Home Introduction MLANGO WA KWANZA – 4.Salini kama mnavyoniona ninasali

MLANGO WA KWANZA – 4.Salini kama mnavyoniona ninasali

176
0

 

Nne:-

Amepokea Imam Ahmad na Albukhary kwa njia ya Malik bnul Huwayrith (r.a) kuwa Mjumbe wa allah rehma na amani ziwe juu yake amesema: ” Salini kama mnavyoniona ninasali”.

Na amri hii inatoka kwake Mjumbe wa Allah na ni ya wajib madamu hakuna dalili ya kuondosha uwajibu huo, na lau kama ingalikuwa kuinua na kufunga mikono ilikuwemo katika swala yake Bwana Mtume (s.a.w) bila shaka yangalikuwa mambo hayo ni wajibu, hivyo kwa nini wanaokubalisha jambo hilo wanasema (kuinua na kufunga mikono) ni sunna na wengine wanasema inapandelewa tu, jee ? Hii si dalili ya kuonyesha kutokusihi jambo hilo.

_____________________________________

[9] – (mujallad ya 2 juuzuu 4/95 chapa ya Daarul-fikriy 1981/1401- )

-Na akasema tena katika ukurasa huo huo : ( أجمعت الأمة على استحباب رفع اليدين عند تكبيرة الاحرام واختلفوا فيما سواها)

Tafsiri yake: “Umma umekubaliana katika kupendelea kuinua mikono wakati wa kupiga takbiratil-ihram na wakakhitilafiana kwenye takbira nyengine”.

 

Previous articleMLANGO WA KWANZA – 5.Dhehebu la kiibadhi ni tokea karne ya kwanza ya Hijria
Next articleMLANGO WA KWANZA – 3.Na simamisheni swala

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here