SWALI LA – (4)
Ni upi upeo wa athari ya zaka katika mujitamaa wa kiislamu?
JAWABU
Zaka huzalisha katika nafsi ya mtowaji urehemevu na upole kwa mafukara na maskini, na inasafisha moyo wake kutokana na ubakhili, na hiyo ndio maana ya kauli ya Allha:
《خذ من أموالهم صدقة تطهرهم وتزكيهم بها 》
《Chukuwa sadaqa (zaka) katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo》
Kwa hiyo inaitwaharisha nafsi na kuitakasa kutokana na athari za ubakhili, kwa maana inanawirisha tabia njema- pia ni kiitaji cha upole na urehemevu, na inatekeleza shida za maskini, na huzifanya nyoyo zao kuelekea kwa ndugu zao matajiri, na huondosha yaliomo katika moyo miongoni mwa chuki kwa wale ambao Allah amewapa neema ya mali.
والله أعلم.
——————————————————————–
{ Na wanao kusanya dhahabu na fedha (mali), wala hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu ilio chungu}
Imetaarishwa Na Kufikishwa Kwako na;
Thuweiniy Seif Al-Ismailiy.
