Home HABARI ZA WAKATI

HABARI ZA WAKATI

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

1. SIKU YA IDDI KUBWA (AL-ADH-HAA).
Assalamu alaykum wa rahmatullahi wabarakatuh.

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad pamoja na Aali zake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Ndugu zangu, tunachukuwa fursa hii kwa kuwapongeza waislamu wote kwa kufikiwa na siku ya Iddi ya Udh-hiyah, nayo ni Iddi kubwa miongoni mwa Iddi mbili za Kiislamu.

Iddi hii inakuwa katika siku ya kumi ya mwezi wa 12 wa kalenda ya Kiislamu, kwa hakika ni furaha kubwa, nayo ni siku kuu ya kutiiwa Allah mtukufu ndani yake na sio kuasiwa.

Ni siku ya kuunganisha ndugu na jamaa na marafiki.

Ni siku ya kufurahi na kumshukuru Allah mtukufu na sio kumkufuru kwa maasi.

Ni siku ya kuchinja kwa mwenye uwezo.

Ni siku ya kutoa sadaka kwa mafakiri, mayatima na wasiojiweza.

Ni siku ya kulisha wasikini na kuwatosheleza ndani yake.

Ni siku ya kumtaja Allah mtukufu kwa wingi.

Kuchinja ni sunna yenye thawabu nyingi sana kwa mwenye uwezo, basi achinje kichinjwa cha Udh-hiyah katika siku hii tukufu, kwa hakika umekuja katika athari tofauti, kuwa mwenye kuchinja katika siku hii basi huandikiwa kwa kila unyoya wa kichinjwa chake jema moja na kuwekwa katika mizani ya mema yake mja huyo.

Inatakiwa kuchinja kwa nia ya uchamungu; kwani Allah mtukufu hataki damu za vichinjwa vyetu wala nyama za vichinjwa vyetu, anachokitaka Allah mtukufu ni uchamungu wetu, basi isiwe kuchinja kwa nia ya kujifakharisha wala kuonekana wala nia nyengine yoyote, bali iwe kwa nia ya kujipamba kwa Uchamungu kwa kushukuru neema alizojaalia Allah mtukufu kwa waja wake.

Mtume wetu (s.a.w) ametuambia kuwa yule atakayechinja kabla ya kusali sala ya Iddi basi kichinjwa chake hicho ni nyama ya kula tu, na yule ambaye atachinja baada ya sala ya Iddi basi huyo imetimia ibada yake ya kuchinja Udh-hiyah na amepatia sunna ya Waislamu, basi tujuwe ndugu zangu, kuwa wakati wa kuchinja ni baada ya sala ta Iddi, kutokana na hapa ni sunna kusaliwa sala ya Iddi ya Udh-hiyah mapema.

Ndugu zangu, tujuwe kuwa aina ya vichinjwa vya siku hii ni mbuzi, kondoo, n`gombe, na ngamia, na kwa mujibu wa wanaelimu wetu ni kuwa umri wa vichinjwa hivi usipunguwe miaka miwili na kuendela, isipokuwa kondoo hakuna tatizo kwa aliyetimiza mwaka mmoja na kuendela, pia Muislamu ajiepushe na kichinjwa chenye aibu kama ya upofu, au kuvunjika, au kukatika sikio au jino, au ulemavu, na mfano wake hayo, na aibu yenye kuzingatiwa ni ile aibu inayompunguzia mnyama wa kuchinja thamani yake.

Mwenye kuchinja anagawa kichinjwa chake sehemu tatu, mbili katika hizo ni za kula yeye na familia yake na moja katika hizo anatoa sadaka kwa wengine.

Na zile za kula yeye na famili yake sehemu moja ni kwa ajili ya siku zinazokuja kwa hiyo inatakiwa kuikausha kama ilivyokuja katika Sunna ya Mtume wetu (s.a.w).

Allah atukubalie mema yetu na atusamehe madhambi yetu.

Tunawatakia barka za Iddi.

Ndugu yenu/Hafidh H. Seif Al-Sawafi.

Asanten sana.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

1. SIKU YA IDDI KUBWA (AL-ADH-HAA).
Assalamu alaykum wa rahmatullahi wabarakatuh.

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad pamoja na Aali zake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Ndugu zangu, tunachukuwa fursa hii kwa kuwapongeza waislamu wote kwa kufikiwa na siku ya Iddi ya Udh-hiyah, nayo ni Iddi kubwa miongoni mwa Iddi mbili za Kiislamu.

Iddi hii inakuwa katika siku ya kumi ya mwezi wa 12 wa kalenda ya Kiislamu, kwa hakika ni furaha kubwa, nayo ni siku kuu ya kutiiwa Allah mtukufu ndani yake na sio kuasiwa.

Ni siku ya kuunganisha ndugu na jamaa na marafiki.

Ni siku ya kufurahi na kumshukuru Allah mtukufu na sio kumkufuru kwa maasi.

Ni siku ya kuchinja kwa mwenye uwezo.

Ni siku ya kutoa sadaka kwa mafakiri, mayatima na wasiojiweza.

Ni siku ya kulisha wasikini na kuwatosheleza ndani yake.

Ni siku ya kumtaja Allah mtukufu kwa wingi.

Kuchinja ni sunna yenye thawabu nyingi sana kwa mwenye uwezo, basi achinje kichinjwa cha Udh-hiyah katika siku hii tukufu, kwa hakika umekuja katika athari tofauti, kuwa mwenye kuchinja katika siku hii basi huandikiwa kwa kila unyoya wa kichinjwa chake jema moja na kuwekwa katika mizani ya mema yake mja huyo.

Inatakiwa kuchinja kwa nia ya uchamungu; kwani Allah mtukufu hataki damu za vichinjwa vyetu wala nyama za vichinjwa vyetu, anachokitaka Allah mtukufu ni uchamungu wetu, basi isiwe kuchinja kwa nia ya kujifakharisha wala kuonekana wala nia nyengine yoyote, bali iwe kwa nia ya kujipamba kwa Uchamungu kwa kushukuru neema alizojaalia Allah mtukufu kwa waja wake.

Mtume wetu (s.a.w) ametuambia kuwa yule atakayechinja kabla ya kusali sala ya Iddi basi kichinjwa chake hicho ni nyama ya kula tu, na yule ambaye atachinja baada ya sala ya Iddi basi huyo imetimia ibada yake ya kuchinja Udh-hiyah na amepatia sunna ya Waislamu, basi tujuwe ndugu zangu, kuwa wakati wa kuchinja ni baada ya sala ta Iddi, kutokana na hapa ni sunna kusaliwa sala ya Iddi ya Udh-hiyah mapema.

Ndugu zangu, tujuwe kuwa aina ya vichinjwa vya siku hii ni mbuzi, kondoo, n`gombe, na ngamia, na kwa mujibu wa wanaelimu wetu ni kuwa umri wa vichinjwa hivi usipunguwe miaka miwili na kuendela, isipokuwa kondoo hakuna tatizo kwa aliyetimiza mwaka mmoja na kuendela, pia Muislamu ajiepushe na kichinjwa chenye aibu kama ya upofu, au kuvunjika, au kukatika sikio au jino, au ulemavu, na mfano wake hayo, na aibu yenye kuzingatiwa ni ile aibu inayompunguzia mnyama wa kuchinja thamani yake.

Mwenye kuchinja anagawa kichinjwa chake sehemu tatu, mbili katika hizo ni za kula yeye na familia yake na moja katika hizo anatoa sadaka kwa wengine.

Na zile za kula yeye na famili yake sehemu moja ni kwa ajili ya siku zinazokuja kwa hiyo inatakiwa kuikausha kama ilivyokuja katika Sunna ya Mtume wetu (s.a.w).

Allah atukubalie mema yetu na atusamehe madhambi yetu.

Tunawatakia barka za Iddi.

Ndugu yenu/Hafidh H. Seif Al-Sawafi.

Asanten sana.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

2. PONGEZI ZA MWAKA MPYA WA 1437 HJ.
بِسْمِ اللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Assalamu alaykum wa rahmatullahi wabarakatuh.

Shukurani zote ziwe kwa Allah mtukufu aliyejaalia wakati kuwa chombo cha matendo, na rehma na amani ziwe kwa kipenzi chetu Mtume wetu Muhammad pamoja na kila aliyeongoka na atayeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Kwa hakika Allah mtukufu -kwa wingi wa fadhila zake na neema zake- amejaalia kuwepo kwa nyakati ambazo ni alama kubwa ya uwezo wake Allah mtukufu na kuwa yeye ndiye muumbaji wa haki na muendeshaji wa mamalaka yake kikamilifu, basi ukapatikana usiku na mchana, jua na mwezi, mabadiliko ya miongo ya mwaka, kiangazi masika kipupwe na vuli, basi zikapatikana wiki, miezi, na mwaka, nazo zote ni sababu kuu ya kujuwa hesabu na kudhibiti mambo, kwa hakika katika haya kuna dalili za wazi kwa wenye kufikiri.

Anatuambia Allah mtukufu:

((Hakika idadi ya miezi kwa Allah mtukufu ni kumi na mbili katika Kitabu cha Allah siku alipoumba mbingu na ardhiو miongoni mwayo ni minne mitukufu, basi hiyo ndiyo dini iliyosawa kabisa, musije mukazidhulumu ndani yake nafsi zenu..)) [Tawba 36]

Pia anatuambia Allah mtukufu:

((Na tumejaalia usiku na mchana kuwa ni dalili mbili, basi tukaifuta dalili ya usiku na tukaijaalia dalili ya mchana kuwa ni yenye kuona ili mutafute fadhila zitokazo kwa Mola wenu na ili mujuwe idadi na miaka na hesabu, na kila kitu tumekipambanua umapambanuo)) [Israa 12]

Kwa hiyo ni wajibu wetu kumshukuru Allah mtukufu kwa kutujaalia kuuanza mwaka mpya wa 1437 tokea kuhamia Mtume wetu Muhammad (s.a.w) katika Mji wa Madina uliopo katika Ardhi ya Hijazi, ni wajibu wa kila muislamu akumbuke wajibu wake katika maisha haya, kuwa kuwepo kwake ni kwa kumuabudu Allah mtukufu kwa kutekeleza maarisho yake na kuepuka makatazo yake, na kuwa umri wake ndicho chambo cha matendo yake ambayo malipo yake atayakutia huko Akhera tunakokwenda sote, mja siku hiyo atajuta kwa nini hakuujaza wakati wake wa faragha kwa yaliyo ya kheri, na kwa nini wakati wake mwengine aliujaza maasi na maovu, na atafurahia wakati wake uliojaa mema ya kuridhiwa na Mola wake mtuku.

Anatuambia Allah mtukufu:

((Na kitawekwa Kitabu, basi utawaona waovu wamefazaika kwa yaliyomo ndani yake, na watasema: Kina nini Kitabu hichi? Hakikuacha dogo wala kubwa isipokuwa kimelidhibiti!!. Na watakutia waliyoyafanya yamehudhuria na hatomdhulumu Mola wako yoyote)) [Kahf 49].

Mtume wetu Muhammad (s.a.w) aliulizwa: Hivi ni nani mbora wa watu? Akajibu: ((Ni yule uliyerefuka umri wake na yakawa mazuri matendo yake)) Kisha akaulizwa: Ni nani muovu wa watu? Akajibu: ((Ni yule uliyerefuka umri wake na yakawa mabaya matendo yake)). [Tirmidhi 2330]

Basi ndugu yangu kumbuka neema ya umri kwa kuwa mwaka huu mpya ambao Allah mtukufu amekujaalia kuufika ni moja ya neema za Allah mtukufu kwako, na kuwa haki yake ni kuujaza yaliyokuwa ya kheri, basi ujaalie umri wako katika malengo ya kuumbwa kwako.

Anatuambia Allah mtukufu:

((Na sikuwaumba majini na watu isipokuwa kwa kuniabudi mimi)) [Tuur 56]

Basi boresha umri wako kwa mema na kutubia kwa uliyokosea na kuteleza katika siku zilizopita.

Mara moja Mtume wetu Muhammad (s.a.w) alimuambia mmoja wa Masahaba wake huku akimnasihi kwa mawaidha:

«اِغْتَنِمْ خَمْسًا قَبْلَ خَمْسٍ: شَبَابَكَ قَبْلَ هَرَمِكَ، وَصِحَّتَكَ قَبْلَ سَقَمِكَ، وَغِنَاكَ قَبْلَ فَقْرِكَ وَفَرَاغَكَ قَبْلَ شُغْلِكَ، وَحَيَاتَكَ قَبْلَ مَوْتِكَ»

((Faidika kwa fursa ya matano kabla ya matano:

Ujana wako kabla ya uzee wako.
Afya yako kabla ya kugonjwa kwako.
Utajiri wako kabla ya ufakiri wako.
Faragha yako kabla ya kushughuishwa kwako.
Uhai wako kabla ya kufa kwao)). [Rabii 896].
Wasiozinduka huhasirika ndani ya neema hizo tano kwa kumilikiwa na matamanio ya nafsi zao ambazo zimeingia katika dira ya shetani aliyelaaniwa kwa sababu ya kumsahau Mola wao Mtukufu.

Basi tusiwe miongoni mwa hao na tuzinduke kwa hizo tano ni neema za Allah mtukufu basi yule aliyemo katika neema yoyote miongoni mwa hizo awemo katika kuitumia neema hiyo katika anayoyaridhia Allah mtukufu kwa waja wake ili aweze kufaidika nayo.

Kwa haya machache www.ibadhi.com inawatakia wasomaji wake na waislamu na watu wote kwa ujumla mwaka wa 1437 wenye kila mafanikio na kheri na baraka.

Asanteni sana

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

3. MDAHALO BAINA YA IBADHI NA AHMADIYAH (QADIYANIYAH)
Asalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh.

Tunamshukuru Allah mtukufu na kumtakia rehma na amani kipenzi chetu Mtume wetu Muhammad pamoja na Aali zake na Masahaba wake na kila aliyemo katika uongofu wake mpaka siku ya mwisho.

Kwa hakika kuelekeana haki na batili ni moja ya sunna za huu ulimwengu, na katika hilo Allah mtukufu huwafanyia mitihani waja wake, na bila ya shaka kundi la Mdaiunabii Mirza Ahmed Ghulaam Al Qadiyanii linalojiita (Jamaatu Ahmadiyah Isalaamiyah) ni moja ya makundi potofu na lilitopea katika batili, na kiuhakika hilo ni kundi linalojipachika jina la Uislamu hali ya kuwa Uislamu uko mbali na kundi hilo kama ilivyo mbali damu ya Mtume Youssuf (a.s) na kanzu yake, basi kama ndugu wa Mtume Youssuf walivyodai kuwa damu ya uongo waliyoitosa katika kanzu ya Mtume Youssuf (a.s) ni damu yake Mtume huyo, ndivyo hivo hivo kundi hilo linavyodai kuwa wao ndio Waislamu sahihi, hali ya kuwa uhakika wao unawafedhehesha kuwa huo wanaojibandika nao ni Uislamu wa uongo.

Amesema Allah mtukufu kwenye Kitabu chake:

((Na nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah uongo au akasema: “Nimepewa Wahayi” hali ya kuwa hajafunuliwa wahayi wa chochote, na mwenye kusema nitateremsha mfano wa aliyoteremsha Allah…))

Al-Anaam 93.

Basi hiyo ndiyo hali ya huyo Mdaiunabii Mirzaa Ahmed Ghulaam Al-Qadiyani (l.a), na -bila ya shaka yoyote- wenye kumfuata Mdaiunabii huyo hao ni wenye kuongozwa na yeye kuelekea katika makasiriko ya Allah mtukufu na katika Moto wa Jahannam.

Basi hivi karibuni amejitokeza mmoja wa watetezi wa kundi hilo la Kishirkina linalojiita Ahamadiyah naye ni mtetezi wao mkubwa katika Afirika ya Mashariki atayeitwa Bakri Abeid Kaluta -Allah mtukufu amuongoe- na kuja kutaka mdahalo baina yake na Wanahaki Maibadhi katika mada:

Jee!! Unabii umekwisha au unaendelea?

Na kwa taufiqi ya Allah mtukufu amejitokeza hodari wa uwanja huu na kuwa tayari kukabiliana kimdahalo naye ni Sheikh wetu Juma Mohamed Rashid Al-Mazrui Al-Zinjibari (h.a), na mdahalo huo umenza na bado unaendelea nao umejengeka kinidhamu katika hatua nne muhimu.

Hatua ya kwanza nayo ni hatua ya kupeana hoja, katika hatua hii kila mmoja baina ya Al-Mazrui na Kaluta anatoa hoja za kutetea usahihi wa anayoitakidi, na wa mwanzo kuanza ni Kaluta.
Hatua ya pili ni hatua ya kujibizana, katika hatua hii kila mmoja kati ya wanamdahalo wawili anabainisha ubatilifu wa hoja za upande mwengine, na wa mwanzo kuanza ni Al-Mazrui.
Hatua ya tatu ni hatua ya kuulizana, katika hatua hii kila mmoja kati ya wanamdahalo wawili atamuuliza mwengine masuali matano, na wa mwanzo kuanza ni Kaluta.
Hatua ya nne ni hatua ya kuulizwa wanamdahalo, katika hatua hii kila mmoja kati ya wanamdahalo wawili ataulizwa na wafuatiliaji wa mdahalo masuali matano.
Mdahalo huu wote ni kwa njia ya sauti na kwa kutumia huduma ya WhatsApp kwa njia ya simu, nao unafanyika katika mjumuiko wa Faidika na Mawaidha, basi anayetaka kufuatilia yanayojiri anaweza kutuma ombi lake kupitia no +968 99420700

Na www.ibadhi.com itaweka -kwa njia ya maandishi- jawabu za matetezi ya kundi hili yaliyowasilishwa na mtetezi wao Ndugu Kaluta -Allah mtukufu amuongoe- kupitia mjadala wake huu, na jawabu hizo zitaanza kuwekwa wiki ijayo kwa idhini ya Allah mtukufu.

Asanateni sana.

Published By Said Al Habsy

4. HONGERA YA IDDI – 1438 HIJIRIA
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu aliyetuneemesha kwa nuru ya Imani na Uislamu na kutujaalia kutimiza funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, na rehma na amani ziwe kwa kipenzi chetu aliyeteuliwa kuwa khitimisho la Manabii Mtume wetu Muhammad pamoja na Aali zake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Assalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.
Tunachukua fursa hii adhimu ya kufanikisha utekelezaji wa Ibada ya funga ya Ramadhani ya mwaka huu 1438 Hijiria kwa kuwapongeza Waislamu wote Duniani kwa mnasaba wa Iddi Al-Fitri iliyobarikiwa, na kumuomba Allah mtukufu atukubalie funga yetu na ya kila muislamu na atujaalie taufiki yake katika anayoyaridhia hadi mwisho wa uhai.

Ndugu Waislamu:
Tunajua kuwa Ibada ya funga ya Ramadhani ni moja kati ya nguzo tano za Uislamu nayo ni nguzo ya nne aliyoijaalia Allah mtukufu kuwa ni kituo cha kuitekeleza kila mwaka mara moja, tusisahau kuwa lengo kuu ya ibada hii ni kuhakikisha uchamungu katika maisha ya Muislamu aliye Muumini wa kweli, na uchamungu huu ndio daraja inayohakikisha mafanikio ya kupata maridhio ya Allah mtukufu hapa Duniani na kesho Akhera, basi tusikubali kuharibu sifa hii baada ya kumaliza mfunguo wa Ramadhani, na tujue kuwa uchamungu unapatikana kwa kujiepusha na kila asiloliridhia Allah mtukufu kwa lengo la kupata maridhio yake Allah mtukufu, na kujiepusha huko hakupatikani isipokuwa kwa kutenda malazimisho ya Allah mtukufu na kuepuka makatazo yake Allah mtukufu, basi tusibatilishe malipo ya funga yetu katika siku za Iddi na zinazofuata kwa kujitosa katika maasi, kwani tukifanya hivo tutamfurahisha sana adui yetu Ibilisi mlaaniwa.
Tujue kuwa siku ya Iddi ni siku ya furaha na kula na kunywa vya halali na katika maridhio ya Allah mtukufu, wala si siku ya kujitosa katika makasiriko yake na michezo ya upuuzi na ubadhirifu wa mali na malaji na wakati, Allah atujiepushe nayo, basi imesemwa kuwa alama ya kukubaliwa funga ya mja ni kujishika kwake na uchamungu baada ya kumaliza Ibada hii tukufu.

Ndugu Waislamu:
Kwa hakika Mtume wetu Muhammad S.A.W. amesema:

((مَنْ صَامَ رَمَضَانَ ثُمَّ أَتْبَعَهُ بِسِتَّةِ أَيَّامٍ مِنْ شَوَّالٍ فَكَأَنَّمَا صَامَ الدَّهْرَ كُلَّهُ))

“Yule atakayefunga Ramadhani kisha akaifuatiliza kwa funga ya siku sita katika Shawwali (Mfunguo mosi) basi huyo ni kama aliyefunga mwaka nzima.”

[Rabii 312]

Basi tujihimu katika kufunga siku sita za mwezi huu wa Shawwali, nao ni mwezi unaofuata baada ya Ramadhani, na tukumbuke kuwa hakuna ulazima wa kuzifuatisha wala kuzifunga mara tu baada ya Iddi, bali mwenye kutaka thawabu yake anatakiwa atimize funga ya siku sita za mwezi huu kabla ya kumalizika kwake, ni sawa ikiwa atazifunga kwa mfululizo au kwa kuachanisha muhimu azimalize kabla ya mwezi kumaliza, pia tujue kuwa siku ya Iddi imeharamishwa kuifunga kwa hiyo haimo katika siku hizo sita.

Ndugu Waislamu:
Tunafahamu sote machafuko yaliyotokezea katika miji mingi ya Waislamu kama vile Syria, Yemen, Somalia, Afgahanistani, Libya, Burma, Palestina n.k, pia tunadiriki vizuri tokeo la kukatika kwa mahusiano ya kimataifa baina ya Qatar na Nchi jirani za Kiarabu (Saudia, U.A.E., Baharain, Misri) hatuna budi kumuomba Allah mtukufu kuzirejesha nyoyo za Waislamu katika fungamano la Uislamu na Imani, pia aondoshe yenye kupelekea machafuko na uhasama katika jamii, basi Allah alete amani baina ya Waislamu na mapenzi na kuhurumiana na kuheshimiana katika waliyotafautiana, na kusaidiana katika wema na uchamungu, kwa hakika tafauti ni maumbile ya Binadamu, basi kuelewana na kuheshimiana ndio dawa yake, na sio uhasama na kugombana.
Allah aondoshe madhila ya vita na maradhi na hasadi na chuki baina ya Waislamu wote. Amin.

RISALA YETU YA IDDI:
Risala yetu kwa Umma wa Kiislamu ni ile aliyoisema Mstahiwa Sheikh Ahmed bin Hamed Al-Khalili Allah amuhifadhi:

“Hakika mimi -kwa jina la Uislamu ambao unakusanya wala hautawanyi, unaunganisha wala haukimbizi, unapoza wala haushongalishi- ninaliita kila kundi ambalo limo katika wimbi la kupigana vita na kuvutana lisimame kwa kujihesabu nafsi yake mwenyewe katika yale ambayo linayafanya, na lichunguze na kuzingatia ndani yake na lijiulize, kuna maslaha ya nani? Na kwa aajili ya nani linajiingiza katika mvitano na kujiangamiza na kudhoofisha Umma?!! Roho ngapi zimetolewa? Nguvu kiasi gani zinapotea? na Mali nyingi kiasi gani zinateketea?.

Kwa hakika linalolazimika kwa wote ni kujiondosha katika marithisho ya thakafa zao za mifarakano, basi waondoshe katika marejeo yao kila lenye uchochezi wa kasumba za kijahilia au kujigamba kibaguzi, na wote wawe ni ndugu kwa ajili ya Allah mtukufu, na wenye kusaidiana katika yenye kheri, na warekebishe kila pengo linalotenganisha baina yao kwa kuwatenga na nuru ya Uislamu inayokusanya, basi wawe tayari kuzima kila fitna inayokokea ukiritimba ili kuzizima kwa maji ya mamiminiko ya mapenzi kwa ajili ya Allah mtukufu ambaye nyoyo za waja wake inalazimika kuimarishwa kwa mapenzi yake.
Ama ikiwa mivutano ni kwa sababu za tafauti za kimadhehebu; kwa hakika sababu hiyo ima itakuwa chimbuko lake ni fahamu pofu ya kupatikana madhehebu tafauti katika safu za Waislamu, au itakuwa imesababishwa na kasumba za kimadhehebu, basi inawalazimu wajue kuwa hizi Madhehebu -iwapo wafuasi wake watakuwa na Ikhlasi kwa ajili ya Allah mtukufu- zinakua ni sababu ya kuimarika na si kidamirika, na kufahamiana sio kufarikiana, kwa sababu kutafautiana katika matawi ni neema na rehma na hazina ya umma isiyokadiriwa kwa thamani, kwani mara ngapi Muislamu anapata katika jitihada za ndugu zake Waislamu katika Madhehebu tafauti yale yenye kutuliza moyo wake na kutatua utata wake na kumfungulia tatizo lake, na hakuna jitihada yoyote iliyopo katika asili ya kisheria isipokua jitihada hiyo inayo kiwango fulani cha haki na kufikisha katika kuijua haki.”

Ndugu Waislamu:

Mpaka hapa tunawatakia Waislamu wote kheri za Iddi na fadhila za funga na taufiqi ya Allah katika kila lenye maridhio yake Allah mtukufu.
Wakullu Aaamin Wantum Bikhairin

Ndugu yenu: Abu Hamed Hafidh Al-Sawafi.

Kwa niaba ya www.ibadhi.com.

HAKI KWA DALILI.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

5.UJUMBE WA IDDI AL-ADH-HAA 1438
Bismillahi wal-hamdu lillahi wa salaatu wa salaamu ala rasulillahi Muhammad wa alaa aalihi wa sahabihi wa sallama.

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Tukiwa katika siku tukufu ya Arafa nayo ni siku ya tisa ya mwezi wa mwisho wa mwaka ambao ni mwezi 12 kwa mujibu wa kalenda ya kiislamu, siku hii ambayo ni sunna kutekeleza ibada ya funga ndani yake kwa asiyekuwemo katika ibada ya Hijja, ibada ambayo Mtume wetu Muhammad S.A.W. ametueleza kuwa ni kafara ya mwaka unaomaliza na mwaka unaofuata, Allah atukubalie funga yake na atukubalie ibada zetu zote na atusamehe tuliyoteleza. Kwa kumaliza siku hii inafuata siku ya Iddi kubwa nayo ni Iddi Al-Adh-haa.

Inatupasa tujue kuwa furaha ya Iddi sio mlango wa kuvamia aliyo haramisha Allah mtukufu na Mtume wake, wala sio siku ya kuvutia katika maasi ya Allah mtukufu, bali siku hii ni siku ya kufurahia katika aliyohalalisha Allah mtukufu pia ni siku ya kuunganisha udugu na kuwaliwaza wagonjwa na manyonge na masikini, ni siku za kula na kunywa na kutoa sadaka.

Mtume wetu Muhammad S.A.W. ametuagiza katika Ibada tukufu ya siku ya Iddi nayo ni Ibada ya kuchinja kwa kusema: “Kuleni na wekeni na mutoe sadaka” kwa hakika hiyo ni ishara kubwa kwa waislamu katika yale yaliyokua muhimu zaidi katika siku hizi ya Iddi, basi ewe Muislamu usikubali kumfurahisha Ibilisi maluuni kwa kuitika vichochezi vyake vya maasi ya Allah mtukufu.

Tukumbuke kuwa Iddi hii ime katika mwezi wa mwisho wa mwaka kwa mujibu wa kalenda yetu ya Kiislamu, basi inatupasa tuienzi kalenda hii kwa kuijua na kuwafundisha watoto wetu miezi yake, kwani kalenda hii ndiyo aliyoiridhia Mola wetu mtukufu katika Dunia yetu na Dini yetu, ni aibu kubwa leo kumkuta mtoto wa Kiislamu anajua miezi yote 12 ya kalenda ya Kizungu lakini ukimwambia akutajie miezi ya kalenda la Kiislamu inakua ni mtihani mkubwa kwake, turejee katika kalenda ya Dini yetu tuwafundishe watoto wake, tufanye jitihada kuiweka katika maisha yetu ya kila siku.

Kumalizika kwa mwaka kutukumbushe kumalizika umri wetu na umri wa Dunia, kwani kama ilivokua tunakaribia katika kifo pia tunakaribia katika Kiama siku ya Malipo. Basi ni wakati wa kujihesabu na kuzirejea nafsi zetu kwa ajili ya kuhakikisha yaliyo bora zaidi ambayo Mola wetu Allah mtukufu anayaridhia kwetu kwa siku zetu zote.

Tunachukua fursa hii kuwapongeza Waislamu wote duniani kwa kuadhimisha siku ya Iddi tukufu ya Al-Adh-haa, na kuwatakia mwisho wa mwaka huu ulio mwema na mwanzo wa mwaka unaofuata wenye kila mafanikio.

Tunawapongeza Mahujaji kwa kufanikiwa kutekeleza Ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano ya Uislamu na tunamuomba Allah awakubalie amali zao.

Tunawaombea dua ya mafanikio wale wote walioma katika mitihani ya kujaribiwa kwa dhulma ikiwa kwa kuwemo vizuizini bila ya haki au vita vilivoripuka katika miji yao na kuteketeza mali na roho na nchi, au mateso ya kudhulumiwa bila ya haki. Allah awalipe hao wote malipo ya yao bila ya hesabu, na awaondoshee madhila na awafariji kwa amani upendo na huruma.

Amina.

Asanteni sana.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

In the name of Allah most gracious most merciful, all praise be to Allah the Lord of the Heavens and earth and peace and blessings be upon our beloved messenger Muhammad PBUH. It is with no doubt a difficult moment for all Muslims around the world.

·         I have mixed feelings about the shooting in New Zealand and every other shooting whether it is in a mosque, temple, church or synagogue where terrorism is expressed in different forms and innocent people are being killed.

·         My first message goes out to the shooter:

 

1.       We welcomed you in our mosque with smiles and peace and you paid us back by bullets and hate.

2.       There is no doubt that what you have done is an act of terrorism despite the justifications out there for what you did, as terrorism has no religion, race or nationality.

3.       The level of hate that you have expressed towards the innocent worshippers clearly indicates the lack of mercy in your heart.

4.       I just fail to understand why would you think that Muslims are a threat to you or your community, while your community has proven you wrong and stood by the Muslims after this horrific tragedy.

5.       If you think that Muslims will retaliate or revenge, then you are mistaken as our faith teaches us to forgive and love.

6.       Do you think that you have achieved your goal by doing this?

7.       This incident will not stop us from worshiping the Creator and for sure it won’t stop us from going to our mosques.

8.       Killing a few Muslims will not eliminate Islam for sure.

9.       You have actually done a favor to all of us, as more people are educating themselves about Islam after this incident.

10.   Despite what you did, we don’t really hate you but we surely hate what you did.

11.   The only competition that you should be in, is the competition towards goodness in this life.

12.   You can never bring back those who departed and it’s hard for people to forgive and forget but never forget that God almighty is all forgiving and you still have the chance to make a difference.

13.   There is no bravery in killing innocent people who cannot defend them themselves.

14.   But true bravery is to admit your mistakes and do the right thing.

15.   You brutally shot every one of them while they are total strangers to you and they have never harmed you in any way or form.

16.   You wanted to be popular by committing this crime on live stream but guess what, you forgot about the 1.8 billion Muslims around the world that you really hurt.

17.   Hate is a disease and can only be cured by love and true faith.

18.   The biggest crime in humanity is to kill innocent people in the name of God, while God is innocent of such atrocities.

19.   If you can’t stop hate and terrorism around the world, then at least do not be part of it and stain your hands with the blood of the innocent.

20.   Take the opportunity in prison to study more about Islam and you will surely realize that you have been eluded by islamophobia and media propaganda.

21.   The masses out there are so frustrated and angry with you, as you don’t have the right to represent them with this act or even claim that you did what you did for their liberty.

22.   If the justice system is merciful on you then never forget that on the day of judgment, God’s decree and punishment is for eternity.

23.   Prophet Muhammad PBUH forgave those who killed his loved ones and even those who tried to kill him, and we will for sure follow his footsteps and forgive you and open our arms for you.

24.   My final advice to you is that, it’s never too late to repent and ask forgiveness from God, the families of the victims and the rest of the world as long as you still have pulse in you.

 

·         To the victims of this horrific tragedy:

1.       We envy you for this great honor of being martyrs.

2.       You will surely be missed by all of us and we promise you to continue worshiping Allah no matter what happens inn shaa Allah.

3.       Our brothers and sisters from all faiths have mourned and grieved your loose.

4.       They were so brave to the extent that they formed human shields around mosques to protect the worshippers from any other attack and to assure them that it is still safe to worship God.

5.       Thousands of people around the world have sent you rosses of love and wrote emotional letters to pass their condolences.

6.       Your lives didn’t parish for nothing, it is the wisdom of God that goodness sometimes comes out of evil.

7.       Tones of people are visiting mosques after this horrific incident and they are eager to learn more about this amazing religion Islam.

8.       May Almighty Allah bless you, and may He reunite us with all of you in Heaven. Ameen

 

·         To the mainstream media:

1.       In such incidents you really come to understand the true colors of some of the mainstream media.

2.       Media agencies are expected to have values and be unbiased to any incident that happens, but unfortunately it is not the case here.

3.       When non-Muslims are killed by terrorism, then that becomes the main focus of the media everywhere in the world, but when Muslims are being slaughtered in a brutal way then it’s just one of those unfortunate events which will be highlighted modestly.

4.       Thank God that we have social media which is more powerful today than any other agency out there.

5.       Media is trying so hard to propagate that Islam is the enemy and that terrorism is a monopoly to Muslims, but day by day the opposite is proven with Muslims being the majority victims in most cases.

6.       It’s a relief to see all the empathy messages on social media from around the world, which shows the love and solidarity of people.

7.       It hurts me more to see the absence of the Muslim media agencies in covering such tragedies as if those who were lost are not so important.

8.       Before I blame the shooter, I would blame main stream media for creating this hate in the world and eluding the public that Islam is the enemy and it’s going to take over Europe.

9.       I am just wondering if the shooter was a Muslim would your reaction be as cold as it is today.

 

·         People of all faiths:

1.       Thank you for your love and support.

2.       Thank you for setting the best example in mercy and solidarity.

3.       Thank you for caring and proving to the world that whatever they do to us they can never break our unity.

4.       Thank you for proving to us that the conscious of this world is still alive and that there is still hope in humanity.

5.       We have a common enemy which is terrorism and if we stick together we will surely defeat it.

6.       Our pain and loose is your pain and loose.

7.       It doesn’t make a difference if a mosque has been attacked or any other house of worship.

8.       The time has come for us to accept our differences and be on the same team.

9.       We shouldn’t be driven by what the media tells us.

10.   We can only prosper if we coexist.

11.   Never fear Islam and Muslims as we are normal people like you and we are only seeking to live a peaceful life.

12.   Our homes and mosques are all open for you and are welcoming people of all faiths.

13.   The mosque doesn’t belong to Muslims, it’s the house of God Almighty and we have no right to restrain anyone from coming to the house of God.

·         The rest of the Muslims:

1.       I know you are all angry, frustrated and your emotions are running high.

2.       But I also know that as believers you all know that this is the decree of Allah and we need to be patient.

3.       You have to understand that God turns every calamity into an opportunity.

4.       This opportunity showed us how much love is out there especially from our New Zealand and Canadian brothers and sisters.

5.       They have expressed the highest level of compassion to the victims, their families and the rest of the Muslims.

6.       We don’t need to go for marches or change our phone profiles or burn some flags to express our frustration as this isn’t the teaching of our beloved prophet PBUH.

7.       But we can surely be more kind and loving towards others and show them how Islam expresses peace even in difficult times.

8.       I urge you all not to curse the west or hold everyone responsible for the mistake of an insensible individual.

9.       Let us not forget those who opened up their lands for us when were prosecuted in our lands.

10.   Be good ambassadors of this faith and conduct yourself in the best morals and ethics.

11.   Never face hate with hate and violence with more violence.

12.   Remember that saving a single soul is as if you are saving the entire humanity.

13.   Follow the footsteps of our beloved prophet Muhammad PBUH and forgive those who have wronged us.

14.   Educate others about your faith and build a community that is based on tolerance and coexistence.

Zakat Calculator

Zakat ( Kiarabu: زكاة zakat , “Hiyo ipi humtakasa ” ) ni aina ya kupewa sadaka – kutoa and Religious kodi katika Uislamu, Ambayo, kwa

Read More »

DIBAJI

Assalaamu alaykum warahmatullahi taala wabarakaatuhu ndugu zangu, baada ya salamu rehma na amani zimfikie Bwana wetu mpenzi Nabii Muhammad na Swahaba zake watukufu na wote

Read More »

UTANGULIZI

  Zimekhitilafiana madhehebu za Kiislamu juu ya sifa na namna ya kuisali swala .. na khilafu kubwa iliyomo na yenye mjadala baina ya madhehebu hayo

Read More »