]

Sema: Safirini duniani muangalie ulikuwaje mwisho wa walio tangulia. Wengi wao walikuwa washirikina.

Na nyingine :
(قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانْظُرُوا كَيْفَ بَدَأَ الْخَلْقَ ۚ ثُمَّ اللَّهُ يُنْشِئُ النَّشْأَةَ الْآخِرَةَ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)
[Surat Al-Ankaboot 20]

Sema: Tembeeni katika ardhi na tazameni jinsi alivyo anzisha uumbaji; kisha Mwenyezi Mungu ndiye anaye umba umbo la baadaye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.

Na aya nyingine nyingi zimetaja suala hili.

Kutokana na hayo maelekezo ya Qur’ani tukufu, Hakuna kizuizi katika kutembelea sehemu kama hizo za hao washirikina na kutazama ibada zao za kishirikina wazifanyazo katika miji yao.

Lakini ni lazima kuzingatia masharti yafuatayo :

1. Safari hiyo isiwe ndio lengo la asili lililomfanya mtu huyo kufunga safari rasmi.

Hii ni kwa sababu mtume s.a.w amekataza kufunga safari kama hizo kwa kuazimiwa ila katika sehemu tatu tu :

لا تُشَدُّ الرِّحالُ إلا إلى ثلاثةِ مساجدَ : المسجدِ الحَرامِ، ومسجدِ الرسولِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، ومسجدِ الأقصى” .
الراوي: أبو هريرة المحدث: البخاري – المصدر: صحيح البخاري – الصفحة أو الرقم: 1189
خلاصة حكم المحدث: [صحيح]

Maana yake ni kuwa :
” Zisifungwe safari kwa kuazimiwa ila katika misikiti mitatu :

1- Msikiti mtukufu (makka )

2 – Msikiti wa mtume s.a.w (Madina ).

3 – Na msikiti wa Aqswaa (palestina )”.

2. Iwe kwenda huko ni makusudio ya daraja la pili, na wala si makusudio ya asili ya safari yake.

3. Isiwe kwa nia ya kutukuza yale ambayo wanayatukuza watu hao wa shirki.

4. Isiwe kuna khofu ya kupata madhara juu ya muisilamu kwa Dini yake na nafsi yake na mali yake.

5. Asishiriki nao katika shirki zao katika mambo yao.

Ikiwa yatatimia hayo Inshaallaah hakuna tatizo wala kizuizi kwa kutembelea sehemu hizo.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

Published By Said Al Habsy

SWALI

Bora ya sala za wanawake ni nyumbani thawabu zake ni nyingi, lakini mwezi mtukufu wa ramdhani wengi tunakimbilia sala ya Tarawehe misikitini.

Je thawabu zinakuwa sawa na anaesali nyumbani au zinaidi au zinapungua?

JAWABU

Sala za jamaa ni faradhi ya lazima kwa wanaume tu misikitini, kama ilivyotajwa katika Ishara ya aya za qurani, na ibara za wazi katika sunna za mtume s.a.w.

Amma wanawake, wao sala zao ni bora zaidi kuwa nyumbani mwao kuliko kuwa katika misikiti.

Na hili limethibiti katika hadithi sahihi nyingi za mtume s.a.w.

Miongoni mwa hadithi hizo ni :

1. عن أمِّ حُميدٍ امرأةِ أبي حُميدٍ السَّاعديِّ أنها جاءتِ النَّبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فقالت: يا رسولَ اللهِ إنِّي أُحِبُّ الصَّلاةَ معك قال: ( قد علِمْتُ أنَّك تُحِبِّينَ الصَّلاةَ معي وصلاتُك في بيتِك خيرٌ مِن صلاتِك في حجرتك، وصلاتُك في دارِك خيرٌ مِن صلاتِك في مسجدِ قومِك، وصلاتُك في مسجدِ قومِك خيرٌ مِن صلاتِك في مسجدي ) قال: فأمَرَت فبُني لها مسجدٌ في أقصى شيءٍ مِن بيتِها وأظلَمِه وكانت تُصلِّي فيه حتَّى لقيَتِ اللهَ جلَّ وعلا
الراوي: أم حميد امرأة أبي حميد الساعدي المحدث: ابن حبان – المصدر: صحيح ابن حبان – الصفحة أو الرقم: 2217
خلاصة حكم المحدث: أخرجه في صحيحه

➡ Ameipokea Ummu humeid r.a, nae ni mke wa Abii Humeid r.a, anasema :
” Alimuendea mtume s.a.w na akasema : Yaa Rasuula llaah; hakika mimi napenda kuswali nawe – yaani msikitini, akasema mtume s.a.w : ” Hakika nimejua kuwa unapenda kuswali pamoja na mimi, lakini sala yako chumbani mwako ni bora kuliko sala yako katika ukumbi wa nyumba yako. …., na sala yako nyumbani kwako ni bora kuliko sala katika msikiti wa watu wa mji wako, na sala yako katika msikiti wa watu wako – yaani karibu – jirani “ni bora kuliko sala kuliko sala yako katika msikiti wangu “

Anasema mpokezi kuwa :
” Akaamrisha ajengewe mama huyo msikiti katika upande wa mbali zaidi katika nyumba yake, tena sehemu yenye giza, akawa anaswali huko mpaka kufa kwake “

➡ Hadithi hii Ameipokea imaamu ibnu Hibbaan.

➡ Na hadithi inaonyesha ubora wa kuswali katika eneo la nyumba ya mwanamke, ndani au karibu ya nyumba yake.

➡ Pia iwe ni sehemu yenye stara Asiwe anaonekana na kila mtu.

➡ Na pia imeonyesha ubora wa kuswali mwanamke katika msikiti wa karibu zaidi kuliko msikiti wa mbali, hata kama msikiti wa mbali utakuwa ni bora zaidi kuliko huo wa karibu.

➡ Na pia haikuonyesha Uharamu wa kuswalia mwanamke katika msikiti.

2. Hadithi nyingine ni :
لا تمنَعوا إماءَ اللهِ مساجدَ اللهِ وليخرُجْنَ تَفِلاتٍ
الراوي: أبو هريرة المحدث: ابن حبان – المصدر: صحيح ابن حبان – الصفحة أو الرقم: 2214
خلاصة حكم المحدث: أخرجه في صحيحه

➡ Amepokea pia ibnu Hibbaan, kutoka kwa Abii huraira r.a, Amesema mtume s.a.w :
” Musiwazuie wajakazi wa ALLAAH – yaani wanawake – misikiti ya ALLAAH, na watoke bila ya kujipamba “

➡ Hadithi hii inaonyesha pia kuwepo ruhusa ya kuswalia wanawake misikitini.

➡ Na ili kujuzu hilo wametakiwa wasijipambe katika kutoka kwao huko.

➡ Na katika Fataawa za maulamaa wengi pia ni kuwa : ” Inajuzu kwa wanawake kuswali sala za jamaa katika misikiti, lakini si wajibu kwao kufanya hivyo.

➡ Amesema samaahatu shaikhinaa Ahmad bin hamad alkhaliily :
” Mtume s.a.w hakuwakataza wanawake kuingia misikitini – yaani kuswali misikiti – bali walikuwa wakiswali nyuma yake, lakini pamoja na hivyo alikuwa akiwaamrisha wasijitie manukato , na alikuwa akiwatahadharisha ikiwa watajitia manukato au udi basi wasihudhurie jamaa.

➡ Na hii ni kwa sababu ya kuhofia fitna kwa sababu ya hilo.

➡ Na Tahadhari pia imetolewa na Bi Aisha r.a aliposema :

” لو أنَّ رسولَ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ رأى ما أحدث النساءُ لمنعهُنَّ المسجدَ . كما مُنعت نساءُ بني إسرائيلَ …
الراوي: عائشة أم المؤمنين المحدث: مسلم – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 445
خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Maana yake ni kuwa :
” lau kama mtume s.a.w angeona yale ambayo wameyazusha wanawake, basi angewakataza kuhudhuria misikitini, kama walivyokatazwa wanawake wa wana wa Israili – Banii israa ili “

➡ Na haya aliyasema Bi Aisha r.a kwa sababu ya kuona mambo ambayo wameyafanya wanawake katika zama hizo.

➡ Na katika maulamaa wengine pia ni Shaikhunaa al allaamah swaaleh bin fauzaan al fauzaan ALLAAH awahifadhi maulamaa wote, yeye amesema :
” Sala ya jamaa kwa wanawake – wao kwa wao – kuna ikhtilafu katika maulamaa, wako waliokataza, na wengine juzisha, na wengi wamesema hakuna kizuizi katika hilo.

➡ Na mtume s.a.w alimruhusu umma waraqa awaswalishe watu wa nyumbani kwake.

➡ Na Pia imekuja jawabu kutoka kwa shaikhinaa Muhammad ibni Abdi I maqsuud kuwa :
” Wanaruhusiwa lakini wasijitie manukato wala kujipamba “

➡ Kwa hayo yote,
Hakuna ubaya kwa mwanamke kuswali msikitini , na hasa msikiti wa karibu zaidi.

➡ Na mwanamke atapata malipo zaidi, ikiwa ataswali nyumbani kwake, kwa kuwa huko ni stara zaidi kuliko kutoka na kwenda misikitini.

➡ Isipokuwa kuswali katika misikiti mitatu mitukufu, makka, madina na palestina, kuswali humo ni bora zaidi kuliko kuswali ndani ya nyumba yake mwanamke.

➡ Na Hakuna dalili yoyote inayo onyesha wazi kuwa malipo kiasi gani atapata mwanamke baina ya kuswali nyumbani au kuswali msikitini.

➡ Na kwa kuwa hakuna dalili ya hayo, inabakia hukmu kuwa ni kwa mujibu wa hali mbili zifuatazo :

1 – Ikiwa kunahofiwa fitna, au mwanamke kutoka bila stara, au kwa kujipamba, basi kuswali ndani ni bora zaidi kuliko misikitini.

2 – Na kinyume na hivyo, itakuwa ubora upo kote kote, na hasa kwa msikitini ikiwa hakukhofiwi kitu kibaya katika kutoka kwake , na pia ikiwa kuna faida za ziada huko, kama mihadhara na darsa mbalimbali.

Na hasa ikiwa kutazingatiwa yafuatayo :

1. Msikiti usiwe mbali sana na nyumba yake.

2. Atoke bila ya mapambo ya aina yoyote wala manukato.

3. Ahifadhi sauti yake.

4. Asiwe katika safu ambazo zipo karibu saba na wanaume.

5. kusiwe kuna khofu juu ya nafsi uhai au mali.

➡ REJEA VITABU VIFUAVYO :

1 – Al mar’atu tas alu, cha Sh Al khaliily juzuu ya 1

2 – Fataawa l mar’ati l muslima, kimekusanya maulamaa wengi.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W AWAHIFADHI WAISILAMU WOTE.

Published By Said Al Habsy

SWALI

Kuhusu wanawake na ghashwa -yaani – kujifunika uso wakati wanapotoka nje, je ni mapendekezo ya mtu binafsi tu au ni shuruti fulani katika maamrisho ya dini yetu?  Na Je Kama mke anapedelea kuvaa hiyo ghashwa kwa kujistiri lakini mumewe hampi ruhsa hukumu yake nini?

JAWABU

➡ Kuvaa niqabu na kufunika uso ni miongoni mwa stara zinazopendekezwa na bora katika sheria ya KIISILAMU.

➡ Lakini hukmu ya kuvaa niqabu inatofautiana kwa mujibu wa hali na mazingira aliyoko mwanamke.

➡ Na maulamaa katika hili wana kauli mbalimbali.

 1. Kufunika uso si wajibu kwa mwanamke,  ila akikhofia fitna katika kuwa wazi uso wake.

 Na hii ni rai mashuhuri kwa maulamaa wengi katika vitabu mbalimbali vya fiqhi,  na hasa katika mlango wa kuhirimia katika Hija au Umra.

 2. Kauli ya pili ni kuwa  :  ” kufunika uso ni lazima,  kwa kuwa uso ni moja katika mambo ya mwanamke,  na uso ni sehemu inayobainisha uzuri wa mwanamke au kinyume chake “

➡ Na ziko hadithi sahihi mbalimbali zimetaja kuhusu kukataza mwanamke kuvaa niqabu akiwa mwanamke huyo katika hija au umra.

➡ Bila shaka hiyo inaonyesha kuwa niqabu zilikuwepo tokea zamani,  na walikuwa wanawake wakivaa,  ndio maana mtume s.a.w akakataza kwa wale wenye kuhiji au kufanya umra wasivae Niqaabu baada ya kuwa wameingia katika ibada hizo.

➡ Na ingekuwa Niqaabu hazipo katika zama hizo basi isingekuwa kuna faida yoyote katika hadithi iliyotangulia kuhusu kukataza Niqaabu kwa walioingia katika ihraamu.

➡Ingekuwa hakuna  hikma kukataza kitu ambacho hakipo.

➡ Amesema mtume s.a.w : لا تنتَقِبُ المرأَةُ الحرامُ ، ولا تلبسُ القفازينِ  الراوي: عبدالله بن عمر المحدث: الذهبي    – المصدر: تنقيح التحقيق – الصفحة أو الرقم: 2/25 خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Amepokea Abdullah bin Omar r.a,  amesema mtume s.a.w : ” asivae Niqaabu mwanamke mwenye kuhirimia,  wala asivae soksi za mikono “

➡ Kwa hiyo niqabu si mapendekezo ya mtu kuvaa au kutokuvaa,  bali hiyo ni sehemu katika sheria,  lakini ulazima wake ni katika hali ya kuwa watakuwa wana onekana wanawake hao kwa wanaume.

➡ Na si lazima iwe Niqaabu ya kufunga moja kwa moja,  bali inawezekana lile juba kubwa linalofunika kichwa na kifua akafunikia uso pale anapokutana na wanaume.

➡ Na kwa kuwa fitna katika zama zetu zimekithiri na kuzidi,  basi ni bora zaidi kuwa na Niqaabu ya moja kwa moja ili kuwa katika stara wakati wa kuwa mwanamke nje ya nyumbani kwake.

➡ Pia inawezekana kuipandisha juu tu panapokuwa fitna hakuna,  na ikuwa hata tokea mtu  basi anaishusha tu kwa haraka bila mashaka yoyote ➡Na wake za mtume s.a.w walikuwa wakifunika nyuso zao ikiwa watapita wanaume karibu yao,  hata wakiwa katika hija.

➡ Na hili limethibiti katika hadithi pia japokuwa baadhi ya maulamaa wanaona kuwa hadithi ina udhaifu,  lakini wengi wanaona kuwa ni sahihi.

➡ Rejea kitabu cha samaahatu shaikhinaa Ahmad bin hamad alkhaliily “Al mar’atu tas alu, juzuu 2”

➡ Pia unaweza kurejea vitabu vikubwa vya fiqhi, na vitabu vya fataawa mbalimbali za maulamaa.

➡ Na mume ambae anamkataza mkewe kusitiri uso wake na hasa pale anapokuwa nje ya nyumba yake,  na kunawezekana kuonekana na wanaume wengine,  huyo ni mwanaume asiejua thamani ya mke,  na hajui daraja na heshima yake kwa mkewe.

➡ Na Hakuna haki ya kumtii ikiwa kutahofiwa fitna,  au kuwa mwanamke huyo hakusitiri vizuri mwili wake.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

➡ NAMUOMBA ALLAAH ATUONGOZE KATIKA KUIJUA HAKI NA KUIFUATA.

ALLAAHU AALAMU.

Published By Sh. Shaaban Al – Battaashy

SWALI

Ikiwa mus’hafu  umesha kuwa mkongwe,  hata baadhi ya kurasa zimesha chanika, vile vile casset za radio zinazo haribika zenye Quran ni ipi njia bora ya kuhifadhi maneno haya adhimu ya subhanallah wa taala?

JAWABU

➡ Maneno ya ALLAAH S.W ni matukufu katika hali zote na pahala popote yawapo.

➡ Kwa kuwa Qur’ani tukufu inaandikwa katika karatasi maalumu kwa njia ya mashine hata ikafikia kuwa misahafu kamili katika kitabu kimoja,  bila shaka karatasi hizo zinaweza kuchanika au kuchoka karatasi zake baada ya kupitiwa na muda mrefu.

➡ Ikifikia hali ya kuwa mus’hafu umekuwa mkongwe sana na hata kusomea tena imekuwa ni vigumu,  basi zitumike njia zifuatazo katika kutunza heshima na utukufu wake :

 1- Ikiwa inawezekana kuutumia katika baadhi ya juzuu zilizomo au sura,  basi uwekwe katika hali nzuri juzuu hizo zenye uzima na watu watumie.

 2 – Ikiwa katika nchi hiyo kuna viwanda vya kuchapisha misahafu,  au nchi jirani ina viwanda kama hivyo,  basi ni muhimu kuulizia kwanza ikiwa wanapokea misahafu ya zamani ili waitie katika viwanda vyao vya kutengeneza karatasi nyingine zije kufanywa misahafu tena kwa mara nyingine.

➡ Hili nalitaja hivi kwa sababu :  ” Kuna miradi mingi sasa kupitia viwanda mbalimbali,  vinanunua vitu vilivyotumika na kutengenezea upya tena vitu vipya kwa mfano ule ule “

➡ Kuna viwanda vinanunua machupa matupu ya plastic kwa ajili ya kutengeneza machupa mengine mapya mfano wake.

➡ Kuna viwanda vya kununua vyuma vilivyomaliza muda wake wa kutumika kwa watu, na baadae kutengenezea vitu vingine vipya pia.

➡ Na mifano ya hayo  iko mingi sana,  hata maboksi matupu,  vikopo vya soda,  chupa za kigae za soda,  na kadhalika.

➡ Lakini sijawahi kusikia kuwa kuna viwanda vinakusanya misahafu ya zamani ili kutengeneza misahafu mingine mipya kutokana na hiyo ya zamani.

 3 – Njia na hatua ya mwisho kabisa ili kuhifadhi maneno ya ALLAAH S.W yasizagae na kutawanyika bila kuhifadhika ni : ” Kuichimbia shimo na kuichoma moto kwa nia ya kuhifadhi maneno hayo,  na si kwa nia ya kuidharau,  na baada ya hapo inafukiwa jivu lake ilipochomewa.

➡ Na pia kuna Kauli nyingine kuwa : ” ifukiwe chini katika sehemu ambazo hazitarajiwi kulimwa au kuchimbuliwa.

➡ Lakini njia ya Kuichimbia na kuichoma ikiwezekana ni bora zaidi ikibidi kufanya hivyo kwa nia tuliyoitaja.

➡ Na ikiwa pengine katika nchi hiyo hakuna uwezekano wa kupata sehemu ya kuchimba au kuichoma,  na hakuna njia nyingine yoyote  ya kuhifadhi maneno hayo,  basi ni bora kuifunganisha na kitu kizito ,  kama jiwe au chuma,  kisha izamishwe baharini, kwa kuwa ikizama kwenda chini kwa kitu kizito itakuwa si rahisi kuibuka tena juu ya maji.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUHIFADHI SISI NA DINI YETU NA KITABU CHETU NA KIZAZI CHETU.

ALLAAHU AALAMU.

Published By Said Al Habsy

SWALI

Tunamuuomba Mwenyezi Mungu atukinge na adhabu ya moto,amini yaraabi !!!, swali ? Je hiki chakula kinachopikwa kwa moto, Je  baada ya kukila, ni wajibu wangu kutawadha udhu?? au si lazima?? Je Ustaadh nini maoni yako kuhusu hilo swali?

JAWABU

➡ Moto siku ya qiyaama umeandaliwa kwa ajili ya Makafiri na watu waovu walikufa hali ya kuwa ALLAAH S.W hayuko radhi nao.

➡ Amesema ALLAAHU S.W : (وَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ) [Surat Aal-E-Imran 131]

Na uogopeni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya makafiri.

➡ Na katika aya nyingine :

(إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ)

[Surat Az-Zukhruf 74]

Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu.

➡ Lakini moto huu unaotumika kupikia chakula katika dunia,  hauna hukmu ya kuwa kama moto wa akhera.

➡ Na kwa mtu aliekuwa na udhu kisha akala chakula chochote ambacho kimepikwa kwa moto,  udhu wake utaendelea kuwa sahihi baada ya kula chakula hicho.

➡ Na mtume s.a.w alikuwa anakula na kisha anaswali kwa udhu ule ule aliokuwa nao kabla ya kuanza kula.

➡ Imepokewa kuhusu hilo katika hadithi zifuatazo :

1.  دعَتْنا امرأةٌ مِن الأنصارِ وذبَحت شاةً وصنَعت طعامًا ورشَّت لنا صورًا، فدعا رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم بالطَّهورِ، فتوضَّأ ثمَّ صلَّى، ثمَّ أتَيْنا بفضولِ الطَّعامِ فأكَله، وصلَّى رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم ولم يتوضَّأ،ْ

➡ Amepokea Jaabir bin Abdillaah Al answaary r.a,  anasema : ” Alitualika mwanamke wa ki answaar, Akatuchinjia mbuzi,  na akatutengenezea chakula,  na akarashia mchuzi, akaagiza Mtume s.a.w maji masafi na akatawadha, kisha akaswali,  alipo kwisha kuswali akala,  kisha akaswali na wala hakutia udhu.

ودخَلْنا على أبي بكرٍ فدعا بطعامٍ لم يجِدْه فقال: أين شاتُكم الَّتي ولَدت ؟ قالت: هي ذِهْ فدعا بها فحلَبها بيدِه ثمَّ صنَعوا لِبَأً فأكَل فصلَّى ولم يتوضَّأ،

“Na tuliingia nyumbani  kwa Abii Bakri r.a,  akaja na akaagiza chakula lakini hakupata,  akauliza :”Yuko wapi mbuzi wenu ambae amezaa? Akajibu mkewe : “Huyu hapa ” Abuu Bakri r.a akamkama maziwa kwa mkono wake ,  kisha akatengeneza chakula kutokana na maziwa hayo,  akala -mtume s.a.w – na akaswali wala hakutawadha”

ْ وتعشَّيْتُ مع عمرَ فأُتي بقصعتينِ فوُضِعت واحدةٌ بينَ يدَيْهِ والأخرى بينَ يدَيِ القومِ فصلَّى ولم يتوضَّأْ

“Na tulikula chakula cha usiku kwa Omar r.a, akaleta – chakula katika  – sahani mbili,  moja akaiweka mbele yake,  na nyingine mbele ya watu – wageni, kisha akaswali mtume s.a.w na wala hakutia udhu “

الراوي: جابر بن عبدالله المحدث: ابن حبان – المصدر: صحيح ابن حبان – الصفحة أو الرقم: 1139 خلاصة حكم المحدث: أخرجه في صحيحه

➡ Hiyo hadithi ni sahihi Ameipokea imaamu ibnu Hibbaan kupitia swahahabiy Jaabir bin Abdillaah r.a.

➡ Na hiyo ndio Kauli sahihi ambayo ni Kauli ya Jamhuri ya maulamaa wengi.

2. Na katika hadithi nyingi pia imethibiti kupitia jaabir bin Abdillaah Al answaary r.a anasema kuwa :

أنَّ النبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلم أكل لحمًا مشويًّا ثمَّ صلَّى ولم يتوضأ،ْ وإنَّ أبا بكرٍ أكل لحمًا ثمَّ صلَّى ولم يتوضأْ، وإنَّ عمرَ أكل لحمًا ثمَّ صلَّى ولم يتوضأْ”

الراوي: جابر بن عبدالله المحدث: السفاريني الحنبلي – المصدر: شرح ثلاثيات المسند – الصفحة أو الرقم: 1/216 خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ “Hakika Mtume s.a.w alikula nyama ya kuchoma kisha akaswali na wala hakutia  udhu.

Na hakika Abuu Bakri r.a alikula nyama ya kuchoma kisha akaswali na wala hakutia  udhu.

” Na hakika Omar r.a alikula nyama ya kuchoma kisha akaswali na wala hakutia  udhu.

3. Na anasema Jaabir bin Abdillaah Alanswaary r.a :

كان آخرُ الأمرَين من رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلم تَرْكُ الوضوءِ ممَّا مسَّتهُ النارُ”

الراوي: جابر بن عبدالله المحدث: السفاريني الحنبلي – المصدر: شرح ثلاثيات المسند – الصفحة أو الرقم: 1/217 خلاصة حكم المحدث: صحيح

” Ilikuwa hali ya mwisho katika mambo mawili kwa Mtume s.a.w,  ni kuacha kutia udhu kutokana na chakula ambacho kimepikwa kutoka katika moto “

➡ Na ziko hadithi nyingi nyingine kuhusu suala hili,  hizi ni baadhi tu miongoni mwazo.

➡ Mtume s.a.w pia imethibiti kuwa : ” Alikula nyama na mkate na akaswali wala hakutawadha “

➡ Na Bi Aisha r.a alikuwa akisema : ” Hakuna – ulazima wa – udhu kutokana na chakula ambacho amekihalakisha ALLAAH S.W “

➡ Lakini inapendekezwa tu kwa aliekula atie maji mdomoni na kusafishwa kinywa  chake tu kutokana na mabaki ya chakula.

➡ Na pia inapendekezwa kutia udhu upya kwa aliekula nyama ya ngamia,  na hii si wajibu kwake,  lakini ni kutoka tu katika ikhtilafu kutokana na kuwepo kauli ya kuwa mwenye kula nyama ya ngamia basi na atawadhe “

➡ Na Kauli hiyo imepokewa  katika baadhi ya hadithi,  lakini hadithi hiyo haikusihi kwa mujibu wa uhakiki wa maulamaa wengi.

➡ REJEA VITABU VYA SUNNA NA FIQHI.

Pia rejea :

1. Al Muutamad fii fiqhi l sswalaah,  sh muutaswim al maawaly.

2. Al mufasswal cha Dk Abdul kariim ziidaan

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

ALLAAHU AALAMU.

Uisilamu dini ya wepesi

Published By Said Al Habsy

SWALI

Je, unapokuwa imamu kuna nia maalumu unanuia au japo moyoni tuu inatosha ? Na kama yapo matamshi ya hio nia, naomaba nifahamishwe.

JAWABU

➡ Nia ni : ”  Kukusudia ndani ya moyo kutekeleza ibada fulani kwa ajili ya ALLAAH S.W “

➡ Na nia pahala pake ni ndani ya moyo tu bila ulazima wa kutamka kwa maneno kwa sauti.

➡ Na hii ni kwa sababu : neno ” nia ” asili yake ni “Kukusudia “.

➡ Na kukusudia ni moja katika miongoni mwa matendo yanayofanywa kwa nyoyo.

➡ Amesema ALLAAHU S.W : (وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ) [Surat Al-Bayyina 5]

Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.

➡ Na pia katika sunna amesema mtume s.a.w : Imepokewa kutoka kwa Omar bin l khatwaab r.a,  amesema : Amesema mtume s.a.w :

إنما الأعمالُ بالنياتِ، وإنما لكلِّ امرئٍ ما نوى…”

الراوي: عمر بن الخطاب المحدث: البخاري – المصدر: صحيح البخاري – الصفحة أو الرقم: 1 خلاصة حكم المحدث: [صحيح]

” Hakika si vinginevo, matendo yote huwa kwa nia,  na kila mtu hulipwa kwa nia akiyokusudia…”

Amepokea imaamu al bukhaary na Imaamu Rabii bin Habiib r.a.

➡ Inantosha huyo imamu kuwa moyo wake umekududia kuwa yeye ni imamu tokea ametangulizwa na watu ili awaswalishe.

➡ Muhimu ni kuwa moyo wake umekusudia hivyo,  na wala hakuna haja ya kutamka nia kwa maneno.

➡ Na hii ndio Kauli sahihi zaidi katika maulamaa wa kiisilaamu kwa mujibu wa dalili zilizo pokewa katika Sunna na mwenendo wa maswahaba r.a.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

Published By Said Al Habsy

SWALI

Naomba kujua suala la UTUMWA yaani KHADIM bado linatumika hadi hii leo? Kijana mwenye asili ya utumwa haifai kuowa asiekuwa na asili hiyo ?

JAWABU

➡ Kwa na kabisa napenda kukumbusha kuwa :

Neno ” khaadim” maana yake ni “mtumishi “

➡ Na mtumishi ni mtu yoyote ambae aneajiriwa na mtu mwingine ili kumfanyia kazi zake ambazo inajuzu kisheria kumuajiri mtu mwingine kuzifanya.

➡ Na wala haifai katika zama hizi kumuita mtumishi muajiriwa kuwa yeye ni mtumwa.

➡ Mtumwa ni mtu ambae alikuwa anaweza kumilikiwa na mtu mwingine kiasi cha kuwa anakuwa hana uhuru wa kufanya jambo lolote ila kwa ruhusa ya bwana wake anaemmiliki.

➡ Na mtumwa huyo pia alikuwa hana haki yoyote ya kumiliki kitu wala mali ya aina yoyote.

Na ikitokea akawa amepata mali basi mali yake yote inakuwa ni haki ya bwana wake hata ikitokea kuwa amefariki mtumwa basi mali yote inarudi kuwa ni miliki ya yule bwana wake.

➡ Hii ilikuwa ni nidhambi ya makabila katika visiwa vya arabuni tokea karne nyingine.

➡ Hata firauni aliwafanya watu wake ni kama watumwa wake na kuwadhiki na kuwanyima hata uhuru wa kuabudu Mola wa haki.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :

(إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ) [Surat Al-Qasas 4]

Hakika Firauni alitakabari katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika mafisadi.

➡Uisilamu ukaja kupitia mtume wetu muhammad s.a.w ukafuta nidhamu zote za utumwa , na kumpa kila mmoja haki yake katika uhai, mali, na hata haki ya kuoa au kuolewa haitazaiwi rangi, ukabila wala uraia wa mtu.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَأَنْكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنْكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ ۚ إِنْ يَكُونُوا فُقَرَاءَ يُغْنِهِمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ ۗ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ) [Surat An-Noor 32]

Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua.

➡ Kwa hiyo hukmu ya utumwa imefutwa kabisa katika uisilamu, wala hakuna mtu kummiliki binaadamu mwenzake na kumfanya kuwa mtumwa wakati amezaliwa huru.

➡ Na kwa kuwa ilikuwa ni ada na dasturi za baadhi ya makabila wakati huo, basi uisilamu ulikuwa na sheria kwa hatua moja baada ya nyingine, hadi jambo hilo likamalizwa jumla.

➡ Zikawekwa sheria za kuchia huru mtumwa kwa mtu mwenye kufanya kosa miongoni mwa mambo mbalimbali ya ibada.

Na mambo hayo kwa tabia za watu hao yalikuwa ni mara nyingi wao hufanya mambo yenye makosa yenye hukmu ya kuacha huru mtumwa.

➡ Na mtume s.a.w ameweka kigezo cha kuchagua mume au mke anaefaa kuoa au kuolewa.

Na kigezo hicho ni kigezo cha Dini na tabia njema tu.

➡ Amma ukabila au kuwa asili ya mtu kuwa alikuwa mtumwa zamani, hicho si kigezo wala sababu ya msingi ya kuzuia kuoa au kuolewa.

➡ Na hii ndio Kauli sahihi ya jamhuri ya maulamaa wengi zaidi.

➡ Na iko mifano hai katika historia ya kiisilaamu kuwa wako ambao walikuwa ni watumwa zamani, lakini walioa wake ambao ni Waarabu na asili yao ni huru.

➡ Na suala hili kwa jumla ni kuwa lina uchambuzi mrefu sana, na dalili mbalimbali karibu sunna.

➡ Na kwa kuwa zamani ilikuwa mtumwa ni miliki ya bwana wake, ilikuwa inakatazwa kuoa ili kuhifadhi kizazi Chao, kwa kuwa akioa mke mwenye kumilikiwa atakuwa anapoteza kizazi chake.

➡ Namuomba ALLAAH s.w atukinge na chuki na shari za kila vyenye shari.

ALLAAHU AALAMU.


LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI

Kuhusu zaka ya dhahabu kuna usemi dhahabu inayo valiwa sana haina zaka hii ni kweli ? Ikiwa mtu kapewa zawadi ya dhahabu na hana uwezo wa kuitoleya zaka hukumu yake nini ?

JAWABU

➡ Zaka ni nguzo miongoni mwa nguzo za uisilamu.

➡ Na miongoni mwa mali zinazotolewa zaka ni dhahabu na fedha.

➡ Na ALLAAH S.W ameahidi adhabu kali chungu iumizayo, kwa wenye kukusanya mali na kujilimbikizia bila kuzitolea zaka .

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ) [Surat At-Tawba 34]

Enyi mlio amini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa baat’ili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu.

➡ (يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنْفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنْتُمْ تَكْنِزُونَ) [Surat At-Tawba 35]

Siku zitapo tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu, basi onjeni mliyo kuwa mkilimbika.

➡ Na kwa kuwa Neno “zaka ” الزكاة “ ni neno la kiarabu, lina maana ya ziada na ongezeko, au usafi na ziada, kutokana na hayo maulamaa wametofautiana kuhusu hukmu ya zaka ya dhahabu ambayo ni pambo tu la mwanamke, ambalo halikuwa na malengo ya kufanyiwa biashara wala kupatiwa faida.

➡ Na ikhtilafu hiyo imekuja kutokana na kuwepo dalili tofauti katika hadithi za mtume s.a.w kuhusu suala hili kama ifuatavyo :

1. Kauli ya kwanza :
Ni Kauli ambayo yenye nguvu na ndiyo inayotegemewa katika jamhuri ya maulamaa wengi.

➡ Na hii Kauli imepokewa kutoka maswahaba wengi r.a, miongoni mwao ni :

1- Omar bin l khatwaab

2 – Abdullah bin masoud

3 – Abdullah bin Abbaas

Na wengine wengi sana katika wao na mataabiina pia r.a.

➡ Na hiyo kauli ndio Kauli katika madhehebu ya Imaamu thaury , al zuhry, Madhehebu ya Hanafy, adhwaahiriya, na zaidia.

➡ Na hiyo ndio Kauli inayotegemewa kwa nguvu katika madhehebu ya ibaadhi, kama alivyosema Imaamu Ismail bin muusa al jaitwaaly katika kitabu chake cha ” Qawaaidu l islaam.

➡ Na pia samaahatu shaikhinaa Ahmad bin hamad alkhaliily na sh said bin mabruuk alqannuuby katika kitabu cha ” Al muutamad fii fiqhi l zzakaat

➡Na wamesema maulamaa wawili hao kuwa : ” Zaka ni wajibu katika dhahabu na fedha, sawasawa ikiwa imevaliwa au haikuvaliwa, ikiwa ni katika pambo la kiume au la kike.

2. Kauli ya pili ni kuwa :
Hakuna ulazima wa kutoa Zaka ya mapambo ya mwanawake , sawasawa ikiwa mapambo hayo ni ya dhahabu au fedha au mengineyo.

➡ Na Kauli hiyo imepokewa kutoka kwa baadhi ya maswahaba r.a, miongoni mwao ni :

1 – Abdullah bin Omar

2 – Aisha bint Abii Bakri

3 – Jaabir bin Abdillaah

4 – Anas bin Maalik

Na wengine pia wengi miongoni mwa maswahaba na mataabiina r.a.

➡ Na hiyo ni Kauli katika madhehebu ya Maalikiya na hanbaly na ni dhaahiri katika madhehebu ya shaafy.

➡ Na kila kauli katika Kauli mbili hapa zina hoja katika fatwa kwa mujibu wa dalili.

➡ Nitatoa kwa ufupi dalili kama ifuatavyo :

1. Waliosema ni wajibu kutoa Zaka wametumia hadithi isemayo :

1 – كنت ألبس أوضاحا من ذهب فقلت يا رسول اللهِ أكنز هو فقال ما بلغ أن تؤدى زكاته فزكي فليس بكنز”

الراوي: أم سلمة هند بنت أبي أمية المحدث: أبو داود – المصدر: سنن أبي داود – الصفحة أو الرقم: 1564

➡Amesema Ummu salama r.a, nae ni Hindu bint Abii umayya: “Nilikuwa nikivaa pambo la fedha, Nikasema : ” Yaa rasuula llaah; je hii ni mali iliyolimbikizwa? Akasema mtume s.a.w : ” Ikifikia kiwango cha zaka itolee zaka itakuwa si katika mali iliyolimbikizwa “

2 – حديثُ عائشةَ: أنَّها دخلَت على رسولِ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ فرأى في يدِها فَتخاتٍ من ورقٍ فقالَ: ما هذا يا عائشةُ؟ فقالت: صنعتُهُنَّ أتزيَّنُ لَك بِهِنَّ يا رسولَ اللَّهِ، قالَ: أتؤدِّينَ زَكاتَهُنَّ؟ قالت: لا. قالَ: هوَ حَسبُك من النَّارِ”

الراوي: عائشة أم المؤمنين المحدث: ابن حجر العسقلاني – المصدر: التلخيص الحبير – الصفحة أو الرقم: 2/764
خلاصة حكم المحدث: إسناده على شرط الصحيح

➡Amepokea imaamu ibnu hajar hadithi kutoka kwa Bi Aisha r.a, amesema : ” Akiingia mtume s.a.w kwa Bi Aisha r.a, na mkononi mwake palikuwa na pambo la madini ya dhahabu, akasema mtume s.a.w :
” Nini hii Ewe Aisha?

Nikasema : ” Nimejiwekea hii kuwa najipamba kwa ajili ya ki Yaa rasuula llaah” Akasema mtume s.a.w :
” Je unaitolea zaka yake?

Nikasema : ” Hapana “
Akasema mtume s.a.w :
” Inakutosha kuwa ni moto “

2. Amma waliosema kuwa si wajibu, hoja zao kwa kufupisha ni kama ifuatavyo :

Amepokea imaamu daaru qutny kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah Al answaary r.a, amesema mtume s.a.w

1 – ليسَ في الحليِّ زكاةٌ”

الراوي: جابر بن عبدالله المحدث: الدارقطني – المصدر: سنن الدارقطني – الصفحة أو الرقم: 2/276
خلاصة حكم المحدث: [فيه] أبو حمزة ميمون ضعيف الحديث

” Hakuna katika mapambo zaka “

➡ Lakini hadithi hiyo ina udhaifu katika mmoja wa wapokezi wake, ambae ni Abuu Hamza, maimuun.

2 – Pia wametumia hoja katika aya iliyotaja adhabu kwa wenye kulimbikiza mali zao, kuwa aya hiyo haikutaja wingi wa dhahabu au uchache wake.

Na bila shaka hadithi za mtume s.a.w zimetaja kiwango maalumu kinachowajibika ndani yake zaka.

➡ Na kama zaka ya mapambo ingekuwa ni lazima basi ingewajibika adhabu hata kwa ambae anamiliki dhahabu kidogo, kwa sababu aya haikutaja kiwango.

➡ Na pia ziko hadithi walizotumia kuwa ni hoja juu ya kutowajibika zaka ya mapambo ya mwanawake, lakini hadithi hizo zina ikhtilafu katika kuthibiti kwake.

➡ Khulaswa ni kuwa kuna Kauli mbili kama tulivyotanguliza mwanzo, na kila kauli ina hoja zenye nguvu .

➡ Dk Abdul kariim ziidaan na sheikh yuusuf al qardhwaawy wamepasisha kauli ya kutowajibika zaka ya dhahabu na fedha ambayo ni katika mapambo ya wanawake.


Kwa yote hayo yaliyotangulia, fanya yafuatayo :

1 – Ikiwa unamiliki mali ya kuweza kutoa thamani ya Zaka ya mapambo hayo, basi toa zaka hiyo, kwa kuwa zaka pia ni takaso kwako na baraka katika mali na nafsi yako.

2 – Na ikiwa huna uwezo wa kumiliki thamani ya mali ili kutoa kiwango cha zaka hiyo basi usinunue mapambo yatakayofikia kwangu cha kuwajibika zaka ya dhahabu au fedha.

➡ Na mapambo mengi ni moja katika uharibifu wa mali na inaweza kukupelekea katika ufakhari.

➡ REJEA VITABU VIFUAVYO :

1 – Al muutamad fii fiqhi l zzakaat, Sh Ahmad Alkhaliily na sh said al qannuby.

2 – Fiqhu zzakaat, sh al qardhwaawy juzuu ya 1.

3- Al mufasswal, cha Dk Abdul kariim ziidaan j1.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

Published By Said Al Habsy

SWALI

Nani walii wa mtoto wa nje ya ndoa ? au pia wazee wake wameoana lakini ni baada ya kuzaa kabla ya ndoa nani anasimama kuwa walii….baba yake inafaa na kama wazee wao wamemzaa bila ndoa na hadi sasa wazee wake hawajaona…..nani walii haswa wa mtoto wa nje ya ndoa ?

JAWABU

➡ Ndoa ni mafungamano sahihi na masafi kati ya mume na mke katika misingi mikuu ya sheria za kiisilaamu.

➡ Na kutokana na umuhimu wa mafungamano hayo, Uisilamu umeweka nguzo na masharti katika ndoa, ili kuhakikisha kufanikiwa maslahi na kuondoa maharibiko .

➡ Walii ni moja katika nguzo kuu za ndoa, na ni sharti katika kusihi ndoa hiyo, na hii ndio Kauli sahihi ya jamhuri ya maulamaa wengi.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ مِنْكُمْ طَوْلًا أَنْ يَنْكِحَ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ فَمِنْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ مِنْ فَتَيَاتِكُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ۚ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِكُمْ ۚ بَعْضُكُمْ مِنْ بَعْضٍ ۚ فَانْكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ

[Surat An-Nisa 25]

Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara.

➡ Hapo ameamrisha ALLAAH S.W kuwa waozeshwe kwa idhini ya watu wao miongoni mwa mawalii, na si ndoa za wahuni wenye ukahaba.

➡ Na walii hawezi kuwa ila katika upande wa ubabani tu, kama vile : vile baba wa mwanamke, au kaka zake wa upande wa baba na kadhalika. …

➡ Na hawa wote ni lazima wawe ni katika wenye nasabu na mke huyo nasabu za asili, si kutokana na natija ya zinaa.

➡ Baba ambae ndie mtoto wa zinaa anatokana nae yeye, hana haki kisheria kuwa yeye ni walii wa mtoto wa nje ya ndoa.

➡ Na mtoto huyo walii wake anakuwa ni kadhi wa kiisilaamu au ambae anatawalia mambo ya waisilamu na yeye mwenyewe ni muisilamu.

➡ Na ikiwa hakuna kadhi basi jamaa katika kundi la waisilamu wa mji watatoa hukmu na kuidhinisha ndoa hiyo.

➡ Na hii ndio Kauli sahihi inayotegemewa katika jamhuri ya maulamaa.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE WEMA KATIKA UHAI NA BAADA YA HAPO.

ALLAAHU AALAMU.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAN ALBATTAASHY

Published By Said Al Habsy

SWALI

Ustaadh ahsante sana kwa jibu la swali hilo hapo juu. Lakini sehemu ya pili hukuigusia … umesema tu aliye na dhahabu, hata ikiwa ni ya mapambo, bora kwake kuitolea zaka, ili kutoka katika ikhtilafu. Lakini sehemu hii ya pili ya swali inauliza:

” iwapo mtu amepewa zawadi, hakununua, na hana uwezo wa kulipia zaka, afanyeje ?

JAWABU

➡ Shukran sana kwa kunikumbusha sehemu ya swali hili.

➡ Tunapo zungumzia kuhusu mtu kumiliki dhahabu, tunamaanisha aina zote za kumiliki mtu mali .

➡ Miongoni mwa njia za kumiliki mtu mali ni :

1 – Kununua mwenyewe kwa mali yake.

2 – Kurithi mali hiyo kutoka kwa mtu wa karibu.

3 – Kupewa zawadi kitu hicho na kuwa milki yako…

➡ Kwa hiyo dhahabu aliyopewa zawadi mwanamke siku ya harusi, au amenunuliwa na mumewe, hiyo inahesabiwa kuwa imeshakuwa ni mali yake mwanamke kisheria.

➡ Kwa hiyo anatakiwa aitolee zaka kila baada ya kutimia mwaka mmoja tokea kumiliki kwake dhahabu hiyo.

➡ Na dhahabu na fedha inayowajibikiwa kutolewa zaka ni ile ambayo imetimia kiwango maalumu cha kuwajibika zaka.

➡ Kiwango hicho ni kama ifuatavyo :

1 – Dhahabu :
Ikiwa inatimia uzito wa gram themanini na tano”85″

2 – Fedha:
ikiwa imetimia uzito wa gram Mia tano na tisini na tano “595 “.

➡ Na kiasi ambacho anatakiwa kukitoa katika zaka hiyo ni robo ya kumi ya dhahabu aliyokuwa nayo mwanamke huyo.

Na hii hesabu yake inakuwa kama ifuatavyo :

* Uzito wa Dhahabu unayomiliki ÷ kwa 40 = Kiwango cha kutoa.

➡ Mfano :
Mwanamke ana dhahabu za kuvaa zenye uzito wa gram 120, atagawa hesabu yake kwa 120 ÷40 = 3

Kwa hiyo atatakiwa kutoa Zaka take ambayo ni gram tatu za dhahabu.

➡ Na yeye katika hilo ana khiyari kutoa dhahabu hiyo gram tatu, au atoe pesa ambayo kiwango chake linalingana na thamani ya gram tatu za dhahabu kwa mujibu wa bei ya soko kuu la dhahabu kwa siku hiyo.

➡ Na kama atakuwa hawezi kutoa dhahabu yenyewe, lakini akauza sehemu ndogo katika dhahabu anayo miliki, ambayo sehemu hiyo ni sawa na uzito wa kiwango kinacho muwajibikia, kisha pesa atakayoipata kwa gram hizo ndio akazitoa zaka, hivyo ni bora na itamtosheleza kuwa ametekeleza wajibu.

➡ Hii ndio fatwa ya maulamaa wengi.

➡ Na wako wengine wanajuzisha kuitolea zaka mwaka mmoja tu, kama alivyosema kauli hiyo Swahahabiy Anas bin Maalik r.a.

➡ Na Na amesema Imaamu al hasan al biswry na Abdullah bin utba, na Qataada, na pia kauli moja miongoni mwa kauli za imaamu Ahmad kuwa :
” Zaka yake ni kumuazina mwenzake avae dhahabu hiyo “.

➡ REJEA VITABU VIFUAVYO :

1 – Zinaa daaru abii said al kudamy, j2.

2 – Al muutamad fii fiqhi l zzakaat.

3 – Fataawa j1 ya samaahati shaikhinaa Ahmad bin hamad alkhaliily ALLAAH awahifadhi

➡NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.

ALLAAHU AALAMU.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAANI AL-BATAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Ustaadhi ningependa kuuliza na kufahamu; hivi kusali sunna nyumbani baada fardhi msikitini, inajuzu au ?

JAWABU

➡Sala za sunna ziko katika daraja mbalimbali kwa mujibu wa hadithi za mtume saw, na kwa mujibu wa sababu ya sunna hizo.

➡Kuna baadhi ya Sala za sunna sababu Zake ni lazima iwe katika msikiti.

➡Mfano huo ni rakaa mbili za maamkizi ya msikiti.

➡Amesema Mtume saw katika hadithi aliyo pokea Abuu Qataada Al answaary r.a : Hakika Mtume saw amesema :

– أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : إذا دخل أحدكم المسجد فليركع ركعتين قبل أن يجلس .

الراوي: أبو قتادة الأنصاري المحدث: البخاري المصدر: صحيح البخاري الصفحة أو الرقم: 444 خلاصة حكم المحدث: [صحيح]

“Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi asali rakaa mbili kabla ya kukaa kitako “

➡Hiyo ni hadithi ameipokea Imaamu Al bukhaary r.a na ni hadithi sahihi.

➡Sunna kama hii ikiwa mtu ataiswalia nyumbani Kisha akaenda msikitini, atakuwa hajapata thawabu ya sunna, kwa kuwa ameifanya sunna pahala ambapo si pake.

➡Na pia sunna ambazo zinakuwa kabla ya Sala za faradhi , ni bora Zaidi kuziswalia msikitini, ila sunna ya kabla ya faradhi ya alfajiri inajuzu kuiswalia nyumbani, Kisha ndio akaenda msikitini.

➡Pia sunna baada ya faradhi ya magharibi, inapendekezwa kuiswalia msikitini, kwa kuwa inatakiwa kuswaliwa baada ya faradhi bila ya kuchekewa.

➡Sunna nyingine zinafaa kuswaliwa nyumbani, kwa sababu ya kuodosha Hali ya kuhisi kujieonyesha kwa watu ikiwa atakhofia Hilo, Bali pia kupata kuwapa Mfano mwema wa kuigwa kutika family yake.

➡Na pia inafaa kuwaswalisha watu wa nyumbani Kwake Sala ya jamaa, baada ya kuwa yeye ameshaiswali Sala Hiyo msikitini.

➡Amepokea Ibnu Hibbaan kutoka kwa Jaabir bin Abdillaahi Al answaary r.a amesema :

كان معاذٌ يُصلِّي مع رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم ثمَّ يرجِعُ فيؤمُّ قومَه فيُصلِّي بهم تلك الصَّلاةَ
الراوي: جابر بن عبد الله المحدث: ابن حبان – المصدر: صحيح ابن حبان – الصفحة أو الرقم: 2404
خلاصة حكم المحدث: أخرجه في صحيحه

➡Akikuwa Muaadh bin Jabal r.a akiswali pamoja na mtume saw , Kisha anarejea na kuwa imaamu wa watu wake – nyumbani – anawaswalisha Sala ile – ambayo aliswali na mtume s.a.w.

➡kwa Hiyo hakuna kizuizi kuswaliwa Sala za sunna nyumbani kwa atakaetaka kufanya hivyo.

➡Na hasa Kuna hadithi inatihimiza kusali baadhi ya Sala majumbani mwetu , yaani Sala za sunna.

➡Ameipokea Imaamu Muslim kutoka Kwa Abdillaahi bin Omar r.a , amesema s.a.w:

اجعَلوا من صلاتِكم في بيوتِكم . ولا تتخِذوها قبورًا”

الراوي: عبدالله بن عمر المحدث: مسلم – المصدر: صحيح مسلم – الصفحة أو الرقم: 777
خلاصة حكم المحدث: صحيح

“Zifanyeni baadhi ya Sala zenu majumbani mwenu, na wala musifanye – majumbani yenu kuwa kama – makaburi “

➡NAMUOMBA ALLAAH
S.W AUJAALIE KUTEKELEZA FARADHI NA SUNNA ZA MTUME S.A.W.

“Zamani, walikuwa watu wema wakizifanya sunna kwa sababu ni sunna, zama hizi watu wanaziacha sunna kwa sababu ni sunna “

ALLAAHU AALAMU.

LIMEJIBIWA NA SH. SHAABAANI AL-BATAASHY.

Published By Said Al Habsy

SWALI 


kuhusu kadhia ya ndoa na talaka ni kuwa:” nilimpa talaka moja mke wangu, lakini kabla ya kumalizika eda nikamrudia, lakini baada ya kumtamkia kuwa nimemrejea yeye akanijibu kuwa hayuko tayari kurudiana na mimi, yaani amenikatalia, na tokea siku hiyo mpaka hii Leo bado ameshikilia msimamo wake ule ule, na sasa unaingia mwaka wa pili.
sasa ndoa ipo au vipi ?

JAWABU 

➡Mke alieachika talaka moja au mbili, mume anakuwa ndie mwenye haki ya kurejea , na wala mke hana haki ya kukataa ila kwa kuwepo sababu za kisheria.

➡Amesema ALLAAHU SW:
(وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنْفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَنْ يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِنْ كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ)
[Surat Al-Baqara 228]

Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka t’ahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuzii kuficha alicho umba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu. Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

➡Ikiwa katika kumrejea kwako ulishuhudisha mashahidi wawili waisilamu wanaume, au mwanaume mmoja na wanawake wawili, japokuwa katika ndugu zake, basi mke atakuwa tayari wewe umeshamrejea.

➡Na hii ni kauli ya baadhi ya maulamaa , na ndio kauli sahihi inayotegemewa katika madhehebu ya ibaadhi wote.

➡ Na kauli hii ni kutokana na kuwa, kushuhudisha katika kumrejea mke ni wajibu katika madhehebu hayo, na wala haisihi kumrejea ila Kwa kufanya hivyo.

➡ Na hoja Yao ni kauli ya Allaah sw kuhusu kuwarejea wake walio achika wakati ambao muda wao wa eda unaekekea kukamilika :

(فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِنْكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا)
[Surat At-Talaq 2]

Basi wanapo fikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyo agizwa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea.

➡Amma jamhuri ya maulamaa wengine wao wanaona Kuwa: “kumrejea mke si sharti la lazima ili kusihi kurejea kwake “

➡Kutokana na hayo, ikiwa umemrejea kwa kumtamkia maneno yenye kumaabisha kumrejea, basi huyo anakuwa ni mke tayari, hata kama atakataa kurejewa wakati muda huo yuko ndani ya eda.

➡Dhaahiri ya suala inaonekana kuwa, mke ana sababu zake ambazo anaona kuwa yeye hawezi kuendekea kusihi na mumewe, au mke huyo hajui kuwa mume ana haki zaidi ya kumrejea wakati wa eda kuliko yeye mwanamke kukataa kurejewa.

➡Na kwa nini mume amekaa muda wote huo na wala haulizi suala kama hili mpaka inafika miaka miwili?

➡Je wewe mume hujui kama unapoteza haki zako na haki za mkeo ndani ya masiku hayo pia?

➡Nakushauri yafuatayo:

1- kufanya sulhu baina yako na mkeo kwa wema na ihsaani.

2- Washirikishe wazazi wako na wazazi wake katika sulhu hiyo.

3- Pia ikiwezekana kuwepo mtu mwenye elimu ya sharia za kiisilamu na mwenye hikma katika maamuzi, basi hivyo ni bora zaidi.

4 – ikiwa hakukubali baada ya yote hayo, na wala wewe hukuwa ukimfanyia madhara yoyote katika ndoa, basi wewe mume una haki ya kushitaki kwa kadhi wa kiusilamu.

Kwa kuwa wewe una haki na mkeo katika muda huo wa eda, na mke hana haki ya kukataa kurejewa ila kwa kuwepo sababu za kisheria, ambazo zinazingatiwa kuwa zinamruhusu kukataa kurudiana na mumewe.

➡ALLAAHU AALAMU.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW AWATENGENEZEE NDOA YAO, NA AWAHIFADHI WAO NA WAISILAMU WENGINE WOTE PIA.

LIMEJIBIWA NA SH.SHAABAAN AL-BATAASHI.

Published By Said Al Habsy

SWALI

Naomba kujua Kuhusu sala ya suna ya al Fajir ambayo inatakwa tusome surat l Fat ha,Kafiruun na Ikhlas.

Je ikiwa unasali baadaye katikati ya sala ukajihisi unasoma sura nyengine hukumu yake nini ?

JAWABU

➡Asili ya kusoma sura nyingine baada ya alfaatiha katika sala ni kuwa : “inajuzu kusoma sura yoyote miongoni mwa sura za Qurani baada ya alhamdu”

➡Na dalili ya hayo ni kauli ya Allaah sw kuhusu sala za kisimamo cha usiku :

(إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِنْ ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِنَ الَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَاللَّهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَنْ لَنْ تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ ۚ عَلِمَ أَنْ سَيَكُونُ مِنْكُمْ مَرْضَىٰ ۙ وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِنْ فَضْلِ اللَّهِ ۙ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ ۚ …ٌ)
[Surat Al-Muzzammil 20]

Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur’ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo…”

➡Lakini ziko baadhi ya sala zimetajwa katika hadithi za Mtume saw sura maalumu za kusoma ndani yake.

➡ Na miongoni mwazo ni hii ulitoitaja katika suali lako , katika sunna ya alfajiri,

rakaa ya kwanza unasoma surata l faatiha, na surata l kaafiruun ( Qul yaa ayyuha l kaafiruun,

Na rakaa ya pili alfaatiha na ikhlaasw ( Qul huwa llaahu ahad ).

➡Ikiwa atakosea katika kusoma kwake akachanganya Aya ya sura hii na aya ya sura nyingine, sala yake itakuwa sahihi inshaallaah, ikiwa atafanya hivyo Kwa kusahau au kukosea.

➡Lakini kusihi Kwa sala hiyo ni Kwa sharti, nalo ni kuwa : “Kukosea kwake kuwe hakusababishi kuharibika maana ya aya “

➡Amma ikiwa atachanganya na maana ikaharibika, basi na sala pia itaharibika .

➡Mfano ameanza kusoma aya inahusu waumini waliotenda matendo mema, Kisha akahitimisha Kwa kusoma aya inathibitisha kuingia motoni , hapo itakuwa kukosea huko kuna haribu sala yake.

➡ikiwa ni kinyume na hayo basi sala yake itakuwa ni sahihi bi idhini llaahi taalaa.
➡Na hiyo pia ni fatwa katika fatwa za imaamu Nuuru ddiin al ssaalimy r.a.

➡NAMUOMBA ALLAAH SW ATUWEZESHE KUHUISHA SUNNA .

ALLAAHU AALAMU.

” Uisilamu dini ya wepesi katika sharia zake “

JAWABU KUTOKA KWA
SH. SHAABANI AL BATTAASHY.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Ndugu Khamis Aziz kutoka Tanzania anauiza:

Swali:

Chanzo cha madhehebu katika uislam ni nini? Nani kaleta haya makundi kwa sababu Qur-an haikutaja sunny wala ibadhi.

JAWABU:

Kwanza: Tujue kuwa Madhehebu kiasili ni neno la Kiarabu, na maana yake kwa kiswahili ni Maendeo, pia Maelekeo, na katika sheria ni mafundisho au msimamo uliotafautiana na wengine katika jambo moja.

Pili: Madhehebu yanapatikana katika yale aliyoingiwa na tafauti kubwa peke yake, kwani tafauti ndogo ndogo zinapatikana hata katika madhehebu moja.

Tatu: Madhehebu vyanzo vyake vikuu ni vitatu:

 1. Siasa: Hii ni moja ya sababu kuu iliyowagawa Waislamu katika Karne ya mwanzo baada ya kufa Mtume S.A.W kwa miaka 27 tu, waligawika Waislamu kwa kunusuru viongozi wa kisiasa waliodhihiri katika jamii, na wengine walijiweka katika kunusuru haki tu bila kujali kiongozi fulani, basi walipatikana watetezi wa Muawiyah aliyeangusha utawala wa Khalifa wa nne Imam Aliy bin Abi Twalib, pia walipatikana watetezi wa Aliy bin Abi Twalib aliyekubali suluhu na Muawiyah iliyopelekea kudhoofika kwa utawala wake hadi kuanguka, pia Walipatikana Muhakkimah nao ni wale waliojitenga kwa kuona kuwa sulhu ya Aliy na Muawiyah ni batili na kuwa suluhu hiyo ni uvunjaji wa wazi wa hukumu ya Allah mtukufu, nao hawa wakachagua kiongozi wao ambae ni Imam Abdullahi bin Wahab Arraasibi (R.A). Kwa upande wa watetezi wa Muawiyah zilipatikana baadae Madhehebu za Kisunni maarufu, na kwa upande wa watetezi wa Aliy zilipatikana baadae Madhehebu za Kishia, na kwa upande wa watetezi wa Muhakkima zipatikana baadae madhehebu za Muhakkimah na miongoni mwa Madhehebu zake ni Ibadhi.
 2. Vyuo vikuu vya Maimamu: Katika mgao wa Kisiasa uliotokezea katika kila upande kulipatikana Maimamu wa kielimu walioheshimika sana katika jamii zao, Maimamu hawa walikuwa na wanafunzi wao na walikuwa ni marejeo katika jamii zao, Maimamu hawa walitafautiana katika mambo ya Kiitikadi, Kimatendo na Kifikra pia, na baada ya Maimamu hao kufariki wafuasi wao wakiwa ni wanafunzi na wapenzi walitetea kauli za Maimamu wao na kuziwekea dalili na kuzilingania, na hapa ndio yakapatikana majina ya kimadhebu kama unavyosikia leo: Ibadhi, Hanafi, Maliki, Shaafii, Hanmbali, Jaafari, Zaidi, n.k. Kwa kweli madhehebu hizi zilipatikana kwa wingi lakini nyengine zilikosa watetezi na kutobakia maadniko yao kama vile Makhawariji (Azaariqah, Najidiyah, Sufroyah), na nyengine zilikosa watetezi na kubakia vitabu vyao kama vile Dhaahiriyah na Muutazilah.
 3. Ufahamu wa maandiko na kuthibiti kwa hadithi: Hili linakuja katika ufahamu wa Aya au Hadithi baina ya wanavyuoni tafauti, na hayo ni kwa kuona kila mmoja kua ufahamu wake wa dalili ni sahihi, na ikiwa katika Itikadi athari yake hua nzito; kwani kila upande huukosoa upande mwengine na kuuona kuwa ni batili, ama ikiwa katika masuala ya matendo (Fiqhi) athari zake hua nyepesi kwani nia ndio asili. Ama hadithi inaweza hadithi ikakubalika kwa upande fulani na kuiitakidi kuwa ni Sunna wakalizimika na mafundisho yake, na upande mwengine ukaiona hadithi hio hio kuwa sio sahihi haikuthibiti kwa hiyo si Sunna na hilo hupelekea kutoaizingatia katika mafundisho yake.

Hizi ndizo sababu kuu zilizopelekea kupatikana Madhehebu tafauti katika safu za Waislamu; kwa hiyo uhakika ni kuwa kila Madhehebu ni sawa na chuo kilichojitegemea katika kuusoma na kuufahamu uislamu kiitikadi kifiqhi na kifikra kwa ujibu wa misingi inayotetewa na wafuasi wake.

Ama kuhusu Quraani kuwa haikutaja Sunni wala Ibadhi, hili halina tafauti ndani yake kuwa Quraani haikutaja Sunni wala Ibadhi wala Shia wala Madhehebu yoyote, na kupatikana Madhehebu tafauti si kwa msingi wa kutajwa ndani ya Quraani, lakini ni kwa msingi wa matokeo ya uhakika wa kijamii, na kuhusishwa kila chuo na mafundisho yake na matokeo yake na wahusika wake ni uadilifu uliotajwa katika Quraani (Na hatabeba mbebaji mzigo wa mwengine) (Sema: Kila mmoja anafanya kwa namna yake na Mola wako ndiye ajuae aliye katika njia ya uongofu zaidi), vile vile Quraani imetutajia Muhaajiriina na Ansaari, pia  imetuekea bayana ya kupatikana Waumini na Wanafiki, yote hayo ni kuzingatia uhakika wa matokeo kama yalivyo; kwa hiyo kupatikana kwa Madhehebu tafauti ni uhakika wa matokeo usioweza kuepukika, kama ukisema leo kuwa wewe hutaki madhehebu utawaita vipi waliokubali madhehebu?! Ukiwakubali kuwa ni waislamu basi tayari umeshakiri umadhehebu na kuwa hapo ulipo pia kiuhakika ni madhehebu; kwani umetafautiana na wengine katika jambo moja.

Kutokana na hapo utagundua kuwa Madhehebu ni tafauti ya kitabia na kimaumbile, na udhaifu wa waislamu si kwa kupatikana madhehebu tafauti, lakini ni kwa kutoheshimu tafauti zilizopatikana katika jamii zao na kupatikana mafundisho ya kufanyiana uadui na kuchukiana, na hayo yanawahusu wale wenye nayo katika Mafundisho ya Madhehebu zao tu; kwa hiyo mwenye kuwatakia nguvu na umoja waislamu wote apige vita mafundisho ya kuchukia na kuwakandamiza waislamu wengine, na ajiondoshe katika safu za Madhehebu hizo.

Ibadhi katika mafundisho yetu ni kuheshimu wafuasi wa madhehebu yengine za Kiislamu kijamii, na hayo yanapatikana katika yote tuliotafautiana ndani yake, na tarehe ya Ibadhi ni shahidi bora katika hili, basi Ibadhi hatuna misingi ya kuwafanyia ubabe, uadui, na uhasama wote waliotafautiana na sisi, kutokana na hapo utatukutia tunaishi na wafuasi wa madhehebu yengine kwa ushirikiano na kuwatuzia haki zao, na hata kama tutakandamizwa sisi hatukandamizi, hukutii katika mafundisho yetu -katika yale yaliyoingiwa na tafauti za Kimadhehebu- kuwa asiyekubali neno letu ima atubie au akatwe kichwa (chinjachinja), hayo kwetu hakuna, na hiyo sio njia yetu.

Aliniambia Msalafi mmoja kuwa Ibadhi inaona wale waliotafautiana na wao katika Itikadi ni Mafasiki, na Mafasiki ni motoni milele.

Nikamuambia: Wewe ikiwa ni Msalafi, hivi Itikadi ya Kiibadhi -katika tuliyotafautina ndani yake- itakudhuru nini huko Akhera na wewe unaiona kuwa ni batili?!!!! Mimi ni Muibadhi sioni kuwa Itikadi yako -katika tuliyotafautina ndani yake- itanidhuru kitu huko Akhera; kwani naiona kuwa ni batili.

Nikamuuliza: Jee! Umeona katika Itikadi ya Kiibadhi himizo la kuwafanyia uadui wasiokua Ibadhi katika jamii?

Akasema: Hapana.

Nikamuambia: Huu ndio wajibu wa kuheshimiana katika jamii ili tushirikiane katika tuliyokubaliana, na katika tuliyotafautiana kila mmoja amuheshimu mwengine na yafafanuliwe kidalili, na hukumu yake ni huko Kiama mbele ya Allah mtukufu. Na hiyo ndiyo nguvu ya kuwa pamoja.

Wabillahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Ndugu Athumani Mlimbo kutoka Tanzania anauliza:

SWALI:

IBADHI WANA MSIMAMO GANI KUHUSU KUAMINI MAKHALIFA WANNE WANAOAMINIWA NA AHLU SUNNA NA MAIMAMU KUMI NA MBILI WANAOFATWA NA MASHIA?

JAWABU:

Ibadhi tunakubali Makhalifa wanne wa mwanzo, na tunaitakidi kuwa wao ni viongozi sahihi waliochaguliwa kwa misingi sahihi ya Uislamu baada ya kufa Mtume wetu Muhammad S.A.W, nao ni kuanzia Abu Bakar bin Abi Kuhaafah kisha Omar bin Al-Khatwab kisha Othaman bin Affaan kisha Aliy bin Abi Twalib, wala hakuna tafauti kuhusu hili katika safu za Ibadhi, lakini Ibadhi tunatafautiana na Ahalu Sunna katika suala la kutetea makosa yaliyotokezea katika vipindi vya uongozi wa Othman na Aliy kwa mwenye kuyajua na kuthibiti kwake bila ya wasi wasi, kwani hakuna katika Ibadhi msingi wa upendeleo, basi wako baadhi ya wanaelimu wetu waliozungumza makosa yaliyotokezea katika miaka sita ya mwisho ya kipindi cha uongozi wa Othman bin Affaan, pia wako waliozungumza makosa yaliyotokezea katika kipindi cha uongozi wa Aliy bin Abi Twalib nayo ni mawili tu:-

 1. Kosa la kwanza: Kuvunja kwake hukumu ya Allah ya kulipiga vita kundi la waasi mpaka kuzima uasi wao, na sio kufanya nao suluhu kama alivyofanya nao Aliy.
 2. Kosa la pili: Kuwapiga vita Ahalu Naharawani -Allah awaridhie- baada ya kuanguka kwa uongozi wake kwa mujibu wa matokeo ya suluhu aliyoiingia mwenyewe kati yake na kundi la Waasi wa Shaam lililoongozwa na Muawiyah bin Abi Sufiayan.

Ama kuhusu Mashia, kwa hakika wao ni makundi yaliyotafautiana, na yote yamejikita katika kumtukuza Aliy bin Abi Twalib na ulazima wa kuteua viongozi katika uzao wake tu kupitia Hassan kisha Hussein kisha waliofuatia katika kizazi cha Hussein, basi wao wanaona kuwa hao ndio Warithi wa Uongozi baada ya Mtume S.A.W, hadi kufikia kudai kuwa hao ni Maimamu Maasumina yaani waliohifadhika na uwezekano wa kukosea. Na Mashia wametafautiana katika hilo, kwa mfano Mashia wa Kizaidiyah wanawakubali Makhalifa Abu Bakar na Omar R.A na wanawaridhia, wanasema kuwa Aliy ni bora zaidi kuliko hao, na kuwa Aliy ndiye aliyekua na haki ya uongozi zaidi kuliko hao, kwa upande mwengine tunakutia Mashia Imamiyah Ithnaashiria wao hawawakubali kabisa Makhalifa watatu na kufikia kuwakufurisha hasa.

Muhimu ni kuwa Ibadhi tunatafautiana na Shia katika suala zima la kuzingatia msingi wa ukoo katika uongozi, si Uhashimu, wala Uali, wala Uhassan, wala Uhussein, kama tulivyotafautiana na Ahalu Sunna katika kuufunga kwao Uongozi na kabila la Uquraishi tu.

Pia tafauti iliyopo kati yetu Ibadhi na Ahalu Sunna ukichanganya na Mashia, ni kuwa Ibadhi tunamtambua Imam Abdullah bin Wahbi Al-Raasibi R.A aliyechaguliwa kwa Shuura na wale waliojitenga kwa kutokubali kwao kushiriki katika kosa la kuvunja hukumu ya Allah lililofanywa na Imam Aliy bin Abi Twalib K.A.W, basi tunasema kuwa Imam Abdullah bin Wahbi Al-Rasibi R.A ni Kiongozi wa haki, na kupigwa vita Ahalu Naharawani kulikua ni batili, na kuwa Imam Abdullah bin Wahb Al-Rasibi na waliouliwa pamoja naye walipata shahada ya haki katika sehemu iitwayo Naharawan ndani ya Iraq, Allah awaridhie.

Kwa hakika Ahalu Naharawani R.A kwetu sisi ni alama ya kushikamana na Kitabu cha Allah mtukufu wakati wengine wakishikana na maoni yao binafsi.

Vile vile Ibadhi hatuufungi Uongozi sahihi wa Kiislamu kwa hao Makhalifa wanne tu, kwani tunamkubali Khalifa Omar bin Abdulaziz R.A, pia Maibadhi walitoa Baia (Ahadi ya kufungana na uongozi) ya Kisheria kwa Maimamu Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya Shuura walioongoza kwa Uadilifu, nao ni wingi unaweza kuwajua kwa kufuata kiunganishi kwa kubofya hapa.

Wabillahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Aslamu alaykum.

Tunaomba mutusaidie hili suala:

Nataka kuchinja udh-hiya, lakini sijui wakati gani nichinje na vipi namna na kutoa sadaka hiyo au haina masharti yoyote?

Shukran.

JAWABU:

Kwa hakika kuchinja Udh-hiyah kuna fadhila kubwa sana ndani yake, kwani ni kuadhimisha matukuzo ya Allah kwa aliyoruzuku katika neema zake za wanyama wa miguu minne, nalo ni alama kubwa ya uchamungu kama alivyobainisha hayo Allah mtukufu, basi Allah mtukufu amemuamrisha Mtume wake S.A.W kwa kumwambia: ((Basi sali kwa ajili ya Mola wako na uchinje)) [Al-Kauthar 2] na katika Aya hii tukufu kuna dalili ya wazi kuwa kuchinja sadaka ya Udh-hiya ni baada ya kusali sala ya Iddi, nayo ndiyo aliyosema Mtume S.A.W: ((Atakaechinja kabla ya sala huyo amejichinjia kwa nafsi yake, atayechinja baada ya sala huyo amepatia sadaka yake na ameipata Sunna ya Waislamu)) [Bukhari 5556].

Na kichinjwa cha Udh-hiya ni katika wanyama wa miguu minne tu, nao ni Ngamia, N`gombe, Mbuzi, na Kondoo, na ufuatao ni ufafanuzi wa umri wa kichinjwa na kwa wanaotoshelezwa, zingatia kama ifuatavyo:

Ngamia: Uchache mwenye kutosheleza ni aliyetimiza miaka miwili.

Miaka 2 kwa mtu mmoja.

Miaka 3 mpaka miaka 5 kamili kwa watu watano.

Zaidi ya miaka 5 na kuendelea kwa watu saba. 

N`gombe: Uchache mwenye kutosheleza ni aliyemo katika mwaka wa pili.

Miaka 2 kwa mtu mmoja.

Kuanzia mwaka wa 3 mapa wa 4 ni kwa watu watatu.

Akiwa katika mwaka wa 4 kwa watu kwa watano.

Zaidi ya miaka 4 na kuendelea watu 7.

Mbuzi: Miaka 2 na kluendelea kwa mtu mmoja.

Kondoo: Katimiza mwaka 1 na kuendelea kwa mtu mmoja.

 TANBIHI:

 1. Tukisema kuwa inamtosheleza mtu mmoja makusudio ni yeye na watu wa nyumba yake ikiwa anao, yaani wale walio chini ya matumizi yake ya lazima katika nyumba yake.
 2. Nyama ya kichinjwa cha udh-hiya kinagawiwa mafungu matatu, fungu la kula mwenyewe mwenye kuhusika na Udh-hiyah, fungu la pili ya limbikiza mwenyewe mwenye kuhusika na Udh-hiyah kwa siku zijazo, na fungu la tatu anatoa sadaka kwa masikini na marafiki na walio wa karibu.
 3. Asili na ndio Sunna kuwa sadaka ya Udh-hiyah inatekelezwa pale anapoishi mwenyewe mwenye kuhusika na Udh-hiyah, basi mwenye uwezo wa kujikurubisha zaidi kwa Allah anayo pia nafasi nzuri ya kuwachinjia mafakiri wa kiislamu na masikini ikiwa wapo sehemu alipo au wako mbali na pale alipo lakini hayo ni baada ya kuhakikisha asili ya kuchinja yeye mwenyewe au kushirkiana na wengine katika sehemu anayoishi.

Mwisho tunawatakia siku njema za kumi za mwanzo za mwezi huu wa Dhul-Hijja na tunakumbusha kuwa Funga ya Afara ina fadhila kubwa sana pia Allah ametuambia hukusiana na vichinjwa vyetu vya Sadaka ya Udh-hiya:

((Hazimfikii Allah nyama zake wala damu zake, lakini unamfikia uchamungu wenu, namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Allah kwa alivyo kuongoeni, na WABASHIRIE WENYE KUFANYA MEMA)) [Al-Hajji 37]

Kwa hakika bishara ya Allah ni kubwa mno katika sadaka hii ya Udh-hiyah, kwa mwenye kukusudia uchamungu.

Allah atutakabalie mema yetu na atufunikie tuliyoteza na alete taufiqi yake katika yote anayoyaridhia.

Wabillahi Taufiiqi. 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Yametufikia Masuali kutoka kwa Ndugu Ismail kutoka Tanzania, nayo ni kama yafuatayo:

 1. Nimefuatilia kitabu kilichosambazwa Tanzania kuwajeruhi Wahabism, sunni na wengine. Mbona mkifika Makka Mwawafuata?. Hili si itakuwa ni non sense. Mji wa Oman haukutajwa katika miji mitukufu hata chembe. Kulazimisha itasaidia nini?.
 2. Nyinyi mumepata wapi katika quran au Hadith sahihi ruhusa ya kuanzisha madhehebu?.
  Hebu tajeni wapokezi wenu wa Hadithi, manake hawa wenzenu huku Tanzania, hawaeleweki. Wanatumia Bukhari na Muslim pia. Wakati nimesoma kitabu chenu kimoja, kuwa muna wapokezi wenu specific wa hadithi. Hebu nitajieni angalau Wapokezi saba. Nina shida nao sana kuwajuwa.
JAWABU:

Ni vizuri tuelewe kuwa mazingatio katika Uislamu ni dalili, na sio sehemu (Miji) wala watu, na ndio maana Allah mtukufu ameteremsha Kitabu Quraani tukufu na kutuma Mtume S.A.W na kutuamrisha kumtii Allah na Mtume S.A.W, na kutuambia kuwa ambaye atakae kengeuka katika utiifu basi Allah hapendi Makafiri, bila shaka hukumu hiyo ya Allah ni sawa kwa wote wanaoishi Makka na Madina na Oman na Tanzania, kwa hiyo katika hilo watu wa miji yote ni sawa, wabora wao ni wenye kufanyia kazi mafundisho bila kuzingatia wapi walipo au kabila walilo, na sisi mpaka hivi sasa hatujaona ulazima wa kuwa haki ni lazima iwe Makka na Madina, na uhakika unajieleza kuwa hiyo ni Miji basi wenye nguvu za kuitawala katika kila zama waliitawala bila kuzingatia kama ni wahaki au ni wabatilifu, na tarehe inatueleza kuwa miji hiyo ilitawaliwa na wafuasi wa madhehebu tafauti.

Ama kufuata kwetu Maimamu wenye kusalisha katika Misikiti ya Miji hiyo hali ya kuwa wao si Maibadhi kimadhehebu, hilo ni kwa kuzingatia mafundisho ya Mtume S.A.W pale alipotuambia:

((Salini nyuma ya mwema na muovu, na msalieni mwema na muovu))

Kwa hiyo tunasali nyuma yao kuwa kuzingatia kuwa Uislamu unatukusanya pamojaو na sio kuwa wao wako katika haki katika yale waliotafautiana na Ibadhi.

Ama kuhusu Oman hakika yanatosheleza yale yaliyomo katika Sahihi Muslim kuwa Mtume S.A.W amesema:

((Lau watu wa omani uliwaendea basi wasingalikutukana wala kukupiga))

[Muslim 2544]

Na bila shaka Mtume S.A.W anawajua zaidi Waomani.

Inafaa turejee tarehe tuone kuwa Uislamu ulienea Oman na kukubalika katika safu na miji ya Waomani kwa hiari zao, hali ya kuwa Maquraishi wa Makka bado wanampiga vita Mtume wetu S.A.W.

Ama kuhusu kuanzisha Madhehebu, tunasema kuwa kupatikana kwa Ibadhi ni kwa njia ya kulazimika kubakia katika asili ya Uislamu na kukamatana na haki wakati wengine wakijifanyia vikundi vyao na madhehebu zao, kwa hiyo sisi tunasema yoyote atayejitoa katika madhehebu zote atajikutia yupo katika Ibadhi.

Ama kupatikana Madhehebu tafauti katika safu za Waislamu hilo ni jambo la kitabia kwa sababu za tafauti ikiwa ni za Kisiasa au Mizani ya kukubali hadithi kuwa ni Sunna na ufahamu wa maandiko ya Kisheria (Quraan & Sunna).

Ama kuhusu kutumia Hadithi zilizopokewa na wasiokua Ibadhi kama vile Bukhari na Muslim au wengineo, hayo ni kwa sababu Ibadhi haijajikomelea milango ya kukubali haki ikiwafikia, na Ibadhi hawaangalii aslan nani kapokea wala nani kasema wanachoangalia Ibadhi ni uhakikisho wa kidalili, basi Hadithi zilizo sahihi kwa mujibu wa Manhaj ya Ibadhi hizo zinakubalika hata kama kapokea Msunni au Mshia, sisi tafauti yatu na wengine ni katika yale waliyoikosa haki ndani yake si katika yale waliyoipatia haki ndani yake.

Ama kuhusu wapokezi wa Hadithi waliomo katika vitabu vya Ibadhi unaweza kurejea katika sehemu ya Hadithi za Mtume S.A.W katika website www.ibadhi.com utapata Hadithi za Al-Imam Rabii bin Habiib Al-Basri R.A, ambaye kafariki kabla ya kuzaliwa Bukhari wa miaka.

Wabillahi Taufiiq.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

SUALI:

Vipi inakua toba ya Mzinifu?

JAWABU:

Mzinifu anatubia kwa Allah mtukufu kwa kuwa mkweli wa dhati (Ikhlaas) katika Toba yake, na Allah anakubali toba yake na anasamehe dhambi yake, kwani yeye ndiye aliyesema: ((Na ambao hawaombi pamoja ya Allah mungu mwengine, wala hawaui nafsi ambayo Allah ameharamisha isipokua kwa haki, wala hawazini, na mwenye kufanya hayo atapata lawama * Ataongezewa adhabu siku ya Kiama na kubakia humo dhalili * Isipokua mwenye kutubia na kuamini na kufanya matendo mema, basi hao Allah anabadilisha mabaya yao kuwa mema…)) [Furqaan 68 – 70].

Na katika Hadithi aliyoipokea Imam Rabii R.A kutoka kwa Abu Ubaidah R.A kutoka kwa watu katika Masahaba R.A hakika Nabii S.A.W amesema: ((Dhambi ni aina mbili, dhambi baina ya Mja na Mola wake na dhambi baina ya Mja na mwenzake, basi dhambi ambayo ni baina ya mja na Mola wake mwenye kutubia anakua kama asiyekua na dhambi, na dhambi ambayo ni baina ya mja na mwenzake hakuna toba kwayo mpaka yarejeshwe yaliyodhulumiwa)) [Rabii 691]

Na kwa hayo:

 1. Ikiwa alizini na wanawake wenye akili waliobaleghe walio huru kwa hiyari zao hapo itamlazimikia kutubia na inatosha.
 2. Ama ikiwa alizini na mwanamke mwendawazimu (asiye kua na akili) au mtoto (Hajafika baleghe) au kijakazi (Mtumwa wa kike) au kwa kutumia nguvu na ubabe (kuwanya, kubaka) hapo itamlazimikia Ukuru katika kila mara aliyofanya hivo pamoja na kutubia kwake, na Ukuru ni nusu ya moja katika kumi ya dia kwa Thayib (aliyewahi kuingiliwa na mume), na moja katika kumi ya dia kwa Bikra (aliyekua hajawahi kuingiliwa na mume), na ikiwa kuzini kwake kumejulikana basi itamlazimu kutangaza kutubia kwake. Wallahu Aaalamu. [Rej. Al-Khalili – Fatawa Al-Aqiidah 2/328]. 
ZINDUO:

Dia ya kisheria ni Dinari za Dhahabu 1000.

Dinari 20 ni sawa na gramu 85.

Dinari 1000 itakua ni sawa na Gramu 4,250 za Dhahabu.

Basi moja katika kumi ya Dia ni Gram 425 za Dhahabu

Na nusu ya moja katika kumi ni Gram 212.5 za Dhahabu.

Hiyo au thamani yake ni haki ya aliyefanyiwa uadui, na kama ni mtoto au mwendawazimu anakabidhiwa walii wake kwa njia yoyote bila kujifedhehesha. 

Wallahu aalamu wabi Taufiiq.

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Tumeambiwa kuwa Ibadhi wanamchukia Othman bin Affaan R.A na kutokana na chuki zao kubwa dhidi yake wamefikia kutowaita watoto wao kwa jina la Othman, hivi hili lina uweli ndani yake?

JAWABU:

Waswahili wamesema: “Akutukanae hakuchagulii tusi”, na waarabu wamesema (Mtu ni adui wa asichokijua); kwa hiyo neno hilo limesemwa na msemaji wake kwa sababu ya chuki binafsi zilizotanda katika nafsi yake dhidi ya Ibadhi, na sisi upande wetu tunasema:

Kwanza: Hakika sisi mpaka hivi sasa hatujaona katika mafundisho ya Maulamaa wetu chochote chenye kuchukiza kupewa mtoto jina la Othman au yoyote katika Masahaba R.A.

Pili: Tunawambia hao wasemaji wasiyoyajua kuwa miongoni mwa Maulamaa wetu wakubwa wenye kutegemewa na kuheshimika sana katika Ibadhi ni Imam Othman bin Abi Abdillahi Al-Azri R.A nae ni maarufu kwa lakabu ya Al-Asamm, mwanachuoni huyu aliishi katika karne ya sita na ya saba Hijiria alifariki mwaka wa 631 Hijiria, naye ametuachia vitabu muhimu sana miongoni mwa hivo ni kitabu ANNUUR katika elimu ya Tauhidi.

Tatu: Ifahamike kuwa suala la majina katika Ibadhi halina uzito wowote, na watu wako huru katika kuwachagulia watoto wao majina wayapendayo, lililo muhimu kwetu jina lisiwe katika majina ya Washirikina; kwa sababu jina ni moja ya alama, basi tuwachagulie watoto wetu majina mazuri yenye maana nzuri na yasiyoleta utata wa kujulikana mtoto kuwa ni Muislamu.

Ama kuhusu Othman bin Affaan kwa upande wetu Ibadhi tunakubaliana kuwa yeye ni miongoni mwa Masahaba R.A, pia ni Khalifa wa tatu aliyefuatia baada ya Abu Bakar na Omar, pia ni mkwe wa Mtume wetu Muhammad S.A.W kwani alioa watoto wawili wa kike wa Mtume wetu Muhammad S.A.W nao ni Ruqaiyah R.A alipofariki akaoa Umu Kulthumu R.A na kutokana na hilo akapewa lakabu ya Dhu Nuraini, na Othman bin Affaan anayo mazuri mengi ya kuigwa aliyoyafanya katika Uislamu tokea kipindi cha Mtume S.A.W, lakini juu ya yote hayo anabakia Othman bin Affaan kuwa ni mkalifishwa asiyekua maasuum yaani upo kwake uwezekano wa kufanya dhambi kubwa na kubakia ndani yake bila ya toba, kwani Othmaan si Nabii, na mazingatio kwa waja ni yale ya mwisho wa umri wao wala si ya mwanzo yaliyotangulia ikiwa hayakumaliziwa kwa mwisho mwema, na katika yenye makubaliano na yasiyokua na shaka yoyote ni kuwa Othman bin Affaan aliuliwa na Waislamu katika mapinduzi ya kuangusha uongozi wake yaliyofanyika mwaka wa 35 Hijira, alizingirwa Othman katika ikulu yake kwa muda wa siku 40 akitakiwa aachie hukumu kwa usalama lakini alikataa na ndipo alipouliwa, na bila shaka washirki wote wa mapinduzi hayo si wengine ila ni Masahaba na Matabiina wakuu peke yao nao ndiwo waliomchagua Khalifa wa nne Aliy bin Abi Twalib K.A.W na kuwa katika safu zake, wengine wakachaguliwa kuwa Magavana wa miji kama vile Ashtar Al-Nukhaii na Muhammad bin Abi Bakar, pia Aliy bin Abi Twalib aliwapiga vita wote waliodai kisasi cha damu ya Othman bin Afaan, na katika hilo vilitokea vita viwili maarufu vya Jamal na Siffain.

Kutokana na hapo, wako baadhi ya Wanavyuoni wetu waliomuweka Othman  bin Afaan katika hukumu ya Baraa-a na kumsema vibaya kwa mujibu wa yale yaliyosihi kwao katika makosa waliyoyaona kuwa ni sababu ya Baraa-a, na bila shaka hukumu yao katika hilo ni alama ya kuenzi uadilifu wa Kiislamu bila ya upendeleo, na hilo limesihi hata kwa baadhi ya Masahaba kama vile Ammaar bin Yaasir R.A; kwani imekuja katika riwaya sahihi kuwa Sahaba Ammaar bin Yaasir R.A alikua akimsema vibaya Othman, akimsifu wa sifa za ufasiki katika mji wa Madina kama ilivokuja katika Twabakati Al-Kubra cha Ibnu Saad riwaya no 3619 na Musnad Imam Ahmad bin Hambal na kuisahihisha Al-Albani katika Silsila Ahaadithi Sahiha.

Basi sisi tunaridhia kuhukumiwa Maulamaa wetu hao kwa hukumu ya Sahaba Ammaar bin Yaasir R.A; kwani wanae wao katika hilo salafu mwema ambae ni Sahaba huyo Mbashiriwa Pepo Ammaar bin Yaasir R.A.

Juu ya yote hayo, tujue kuwa Ibadhi haijasimama juu ya msingi wa kumsema vibaya Othman bin Affaan wala yoyote katika Masahaba R.A, wala hakuna Muibadhi yoyote aliyeshurutishwa kumsema vibaya Othman wala yoyote katika Masahaba R.A ili awe muumini, na lau si shutuma mbaya tunazotupiwa basi tusingeliweka herufi moja ya kufafanua mambo yalivojiri na yalivotokea baina ya Masahaba R.A.

Wabillahi Taufiqi.

Wallahu aalamu wa ahakamu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Tumeambiwa kuwa mtenda dhambi kubwa hayakubaliwi matendo yake mema tunaomba ufafanuzi katika suala hili.

JAWABU:

Mtenda dhambi kubwa aliye mkaidi wa kutubia huyu ndiye ambae matendo yake mema hayakubaliwi mpaka atubie kwa Allah mtukufu, ((Hayo ni kwa sababu amefuata yanayomkasirisha Allah na kuchukia maridhio yake basi akaporomosha matendo yao)) [Muhammad 28]; kwa hiyo dhambi yake kubwa itakua ni kizuizi cha kunufaika yeye na mema yake iwapo atafikiwa na mauti naye hajatuibia, hayo ni kwa sababu Allah mtukufu ameshatuambia kuwa: ((Hakika Allah mtukufu anawakubalia Wachamungu)) [Maaidah 27] kama ilivyo katika kisa cha haki cha wana wawili wa Baba yetu Adamu A.S; kwani wote wawili walipeleka sadaka zao, basi yule mwana mchamungu sadaka yake ilikubaliwa na mwana mwengine asiyekua mchamungu sadaka yake haikukubaliwa, basi kila Muislamu anatakiwa ahifadhi mema yake kwa kujiuepusha na madhambi yote makubwa na kuharakisha kutubia iwapo ameteleza katika dhambi yoyote ile, na Allah anawapenda wenye kutubia na kujitoharisha.

Atujaalie Allah kuwa miongoni mwao na kupata mwisho mwema. Amin.

Wabillahi Taufiiq.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Assalaam ‘alaykum.

Naomba kueleweshwa kuhusu misingi ya dhehebu hili la ibaadhi, ambalo inasemekana ni dhehebu kongwe kuliko hili la Sunni.

Naomba kuelewesha misingi yake, maana huwa naona katika baadhi ya miji hasa kule bara, misikiti ya ibaadh inaitwa misikiti ya waarabu.

Nakuomba ndugu yangu Mohmd Sali, au mwingine yoyote anayeweza kunielewesha basi anipe elimu hiyo, tafadhali.

JAWABU:

Waalaykum salam wa rahmatullahi wa barakatuh.

Ni kweli madhehebu hii ya Ibadhi ni kongwe zaidi kuliko madhehebu za Kisunni, hili halina shaka ndani yake, kielimu Madhehebu ya Ibadhi inajishika na Imam wake Jabir bin Zaid Al-Uzdi Al-Omani aliyezaliwa Firq Oman mwaka wa 18 Hijiria naye alichukua elimu yake kwa Masahaba wa Mtume S.A.W moja kwa moja, na hakuna tafauti kuhusu uadilifu wa Imamu huyu na kuwa yeye ni mmoja wa Matabiina wakubwa waliobobea kielimu hadi kufikia Sahaba Ibnu Abbaas R.A kusema: “Ajabu kwa watu wa Iraqi, vipi wanatuhitajia sisi hali yuko kwao Jabir bin Zaid?!! Lau wangalimkusudia watu wa Mashariki na Magharibi basi ingaliwatosheleza Elimu yake.”

Kwa upande mwengine tunakutia unasibisho wa Madhehebu hii uko kwa Imam Abdullah bin Ibadhi Al-Tamimi R.A, naye kwa makubaliano aliishi -akiwa ni mwanaharakati wa upinzani dhidi ya Dola ya Bani Umayyah- katika zama za Masahaba R.A.

Pia Madhehebu ya Ibadhi haijawahipo kukosekana katika tarehe nzima ya Waislamu juu ya kushambuliwa na kufanyiwa uadui wa kivita na upotoshaji wa uhakika wake, nao uadui uliosababisha kumaliza uwepo wao katika baadhi ya miji kama vile Yemen na Hijaz, Maibadhi wengi waliuliwa kidhulma, pia kuchomwa moto vitabu vingi, na fatwa za kukandamiza Ibadhi mpaka leo hii bado hazijakatika, lakini juu ya yote hayo Ibadhi ilibakia kuwa ni mti uliokita vizuri kidalili na hoja bila kujiingiza katika dhulma za wengine, na kunufaika kwa matunda yake kila mtaka haki kwa dalili katika safu za Waislamu katika kila zama.

Ama misingi ya Madhehebu hii ni:-

 1. Kujifunga vizuri na Kitabu cha Allah mtukufu, na Sunna ya Mtume Muhammad S.A.W, na Malazimisho ya Kiakili.
 2. Kujiweka katika nafasi yenye usalama zaidi katika yale waliyotafautina Waislamu.
 3. Na kulazimika na uadilifu wa Kiislamu bila kujali upendeleo wa aina yoyote.

Ama kuhusu Misikiti ya Ibadhi kuitwa Misikiti ya Waarabu, na pengine kuitwa Ibadhi kuwa Madhehebu ya Waarabu, hilo halihusiani na Mafundisho ya Ibadhi, bali hayo ni kwa sababu ya wenyeji wa miji ya Uswahilini walipoona kuwa Misikiti hiyo inashughulikiwa na Waarabu wa Oman, pia hawajazoea kumuona Muibadhi asiyekua Muomani basi wao wenyewe wakajiwekea kizingiti hicho cha Uarabu ili kutokubali haki kwa dalili; kwani mwenyeji wa asili ya kiafrika akisikia kuwa Msikiti wa Waarabu na Madhehebu ya Waarabu huwa tayari ameshajiwekea kizuizi cha kinafsi baina yake na Ibadhi ikilichosimama juu ya misingi ya ubaguzi.

Na sisi tunawahakikishia watu wote, kuwa Ibadhi ni Madhehebu pekee katika Uislamu isiyobeba mafundisho ya kibaguzi, watu wote mbele ya Dini ni sawa, na kila mtu anayo haki ya kuwa Muibadhi bila kujali rangi yake wala kabila lake wala utaifa wake wala cheo chake wala mali yake, wako Maibadhi wengi sana ambao sio Waarabu wa Omani kama vile Maibadhi wa Algeria na Senagal na Mali na Libya na Tunisia, bali hata Afrika Mashariki wapo wenyeji wa asili ya Afrika walio Maibadhi.

Na ili tulijue hili kwa wazi kama tutatizama suala la kupatikana kiongozi wa kuongoza Taifa la Kiislamu, tunakutia katika Madhehebu za Kisunni kunazingatiwa shuruti ya Uquraishi ambayo ni shatri ya Ukabila kuwa ni Shuruti ya msingi, pia tukenda kwa Shia tunakutia kunazingatiwa shuruti ya Uahli Baiti ambayo ni Sharti ya Ukabila na ukoo hasa kuwa ni shuruti ya msingi, ama ukija katika Ibadhi hakuna sharti hiyo aslan, Muislamu yoyote mwenye elimu na uchamungu na uwezo wa kuongoza akiridhiwa na Waislamu kuwa kiongozi wao basi atakuwa ni Khalifa Amiri wa Waumini hata kama atakua ni Muhabeshi mweusi iliyobonyea pua yake basi utiifu wake kwa Waumini utalazimika.

Ama zaidi yaliyoitafautisha Ibadhi na Madhehebu nyengine za Uislamu baada ya hilo la Uongozi ni:

 1. Kumuitakidi Allah mtukufu kuwa ni mkwasi aliyetangulia kila kisichokua yeye, basi ametakasika na sifa za viungo na harakati, pia ametakasika na uwezekano wa kuonekana kwa macho duniani na akhera, pia ametakasika na uwezekano wa kusifika kwa sifa zisizokua dhati yake au zenye kuhitajia viumbe vyake, basi kusifika kwake ni kidhati na si kwa kutegemea sifa.
 2. Ulazima wa kuitakidi kuwa kila kisichokua Allah mtukufu ni kiumbe, basi Quraani ni kiumbe bila shaka yoyote, na maneno ya Allah yote ni viumbe miongoni mwa viumbe vyake, kwani maneno hayo ni athari ya sifa ya Usemaji wa kidhati wa Allah mtukufu.
 3. Ulazima wa kuitakidi kuwa Imani kisheria haikubaliani na dhambi kubwa yoyote, basi yoyote atakayeasi kwa dhambi kubwa atakua yuko nje ya duara la imani na kuwa ndani ya duara la ukafiri mpaka atubie kwa Allah mtukufu, ni sawa dhambi kubwa hiyo ni ya kishirkina au si ya kishirikina, basi hakuna ulazima wa kuwa Kafiri ni Mshirkina, ingawa kuna ulazima wa kuwa Mshirkina ni kafiri, basi kila Mshirikina ni Kafiri lakini si kila Kafiri ni Mshirkina, kutokana na hapo wanavyuoni wetu wakasema kuwa ukafiri uko aina mbili:-
  1. Ukafiri wa kishirkina kwa waliomo katika madhambi ya kishirkina.
  2. Na ukafiri wa kinafiki pia umeeitwa ukafiri wa neema kwa aliyemo katika dhambi kubwa isiyokua ya kishirkina, na huyu anazingatiwa kuwa ni Muislamu ana haki zote za Waislamu isipokua Walaa-yah tu, basi kwa yule mwenye kujua dhambi yake atamuweka katika Baraa-a mpaka atubie kwa Allah mtukufu.
 4. Tunaitakidi kuwa Muumini siku ya kiama hapatwi na khofu wala huzuni, na makosa yake aliyotubia kwayo yote yatasitiriwa kwa uombezi wa Mtume S.A.W na wenye kuombea (Shafaa), basi hatuna itikadi ya Muumini yoyote kuingia katika Moto wala kupata khofu wala fazaa siku ya Kiama.
 5. Kunaitakidi kuwa mwenye kukubaliwa mema yake zimekua nzito mizani zake, na ambaye tayakataliwa mema yake ndiye ziliyefifia mizani zake, na Allah anawakubalia Wachamungu nao ndio aliowaandalia Pepo, wala hawakubalii Mafasiki waliojitosa katika kumuasi Allah mtukufu na wakafa wakiwa ni wakaidi wa kutubia, hakika hao hawaridhii Allah mtukufu, nao ndio Madhalimu waliotakabari, na hao ndio Makafiri ambao Allah kawaandalia moto.
 6. Tunaitakidi kuwa Pepo ina milango yake ambayo Waumini Wachamungu wataingia kupitia milango hiyo, pia Moto una milango yake ambayo Waovu Mafasiki wataingizwa kupitia milango hiyo, wala hatuamini kuwepo Daraja liitwalo Swiraati juu ya Jahannamu ambayo waovu watingia motoni kwa kuanguka kutokea mwenye Daraja hilo, tunasema kuwa Itikadi hiyo ya Sirati juu ya Jahannamu ni batili; kwani iko kinyume na Quraani tukufu.
 7. Tunaamini kuwa atakaeingia Peponi atabakia humo milele akineemeka bila kutoka wala kufa wala kumalizika, na atakaeingia Motoni atabakia humo milele akiadhibika bila kutoka wala kufa wala kumalizika, basi hatuna sisi itikadi ya kutolewa motoni, wala itikadi ya kusamehewa bila ya kutubia, na tunasema kuwa Itikadi ya kutoka motoni na kusamehewa bila kutubia ni itikadi batili iliyojengeka juu ya uzushi wa matarajiohewa.
 8. Tunaamini ulazima wa kumpenda kila Muumini Mchamungu kwa ajili ya Allah mtukufu nao ndio Walaa-yah. Pia tunaamini ulazima wa kumchukia kila Kafiri Fasiki uliebainika ufasiki wake kwa jili ya Allah mtukufu nayo ndiyo Baraa-a, na ulazima wa kutomuweka katika mapenzi wala katika chuki kwa yule ambaye imetatiza hali yake au kutobainika uchamungu wake au ufasiki wake nao ndio Wuquufu.
 9. Hatuoni usahihi wa ndoa ya Muislamu kwa aliyezini naye hata kama watatubia, basi Muibadhi ikiwa ni mwanamke au mwanaume anajua vyema kuwa kuzini ni kujifungia mlango wa ndoa milele baina yake na yule aliyezini naye.
 10. Hatuoni usahihi wa kunyanyua au kunfunga mikono katika sala, wala kuitikia amina, wala kuleta dua ya kunuti, wala kusoma kisomo zaidi Alhamdu katika rakaa zote za Adhuhuri na Alaasiri.

Haya ndiyo muhimu iliyopambika kwayo Madhehebu ya Ibadhi kwa mafundisho yake.

Na mwisho tunasema kuwa jina la Ibadhi tumeitwa na wengine, na sisi baada ya muda tumekubali jina hilo kuwa ni anuani (Title) kwa kuona dharura ya kudhibiti tafauti zilizotokea baina ya Waislamu na kuhusisha athari za tafauti hizo kwa wahusika wake ili kila chuo kibebe mzigo wake na kihusishwe na mambo yake, basi tusibebeshwe ya wengine katika yenye tafauti ndani yake.

Ibadhi hatuoni uhalali wa kumfanyia ubabe wa kumkandamiza Muislamu yoyote aliyetafautina na sisi kimadhehebu kwa sababu ya tafauti ya kimadhehebu, basi hatuna sisi Fatawa chinjachinja dhidi ya Waislamu wa Madhehebu nyengine zilizo tafauti na Ibadhi, bali tunaona wajibu wa kushirikiana na wengine katika yale yenye makubalino na kuheshimiana katika yenye fatauti.

Lau kuwa Ibadhi ina mafundisho ya kuwafanyia ubabe waislamu wa Madhehebu nyengine za Waislamu, basi Afrika Mashariki kungelimwagika damu nyingi sana ya wasiokuwa Maibadhi kuanzia Karne ya 17 A.D mpaka ya 20 A.D; kwani jeshi la Imamu Muadilifu wa Oman Seif bin Sultan Al-Yaarubi R.A liliingia Afrika Mashariki kwa kuitika wito wa Waislamu wa miji ya Afrika Mashariki wa kumtaka msaada wa kukombolewa kutokana na uvamizi na ulowezi na unyanyasaji wa Wareno, basi Imam Seif Al-Yaarubi R.A aliitika wito huo na kutuma jeshi la kupambana na Wareno na wakomboa Wasilamu kutokana na mavamizi ya Wakiristo hao wa Kireno, Basi Imam Seif Al-Yaarubi R.A kwa kushirikiana na Waislamu wenyeji wa miji ya Afrika Mashariki aliweza kuwashinda vita wavamizi hao mpaka kuwazingira katika Ngome yao ya Mombasa (Fort Jesus) kwa muda wa Miaka miwili na miezi tisa mpaka wakasalimu amri na kuwatokomeza kabisa katika mwaka 1698 A.D, basi lau kuwa Ibadhi inahimiza kuwafanyia ubabe na kukandamiza Waislamu kwa misingi ya tafauti za kimadhehebu kwa hakika asingalibakia muislamu yoyote Afrika Mashariki akiwa salama isipokua Muibadhi tu; kwani Serikali ya Imam Seif bin Sultan Al-Yaarubi R.A ilikua ni Serikali iliyosimama kwa misingi ya Kiislamu nayo iliheshimu mafundisho yake kikamilifu kupitia Madhehebu ya Ibadhi na Maulamaa wa Dini ambao mapitisho ya kisiasa yalikua mikononi mwao, nayo ilikua ni Dola yenye nguvu sana, na kuanzia hapo miji yote ya Afrika Mashariki iliendelea kuwa chini ya himaya ya Serikali ya Oman na Watawala wake waliofuata mpaka kumalizika kwa Ufalme wa Kibusaidi katika visiwa vya Zanzibar mwaka 1964 A.D.

Wabillahi taufiqi.

 

Published By Said Al Habsy

30:imi nauliza juu ya maana ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) aliposema kwamba Ummat utagawanyika katika mapote/makundi 73

SWALI:
Assalaam alaikum. Mimi nauliza juu ya maana ya hadithi ya Mtume (S.A.W.) aliposema kwamba Ummat utagawanyika katika mapote/makundi 73 na yote hayo yatakwenda motoni isipokuwa kundi moja , je haya makundi yaliyopo leo si katika makundi yale 73 aliyoyasema Mtume ? Mfano wa makundi hayo ni Shiaa, Ibadhi, Sunni na mengineyo. Shukran.


JAWABU.
Waalaykum salaam.
Hadithi hiyo uloitaja ndugu yangu ni hadithi sahihi imepokewa na wengi katika wanachuoni sahihi kwa njia sahihi, katika hao ni Imaam Rabii bin Habib R.A. katika Musnad yake no: 41 amepokea Imaam Abu Ubaidah kutoka kwa Imaam Jabir bin Zaid kutoka kwa Ibn Abbas R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema “Ummah wangu utagawanyika makundi sabini na tatu, yote yatakwenda motoni ispokuwa moja tu, na kila kundi linadai kuwa ndio hilo moja” pia wameipokea Abu daawud, Tirmidhi, Nasaai, n.k.kwa lafdhi zenye tofauti ndogo.
Katika hadithi zingine Mtume s.a.w. ametaja kundi hilo ni lile litakaloshikamana na Sunna zake na mwenendo wa Makhalifa waongofu, walioongoka na kujiweka mbali na yatakayozuka katika dini kwani kila uzushi mbaya ni upotevu. (( kapokea Abu Daawud na Tirmidhi )).
Na makubaliano ya Ummah yapo kuwa makhalifa Abubakri, Umar na nusu ya utawala wa Uthman na Ally ilikuwa ni uadilifu, na nusu nyingine ya ukhalifa wa Uthman na Ally masahaba walitofautiana hata wakapigana vita, na kuuana.
Na wamekubaliana kuwa ufalme wa Banii Umayya na Bani Abbasi ulikuwa uasi wa wazi dhidi ya dola ya uongofu wa Mtume s.a.w.
Kwa maana hiyo, muislam atakayeshikamana na Sunnah ya Mtume s.a.w. na mwenendo wa makhalifa waongofu kabla ya kukhitalafiana baina yao, atakuwe,o katika kundi litakalo okoka, inshalla.
Pia hapana budi kuyapima yale yalopokewa kuwa ni ya Mtume S.A.W. au ni ya makhalifa wake waongofu kabla ya kutofautiana baina yao, kwa kuwa waongo wengi wameyaegemeza mambo yao kwao, kwa kutunga hadithi na riwaya.

Hivyo si kila kitakachosemwa kuwa kimetoka kwa Mtume na makhalfa waongofu kitakubaliwa mpaka kipimwe katika mizani tatu:
1. ISIPINGANE NA QUR AN


Abu Ubaidat kutoka kwa Jabir bin Zaid kutoka kwa Ibn Abbas R,A, kutoka Mtume S.A.W. amesema “ Hakika nyinyi mtatofautiana baada yangu, basi kila kitakachokujieni kutoka kwangu kipimeni katika kitabu cha Allah mtukufu, kitakachokubaliana nacho basi kimetoka kwangu, na kitakachopingana nacho hicho hakijatoka kwangu” ameipokea Rabii bin Habiib katika musnad no 40.
2. ISIPINGANE NA SUNNAH ILIYOKUBALIKA


Amesema Mtume s.a.w. “ Haiwi kwa Allah mtukufu kuukusanya ummah wake katika upotofu” Musnad Imaam Rabii R.A. no 39
3. ISIPINGANE NA MALAZIMISHO YA KIAKILI

Amesema Allah mtukufu: Watasema watu wa motoni “Na watasema: Lau kuwa tungeli sikia, au tungeli kuwa na akili, tusingeli kuwa katika watu wa Motoni!” Mulk : 10
4. ITATAZAMWA MFUATANO WA WAPOKEZI

Amesema Allah mtukufu: “Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda” Hujuraat:06
5. ISIWE NA MAGONJWA YA MATN kama mgongano n.k.

Amesema Allah mtukufu: “Hebu hawaizingatii hii Qur’ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi” Nisaa: 82
Habari hii ikitimiza masharti haya, ikiwa ni Mutawaatir (( imepokewa na wengi wasioweza kukubaliana katika uongo )) itachukuliwa katika mambo ya itikadi na mengineyo, amma ikiwa imepokelewa na wachache basi haitotumika katika itikadi, kwa kuwa bado itakuwa na dhana ya kutosihi na itikadi yatakiwa yaqini moja kwa moja. Kwa kuwa itikadi inayohusiana na kumjua Allah mtukufu ambaye yeye ni Yaqinii isiyokubali shaka, Amesema Allah mtukufu: “Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu,” Muhammad:19
Hivyo madhehebu, vikundi, watu, sharia zote, na mienendo yote itapimwa hapo na kupewa hukumu ya upotevu au uongofu sio kwa kutazama majina. Amma idadi iliyotajwa haikukusudiwa umaalumu wake bali wingi wake yaani njia nyingi zitakuwa upotevu na njia ya Mtume S.A.W. na makhalifa wake waongofu itakuwa ni haki.
Mwisho: Allah mtukufu amufupishia njia ya kundi hili kwa kuwaita wachamungu na kusema pepo wameandaliwa wao, si mwingine yoyote, Amesema Allah mtukufu: ” Hiyo ndiyo Pepo tutayo warithisha katika waja wetu walio kuwa wachamngu” Maryam:63, kwa hivyo jitahidi uwe katika wao kwa kuifauata HAKI KWA DALILI.
Wassalaam Alaikum warahmatullah wabarakatuhu.


Sh. Abu Muslim Khamis Alghammawi

Published By Said Al Habsy

31:Naomba kujua fadhila za kumsalia Mtume s.a.w. mara 1, 10, 100, na mara 1000 na marejeo yake. Mazingatio: Kitabu gani ? Kurasa namba ngapi ? Na kaipokea nani ?

SWALI:


Assalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh, Naomba kujua fadhila za kumsalia Mtume s.a.w. mara 1, 10, 100, na mara 1000 na marejeo yake.
Mazingatio, Kitabu gani ? Kurasa namba ngapi ? Na kaipokea nani ? Ahsantuma natumai maombi yangu yatajibiwa kama nilivyotaja.

JAWABU:


Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuhu.
Kumsalia Mtume s.a.w. ni katika wajibu ulokuja katika Quran kila atajwapo, sawa kama atatajwa mara moja au mara laki moja, na fadhila zake katika hilo ni kubwa kwani ni utekelezaji wa wajibu aliotuklifisha Allah mtukufu katika kitabu chake aliposema:
“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.” Ahzaab:56
Hivyo mwenye kutekeleza wajibu huu atapata yote wanayopata wenye kutekeleza amri za Alla mtukufu, ya kuandikiwa kwa wema mmoja, malipo ya kumi amesema Allah mtukufu:
“Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa” An’am:160
Na zimekuja riwaya nyingi zinzotaja malipo na fadhila za kumsalia Mtume s.a.w. katika hizo. Riwaya alioipokea Imaam Muslim katika sahiha yake riwaya no: 939, Sahiih Ibn Hibban no 906, Nassai katika Sunan yake 1296 na wengineo wengi kuwa Mtume S.A,W, amesema “ Mwenye kunisalia mimi mara moja, Allah mtukufu atamsalia mara kumi”
Na katika riwaya aloipokea Bukhari katika Adabul mufradi no 643, Ahmad katika musnad yake no 12017, Nasaai kkatika sunan alkubra 9891, Alhakim katika sahiha yake no 20118 na akasema Alhaakim isnadi yake ni sahihi, Mtume amesema “ atakayenisalia sala moja, Allah mtukufu atamsalia kwa sala yake hiyo, sala kumi, na atmfutia makosa kumi na atampandisha daraja kumi”
Pia amepokea Tabarani kwa Isnad mbili katika muujamu l kabiir ((majmau l fawaaid no 17022)), kutoka kwa Abi dardai, kuwa Mtume s.a.w. amesema “ Atakayenisalia inapoingia asubuhi mara kumi, na inapoingia jioni mara kumi, utamfikia uombezi wangu siku ya qiyama”
Na katika kitabu Majmaul Fawaaid, riwaya no: 17298 kutoka kitabu cha Altabarani kwa isnadi yake kutoka kwa Anas bin Malik amesema, Amesema Mtume s.a.w. “ Atakayenisalia sala moja, Allah mtukufu atamsalia sala kumi, na atakayenisalia mara kumi, Allah mtukufu atamsalia mara mia moja, na atakayenisalia mara mia moja, Allah mtukufu atamuandikia kukingwa kwa namna mbili, kinga ya unafiqi baina ya maho yake na kinga ya moto wa Jahannam, na siku ya Qiyama Allah mtukufu atamuweka pamoja na mashuhadaa” Amesema Alhaithami “ ndani yake yumo Ibrahim bin Salim bin Shibli Alhujaimi sikumjua na waliobaki wote katika wapokezi wake ni thiqa” pia wapo walio idhoofisha hadithi hii.
Riwaya katika maudhui hii ni nyingi, zipo zilokuwa sahihi na zipo dhaifu na za kutunga, na kanuni ya kudhibiti fadhila na ubora wa kumsalia Mtume s.a.w. ni kuwa kila ikizidi ndio fadhila zake na ubora wake unakuwa mwingi, kama ilivyokuja katika athari kuwa Mtume s.a.w. amesema “ basi akitaka mtu azidishe au apunguze” Kashful khafaa 2517.
Wallahu aalam.


Abu Muslim Alghammawi
20 – 03 – 2017

Published By Said Al Habsy

SWALI

Asalamu alaikum warahmatullahi wabarakatu, nauliza . je nyaraka za QUR ANI tukufu na Majina ya ALLAH yakiwa yamechanika ,yamekatika katika.mfano mas hafu imekatikakatika je kuichoma au kuitupa baharini ni vibaya.?ili kuepusha watu wasiitumie vibaya. naomba jibu.

JAWABU:

Waalaikum msalaam warahmatullah wabarakatuh.


QURAN ni Maneno ya Allah mtukufu, yeye ndiye aliyeyaanzisha kwa kuyaumba na kutuletea sisi. Kuyaheshimu ni kumuheshimu Allah mtukufu,
Amesema Allah mtukufu:
“Na isomwapo Qur’ani isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa.” Al aaraf:204

Hivyo msingi unaofuatwa katika Kutaamal na Quran ni kuwa kila kinachokuwa na heshima na adabu na Qur an hakikatazwi kufanywa ispokuwa kwa dalili ya kukataza kama ipo. Na kila kinachoivunjia heshima Qur an kinakatazwa, hata kama kitapendeza katika macho ya watu.
Mfano wa yanayoruhusiwa ni kuitia cover, kuhifadhi vipande vya karatasi zake sehem nzuri, ikishindikana kuitupa baharini kwa kuiwekea kitu kizito ili isirudi nchi kavu, kuichoma moto katika shimo litakalokuwa sehemu safi bila kuchanganya na chochote na kufukia jivu lake katika shimo hilo na jambo hilo alilifanya sayyidna Uthman katika zama za utawala wake mbele ya masahaba na wala.hawakumpinga n.k.

Na inakatazwa kuiweka katika sehemu ya kupigwa vumbi, kama katka vioo vya gari, au mashuka ya kulalia na kufunikia jeneza, n.k.

Nataraji jawabu yako imo ndani ya maelezo hayo, na muhimi ni kuizingatia kanuni ya kuiheshimu, nawe ni mjuzi wa yale yatokanayo na heshima katika matendo na yavunjayo adabu kwa qauli na vitendo.
Wallahu aalam.


Abu Muslim Alghammawi
20 – 03 – 2017

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Asalaam alee’kum Sheikh. Baada ya kuumbwa mbingu,dunia na vingemevyo, Allah alimuumba Adam na pia akampatia mfariji wake ambaye sote tunajua kwa jina BIi Hawa, lakini ukiuangalia msahafu kwa makini. hakuna sura ye yote katika Qur’aani, ambapo Allah kamtaja Bi Hawa kwa jina hili.ila Allah kataja majina ya manaabii kwa majina yao, pia katajwa Bi Maryam basi kwa jina lake,ikiwa ni mwamke pekeyake kutajwa jina katika Qur’aan Kareem. Je? hili jina la Hawa lilitoka wapi?? nani alikuwa akiitwa mke wa Adam [AS}

JAWABU:
Waaleykum salaam warahatullah wabarakatuh.

Qur an tukufu imetutajia kila lilokuwa linahitajika katika maisha yetu, na lenye tija kwa dini na dunia yetu, Amesema Allah mtukufu:
Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa. An’am :38

Na wale alowataka Allah mtukufu tuwajue kwa majina yao aliwataja katika kitabu chake, na wengine alitaka tujue matendo yao na misimamo yao tu, mfano wa hao ni: Mke wa Nabii Lut, Mke wa Nabii Nuh, na wengineo.
Hivyo mke wa Adam si yeye tu ambaye hakutajwa.

Amma katika Sunnah, Amesema Sheikh Ismail bin Nassor Al oufi – Allah amuhifadhi – “Hakuna lilothibiti katika kulitaja jina la Hawa kama mke wa Adam,” na yale yalotajwa imma yanaingia katika udhaifu au kuwa hayatoi hukmu ya Yaqini, na makadirio ya juu yamechukuliwa kutoka katika riwaya za Ahlil kitaab.

Miongoni mwa riwaya hizo :
Amepokea Bukhari 3399, Muslim 1470, Tirmidhi 3077
Kutoka kwa Abi Huraira kuwa Mtume s.a.w. amesema

لولا بني إسرائيل لم يخنز اللحم ، ولولا حواء لم تخن أنثى زوجها الدهر

“Kama si bani Israil isingeharibika nyama, na kama si Hawa basi hakuna mwanamke ambaye angemfanyia khiyana mme wake”

Na Riwaya nyingine aloipokea Al uqeily jz 3 uk 327 mesema :
لولا بنو إسرائيل خبئوا اللحم ما خنز اللحم ولولا حواء خانت آدم في قولها لإبليس ما خانت امرأة زوجها
Kama si Bani Israil kuficha nyama, nyama zisingeharibika na kutoa harufu, na kama si Hawa kumfanyia khiyana Adam kwa kumwambia Ibilisi, basi kusingekuwa na khiyana ya mke kwa mmewe”

Na haijifichi kwako baadhi ya ishkaalat zilizopo katika hadithi hizi, ikiwemo kugongana kwake na Qur an, kwani Qur an inatuhadithia kuwa uasi uliwapata wote sawia, bali majukumu yote na lawama tunaona alibebeshwa Adam, na katika biblia toleo la kale tunakuta mithali ya ibara hizi zenye kuashiria kuwa mwanamke ndiye asili ya upotevu, na hivyo alistahiki kuzaa kwa uchungu, na mwanamme kwa kupotezwa kwake akastahiki kutafuta rizki kwa jasho. Hayo nimeyasoma zamani katika biblia ya agano la kale.

Pia katika riwaya hizo kuna kuwabebesha mzigo wa dhambi ya kufuatia wanawake wote wa dunia, kwa khiyana moja ilozushwa kutokea, wakati Allah mtukufu anasema :
Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume. 17:15

Kutokana na hayo inapata nguvu kauli ya kuwa inawezekana kuwa hilo limesikiwa kutoka kwa banii Israil, na wapokezi wakalichanganya wakalielekeza kuwa Mtume s.a.w. ndio kalisema, kwani ni maarufu kuwa Sahaba Abi Huraira R.A. alikuwa akihadithia kutoka katika baadhi ya vitabu vya bani Israil, na wapokezi wakichanganya hayo na kuyaegemeza kwa Mtume kama alivyosema Saeed bin Wahb ” jichungeni sana na hadithi, kwani tumewaona watu wakichanganya mapokezi ya Abu huraira kutika kwa Kaab na kutoka kwa Mtume s.a.w., wakiyafanya ya Mtume s.a.w. kuwa ya Kaab na wakiyafanya ya Kaab kuwa ya Mtume s.a.w.”

Hivyo, hilo si jambo la kiitikadi, na si muhimu kwetu sisi kujua jina lake, kwani angelitaka Allah mtukufu tulijue angetutajia katika kitabu chake kitukufu.

Wallahu Aalam.
Abu Muslim Alghammawi
21.03.2017m

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Asalam alaikum.
mimi ninapofanyakazi na ninapoishi ni masafa yanayoruhusiwa kusali safar.salaa ya adhuhuri inanikuta kazini na salaa ya Alasar vile vile inanikuta kazini.JE ni vizuri kisheria kusali Salat dhuhur pekee yake kwa wakati wake na Alasar peke yake kwa wakati wake AU kuzichanganya rakaa mbili za dhuhur na rakaa mbili za asar(Qaras) kabliya au taakhir ?

JAWABU:


Sala zilifaradhishwa rakaa mbili mbili kwanza wakati wa Makka, kabla ya Mtume s.a.w. kwenda Israa na Miiraj.
Amepokea Bii Aisha R.A.


” Sala za faradhi zilifaridhishwa rakaa mbili mbili, kisha zikazidshwa rakaa mbili kwa wakazi na kubakishwa mbili mbili kwa wasafiri” ispokuwa maghribi yenyewe ni rakaa tatu bila kupunguwa.
Hivyo katika sala hii kuna mas ala mawili :

1. KUPUNGUKA RAKAA KWA MSAFIRI.

Ikiwa msafiri anasali peke yake au anasalisha basi inamlazimikia kusali sala zote za rakaa nne kwa rakaa mbili tu. Na ikiwa ataisali kwa rakaa nne sala yake itakuwa imeharibika.

Amma akisali nyuma ya Imam Mkazi (ambaye si msafiri), basi inamlazimu kusali rakaa zote nne, na kuingia katika sala kwa nia ya kusali kwa mujibu wa rakaa za Imam mkazi.

2. KUCHANGANYA SALA MBILI PAMOJA

Hili limewekwa kwa yule aliye katika mwendo na kuwa hawezi kuipata kila sala kwa wakti wake kutokana na dhurufu za safari, sio kwa vingine.

Naye halazimishwi katika hili, bali ni khiyari kwake. Amma aliye katika hali ya utulivu anaambiwa asali kila sala kwa wakati wake, kwa jamaa msikitini.

Hivyo Jawabu ya swali lako:
KASALI NA JAMAA MSIKITINI KILA SALA KWA WAKATI WAKE, BILA KUZICHANGANYA.

Wallahu Aalam.

Abu Muslim Khamis Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com

Published By Said Al Habsy

SWALI:

Swali kutoka Somalia, kwa Saida Abdul kadir

Je ipo hadithi inayosema mtu hafai kusema huyu ni mke wangu au huyu ni mume wangu, wakiwa hawajaoana hata kwa mzaha na mtu kusema mimi si muislamu yafaa asilimu.

JAWABU:

Katika mambo ambayo yatakiwa watu kutoyachukulia mzaha ni kuyatumia maneno ya kidni na kisheria katika sehemu isokuwa zake na kuleta matatizokwa mtu akiwa anjua au hajui. Allah mtukufu ametutakataza kwa kutaja hali za wanafiki waulizwapo kuhusu maneno yao:

وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ قُلْ أَبِاللَّهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنْتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ (65)

“Na ukiwauliza, wanasema: Sisi tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Mlikuwa mkimfanyia maskhara Mwenyezi Mungu na Ishara zake na Mtume wake?” Tawba: 65
Na Allah mtukufu akaweka wazi kuwa maneno hayo yakiwa yanapelekea ukafiri basi watakuwa wamekufuru bila kujali neno lao kuwa ilikuwa ni utani na mchezo akasema:
“Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu.” Tauba:66
Na wala haisemwi kuwa walikuwa wanafiki ndani ya nafsi zao kwa hivyo haiwi sawa kuileta hukmu hiyo kwa wenye kusema bila ya unafiqi, kwani Allah mtukufu anatutakaza kutumia lafdhi mbaya zenye tafsiri ya ukafiri hata kama ni zetu ni njema, alipowakataza waislamu kwa kusema :

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انْظُرْنَا وَاسْمَعُوا وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ (104)

“Enyi mlio amini! Msiseme: “Raa’ina”, na semeni: “Ndhurna”. Na sikieni! Na makafiri watapata adhabu chungu” Baqarah:104
Na yalikuja makatazo hayo kwa kuwa ni neno ((rainaa)) walikuwa wakilitumia wasiokuwa waislamu kumfanyia istihzai Mtume s.a.w. kwa lugha ya kiebrania lakini kwa Kiarabu lina maana sawa na neno la pili ((undhurnaa)) waliloambiwa watumie, yote hayo ni kuondosha kujifananisha na makafiri na kutotumia maneno yenye utata wa kimaana ndani yake.
Na Muislamu daima anaweka katika akili yake katika lafdhi na maneno ayatoayo kwani atahesabiwa kwayo, Amesema Allah mtukufu:

مَا يَلْفِظُ مِنْ قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ (18)

“Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.” Qaaf : 18
Na yamekuja makatazo khasa katika kutumia lafdhi za ndoa, talaka, kumrejea mke, na kumuachia huru mtumwa, amesema Mtume s.a.w.


“ثَلاثٌ جِدُّهُنَّ جِدٌّ ، وَهَزْلُهُنَّ جِدٌ : الطَّلاقُ ، وَالنِّكِاحُ والرُّجْعَةُ”

“Mambo matatu, ukweli wake ni kweli na utani wake ni kweli, talaka, ndoa na kumrejea mke” kaipokea Abi Dawud 2194, Tirmidhi 1184, Ibn Maja 2048.
Nayo ina Daraja ya Hassan, kwa Muhadddith wa zama zetu Sheikh Saeed Bin Mabrouk Alqannubi – Allah mtukufu amuhifadhi -.
Kama ambavyo haijifichi ndani yake kuwa kuna uongo katika qauli hiyo, nayo si katika tabia za waislamu wala si katika mwenendo wa Mtume S.A.W. kwani yeye alikuwa akitaniana lakini akisema kweli katika utani wake.
Hivyo muislamu ajiepushe na yale yatakayomuweka katika makosa, na ikiwa jambo limekubainikia ukweli wake lifuate, na lilokubainikia liwache, lenye utata usiliingie na kulisemea bora kukaa kimya na kufanya yaliyothibiti kwa usalama wa dini, dunia na akhera yetu.


Wassalaamu alaykum warahmatullah wabarakatuh.


Khamis bin Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com

Published By Said Al Habsy

36:HEDHI YAKE IMEPANGUKA

Hamed Al mahmudi from

Oman

————————————–

SWALI:

Asalamu alaykum
Mwanamke iliwakuwa hedhi yake siku 5 kwa miaka mingi baada yakujifungua mtoto wa mwisho anaijiwa hedhi siku 4 badaye inakatika kwa siku 2 halafu inakuja mara moja siku ya saba nini hukumu ya dini?lini anaoga?
Baaraka Allahu Fiikum.

JAWABU:
Masuala haya yana khilafu kubwa baina ya wanachuoni wetu, katika Qauli zinazofikia kumi na tatu kwa ujumla wake.
Sheikh wetu Ahmed Alkhalili – Allah amuhifadhi na ampe izzi- amezitaja baadhi tu ya Qauli hizo bila kuweka uzito katika moja ya qauli hizo. Nyingine kazitaja Sheikh Aljiitali katika Qawaaid na Sh Alqutb katika Sharh Niil.

Amesema Sheikh Abul Arab Ismail Aloufi – Allah amuhifadhi –
” Qauli inayoweza kuwa ya wastani katika mas ala haya ni kuwa itambidi asali katika hizo siku mbili za baina ya kutokwa damu”

Amesema Mja dhaifu Abu Muslim Alghammawi – Allah amuafu –

“Ikiwa ameona alama ya usafi katika hiyo siku ya nne, naye ada yake ilikuwa ni siku tano, basi kwa kuchukua msingi wa kuteremka kwa siku za hedhi, atasubiri kwa miezi miwili (( yaani kwa miezi miwili atahesabu bado ada yake ni siku tano, kisha wa tatu ataanza siku nne, yaani zitakuwa zimeteremka siku zake kutoka tano kurudi nne )).

Mabadiliko haya ya kuteremka kwa siku za ada yake ili yatimie inashurutishwa mambo matatu, kwa miezi hiyo miwili :
1. Kufuatana – miezi miwili mfululizo- n.k.

2. Kuwa sawa kwa siku zilopungua – nne kwa miezi miwili -.

3. Kupangika – isiwe tofauti tofauti -.

Amma damu itakayokuwa inakuja baada ya hapo bila ya kufuatanisha kama ilivyo katika swali, zikiwa hazijapita siku kumi tangu kumalizika kwa siku za ada yake, basi itahesabiwa kuwa ni damu ya ugonjwa, haimkatazi kufanya mambo ya ibada zake.

USHAURI.
Ikiwa yeye mwenyewe mwanamke atampata katika wanawake wenye fiqh katika dini, akawauliza ni bora zaidi kwani inawezekana kuna hali aliyonayo mwanamke, wanaweza kufahamiana baina yao zaidi.

Allah atuwafqishe katika kheri, atupe qauli za sawa, atyelimishe yenye manufaa na atunufaishe kwa ilmu hiyo, atusamehe tulipokosea na aturuzuku Touba kabla ya kufa.

Wallahu Aalam.

Mja dhaifu

Khamis Yahya Khamis Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
26 March 2017m

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.
Mimi niko na suali tafadhalini kwa Ibadhi.
naomba dalili ya Hadithi na Quraani kwa mujibu wa Swala zenu mnavyo sali kwamba katika swala ya Adhuhuri na Lasiri mnasoma Suraatu Faatiha peke yake kwa nini.?
Na kwa nini hamufungi mikono?.
Na mbona Mtume Muhammad (S.A.W) alisali kama sisi Sunni?
JAWABU:
Waalaykum salam wa rahmatullahi wa barakatuh.
Ndugu yangu inapasa ufahamu kuwa Waislamu wametafautiana baada ya kufa Mtume wetu Muhammad (S.A.W) na ndio sababu tukaona leo kuwepo Madhehebu tafauti, ikiwa wewe unitakidi kuwa Mtume Muhammad S.A.W alisali kama wanavosali Sunni, basi na sisi tunaitakidi kuwa Maibadhi wanasali kama alivokua Mtume (S.A.W) akisali.
Unapaswa ufahamu kuwa Ibadhi ni Madhehebu kongwe kuwepo kwake ni kabla ya kuzaliwa Imam yoyote katika Mimamu wanne wa Kisunni; kwani Imam wa Madhehebu hii alikua ni marejeo tegemewa ya kifatwa katika kipindi cha nusu ya pili ya karne ya mwanzo naye ni Imam Jabir bin Zaid Al-Uzdi R.A aliyezaliwa mwaka wa 18 Hijiria katika kijiji cha Firq Oman na kuchukua elimu yake kwa Masahaba wa Mtume S.A.W, na hakuna kutafautiana katika masuala ya msingi kama haya katika safu za Ibadhi, sasa wewe unaedai kuwa Mtume S.A.W alisali kama nyinyi Sunni munavosali hebu jiulize kama Sunni  wapi? Hanafi au Maliki au Shaafii au Hanmbali? Jambo la Sunni lina utata na haki haigawiki namna hiyo.
Napenda kukuambia ndugu yangu kuwa Sala kama tunavoisali sisi Ibadhi haina utata wowote nayo ni sahihi kwa madhehebu zote; kwa sababu hakuna tendo ambalo halimo katika sala kwetu sisi na wengine wanalifanya kisha tendo hilo likapelekea kuharibika sala ya asiyelifanyia kazi kwa mujibu wa mafundisho ya madhehebu yanayolithibitisha.
Ama kuhusu suala ya kufunga mikono unaweza kurejea jawabu yake kwa kubofya hapa.
Ama kuhusu suala la kusoma zaidi ya Al-Faatiha (Alhamdu) katika sala za Adhuhuri na Laasiri amesema Imam Abu Ghaanim Al-Khurasani R.A: Nilisema: Jee Inasomwa katika ya Mwanzo (Adhuhuri) na Laasiri chochote isipokua Al-Faatiha? Wakasema wote: Haisomwi isipokua Faatihatu Al-Kitaabi kwa siri baina yake (mwenye kusali) na nafsi yake tu. Nikasema: Jee Inasomwa katika Rakaa nne zote kwa Ummu Al-Quraani (Alhamdu) peke yake?. Wote wakasema: Ndio, hilo ni bora zaidi kwetu na kwa hilo tunachukua. [Mudawwana Abi Ghaamin Al-Khurasani uk. 69]. 
Wote wakasema yaani Mashekhe wake nao ni Imam Rabii bin Habiib, na Abu Al-Muhaajir, na Abu Al Murrij, na Abu Saidi Abdullahi bin Abdulazizi, na Abu Ghassaan Mukhallad bin Al A`mrad, na Abu Ayoub, na Hatim bin Mansour Allah awaridhie. Nao wote hao wamechukua elimu yao kwa Matabiina ambao wamechukua elimu yao kwa Masahaba ambao wamechukua elimu yao kwa Mtume S.A.W. Sasa sisi tuwe na wasi wasi gani katika Dini yetu?!!!
Amesema Sheikh Aamir Al-Shammakhi R.A katika Al-Iidhahi: ((Wamekubaliana watu (Maulamaa) ya kuwa Sala ya Adhuhuri na Laasiri haisomwi kwa sauti ndani yake, na tumeona kila rakaa ambayo ndani yake haisomwi isipokua Al-Hamdu inakua ni ya kisomo cha siri, hayo ni usiku na mchana, hivi huoni Sala ya Ijumaa na Sala ya Iddi mbili kisomo ndani yake kinakua kwa sauti kwa sababu ya Sura hata kama itakua ni mchana?!! Kutokana na hapo As-habu wetu (Ibadhi) wamelipa nguvu neno ya kutosoma zaidi ya Al-Faatiha katika Rakaa mbili za mwanzo za Adhuhuri na Laasiri. Na Allah ndiye anaejua zaidi. Na amepokea Ibnu Maajah Hadithi kutoka kwa Nabii S.A.W kuwa Nabii S.A.W hakua akisoma ndani yake, kama linavotiwa nguvu hilo kuwa kisomo cha Sura kimewekewa kunyamaza na kusikiliza kwa Maamuma na hilo halipatikani kwa yanayosomwa kwa siri. ))
Amesema Msitahiwa Sheikh Ahmed Al-Khalili Allah amuhifaadhi: 
((Dalili ya As-habu wetu (Ibadhi) ya kutosoma isipokua Al-Faatiha katika Adhuhuri mbili (Adhuri na Laasiri) ni Hadithi  ya Ibnu Abbaas -Allah awaridhie- ambayo kaipokea Ibnu Maajah kuwa Nabii S.A.W hakua akisoma ndani yake, na hilo linatiliwa nguvu kwa kulinganisha kuwa rakaa zote ambazo kisomo kinakua cha siri hua haisomwi ndani yake isipokua Al-Hamdu tu, vile vile linatiliwa nguvu kuwa kisomo cha Sura kimeekewa ulazima wa kunyamaza na kusikiliza kwa upande wa Maamuma na hilo haliwezekani katika rakaa za kisomo cha siri. Na Allah anajua zaidi.))
Amesema Al-Allaamah Sheikh Said Al-Qannubi Allah amuhifadhi:
((As-habu wetu (Ibadhi) -radhi za Allah ziwe kwao- wametolea dalili katika kutofaa kusoma zaidi ya Al-Faatiha katika Adhuhuri na Laasiri kwa hadithi ya Ibnu Abbaas R.A amesema: “Amesoma Nabii S.A.W katika aliyoamrishwa na amenyamaza katika aliyoamrishwa na hakua Mola wako asahau” Ameipokea Bukhari katika Sahihi yake.
Na kwa Hadithi yake nyengine aliyoipokea Nasaai na Abu Daudi na Tahawi katika Sherhu Maani Al-Aathari kwa njia ya Abdullahi bin Ubaidillahi bin Abbaas amesema: Niliingia kwa Ibnu Abbaas nikiwa katika vijana wa Bani Hashim basi tukasema kumwambia kijana kati yetu: Muulize Ibnu Abbaas jee! Mtume S.A.W alikua akisoma katika sala ya Adhuhuri na Laasiri? Akasema Hakua akisoma, hapo ikasemwa: Pengine alikua akisoma katika nafsi yake? Akasema: Khashman (Upongo) hilo ni baya kuliko la mwanzo, alikua ni Mja aliyeamrishwa amefikisha aliyotumwa kwayo.))
Basi kama tunavoona jinsi Ibnu Abbaas R.A alivokemea neno lao la kusema kuwa pengine alikua akisoma katika nafsi yake. Na kubainisha kuwa Mtume S.A.W alikua ni mja aliyeamrishwa kufikisha na kufundisha kwa hiyo lau kuwa kuna kisomo baada ya Al-Faatiha katika adhuhuri na Laasiri basi Mtume S.A.W angalifundisha hilo wala asingalilihusisha kwa nafsi yake peke yake kama munavozua.
Wallahu Aalamu.
 

Published By Said Al Habsy

Swali:

Asalamu aleykum warahmatullahi wabarakatuh ,
Naomba kuuliza sheikh je sijdah Tilawa ni sunna au faradhi ?
Shukran


JAWABU:

Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.
Kuna khilafu katika hukmu yake, wapo waliosema ni Faridha ((lazima)), na wapo waliosema ni Sunnah.
Na Muislam yatakiwa achukue lenye usalama katika dini yake, hivyo asujudu kila impitiapo ay miongoni mwa aya za sijda.

Sheikh Ahmed bin Hamed Alkhalili – Allah mtukufu amuhifadhi – anaona lazima mtu awe na udhu na kuelekea kibla, kila anaposujudu sijdat tilaawa.

Na Sheikh Muhaddith Saeed Alqannubi – Allah mtukufu amuhifadhi – anaona kuwa sio lazima kuwa na udhu, au kuelekea kibla kwa kuwa sijda hiyo ni kama adhkaar zingine.

Nimesema (( Khamis Alghammawi )) : “Mwenye kuchukua moja ya rai mbili, ameshikana na nguzo imara ya kielimu”

Sehemu hizo 11 nazo ni:


1. Aaraf : 206
2. Raad : 15
3. Nahl : 50
4. Israa : 109
5. Alhajj : 77
6. Furqaan : 60
7. Naml : 26
8. Sajdah : 15
9. Saad : 24
10. Fussilat: 38
11. Maryam : 58

Sehemu tatu zifuatazo maulamaa wametofautiana wapo walosema kuna Sajdah na wapo waliokataa:

12. Alaq : 19
13. Inshiqaaq : 21
14. Najm : 62

RAI YENYE NGUVU KWA MAULAMAA WETU WA SASA SEHEMU HIZO NI SAJDAH PIA.

Ukisujudu Sijdah hiyo ndani ya sala soma : ((Subhaana rabbiya l aalaa))

Ikiwa umesujudu nje ya sala sema ((Subhaana rabbinaa in kaana waadu rabbinaa lamaf uula.))

Atakaponyanyuka kutoka Sijdah ikiwa yupo nje ya Sala atasema: ((Sajada wajhiya lillaahi lladhi shaqqa sam’ahu wabaswarahu, Rabbi aatinii bihaa ajran, wadha’a annii bihaa wizran, warzuqnii bihaa shukran, wataqabbalhaa minnii kamaa taqabbalta min ibaadika Daawud sajdatahu))

Qauli nyingi zimetokana na Duruus alizotusomesha Mlezi wetu Sheikh Hamoud bin Humeyd Al sawwafi – Allah mtukufu amuhifadhi, ampe umri mrefu wenye sihha na afya. Ewe Allah tunufaishe kwa elim yake.

Ameyaandika Alhaqiir :
Abuu Muslim Alghammawiy
khamis.alghamawi@ibadhi.com
31 March 2017.

Published By Said Al Habsy

Sultan Nasser from

Oman

————————————–

Swali:

Assalaam Alaikum,
Nimeweka nia ya kwenda Umra Insha Allah, Swali langu ni vp kinachotakiwa kukifanya kuanzia nyumbani mpaka utakapo jaaliwa kurudi safari yako ?

Asanteni.

JAWABU :

Umra ni kwenda kuitembelea Alkaaba na kuiimrisha kwa ibada mbalimbali maalumu kama Ihram, kuzunguka nyumba tukufu, kuzunguka Swafaa na Mar wa, kunyoa nywele au kuzipunguza.

Amesema Allah mtukufu :(( Timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Allah mtukufu ))

Wametofautiana wanachuoni kuhusu Hukmu yake, baina ya Wajib na Sunnah iliokokotezwa.

Ili Umra iwajibike lazima yafuatayo yatimie 1. Akili, 2. Kubaleghe 3. Kuwa huru 4. Kuweza kufanya 5. Kuwa na Mahram kwa mwanamke.

Na Ili umra isihi lazima yafuatayo yatimie 1. Muislam 2. Iwe katika wakati wake unaoruhusiwa (( hairuhusiwi wakati wa hijja yaani kuanzia mwezi 8 dhulhijja mpka mwezi 13 ))

MAMBO YA WAJIB KATIKA UMRA:
1. Ihraam katika sehem yake
2. Kutokana na Ihram kwa kunyoa nywele au kupunguza.
3.Tawafu – kuizunguka Alkaaba – kuiaga.

VINAVYOHARIBU UMRA:


1. Kutotimia Sharti miongoni mwa sharti zake.
2. Kuacha nguzo miongoni mwa nguzo zake.
3. Kumuingilia mwanamke au kuingiliwa na vyote vinavyoendana navyo kama kujitoa manii.

NGUZO ZA UMRA:


1. Kuvaa Ihram kwa ajili ya Ibada.
2. Kuzunguka Alkaaba
3. Kuzunguka Safa na Mar-wa

AINA ZA UMRA:
Umra zipo aina tatu:
1. Ifraadu 2. Tamattuu 3. Alqiraanu

NAMNA YA KUFANYA UMRA
Atavaa Ihram katika Miiqat, kisha ataelekea Msikiti mtukufu wa Makka, Atazunguka Alkaaba, kisha atasali katika Maqam ya sayyidna Ibrahim kisha ataelekea Swafa na Mar wa, kisha ataondokana na Ihram kwa kunyoa au kupunguza nywele.

BAADHI YA TANBIHI:


1. Kuvaa Ihram katika Miiqat ni maalumu kwa wanaotoka nje ya Miiiqat hiyo.
2. Aliyopo Makka atavalia Ihram yake katikaa Alhilli.
3. Sunnah ni kuingia msikiti wa Makkah kupitia mlango wa Bani Shaibah.
4. Tawafu ya Umra inahesabiwa kuwa ni Tawafu ya Kuingia makka kwa anayehijji.
5. Sunnah ya kunywa maji ya Zamzam ni maalumu kwa Tawwafu ya ziara sio Tawwafu ya Umra.
6. Kuondokana na Ihram ((Kuvua Ihram)) ni kwa anayefanya Umra tu, au Mutamattia.
7. Inajuzu kufanya zaidi ya Umra moja na ni sunnah ni kufanya umra moja kwa safari moja.
8. Kwa anayefanya Umra kutokea Alhilli haihesabiwi kuwa ni safari moja.
9. Tawafu ya kuaga ni Wajib kwa mwenye kufanya Umra kwa anayekaa Makka atafanya Tawwaf atakapomaliza tu kufanya aamal za Umra.
10. Umra ni kama Hijja, ni lazima mara moja tu, kwa umri wote.
11. Wamekubaliana wanachuoni uwajib wa Umra baada ya kuwa muislam ameingia ndani yake.
12. Kufanya touba na dua ni kama vile vile katika Hijjah
13. Kufanya Umra hakuondoshi faridha ya Hijja.

Imetimia, walhamdulillah.

Imetolewa kutoka kitabu cha Muutamad cha Sh. Muutasim Almaawali.

Imenukuliwa na mja dhaifu:
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
Ibadhi.com

 

Published By Said Al Habsy

KHALFAN SALIM from

Kenya

————————————–

Swali:

asalam alaikum warrahamatu Allah wabarakatu je maulid (mazazi ya mtume) yako katika dini yetu ya kiisilamu.

JAWABU:

Walaykum Salaam warahmatullah wabarakatuh.

Maulidi haikuwepo katika zama za Mtume s.a.w. wala masahaba wala wafuasi
wao. Ni kitu kimeanzishwa baada ya muda kupita kama uanzishaji wa vingine
kama mashindano ya Quran, kuweka Maquba msikitini, n.k.
Na kuhusu nani muanzishaji wake kuna khilafu baina ya wanachuoni, na kumjua au kutomjua si muhimu kwani kinachotazamwa ni kuwafikiana na sheria.

Hukmu ya Maulid itategemea malengo na namna ya kuyafanya hayo maulid yenyewe. Ikifanywa vizuri itakuwa nzuri na kinyume chake ndio ubaya wake.

Maulid zinazofanywa katika nchi zetu za Kiafrika na Asia, nyingi zinakuwa na mambo yasiyokubalika kisheria mengi na kuleta madhara hasa katika
kufanyika kwake usiku, kutoka kwa mabinti wa kiislam wari, kuenea kwa
zina, n.k.
Hivyo yakirekebishwa hayo na yakafanyika maulid kwa namna bora kama
kukutana msikitini kukatolewa historia ya Mtume au mawaidha na anasheed za
bila kuruka na kurukaruka, bila madufu, na bila ya kuchanganyika wanaume
na wanawake hakuna dhambi katika hilo bali watapata thawabu.
Na kwa hivyo ametoa fat wa Sheikh wetu Shaban Albattashi – Allah mtukufu amuhifadhi- kuhusu uharam wa maulid hizo zenye hayo makosa tuloeleza.

Na ametazama Sheikh wetu Ahmed Alkhalili – Allah amuhifadhi – uzuri wa yapatikanayo katika maulid zenye nidhamu, na taratibu nzuri akatoa fat wa ya kujuzu kwake, pamoja na kuelekeza kuwa iwe ni msimu wa kujipima kimaendeleo, na njia ya kuelekea katika mapenzi ya vitendo na kumuiga yeye Mtume s.a.w.
Amesema Allah mtukufu:
Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. 3:31

Pia Amesema Allah mtukufu:
“Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.” 33:61

Wallahu aalamu.

Abu Muslim Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
Ibadhi.com

Published By Said Al Habsy

a/alykum je ? inajuzu sala ya mwanamke anaesali na help me ?

JAWABU:


Sala iliyochanganyika na maasi haikubaliwi, kwani sala ni utiifu na ((help me)) ni uasi, basi vipi vyenye kupingana vikutane ??

Amepokea Ibn Abbas kutoka kwa Mtume s.a.w. kuwa amesema: ” Sala inajuzu nyuma ya kila mwema na muovu muhim asiweke kinachoiharibu sala hiyo” Musnad Imam Rabii no 208

Na Mtume s.a.w. amekataza kuweka hilo “Help me”, na bila shaka kuiweka ni madhambi makubwa basi vipi mtu atakuwa muasi na hapo hapo mtiifu kwa wakati mmoja.
Amesema Mtume s.a.w.: ” Makundi mawili ni katika watu wa motoni bado sijawaona, wakiwa na mijeledi kama mikia ya ng’ombe wakiwapiga watu, na wanawake wakiwa wamevaa kama wako uchi, vichwa vyao kama nundu ya ngamia, wapotovu wanapotosha, hawataingia peponi wala hawatoipata harufu yake japokuwa harufu yake inapatikana kwa mwendo wa kadha na kadha” Muslim 7373.

Hivyo sala yake ni batili, arudie tena.
Wallahu aalam.

Abu Muslim Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
Ibadhi.com

Published By Said Al Habsy

Salim Bafagih from 

Germany

————————————–

Swali:

Assalam Aleykum
1)Je Mtu asieswali zaka yake inakubaliwa ?

JAWABU:
Hakika Allah mtukufu ameweka sharti kuu za kukubali mema ya waja, sharti hiyo ni uchamumgu, amesema Allah mtukufu:

Akasema: Hakika Allah mtukufu huwapokelea wachamungu. Maida : 27

Kama ambavyo Allah mtukufu ameikutanisha Zaka na Sala sehemu moja, katika aya zote taqriban, hivyo kuviachanisha alivyovikusanya Allah mtukufu ni kuifanyia uadui zaka na sala kwa pamoja bali ni kumfanyia uadui Allah mtukufu na Mtume wake.
Amesema Allah mtukufu:

(وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ)
“Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt’iini Mtume, ili mpate kurehemewa.”
[Surat An-Nur 56]

Kama ambavyo Zaka inampa utakaso na usafi wa kumfanya ajue ukubwa na cheo cha sala na ibada zingine, Amesema Allah mtukufu:
(خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِمْ بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَهُمْ ۗ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ)

Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Allah mtukufu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua
[Surat At-Tawbah 103]

Kwa hivyo Zaka yake itakuwa ni imesimamishwa kukubaliwa kwake, akitubia madhambi yake mengine itakubaliwa na atapewa thamani ya malipo yake kamili bila kupunjwa, kama hakutubia yataporomoka yote aloyatenda katika wema. Anasema Allah mtukufu:
(أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ)
Je! Hawajui ya kwamba Allah mtukufu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaka, na kwamba Allah mtukufu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?
[Surat At-Tawbah 104]

TANBIIHI:
Haimaanishi maana hiyo kuwa awache kutoa yaliyomuwajibikia mpaka atakapoanza kusali, haasha wakallaa,…
Kwani atakapoacha atakuwa na deni, atakapotubia itambidi alipe na deni hilo la zaka kwa miaka yote itakayompita. Hivyo aendelee kutoa zaka, na amuombe Allah mtukufu tawfiiq ya kuweza kutekeleza ibada zote.

Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
09 April 2017m

 

Published By Said Al Habsy

Salim Bafagih from

Germany

————————————–

Swali:

Assalam Aleykum
Huku ulaya kuzama kwa jua ni muda mrefu kuliko afrika na arabuni je inafaa kuswali sunna ya kablia baada ya adhana ya magharibi?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Kilichothibiti kwetu sisi ni kuwa Hakuna Qabliya kabla ya Magharibi.

Ispokuwa inajuzu kusali Nafla, kwani imetolewa ruhusa hiyo na Mtume s.a.w.
Kwani yeye alisema :
Salini kabla ya Magharibi, salini kabla ya magharibi, salini kabla ya Magjaribi Mkitaka.

Kwa hivyo inaruhusika kusali kabla ya Magharibj kwa nia ya nafla sio kwa nia ya Qabliya.

Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com

09 April 2017m  

Published By Said Al Habsy

Jee nyny swala za Jahra. Akisoma imamu jee maamuna nao wawe wanasoma Fatha. Au inatosha ?

JAWABU:
Haimlazimikii Maaamuma nyuma ya Imam chochote cha kusoma ispokuwa Suratil Faatihaa.

Kwa hivyo atakaposoma Imam Suuratil faatiha, Maamuma atamfuatisha nyuma yake, asiwe sawa sawa naye, wala asimpite.

Yaani iwe kama mwalimu na mwanafunzi, kila anaposoma Imam naye anafuatisha katika Suuratil faatiha tu. Amma sura nyingine atakaa kimya kusikiliza kama alivyosema Allah mtykufu :

(وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنْصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ)
“Na isomwapo Qur’ani isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa.”
[Surat Al-A’raf 204]

Na imelazimishwa kusoma Alfaatiha kwa yalopokewa kuwa Mtume wa Allah S.A.W. amesema:
“Kila sala ambayo haikusomwa ndani yake Alfaatiha basi ina upungufu” Kaipokea Imam Rabii.

Na Amepokea Abu Daawud kuwa Mtume s.a.w. alisoma Sura baada ya Alhamdu, kikawa kizito kwake yeye kisomo, alipomaliza kusalisha aliuliza ” Je mnasoma chochote nyuma ya Imam wenu ?” Wakajibu masahaba ” Naam” akasema Mtume s.a.w. ” msifanye hivyo ispokuwa kwa Alhamdu pekee, kwa kuwa hana sala asiyesoma Alhamdu”

TANBIIHI:
Alfaatiha ni nguzo kwa Imam na Maamuma, na haitakiwi kuiwacha kwa yeyote baina yao.

Bismillahi ni sehemu ya Alhamdu, nayo ni aya yake ya kwanza, mwenye kuiwacha hana sala, na inaposomwa kwa sauti nayo isomwe kwa sauti, na ikisomwa alhamdu kwa siri nayo itasomwa hivyo hivyo.

Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
10 April 2017m

 

Published By Said Al Habsy

Ally Makame from

Tanzania

————————————–

Swali:

Asa alaikum nimesoma hukmu ya udhu nikaona kushika msahafu mpaka uwe na udhu , swali langu mie siana janaba , lakini sina udhu na niko duko hapana maji ya kutilia udhu ili nisome qur ani vp huku yake itafaa kusoma ?

JAWABU:
Waalaikum salaam warahmatullah wabarakatuh

Ni katika yenye kujulikana kuwa masuala ya udhu kwa mwenye kusoma Qur an yana khilaf baina ya wanachuoni.

Baina ya walioharamisha na kuhalalisha wapo waliosema ni Karaha na kupendelea kuwa mtu awe na udhu.

Lakini dalili za waliokataza zina nguvu, kwa kuwepo Hadithi sahihi ya Mtume s.a.w. upande wao, nayo ameipokea Imam Rabii bin Habiib R.A. katika Musnad yake kuwa Mtume s.a.w. amekataza kwa mwenye hedhi, nifasi, janaba na wale wasio na udhu kukamata msahafu na kusoma Qur an mpaka wasafike.

Baadhi ya Maulamaa wametoa ruhusa kwa wale inaokuwa vigumu kwao wao kukamata udhu kila mara mfano watoto wadogo wa Madrasa, mwenye ugonjwa wa kutokwa na mkojo au upepo, wagonjwa wasioweza kukamata maji kila mara n.k.

Hivyo ikiwa kuna uwezekano wa kuyapata maji bora kwako kutia udhu, kwa vile kuna kujitoa katika khilafu, pia ndani yake kuna kumtukuza Allah mtukufu kwa kuyatukuza maneno yake.


Na yanaruhusika katika dharura yasiyolazimika wakati wa khiyari.
Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
10 April 2017m

17. JE NISOME QUR AN BILA UDHU ?

You have a new Question by:

Ally Makame from

Tanzania

————————————–

Swali:

Asa alaikum nimesoma hukmu ya udhu nikaona kushika msahafu mpaka uwe na udhu , swali langu mie siana janaba , lakini sina udhu na niko duko hapana maji ya kutilia udhu ili nisome qur ani vp huku yake itafaa kusoma ?

JAWABU:
Waalaikum salaam warahmatullah wabarakatuh

Ni katika yenye kujulikana kuwa masuala ya udhu kwa mwenye kusoma Qur an yana khilaf baina ya wanachuoni.

Baina ya walioharamisha na kuhalalisha wapo waliosema ni Karaha na kupendelea kuwa mtu awe na udhu.

Lakini dalili za waliokataza zina nguvu, kwa kuwepo Hadithi sahihi ya Mtume s.a.w. upande wao, nayo ameipokea Imam Rabii bin Habiib R.A. katika Musnad yake kuwa Mtume s.a.w. amekataza kwa mwenye hedhi, nifasi, janaba na wale wasio na udhu kukamata msahafu na kusoma Qur an mpaka wasafike.

Baadhi ya Maulamaa wametoa ruhusa kwa wale inaokuwa vigumu kwao wao kukamata udhu kila mara mfano watoto wadogo wa Madrasa, mwenye ugonjwa wa kutokwa na mkojo au upepo, wagonjwa wasioweza kukamata maji kila mara n.k.

Hivyo ikiwa kuna uwezekano wa kuyapata maji bora kwako kutia udhu, kwa vile kuna kujitoa katika khilafu, pia ndani yake kuna kumtukuza Allah mtukufu kwa kuyatukuza maneno yake.


Na yanaruhusika katika dharura yasiyolazimika wakati wa khiyari.
Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
10 April 2017m

Published By Said Al Habsy

Je nitawezaje kujifunza kuongea lugha YA kiarabu ktk ibadhi.com ?

JAWABU:
Lugha ya kiarabu ni lugha ya waislamu, kwani kwa lugha hiyo Allah mtukufu amewaletea ujumbe wa uongofu.

Na kwa hakika tunampongeza kwa dhati ndugu yetu kwa himma yake hiyo ya kutaka kujifunza lugha hii tukufu. Allah amuwafiqishe katika yenye kheri.

Amesema Allah mtukufu:
” Na namna hivi tumeiteremsha Qur’ani kwa Kiarabu, na tumekariri humo maonyo ili wapate kuogopa na kujilinda na iwaletee makumbusho_.” 20:113

Ibadhi ni katika walioshiriki katika kuiendeleza lugha ya kiarabu na katika wao wapo wanachuoni wakubwa wa lugha. Wakiwemo Ibn Duraid Al Umaani, Khalil bin Ahmad Alfaraahidi n.k.

Katika website yetu kuna vitabu vizuri vya Sheikh wetu Khalfan bin Suleiman Altiwani – Allah amuhifadhi -, ambavyo ni mfululizo mwepesi na mzuri wa kuifahamu lugha ya kiarabu, vyenye anuani KIARABU CHAPU CHAPU, ingia katika website sehem ya vitabu utavikuta navyo viko juzuu tatu nzuri, hakuna kama utunzi huo kwa nchi zetu za Afrika ya Mashariki.

Vitegemee vitabu hivyo, utapata faida kubwa, hifadhi maneno yake, yatumie katika maongezi yako, utafungukiwa.

Pia mja faqiri Abu Muslim Alghammawi anazo darsa za kiarabu, nyepesi za audio, zinazotolewa kila wiki mara moja katika ukumbi wa wanawake Elimu ni Nuru, na zinahifadhiwa darsa hizo katika website yetu pia, ingia sehemu ya audio utazipata.

Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 April 2017m

Published By Said Al Habsy

Salim Mohamed AlMahrizi from Oman

————————————–

Swali:

Asalamu alaikum warahmatullahi wabarakatu.
swali langu ,naomba uniandikie tahiyatu zote mbili zinavyosomwa kikamilifu na kiuhakika.
shukran.

JAWABU:
Waaleykum salaam warahmatullah wabarakatuhu.

TASHAHHUD YA MWANZO (( TAHIYYATU NDOGO))

التَّحِيَّاتُ لِلَّهِ وَالصَّلَوَاتُ وَالطَّيِّبَاتُ ، السَّلَامُ عَلَيْك أَيّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ ، السَّلَامُ عَلَيْنَا وَعَلَى عِبَادِ اللَّهِ الصَّالِحِينَ،  أَشْهَدُ أَنْ لَا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ

“Attahiyyat lillaahi, wasswalawaatu wattayyibaatu, Assalaam alaika ayyuha Nabiyyu warahmatullah wabarakatuhu, Assalaam alaynaa wa alaa ibaadillahi saalihiin. Ash-hadu an laailaaha illallah wahdahuu laa shariika lahuu, wa anna Muhammadan Abduhuu warasuuluhuu”


“Ufalme ni wa Allah mtukufu, Ibada zote ni zake, na sifa njema ni zake. Amani iwe juu yako ewe Nabii Muhammad na rehma za Allah mtukufu na Baraka zake. Amani iwe juu yetu na iwe juu ya waja wote walio wema, Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah mtukufu peke yake, na Muhammad ni mja wake na mjumbe wake.”
 
TASHAHHUD YA PILI ((TAHIYYAT KUBWA))

التَّحِيَّاتُ لِلَّهِ وَالصَّلَوَاتُ وَالطَّيِّبَاتُ ، السَّلَامُ عَلَيْك أَيّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ ، السَّلَامُ عَلَيْنَا وَعَلَى عِبَادِ اللَّهِ الصَّالِحِينَ،  أَشْهَدُ أَنْ لَا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ،اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى نَبِيِّنَا محمَّدٍ وَعَلَى آلِ محمَّدٍ كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلَى آلِ إِبْرَاهِيْمَ وَبَارِكْ عَلَى محمَّدٍ وَعَلَى آلِ محمَّدٍ كَمَا بَارَكْتَ عَلَى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلَى آلِ إِبْرَاهِيْمَ فِيْ الْعَالَمِيْنَ إِنَّكَ حَمِيْدٌ مَجِيْدٌ، اللّهُمَّ إِنـــــِّيْ أَعُوْذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ وَأَعُوْذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَسِيْحِ الدَّجَّالِ ، وَأَعُوْذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ ربنا آتنا في الدنيا حسنة وفي الأخرة حسنة وقنا عذاب النار.

“Attahiyyat lillaahi, wasswalawaatu wattayyibaatu, Assalaam alaika ayyuha Nabiyyu warahmatullah wabarakatuhu, Assalaam alaynaa wa alaa ibaadillahi saalihiin. Ash-hadu an laailaaha illallah wahdahuu laa shariika lahuu, wa anna Muhammadan Abduhuu warasuuluhuu, Allahumma salli alaa Nabiyyina Muhammad wa alaa aali Muhammadi kamaa sallaita alaa Ibraahima wa alaa aali Ibraahima, wabaarik alaa Muhammad wa alaa aali Muhammad kamaa baarakta alaa Ibraahim wa alaa aali Ibrahim, fil aalamiin innaka hamiidun Majiidun. Allahumma innii audhubika min adhaabil qabri, wa audhubiika min adhaabi Jahannam, wa audhubiika min fitnatil mahyaa wal mamaat, Rabbanaa aatinaa fidduniyaa hasana, wafil aakhirat Hasana, waqinaa adhaaba nnaari.

TAFSIRI:

“Ufalme ni wa Allah mtukufu, Ibada zote ni zake, na sifa njema ni zake. Amani iwe juu yako ewe Nabii Muhammad na rehma za Allah mtukufu na Baraka zake. Amani iwe juu yetu na iwe juu ya waja wote walio wema, Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah mtukufu peke yake, na Muhammad ni mja wake na mjumbe wake. Ewe Allah mtukufu mpe rehma nabii wetu Muhammad na wema wa ummah wake, kama ulivomrehemu Ibrahim na wema wa ummah wake, na umpe Baraka Muhammad na wema wa ummah wake, kama ulivyompa Baraka Ibrahim na wema wa Ummah wake, hakika wewe ni mwenye kusifiwa, Mtukufu. Ewe mola wetu mimi ninajikinga kwako kutokana na adhabu za kaburi, najikinga kwako na adhabu ya Jahannam, najikinga kwako na masihi dajjal, najikinga kwako na fitna ya uhai na kifo, ewe mola wetu, tupe katika dunia wema na akhera tupe wema, na utukinge na adhabu ya moto”

Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com

Published By Said Al Habsy

Rashid hassan from

Tanzania

————————————–

SWALI:

Assalaam aleykum warahmatullah wabarakatuh,
Naomba kujulishwa namna ya kuswali swala ya haja na dua zake,

shukran.

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Sala ya haja ni sala ya kawaida anayo sali mja kwa ajili ya shida maalumu ilompata au ombi maalum kwa Allah Mtukufu.

Maulamaa wametofautiana kuhusu uhakika wa kupokewa kwake, wanachuoni wetu wa Mashariki hawajaipokea wala kuihadithia katika mapokezi yao kwa inavyonidhihirikia kwa mujibu ya majibu ya wenye ilmu.

Maulamaa wetu wa Magharibi wameitaja katika sala za ziada, na wakaiweka katika misingi ya kukubalika kwa kuwa ni utiifu na inaingia katika dalili za kukithirisha sala na ibada zingine.

Wametaja baadhi ya walioitaja sala hiyo kuwa atasali rakaa mbili za kawaida, atasoma ndani yake Alhamdu na Suratil Alkaafirun kwa rakaa ya mwanzo na Alhamdu na Qulhuwallahu rakaa ya pili.

Anaweza kuomba dua zake kwa lugha ya kiarabu ikiwa atazisoma ndani ya sala, na kwa lugha yoyote aitakayo ikiwa ni nje ya sala. Na ndani ya sala hiyo inaruhusika katika sijda au baada ya tahiyyat na kabla ya salam.

Na imetajwa kuwa baada ya sala, utamuomba Allah mtukufu kupitia majina yake matukufu hasa lile lenye kuendana na shida yake mfano Yaa aliimu ikiwa anaomba yanayohusiana na elimu, Yaa Haafidh ikiwa anaomba ulinzi na kinga, Yaa Ghaniyyu ikiwa anaomba utajiri, n.k.

Pia amdhukuru Allah kwa kumpwekesha kwa kusoma tahilil, Kusoma Istighfaar na kutubia kwani madhambi ni milango ya kuifunga rizki na maombi na kumsalia Mtume s.a.w. kwa idadi nyingi kisha ataomba haja yake kisha atamsalia tena Mtume S.A.W.

Muda wote inafaa kusaliwa sala hii, ispokuwa nyakati zilokatazwa. Na inapendelewa zaidi wakati wa mwisho wa usiku, kwa kuwa wakati huo Allah mtukufu humuamrisha Malaika aseme kuwa Allah anasema ” Je kuna mwenye kuniomba msamaha nimsamehe, Je kuna mwenye shida nimtatulie shida yake”
Pia kama itakuwa baada ya Asri ya Ijumaa mpaka kabla ya kuzama kwa jua. Kwa kuwa ndani ya wakati huo kuna saa haimkuti mtu akiomba ispokuwa hujibiwa maombi yake.

Na kwa kuwa kuthibiti kwake kuna maneno baina ya wenye ilmu, bora kutoita Sunnatul haaja, bora iwe Naafilatul haaja.

Na maudhui inataka tahqiiq zaidi, asaa nikinafasika nikajaribu kuitazama kwa jicho pana zaidi, tunamuomba Allah mtukufu Wallahu aalam.


Ameyaandika :
Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
Ibadhi.com
07 may 2017

 

Published By Said Al Habsy

Salum mohammed from

Malaysia

————————————–

Swali:

Assalam Alaykum…hivi katika dhehebu la kiibaadhi wana itikadi kwamba baadhi ya masahaba wataingia motoni kutokana na khitilafu zilotokea baadhi yao na kupelekea kufanya makosa baadhi yao na vipi kuhusu ile sura (4) aya (97) ambayo imewatakasa masahaba na ile hadithi ya mtume ambayo imesema “wasisemwe mabaya masahaba wake”….nimeuliza hilo swali baada ya kusoma tofauti ya ibaadhi na sunni katika web yao ya kissunni ya alhidaya baada kuona hayo nilitaka kujua ukweli juu ya hili. Na pia ikiwezekana nilikua naomba kama kutakua na kitabu ambacho kimezungumzia chimbuko la dini basi nilikua nahitajia kukisoma ili kuelewa.
ahsante

JAWABU :
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

UTANGULIZI WA JAWABU:
Tunakupongeza sana ndugu yetu kwa kule kuhakikisha kisemwacho na wengine dhidi ya Ahlulhaqq wal istiqama kutoka kwao wenyewe, kwani Uongo katika kupandisha taasuubi za kimadhehebu imekuwa ni bidhaa ya wajinga kutaka kueneza batili yao, na hivi ndivo tulivoelekezwa katika Qur an aliposema Allah mtukufu :
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ)
Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.
[Surat Al-Hujurat 6]

Na wengi katika wafasiri wa Qur an wamepokea kuwa aya hiyo ilimshukia Sahaba Waliid bin Uqba bin Abi Muit pale Mtume s.a.w. alipomtuma Kwenda kuchukua Sadaka kwa Banii Mustalaq, alivokuwa njiani akaogopa akarudi kwa Mtume s.a.w. akisema “Banii Mustalaq wamekataa kutoa zaka, na wametaka kuniua” Mtume alikaribia kutuma jeshi au alituma Jeshi likahakikishe habari hiyo na ikabainika kuwa Si kweli yale aloyasema sahaba yule na ikashuka aya hiyo” Rejea Tafsir Ibn Kathir na Tabari.

SWALI LA KWANZA:
MASAHABA KUINGIA MOTONI AU PEPONI.

CHEO CHA MASAHABA:
Bila shaka cheo chao ni kikubwa kwa ule ujumla wa dalili ulokuja katika Qur an na sunnah toharifu na athari ya Maimam wetu wema waliotutangulia na waliopo.
Amesema Allah mtukufu:
(وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ)
Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
[Surat At-Tawbah 100]

Pia Qauli yake :
(مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِمْ مِنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنْجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُمْ مَغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا)

Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.
[Surat Al-Fath 29]
Pia aya uloitaja na nyinginezo.

Na katika hadithi amepokea Bukhari kutoka Imran bin Huswain kuwa Mtume s.a.w. amesema “Bora ya ummah wangu ni karne yangu, kisha inayowafuatia, kisha inayowafuatia”

Na alikuwa Imaam Ubaidah Muslim bin Abi Kariima Altamiimi R.A. akijifakhari kwa kuwa na walimu katika masahaba na kupokea kwake hadithi kutoka kwao”
Rejea Imam Abu Ubaidah na fiqh yake cha Dr. Mubarak Alraashidi.

Al Imam Abu Yaaqub Alwarjalani alisema alipofikia kabri la Mtume s.a.w. “Hakuna wa kumuiga ispokuwa aliyomo katika kaburi hili, Amma Masahaba wa Mtume s.a.w. wao ni bora kuwafuata kwa ule ukaribu uliopo baina yao na Mtume s.a.w.”

Na hayo tunayakuta kwa wanachuoni wetu wote, waliopita na waliopo, na imetosha yale aloyaandika Samaahat Sheikh Ahmed bin Hamed Alkhalili – Allah mtukufu amuhifadhi – katika risala yake ya kiarabu cheo cha Masahaba. Na makala ya mwisho nzuri aloiandika Sheikh Hafidh Alsawwafi – Allah amuhifadhi – imeshawekwa katika website tayari.

PEPO NA MOTO
Masuala ya kumhukumia fulani pepo au moto kwetu sisi yanataka dalili isiyo na shaka kama Qur an, na kwa hivyo wanachuoni wetu hawamhukumii fulani kwa dhati yake moto au pepo ispokuwa kwa dalili yenye uzito kama wa Qur an. Kwa hivyo kuwaegemezea Maibadhi kuwa wamewahukumia watu fulani moto ni uongo wa wazi usio na chembe ya shaka.

HAKUNA MWANACHUONI WETU HATA MMOJA ALIYESEMA FULANI ATAKWENDA MOTONI

Pamoja na hayo; sisi tunakutia katika hadithi wanazopokea masunni kuwa masahaba wataingia motoni bali imethibiti kwa tawaaturi kuwa baadhi ya kundi la masahaba walikuwa wanaita katika moto,…

Amepokea Bukhari na Muslim na wengineo kwa lafdhi tofauti kuwa Mtume S.A.W. alisema ” Maskini Ammar, atauwawa na kundi la waasi, anawaita katika pepo nao wanamwita katika moto”

Baada ya Mtume s.a.w. kulihukumia kundi hilo kuwa wanaitia motoni, akasema ” Atakayemuua Ammar na kuchukua mali yake atakwenda Motoni” Na aliyemuua mubashara ni Abulghaadiya naye ni katika masahaba walioshiriki baia ya Ridhwani.
Pia tunakutia katika hadithi sahihi kwao wao kuwa Mtume s.a.w. atawaona masahaba wake siku ya Qiyama wakitaka kunywa maji katika hodhi lake tukufu, atasema njooni, njooni, mara watafukuzwa kama wanavyofukuzwa ngamia, ataita Mtume S.A.W. MASAHABA WANGU, MASAHABA WANGU… patasemwa ” hujui walichozusha baada yako” atasema Mtume S.A.W. ” WAANGAMIE… WAANGAMIE”
Bali tunaona katika wao masunni wanaosema kuwa Hadithi hiyo inawahusu Muawiya bin Abi Sufian na kundi lake.

Bali tumekutia katika Masunni wanaomsifu Ally bin Abi Talib kuwa hali yake ni kama ya Firauni, wala hakuwa anapendwa na masahaba wengine.. N.k.
Basi itakuwaje hukmu ya masunni kwa nafsi zao ? Je watajikafirisha pia ?… Hapo watasema laaa hizo ni rai za watu hao binafsi, jawabu yetu ikiwa ni hivyo kwa nini – kama ni kweli – hayo msemayo kuhusu Ibadhi isiwe ni kwa wale waliosema tu ?, na siyo kwa wote.

Lakini taassubi inatia upofu, waandishi waovu wanazusha uongo kisha wanaujadili uongo huo na kuwakafirisha wengine kwa uongo walioutunga wenyewe. Wallahu l mustaan.

MASAHABA NA MAKOSA.
Waislam wamekubaliana kuwa Mitume pekee katika binadamu ndio waliokingwa na makosa na kukosea, na yoyote asiyekuwa yeye anakosea bila shaka yoyote.

Na hali ya masahaba katika kukosea ni kama hali ya mwingine yoyote katika viumbe, kwani imethibiti kuwa wapo masahaba waliosimamishiwa Hukmu ya Zina, na waliokatwa mikono kwa wizi, na waliotiwa adabu kwa kumtupia uchafu wa Zina mke wa Mtume S.a.w., walokuwa walevi, na waliouwawa masahaba wenzao n.k. yote hayo yameandikwa na wao masunni kabla ya maibadhi, na unaweza kurejea kitabu cha Al istibdaad cha Samaahat Sheikh Ahmed Alkhalili – Allah amhifadhi – utayakuta hayo na mengineyo.
Na hukmu kwa Allah mtukufu haina upendeleo, siku ya Qiyama sababu na nasabu ni uchamungu tu.
Atakayekwenda Amesalimika na uchafu, ameepukana na mizigo, ametubia kwa aliyoangukia ndani yake, awe sahaba au asiwe sahaba… Huyo atakuwa amesalimika.

Ibadhi ni katika wa mwanzo waloita watu kuyakalia kimya yalotokea baina ya waliopita, na sote tuzingatie ile hali tuliyo nayo sasa, lakini uovu wa baadhi ya watu haukutaka kuyakalia kimya, wakakafirishwa Ahlu nahrwaani na kutukanwa nao ni katika MASAHABA WASOMI, WACHAMUNGU, wala haukuwafalia kitu usahaba wao. Na haikuwatosha hilo bali wakawafirisha Ibadhi kwa kuwa wao wanaitakidi kuwa Ahlu nahrawan walipatia, na wanawaheshimu na kuwapenda… Basi mizani gani hizo zinatumiwa katika hukmu ?

Hapo wakasimama baadhi ya wanaelimu wetu na kuonyesha yale yalokuwepo kwa wenzetu, pamoja na kuzirudisha Tuhuma mbovu zilotungwa, na ikiwa kutaja makosa yalotokea ni kosa basi ummah mzima umekosea, na Mtume s.a.w. kasema ummah haukubaliani katika upotevu, kwani hakuna Madhehebu ambayo haikutaja yalotokea baina ya masahaba, basi sote tusafishe nyoyo zetu, tuyakalie kimya yaliyopita, Wasisemwe vibaya Ahlunahrawaan na kuzushiwa ya Uongo yatakayotulazimisha kubainisha Uongo wa madai hayo na kutaja yalotokea kwa uadilifu bila upendeleo wowote.
Wallahu aalam.

Ameyaandika
Mja dhaifu kwa mola wake
Khamis bin Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
10 May 2017

 

Published By Said Al Habsy

Nasra Thomas from 

Tanzania
————————————–
Swali:

Sala kabla na baada ya kulala..

JAWABU:
Sala ya mwisho kabla ya kulala ni Witri, husaliwa rakaa tatu. Rakaa ya mwanzo Alhamdu na Sabbihisma, na Rakaa ya pili Alhamdu na Qulya ayyuha l kaafiruun. Na rakaa ya tatu Alhamdu na Qulhuwallahu.
Inasaliwa kama unavyosali Faridha ya sala ya Magharibi.

Na sala ya mwanzo baada ya kuamka ni Sunnah ya alfajiri, ambazo ni rakaa mbili khafifu, na maana ya khafifu yaani husomwa kwa kisomo kifupi sio kirefu.

Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis binYahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
10 May 2017

Published By Said Al Habsy

1) unaweza kumpa zakka mtu anaetaka kwenda kutibiwa? Ana gari, biashara lakini hana cash na pia ana madeni?

JAWABU:
Nimemuuliza Sheikh wangu Ismail bin Nassor Al- oufi – Allah amuhifadhi – Akasema : “Inajuzu kumpa kwa kule kuwa kwake ana madeni, kwani gari yawezekana katika maisha ya sasa ni muhimu kwa ajili ya familia, watoto na dharura mbali mbali za kimaisha.”

Nimesema:
Wanachuoni wetu – Allah awaridhie – wamesema deni hilo lisiwe linatokana na mambo ya haram kama kamari n.k. au lisiwe latokana na israfu au mambo ya ziada yasiyo ya lazima katika maisha pia iwe ameshindwa kulipa au akitumia katika matibabu hayo atashindwa kulipa deni lake hilo.”

Litazamwe hilo wala lisichukuliwe ispokuwa kwa uadilifu wake.
Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
14 May 2017

Published By Said Al Habsy

Suleiman Rashid from

Tanzania
————————————–
Swali:

Assalamu Alaikum
Mume kamwambia mkewe ukiramba jungu si mke wangu.
Mke akachovya kidole katika jungu kisha akaramba au akachota kwa kijiko kisha akaramba au akaingiza kichwa ndani yake.Je ni talaka tayari ?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Hakika ni katika yenye kusikitisha kukutia vitendo kama kwa wanaume waloekewa amana ya talaka katika shingo zao.
Imekuwa hakuna tofauti na wanawake katika haraka zao bila kufikiri. Kuna mahusiano gani baina ya ulambaji vyungu na talaka ? Kama sio wehu usio na tiba, na ujinga uliopitiliza ?
Na ikiwa yote hayo hana basi huenda ni mtoto bado, asubiriwe akue hata aozeshwe mke mwingine.

Amma talaka tayari imetokea, kwa kuwa yote yaliyofanywa ndio maana ya kulamba jungu. Na bila shaka jungu halilambwi lenyewe kama lenyewe bali vilivyomo ndani yake.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Mja faqiri kwa mola wake
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
16 may 2017

 

Published By Said Al Habsy

Rahma Minya from

Oman
————————————–
Swali:

Saslaam aleiku warahmatullahi wabarakatuh.sswali langu ni je nikakh ya simu ni halal ?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmayltullah wabarakatuh.

Ndoa ni mafungamano ya baina ya mwanamke na mwanamme ya maisha yote hapa duniani kama watapewa tawfiiq.
Na kwa hivyo inapewa uangalizi mkubwa na heshima kubwa katika kuchagua na kuiendeleza.

(وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ)
Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
[Surat Ar-Rum 21]

Wanachuoni wameweka sharti la kusihi mkusanyiko wa ufingishaji ndoa kuhudhuria kwa muowaji na muozeshaji. ((Walii au aliyepewa idhni na walii )).
Ikiwa muowaji hawezi kuhudhuria ameruhusiwa kisheria kuweka wakala atakayekuwa badala yake.
Na yote haya ni kuondosha kutojua au kutokuwa na uhakika wa kifanyikacho.

Kwani sote tunajua kuendelea kwa teknolojia kumekuwa na kheri nyingi na madhara mengi, na katika madhara yake ni kukosekana kwa uhalisia na ukweli. Kila kitu kinatengenezwa sasa hivi, sauti, video, picha n.k. hata mtu asiyejua aweza kujua ni uhalisia kumbe ni uongo.

Na kwa msingi huu, haiwezi kutegemewa ndoa ya simu, bali litabaki sharti la wahusika kuhudhuria, sawa ikiwa wenyewe au kwa niaba.
Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
25 May 2017.

 

Published By Said Al Habsy

Abdul hamad from

Tanzania

————————————–

Swali:

assalamu alaikum.naomba kuulza je?kupokea chakula kW makafr walichpika kw pasaka inafaa

JAWABU:
Muislam anatakiwa ajue kuwa katika mambo ya wajibu kwake ni kuwachukia katika moyo makafiri wote na waovu.

Huu ni wajibu wa kidini alotuelekeza Allah mtukufu katika Qur an, amesema:
(قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنْكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ شَيْءٍ ۖ رَبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ)
Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Allah mtukufu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Allah mtukufu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Allah mtukufu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo.
[Surat Al-Mumtahana 4]

Na hili la kuwachukia halikataani na kufanyiana nao wema ikiwa hawaupigi vita uislam na waislam, Allah mtukufu amesema :
(لَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ)
Allah mtukufu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Allah mtukufu huwapenda wafanyao uadilifu.
[Surat Al-Mumtahana 8]

Pia kufanyiana wema kusiingie mpaka muislam kuidhuru dini yake, Amesema Allah mtukufu:
(بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ * لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ * وَلَا أَنْتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ * وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَا عَبَدْتُمْ * وَلَا أَنْتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ * لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ)
Sema: Enyi makafiri!, Siabudu mnacho kiabudu; Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.Wala sitaabudu mnacho abudu.Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
[Surat Al-Kafirun 1 – 6]

Na sote tunajua kuwa Pasaka ni sherehe ya kidini, bali kuisheherekea kwa namna moja au nyingine ni sehem ya ukafiri. Na kwa hivyo mwambie kuwa mipaka ya dini yangu hainiruhusu katika vyakula vinavyohusiana na sherehe za dini yenu. Na zipo sherehe nyingine nyingi za kijamii ambazo mnaweza kushirikiana. Hiyo ndiyo fat wa inayofanyiwa kazi kwa wanachuoni wetu.
Wallahu aalam

Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
07 May 2017

Published By Said Al Habsy

Abdul hamad from
Tanzania
————————————–
Swali:
assalamu alaikum. naomba kuuliza kussali na nguo into picha inafaa.?na IPI picha inofaa kusali nayo?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.
Picha zipo za namna tatu.

1. Picha ya kuchonga:
Na picha hizi ndio ziliokuwa nyingi wakati wa Mtume – Sallallahu alayh wasallam – nazo ndio yamekuja makatazo ya wazi yasio na khilafu baina ya wanachuoni. Kuwa wachongao picha za namalna hii wamelaaniwa. Na siku ya Qiyama wataambiwa vipeni roho vile mlokuwa mkivitengeneza katika maisha ya Dunia. Bila shaka namna hii ya picha haikubaliki ndani ya sala ispokuwa kwa dharura kama katika pesa za coins. Na zipo baadhi ya nguo katika jeans na mashati vishikizo vyake vina namna hii ya picha, basi watazame sana wenye kuvaa. Katuni pia zinaingia katika hukmu ya picha hizi kwa fatawa ya Samaahat Sheikh Ahmed Alkhalili – Allah mtukufu amuhifadhi –

Izingatiwe kuwa kuna Hadithi ya Bii Aisha – Allah amridhie – kuwa Mtume – Sallallahu alayh wasallam – aliruhusu visanam vya kuchezea watoto.

2. Picha za kuchora
Picha hizi zilikuwepo pia wakati wa Mtume – Sallallahu alayh wasallam – na uhakika ni kuwa kuchora ni sehem ya kuchonga, na kwa hivyo Jumhuur ya wanachuoni wameharamisha aina hii ya picha pia ispokuwa katika vitabu vya kusomeshea. Hivyo aina hii pia Haifai kusali nayo kwa kule kuwa kwake ni maasi na haukutani utiifu na uasi sehem moja.

3. Picha ya photograph
Nayo ni kukifunga kivuli sehem fulani, kama ilivyo kioo. Na huku sio kuchora wala kuchonga.
Jumhuur ya wanachuoni wameruhusu watu kupiga picha za namna hii. Lakini pia isiwe kwa kupitiliza mipaka hata imefikia watu badala ya kushughulika na ibada mfano katika hijja au umra hata imekuwa baadhi yao hawana walifanyalo kwa siri baina yao na mola wao. Tunamuomba Allah mtukufu stara yake.

Wametofautiana wanachuoni kwa watakaosali na picha ya namna hii na lenye nguvu kwa Sheikh Almuhaddith Saeed Alqannubi – Allah mtukufu amugifadhi – ni kuwa Haifai kusali na nguo zenye mapicha kwa kuwa ni sababu ya kuondoka kwa khushuu. Imepokewa kuwa Mtume – Sallallahu alayh wasallam- alipewa zawadi ya nguo yenye michirizi ya rangi rangi, baada ya muda akairejesha akisema imekaribia kunifitini – kiniharibia- katika sala yangu.

Pia katika tanbiihi ni kusali na nguo zenye nembo za ukafiri kama toxic, misalaba, vilabu vya mipira vya makafir n.k. yote haya hayafai.

Wallahu aalam.

Mja dhaifu
Khamis Bin Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
25 May 2016

 

Published By Said Al Habsy

abdul hamad from

Tanzania

————————————–

SWALI

assalamu alaikum.naomba kuullza tnswaona katk maziko wanamwaga maji juu ya kabur na kwa watoto huwekewa kuti juu ya kabur nini kauli yenu kuhusu hili ?

 

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Amesema Sheikh Saeed Alqannubi – Allah amuhifadhi –

“Zimekuja baadhi ya Hadithi zinajulisha hilo -la kumwagia maji juu ya kaburi- na wenye ilmu zaidi ya mmoja wamesema hadithi hizo zapeana nguvu, na kwa hivyo hoja inasimama kwa hadithi hizo, na hili lilosemwa limeipatia njia ya sawa”
Rejea Suaal ahl dhikr 19 Ramadhan 1424 sawa na 13/11/2003.

Amma hilo la kuweka kuti juu ya kaburi, Allahu aalam.

Kinachotajwa katika baadhi ya mapokezi ni kuwa Mtume sallallahu alayh wasallam aliweka tawi la mti kwa kulichomeka, na riwaya yenyewe inataka kuthibiti kwanza lhalaf hata ikithibiti hakuna dalili ndani yake ya hilo walifanyalo.

Na imethibiti kwa Sheikh wetu Alqannubi- Allah amuhifadhi- kuweka jiwe moja kama alama ya kujua kaburi la maiti wake kama alivofanya Mtume s.a.w. kwa ndugu yake wa kunyonya Uthman bin Madhuuni -Allah mtukufu amridhie –

Wallahu aalam.

Ameyaandika
Mja dhaifu kwa mola wake
Khamis bin Yahya Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
28 May 2017m

Published By Said Al Habsy

ALI SALEH from

Tanzania

————————————–

Swali:

s’alaikum,
mm naoba kuuliza kuhu uhalali wa kula nyama ya sungura
Naomba ufafanuzi na kama ikiwezekana kuwe na ushahidi wa aya au hadithi .

Wabillahi taufiq

JAWABU:
Sungura ni mnyama kama wengine ambaye hakuna dalili ya kukataza kula nyama yake.

Na Allah mtukufu na Mtume wake -Sallallahu alayh wasallam- wametaja wanyama waloharimishwa na kuruhusu kila wasiokuwa haram.
Amesema :

(قُلْ لَا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَنْ يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنْزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَحِيمٌ)

Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Allah mtukufu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
[Surat Al-An’am 145]

Na kikawekwa kipimo cha ujumla cha vyakula vyenye kuliwa na vinywaji vya kunywewa kuwa vizuri visiwe vichafu.

يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُمْ مِنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ

Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyo kufunzeni Allah mtukufu. Basi kuleni walicho kukamatieni, na mkisomee jina la Allah mtukufu. Na mcheni Allah mtukufu; hakika Allah mtukufu ni Mwepesi wa kuhisabu.

{Sura Al-Ma’idah, Ayah 4}

Na Allah mtukufu amekataza kuharamisha hovyo, vile vizuri alivohalalisha

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ)
Enyi mlio amini! Msiharimishe vizuri alivyo kuhalalishieni Allah mtukufu, wala msikiuke mipaka. Hakika Allah mtukufu hawapendi wakiukao mipaka.
[Surat Al-Ma’idah 87]

Na Mtume Sallallahu alayh wasallam akatubainishia aina ya wanyama wasiofaa kuliwa akasema:
387) … أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيءِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «أَكْلُ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنَ السِّبَاعِ وَذِي مَخَالِبَ مِنَ الطَّيْرِ حَرَامٌ».
Abuu Ubaida kutoka kwa Jabir bin Zaid kutoka kwa Abi Huraira kutoka kwa Mtume Sallallahu alayh wasaalam, amesema:
“Kula kila mnyama mwenye chonge au ndege mwenye kuwinda kwa kucha ni haram”

Na katika athari za wanachuoni wetu amesema sheikh Muhammad Alkindi – Allah mtukufu amrehemu- katika kitabu chake Bayaanu shar’i jz 7 uk 87 ” Hapana ubaya kula nyama ya sungura”
Pia ametaja hivyo hivyo Sheikh Athumeini katika Taajul mandhuum.

Na wapo waliosema ni Makruhu kwa sababu inasemwa kuwa anapata hedhi.
Ametaja hayo Sheikh Shammakhi – Allah amrehem – katika kitabu al iidhaah jz 1 uk 330. Pia Sheikh Athumeini katika Taaj na Sharh nniil jz 1 uk 399

Na zimekuja baadhi ya riwaya kuwa Mtume aliletewa nyama ya Sungura, hakuila wala hakukataza kapokea Baihaqi na Abu Daawud.

Na zipo riwaya zingine zisemazo kuwa Abu Talha aliwinda Sungura, akamchinja akampelekea sehem ya nyama Mtume -Sallallahu alayh wasallam- akaikubali.
Bukhari 2572, Muslim 1953.

Amesema Imaam Qutbul aimmah – Allah mtukufu amridhie – katika Sharh nniil jz 2 uk 203 kuwa hiyo Qauli ya kuhalalisha ndiyo Qauli ya Imam Shaafi.

Dalili ni hizo, Wallahu aalam.

Amezikusanya
Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
4 Ramadhan 1438h
30 May 2016m

Published By Said Al Habsy

 

Ally Akizimana from

28. KUMKUMBATIA MKEWE WAKATI WA MCHANA WA RAMADHANI.

Sweden

————————————–
Swali:

Aslam aleykum
Swali langu nilikua nataka kujua inaruhusiwa kumshika,kumkumbatia mke wako katika mchana wa mwenzi wa Ramadhani?
Mvh Ally
JAWABU:
Waaleykum salaam warahmatullah wabaarakatuh.

Muislam ajiepushe na kila ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa swaumu yake.
Ajue hii ni fursa adhimu ambayo kupoteza siku moja ni msiba usioweza kupozwa na maombolezo ya zama zote.

Usiku upo na Allah mtukufu ameruhusu mke na mme kufanya yote wayatakayo katika waliohalalishiwa, Amesema Allah mtukufu:
أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَكُمْ وَأَنْتُمْ لِبَاسٌ لَهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَخْتَانُونَ أَنْفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنْكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنْتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Allah mtukufu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Allah mtukufu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Allah mtukufu, basi msiikaribie. Namna hivi Allah mtukufu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate kumcha.

{Sura Al-Baqarah, Ayah 187 }

Tazama aya hiyo ndugu yangu, yasema ni mipaka ya Allah mtukufu msiikurubie, basi vipi anajiaminisha na anakwenda kuchezea pesa karibia na lindi?

Swaumu ni kujizuia na matamanio.

Allah mtukufu atuwezeshe kufikia malengo ya swaumu, atukubalie, na atuweke katika watakaosamehewa na kustahiki pepo ya juu ya Firdaws.

Wallahu aalam.

Ameyaandika
Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
4 Ramadhan 1438h
30 May 2017m

Published By Said Al Habsy

Said Mohamed Abdallah Al Harthy from

Oman
————————————–
Swali:

Asalaam alee”kum, Shekhe napenda kueleweshwa ya kwamba kila mara baada ya ikama ya sala, naona waumini wakiwa nyuma ya imam, wananza kuvutana na kusukumana, hadi imam anaanza kwa takibirat ihram, je?? Shekhe hii mivutano nyuma ya imam ina maana gani??

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Sala ni unyenyekevu wa moyo unaopelekea utulivu wa viungo, mmoja katika wema waliopita alimuona mtu akicheza cheza ndani ya sala akasema : “Law ungetulia moyo wake vingetulia viungo vyake pia”
Na walikuwa wema waliopita wakiingiwa na khofu hata wakibadilika rangi wakati wa kutia udhu, wakiulizwa hujibu kuwa ni khofu ya kwenda kusimama mbele ya Allah mtukufu katika sala.
Na kwa hivyo Uislam ukaweka utaratibu mzuri wa kupanga swafu za sala, kuwa wafuate nyuma ya Imam watu wasomi au wenye kujua heshima na uzito wa sala kwa akili zao nyingi.
Pia imeweka utaratibu wa kuwa watu waanzie katikati wakielekea kulia na kushoto bila vurugua wala zogo.
Pia imemkataza aliyechelewa kuja mbio bali aje hali ana utulivu na amechunga heshma yake. Atakachokikuta atasali pamoja na Imam na kilichompita atakilipa. Hadithi hiyo ameipokea Imaam Rabii bin Habiib katika Sahih Musnad yake no 217.

Pamoja na haya pia kuna adabu za msikiti ambazo bila shaka wengi katika sisi tunazijua. Ambazo zote zinewekwa kulinda utulivu ndani ya msikiti na unyenyekevu kwa wenye kuabudu.
Kama kutoongea kwa sauti, au kuto ongea yasiyohusiana na amali za msikiti, bali zipo riwaya amezipokea Imaam Rabii no 227, Nasaai no 3360, Malik katika Muwatta 17

zinazomkataza mtu kusoma Qur an kwa sauti kubwa sana ikiwa kuna wengine wanasali au na wao wanasoma Qur an basi wasije wakavurugana na kupandishiana sauti.

Pia yapo makatazo ya kukaa vikundi vya maongezi kabla ya sala ya ijumaa.

Na katika Riwaya ya Tabrani no 7601 Mtume Sallallaahu alayhi wasallam amesema ” wawekeni mbali na miskiti yenu wendawazimu, watoto, magomvi yenu, sauti zenu, kunyanyuliana panga zenu, na kusimamishia huduudi zenu…”

Na katika hadithi aloipokea … Amesema Mtume Sallallahu alayh wasallam:
>
Watakuja watu katika ummah wangu wanaokwenda msikitini wakakaa kwa vikundi, ikawa mazungumzo yao ni dunia na kupenda dunia, basi msikae nao kwani Allah mtukufu hana haja nao”

Kwa hivo haitakiwi wao kufanya hilo zogo, na hakuna linalopelekea hilo zogo kwani utaratibu wa upangaji wa sala unajulikana.
Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 Ramadhan 1438h
8 June 2017

Published By Said Al Habsy

Rashid Mahrooqi from

Oman
————————————–
Swali:

Nini hukumu ya kuvaa jambia bila kuuliza wanao husika katika urithi wa ile mali ?

JAWABU:
Uislam umeweka utaratibu wa namna ya kutumia mali ya mwengine lazima iwe kwa ridhaa ya mwenye mali.

Na binadam muislam anapofariki mali inakuwa ni ya warithi wake, kila mmoja analo fungu lake kapewa na mola wake kama ulivokuja utaratibu katika Suurat Nisaa aya 11 na 12 na aya ya mwisho.

Na inakatazwa kuchukua mali ya wengi kabla ya ugawaji ikiwa yeye yumo katika warithi au wenye kustahiki, na inahesabiwa kuwa hiyo ni ghuluul (( khiyana)) ambayo imekatazwa katika Qur an aliposema Allah mtukufu:

وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَنْ يَغُلَّ ۚ وَمَنْ يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana. Na atakaye fanya khiyana, atayaleta Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila mtu atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa.

-Sura Aal-E-Imran, Ayah 161.

Pia katika hadithi Mfanyakazi wa Mtume sallallahu alayhi wasallam ulipomjia mshale na kumuua, Masahaba wakamfurahikia kuwa ameipata pepo kwa kuwa kwake katika Jihaad.
Mtume akasema : ” Hakika shuka aloichukua kabla ya kugawa mali tulizopata vitani inamuwakia moto”

Basi hiyo ndiyo hali shuka basi vipi itakuwa Jambia ?

Na hiyo ndiyo hali ilompata swahaba aliyefia vitani basi vipi sisi?

Amepokea Imam Rabii katika Musnad yake hadithi no 660 kuwa Mtume – Sallallaahu alayhi wasallam-
“Atakayejichukulia haki ya Muislam kwa kiapo cha Uongo, Allah mtukufu amemuharamishia pepo na amemuwajibishia moto” akasema mtu mmoja “hata kitu kidogo ewe Mjumbe wa Allah ?” Akasema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-: “hata ikiwa ni mswaki wa mti”

Amma ikiwa watamridhia warithi wote hakuna katazo kwa sababu ni mali yao, na bora mirathi igawiwe ili kila mmoja abakie na mali yake akiwa na milki kamilifu ya matumizi.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu:
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 Ramadhan 1438h
8 June 2017m

Published By Said Al Habsy

MME HANA UWEZO WA KUNITIMIZIA HAKI ZANGU ZA MSINGI

Swali:

asalam alaykm
shekh naomba uniambie nini hukmu ya suala langu na mimi natakiwa nifanye nini
Mume wngu alishindwa kimaisha na tukaamua kwa pamoja nirudi nyumbani kwetu ili nisubiri mpka hali itakavyo tulia nilikaa hapo nyumbani kwa muda wa mika miwili na katika muda huo mimi na mume wngu tunaona mara moja kwa mwenzi sababu yy yupo tanzania bara mimi nipo zanzibar na kisogizio kuwa hana pesa na pia matumizi ya mimi na watoto nafaya mimi yeye analeta kidogo sana
Alahmdulilah nimestahamili lakini nikaja kukundua kuwa ana mke kwa mwaka sasa lakini mimi hakuniambia
Nimedai haki zangu za msingi kama mke basi ananiambia kuwa hana uwezo kwa sasa sio kuwa hataki lakini uwezo hanaa
anakuja kwa mwezi siku 4
matumizi hamna

samahani kwa maelezo mengi.

JAWABU:
Allah mtukufu akupe subra na uvumilivu katika hali hii unayopitia.

Sisi tunawakumbusha wanamme wajue kuwa wanawake walowaoa ni amana katika shingo zao walizozibeba kwa jina la Allah mtukufu na Jina la Mtume wake Muhammad -Sallallahu alayh wasallam- kuifanyia khiyana amana hiyo ni kumfanyia khiyana Allah mtukufu na Mtume wake Sallallaahu alayh wasallam –
Amesema Allah mtukufu:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ

Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Allah mtukufu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.
{Sura Al-Anfal, Ayah 27}

Na amesema Mtume -Sallallahu alayh wasallam- katika khutba yake ya kuaga ummah wake:
” Mcheni Allah mtukufu kuhusu – haki za wanawake – hakika nyinyi mmewachukua kwa amana ya Allah mtukufu, na mmehalalishiwa tupu zao kwa neno la Allah mtukufu… Na wana haki zao kwenu nyinyi ya kuwalisha na kuwavisha kwa wema”

Na ni katika haki ya mwanamke pia: kupewa sehemu ya kukaa, na kupata haki ya kitanda.

Na imelazimishwa katika kuongeza wake wengine upatikane uadilifu kwa wake wote, kama alivosema Allah mtukufu:
وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانْكِحُوا مَا طَابَ لَكُمْ مِنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا

“…Oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu…”
{Sura An-Nisa’, Ayah 3}

Na imekatazwa kumuacha mke mwingine bila kumhudumia ikawa kama aliyetundikwa amesema Allah mtukufu:

وَلَنْ تَسْتَطِيعُوا أَنْ تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِنْ تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا

“…Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamcha Allah mtukufu basi Allah mtukufu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu.
{Sura An-Nisa’, Ayah 129}

Na Mtume sallallahu alayhu wasallam amesema :

“من كانت له امرأتان فمال إلى إحداهما، جاء يوم القيامة وأحد شقيه ساقط”
” Atakayekuwa na wake wawili akamili kwa mmoja wao, atakuja siku ya Qiyama hali upande mmoja wa mwili wake umeporomoka”
Kaipokea Imam Ahmad, na Wapokezi wa Sunan, Tayalisi 1597, Abu Daawud 2133, Tirmidhi 1141.

Hivyo tunamshauri dada yetu, amfahamishe haya tuloyaandika asaa ikawa ni moja ya njia ya kumtoa katika hilo aliloingia la kutotekeleza wajibu wake vyema.

Na ikishindikana basi wafahamishe walio juu yake kama wazee wake, au wanachuoni anaowasikiliza. Na usiache kupita njia ya kuitaka sulhu kwani Sulhu ni bora kuliko kuachana.
Amesema Allah mtukufu:

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِنْ بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَنْ يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنْفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِنْ تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا

Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamcha Allah mtukufu basi hakika Allah mtukufu anazo khabari za yote mnayo yatenda.
{Sura An-Nisa’, Ayah 128}

Na amesema Allah mtukufu:
وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِنْ أَهْلِهَا إِنْ يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا

Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Allah mtukufu atawawezesha. Hakika Allah mtukufu ni Mjuzi Mwenye khabari.
{Sura An-Nisa’, Ayah 35}

Allah mtukufu akupeni yenye kheri nanyi daima.
Wallahu aalam.


Ameyaandika
Mja faqiri kwa mola wake
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 Ramadhan 1438h
8 June 2017m.

 

Published By Said Al Habsy

HADITHI ZA KUTABIRI KUSHUKA KWA NABII ISSA A.S.

You have a new Question by:

Ahma Muhama from

Tanzania

————————————–

Swali:

Wakati mnaamini kwamba Nabii Isa as ameshafariki sawa na wanadamu wengine, basi mnazionaje Hadithi zinazotabiri juio na ushukaji wa Isa mwana wa Mariamu ?

JAWABU:
Waalaykum salaam.
Ndugu yetu mpenzi katika madhehebu yetu ya Ahlilhaqq wal istiqama mambo ya kurudi kwa Nabii Issa -Alyh salaam- siyo mambo ya asili ya itikadi, kwa kukosekana dalili ya wazi isiyo na shaka kuhusu maudhui hiyo. Na kwa hivyo inajuzu kutofautiana katika masuala haya baina ya watu kwa mujibu wa uchukuaji dalili na kuzitolea hoja. Kosa hupatikana katika maudhui hii ni kule kulifanya jambo hili ni la kiitikadi kiasi ikawa haifai kutoafautiana, hilo ndio kosa ambalo waislam wote kwa mujibu wa madhehebu zao inatakiwa kujiepusha nalo.
Hivyo kusema kwako mnaamini kuwa Nabii Issa alayh salaam hatorudi hiyo haina maana kuwa sisi tunasema mwenye kuamini amehiliki, haasha.
Kwa wanachuoni wetu kuna rai tatu katika masuala haya:
1. Kuyakalia kimya masuala hayo nayo ndio rai ya Jumhuur ya wanachuoni wa mashariki (( Iraq, Oman, Zanzibar))
Imam Nuruddin Alssalimi – Allah mtukufu amrehem – alipoulizwa kuhusu hili ” imewatosha kukaa kimya waliopita kabla yetu, nako hakujawa dhiki kwetu”
Na katika yanayonukuliwa kutoka kwa samaahat Sheikh Ahmed bin Hamed Alkhalili – Allah mtukufu amuhifadhi- alisema ” ikiwa atakuja tutamuona na kama hatokuja haitudhuru kitu” au kama alivosema.

2. Ameshakufa kama wengine wala harudi, nayo ni rai ya baadhi ya wamashariki na huenda baadhi ya wamagharibi. Na katika walio mashuhuri katika hilo ni sh. Ibn Abi Nabhaan Nassor Bin Jaeed amesema kuwa khabari za Issa bin Maryam kwake yeye hazijathibiti. Na samaahat sheikh Ahmed Bin Ahmed Alkhalili – Allah mtukufu amuhifadhi – amemili katika rai hii baada ya kunaqishi vizuri dalili za kila upande na ruduud zake kama ilivyo katika kitabu cha fatawa za Itikadi.

3. Atarudi na bado hajafa, nayo ni rai ya jumhuur ya wanachuoni wetu wa magharibi waliopita. Kwao wao walizipokea riwaya hizo kutoka kwa wasiokuwa maibadhi na kwa vile walizihukumu kuwa zimethibiti wakaziamini na kuzichukua kwa dhana kubwa sio kiitikadi ya yaqini.

Kwa hivyo kwetu sisi hazijathibiti kufikia Mutawaatir. Hivyo si suala la itikadi.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
26 Ramadhan 1438h

Published By Said Al Habsy

abdul hamad from

Tanzania

————————————–

Swali:

assalamu alaikum. naomb kuulza nn kauli yenu kuhusu muislamu alirtad kisha aksilimu tena kW Mara ya pili?

JAWABU:
Qauli yetu ni qauli ya Allah mtukufu :

قُلْ لِلَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ يَنْتَهُوا يُغْفَرْ لَهُمْ مَا قَدْ سَلَفَ وَإِنْ يَعُودُوا فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ الْأَوَّلِينَ

Waambie wale walio kufuru: Wakikoma watasamehewa yaliyo kwisha pita. Na wakiyarudia basi imekwisha pita mifano ya wa zamani.

{Sura Al-Anfal, Ayah 38}

Allah mtukufu amthibitishe katika touba yake na kumkubalia.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
22 june 2017m

Published By Said Al Habsy

KUBEBANA KWA SUNNAH


You have a new Question by:


Rashid Suleiman from

Tanzania
————————————–


Swali:

SALAAM: Naomba ufafanuzi kuhusu sala za sunna na hoja ya niya ya kubebana. Mfano nimeingia msikitini nahitaji kusali sunna ya kabliyya alfajiri na tahiyyatul-masjid kwa bahati muda hauruhusu kusali zote. Nini nifanye?
1. kwa mazingira hayo naomba nijue jee hii hoja ya kusali kabliyya kuibeba tahiyyatul-masjid inakubalika(kama ipo hadithi ni vizuri)
2. Kama haikubaliki kwa muktadha huo ni sali ippi kabliyya ya alfajiri au tahiyyatul-masjid

JAWABU:


Sunna zinazosaliwa zipo za aina nyingi, zipo zinazoitwa “Sunanun raatibatun” yaani zilopangiwa namna na wakati maalum wa kuziswali na na zingine hazijapangiwa na kwa hivo huitwa nafla yaani sunna za ziada ambazo mtu anajikurubisha kwa Allah kwa sunna hizo. Na zote hizo zina dalili thabiti katika Sunnah toharifu.
Katika sunnah zilopangwa ni Tahiyyatul masjid yaani maamkizi ya msikiti.
Nazo ni rakaa mbili za kabla ya kukaa katika msikiti. Hivyo sala yoyote ile isaliwayo kabla ya kukaa baada ya kuingia msikitini itastahiki kuitwa Tahiyyatul Masjid hata ikiwa ni Faridha au Sunna nyingine yoyote.
Hii inatokana na hadithi ya Mtume -Sallallahu alayh wasallam- isemayo:
” Atakapoingia msikitini mmoja wenu asikae kitako mpaka asali rakaa mbili”
Hivyo kinachotakikana ni rakaa mbili kabla ya kukaa sawa sawa zitakuwa ni qabliya au za sala ya Alfajiri. Na hizo hizo ndizo zitakuwa maamkizi ya msikiti.
Wallahu aalam.

Kwa kalam ya mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
6 July 2017

Published By Said Al Habsy

HUKMU YA ANAYEMILIKI DHAHABU NA HAZITOLEI ZAKA.


You have a new Question by:


Hamed Shaffi from


Oman
————————————–


Swali:

Nini Hukumu ya mtu anaemiliki dhahabu na hazitolei zakaa

JAWABU:


Hukmu yake ipo wazi katika Qur an na Sunnah, Duniani na Akhera.

Amma duniani mwenye kuzuia Zaka kwa makusudi hukmu yake ni kuuwawa ikiwa kuna dola ya kiislam ambayo ndiyo yenye jukumu la kukusanya zaka kiasili, Amepokea Imam wetu Rabii bin Habib katika Musnad yake ya Hadithi sahihi, kuwa Mtume sallallaahu alayh wasallam amesema ” Mwenye kuzuia Zaka, auwawe” na hukmu hii aliitekeleza Sayyidna Abu bakri – Allah mtukufu amridhie – alipowapiga vita walozuia Zaka baada ya Mtume kufariki na akasema Sayidna Abu bakri ibara yake maarufu ” Law wangezuia kutoa Iqaal ((kamba ya kumfungia Ngamia)) ningrwapiga vita kwa hiyo mpaka waitoe”

Na bila shaka Akhera adhabu kali inawasubiri kama watakufa bila kutubia, Amesema Allah mtukufu :
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ** يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنْفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنْتُمْ تَكْنِزُونَ

Enyi mlio amini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa baat’ili na wanazuilia Njia ya Allah mtukufu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Allah mtukufu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu.
Siku zitapo tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu, basi onjeni mliyo kuwa mkilimbika.

((Sura At-Tawbah, Ayah 34 – 35))

Na Mtume sallallahu alayh wasallam amesema:


343) … وَعَنْهُ عَلَيْهِ السَّلاَمُ قَالَ: «مَنْ كَثُرَ مَالُهُ وَلَمْ يُزَكِّهِ جَاءَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِي صُورَةِ شُجَاعٍ أَقْرَعَ لَهُ زَبِيبَتَانِ مُوَكَّلُ بِعَذَابِهِ حَتَّى يَقْضِيَ اللَّهُ بَيْنَ الْخَلاَئِقِ».
قَالَ الرَّبِيعُ: يَعْنِي ثُعْبَانٌ أَقْرَعُ فَيَكُونَ (3) فِي فَمِهِ مِنْ كِلاَ الْجَانِبَيْنِ رَغْوَةُ السُّمِّ بِمَنْزِلَةِ الزَّبِيبَتَيْنِ فِي الْتِمَاحِهِمَا، وَلَمْ يُرِدْ بِهِمَا الْعَيْنَيْنِ.

____
(3) / خ: يكون.

 

Published By Said Al Habsy

MASTERBATION INAFUNGUZA


You have a new Question by:


athumani mohamedi from

Uganda
————————————–


Swali:
marstabetion ina mfunguza saumu.

JAWABU:
MASTER BATION ni katika madhambi makubwa yaa uuaji wa kiuficho.

Pia ni kupoteza neema ya mbegu za uhai, alizotupa Allah mtukufu.

Nimesema katika moja ya majibu :

“Allah mtukufu atukinge na shari hii yenye kuangamiza duniani kwa :

1 – kupoteza nguvu za kiume
2 – kupoteza nguvu za macho
3 – inaleta msongo wa mawazo
4 – Kuleta matatizo ya kufahamu
5 – inayoua kizazi, na kusababisha mtu kukosa uzazi kabisa au kupata kwa tabu kubwa.
6 – mupoteza wakati ambao law ungetumiwa vizuri ungekiwa na tija njema.
7 – kupoteza nguvu ya kifikra na kiuchumi
8 – kiwa na hasira za haraka.

Na maafa mengine mengi.

Pia yaleta machukizo ya Allah mtukufu, kwa vile tendo hilo halina tofauti na wale walokuwa wakiwaua watito wao wa kike kwa kuhofia ada na desturi za jamii zao, hivyo kila tone moja la manii linalopotezwa kwa njia hiyo binadam ataulizwa kuhusu hilo, na wapi atapata jawabu ya maswali hayo ❓

وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ
بِأَيِّ ذَنْبٍ قُتِلَتْ

Na aliye zikwa hai atapo ulizwa,Kwa kosa gani aliuliwa?

Pia ataulizwa vipi aliipoteza neema hiyo inayotakiwa iwe kwa wanawake mpaka wanne alowekewa kisheria,

فَانْكِحُوا مَا طَابَ لَكُمْ مِنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا

Basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana. 04:03

Na bila shaka kupiga punyeto ni uadui wa wazi kwa ubinadamu, na tabia ya kisheitan, na ni mwisho wa dhulma ya kijamii. Amesema Allah mtukufu:

(وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ * إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ * فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ)
Na ambao wanahifadhi tupu zao. Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi – Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka.
[Surat Al-Ma’arij 29 – 31]”
Mwisho wa kunukuu.

Na katika jawabu yangu nyingine, ilikuwa :

Swali:
Salam alykum
Naomba kuuliza mtu ambae anae jitoa shahawa au anae fanya masterbution na akaoga janaba anaruhusiwa kufunga

JAWABU:

Subhaanallah… Allah mtukufu aturuzuku touba ya kweli. Hivi atamueleza nini mola wake mtu huyu ? Au anajiona mjanja kwa kubaki hai mpaka sasa ? Haoni ni fadhila kubwa kapewa kuudiriki mwezi huu wa Ramadhan ?

Subhanallah…!!!

Amma kuruhusiwa, naam anaruhusiwa bali ni wajibu kwake kama ilivyo kwa wengine, na kama atafanya huo uchafu wake wakati wa mchana atalazimika kuilipa hiyo siku na kufunga miezi miwili mfululizo baada yake.

Na ajue pamoja na kulazimika huko, malipo ya funga yatamfaa ikiwa tu atatubia na kuacha dhambi zake na kurudi kwa mola wake, kama hakutubia na akakutwa na mauti atakuwa hana malipo ispokuwa moto wa Jahannam wa milele bila kutoka wala kupunguziwa.

Allah atukinge na khidhlan, aturuzuku Toubah kabla ya mauti na atukubalie touba hiyo.
Wallahu aalam.
Mwisho wa kunukuu.

Na hukmu yake katika swaumu ni sawa sawa na hukmu ya mzinifu au mwenye kumuingilia mkewe mchana wa Ramadhani.

Inafunguza swaumu, na inawajibisha kafara ya kufunga miezi miwili mfululizo akiyafanya hayo mchana pamoja na toba, Na ikiwa ni usiku basi inazuiwa kukubaliwa kwa amali yake hiyo mpaka atubie kwa Allah mtukufu.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis Bin Yahya Alghammawi
10 July 2017.

Published By Said Al Habsy

AQIIQA KWA MTOTO WA SIKU 35.

SULEIMAN ABDALLA from

Tanzania
————————————–
Swali:

assalaam alaykum
mimi sikuwahi kumfanyia mwanangu aqiqa kwa kuwa nilikuwa sina uwezo jee naweza kumfanyia siku ya 35 au 42 AU 49 AU::::

JAWABU:

Aliulizwa Mtume kuhusu Aqiiqa akasema mimi silipendi hili jina la Uquuq (( kwa ubaya wa maana yake )) kisha akasema ” atakyezaliwa Mtoto kwake na akapenda kumchinjia basi afanye”

Na wametofautiana wanachuoni kuhusu Muda unaotakiwa kwa hilo.

Amesema Imam wetu Qutb al Aimmah Muhammad Atfeyyish katika Sharh Niil jz 4 uk 540
“Imesemwa ni siku atakayozaliwa, au siku ya saba, au ndani ya miaka saba yaani mpaka atakapoanza kuamrishwa kusali”

Na wapo waliosema atazingatia siku kwa witri yaani siku saba, au tisa au kumi na moja.. N.k.

Lakini ubora upo katika kufuata sio kuleta jambo jipya.

Amesema Sheikh wetu Said bin Mabrouk Alqannubi – Allah mtukufu amuhifadhi – “Vile vile imethibiti kutoka kwa Mtume Sallallahu alayh wasallam amri ya kuchinja Aqiiqa katika siku ya saba tangu kuzaliwa mtoto, lakini wengi katika watu wanachinja pia mtot afikishapo mwaka mmoja, na wengine wanafanya hilo ni Eid kwa mwaka wa pili, mwaka wa tatu, mwaka wa nne, wa tano, wa sita, wa saba… Hakika haya ni katika ambayo hayakuthibiti katika Sunnah ya Mtume sallallaahu alayh wasallam.”

Kwa hivyo kila unapokuwepo uwezekano wa kufanya lile lilothibiti inakuwa ni vizuri na bora zaidi. Lakini ikiwa imeshapita ile siku ya saba na akachukua qauli ya wenye kujuzisha kuchinja baadabya hapo kwa kutazama kuwa ni shukrani kwa Allah mtukufu basi atakuwa amepatia Qauli katika Qauli za wanachuoni.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu
K?Khamis bin Yahya Alghammawi
10 July 2017

 

Published By Said Al Habsy

KUOMBA DUA KATIKA SIJDA.


Assalaam alayikum warahmatullah wabarakat.
Niulize jamani nisaidien hili.

Hivi kuomba dua binafsi katika sijda kwa lugha yoyote baada ya kushamtaja Allah(subhana wata’ala) inafaa?


JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Kuomba dua katika sijda ya sala ni katika waliyotafautiana wenye ilmu ndani yake, baada ya makubaliano kuwa sala imetengenezwa kiarabu, hivyo yote yanayohusiana nayo yatakuwa kwa lugha ya kiarabu hata kama ni dua anayojiombea yeye mwenyewe.
Walioruhusu kuomba dua wametumia hadithi zenye kuhimiza kuomba dua, na waliokataza wametumia hadithi zenye kukataza ongezeko lololte ndani ya sala, na wapo waliosema inajuzu katika Sunnah sio faridha kwa kupokewa hayo kutoka kwa Mtume sallallaahu alayh wasallam.

Na Nimetangulia kujibu katika ukumbi wa Faidika kama ifuatavyo:

001064 – KUOMBA DUA KWA KISWAHILI.

Asalam aleykum vp hali zenu?nina swali.kuna kauli inasema sehemu moja wapo ya kuomba dua na ikakubaliwa ni wakat wa sujud na wakat wa kutoa shahada sasa nataka kuuliza wakati naswali naweza kuomba kwa kiswahili sehemu hizo.mbili au cwez.

JAWABU:
Waaleykum salam warahmatullah wabarakatuh.

Sala imetengenezwa kwa mfumo mmoja wa lugha moja ya kiarabu ambayo ni lugha ya waislam wote duniani, na kwa hivyo haifai kuweka chochote kwa lugha nyingine.

Amma wakati wa tahiyyat kubwa hapo bila shaka inafaa kuomba dua, amma wakati wa sijda ni katika sala za sunna tu sio za faridha, kwa fat wa ya Samahat Sheikh Alkhalili – Allah ampe izzi – ambayo ndio ifanyiwayo kazi.i

Amma kwa kiswahili aombe akiamliza tu kutoa salam, bali anaruhusiwa kusujudu baada tu ya kutoa salam na kuomba dua yake kwa lugha yoyote aitakayo.
Wallahu aalam.

Pia katika jawabu nyingine nimeandika:

000047 – KUOMBA DUA KATIKA SIJDA.?

Asante sn Sheikh kwa majibu yako ALLAH akupe kila la kheri hapa na uko akhera Amen Sheik Abuu Muslim Alghammawiy ningependa unisaidie suali hili jengine kwa uwezo wa ALLAH akufanyie wepesi Ameen Ivi tunaruhusiwa kuomba dua wakati wa Sijda ya mwasho na km inaruhusiwa kuna dua maalum au unaweza kusoma dua yoyote tu…?

MAJIBU:
Haijuzu kusoma dua yoyote wakati wa sijda ya sala ya faridha.
Kwa kuwa hiyo ni sala yenye mipaka yake na wala haisihi kuongeza chochote wala kupunguza chochote, ikiwa tatizo
Ikiwa ni sala ya Sunah baadhi ya maulamaa akiwemo Mufti wa zama hizi Sh. Ahmed Alkhaliliy H.A. wamejuzisha kuomba dua katika sijda ya mwisho kwa sala za sunnah tu.
Ikiwa hapana budi kuomba dua katika faridha basi omba baina ya kumaliza tahiyyaat na Salam ,hilo limethibiti na iwe kwa lugha ya kiarabu.
Wallahu aalam.

Na ilikuja Challenge ndogo kutoka kwa baadhi ya Wafuatiliaji na ikawa majibu yake ni kama ifuatavyo:

000231 – SIKUBALIANI NA KUTOKUSOMA DUA KATIKA SIJDA

Ukhty Ilam Samahani hiyo post yako kuhusu kuomba dua katika Sijda kuwa haijuzu sikubaliani nayo.

Amesema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ((Mja huwa karibu kabisa na Mola wake anapokuwa anasujudu, kwa hiyo zidisheni Du’aa))[Muslim]

Hiyo hadithi ni sahihi na tunaposwali huwa karibu na Allah kwa nini isijuzu kusoma duaa katika Swalah

JAWABU:
Amma kusoma dua katika sijdah hilo halifai katika sala ya faridha tu, kwa hadithi nyingine iliyo sahihi na kukubaliwa na wapokezi wote kuwa Mtume s.a.w. amesema ” Sala yetu hii haiswihi kuingiza neno lolote la kibinadamu – yaliyo nje ya sala – ispokuwa – yaliyoamrishwa nayo ni – tasbiihi, tahmiid, takbiirah na Quran”
Na imekubaliwa katika sala za sunnah kwa riwaya hiyo uliyoileta, na riwaya ya bibi Aisha kuwa Mtume s.a.w. alikuwa akisujudu katika witri sijda ndefu kiasi cha kusoma aya 50″ rejea maarijul aamal juz 7, cha Imaam Saalimiy – Allah amridhie –

Tatu, uwepo wa riwaya sahihi katika sahiih musnad Imaam Rabii, na Sahiih bukhary na wengineo riwaya za kukhiarisha kusoma dua, na riwaya zingine kuzifundisha hizo dua, baina ya salam na tahiyyat ya mwisho, tukajua kuwa hilo ni katika yaliyoruhusiwa katika sala za faridha na sunnah.

Huo ndio ufafanuzi wa masuala hayo, katika niliyohifadhi kutoka kwa wanazuoni wetu wema, na masuala haya yana khilafu baina ya wanazuoni, lakini sisi tumetosheka na lenye nguvu kwa mufti wa zama zetu SH. Ahmed Alkhaliliy – Allah amuhifadhi -. Wallahu aalam.

Nafkiri katika haya nilionukuu kuna jawabu tosha ya mengi katika mas – ala haya.
Wallahu aalam.
Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis Alghammawi

 

Published By Said Al Habsy

ANA MARADHI YA ANEMIA

You have a new Question by:

Mishi Athman from

Kenya

————————————–

Swali:

Assalam Alaykum, Mwenye ugonjwa wa upungufu wa damu (anaemia) ashindwa kufunga katika mwezi wa Ramadhan. Je siku atakazokosa kufunga itamlazimu kulipa? na kama bado hali ya afya haimuwezeshi kufunga ipo njia nyengine ya kulipa swaum kando na kufunga?

Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Allah mtukufu awape sihha na afya njema wagonjwa wetu, hakika yeye ni muweza wa hayo.

Allah mtukufu amewapa wagonjwa na wasafiri katika mwezi wa Ramadhani ruhusa ya kula mchana wa Ramadhani kwa kulazimika kulipa pale watakapopowa. Akasema Subhaana.

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Allah mtukufu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Allah mtukufu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.

((Sura Al-Baqarah, Ayah 185))

Lakini katika dhahiri ya maradhi yapo maradhi mepesi ambayo mtu anaweza kufunga wala hakuna hatari yoyote itakayompata kwa kufunga… Basi huyo bado hajapewa ruhusa ya kula kwa Qauli ya Allah mtukufu :
فَاتَّقُوا اللَّهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنْفِقُوا خَيْرًا لِأَنْفُسِكُمْ ۗ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

Basi mcheni Allah mtukufu kama mwezavyo, na sikieni, na t’iini, na toeni, itakuwa kheri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio walio fanikiwa.
((Sura At-Taghabun, Ayah 16))
Na bila shaka swaumu bado imo ndani ya uwezo wao.
Pia yapo maradhi ambayo hayapou kabisa kwa mujibu wa taqrir za Matabibu makhsusi wa maradhi hayo, na hayamuondoki mwanadamu mpaka mwisho wa uhai wake, na ikawa ni mazito hawezi mgonjwa kufunga ispokuwa hatari ya kuzidi maradhi hayo na Kifo, vitakuwa vimemfikia, basi Uislam umeweka njia ya kulisha chakula kwa kila siku ya Ramadhani, Amesema Allah mtukufu:

أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ ۚ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَنْ تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ ۚ وَأَنْ تَصُومُوا خَيْرٌ لَكُمْ ۖ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ

(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.

((Sura Al-Baqarah, Ayah 184))

Kwa hivyo ayapime maradhi hayo ya Anemia katika vigawanyo hivyo tulivyovitaja. Na pale yatakapokaa ndio itakuwa hukmu yake.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis Bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
17 Shawwal 1438h
12 July 2017m
Zanzibar – Tanzania.

Published By Said Al Habsy

HUKMU YA MWENYE KUFUNGA HALI ANALALAMIKA NJAA


You have a new Question by:


Abdul basit al loufy from


Tanzania


Swali:

salam alaikum nini hukmu ya mwenye kufunga hali ya kuwa baadae analalamika njaa akiwaona watu.

JAWABU:


Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Kwa hakika Swaum ni ibada kubwa na tukufu ambayo ikhlas yake yatakiwa kuwa baina ya mja na mola wake.
Kwani Mtume sallallahu alayh wasallam anasema kuwa Allah mtukufu amesema :
“الصوم لي وأنا أجزي به”
Swaumu ni ya kwangu na mimi ndio nitakayoilipia

Na bila shaka kukhusisha malipo ya funga na yeye mwenyewe Allah mtukufu ni kwa kuonyesha sharafu yake na ukubwa unaotokana na Kule kufichika kwake kwani si aghalab kumjua aliyekula na asiyekula.

Ibara uloileta inachukua zaidi ya maana moja katika kuifaham, Amma ikiwa imekusudiwa kusema hivyo kwa kuisema swaumu yenyewe na kujitangaza kuwa amefunga bila shaka litakuwa hilo halifai, na itakuwa ni katika kujionyesha kulikokatazwa kisheria kwa dalili za wazi.
Amesema Allah mtukufu:
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَنْ كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

Sema: Mimi ni mwanaadamu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.
((Sura Al-Kahf, Ayah 110))

Na ikiwa ni kuonyesha kuchukia hukmu za mola wake, zilohukumia ulazima wa kufunga itakuwa ni makosa pia, bali hilo laweza kumpelekea katika shirki akiwa ataitakidi hivyo…
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا

Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Allah mtukufu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Allah mtukufu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.
((Sura Al-Ahzab, Ayah 36))

Na ikiwa anasema akimaanisha hali ya ugumu maisha, basi ikiwa ni kweli kuna ugumu wa maisha basi itakuwa kweli, ikiwa ni uongo basi dhambi ya uongo itamganda na haitokubaliwa kwake chochote mpaka atubie kwa Allah mtukufu.

Wallahu aalam.
Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
21 July 2017.

 

Published By Said Al Habsy

ISBAAL

You have a new Question by:

Khalfan Salum from

Tanzania

Swali:

Assalam aleykum nilikua nauliza kuhusu isbal inafaa au haifai

JAWABU:

Isbaal ni kuvaa nguo ilorefuka hata ikavuka vifundo vya miguu.
Na bila shaka jambo hilo halifai kwa kule kupingana kwake na msingi wa usafi kwa muislam kama alivyosema Allah mtukufu:
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ

Na nguo zako, zisafishe.

((Sura Al-Muddaththir, Ayah 4))
Na bila shaka kuiburura nguo ni katika kuichafua sio kuisafisha. Kwa hivyo ni kuikhaikhalifu amri ya Allah na mtume ((sallallahu alyh wasalla.))
Sayyidna Umar – Allah mtukufi amridhie – alimuona kijana akiwa musbil naye amekwenda kumtazama Sayyidna Umar, akasema Sayyidna Umar “Pandisha nguo yako, kwa huo ndio uchamungu wa moyo wako, na ni usafi wa nguo yako”

Na Mtume sallallahu alayh wasallam – amekataza katika hadithi zaidi ya sabini kuvaa isbaali.
Amesema ” Mtu mmoja akiwa katika vazi lake zuri jipya, alipopita hali akiwa ni musbil na mwenye kujiona ghafla ardhi ilimmeza na ameendelea kuzama katika ardhi mpaka siku ya Qiyama”

Pia Mtume sallalallhu alimuona mtu akisali hali amevaa Isbaali, akamwambia arudie sala… Alipoulizwa akasema “Hakika Allah mtukufu hakubali sala ya mwenye Isbal”

Na riwaya nyingine zasema ” Hakika Allah mtukufu hampendi Musbil”

Hivo hakuna njia ya kuihalalisha Isbaal.

Kitabu changu kilichokusanya sehem ya hadithi hizo kipo katika maandalizi ya mwisho ya kutoka na kuwekwa katika Ibadhi.com
Wallahu aalam..

Ameyaandika Mja dhaifu:
Khamis Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
8 July 2017

 

Published By Said Al Habsy

BAINA YA MAMA NA MME.

You have a new Question by:

Hussul Suleiman from

Tanzania

————————————–

Swali:

Assalam alaykum,mm sina swali ila naomba msaada kutoka kwenu,mm ni mwanamke niliyeolewa na kujaliwa watoto ,alhamdullilah tatizo langu ni kwamba najitahidi kupenda mama yangu na ninachokipata na yy namsaidia baba yangu alishafariki kitambo sasa,mama yangu anaishi na watoto wangu wa kambu (watoto wa mume wangu)mkewe alisha muacha zaman mkewe wa 1,nikienda kutembea kwa mama lazoma nikitaka kuondoka panakua na kizingiti nisiondoke,nikienda kutembea nina kaa muda lkn tabu ndio hiyo,nikitaka kurudi kwa mume wangu lazima tugombane,panakua na mvutano baina ya mume na mama ,je masheikh mm nifanye nn kwahaki nibaki kwa mama nikose mume au niende kwa mume,hii ni mara ya tatu saiv nataka kuondoka pana kizingiti naomba msaada mume wangu nampenda na anataka nirudi kesho inshaallah,naomba jibu la sheria ya kiislam,wabilahi Taufiq.

JAWABU:
Ndoa ni mafungamano na makutano ya jamii mbili zilokuwa mbali kuws pamoja kama mwili mmoja wenye kusaidiana katika kila hali, kufanya dunia iende mbele kwa namna iliyo bora kabisa, kama alivyotaka Allah mtukufu.
Amesema Allah mtkufu:
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.

((Sura Ar-Rum, Ayah 21))

Hivyo jamii hiyo yatakiwa ijue haki na wajibu wake kwa kila mmoja, na kumpa kila mmoja kwa kadri ya inavyotakiwa bila kumpunja mmoja kati yao.

Kuoa au kuolewa si sababu ya kukata ujamaa na udugu, wala si sababu ya kuwanyima wengine haki zao wanazostahili.
Amesema Allah mtukufu:
فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ

Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?

((Sura Muhammad, Ayah 22 ))

Hivyo yatakiwa Mume ajue, kuwa kutawala kwakw familia yake haina maana ya kuzivunja haki za wengine katika kutembelewa, kusaidiwa n.k.
Na bila shaka ndugu na jamaa wa Mme ni ndugu na jamaa wa mke, na hivyo hivyo ndugu na jamaa wa mke ni ndugu zake na jamaa zake mme. Na mama huyo ni mama yenu nyote kwa hivo hakuna haja ya kugombana.

Lakini pia utembeleaji wa jamaa usiwe sababu ya kuvunja haki za mume, kwani naye anamhitaji mkewe kwa malezi na utaratibu wote wa nyumba yao, na kwa hivyo Allah mtukufu akaweka sharia ya kuwa wabaki nyumbani bila kutoka toka hovyo bila mpango. Akasema:
وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا

Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt’iini Allah mtukufu na Mtume wake…
((Sura Al-Ahzab, Ayah 33))

Sasa isiwe mwanamke kila siku kiguu na njia, kisa nakwenda kumuona flani, ikawa hatulii nyumbani kwake au akienda akazamia kabisa hata akasahaulika kwa mumewe na familia yake, hili litapelekea mme kuchukia na kuchukua hatua ya kupits wajib wake.

Hivyo Utatuzi hapa ni kufanya kila kitu kwa wastani, na hili linawezekana kwa kukaa na mumeo muwekane wazi juu ya hilo tatizo lililopo, na kuamua kulitatua kwa namna bora ya kila mmoja kupewa haki yake bila ya ziada wala nuqsan.
Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
22 July 2017m

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Aslaamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Nauliza.

Kichinjo cha Iddilhajji ni mafungu mangapi na yangawiwa vipi? Kullu aamin wa antum bikhairin.

JAWABU:

Ni ibada kubwa sana na yenye thawabu sana kuchinja Udh-hiya naye mnyawa wa miguu minne (Ngamia, N`gombe, Mbuzi, Kondoo) baada ya sala ya iddi kubwa (Iddi Al-Adh-haa), Muislamu mwenye kuchinja ajiepushe na mnyama mwenye aibu kama vile ulemavu, au upofu, au chongo, au sikio kibutu, au kukonda sana, au kukatika mkia….

Muhusika wa kichinjwa hichi anatakiwa akigawe mafungu matatu, mawili ni yake na fungu moja ni sadaka kwa masikini wanyonge katika siku hii ya Iddi.

Ama mafungu mawili moja ni kwa ajili ya kula yeye na watu wake wa nyumbani katika siku hii ya iddi na siku tatu zinazofuata, na moja ni la kujilimbikizia siku zifuatazo ikiwa atakausha nyama yake au ataihifadhi kwa njia yoyote inayowepesika kwake, na akitaka kula katika siku hizi za Iddi pia hakuna tatizo.

Na Waislamu saba wanaweza kushirikina katika kuchinja udh-hiya ya ngamia au n`gombe, kwa sharti ngamia asipungue umri wa miaka 5 na n`gombe asipungue umri wa miaka 2 na vizuri zaidi afikie miaka 3.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

 

Published By Said Al Habsy

SWAli:

asalam alykum. mimi na swali ningependa kujibiwa kama inawezekana.mimi nauliza. mbona hawa ndugu zetu wakiristo yaani hawamwamini kama muumba wa kila kitu. ALLAH. yupo wao wanamwamini yesu ndie MUNGU. na.ndie wanamwamini kwa kila kitu.

JAWABU:
Ukristo na Uyahudi ni ubunifu wa washirikina katika kuyachafua mafundisho matukufu ya Mtume Mussa A.S. na Mtume Issa A.S. baada ya kushindwa kihoja na Mitume wao.

ثُمَّ قَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِمْ بِرُسُلِنَا وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَآتَيْنَاهُ الْإِنْجِيلَ وَجَعَلْنَا فِي قُلُوبِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ رَأْفَةً وَرَحْمَةً وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَاهَا عَلَيْهِمْ إِلَّا ابْتِغَاءَ رِضْوَانِ اللَّهِ فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا ۖ فَآتَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا مِنْهُمْ أَجْرَهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ فَاسِقُونَ

Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na tukampa Injili. Na tukajaalia katika nyoyo za walio mfuata upole na rehema. Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Allah mtukufu. Lakini hawakuufuata inavyo takiwa kuufuata. Basi wale walio amini katika wao tuliwapa ujira wao. Na wengi wao ni wapotovu.

((Sura Al-Hadid, Ayah 27))

Na kwa hivyo imekuwa kuamini kwao muumba ni bure na upotovu, kwa kule kuwavisha viumbe sifa za muumba mtukufu. Amesema Allah mtukufu:

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنْصَارٍ

Hakika wamekufuru walio sema: Allah mtukufu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Allah mtukufu, hakika Allah mtukufu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.

((Sura Al-Ma’idah, Ayah 72))

Na vipi awe Muumba hali ana sifa za viumbe kama kula, kunywa, kwenda chooni n.k. amesema Allah mtukufu:

مَا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انْظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انْظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyo wabainishia Aya, kisha angalia vipi wanavyo geuzwa.

((Sura Al-Ma’idah, Ayah 75))

Kama walivyozusha wengine kuwa ni mtoto wa Mungu, Na hii ni dalili ya upotovu wao… Amesema Allah mtukufu:
وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُمْ بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ


Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Allah mtukufu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!

((Sura At-Tawbah, Ayah 30))

Ajabu yao watu hawa…

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَٰهًا وَاحِدًا ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo.

((Sura At-Tawbah, Ayah 31))

Kwa hivyo Imani yao hiyo ni upotovu kidalili na kiakili.

Na kwa hivyo Allah mtukufu atamuuliza Issa bin Maryam siku ya Qiyama naye atakawakataa. Amesema Allah mtukufu:
وَإِذْ قَالَ اللَّهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنْتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَٰهَيْنِ مِنْ دُونِ اللَّهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِنْ كُنْتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنْتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.

-Sura Al-Ma’idah, Ayah 116

مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنْتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنْتَ أَنْتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنْتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu.

-Sura Al-Ma’idah, Ayah 117

Kwa hivyo kama hawakutubia wakaondokana na ushirikina wao watakwenda motoni milele, Allah mtukufu awape hidaya.
Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamwi@ibadhi.com

Published By Said Al Habsy

Assalam alykum.

Swali
Ni IPI hukmu ya kumfuata imam wakati anasoma Surat fatiha katika sala ya sauti?

JAWABU:
Waalaykum Salaam, Kusoma Alhamdu kwa aya zake zote saba ikiwemo na Bismillahi ni nguzo katika nguzo za sala. Ikipungua au kama haikusomwa basi Sala itakuwa imebatilika.

222) … أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ صَلَّى صَلاَةً لَمْ يَقْرَأْ فِيهَا بِأُمِّ الْقُرْآنِ فَهِيَ خَدَاجٌ».
قَالَ الرَّبِيعُ: الْخَدَاجُ، النَّاقِصَةُ وَهِيَ غَيْر التَّمَامِ.
Amepokea Imam Rabii kutoka kwa Abu Ubaida kutoka kwa Jabir bin Zaid kutoka kwa Anas bin Malik Amesema: Amesema Mtume Sallallahu alayh wasallam “Atakayesali sala yoyote hakusoma ndani yake Suuratil Faatiha sala hiyo itakuwa haijatimia”

Na kwa hivyo Imam na Maamuma wote wanalazimikiwa na kuisoma Suuratil faatiha -:
226) … قَالَ الرَّبِيعُ عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ قَالَ: صَلَّى بِنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلاَةَ الْغَدَاةِ، فَثَقُلَتْ عَلَيْهِ الْقِرَاءَةُ، فَلَمَّا انْصَرَفَ قَالَ: «لَعَلَّكُمْ تَقْرَؤُونَ خَلْفَ إِمَامِكُمْ»، قَالَ: قُلْنَا: أَجَلْ، قَالَ: «لاَ تَفْعَلُوا إِلاَّ بِأُمِّ الْقُرْآنِ، فَإِنَّهُ لاَ صَلاَةَ إِلاَّ بِهَا».

Amesema Ubaadah bin Saamit ” Mtume – Sallallahu alayh wasallam – Alitusalisha sala ya Isha, kikawa kizito kisomo juu yake, alipomaliza akasema : Huenda nyinyi mnasoma nyuma ya Imam wenu. Tukasema : ndio. Akasema : Msifanye hivyo kwa kuwa hakuna sala ispokuwa isomewe ndani yake Mama wa Qur an (( suuratil faatiha))”

Kwa hivyo yatakiwa Maamuma wasome Alfaatiha kila asomapo Imam, kama asomavyo mwanafunzi akimfuatisha mwalim wake.

Na pale Imam atakapoanza kusoma sura nyingine, Maamuma atakaa kimya kusikiliza kwa Qauli ya Allah mtukufu:
وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنْصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

Na isomwapo Qur’ani isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa.
((Sura Al-A’raf, Ayah 204))

Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja Dhaifu:
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 Dhulhajj 1438h
3 september 2017

Published By Said Al Habsy

Assalam alykum 

SWALI: 

Ni zipi hukmu za fungal ? 2) ifraad ni aina gani ya hija na inahusika na matend gani ?

JAWABU:


W/salaam.

Funga inaweza kuwa na hukmu tofauti kutokana na aina yake:

1. Waajib ((Lazima)) nayo ni Funga ya Ramadhani, Funga ya Kafara, na Funga ya Nadhiri.

2. Manduub ((Sunnah)) nazo ni nyingi mfano Shaaban, Jumatatu na Alkhamis, siki nyeupe ((13,14,15)) za kila mwezi wa kiislamu n.k.

4. Karaha mfano kufunga mwezi 11, 12, na 13 ya mwezi dhulhijjah.

5. Haram kam kufunga siku za Eid, au kwa mwenye Janaba na Hedhi n.k.

Amma Ifraad ni hali ya mtu kwenda Kuhiji tu pasina kufanya na Umra katika safari yake hiyo.
Na vitendo vyake ni vitendo vyote wanavyofanya Mahujjaaj. Unaweza kurejea sehem ya Fiqh katika Website yetu ibadhi.com utaona vitendo vya Mahujjaj.
Aina nyingine za Hijaa ni Qiraan na Tamattui.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu


Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 Dhulhajj 1438h
3 September 2017m

 

Published By Said Al Habsy

JINSI YA KUHESABU NAMNA YA KUTOA ZAKA

You have a new Question by:

Hamed Shaffi from

Oman

————————————–

Swali:

Jinsi ya kufanya hesabu ya kutoa zaka kwa mtu anemiliki dhahabu?

JAWABU:
Ikiwa anataka kuitoa dhahabu yenyewe basi itamlazimu aende kwa sonara au kama yeye ana utaalam huo basi atatoa gr 2.5 ya asilimia mia ya dhahabu hiyo ambayo ni sawa na kugawa gram zote za dhahabu hiyo kwa arobaini.

Na ikiwa anataka kutoa thamani ataulizia thamani ya gram alizonazo kwa mwaka ule, kisha atagawa thamani hiyo kwa Arobaini, na kile atakachopata kitakuwa ndio kitolewacho Zaka kupewa wenye kustahiki.

Mfano: Ikiwa thamani ya dhahabu hiyo ni Tsh 1,000,000 hivyo ukiigawa kwa 40 utapata ni Tsh 25,000 basi hiyo ndio stahiki ya kutolewa.
Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 Dhulhajj 1438h
3 September 2017m

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Abdul basit al loufy from

Tanzania

————————————–

Swali:

salam alaikum nini hukmu ya mwenye kufunga hali ya kuwa baadae analalamika njaa akiwaona watu.

JAWABU:
Waalaykum salaam.
Kwa hakika neno kulalamika njaa akiwaona watu lina maana zaidi ya moja kwa mujibu wa matumizi yake. Katika hizo:

1. Hali ngumu ya maisha kiujumla. Na ikiwa kamaanisha maana hii – nayo ndio inayonidhihirikia – basi ikiwa kweli itakuwa kweli na ikiwa uongo itakuwa uongo, japo kwa sasa hali za wengi kimaisha zimetetereka.

2. Kutokuwa na chakula siku hiyo… Nayo ni njia ya uombaji wa chakula. Kuomba kumekatazwa kisheria, ispokuwa kama kutakuwa na dharura ya kuhitajika hilo. Kwa hivyo ikiwa ana nguvu ya kazi, au ana uwezo lakini ikawa anaomba basi itakuwa ni kula mali za watu kwa haram, nalo limekatazwa amma ikiwa anastahiki kwa dharura wala hachukui zaidi ya haja yake ilompelekea hilo, Si kosa na tunamuomba Allah mtukufu amtosheleze.

3. Kulalamikia uzito wa Saumu.. Kwa hakika mwanadamu hatakiwi kwa ni mwenye kualalamikia amri za Allah mtukufu kwani yote tuliyoamrishwa ni mepesi. Amesema Allah mtukufu:

لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ

“Allah mtukufu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia.”

((Sura Al-Baqarah, Ayah 286))

4. ((Riyaa)) Kujionyesha kuwa Amefunga: nayo ni shirki ndogo. Amesema Allah mtukufu:

“فَمَنْ كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا”

“Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi na atende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.”

((Sura Al-Kahf, Ayah 110))

Na ajue kuwa Allah mtukufu anajua yaliyojificha ndani ya nafsi yake, na asijiweke katka yenye kuhatarisha dini yake na aamali zake.
Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis Bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 Dhulhajj 1438h
3 September 2017m.

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Mfaume Mahmoud from

Tanzania

————————————–

Swali:

Assalamu Alaikum, swali langu ni kwamba je inajuzu kuweka akiba yako kwenye mifuko ya kijamii (pension funds) ambayo mwisho wa siku wapata ongezeko la fedha zako ulizoweka mwanzoni kwa kudai kua wanacompesate muda na mfumuko wa bei? hiyo sio riba? Jazaakum Allahu Khairah.

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Bila shaka Kwa sura hiyo ni riba, mfano wa benki, ispokuwa wamepishana kuita majina na kutoa sababu.

Na vizuri ukaonekanwa mkataba ulioingiwa baina ya mteja na mfuko huo ili hukmu itoke kwa uhalisia zaidi.

Allah mtukufu atukinge na riba kwa njia zake zote.
Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
12 Dhulhajj 1438h
3 September 2017m

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Tunataka kujua funga ya Ashuraa na fadhila zake, na jee ikiangukia siku ya Jumamosi tunaweza kuifunga? Kwa sababu tunasikia kuwa Mtume S.A.W. amekataza kufunga siku ya Jumamosi ila ikiwa ni funga ya Faridha tu.

Asante.

JAWABU:

Funga ya Ashuraa imethibiti, na Mtume wetu S.A.W. alikua akiifunga kabla ya kupata sharafu ya Ufunuo (Wahyi), pia aliendelea kuifunga katika kipindi cha Utume wake hadi mwisho wa maisha yake, lakini ilipofika karibu ya kufa alisema ikiwa Allah atanijaalia uhai mpaka mwaka ujao basi atafunga Taasuaa, aliyasema hayo ili kutafautiana na Mayahudi; kwani na wao walikua wanaifunga kwa mnasaba wa kuangamizwa Firauna L.A. ndani ya siku hiyo; kwa hiyo daraja nzuri ya kupata fadhila zake ni kufunga Taasuaa na Aashuraa, yaani siku ya tisa na ya kumi za mwezi wa Al-Muharramu (Mfunguo nne).

Ama kuhusu fadhila zake imethibiti katika mapokezi ya Maulamaa wetu kuwa Mtume S.A.W. amesema funga ya Aashuraa ni kafara ya miezi sitini (60) au kuachia huru watumwa kumi walio waumini katika wana wa Ismaili -alaihi salaam-, na kafara maana yake ni kusitiriwa madhambi ambayo mja ameyafanya kwa kuteleza au amesahau kutubia kwayo au makoseo yasiyo ya kukusudia katika ibada zake, ama dhambi ya makusudi ambayo mja anaijua hasa, hiyo itamlazimikia kuihusisha kwa kutubia.

Ama suala la hadithi iliyokuja katika katazo la kufunga siku ya Jumamosi isipokua ikiwa faridha, hadithi hiyo haizingatiwi, Mtume wetu S.A.W. amekataza kuihusisha siku ya Ijumaa kwa kuifunga peke yake na akasema tusiifunge ila pamoja na siku kabla yake au baada yake, na inafahamika kuwa siku ya baada yake ni Jumamosi, basi vipi Mtume S.A.W. akataze kuifunga hali ya kuwa ameruhusu kuifunga?!!

Kwa hiyo ikiangukia Aashuraa siku ya Ijumaa au Jumamosi au yoyote ile hukumu yake iko pale pale na fadhila zake ziko pale pale; kwani Muislamu anafunga Aashuraa hafungi Ijumaa wala Jumamosi.

Wallahu Aaalamu. 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Tunataka kujua funga ya Ashuraa na fadhila zake, na jee ikiangukia siku ya Jumamosi tunaweza kuifunga? Kwa sababu tunasikia kuwa Mtume S.A.W. amekataza kufunga siku ya Jumamosi ila ikiwa ni funga ya Faridha tu.

Asante.

JAWABU:

Funga ya Ashuraa imethibiti, na Mtume wetu S.A.W. alikua akiifunga kabla ya kupata sharafu ya Ufunuo (Wahyi), pia aliendelea kuifunga katika kipindi cha Utume wake hadi mwisho wa maisha yake, lakini ilipofika karibu ya kufa alisema ikiwa Allah atanijaalia uhai mpaka mwaka ujao basi atafunga Taasuaa, aliyasema hayo ili kutafautiana na Mayahudi; kwani na wao walikua wanaifunga kwa mnasaba wa kuangamizwa Firauna L.A. ndani ya siku hiyo; kwa hiyo daraja nzuri ya kupata fadhila zake ni kufunga Taasuaa na Aashuraa, yaani siku ya tisa na ya kumi za mwezi wa Al-Muharramu (Mfunguo nne).

Ama kuhusu fadhila zake imethibiti katika mapokezi ya Maulamaa wetu kuwa Mtume S.A.W. amesema funga ya Aashuraa ni kafara ya miezi sitini (60) au kuachia huru watumwa kumi walio waumini katika wana wa Ismaili -alaihi salaam-, na kafara maana yake ni kusitiriwa madhambi ambayo mja ameyafanya kwa kuteleza au amesahau kutubia kwayo au makoseo yasiyo ya kukusudia katika ibada zake, ama dhambi ya makusudi ambayo mja anaijua hasa, hiyo itamlazimikia kuihusisha kwa kutubia.

Ama suala la hadithi iliyokuja katika katazo la kufunga siku ya Jumamosi isipokua ikiwa faridha, hadithi hiyo haizingatiwi, Mtume wetu S.A.W. amekataza kuihusisha siku ya Ijumaa kwa kuifunga peke yake na akasema tusiifunge ila pamoja na siku kabla yake au baada yake, na inafahamika kuwa siku ya baada yake ni Jumamosi, basi vipi Mtume S.A.W. akataze kuifunga hali ya kuwa ameruhusu kuifunga?!!

Kwa hiyo ikiangukia Aashuraa siku ya Ijumaa au Jumamosi au yoyote ile hukumu yake iko pale pale na fadhila zake ziko pale pale; kwani Muislamu anafunga Aashuraa hafungi Ijumaa wala Jumamosi.

Wallahu Aaalamu. 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu Alaykum Wa Rahmatullahi wa Barakatuh.

Sheikh naomba kukuliza Swali ambalo nimeulizwa na rafiki yangu ambaye anafuata Madhehebu ya Sunni.

Anataka kujuwa kwa nini Ibadhi tunatafautiana na Sunni katika ibada ya Sala?

Asante.

JAWABU:

Tunatakiwa tufahamu kuwa kutafautiana ni katika maumbile ya watu, nako ndiko kulikosababisha kupatikana Madhehebu tafauti ili kudhibiti tafauti zilizotokea, kwa hiyo tafauti zilizopo si jambo la ajabu, na wajibu wetu ni kuvumiliana katika yenye tafauti na kushikamana pamoja katika yenye makubaliano.

Kwa upande wetu Sala ni Ibada iliyonakiliwa kivitendo kizazi kwa kizazi mpaka hivi leo, nayo ni nguzo ya pili katika Uislamu inayofuatiwa baada ya nguzo ya mwanzo ambayo ni Itikadi, kwa hiyo Ibadhi ambao Maimamu wao wa Mwanzo waliishi baina ya Masahaba R.A. hawakukubali kuathiriwa na mapokezi ya riwaya ambazo zimefikiwa na aina nyingi za utata, na utata huo unadhihiri katika kutafautiana hao wenye kuzikubali na kuzifanyia kazi ambao ni Sunni; kwa hiyo Ibadhi imetosheka na yenye makubaliano baina ya Waislamu, sala yetu utaipata kwa kujiepusha na kila lililoingiwa na tafauti na ambalo kujiepusha nalo hakupelekei kuharibu Ibada hii adhimu.

Na hapa utadiriki kuwa sababu kubwa ya kutafautiana baina Ibadhi na Sunni katika mlango huu wa sala ni kujiepusha Ibadhi na riwaya zenye utata ambazo Sunni wamezifanyia kazi.

Na sababu ya pili ni kutafautiana katika ufahamu wa dalili ambayo inakubalika kwetu na kwao, na hili linadhihiri katika suala la kudiriki sala ya jamaa.

Mtume S.A.W. amesema: ((Ikikimiwa sala musiiendee mukiwa na pupa na haraka, bali iendeeni mukiwa watulivu na wapole, na kile mutakachokiwahi mukisali, na kile kilichokupiteni mukitimize))

Sisi tunaona kuwa Mtume S.A.W. ametuamrisha kusali tulichokiwahi katika sala ya jamaa nacho ni sehemu ya mwisho ya sala hiyo, na ametuamrisha kukitimiza kile kilichotupita katika sala ya jamaa nacho ni sehemu ya mwanzo ya sala hiyo na ambayo hatukuiwahi tokea kukimiwa kwake mpaka pale tulipoingia katika sala ya jamaa.

Kutokana na hapa tukasema kuwa mwenye kudiriki Sala ya Jamaa itamlazimu -baada ya Imamu kutoa salamu- kusimama bila ya Takbira, na hapo ataanza mwanzo wa sala hadi afike katika ile sehemu aliyoingia katika sala husika, hata kama itakua alhamdu peke yake.

Ama Sunni wao wanona kuwa Maamuma anasali na Imamu sehemu ya mwanzo wa sala yake, na baada ya Imamu kutoa salamu yeye atatimiza kilichobakia katika sala yake.

 Wallahu aalamu wa ahkamu.

 

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

abdul hamad from

Tanzania

————————————–

Swali:

assalaamu alaikum naomba kuuliza Mimi ni muibadhi inaniwajibikia mini ikiwa ntasali na imamu anaekunuti ?

JAWABU:
Kwa hakika jambo la Kukunuti si katika matendo ya sala, kwani hiyo ni dua, Mtume sallallahu alayh wasallam aliwaombea dua wale waliowaua masahaba wake ilipokuwa inaruhusiwa kuongeza maneno yoyote katika sala, na alipokatazwa kuongeza chochote katika sala aliyawacha yote hayo wala hakuyarudia.
Amesema Allah mtukufu:
لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ

Wewe huna lako jambo katika haya – ama atawahurumia au atawaadhibu, kwani wao ni madhaalimu.

((Sura Aal-E-Imran, Ayah 128))

Wamesema baadhi ya masahaba – Allah mtukufu awaridhie – : ” Mtume aliqunuti sala ya alfajiri siku thelathini, akiwaombea dua watu wa Banii Suleim, kisha akaacha” Rejea Jaamii Abil Hassan jz 2 uk 81.

Na amepokea Imam Rabii -Allah mtukufu amrehem- kutoka kwa Ibn Abbas – Allah mtukufu amrehemu- amesema “Sikumuona Mtume – Sallallaahu alayh wasallam – akiqunut hata siku moja”

Na Mtume sallallahu alayh wasallam amesema : “Hakika sala yetu hii haifai kuongea ndani yake chochote katika maneno ya kibinadamu”
Na bila shaka Qunut ni katika maneno ya kibinadam yasiyokuwemo.

Kwa msingi huu wamesema baadhi ya wanachuoni wetu kuwa akisali muibadhi nyuma ya mwenye kuqunuti itamlazimikia kurudia sala yake ispokuwa kama hayo watakayoqunuti ni riwaya waliopokea. Kwa mujibu wa rai ya Sheikh Said Alqannubi – Allah mtukufu amuhifadhi-.
Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
08 Muharram 1438h
29 september 2017m.

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

abdul hamad from

Tanzania

————————————–

Swali:

assalaamu alaikum naomba kuuliza ikiwa umediriku tashahhudi tu katka sala ya ijumaa jee utalipa ulichokikosa au utalipa adhuhuri ?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Amepokea Imaam Rabii R.A. riwaya no 217 kuwa Mtume -Sallallahu alayh wasallam- amesema :

أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِذَا ثُوِّبَ لِلصَّلاَةِ فَلاَ تَأْتُوهَا وَأَنْتُمْ تَسْعَوْنَ، وَأْتُوهَا وَعَلَيْكُمُ السَّكِينَةُ وَالْوَقَارُ، فَمَا أَدْرَكْتُمْ فَصَلُّوا، وَمَا فَاتَكُمْ فَاقْضُوا، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ فِي صَلاَةٍ مَا كَانَ يَعْمَدُ إِلَى الصَّلاَةِ».
“Itakapoqimiwa sala basi msiijie mbio, njooni mkiwa watulivu na wapole, Mtakachokidiriki salini pamoja na Imamu, na kilichokupiteni kikamilisheni”

Na riwaya nyingine inasema :
“إذا جئتُم إلى الصلاةِ ونحن سجودٌ فاسجدوا ، ولا تعدُّوها ، ومن أدركَ الركعةَ فقد أدركَ الصلاةَ.”
“Mtakapokuja kusali hali sisi tupo katika sijda, sujuduni wala msiihesabu, na atakayeiwahi rakaa moja atakuwa amediriki sala yote”

Na riwaya nyingine inasema :
“مَن أدرَك الرُّكوعَ فقد أدرَك الركعةَ”
“Atakayediriki Rukuu atakuwa amediriki rakaa”

Kwa hadithi hizi, akiwakuta watu tahiyyat ya siku ya Ijumaa ataingia pamoja nao, lakini hatoihesabu, wala haitohesabika kuwa kaipata Ijumaa, kwani atakuwa ameikosa rakaa, kwa hivyo atalipa rakaa nne za adhuhuri. Kama ilivyo fatwa ya Masheikh wawili watukufu, Alkhalili na Alqannubi -Allah mtukufu awahifadhi-.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
08 Muharram 1438h
29 September 2017m.
[5:47 PM, 9/29/2017] Khamis@ghamawi>

Published By Said Al Habsy

Riziki Liz from

Saudi Arabia

————————————–

Swali:

A. Aleikum…. Jee Kuna madhara yoyote ya Ki Afya kwa mtoto mchanga ambae hajamaliza arubaini kubebwa na mtu mwenye janaba.. Mbali na wazazi wake.. Kama vile ndugu yako ama jirani yako..

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Janaba ni hali inayomzuia mtu na baadhi ya Ibada tu.
Na anaruhusiwa mwenye Janaba kufanya yote ambayo hajazuiwa kisheria.

Mimi sihifadhi kutoka kwa yoyote miongoni mwa wanachuoni aliyesema kuwa mwenye Janaba akimbeba mtoto ambaye si wake ataathirika kiafya… Hili sijaliona wala sijamsikia yoyote katika wanachuoni wetu waliolitaja.

Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- alikuwa akiishi na kukaa na watu nao wakiwa katika hali tofauti tofauti hata akamwambia mkewe siku moja alipokuwa katika siku zake “Hedhi yako haipo mikononi mwako” yaani hakuna athari ya hedhi yako katika kitu utachokishika.

Hivyo, Janaba yake haina athari kwa yoyote katika wale watakaomshika au yeye kuwashika ispokuwa kama atampa vitu vichafu.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu:
Khamis Alghammawi
09 January 2018m.
Alkhuweir- Muscut, Oman.

Published By Said Al Habsy

Zubeir Salim from

United Kingdom

————————————–

Swali:

Assalaam Alaykum,,

(1)Jee inafaa kusali nyuma ya Imam anayetia udhu kwa kupangusa juu ya soksi?Yaani haoshi miguu.
(2)pia hasomi bismillah rahman rahiym.

JAWABU:

KUPANGUSA JUU YA SOKSI.

Mas- ala haya yanarejea katk khilaf iliyopo baina ya Ibadhi na Jumhur kuhusu upangusaji khufa mbili (( Viatu vya msafiri)).

Ibadhi wanaona jambo hilo halijathibiti, na kama lilikuwepo basi limefutwa kwa aya ya Udhu ya Suratil Maida.

123) … أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ قَالَ: أَدْرَكْتُ جَمَاعَةً (1) مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَسَأَلْتُهُمْ: هَلْ يَمْسَحُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى خُفِّيْهِ؟ قَالُوا (2): لاَ.
قَالَ جَابِرٌ: كَيْفَ يَمْسَحُ الرَّجُلُ عَلَى خُفَّيْهِ وَاللَّهُ تَعَالَى يُخَاطِبُنَا فِي كِتَابِهِ بِنَفْسِ الْوُضُوءِ؟! وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يَرْوِيهِ مُخَالِفُونَا فِي أَحَادِيثِهِمْ.


Abu Ubaidah kutoka kwa Jabir bin Zaid Amesema: Nilikutana na kundi la masahaba, nikawauliza: Je Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- alikuwa anapangusa juu ya khufu zake” wakajibu “hapana”

Amesema Imam Jabir -Allah mtukufu amridhie- “Vipi Mtu apake juu ya khufu zake hali Allah mtukufu anatuhadithia kuhusu udhu wenyewe, na Allah mtukufu ndio mjuzi wa hayo yanayopokewa na wanaotukhalifu” Imam Rabii katika Musnad.

Na hivi ndivyo alivyosema Bi Aisha mama wa waumini – Allah mtukufu amridhie- hata akasema bora mtu kukatwa mguu kuliko kupaja juu ya khufu.

Na aya aliyoikusudia Imam Jabir bin Zaid -Allah ntukufu amridhie – ni:


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ مِنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُمْ مِنْ حَرَجٍ وَلَٰكِنْ يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Allah mtukufu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.

((Sura Al-Ma’idah, Ayah 6))

Amma wale waliotoa ruhusa ya kutumia khufu pia wameiwekea kanuni, masharti ikiwa yatatimia basi hakuna kusali nyuma yao kwa kuwa ni khilafu ya kifiqhi, ilojengeka tangu zamani katika dalili

Khufu kisheria ina sifa tatu:
1. Iwe ni nzito ((Inaweza kuzuia maji kufika chini))
2. Ikae mguuni yenyewe bila kufungwa ((sio kama mabuti))
3. Isiwe nyepesi yenye kuonyesha ndani.
4. Maalikiyya wameongeza sharti la nne iwe hiyo Khuffu ni ya ngozi. ((Lakini wengi hawajaweka sharti hili))

Kwa hivyo Soksi ikitimiza sharti hizi tatu ndio itapewa hukmu ya khuffu.

Masharti yake ni mengi lakini masharti mashuhuri ni:
1. Khuffu isiwe na Najisi
2. Isiwe pana sana isitulizana katika mguu.
3. Iwe ni Milki yake kisheria isiwe ya wizi au ya kuporwa.
4. Isiwe wazi wala isiwe imetoboka
5. Iwe imefunika nyayo yote, wengine wamesema iwe imefikia vifundo vya miguu.
6. Awe Alitia udhu kwa maji kwanza kabla ya kuivaa.
7. Awe anaweza kutembea nayo masafa maalumu kisha wakatofautiana kuhusu hayo masafa ni kiwango gani.
8. Kusiwe kinachozuia hilo tendo la kupaka juu yake.

Na yapo masharti mengine kwa mujibu wa madhaahib za Ahli sunnah.

Kama ambavyo imewekewa muda maalumu nao ni usiku na mchana kwa asiye msafiri, na siku tatu kwa msafiri.

Kwa hivyo ikiwa soksi za bwana huyo zimefikia hayo yaliyosemwa hapana neno kusali nyuma yake, naye kutia udhu ni bora kwake kuliko kujitia katika khilafu.

2. KUTOSOMA BISMILLAHI RAHMAANI RAHIIM.

Masuala yana khilafu pia baina ya wanachuoni, ikiwa madhehebu yake inamruhusu yeye kufanya hivyo basi sisi tunaruhusika kusali nyuma yake.

— Ibadhi, Shafi na Shia wote wanaona kusoma Bismillah kunaenda sambamba na usomaji wa Alhamdu ikiwa itasomwa kwa sauti basi na Bismillah isomwe kwa sauti, ikiwa kimya basi nayo isomwe kimya.
Na hii ni kwa kuwa Kwao Bismillahi ni aya ya kwanza katika Suratil Fatiha.

Wengine wanaona kuwa Bismillahi ni aya pweke imekuja kwa ajili ya kupambanua baina ya sura na Sura tu, hivyo wakaipa hukmu ya peke yake.
Mahanafi wakasema si lazima kuisoma, kama ilivyo kwa Alhamdu kwao wao si lazima, na mwenye kuacha sala yake haiharibiki lkn atapata dhambi.

Amma Mahambali wao wanaificha wanaisoma kimya kimya bila kuitolea sauti. Na wanazo baadhi ya riwaya dhaifu walizotegemea.
Lakini riwaya sahihi zinaonyesha kuwa Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- alisoma Bismillahi na suratilfatiha kwa sauti ya wazi yenye kusikika.
Amesema Abu Huraira ” Mtume alikuwa akisoma Bismillahi kwa sauti watu wakaacha hilo” Albayhaqi ((Alkubra)) no 2448, Alhakim ((Almustadrak)) no 848, Aldarqutni ((Alsunan)) no 7.

Na walioacha hilo ni Muawiya na wafuasi wake kama ilivyopokewa kuwa Muawiya alipokwenda Madina aliwasalisha watu bila kusoma Bismillahi katika sala ya kutoa sauti, basi alipomaliza Masahaba ((Muhaajirina na Ansari)) wakamwambia “Ewe Muawiya, Umeiiba ((umeipunguza)), iko wapi Bismillahi… Tangu siku hiyo ikawa akisoma Bismillahi…”

Imam Shafi ((Ul ummu)) no 174, Baihaqy ((Alkubra)) no 2460, 2461, 2462, na 2463. Almmaarifa no 714, Aldarqutni ((Alsunan)) no 34, Alhakim ((Almustadrak)) no 850.

 

Hivyo, ikiwa yeye ni katika madhehebu zenye kuficha kama mahambali au ambazo haziwajibishi kama Mahanafi inajuzu kusali nyuma yake.

Amma akiwa katika madhehebu zenye kulazimisha kusoma kwa sauti lakini anaiga kukaa kimya bila ilmu basi bora kutosali nyuma yake kwa kuwepo shaka ya usahihi wa sala yake.
Wallahu aalam.

Note:
Sheikh wetu Juma bin Mohammed Almazrui -Allah mtukufu amuhifadhi- katika tafsiri yake ya Qur an ameweka ufafanuzi mzuri wa ki ilmu kuhusu mas-ala haya. Unaweza kuirejea itakapotoka.

Ameyaandika Mja dhaifu:
Khamis Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
10 January 2018m.
Alkhuweir – Mascut, Oman.

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

abdulla suleiman from

Tanzania

————————————–

Swali:

assalam alaykum. mm ni mkazi wa zanzibar na nimekuja mkoani mbeya kwa ajili ya masomo kwa muda wa miaka mitatu in shaa allah, jee mm ni bado msafiri, na kama ndio vipi nitaswali swala ya safari kwa muda wote ninapokua chuoni?. ukizingatia kua vipindi vya chuoni havizingatii muda wa swala, unaweza kua na kipindi katika muda wa swala na hadi muda wa swala ukapita bado upo darasani, vpi nitaswali katika hali hio. naomba majibu katika hili na allah atakulipeni kheri.

 

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Imepokewa kuwa Mtume sallallahu alayhi wasallam alipokwenda katika Ufunguzi wa Makka alikaa siku 15, na alikuwa akisali sala ya msafiri, anapomaliza hugeuka na kusema “Kamilisheni -Rakaa nne -hakika sisi – tumesali rakaa mbili kwa kuwa- ni watu wasafiri”

Kama ambavyo Sahaba mmoja wa Mtume sallallahu alayh wasallam imepokewa alikwenda Uzbeirjan na akazuiliwa na theluji kwa mwaka mzima ana aliendelea kusali sala ya safari.

Kwa kuwa wewe hujaweka nia ya kuifanya mbeya kuwa makazi yako ya kudumu hivyo wewe ni msafiri, na hukmu yako ni ya sala ya safari.

Na sala ya safari ni kuwa ukisali peke yako au ukiwa wewe ndiye Imam basi itakuwajibikia kusali rakaa mbili kwa kila sala ya rakaa nne.

Kama ambavyo umeruhusiwa kuunganisha baina ya sala mbili:

1. Adhuhuri na Asri ((Ukitaka katika wakati wa Adhuhuri au wakati wa Asri ))

2. Maghrib na Ishaa ((Ukitaka katika wakati wa Maghribi au wakati wa Ishaa))

Hivyo pale vipindi vinapozongana kwa hukmu yako ya usafiri basi unaweza ukasali kwa kuunganisha kama tulivokuelekeza yaani ikiwa kipindi cha Masomo kipo wakati wa Adhuhuri basi utaisali dhuhuri na Asri wakati wa Asri (( yaani utaichelewesha mpaka wakati wa pili))

Na kama unajua kuwa Asri utakuwa katika kipindi cha Masomo basi isali kabisa wakati wa Adhuhuri.
Na hivyo hivyo waweza kufanya ikiwa kipindi ni Isha na Maghribi. Yaani ikiwa kipindi cha Maghribi kimepitiwa na kipindi cha Masomo basi utaisali na Isha katika wakati wa Isha. Na ikiwa Maghribi imekukuta hujaingia katika kipindi cha Masomo, lakini Isha itapitiwa na kipindi cha masomo basi utaivuta Isha mpaka wakati wa Magharibi utaisali kabisa.

Na unapokuwa huna kipindi basi sali sala zote kwa nyakati zake na kwa jamaa.

* TANBIIHI:
1. Alfajiri haiunganishwi na sala yoyote.
2. Asri haiunganishwi na Maghribi.
3. Ukisali nyuma ya Imam basi utamfuata yeye, sala ya rakaa nne utaisali rakaa nne bila kupunguza kitu.
4. Sala zenye kupunguzwa rakaa ni zile za Rakaa nne tu, tena ikiwa unasali peke yako, au ukiwa wewe ni Imamu, au ukisalishwa na msafiri mwenzio.
5. Kwa hivyo, Sala ya Maghrib na Alfajiri hazina kupunguzwa Rakaa.

NAMNA YA KUSALI:

Utakimu sala kisha utanuia moyoni kusali sala ya safari, kwa kuunganisha baina ya sala mbili ((Ikiwa unaunganisha)).

Utaanza sala ya dhuhri kisha Asri, hata kama itakuwa unazisali katika wakti wa Asri.

Na utaanza sala ya Magharibi kisha Ishaa, hata kama utakuwa unazisali kwa pamoja wakati wa Ishaa.

Ukimaliza sala ya kwanza, kwa kutoa salam, utasimama bila kuongea chochote na yoyote, Utakimu sala kisha utaanza sala ya pili mpaka mwisho.

Huu ndiyo ufupisho wa sala ya safari, na huenda Kitabu cha Sala ya Safari anachokiandika Sheikh wetu Juma Almazrui -Allah mtukufu amuhifadhi- kitamalizika hivi karibu na kitawekwa katika website yetu ibadhi.com , hivyo kingojee kwa faida zaidi na ufafanuzi yakinifu.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu:
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
20 January 2018m.

Published By Said Al Habsy

A/MALLEKUM nauliza kuhusu wale tabligh wanaotoka miezi 4 au sku 40 wapo katika sheia ya kiislam ?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Kwanza sisi Ibadhi tunaona kila anayeleta “Jumla” yaani Shahada tatu (( Kushuhudiwa kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah mtukufu, na Kushuhudia kuwa Mtume Muhammmad ni mtume wake na mja wake, na Kushuhudia kuwa kila alichokuja nacho Mtume Muhammad ni Haki itokayo kwa Allah mtukufu”

Na ikawa hakuleta chochote cha kuvunja Jumla hiyo huyo ni “NDUGU YETU KATIKA TAWHIID” hata kama yeye sio Ibadhi.

Kwa hivyo Sisi Ibadhi hatuna Shaka juu uislam wa kundi la Jamaat Tabliigh.

Amma yanayohusiana na kutoka katika njia ya Daawa, bila shaka hakuna Muislam anayekataa usahihi wa kutoka kwa ajili ya Daawa. Kwani atagongana na aya za wazi na Hadithi na mienendo ya wema waliotangulia.
Kwa hivyo hili pia halina shaka juu ya usahihi wake.

Kilichobaki ni Kuhusu nyakati walizoziweka katika nidhamu zao za kutoka, hapo ndio palipotikea khilaafu baina ya Tabliigh na wanaojiita Salaf (( Mawahabi)).

Khilafu nyingine ni katika baadhi ya mafundisho ya Matendo bora ambayo Wengine wanaona hayajathibiti.

Kwetu sisi Ibadhi, nimemuuliza Sheikh Abdallah bin Said Almaamary -Allah mtukufu amuhifadhi- akasema ikiwa yatarekebishwa yale mafundisho yenye upofu wa kiitikadi, kama itikadi ya kiyahudi ya kuonekana Allah mtukufu, kutoka motoni n.k. basi hakuna tatizo katika kutoka pamoja nao, na vizuri zaidi mtu kuchukua vitabu vya Ahlilhaqq wal istiqaama.

Pia Sheikh wetu Khalid Alssiyaabi ni katika wanaotoka na kushiriki katika jamaat za Tabligh, naye kasema hakuna tatizo kutoka nao, na akaongeza “Sijaona kundi linalonikubali hivi nilivyo kama Ibadhi kuliko kundi la Tabliigh, kwani wao wako tayari kuacha kuongelea yote yenye khilaf baina yetu ili kuzitengeneza Imani zetu na kuweka umoja wa ummah”

Naye alimfikishia Samaahat Mufti wetu, Sheikh Ahmed bin Ahmed Alkhalili – Allah mtukufu amuhifadhi- na wala hakutunukulia kutoka kwake kupingana na hilo.

Kwa misingi hiyo, Haikatazwi kufaidika na Majaribio ya wengine, na katika Ibadhi kuna kila kihitajiwacho na nafsi na mwili katika mfumo kamili wa maisha.
Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis Alghammawi
Khamis.alghamawi@ibadhi.com
20 January 2018

 

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Hassan Mnende from

Tanzania

————————————–

Swali:

Je mwanamke kuolewa akiwa ktk hedhi, inaswihi ?

JAWABU:

Hakuna Ulazimisho wala sharti la mwanamke kuwa katika usafi wakati wa kuolewa.

Sharti hilo limewekwa katika talaka nalo si sharti la kusihi ni sharti la ukamilifu, na kwa hivyo akitoa talaka itakuwa lkn itakuwa amekosea.

Na baada ya kufunga ndoa hataruhusiwa kumuingilia mkewe mpaka atoharike na ajitajihirishe kwa kukoga.
Amesema Allah mtukufu :
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ

Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat’ahirike. Wakisha t’ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Allah mtukufu. Hakika Allah mtukufu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.

((Sura Al-Baqarah, Ayah 222)).

Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
28 January 2018

Published By Said Al Habsy

WAZAZI WANALAZIMISHA NIMUOE MWANAMKE NISIYEMTAKA.

Assalaykum sheikh ! Shekhe mm ni kijana mwenye umri wa miaka 24, nimempenda binti fulani ambaye nataka kumuoa ila upande wa kwetu mm mwanaume wazee wanaleta pingamizi zao kwa kuleta dosari kuwa hawataki nioe mke kutoka upande fulani wa nchi, je nawezafunga ndoa bila ya kuwashirikisha wazee wangu? Kwasababu wao wamekataa na wanataka wanichagulie ambae mm simtaki! Naomba msaada / majibu sheikh!

JAWABU;
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Ndugu yangu Kijana, jua kuwa ndoa ni muunganiko wa familia moja na nyingine, kwani mwanamme atapata mama na baba wengine, na mashemeji na watoto wake watakuwa na ma anko na makhaloo. Kama ambavyo mwanamke pia.
Na kwa ajili hii inatakiwa kuwe kuna muwafaqa wa familia mbili pale inapotokea kutaka kuoana baina ya familia moja na nyingine. Lakini kukubaliana huku si lazima kisheria ispokuwa ni kwa ajili ya kuhakikisha utulivu wa hao wanandoa wawili.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
((Sura Ar-Rum, Ayah 21))

Basi hebu niambie ndugu yangu, ataishi vipi mwanamke hali hakubaliki na wazazi wako wawili na inawezekana na ndugu zako wengine ? Atautoa wapi utulivu na furaha ya nafsi? Bali hata wewe utakuwaje uhusiano wako na wazazi wako baada ya kuasi amri yao ?

Kwa hivyo usilitazame jambo hili kwa mtazamo wa kushibisha matamanio ya nafsi yako tu..!!

Pamoja na haya wazazi sehem yao ni kubwa maadam hawakukhalifu sheria katika waliloamrisha, Amesema Allah mtukufu:
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِنْدَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُلْ لَهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُلْ لَهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.
((Sura Al-Isra’, Ayah 23))

Haya tuliyosema hayana maana kuwa wazazi wana haki ya kuwalazimisha watoto wao katika kuchagua mwenzi wa maisha yao, haasha..!!

Pia wao inatakiwa wawasikilize watoto matakwa yao, wawaelekeze kwa mashauriano na majadiliano matulivu yenye lengo ya kujenga sio kubomoa. Pia wafahamishwe kwa uzuri rai ya dini yetu tukufu kuwa mazingatio sio utaifa ambao ni harufu mbaya ilopandikizwa na wakoloni katika kugawa taifa kubwa la waislam linalotakiwa kuwa chini ya Khalifa wa kiislam. Mazingatio ni Dini na Akhlaaq. Na haiwi kwao wao wazazi kupingana na amri ya Allah mtukufu na Mtume wake kwa matamanio ya nafsi zao.

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا

Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Allah mtukufu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Allah mtukufu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.

((Sura Al-Ahzab, Ayah 36))

Pia tunaona kuwa wewe uwakinaishe wazazi wafaham kwa nini umemchagua huyo binti, na kwa nini humtaki huyo alochaguliwa na wao kwa hishma na adabu, au kwa kuwatuma wanaoweza kuwaambia vizuri wakafahamu. Na ikiwa hapana budi kuyakhalifu matamanio ya nafsi yako kwa kuwaridhisha wao basi ni ujira mkubwa ulioje huo…!!

Katika athari imesemwa:

Radhi za Allah mtukufu zipo katika Radhi za wazee wawili, na Machukizo ya Allah mtukifu yapo katika Machukizo ya wazee wawili.
Wallahu aalam.

Ameyaandika mja dhaifu
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
8 Febr 2018
Makkatul Mukarrama.

Published By Said Al Habsy

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

SWALI:
Nauliza swali jee Inafaa mkilisto kujenga msikiti na ukatumiwa na waislam kwa kusalia au kuna Aya ipi ya qurqn inayo kataza kwa mkilisto kuto saidia mwislaam.

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Ninachohifadhi kutokana na majibu ya wanachuoni wetu ni kuwa msikiti yatakiwa kujengwa na muislam, kwa mali za halali zisikowa na uchafu ndani yake.

Amma kumzuia asiyekuwa muislam ni kwa kauli ya Allah mtukufu:
إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا اللَّهَ ۖ فَعَسَىٰ أُولَٰئِكَ أَنْ يَكُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِينَ

 

Hakika wanao amirisha misikiti ya Allah mtukufu ni wale wanao muamini Allah mtukufu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Allah mtukufu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.

((Sura At-Tawbah, Ayah 18))

Na bila shaka wasiokuwa waislam hawajamuamini Allah mtukufu wala mtume wake.

Amma kushurutisha uzuri na uhalali wa mali ni kwa dalili nyingi za Qur an na Sunnah, na tutosheke na Qauli ya Mtume -sallallahu alayhi wasallam-: “Hakika Allah mtukufu ni Mzuri hakubali ispokuwa vizuri”

Na ifahamike kuwa hii haina maana ya kukataa msaada wa wasiokuwa waislam, haasha..!! Lakini wanaweza kusaidia katika maeneo mengine mengi yasiyokuwa kujenga msikiti mfano mayatima, nyumba za walimu, Madrasa n.k.

Na bora ikitokea katika hayo waumink wa msikiti huo wamrejee mwanachoni Mujtahid wa zama zao ili awape fat-wa.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi
09 February 2018
Jeddah, Saudi Arabia.

 

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

sheykha sinan from

Tanzania
————————————–
Swali:

Kuna ulazima wowote kwa mwanmke kuvaa vazi la nikabu ?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Bila shaka sitara ni kitu kitakiwacho sana kwa mwanamke na mwanamme. Na ikitokea chakula kufuatwa na Nzi basi wa kulaumiwa si nzi, bali yule aliyekiacha chakula wazi. Na kwa hivyo ndiyo imekuja amri ya mwanamke kujistiri, Akasema Allah mtukufu:
وَقُلْ لِلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِنْ زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Allah mtukufu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.
((Sura An-Nur, Ayah 31))

Kwa hivyo malengo ya sitara yanapopatikana katika Niqaab bila shaka hiyo ni fadhila, usafi, utakaso na nadhafa ya nafsi ya mwanamke.

Kama ambavyo mwanamke ametakiwa kujizuia na kutoka hovyo nyumbani kwake bila mpango, na kwa hivyo hatohitajia sana Niqabu kwa kuwa atakuwa nyumbani kwake. Amesema Allah mtukufu:
وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا

Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt’iini Allah mtukufu na Mtume wake. Hakika Allah mtukufu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara.
((Sura Al-Ahzab, Ayah 33))

Kama ambavyo fitna katika zama zetu imekuwa ni nyingi, na wanaume wangapi wanafitinishwa na sura ya mwanamke fulani, au akafitinishwa na moja ya vilivyopo katika sura yake kama pua, au macho, au nyusi au kope au midomo n.k. na ubaya ulioje wa fitna hii yenye kudamirisha familia zilizotulizana, na yenye kuwachafua wanawake na wanamme waliokuwa ni wasafi !

Kwa ajili hii ndio ametoa Fat wa Samaahat Sheikh Alkhalili – Allah mtukufu amuhifadhi- ulazima wa kuvaa Niqab kwa mwanamke ikikhofiwa fitna.

Na kwa sababu ya kuenea fitna kila sehemu, Ametoa fatwa Sheikh wangu Shaban Albattashi – Allah mtukufu amuhifadhi- ya Uwajibu wa kuvaa Niqabu kwa Mwanamke.

Jilazimishe na hilo utakasike, Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
09 February 2018
Jeddah, Saudi Arabia.

 

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Hamed Shaffi from

Tanzania

————————————–

Swali:

Jinsi ya kuosha maiti.

JAWABU:

Waalayku Salaam.
Ni wajibu wa kutoshelezana kwa walio hai kumkosha aliyekufa akiwa muislam, na ikiwa maiti wa kiislam hatokoshwa basi dhambi zitawaenea wanajamii husika wote.

Jambo la mwanzo afanyiwalo maiti wa kiislam ni kufunikwa macho yake na mdomo wake, kisha huvuliwa nguo zake za kawaida na kufunikwa shuka, kisha maiti hutayarishwa kwa kukoshwa (( kunyooshwa viungo vyake, na kuondosha vilivozidi katika mwili wake))

Maji ya moto yasiyounguza ((uvuguvugu)) hutumika katika kumkosha maiti, pia sabuni yenye manukato au majani ya mkunazi au vinavyoweza kusimama sehemu yake hutumika.

Maiti huanzwa kwa kutolewa haja kubwa na ndogo zilizobakia katika njia zake, hii inakuwa kwa kulibinya kwa upole tumbo lake, na ili iwe rahisi zaidi, ni vyema kumkalisha kwa mtu kumuegemeza katika magoti yake, kiasi itakuwa njia ya tumbo lake imeelekea kwa chini na kila kisichohitajika kitateremka kwa wepesi kabisa. Wakati huo itakuwa anamiminiwa maji ili kutoka kwa haja yake kuendane na kusafika.

Anayekosha atamstanji mpaka ahakikishe najisi yote imemalizika wala haitoki tena, na hiyo itakuwa kwa kuchukua kitambaa kisafi cheupe au gloves na kumstanjia ili kuhakiki kuwa hakijachafuka hat kidogo, hapo atajua kuwa tayari amesafika.

Baada ya hapo, atapigishwa mswaki kwa kitambaa safi kukipitisha katika meno, kisha atatilishwa udhu kama wa sala.

Kisha ataanzwa kumwagiwa maji sehem za kichwa pamoja na kuzuwiya matundu yote yasipitishe maji kuingia ndani.

Kisha atakoshwa sehem za kulia kwa mbele, kisha Sehem za kushoto kwa mbele.

Kisha atalazwa upande wa kushoto ili akoshwe upande wa kulia wa mgongoni kwake kuteremka chini mpaka miguuni, kisha atalazwa upande wa kulia ili akoshwe upande wa kushoto wa mgongo wake kuteremka chini mpaka miguuni. Si vibaya kutumia sabuni katika josho hili.

Kisha atamwagiwa maji yalotewa mafuta mazuri au majani ya mkunazi mwili mzima kufuata Sunnah ya Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-.

Atakaushwa maji yake kwa kubadilisha shuka bila kumfunua mwili wote akaonekana.
Na hapo atakuwa tayari kwa kuvikwa sanda.

Muhimu ni kuwa hatua zote hizo zitatimia hali ya kuwa amefunikwa na kusitiriwa, pia mkoshaji awe amevaa kitambaa na ajiepushe kufanya lolote linalovunja heshima ya maiti huyo, na wala asiuguse utupu wake ispokuwa kwa dharura tu.

Mwisho, uandishi si kama kuona amali yenyewe, hivyo nakushauri uingie katika wakoshaji ili upate mazoezi na uzoefu.
Wallahu aalam.

Ameyaandika Mja dhaifu:
Khamis bin Yahya Alghammawi
khamis.alghamawi@ibadhi.com
8 February 2018m
Jeddah, Saudi Arabia.

Published By Said Al Habsy

Swali:

Assalam Alaykum. Afanye nn asieweza kuchunga udhu, mda mwengine unatenguka Kati Kati ya swali msaada wenu tafadhali.

JAWABU:
Waalaykum salaam.

Asiyeweza kuchunga udhu kwa kutoweza kujizuia kutokana na maradhi aliyonayo kama kutokwa na haja ndogo mfululizo, Au upepo kiasi hawezi kujizuia kwa kulegea misuli inayozuia hilo kwanza aende hospitali ili apate tiba ya maradhi yake hayo.

Amma yanayohusiana na Sala yake:

– Ikiwa anapata fursa ya wakati ambao udhu wake hautenguki kiasi cha yeye kuweza kusali na kumaliza basi atasubiri wakati huo, Ili asali muhimu muda wa sala usipite wote naye hajasali.

– Ikiwa hapati muda huo – yaani wakati wote yeye anakuwa katika najasa – basi hapo maulamaa wanasema atajisafisha ikikaribia karibu na sala kisha ataweka chenye kuzuia ile najisi kufika katika nguo zake za nje, kisha atatia udhu na atasali mpaka amalize.

– Udhu wake atautia kwa niya ya kuhalilikiwa kusali kama walivyosema kundi kubwa la wanachuoni.

– Amepewa ruhusa ya kukusanya sala mbili kwa pamoja ((Adhuhri na Asri)) au ((Maghribi na Isha)) katika wakati wa moja ya sala mbili hizo bila kurudia udhu wake.

– Akisali kila sala peke yake basi itanlazimikia kutia udhu kwa kila sala.

Na Asili ya hukmu katika mlango huu ni yaliyopokelewa na Bukhari 228, Muslim na wengineo kuwa Mtume sallallahu alayhi wasallam alisema Kuhusu mwanamke (Fatma bint Hubaishi) ambaye damu yake inaendelea kutoka bila kukatika “Hiyo ni damu ya mshipa, zikianza siku za hedhi yako acha kusali zikimalizika sali” Amesema Ur’wa “Kisha atakuwa anatia udhu kwa kila sala”

Amesema Bii Aisha Mama wa waumini – Allah mtukufu amridhie – “Mmoja wa wake wa Mtume -sallallahu alayhi wasallam- Alikaa naye Itikafu, Ikawa anapata damu na umanjano, ikawa ana sali” Bukhari

Na amepokea Bii Aisha pia kiwa Ummu Habiiba alipata damu ya Ugonjwa miaka saba, Akamuuliza Mtume – sallallahu alayhi wasallam- Mtume akasema ” Hiyo ni damu ya mshipa” na alikuwa Ummu Habiba anatia udhu kwa kila sala” Bukhari 327.

Wallahu aalam.
Khamis Alghammawi
kalghammawy@gmail.com

Published By Said Al Habsy

Swali:

Je ina ruhusiwa kuomba dua katika sijda na ni katika sijda ya swala ya faradhi au suna na je nikatika sijda yeyote ?

JAWABU:
Kuomba Sijda katika sala ni katika mambo yaliyoingiwa na khilafu za wenye ilmu.
Na ufupisho wa Jawabu ni Kukatazwa katika sala ya faridha kwa yale yaliyopokewa kuwa – Mtume sallallahu alayhi wasallam – Alisema:
“إنَّ صلاتَنا هذه لا يصلُحُ فيها شيءٌ مِن كلامِ النَّاسِ إنَّما هي التَّكبيرُ والتَّسبيحُ وتلاوةُ القرآنِ”
Hakika ya sala yetu hii hakuna kinachofaa kuingizwa ndani yake ispokuwa Takbira, Tasbiihi, na kusoma Qur an” Sahiih Nasaai 5/565, Baihaqii Sunan Saghiir 1/316 Sahiih Ibn Hibban 2248.

Amma kuhusu hadithi isemayo :
((أقرَبُ ما يكونُ العبدُ من ربِّه وهو ساجِدٌ؛ فأكثِروا الدُّعاءَ))

” Sehem anayokuwa mja yupo karibu zaidi na mola wake ni pale anapokuwa amesujudu”

Hadithi hii inaeleza kwa Ujumla wa sala zote na hadithi ilopita inazungumzia sala za faridha kwa mujibu wa sababu ya utamkaji wake. Kwa hivyo hadithi hii itakuwa ni kwa ajili ya sala za Sunna tu sio faridha.

Kwa hivyo dua inajuzu kuomba katika sala za Sunnah tu sio za Faridha, wallahu aalam.

Khamis Alghammawi
kalghammawy@gmail.com

Published By Said Al Habsy

Swali:

Asalamu alaikum warahmatullahi wabarakatu. Naomba kuliza swali langu. Mke wangu kaniambia nimsaidie kumvalisha mtoto pampers wakati ameshamuosha na mm niko na udhu wangu ktk kitendo cha kumvalisha hiyo pampers imepelekea sitokwakukusudia mkono wangu ukagusa sehemu za siri za mtoto. Jee udhu wangu bado upo au nikatie udhu mwengine? Shukran.

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

lililo bora ni kurudia kutia udhu tena ili kutoka katika khilafu zilizopo katika masuala haya.

Amesema Mtume sallallahu alayhi wasallam

“دَع ما يريبُكَ إلى ما لا يريبُكَ”
“Wacha lenye kukutia shaka na  liendee lile lisilokutia shaka”

 Amepokea Abu Daawud 1425, Tirmidhi 464, Nasaai 1765.

Wallahu aalam.

Khamis Alghammawi
kalghammawy@gmail.com

Published By Said Al Habsy

Swali:

Assalam alaykum , Shekh naomba kukuuliza swali; Kwa ibadhi,swala ya tarawekh inaswaliwaje ?
Yaani ni rakaa 8, na zimegawanyika rakaa mbili mbili, na baada ya rakaa 4, imam anasoma dua,


Swali langu ni; katika kila rakaa 2, attahiyatu unaisoma yote ?, au unaishia tashahhud ,Na katika witi, huswaliwa rakaa 3, rakaa 2 za kwanza unatoa salaam, halaf unamalzia rakaa 1, jee katika hizi rakaa 2 za kwanza za witri tahiytatu unaisoma yote au unaishia tashahhud ?

Plzzzz naomba sheikh unipatie elimu ya hilo.

JAWABU:


Waalykum salaam warahnatullah wabarakatuh.

Tarawehe ni rakaa nane kwa rakaa mbili mbili kila baina ya rakaa mbili atatoa salam.

Amma dua husomwa baada ya Rakaa ya nne kwa kupumzika na wengine huiwacha dua mpaka imalizikapo witri. na yote mawili kwetu sisi hayana tatizo.

Amma namna ya kusali witri basi husaliwa na wengi katika Ibadhi kama isaliwavyo  Magharibi yaani Rakaa tatu bila kuachanisha. Nayo ndiyo rai ya Jumhuur ya wanachuoni.
Na kwa hivyo Tahiyyat hapa itasomwa ndogo katika rakaa ya pili na kubwa katka rakaa ya tatu.

Na wengine huachanisha baina ya rakaa mbili na moja kama afanyavyo Samaahat Sheikh Ahmed Alkhalili – Allah amuhifadhi- . Na kwa njia hii katika rakaa mbili itasomwa tahiyyat kubwa na katika witri itasomwa tahiyyat kubwa.

Na njia zote zimepokewa katika hadithi sahihi zilizothibiti.
Amepok

أوتر بسبع وكان لا يَقعُدُ إلا في السادسةِ ثم يَنهَضُ ولا يُسلِّمُ ثم يُصلِّي السابعةَ ثم يُسلِّمُ تسليمةً
الراوي: عائشة أم المؤمنين
Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- Alisali witri kwa rakaa saba hakukaa ispokuwa rakaa ya sita kisha hunyanyuka wala hatoi salam kisha husali rakaa ya saba kisha hutoa salam moja” Imepokewa hadithi hii kutoka kwa Bii Aisha.

 Riwaya nyingine zasema alikuwa akikhofia kuwa Alfajiri karibu kuingia husimama na kusali witri ya rakaa moja.

Na yote haya ni dalilj ya kuwa njia zote mbili, hazina katazo.
Wallahu aalam.

Khamis Alghammawi
kalghammawy@gmail.com

Published By Said Al Habsy

Swali:

Je Swaum inaswihi ikiwa utafunga bila kula daku?

JAWABU:


Swaumu itaswihi bila shaka yoyote. kwani daku ni fadhila na ubora sio sharti wala nguzo ya swaumu.
Wallahu aalam.

Khamis Alghammawi
kalghammawi@gmail.com

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalam aleykum.

Nina suali kidogo.

Mimi ni muibadhi, jee naweza kufata imamu wa madhehebu mengine mfano ni Imamu msunni na wengineo, na jee wao wa mengine wanaweza wakafuata Imamu Muibadhi?

JAWABU:

Inajulikana kuwa Waislamu wamegawika kimadhehebu, na hili halikuanza leo wala jana bali ni makarne yaliyotangulia, na kwa sababu hiyo kila madhehebu ya Waislamu yamehusika na mafundisho na misimamo iliyowatafautisha na wengine, ndio, bila shaka yako mengi tuliyokubaliana na hayo hayana umadhehebu ndani yake, na kuna machaache ambayo yameingiwa na kupatikana tafauti ndani yake ni sawa za kiitikadi au kifiqhi au misimamo ya kitarehe katika matokeo muhimu yaliyotokezea katika safu za Waislamu, na katika haya yaliyoingiwa na tafauti kila Madhehebu inahusika na mambo yake, wala si halali kubebeshwa wengine yasiyo wahusu, kutokana na hapa Umadhehebu ni uhakika uliopo, kuna Masunni kiujumla nao wana Madhehebu zao za Kifiqhi na Kiitikadi pia, kuna Mashia nao pia hali yao ni hiyo hiyo wana Madhehebu zao za Kifiqhi na Kiitikadi, na tuko sisi Maibadhi tuna misimamo yetu ya Kifiqhi na Kiitikadi ambayo ni tija ya kujishika na haki kwa dalili kila tafauti zilipotokea.

Inafahamika kuwa Ibadhi tumefikwa na misukosuko mingi ya kufanyiwa uadui kwa namna moja au nyengine, na fatwa za kutofaa kusali nyuma yetu au kupandikiza chuki dhidi yetu katika jamii mara nyengine hurushwa hewani kwa hamasa kubwa bila ya kuhakikisha wala kujua mafundisho ya Ibadhi na usuli wake, wala kuangalia athari zake za kusababisha mfarakano na kuhasimiana katika jamii.

Lakini sisi upande wetu juu ya yote hayo ni wajibu wetu kulazimika na uadilifu; kwani ndivo mafundisho yetu yalivotutaka, basi kauli yetu ni kufaa kusali nyuma ya kila muislamu ikiwa tu hajaingiza katika sala yake yenye kutengua sala, tunasali tuma ya Imamu Msunni katika hali zote bila kujali ni Msunni wa Madhehebu gani, isipokua kama ataleta katika sala dua ya Kunuti hapo tunarudia tena sala yetu hiyo tuliyo sali nyuma yake, kwani kwetu sisi haifai kuleta dua ya kunuti katika sala kwa sababu ni maneno mengi ya watu.

Ama Mashia Imamia (Ithnaashiria) tunajizuia kusali nyuma yao, lakini tunasali katika misikiti yao ikiwa hawakutuzuia kusali ndani yake.

Kuna Mashia Zaidia hawa tunasali nyuma yao wala hakuna tatizo lolote.

Kuna wenye kujiita Waislamu lakini si Waislamu kiuhakika, hao haifai kusali nyuma yao kabisa, nao ni Maahmadia (Makadiani), ama kufaa kusali ndani ya nyumba zao za Ibada ikiwa wameruhusu na hakuna msikiti wala sehemu ya kuweza kusali kiurahisi isipokua humo tunasali ndani yake, na hukumu hii inamuhusu kila mwenye kuamini mdai unabii yoyote baada ya Muhammad S.A.W.

Pia hatuoni usahihi wa kusali nyuma ya mwenye kukanusha ulazima wa kujishika na Sunna ya Mtume S.A.W. na sio mwenye kukataa riwaya kwa hoja ya kuiona si sahihi kwa vielelezo vinavokubalika ndani ya Uislamu.

Ama suali la kusali wafuasi wa Madhehebu nyengine nyuma ya Imam Muibadhi, kwetu sisi inafaa Muibadhi kuwasalisha waislamu wa madhehebu nyengine zote za Kiislamu wala hakuna tatizo katika hilo.

Wallahu aalamu.

 

Published By Said Al Habsy

KASAHAU QURAN KWA UZEE.

You have a new Question by:

Asma Sultan from

Oman

————————————–

Swali:

Ikiwa umehifadhi Baathist ya sura kwenye Qur an Karin Abada ya kufikia umra mkubwa ukaanza kuzisahau jee kuna hukumu gain?

JAWABU:

Allah mtukufu anaujua udhuru wake, naye ndiye aliyekadiria hayo kama alivyosema :

(وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّاكُمْ ۚ وَمِنْكُمْ مَنْ يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ قَدِيرٌ)
Na Allah mtukufu amekuumbeni kisha anakufisheni, na katika nyinyi wapo wanaorejeshwa katika umri wa udhalili, wawe hawajui chochote baada ya kuwa walikuwa wanajua, hakika Allah ni muweza mwenye elimu.
[Surat An-Nahl)

Na Allah mtukufu atampa kwa ukarimu yale aliyodumu nayo katika mema na akashindwa kuyafanya kwa kusogea kwa umri wake.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis Alghammawi

Published By Said Al Habsy

JE NIUSIE DHAHABU ZANGU WAPEWE WANANGU ?

You have a new Question  from :

Oman

————————————–

Swali:

Nauliza kama naweza kuandika wasia nikifa dhahabu zangu wapewe binti zangu?

JAWABU:
Haifai kuwaandikia wasia warithi, Kwa hadithi sahihi ya Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- :

لا وصية لوارث
Hana wasia mrithi.

Na ikiwa mtu atawaandikia warithi wasia atakuwa amefanya makosa, na wasi huo utakuwa Batili na mali itarejeshwa katika Mirathi.

Allah mtukufu ameahidi kumuingiza  mwenye  kuchupa mipaka ya mirathi ilowekwa pale aliposema :
(وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُهِينٌ)
Na atakayemuasi Allah mtukufu na Mtume wake na kuchupa mipaka yake, Atamuingiza motoni, Akiwa ni mwenye kubakia humo na anayo adhabu yenye kudhalilisha.
[Surat An-Nisa’ 14]

Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis Alghammawi

Published By Said Al Habsy

KAMPIGA MKEWE KWA KUMTUKANIA MAMA YAKE.

You have a new Question by:

Juma Zuberi from

Tanzania

————————————–

Swali:

Nini Hukumu ya Qur’an na Hadithi kwa mume aliempiga mkewe kwa kosa la kutusiwa mama yake mzazi katika uislamu.

JAWABU:
Waalykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Uislam ni dini ya nidhamu nao umeweka mfuatano katika adabu atakazozitoa mume kwa mkewe.
Allah mtukufu amesema:
(الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنْفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا)

…Na wale mnaohofia ukorofi wao basi wapeni mawaidha, na muwahame vitandani, na muwapige, ikiwa watakutiini basi msiwataftie sababu….
[Surat An-Nisa’ 34]

Kwa hivyo utaratibu ni kuanza na mawaidha, kisha kutompa haki ya ndoa kwa kumuhama, kisha ndio inakuja marhala ya kupiga.

kama ambavyo pia ni Muhimu kujua sababu ya ugomvi huo kwanza, ili ueze kuona namna bora ya kuutatua.

Uislam pia umeweka kipigo kisiwe cha kuvunjana mikono na miguu, au kumuharibu sura, n.k. kwani huko ni kutia adabu sio kumvunja mgomvi… kwa hivyo hilo nalo lazima zingatiwe.

Lakini pia katika baadhi ya Kanuni za baadhi ya dola wanazuia kumpiga mke, naam bila shaka huko ni kwenda kinyume na sheria lakini wewe usijiweke katika matatizo ya kikanuni maadam kuna njia nyingine za adabu zilowekwa na uislam.

Mkishindana kabisa basi umewekewa njia ya kumrejesha nyumbani kwao akafunzwe tena namna ya kuheshimu wazazi wa wengine.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis Yahya Alghammawi

 

Published By Said Al Habsy

JE KUPIGA PUNYETO NI SAWA NA KUZINI NA MAMA MZAZI ?

You have a new Question by:

khalfan khu from

Oman

————————————–

Swali:

Asalam alaikum warahmatullahi wabarakatuhu
suali langu ivi nikweli watu wanao jichuwa yani kupiga punyeto nikama wamezini na mama zao wazazi ?

JAWABU:

Waalykm salaam warahmatullah wabarakatuh.

Bila shaka kupiga punyeto ni katika madhambi makubwa yanayowatesa vijana wengi ambao hawajaoa.

Na hapana Shaka kuwa madhara yake kiafya yapo wazi kama ;

1. Kupoteza hamu ya kufanya tendo hilo kawaida.

2. Kulegeza misuli ya sehem za siri na kupelekea kukosa uwezo wa kumuingilia mwanamke.

3. Inapunguza uwezo wa kufaham kwa sababu upandishaji wa hisia unaendana na sana na mishipa ya faham na hivyo kupoteza nguvu nyingi katika lisilo na tija na lisilo na uhalisia.

4. Kupoteza kujiamini na kujihisi unyonge wa daima na upweke, hili hupelekea msongeko wa mawazo hali ambazo hupelekea mtu hata kujinyonga wakati mwingine.

5. Hupatwa na tatizo la kutokwa na Manii au Madhii bila taarifa, kutokana na ulegevu wa misuli yake.

6. Wanakuwa katika hatari ya kuingia katika Ushoga (Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile kwa wanaume), kwa kuathirika akili yake na njia ziziso salama za kumfikisha katika starehe na hasa baada ya kupoteza uwezo wa kuingilia kikawaida.

Amma kisheria; Bila shaka Punyeto ni haram kwanza kwa madhara tuliyoyataja hapo juu lakini pia kwa sababu si njia ya kisheria ya kumaliza matamanio, Amesema Allah mtukufu:

(وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ * إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ * فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ)
“Na waumini ni wale ambao ni wenye kuzihifadhi tupu zao, Iapokuwa kwa wake zao au wajakazi wao hapo si wenye kulaumiwa. Basi atakayetaka tofauti na hayo ndio maadui”
[Surat Al-Mu’minun 5 – 7]

Na Mtume -sallallahu alayhu wasallam- Amewaelekeza vijana njia mbili, Imma kuoa au kufunga ili kuvunja matamanio.

Na Maulamaa huita punyeto ni kuua viumbe hai kulikojificha.


Kwa hivyo Muislam ajiweke mbali na vitendo hivi viovu, amuogope Allah mtukufi na ajue kuwa ataulizwa kuhusu neema anayoipoteza kwa mkono wake.

Amma kuhusu kulingana kwake na kumuingilia mama mzazi, Sijaona pahala palipoandikwa hayo..

Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis bin Yahya Alghammawi

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Nassir Salim from

Tanzania

————————————–

Swali:

Assalam alaykum ,sheikh mimi nauliza hivi:-

Je mtu kama alikua yupo ktk hedhi kwa mwanamke na ikafka cku ambayo aweze kutoharika lkn ucku wake ama kwa kukusudia,kuzembea ,kusahau au bila kujua hakuweza kukoga mpka asubuh jee inafaa kukoga asubuh akafunga ??
katika swali hilo hilo je kwa mwanaamme ambae aliota uck akapata janaba je ,nae kama hakuoga uck ima kwa kukusudia au bila kusudia je nini hukumu yke inamfaa kuoga asubuhi akafunga…

Mashkuriin

JAWABU:
Waalaykm salaam watahmatullah wabarakatuh.

Amma ikiwa ni kwa uzembe sawa ikiwa ni baada ya kumalizika hedhi au Nifasi au Janaba, Itatakiwa yeye asile siku ile aloamka hivyo na akoge asubuhi hiyo lakini pia Airudie pamoja na kutubia.

Kwa hadithi:

من أصبح جنبا أصبح مفطرا

“Atakayeamka akiwa na Janaba ataamka akiwa amefungua”

Amma kuhusu Hedhi nimemuuliza Sheikh wangu Nassor Alharrasi -Allah mtukufi amuhifadh- Akasema hukmu ni hiyo hiyo kwa sharti awe ametoharika usiku kabla ya Alfajiri.

Amma ikiwa bahati mbaya basi afanye haraka kukoga na itakuwa hakuna kitu juu yake.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Omary Mbaji from

Tanzania

————————————–

Swali:

Mimi ni Muislam na ninaipenda dini yangu.

Swali langu ni kwamba, je ukiwa na akili timamu yaani hujarukwa na akili, na pia kwa kutambua kwamba Mungu anajua lugha zote, je ni lazima kuombewa unapopatwa na matatizo? Kwamba ukijiombea mwenyewe dua haiswihi mpaka shehe akuombee ndo dua inakubaliwa na Allah?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Katika moja ya mazuri ya dini yetu hii tukufu ni kuwa haina mtu wa kati baina yako na Allah mtukufu, Allah mtukufu amesema :

(وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ)
“Na amesema Mola wenu: Niombeni nitakujibuni…”
[Surat Ghafir 60]

Na Amesema:
(وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ)

“Na watakapokuuliza kuhusu mimi, basi mimi nipo karibu, ninajibu maombi ya muombaji pale anaponiomba, basi waniombe mimi, na waniamini mimi, ili wapate kuongoka”
[Surat Al-Baqarah 186]

Na Allah mtukufu ameweka lugha tofauti ili kujulisha ukubwa wa uwezo wake, na ishara ya kuwepo kwake amesema:

(وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِلْعَالِمِينَ)
Na katika ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutofautiana kwa ndimi zenu na rangi zenu, hakika katika hayo kuna ishara kwa walimwengu”
[Surat Ar-Rum 22]

Hivyo muombe Allah mtukufu kwa lugha yoyote utakayo, Bila kurudi kwa Sheikh yoyote yule, Allah mtukufu atakujibu maombi yake, Hakika yeye ndiye msikivu, mjuzi.

Lakini zingatia pia kuwa katika sala za faridha kumewekwa shuruti na taratibu, hivyo humo imekatazwa lugha isiyokuwa lugha ya Qur an, Na unaweza kusujudu baada ya kutoa salam na ukamuomba Allah mtukufu ulitakalo.

kama ambavyo wapo waliotoa ruhusa katika sala zisizo za faridha. Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi

 

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Abdulla suleiman from

Tanzania

————————————–

Swali:

assalaam alaykum.
Mm nauliza , nini hukumu ya ibadhi anapokaribishwa kusalisha katika misikiti ya masunni au masalfi..?,
ukizingatia wao hufunga mikono na kutodhihirisha BISMILLAH nk.

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Kwetu Sisi Ibadhi hakuna katazo la kuwasalisha ndugu zetu Masunni, Wala hakuna katazo la kusali nyuma yao maadam wanatekeleza sala yao kwa mujibu wa Mafundisho sahihi ya Madhehebu zao.

Ispokuwa anatakiwa Muibadhi asiache chochote katika Mafundisho ya Madhehbu ya Ibadhi wakati anawasalisha. kwa hivyo:

Atasoma Tawjiih kabla ya Takbirat Ihraam
Atasoma Istiadha kimya kimya.
Atasoma bismillah kwa sauti kama sala ni ya sauti.
Hatoitika Aamin baada ya Alhamdu.
Hatonyanyua mikono wala kuifunga bali ataiwachia.
hatonyanyua kidole cha Shahada wakati wa tahiyyat.
Wala Hatotoa salam mbili bali atatoa salam moja tu.

* Tanbiihi pia ikiwa atasali nyuma yao ispokuwa katika Kukuqunuti tu na ikiwa mmoja wao ni Musbil yaani nguo zake zimepita vifundo vya miguu… hapo itambidi Muibadhi arudie sala yake.
Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis bin Yahya Alghammawi

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

SUALI:

A. Aleykum.

Mimi ni Bint wa Kiislam, nilikuwa ninahitaji kujua kwamba msichana na mvulana wa kiislam wakifanya zinaa, na wakalijua kosa lao, kisha wakamrudia Allah na kutaka msamaha kwake. Je! Inaruhusiwa wao kufunga ndoa? Na kama wanaruhusiwa je kuna masharti yapi wanatakiwa kuyafanya ili kuweza kufunga ndoa na ikakubalika kwa Allah?

JAWABU:

Wa alaykum salam wa rahmatullahi wa barakatuh.

Allah azihifadhi jamii kwa kuziepushia janga la uzinifu.

Uzinifu ni kosa kubwa, na iwapo mja aliyelifanya hakutubia basi linamuangamiza katika laana za Allah na ghadhabu zake na adhabu ya milele motoni. Allah atuepushie.

Na katika athari za uzinifu ni kutofaa tena kuoana walioonjana kwa uzinifu, na pindi wakikaidika na kuamua kufunga ndoa basi uhakika wao unabakia kuwa ni wenye kuendelea na uzinifu tu.

Huu ndio msimamo wa Madhehebu ya Ibadhi katika suala hili.

Hayo ni kwa sababu Allah mtukufu ametueleza kuwa kuoana na mzinifu ni sawa na kuoana na mshirikina pale aliposema:

﴿الزّاني لا يَنكِحُ إِلّا زانِيَةً أَو مُشرِكَةً وَالزّانِيَةُ لا يَنكِحُها إِلّا زانٍ أَو مُشرِكٌ وَحُرِّمَ ذلِكَ عَلَى المُؤمِنينَ﴾ [An-Nûr: 3]

((Mzinifu wa kiume haoi isipokua mzinifu wa kike au mshirikina, na mzinifu wa kike haolewi isipokua na mzinifu wa kiume au mshirikina. Na hilo limeharamishwa kwa Waumini.)) [Nuur.3]

Kwa hiyo ndoa ya kuoana na mzinifu ni haramu kama ndoa ya kuoana na mshirikina, basi ndoa hiyo ni haramu kwa Waumini kama Aya ilivoeleza.

Aliulizwa Imam Jabir R.A. kuhusu waliozini kisha wakataka kuoana akajibu: “Jaalieni baina yao bahari kijani, na akiweza hata asimtazame mwenzake basi asimtazame.”

Imekuja katika Muwataa wa Imam Malik kuwa Amiri wa Waumini Omar bin Al-Khattabi R.A. alifikishiwa kosa la mwanamke kuolewa akiwa katika eda ya mumewe. Basi Omar R.A. akapitisha hukumu ya kuvunjwa ndoa hiyo, kisha akasimama na kusema kuwa: Mwanamke yoyote atakayeolewa akiwa bado hajamaliza eda, itavunjwa ndoa hiyo, na iwapo huyo aliyeoa hakuwahi kumuingilia, basi yule mwanamke atamaliza eda ya mume wake wa mwanzo kisha huyu aliyeoa atakua ni mposaji akimtaka yule mwanamke kuwa mkewe, ama ikiwa alimuingilia, basi ndoa itavunjwa, kisha mwanamke atamaliza eda ya mume wa mwanzo, kisha atakaa eda ya mume wa pili, kisha haitakuepo ndoa baina yao milele.

Bila shaka hukumu ya kutokuwepo ndoa baina yao milele ni kwa sababu ya kumuingilia kwake katika ndoa batili ambako kumepitia fungo batili la ndoa, kwa hiyo kukaingizwa katika hukumu ya uzinifu.

Leo Mabanati wangapi wanaingizwa katika uzinifu kwa tamaa za kuolewa? Lau kuwa wanafanyia kazi msingi huu usemao kuwa uzinifu ukipita ndoa haipo tena baina ya waliozini, kwa hakika wanawake wasingekhadaiwa kupitia tamaa ya kuolewa, wala vijana wasingekubali kuanzisha ndoa juu ya uzinifu, na Jamii ingaliepukana na janga la uzinifu kwa asilimia kubwa.

Kutokana na hilo ikiwa mja kaingia katika dhambi ya uzinifu anatakiwa ajiwahi kwa kutubia na ajisitiri nafsi yake, na iwapo atatokezea wa kuoana nae -ambae si yule aliyezini nae- atafunga nae ndoa, na asije akaifedhehi nafsi yake kwa dhambi aliyoifanya; kwani mwanandoa akijua tu kuwa mwenzake ni mzinifu na akawa na yakini na hilo haitakua halali kwake kubakia nae katika ndoa.

Allah azihifadhi jamii.

Wallahu aalamu wa ahkamu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum.

Tumeambiwa kuwa Makka ndio mama wa miji, na kuwa miji yote iliyobaki ni watoto wake; kwa hiyo ni wajibu wa watoto kufuata mama yao, hasa hasa katika yenye tafauti ndani yake; kwa hiyo inalazimika kufuata Makka katika funga ya Arafa. 

Jee! Hii ni kweli? Na kama sio kweli kuna jawabu gani ndani yake?

JAWABU

Neno hilo halina ukweli wowote ndani yake; kwa sababu Allah mtukufu kwenye kitabu chake hakutuambia tufuate Makka kwani ndio Mama wa miji kama alivodai huyo msemaji, bali ametuambia tumtii yeye na tumtii Mtume wake na Viongozi waumini waliojifunga na utiifu wa Allah na mtume wake, na kama tutavutana katika jambo lolote na kutafautiana wajibu wetu tulirejeshe jambo hilo  kwa Allah mtukufu na kwa Mtume wake, na kulirejesha kwao yaani kurejesha katika Kitabu chake na Sunna ya Mtume wake S.A.W. wala hakutuambia tufuate Makka.

Vilevile inajulikana vizuri kuwa hukumu ya Umama wa Makka ni ya kale kabla ya Utume wa Mtume wetu Muhammad S.A.W. na aya iliyotaja Umama wa Makka imekuja ndani yake ili uuonye mama wa Miji na walio pemezoni yake. Kwa maana hiyo pana uwezekano wa Mama huyu kuwepo katika makosa, bali ilifikia kuwa ndio kitovu cha kuabudia Masanamu kwa Waarabu kabla ya ujio wa Mtume S.A.W. na katika kipindi cha daawa yake S.A.W. cha miaka kumi nane takariban, kwa hiyo Mama huyu akiwemo katika makosa hakuna haki ya kumtii.

Likibainika hili itabainika wazi wazi kuwa hoja ya kufuata Makka ni hoja hewa imejengwa juu ya mapendwa moyo.

Amesema Sheikh Massoud Al-Miqbali Allah amuhifadhi akimjibu aliyekuja na neno hilo:

Inaonesha kuwa huyu msemaji hajui tafauti baina na Mama na Imamu.

Makka ni Mama wa Miji na sio Imamu wa Miji.

Na umama haulazimishi kufuatwa, kwani tunajua kuwa Mama anaweza akasali safari hali ya kuwa Binti yake ataitimiza kwa kufuata Mumewe…

Kisha, kwa mujibu wa maneno ya Sheikh huyu (aliyekuja na hoja ya kufuatwa mama wa miji) itawalazimu watu wafuate Makka katika nyakati za Sala vilevile!!!!

Nami ninaona maneno yake hayo (huyo Sheikh wa hoja ya umama) ni uzushi baridi sana, basi hauna nafasi yoyote katika soko ya wenye akili zao timamu achilia mbali Wanavyuoni.

Na Allah ndie anajua zaidi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

SUALI:

Mtu alie zini hutoharika kwa muda gani?

JAWABU:

Uzinifu ni dhambi kubwa na iliyo mbaya sana, basi dhambi hiyo humuondosha mwenye kuifanya katika duara la Imani na kumuingiza katika duara la ukafiri wa neema na laana za Allah na makasiriko yake, na atabakia huko mpaka utubie kwa Allah mtukufu toba ya kweli ndio atarejea katika duara la Imani la kuridhiwa na Allah mtukufu, na pindi akifikwa na mauti bila kujiwahi na toba basi mafikio yake ni Motoni milele Allah atuepushe nao.

Ama kwa upande wa tohara, ujue kwamba mwenye kuingia utupu wake katika utupu wa mwengine hua amifikiwa na hali ya janaba nayo ni Hadathi kubwa inayohitajia kujitoharisha kwa kuoga josho la janaba.

Kwa mafunshisho ya kujitoharisha janaba fuata viunganishi vifuatavyo.

 1. https://ibadhi.com/sw/vipindi/142-kukoga/1559/kuoga-janaba
 2. https://ibadhi.com/sw/vipindi/jamii/142-kukoga

Wallahu aalamu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

SUALI:

Mume wangu ameritadi na kuacha Uislamu ni ipi hukumu ya doa yetu?

Tunaomba jawabu kwa dalili.

JAWABU:

Allah mtukufu ameharamisha doa baina ya Muislamu na Mshirikina kama alivotueleza katika Kitabu chake:

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

Na musioe wanawake washirikina mpaka waamini, na mjakazi muumini ni bora kuliko mwanamke mshirikina hata akikupendezeni, na musiwaozeshe wanaume washirikina mpaka waamini, na mtumwa muumini ni bora kuliko mwanamme mshirkina hata akikupendezeni. Hao wanaita katika Moto, na Allah anaita katkika Pepo na usamehevu kwa idhini yake, na anabinisha aya zake kwa watu ili wakumbuke. (Al-Baqarah 221)

Vile vile Allah mtukufu anatuambia:

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

Hao (wanawake waumini) si halali kwao hao (wanaume washirikina), na hao (wanaume washirikina hawawi halali kwao hao (wanawake waumini). [Mumtahina 10].

Na kwa maana hiyo muislamu hawezi kubakia na mshirkina katika doa kamwe.

Likibainika hili itakulazimu uachane nae huyo Murtadi aliyeacha Uislamu na kuingia katika mila nyengine ya Kishirkina au ya Kupingamungu, kisha utakaa eda, na baada yake akitokezea mume muislamu mposaji unaweza kuolewa nae.

Wallahu aalamu.

Published By Said Al Habsy

SHAFI SHAFI from 

Kenya

————————————–

Swali:

mume ameteta na mkewe hapiti wala hamshuhulikii miezi sita sasa je ndoa iko ?

JAWABU:

Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

 

NDOA IPO.

 

Lakini mke ana haki ya kuomba kuachwa, kwa vile hatimiziwi haki zake, na kama mume atakataa basi alipeleke jambo la kwa Kadhi ambaye Sheria imempa uwezo wa kumuandikia talaka hata kama mume atagoma.

 

Na wote wawili wamuogope Allah mtukufu, wasikiache kibri kikaharibu ndoa yao, waombane msamaha, warudi kama zamani. Allah mtukufu anasema kuwaambia wanamme :

 (…وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَنْ يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِنْ كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا)

Wala msiwadhiki wanawake ili mpate kuchukua vile mlivowapa, Ispokuwa kama wataleta uovu uliowekwa wazi, na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mtawachukia basi huenda mkachukia jambo na Allah mtukufu akajaalia ndani yake kheri nyingi”

[Surat An-Nisa’ 19]

 

Na Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- amewausia wanawake wasiwe wenye kuzikana neema za waume zao, aliposema :

>

《 Nimeona Wengi katika watu wa motoni ni wanawake. wakasema : kitu gani kinachosababisha ewe Mjumbe wa Allah ? Akasema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-: Kwa kukufuru kwao, wakasema: Je wanamkufuru Allah mtukufu ? Akasema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-: Wanakufuru mahusiano mazuri, law kama utamfanyia wema mmoja wao zama zote kisha akaona kwako jambo moja – hakulipenda- atasema: Sijaona kheri yoyote kwako”

 

Na Allah mtukufu amewanasihi wote kwa kusema :

( ۚ وَلَا تَنْسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)

Wala msisahau fadhila zilokuwa baina yenu, Hakika Allah mtukufu ni muoni kwa myafanyayo.

[Surat Al-Baqarah 237]

 

Na mengi ya matatizo ya ndoa yanaanzia katika kuchagua basi tunawaomba wazingatie wanamme na wanawake haya mambo ya ndoa katika dini.

Wallahu aalam.

 

Ameyaandika:

Khamis Yahya Alghammawi

kalghammawy@gmail.com

Published By Said Al Habsy

Mohammed Al – Hashmy from 

Tanzania

————————————–

Swali:

As salaam alaykum warahmatullah wabarakatuh. 

Mimi naomba mtufunze jinsi ya kuishwali hii swala ya Dhuhaa. 

Ahsante shukran.

JAWABU:

Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

 

Sala ya dhuha ni sala ya Sunna inayosaliwa katika muda wa baada ya kuchomoza jua lote mpaka kabla ya kufikia jua kati kati ya anga.

Ikisaliwa mapema huitwa Ishraaqi kwa jina lingine, Ikisaliwa taqriban saa nne kiswahili (Saa kumi oman) inakuwa bora na ikicheleweshwa pia inajuzu.

Bora ya rakaa zake ni nane

 197) … أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ قَالَ: بَلَغَنِي عَنْ أُمِّ هَانِئٍ بِنْتِ طَالِبٍ قَالَتْ: صَلَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بَيْتِي صَلاَةَ الضُّحَى ثَمَانِيَ رَكَعَاتٍ>>

Amesema Ummu haani bint Taalib :

《Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- alisali nyumbani kwangu sala ya dhuha rakaa nane》

Lakini inajuzu kusali rakaa mbili, au nne au sita n.k.

Nayo husaliwa rakaa mbili mbili kwa kutoa salam baina yake.

Nayo ndiyo huitwa sala ya waliotangulia au waliorejea kwa Allah mtukufu.

Baadhi ya riwaya zajulisha kuwa wenye kuisali watakuwa na malipo yao maalumu siku ya Qiyama.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:

Khamis Alghammawi

 

Published By Said Al Habsy

issa haruna from 

Tanzania

————————————–

Swali: 

Dua gani isomwe kumrudisha mtu aliyepotea ? 

JAWABU:

Waalkm salaam warahmatullah wabarakatuh.

Qur an yote ni ponyo na Rehma kama alivyoeleza Allah mtukufu :

(وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِلْمُؤْمِنِينَ ۙ )

《Na tunateremsha Quran ambayo ni ponyo na Rehma kwa waumini》

[Surat Al-Isra’ 82]

Na imepokewa kuwa Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- amesema

“اقرؤوا القرآنَ ، و سلوا اللهَ به”

《Someni Quran, na muombeni Allah mtukufu kwa Quran hiyo》

Na katika baadhi ya athari zilizopita wamesema :

 “خذوا من القرآنِ ما شئتم لما شئتم”

《Chukueni katika Qur an mkitakacho kwa muyatakayo》

 

Kwa Misingi hiyo Sura yoyote katika Quran ukaichukua na kuisoma kwa Ikhlas na yaqini kisha ukqmuomba Allah mtukufu basi Allah mtukufu atakupa ukitakacho.

 

Na katika Sura ambazo tumeskia wengi wakizisoma Suurat Yasin, pia wakirudia rudia vaya zifuatazo:

حسبنا الله ونعم الوكيل

“Hasbunallahu waniimal wakiil”

au

“فسيكفيكهم الله وهو السميع العليم”

“Fasayakfiikahumullah wahuwa samiul aliim”

Bila kusahau kuamka usiku na kusali rakaa za kumumomba Allah mtukufu kwani nyakati hizo dua hujibiwa.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:

Khamis bin Yahya Alghammawi

alghammawy@gmail.com

Published By Said Al Habsy

issa haruna from

Tanzania

————————————–

Swali:

je talasimu ni halali katika dini maana kuna talasimu kama za mvuto wa biashara je zinafaa kutumia ?

JAWABU:
Allah mtukufu ametuamrisha tumuombe yeye katika kila tukitakacho katika maisha ya dunia.
Amesema :
(وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ)
Na Amesema mola wenu: Niombeni nitakujibuni, hakika wale ambao wanafanya kibri kunako ibada yangu wataingia motoni kwa udhalili.
[Surat Ghafir 60]

Na riwaya zimekuja nyingi zenye kuonyesha kuwa bora ya Ibada ni mtu kujiombea mwenyewe, na mwenye kushindwa kuliko wote ni aliyeshindwa kujiombea dua mwenyewe.

Hivyo inapendelewa kwa muislam kuishika nguzo hii muhimu, pamoja na kutazama kwake nyakati ambazo kisheria zimependelewa katika kuomba dua iliyo muhimu katika zote ni kila baada ya wema, mfano: kila baada ya sala, kila baada ya kutoa sadaka, kila baada ya kusoma Qur an n.k.

Kwa Msingi huu Talasimu kama yenyewe haina uwezo wa kuleta manufaa wala kuondodha madhara, haiponyi wala haikingi, Mwenye kuitakidi tofauti na haya anaweza kuingia katika shirki, Allah mtukufu atukinge nayo.

Amma ikiwa talasimu hiyo imendikwa Quran au dua ya kawaida yenye kujulikanwa maana yake, Pamoja na usalama wa itikadi ya kuwa mwenye kunufaisha na kudhuru ni Allah mtukufu haikatazwi talasimu ya aina hiyo.

Amma ikiwa hiyo talasimu ni michoro isiyofahamika au maneno yasiyosomeka wala kujulikanwa au yenye kujulikanwa maana yaka lkn ikawa kuna kumuomba asiyekuwa Allah mtukufu kama majini au malaika basi itakuwa haifai.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawy
kalghammawy@gmail.com

Published By Said Al Habsy

Bizabishaka Aisha from

Burundi

————————————–

Swali:

Duwa gani ao aya gani ndani ya qur’an Unaweza kuitumiya kutaka ALLAH akubali maombi yako haraka. Na unaweza ku swaum siku ngapi?

JAWABU:

Dua ndio msingi wa Ibada, Allah mtukufu ametutaka tuelekee kwake moja kwa moja tuombapo dua zetu.

Akasema :

((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ ))

?? Na amesema Mola wenu: Niombeni nitakujibuni??

Kisha akabainisha ya kuwa yeye yupo karibu nasi kuliko tinavyofikiri akasema :

(وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ)

??Na watakapokuuliza waja wangu kuhusu mimi: basi mimi nipo karibu, hujibu maombi ya muombaji aniombapo, basi waniitikie mimi na waniamini ili wapate kuongoka??

[Surat Al-Baqarah 186]

Pamoja na hayo, Allah mtukufu hajaweka baina yake sababu wala nasabu yenye ukaribu kama uchamungu, Wachamungu wakitakacho hupewa, waliombalo hujibiwa, walisemalo husikilizwa, basi Njia bora ya kukubaliwa maombi yetu ni kuwa wachamungu, Amesema Allah mtukufu:

(وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ)

??wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa haki, pale walipotoa vikurubisho basi kikakubaliwa -kikurubisho- cha mmoja na kingine hakikukubaliwa, akasema-yule ambaye hakukubaliwa- nitakuua, Akasema yule -aliyekubaliwa- : Hakika Allah mtukufu huwakubalia wachamungu tu.??

[Surat Al-Ma’idah 27]

Maneno haya yametiliwa mkazo na Bwana Mtume Muhammad -Sallallahu alayhi wasallam- aliposema:

اللهَ قال ، …وما تقرَّب إليَّ عبدي بشيءٍ أحبَّ إليَّ ممَّا افترضتُ عليه ، وما يزالُ عبدي يتقرَّبُ إليَّ بالنَّوافلِ حتَّى أُحبَّه ، فإذا أحببتُه : كنتُ سمعَه الَّذي يسمَعُ به ، وبصرَه الَّذي يُبصِرُ به ، ويدَه الَّتي يبطِشُ بها ، ورِجلَه الَّتي يمشي بها ، وإن سألني لأُعطينَّه ، ولئن استعاذني لأُعيذنَّه >>

Allah mtukufu amesema: Hakuna jambo ninalolipenda zaidi kwa mja wangu kujileta karibu yangu kuliko yale niliyomfardhishia, na ataendelea kusogea karibu yangu kwa ibada za ziada (Sunnah) mpaka nitampenda, Nikishampenda nimuwafiqisha katika maskio yake anayosikizia, macho yake anayo onea, mikono yake anayoshikia, na miguu yake anayotembelea, -katika utiifu-, Ikiwa ataniomba nitampa, na akijikinga kwangu nitamkinga” Bukhari 6502

Pia Allah mtukufu ametutaka tumuombe kwa majina yake na sifa zake tukufu aliposema :

(قُلِ ادْعُوا اللَّهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَٰنَ ۖ أَيًّا مَا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا)

??Sema: Muiteni Allah mtukufu au muiteni Alrahmaan, lolote mtakalotumia kati ya hayo yeye anayo majina mazuri matukufu,…??

[Surat Al-Isra’ 110]

Pia amesema :

(وَلِلَّهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ)

??Allah mtukufu anayo majina mazuri basi muiteni/muombeni kwa majina hayo…??

[Surat Al-A’raf 180]

Katika hadithi amesema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam-

إنَّ للهِ تسعةً وتسعين اسمًا ، مائةً إلا واحدًا ، من أحصاها دخل الجنةَ .”

??Hakika Allah mtukufu ana majina tisini na tisa, Mia moja kasoro moja, atakaeyahifadhi ataingia peponi??Bukhari 7392.

Pia Allah mtukufu ametujulisha katika njia za kuomba dua ni baada ya kumaliza kufanya amali yoyote ya kheri, Kama sala, kusoma quran, kutoa sadaka n.k. kwa qauli yake:

(فَإِذَا فَرَغْتَ فَانْصَبْ)

??Utakapomaliza -ibada- basi jichokeshe -katika kuomba dua-??

[Surat Al-Sharh 7]

Wamesema baadhi ya wanachuoni : “Anayemaliza sala kisha asiombe dua ni kama mtu aliyetikisa mti wa matunda yalipodondoka akaondoka bila kuyachukua”

Pia wakati wa kuteremka mvua, wakati wa kabla ya alfajiri, wakati wa baina ya adhana na Iqama, Lailatul qadri n.k.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:

Khamis bin Yahya Alghammawi

 

 

Published By Said Al Habsy

Munira Miraji from

Tanzania

————————————–

Swali:

Je inaruhusiwa kwa mtu aliye na matatzo ya kutokwa na upepo kusoma Quran baada ya swala ya faradhi au sumna?

JAWABU:
Waalykm salaam warahmatullah wabarakatuh.

Wanachuoni wametofautiana kuhusu mtu asiyekuwa na udhu (Uchafu mdogo)  kusoma Qur an tukufu.
Wapo walioruhusu moja kwa moja baada ya kuona kutothibiti au kutokuwepo kwa hoja katika dalili zitolewazo na wenye kukataza.

Wapo waliokataza moja kwa moja kwa dalili walizoziona zimethibiti katika sunnah na wengine wakatoa dalili katika Quran kwa aya :
(لَا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ)
‘Hawaigusi Quran ispokuwa waliotakaswa”
[Surat Al-Waqi’ah 79]

Amma hadithi ni kwa aliyoyapokea Imam Rabii katika Musnad yake:
11) … أَبُو عُبَيْدَةَ عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ قَالَ: قَالَ رَسُول اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْجُنُبِ وَالْحَائِضِ وَالذِينَ لَمْ يَكُونُوا عَلَى طَهَارَةٍ: «لاَ يَقْرَؤُونَ الْقُرْآنَ، وَلاَ يَطَؤُونَ مُصْحَفًا بِأَيْدِيهِمْ حَتَّى يَكُونُوا مُتَوَضِّئِينَ».
Abu Ubaidah kutoka Jabir bin Zaid Amesema: Amesema Mtume -Sallallahu alayhi wasallam- kuhusu wenye janaba na wenye hedhi na wasiokuwa na udhu : wasisome Quran,  sala wasiukamate kwa mikono yao mpaka wawe wana udhu- wamesafika-“

Na bila shaka dalili hii iliothibiti inaipa nguvu qauli ya waliokataza.

Na wapo waliopita njia ya kati kati wakaona kuwa katazo ni la hadathi kubwa (Janaba, Hedhi,  na Nifasi)  Amma kutokuwa na udhu kikawaida basi inapendelewa atie udhu kabla ya kusoma au kushika Qur-an.

Pamoja na khilafu lakini wanachuoni wanasema dharura na hali tofauti zina hukmu zake.
Wakatoa ruhusa kwa wanafunzi wadogo w a Qur an ambao wanapata tabu ya kutia udhu kila Mara, kupitia mlango :
(وَجَاهِدُوا فِي اللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ  مِلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِنْ قَبْلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ)
[…Allah mtukufu hajaweka juu yenu uzito katika dini…]
[Surat Al-Hajj 78]

Na aliposema katika aya ya udhu:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ مِنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُمْ مِنْ حَرَجٍ وَلَٰكِنْ يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ)
[…Allah mtukufu hataki kukuwekeeni uzito juu yenu lakini anataka kukutakaseni na akutimizieni neema yake juu yenu ili mshukuru”
[Surat Al-Ma’idah 6]

Na ni kupitia msingi huo wanachuoni wamemruhusu mwenye mkojo au damu au kutokwa na upepo kwa kuendelea kusali faridha, sunnah na kusoma Quran kwa udhu ule wa sala husika kwa vile ni jambo zito kwake kutia udhu kila akitokwa na chochote katika hayo niliyoyatanguliza.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi

Published By Said Al Habsy

Hamed from

Tanzania

————————————–

Swali:

Nini Hukmu ya mwanadamu mwenye kiburi na dharau?

JAWABU:

Hawi na dharau na kibri ispokuwa mtu aliye na mapungufu mengi anayotaka kuyafunika kwa kujipandisha na kuwadharau wengine.

KIBRI ni sifa ya Allah mtukufu basi atakayejipa sifa hiyo atakuwa amestahiki adhabu ya milele katika moto wa Jahannam kama atakufa bila kutubia.

Kwani imepokewa katika hadithi sahihi kuwa Mtume amesema:

(لا يدخُلُ الجنَّةَ عبدٌ في قلْبِهِ مثقالُ ذرَّةٍ مِنَ الكبرِ )

[Haingii peponi Mja ambaye moyoni mwake muna chembe ya kibri]

Na imepokewa katika hadith Qudsi kuwa Allah mtukufu amesema :

الكبرياءُ رِدائي ، والعظمةُ إِزاري ، فمن نازعَني واحدًا منهما ، قذفْتُه في النارِ .

[Kibri na utukufu ni mavazi yangu (sifa zangu), atakayeninyang’anya moja ya viwili hivyo nitamtupa motoni]

Na bila shaka sifa ya kibri si sifa ya waumini bali ni sifa ya waovu, wanafiki, na makafiri na wote hao wameiga kutoka asili ya shari, Ibilisi – Allah mtukufu amlaani-; Amesema Allah mtukufu:

(إِلَّا إِبْلِيسَ اسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ)

[Ispokuwa Ibilisi -hakusujudu- alifanya kibri na akawa katika Makafiri]

{Surat Sad 74}

Kama ambavyo dharau pia ni katika sifa za Unafiki, ambazo zimeigwa kutoka kwa wapingaji wa Mitume nao wakiiga kutoka kwa Ibilisi aliyelaaniwa, kwani ni yeye aliyeweka misingi ya kudharau wengine pale alipomdharau Adam kwa sababu ya asili yake ya udongo akasema kwa majivuni:

(قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِنْهُ ۖ خَلَقْتَنِي مِنْ نَارٍ وَخَلَقْتَهُ مِنْ طِينٍ)

[Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye; umeniumba kwa moto na umemuumba yeye kwa udongo]

{Surat Sad 76}

Kwa hivyo mwenye kuchukua tabia hiyo amejufananisha na mlaanifu huyo, basi ajiandae ukaaji wa milele katika Moto wa Jahannam kama hakutubia.

Pamoja na hayo mtu huyo aitapata adhabu ya Allah mtukufu hapa duniani ili akumbushwe kwani maradhi hayo ni maradhi ya moyoni, ambayo yamejificha katika nafsi kama mdudu chungu mweusi katika weusi wa kiza cha usiku akiwa katika jiwe kubwa. Hivyo atakayekuwa katika madhambi haya atapata adhabu za kumkumbusha na kumrejesha akikumbuka basi kheri yake akisahau au akadharau basi khasara iliyoje ya kughafilika huko. Na itoshe hali ya mwenye bustani kuwa ni mazingatio pale apoingia bustanini kwale akijivika kibri na kuwadharau wana bustani wenziwe kwa kusema :

(وَدَخَلَ جَنَّتَهُ وَهُوَ ظَالِمٌ لِنَفْسِهِ قَالَ مَا أَظُنُّ أَنْ تَبِيدَ هَٰذِهِ أَبَدًا * وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِنْ رُدِدْتُ إِلَىٰ رَبِّي لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِنْهَا مُنْقَلَبًا)

Akaingia bustanini kwake akiwa ni mwenye kuidhulum nafsi yake, akasema: Sidhani kama hivi vitu vitakwisha, wala sidhani kwamba Qiyama kitasimama]

[Surat Al-Kahf 35 – 36]

Akaonesha dharau ya wazi kwa mwenziye aliyepewa mtihani wa uchache wa rizki kwa kumwambia kwa fakhari na majivuni:

(وَكَانَ لَهُ ثَمَرٌ فَقَالَ لِصَاحِبِهِ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَنَا أَكْثَرُ مِنْكَ مَالًا وَأَعَزُّ نَفَرًا)

[Na alikuwa na matunda -bustanini kwake- akasema kumwambia mwenziwe walipokuwa wanajadiliana: Mimi Nina Mali nyingi zaidi na mwenye nguvu ya watu wengi zaidi]

[Surat Al-Kahf 34]

Allah mtukufu akaiharibu ile mali ilokuwa ikimpa kibri na dharau kwa wenziwe akatueleza hayo kwa kusema:

(وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَىٰ مَا أَنْفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّي أَحَدًا)

[Yakazungukwa matunda yake usiku ule kwa adhabu, ikawa asubuhi yake anajuta kwa Yale aliyotoa kuihudumia bustani, nayo ipo tupu haina chochote, hali akisema: Yaa leit nisingemshirikisha mola wangu na yoyote]

{Surat Al-Kahf 42}

Basi hiyo ndiyo hali ya mwenye kibri na dharau hapa duniani, Allah mtukufu humuadhibu hapa duniani na kesho Akhera hali yake itakuwa mbaya zaidi.

Basi amche Allah mtukufu mwenye sifa hii mbaya, na kwa lipi kubwa alilofanya mwanadamu hata awe na kibri na dharau kwa wengine ?

Allah mtukufu atukinge na sifa hizi mbaya.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:

Khamis Yahya Alghammawi

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Hafiid Muhammad from

Tanzania

————————————–

Swal

 

Hafiid Muhammad from

Tanzania

————————————–

Swali:

Assalamu alaykum


Ninauliza hivi “mali iliyokopeshwa kwa mtu ikiwa imefika nisaab na ikafika muda wa kutoa zaka je mkopeshaji anatakiwa kuitolea zaka hali ya kuwa hajarudishiwa mali yake hiyo?”

JAWABU:
Waalaykm salaam warahamtullah wabarakatuh.

Deni au mkopo ukitimiza mambo matatu basi itamuwajibikia Yule anayedai atolee yeye Zaka amma ikipungua moja kati ya hayo matatu au mawili au yote basi itamlazimikia anayedaiwa.

Mambo hayo:
1. Imefika muda wake wa kulipwa.
2. Aliyekopeshwa awe muaminifu mlipaji.
3. Aliyekopeshwa awe na Mali ya kulipia hilo deni.

Yakitimia hayo hata kama ile Mali hajapewa bado basi itamuwajibikia aiweke katika hesabu ya Zaka zake kwa mwaka ule.
Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Ahil Haroon from

Tanzania

————————————–

Swali:

1. Nampenda mwanamke lakini simpati na huwa tunagombana
2. Watu huwa wananichukia sana
3. Kitu chochote nikifanya huwa inaharibika
4. Nikipata pesa huwa hazikai mkononi ila zinapotea nakua sijui nimetumia wapi
5. Mimi ni mwanaume lakini na matatizo sehemu ya siri
6. Mimi huwa napata ndoto mbaya sana wakati nikilala mpaka natoka na manii
7. Mimi nina shida na maisha yangu badala ya kwenda mbele narudi nyuma.

JAWABU:
Waalaykm salaam warahmatullah wabarakatuh.

 Jumla ya nasaha zifuatazi zinaweza kukufaa.

1. Rekebisha mahusiano yako na mola wako, kwa kufanya touba ya kweli na kuacha kila maovu pia kusoma Quran na kujilazimisha na adhkaar za kila pahala kama kulala, kula, n.k. Pamoja na kujikurubisha kwake kwa Ibada hasa sala, Funga na kutoa Sadaka.

2. Fungua akaunti benki ya kiislam, na ukipata pesa kaziweke huko.

3. Weka mipango ya matumizi yako ya kila mwezi ili kuzuia kununua visivyokuwemo katika budget. Pamoja na kuandaa sehem nyingine ya kuandika kila matumizi.

4. Kama hujaoa basi fanya Istikhara umuombe Allah mtukufu akusahilishie ikiwa ni kheri kwako na akuepushie ikiwa ni shari kwako, kisha penda kilichopo kama ulichokipenda hakipo.

5. Jihadhari na waganga watakutapeli.

Wallahu aalam.

Ameyaandika:
Khamis bin Yahya Alghammawi

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Bakari Omary from

Tanzania

————————————–

Swali:

Je inajafaa kumuoa mwanamke ulliye zini nae..? Na ipi hukumu yake…?

JAWABU:
Waalykum salaam warahmatullah wabarakatuh.
NDOA HIYO NI HARAMU kwa sababu:

KWANZA: inajulikanwa kuwa ndoa ni fungamano tukufu linalojengwa katika kuaminiana ili kupata upendo na huruma kwa wanandoa. Na bila shaka baina ya waliokwisha kuzini inakosekana kuaminiana baina ya hawa watu wawili kwa kila mmoja kuijua khiyana ya mwingine, kama ambavyo anakosa amani ya kwamba mwenzie hatomkhini huko alipo.

Pili: Zinaa ni kuivunja heshima ya mwanamke na familia yake kwa ujumla, na mvunjifu wa heshima hatakiwi kupewa zawadi Bali kupewa adabu ya uvunjifu wake wa heshima, na kwa ajili hiyo uislam umeweka mijeledi mia moja ikiwa hajaoa au kuolewa, amma ikiwa ameoa au kuolewa kabla basi adabu yake ni kupigwa mawe mpaka afe ili akome yeye na wengine kuchezea heshima za watu, ajabu ya zama hizi ni kuwa mzinifua badala ya kupewa adabu anapewa mke kwa ndoa za mkeka au kwa njia nyingine, yaani kwa ufupi anapongezwa hadharani kwa kuvunja heshima na anapewa zawadi. Subhaanallah… Basi kuna udhalili kuliko huo?

TATU: Mtu akifanya madhambi yatakiwa ajistiri, aombe touba sio kuhalalisha madhambi yake, kama wafanyavyo wazinifu, na uislam umeharamisha mtu kumuuliza mwanamke kwa vipi imeondoka bikira yake? Bali hata akilazimishwa kusema uislam unamtaka mwanamke atafute lolote la kusema lakini asiseme yaliyopita kama aliingia katika uchafu wa zinaa, kwani akikiri tu kuwa alizini ndoa itakuwa imevunjika, na kwa utaratibu huu khofu ya kusema ataolewa na nani haipo aslani, kama ambavyo Allah mtukufu ndio mpangaji wa riziki.

NNE: Ikiwa wanandoa watalaaniana kwa kutuhumiana kuzini basi ndoa itakuwa imekufa hapo hapo kwa makubaliano ya waislam wote, basi ikiwa kutuhumiana zina tu kunaharibu vipi itakuwa hukmu ya waliozini kabisa?? Bila shaka ni wasikutane kabisa milele.

TANO: Kulinda heshima na utukufu wa watoto, kwani kikawaida watoto hujihisi unyonge pale wajuapo kuwa wazee wao walikuwa vimada kabla, kama ambavyo hilo litapelekea kuingia tabia hiyo kwao wao na hivyo kueneza uchafu wa zinaa katika jamii.

SITA: kuhalalisha ndoa hizi kunapelekea kuenea kwa uchafu wa kuwazini wanawake kwa hoja ya kuwadanganya kuwa watawaoa, na hili lipo wazi kuliko jua LA mchana, mabinti wangapi wameharibiwa kwa kuambiwa wataolewa kisha wakaachwa na mizigo ya malezi ya watoto wa nje hata imekuwa kila mtoto ana baba yake… Wallahu l mustaan. Bora mlango huu ufungwe na ajue kila binti kuwa akiziniwa na ndoa hakuna… Ili ajistiri na asidanganywe na mbwa mwitu.

SABA: Kuchanganyika kwa mirathi, nasabu, na haki, kwani wengi katika wazinifu huficha mimba walizozipata katika uzinifu wao, kwa kuoana haraka.. Na hili lina athari mbaya ya dhulma katika haki mbali mbali. Bali linapelekea kutokea kwa ndoa za haram baadaye.

NANE: Kuchanganyika kwa watoto wa wengine kwa baba huyo. Kwani inajulikana kuwa mwanamke mzinifu au mwanamme mzinifu sio wa mtu mmoja, basi nini kijulishacho kuwa watoto wote ni wake, utaona watu wanaishi kwa wasiwasi.

TISA: kuwepo kwa Qauli ya Allah mtukufu yenye kuharamisha ndoa hizo aliposema:
(الزَّانِي لَا يَنْكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنْكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ)
(Kikawaida) Mzinifu mwanamme hapendi kuoa ispokuwa mzinifu au mshirikina, na mzinifu mwanamke hapendi kuolewa ispokuwa na mzinifu au mshirikina, NA NDOA HIYO IMEHARAMISHWA KWA WAUMINI”
[Surat An-Nur 3]

KUMI: Pia imeharamishwa na Allah mtukufu katika Kauli yake:
(…. ۚ فَانْكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ… )
“Waoeni kwa idhni ya watu wao, na wapeni mahari yao kwa wema, wanawake waliojihifadhi sio Malaya wala waliofanywa vimada (Uhawara)…
[Surat An-Nisa’ 25]
Basi tuambiane tangu lini mtu anayemjua mwenziwe kuwa ni mzinifu amekuwa aliyejihifadhi???

KUMI NA MOJA:
Kuchukua hukmu yenye salama katika masuala, kwani ikiwa wataoana ambao hawajaziniana ummah mzima wanasema ndoa imetimia, amma akimuoa aliyekwisha mzini basi atakauwa ameingia katika Khilaf za wanachuoni, na kutoka katika khilafu ni bora kuliko kuingia.

KUMI NA MBILI:
Wanachuoni wameweka Kanuni mashuhuri ya kuwa MWENYE KUHARAKISHA JAMBO KABLA YA WAKATI WAKE ANAHUKUMIWA KUNYIMWA KWAKE.

Na mwenye kuharakisha kulamba asali kabla hajaruhusiwa kuilamba anaharamishiwa bila shaka. Kwa mujibu wa kanuni hii.

KUMI NA TATU: IJMAA YA MASAHABA
Wamekubaliana Masahaba kuwa ndoa hiyo ni haramu, kupitia hukmu ya Sayyidna Omar pale wakipoletwa waliooana katika EDA ya mwanamke, akawaachanisha kisha akasema: Ikiwa amemuingilia basi itakuwa haram kukutana kwao tena milele na ikiwa hajamuingilia ataruhusiwa kumuoa baada ya eda”
Na bila shaka hapa Sababu ya kutooana tena milele ni Zinaa, kwani kumuoa ndani ya EDA, ndoa haitimii na kwa hivyo inakuwa ni Zina. Ndio akasema: law angemuingilia angemharamikia milele.
kaipokea Imam Malik Amesema Albaaji naye ni mwananchuon wa kimaaliki kuwa hiyo ilikuwa ni Ijmaa ya masahaba kwa sababu haikupokewa kuwa yupo aliyepinga.

KUMI NA NNE:
Kuthibiti kwa riwaya za wazi kutoka kwa baadhi ya masahaba zikipandishwa mpaka kwa Mtume -sallallahu alayhinwasallam- kukataza ndoa hii, kutoka kwa Bii Aisha, na Sahaba Albaraa bin Aazib, na wengineo kuwa wamesema kuhusu wazinifu wawili watakao oana “Wao watakuwa wanaendeleza zinaa muda wote wakiwa pamoja” Amesema Sheikh Alqutb Allah amrehem katika kitabu Sharh Niil : “Hizi ni riwaya zinazonyanyuliwa mpaka kwa mtume -Sallallahu alayhi wasallam- kwani haya ni katika mambo yisyoongelewa kwa rai”
Na riwaya nyingine inasema kuwa wamesema: [- Mwanamke na mwanamme waliozini wakataka kuoana- wekeni baina yao bahari ya kijani – ili wasikutane milele-“

KUMI NA TANO:
MAKUBALIANO YA MADHEHEBU YA IBADHI.

wamekubaliana wanachuoni wote wa madhehebu ya Ibadhi kuwa ndoa hiyo ni batili, na katika lisilo na shaka ni kuwa Maimam wa Kiibadhi wa mwanzo walikuwepo kabla ya wanachuoni wengine wote, kwani Imam wao wa kwanza Imam Jabir bin Zeid kazaliwa mwaka 18 au 21 hijri katika zama za Ukhalifa wa Sayyid Umar bin Alkhattab. Wakati Imam wa mwanzo wa madhehebu za kishia na kisunni wamezaliwa mwaka 80h. Au kabla ya hapo kwa kidogo.
Kwa hivyo Ijmaa ya wanachuoni wa kiibadhi imezitangulia khilaf za wanachuoni wengine. Na hivyo yenyewe ni yenye kutangulizwa.

Haya ni kwa alivotuwezesha Allah mtukufu kunukuu kwa haraka, bila ya kurejea na bila shaka kwa kurejea kuna dalili zaidi ya hizo, tunamuimba atulipe katika kupatia na atughufurie tulipokosea. Na kwa ufupi zaidi waweza kurejea risala aloiandika Sheikh wangu Hafidh Alsawwafi -Allah mtukufu amhifadhi- juu ya ndoa kama hii, nayo IPO katika website yetu [ibadhi.com] sehemu ya vitabu, kwa lugha ya kiswahili.
Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis Yahya Alghammawi

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Bakari Omary from

Tanzania

————————————–

Swali:

Je inajafaa kumuoa mwanamke ulliye zini nae..? Na ipi hukumu yake…?

JAWABU:
Waalykum salaam warahmatullah wabarakatuh.
NDOA HIYO NI HARAMU kwa sababu:

KWANZA: inajulikanwa kuwa ndoa ni fungamano tukufu linalojengwa katika kuaminiana ili kupata upendo na huruma kwa wanandoa. Na bila shaka baina ya waliokwisha kuzini inakosekana kuaminiana baina ya hawa watu wawili kwa kila mmoja kuijua khiyana ya mwingine, kama ambavyo anakosa amani ya kwamba mwenzie hatomkhini huko alipo.

Pili: Zinaa ni kuivunja heshima ya mwanamke na familia yake kwa ujumla, na mvunjifu wa heshima hatakiwi kupewa zawadi Bali kupewa adabu ya uvunjifu wake wa heshima, na kwa ajili hiyo uislam umeweka mijeledi mia moja ikiwa hajaoa au kuolewa, amma ikiwa ameoa au kuolewa kabla basi adabu yake ni kupigwa mawe mpaka afe ili akome yeye na wengine kuchezea heshima za watu, ajabu ya zama hizi ni kuwa mzinifua badala ya kupewa adabu anapewa mke kwa ndoa za mkeka au kwa njia nyingine, yaani kwa ufupi anapongezwa hadharani kwa kuvunja heshima na anapewa zawadi. Subhaanallah… Basi kuna udhalili kuliko huo?

TATU: Mtu akifanya madhambi yatakiwa ajistiri, aombe touba sio kuhalalisha madhambi yake, kama wafanyavyo wazinifu, na uislam umeharamisha mtu kumuuliza mwanamke kwa vipi imeondoka bikira yake? Bali hata akilazimishwa kusema uislam unamtaka mwanamke atafute lolote la kusema lakini asiseme yaliyopita kama aliingia katika uchafu wa zinaa, kwani akikiri tu kuwa alizini ndoa itakuwa imevunjika, na kwa utaratibu huu khofu ya kusema ataolewa na nani haipo aslani, kama ambavyo Allah mtukufu ndio mpangaji wa riziki.

NNE: Ikiwa wanandoa watalaaniana kwa kutuhumiana kuzini basi ndoa itakuwa imekufa hapo hapo kwa makubaliano ya waislam wote, basi ikiwa kutuhumiana zina tu kunaharibu vipi itakuwa hukmu ya waliozini kabisa?? Bila shaka ni wasikutane kabisa milele.

TANO: Kulinda heshima na utukufu wa watoto, kwani kikawaida watoto hujihisi unyonge pale wajuapo kuwa wazee wao walikuwa vimada kabla, kama ambavyo hilo litapelekea kuingia tabia hiyo kwao wao na hivyo kueneza uchafu wa zinaa katika jamii.

SITA: kuhalalisha ndoa hizi kunapelekea kuenea kwa uchafu wa kuwazini wanawake kwa hoja ya kuwadanganya kuwa watawaoa, na hili lipo wazi kuliko jua LA mchana, mabinti wangapi wameharibiwa kwa kuambiwa wataolewa kisha wakaachwa na mizigo ya malezi ya watoto wa nje hata imekuwa kila mtoto ana baba yake… Wallahu l mustaan. Bora mlango huu ufungwe na ajue kila binti kuwa akiziniwa na ndoa hakuna… Ili ajistiri na asidanganywe na mbwa mwitu.

SABA: Kuchanganyika kwa mirathi, nasabu, na haki, kwani wengi katika wazinifu huficha mimba walizozipata katika uzinifu wao, kwa kuoana haraka.. Na hili lina athari mbaya ya dhulma katika haki mbali mbali. Bali linapelekea kutokea kwa ndoa za haram baadaye.

NANE: Kuchanganyika kwa watoto wa wengine kwa baba huyo. Kwani inajulikana kuwa mwanamke mzinifu au mwanamme mzinifu sio wa mtu mmoja, basi nini kijulishacho kuwa watoto wote ni wake, utaona watu wanaishi kwa wasiwasi.

TISA: kuwepo kwa Qauli ya Allah mtukufu yenye kuharamisha ndoa hizo aliposema:
(الزَّانِي لَا يَنْكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنْكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ)
(Kikawaida) Mzinifu mwanamme hapendi kuoa ispokuwa mzinifu au mshirikina, na mzinifu mwanamke hapendi kuolewa ispokuwa na mzinifu au mshirikina, NA NDOA HIYO IMEHARAMISHWA KWA WAUMINI”
[Surat An-Nur 3]

KUMI: Pia imeharamishwa na Allah mtukufu katika Kauli yake:
(…. ۚ فَانْكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ… )
“Waoeni kwa idhni ya watu wao, na wapeni mahari yao kwa wema, wanawake waliojihifadhi sio Malaya wala waliofanywa vimada (Uhawara)…
[Surat An-Nisa’ 25]
Basi tuambiane tangu lini mtu anayemjua mwenziwe kuwa ni mzinifu amekuwa aliyejihifadhi???

KUMI NA MOJA:
Kuchukua hukmu yenye salama katika masuala, kwani ikiwa wataoana ambao hawajaziniana ummah mzima wanasema ndoa imetimia, amma akimuoa aliyekwisha mzini basi atakauwa ameingia katika Khilaf za wanachuoni, na kutoka katika khilafu ni bora kuliko kuingia.

KUMI NA MBILI:
Wanachuoni wameweka Kanuni mashuhuri ya kuwa MWENYE KUHARAKISHA JAMBO KABLA YA WAKATI WAKE ANAHUKUMIWA KUNYIMWA KWAKE.

Na mwenye kuharakisha kulamba asali kabla hajaruhusiwa kuilamba anaharamishiwa bila shaka. Kwa mujibu wa kanuni hii.

KUMI NA TATU: IJMAA YA MASAHABA
Wamekubaliana Masahaba kuwa ndoa hiyo ni haramu, kupitia hukmu ya Sayyidna Omar pale wakipoletwa waliooana katika EDA ya mwanamke, akawaachanisha kisha akasema: Ikiwa amemuingilia basi itakuwa haram kukutana kwao tena milele na ikiwa hajamuingilia ataruhusiwa kumuoa baada ya eda”
Na bila shaka hapa Sababu ya kutooana tena milele ni Zinaa, kwani kumuoa ndani ya EDA, ndoa haitimii na kwa hivyo inakuwa ni Zina. Ndio akasema: law angemuingilia angemharamikia milele.
kaipokea Imam Malik Amesema Albaaji naye ni mwananchuon wa kimaaliki kuwa hiyo ilikuwa ni Ijmaa ya masahaba kwa sababu haikupokewa kuwa yupo aliyepinga.

KUMI NA NNE:
Kuthibiti kwa riwaya za wazi kutoka kwa baadhi ya masahaba zikipandishwa mpaka kwa Mtume -sallallahu alayhinwasallam- kukataza ndoa hii, kutoka kwa Bii Aisha, na Sahaba Albaraa bin Aazib, na wengineo kuwa wamesema kuhusu wazinifu wawili watakao oana “Wao watakuwa wanaendeleza zinaa muda wote wakiwa pamoja” Amesema Sheikh Alqutb Allah amrehem katika kitabu Sharh Niil : “Hizi ni riwaya zinazonyanyuliwa mpaka kwa mtume -Sallallahu alayhi wasallam- kwani haya ni katika mambo yisyoongelewa kwa rai”
Na riwaya nyingine inasema kuwa wamesema: [- Mwanamke na mwanamme waliozini wakataka kuoana- wekeni baina yao bahari ya kijani – ili wasikutane milele-“

KUMI NA TANO:
MAKUBALIANO YA MADHEHEBU YA IBADHI.

wamekubaliana wanachuoni wote wa madhehebu ya Ibadhi kuwa ndoa hiyo ni batili, na katika lisilo na shaka ni kuwa Maimam wa Kiibadhi wa mwanzo walikuwepo kabla ya wanachuoni wengine wote, kwani Imam wao wa kwanza Imam Jabir bin Zeid kazaliwa mwaka 18 au 21 hijri katika zama za Ukhalifa wa Sayyid Umar bin Alkhattab. Wakati Imam wa mwanzo wa madhehebu za kishia na kisunni wamezaliwa mwaka 80h. Au kabla ya hapo kwa kidogo.
Kwa hivyo Ijmaa ya wanachuoni wa kiibadhi imezitangulia khilaf za wanachuoni wengine. Na hivyo yenyewe ni yenye kutangulizwa.

Haya ni kwa alivotuwezesha Allah mtukufu kunukuu kwa haraka, bila ya kurejea na bila shaka kwa kurejea kuna dalili zaidi ya hizo, tunamuomba Allah mtukufu atulipe katika kupatia na atughufurie tulipokosea. Na kwa ufupi zaidi waweza kurejea risala aloiandika Sheikh wangu Hafidh Alsawwafi -Allah mtukufu amhifadhi- juu ya ndoa kama hii, nayo IPO katika website yetu [ibadhi.com] sehemu ya vitabu, kwa lugha ya kiswahili.
Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis Yahya Alghammawi

Published By Said Al Habsy

Assalaam aykum warahmatullah wabarakaatuh

kuna ndugu yetu ni mfanyabiashara ilikua biashara yake ikienda vizuri ila katika miaka mitatu iliopita amepata misukosuko ya kuchukuliwa pesa kwa njia za kimazingara (uchawi) na hadi sasa amekuwa na deni kubwa ambalo hawezi hata kulilipa anaomba asaidiwe atumie njia gani ili asalimike na hasadi, hiyo na aweze kurudisha biashara na pesa za watu?

Yaani nakusudia dua zipi anatakiwa afanyiwe ili kama kuna anaemchukulia hiyo pesa aache?

JAWABU:
Waalaykm salaam warahmatullah wabarakatuh.

1. Kithirisha Istighfaar sana na kuomba touba kwa Allah mtukufu isije kuwa ni adhabu kutoka kwa Allah mtukufu kutokana na baadhi ya makosa aliyonayo mja.

2. Jilazimishe kusoma Adhkaar za asubuhi na jioni. Kisha kumuomba Allah mtukufu baada yake akufungukie kheri za siku hiyo na akukinge na shari zake.

Alamnasharaha ×7
Qulhuwallahu ×7
Suuratulfalaq ×7
Suuratunnas ×7
Aayatulkursiyy ×7

Bila kusahau adhkaar za baada ya sala. Hasa Aayatulkursiyy, Qulhuwallah, Suratulfalaq na Suratunnas Mara moja moja ispokuwa Magharb na Alfajri inakuwa Mara tatu tatu, na Subhaanallah wabihamdihi ×100

Pia soma au weka recording ya Suratilbaqara daima katika sehem yako ya kuwekea pesa kwani Suratil baqara huwafukuza masheitani. Kama ilivyokuja katika hadithi.

Wallahu aalam.

Ameyaandika
Khamis Alghammawi

Published By Said Al Habsy

You have a new Question by:

Nurudn Saidi from

Tanzania

————————————–

Swali:

Ugumu wa maisha unatokana na nini?

JAWABU:
Waalaykum salaam warahmatullah wabarakatuh.

Ugumu wa maisha unatokana na kuacha mfumo wa maisha alouchagua Allah mtukufu kwa viumbe wake, na kufuata mifumo inayotokana na akili finyu za mwanadamu.

Mifumo ya kijamaa ukomunisti na ubepari ambayo imetungwa na wanadamu imeshindwa kumletea mwanadamu furaha aloitarajia.

Ukomunisti ni zao LA kushindwa kwa Ubepari, Ujamaa ni marekebisho ya Ukomunisti.
Ubepari ni zao LA kushindwa kwa Mafunzo ya kanisa katika karne ya 18 kuleta furaha kwa mwanadamu.

Kwa hiyo mifumo yote iliyotawala na inayotawala ulimwengu Leo hii imeshindwa na umebaki mfumo mmoja tu. Nao ni mfumo wa Allah mtukufu.

Mfumo huo sio katika baadhi ya mambo na kuacha mengine, Bali inatakiwa ufanyiwe kazi mfumo huo katika kila kitu ili uje na matunda yaliyotarajiwa.
Uislam ulivyokuwa umetamalaki uliweka mfano bora wa ubinadamu ambao haujawahi kutokea mpaka Leo.
Anasema Allah mtukufu:
(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)
Allah mtukufu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakafanya mema, atawatawalisha katika ardhi kama alivyowatawalisha waliopita kabla yao, na atawasimamishia dini yao [mfumo wa maisha] alouridhia kwao wao, na atawabadilishia khofu yao kuwa ni amani, wakiniabudu mimi hawanishirikishi na chochote, watakaokufuru baada ya hapo hao ndio waovu.
[Surat An-Nur 55]

Kwa hivyo inatakiwa ziwepo jitihada za Makusudi za kusimamisha dini ya Allah mtukufu katika ardhi, kisiasa, kiuchumi, kifikra, kitamduni, lugha, na mengineyo.

Hayo hayatimii ispokuwa ni kwa jamii kwanza kuwa na ilmu na yaqini juu ya uislam wao, wausimamshe katika nafsi na familia zao, kila mmoja awe ni Quran inayotembea, kila mmoja aone haja ya kuutaka uislam usimamie maisha yake na hata kama si wote lakini inatosha nusu ya waislamu kuwa na hisia hizo katika eneo miongoni mwa maeneo au nchi miongoni kwa nchi ili waweze kusimamisha uislam kama itakiwavyo.

Inapokuwa hakuna utayari huo kwa wengi, au utayari ukawepo bila ya ilmu ya kutosha inakuwa ni vurugu kama tunavyozishuhudia katika baadhi ya makundi.
Na hapo mambo huzidi ugumu na kuharibika kwa kuitumia dini katika Yale yasiyokubaliwa na dini kama kuuwa hovyo, n.k.

Tunamuomba Allah mtukufu atuandikie kuona uislam,waislam na mfumo wao ukisimamia furaha ya mwanadamu.
Wallahu aalam.

Ameyaandka
Khamis Alghammawi

Published By Said Al Habsy

JAWABU KUHUSU RIWAYA ZA KISHIA ZINAZOJULISHA KUBADILISHWA KWA QURAN – BOFYA HAPA

Published By Said Al Habsy

KUMUOA MTOTO WA BINAMU KWA MAMA MKUBWA.
 
Asalam Aleykum..
Napenda kuuliza inajuzu kumuowa mtoto wa binamu yako kwa mama mkubwa.
Naomba nijibiwe
 
Shukran
Aziz Hamed Al Hatmi
 
JAWABU:
Waalykum salaam warahmatullah wabarakatuh.
Naam inajuzu, Maadam hakuna kingine chochote kizuiacho kama kunyonya pamoja n.k.
Wallahu aalam.
 
Khamis Alghammawy
2 Rabiul awwal 1440h.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

SUALI:

Tunaomba muusikilize Ujumbe huu wa sauti kisha mutujibu suali hili, jee! hamuoni kushirikiana na Mawahabi ni kudhalilisha Maibadhi?

JAWABU:

Ujumbe wa sauti tumeusikiliza nao umedhamini tuhuma kwa viongozi wa Istiqamah na baadhi ya Masheikh wetu waliopo Oman ambao walihudhuria katika hafla ya Mashindani ya Quraani yaliyofanyika jijini Dar-Ess-Salaam chini ya Uongozi wa Al-Hikma Foundation katika Ramadhani ya mwaka jana (1439), na uwepo wa mchango wa Maibadhi wa kifedha katika harakati za Mawahabi Tanzania.

Kwanza: Sisi hatumjui ni nani muhusika wa ujumbe huo, alikua ajitaje jina lake; kwa sababu ujumbe umedhamini lawama ambazo kikawaida hata Mawahabi wa Tanzania wanaweza kuziunda na kuzieneza katika Jamii kwa lego kuwapiga vita vya kinafsi Maibadhi, vita ambavyo lengo lake ni kudhoofisha mahusiano mazuri kati ya Maibadhi na Maduati wao, hususan wale ambao wameonekana katika shughuli za mashindani ya Quraani.

Inafaa ifahamike kuwa Mawahabi wanajulikana kuwa wanatukufirisha na kututoa nje ya Uislamu, nao ni watu wenye misimamo mikali inayofikia hata kushutumiana wao kwa wao, na Mawahabi hao kamwe hawawezi kukubali ushiriki wa Maibadhi katika shughuli zao husasan za Kidini, kwa hiyo sio kila msunni ni muwahabi.

Ama upande wetu Ibadhi kwanza hatuwatoi Mawahabi nje ya duara la Uislamu hata kama tunawaona kuwa wamo katika upofu na upotevu wa kiitikadi, inajulikana kuwa Imamu mkubwa wa kiwahabi -katika zama hizi- Ibnu Baaz alitoa fatwa ya kukufurisha Maibadhi na kuharamisha kusali yuma ya Ibadhi na kuoana na Maibadhi, basi Sheikh wetu Imam Al-Allaamah Ahmaed bin Hamed Al-Khalili -Allah amuhifadhi- alipomjibu aliulizwa. Jee! Inafaa kwetu sisi kusali nyuma yao? Akajibu: “Sisi hatufanyi kama alivofanya yeye akitangulia katika kusalisha tunasali nyuma yake……”

Ndugu yangu hiyo ndiyo Ibadhi, sisi tunakwenda kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu na si kwa mujibu wa kulipizana kisasi, Madhehebu yetu yanajenga jamii, kamwe hayavunji wala hayasambaratishi jamii, Madhehebu yetu inatutaka tuwe waadilifu, tujiepushe na aina zote za kudhulumu, Madhehebu yetu imetutaka tujifunge vizuri na Quraani na tujiepushe na mapendwa moyo na hasadi na dhana mbaya na uadui.

Pili: Maibadhi walifika Afrika Mashariki mapema sana, pia walifika tena kwa kuwatokomeza walowezi wa Kinasara wa Kireno na kuondosha madhila ya walowezi hao kwa ndugu zetu wa Kiislamu walioishi katika mwambao wa Afrika, hayo yalikua  katika kipindi cha Imam Seif bin Sultan Al-Yaarubi -Allah amridhie- katika Karne ya 12 Hijiria 17 Miladi, na Maibadhi waliweza kuishi pamoja na Waislamu wenzao kwa mashirikiano, na heshima kubwa sana, na mapenzi, bila kujali tafauti zao za Kimadhehebu, wala za urangi, wala za ukabila, hawakukubali kabisa kuzifanya tafauti hizo ziwe kichochezi na kuni za uhasama wa kuibomoa jamii, kwa hiyo mahusiano kati ya Waislamu wa Madhehebu ya Ibadhi na Waislamu wa Madhehebu nyengine katika Afrika Mashariki ni ya zamani sana, wala si aibu, bali ni neema ya kujivunia, Allah aidumishe.

Kwa itkadi yetu Maibadhi tunasema sisi sote -Ibadhi na Sunni- Uislamu umetukusanya hata kama zipo fatauti kati yetu, basi wajibu wetu ni kushirikiana katika tuliyokubaliana na kuheshimiana katika tuliyotafautiana.

Sisi tunatoa Shukurani kwa Al-Hikma Foundation chini ya Uongozi wa Sheikh Kishk kwa kutuletea mwaliko wa kuhudhuria hafala ya Khitimisho la Mashindani ya kuhifaadhi Quraani tukufu ya mwaka 1439/2018, na kwa mapokezi yao mazuri sana ya kupigiwa mfano Allah awajaze kila la kheri.

Na Allah ni shahidi kuwa kipindi chote cha kuwepo kwetu katika Jiji la Dar-Ess-Salaam tulikua bega kwa bega na ndugu zetu wa Kiibadhi ambao nao -kwa taufiqi ya Allah- waliweza kushirikiana na sisi katika kuendeleza daawa, kwa kweli tunatoa shukurani kubwa kwao pia, na sisi tulihudhuria katika mashindani ya Quraani tukufu ya Kitaifa ambayo Istiqamah waliyafanya hapo hapo Dar-Ess-Salaam.

Ama masuala ya kusaidia katika milango ya kheri hayo yanaihusu jumuia husika ile inayotoa misaada na misingi yake katika hilo, na sisi si wasemaji wa Jumuia yoyote.

Allah azikubali amali njema na asamehe katika mapungufu na kuteleza.

Tunawambia tu: “Wa karibu wana haki zaidi katika kutendewa wema.”

Wallaahu aalamu.