Home MADHEHEBU YA UISLAM YA MWANZO MADHEHEBU YA HAKI YA KIISLAMU

MADHEHEBU YA HAKI YA KIISLAMU

0
3175

 بسم الله الرحمن الرحيم

UTANGULIZI

Shukurani zote ni kwa Allah mwenye kuneemesha kila neema juu ya waje wake, na Rehma na Amani ziwe kwa Mjumbe wake Muhammad (s.a.w) na Aali zake na Sahaba wake na kila anayefuata njia ya uongofu wake mpaka siku ya malipo (Amin)

Ama baada ya hayo:

Assalamu alaykum wa Rahmatu Llahi wa barakatuh”

Ewe Allah tufungulie milango ya Maarifa ili tuone Haki na kuifuata, na kuigundua Baatil na kuihama, tueke katika Maridhawa yako popote pale yalipo, kwa hakika Taufiq inatoka kwako.

Mdugu yangu Muislamu:

Hakika baada ya kutembea katika utunzi wa Kiswahili katika medani ya Dini, sijaona kitabu kinachoelezea kwa undani uhakika wa IBADHI  katika Itikadi zao na Fiqhi yao, ingawa vipo vitabu vinavyotoa Ishara za Mbali katika uwanja huu, lakini ili kuweka karibu na kwa ufafanuzi zaidi kwa kila mwenye hamu ya kusoma, na ili kuupata Uhakika au kujiongezea maarifa, basi nimeona nijiingize katika Bahari hii yenye mawimbi makali, ili kila mmoja aweze kuyajua ukali wake, na mimi nikajihisi kua ni mwepesi baada ya kumuomba Allah katika kuikamilisha kazi hii, juu ya ugumu wake na uzito wake na nimeipa jina:

MADHEBU YA HAKI YA KIISLAMU IBADHI.

Uhakika wa utunzi huu:

Ndugu yangu msomaji; kazi hii imezamia zaidi katika Masuala yaliyojaa mizozano ya khilafu baina ya Ibadhi na wale walioko nje ya misimamo yao hiyo, basi kazi yetu humu ni kuonyesha na kukaribisha ufahamu wa Hoja za Madhehebu hii, ambayo wengi hawaijui uhakika wake, kutokana na kuharibiwa Sura yake ya Uhakika katika vitabu vinavyotegemewa katika Ulimwengu wa Kiislamu katika kuyajua Madhebu yoyote ya Kiislamu, basi kutokana na uharibifu huo, nimejiona niwe mbali na vitabu hivyo ambavyo havina uhakika wa kielimu katika Mada zake, na nikajiingiza katika Usomaji wa vitabu vya Maibadhi wenyewe, ili kujivulia uhakika wao wenyewe, ninayesema haya hali ya kua mimi mwenyewe nimekinaika na Madhehebu haya, na Baada ya kusoma na sio kuzaliwa nayo tu. Basi ndugu yangu nakutaka ujishikie kitabu hichi katika njia ya Uadilifu, wala usije ukajihukumia mwenyewe katika Watu wasiojua Uhakika wa Maibadhi, wala kutegemea nje ya yanayotegemewa na wao wenyewe, utajikuta uko nje ya Uhakika umbali wa Mashariki na Magharibi.

Wako wengi katika watoto wa Maibadhi, wameamua kuyaacha Madhehebu yao, ima kwa sababu zao binafsi zinazorejea -agh-labu zake- katika baadhi ya chuki zinazokaa baina yao na wengine, sababu hizo sio zenye maudhui kuihakika, na wako wengine wameyahama kutokana na kutojua uhakika wa Madhehebu yao, na wakanyakuliwa na yaliyopendwa na nafsi zao, wako wengine wameyahama kutokana na kusoma kwao, kwani wao walisoma masomo yao nje ya Madhehebu yao, kisha wakaridhika na masomo hayo, bila kuangalia yale yaliyokua ya Asili yao, na wako wengine wameweza kuvutwa na Baadhi ya misimamo ya watu fulani au maneno matamu yanayotoka katika vinywa vyao, na kuja kutahamaki haoni thamani ya kile alichonacho; Basi maandishi haya yanaingia zaidi katika kubainisha ukweli wa mambo yalivyo na kua hawa wamekosea kiuhakika na kua wanatakiwa -sio wao tu- bali kila mwenye kuitaka Haki,  wasiwe nje ya msingi huu usiokua na wasi wasi wowote ule, na wenye nguvu madhbuti sana za Hoja, na wenye kua mbali sana na kila Hoja ya Nguvu.

Ndugu yangu Muislamu;

Hakika ya maandiko haya nimeyaandika kwa mujibu wa Ufahamu wa dalili na pengine nikategemea katika maandiko ya Waandishi, katika hali ya pili ninaonyesha Msemaji wa maneno hayo na mwisho wa maneno yake ninaweka alama hii “, na sitaji kitabu chake isipokua kwa Nadra sana, nimefanya hivi kwa sababu nimeandika haya katika hali ya kuyakinai kua ndio haki inayotakiwa kufuatwa na Nafsi yangu kwanza, kwa hivyo ninayaweka wazi mbele ya wenzangu, ili iwe ni njia ya kuifikia Haki hiyo kama ilivyo upande wangu. Sisemi hivi kama mimi ni Muj-tahidi –hasha lilahi-, lakini naamini kua penye uwezekano wa mtu kupaona hoja inasimama kwa kuona mwenyewe, na pale palipokua nje ya uoni wake, anatakiwa awategemee wenye kuona kwa uoni wao. Basi namna hivi nikaweza kuyagawa maandiko haya katika sehemu mbili kubwa.

Tarekhe:-

Nimetoshelezeka kueleza sehemu hii kama vile ilivyoletwa na ufahamu wangu baada ya kujisomea vitabu tofauti katika Maudhui hii, na kutokana na hayo ikaweza kua ni Tarekhe ya kupatikana Maibadhi kwa njia Fupi kabisa, na kutokana na uoni huo wa Tarekhe nikatoa Utambulisho wa Maibadhi, sikujiingiza katika kuyaeleza malumbano yaliyopo katika Tarekhe kwa sababu ni mambo ambayo yameshapita zamani sana, wala sisi hatuendi ulizwa nini wao walifanya, lakini twenda ulizwa kuhusu yetu, kwa hivyo lengo hasa sio kujadili masuala hayo bali ni kuonyesha vipi Maibadhi walipatikana.

Na vile vile nimeweka Bayana ya kutofautisha baina ya Ibadhi na Khawarij, ili kuelezea udhaifu wa yanayotegemewa na wengi katika Fikra ya  kuwachanganya Ibadhi na Khawarij.

Ama kuhusu Tuliyoyaeleza katika matendo ya baadhi ya Masahaba, hatujakusudia kuawatusi, au kuwalaani, lakini lengo ni kubainisha tu kua kosa limefanyika sio kuondosha cheo cha aliyefanya hilo kosa katika wao, cheo chake hicho hakisababishi kua kila atakalolifanya likubalike, kwa sababu sura kama hizo hata wakati wa Mtume (s.a.w) zilipatikana, kwa mafano Swahaba wake Haatib bin Abi Balqaah (r.a) alifanya khiyana ya kuwaandikia Washirikina wa Makka kwa kuwahadharisha na kuvamiwa na Mtume (s.a.w), na hayo yakagunduliwa na Mtume (s.a.w) kwa njia ya Wahyi, na ikafedheheka Khiyana yake, hata ikapelekea Omar bin Khattab (r.a) kutaka Ruhsa ya Mtume (s.a.w) katika Kumuua Sahaba huyo, na kumtuhumu kwa Unafiki, lakini Mtume alimjibu hivi:

إنه قد شهد بدرا وما يدريك لعل الله اطلع من شهد بدرا فقال: اعملوا ما شئتم قد غفرت لكم

Hakika yeye ameshuhudia Badri, na kipi kinachokujuilisha; pengine Allah ameangalia walioshuhudia Badri na akasema: Fanyeni munavyotaka hakika nimeshasamehe kwenu” [Bukhari 3007. Muslim 2494]

Basi hatuoni kumtusi Sahaba katika Masahaba wa Mtume (s.a.w), lakini vile vile hatuoni kuficha Kosa lililofanyika baada ya kubainika, na hukumu yao baina yao na Allah ni baina yao.

Itikadi:-

Kwa sababu ni msingi muhimu katika dini iliyosalimika, na kua ndio njia kuu inayopeleka katika Matendo, na ndio njia Pekee ya kumjua Aliyeumba; basi nikaingia katika kuelezea mambo haya kwa undani, na kuyarejesha baadhi ya yanayo aminiwa na wengi katika Watu ikiwa yako nje ya Haki, basi nimeelezea vigao vya Watu na Dalili zake, kisha nikaingia katika Kumjua Muumba na Sifa zake, nikaingia katika Kutomuona Muumba, na katika Kuumbwa kwa Qur-ani, na Adhabu ya watenda wakubwa katika Maasi, nikaingia katika Shafaa ya Mtume (s.a.w), na pia nikaelezea kuhusu Mizani siku ya Kiama, na nikaingia kubainisha kukubaliwa kwa Mema na kuporomoka kwake, na pia nimeelezea mlango wa Toba, na mwisho nimeweka Mlango wa waliyoyasema Wanavyuoni wasiokua Maibadhi kuhusu Madhehebu hii ya Ibadhi, na nikamalizia kwa Utenzi unaomnasihi Ndugu aliyeacha Madhehebu, na pia nimeweka baadhi ya Masuala ya Kifiqhi yanayokamatana na Sala, ambayo yanababaisha wengi katika Waislamu.

Ndugu yangu Msomaji;

Unayoyasoma humu, huna ruh-sa kuyasema isipokua kama yalivyo, ama kujisemea vile utakavyo mwenyewe ujue kua mzigo wa hayo utakayoyasema utaubeba mwenyewe, ama ikiwa kama tulivyoyaandika basi hoja tulizotegemea tumezionyesha, unayo ruhsa ya kuzitegemea kama tulivyozitegemea, kwa sababu Dalili sio Milki ya Mtu fulani, kila mmoja ana Haki ya kuijua na kuifanyia kazi, na tutashukuru sana -na Allah ampe kila la Kheri- kila msomaji atakayetuletea maoni yake, katika jambo lolote lile, katika maandishi haya, au katika Maudhui hii, na sisi tutajitahidi iwezekanavyo kuyaangalia maoni yake hayo, kwa sababu hakuna Mkamilifu isipokua Allah peke yake, na juu ya kila mwenye Elimu kuna Mwenye Elimu.

Tahadhari:

Haukua utunzi huu katika lengo la kugombanisha Umma, lakini lengo lake kubwa ni kubainisha Haki kwa mujibu wa Dalili na Hoja, na mimi ninaamini kua kubainisha ni Haki ya kila mtu, kwa hivyo yaliyomo humu tuyachukue kwa njia ya kukinaishana, na sio kwa njia ya kulazimishana, kwa sababu Allah amemuambia Mtume wetu: Hakika wewe huwezi kumuongoa unayempenda lakini Allah ndiye anayemuongoa anayemtaka” basi yachukue haya kama ni mwangaza wa kujua ulichonacho, au kujua kile alichonacho mwengine, na wala haiwi kujua ndio kufuata, lakini kufuata ni hatua nyengine inayokuja baada ya kukinai kile ulichokijua, kwa hivyo soma ujue, kisha ukikinai utafuata, wala usijifungie Pazia, ukakataa kujua, utabakia katika kiza ambacho lau kua unakijua uhakika wake usingelikubali kubakia ndani yake, na yeyote yule atakaye yachukua maandiko haya kua ni sababu ya kugombanisha baina ya Waislamu, au kueneza Fitna, kwa sababu yamekwenda kinyume na yale aliyoyazoea, basi ajue kua Mzigo huo anauchukua mwenyewe, na kua hilo sio Lengo letu.

Shukurani:

Ninawatakia Kheri wale wote walioshirikiana na mimi katika kuitimiza Kazi hii, katika kuipitia, kuirejea, fikra, kuichapisha, na Mashauri, kwa hakika kusaidiana katika wema na uchamungu, ni Amri ya Allah na Mtume wetu Muhammad (s.a.w) basi awalipe Allah kila la kheri ya Dunia na Akhera (Amin).

Mtungaji ni Ndugu yenu:

TAREKHE  YA IBADHI

KWA UFUPI

Baada ya kufa Mtume (s.a.w) waislamu walikubaliana kua Abu Bakar (r.a) awe kiongozi wao kwa mujibu wa kitabu cha Allah na Mtume wake (s.a.w), na Abu Bakar aliongoza kwa uadilifu kwa makubaliano ya Waislamu wote, ilipokaribia ajali yake ya kuondoka Duniani alimpendekeza Omar bin Khattab (r.a) kwa Maswahaba wenzake ili awe kiongozi baada ya kufa kwake, na Waislamu hawakupinga jambo hilo, bali waliliunga mkono, na Omar bin Khattab (r.a) akawa ni kiongozi wa Waislamu baada ya Abu Bakar (r.a), na Abu Bakar (r.a) aliongoza kwa muda wa Miaka miwili (11-13H).

Omar bin Khattab (r.a) aliongoza kwa uadilifu mkubwa kwa makubaliano ya Waislamu wote, na ilipokaribia ajali yake Omar bin Khattab (r.a) alipigwa upanga na Mmajusi mmoja jina lake ni Abu Lu-lua (l.a), na khatimae aliondoka duniani kutokana na jeraha hilo la Upanga, katika hali ya kuumwa kwake Maswahaba walimtaka afanye kama alivyofanya Abu Bakar  kumchagua mmoja katika wao, lakini yeye baada ya kuangalia nani anafaa zaidi katika suala la utawala, akaona aliweke kua ni  Shuraa baina ya watu sita katika Maswahaba, nao ni Aliy bin Abi Taalib na Oth-man bin Afaan na Twalha bin Ubaidllah na Zubeir bin Awaam na Abdu-rahman bin Auf na Saad; na Abdullah bin Omar mtoto wake (r.a) akiwa ni mshauri wao katika hilo, kisha akawausia wasije wakakhitalifiana na ikitokezea kukhitalifiana basi wawe pamoja na Abdu-rahman bin Auf (r.a).

Omar bin Khattab (r.a) alikufa na uongozi ukamuangukia Oth-man Bin Affaan, na uongozi wa Omar bin Khattab (r.a) ulidumu kwa Miaka kumi (13-23H).

Oth-man aliongoza kiuadilifu kwa muda wa miaka sita kwa makubaliano ya Waislamu wote, kisha baada ya hapo mambo yakaanza kubadilika, kwani tayari uzee ulikua umeingia kwake na mapenzi mengi ya jamaa zake yalipekea kuharibu uadilifu katika kipindi kilichobakia, na kuinamia zaidi kwa jamaa zake katika Utawala na ugawaji wa mali ya Dola,  miongoni mwa hayo ni kule kumrejesha Hakam bin l-aasi na mtoto wake Mar-wani hali ya kua aliwafukuza Mtume (s.a.w) na kuwahamishia Taaif na kusema kua wasirudi tena katika mji wa Madina, lakini Oth-man aliwarudisha katika utawala wake na akamfanya Mar-wan kua ni Mshauri wake mkuu katika Nyumba ya uongozi Madina. Waislamu wakiwemo Maswahaba walifanya kazi kubwa sana ya kumkumbusha Oth-man, na Oth-man alikubali makosa na kutubia mbele ya Waislamu, lakini baadae hakuna linalofanyika na mambo yalizidi kua magumu na mabaya zaidi, ndipo mwisho Waislamu wakiwemo Maswahaba walipoitana na kutaka kufanya jihadi ya kusimamisha uadilifu katika utawala uliotoka nje ya Uadilifi wa Uislamu, kama alivyoamrisha Allah na Mtume wake (s.a.w), walimzunguka Oth-man katika nyumba ya utawala kwa muda usiopungua siku arobaini, wakimtaka Oth-man aache uongozi, lakini alikataa kata kata na ndipo walipomuua, na Maswahaba wapo na khabari wanazo, na lau kama hawakuridhia hayo wasingaliyaacha namna hiyo, bali wangalipigana na kuunusuru utawala wa Kiislamu, wao waliushinda ulimwengu katika vita vipi washindwe kumuhami kiongozi wao? Lakini alifanya makosa yaliyopelekea kuitana wao kwa wao kwa ajili ya kuondosha utawala ulitoka katika njia sahihi aliyoiacha Mtume (s.a.w) na Abu Bakar  na Omar bin Khattab (r.a). Oth-man aliuliwa na utawala ukamuangukia Aliy bin Abi twaalib (k.a.w) na utawala wa Oth-man ulidumu kwa miaka 12 (23-37H).

Aliy alishikilia utawala kwa nguvu za uadilifu, na alianza kubadilisha watawala wa miji ya mbali, ili kurejesha hali kama ilivyokua, lakini mambo yalibadilika yakawa ni magumu sana upande wake, kwa sababu ilianzishwa siasa ya kudai Damu ya Oth-man, na walioongoza siasa hii kwa mara ya kwanza ni Twalha bin Ubaidi llahi na Zubair bin L-awwam na Bibi Aisha (r.a), hawa waliita watu katika kuinusuru damu ya Oth-man kwa kulipiza kisasi, nao walikataa kumtii Aliy, lakini wamlitaka Aliy awe pamoja na wao katika suala lile, na Aliy alipinga siasa hiyo Baatil, na kuwahukumu kua wao ni kundi lilioasi, kwa kivyo ni kusimamishwa hoja za kuwataka watubie na warejee katika Amri ya Allah inayowataka kuwatii viongozi waadilifu, lakini jambo hilo lilishindikana na hapo ikawa hakuna dawa nyengine isipokua ni kuwapiga vita, basi walipigana katika vita vikali vinavyoitwa Vita vya Jamal. Twalha na Zubair waliuliwa na Bibi Aisha alichukuliwa, na yeye alikubali kua alikuwemo katika makosa, na alitubia, ilikua  kila  akikumbuka au kukumbushwa vita vile machozi yakimtoka kwa kulia na kutubia, vita hivyo alishinda Imam Aliy, lakini haikupita muda Mtwala wa Sham Muawiya bin Abi sufyaan akishirikiana na Amru bin L-assi walikuja na siasa ile ile ya kudai Damu ya Oth-man, nao walikusanya jeshi kubwa sana na wakaaza kuja zao Iraq, Imam Aliy aliwahukumu kwa hukumu ya Allah kama ilivyokua kwa waliopita kabla yao, nao walikataa hukumu hiyo ikabidi vita vianze, vita vilikua ni vikali sana, na kundi la Muawiya bin Abi Sufiyaan likaanza kushindwa, hapo waliona kua hakuna njia nyengine isipokua ni kusimamisha vita na kuingia katika njia nyengine ya kumvunja  adui yao, na fikra hiyo aliitoa Amru bin L-assi, basi walisimamisha misahafu ikiwa ni alama ya kusimamisha vita. Vita vilisimama na Aliy alipeleka wajumbe wake wa kuwataka warejee katika haki, nao wakaleta fikra ya kuchagua kila upande Msuluhishi, kisha hao wawili wakae pahala pamoja na wahukumu kwa mujibu wa Qur-ani, na kua vyovyote vile watakavyohukumu kila upande uridhike na hukumu hiyo, fikra hii ilipofika katika safu za Imam Aliy ilipelekea kugawika sehemu mbili; kundi moja ni la wale wasomi (Quraai), wao walipinga na kumtaka Imam Aliy aendelee na vita kama alivyoamrisha Allah ima vita au lirejee lile kundi lilioasi katika Amri ya Allah, na Muawiya bin Abi sufyaan na kundi lake ni kundi lilioasi kwa ubainisho wa Mtume (s.a.w) kwa sababu Mtume (s.a.w) alimuambia Ammar bin Yaasir: Ammar litakuua kundi lililoasi” na Ammar ameuliwa katika vita hivi akiwa upande wa Imam Aliy akilipiga vita kundi la Muawiya bin Abi Sufiyaan, kwa hivyo kundi la Muawiya bin Abi Sufiyaan ndio kundi lilioasi bila shaka yoyote ile, na hukumu yake ni kulipiga vita mpaka lirejee katika Amri ya Allah mtukufu ya kuacha Uasi wao na kua chini ya uongozi wa uadilifu, waliokua na fikra hii na kiuchukulia msimamo ni wasomi (Quraai), nao walikua ni kidogo ukilinganisha na wale waliokubali fikra za kusuluhisha, kwani wao walikua wengi, nao walimtaka Imam Aliy akubali kumtoa msuluhishi wa kwenda kusuluhisha na kuacha vita vinavyopelekea kumwagika damu nyingi ya Waislamu, na kwa sababu ya wingi wa kundi hili Imam Aliy alikubali rai yao na alimpeleka Abu Mussa L-ash-ary kua ni msuluhishi wa upande wao, na Muawiya bin Abi sufyaan bila kukawia alimpeleka Amru bin L-assi kua ni msuluhishi wa upande wake vile vile. Sulhu hiyo ililazimisha lile jina la uongozi wa dola ya Uislamu lifutwe kwa Imam Aliy kwa sababu watu wa Shaam walimkataa kama ni kiongozi wa Waislamu, kwani wao hawakutoa ahadi ya kumtii bado, na lau yeye ni kiongozi wa Waislamu wote, basi wasingalimpiga vita, kwani na wao ni Waislamu, ilipofika hatua hiyo ya kufanywa sulhu hiyo wale waliopinga jambo hilo, ambao ni sehemu ya jeshi na wasomi wa Imam Aliy waliamua kujitenga na kusema kua “hakuna Hukumu isipokua aliyohukumu Allah”  na kumtia makosani Imam Aliy kwa kuacha hukumu ya Allah na kufuata mapendwa moyo, basi wao walikwenda katika sehemu iliyoitwa Hairuraa, na khatima ya sulhu ambayo Imam Aliy alitoa ahadi ya kukubali matokeo yake ikawa ni kuachwa Umma bila kiongozi na kuondoshwa Imam Aliy katika uongozi, hali ya kua Muawiya bin Abi Sufiyaan ameshikilia uongozi wake wa Shaam, basi wale wa Hairuraa walichagua kiongozi kwa njia ya Shuraa kama alivyoamrisha Allah na uongozi huo ukamuangukia Abdullahi bin Wahabi Raasibiy na yeye alikua ni miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (s.a.w).

Imam Aliy aliwataka watu wa Hairuraa kurejea tena katika upande wake, lakini wao walikataa bali walimtaka Aliy aje katika utiifu wa Kiongozi mpya wa Waislamu, na hapo akashindwa la kufanya isipokua kwenda kumpiga vita Muawiya bin Abi sufyaan, lakini washauri wake walimshauri kwanza aende kwa hawa waliosimamisha uongozi katika misingi ya sheria, kabla ya kujiimarisha na kua kubwa Dola yao, naye Imam Aliy alikubali ushauri huo, alikwenda kuwapiga vita vikali sana, nao walipigana kwa kujitetea, lakini walizidiwa kwa uchache wao na wingi wa jeshi la Aliy, waliuliwa wengi wao akiwemo kiongozi wao Abdullahi bin Wahab Ar-asibiy katika vita hii ya kidhalimu, na wengine waliookoka walitawanyika ndani ya miji ya Iraq, miongoni mwao alikua ni Abu Bilal Mir-daas bin Hudair , na baada ya kumalizika vita Imam Aliy alijuta sana, na kubainika katika jeshi lake kua vita ile ilikua ni ya kidhalimu, walimuasi baadhi yao na kukimbilia katika safu za Muawiya bin Abi sufyaan, kisha zilifanywa njama za kumuuwa Imam Aliy, na ndio kama yalivyopangwa Imam Aliy aliuliwa kwa mkono wa Abdul-rahman bin Muljim na akabakia Muawiya bin Abi Sufiyaan peke yake katika safu ya kisiasa, na hapo aliendeleza utawala wake katika siasa mbaya sana ya kutisha na kuua kila anayepinga siasa hiyo, hali ikawa ni ya kutisha sana, hapo wale waliookoka katika vile vita vya Imam Aliy walifanya mwito katika haki kwa njia ya siri, nao waliongozwa na Abu Bilal Mir-daas bin Hudair,  hawa walipinga siasa ya dola ya Muawiya bin Abi sufyaan na waliotawala baada yake, nao walifanya kazi kubwa sana ya kuwafikishia watu haki kwa njia ya siri kabisa, nao walitungiwa kila jina baya lisilopedwa na watu ili kuharibu sura yao katika vichwa vya Raia kwa ujumla, lakini waliendelea na katika Jamaa hii alijiunga mwanachuoni mkubwa anayekubalika na wote naye ni Imam Jabir Bin Zaid Al-uzdy, na kutokana na Elimu yake kubwa iliyoshuhudiwa na Maswahaba, akawa yeye ndio marejeo ya wote, na akawa ndio kiongozi wa kielimu baina yao, kila siku zilivyoendelea ndio siasa ilivyokua mbaya zaidi, na dhulma iliongezeka vibaya sana, na usalama wa wapenda haki ulipungua, na maisha yao kua hatarini, katika hali hiyo aliamua Mir-daas bin Hudair  huihama Iraq na kwenda katika Ardhi isiyofika hukumu ya viongozi wale madhalimu, naye alifuatwa na baadhi ya wafuasi wake, kiasi wote walifikia idadi yao Arobaini, nao walitoka katika miji ya Iraq, lakini mara khabari za kuhama kwao zilifika kwa mtawala wa Iraq, naye aliamrisha jeshi la wapiganaji elfu mbili litoke mara moja liende kuwarudisha au kurudi na vichwa vyao, jeshi hili lilikutana na wale Arobaini, na ikabidi vifanyike vita vikali sana, nao Elfu mbili walishindwa na kuuliwa baadhi yao, na kukimbia wengine waliobaki, ilikua ni fedheha kubwa sana kwa utawala, na hamaki na ghadhabu zilipanda kwa mtawala wa Iraq, na hapo alitowa jeshi la watu elfu nne, na hawa elfu nne walipofika katika uwanja wa mapambano waliwadoelea wale waliobaki katika arubaini, wakati wamo katika sala ya Ijumaa baina ya kusujudu, hapo waliwavamia na kuwaua wote bila kutoka hata mmoja, bila ya mmoja wao kujua mavamizi yale kutokana na unyenyekevu waliokua nao katika Sala zao, ilikua ni mwaka 61H.

Khabari hizo zilopofika katika miji ya Iraq ziliwakasirisha sana wale wafuasi wake waliobaki katika miji ya Iraq, na kupandisha hamasa zao, na kuazimia kulipiza kisasi, huku mwanachuoni wao Imam Jabir Bin Zaid akiwatuliza na kuwarejesha katika njia ya uadilifu, na hayo yalipelekea kuleta mgawiko baina yao katika mwaka wa 64H, na kujitokeza makundi matatu yaliyoongozwa na viongozi wao watatu, na kumuacha Imam Jabir Bin Zaid na waliobakia, hayo makundi matatu yaliitwa kwa majina haya Najidiya lililoongozwa na Najdatu bin Aamir, Azariqah lililoongozwa na Naafii bin Azraq, na Suf-riya lililoongozwa na Abdullahi bin Saffaar, makundi haya matatu yakaamua kuingia katika vita vikali sana, kwani walikuja na hukumu mpya wasiyoijua Waislamu, na hukumu hiyo ni kua: kila anayemuasi Mwenyezi Mungu huyo ni Mshirikina, damu yake na mali yake ni halali, kwa hivyo ukikataa kwenda katika vita unakua ni Mshirikina, kwa sababu kuwapiga Washirikina ni lazima katika sheria ya Allah. Hawa kutokana na itikadi yao hii kali sana,  ilikua vita vyao ni vibaya sana, nao walifanikiwa kukamata baadhi ya Miji lakini watu wenye itikadi hii inaonekana wazi kua hawatoendelea, kwa sababu vita viliwamaliza hawakuvuuka miaka mingi isipokua hakuna aliebakia katika wao, na Hawa ndio Khawariji kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya Mtume (s.a.w) kwa sababu katika mafundisho hayo inabainika kwa uwazi, kua Khawariji watahukumu Waislamu kua ni Washirikina na hawa ndivyo walivyofanya. Ama wale waliobakia na Imam Jabir Bin Zaid, wao waliendelea katika msimamo sahihi, ule ule wa Abu Bilal Mir-daas bin Hudair, wa kujiimarisha kwanza kisha ndio kusimamisha Dola ya Kiislamu katika Uadilifu wa Uislamu, na hawa kwa sababu ya mgawiko uliotokea baina yao ililazimika kutangaza upotevu wa yale wakundi matatu, na kuidhihirisha Haki na upotevu walioufanya, lakini kutokana na siasa ilivyokua, ililazimika kazi hii aifanye mtu anayeweza kupata Himaya ya Kabila kubwa ndani ya Iraq, basi hakuwa mwengine isipokua ni kijana aliyejulikana kwa jina la Abdullahi bin Ibadh, na hapo ikapelekea kuitwa wale waliomo katika msimamo ule kua ni wafuasi wa Ibn Ibadhi, na ndio mwazo wa kuitwa Ibadhi, kwa hivyo hapa tunaweza kuwatambulisha maibadhi kwa kusema:

Maibadhi ni wale waliobakia katika mafundisho sahihi ndani ya Uislamu baada ya kuzuka  Fitna mapaka hivi leo”

MAIMAMU WA IBADHI

Imamu wao wa mwanzo baada ya kuzuka Fitna ni Imam Jabir Bin Zaid (r.a), na aliyedhihirisha misimamo yao ni Abdullahi bin Ibadhi na barua yake aliyomjibu mtawala mkuu wa wakati huo Abdulmalik bin Marwan katika mwaka wa 64H ni maarufu ndani Uislamu.

Imam Jabir Bin Zaid (r.a) alipokufa, aliacha Wanafunzi waliobobea katika Elimu, miongoni wao ni Yule aliyekamata hatamu zake za uongozi na kua ni Marejeo ya wote naye ni: Imam Abu Ubaidah Muslim bin Abi Karimah (r.a), na huyu alizaliwa mwaka 45H na alikufa mwaka 145H, kwa hivyo aliishi miaka 100, na yeye alikua na asili ya utumwa, kwa sababu baba yake alikua ni mtumwa katika Bani Tamim, na yeye alikua mweusi, lakini kwa wingi wa elimu yake na uchamungu wake na kua hakuna utukufu ndani ya Uislamu unaopimwa kwa mizani nyengine isipokua Uchamungu na Elimu, alikubalika kua ni kiongozi na marejeo ya wote, ama Imam Jabir Bin Zaid alizaliwa mwaka 21H katika ardhi ya Oman, na alikufa mwaka 93H huko Iraq katika mji wa Basra. Imam Abu Ubaidah, aliweza kupanga nidhamu madhubuti ya masomo na siasa kwa ujumla, na yeye ingawa aliishi Iraq lakini aliweza kusimamisha Dola za Uadilifu katika Ardhi ya Yemen katika mwaka 127H na Dola hiyo ilipata nguvu za ushidi mpaka ikashika miji ya Makka na Madina, Dola hii ilizidiwa kwa uchache wa jeshi lake na ukubwa wa eneo lake la Utawala, kwa hivyo ilipigwa vita na mabeberu wa Bani Umayyah, nao walishindwa mwanzo, lakini kila vita vikiendelea na Udhaifu wa dola changa ulizidi, na mwisho walishindwa na kuangushwa Dola hii iliyopigiwa mfano na waandishi wote kwa Uadilifu wake, ilianguka mwaka 132H, ilipoanguka Dola hiyo ilisimamishwa dola nyengine ya Uadilifu katika misingi ya msimamo huo huo ndani ya Ardhi ya Oman, katika mwaka 132H, na dola hiyo ilendelea, nayo ilipigwa vita na kushindwa na kuuliwa jeshi lake lote na Mabeberu wa Bani Abbaas, lakini bila kupita muda Dola ilirejeshwa tena katika Ardhi hiyo, na uadilifu ulirudi katika nidhamu ya Uislamu, na ndio uliotawala katika Ardhi ya Oman kuanzia karne ya pili mpaka mwaka 1373H Maimamu waliongozwa na Uislamu katika Ardhi ya Oman.

Dola nyengine ilisimamishwa katika Ardhi ya Afrika kaskazini katika nchi za Algeria, Libya na Tunis nayo ilijulikana kwa jina la Dola ya Warustum, nayo ni dola ya uadilifu, iliyodumu karibu karne moja na nusu, ilisimamishwa mwaka 145H nayo iliendelea mpaka mwaka 296H. Imam Abu Ubaidah  Jina lake ni Muslim bin Abiy Karimah, yeye aliacha Wanafunzi wengi waliosimamisha Uadilifu katika Ardhi, waliokua ni hoja Juu ya Watu, Miongoni mwao ni yule aliyeshika khatamu zake na kua ni marejeo ya Wote katika Zama zake naye ni Imam Rabii Bin Habib Farahidiy (r.a) aliyezaliwa mwaka 75H na yeye aliishi mpaka mwaka 170H , na huyu ndie aliyeandika kitabu cha Mwanzo cha Hadithi za Mtume (s.a.w), na mengi ya mapokezi yake katika kitabu hicho ni kutoka kwa Mwalimu wake Imam Abu Ubaidah (r.a) kupitia kwa Imam Jabir Bin Zaid (r.a), kupitia kwa Sahaba mpaka kwa Mtume (s.a.w), kwa hivyo mapokezi hayo yana haki ya kuthaminiwa zaidi, na kukubaliwa, kuliko mapokezi yoyote yale, kwani ni Mapokezi ya Maimam na mafupi yako karibu zaidi na Zama za Mtume (s.a.w), na yako mbali zaidi na Uongo, ambao umeenea katika Mapokezi ya wengine, na kitabu hicho Allah mtukufu amejaalia kubakia mpaka hivi leo, nacho ndio Tegemeo la mwanzo katika Hadithi za Mtume (s.a.w), na Maswahaba (r.a) katika Madhehebu ya Ibadhi, na jina lake kinaitwa: الجامع الصحيح مسند الإمام الربيع بن حبيب   -Ina Shaa Allah- tukijaaliwa tutafanya Kazi ya Kuzifasiri Hadithi zake katika Lugha ya Kiswahili, ili ienee Faida kwa Waislamu wanaofaidika kwa Lugha ya Kiswahili, kwa hakika kazi hii sijamuona aliyeifanya mpaka hivi sasa, Allah atuwezeshe katika kila lenye kheri na maridhawa yake(Amin).

Basi hii ndio historia fupi ya Maibadhi, wao ni watu wa Haki tokea wakati wa Maswahaba mpaka hivi leo, na jina hilo la kuitwa Ibadhi, wao walilikataa mwanzo, lakini baada ya kuzuka Madhehebu na kujiita majina tofauti, na wote walilazimisha jina hili la Ibadhi, ikawa hakuna Budi kulikubali kama ni Utambulisho katika tofauti zilizozuka baina ya Waislamu.

KWA NINI MAIBADHI WAKAWA NI KIDOGO ULIMWENGUNI?

Kwanza kabla ya kujibu suala hili inatakiwa ifahamike kua udogo au wingi hauna thamani mbele ya Haki, kwa maana Haki ni kitu kilichojitosheleza hakiathiriwi na wingi wa wafuasi wake au udogo wao, kwa sababu kila mmoja wetu ukimuuliza jee haki inafuata au inafuatwa? bila shaka atakujibu kua: Haki inafuatwa” na hili ndio jibu sahihi, linalokubaliana na maumbile.

Ndugu yangu Muislamu Allah mtukufu katika kitabu chake anatuelezea tabia ya Binadamu kua wengi wao wanaichukia Haki, na hii ni tabia ya Binadamu kwa sababu wengi katika watu ni wale wanaofuata mapendwa moyo yao, bila kuangalia jee ni haki au Batili, isipokua wale walioamua kuyaasi mapendwa moyo yao na kujiingiza katika Sheria ya Aliyeumba na wakakubali kuhukumiwa na Sheria hiyo kwa kuridhika kwa Nafsi zao, na kujilazimisha kufuata njia hiyo, na hawa kitabia ni kidogo, kwa sababu kuiasi nafsi ni jambo kubwa sana, na hasa hasa ikiwa kukamatana na Haki kutapelekea Kupoteza kilichokua na thamani kubwa katika maisha haya, au kukikosa kitu chenye hadhi hiyo, kama vile kukubali kufa, au kuteswa, au kuingizwa katika khofu, kukoseshwa ya kidunia anayoyategema mmoja wetu katika maisha yake, kama vile Mshahara, kazi, au kupambiwa vitu kama vile, kuitwa katika ufalme wa kiutawala, na kuahidiwa cheo fulani, na mengi mengine ambayo yanapelekea kata kuanzisha vita na kuendelea kwa muda mrefu katika njia ya Batili kwa sababu za kibinafsi tu, na haya ndio mengi katika maisha yetu kwani ndio Mitihani yenyewe ambayo tunafanyiwa na Muumba wetu, kwa hivyo kitabia ukiwa uko kwenye haki, na haki ndio inayokuongoza vitu kama hivyo vyote vitakua havina thamani mbele yako, na kuondosha nguvu zake ni jambo gumu sana linalopelekea kufeli wengi katika jambo kama hilo, basi kimaumbile Haki inakua na wafuasi wadogo, na hiyo ndio hali yake kikawaida, na inawezekana kupata wafuasi wengi lakini si kitu cha kuzoeleka, kwa maana hii itakuta wazi kua kipimo cha kua wengi ndio wenye Haki hakina thamani kwa wanaofahamu ukweli kwa sababu Haki haifuati lakini inafuatwa.

Kwa hivyo kutokana na utangulizi huo mdogo inafaa kulijibu lile suala, basi tunasema: Sababu za kufanya Maibadhi wawe ni kidogo zipo nyingi sana na hapa tunakueleza zifuatazo:

Maibadhi hawajalazimisha mtu kua katika msimamo wao wa haki hata mara moja, kwa hivyo anayefuata anakua amefuata kutokana na khiyari yake binafsi.
Maibadhi hawakupata fursa ya kutawala Jamhuri yote ya Waislamu, na kuweza kuonyesha Haki kwa watu wote.
Maibadhi walitangaziwa uadui tokea uliposimama udahlimu, mapka hivi leo.
Sura sahihi ya Itikadi yao na uhakika wao imaharibiwa kwa njia nyingi za Uongo, ni sawa katika upande wa siasa au katika upate wa Dini, kiasi cha kua hakuna Muislamu anayetaka kujua uhakika wa Ibadhi, isipokua atarejea katika Maandiko yaliyoandikwa na Wanavyuoni waliopita yaliyokusanya mambo ya uongo mengi sana, ambayo hata huyo Muibadhi mwenyewe akiambiwa mambo hayo na akatakiwa kutoa hukumu, bila shaka atahukumu kua mwenye kuyakubali hayo si Muislamu bali ni Mshirikina.
Maibadhi hawaja wahi kupewa fursa ya kuendesha mambo yao Hadharani, na kutangaza na kuelimisha mfumo wao sahihi, katika fikra za waislamu, kwa sababu wakifanya hivyo tu uadui dhidi yao unatangazwa, bali hata kuuliwa, kutokana na hayo waliuliwa wengi sana, na ilikuwa wakishindwa katika vita wanauliwa wote, na watawala wanapoingia katika Miji yao wanawakusanya na kuwauwa, na kuchoma moto vitabu vyao,  ili isije ikawa ni khatari katika Dunia yao, kwa hivyo mtu alikua anaogopa hata kujulikana au kuitwa kua ni Muibadhi.
Maibadhi hawakusalimika na vita dhidi ya madhalimu katika Tarekhe yao yote.
Kutoenea vitabu vyao katika ulimwengu, kwa sababu kukipata kitabu cha Ibadhi ni shida sana, havipatikani isipokua katika zile sehemu zao walizobakia mpaka hivi leo, kama Oman na Algeria, tena vitabu vyao ni ghali sana.
Kukatika usomeshaji wa wanafunzi wa miji mengine kwa wingi, na kukosekana ufuatiliaji wa baadhi ya wanafunzi katika mafundisho ya Dini, jambo ambalo limepelekea kukosekana Mashekhe na wasomi katika miji ya mbali na walipo wao, na hata kama Mwanafunzi akisoma kwao, anaporejea katika mji wake inakua ni vigumu sana kuendeleza Mafundisho yaliyokua ni sahihi kutokana na sababu tulizozieleza hapo juu, bali ikiwa anataka kupata sehemu yake ya kidunia kama Heshima au mshara au kukubalika na watu inabidi mara nyengine aache Madhehebu yake, kuingia katika Madhehebu nyengine, kwa maslaha yake ya Kidunia, Allah atulinde (Amin).
Kutokana na kulinda Maslaha ya Kimaisha Mashekhe wengi wanakataa kufuata Madhehebu ya Ibadhi, baada ya kupambazukiwa na jua na kuona kua haki imo ndani yake
Majina mabaya yanayochukiza katika fikra za Waislamu wamepewa Maibadhi kidhulma kama vile Khawarij, Muattilah, Maariqah, Jahamiyah, na mengineo.

BISHARA NJEMA KWA IBADHI

Juu ya yote hayo tulioleza katika sababu za kua Maibadhi ni kidogo sana, ipo bishara kubwa kabisa ya kupanada juu Madhehebu hii baina ya waislamu, kwa sababu haki imo ndani yake, tunakuta Wanavyuoni wengi waliojaribu kutafuta Haki kwa kutumia Dalili, katika Mas-ala waliyokhitalifiana Waislamu mwisho wanaangukia katika msimamo wa Kiibadhi bila ya wenyewe Kujua, na muhimu sio Jina bali ni Misimamo iliyo Sahihi tu, basi ni wazi kua Haki itanusuriwa.

Ulimwengu kila ukisogea mbele maendeleo yake katika Elimu yanaongezeka, nalo ni jambo linalosababisha kua wazi  zaidi mafundisho ya Madhehebu hii ya Ibadhi kwa wanaotaka Uhakika, kwa sababu Fikra zake hivi sasa zinaenea kwa kasi, na tayari hata Wenyewe Maibadhi wanachukua hima katika kuwasiliana na Wanavyuoni wao, na kuanzisha Masomo na kupatikana Mashekhe wenye msimamo huu sahihi, bila shaka yote hayo yanapelekea kuongezeka Wafuasi na nguvu ya Haki kupanda juu. Kwa hivyo mwisho mwema ni katika kuifuata Haki ile ile walioishikilia Maibadhi tokea Mwanzo mpaka hivi leo, kwa sababu ndio Uislamu ilio safi, ama kuitwa kwao Ibadhi ni kwa kutafautisha misimamo yao na ile iliyoko inje ya misimamo hiyo, na hili bila ya shaka ni jambo zuri, kwa sababu kuilinda Haki ni jambo la lazima Kisheria, kwa hivyo kuitwa jina hili ni katika sababu za kuhakikisha ulinzi wa Haki, ili isiingiwe na upotoshaji.

TOFAUTI BAINA YA IBADHI NA KHAWARIJ

Katika mafundisho mengi tunayoyaona, yanatupa picha na kujaalia msomaji aamini kua Maibadhi ni kundi miongoni mwa makundi ya Makhawarij, vitabu vingi vimetungwa zamani na sasa, ili kueneza Jambo hili, imefikia hadi ya kua Mwanafunzi wa Sheria ya Kiislamu katika Ulimwengu huu, anapotakiwa kufanya Uchambuzi kwa kupiga mbizi katika Bahari ya Maarifa ya Wanavyuoni kwa lengo la kujua uhakika wa Maibadhi, mara moja atajikuta kua yeye ni Mateka wa Fikra itakayojengwa na hukumu nyingi za kuyahukumu Madh-hebu hii ya Ibadhi miongoni  mwa hukumu hizo ni hii ya kua Wao ni miongoni mwa Khawariji.

Haya ndiyo ya uhakika, lakini –masikini- kumbe uhakika wa mambo uko mbali kabisa na Fikra hizo, wala hakuna uhusiano wowote baina yao, atayajua haya atakaye wasoma Maibadhi.

Maibadhi sio Khawariji wala sio miongoni mwa Makundi ya Khawariji, huu ndio Uhakika kwa anayeutaka, bali Maibadhi walipiga vita Makhawariji kifikra, kiitikadi na kisilaha.

Na ikiwa Maibadhi sio Khawarij, basi fikra hiyo italazimika kurejeshwa kwa kila mwenye nayo, na kumwambia kua Imani yako hiyo haina pa kukaa, na mafundisho yako hayo hayana uhakika, kwa hivyo akawatafute Maibadhi wengine na awahukumu kwa hukumu yake hiyo sio Maibadhi hawa tunaowajua sisi, kwa sababu jina sio Muhimu, muhimu ni yale yaliyopewa jina hilo, anaweza kuitwa Mtu Abdullahi kumbe kiuhakika ni Adbushaitani ikiwa itachukuliwa maana ya jina, na wako Muhammad wengi lakini Mtume wenye jina hilo ni Mmoja, kwa hivyo inawezekana Ikawa wako Maibadhi wengine wenye kuhukumiwa kua ni Khawariji lakini hao sio hawa tunaowajua, na ikiwa itatubainikia kua sisi tumedhulumiwa na Mtu jina lake ni Adili –kwa mfano-, kisha tukamkamata kila anayeitwa kwa jina hilo na tukampa hukumu ya kua yeye ndie mwenye kudhulumu, Jee!! haitokua kosa upande watu, Basi  – Wallahu Aalamu- inawezekana kuwepo Maibadhi wengine katika Tarekhe wao wanajulikana kwa sifa hizo na maelezo hayo ambayo yanalazimisha kuhukumiwa kwa kila hukumu kali, na kua wao ni Khawarij, hayo yanawezekana, ikiwa hayawezekani kuwepo kiuhakika inawezekana kuwepo kiutunzi, na hili la pili naona liko karibu zaidi kiuhakika kuliko hilo la mwanzo, kwa sababu sisi hatujui Maibadhi katika Tarekhe isipokua hawa tunaowajua, kwa hivyo hao walioelezewa mafundisho yao katika vitabu hivyo vya kina Abi Hasan L-ash-ary, na Bagh-dady, Ibn Hazm, na wengineo sio Maibadhi hawa tunaowaelezea sisi, hao ni Maibadhi wengine, wao wanawajua sisi hatuwajui, ifahamike njia yetu vizuri, na tunaona kuwahukumu Maibadhi hawa kwa maelezo ya waandishi hao ni dhul-ma kubwa sana sana, kwa sababu kumhukumu asiyefanya kosa, kwa sababu ya kufanana majina tu, inakua kosa ni kule kufanana Majina tu, Jee!! kuna dhul-ma iliyokua iko wazi zaidi kuliko hii kwa kila mwenye kufahamu ukweli? Basi haya yamekaa Dhidi ya Ibadhi.

Mimi sisemi mengi, naona Mapambano haya nimuachie mmoja katika Mashekhe wenye kutegemewa katika Maibadhi kingia katika vita hivi vikali, na Sheikh huyu sio mwengine isipokua ni Abu Is-haaq  Ibrahim It-faish (r.a), yeye aliandika uchambuzi huu baada ya kuombwa na Ibrahim Muhammad Abdulbaaqi ambae ni Mmoja wa Wanavyuoni wa Az-har na yeye aliyaingiza hayo katika kitabu chake الدين والعلم والحديث, basi yeye aliadika haya katika kitabu chake hicho: Na kwa vile wakati una hamu kwangu katika uchambuzi wao –yaani Ibadhi na Khawarij- na kuzamia, nimewasiliana na yule mwenye Maarifa nao, na yeye ni Kiongozi wa Kundi katika wao linaitwa Ibadhi, kiongozi huyu anaitwa Abu Is-haaq Ibrahim It-faish, yeye anafanya kazi katika Daar l-kutub lmisriyah, amenitosheleza na kazi ya upekuzi”.

Kwa hivyo anasema kiongozi huyo:

Khawarij ni makundi ya watu katika wakati wa Matabiina na Matabii Taabiina, viongozi wao ni Nafii bin L-azraq, na Najdatu bina Aamir, na Abdullahi bin Saffaar na walio wakubali. Waliitwa Khawarij kwa sababu wao walitoka katika Haki na katika Umma kwa kuhukumu juu ya mwenye kufanya Dhambi kua ni Mshirikina, basi wakahalalisha aliyoyaharamisha Allah katika Damu na Mali kwa Maasi, wakishikilia neno la Allah: Na mukiwatii hakika nyinyi mutakua Washirikina” An-aam 121, wakazua kua Maana ya Aya ni: Mukiwatii katika kula Maiti” Basi wakakosea katika Taawili yao, na kwa Haki maana ya Aya: Mukiwatii katika kuhalalisha Maiti”, na kuhalalisha alichoharamisha Allah ni Ushirikina.

Basi walipokosea katika Taawili hawakumalizia kwenye Neno tu, bali walipindukia wakaingia katika Matendo, wakahukumu juu ya mwenye kufanya Asi kua ni mshirikina, basi wakahalalisha Damu za Waislamu na Mali zao kwa Maasi, na wakaua bila ya hatia Wanawake na Watoto na Wazee.

Na alikua Imam Muhifadhi Hoja: Rabii bin Habib bin Amru L-basariy L-farahidiy L-ibadhiy  mtungaji wa Mus-nad Sahih -Allah amrehemu- alipofikiwa na Jambo lao akisema: Waacheni mpaka wavuuke Neno na kuingia katika Tendo, ikiwa watabakia katika Neno lao kosa lao litachukuliwa juu yao, na wakilivuuka kwenda katika Tendo tutahukumu kwao kwa Hukumu ya Allah”

Basi ilipodhihiri Bidaa yao walifukuzwa na As-habu wetu katika vikao vyao, na kuwafukuza katika kila sehemu wakieka wazi kua mbali nao. Na walipovuuka Neno lao na kuingia katika Tendo wakatoa Ilani ya Kukufuru kwao –kwani Ukafiri katika kuhalalisha aliyoharamisha Allah ni maneno katika Kitabu cha Allah yasiyokua na Shaka- hakika vilienea vitendo vyao wakati huo ikawa ni Jambo zito juu ya watu wa Tauhidi kwa Fitna zao, waliziweka Panga zao katika Shingo kinyume na aliyoteremsha, Allah ukawa ni mkubwa Mtihani wao, na likawa ni Balaa kubwa.

Walikua Waomani ni katika waliothibiti katika kuwapiga Khawarij pamoja na Muhallab wakati Khawariji walipotoa Majeshi yao, angalia الكامل cha Mubarid.

Basi alitawalia kuwapiga vita Muhallab bin Abi Sufrah L-uzdiy Umaniy kiongozi wa Kiumawiy aliyemashuhuri, na yeye alikua akitunga Hadithi katika kuwahimiza watu kwenda vitani, ukawa mkubwa mtihani wao pande mbili: Kuwapiga vita Waislamu, na kuenea Hadithi za uwongo katika kuwapiga vita wao, mpaka ikafikia upeo katika Shari, ikawa ni Balaa zito. Na kwa vile hawa Khawarij ni katika waliokataa Tah-kiim, basi wametawalia wengi katika wanaojinasibisha na Madhehebu Mengi kuwazamisha Maibadhi katika hawa Makhawarij kwa Dhulma na Uwadui, na sababu katika hilo ni njia nyingi:

Njia ya kwanza:

Hakika As-habu wetu Maibadhi –wanaona Ufalme wa kuhodhi hailazimiki kuutii, bali ni lazima iwe Hukumu juu ya Mwendo wa Viongozi Waadilifu kutokana na yale yaliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w): Jifuatisheni kwa Wawili baada yangu Abu Bakar na Omar” Hadithi sahihi Mutafakun Alaih. Na kwa yaliyopokewa katika Ammaar bin Yaasir Allah amrehemu” Litakuua Kundi lilioasi” na wametolea ushahidi hadithi hizi Waliokataa Tah-kiim wala haukupinga upande mwengine, ikathibiti kua ni Maneno ya uhakika wameyaridhia Makundi mawili hata kama wamekhitalifiana katika Taawili yake, kwa sababu kundi jengine wameyachukua katika Maana isiyokua Sahihi, na yaliyopelekea katika uchukuaji huo ni kwa mujibu wa kufuata Mpendwa Moyo.

Njia ya pili:

Kudhihiri Wafuasi wa Mapendwa Moyo katika Tukio la Nah-rawaan, kwa sababu walidai kua lilikua ni kutoka kwa Ajili ya kumpiga vita Imam Aliy na yeye ni Imam wao; Na hakika ambayo haina shaka ndani yake kua Watu wa Nah-rawaan hawakutoka kwa kumpiga vita Imama Aliy kamwe, lakini wao walipokataa Tah-kiim na wakashikilia hilo, alielekea Baba yake Hasan upande wa Tah-kiim, basi waliona waliokataa Tah-kiim kua Ahadi ya kutii haipo katika shingo zao bali wao wako mbali na hilo, kwa sababu Tah-kiim katika jambo maana yake haijathibiti Hukumu, na kama sio hivyo ya nini Tah-kiim? Wakazingatia Tah-kiim kua ni kujitoa Imam Abi L-hasan katokanaa na Ahadi ya Kumtii, kwa hivyo waliokataa Tah-kiim wako huru katika Jambo lao na wao wanayo Haki ya kumchagua wanayemtaka kua ni Imam wao, wakamchagua Kijana katika wabora wa Watu siku hiyo naye ni katika Masahaba watukufu huyo ni Abdullahi bin Wahab Raasibiy L-uzdiy. Na walipompa ahadi ya Utawala walipeleka kwa As-habu wao siku hiyo -miongoni mwao ni Imam Aliy- kua waingie katika Ahadi ya waliomchagua kua ni Imam.

Akaona Aliy bin Abiy Taalib kua Ahadi imepatikana kwa Uzudiy na sio Quraishiy, na akawapiga Vita kabla haijapata Nguvu  Amri yao ya kutoka Uimam na kua kwa asiyekua Quraish, na hii ndio Sababu pekee ya Tukio la Nah-rawaan.

Na kutokana na Hili aliwaita pale alipopeana nao Hoja waende kumpiga Vita Adui yao Muawiya na walio pamoja nae, lakini Hukumu imeshapita, na kuichukua Hukumu Muawiya kwa waliohukumu: Amru bin L-assi na Abi Mussa L-ashariy katika Daumati L-jandal, na kua Waislamu wako huru na Jambo lao. Na kwa sababu Ahadi ya Adbullahi bin Wahab haikukaa isipokua baada ya kupatikana matokeo ya kupatikana waliyompa hadhari kwayo Wenye Uoni  katika waliokataa Tah-kiim, nalo ni kua Tah-kiim ni kuichezea Hukumu, ameutawalia ulinganio wake Ash-ath bin Qais ambaye ni mbegu ya sumu iliyotiwa juu ya wafuasi wa Aliy inayotoka kwa Muawiya.

Na siyo –kwa hivyo- wanayoyazua Wabadilishaji wa Tarekhe na Washabiki wa Kimadhehebu kua Tukio la Nah-rawaan lilikua kwa sababu ya Kutoka kwa kumpiga vita Aliy, kwa sababu wao hawakutoka na Ahadi iko katika shingo zao, alizingatie hili Mwenye kutaka kuona asije akateleza katika sehemu hii, hakika Mapendwa Moyo yana keketa keketa katika waliyonayo bila ya kuwepo uficho ndani yake.

Njia ya tatu:

Hakika uitwaji wa Khawarij haukuzoeleka wakati wa Mwanzo, lakini ulienea baada ya kuja juu Jambo la Azaariqah –kama nilivyosema- wala halikujuilikana Jina hili kwa waliokua na Aliy, wale waliokataa Tah-kiim na Walioridhia Tah-kiim, na pengine mwanzo wa kudhihiri kwake Tamko hili ni baada ya Kuthibiti Hukumu kwa Muawiyah na Kutulizana upande wake, pale alipotembelewa na Ahnaf bin Qais Tamimiy na yeye ni katika Watu wa Nah-rawaan akasema Muawiya: Kwa nini wanakupenda watu na wewe ni katika Khawarij? na yeye akamwambia: Kama Watu watayatia Aibu Maji sitoyanywa”

Yaani wale waliokua hawakuridhia Ahadi yake na kuingia katika Hukumu yake –rejea الأمال cha Abi Aliy Lqaliy.

Jee!! unaona kua Muawiya anamsifu Ahnaf bin Qais kwa Ukhawarij kwa sababu alikua pamoja na aliowapiga vita Aliy siku ya Nah-rawaan? au kwa sabau alikua hayumo katika Ahadi ya Muawiyah? Na kama ingalikua Muawiya kumsifu Ahnaf kwa Ukhawarij ni kule kua kwake katika Watu wa Nah-rawaan basi ingalikua Muawiya na walio pamoja naye ni bora zaidi kwa Sifa hiyo, kwa sababu yeye ndie aliyetoa Upanga kumpinga Aliy na walio pamoja naye siku ya Siffain, na kwa sababu yeye ndie alikaa mbali na Ahadi ya Imam Aliy, na hali walimpa Ahadi hiyo Ahl L-hall wa L-aqd na kua Ahadi yake ni Haki inalazimika kuifuata na kuingia ndani yake juu ya kila mmoja katika Waislamu.

Njia ya nne:

Hakika Maibadhi hawakutoa Upanga juu ya Yeyote katika watu wa Tauhiid hata mara moja, wala havikukaa vita baina yao na Yeyote katika Waislamu, na hata katika hali ngumu ya Hajjaaj bin Yousuf Athaqafiy na Ziyaad bin Abiihi kwani wao walizidisha katika kuwafukuza Waislamu kwa Dhana tu, mpaka walitoka kuwapiga Vita viongozi walioitwa Tawwabuun wakiongozwa na Said bin Jubair na Ibrahim Nakhaghiy na wao wawili ni Maimamu, na Hajjaaj alimuua Said bin Jubair mmoja katika Maimamu wa Tafsiri, Na ajabu kila ajabu kua Kundi hili kubwa la Wanavyuoni ambao walichukua Upanga mbele ya Ujeuri  uliodhihiri Ukorofi wake kwa Hajjaaj hakuwaita yeyote kwa jina la Khawarij, bali wamewapa jina la Tawwabuun, na wao wote ni katika waliochukua bendera ya Elimu, na wote walikufa katika Vita isipokua watatu: Said bin Jubair, na Ibrahim  Nakhaghiy, na Abdullahi bin Matraf. Hakika Akili inasimama kwa mshangao mbele ya Fedheha hii kubwa na juu ya yote hayo linapita kwa wasomaji kwa Amani.

Lakini yule atakae zingatia Tarekhe kwa uadilifu na akajua ataona kuekwa jina la Khawariji juu ya Ibadhi –nao kwa Khawariji wako mbali- kua ni Kitendawili, na hayo ni kwa Sababu wanaona kua Uongozi sio kwa Quraish tu, bali utakua sahihi kwa yeyote watakae mchagua Waislamu kwa Siasa ya Dola yao na kua Kiongozi wao, na hii ndio Haki ambayo inaonyesha ukamilifu wa Uoni, kwani sio katika Hekima ajaalie Allah Hukumu ya Watu kwa Jinsi zao Zote na Mataifa yao yote ifuate Kabila Moja ni sawa kama litafanya vibaya au vizuri, na muweko wa kitabia katika watu ndio uliokubaliana na waliyoyaona Ashabu wetu na wakaichukua juu yake Hadithi: Maimamu katika Quraish” ni katika kujitia Ukubwa na kukaa mbali na Haki, na ni kuzua wenye kuzua ili Siasa ya Mataifa iwe kwa Kabila la Quraish tu, na hawakuliridhia Answari na wao ni watu wa Fahamu kwa aliyopelekwa kwayo Muhammad (s.a.w) pale walipomwambia Abu Bakar: Kwetu sisi Amiri na kwenu nyinyi Amiri” wala Abu Bakar  alipo waambia: Kwetu sisi Maamiri na kwenu nyinyi Mawaziri hakika Waarabu wanafuata Kabila hili” yaani Quraish; basi akatoa Sababu ya Hukumu kwa kufuata Waarabu Quraish na sio kitu chengine katika wanayozua Wa mapendwa Moyo na Kimadhehebu. Jee!! unaona kua Mataifa yote kwa jinsi zake yatafuata Mtu katika Quraish kwa sababu yeye ni Quraish? Hapana Wallahi.

Uadilifu katika Ibadhi:

Hakika Maibadhi wanataka Uadilifu, na wanaeneza Matendo kwa Kitabu na Sunna na Mwendo ulio katika njia za Kisiasa ambayo waliifuata Viongozi Waadilifu, ni Sawa kama Amri itakua kwa Mquraish au Mhabashi, Mwarabu au Asiye Mwarabu kama ilivyokuja katika Hadithi Sahihi, na kwa hili waliridhia Mwendo wa Omar bin Abdu L-aziz pale walipotuma kwake Uajumbe kutoka Basra uliofanyika kwa Wanavyuoni Sita Waliobobea: Jaafar bin Sammaak, na Abu L-hur Aliy bin L-huswain L-ambariy, na Hattaat bin Kaatib, na Habbaab bin Kulaib, na Abu Sufyaan Kummbury L-basariy, na Salim bin Dhakwan, na pengine walikua zaidi ya hawa isipokua niliopata majina yao ni hawa -Allah awarehemu wote-. Lakini walipotaja wanatarekhe wa kaumu yetu Ujumbe huu kwa Omar bin Abdu L-aziz walisema kama ilivyo Ada yao katika kejeli: Walituma kwake Khawarij Ujumbe” wala hawakutaja yaliyopita baina yao na Kiongozi Omar katika mazungumzo na kuyakubali kwao yote waliyoyataka kwake katika kueneza Uadilifu, na kusafisha Nchi na Majukwaa (Membar) kutokana na Laana ambayo waliifanya Maumawiy kua ni Sunna. Hakika Ujumbe ulisema kwake: Hakika Waislamu wanalaani juu ya Majukwaa hapana budi kuanza kubadilisha Ubaya huu” ikabadilishwa Laana kwa Neno lake Allah :

إن الله يأمر بالعدل والإحسان وإيتاء ذي القربى وينهى عن الفحشاء والمنكر والبغي يعظكم لعلكم تذكرون”

Hakika Allah anaamrisha Uadilifu na Wema na kuwapa walio wa karibu, na anakataza Uovu na Ubaya na Uasi; anakupeni mawaidha ili nyinyi mukumbuke” Nahli 90.

Hazikusamehe Nafsi za Waandishi hao ambao yamepofua Mapendwa Moyo uoni wao kutaja Mazuri hayo ambayo yamedhihiri kwa Maibadhi katika kuita kwao katika Haki na Kusimama katika Uso wa Madhalimu kwa kupeana maneno kama alivyofanya Imam Abdullahi bin Abaadhi pamoja na Abdulmalik bin Marwani, na Abu Bilal Mir-daas bin Hudair  pamoja na Ziyaad bin Abiih wala wao hawakutoa Upanga kama walivyofanya Khawarij, lakini walifuata njia ya Ubaisho wakikaa mbali na ncha za mikuki, kwa sababu wao wanaona kulindwa Damu kwa Tawhiid ya لا إله إلا الله na kulindwa mali vile vile, wala hayakua kwao katika Matendo ya wasio kua wao katika Njia ya kuanzisha Ufalme, au kuchukua watu katika Madhehebu yao kwa Upanga na kuondoa Dharura; lakini waliacha watu kua Huru katika Rai zao na kukaa mbali na Dunia ikiwa itakuja nje ya Uhalali wake, na wameacha mabwana wa kimadhehebu na madhehebu yao katika Uhuru uliotimia, kwa sababu hakuna kulazimishana katika Dini. Basi Haki inakubaliwa kutoka kwa Yeyote, na Batili inerejeshwa kwa mwenyewe na kuchukulishwa mwenyewe; watu wa Kibla kwao wao wote ni sawa sawa katika Haki, na Uhuru katika kuelezea Rai zao, na Uhuru unatosha kwa kila Mtu baada ya kukubali Upweke wa Allah, na Uhuru ndio Asili katika Watu, hata Mtumwa wa kujikomboa kwa kuandikiana kwao anakua Huru katika siku ya Mwanzo ya kuandikiana, na Deni litakua juu yake alilipe, na hakuna aliyesema haya isipokua Maibadhi, kwa sababu wao wamediriki katika Sheria iliyowafanya wawe juu ya Wasio kua Wao.

Imetambulika umbali wao na Khawarij kwa tuliyotaja katika Mabaya yao na Makubwa yao, wala hawana fungamano kwao na Ibadhi mpaka isemwe kua wao ni Makhawarij. Kwa hakika zimekua wazi kwa Waadilifu wa Kaumu yetu tofauti hizi nao wakaidiriki Haki na kuikubali, na kurejea katika Haki ni Faridha na Utukufu.

Tofauti baina yao:

Maibadhi wanakubalisha Kuoana baina yao na Wenye kumpwekesha Allah wote (Muwahhidina) na Khawarij hawakubalishi Kuoana na wasio kua wao, kwa sababu wao wanaona wasio kua wao ni Washirikina kama tulivyobainisha na kueka wazi, na kutokana na hili haifai kurithiana baina yao na walioko kinyume na wao kitabia, kwa sababu Ushirikina ambao umezuia Kuoana na Ukwe umezuia kurithiana.

Jee!! wamekua vipofu katika tofauti hizi wale ziliofunga Nafsi zao na kupatwa Macho yao na Kifuniko, na haya ndio atakayoyaona mwenye kuangalia migeuko ya Tarekhe katika maandiko ya Kaumu yetu, wala hawakuzingatia Neno lake Allah mtukufu:

إن الذين يؤذون المؤمنين والمؤمنات بغير ما اكتسبوا فقد احتملوا بهتانا وإثما مبينا

Hakika wale wanaowaudhi Waumini wa Kiume na Waumini wa Kike kwa waliyokua hawakuchuma; kwa hakika wamejichukulisha Uzushi na Dhambi iliyowazi” Ahzaab 58, Na Neno lake Mtukufu:

ولا يجرمنكم شنآن قوم على ألا تعدلوا. اعدلوا هو أقرب للتقوى

Wana yasikuingizeni katika Makosa Mambo ya Watu juu ya kua Musifanye Uadilifu. Fanyeni uadilifu hilo ndio Karibu zaidi na Uchamungu” Maidah 8

Hakika Muislamu anababaika kutokana na Jambo la wale wanaojisemea juu ya Watu wa Haki na Kunyooka –Maibadhi- vipi wamejichukulia hayo kwa Nafsi zao, si kwa chochote isipokua kwa Pendo la Moyo na Matamanio yaliyojificha, tunajitenga kwa Allah kutokana na Pendo ya Moyo na kuikataa Haki. Jee!! hawakumbuki kua wao watakutana na Allah na Uzushi huo. Au Itikadi ya Kutoka Motoni imewafanyia wepesi kila kitu katika njia ya Matamanio.

Tofauti nyengine:

Maibadhi walielekea katika kuufanyia kazi Uislamu Kielimu na Kimatendo tokea zilipoanza Fitna, walijishughulisha na Uandishi wakawa ni wa Mwanzo walioandika Hadithi, kwani Imam wetu Jabir Bin Zaid ni wa mwanzo  kuandika Hadithi na Maneno ya Masahaba katika Diwani yake ambayo wameisifu kua ilikua ni shehena ya Ngania, Wanafunzi wake baada yake wao ndio Wachukuaji Elimu kuelekea Mashariki na Magharibi, Na Khawarij walielemea katika kumwaga Damu na kukhofisha Njia na Kuvunja Hukumu, wala haikutajwa kutoka kwa yeyote katika Khawarij kua ametunga Kitabu, na hao waliotaja Matunzi ya Khawarij kwa hakika wanataja Maibadhi, na wao bila Shaka wanataka kwao kuwaharibu na kuwakimbiza, ama Suf-riyah na Azaariqah na Najdiyah haikutajwa kwao upokezi wala utungaji, hata kama amekua peke yake Najdatu bina Aamir kwa upokezi wa Hadithi, na Nafii bin L-azraq kwa masuala aliyomuuliza Ibn Abbaas, hayo sio Pahala pake, ninachokitaka ni kua wao walielemea katika Vita na sio katika Utungaji na Upokezi wa Elimu, Basi wote waliotaja Kaumu yetu katika watu wa Elimu na wakawanasibisha kwa Khawarij hawakua hao isipokua ni katika Maibadhi.

Kwa hakika wameleta As-habu wetu katika Utungaji wa Elimu Ajabu ya Ajabu, na wamejulikana kwa Ukweli na Uaminifu na Kujitakasa wasiyofika katika kilele chake wasiyokua wao, wakaelemea baadhi ya Waandishi wa Kaumu yetu kuharibu ya Uhakika na Utangazaji Mbaya na Uwongo pale walipobabaishwa na Nuru zile zenye kughara, na hawakuchanganya baina ya Maibadhi na Khawarij isipokua kwa kuzima yaliyojuu katika Haki na Uhakika, ni Uhasidi uliomo katika Nafsi zao, na vipi kwa aliyefanya Uharibifu kua njia yake aweze kuikubali Haki na Uhakika na umeshapofuka Uoni wake? Na hakika utawaona Hawa katika Kazi ya kuficha wanayoyaona katika As-habu wetu katika Ukamilifu wa Dini na Ukubwa wa Kimatendo yanayowafanya wasitaje katika yanayolazimika kutajwa chochote, na hakika mimi nimeona Matunzi yaliyoandikwa katika Tarekhe na Adabu na Furugh ya baadhi ya Kaumu yetu inalazimika kuwataja As-habu wetu kwa yaliyo yao bia pingamizi, basi haoni shida kujitia ujinga wa utajo wao kama kwamba wao hawakuwepo, na hayo ni kupindukia Mipaka na kuzamia katika kuizima Haki, na hutokuta katika As-habu wetu kitu katika njia hiyo mbaya, na shukurani zote ni kwa Allah mtukufu.

Kuchanganya Haki na Batili

Hakika Kaumu yetu walipo kusanya Matokeo ya Kitarekhe na ikalazimika wataje kuhusika na matokeo hayo, walifeli katika kuusema ukweli, na wakachanganya baina ya Maibadhi na Khawarij, mara wanayachukua ya Maibadhi wanayaweka kwa Khawarij na mara wanayachukua ya Khawarij wanayaweka kwa Maibadhi, kama walivyofanya wengi katika Maandiko ya Usuli na Furughi na katika kuongezea Maneno ya Muutazila kwa Maibadhi, na kinyume cha haya, mambo ambayo yamelazimisha kuchanganyika na kushawishi basi wanakwenda Waandishi ambao wanategemea kunakili na kuelezea mambo yanayofanana na Uuwaji, wala hawana Udhuru hawa upande wangu kwa vyovyote vile, kwa sababu anayetaka kueneza haki anaitafuta katika chemchemu zake na sio aivae kwa mujibu wa Matamanio yake.

Hakika sisi tunakuta anayezua kua Abu Bilal Mirdas bin Hudair ni katika Khawarij na Qatariy bin Lfujaah ni katika Maibadhi na uhakika ni kinyume na hivyo, na mwengine anataja kua Imam Taalib Lhaki Abdullahi bin Yahya L-kindiy ndiye Imam Abdullahi bin Abadhi na Haki ni kinyume na haya, kwa sababu Imam Abdullahi bin Abadhi alikufa mwisho wa utawala wa Abdulmalik bin Mar-wan na Abdullahi bin Yahya Taalib Lhaki alidhihiri siku za Marwan Lhimaar mwaka 130H. Basi namna hivi wanachangacha waandishi katika Kaumu yetu Hakika hizi muhimu kwa kuziharibu na kuzipoteza, angalilia Tarekhe ya Indalos (Spain) ambayo ipo baina yetu leo hakuna hata utajo wa Maibadhi na Hali Maibadhi walifikia katika Indalos upeo mkubwa katika Elimu na Mali mpaka kisiwa cha Yaabisah ambacho ni sehemu ya Indalos kilikua chote ni Maibadhi mpaka Karne ya Sita bali mpaka kuporomoka kwa Indalos kubwa.

Na hakika wewe unasoma Tabakaat cha Ibn Saad kwa mfano, huoni utajo wa Maibadhi isipokua Imam Jabir bin Zaid hakika yeye amemtaja hata kama hakupenda kwa umashuhuri wake ambao umeenea kila sehemu na namna hivi. Na Haki ambayo haina shaka ndani yake ni kua Watu wa kila Kaumu; Kaumu ya Watu hao wana Haki zaidi na Watu hao, na Tarekhe watu wake wana haki zaidi katika Tarekhe yao nao wanaijua zaidi kuliko wasio kua wao na Allah anasema Haki na yeye anaongoza katika njia.

Kwa hakika imelazimisha Bidaa ya Khawarij Hukumu za Kisheria, basi Wamesema Waislamu: Inalazimika kuyabagua makosa makubwa isije ikapelekea kuingia Mtu katika kosa la Khawarij, kwa hivyo Makosa makubwa yana vigao viwili; Makubwa ya Kishirikina nayo ni kila Kubwa linalovunja Itikadi kama kuhalalisha alichoharamisha Allah au kuharamisha alichohalalisha Allah, au kukataa kinachojulikana katika dini kidharura, au kupinga Hukumu isiyokua na shaka, kama Rajm (Kupigwa mawe aliyezini ambaye ameshingia katika Ndoa) na mfano wake. Makubwa ya Kinafiki na hayo ni makubwa ya Ukafiri wa Neema za Allah –nayo yameitwa na watu wa Hadithi Ukafiri ulio chini ya Ukafiri- na hayo ni Makubwa ya Ufasiki katika Kaumu yetu, kwa mfano kufanya chafu katika Uzinifu, kuingilia Nyuma, kula la Haramu, Shahada ya uongo, kuvunja Haki za Wazazi na mfano wa hayo katika Makubwa ya kimatendo, na kama Kuacha Faridha katika Faridha za Allah -ikiwa hakualalisha katika yote hayo- hayo yanaitwa na As-habu wetu kua ni Makubwa na Kinafiki na Makubwa ya Ukafiri wa Neema, na wanaposema As-habu wetu Ukafiri basi utaingia kwa vielelezo katika Hukumu yake, Jee!! ni katika yanayoharibu Itikadi au ni katika Kutenda au Kuacha? basi inajulikana aina ya Ukafiri, jee!! ni Ukafiri wa Kinafiki au Ukafiri wa Kishirikina, na juu ya yote haya As-habu wetu hawakufurishi kwa Kupenda tu, wala hawakufurishi watu wa Kibla ikiwa walikubali Neno la Ikh-las, na kwa hakika wao ni peke yao kwa jambo hilo, hata kama watalidai Wakuu wa Madhehebu nyengine, na utakapolifahamu hili utajua kua kuna umbali mkubwa baina ya Maibadhi na Khawarij wala hakuna linalowakusanya isipokua kukataa Tah-kiim, nayo ni Haki ambayo inakubaliwa na Kitabu cha Allah na Sunna ya Mjumbe wa Allah (s.a,w)  na mwendo wa Maomari wawili (Abu Bakar  na Omar bin Khattab (r.a)) na Makubaliano ya Waislamu. Basi shikilia kwa Mkono wako hili la Haki, na mwenye kujilinda kwa Allah ataongozwa katika njia ya Usawa.

Uhakika wa Rajm (Kumpiga mzinifu kwa Mawe)

Hakika wamesema baadhi ya As-habu wetu, na kwa hilo wamesema Kaumu yetu kua Khawarij wanapinga Rajm, na ambalo liko kwangu kua Neno hili sio Sahihi, isipokua kama tutazingatia Hukumu yao, kua Mtenda kosa Kubwa ni Mshirikina halali Damu yake, kwa hivyo Mzinifu kwao anauliwa kwa Kuritadi na sio kwa Haddi, na hili ni katika Mazaliwa ya Hukumu yao bila wasi wasi, kwa hivyo haihitaji madai ya kupinga Rajm, na Ukweli wa mambo kwangu mimi sivyo kama inavyofikiriwa, lakini anazua anayezua katika Kaumu yetu kua Khawarij wanapinga Rajm kwa lengo jengine, lakini linarejea kwa Waliozua kwa Ubaya. Nayo ni kua Kaumu yetu wanaona kua katika yaliyokua yakisomwa katika kitabu cha Allah katika Suratu L-ahzaab:

الشيخ والشيخة إذا زنيا فارجموهما البتة نكالا من الله والله عزيز حكيم

Mzee wa kiume na Mzee wa Kike watakapo zini Wapigeni Mawe hao wawili moja kwa moja; ni Adhabu itokayo kwa Allah na Allah ni mwingi wa nguvu na mwingi wa hakima” lakini Aya hii ililiwa na Anzah. Basi yanafuatilia juu ya maneno haya kua Hakika Qur-ani imekaa ndani yake upungufu –Tunajikinga kwa Allah-, na Ubaya huu unawalazimu wao hata kama wakiukimbia kwa kuzua kwao kua hii ni katika yaliyofutwa Tamko lake na kubakia Hukumu yake; lakini As-habu wetu wanasema kua Rajm ni Faridha isiyokua katika ubainisho wa Qur-ani lakini katika Ubainisho wa Hadithi, kwa sababu amepokea Hafidh Lhujah Rabii (r.a) katika Sahihi yake kutoka kwa Imam Jabir Bin Zaid:

الاستنجاء والاختنان والوتر والرجم سنن واجبة

Kustanji, na Kutia jando na Witri na Rajm ni Sunna za Lazima”

Akalinda Allah As-habu wetu kutokana na Ubaya, na Shukurani zote ni za Allah  na Arehemu Allah kwa Bwana wetu Muhammad na Aali wake na Sahaba wake.

Abu Is-haq Ibrahim Et-faish.

ITIKADI SAHIHI KATIKA  UISLAMU.

Itikadi sahihi ni jambo muhimu sana katika Maisha ya Mwanadamu, kwa sababu Itikadi ndio kiongozi wa mtu katika Maisha yake, nayo ndio sababu ya kila neno au tendo au Fikra katika maisha yake, kutokana na haya basi kila upande ni lazima uwe katika Itikadi ambayo itakua ni sababu kubwa ya kumfanya yule aliyeridhika na Upande huo ayaone mambo na ayahukumu na ajiweke yeye mwenyewe kwa mujibu wa Itikadi yake, basi Itikadi ina umuhimu mkubwa katika Maisha ya kila Mtu, na kutokana na hapa inatokezea mivutano, baina ya Watu, na inakua ni sababu ya kukosoana, na pengine hata kupotezana, na kukufurishana, kwa sababu ya kutofautiana tu katika Itikadi. Itikadi haina Ruhsa ya kutofautiana ndani yake, kwa sababu haiwezi kuwa ni Haki pande zote mbili katika tofauti, kwani Itikadi ni Khabari, na khabari haiwezi kutofautiana, ikitokezea tofauti katika Khabari ni lazima moja tu katika Tofauti hizo ndio Haki, na nyengine ni Batili, kwa Mfano; katika kuonekana Mungu siku ya Kiama kuna misimamo miwili; Ataonekana na Hatoonekana, Sasa jee!! inawezekana kutokezea yote mawili, haiwezekani ni lazima moja tu ndio la Haki  ima ataonekana au Haonekani, na njia pekee ya kuijua Haki ni kuziacha Dalili zihukumu, na sio tuangalie Watu tu katika waliyohukumu, ni wajibu wa kila Mmoja kujua uhakika wa anayoitakidi.

MSINGI WA ITIKADI KATIKA SAHIHI

Basi kutokana na haya Maibadhi wamepinga Dalili yoyote ile inayothibitisha Itikadi kwa njia ya Dhana au Shaka, na wanayakubali hayo katika kutilia mkazo Itikadi baada ya kuthibiti katika Dalili zilizokua hazina Shaka wala Dhana ndani yake, ama kuanzisha Itikadi kwa Dalili za Dhana na Shaka haikubaliki upande wao, kwa sababu Itikadi ni tunda la Yakini.

Na kutokana na Haya, bila shaka kila mmoja ana hamu ya kujua Itikadi ya Ibadhi ndani ya Uislamu, basi tunamuambia kua anaetaka itikadi Sahihi hawezi kuipata isipokua ndani ya Ibadhi, na vile vile yeyote yule atakayeziacha Dalili sahihi zihukumu katika itikadi yake atajikuta anaanguka katika ile Itikadi waliyoikubali Maibadhi, na kutokana uhakika huu tunaona Wanavyuoni wengine ambao sio Maibadhi aslan wameitakidi itikadi zao bila ya wenyewe kujua, kiasi cha kua hakuna hata Mas-ala moja waliyokubaliana Maibadhi katika Itikadi isipokua unaikuta ipo katika Itikadi ya Mwanachuoni wa Madhehebu nyengine, na ameleta kila Ushindi juu ya walikwenda kinyume na yeye, yote haya yanatilia mkazo uhakika wa Maibadhi; na hapa ninaeleza Itikadi Sahihi ambayo Maibadhi wanaifuata.

KUA MUISLAMU.

Maibadhi waitakidi kua Mtu hawi Muislamu mpaka akubali Shahada, na Shahada maana yake kufunga ahadi baina ya mwenye kuitamka na Allah aliyeumba. Kwa sababu yote yatakayofuatia Baada ya Shahada yanatokana na msingi huu wa Ahadi hiyo, basi wao hiyo Shahada wameipa Jina na kuiita JUMLA, yaani MKUSANYO, kwa sababu ndio asili ya kila Amri na Katazo ambalo Mwanadamu anatakiwa alifanyie kazi.

Na Shahada nikusema hivi:

أشهد ألا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله  وأن ما جاء به محمد حق من عند الله

Maana ya maneno haya ni hivi: Nashuhudia kua Hapana Mungu isipokua Allah na Hakika Muhammad ni Mtume wa Allah, na Hakika aliyokuja nayo Muhammad ni Haki inayotoka kwa Allah” Na hii ndio maana ya Uislamu, kwa sababu Uislamu katika lugha maana yake ni kujisalimisha na kutii, kwa hivyo unaposema maneno hayo tayari wewe umeleta maana ya Kisharia na neno hilo nayo ni kujisalimisha kwa Aliyeumba katika kila kitu, na yeye huyo jina lake ni Allah, na katika kujisalimisha huko kwanza ni kule  kukubali kua Muhammad ni Mtume wa Allah aliyeumba, na Kukubali kua aliyokuja nayo Muhammad Ni Haki” Kwa hivyo hii ndio ahadi anayoiweka Muislamu kwa Mola wa walimwengu wote.

Kutoka na Shahada hiyo Maibadhi wamewagawa watu katika vigao viwili tu navyo ni UISLAMU au USHIRIKINA, yeyote yule aliyekubali na kutamka Shahada huyo ni Muislamu, na asiyekubali na kutamka huyo sio Muislamu tena ni Mshirikina.

Maibadhi wameleta Shahada hiyo katika mfumo huo uliokubalika na Waislamu wote, na ndio uliokuja ndani ya kitabu cha Allah katika surail-taghaabun (64:8) amesema Allah:

فأمنوا بالله ورسوله والنور الذي أنزلنا

“Na mumuamini Allah na Mtume wake na Nuru ambayo tumeiteremsha”

Kwa hivyo ni vitu vitatu hivi tulivyoamrishwa, navyo ndio vile vilvyomo katika ile JUMLA, kwa hivyo hii ndio Haki.

TOFAUTI BAINA YA MUUMIN NA MUISLAM.

Mtu yeyote yule aliyeukubali Uislamu katika maana hiyo tuliyoieleza hapo juu, akiwa ndani ya Uislamu ima ataitimiza ahadi yake aliyoitowa, au hatoitimiza ahadi hiyo; Kutokana na mtazamo huu itakua Waislamu vile vile wamegawika sehemu mbili:

Wale waliyokubali ahadi na kuitimiza kama inavyotakiwa hawa wanaitwa WAUMINI, nao ndio wale watakaofaulu na kuridhiwa na Allah katika Maisha ya Duniani na Akhera nao ndio Wachamungu, hawa wamepewa sifa hii kutokana na Neno lake Allah mtukufu, pale aliposema:

وما كان لمؤمن ولا مؤمنة إذا قضى الله ورسوله أمرا أن يكون لهم الخيرة من أمرهم ومن يعص الله ورسوله فقد ضل ضلالا مبينا

Wala haiwi kwa Muumini wa Kiume wala Muumini wa Kike anapohukumu Allah na Mtume wake jambo ikawa kwao kuna khiyari katika jambo lao; na mwenye kumuasi Allah na Mtume wake kwa hakika ameshapotea upotevu ulio wazi”

Kwa hivyo hii ndio sifa ya wenye imani Kisheria, ya kua wao hamuasi Allah na Mtume wake katika Amri zao na Makatazo yao, na wamufunga khiyari zao kwa Allah na Mtume wake katika kila Jambo linalotoka kwao.

Ama wale waliokubali Ahadi kisha hawakuitimiza katika Imani zao kwa kuyapinga yaliyokua na haki ya kukubalika, au wakayakubali katika Imani zao lakini Wakadharau katika Matendo yao; hawa wote ni WANAFIKI, na mfano wao ni wale waliokubali Uislamu katika Ulimi tu lakini katika itikadi yao wao wanaukataa Uislamu, na kuupinga, na wengine ni wale waliokubali Uislamu na kuikubali ahadi waliyoitoa ndani ya nyoyo zao lakini ahadi ile hawaitekelezi katika vitendo vyao kwa mfano wao Hawasali au wanapuuza baadhi ya vipindi, au wanalewa, na mfano wa hayo katika kila Amri ya Allah au Mtume wake (s.a.w) wao hawaifanyii kazi, na katika kila katazo la Allah au Mtume wake (s.a.w) wao wanaliingia na kulifanya hali ya kua wanaitakidi kua wao wanamuasi Allah na Mtume (s.a.w). Hawa wote ni wanafiki amesema Allah katika kuwaondoshea sifa ya Imani watu wa aina hii:

ويقولون آمنا بالله وبالرسول وأطعنا ثم يتولى فريق منهم من بعد ذلك وما أولئك بالمؤمنين

Nao wanasema tumemuamini Allah na  Mtume na Tumetii kisha wanayapa mgongo (wanayapuuza hayo) kundi katika wao baada ya hayo (waliyoyasema) na haiwezekani  hao (waliyoyapuuza) kua ni Waumini”

Pia amesema Allah mtukufu:

كذلك حقت كلمة ربك على الذين فسقوا أنهم لا يؤمنون

“Namna hiyo inakue ni Haki Neno la Mola wako juu ya wale wanaoasi kua Hakika wao sio wenye Kuamini”

Na vile vile amesema Mtume (s.a.w):

آية المنافق ثلاث: إذا حدث كذب وإذا وعد أخلف وإذا اؤتمن خان

Dalili za Mnafiki ni tatu: Ikiwa atasema anakua ni Muongo, anapoahidi anakwenda kinyume, na anapoaminiwa anafanya khiana” Anasema mwanachuoni Ibn Hajar: Hakika asili ya kufuata dini inavyotakiwa ni katika mambo matatu tu: Maneno, Vitendo, na Nia; basi Mtume (s.a.w) anaonyesha kuharibika kwa Maneno kutokana na uongo, na kuharibika vitendo kutokana na Khiyana, na kurabika kwa Nia kutokana na Kwenda kinyume na ahadi”.

Ndugu yangu; kutokana na haya yote utagundua kua mtu yoyote yule hatokua nje ya moja katika makundi matatu: Ima atakua ni MUUMIN, au atakua ni MFAFIKI, au atakua ni MSHIRIKINA, na wewe tayari umeshamjua MUISLAMU, na kua hutobabaika kusema kua MUUMIN na MNAFIKI ni WAISLAMU, sasa bado hujamjua ni nani KAFIRI? Lakini kabla ya kuingia katika mlango huo faidika na Aya hii tukufu inayozungumzia makundi hayo matatu ya watu:

ليعذب الله المنافقين والمنافقات والمشركين والمشركات ويتوب الله على المؤمنين والمؤمنات وكان الله غفورا رحيما

Ili aadhibu Allah Wanafiki wa kiume na Wanafiki wa Kike, na Washirikina wa Kiume na Washirikina wa Kike na Asamehe Allah juu ya Waumini wa kiume na Waumini wa Kike na Amekua Allah ni Mwingi wa Kusamehe na Mwingi wa Kurehemu”

UHAKIKA WA UKAFIRI

KAFIRI ndugu yangu -katika msimamo sahihi usiokua na doa- ni kila anayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa Kosa kubwa mpaka atubie, ikiwa hakutubia atabakia katika Hukumu yake hiyo hiyo kua yeye ni Kafiri, ili uyafahamu vizuri mafundisho haya inakufaa usome kwanza neno la Allah:

هو الذي خلقكم فمنكم كافر ومنكم مؤمن والله بما تعملون بصير

Yeye ndiye aliyekuumbeni katika nyinyi ni Kafiri na katika nyinyi ni Muumin, na Allah kwa munayoyafanya ni mwenye Kuyaona”

Aya hii imewagawa watu sehemu mbili tu Ima KAFIRI au MUUMIN, pia inafaa kusoma neno lake Allah mtukufu:

إنا هديناه السبيل إما شاكرا وإما كفورا

Hakika sisi Tumemuongoza Njia Ima atakua mwenye kushukuru au atakua ni mwenye kukufuru” Unaona hakuna sehemu ya tatu, kwa hivyo Mtu yeyote yule ima atamshukuru Allah kwa kuzitumia Neema za Allah katika maridhawa yake, au atakufuru kwa kumuasi Mwenyezi Mungu kutokana na kuzitumia Neema zake katika makasiriko yake, basi uhakika huu ameueleza Allah katika aliyoyasema Mja wake Mwema Mtume Sulleiman (a.s):

هذا من فضل ربي ليبلوني أأشكر أم أكفر ومن شكر فإنما يشكر لنفسه ومن كفر فإن ربي غني كريم

“Hizi ni katika fadhila za Mola wangu, ili kunifanyia mimi mitihani ya kua nitamshukuru au nitamkufuru; Na mwenye kushukuru hakika anashukuru kwa ajili ya nafsi yake na mwenye kukufuru hakika Mola wangu ni Mkwasi {aliyejitosheleza} mwingi wa kukirimu”

Na maana ya ukafiri katika maneno haya ni kuzitumia zile neema za Allah kinyume na kuridhia kwake tu, sio Ushirikina.

Basi hii ndio maana sahihi ya UKAFIRI, kutokana na mfumo huu sahihi utaona kua kama ilivyokua Uislamu umekusanya Waumini na Wanafiki, basi vile vile Ukafiri umekusanya Washirikina na Wanafiki, kwa hivyo kila Mshirikina ni Mkafiri na sio kila Mkafiri ni Mshirikina. Basi neno la Ukafiri likitumika ifahamike kua ni kumuasi Allah tu katika Amri au Makatazo yake yaliyomo katika kitabu chake au yaliyothibiti ktoka kwa Mtume wake, isipokua ikiwepo ishara ya Uwazi kua aliyekusudiwa katika Maneno hayo ni Mshirikina ndio itachukuliwa maana hiyo kwa sababu Ushikina ni kumuasi Allah vile vile, na Mshirikina ni yule anayeirudi na kuikataa hukumu ya Mwenyezi Mungu isiyokua na shaka ndani yake, kwa mafano mtu hasali na huku anapinga kwa kusema “hakuna sala” na mwengine anaabudu sanamu hali ya kua Allah amekataza kumfanyia ibada asiyekua yeye, na ibada haiwi  kwa kuukubali Uungu kwa njia ya Ushirikishaji au kwa kukubali sifa miongoni mwa sifa za Kiungu kwa njia ya kushirikisha, kwa hivyo anayefanya hivyo haiwezekani isipokua yeye ni Mshirikina kwani ameirudi na kuipinga Amri ya Mwenyezi Mungu.

Huenda mtu akasema nini unasema kuhusu neno lakeAllah mtukufu:

إن المسلمين والمسلمات والمؤمنين والمؤمنات والقانتين والقانتات والصادقين والصادقات والصابرين والصابرات والخاشعين والخاشعات والمتصدقين والمتصدقات والصائمين والصائمات والحافظين فروجهن والحافظات والذاكرين الله كثيرا والذاكرات أعد الله لهم مغفرة وأجرا عظيما

Hakika Waislamu wa Kiume na Waislamu wa Kike, na Waumini wa Kiume na Waumini wa Kike, na Wanyenyekevu wa Kiume na Wanyenyekevu wa Kike,  na Wakweli wa Kiume na Wakweli wa Kike, wenye khushui wa Kiume na Wenye khushui wa Kike, na Wenye kutoa Sadaka wa Kiume na Wenye kutoa Sadaka wa Kike,                                                                                                                                                                                na Wenye kufunga Wa kiume na Wenye kufunga wa Kike, na Wenye kuhifadhi Tupu zao wa kiume na Wenye kuhifadhi wa Kike, na Wenye kumtaja Allah kwa Wingi wa  kiume na wenye kumtaja wa kike, Ameandaa Allah kwa ajili yao usamehevu na Malipo makubwa”

Kwa sababu katika neno hili inaonekana hukumu ya Wazi kua Waislamu pia wamo katika mafanikio makubwa aliyoyaandaa Allah kwa ajili ya Waja wake?

Jawabu:

Katika Aya hii na mfano wa hii, waliokusudiwa ni wale Waislamu waliotimiza ahadi ya Allah kama inavyotakiwa, kwani wewe huoni kua hizo zilizotajwa hapo ni Sifa wanazotakiwa kuwa nazo hao walioandaliwa Usamehevu huo na Malipo hayo Makuu, kwa hivyo aneyetimiza sifa hizo ndie huyo aliyeandaliwa hayo, hii ni jawabu kwa upande mmoja, na kwa upande mwengine tunasema sisi tuliposema kua Mnafiki anaitwa Muislamu tulikusudia kwa Mujibu wa Lugha, basi vile vile huyu Mnafiki kumwita Muumini kwa kujibu wa Lugha hakuna Matatizo, Ama kwa Mujibu wa Uhakika wa Kisheria Mnafiki hawezi kuitwa Muumini wala Muislamu, bali yeye ni Mnafiki, Mpotovu, Muasi, Kafiri, lakini hatuwezi kumwita Mshirikina ifahamike vizuri. Na haya tunayoyaeleza wameyaona Wanachuoni wa Kiibadhi, na mfano wa Aya hiyo ni lile neno lakeAllah mtukufu:

ياأيها الذين آمنوا اتقوا الله حق تقاته ولا تموتن إلا وأنتم مسلمون

Enyi mulioamini muogopeni Allah haki ya kumuogopa, na wala musije mukafa isipokua na nyinyi ni Waislamu” Basi tunaona katika Aya hii kua wanahutubiwa Waumini, kisha wanaambiwa kua kufa kwao kusije kua nje ya Uislamu tu, na sisi tumesema kua kinyume cha Uislamu ni Ushirikina, kwa hivyo inafahamika kua wao wasije wakaritadi tu na kuingia katika Usirikina, na hata kama wakiondoka Duniani na wao ni Wanafiki kutakua hakuna Tatizo juu yao, kwa sababu sifa ya Uislamu itakua ipo juu yao; tunasema kua Ufahamu huo ni Batili na usije ukapata nafasi katika akili ya Muislamu wa kweli, na kutokana na Aya hii Wanavyuoni wa Kiibadhi wako waliosema kua Hakuna Tofauti Baina ya Uislamu na Imani kwa hivyo Waumini ndio Waislamu, na wako waliosema kua hapa wanakusudiwa wale Waislamu waliotimiza Ahadi yao -kama tulivyoeleza hapo mwanzo- kwa hivyo Maana ya Aya hiyo ni kua Wao tayari wameshaipata Sifa hiyo ya Imani katika uhai wao huu wa Duniani, kwa kua kwao Waislamu wa Kweli, basi waendelee katika njia hiyo ya haki mpaka katika mwisho wa Maisha yao, nao wamo katika hali ya kuondoka Duniani na huku ni Waislamu wa kweli kama walivyokua. Na misimamo yote miwili haina tatizo kwa sababu tofauti ni katika matamshi tu ama kiuhakika hakuna tofauti baina yao, na mimi naona kua zote mbil –Imani na Uislamu- ni sifa za mtu mmoja kwa Maana Muumini ni Muislamu na Muislamu na Muumini wala hakuna tofauti, na kua Mnafiki wala Mshirikina hawezi kua na sifa yoyote katika hizo mbili mpaka Atubie, kwa hivyo Kafiri hawezi kuitwa kwa moja katika sifa hizo mbili, na kila msomaji azinduke nimesema Sifa na sio Jina; na hili ni la Haki katika tuliyoyaeleza huko mwanzo, kwa sababu hawa wanaelezewa vipi wanatakiwa wawe katika hali ya Kufa kwao, kwani mja anapoondoka katika uhai huu anaingia katika hukumu ya Uhakika wake kwa yule ambaye hakifichiki kitu upande wake, ama sisi waja baina yetu tunahukumu kwa mujibu wa Dhahiri ilivyo upande wetu tu, na Allah anayajua uhakika wa Nafsi. Na wewe ukiisoma Qur-ani na mafundisho sahihi yanayotoka kwa Mtume (s.a.w) katika ufahamu huu wa Sheria utaona uhakika wa maana zake zisizoweza kugongana na kupingana aslan, na mifano ni mingi.

UKAFIRI KATIKA MAFUNDISHO YA MTUME (S.A.W)

Na kabla ya kuuhama mlango huu inafaa tuweke dalili zinazothibitisha Ukafiri wa wanaofanya makosa makubwa, na dalili hizo tutazitoa katika mafundisho sahihi ya Mtume (s.a.w) ili liwe wazi zaidi suala hili:

Katika Sunna  ya Mtume (s.a.w) ziko dalili nyingi sana na sisi tutachukua baadhi tu ili kukinaisha kua Maibadhi wamechukua hukumu hii  katika misingi ya Sheria:

Neno lake Mtume (s.a.w)

سباب المسلم فسوق وقتاله كفر

“Kumtukana Muislamu ni ufasiki na kupigana nae ni Ukafiri”

Tunaona wazi hapa kua kumpiga Muislamu vita vya kumuua ni ukafiri. Nalo ni kosa kubwa ambalo Allah ameliharamisha na Mtume (s.a.w) pia ameliharamisha isipokua kumuua Muislamu kwa haki.

Neno lake Mtume (s.a.w)

لا ترجعوا بعدي كفارا يضرب بعضكم رقاب بعض

“Musirejee baada yangu Makafiri wanapiga baadhi yenu shingo za wengine”

Tunaona hapa kua Mtume (s.a.w) anahukumu kupigana Waislamu wao kwa wao ni ukafiri kwani ni kumuasi Allah mtukufu.

Neno lake Mtume (s.a.w)

ليس بين الرجل والكفر إلا تركه الصلاة

“Hapana baina na mtu na ukafiri isipokua kuacha kwake sala”

Na hapa pako wazi kabisa kua kuacha kusali ni ukafiri, na sio kupinga kusali, kwani kupinga ni kosa jengine hilo, nalo linamuingiza aliyenalo katika Ushirikina, kwani anaepinga hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w) atakua ni Mshirikina kama tulivyobainisha.

Neno lake Mtume (s.a.w)

العهد الذي بيننا وبينهم الصلاة فمن تركها فقد كفر

“Ahadi iliyopo baina yetu na baina yao ni Swala basi mwenye kuiacha Swala ameshakufuru”

Na hapa ni kama hadithi iliyopita.

Neno lake Mtume (s.a.w)

لا ترغبوا عن آبائكم فمن رغب عن أبيه فقد كفر

“Musiwakatae Baba zenu na mwenye kumkataa Baba yake ameshakufuru” Na hapa tunaona wazi kua kumkataa baba ni ukafiri na wala sio Ushirikina.

Neno lake Mtume (s.a.w)

ليس من رجل ادعى لغير أبيه وهو يعلم إلا كفر ، ومن ادعى قوما ليس له فيهم نسب فليتبوأ مقعده من النار

“Hakuna mtu atakaye dai asiyekua Baba yake na yeye anajua isipokua atakufuru, na mwenye kudai kua yeye ni katika watu Fulani, naye hana kwao nasabu basi ajitafutie makazi yake motoni”

Basi na hapa tunamuona Mtume (s.a.w) anatuambia kua mwenye kujinasibisha na Baba asiyekua Baba yake na yeye anajua basi huyo ameshaingia katika Ukafiri, na anayejiingiza katika ukoo usiokua wake ajiwekee kabisa pahala pake katika moto. Nayo ni kusema ikiwa hakutubia yeye ni kuni ya moto tu Allah atueke mbali na Adhabu ya Motoni (Amin).

Neno lake Mtume (s.a.w)

أريت النار فإذا أكثر أهلها النساء يكفرن،قيل أيكفرن بالله؟ قال: يكفرن العشيرة ويكفرن الإحسان، لو أحسنت إلى إحداهن الدهر ثم رأت منك شيئا قالت: ما رأيت منك خيرا قط

Nimeoneshwa moto nikaona wengi wa motoni ni wanawake kwani wanakufuru” ikasemwa: Wanamkufuru Mwenyezi Mungu? Akasema: Wanakufuru unyumba na wanakufuru hisani, ikiwa utafanya wema kwa mmoja wao kwa miaka yote kisha akaona kwako kitu atasema: sijaona kwako kheri hata mara moja”

Na hadithi iko wazi kabisa kwani Mtume (s.a.w) ameulizwa: jee!! wanamkufuru Mwenyezi Mungu? na yeye akasema: hapana bali wanakufuru unyumba na wema wa waume zao, nazo ni neema za Allah alizozijaalia kua ni Haki ya Mke juu ya Mume wake.

Hizo zilikua ni baadhi ya Dalili tu zinazoonyesha kua makosa makubwa yasiyokua ya Kishirikina yote ni Ukafiri, kwa hivyo anayeyafanya atakua ni Kafiri vile vile. Na kutokana na Haya Ukafiri umegawika Sehemu mbili Ukafiri wa Kinafiki, na Ukafiri wa Kishirikina.

KUMJUA ALLA MTUKUFU

ALIYEUMBA

Kumjua Allah aliyeumba ni jambo muhimu sana katika Uislamu, kwa sababu Allah ndie Mwenyezi Mungu ambaye anatakiwa kuabudiwa kwa haki, na waungu wote wengine wanaoabudiwa ni Wa battili bali sio Waungu kiuhakika, na sisi kuwaita Waungu katika maneno haya ni kwa maana ya Madai yao, au kwa Maana ya kuelekezewa Ibada, kama ilivyo katika Aya nyingi za Qur-ani, -uyafahamu haya vizuri-. Kwa hivyo anatakiwa kila Muislamu amjue Allah. Na pindi  anapoulizwa Allah ndio nini? Muislamu anatakiwa kujibu kua: Allah ni jina la yule aliyeumba kila kitu, asiyekua na mwanzo wala mwisho, kuwepo kwake ni kwa lazima, yeye ni mkamilifu wa dhati”, Allah huyu tunamjua kwa utukufu wake na sifa zake zilizokamilika, wala haiwezekani kumjua kwa sura Fulani au jengo Fulani, kwa hivyo Muislamu anatakiwa azijue sifa za Mola wake, na kua lazima Allah atasifika na kila sifa kamilifu, na italazimika kua mbali na kila sifa pungufu.

Sifa za Allah haziwezi kufanana na zile za viumbe wake kwa hali yoyote ile, kwa sababu sifa zote za viumbe zina Upungufu wa kutegemea, na tayari yeye ametuambia kua:

ولم يك له كفوا أحد

“Na hakuna aliyesawa na yeye hata mmoja”

Pia amesema:

ليس كمثله شيء

“Hakuna mfano wake kitu chochote”.

قل الله خالق كل شيء

“Sema Allah ndie Muumbaji wa kila kitu”

Na amesema Mtume (s.a.w):

كان الله ولا شيء معه

Alikua Allah wala hakuna kitu pamoja na yeye”

Pia amesema (s.a.w):

كان الله ولا شيء غيره

Alikua Allah wala hakuna kitu kisichokua yeye”

Kwa hivyo huu ndio msingi wa kumtakasa na kila sifa ya kiumbe au na kila sifa inayopelekea yeye kufanana na kiumbe chake chochote kile, Basi sifa zake ni kujuilisha na kuitakidi ukamilifu wa Dhati yake, kutokana na msingi huu muhimu Maibadhi wao wanaitakidi kua Sifa zote za Allah ni za Dhati yake na sio kitu chengine ambacho kiko nje ya Dhati yake, basi wao wanasema Allah anajua kwa Dhati yake, au Allah anajua kwa Elimu yake ya Kidhati sio kitu chengine kisichokua Dhati yake, wanasema pia: Yeye ni muweza kwa Dhati yake, na yeye ni hai kwa Dhati yake, na yeye ni mwenye kusikia kwa Dhati yake, na mwenye kuona kwa Dhati yake, na namna hivi kila sifa inajuilisha ukamilifu wa Dhati yake tu, Uoni wake ni wa dhati, Usikivu wake ni wa Dhati, Uwezo wake ni wa Dhati, Uhai wake ni wa Dhati, Usemi wake ni wa Dhati, Kutaka kwake ni kwa Dhati, Hekima yake ni ya Dhati, na vyote hivyo anasifika navyo kwa njia ya Ukamilifu wa Dhati yake na sio kama tunavyosifika sisi katika sifa hizo au kama hizo, kwa sababu sisi tunasifika kwa njia ya Kutegemea Sifa, kwani Sifa za Viumbe ni vitu vyengine sio Dhati zao, na Allah hawezi kusifika kama wanavyosifika Viumbe wake, kwa sababu Allah hajafanana na yeyote katika Viumbe wake. Hakuna yeyote asiyekua Allah isipokua kuwepo kwake si lazima kwa sababu atakua ni kiumbe alikua hayupo, na kuwepo kwake kunategemea Uwezo wa Dhati wa Allah mtukufu.

Sisi viumbe tunazo sifa nyingi sana kama vile Elimu, Kuona, Kusikia, Kutaka, Kujua, Kusema, Uhai na nyenginezo, lakini sifa zote hizo tulikua hatunazo, ikiwa ni Elimu ni kitu chengine sio Dhati yetu, ikiwa ni Uhai ni kitu chengine sio dhati yetu, ikiwa ni Uwezo ni kitu chengine sio dhati yetu, na namna hii, kila sifa tuliyonayo ni kitu chengine sio dhati yetu, bali tunategemea sifa hizo, na zinaweza kuondoka wakati wowote ule, Basi Allah hajafanana na sisi yeye sifa zake ni za Dhati, kwa maana Dhati yake emekamilika kabisa haihitaji chochote kile, kutokana na ukamilifu wake ndio ikalazimika kusifiwa na kila sifa kamilifu Kidhati, na kuwekwa mbali na kusifiwa na kila sifa pungufu, kwa hivyo ukamilifu wa Allah hauna mwanzo, na ndio maana viumbe wake wanapotaka kumsifu wanalazimika kumsifu kwa Ukamilifu wa Sifa zake zinazobainisha ukamilifu wa Dhati yake. Na hapa inafahamika kwa uwazi kabisa kua kule kusifu kwetu ni jambo ambalo lilikua halipo, kisha likapatikana kwa kupatikana viumbe, ama Sifa za dhati ya Allah ni jambo la Dhati halina mwanzo kwa sababu ukamilifu wa Dhati ya Allah hauna mwanzo. Na hii ndiyo itikadi sahihi katika kuzijua Sifa za Allah, kwa sababu lau ingalikua sifa hizo ni kitu chengine ambacho sio Dhati yake Allah, ingalilazimika kitu hicho kua na mwanzo au kua hakina mwanzo, na ikiwa kitakua na mwanzo itakua Allah alikua hasifiki na moja katika sifa yoyote kwa sababu yeye hana mwanzo, sasa vipi itawezekana kuvipata vitu bila ya kupatikana sifa ya kuvipata vitu hivyo? na hapa itakua ni kufungua mlango wa kumtukana Allah aliyeumba tu, kwa sababu itakubalika kua alikuwepo na yeye ni Mjinga, na alikuwepo na yeye hana Uhai wala Uwezo, wala usikivu, wala sifa yoyote, na kusema hivi ni Kukufuru kukubwa kabisa, bali ni Ushirikina wa Kumtukana Allah aliyeumba. Allah ametakasika na hali kama hiyo. Na ikiwa sisi tutasema kua Sifa hizo vile vile hazina mwanzo bali Allah anasifika nazo tokea Azal (Azali ni kutokua na mwanzo) tutakua tumeingia katika jambo jengine zito sana na baya lisilokubalika ndani ya Sheria wala Akili, na jambo hilo ni kuitakidi kua hakuna Upweke kwa sababu Allah alikua yeye pamoja na sifa zake, na sio alikua na yeye ni mkamilifu wa sifa, na kuitakidi kua Allah alikua na vitu vyengine visivyo kua na mwanzo ni Ukafiri, bila shaka yeyote ile, kwa hivyo Uhakika wa sifa zake ni Dhati yake, kinyume na itikati hii ni makosa bila shaka yeyote ile. Huenda mtu akasema, ya nini sisi kuingia katika upekuzi kama huu? Huyo tunamjibu kua, imelazimika kuingia katika ufafanuzi huu kutokana na kuenea Upotevu katika kuzijua sifa za Allah, na kua atakavo fikia Mwanadamu katika kuzijua Sifa za Allah hawezi kutoka katika Fikra zake nje ya Hizi fikra tatu tu, peke yake, na katika hali kama hiyo –ikitokea- hatuna budi kushikamana na ile njia isiyokua na Doa la Battili ndani yake na inayokubaliana na ulazimisho wa Dalili za Yakini, kwa hivyo hapo ikatubidi tueke ubainisho huu katika kuzijua sifa za Allah aliyetuumba na Aliyeumba kila kitu, Allah atuongoze katika Haki (Amin).

JEE!! ALLA ANASIFIKA KWA SIFA ZA VIUMBE WAKE?

Kwa hakika haiwezekani kwa yeyote yule anayesoma kitabu cha Allah au akakubali kutumia Akili yake vizuri kabisa, akubali au afikie kua Allah anasifika na sifa za viumbe wake, hakika mtu akisema haya atakua amefanya makosa makubwa kabisa na kua yeye anaabudu kiumbe katika ufahamu wake katika njia ya kukipa Uungu, kwa sababu tayari zimesimama dalili zisizokua na shaka kua Allah hajafanana na kitu chochote kile, kisha vipi urejee umuweke yeye na kiumbe chake kua ni sawa katika sifa? Kutokana na haya ikalazimika kumtakasa Allah na kila sifa iliyoko katika viumbe wake, Kwa hivyo Allah hatuwezi kumsifu kua ana viungo kwa maana tunayoifahamu kwa sababu yeye hana umbo wala umbile; umbo na umbile ni sifa za viumbe na yeye hajafanana na yeyote katika viumbe wake, Allah ametakasika na kua na Macho, Mikono, Miguu, Masikio, Mdomo, Pua,Upande wa kulia au Kushoto, Sura, na kila sifa anayosifika kuimbe wake yeyote yule, hatuwezi kumsifu Allah kua anatembea, au anashuka, au yuko katika sehemu Fulani ikiwa ni Mbinguni au Juu ya kiti, kwa maana ya uhakika ya maneno hayo. Yote hayo haiwezekani kusifika nayo Allah aliyeumba, kwa sababu ni Sifa za Viumbe vyake na yeye hajafanana na kitu chochote kile, kama alivyosema, basi itakuwa ametakasika na sifa hizo hatika uhakika wake.

Tumesema hivi kwa sababu tuliyoieleza inayotoka katika kitabu chake kitukufu cha Qur-ani, mafundisho ya Mtume wake Mtukufu, na haya yanatiliwa nguvu na fahamu sahihi aliyo nao kila Muislamu, bali kila Mwanadamu katika Hali ya kufikiri kiusahihi kua Allah ndiye muumba aliyeumba kila kitu, na kua vitu vyote vina mwanzo isipokua yeye Aliyeumba peke yake, na haiwezekani kwa hali yoyote ile kuleta sifa hizo tukampa Allah mtukufu aliyeumba kisha ikawa hayumo katika sehemu, na sote tunakubaliana kua sehemu ni kiumbe kwa hivyo Allah yupo kabla ya kuwepo sehemu, kwa hivyo haiwezekani kusifika na sifa zinazolazimisha kuwepo sehemu ili zipatikane, kwa hivyo sifa hizo ni Batili haifai kuitakidi kua Muumba wa Viumbe wote anasifika na sifa moja katika sifa yeyote ile itakayolazimisha kukosekana Upweke wake au Ukamilifu wake, kwa hivyo achilia mbali kusifika na sifa hizo, bali hata kuuliza Suala linalohusu Sifa za Allah, ikiwa suala hilo limeulizwa kwa njia ambayo inalazimisha kuwepo sifa katika sifa hizo, itakua ni Batili. Kwa mfano mtu aulize: Allah yuko wapi? Hili suala ni Batili, kwa sababu ya lile neno “Wapi” ambalo linalazimisha Sehemu, na yeye yupo kabla sehemu, wala haiwezekani kusifika na sifa inayolazimisha yeye awepo hakika sehemu, kwa sababu kufanya hivyo ni kuvunja Upweke wake au kubadilisha uhakika wake na kila kinachobadilka ni kiumbe kwa sababu kubadilika ni sifa inayopatikana baada ya kukosekana.

UHAKIKA WA SIFA ZA KUSHABIHISHA.

Suala litakuja; Mbona tunaona Aya nyingi za Kitabu cha Allah Qur-ani, na Hadithi Sahihi kutoka kwa Mtume (s.a.w) zinazoonyesha Sifa hizo?

Jawabu:

Sisi tunakubali kua Aya hizo zipo na Hadithi hizo zipo, lakini Aya hizo na Hadithi hizo hazitoki nje ya Lugha ya Kiarabu, kwa hivyo zilitumiwa Sifa hizo kumsifu Allah mtukufu kutokana na vile inavyotumika Lugha ya Kiarabu, kwa sababu Allah mtukufu amesema:

وما أرسلنا من رسول إلا بلسان قومه ليبين لهم

Na wala hatukumtuma Mtume yeyote yule isipokua kwa Ulimi wa kaumu yake ili awabainishie wao”

Katika Aya hii kuna neno “Ulimi” na kila mmoja katika sisi anafahamu ni nini ulimi, kua ni kiungo kinachotumika katika Kujua Ladha ya vitu na pia kazi yake Kubwa ni Kusema, na kila mmoja anayesoma Aya hii anafahamu kua maana hii ya uhakika wa neno hili siyo iliyokusudiwa, kwa sababu maana hiyo inakataliwa na Akili, na Akili inalazimisha kulifahamu neno hilo kwa Maana la Lugha, na inapokuja maana hiyo ndio Aya italeta maana kamili isiyokua na shaka yeyote ile, kwa hivyo katika Aya hii tunapata mafunzo mawili:

Kua katika Kitabu cha Allah kunatumika Maneno kwa kukusudiwa Ufahamu unaoletwa na neno lile kwa Dalili na vielelezo  sahihi, na kuacha Maana ya Uhakika ya neno lile kwa sababu ya kuleta maana isiyowezekana.
Kua hii ndiyo Lugha ya Kiarabu, katika utumiaji wa maneno, kwa hivyo ikawa hakuna budi kutufikia maneno hayo katika mfumo wa Lugha yetu, kwa hivyo huu ndio mfumo wa Lugha ya Kiarabu, na Allah anasema katika kuisifu Qur-ani:

وهذا لسان عربي مبين

Na huu ni Ulimi wa Kiarabu uliowazi”

Na hii ni dalili tosha ya kuyachukua Maneno ya Qur-ani kwa mujibu wa utumiaji wa Lugha ya Kiarabu.

Tanbiih:

Haya tunayoyasema hapa inaweza kuja fikra ya kua sasa tunataka kusema: Kwa maana hiyo itakua ni uongo; hapana sio uongo, kwa sababu Allah ametuletea maneno kwa kufahamu maana yake, kwa mujibu wa makusudio ya yale maneno katika matumizi yake, wala sio kwa kuangalia uhakika wa yale maneno, kwa hivyo huyo anayesema kua ni lazima tushikamane na uhakika wa Maana za maneno ndie anayetaka kumtukana Allah kua anatuambia vitu vilivyokua haviwezekani Kiakili, kwa Mfano Allah anasema:

صم بكم عمي فهم لا يعقلون

Viziwi, mabubu,vipofu, na wao hawana Akili” Sasa zichukue sifa hizi katika uhakika wake kisha angalia ni nani waliopewa sifa hizi? Jee!!  wao wanazo katika uhakika wao baina yetu? kwa hivyo ukisema kua maneno haya yamekusudiwa Uhakika wake basi ni kusema kua Allah ni muongo, au hajui kupanga maneno, wala hana Hekima, kwa hivyo ni mjinga; na sifa hizo Allah ametakasika nazo, wala hawezi kua nazo Muumba wa mbingu na Ardhi na kila kitu kilichomo ndani yake; lakini kila mwenye Akili na msomi wa Lugha ya Kiarabu anafahamu kwa uwazi kabisa kua Uhakika wa Maana ya maneno hayo siyo unaokusudiwa, lakini maneno hayo yamekusudiwa kufananishwa hali yao kama hali ya wanaosifika na sifa hizo kiuhakika, kwa sababu wao hawanufaiki na chochote katika viungo hivyo katika kuijua Haki, na hivyo ndivyo inavyotumika Lugha ya kiarabu, na hata katika Lugha yetu ya Kiswahili sura kama hizo zipo, kwa mfano utamkuta mtu anampa mwenzake jina la Mnyama kwa mfano anamwita Simba, au Punda au mfano wa hayo, jee!! anakusudia uhakika wake? Ikiwa anakusudia uhakika wake basi kila mtu atamuona kua ni muongo au hana Akili, na sifa hizi haiwezekani kupewa mtu anayesema maneno hayo, kwa sababu sifa zote hizo hanazo, kwa hivyo tunafahamu sote kua yule aliyemwita Simba alikua anakusudia kua ni Shujaa, na yule aliyemwita Punda alikua anakusudia kua ni Mjinga. Na yote hayo yanajulikana kutokana na vielelezo ambavyo vimalazimisha Maana hiyo, na kupoteza neno maana yake ya asili.

Na kitu gani mtu atasema katika neno la Allah:

وما رميت إذ رميت ولكن الله رمى

Na hukulenga ulipolenga lakini Allah amelenga” Jee!! tutayachukua katika uhakika wake, itakua lazima utapatikana uongo ndani yake kwa sababu vitendo viwili tofauti vinaelezewa kutokea kwa mtu mmoja tena katika wakati mmoja, ni jambo lisilowezekana ni lazima ima vyote havikutokezea, au kimetokezea kimoja tu, kwa hivyo vyote itakua ni uongo au kimoja ni uongo, lakini unapochukua maana hiyo kwa vilelezo vinavyoleta maana yenye kukubalika na kuwekwa mbali maana ya uhakika ya maneno hayo, mush-kila huo unaondoka, na kielelezo kikubwa hapa ni uwezo wa Allah aliyeumba, kwa maana kitendo cha kulenga na Athari zake hazikua kwa uwezo wako lakini kwa uwezo wa Allah na Amri yake, tazama utamu unaokuja ndani ya Ufahamu huu sahihi wa maneno hayo ya mwingi wa Hekima!!.

Sasa baada ya kufahamu maelezo hayo mafupi tayari umeshatambua na kujua sababu zinazofanya Allah asiweze kusifika na Sifa zote zile zilizotajwa katika Kitabu chake au Katika Maneno ya Mtume (s.a.w) ikiwa sifa hizo zitapelekea kusifika Allah na sifa yeyote ile ya Upungufu, kama kuhitaji, ujinga, kushindwa, umauti, kudhulumu, upofu, uziwi, na mafano wa hayo katika kufanana na wengine.

MSINGI MUHIMU WA KUZIJUA SIFA ZA ALLAH

Na kabla sijakuacha katika maelezo yanayokuja ni vizuri kuchuku msingi muhimu ambao hauna shaka ndani yake nao ni:

KILA SIFA YA DHATI INAYOLAZIMISHA KUPATIKANA KITU CHENGINE KISICHOKUA DHATI YA MUUMBA ILI IPATIKANE SIFA HIYO YA DHATI BASI SIFA HIYO NI BATILI KUSIFIKA NAYO MUUMBA

Basi kamata msingi huu katika uhai wako wote, wala usibabaike utakaposikia neno lolote, na kamwe Muumba hawezi kujisifu nje ya uhakika wake, wala hawezi kua muongo katika maneno yake.

Tunamuomba Allah atufahamishe na awaongoze waliopotea waweze kumjua Mola wao aliyeumba kila kitu, na awawezeshe kufuata sheria yake tukufu, ili tuweze kufaulu sote kwa Pamoja kesho Akhera kwa kupata Bora ya Thawabu zake ambayo ni Kuridhiwa na yeye peke yake, na atuokoe na wao pamoja kutokana na Adhabu ya Milele motoni, kwa hakika anayeingia katika Adhabu hiyo hana Bishara tena, na atusafishe na kushikilia yasiyokua yake, na atuongoze sote katika Kumjua yeye, na kumuabudu haki ya Kumuabudu, na yeye ndiye muwezeshaji wa yote, na Rehma na Amani ziwe kwa Mtume wake (Amin)

UHAKIKA WA SIFA ZA ALLA ZINAZOFANANA

NA SIFA  ZA  VIUMBE WAKE.

Sifa hizo ima zitakua ni za maana kama vile kusikia, kuona, kujua, uwezo, uhai, kutaka, na elimu; sifa hizi kama tulivyosema kua ni za dhati yake, kwa maana dhati yake imekamilika wala haihitaji kitu chengine, kwa hivyo tukisema kua Allah anasifika na sifa ya kuona, tunakusudia kua hakuna cha kuonekana isipokua kipo wazi upande wake bila ya kuhitaji kitu chengine katika kuona huko, na tukisema kua na sifa ya kusikia tujue kua hakuna cha kusikilikana isipokua kiko wazi katika dhati yake bila ya kuhitaji kitu chengine katika kusikia huko, na tunaposema kua Anajua tujue kua hakuna kinachofichika katika elimu yake, na namna hii kila sifa inamaanisha ukamilifu wa Dhati yake.

Au sifa hizo zitakua ni za kumfananisha Allah na viumbe wake kama zile sifa za viungo: Mikono, Macho, miguu, upande wa kulia na kushoto, kutembea, vidole, mdomo, kukaa, kutembea na mfano wa hayo. Sifa hizi zote tunatakiwa kujua kua uhakika wake tunaoufahamu sio uliokusudiwa, kwa sababu tulizozieleza kua zinalazimisha kufanana Allah na viumbe wake, na jambo hilo amelikataa katika kitabu chake bila shaka yeyote ile, na vile vile ikiwa sisi tutamsifu Allah na sifa hizo tutalazimisha upungufu na kua Allah anasifika na kila sifa ya kuhitaji, na tutavunja lile neno la kua yeye hana aliyefanana naye, na kua yeye ndie Muumba na kila kitu ni Kiumbe, kwa sababu kama tulivyofafanua kua sifa hizo haziwezi kupatikana isipokua yale yanayolazimika kuwepo ili zipatikane yawepo pia, na huko ni kuvunja Upweke wa kuwepo kwake, na kuingia katika kushirikisha vitu vyengine katika Utangu wake, kwa  kua vitu hivyo pia havina Mwanzo na kuitakidi hivi na Ukafiri, na hii ndio Khatari ya Itikadi ya Mambo yaha au kama haya, kwa hivyo tujiepushe na kila fikra au mafundisho yatakayo tupelekea kuingia katika Itikadi ya Mambo yote ya kumfananisha Allah aliyeumba.

Sasa ikiwa hivi ndivyo mambo yalivyo itakua sisi hatuna njia isipokua mbili tu katika kujua uhakika wa Sifa hizo:-

Ni kujisalimisha kua sifa hizo hazijakusudiwa maana yake ya uhakika tunayoifahamu katika Akili zetu, na maana yake iliyokusudiwa hatuwezi kuijua kiuhakika kwa hivyo tunayaacha maneno hayo kama yalivyo, bila kuyafasiri kwa maana yoyote ile, na tunasema kua tumeamini kama inavyopasa kusifiwa Allah katika Ukamilifu wake bila kuitakidi maana yeyote ile na kukaa mbali na maana ya Uhakika ya maneno hayo, kutokana na Khatari ya kuitakidi kwake.

Na njia hii ina Khatari yake kwa sababu, asili ya maneno ni kubeba Maana, na Allah amatuelezea hizo sifa kwa maneno hayo, basi vipi atuambie maneno tunayoyafahamu bila ya kuyafahamu? Hakika njia hii hatuwezi kuikubali moja kwa moja bali njia ya pili ndiyo yanye kukubalika, kwa sababu kila chenye kupelekea katika Haramu nacho pia ni Haramu, na Allah ametukhutubia kwa Maneno yanayofahamika.

Ni kukubali vile vile kua maana za sifa hizo za uhakika hawezi kusifika nazo Allah aliyeumba, bali atasifika kwa maana iliyobebwa na sifa hizo katika kuhakikisha ukamilifu wa Dhati yake, kwa hivyo hapana budi kuichukua katika Akili zetu maana hiyo inayoletwa na vielelezo vinavyohakikisha ukamilifu wa Allah, kwa hivyo tunasema kua maana ya Sifa hizo ni kama ifuatavyo:

Amesema Allah mtukufu:

جنب الله

Uhakika wake kimaaana ni: Ubavu wa Allah”, na Maana yake iliyokusudiwa ni Amri ya Allah, au Haki ya Allah, yaani Maamrisho na Makatazo yake.

Katika hadithi[12]:

فيضع الجبار قدمه في النار فتقول قط قط”

Maana yake ya uhakika wa maneno: Ataweka Jabaar (sifa ya Uungu inayoonyesha Utukufu wake wa kushinda) mguu wake katika Moto, nao utasema: Nimetosheka nimetosheka” Unaona katika hadithi umetajwa Mguu wa Jabaar ikiwa tutachukua Jabaar kwa maana ya Allah, kwa mujibu wa kua ni moja katika Majina yake matukufu, basi itakua tayari yeye unampa mguu kiuhakika, kwa hivyo sifa hiyo hawezi kuwa nayo katika uhakika wake, na itabidi ichukuliwe ima kwa maana ya kua ni Kiumbe chake, au kwa Maana ya Amri mzito inayotoka kwake, na Waarabu wanatumia maana hii katika maneno yao, katika vita vyao, iwapo wameshinda wanasema kua tumweka Mguu wetu juu yao, kwa maana ya kuwadhalilisha Maadui zao kutokana na Ushindi tulioupata juu yao, na kuwatawala, na maana hii imekuja katika Aya ya Qur-ani:

يوم سكشف عن ساق ويدعون إلى السجود فلا يستطعون

Siku utakapoekwa wazi mguu, na wataitwa kwenye kusujudu nao hawataweza” Mguu hapa ni Mazito ya siku ya Kiama. Ama Hadithi hiyo tukiichukua kwa maana ya kila ayejivika sifa hiyo ya Uungu -yaani kila Dhalimu aliyejipa sifa za Uungu- aweke mguu wake katika moto, itakua hakuna matatizo katika ufahamu wa Hadithi hiyo na hii ndio maana inayokubalika na Aya za Qur-ani, lakini iko mbali na matamshi ya Hadithi.

Imekuja katika Hadithi:

إن قلب المؤمن بين أصبعين من أصابع الرحمن

Maana ya Hadithi: Hakika Moyo ya Muumini uko baina ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa Rehema” tukichukua maana ya uhakika ya maneno haya tutapata kua Mwenyezi Mungu ana vidole vingi, na moyo wa muumini upo baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole hivyo, na vidole kila mmoja wetu anavijua, ikiwa tutaitakidi maana hii ya uhakika ya neno kidole itakua tumempa Allah umbile na tumemfananisha na viumbe wake, na yeye hajafanana na kitu chochote kile kwa hivyo maana sahihi kwa mujibu wa ufahamu wa maneno hayo inabainika kua ni Uwezo wa Allah, kwa Maana Moyo wa Muumini umo katika Uwezo wa Allah anaufanya anavyotaka.

Amesema Allah:

ويبفى وجه ربك

Na utabakia uso wa Mola wako”

Na mesema:

كل شيء هالك إلا وجهه

Kila kitu kitaangamia isipokua Uso wake”

Tukichukua uhakika wa maneno yalivyo tutapata kua Allah ana Uso, na uso ni sehemu ya dhati yake, na kwamba vitu vyote vitaangamia mpaka yeye mwenyewe isipokua Uso wake tu, na maana hii haikubaliki kwa hali yoyote ile, kwa sababu italeta kila upungufu katika Dhati ya Allah aliyetakasika na kila Upungufu. Basi maana sahihi inayofahamika katika Lugha ya kiarabu yanaposemwa maneno hayo nikua Uso maana yake ni Dhati, nao wanasema: قصدت وجهك Nimekusudia Uso wako, kwa maana nimekukusudia wewe mwenyewe dhati yako.

Amesema Allah:

تجري بأعيننا

Inakwenda kwa Macho yetu” na anasema:

ولتصنع على عيني

Na ufanywe juu ya Jicho langu” Ukichukua maana ya uhakika tunayoifahamu katika neno Jicho, itakua Allah ana Macho na kua hiyo Jahazi ya Nuuh ilikwenda kwa Macho ya Allah, na kua Mtume Mussa (s.a.w) alitengenezwa juu ya jicho la Allah, itakua ni maana ya Ajabu sana isiyokubalika, lakini Waarabu wanatumia maneno kama hayo kwa Maana ya Hifadhi, wanamuambia mtu أنت على عيني  Wewe uko juu ya jicho langu” kwa maana Hifadhi yangu, kwa hivyo hii ndiyo maana inayokubalika katika ulimi wa Kiarabu.

Amesema Allah:

يد الله فوق أيديهم

Mkono wa Allah uko juu ya mikono yao”

Na pia amesema:

لما خلقت بيدي

Kwa niliyoumba kwa Mikono yangu miwili”

Pia anasema:

مما عملت أيدينا

Katika iliyofanyakazi Mikono yetu” Ukichukua maana ya uhakika tunayoifahamu katika neno Mkono, italazimika kua Allah anayo mikono hiyo, na huko ni kumfananisha Allah na Viumbe wake, lakini Waarabu -iliyoteremshwa Qur-ani kwa Lugha yao- wanayafahamu maneno hayo kua Mkono hapo ni kwa maana ya Uwezo, na hayo yote yanatiliwa nguvu zaidi ni lile neno lake Allah mtukufu:

إنما قولنا لشيء إذا أردناه أن نقول له كن فيكون

Hakika Neno letu kwa kitu tunachokitaka ni kukiambia Kua na hapo hapo kinakua” Na neno hilo “Kua” Linaonyesha kua kila kitu kinakua kwa Uwezo wa kutaka  kwa Allah tu.

Amesema Allah:

بل يداه مبسوطتان ينفق كيف يشاء

Bali mikono yake miwili iko wazi anatoa anavyopenda” tukiichukua maana ya dhahiri inayobebwa na neno hilo itakua Allah anayo mikono miwili na sifa hiyo ametakasika nayo Allah, lakini Waarabu wanapoambiwa maneno hayo wanafahamu kua inakusudiwa Ukarimu mwingi wa kutoa, na hapo kwa vile imetajwa mikono miwili inaonyesha Ukarimu uliotimia wa Allah mtukufu kwa waja wake kwa kuwaneemesha kwa Neema zilizokua Dhahiri na nyengine zimefichika. Na hii ndio maana sahihi inayotakiwa watu waifahamu.

Amesema Allah mtukufu:

وما قدروا الله حق قدره والأرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطويات بيمينه سبحانه وتعالى عما يشركون

Na hawajamkadiria Allah haki ya Ukadirio wake, na Ardhi yote ni fumbato lakesiku ya kiama, na Mbingu zitakunjwa kuliani kwake, ametakasika yeye na yuko safi na hayo wanayomshirikisha”

Katika Aya hii kuna maneno mawili:

1.      La kwanza “FUMBATO” na maana yake ikiwa wewe utatia mkono wako katika gunia la mchele kisha ukachukua ule mchele kwa kuubana katika Mkono wako ukautoa mkono huo hali ya kua umeubana vile vile, tunasema kua Mkono wako umefumbata Mchele, kwa hivyo maana hii haiwezekani kupatikana, kwa sababu tukileta maana hii tutaleta Sura kubwa sana kama ya Mtu, kisha ataikamata Dunia yote na kuifumbata katika Mkono wake, kama wewe unavyofumbata tonge ya ugali, na maana hii inaleta sura ndani ya kichwa na sura ni kitu, na yeye hajafanana na kitu chochote kile kwa hivyo maana hiyo ni Batili, lakini Waarabu wanapoambiwa maneno haya au kama haya manafahamu kua ni Ushidi, Hukumu na Ufalme, kwa sababu Mtawala anaweza kusema: هذه الأرض في قبضتي Ardhi hii imo katika Fumbato langu” kwa maana ya Ufalme wake na hukumu yake. Kwa hivyo hii ndio maana sahihi inayotakiwa kuchukuliwa katika  vichwa vya Waumini, nayo ni maana inayokubaliana na ukamilifu wa Allah, kua Ardhi yote siku hiyo itakua katika Amri yake peke kaye, hakuna Khalifa wala Amiri, wala yeyote yule, ambao tumewazoea hapa Duniani.

2.      La pili “KULIANI KWAKE” na hapa ikiwa tutachukua udhahiri wake wa maneno, itakua Mbingu zote zitafungwa fungwa na kukunjwa kisha zitawekwa ima katika Mkono wake wa Kulia au katika Ubavu wake wa kulia, na tukichukua maana hii itatufanya tukamilishe ile sura ya mwanzo, na hapo itakuwa ni kupata Sura ile ile isiyowezekana kupatikana katika kumsifu Allah mtukufu. Lakini Waarabu yanapotwajwa maneno hayo wao wanafahamu kua ni Nguvu na Ushindi, kwa hivyo hii ndio Maana sahihi inayotakiwa kufahamika yanapotajwa Maneno hayo au kama Hayo.

Amesema Allah:

الرحمن على العرش استوى

Mwingi wa rehema juu ya Arshi ameungama”

Mwingi wa Rehema ni Allah, na Arshi ni kiti cha Enzi cha Ufalme, na Kuungama ni kukaa kwa kuenea; Tukichukua Uhakika wa Maneno haya tutaleta Sura ya Mungu aliyekaa juu ya kiti cha Enzi, hali ya kua Kiti hicho kimembeba, na maana hii haiwezekani kuileta katika kumsifu Allah, kwa sababu yeye hajafanana na kitu, lakini Waarabu wanaposema maneno hayo wahawana jengine wanalolifahamu isipokua ni Ukamilifu wa Utawala, kwa sababu kwao kiti cha Enzi ndio kitu kinachoashiria Ufalme, ikiwa yeye amekimiliki, atakua tayari amekua Mfalme, kwa hivyo Allah anatuambia kua Ufalme wote ni wake hakuna kitu kinachotoka katika Milki yake, na Hii ndio maana sahihi, kua Mwingi wa rahema ametawalia Ufalme wake wote anakuhumu anavyopenda, haulizwi kwa analolifanya.

Amesema Allah:

فلا يأمن مكر الله إلا القوم الخاسرون

Hajiaminishi na Njama za Allah isipokua ni Kaumu waliokhasirika” Unaona kua katika Aya hii Allah anafanya Njama, na ikiwa tutalichukua neno hili kwa maana yake ya Uhakika na dhahiri yake tutashabihisha Allah na Viumbe wake, lakini Waarabu wanaposomewa Maneno haya wanafahamu kua Njama hapa inakusudiwa “Adhabu”

Amesema Allah:

وجاء ربك والملك صفا صفا

Na amekuja Mola wako na Malaika Safu Safu” ikiwa tutachukua maana hii iliyo dhahiri, tutaleta Picha kua Allah anakuja na Malaika wako Safu nyingi sana katika Siku ya Kiama, lakini maana hii haiwezekani kukubalika kwa sababu ya kumshabisha Allah na Baadhi ya viumbe wake, na yeye hajafanana na kitu, kwa hivyo hapa inafahamika kua ni Kuja Amri ya Allah, katika Siku ya Kiama na Malaika wako safu safu. Na hivyo ndivyo wanavyotumia Waarabu maneno yao, kua kila sehemu iliyofika Amri ya Mfalme kua ameshafika Mfalme katika eneo hilo, la kila jambo linalofanywa kwa Amri ya  Mfalme kua amelifanya Mfalme jambo hilo.

Basi hivi ndivyo unavyotakiwa ufahamu na umtakase Mola wako, na Huu ndio msimamo wa Madhehebu ya Kiibadhi, katika kuzijua Sifa hizi, au kama hizi, kwa njia inayokubalika katika kusifiwa Muumba wa kila Kitu, na sio kwa njia ya kushabihisha.

Tunamuomba Alla atukinge na wasi wasi wa Sheitani, na atuweke mbali na fitina ziliziwakokota wengi katika Upotevu wa kumshabihisha Allah, na atuhuishe katika Itikadi ya kumtakasa na kila upungufu, na atuhuishe katika Kumuabudu yeye peke yake, na atufishe katika hayo anayoyaridhia, na atufufue katika Uoni wake, na Rehma zake, na atuongoze katika anayoyaridhia (Amin, Amin)

JEE!! ALLA MTUKUFU ATAONEKANA?

Hakika linapotajwa suala hili kila Mwenye kumjua vizuri Mola wake anapatwa na mshangao mkubwa sana, na kumjia suala katika Fikra yake, Hivi kuna Muislamu anaitakidi kumuona Allah Muumba wa Mbingu na Ardhi na kila kitu? Kwa kweli kuonekana Allah ni moja katika mambo ambayo hayawezekani Kiakili na Kunakili, ikiwa tutachukua maana ya Kuona kiuhakika ambayo sisi tunaijua, kama anavyouona mmoja wetu Mwezi, au Bahari, au Baba yake, au Mama yake, au anavyouona Mji wake, kwa maana ya kuona kwa macho, na sio kuona Kielimu, na hii ndio Maana ya Kuona inayojulikana na kila mtu. Basi kuonekana kwa Allah ni katika mambo ambayo haiwezekani kupatikana, sio kwetu sisi tu bali kwa viumbe wake wote, na sababu zilizopo ambazo zinabainisha kua Allah hawezi kuonekana, ambazo hazibakishi Shaka yoyote katika Fikra za mwenye kufikiri, kwa sababu haiwezekani kuonekana kisichokua na Umbile, na Allah ametakasika na Umbile, kwa sababu hakiwezi kuonekana Kisichokua na rangi na Allah ametakasika na Kua na Rangi, kwa sababu kakiwezi kuonekana kilicho kua hakipo katika sehemu, na Allah ametakasika na Sehemu, vingapi vipo katika Viumbe vyake ambavyo hatuwezi kuviona kama vile Roho, Hewa tunayovuta, Sauti tunayosema, Akili tunayofikiria, na vitu vingi tu, hatuwezi kusema kua kama hivi tunavyosema ni kweli, basi tayari tumethibitisha kua Allah tumemfananisha na vitu hivyo ambavyo hatuwezi kuviona kwa sababu vimeshirikiana katika sifa hiyo ya kutoonekana; hayo hayawezekani kwa sababu vitu hivyo vimefichika kwetu sisi tu, Ama Allah kwake yeye hakufichiki kitu, kila kitu yeye anakiona, kwa hivyo yeye anaviona viumbe vyake vyote, sasa utukufu wake na ukamilifu wake umetimia kwa sifa ya kutoonekana na viumbe wake, na kutokua na mfano na kiumbe chochote kile, na ikiwa ataonekana tayari ameshashirikiana na baadhi ya viumbe wake -amabao wanaonekana- katika sifa ya kuonekana.

Na isisemwe kua na sisi tutabadilika kesho Akhera, na kua Allah atatupa nguvu zaidi kuliko hizi tulizonazo, na kua huko itakua ni kinyume tabia yake na  hii tuliyoizoea hapa Duniani, kwa sababu sisi tunasema: Hii ndio maana ya kuonekana, na kama kuna maana nyengine sisi hatuijui, na sisi tunamtakasa Allah na hii maana tunayoijua Duniani na Akhera, kama kutakua na mabadiliko ya Maumbile huko Akhera kubadilika huko ni kwa viumbe tu, na hiyo ni sifa yao, kwani kila kinachobadilika ni kiumbe kwa sababu kubadilika ni kupatikana kitu kipya kilichokua hakipo, basi sifa hii ya Kubadilika ametakasika nayo Allah mtukufu yeye hawezi kusifika na sifa ya kubadilika, kwa hivyo tutakavyo badilika hatuwezi kufikia katika sifa yoyote ya Uungu katika mabadiliko yetu, au ikapelekea kubadilika Sifa miongoni mwa Sifa za Dhati ya Allah aliyeumba, na ndio maana tutakua ni wenye kuhitaji tu kwa Muumba wetu, kwa hivyo hatuwezi kuathiri kitu katika sifa zake, mabadiliko ni yetu sisi yanaathiri baina yetu tu na viumbe wengine, na kutoonekana ni sifa thabiti ya Allah na sifa yake haiwezi kuondoka kwa hali yoyote ile, kwa hivyo haiwezekani kuonekana na Viumbe wake.

Iwapo mtu atasema hayo yote ni miongoni mwa dalili za kiakili;  Jee!! zipo dalili ya hayo munayoyasema katika kitabu cha Allah Qur-ani na Sunna ya Mtume (s.a.w) iliyothibiti?

Jawabu:

Ndio haya tumeyasema kwa kutumia dalili za Kiakili, lakini kwanza ifahamike kua Dalili hizo tumezitoa kwa mujibu wa Roho ya Sheria ya Kumtakasa Allah na kila Sifa ya viumbe wake, na hayo yanapatikana katika neno lake pale aliposema:

ليس كمثله شيء

Hakuna kama mfano kitu”

Na Neno lake:

ولم يك له كفوا أحد :

Na wala hakuna aliyefanana na yeye”

Na ukitaka Dalili nyengine zinazothibitisha kua Allah haiwezekani kuonekana ni hizi zifuatazo:

Dalili ya kwanza:

Amesema Allah:

لا تدركه الأبصار وهو يدرك الأبصار وهو اللطيف الخبير

Hayamdiriki yeye Macho na yeye anayadiriki Macho na yeye ni Mpole mwenye khabari ya yote” Allah anajisifu katika Aya hii kua Macho hayamdiriki, na kudiriki kwa macho ni kule kuona kwake, wala hakuna maana nyengine inayoweza kukubalika katika maana ya kudiriki kwa jicho isipokua kuona tu peke yake, kwa hivyo kutokana na Aya hii inathibiti Sifa ya Dhati ya Muumba kua haiwezekani kuonekana, kwa hivyo kuiondosha Sifa hii tukufu ni kumtukana Allah, na pia ni kurejesha hukumu yake, na dalili inayoonyesha kua Kudiriki hapa ni kuona ni ile Hadithi aliyoipokea Imam Rabii (r.a) na Bukhari na Muslim kua Mas-ruuq alisema: Nilikua nimeegemea niko kwa Bibi Aisha; akasema Bibi Aisha: Ewe Baba wa Aisha matatu atayesema moja katika hayo amezua jambo kubwa sana kwa Allah; atakazua kua Muhammad (s.a.w) alimuona Mola wake amezua uongo mkubwa sana kwa Allah. Akasema Mas-ruuq: Nilikua nimeegemea nikakaa kitako vizuri kisha nikasema: Ewe Mama wa Waumini nisubirie wala usinifanyie haraka, je!! hakusema Allah mtukufu: Kwa hakika amemuona katika upeo wa juu ulio wazi, Hakika amemuona katika mashuko mengine” Akasema Bibi Aisha: Mimi ndio wa mwanzo niliemuuliza kuhusu Aya hizo Mjumbe wa Allah (s.a,w) na yeye alisema: Hakika huyo ni Jibrilu sijamuonapo katika Sura yake ambayo ameumbwa katika Sura hiyo isipokua mara mbili hizo, nilimuona akishuka kutoka Mbinguni, limeenea Umbile lake Kubwa baina ya Mbingu na Ardhi” Akasema bibi Aisha: Jee!! hujasikia kua Allah anasema:

لا تدركه الأبصار وهو يدرك الأبصار وهو اللطيف الخبير

Hayamdiriki yeye Macho na yeye anayadiriki Macho na yeye ni Mpole mwenye khabari ya yote” Tunaona Bibi Aisha (r.a) anatoa Dalili kwa Aya hii Tukufu na kuonyesha kushangazwa na hayo aliyoyajadili Mas-ruuq kama kwambwa hajawahi Mas-ruuq kuisikia Aya hiyo, ili iwe ni hoja ya kutosheleza kwake yeye ya kuamini kua Allah hawezi kuonekana hata na Mtume wake Muhammad (s.a.w) ambaye ndiye mbora wa Viumbe wake wote. Na wala haiwezekani vile vile kusema kua Aya imakataa kumuona Macho yote ya Waja wake kwa hivyo haipingi kumuona Baadhi ya macho ya Waja wake nayo ni ya Waumini peke yao; kwa sababu vile vile yakimuona Macho ya Baadhi ya viumbe wake hata kama ni mmoja tu, itakuwa tayari macho yamemdiriki, kwa hivyo sifa hiyo itakosekana, na vile vile atakua Allah ameshirikiana na viumbe wake wote katika sifa hiyo, kwa sababu hakuna kiumbe ambacho kinaonekana na Wote, au na Macho ya Wote. Kisha kusema maneno hayo kutapelekea vile vile kuzivunja sifa nyingi za Allah zilizokuja katika mfumo huo wa maneno, kwa mfano:

Allah amesema:

إن الله لا يحب المعتدين

Hakika Allah hawapendi wenye kufanya Uadui” Itakua Allah anawapenda Baadhi ya Maadui ambao tayari Uadui ndio sifa yao, sio kwa kuwapeleka katika toba kwani anayetubia kutokana na Uadui wake huyo hana sifa ya Uadui.

Amesema:

إنه لا يحب المسرفين

Hakika yeye hawapendi wanaofanya Is-rafu” itakua anawapenda wengine ambao kufanya Is-rafu ndio sifa yao.

Amesema vile vile:

والله لا يحب الظالمين

Na Allah hawapendi Madhalimu” itakua anawapenda Baadhi ya Madhalimu ambao wameshaandikwa kuwa wao ni Madhalimu.

Pia amesema Allah:

إن الله لا يحب كل مختال فخور

Hakika Allah hampendi kila wenye maringo na kujifakharisha” Itakua anawapenda baadhi yao ambao wao hiyo ndio sifa yao.

Aya zote hizi hazina tofauti na ele ya mwanzo ka sababu zote zimekuja kuthibitisha Sifa za Allah, na atakayesema kua anawapenda Baadhi ya hao wote uliowataja kwa kuwapeleka katika Toba, atajibiwa kua hao hawasifiki tena na Sifa hizo alizozitaja Allah katika Aya hizi kwa sababu ya kutubia kwao, na sisi tunazungumzia hawa ambao sifa hizo zimetajwa katika Aya hizo kua ni sifa zao.

Vile vile haiwezekani kusema kua Aya hii inahusu Maisha ya Duniani tu, kwa sababu Aya hii inathibitisha Sifa ya Allah, na Allah haathiriwi na mabadiliko yoyote yale kama Macho hayamuoni, basi hayawezi kumuona popote pale kwani hiyo ni sifa yake, kuiondosha haiwezekani, kwa hali yoyote ile. Na kwa uthibitisho wa haya pia tunaleta Aya nyengine zilizoko katika mfumo kama huo bila kuzisahau zile zote tulizozieleza hapo juu:

Amesema Allah:

لاتأخذه سنة ولا نوم

Haumchukue yeye kusinzia wala kulala” Itakua sifa hii ni katika Uhai huu wa Duniani tu lakini Akhera atakua hasifiki tena, na sifa hii, na hili hakuna anayesema bali kila Muislamu anaamini kua Sifa za Allah hazibadiliki ikiwa ni Duniani au Akhera.

Pia amesema:

ما اتخذ صاحبة ولا ولدا

Hajajifanyia Mke waka Mtoto” Ndio tuseme kua sifa hii ni hapa Duniani tu lakini Akhera atajifanyia Mke na Mtoto, na hakuna Muislamu anayeitakidi hivi bali wote wanasema kua Hiyo ni Sifa Ya Allah sawa Duniani na Akhera sifa yake haibadiliki.

Na mfano wa Aya hizi ni nyingi tu, ambazo katika kumsifu Allah hazina tofauti na ile iliyomsifu kua Macho hayamdiriki, kwa hivyo zote ni sifa za Allah Duniani na Akhera bila Kubadilika.

Dalili ya pili:

Amesema Allah mtukufu:

ولما جاء موسى لميقاتنا وكلمه ربه قال رب أرني أنظر إليك قال لن تراني ولكن انظر إلى الجبل فإن استقر مكانه فسوف تراني فلما تجلى ربه للجبل جعله دكا وخر موسى صعقا فلما أفاق قال سبحانك تبت إليك وأنا أول المؤمنين

Na alipokuja Mussa katika Miikati yetu, na akamsemeza Mola wake, alisema: Ee Mola wangu nionyeshe ikuangalie wewe” Akasema: Hutoniona, lakini angalia katika Mlima ikiwa utatulizana pahala pake huenda ukaniona, basi alipojitokeza Mola wake kwa Mlima aliujaalia kupasuka pasuka, na akaanguka Mussa kwa mshituko mkubwa, basi alipozinduka alisema Utakatifu ni wako, nimetubia kwako, na mimi ni wa Mwanzo wa Walioamini”

Aya hii tukufu inatufahamisha Wazi kua Allah hawezi kuonekana na Mussa (a.s), kutokana na lile neno lake Allah mtukufu “HUTONIONA” ikiwa ataonekana na Mussa (a.s) katika wakati wowote ule au pahala popote pale, itakua neno hilo halija ukweli ndani yake, kwa sababu neno hilo linakataa kupatikana Kitendo cha kuonekana Allah na Mussa (a.s) bila kufungwa na wakati wowote ule au pahala popote pale. Na ikiwa Mussa (a.s) ambaye ni Mtume wa Allah hatomuona Allah vipi aonekane na Waumini wa kawaida.

Na akitokezea mtu akisema kua bila shaka Mussa (a.s) alimuomba Allah aione Dhati yake, kama ilivyo katika Aya, sasa inawezekana Mussa (a.s) ambaye ni Mtume wa Allah awe hazijui sifa za Mola wake, hata aombe kitu kisichowezekana, basi Utume wake utakua na Faida Gani?

Jawabu:

Ni kua Mussa (a.s) alijua kua anaomba kitu kisichowezekana, na aliomba kwa makusudi, kutokana na Kaumu yake ambayo ilimuambia kua: Hatutokuamini wewe mpaka tumuone Allah wazi wazi” Kwa hivyo wao wanajua kua Mussa (a.s) ndio mbora wao, na yeye ni Metume wa Allah upande wao, ikiwa suala hilo halitowezekana kulipata yeye, basi bila shaka wao walio chini hawawezi kulipata, kwa hivyo aliomba ili kuwakatisha tamaa katika sharti yao waliompa Mtume wao kua kuamini kwao kutapatikana tu, iwapo watamuona Allah.

Haya tunayojibu kutokana na suala hilo yanatiliwa nguvu na Aya nyingi sana katika Kitabu cha Allah miongoni mwa Aya hizo ni zile zilizokuja kua Mtume Ibrahim (a.s), aliwatangazia kaumu yake mara tatu ikivipa Uungu vitu tofauti, mara ya kwanza Alisema alipoiona Nyota: Huyu ndie Mola wangu” Akiashiria ile nyota, Mara ya pili alisema maneno hayo hayo: Huyu ndiye Mola wangu” Alipouona Mwezi umetokeza, na mara ya Tatu aliongeza zaidi akasema: Huyu ndiye Mola wangu huyu ni mkubwa” alipoliona Jua likichomoza, baadae akitoa dalili kua haviwezi kua Waungu vitu hivyo kutokana na kule kupotea kwake; halafu tonamuona Allah anamsifu Ibrahim (a.s) katika kitabu chake akisema kua zote hizo zilikua ni Hoja alizompa Mja wake, basi ndio tuseme kua Ibrahim (a.s) alikusudia kuvipa Uungu vitu vile, na hamjui Mungu wa Haki na wala hazijui Sifa zake? Hapana lakini alikua anakusudia kusimamisha Hoja tu juu ya Umma wake na sio Kuamini yeye katika nafsi yake kua vitu vile ni Miungu; bila shaka inabainika kua ni njia tu aliitumia Ibrahim (a.s) ili asimamishe hoja juu ya Umma wake, basi vile vile Mussa (a.s) alijua kua Allah hawezi kuonekakana lakini alitumi njia hiyo ili asimamishe Hoja juu ya Kaumu yake, kua kitu hicho hakiwezekani kabisa kabisa. Kisha tukirejea katika kitabu cha Allah tunaona kua Allah amewashambulia watu wa Mussa (a.s) sana kutokana na kosa lao hili la kuomba kumuona Allah mapaka anamshushia Mtume wake Muhammad (s.a.w) neno lake:

يسألك أهل الكتاب أن تنزل عليهم كتابا من السماء فقد سألوا موسى أكبر من ذلك فقالوا أرنا الله جهرة

Wanakuomba Ahalul-kitabi uwateremshie juu yao Kitabu kutoka Mbinguni; kwa hakika walimtaka Mussa zaidi kuliko hilo, walisema Tuoneshe Allah kwa Uwazi” Basi tumuweke Mussa (a.s) kua sawa sawa na Kaumu yake na yeye pia alitaka kumuona Allah, hakika Akili haikubali jambo hilo, kwa hivyo Mussa (a.s) hakutaka kumuoana Allah, lakini alitaka kusimamisha Hoja juu ya Kaumu yake, kua hicho munachokitaka ni kitu kisichowezekana, kabisa tena mukate Tamaa zenu.

Wako watakaosema kua ikiwa haiwezekani kwa nini aliambiwa autizame mlima kama utatulizana sehemu yake basi ataweza kumuona Allah  vile vile, na kutulizana mlima ni jambo linalowezekana kwa hivyo kuonekana Allah vile vile inawezekana.

Jawabu:

Hawa ni kuwaambia: kua katika maneno yale vile vile kuna dalili isiyokua na Shaka kua kuonekana Allah ni jambo lisilowezekana na kukatisha tamaa katika kupata kumuona Allah, kwa sababu mlima ule haukuweza kutulizana pahala pake, na haiwezekani kwa hali yoyote ile mlima ule utulizane katika sehemu yake, kwa sababu Amri ya Allah imeshapita kua mlima ule upasuke pasuke katika wakati ule, na haiwezekani kubadilika jambo ambalo Allah ameshalihukumu, kwa sababu yeye hakosei na hakifichi kitu upande wake, na Amri yake haishindwi.

Wako watakao sema ni kwa sababu gani basi iliyomfanya Mussa (a.s) atubie kwa Allah na afikwe na yaliyomfika katika Adhabu?

Jawabu

Allah anajua zaidi, lakini alifikwa na hayo na ikabidi Atubie, kutokana na kule kuleta suala zito kama lile lisilowezekana kabisa kabisa, na kua suala lile limeshikana na Dhati Yake Allah mtukufu, na ili ipatikane jawabu mzito kwa kaumu yake, na kuondosha kabisa tamaa zao, na kuwaonyesha njia aliyopita Mtume wao kua hata yeye katubia, wala hajakusudia kosa, basi na wao waliokusudia hasa wanatakiwa kutubia mara moja, na kurejea katika itikadi sahihi inayotaka kumtakasa Allah na sifa ya kuonekana, na pia Mussa (a.s) alitubia kwa sababu alileta Suala bila ya Idhini, au kwa kuhisi kufanya Makosa, kutokana na yaliyomfika, na ndio kule kusalimu Amri maramoja ili iwe ni ulingano kwa Kaumu yake, kua yeye ni wa mwanzo anayeamini kua Allah awezi kuonekana, basi na wao wafuate baada yake. Na Aya hii inatufunza sisi tusifuate nyayo za Makafiri katika itikadi zao na tujisalimishe kwa Allah kwa mujibu wa Ukamilifu wake wa Sifa zake, bila kujitia Tamaa katika mambo wao walijipa tamaa kuyapata nayo haiwezekani kupatikana.

Dalili ya tatu:

Amesema Allah:

وما كان لبشر أن يكلمه الله إلا وحيا أو من وراء حجاب أو يرسل رسولا فيوحي بإذنه ما يشاء إنه علي حكيم

Na haiwi kwa Mtu kusemezwa na Allah isipokua kwa Wahyi, au kwa Nyuma ya pazia, au anatuma Mtume anampa Wahyi kwa idhini yake kwa anayoyataka hakika yeye ni Mtukufu Mwingi wa Hikima.” Na Aya hii iko wazi, kua mtu yeyote yule hatoweza kupata njia ya kusemeshwa na Allah isipokua katika njia hizo Tatu tu, wala kahuna ya nne iliyothibiti, na kutokana na mfumo wa maneno hayo, haiwezekani kupatikana njia ya nne, kwa hivyo kuthibitisha njia ya Kumuona Allah ni kutoka nje ya Maneno haya yasiyo kua na Doa lolote lile. Na hizi njia tatu ndio zinazotumika kwa Mitume (s.a.w) na kutokana na uwazi wa Aya hii ndio zitakazotumika Siku ya Kiama vile vile.

Dalili ya nne:

Aya zilizokuja kuwafedhehesha Makafiri na kuwakemea vibaya sana wale wote walioomba kumuona Allah ikiwa ni Ahlul-kita, au Washirikina, miongoni mwa Aya hizo ni hizi zifuatazo:

وقال الذين لا يرجون لقاءنا لولا أنزل علينا الملائكة أو نرى ربنا لقد استكبروا في أنفسهم وعتوا عتوا كبيرا

Na wamesenma wale wasiotaraji Makutano yetu, lau wangalishushwa juu yetu Malaika au tungalimuona Mola wetu; Hakika amejiingiza kibri katika nafsi zao na wamepindukia kupindukia kukubwa kabisa” Basi kuna sehemu katika Qur-ani iliyowakemea watu kuliko sehemu hii, na wewe unaona kosa lao lililowatia katika makemeo hayo ya Allah mtukufu, kisha Allah anawajibu baada ya Aya hiyo kwa kusema:

يوم يرون الملائكة لا بشرى يومئذ للمجرمين ويقولون حجرا محجورا

Siku watakayowaona Malaika, hakuna Bishara njema siku hiyo kwa Waovu na watasema: Mungu apishie mbali” Basi shauri yao wanathibitisha kuonekana Allah au uwezekano wa kuonekana, na hali ya kua kitabu cha Allah kiko wazi kabisa hakikuacha doa.

Wako watakao sema: Vipi mbona mumezisahau Aya za Suratul-Qiyamah, au hamukuziona?

Tunawajibu kua Aya za Suratul-Qiyamah hazina dalili ya kuonekana Allah, na Aya hizo ni hizi:

وجوه يومئذ ناضرة* إلى ربها ناظرة

Nyuso siku hiyo ni zenye kughara * kwa Mola wake zinaangalia” Na dalili ya wenye ulizo hilo hapa ni lile neno “Zinaangalia” Wao wanasema kuangalia maana yake ni kuona kwa maana zinamuona, kwa hivyo wakalifasiri neno kuangalia kwa maana ya kuona.

Jawabu:

Ndugu yangu kuangalia au kutizama sio kuona, kwa sababu tunaweza kusema tumeangalia lakini hatukuona, au tumetizama lakini hatukuona” haya maneno ni sahihi kabisa wala hayana doa ndani yake, lakini unaweza kusema tumeona hatukuona” inawezekana ikiwa maneno hayo hayatobeba maana moja lakini ikiwa yatabeba maana moja haiwezekani, Na kuangalia kuna maana nyingi katika Lugha, kwa mujibu wa maneno yalivyotumika, kwa mfano tunaweza kumuandikia Raisi:

السيد الرئيس نحن ننظر إليك

Bwana Rais sisi tunakuangalia wewe” au “Tunakutazama wewe” wala hakuna anayesema kua hapa ni maana ya kuona, bali sote tunakubaliana kua hapa inakusudiwa ni Kumtaraji yeye tu, na kusubiria fadhila zake” Basi Jee!! sisi tukiichukua maana hii katika kuifahamu Aya ile tutakua tuna makosa, kwa hakika kila anayeangalia kwa makini kisha akaiacha Akili yake ihukumu ataona kua hii ndio maana Hasa iliyokua Sahihi katika ufahamu wa Aya hiyo, hasa hasa tukiangalia mtirirko wa Aya hizo, kwani mtirirko huo unatuonyesha kua hali hiyo itapatikana katika siku ya malipo, kabla ya kuingia Peponi au Motoni, na tukiangalia vishindo vya siku hiyo ya Kiama utaona wazi kua waja wema watakua katika hali kubwa sana ya Kusubiri ni wakati gani itafunguliwa upande wao Milango ya pepo, furaha imewajaa katika nyoyo zao, na huku wantaraji wepesi katika Hesabu zao ili ziwe mzito Mizani zao, wanataraji Kukubaliwa Shafaa ya Mtume (s.a.w) upande wao. Baada ya kusoma haya sasa angalia Aya zilizofuata ili kahakikisha maana hii sahihi:

ووجوه يومئذ باسرة * تظن أن يفعل بها فاقرة

Na nyuso siku hiyo zitakunjana * Zitajua kua zitafikwa na livunjalo uti wa mgongo” kwa hivyo zile kule zinazoghara zinasubiria mazuri yanayotoka kwa Mola wao, na hizi huku zilizokunjana zinasubiria Adhabu, na maana ya nyuso katika Aya hizi ni Dhati sio hicho kiungo tunachokijua, na maana hii ndio inayotumiwa na Waarabu. Aya hizo vile vile zinabainishwa na Aya za mwisho za Surtu-Abasa amesema Allah:

وجوه يومئذ مسفرة * ضاحكة مستبشرة * ووجوه يومئذ عليها غبرة * ترهقها قترة

Nyuso siku hiyo zitanawiri * zitacheka zitachangamka * Na nyuso siku hiyo zitakua na mavumbi * giza totoro litazifunika” Basi haya ndio yasiyo kua na wasi wasi amabayo yanakubaliana na Aya zote za Qur-ani tukufu.

Wako watakaosema kua neno hili la kiarabu نظر linakua na maana ya kusubiri na kutaraji ikiwa halijafunganisha na herifi إلى ama likifunganishwa na herufi hiyo hapo halina maana nyengine isipokua ” kuona” tu, hasa hasa katika Aya tukufu amabyo inaonyesha kua kitendo hicho kinafanywa na Uso ambao ndio sehemu ya Macho, kwa hivyo maana yake itakua ni Kuona tu.

Jawabu:

Tunasema kua neno hili la kiarabu نظر linakuja kwa maana zote mbili ya Kuona na Kusubiri, katika hali zote mbili ya kuegemezwa na herufi إلى  na bila kuegemezwa na herufi hiyo, na Ushahidi ya haya umo katika Maneno ya Allah na Mtume (s.a.w) na pia yamekuja katika Ulimi wa Kiarabu:

1.      Amesema Allah: وإن كان ذو عسرة فنظرة إلى ميسرة Na ikiwa hali yake ni mzito basi ni kusubiria mpaka apate Wepesi” Hapa limetumika neno lile lile na Hii hapa ni Ms-dar kama wanavyosema na Mas-dar inafanya kazi ya Kitendo kwa makubaliano ya wote, na ile kule ni Ismu Faail, ya kitendo ambacho Mas-dar yake ni neno hili hapa نظرة, na zote zina Maana moja, kwa hivyo neno hilo ni moja limebeba maana nyingi, na sisi tutaijua maana iliyokusudiwa kwa mujibu wa vielelezo vilivyomo katika Maneno.

2.      Amesema vile vile:

إن الذين يشترون بعهد الله وأيمانهم ثمنا قليلا أولئك لا خلاق لهم في الآخرة و لا يكلمهم الله ولا ينظر إليهم يوم القيامة”

Hakika wale wanaonunua kwa Ahadi ya Allah na Viapo vyao thamani ndogo; Hao hawana sehemu ya kupata katika Akhera, wala hatowasemesha Allah, wala hatowaangalia ( au Hatowatizama) siku ya Kiama” Allah anasema kua hatowatizama (au hatowaangalia ) kwa tarjima nyengine, na kitendo ni kile kile, na kimetegemezwa na herufi ile ile, sasa ni nani anayesema kua Allah hatowaona Watu hao siku ya kiama? Hakuna anayesema hayo, lakini Waarabu wote na kila anayefahamu inavyotakiwa maneno haya wanajua kua maana iliyokusudiwa hapa kua Hatowarehemu wato hao, basi huku ndiko kuangaliwa na Allah Aliyeumba waja wake, kwa maana ya kutowarehemu, na sisi tukiangalia maneno haya inabainika kwa uwazi kabisa kua Mwenye uwezo akimwangalia Dhaifu maana yake ni Kumrehemu na kumsaidia, basi vile vile Dhaifu akimuangalia Mwenye uwezo inakuwa ni kutaraji na kusubiri Rehma zake na msaada wake, na haya ndiyo ambayo tutayaona katika maneno ya Waarabu katika dalili zinazofuata.

Amepokea Imam Rabii (r.a):

الإمام الربيع رحمه الله عن سفيان بن عيينة عن الأعمش عن أبي راشد أن مولاة لعتبة بن عمير قالت: إنما أنظر إلى الله وإليك” فقال لها: لا تقولي كذلك, ولكن قولي: إنما أنظر إلى الله ثم إليك”

Amipokea Imam Rabii (r.a) kutoka kwa Uyaina bin L-aghmash kutoka kwa Abi Rashid kua Mjakazi wa Ut-ba bina Umair alisema: Hakika Ninamuangalia Allah na wewe” Ut-ba akamuambia kumjibu: Usiseme namna hivyo, lakini sema: Hakika Ninamuangalia Allah kisha wewe. Na kuangalia katika maneno hayo haifahamiki isipokua Kutaraji na kusubiria kama alivyosema Mtaalamu mkubwa naye ni Mtungaji wa Kamusi la Kiarabu inayokubalika na Wanavyuoni wote لسان العرب naye ni Ibn Man-dhoor, amesema kwenye kitabu chake hicho:

ويقول القائل للمؤمَّل يرجوه: إنما ننظر إلى الله ثم إليك” أي: إنما أتوقع فضل الله ثم فضلك

Anasema Mwenye kusema kumwambia Mwenye kusubiria yeye anamtaraji: Hakika tunaangalia kwa Allah kisha kwako wewe” kwa maana: hakika Tunatarajia Fadhila za Allah kisha Fadhila zako”

Amesema Mshairi wa Mtume (s.a.w) Hassan bin Thabit:

وجوه يوم بدر ناظرات *  إلى الرحمن يأتي بالفلاح

Nyuso siku ya Badr Zinaangalia *  Kwa Mwingi wa Rehema alete Mafanikio” Jee!! Hapa tuchukue kua Zilimuona? Haiwezekani lakini maana yake Zinasubiria kwa Kutaraji mafanikio” Hivi ndivo walivyo fahamu, na ndivo Lugha inavyotumika, wala hakuna tatizo kikwa utamuomba Allah katika haja Zako kisha ukasema: اللهم إني أنظر إليك Ee!! Mola wangu Hakika mimi ninaangalia Kwako” Kwa maana ya kusubiri katika matarajio yako.

Dalili ya Tano:

Amepokea Imam Bukhari na Muslim na wengineo kutoka kwa Abi Mussa L-ash-ary kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s.a,w) kua alisema hivi:

جنتان من فضة آنيتهما وما فيهما, وجنتان من ذهب آنيتهما وما فيهما؛ وما بين القوم وبين أن ينظروا إلى ربهم إلا رداء الكبرياء على وجهه في جنة عدن”

Pepo mbili za Fidha vyombo vyake na yaliyomo ndani yake, na Pepo mbili za Dhahabu vyombo vyake na vilivyomo ndani yaki; na wala hapana baina ya Watu na baina ya Kumuangalia Mola wao isipokua nguo ya Kibiri chake juu ya Uso wake katika Pepo mzuri kabisa”

Katika hadithi hii haiwezekani kufahamu maana ya Neno Kuangalia isipokua kwa maana ya Kuona kwa sababu maana yoyote ile utakayoichukua haitakubalika na ufahamu wa Akili na itapingwa ufahamu huo, kwa hivyo Hadithi hii inatufahamisha kua kilichozuia kumuona Allah ni sifa yake ya Dhati inayoitwa Kibri[13], na Sifa za Allah haziwezi kuondoka wala kubadilika, na yeyote yule anayethubutu kuiondoa Sifa hiyo, kwanza huyo Asome tena Sifa za Mola wake, kisha ndio aseme hayo atakayosema, na hata akisema maneno yanayoleta maana ya kuondosha sifa hiyo, basi uhakika haubadiliki, na wako Wanavyuoni waliofanya hivyo, kwa sababu wao wanaitakidi kumuona Allah, hali ya kua Allah ametakasika na kuonekana, ikawa hawana budi walipofika katika Hadithi hii, kuondosha Sifa ya Dhati ya Allah inayoitwa Kibri, Allah atueke mbali na Elimu isiyofaa, na atuongoze katika Uongofu wake.

Dalili ya sita:

Ameipokea Imam Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Abi Mussa L-ash-ary kua alisema hivi:

قام فينا رسول الله صلى الله عليه وسلم بخمس كلمات:

1.        إن الله عز وجل لا ينام ولا ينبغي له أن ينام

2.         يخفض القسط ويرفعه

3.         يرفع إليه عمل الليل قبل النهار وعمل النهار قبل الليل

4.         حجابه النور – وفي رواية النار-

5.         لو كشفه لأحرقت سبحات وجهه ما انتهى إليه بصره من خلقه

Alisimama kwetu sisi Mjumbe wa Allah (s.a,w)  kwa maneno matano:

Hakika Allah mtukufu aliyetukuka halali wala haipasi kwake yeye kulala.
Anateremsha Uadilifu na anaupandisha.
Yanapandishwa kwake yeye matendo ya Usiku kabla ya Mchana, na Matendo ya Mchana kabla ya Usiku.
Pazia lake ni Nuru –na katika mapokezi mengine ni Moto-
Lau Pazia hilo lingalimueka wazi, ungaliunguza Utukufu wa Dhaki yake kila kilichofikiwa na Uoni wake katika viumbe wake.

Basi hadithi nyengine  ambayo haina wasi wasi, inaondosha kila Shaka kwa walionazo, kua lau angalikua Allah wa kuonekana kwa kuondoka sifa yake hiyo, basi Ungalimalizika Uungu na kupotea kila kiumbe, na hii ndio sifa ya Allah, Uungu wake umepatikana kwa Sababu ya Ukamilifu wake, na Hadithi iko wazi, ikiwa Duniani au Akhera, kwa sababu Popote pale patakapokua ikiwa ni hapa duniani au Akhera, Yeye ndie Mungu na waliobaki wote ni Viumbe, kwa hivyo hadithi iko wazi kwa njia ya Mfano usiokua na Shaka, kwa anayetaka hii ndio Haki.

Dalili ya Saba:

Amepokea Imam Muslim kutoka kwa Abi Dhar (r.a) Kua hakika Mtume (s.a.w) alipoulizwa kuhusu kumuona kwake Mola wake,alisema:نور أنَّى أراه Nuru vipi nimuone” Na hapa tunapata Dalili kua Mtume (s.a.w) aliona Nuru tu, ambayo alimtunukia Mtume wake Muhammad (s.a.w), na kua katika lile neno lake أنَّى أراه Vipi nimuone” ilikua ni kueka Mbali jambo hilo, na kuonesha Mshangao kuhusu Suala hilo, kwa hivyo hiyo ni Dalili tosha kua Allah hawezi kuonekana, kabisa kabisa.

Wako watakaosema: Munasema nini kuhusu zile Hadithi zinazithibitisha Kuonekana Allah, nazo ni Sahihi zimekuja kwa Njia Sahihi kabisa?

Jawabu:

Kwa hakika Hadithi hizo kwanza haziko katika Msingi unaotumika katika Kujenga Itikadi Juu yake, kwa sababu –hata kama zimehukumiwa kua ni Sahihi kwa njia ya Mapokezi yake- bado zipo katika fungu la AAHADIY, na Hadithi zote zilizomo katika Fungu hili hazifikii daraja ya Yakini ambayo ndio inayotumiwa katika kujenga Itikadi, kwa sababu Hadithi zilizomo katika fungu hili zinatupa Dhana tu, basi hadithi za Fungu hili zinatumika katika

kuthibitisha Matendo na hukumu zake, na humo ndimo zinamotumika hadithi zote zenye hukumu hiyo, na vile vile zinaweza kutumika katika kutilia nguvu jambo la Itikadi baada ya kuthibiti kwa njia isiyo kua na chembe ya shaka.

Hadithi hizo ikiwa tutazichukua kwa Udhahiri wake, zitakua ni Dhaifu bali zitaingia hata katika Fungu la Uzushi (الموضوع مخترع مصنوع), kwa sababu makubaliano ya Wanavyuoni wa Hadithi yamehukumu kua Hadithi, ikipingana na Qur-ani, basi Hadithi hiyo ni Dhaifu inawekwa Upande, Bali wamehukumu hata ikipingana na Hadithi iliyokua na Nguvu zaidi, basi Hadithi inaingia Doa na kutozingatiwa, amesema Mwanachuoni Muhammed Rashid Ridha, katika tafsiri Al-manaar:

وإذا كان من علل الحديث المانعة من وصفه بالصحة مخالفة راويه لغيره من الثقات فمخالفة القطعي من القرآن المتواتر أولى بسلب وصف الصحة عنه”

Ikiwa katika sababu za Hadithi zinazozuia, kusifiwa hadithi kuwa ni Sahihi ni kule kupingana Mpokezi wake na mwengine katika Wapokezi wenye kuaminika, basi kupingana kwake na Yasiyokua na shaka katika Qur-ani iliyopokewa kwa njia ya Wote kuna haki zaidi kuondosha sifa ya Usahii wa Hadithi hiyo”

Haya tuliyoyaandika, ifahamike pia kua Hizo Hadithi zinazothibitisha Kumuona Allah, zimepingana wenyewe kwa wenyewe, nyengine zinathibitisha kua Ataonekana kabla ya Kuingia Peponi, na nyengine zinathibitisha kua kuonekana kwa Mungu hakutokua isipokua katika Pepo, tena huko Peponi itakua ndio kitu cha mwisho kupatikana, nao wanadai kua itakua ndio Neema kubwa kabisa, basi Neema kubwa kabisa isitajwe katika Qur-ani kwa uwazi kabisa, bali hata kuashiria; wakati Neema ndogo ndogo zimetajwa kwa uwazi usioweza ukingiwa na Shaka yoyote ile.

Wako watakaosema: Sasa ile Aya ya Qur-ani inayosema

إنهم عن ربهم يومئذ لمحجوبون

Hakika wao kwa Mola wao siku hiyo ni wenye kuwekewa Pazia” mumeisahau kua ikiwa Hawa wamewekewa pazia basi wengine wanatua hawajaekewa pazia kwa sababu hawawezi kua sawa sawa Wema na Wabaya, kwa hivyo kama pazia litakua halipo upande wao siku hiyo itakua ni kumuona Mola wao, kwa hivyo inathibitika kumuona Allah kwa Ayah ii vile vile.

Jawabu:

Hayo muliyoyasema hayana Dalili ya kumuona Allah mtukufu, kwa sababu kama ni hivyo munavyosema ungalilazimika vile vile kua Pazia hilo limewekwa baina yao na Allah mtukufu katika siku hiyo tu, na kua kabla yake lilikua halipo, kwa hivyo italazimika kua walikua wakimuona kabla ya siku hiyo, Allah ametakasika na sifa hiyo.

Hayo tuliyosema; na sisi tunaona kua Pazia hilo lililowazuia Baina yao na Mola wao lilikua halipo Bakla ya siku hiyo sio upande wao wala upande wa aliobakia wasiokua wao, kwa sababu hilo sio Pazia la kumuona Allah kwa Macho, lakini ni Pazia la Rehma na Usamehevu wa Allah, kwa hivyo wao hawatopata Rehma za Allah wa Usamehevu, kwa sababu wamekutana na Allah bila ya kutubia, kwa hivyo Mazuri yote ya Siku hiyo ambayo Waumini watayapata watu hao wamewekewa Pazia linalowazuia kuyapata, Allah atujaalie tuwe miongoni mwa wale wasioekewa Pazia katika Kuzipata Rehma na Usamehevu wake (Amin).

Wako watakaosema:

Amesema Allah mtukufu:

للذين أحسنوا الحسنى وزيادة

Na wale waliofanya Vizuri watapata Mazuri na ongezo” Basi Mazuri ni Malipo yao katika Pepo na Ongezo ni kumuona Allah mtukufu, kwa sababu amepokea Imam Muslim na wengineo kua Mtume (s.a.w) alisema:

إذا دخل أهل الجنة الجنة قال يقول الله تبارك وتعالى  تريدون شيئا أزيدكم فيقولون ألم تبيض وجوهنا ألم تدخلنا الجنة وتنجينا من النار قال فيكشف الحجاب فما أعطوا شيئا أحب إليهم من النظر إلى ربهم عز وجل

Watakapoingia Wa Peponi katika Pepo alisema: Atasema Allah Mtukufu aliyetukuka: Jee!! Munataka kitu nikuongezeni? Watasema: Jee!! hukutugharisha Nyuso zetu? Jee!! hukutuingiza katika Pepo na ukatuokoa kutokana na Moto? Akasema: Ataondosha Pazia; basi hawajapewa kitu kinachopendeza zaidi kwao kuliko kuangalia kwa Mola wao Mtukufu” Basi Hadithi ya Mtume (s.a.w) ndiyo iliyo bora Zaidi katika Kutegemea ndani ya Tafsiri, kwa hivyo kumuona Allah mtukufu ndio Neema kubwa ndani ya Pepo, hata wamefikia kusema: Lau kua sio kumuona Allah nisingalimuabudu”

Jawabu:

Ama kwa hakika kupenda kitu kunapofua, Allah anajua zaidi kuhusu Mapokezi hayo, lakini sisi tunakamatana na Mapokezi yanayokubaliana na Qur-ani tukufu, kwa sababu ongezeko linakua kwa mujibu ya malipo, na Allah mtukufu amesema:

من جاء بالحسنة فله عشر أمثالها”

Atakayekuja na Zuri atapata yeye kumi Mfano wake” Hivi ndivyo alivyotuambia Mola wetu, na hili ndio Ongezeko, ama mapokezi hayo tunarejesha kwa Mapokezi yenye nguvu zaidi, nayo ni Mapokezi ya Imam Malik , Bukhariy, na Muslim na wengineo, kua Mtume (s.a.w) amesema:

إن الله تبارك وتعالى  يقول لأهل الجنة يا أهل الجنة فيقولون لبيك ربنا وسعديك فيقول هل رضيتم فيقولون وما لنا لا نرضى وقد أعطيتنا ما لم تعط أحدا من خلقك فيقول أنا أعطيكم أفضل من ذلك قالوا يا رب وأي شيء أفضل من ذلك فيقول أحل عليكم رضواني فلا أسخط عليكم بعده أبدا

Hakika Allah Mtukufu aliyetukuka atawaambia Wa Peponi: EnyiWa Peponi… Nao watasema: Tumekuitika na Utukufu ni wako” Atasema: Jee!! mumeridhia? Watasema: Na vipi sisi tusiridhie na hakika umetupa ulikua hukumpa yeyote katika vuimbe wako? Atasema: Mimi ninakupeni Bora zaidi kuliko hayo.. Watasema: Ewe Mola na kitu gani ni bora Zaidi kuliko hayo? Atasema: Ninaweka juu yenu Maridhawa yangu sitokasirika juu yenu baada yake milele”

Basi Maridhawa ya Allah ndio kilicho bora Zaidi kuliko chochote kile, nayo imekuja katika Qur-ani amesema Allah:

وعد الله المؤمنين والمؤمنات جنات تجري من تحتها الأنهار خالدين فيها ومساكن طيبة في جنات عدن ورضوان من الله أكبر ذلك هو الفوز العظيم

Amewaahidi Allah Waumini wa kiume na Waumini wa kike Pepo itakayopita chini yake Mito, wakae humo milele, na Makazi mazuri katika Pepo Mzuri, na Maridhawa kutoka kwa Allah ndio Kubwa zaidi, na huko ndio kufaulu kukubwa”

Basi sisi hatuabudu kwa ajili ya Kumuona Allah lakini kwa ajili ya Kuridhiwa na Allah mtukufu, na hatujui kikubwa zaidi kuliko kuridhiwa na Allah. Tunamuomba Allah atuongoze katika Maridhawa yake (Amin).

JEE!! QUR-ANI NI KIUMBE?

Hili ni moja katika masuala yanyobabaisha wengi, na wanalolitumia wengi wanapotaka kuikosoa Itikadi ya Maibadhi, hawajui kua wanakosoa hata kitabu cha Allah ambacho ndio hiyo Qur-ani, basi hatuna budi kuliweka wazi jambo hili mbele ya kila Muislamu ili aijue Haki ipo mahala gani, na aweze kuifuata bila kubabaika ikiwa atakubali, na ikiwa hatokubali inatosha kusimama hoja juu yake, kwa sababu hoja ikisimama ujinga unan`golewa.

Basi kila Muislamu anatakiwa kujua kua hakuna kitu kinachotoka nje ya hukumu mbili, ima ni kiumbe au si kiumbe, na kila Muislamu anatakiwa kujua kua aliyekua si kiumbe ni yule aliyeumba naye ni Allah mtukufu, na vilivyobakia vyote ni viumbe vyake, kwa hivyo ichukue Qur-ani na uiweke katika mizani hii, Jee!! Qur-ani ni Mungu? Yeyote yule atakayesema kua ni Mungu huyo si Muislamu, kwa hivyo Qur-ani sio Allah, Jee!! Qur-ani ni kitu? Yeyote yule atakayesema kua sio kitu, huyo atakua yuko nje ya jambo tunalolizungumzia kwa sababu sisi tunaitakidi kua Qur-ani ni kitu, kwa sababu ndio chenye sifa ya kuwepo, na vipi tukhitalifiane juu ya kisichokuwepo? Kwa hivyo Qur-ani ni kitu na sio Allah kwa kivyo Qur-ani itakua ni Kiumbe kama viumbe wengine wa Allah.

Na iwapo mtu atasema:

kua vipi nyinyi munasema kua Qur-ani ni kiumbe hali ya kua Qur-ani ni maneno ya Allah?

Tutamjibu kua sisi hatupingi kua Qur-ani ni maneno ya Allah, bali tunasema Qur-ani ni maneno ya Allah, bila ya wasi wasi wowote ule, na anayepinga kua Qur-ani ni maneno ya Allah huyo sio Muislamu, lakini kuitwa Qur-ani kua ni maneno ya Allah ni kwa njia ya kunasibishwa, na sio kwa njia ya kusifika, na sisi tumebainisha vya kusotasha kua Sifa za Allah haziko nje ya Dhati yake, kwa maana Sio vitu vyengine bali ni  undani wa Sifa za Ukamilifu wa Dhati na Muumba, na Qur-ani, haimo katika Sifa, au yuko anayeweza kuthibitisha sifa ya Allah inayoitwa Qur-ani, kwa hivyo Qur-ani ni Maneno ya Allah kwa kunasibishwa, kama tunavyonasibishwa sisi kua ni Waja wa Allah, na unavyonasibishwa Msikiti kua ni Nyumba ya Allah, na Ngamia aliyepewa Mtume Swaleh (s.a.w) kua ni ngamia wa Allah, yote hayo ni kwa sababu Allah ndiye aliyetawalia Amri yake, na vimeitwa hivyo kwa sababu Amri ya kua kwake imetofautiana na Amri yake katika vitu vyengine vyenye jinsi hiyo. Haya tuliyoyasema yametokana na Dalili za Qur-ani wenyewe, miongoni mwa hizo ni hizi zifuatazo:

Dalili ya kwanza:

Amesema Allah mtukufu:

قل الله خالق كل شيء

Sema Allah ndie Muumba wa kila kitu” na pia neno lake:

وخلق كل شيء فقدره تقديرا

Na ameumba kila kitu na akakikadiria makadirio”

Basi aya hizi na mfano wa hizi zinatubainishia kua Qur-ani imeumbwa vile vile, kwa sababu ni kitu, tena kimekadiriwa Sura tunazisoma, nazo zimekadiriwa Aya zake, maneno yake, na Herufi zake, na kisomo chake, na maana zake, hekima zake, na hukumu zake, na khabari zake, na mifano yake.

Ikiwa mtu atasema:

Kama ni hivyo basi na Allah pia ni kitu kwa hivyo italazimika kua amejiumba Mwenyewe, na kama yeye hakujiumba basi vile vile na sifa zake hakuziumba na miongoni mwa hizo ni Maneno yake ambayo ndio hii Qur-ani.

Tunamjibu:

Yeye Allah, ndie mtendaji wa kitendo cha Kuumba kwa hivyo mtendaji wa kitendo hasifiki kua yeye ndie kitendo, lakini anasifika kwa kukifanya kile kitendo, kwa hivyo yeye ni Muumbaji na alivyoviumba ni Viumbe, na sifa zake ni ukamilifu wa dhati yake na sio kitu chengine isipokua Dhati yake, na Qur-ani haimo katika sifa hizo, isipokua kama tutakusudia neno Qur-ani kumaanisha sifa ya dhati ya Allah ambayo sio hichi kitabu ambacho kimeteremshwa kwa Muhammad (s.a.w), na sisi tunakisoma na kuandika maneno yake, na kutafakari maana yake, na sisi tunakusudia Qur-ani hii ya mwisho, wala hatujui Sifa ya dhati ya Allah inayoitwa Qur-ani, lakini tunajua kua Allah anayo sifa ya uwezo usioshindwa, na kwa uwezo huo ndio yakapatikana Maneno yake, na vitu vyote.

Dalili ya pili:

Amesema Allah:

إنا جعلناه قرآنا عربيا

Hakika sisi tumeijaalia Qur-ani kua ni ya Kiarabu”

Basi Qur-ani ijejaaliwa, na kujaalia ni kitendo cha Allah katika viumbe wake kwa hivyo Qur-ani ni Kiumbe vile vile, na Aya hizi zilazozungumzia kua Allah ameijaalia Qur-ani ziko nyingi, ndani ya Qur-ani, hakuna anayesema kua kitendo kinapatikana kabla ya Mtendaji, bali kitendo kitakua Baada ya kuwepo mtendaji na kujaalia ni kitendo, kwa hivyo Allah ndio aliyojaalia na Qur-ani ndiyo iliyojaaliwa, na kwa sababu kimepatikana kitendo juu yake itakua ni kiumbe tu.

Na mfano wa haya ni mengi katika kitabu cha Allah kwa mfano:

هو الذي جعل لكم الليل لتسكنوا فيه والنهار مبصرا

Yeye ndiye aliyejaalia kwenu Usiku ili mupumzike ndani yake na Mchani uwe ni wenye kukuonyesheni”

Huenda mtu akasema:

Kama ni hivyo basi na Watu pia wanajaalia, na hayo yametajwa ndani ya Qr-ani vile vile kwa hivyo tufahamu vipi?

Tunawajibu:

Kitendo hicho kinakuja kwa Maana nyingi, na maana inayokubalika inapatikana kwa mujibu wa ufahamu wa Maneno kutokana na Vielelezo vilivyomo, kwa hivyo kinakuja kwa maana ya madai, kwa mfano neno la Allah:

وجعلوا الملائكة الذين هم عباد الرحمن إناثا

Na wanawajaalia Malaika ambao wao ni Waja wa Mwingi wa rehma kua ni wanawake” Basi hapa ni kwa maana ya Kuzua maneno yao na itikadi yao hiyo ya kua Malaika ni wanawake” na sio kuumba.

Basi ama kitendo hicho kinapoegemezwa kwa Allah muumbaji haiwezekani kua ni uongo ndani yake, kwani atakayekikataa atakua ameshakufuru, na ikiwa Allah ameijaalia Qur-ani basi hiyo Qur-ani itakua ni kuimbe tu, kwa sababu itakua ni kitu chengine sio Allah mtukufu, kwa hivyo inabainika kua Qur-ani ni kiumbe.

Huenda mtu akasema:

Sasa inamaana Sifa za Allah ni viumbe vile vile.

Tunamjibu:

Allah mtukufu anasifika na sio anazo sifa, kwa maana yeye ni mkamilifu wa Dhati kutokana na Ukamilifu huo ndio ikalazimika kusifiwa kwa kila sifa kamilifu, na sio yeye anazo sifa kwa maana yeye anazitegemea hizo sifa, kwa hakika yeye hajafanana na Kitu, basi utakapofahamu haya utajua kua Sifa zake za Dhati ni Dhati yake mwenyewe na sio kitu chengine, Allah atueke mbali na Itikadi ya kuwepo Watangu wengi wasiokua na mwanzo, kwa hakika Allah peke yake ndie asiyekua na Mwanzo, yafahamike haya vizuri.

Dalili ya tatu:

Amesema Allah:

وما يأتيهم من ذكر من الرحمن محدَث إلا كانوا عنه معرضون

Na wala hauwajii ukumbusho -kutoka kwa Mwingi wa Rehma- ulio mpya ila wao wanakua wenye kujitenga nao” na pia amesema:

ما يأتيهم من ذكر من ربهم محدَث إلا استمعوه وهم يلعبون

Hauwajii ukumbusho -utokao kwa Mola wao- ulio mpya isipokua wanausikiliza nao wamo katika kucheza”

Hapa tunaona kua Mwenyezi Mungu anasifu kitabu chake kua ni ukumbusho, tena anausifu kua ni mpya; na kitu kipya kinakua kipya kutokana na mwanzo wake, na sisi tumefasiri neno محدَث kwa neno mpya, lakini kuihakika neno hilo lina ufahamu ya uwazi kabisa kuliko hiyo, katika lugha ya kiarabu, na ufahamu wake  ni kule kupatikana kitu baada ya kukosekana kwake, kwa hivyo neno hilo likitamkwa ni kuafahamisha kua kilichokusudiwa  ni kiumbe bila shaka yoyote ile, na maana hiyo inapatikana ikiwa herufi ya dali  ina fat-ha tu, kama ilivyo katika aya tukufu.

Kwa hivyo Qur-ani yenyewe inashuhudia kua yeye ni kiumbe, sasa vipi tena Maibadhi wende kinyume na Qur-ani?.

Dalili ya nne:

Amesema Allah:

كتاب أحكمت آياته ثم فصلت من لدن حكيم خبير

Kitabu vinefanywa vizuri Aya zake, kisha zikapambanuliwa kutoka kwa Mweingi wa Hekima Mwingi wa kujua.”

Na hapa tunaona vile vile kua Allah ndie iliyekifanya kua na Sifa hizo, na kua Hicho ni Kitabu, sio Sifa ya Dhati ya Muumba, kwa hivyo ni wazi kua Qur-ani ni kiumbe.

Dalili ya tano:

Amesema Allah mtukufu:

شهر رمضان الذي أنزل فيه القرآن

Mwezi wa Ramadhani ambao imiteremshwa ndani yake Qur-ani”

Hapa tunaona kua Qur-ani imeteremshwa, na kuteremshwa ni kuondolewa katika sehemu na kupekekwa katika sehemu nyengine, na kisichokua na mwanzo hakiwezi kuwa na sehemu, kwa sababu vipi kilikuwepo kabla ya kuwepo sehemu? kwa hivyo kama hakina mwanzo haiwezekani kusifiwa kua kimeteremshwa.

Haya,,, na Aya nyingi sana zinaonyesha kwa Uwazi kua ni viumbe tu ndio vinaathirika na kitendo cha Kuteremshwa.

Pia ziko dalili nyingi katika Qur-ani zinazothibitisha kua Kimefanywa, na kua ni Kiumbe, naona tutoshelezeke na hizi tulizozitaja.

Dalili katika Sunna:

Na katika Sunna ya Mtume (s.a.w) ziko dalili za Uwazi kua katika Qur-ani kuna Sehemu Kubwa kuliko nyengine na kua ni bora zaidi, kwa mfano: Mepokea Imam Rabii (r.a), na Bukhari, na Imam Ahmed, na wengineo: Kua Mtume (s.a.w) alisema kuhusu Suratil-Ikh-laas :

والذي نفسي بيده إنها تعدل ثلث القرآن

Naapa kwa yule ambaye Nafsi yangu imo katika Mono wake (Uwezo wake) Hakika Hiyo (Suratil-Ikhlaas) iko sawa na Thuluthi ya Qur-ani”

Na thuluthi ni sehemu moja katika sehemu tatu za kitu kizima, Kwa hivyo inabainika wazi kua Qur-ani imegawika, sasa vipi sifa ya Allah igawike? kwa hakika haikuwa kugawika kwa Kitu isipokua ni dalili ya Kuumbwa kwake.

Naona tutoshelezeke na haya katika Kuumbwa kwa Qur-ani, kwa sababu hoja zake ziko wazi kuliko jua wakati wa Mchana. Na la Ajabu utaona wale wanaokataa kua Qur-ani ni kiumbe ukiwauliza utawakuta wanasema hivi:

هو كلام الله منه بدأ وإليه يعود غير مخلوق

Hayo ni Maneno ya Allah kwake yeye ndiko yalikoanza na kwake yeye yatarejea na wala hayakuubwa”

Masikini ikiwa haya ndiyo maneno yao, inafaa kila mmoja wetu ayazingatie, vipi kitu kisichokua kiumbe, kimeanza na kitamalizika, hakika sisi sote tumeanza kwa Allah na kwake yeye ndio Marejeo yetu, na hakuna kitu kilichoanza isipokua hicho ni kiumbe, kisha la karibu zaidi, kuwaambia hawa Watu ni kuwauliza:

Jee!! Hii lugha ya kiarabu amabayo ndiyo iliyotumika katika Qur-ani ni kiumbe au sio kiumbe?

Na hapo hawana jawabu isipokua ni Kiumbe tu, kwa sababu Lugha zote ni viumbe, Allah ameziumba, na wakisema kua Lugha ya Kiarabu ni kiumbe bila Shaka tayari wameshakiri kua Qur-ani pia ni kiumbe kwa sababu Allah ameisifu kwa kusema:

وهذا لسان عربي مبين

Na hii (Qur-ani) ni ulimi (lugha) na kiarabu kwa wazi”.

TAHADHARI

Tazama ndugu yangu Muislamu, mayahudi wamempa Uzair sifa ya Uungu, na Manasara wamempa Issa Mwana wa Mar-yam sifa ya Uungu, na Waislamu wako wanaoipa Qur-ani Sifa ya Uungu.

Wakati huo huo wanakubaliana kua كان الله ولا شيء معه Alikua Allah wala hakuna kitu pamoja na yeye” كان الله ولا شيء غيره Alikua Allah wala hakuna kitu kisichokua yeye” , halafu baada ya hapa lije neno la kutuambia kua kuna cha tangu kisichokua na Mwanzo nacho ni kitu sio Allah mwenyewe? Tunamuomba Allah atuwezeshe katika anayoyaridhia, na atuoneshe Haki na atuwezeshe kuifuata (Amin).  Ndugu yangu usishindane na mtu, ima akubali kua wa Tangu wasiokua na Mwanzo ni wengi, au akubali kua Allah ameumba kila kitu kisichokua yeye, la mwanzo ni Ukafiri kwa makubaliano, la Pili ni Tawhidi kwa makubaliano, wala hakuna njia ya tatu, iliyo baina yake.

JEE!! WASIOTUBIA WATAKUA MOTONI MILELE?

Bila shaka ndugu yangu ulisoma katika yaliyopita kua kuna hukumu ya Ukafiri ndani ya Uislamu, na kua hukumu hiyo kiuhakika inamkamata kila ailiyemuasi Allah kwa Kosa kubwa, ni sawa kua kosa hilo ni la kishirikina au sio la kishirikina, na kua Makafiri wamegawika sehemu mbili Makafiri waliokua ni Washirikina, wao wana hukumu zao za Kishirikina, na Makafiri ambao sio Washiriki nao ni Wanafiki wote, na hawa ni Waislamu, na wengine katika sisi wamekataa kuwaita Waislamu, lakini vile vile wamekataa kuwaita Washirikina juu ya kukubaliana kua hukumu zao ni za Mila ya Kiislamu.

Wanafiki hawa wanatakiwa kutubia kutokana na Makosa yao, ama hukumu  zao baina yetu ni za Kiislamu isipokua Mapenzi kwa ajili ya Allah (tutayaeleza).

Basi baada ya kuyajua hayo, unatakiwa kujua vile vile; kua yoyote yule atakayemuasi Allah kwa kosa Kubwa, na akaondoka Duniani bila ya kutubia na kosa lake hilo, ikiwa ni la kishirikina au sio la kishirikina, huyo atakua ni miangoni mwa watakao kaa milele katika adhabu ya Allah ambayo ni  moto, na hii ndio itikadi  Sahihi kabisa isiyoingiwa na chembe ya doa, na ubainisho wa Usahihi wake unakuja katika Dalili zifuatazo:

Dalili ya kwanza:

Amesema Allah Mtukufu:

وقالوا لن تمسنا النار إلا أياما معدودة قل أتخذتم عند الله عهدا فلن يخلف الله عهده أم تقولون على الله ما لا تعلمون * بلى من كسب سيئة وأحاطت به خطيئته فأولئك أصحاب النار هم فيها خالدون

Na wamesema: Hautotugusa Moto isipokua siku chache” Sema: Jee!! mumechukua Ahadi kwa Allah, na hatovunja Allah Ahadi yake, au munayasema kwa Allah musiyoyajua * Ndio; yoyote atakayechuma Ovu, na likamzunguka yeye Kosa lake, basi hao ni wa Motoni wao ndani yake watakaa milele”

Na Aya hizi ziko wazi kabisa kwa njia zifuatazo:

Itikadi hiyo, imetoka katika mizizi ya Kiyahudi kwa sababu Aya hizi zimekuja kufedhehesha Upotevu wao.
Ulizo lililokuja la kuwauliza ndani yake, ni ubainisho kua Itikadi hiyo haina Ahadi ya Allah, na kua hayo yamekuja katika Uzushi tu bila ya Elimu. Na hii peke yake inatosheleza kwa mwenye macho kua vipi na sisi tufuate nyayo zao?
Katika Aya hizo kuna ubainisho wa Uwazi kabisa, kua mwisho wa mwenye kufanya Kosa lolote lile, na akalazimika na kosa hilo, kwa kukosa kutubia kwa Allah – kwa sababu kosa haliondoki mpaka kwa Toba- huyo atakaa Motoni milele. Na hii ni kuwarudi mwenye malengo hayo, na kuzikata tama zao.

Wako watakaosema:

Kosa hapa ni Ushirikina.

Jawabu:

Maana hiyo ni kotoka nje ya Udhahiri wa neno lililokuja katika Aya, tena neno hilo linafahamisha kua Kosa lolote lile lina hukumu hiyo, watu wa Usuli wanaita مطلق  Muttlaq, na Muttlaki ikija katika الشرط Sharti, inaonyesha kua ni mkusanyo wa kila linalokua na maana ya neno hilo, na hiyo wao wanaiita  العام kwa hivyo inaingia kila Kosa dani yake ikiwa ni Kubwa au Dogo, na ukitaka uhakika wa haya angalia katika maneno haya: Atakaenijia na mtoto atapata nyumba. Unaona hapo anaingia kila Mtoto yeyote yule, ikiwa ni mkubwa au mdogo, mweupe au mweusi, Tajiri au Masikini, Muislamu au Mshirikina, cha muhimu ni Mtoto tu, basi hii ndio maana iliyoko katika Aya, kua kosa lolote lile. Na haya yote yanatiliwa mkazo na Hadithi ya Mtume (s.a.w) pale aliposema:

إن العبد إذا أذنب ذنبا نكتت في قلبه نكتة سوداء فإن تاب ونزع واستغفر صقل قلبه وإن عاد زادت حتى تعلو قلبه فذلك الران الذي ذكر الله تعالى في القرآن { كلا بل ران على قلوبهم ما كانوا يكسبون}

Hakika Mja anapofanya Dhambi linapiga katika Moyo wake Doa jeusi, ikiwa atatubia, na kujivua, na kuomba msamaha utasafika moyo wake, na akirejea linazidi mpka linaufunika Moyo wake, basi hiyo ndio Chapa aliyoitaja Allah Mtukufu katika Qur-ani {Hapana; bali yamepiga chapa juu ya Mioyo yao yale waliyokua wakiyavhuma}”

Basi Dhambi yoyote ile itaingia katika hukumu hii ya Haki.

Dalili ya pili:

Amesema Allah:

فمن جاءه موعظة من ربه فانتهى فله ما سلف وأمره إلى الله ومن عاد فأولئك أصحاب النار هم فيها خالدون

Na yatakayemjia Mawaidha yanayotoka kwa Mola wake na yeye akajizuia basi ni yake yaliyopita, na hukumu yake iko kwa Allah, na Atakayerudia; basi hao ni wa Motoni wao humo watakaa milele”

Aya  hii imeshuka katika kuharamisha Riba, na Riba ni dhambi Kubwa tu nayo siyo Ushirikina, na sisi tunamuona Allah kwenye kitabu chake anatueleza kua Atakayerudi katika Kosa hilo la kula Riba atakua ni miongoni mwa wenye kosa hilo ambao watakaa Milele motoni.

Basi wakisema:

Waliokusudiwa hapa ni wale wanaohalalisha kula Riba tu, na mtu akihalalisha Riba huyo ni Mshirikina kutokana na kuirudi Hukumu ya Allah, kwa hivyo maana yake atakayerudi kula Riba kwa kuiona kua ni Halali.

Tutawajibu:

Hakika kuhalalisha ni kosa jengine hilo, sio kula Riba, na ikiwa hivyo munavyosema ndio makusudio ya Aya, basi Watangazieni watu kua kula Riba hakuna Matatizo kwa sababu sisi tumeharamishiwa kuhalalisha kula riba na sio kula riba, kwa hivyo kuleni Riba na nyinyi mukiitakidi kuwa ni Haramu tu, mukifanya hivyo mutakua hamuna makosa. Na hapo itakua hakuna maana ya kuharamishwa kitu bali ni kuitakidi Uharamu wake tu na kua makosa yote anayetaka kuyafanya na ayafanye lakini aitakidi Uharamu wake tu; Kwa hakika haya ndio yale aliyoyasema Allah katika kitabu chake:

ألم تر إلى الذين أوتوا نصيبا من الكتاب يدعون إلى كتاب الله ليحكم بينهم ثم يتولى فريق منهم وهم معرضون * ذلك بأنهم قالوا لن تمسنا النار إلا أياما معدودات وغرهم في دينهم ما كانوا يفترون

Jee!! hujawaona wale waliopewa sehemu ya Kitabu, wanaitwa katika Kitabu cha Allah ili kihukumu baina yao, kisha linakataa kundi kati yao na waao wanayapa mgongo * hayo ni kwa sababu wao wamesema: Hautotugusa Moto isipokua ni siku chache tu, na yamewadanganya katika Dini yao yale waliyokua wakiyazua” Basi ndio kama hivi Qur-ani inafedhehesha Mabaya ya itikadi hii, ya kuadhibiwa kwa Muda tu, kua inapelekea katika Maasi, kama tulivyoonyesha.

Dalili ya tatu:

Amesema Allah mtukufu:

من يعص الله ورسوله ويتعد حدوده يدخله نارا خالدا فيها وله عذاب مهين

Na atakayemuasi Allah na Mtume wake na akaivuuka mipaka yake atamuingiza motoni atakaa Milele ndani yake na atapata Adhabu yenye kufedhehesha”

Aya hii imekuja Baada ya kubainishwa hukumu za Mirathi, na kuisema kua ni Mipaka ya Allah, kisha ikaja Aya hii kuonyesha Adhabu itakayowapata wale watakaomuasi Allah na Mtume  wake kwa kuivuuka mipaka hiyo, kua watakuwa ni watu wa motoni milele. Na kama tonavyoona kua Aya haikuzungumzia Atakayemshirikisha Allah lakini atakayemuasi, kwa kivyo yanaingia Maasi yote bila ya wasi wasi.

Dalili ya nne:

Amesema Allah:

ومن يقتل مؤمنا متعمدا فجزاؤه جهنم خالدا فيها وغضب الله عليه ولعنه وأعد له عذابا عظيما

Na yeyote atakayemuua Muumini kwa makusudi basi malipo yake ni Jahannam Atakaa Milele humo na Ataghadhibika Allah juu yake (huyo aliyeua), na atamlaani na amemtayarishia Adhabu kubwa”

Tunaona katika Aya hii, kua Allah Atamtia motoni milele yoyote yule -ikiwa ni Muislamu au Mshirikina- iwapo atafanya kosa la kumuuwa Muumuni, na kuuwa ni kosa Kubwa tu sio Ushirikina, isipokua yule atayehalalisha Kuua bila ya Haki, itakua huko kuhalalisha kwake ndio Ushirikina.

Wala asiseme mtu:

Kua Aya ilishuka kutokana na Mshirikina aliyemuua Muumin, kwa sababu makubaliano yamepita kua; hakuna mazingatio ya Sababu katika ukusanyo wa Tamko, na Tamko hapa limekusanya kwa yeyote yule atakayefanya kosa hilo.

Wako watakaosema:

Mwanzo wa Aya iliyopita kabla ya Aya hiyo imekuja hivi:

وما كان لمؤمن أن يقتل مؤمنا إلا خطأ

Wala haiwi Muumini kumuua Muumin isipokua ni kwa kukosea”

Kosa hilo la kuua likitokezea kwa Muislamu haliwezi kuingia katika mkusanyo huo, kama ilivyoeleza Aya hii.

Tunawajibu:

Hiyo Aya imebainisha Uhakika wa Imani na sisi tumebainisha kwa Dalili za kutosha kua Anayemuasi Allah kwa kosa kubwa hawezi kusifika na Sifa hiyo ya Imani bali yeye ni Mkafiri wa kinafiki au kishirikina, na wa mwanzo ni Muislamu, kwa hivyo umefahamu, na unaona jinsi Aya zinavyokubaliana kutokana na Itikadi Sahihi katika kuifahamu Qur-ani.

Dalili ya tano:

Amesema Allah:

للذين أحسنوا الحسنى وزيادة ولا يرهق وجوههم قتر ولا ذلة أولئك أصحاب الجنة هم فيها خالدون * والذين كسبوا السيئات جزاء سيئة بمثلها وترهقهم ذلة ما لهم من الله من عاصم كأنما أغشيت وجوههم قطعا من الليل مظلما أولئك أصحاب النار هم فيها خالدون

Wanapata wale waliofanya Vivuri Mazuri na ongezo, wala hawatofikwa na Taabu ya udhalilifu; Hao ni wale wa peponi humo watakaa milele * Na wale waliochuma Mabaya malipo ya mabaya ni kwa mfano wake, na watafikiwa na udhalilifu na wala hawatopata kwa Allah wa kuwahifadhi, kama kwamba zimefunikwa nyuso zao kwa kipande cha Usiku wenye Kiza; Hao ni wale wa Motoni humo watakaa milele”

Na Aya hihi iko wazi kabisa na wala haina doa inajieleza wenyewe, kwa sababu Allah amewagawa watu mafungu mawili tu, waliofanya mazuri na waliochuma mabaya, kisha akaeleza malipo watakayopata, kwanza waliofanya vizuri hawatopata Taabu wala Udhalilifu na kuingia Motoni ni Taabu na Udhalilifu, kwa hivyo hawawezi kuingia kamwe katika moto, kisha wakatolewa; na wale waliochuma Maovu – na hayawi maovu isipokua kwa kukosa toba, kwa sababu toba inaondosha Maovu- wao watafikwa na matatizo, na udhalilifu na kuingia Motoni milele kama ilivyoeleza Aya tukufu.

Dalili ya sita:

Amesema Allah:

ومن يعص الله ورسوله فإن له نار جهنم خالدين فيها أبدا

Na yeyote atayemuasi Allah na Mtume wake kwa hakika atapata yeye Moto wa Jahannam; nao watakaa humo Milele”

Aya iko wazi kwa atakate muasi Allah kwa hivyo ima mwenye kufanya kosa Kubwa kisha Hakutubia atakua Amemuasi Allah au hajamuasi Allah, na ikiwa hajamuasi Allah basi itakua hakuna haja ya kukatazwa wala kuamrishwa, la hili hakuna anayeweza kulikubali, kwa hivyo ikiwa ni mwenye kumuasi Allah bila shaka Ahadi hii ya Moto wa milele itamkuta kwa sababu Allah hasifiki kwa sifa ya Uongo.

Dalili ya saba:

Amesema Allah:

إن الأبرار لفي نعيم * وإن الفجار لفي جحيم * يصلونها يوم الدين * وما هم عنها بغائبين

Hakika waliowema watakua katika Neema * na hakika walio wabaya watakua katika Jahiim (Muwako mkali wa moto) Wataifikia siku ya malipo wala wao humo si wenye kukosekana”

Hakuna Aya iliyo kua Wazi kabisa na kuzikata tama za wanaojipa watamanio ya Pepo, kwa kujiita Waislamu tu na wakayavamia Maasi kama hii, kwa hakika Ima watu hao wawemo hatika watu wema au waovu, na kisha waeke katika hukumu hii ya Allah utaona matokeo yake, jee watatoka motoni, kwa hivyo wale wanaosema kua waliokua si Washirikina wataadhibiwa kwa muda kisha watakwenda katika Makazi ya Milele peponi itawalazimikia wawasifu watu hao kama ni watu wema na sio Wabaya, na tukifanya hivyo mizani zitabadilika, hata siku moja hukumu ya Allah haibadiliki.

Hizi ndizo baadhi ya Dalili ambazo zinatoka katika Kitabu cha Allah, na ukichunguza utakuta Dalili nyingi sana, na wala hutokuta Dalili hata moja iliyokua Wazi kua kuna watu watatoka motoni, kwa hivyo hii ndiyo hukumu isiyokua na Shaka yoyote ile.

Na huenda wakasema:

Vipi mbona umeisahau Ile Aya inayosema:

إن الله لا يغفر أن يشرك به ويغفر ما دون ذلك لمن يشاء

Hakika Allah hasamehe kushirikishwa yeye, na anasamehe sasiyokua hayo kwa Anayetaka”

Aya ambayo inatubainishia kwa uwazi kua Allah hasamehe kosa moja tu nalo ni Ushirikina, ama makosa mengine amabayo siyo Ushirikina hayo yako katika kutaka kwake, kwa hivyo akitaka atasamehe na Akitaka hatosamehe.

Basi hawa tunawajibu kwa kusema:

Hakika Allah hasemi uongo wala hukumu yake haibadilishwi, na yeye amesema:

وليست التوبة للذين يعملون السيئات حتى إذا حضر أحدهم الموت قال إني تبت الآن ولا الذين يموتون وهم كفار أولئك أعتدنا لهم عذابا أليما

Na hawana Toba wale wanaofanya makosa mpaka yanapomfika mmoja wao mauti anasema: hakika mimi natubia hivi sasa, wala wale ambao wanakufa na wao ni makafiri hao tumewaandalia Adhabu yenye kuumiza”

Na tukisoma katika Kitabu cha Allah tunakuta hata huyo Anayemshirikisha Allah anasamehewa Madhambi yake iwapo atatubia, amesema Allah:

والذين لا يدعون مع الله إلها آخر ولا يقتلون النفس التي حرم الله إلا بالحق ولا يزنزن ومن يفعل ذلك يلق أثاما يضاعف له العذاب يوم القيامة ويخلد فيها مهانا

Na wale wasiyomuomba Allah pamoja na Mungu mwengine, wala hawauwi nafsi ambayo ameiharamisha Allah isipokua kwa Haki, wala hawafanyi Uzinzi, na mwenye kufanya hayo atapata Makosa; ataongezewa yeye Adhabu siku ya kiama na atakaa humo milele akidhalilika” Kisha akasema: إلا من تاب  Isipokua atakayetubia” Kwa hivyo Allah anasamehe makosa yote kwa atayetubia, na hawa ndio anaotaka Allah kuwasamehe, ama ambaye hakutubia na makosa yake huyo kama tulivyoeleza kwa uwazi atakua ni kuni ya Motini humo atakaa milele; sasa ikiwa ni hivi ni nini jawabu ya Aya hiyo ambayo inathibitisha kusamehewa atakao taka Allah isipokua Washirikina?

Tunasema:

Ufahamu huo sio uliokusudiwa katika Aya hiyo. Bali Aya hiyo ni dalili ya uwazi kabisa kua Mshirikina anaposilimu, Allah anamsamehe makosa yake yote, na haya yako wazi kabisa katika mafundisho ya Uislamu, kwa sababu imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w) kua amesema : الإسلام يجب ما قبله Uislamu unafuta yaliyo kabla yake” kwa hivyo maana sahihi ya Aya hiyo ni kama ifuatavyo: Hakika Allah hasamehe Kushirikishwa na kitu chengine, na Anasamehe yote yasiyokua Ushirikina katika makosa kwa anayetaka Allah kumuongoza katika washirikina kwa Uingia katika Uislamu” kwa hivyo Kusilimu kwake ndio Toba yake, kwa makosa yote, amesema Allah mtukufu:

قل للذين كفروا إن ينتهوا يغفر لهم ما قد سلف

Sema kuwaambia wale waliokufuru: Ikiwa wataacha (Ukafiri wao kwa kutubia) watasamehewa wao yale yaliyopita” Tizama jinsi gani Aya zinavyokubaliana, Allah atuongoze katika anayoyaridhia (Amin).

Wako watakaosema:

Sasa unasema nini kuhusu zile Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w), kuwa Waislamu wote wataingia peponi, hata watakaoadhibiwa ni kwa muda tu kisha watatolewa na kuingia Peponi?

Jawabu:

Hakika hadithi hizo zinajibiwa kama tulivyozijibu zile Hadithi za kumuona Allah, tena hapa hakuna mchezo, hizo Hadithi hata awe amezipokea nani, zimepingana na Kitabu cha Allah kwa uwazi kabisa, bali zimepingana na Hadithi nyengine zina nguvu zaidi kuliko hizo, kwa hivyo hadithi hizo ikiwa zinazungumzia kua kila muislamu ataingia Peponi, italazimika kuzifunga na sharti ya Toba, au Muislamu Kisheria, ama zile za kutoka motoni hizo ni Dhaifu wala haziwezi kusemwa kuwa ni Hadithi za Mtume (s.a.w) kwa sababu Mtume (s.a.w) hawezi kusema maneno yanayopingana wenyewe kwa wenyewe, wala kupingana na Kitabu cha Allah Qur-ani.

Amesema Mtume (s.a.w) aktika Hadithi Sahihi aliyoipokea Imam Rabii (r.a) kwa njia ya Ibn Abbaas (r.a) kua Mtume (s.a.w) alisema:

إنكم ستختلفون من بعدي فما جاءكم عني فأعرضوه على كتاب الله فما وافقه فعني وما خالفه فليس عني”

Hakika nyinyi mutakhitalifiana baada yangu, kitakachokuja kwenu kutoka kwangu kuwekeni katika Kitabu cha Allah kitakacho kubaliana nacho kinatoka kwangu, na kitakacho kwenda kinyume nacho hicho sio changu”

Basi huu ni Msingi uliothibiti kwa njia hii ya Juu kabisa kwani imekuja kwa njia Imam Abu Ubaidah (r.a) kutoka kwa mwalimu wake Imam Jabir Bin Zaid (r.a), basi ushike msingi huu wala usibabaike.

Dalili katika Sunna:

Na hapa tunaziweka Baadhi ya Hadithi ambazo zinathibitisha kua mwenye kufanya kosa kubwa ikiwa hakutubia na kosa lakeatakwenda katika Adhabu ya milele motoni:

Amepokea Imam Bukhariy na Muslim na wengineo kutoka kwa Ibn Omar (r.a) kua Hakika Mtume (s.a.w) alisema:

يدخل أهل الجنة الجنة وأهل النار النار ثم يقوم مؤذن بينهم يا أهل النار لا موت ويا أهل الجنة لا موت كل هو خالد فيما هو فيه

Wataingia wa peponi katika pepo na wa motoni katika Moto kisha atasimama mwenye kunadi: Enyi wa motoni hakuna Kufa, Enyi wa Peponi hakuna Kufa kila mmoja ni wa milele katika humo alimo”

Amepokea Imam Ahmed na Bazzaar na Hakim na Nassaiy na kutoka kwa Ibn Omar (r.a) hua hakika Mtume (s.a.w) alisema:

لا يدخل الجنة عاق ولا مدمن خمر

Hatoingia peponi mwenye kuvunja haki za wazazi wala mwenye kuendelea na Ulevi” na katika Mapokezi mengine:

ثلاث قد حرم الله عليهم الجنة مدمن خمر والعاق لوالديه والديوث وهو الذي يقر السوء في أهله”

Watatu hakika amewaharamishia Allah Pepo: Mwenye kuendela na Ulevi, na mwenye kuvunja Haki na Wazazi wake wawili, na Dayyuth, na yeye ni yule anaekubali kufanyiwa uovu (zinaa)  mkewe”

Wameipokea Imam Bukhariy na Muslim na wengineo kwa njia ya Abi Hurairah (r.a) kua alisema Mtume (s.a.w):

من قتل نفسه بحديدة فحديدته في يده يتوجأ بها في بطنه في نار جهنم خالدا فيها أبدا ومن قتل نفسه بسم فسمه في يده يتحساه في نار جهنم خالدا فيها أبدا ومن نزل من جبل فقتل نفسه فهو ينزل في نار جهنم خالدا مخلدا فيها أبدا

Mwenye kuiua nafsi yake kwa Chuma basi chuma chake kitakua mkononi mwake anajipiga nacho tumboni mwake katika moto wa Jahannam akikaa humo Milele, na mwenye kuiua nafsi yake kwa Sumu basi sumu yake itakua mkononi mwake akiinywa katika Moto wa Jahannam akikaa humo Milele, na mwenye kujitupa katika Jabali na akaiuwa Nafsi yake basi anajitupa katika moto wa Jahannam ni mwenye kukaa humo milele”

Imeipokea Imam Muslim kua Mtume (s.a.w) alisema:

صنفان من أهل النار لم أرهما بعد قوم معهم سياط كأذناب البقر يضربون بها الناس, ونساء كاسيات عاريات مائلات مميلات رؤوسهن كأسنمة البخت المائلة لا يدخلن الجنة ولا يجدن ريحها وإن ريحها ليوجد من مسيرة كذا وكذا

Makundi mawili ya walio wa Motoni sijayaona Bado; Watu watakua na Bakora kama mikia ya n`gombe wanawapiga watu, na Wanawake waliovaa waliouchi walioinama, na vilivyoinama vichwa vyao kama nundu ya Ngamia zilizoinama; hawatoingia Peponi wanawake hao wala hawatapata harufu yake, na hakika harufu yake inapatikana mwendo Kadha wa Kadha”

Amepokea Bukhariy na Muslim kutoka kwa Saad na Abi Bak-rah (r.a) kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s.a,w):

من ادعى إلى غير أبيه وهو يعلم أنه غير أبيه فالجنة عليه حرام

Mwenye kudai Baba asiyekua wake, na yeye anajua kua si baba yake basi Pepo kwake yeye ni Haramu”

UBAINISHO

Hatuna Haja na kurefusha sana, kwa sababu mapokezi kama haya ni mengi, nayo yamekubaliana na dalili za Qur-ani, wala hakuna shaka katika hilo.

Na mwisho ikiwa Mtu atashikilia kua waliomuasi Allah na wao ni Waislamu kua watatoka Motoni basi tunamjibu; kua na sisi tutakua miongoni mwa hao ikiwa hiyo itikadi yenu ni sahihi.

Ninatoa kisa kidogo hapa mwenye macho atafahamu:

Inaelezewa kua Bedui mmoja alisilimu, na kuukubali Uislamu vizuri kabisa, basi mara moja alikutana na Mganga na Mtaalamu wa nyota, na hawa wawili wao si Waislamu na wao hawaamini kua kuna kufufuliwa ikabidi wajadiliane na yule Bedui, Bedui aliwasikiliza hoja zao kisha aliwajibu hivi: Ikiwa kufufuliwa ni Uongo tutastarehe sote mimi na nyinyi kutokana na matatizo ya kidunia, na ikiwa ni kweli basi Khasara itakua ni Juu yenu”

Kwa hivyo sisi hatuna Shaka katika itikadi hii sahihi, na tunasema kuwaambia wenye kuitakidi kutoka Motoni kua ikiwa kutoka ni kweli basi na sisi tutakwenda Peponi tu, na kama ni Uongo basi nyinyi mutabakia humo milele kama hamukutubia na Itikati hiyo Batili na kila kosa kubwa, baada ya kubainikiwa na Hoja,.

Hoja ikisimama ujinga hauna nafasi.

AJABU KATIKA KUSHINDWA

Utawaona baadhi ya watu baada ya kubainikiwa na Dalili, wanakua hawataki kufuata tu, kwa sababu imekwenda kinyume na waliyoyarithi, jamani Mtume wetu ametuambia:

الكبر بطر الحق و غمط الناس

Kibri ni kuifanyia jeuri Haki, na Kudharau Watu”

Allah atuweke mbali na Kibri na kila Maradhi ya Nafsi, na atuepushe na Kila Baya na atuongoze katika yenye Maridhio yake (Amin).

SHAFAA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

Kwa kawaida linaweza kuja suali kuhusu Shafaa ya Mtume (s.a.w) kwa umma wake; Jee!! ni nini msimamo wa Maibadhi katika jambo hili?

Kwa hakika Maibadhi katika jambo hili wapo katika haki isiyokua na Chembe ya Doa, basi Maibadhi ni katika wanaokubali Shafaa ya Mtume (s.a.w), wala hawalipingi suala hilo, lakini kwao lina mipaka yake maalum, nao wanasema kua Shafaa ya Mtume (s.a.w) ni kwa ajili ya Wachamungu peke yao, sio kwa watu wa motoni, kwa hivyo Shafaa ya Mtume (s.a.w) itakua kwa kuharakishwa hesabu na kuongezewa daraja katika Pepo peke yake, na sio katika kuwatoa watu motoni, anasema Sheikh Saalimy (r.a):

شفــاعــة الرســول للتـقــي * مـن الـورى وليـس للشـقي

Shafaa ya Mtume ni kwa Mchamungu * katika waja na sio kwa Muovu.

Lakini haya ni maneno ya Sheikh tu, jee ziko dalili walizotegemea katika hili?

Ndio dalili zipo nazo zimegawika katika kitabu cha Allah Qur-ani na kutoka kwa Mtume (s.a.w)

Dalili katika Qur-ani:

Qur-ani inatubainishia bila ya kutuachia chembe ya Shaka katika sula hili, nayo imekuja na maelezo mazito sana amabyo hayakubali kinyume chake, kwa hivyo sio katika busara kuziacha Dalili zake na kuelekea katika kuziwekea Pazia, eti kwa kuonisha na yale yaliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w), jambo ambalo linapingana na misingi iliyomo katika Uislamu katika kuonisha Dalili zilizopingana, na kupelekea hilo kuondosha kila kemeo la Allah juu ya waja wake, na kuelekea katika kila Ovu ambalo Sheria imekuja kuliondosha, basi angalia uzito wa Dalili za Qur-ani, na uondoshe shaka katika fikra zako na uikubali Haki.

Dalili ya kwanza:

Amesema Allah:

ولا يشفعون إلا لمن ارتضى

Wala hawatotoa shafaa isipokua kwa wale aliowaridhia.

Basi aya hii iko wazi kua shafaa ya ni kwa wale ambao amewaridhia Allah mtukufu peke yake, na sio kama wanavyodai na kujipalilia matarajio juu ya jambo ambalo hawana ushahidi nalo, bali ushahidi unakua juu yao, kwani Allah mtukufu hawaridhii watu waovu, amesema yeye mwenyewe katika kitabu chake kwa uwazi kabisa:

فإن ترضوا عنهم فإن الله لا يرضى عن القوم الفاسقين

Na hata kama mutaridhia kwao, kwa hakika Allah haridhii kwa watu mafasiki” yaani wanaomuasi yeye bila kutubia.

Dalili ya pili:

Amesema Allah:

ياأيها الذين آمنوا أنفقوا مما رزقناكم من قبل أن يأتي يوم لا بيع فيه ولا خلة ولا شفاعة..

Enyi mulioamini toeni katika tuliyokupeni Rizki kabla ya kuja siku isiyokua na bei ndani yake wala urafiki wala shafaa (uombezi).

Na aya hii iko wazi kabisa kama uwazi wa nuru wakati wa mchana, kwani aya inawahusu waumini, tena kwa kuhadharishwa kua siku hio haitokua na uombezi wala urafiki, wala kuuziana ndani yake; Basi sijui wale wanaojipa amani wapi wamekamatia wakati kitabu cha Allah kinawakanusha na kuwaambia:

ليس بأمانيكم ولا أماني أهل الكتاب من يعمل سوءا يجز به ولا يجد من دون الله وليا ولا نصيرا

Sio kwa Matarajio yenu wala Matarajio ya Wa Kitabu; Atakefanya ovu atalipwa kwalo, wala hatopata asiyekua Allah kipenzi wala muokozi”.

Dalili ya Tatu:

Amesema Allah:

ما للظالمين من حميم ولا شفيع يطاع

Na hawana Madhalimu yeyote wa kua kipenzi, wala Muombezi atakaekubaliwa”

Basi na aya hii iko wazi kabisa kua Dhalimu yeyote yule kutoweza kufaidika na Uombezi wa yeyote yule, basi huyu ambaye amekufa na madhambi makubwa bila ya kutubia kwa mola wake ikiwa dhambi hiyo ni ya kishirikina au sio ya kishirikina hakika yeye yumo katika Madhalimu wa nafsi zao, kwa sababu sifa hii ya udhalimu inapatikana tu iwapo mtu ataidhulumu nafsi yake kwa kumuasi Mola wake, kwa sababu Allah mtukufu amesema:

ومن يتعدى حدود الله فأولئك هم الظالمون

Na mwenye kuichupa Mipaka ya Allah basi hao ndio Madhalimu” na yeye pia amesema kua kuua katika Miezi ya Haram ni Dhulma na akasema:

فلا تظلموا فيهن أنفسكم

Na wala musidhulumu katika miezi hiyo nafsi zenu”, na vile vile anatuelezea kua Baba  yetu Adam na Mama yetu Hawa (r.a) alisema hivi:

ربنا ظلمنا أنفسنا

Ee! Mola wetu tumezidhulumu nafsi zetu”

Vile vile Mtume Yuunus (A.S) alisema:

لا إله إلا أنت سبحانك إني كنت من الظالمين

Hakuna mungu isipokua wewe  umetakasika hakika mimi nilikua katika Madhalim”

Na vile vile Mtume Mussa (a.s) alisema:

رب إني ظلمت نفسي

Ee!! Mola wangu hakika mimi nimeidhulumu Nafsi yangu”

Na wote waliyasema haya baada ya kujua, kua wao walikosea katika aliyoamrisha Allah mola wao, wala hakuna anayethubutu kusema kua wao Walimshirikisha Allah, kwa sababu wale Wazee wetu wao walikula katika mti waliokatazwa na wakamuasi Mola wao, na Mtume Yuunus (a.s) alikimbia watu wake baada ya kuona kua Adhabu itamkumba na yeye, nalo likawa ni kosa kwani Mtume hatakiwi kufanya hivyo isipokua kwa Amri ya Allah, akatubia, na Mtume Mussa (a.s) Aliuwa Nafsi bila ya Kukusudia, akahisi kua amemuasi Allah, basi aya hii inawakatisha tama wale wote wanaojitia tamaa ya Pepo kwa kua wao ni Waislamu tu, na wakajiweka mbali na mafundisho ya Dini yao, wamefanya hayo kwa kufuata mapendwa moyo yao.

UHAKIKA WA DHULMA:

Wako wataosema:

Dhulma hapa ni Ushirikina, kwa sababu Allah amesema:

إن الشرك لظلم عظيم

Hakika Ushirikina ni Udhalimu mkubwa” na kutoka na hapa imepokwa kua liliposhuka Neno lake Allah mtukufu:

الذين آمنوا ولم يلبسوا إيمانهم بظلم أءلئك لهم الأمن وهم مهتدون

Wale walioamini na hawakuingiza Imani yao na dhulma; hao kwao ni Amani na hao ndio walioongozwa” Walihuzunika Maswahaba mpaka akasema Abu Bakar (r.a) : Ewe Mjumbe wa Allah ni nani katika sisi aliyekua hakuichanga imani yake na Dhulma? hapo akasema Mtume (s.a.w): Sio haya ewe Abu bakar hakika Dhulma ni Ushirikina katika sehemu hii, Jee hujaona wewe neno la Luq-man:

يا بني لا تشرك بالله  إن الشرك لظلم عظيم

Ewe kitoto changu usimshirikishe Allah hakika Ushirikina ni Dhulma kubwa” basi ikiwa hivi ndivyo alivyofasiri Mtume (s.a.w) inabainika kua Madhalimu ni Washirikina katika Aya kwa hivyo hao hawapati Uombezi wa Mtume Muhammad (s.a.w) kwa makubaliano ya wote.

Jawabu:

Hakika kuufunga Udhalimu katika Ushirikina tu ni kitu ambacho hakiwezi kukubalika kwa kila anayeangalia na kukisoma vizuri kitabu cha Allah, kwa sababu Dhambi nyingi zimeelezewa na Allah kua ni Dhulma, hata Riba Allah anatuambia kua ni Dhulma kwa sababu amesema:

فإن تبتم فلكم رؤوس أموالكم لا نظلمون ولا تظلمون

Na ikiwa mutatubia basi yenu nyinyi Mali yenu ya Asili tu musije mukadhulumu wala musije mukadhulumiwa” basi tunaona kua kuichukua Riba ambayo ni ongezeko analolichukua anayedai kwa anayemdai kwa mujibu wa wakati, Allah anasema kua ni kudhulumu kwa hivyo Riba hiyo irejeshwe kwa waliodhulumiwa, na mimi nimeona maelezo mazuri sana yanayohusu shub-ha hiyo, na maelezo hayo ameyatoa Sheikh Ahmed bin Hamad Al-khaliliy -Allah amuhifadhi na atupe faida katika Elimu yake-, amesema hivi:

Kama ilivyokua kuikusanya Dhulma katika neno lakealiyetukuka: Wale walioamini na hawakuingiza katika Imani yao Dhulma hao ndio watakaopata Amani na wao ndio walioongozwa”  kua ni Shirki tu peke yake bila kuingia mengine katika madhambi. Na kuifasiri Aya kwa maana hiyo, hakika huko ni khatari kubwa sana juu ya Uislamu kuliko kila Khatari, kwani ufahamu huo utakua ni shoka la kuvunja misingi yake yote, na kuporomosha mazuri yake yote, na kufuta dalili zake zote, kwa sababu haitokua ufahamu wake isipokua yoyote yule anayehisabiwa kua ni katika Walioamini hadhuriki na chochote kile katika atakayofanya katika Maasi isipokua Ushirikina tu, hata kama Ataacha Kusali, na kufunga, na akazuia Zaka, na kutohiji, na akafuata matamanio yake na kutoacha Dhambi yoyote ile bila ya kuifanya, wala hakuna chafu isipokua analivamia, wala Faridha isipokua amekaa nayo mbali, basi yeye hakitokua kitu juu yake ikiwa atakutana na Allah akiwa amejivisha yote hayo ambayo yeye amemlazimisha na yeye hakuyafanya, na yote aliyomkataza na yeye ameyavamia, akiwa ni mzinifu, mwenye kulawiti na kulawitiwa, kuuwa nafsi iliyoharamishwa kuuliwa bila ya Haki, kuasi Wazazi wawili, kukata undugu na mengineyo, ikiwa tu yeye hajajiingiza katika Ushirikina, basi yeye atakua katika wale waliona Amani tena walioongoka, kwani ndivyo Aya inavyosema, basi itikadi hii inafuta kila kemeo lililokuja katika Kitabu cha Allah ambalo limekuja katika Makubwa katika Madhambi yasiyokua ya Kishirikina, na ikiwa itasemwa kua tafsiri hii hakika imepatikana katika mapokezi aliyoyapokea Bukhari na Muslim kwa njia ya Ibn Mas-uud (r.a) mpaka kwa Mtume (s.a.w), na tafsiri iliyosalimika na iliyobora kufuatwa ni ile aliyoifasiri Mtume (s.a.w) mwenyewe; Itajibiwa kua sio kila linaloegemezwa kwa Mtume (s.a.w) ni Hoja, hata kama amepokea Bukhari na Muslim . Kwa sababu Mizani ya usahihi wa mapokezi yanayotoka kwake na udhaifu wake ameiweka mwenyewe Mtume (s.a.w) pale aliposema:

إنكم ستختلفون من بعدي فما جاءكم عني فأعرضوه على كتاب الله فما وافقه فعني وما خالفه فليس عني

Hakika nyinyi mutathitalifiana baada yangu basi litakalo kujieni kutoka kwangu liwekeni katika kitabu cha Allah litakalo kubaliana nacho hilo linatoka kwangu na litakalo pingana nacho basi hilo halitoki kwangu” ameipokea Imam Rabii (r.a) kwa mapokezi sahihi kwa njia ya Ibn Abaas; wala hakuna mazingatio ya kudhoofisha ya waliyoidhoofisha katika Kaumu yetu baada ya kuthibiti  kwetu sisi kwa mapokezi haya makuu, na kuyafanyia kazi Maswahaba (r.a) bila kukhitalifiana baina yao kwa mujibu wa hadithi hii, kwani wangapi katika wao wamerejesha mapokezi ya Maswahaba wenzao waliyokua wakiyasimulia kutoka kwa Mtume (s.a.w), kwa kuona tu kua hayakubaliani na dalili za Qur-ani, kama alivyofanya Omar bin Khattab (r.a) kwa hadithi ya Fatima bint Qais (r.a), na alivyofanya Mama wa Waumin Bibi Aisha (r.a) kwa mapokezi ya Omar na Mtoto wake (r.a) katika kuadhibiwa Maiti kwa kilio cha Jamaa zake juu yake, na alivyofanya Ibn Abaas (r.a) katika kuyarejesha mapokezi ya Hakam bin Amru Al-ghafaariy (r.a) katika kuharamisha Punda wa kufuga, na ikiwa hayo yalitokea katika wakati ule usiyo kua na Doa, na katika  mazingira ya Imani yaliyoko mbali na kila mapendwa moyo, na Bidaa, na uchafuzi wa wapotoshaji, pamoja na ukaribu wake na wakati wa Mtume (s.a.w), basi vipi iwe hivi leo baada ya kupita Muda mrefu, na kuharibika mafundisho kwa wingi wa Bidaa na upotevu na mapendwa moyo, mpaka inachanganyika Haki katika Batili; Jee!! isiwe bora zaidi na usalama zaidi kufuata mwendo uliosalimika, juu ya yote haya sisi tunaona Wanavyuoni wa Hadithi wenyewe hawatofautianai kua katika Sharti za kua hadithi ni sahihi; hadithi hiyo isije ikapingana na Qur-ani, basi vipi zipigiwe pazia Aya zilizo nyingi na hadithi zilizo nyingi kwa ajili ya mapokezi haya peke yake, juu ya kua mapokezi hayo lau kua hayakupingana na kitu chochote, basi inatosheleza upweke wake kutoyafanyia kazi katika mambo ya Itikadi kama walivyoyakubali wenye kuhakikisha katika sisi na wasiokua sisi, juu ya kua yeyote atakaye zingatia uwazi wa Aya yenyewe kwa kutaka kuona ukweli kwa mujibu wa Ulimi wa Kiarabu ambao umetumika katika kushuka Qur-ani, hali ya kua anaongozwa na misingi ya Kiusuli iliyokubalika katika kutolea dalili kwa kuzingatia maana ya maneno ya Sheria, ataona umbali wa kua mbali sana na yale yanayoelezewa na Mapokezi yale ya kua Dhulma ni Shirki tu peke yake kwa hakika neno ظلم  Dhulma limekuja Nakira katika mfumo wa kukataa, na maneno yenye kua na mfumo huo yanaleta maana ya Mkusanyo عام bila khilafu, kwa hivyo kila aina ya udhalimu inaingia ikiwa ni kubwa au ndogo, na kama hivyo haitokubalika basi tutasema nini katika neno lake Allah:

ما اتخذ الله من ولد وما كان معه من إله

Hakujifanyia Allah katika watoto wala hakua mapoja na yeye katika Mungu yeyote” Jee!! itawezekana kuchukua yaliyokataliwa na Aya hii katika Mtoto na Mungu waliokataliwa katika aya Bila ya mkusanyo? Hapana ninaapa hawezi kuyasema hayo mwenye kua na chembe ya Imani katika Moyo wake, na mwenye kutumia Akili yake, kwa sababu maneno yake hayo yataporomosha Upweke wa Allah wa kujuzisha kua na Allah Watoto kwa kuyahukumu yaliyokataliwa katika Aya kua ni Baadhi ya Watoto tu na vile vile katika Uungu, na lau hayo yangalifaa yasingelikua maneno haya لا إله إلا الله Hapana Mungu ispokua Allah” kua ni maneno ya Kumpwekesha Allah nayo ni Kumpwekesha Allah wa Makubaliano, basi namna hivi kutokana na kua Dhulma haingii katika Ushirikina tu Peke yake bali na katika Makosa mengine, kwa sababu maana yake ni kuweka kitu pasipo kua pahala pake, wameikubali Manabii -Juu yao iko Amani-, na wao wako mbali na Ushirikina, kwani amesema Mussa (a.s) Ee!! Mola wangu hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu” aliyasema hayo kwa kumuua Kib-tiy, na amesema Yuunus (a.s): Hapana mola isipokua wewe umetakasika hakika mimi nilikua katika Madhalimu” na amesema Adam na Hawa: Ee!! Mola wetu tumedhulumu nafsi zetu na ikiwa hukutusamehe sisi na ukaturehemu kwa hakika tutakua miongoni mwa waliokhasirika” nao wanakusudia kule kula kwao Mti, na amesema Allah katika kuwasifu Wachamungu: Na wale ambao wanapofanya Uchafu au wakadhulumu Nafsi zao wanamkumbuka Allah na kuomba msamaha kwa madhambi yao na nani wa kusamehe Makosa isipokua Allah” na amesema baada ya kuelezea Adabu ya Mwizi wa kiume na wa kike: Na atakaetubia baada ya Dhulma yake na kufanya Mazuri kwa hakika Allah Atatubia juu yake” na Dhulma hapa ni Wizi na amesema vile vile: Hakika Idadi ya Miezi kwa Allah ni miezi kumi na mbili katika Kitabu cha Allah  siku alipoumba Mbingu na Ardhi; katika hiyo; Minne ni mitakatifu, hiyo ndiyo Dini iliyosafi basi Musidhulumu ndani yake Nafsi zenu” Yaani kwa Kupigana katika Miezi ile mitakatifu, na ametaja baada ya kutaja katika hukumu za Talaka: Hiyo ni mipaka ya Allah na mwenye kuichupa mipaka ya Allah kwa hakika amedhulumu Nafsi yake” na amesema katika Walioachwa: Na wala musiwazuie kwa kufanya madhara mukaja mukafanya Uadui na mwenye kufanya hayo kwa hakika amedhulumu nafsi yake” Na amesema baada ya kutaja Hukumu za Kujikomboa na Talaka: Hiyo ni mipaka ya Allah na mwenye kuichupa mipaka ya Allah basi hao ndio Madhalimu” na amesema Allah: Enyi mulioamini: wasiwadharau watu katika watu kwani huenda wakawa ni bora kuliko wao; na wanawake katika wanawake huenda wakawa ni bora kuliko wao; wala musivunjiane heshima wala musiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu hao ndio wenye kudhulumu” na yamekuja katika mapokezi mengi sana yanayoonyesha kuingia Madhambi katika Dhulma, miongoni mwa hayo neno lake (s.a.w): Kuchelewesha Tajiri ni Dhulma” Yaani kulipa Deni”.

Basi jawabu hii inatutosheleza kutokana na Ubainifu uliomo ndani yake usioingiwa na Chmbe ya Shaka kwa mwenye kutaka Haki iko wazi.

Dalili katika Sunna

Na katika Sunna ya Mtume (s.a.w) yamekuja mafundisho sahihi kabisa kua Shafaa yake itakua mbali na wale wote wanaotenda makosa Makubwa nao wakaondoka hapa duniani bila ya kutubia, na miongoni mwa Hadithi hizo ni hizi zinazofuata:

عن أبي هريرة-رضي الله عنه- أن النبي –صلى الله عليه وسلم- قال: يا بني عبد مناف اشتروا أنفسكم من الله يا بني عبد المطلب اشتروا أنفسكم من الله يا أم الزبير بن العوام عمة رسول الله صلى الله عليه وسلم يا فاطمة بنت محمد اشتريا أنسكما من الله لا أملك لكما من الله شيئا سلاني من مالي ما شئتما

Kutoka kwa Abi Hurairah (r.a) kua Hakika Mtume (s.a.w) alisema: Enyi Watoto wa Abid Manafi zinunueni Nafsi zenu kwa Allah, Enyi Watoto wa Abid Muttalib zinunueni Nafsi zenu kwa Allah, Ewe Mama wa Zubeir Bin Awwaam Shangazi wa Mjumbe wa Allah (s.a,w)  Ewe Fatima mtoto wa Muhammad zinunueni Nafsi zenu kwa Allah; Similiki kwa Allah kwa ajili yenu chochote, niombeni katika Mali yangu munayopenda”

Amesema Mtume (s.a.w) kwa kupitia njia ya Abi Hurairah:

لا ألفين أحدكم يأتي يوم القيامة على رقبته فرس له حمحمة, يقول: يا رسول الله أغثني,, فأقول لا أملك لك من الله شيئا, قد أبلغتك. وعلى رقبته بعير له رغاء؛ فيقول: يا رسول الله أغثني,, فأقول لا أملك لك من الله شيئا, قد أبلغتك. وعلى رقبته صامت فيقول: يا رسول الله أغثني,, فأقول لا أملك لك من الله شيئا, قد أبلغتك. وعلى  رقبته رقاق تخفق فيقول: يا رسول الله أغثني,, فأقول لا أملك لك من الله شيئا, قد أبلغتك.

Nisije nikakuta na mmoja wenu anakuja siku ya Kiama na yeye amelazimika na Farasi naye ana Hamahamah (Milio wa Farasi) Atasema: Ewe!! Mjumbe wa Allah Niokoe,, Na mimi nitamwambia: Similiki kwa ajili yako kwa Allah kitu chochote, kwa hakika Nilifikisha. Na mwengine amelazimikiwa na Ngamia naye ana Rughaau (Mlio wa Ngamia);  Atasema: Ewe!! Mjumbe wa Allah Niokoe,, Na mimi nitamwambia: Similiki kwa ajili yako kwa Allah kitu chochote, kwa hakika Nilifikisha. Na mwengine Amelazimikiwa na Saamit ( Dhahabu na Fedha),,  Atasema: Ewe!! Mjumbe wa Allah Niokoe,, Na mimi nitamwambia: Similiki kwa ajili yako kwa Allah kitu chochote, kwa hakika Nilifikisha. Na mwengine amelazimikiwa na Nguo Inayon`gara,,  Atasema: Ewe!! Mjumbe wa Allah Niokoe,, Na mimi nitamwambia: Similiki kwa ajili yako kwa Allah kitu chochote, kwa hakika Nilifikisha.

عن كعب بن عجردة قال: خرج علينا رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: اسمعوا أنه سيكون من بعدي أمراء, فمن دخل عليهم فصدقهم بكذبهم وأعانهم على كذبهم فليس مني ولست منه وليس بوارد على الحوض”

Yamepokewa kutoka kwa Kaab bin Aj-radah kua alisema: Alitoka kwetu sisi Mjumbe wa Allah (s.a,w)  na akasema: Sikilizeni, Kwa hakika watakua baada yangu viongozi, atakayeingia kwa viongozi hao akawasadiki kwa uongo wao, au akawasaidia katika uongo wao, huyo hayuko pamoja nami wala siko pamoja naye wala hawezi kulifika Hodhi langu”

حديث سهل بن سعد رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: أنا فرطتكم على الحوض، من ورده شرب منه، ومن شرب منه لم يظمأ بعده أبدا، وليردن علي أقوام أعرفهم ويعرفونني، ثم يحال بيني وبينهم”

Hadithi ya Sahal bin Saad (r.a) alisema: Alisema Mjumbe wa Allah (s.a,w): Mimi ninawasubiri katika Hodhi, atakaye lifika atakunywa humo, na atakayekunya kumo hatopata kiu baada yake milele, na watanijia watu Nawajua na wao wananijua, kisha watazuiwa baina yangu na baina yao”

Kwa hakika Hadithi hii, inaonyesha wazi kua kuna watu watazuiwa kulifika Hodhi la Mtume (s.a.w), na kuzuiwa huko ni Dalili ya kukatika mahusiano baina ya Mtume (s.a.w) na watu hao, Jee!! Ni watu gani hao? Amepokea Bukhari na Muslim na wengineo kwa njia ya Abi Saidi L-khudriy na nyongeza:

فأقول: إنهم مني. فيقال: إنك لا تدري ما بدلوا بعدك” فأقول: سحقا لمن بدل بعدي”

Nitasema: Hakika hao ni katika mimi. Itasemwa: Hakika wewe hujui waliyobadilisha baada yako” Nitasema: Mbali (Adhabu) kwa aliyebadilisha Baada yangu”

Basi mambo ni kama hivyo, ni miongoni mwa waliokua pamoja na Mtume (s.a.w), kama ilivyokuja katika baadhi ya Njia zake:

أعرفهم ويعرفونني”

Ninawajua na wananijua” Amesema Sheikh Qannubiy (h.a) :

وقد نص ابن عبد البر في “التمهيد” على أنه حديث متواتر، وهو كما قال”

Na ameweka wazi Ibn Abd L-bar katika “TAMHID” ya kua ni MUTAWATIR, nayo ni kama alivyosema” Basi Hadithi hiyo ni Mutawatir ambayo inatupa Elimu ya Yakini isiyokua na Shaka” Sasa hao wanafukuzwa na Mtume (s.a.w) nao ni miongoni mwa waliokua Masahaba wake, tena hali ndio kama inavyoelezwa, haina haja kurefusha sana.

Naona Hadithi hizi zote ambazo Zinaelezea kwa uwazi kabisa kua hakuna fungamano baina ya Mtume (s.a.w) na watu waliokufa na Madhambi makubwa bila ya Kutubia, zinatosha kua ni Dalili kwa mwenye Macho, na pia ikibainika kua mwenye kufanya Dhambi kubwa hawezi kutoka katika adhabu ya moto milele basi itafahamika kua maombezi ya Mtume (s.a.w) hayawezi kupatikana kwa watu wa  motoni, kwa sababu vitu viwili hivyo, haviwezi kukutana lazima kimoja kitakua ni Batili, na kwa sababu hoja za kukaa milele motoni ziko wazi, basi hakuna njia nyengine isipokua ni kusema kua Shafaa ya Mtume (s.a.w) kwa wanaotenda makosa makubwa bila Kutubia ni tamaa isiyokua na uhakika, na kwa Yakini ni jambo la uzushi, na lisilokuwa isipokua kwa Wachamungu tu Ambao Allah aweradhia, kwa sababu Allah Haridhii watu Mafasiki kama alivyo sema kwa Uwazi kabisa , na Mtu aliyekufa na makosa makubwa bila ya kutubia ni Fasiki bila ya Shaka yeyote ile, na vipi aingie peponi mtu asiyekua na Toba? Kwa sababu Allah mtukufu amesema:

وليست التوبة للذين يعملون السيئات حتى إذا حضر أحدهم الموت قال إني تبت الآن ولا الذين يموتون وهم كفار أولئك أعتدنا لهم عذابا أليما

Wala hakuna Toba kwa wale wanaofanya Makosa mpaka yanapofika kwa mmoja wao Mauti akasema: Mimi ninatubia hivi sasa” wala wale waliokufa na wao ni Makafiri; hao tumewaandalia Adhabu inayoumiza”

Pia ifahamike kua Hadithi zote zile zinazoonyesha kua wenye kufanya Kosa kubwa; kama vile Wanawake wanaovaa Miili yao ambao wameenea hivi sasa, na wale waliojiua nafsi zao, na wale aliokula riba na wengineo ambao makosa yao sio Ushirikina nao wamehukumiwa katika hadithi hizo kua ni wa kukaa Motoni Mielele, zote hizo ni dalili kwa mujibu wa tulivyoeleza kua uombezi huo hauwezi kukutana na Adhabu hiyo.

Na kushikamana na yaliyokubaliana na Ufahamu sahihi wa Qur-ani ni bora zaidi, na vile vile kujiweka katika yakini ni bora zaidi, kuliko kujiweka katika Shaka na khilafu, kwa sababu ikiwa hiyo Shafaa itapatikana, basi bila ya Shaka na hawa wanaoitakidi kua hakuna Shafaa itawakuta na wao, kwa sababu wao ni Waislamu tena kwa mujibu wa itikadi hiyo ambayo kwao ndio Sahihi watakua na hadhari kubwa sana katika Makosa ambayo wao wameteleza ili wasije wakatoka katika Ulimwengu huu wakiwa wenye kuangamia katika Adhabu ya mielele.

KISA KIDOGO KATIKA SHAFAA:

Walikutana Mashekhe wawili, mmoja ni miongoni mwa wanaokataa Shafaa ya Mtume (s.a.w) ya kuwatoa waliotenda makosa makubwa motoni; tamuhifadhi jina na hapa tutamwita Y, na mwengine ni katika wale wanaoshikilia jambo hilo kwa kila hali ya yeye tutamwita X, na yakawa malumbano baina yao katika suala hili kama ifuatavyo:

X: Unasemaje kuhusu wanaokufa hali ya kumuasi Mwenyezi Mungu nao sio Washirikina na wala hawakutubia kwa makosa yao?

Y: Watu wenye sifa hizo ulizozitaja bila shaka, hukumu ya Allah juu ni kua watahukumiwa kua ni watu wa motoni milele.

X: Vipi unasema hivyo ndugu yangu wakati yamepokewa kua Mtume (s.a.w) amesema: شفاعتي لأهل الكبائر من أمتي  Shafaa yangu ni kwa ajili ya waliofanya Makosa makubwa katika Umma wangu”

Y: Ndio mimi siyapingi hayo lakini kwa sharti ya kutubia kabla ya kufa.

X: Vipi unasema?! Mtume anasema kwa walio kua na makosa makubwa, wewe unasema kama wakitubia, kwani anayetubia atakua hana makosa makubwa tena, sasa vipi utakua na ukweli usemi wa Mtume(s.a.w)?

Y: Ndugu yangu unaonyesha wewe ni mkali sana na mwenye tama sana ya pepo kwa hali yoyote ile.

X: Kwa nini ukasema hivyo?

Y: Ndio kwani kutokana na maneno yako, inaonekana wazi kua Mtume (s.a.w) hawezi kusema maneno hayo kwa maana hiyo unayoisema wewe.

X: Kwa nini?

Y: Ndio kwa sababu atakua Mtume (s.a.w) anawaamrisha Waislamu kufanya makosa. Nalo ni jambo lisilowezekana kiakili na kunakili.

X: Vipi lisiwezekane wakati Allah ndivyo alivyohukumu?.

Y: Hapana shaka, basi kwa anayetaka Shafaa ya Mtume (s.a.w) na ajikaribishe kwenye Shafaa hiyo kwa kufanya makosa makubwa, ili awe katika wale watakaopata Shafaa ya Mtume (s.a.w) kiuhakika kabisa, kwa hivyo tusisali tusifunge, tena tukazini na kulawitiana, na tuuwe na kuiba, tuwapige wazazi wetu, na tujitahidi kumuasi Mwenyezi Mungu kwa sharti la kujiweka mbali na kosa la Ushirikina tu, ili tukaribie zaidi katika Shafaa ya Mtume (s.a.w). Unasemaje ndugu yangu?

X: Hapana mimi sisemi hivyo.

Y: Sasa una maana gani?

Kimya.

TAHADHARI

Ndugu Muislamu unajua Allah mtukufu ametuelezea kwa uwazi kabisa yale waliyoyafanya waliopita kabla yetu, ili iwe ni fundisho kwetu tusije tukajiingaza katika mambo hayo, na miongoni mwa hayo ni yale aliyosema Allah:

فخلف من بعدهم خلف ورثوا الكتاب يأخذون عرض هذا الأدنى ويقولون سيغفر لنا وإن يأتهم عرض مثله يأخذوه ألم يؤخذ عليهم ميثاق الكتاب أن لا يقولوا على الله إلا الحق ودرسوا ما فيه والدار الآخرة خير للذين يتقون أفلا تعقلون

Wakafuatia baada yao Waliofuatia walirithi Kitabu wanachukua Pato hili la chini na wanasema Tutasamehewa sisi” na likiwajia Pato mfano wake walichukua; Jee!! haikuchuliwa juu yao Ahadi ya Kitabu kua wasije wakasema juu ya Allah isipokua la Haki na wakasoma yaliyomo ndani yake? Na nyumba ya Akhera ni bora kwa ajili ya Wachamungu jee hamuzingatii” Basi huu ndio uhakika kua “Tuyafenye bwana kisha si tutasamehewa”.

Allah atuepushe na kufuata Nyayo za waliopita kabla yetu, kwani wao walipotea kwa kukaa mbali na uhakika wa mafundisho waliyoletewa, na kuingiwa na Mapendwa moyo ndani yake, basi yalibadilika na yakawa kama hivyo ulivyoona.

MIZANI SIKU YA MALIPO.

Huenda likaletwa suala la Mizani, kwa hivyo inalazimika kuliweka wazi ili njia yetu ifahamike, basi tunasema kua mizani ya siku ya Kiama itakua katika mfumo alioueleza Allah katika kitabu chake kwani yeye amesema:

ونضع الموارين القسط ليوم القيامة فلا تظلم نفس شيئا وإن كان مثقال حبة من خردل أتينا بها وكفى بنا حاسبين”

Na tutaeka Mizani Adilifu kwa aliji ya siku ya Kiama; hakuna kudhulumiwa Nafsi chochote, na ikiwa ni uzito wa tembe ya khardali tutakuja nayo, na inatoshelesha kua sisi ni wenye kuhesabu” kwa hivyo Mizani ni jambo lililothibiti katika kitabu cha Allah mtukufu na amesema vile vile:

والوزن يومئذ الحق  فمن ثقلت موازينه فأولئك هم المفلحون * ومن خفت موازينه فأولئك الذين خسروا أنفسهم بما كانوا بآياتنا يظلمون

Na Mizani siku hii ni Haki; Atakaye kua Mizani zake ni mzito; hao ndio waliofaulu * Na atakaye kua Mizani zake ni nypesi; hao wamekhasirika nafsi zao kutokana na walivyokua kwa aya zetu wakidhulumu” kwa hivyo mpaka hapa unapata uoni wa Haki, kua vipi mezeni ya Haki itakavyokua siku ya Malipo? Ni Haki tu nayo ni kupimwa ya waja, ima hayo yanayopimwa yatakua ni mazito, au yatakua ni mepesi. Wale ambao Mizani zao zitakua ni mzito wao wamefaulu, na wale ambao mizani zao ni nyepesi wao wamekhasirika; wala hakuna Aya inayoonyesha kwa uwazi kua mizani za waja hazitokua nyepesi wala mzito, Ima Mizani ziwe mzito au nyepesi tu, zikiwa mzito huko ni kufaulu katika neema za milele, na zikiwa nyepesi huko ni kukhasirika katika Adhabu ya milele –Allah atuepushe nayo- Na hivi ndivyo zilivyo aya zote zinazoelezea Mizani katika kitabu cha Allah Qur-ani, sasa vipi Mizani zitakua nyepesi au mzito?

UHAKIKA WA MIZANI

Pengine tunaweza kua na fikra ya kua siku ya Malipo kutaekwa Mizani kubwa kama hii tunayoifahamu hapa Duniani, na kua Mizani hiyo itakua na Vitanga viwili; kimoja kiko upande wa kushoto, na kingine kiko upande wa kulia, na kua vitanga hivyo viwili vimeshikiliwa na fungo au mlingoti kwa kutopendelea upande wowote wa hivyo vitanga, Mja atapimiwa matendo yake kwa kuwekwa Mema yake katika kitanga cha Kulia na Mabaya yake katika Kitanga cha Kushoto, kisha ima kitanga cha kulia kitakua kizito na kukizidi kile cha kushoto, hapo itakua Mizani yake ya mambo mema imekua mzito, au kitanga cha mambo mema kitazidiwa na kile kitanga cha mabaya na hapo itakua Mizani yake ya Mema imekua nyepesi kwa kuzidiwa na mabaya, hii ni picha ya Mizani ya kupimiwa matendo ya waja.

Basi tunasema kua picha hii sio muhimu kuwemo katika vichwa vyetu, bali ikiwa kwa maana ya kushindanisha uzito wa mema na mabaya basi Mizani hiyo itakua ni Batili, kwa sababu itapeleka kughururika katika kushindanisha mema na mabaya, kwa maana mtu na afanye mabaya, kisha afanye mema tu bila kutubia kutokana  na yale mabaya, na hii ndio ghururi.

Basi tunasema kua mizani ya Mja itakua mzito kwa kukubaliwa matendo yake Mema na itakua nyepesi kwa Kukataliwa matendo yake mema, kwa hivyo hii ndio Mizani ya uadilifu kabisa, na ndio Haki ya kuikubali katika Itikati Sahihi, basi ikiwa yamekubaliwa Mema yake hapo malipo yake katika Daraja za Pepo, itakua kwa mujibu wa matendo yake mema, na Mema yataondosha Mabaya aliyoyafanya ambayo ametubia kwayo, na ikiwa yatakataliwa Matendo yake Mema hapo imekua nyepesi Mizani yake, na yeye atakua katika Daraja za Motoni kwa Mujibu wa Matendo yake Mabaya, na kua mema yake yataporomoka wala hatopata malipo yake. Basi huu ndio uhakika wa kushikamana nao, na ndio haki isiyokua na Chembe ya doa. Basi huu ndio uhakika kama alivyosema Allah mtukufu:

فمن ثقلت موازينه فأولئك هم المفلحون * ومن خفت موازينه فأولئك الذين خسروا أنفسهم في حهنم خالدون

Na mwenye kua mzito Mizani zake; hao ndio watakaofaulu * Na mwenye kua nyepesi Mizani zake; hao ndio wale waliozikhasiri nafsi zao katika Jahannam watakaa milele.

KUKUBALIWA MATENDO MEMA.

Allah mtukufu ametuelezea katika kitabu chake kwa uwazi kabisa kwa kusema: إنما يتقبل الله من المتقين  Hakika mambo yalivyo; anakubali Allah yatokayo kwa wachamungu” Kwa hivyo hawa ndio watakaofanikiwa kwa kua mzito Mizani zao, na kama tulivyobainisha kua hakuna Toba kwa wale watakaoondoka Duniani hali ya kua wao wamebeba mizigo ya Dhambi kubwa bila ya kutubia, na kua hao wameandaliwa adhabu kali inayoendelea, basi inabainika kua wao ndio watakao haribikiwa kwa kuporomoka mema yao kutokana na Makosa hayo, na hapo kutapelekea kukosa malipo yake huko Akhera amesema Allah mtukufu:

ووصينا الإنسان بوالديه إحسانا حملته أمه كرها ووضعته كرها وحمله وفصاله ثلاثون شهرا حتى إذا بلغ أشده وبلغ أربعين سنة قال رب أوزعني أن أشكر نعمتك التى أنعمت علي وعلى والدي وأن أعمل صالحا ترضاه وأصلح لي في ذريتي إني تبت إليك وإني من المسلمين * أولئك نتقبل عنهم أحسن ما عملوا ونتجاوز عن سيئاتهم في أصحاب الجنة وعد الصدق الذي كانوا يوعدون

Na tumemuusia Mtu kwa wazazi wake wawili Wema; amemchukua mama yake kwa machukivu na amemzaa kwa machukivu; na Mimba yake na kuachizwa kwake ni miezi thelathini; mpaka atakapo fikia ukomo wake na akafikia miaka arobaini anasema: Ee!!Mola wangu niwezeshe mimi nishukuru Neema zako ambazo umeneemesha juu yangu na juu ya wazazi wangu wawili, na nifanye mazuri unayoyaridhia, na nitengenezee vizuri katika kizazi changu, hakika mimi ninatubia kwako na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu * Hao tunakuli kutoka kwao Mazuri waliyoyafanya na tunawasamehe makosa yao, ni katika wa Peponi, ni ahadi ya kweli ambayo walikua wameahidiwa”

Basi ndio kama hivi; uhakika unan`gara kama jua kwa mwenye macho, ndio maana Allah akasema kwa uwazi kabisa:

يوم لا ينفع مال ولا بنون إلا من أتى الله بقلب سليم

“Siku ambayo haitofaa mali wala watoto, isipokua atakayemwendea Allah kwa moyo uliosalimika” Yaani uliosalimika na Maasi. Na haya ndiyo yanayokwenda sambamba na lile neno lake la uadilifu: :

الذين آمنوا ولم يلبسوا إيمانهم بظلم أءلئك لهم الأمن وهم مهتدون

Wale walioamini na hawakuingiza Imani yao na dhulma hao kwao ni Amani na hao ndio walioongozwa” na kama tulivyobainisha kua Dhulma hapa ni kila kosa kubwa, basi Wachamungu ndio watakaokubaliwa matendo yao mema na kwao ndio mwisho mwema والعاقبة للتقوى  Na mwisho mwema ni kwa Uchamungu” والعاقبة للمتقين Na mwisho mwema ni kwa Wachamungu”. Na ili kuwakatisha tamaa wenye tama zao, amesema Allah kwa uwazi unaon`gara kama jua wakati wa mchana:

تلك الجنة التي نورث من عبادنا من كان تقيا

Hiyo ni pepo ambayo tutawarithisha katika waja wetu aliyekua ni Mchamungu” Basi vipi aingie ndani yake asiyekua Mchamungu? Vipi aingie wakati yeye hakuwaridhia

فإن ترضوا عنهم فإن الله لا يرضى عن القوم الفاسقين

Na hata kama mukiridhia kwao hao; kwa hakika Allah haridhii watu mafasiki” yaani wanaomuasi yeye bila kutubia.

Hakika Allah anatuelezea kosa amablo sio la Ushirikina kwa Makubaliano, kisha analisema kua kama tutalifanya itakua ni Ufasiki kwetu, na hayo yako wazi katika neno lake:

ولا يضار كاتب ولا شهيد وإن تفعلوا فإنه فسوق بكم

Wala asidhuriwe muandikaji wala shahidi, na mukija mukifanya, hakika hilo litakua ni Ufasiki kwenu” basi tunaona kwa uwazi kua kosa hilo la kumdhuru Muandikaji au Shahidi ni Ufasiki, kisha sisi turejee kwa kusema kua Ufasiki ni Ushirikina tu, uyajue haya vizuri, usije ukafuata nyayo za upotoshaji, na Allah atuhifadhi, kwa kuwemo katika Maridhawa yake (Amin).

KUPOROMOKA MEMA YA WALOONDOKA

BILA KUTUBIA.

Basi kama tulivyoona hapo juu, kua ikiwa Mtu ameondoka katika maisha haya na yeye Hajatubia na makosa yake makubwa, kwa hakika mtu huyo yumo katika khasara kubwa ya kuadhibiwa katika adhabu ya Moto milele bila ya kutoka humo, na kutokana na msingi huo usio kua na shaka yoyote ile, bila shaka yale mazuri ambayo ameyafanya yataporomoka malipo yake, kwa hivyo huyo atalipwa kwa mujibu wa mabaya yake, na dalili za haya tunayoyasema zipo kwa wingi kabisa ndani ya kitabu cha Allah mtukufu, na ndio maana Mtume (s.a.w) alisema: هلك المصرون  Wameangamia wenye kuendelea na Maasi” Na hali hii ya kuporomoka malipo ya mema kwa sababu ya makosa makubwa, Allah ameileza na kuitahadharisha kwa Waumini kwa kusema:

ياأيها الذين آمنوا لا ترفعوا أصواتكم فوق صوت النبي ولا تجهروا له بالقولكجهر بعضكم لبعض أن تحبط أعمالكم وأنتم لا تشعرون

Enyi muliomini musinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii; wala msidhihirishe kwake maneno kama Udhihirisho wa Baadhi yenu kwa Baadhi, zisije zikaporomoka Aa-mali zenu na nyinyi hamuhisi”

Basi katika Aya hii inaonekana kua kunyanyua sauti tu mbele ya Mtume (s.a.w) au kusema nae kwa maneno bila kujali heshima yake na cheo chake alichopewa na Allah, kunapelekea kuporomoka kwa Matendo yote ya mja aliyomtii Mola wake, tena maneno hayo yanawaelekea Walioamini. Na pia Allah amewahadharisha wanaotoa Sadaka kwa kusema:

ياأيها الذين آمنوا لا تبطلوا صدقاتكم بالمن والأذى

Enyi mulioamini musibatilishe sadaka zenu kwa kusimanga na maudhi” Basi tunaona kua kosa la kusimanga au kuudhi linapelekea kubatilika kwa matendo ya kumtii Allah mtukufu, na hapa ni Sadaka ambayo wengi wa Waumini wanajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kupitia ibada hiyo, Basi ndio maana Allah akatuhadharisha kwa ujumla kwa kusema:

ياأيها الذين آمنوا أطيعوا الله وأطيعوا الرسول ولا تبطلوا أعمالكم

Enyi mulioamini mumtii Allah na mumtii Mtume wala musibatilishe Aa-mali zenu”.

Na Aya hii inaonyesha kua Waumini wanatakiwa kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w), kisha ikamalizia kua wasizibatilishe Aa-mali zao, inaonyesha wazi kua Aa-mali hizo zitabatilika tu iwapo watatoka nje ya Amri hiyo aliyowaamrisha, kwa hivyo kila Kosa kubwa linabatilisha Matendo ikiwa aliyelifanya Hakutubia; Basi ni nani anaethubutu kusema kua anayezini au kulewa au mfano wa hayo katika aliyoyakataza Allah mtukufu, au atakayewacha kutenda aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kama Sala au kufunga Ramadhani, au kwenda Hija, kua mtu wa aina hiyo hayumo katika kumuasi Mwenyezi Mungu?

Kwa hivyo ni kusema kua kumuasi Mwenyezi Mungu au Mtume (s.a.w) kunapelekea kubatilisha Aa-mali za mja, na uhakika huu unapatikana katika Aya hii tukufu:

ذلك بأنهم اتبعوا ما أسخط الله وكرهوا رضوانه فأحبط أعمالهم

Hayo ni kwa sababu wameyafuata yanayomkasirisha Allah na wakachukia Maridhio yake, basi akaporomosha Matendo yao”

Na Aya iko wazi kabisa kua sababu kubwa iliyopekea kuporomoka matendo yao ni kule kufuata yanayomkasirisha Allah, nao wakachukia kuingia katika Maridhawa yake; yaani kutubia kutokana na Makosa yao kabla ya kuwafikia Mauti, kwa sababu Mwenye kufa na kosa kubwa Huyo ni Fasiki na Allah amesema:

فإن ترضوا عنهم فإن الله لا يرضى عن القوم الفاسقين

Na hata kama mukiridhia kwao hao; kwa hakika Allah haridhii watu mafasiki”

Basi haya ndio ya uhakika yanayokwenda sambamba na mafundisho ya Qur-ani tukufu, basi tuwe macho katika dini yetu, na tuyafuate yale anayoyaridhia Allah na tuyaepuke yale yote aliyoyakasirikia kabla ya kufikiwa na Mauti, ili tupate mafanikio huko tunakokwenda, na ndio Allah akasema katika kitabu chake:

يوم تجد كل نفس ما كسبت من خير محضرا وما كسبت من سوء تود لو أن بيتها وبينه أمدا بعيدا ويحذركم الله نفسه والله رؤوف بالعباد

Siku itakayokuta kila Nafsi yale iliyofanya katika Mema yameletwa, na iliyochuma cha mabaya itatamani lau kua baina yake na baina ya hayo (Mabaya) kuna umbali wa mbali; anakuadharisheni Allah na Nafsi yake (hukumu yake au Adhabu yake) na Allah ni Mpole kwa Waja”.

Basi kutokana na Rehma na Upole huo wa Allah, yeye amefungua mlango wa Toba, ili tuhakikishe Uchamungu ambao ndio silaha pekee ya kujiokoa na Adhabu kali yenye kuendelea katika Moto, kwa hivyo tujivike sifa hiyo kama alivyoitaja Allah kwenye kitabu chake pale aliposema:

والذين إذا فعلوا فاحشة أم ظلموا أنفسهمذكروا الله فاستغفروا لذنوبهم ومن يغفر الذنوب إلا الله ولم يصروا على ما فعلوا وهم يعلمون

Na wale ambao wanapofanya uovu au wakadhulumu nafsi zao wanamkumbuka Allah na wakaomba msamaha kwa madhambi yao – na nani wa kusamehe madhambi isipokua Allah – wala hawakuendelea na hayo waliyoyafanya nao wanajua”

Sasa haya tuliyoyaeleza jee!! yamepatikana vile vile katika Sunna ya Mtume (s.a.w) na katika Misimamo ya Masahaba wake (r.a)?

Jawabu:

Ndio haya yamepokewa, na hapa tunaleta Hadithi nyengine mbali ya Ile inayosema ” Wameangamia wenye kuendelea na Madhambi” ambayo tumeieleza hapo nyuma: Basi yamepokewa kutoka kwake Mtume (s.a.w) kua alisema:

واعلموا أن الله قد افترض عليكم الجمعة في مقامي هذا، في يومي هذا، في شهري هذا، من عامي هذا إلى يوم القيامة، فمن تركها في حياتي أو بعدي وله إمام عادل أو جائر اسخفافا بها أو جحودا لها فلا جمع الله له شمله ولا بارك له في أمره ألا ولا صلاة له ولا زكاة له ولا حج له ولا صوم له ولا بر له حتى يتوب فمن تاب تاب الله عليه”

Na mujue Hakika Allah amelazimisha juu yenu Ijumaa katika   kisimamo changu hichi, katika siku yangu hii, katika mwezi wangu huu, katika mwaka wangu huu mpaka siku ya Kiama, basi atakayeiacha katika Uhai wangu au baada yangu, na yeye anaye kiongozi muadilifu au mjeuri, kwa kudharau haki yake, au kuipinga hiyo, Ee!! Hatokusanya Allah kundi lake, na hatobariki kwake katika Jambo lake, Ee!! wala hana sala huyo, wala hana Zaka huyo, wala hana Hija huyo, wala hana Funga huyo, wala hana Wema huyo, mpaka atubie, atayetubia basi Allah atamsamehe”

Basi hadithi hii hapa inatuonesha wazi kabisa, kua yeye hana kitu, na kua huko kuzuiliwa kunufaika na Kitu katika Hayo, ni moja katika Adhabu ya Kosa lakehilo, na ikiwa atatubia na kujivua na kosa hilo basi Allah atakubali Amali zake zote, basi ndugu zangu tuyajue haya vizuri wala tusihadaike.

Na yamepokewa kutoka kwa Bibi Aisha Mama wa Waumini (r.a) kua alimwambia Suriya wa Zaidi bin Arqam (r.a):

أبلغي زيدا أنه قد أبطل غزوه وجهاده مع رسول الله صلى الله عليه وسلم، وأبطل حجه وصلاته وصيامه إن لم يتب”

Nenda ukamfikishie Zaid kua hakika Ameshabatilisha kupigana kwake, na Jihadi yake pamoja na Mjumbe wa Allah (s.a,w), na kua ameshabatilisha Hija yake na Funga yake ikiwa hakutubia” unaona Hukumu mzito kama hii inatoka kwa nani inamuelekea nani? Jee!! anaweza kusema jambo asilolijua? Jee!! yuko aliyemrudi katika Masahaba (r.a)? Jee!! aliyeelekezewa hukumu hii aliritadi? Hapa hakuritadi, bali kosa lakelinaezwa:

وذلك أن زيدا ابتاع جارية من سريته بثمانمائة درهم إلى خروج العطايا فاشترتها منه السرية نقدا بستمائة درهم ”

Na hayo ni kwa sababu Zaidi alinunua Mjakazi kwa Suria wake kwa Dir-ham mia nane mpaka itakapotoka Mishahara, kisha akanunuliwa Mjakazi, na Suria wake kwa malipo ya Dir-ham mia sita za hapo hapo” Hili ndio kosa, na kosa hili ni kua umefanyika Ujanja wa kula Riba tu, kwa kua Zaid bin Arqam (r.a) kachukua Dir-ham mia sita na atakuja lipa Dir-ham mia nane; kwa hivyo kwa sababu ya kosa hilo ikabidi Bibi Aisha (r.a) atoe hukumu ile kali, na yote hayo inaonyesha kua Bibi Aisha (r.a) aliona kua Zaid bin Arqam (r.a) amefanya Kosa kubwa la kuingia katika Laana za Allah, na katika yanayokubalika katika Itikadi Sahihi ni kua Mema na Mwenye kosa Kubwa yanaporomoka Malipo yake ikiwa mwenye makosa hayo hakutubia.

Basi naona tutosheke na Dalili hizi za Uwazi kabisa kwa mwenye macho na Busara anafahamu usahihi wa tunayoeleza.

HADITHI YA MTUME (S.A.W)

imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w) kua alisema:

الكيس من دان نفسه وعمل لما بعد الموت والعاجز من اتبع نفسه هواها وتمنى على الله الأماني

Mwenye Akili za Busara ni yule atakayeidhibiti Nafsi yake na akafanya yaliyo kwa ajili ya Baada ya Kifo, na Mwenye kushindwa ni yule anayeifuata Nafsi yake katika Matamanio yake na akatarajia kwa Allah kua Ataokoka”

Basi ndugu chukua yale yatakayo kuhakikishia Kufaulu baada ya kuondoka kwako hapa Duniani, huko hueni na Urafiki, wala Ujamaa, wala Umadhehebu, huko ni Haki tu ndie rafiki wa aliyeikubali, kwa hivyo jifanyie Pupa kwa yatakayokufaa, wala usijitie Uvivu, wala usimpe Sheitani sehemu katika Maisha yako, kwa hakika yeye ni Adui, basi usihadaike na Wingi, wingi hauna Thamani ikiwa upo katika Batili, kwa hakika Haki ndio yenye hadhi kwa Muislamu wa kweli, na kila lenye kwenda kinyume na haki hilo ni lenye kudanganya na Mapato yake ni yenye kupita.

Tunamuomba Allah atuongoze katika yenye Manufaa (Amin)

KUTUBIA

Kutokana na yote tuliyoeleza, inaonekana Umuhimu wa Toba katika Maisha haya, na bila Shaka kila mmoja anataka kujua Uhakika wa Toba, na yuko katika hali ya kubabaika vipi ataweza kutekeleza Toba? Yote hayo ni kwa sababu ya kuyawahi Mema yake kabla ya Kuporomoka kutokana na Mabaya yake; Yote hayo; asije akaondoka katika Maisha haya na yeye Yumo katika wale Mafasiki asiowaridhia Allah Mtukufu, Yote hayo ni kwa sababu Mauti ni mlango, na kila Mmoja ataupita, na hajui wakati wa Kuupita, Yote hayo ni kwa Sababu Makosa makubwa yanahakikisha mtu kuingia katika Adhabu isiyomalizika, Na Allah amesema:

قوا أنفسكم وأهليكم نارا وقودها الناس والحجارة عليها ملائكة غلاظ شداد لا يعصون الله ما أمرهم ويفعلون ما يؤمرون

Okoeni Nafsu zenu na Watu wenu kutokana na Moto, kunizake ni Watu na Mawe, ulioekewa Malaika wasio na Huruma walio Wakali hawamuasi Allah kwa aliyowaamrisha na wanafanya yale waliyoarishwa”

Na Kila jambo lina Milango yake, basi na kuokoka na Adhabu pia kuna Sababu zake, nazo ni kukaa mbali na kila lenye kufikisha katika Moto, ni kazi kubwa sana Ndugu yangu kwa sababu Mtume (s.a.w) amesema:

حجبت النار بالشهوات وحجبت الجنة بالمكاره

Umewekewa Pazia Moto kwa yanayopendeza, na imewekewa Pazia Pepo kwa yanayochukiza”.

Basi tukaona ni lazima kuulezea Mlango huu Muhimu katika Maisha ya kila Mtu, na kua ni mlango wa Kurejea kila aliyemo katika Makasiriko ya Allah aliyeumba, na iwe ni kisaidizi cha kumrejesha katika kuridhiwa na Aliyeumba Allah mtukufu.

UHAKIKA WA TOBA.

Toba ni mlango wa kupita na kufika katika Rehma za Allah kwa kufanikiwa kupata Usamehevu wa Makosa ambayo Mja ametenda, na Kosa ni kila ambalo Mja amelifanya hali ya kua Allah amelikataza, na kila ambalo Mja hakulifanya baada ya kumlazimikia hali ya kua Allah ameliamrisha, ni sawa Katazo hilo au Amri hiyo imekuja kwa njia ya maneno ya Qur-ani tukufu, au kwa maneno ya Mjumbe wa Allah Muhammad (s.a.w).

Toba hii itamlazimikia kila mwenye kumuasi Allah, kwa Makosa makubwa, basi kutokana na sababu hiyo Allah ameamrisha kwa kusema:

وتوبوا إلى الله جميعا أيها المؤمنون لعلكم تفلحون

Na Mutubie kwa Allah nyote Enyi Mulioamini ili mupate kufanikiwa”

Na akesema vile vile:

وتوبوا إلى الله توبة نصوحا

Na mutubie kwa Allah Toba ya Kweli”

Na yamekuja mafundisho Mengi sana kutoka kwa Mtume (s.a.w) yanayohusu Toba, miongoni mwa Hayo:

لله أفرح بتوبة عبده من أحدكم سقط على بعيره وعليه زاده وشرابه وقد أضله في أرض فلاة

Naapa kua Allah anafurahi zaidi kwa toba ya Mja wake, kuliko mmoja wenu amekutana na Ngamia wake, juu yake kuna chakula chake na kinywaji chake, ikiwa amempotea katika Ardhi kame ya mbali”

Yote haya ni kuelezea Rehma za Allah mtukufu kwa Waja wake, basi tukimbilie katika Mlango huu wenye kuridhiwa na wenye matumaini yasiyokatika, kwa sababu Allah amesema:

وإني لغفار لمن تاب وآمن وعمل صالحا ثم اهتدى

Na hakika Mimi ni mwingi wa kusameha kwa atayetubia, na kuamini, na akafanya Mazuri kisha akaongoka”

Na amesema kwa Uwazi zaidi:

قل يا عبادي الذين أسرفوا على أنفسهم لا تقنطوا من رحمة الله إن الله يغفر الذنوب جميعا إنه هو الغفور الرحيم * وأنيبوا إلى ربكم وأسلموا له من قبل أن يأتيكم العذاب ثم لا تنصرون

Sema: Enyi waja wangu -amabo wamepindukia mipaka juu ya Nafsi zao- Musikate tamaa katika Rehma za Allah; Hakika Allah anasamehe Madhambi yote, Hakika yeye huyo ndie Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu * Na munyenyekee kwa Mola wenu na Mujisalimishe kwake, kabla haijakufikieni Adhabu kisha Hamutonusuriwa”

Basi Aya za Allah zinaeleza namna hivyo, kwa hivyo ndugu yangu hata kama umefanya kosa gani, unatakiwa ujue elimu isiyokua na Shaka kua ukirejea kwa Allah kwa kupitia Mlango huu wa Toba basi Allah atakukubali kama alivyoahidi, na yeye ndie mbora zaidi wa kutekeleza Ahadi, ومن أصدق من الله قيلا Na nani aliyemkweli wa Maneno kuliko Allah? Hakuna.. Hakuna.

MSINGI WA KUTUBIA

Msingi mkubwa wa kutubia ni Majuto, nao ndio msingi muhimu wa Toba, na Majuto ndio Roho wa Toba, na ndio ikasemwa التوبة الندم Toba ni Majuto” Na majito ni Hali ya Dhiki ya kinafsi inayompata Mtu na akatamani yale yaliyomfika kua hayakumfika” na Majuto kwa maana hiyo hayawezi kuja hivi hivi tu, lakini yana sababu zake, ikiwa mtu ataziweka katika Nafsi yake, na akaweza kuziacha zihukumu kikweli kweli basi inatarajiwa -kwa Uwezo wa Allah- kupatikana Majuto ya uhakika, na kila kitu kina sababu zake, basi sababu za Majuto ni hizi:

Kujijua Mtu kua yeye si chochote mbele ya Amri ya Allah, kwa hivyo hana uwezo wowote kiuhakika isipokua aupate kwa Idhini ya Allah, basi ni wajibu wake kujiwacha kwa kujilazimisha katika anayoyaridhia Muumba wa kila kitu ambae ni Allah, ili aweze kuridhiwa katika maisha yake.
Kujipa hisia za dhati ndani ya Nafsi, kua yeye yuko mbali na Maridhio ya mwenye Uwezo wote, na aliyekua ni mkali wa Kuadhibu, yote hayo kutokana na yale makosa ambayo ameyafanya katika kuvuuka mipaka ambayo Allah ameiweka, na kila mwenye kuivuuka ni dhalimu.
Kujipa hisia, kwa uhakika wa yale ambayo yamefuata juu yake katika Hukumu za Muumba wake Baada ya Kufanya Makosa, na kua Laana na Ghadhabu, na makasiriko ya Muumba yako juu yake ألا لعنة الله على الظالمين Ee!!mambo yalivyo Laana ya Allah iko juu ya Madhalimu”

Na kila kosa la kumuasi Muumba ni Udhalimu.

Kujijua kua kuendelea na Kosa bila Kutubia ni kuhatarisha Amani, na Usalama wa Kinafsi katika maisha haya na Kesho Akhera, kwa sababu ni njia ya Adhabu isiyomalizika, na kukasirikiwa.
Kujua kua Hakuna anayemiliki kusamehe isipokua Allah peke yake, na kua Toba ni Maombi na Mwenye kuombwa anayo khiyari ya Kuyakubali maombi hayo au Kuyakataa, basi kila majuto yanapokua mengi kwa kujidhalilisha inakua ni sababu zaidi ya kukubalika Maombi na kuvuta Huruma zake.
Kuleta mfzaiko katika Nafsi, kwa kuona na kuleta Hisia za kua kutokana na Maasi uliyofanya umo katika Khatari kubwa sana ya kukataliwa, kwa hivyo ili kujikurubisha Zaidi, na kujipendekeza zaidi ili ukubaliwe katika Maridhawa ya Allah, basi imelazimika kujuta kwa Yale uliyoyafanya kutokana na ukubwa wa khasara yake.
Kujua kwa Yakini kua Hoja ya Allah imeshasimama juu yako, kwa kupatikana sababu ya kukuadhibu, na kua Fursa ya kujiepusha kuingia katika Sababu hiyo imepita, kwa hivyo hakuna njia nyengine ya kusamehewa kwa Uliyofanya isipokua ni Kujuta na kurejea kwa Allah hali ya kukubali Makosa na kutaraji Usamehevu, na Rehma za Allah, hakika yeye ni mwingi wa kurehemu na kusamehe.
Kuingiza katika Nafsi makaripio Makali ya kuidhalilisha Nafsi, na kuilaumu, na kujipa Majuto makubwa, kwa kule kuyatii matamanio ambayo yaliyokuingiza katika khatari uliyonayo.
Kujijua na kutia Yakini isiyokua na chembe ya Shaka kua Ovu ulilolifanya tayari limehifadhiwa, na kudhibitiwa, na ushahidi wa kulithibitisha umetimia, na kua Fedheha yake tayari imeshaandaliwa, na kua yote yatawekwa Wazi mbele ya viumbe wote unaowajua na usio wajua, basi ni Fedheha ya namna gani hiyo itakayokupata, uhakika unadhihiri na uongo unajitenga, yote hayo yatakua katika Uwanja wa Hesabu, basi ni nani ya kuyasitiri, na kuyahifadhi isipokua Allah muweza wa Mambo yote, kwa hivyo ni kujuta kwa uliyofanya, na kuomba msamaha tu.

10.              Kuingiza yakini ndani ya Nafsi, kua uko mbali na Rehma na kua umo katika Sababu ya kuadhibiwa kwa Adhabu yoyote ile katika Maisha haya haya, hapa Duniani kabla ya kuondoka, kwa hivyo njia pekee ni Kujuta kwa uliyokosea kwa uliyemkosea -Allah mtukufu- mwenye Uwezo wa kila jambo, ili akusamehe na akurehemu.

Naona haya mambo kumi yanatosha na ikiwa Mtu atayaingiza katika Nafsi yake, na kuyafanyia kazi, kihakika yatakuja mengi mengine ya kumfanya yeye aingie katika Majuto kwa yale aliyomkosea Allah. Na yote haya hayatimii isipokua Mtu awe mbali na Watu, pahala pa peke yake, na ikiwa ni wakati wa Usiku mkubwa ni Bora zaidi, na haya anaweza kuyafanya yoyote yule, kwa sababu hakuna Mkamilifu katika Waja, kwani yamepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w):

كل ابن آدم خطاء وخير الخطائين التوابون

Kila Bin Aadam ni mwenye kukosea, na mbora wa wenye kukosema ni Wanaotubia”

Basi huo ndio Mzizi wa Toba ya Kweli.

TAHADHARI.

Wengi katika watu wanafanya kosa kubwa sana bila ya wao wenyewe kujua, na kosa hili sio jengine, lakini ni lile la kujifedhehesha mbele za Watu, kwa kujiweka wazi katika Makosa aliyoyafanya; Utamkuta Mtu anajisifu Eti amezini na wanawake Khamsini, na Mwengine ati Ameiba, na mwengine eti Ameua, na mwengine eti amemaliza wanaume wa Mtaa, na Mfano wa haya, hii ni khatari, tena ni Kosa mtu kueleza Kosa, amesema Allah mtukufu:

إن الله لا يحب الجهر بالسوء من القول إلا من ظلم

Hakika Allah hapendi kuweka wazi Kosa kwa Neno isipokua aliyedhulumiwa”

Basi jambo hili halifai, na limekatazwa na Sheria, jisitiri kwa sitara ya Allah, na ufanye haraka Utubie kwa Allah kabla kupitwa na wakati, wakati ukipita kuupata ni muhali.

Utamkuta mtu mwengine eti anajisifu kua yeye katubia kwa Allah; Toba ni siri baina yako na Allah, na hasa kwa Yale makosa ya Siri, Ama makosa ya Dhahiri pia haitakiwi Mtu kujisifu, kwa sababu ni kosa, na nani mwenye yakini ya kukubaliwa Toba yake? Hakuna kwa Sababu Wahyi haushuki tena, kwa hivyo sisi bado tunatakiwa tumuombe Allah azikubali Toba zetu, na Matendo yetu. Na khatari zaidi Jambo hili linaweza kupelekea kwa mwenye nalo kuingia katika Dhambi ya kujifedhehesha, na pengine ikapelekea kuingia katika kujionyesha, na kujiharibia mambo yote, kwa sababu kujionyesha kunaharibu Tendo kutokana na kubadilika Nia, kumbe umefanya ili uje upate la kusema na kujifakharisha, utakua huna lako, tujihadhari.

Utawaona wengine eti wanajipa moyo wa kuchelewesha Toba, hajui kama kufanya hivyo pia ni kosa, kwa sababu kuendelea na kosa ni kosa vile vile, itakua mizigo inajikusanya juu ya mengine, na mwisho jambo hili linaweza kupelekea kupigwa chapa katika moyo wa mja kutokana na Kosa hilo hata kama ni moja, na kushindwa tena kuliacha, na hata kama utatubia toba inakua ya Uongo kwa sababu inakadhibishwa na yaliyomo Moyoni. Allah atulinde na kuendelea na Makosa zamani Waarabu walisema:

لا تفتح بابا يعييك سده ولا ترسل سهما يعجزك رده

Usije ukafungua Mlango utakufanyia shida kuufunga kwake; wala usije ukarusha Mshale utakushinda kuurejesha kwake”

Basi kufanya Kosa ni kujifungulia mlango wa Kosa, vile vile ni kurusha Mshale wa Kosa; kwa sababu aliyelifanya hawezi kua hakulifanya, ni jambo lisilowezekana kukosekana katika sehemu kitu kilichokaa katika Sehemu hiyo.

NGUZO ZA TOBA

Toba ina nguzo zake muhimu kama hazikutimia nguzo hizo Toba hiyo haiwezi kutimia, na ili tuzijue nguzo hizo za Toba inatufaa tumuachie nafasi Sheikh Nuru Dini Saalimiy (r.a) basi yeye anasema:

أركانها ندم مع استغفار * والعزم والرجوع بانكسار

Nguzo zake ni Majuto na Kuomba Usamehevu * Na Kuazimia na Kurejea kwa kujidhalilisha.

Basi hizi ndio Nguzo za toba, nazo ni nne imepokewa kutoka kwa Ibn Abbaas (r.a) kua yeye ilisema:

التوبة النصوح الندم بالقلب والاستغفار باللسان والإقلاع بالبدن والإضمار على أن لا يعود

Toba ya kweli ni Majuto kwa Moyo, na Kuomba Msamaha kwa Ulimi, na Kujivua kwa mwili, na Kuazimia kua Hatorejea” Haya yote yana misingi muhimu ya kutegemea katika Kitabu cha Allah, kwa hivyo tuanze kuzifafanua Nguzo hizi Moja baada ya nyengine ili tupate mwangaza ulio safi wa kutuongoza katika Njia ya Toba, ili Toba zetu ziwe ni za kweli kama alivyoamrisha Allah mtukufu.

Nguzo ya kwanza:

MAJUTO

Majuto ndio nguzo ya kwanza ya Toba, na ndio msingi muhimu wa kutubia na ndio Roho ya Toba ya kweli, na Njia za kuihakikisha tumezieleza na Maana yake tumeielewa, kwa hivyo Majuto yanatakiwa kupatikana kila mja anapokumbuka kosa lake alilolifanya na yeye atamani lau kama hakulifanya, na ahisi dhiki katika Nafsi yake, na kama tulivyoeleza kua Majuto njia zake zote zinapatikana katika Kumkumbuka Allah mtukufu, na Uwezo wake, na Adhabu yake, na mengineyo ambayo Mja hawezi kuokoka nayo isipokua kwa kuokolewa na Allah peke yake, basi kutokana na jambo hili ndio Allah mtukufu akasema kwenye Kitabu chake:

والذين إذا فعلوا فاحشة أو ظلموا أنفسهم ذكروا الله فاستغفروا لذنوبهم….

Na wale ambao wanapofanya ovu au wakadhulumu Nafsi zao wanamkumbuka Allah na waomba Msamaha kwa Madhambi yao..”

Basi hiyo ndio Nguzo ya mwanzo ya Toba, kwa hivyo tunatakiwa Tumkumbuke Allah, na hakika Aya imekuja katika mfumo huo, kwa sababu Usamehevu ni wake Alla peke yake, wala hakuna mwengine wa kumiliki, na mwenye kuhitaji analazimika kutaka mahitaji yake kwa njia anayoiridhia mwenye kumiliki ya kuondosha Mahitaji ya mwenye kuhitaji, basi Allah amesema:

ربكم أعلم بما في نفوسكم إن تكونوا صالحين فإنه كان للأوابين غفورا

Mola wenu anayajua zaidi yaliyomo katika Nafsi zenu; ikiwa mutakua Wema; hakika yeye kwa mwenye kunyenyekea ni mwingi wa kusamehe”

Basi ukihakikisha unyenyekevu katika hali ya Majuto, na kurejea kwa Muumba, na ndio maana yakaja mafundisho haya, katika zile Aya za Suratu Zumar, baada ya kufungua Mlango wa Matarajio kua Mja yoyote yule hata kama amepindukia mipaka ya Allah namna gani, basi anaporejea kwa Mwingi wa kusamehe atakubaliwa, na atasamehewa, basi baada ya kuja Matarajio hayo imekuja Aya hii:

وأنيبوا إلى ربكم وأسلموا له من قبل أن يأتيكم العذاب ثم لا تنصرون

Na munyenyekee kwa Mola wenu na Mujisalimishe kwake, kabla haijakufikieni Adhabu kisha Hamutonusuriwa”

Yote haya yanaleta Maana hii ya Majuto ambayo yatahakikisha Unyenyekevu katika Nafsi ya mwenye nayo, na kuleta Athari zake katika Maungo yake yote.

Nguzo ya pili:

IS-TIGH-FARI (KUOMBA KUSAMEHEWA)

Bila shaka Majuto yanapohukumu, katika Nafsi ya mwenye kumuasi Mola wake, atataka huyo Mja kusamehewa Makosa yake, ambayo ameteleza kuyafanya, basi hapo atakua hana budi isipokua kuomba Msamaha wa kusamehewa Makosa hayo, kwa mwenye uwezo kwa Kusamehe, naye ni Allah aliyeumba kila kitu, aliyeleta Amri na Katazo ambalo Mja wake huyo, ameingia katika Maasi kwa kulifanya lililokatazwa au kutolifanya lililoamrishwa, Basi nguzo hii inapatikana katika Aya tulioitaja hapo juu lakini hapa ni bora tuiendeleze kidogo ili kuyatimiza Mafundisho yaliyomo ndani yake katika Nguzo hii:

والذين إذا فعلوا فاحشة أو ظلموا أنفسهم ذكروا الله فاستغفروا لذنوبهم ومن يغفر الذنوب إلا الله

Na wale ambao wanapofanya ovu au wakadhulumu Nafsi zao wanamkumbuka Allah na Waomba Msamaha kwa Madhambi yao –na nani wa kusamehe Madhambi isipokua Allah?-”

Hakuna isipokua wewe Allah uliyeumba mwenye Ufalme wa kila kitu, unaehukumu kwa Unavyotaka, usieulizwa katika unachotaka, na kwa Rehma zako umeufungua Mlango wa Toba umsamehe kwa anayetaka na unayemtaka, basi tumeujia tukubalie, na uturehemu, na utusamehe, na utuweke katika Waja wako wema, ewe mwingi wa Kusamehe, ewe Mwingi wa kurehemu.

Tuombe msamaha kwa kumtakasa Allah na kila Upungufu, kwa kujisalimisha upande wake, na kuukubali Utukufu wake, na kutaraji Rehma zake, na Usamehevu wake, ni bahari kila Mmoja anaweza anaogelea kwa mujibu wa uwezo wake, tahadhari usije ukaingia katika maji yaliyoko nje ya Uwezo wako utakuja zama bila ya kujijua, wala usije ukafuata usilokua na Elimu nalo, ukaja Ukamsifu Muumba kwa sifa zisizokua Zake, na Allah atuhifadhi na kila Alilolikasirikia  na atuongoze katika njia anayoiridhia (Amin).

Amesema Mtume (s.a.w):

توبوا إلى الله واستغفروه فإني أستغفر كل يوم سبعين مرة

Tubieni kwa Allah na Mumuombe Msamaha Hakika mimi Ninaomba Msamaha kila Siku Mara Sabiini”

Basi ikiwa hivi ndivyo alivyokua Mtume wetu (s.a.w), na yeye amesamehewa makosa yake yote,  yaliyopita na yalikuja, yuko safi ametakaswa na kila kosa Kubwa, vipi iwe mimi na wewe, kwa hakika tujiingize katika Ibada hii inayozidisha Imani, inayoleta Barka, inayohakikisha Utulivu, na Kuridhika, yenye kila Bishara njema, na Allah atatusaidia.

Nguzo ya tatu:

KUAZIMIA

Kuazimia au Kujivua kwa mwili, ni kuleta Nia thabiti katika Nafsi, bila kupatikana chembe ya khiyana ndani yake, kua Mwili wako wote unauvua na Kosa lile, kwa Maana hutorejea tena katika Maisha yako katika Kosa lile, kama yalivyokua Maziwa hayarejei katika chuchu zake. Basi kujivua huku ndiko kunakoambiwa “kutoendelea na Kosa”, na ikiwa haikupatikana maana hii basi Bado kosa hilo unalo, na Hapa inatakiwa ipatikane Yakini ya kweli kweli, kwa Sababu Allah mtukufu hakifichiki kitu upande wake, na ikiwa wewe unaleta Toba, na huku Nafsi yako inakukadhibisha basi jua bado hujafika katika sehemu unayotakiwa uwe, hapo unatakiwa urejee katika Misingi ya Majuto, na uilee Nafsi yako kwa Mujibu Allah atakavyokujaalia, na Allah hailazimishi Nafsi nje ya uwezo wake, basi muombe Allah akuondoshee hali hiyo ya kukadhibishwa na Nafsi, na weka Azma yako wala usirudi Nyuma, na Allah atakusaidia tu, na msingi huu unapatikana Katika Aya ya Qur-ani takatifu:

ولم يصروا على ما فعلوا وهم يعلمون

Na wala wakuendelea na waliyoyafanya na wao Wanajua”

Wanajua kua kuendelea na Makosa ni Sababu ya kuangamia, na kukasirikiwa, na wanajua kua wanapofanya Toba hatika misingi hiyo iliyowekwa na Allah, basi Allah yuko tayari kuwapokea, basi tujitahidi na Allah atatusaidia, kwani huko ndio kuchukua Sababu za kufanikiwa, na Allah yuko pamoja na wale wanaomuogopa na wanaofanya vizuri, basi tujitahidi tuwe wazuri kwa kufanya Mazuri.

Nguzo ya nne:

KUREJEA KWA KUNYENYEKEA.

Hii ndio nguzo wa mwisho ya Kutubia, nayo ni kurejea kwa Allah mtukufu katika Hali ya kunyenyekea kukubwa kabisa, ukijiona kua wewe uko katika hali ya Udhalilifu mkubwa, huna Matarajio isipokua kwa Allah aliyekuumba, unailea Nafsi katika udhalilifu, kwa kujisalimisha katika Utukufu na Uwezo wa Allah, ukitaraji kupokelewa, huku unajiona  kua njia –kwako- zimekatika, ujanja umemaliza, mwangaza umeondoka, unataraji kwa kwenye kumiliki kila kitu, akusamehe na kukurehemu katika kila kosa ambalo wewe umetenda, unairejesha tena Nafsi yako ukiilea katika malezi na dawa ya Nafsi, unamomba Allah akuwezeshe katika kuhakikisha Toba yako. Basi hii ndio hali anayotakiwa kuwa nayo kila mwenye kutubia, na hii inahakikisha maana ya Ikhlaas katika Ibada hii muhimu, inayopelekea kusamehewa makosa ambayo Mja ameyafanya, Basi Allah anasema:

قل إني أخاف إن عصيت ربي عذاب يوم عظيم * قل الله أعبد مخلصا له ديني

Sema: Hakika mimi ninakhofia nikimuasi Mola wangu Adhabu ya Siku kubwa * Sema: Allah ndie ninaemuabudu katika hali ya Kusafisha kwake Dini yangu”

SHAR-TI ZA KUTUBIA

Tumeziona nguzo za Toba, kwa hivyo hapana budi kuzijua vile vile Shar-ti za Toba, kwa sababu kila litu kina Majengo yake, na hizi ni katika Majengo Muhimu ya Jengo la Toba, nayo ni kuzitimiza Sharti za Toba ili uweze kutekeleza Ibada hii muhimu, kama ilivyokua huwezi Kusali mpaka uwe na Udhu kwa sababu udhu ni katika Shar-ti za Sala, basi vile vile kuna Mambo ambayo ni lazima yapatikane ndio Mja aweze kutekeleza Ibada hii, kama Shar-ti hizo hazikutimia basi pana hatari na Tiba pia kutotimia kama Inavyotakiwa, na hilo linaweza kuathiri na kua Toba haikutimiza Masharti yake, na hapa tutaweza kuzieleza Sharti hizi za Toba kwa mujibu wa Mafundisho yanayopatikana katika Aya za Qur-ani na Hadithi za Mtume (s.a.w), kwa hivyo kila Mtu anatakiwa azijue moja baada ya nyengine ili aifanye Ibada hii kwa uoni wa Uwazi, na Allah hailazimishi Nafsi isipokua katika Uwezo wake tu, kama alivyosema, basi sharti za kutubia ni kama zifuatanyo:-

Sharti ya kwanza (Uislamu):

Uislamu ni Sharti muhimu katika Toba, na asiyekua Muislamu Toba yake ni kuingia katika Uislamu, akifanya hivyo basi tayari yeye ameshatubia, kwa sababu yalikua makosa aliyoyafanya kwake yeye ni makosa yaliyozidiwa na kosa kubwa lao, kutokana na itikadi yake Potofu ya ushirikina, alikua hakubali kitu katika maamrisho ya Allah wala Mtume (s.a.w), wala haamini, kwa hivyo hili ndio kosa kubwa  kuliko yote, na hii ndio Dhulma kubwa kabisa ya kuidhulumu nafsi, kwa hivyo Mshirikina anapoingia katika Uislamu, tayari ametubia na amesamehewa makosa yake yote kutokana na Rehma za Allah, basi katika uhakika huu Allah anasema:

إن الله لا يغفر أن يشرك به ويغفر ما دون ذلك لمن يشاء ومن يشرك بالله فقد ضل ضلالا بعيدا

Hakika Allah hasamehe kushirikishwa yeye, na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa anayemtaka na mwenye kumshirikisha Allah kwa hakika amepotea Upotevu wa mbali”

Kwa hivyo Allah hasamehe kosa la Ushirikina, na anasamehe yote yasiyokua Ushirikina kwa anayemtaka Allah, yaani anayemtaka Allah kumuongoza kwa kuacha kosa lake hilo la ushirikina, kwa maana akiacha kosa lake hilo la ushirikina makosa yote yasiyokua Ushirikina kama vile Kulewa, Kuzini, kuwatusi Wazazi na mengineyo, makosa hayo yatakua yamesamehewa, kwa kuingia kwake katika Uislamu, na mwenye Kumshirikisha Allah amepotea Upotevu ilio wazi na wa Mbali kabisa, Na ndio Ikaja Hadithi kutoka Mtume (s.a.w):

الإسلام يجب ما قبله

Uislamu Unafuta yaliyopita kabla yake”

Sasa hapo yatabakia makosa yale ambayo wanayafanya Waislamu, makosa haya ni lazima aliyeyafanya Atubie kwa Mola wake kabla ya Kuondoka Duniani, na ndio makosa yaliyokusudiwa hasa katika mlango huu, na haya ndiyo yaliyokuja ndani ya Kitabu cha Allah:

وتوبوا إلى الله جميعا أيها المؤمنون لعلكم تفلحون

Na tubieni kwa Allah nyote enyi mulioamini ili mufanikiwe”

Sharti ya pili: (Akili)

Hii ni Sharti muhimu, kuemo mtu katika Akili timamu, na awe anajua ni kitu gani yeye anakifanya, na sio awe mbali katika uhakika wa hayo, kwa hivyo hawezi Mtu kutubia na yeye yuko katika hali ambayo hana Akili, au inayochukua hukumu yake, na Maana hii ndio Anayoieleza Mtume (s.a.w):

رفع القلم عن ثلاث عن النائم حتى يستيقظ وعن المجنون حتى يفيق وعن الطفل حتى يحتلم

Imenyanyuliwa kalamu (ya kuandikiwa) kwa watatu: Kwa aliyelala Mpaka Aamke, na kwa Mwenda wazimu Mapka Azinduke, na Kwa Mtoto mpaka Abaleghe”

Basi katika hali mbili za Mwanzo ndio zilizokusudiwa katika Kuelezea Sharti hii, nazo ni hali ya kua katika usingizi, na hali ya Kukosekana Akili, na hali zote hizi zimepewa Hukumu hii, kwa sababu inakosekana fikra ya kupambanua mambo, na kupelekea hilo kukosekana hukumu ya kuhukumiwa, kwa sababu ikipatikana hukumu hiyo itakua ni Ulazimisho usiowezekana, na hilo halina Hekima Ndani yake, na Allah ametakasika na jambo hilo la kulazimisha kisichowezekana.

Haya tunayoyasema hapa ifahamike wazi kua sisi viumbe hatumiliki kitu, basi hata hiyo akili sio milki yako, aliyekupa anaweza kuihukumia kuondoka wakati wowote ule, na kuwepo kwake katika Fikra zako, ni hoja tosha na Sababu ya kuhesabiwa na kuulizwa mbele ya Allah, na kuhukumiwa, basi jitahidi kuitumia katika Anayoyaridhia Allah mtukufu, kabla ya kumaliza hukumu ya kufanya kazi yake upande wako, na hujui wakati gani inaweza kumalizika hukumu hiyo, yote hayo azinduke mwenye kuzinduka, na azingatie mwenye kuzingatia, ili amshukuru Allah mwenye kuneemesha.

Sharti ya tatu (Kubaleghe):-

Na hii ni Sharti nyengine muhimu, nayo inapatikana katika Hadithi iliyopita: Na Mtoto mpaka Abaleghe” kua na yeye pia Kalamu imenyanyuliwa haandikiwi kitu kisheria, lakini juu ya yote haya ifahamike kua Mtoto sio aachiliwe tu afanye anavyotaka, bali yeye anatakiwa awe chini ya Malezi mazuri ya Walezi wake, na wao wataulizwa na Allah jinsi gani walivyolea watoto wao, na ndio yakaja mafundisho kwa Walezi kua wawafundishe Sala wanapofikia miaka saba, na wawapige wanapotimia miaka Kumi, na wawatenganishe katika malazi, kwa hivyo Mtoto anatiwa Adabu na Mlezi wake anapofanya kosa, na hiyo ndio adabu yake kwa mujibu wa sheria, na Mlezi ndie atakayeulizwa kuhusu malezi yake, na akifikia Baleghe tu, na huku anazo akili, basi mambo yake ni yake mwenyewe na kalamu yake ya kuja kuhukumiwa Mbele ya Allah inaanza kufanya kazi, kwa hivyo Makosa yanayofuata baada ya Kubaleghe anatakiwa aliyeyafanya ajivue nayo kwa kurejea kwa Mola wake kwa kupitia Mlango huu wa Toba.

Sharti ya nne (Kurejesha ya kudhulumu):

Hili ni sharti Muhimu sana, na Shatri hii inaingia katika Makosa yote ya Kudhulumiana waja, kwani makosa hayo yamekua ni makosa kwa Hukumu ya Allah, na yamekua ni Dhulma kwa Hukumu yake Allah, kwa hivyo aliyedhulumiwa italazimika arejeshewe Haki yake, na Sharti hii inapatikana katika Kitabu cha Allah mtukufu pale aliposema:

فإن تبتم فلكم رؤوس أموالكم لا تظلمون ولا تظلمون

Na mukitubia basi mutapata nyinyi Mali yenu ya Asili tu, musije mukadhulumu wala musije mukadhulumiwa”

Na aya hii inazungumzia Toba ya Kosa la Riba; Kosa la kula Mali ya Watu kwa njia ya Battil, kwa kutumia Fursa ya mwenye kuhitaji, na Riba ni lile ongezeko la Pato linalochukuliwa kwa mujibu wa Wakati, kwa hivyo Ongezeko hilo ni Dhulma kwa Hukumu ya Allah, ni lazima atakayetubia na kosa Hilo arejeshe Dhulma hiyo kwa aliyedhulumiwa kwa hukumu ya Allah, ili itimie Toba yake, na kutokana na jambo hilo imekuja hadithi kutoka Kwa Mtume (s.a.w) kua amesema:

الظلم ظلمات يوم القيامة

Dhulma ni Kiza kingi siku ya Kiama”

Na akasema vile vile:

القليل من أموال الناس يورث النار

Kidogo katika Mali za Watu kinarithisha Moto”.

Na sharti hii inawekwa wazi zaidi na hadithi ya Mtume (s.a.w) pale aliposema:

الذنوب على وجهين ذنب بين العبد وربه ذنب بين العبد وصاحبه فالذنب الذي بين العبد وربه إذا تاب منه كان كمن لا ذنب له وأما ذنب بينه وبين صاحبه فلا توبة له حتى يرد المظالم إلى أهلها”

Madhambi ni Aina mbili: Dhambi baina ya Mja na Mola wake, na Dhambi baina ya Mja na Mwenzake; Basi Dhambi ambayo ni baina ya Mja na Mola wake akitubia na dhambi hiyo amekua kama yeye asiyekua na Dhambi,, Ama Dhambi iliyo baina yake na Mwenzake hapana Toba mpaka arejeshe aliyodhulumu kwa wenyewe”

Basi tujitahidi katika toba, na ikiwa Mtu alidhulumu, na uwezo wa kurejesha aliyodhulumu hanao, basi na aandike wasia kwa warithi wake, kwa sababu hilo litakua ni Deni, na litaingia katika hukumu ya madeni baada ya Kufa na halitakua katika Kuhumu ya Wasia.

Sharti ya tano (Kulipa yanayolazimika)

Hapa tunakusudia katika masuala ya Ibada, kwa sababu Makosa pia yamegawika sehemu mbili, makosa ambayo Mja aliyafanya kwa kuacha Amri ya Kutenda katika Ibada kama vile Kusali na kufunga, na makosa yaliyofanywa kwa kuingia katika Katazo, kama vile Kuzini na Kulewa.

Basi yale makosa yaliyomo katika sehemu ya mwanzo, anatakiwa yule aliyeyafanya alipe alichoacha katika Amri zile, na haya yanaingia katika Makosa haya yafuatayo: Kuacha Kusali[14], kuacha Kufunga[15], Kuacha kutoa Zaka, kuacha kutekeleza Ahadi iliyokulazimu katika wakati wake kama kuacha kutekeleza Nadhiri, kuacha Kutoa Dia, kuwatupa Wazazi wawili, kuukata Udugu.

Sharti ya sita (Kubainisha Upotevu)

Sharti hii inawakamata wale waliofanya Kosa kisha kosa hilo halikumaliza upande wao tu, bali walifanya kazi ya kuita katika Kosa hilo, kwa kujipatia wafuasi, katika hali hii italazimika kuwabainishia wale waliofuata kosa lile ubaya wake, na uharamu wake, na Kua yeye ametubia na kosa hilo, ni sawa ikiwa alifanya kwa njia ya Maandishi itambidi abainishe upotevu wake alioufanya vile vile kwa njia ya maandishi, na kuujibu upotevu wake, na ikiwa kwa njia ya maneno pia abainishe kwa njia ya maneno; Na sharti hii inapatikana katika neno lake Allah mtukufu:

إن الذين يكتمون ما أنزلنا من البينات والهدى من بعد ما بيناه للناس في الكتاب أولئك يلعنهم الله ويلعنهم اللاعنون

Hakika wale walioficha yale tuliyoyateremsha katika ubainifu na uongofu, Baada ya kuyabainisha kwa Watu katika Kitabu, Hao anawalaani Allah na wanalaaniwa na Wenye kulaani”

Huo ulikua ni Ubainisho wa Kosa ambalo wako watakaolifanya, sasa baada ya Aya hiyo, inakuja Aya inayobainisha kukubaliwa Toba yao kwa watakaotubia:

إلا الذين تابوا وأصلحوا وبينوا فأولئك أتوب عليهم وأنا التواب الرحيم

Isipokua wale watakaotubu, na wakafanya Mazuri na Wakabainisha Hao nitasamehe juu yao na mimi ni Mwingi wa Kusamehe na Mwingi wa Kurehemu” Kwa hivyo hii ndio Sharti yake ili ikubaliwe Toba ya mwenye kosa hilo.

Sharti ya Saba (Kabla ya Kufa)

Nayo ndio Sharti yenye kila Mawaidha ndani yake, na yenye kila sababu ya kukimbilia katika Toba; yote hayo ni kwa sababu hakuna anayejua wakati wake wa kufa, na kua jambo hilo halina shaka kwa mwenye Uhai katika viumbe, na hapo kila mmoja anajijua kua yumo katika Safari lakini wakati wa kuondoka haujui, kwa hivyo atajitahidi kukusanya ya kumsaidia na kumfaa katika Safari yake hiyo kabla ya wakati kufika, kwa sababu ikiwadia hakuna kusubiri, ukitaka utakwenda hutaki utakwenda, basi Allah amesema kwa uwazi kabisa usioingiwa na chembe ya Doa:

وليست التوبة للذين يعملون السيئات حتى إذا حضر أحدهم الموت قال إني تبت الآن ولا الذين يموتون وهم كفار أؤلئك أعتدنا لهم عذابا أليما

Wala hakuna Usamehevu kwa wale wanaofanya Mabaya mpaka yanapomfika mmoja wao Mauti akasema: Hakika mimi ninatubia hivi sasa” wala wale wanaokufa nao ni Makafiri, hao tumeandaa kwa ajili yao Adhabu nyenye kuumiza”

Naona Aya hii haitaki maelezo, kwa hakika Allah amekataa kata kata kua wanaofikiwa na mauti na wao wamebeba Mabaya bila ya kutubia kabla ya hapo, kua hawana toba kabisa, na kua wao na Makafiri waliokufa nao ni Makafiri ni sawa wote Adhabu yao mzito inawasubiri, basi tujihadhari, Tujihadhari na mafundisho ya Mapendwa moyo yanayosema, mtu ikiwa neno lake la mwisho ni لا إله إلا الله ataingia peponi tu, nao wanaichukua hadithi hiyo kwa ufafanuzi wa imani ya Fir-auni (l.a) basi wanafundisha Imani hiyo ya Kifirauni, ole wao shauri yao, sisemi hili kwa Nafsi yangu lakini kwa Ubainisho wa Kitabu cha Allah, kwa sababu Allah ameibainisha Imani hii ya Kifir-auni katika Kitabu chake, ili iwe fundisho kwetu sisi, tusije tukachukuliwa na Imani hiyo, lakini la Ajabu utawakuta waliovaa nguo za Uislamu, na kujiita kwa kila jina zinalopendeza, wanaita katika Imani hii, basi tumsikilize Allah nini anatuambia kuhusu Imani hii:

حتى إذا أدركه الغرق قال آمنت أنه لا إله إلا الذي آمنت به بنو إسرائيل وأنا من المسلمين

Mpka ilipomdiriki Kuzama (Gharak) alisema: Nimeamini hakika mambo yalivyo hakuna Mungu isipokua ambaye wamemuamini huyo Bani israili na mimi ni katika Waislamu”

Basi hii ndio khabari ya Fir-auni (l.a), yeye alilisema neno hilo, kwa uwazi usioingiwa na shaka, na tazama Allah alivyomjibu:

آلآن وقد عصيت قبل وكنت من المفسدين

Hivi sasa na uliasi hapo Kabla na ulikua katika Waharibifu”

huo sio wakati tena wa kufaliwa na neno la Tauhidi, malango wa Mauti ukifunguka mlango wa toba unafunga, na ndio maana yakapokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w) kua alisema:

إن الله يقبل توبة عبده ما لم يغرغر

Hakika Allah anaikubali Toba ya mja wake ikiwa hajafikia wakati wa Kufa”, tujihadhari ndugu zangu, na penye Usalama zaidi tuwepo na sio tujidanganye au kudanganywa na kudanganyika.

Sharti ya nane (Kabla Dalili kubwa za Kiama)

Hapa yapo mambo kadhaa yakitokezea, au likitokezea Moja wapo itakua hakuna tena kukubaliwa Toba, mambo hayo ni Ishara tosha kua Mlango wa Toba umefungwa, na Allah ametuhadharisha na mambo hayo ambayo yatakua ni Dalili kubwa ya Kiama kwa neno lake pale aliposema:

هل ينظرون إلا أن تأتيهم الملائكة أو يأتي ربك أو يأتي بعض آيات ربك يوم يأتي بعض آيات ربك لا ينفع نفسا إيمانها لم تكن آمنت من قبل أو كسبت في إيمانها خيرا قل انتظروا إنا منتظرون

Jee!! wanasubiri isipokua wawafikie Malaika, au iwafikie (Amri ya) Mola wako, au Iwafikie baadhi ya Dalili za Mola wako, Siku zitakapofika Baadhi ya Dalili za Mola wako haitoifaa Nafsi Imani yake iliyokua Haikuamini toka Kabla, au ikachuma katika Imani yake Kheri; sema subirini sisi ni wenye kusubiri”

Amesema Allah kuhusu Dalili hizo:

وإذا وقع القول عليهم أخرجنا لهم دابة من الأرض تكلمهم أن الناس كانوا بآياتنا لا يوقنون

Na itakapo kaa hukumu juu yao, tutawatolea wao Mnyama katika Ardhi atawasemesha: Hakika watu walikua kwa Aya zetu hawana yakini nazo”

Na katika Dalili hizo ni zile zilizokuja katika Hadithi za Mtume (s.a.w) nazo ni Kuchomoza Jua upande wa Magharibi, na Kuja wa Masihi Issa mwana wa Mar-yam (s.a.w)[16].

YALIYOSEMWA KUHUSU IBADHI

Haya ni Baadhi ya yalisemwa na Wanavyuoni wasiokua Maibadhi, kuhusu Madhehebu hii, na yote tumayatoa katika kitabu الحق الدامغ, na نبذ التعصب المذهبي vya Sheikh Ahmed L-haliliy (h.a)

1.      Mwanachuoni Abdulmuiz Abdulsataar:

Lau Umma ungelichukua Itikadi yenu Maibadhi katika kukaa milele mwenye kosa kubwa katika Adhabu, ingalikua kwa Umma huu ni jambo kubwa katika kutengenea na kunyooka na kujitakasa na kujitosheleza kinyume na hivi tunavyoona”

2.      Mwanachuoni Izu Dini Tanukhi:

Kila mwenye kutuhumu Ibadhi kwa kupotea na upotevu huyo ni katika waliofarikisha Dini yao na wakawa Makundi, na yeye ni katika mwenye kudhulumu walio wajinga”

3.      Mwanachuoni Abdu L-hafidh Abdu Rabih:

Kwa hakika wamechukua Madhehebu yao katika Qur-ani Tukufu, na wameyafuata yaliyomo katika Sunna iliyotoharika, na wamefuata katika mwendo wao wa kumuabudu Allah njia ile ile waliyoifuata Maswahaba, na ikaridhiwa na Makubaliano, na wakafanya kila Pupa ziwe hatua zao juu ya uhakika, na njia ile ile, na katika misingi ya sheria ambayo aliipita Mtume (s.a.w) katika Mashauri yake marefu ndani ya miaka Ishirini na Tatu, na wao wanachunga Ukweli, na kuhakikisha Haki, na kushindana na Nafsi, na kusubiria Matatizo, na mazoezi na kujizoesha katika Mashaka na yenye kuumiza mpaka ikabaina kwao Haki, na ikawa wazi mbele yao Njia, na ikabainika kwa Ulimwengu wote, au wenye kutaka kujua Haki, kua hawa ndio Watu wa Istiqamah, au wao katika muweko na uhakika ndio KUNDI LILILOOKOKA, ambalo alilizungumzia Mkweli Aliyehifadhiwa, na ambalo amemuamrisha Allah Mtume wake kulichagua na kulifuata kua ndio njia  ya kumfikisha katika Kumuabudu yake, na Maridhawa yake katika neno lake aliyetukuka: Sema hii ndio njia yangu, ninaita kwa Allah juu ya Uoni, mimi na anayenifuata, na ametakasika Allah, na sikua mimi katika Washirikina}”

4.      Ustadh Muhammed Shahaatah:

Mimi simuonei haya yoyote katika msimamo wangu huu, basi mimi nasema: Hakika Watu wa Madhehebu hii ambayo wamejichukulia mizigo juu yake wengine, hakika wao ni zaidi kuliko sisi kusameheana na kuitikia Amri ya Allah aliyetukuka katika  kupendana, kwa hakika nimeishi baina ya Migongo yao, nikisomesha Mada ya Tafsiri katika Chuo ya Kadhaa Shar-ii kipindi kilichozidi miaka kumi na mbili sijaonapo linaloharibu uzuri, wala yaliyonichukua kusema Neno bila ya Dalili, juu ya Khilafu katika baadhi ya Masaili, na tulikua mimi na Wanafunzi wangu na Wanavyuoni Wakuu katika Madhehebu tunafuata Dalili yenye Nguvu”

5.      Dr. Abdul Aziz L-madhuub:

Na hayo kwa sababu Wafuasi wake walihifadhi usafi wa Mafundisho wa Muhammad katika Misingi ya madhehebu yao, wala hawakutoka katika mwendo bora ambao alikua nao Mjumbe wa Alla (s.a,w), na Maswahaba wake walio Wema katika Mienendo yao na Mambo yao ya Maisha, wala hawakufanya Viongozi wao Dhambi, wala hawakua wakijifanyia katika uongozi wao Dhulama, wala hawakufanya lolote katika mambo yasiyofaa ambayo hakuweza kujiepusha mwengine katika Viongozi sisipokua wachache”

6.      Ustadh Ahmed Amin:

Na wao hata kama wakiangalia Watu ni kwa Mwangaza kwa Itikadi, sioa kama wanavyofanya wasiokua wao kuangalia Itikadi katika Mwangaza wa Watu”

7.      Ustadh Mahdiy Twalib Hashim:

Ilikua siasa ya Abdullahi bin Yahya ni usadikisho wa kulazimika na Sheria ya Kiislamu, katika kua kwake na waliokhitalifiana nay eye kimadhehebu katika Waislamu, aliweza kuambatanisha baina ya Fikra na Kufanya kazi, bila ya kusamehe hukumu ya Hamasa katika Wakati mzito, kama wakati wa Vita ambao zinakuja juu hamasa ndani yake, na kulipiza kisasi…..kwa sababu Maibadhi hawakubali kujitayarisha na kumfuata aliyekimbia katika vita, na haya yanaonyesha tabia ya uadilifu katika mwendo wa kundi hili hata katika wakati wa vita, na lau tutalinganisha baina yao na Umawiyiina tutakua tofauti kubwa sana katika uwanja huu, kwa hakika vimedhihiri vita vya Umawiyiina kiunyama, na tabia ya Kibedui, na kutoka katika mazuri ya Kiislamu katika vita vyao dhidi ya Maibadhi”

SHAIRI LA KUNASIHI

NDUGU NINAKUNASIHI

Bismillahi naanza,   kumshukuru Muweza.

Salamu naelekeza,   kwa Mtume mueneza,

kwa Masahaba ruwaza, hadi kwetu nafikiza,

Ndugu yangu nakusihi, kutoacha Madhehebu.

Umeacha Madhehebu, bila kuacha sababu,

za kukuona kusibu,  hapo ulipo ratibu,

wala hutaki jaribu, ukweli kuunasibu,

Ndugu yangu nakusihi, kutoacha Madhehebu

Kwa Tarekhe nabaini, Dhehebu Haki indani,

Masahaba kwa yakini, ndipo walipobaini,

ukweli kuuthamini,  haki kutoweka chini,

Ndugu yangu nakusihi, kutoacha Madhehebu.

Imam wake wa Mwanzo,  Rasibiyu chambalizo

si Sahaba wa mchezo,  kura zote hizo hizo,

baada ya kuja nazo,  Harurai mafikizo,

Ndugu yangu nakusihi, kutoacha Madhehebu.

Yote baada kutweka, Imam Ali kaweka,

kofia kaibanduka,  kwa Adui kuiweka,

Amru akazinduka, Muawiya kaibaka.

Ndugu ukweli sikiza, kutoacha Madhehebu.

Muawiya akatwaa,  kitini akapakaa,

kisha akawakataa,  wote walomkataa,

Na njama akazivaa,  hadi Ali kuuwawa,

Ndugu ukweli sikiza, kutoacha Madhehebu.

Zikaenea fitina, Basira hadi Madina,

Misiri hadi Omana, Makka pia zikanana,

Na Sunna kutoibana, kwa Aliyu Mulaana,

Ndugu ukweli sikiza, kutoacha Madhehebu.

Na wale wa Rasibiyu, Khawariji huyu huyu,

Lakini Haki ya huyu, itabakia Hisiyu,

Amari kwa Muawiyu,  kauwawa mbiyo mbiyu,

Ndugu Haki ikubali, kutoacha Madhehebu.

Itikadi nakhitimu,  ndio kwanza la muhimu,

katika Dini salimu, tusije tukalaumu,

Allah katupa Elimu, hoja yake imedumu,

Ndugu Haki ikubali, kutoacha Madhehebu.

Sifa za wetu Muumba, ni za Tangu taziamba,

hazina mwanzo kuumbwa, ni za Dhati ya Muumba,

hana Umbile Muumba, Ndugu Aya zinaamba

Ndugu Haki ndio hii, usiache Madhehebu.

Uoni haumfiki, wa Mja wake hakiki,

atakalo hashindiki, yeye atalihakiki,

Adhabu yake kwa Haki, Makafiri hawatoki,

Ndugu Haki ndio hii, usiache Madhehebu.

Na Kafiri umjue,  ni kila amuasiye

vigao uvitambue, viwili nakupashaye,

kudharau Neemaye, au kumsawi yeye,

Ndugu Haki ndio hii, usiache Madhehebu.

Wa mwanzo wala wa pili, Shafaa haihasili,

wamchao lao hili,  si Fajiri asosali,

alewaye asojali,  kutubia kwa Jalali,

Ndugu Haki ndio hii, usiache Madhehebu.

Kuumbwa kwa Kuruani, hili nalo libaini,

kwani lililo yakini, kiumbe au Manani,

Maneno yake Manani,  kwani vyengine vya nani?

Ndugu Haki ndio hii, kutoacha Madhehebu.

Tutubieni jamani,  isififie mizani,

kwani Allah kabaini,  akubali Muumini

na Fasiki yuko chini,  mizaniye adhabuni

Ndugu Haki ndio hii, kutoacha Madhehebu.

kwa heri ya kuonana,  kupeana ya maana,

namuomba Subuhana,  atupe ya kufaana,

tusamehe Maulana,  utufanye Ikh-wana

Ndugu Haki ndio hii, kutoacha Madhehebu.

BAADHI YA MASAILI YA KIFIQHI.

Kwa hakika wengi katika waislamu wanaona kua Maibadhi hawafanyi Baadhi ya matendo ambayo yamekua ni Maarufu kwa waislamu wengine, na pengine wao wanataka Dalili katika hayo, na matendo hayo ni haya kunyanyua na kufunga mikono katika sala, na kunyoosha au kutikisa kidole katika Sala, na kua wao hawakubali Qunuti katika Sala, basi nimeona upo umuhimu mkubwa wa kuyaweka yele wanayoyategemea Maibadhi katika mambo yao hayo.

KUNYANYUA NA KUFUNGA MIKONO KATIKA SALA

Kunyanyua na kufunga Mikono katika Sala, ni matendo ambayo Waislamu wametofautiana ndani yake, lakini juu ya kutofautiana kwao huko wamekubaliana kua hayo sio mambo ya Lazima kuyafanya katika Sala, kwa hivyo tofauti hiyo ipo katika kuyatenda na siyo kuyaacha matendo hayo, na hapa utaona ndugu yangu Muislamu kua wale wanaitwa Maibadhi wameacha vitendo ambavyo vina khilafu ndani yake na hakuna tatizo kuviacha, kwa hivyo wao wamekaa mbali na mambo hayo yenye Shubuhati, na kuleta tofauti na mizozano ndani yake katika Safu za Waislamu na mwenye kujiweka mbali na hayo kwa hakika ameitakasa Dini yake kama yalivyothibiti kutoka kwa Mtume (s.a.w). Lakini Jee!! Maislamu hawa wanazo Dalili na Hoja katika Kuacha kwao Matendo hayo? Ndio wanazo; basi tuangalie mtazamo wao katika suala hili, baada ya kuona kusalimika kwao katika msimamo wao huu.

Amepokea Imam Rabii (r.a) kutoka kwa Abu Ubaidah Muslim bin Abi Kariimah kutoka kwa Imam Jabir Bin Zaid kutoka kwa Ibn Abbaas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) kua alisema:

كأني بقوم يأتون من بعدي يرفعون أيديهم في الصلاة كأنها أذناب خيل شمس

Kama kwamba mimi ninaona watu watakuja baada yangu watanyanyua Mikono yao katika Sala kama mikia ya Farasi washupavu.”

Na hapa tunaona kua tendo hilo lilikua halipo wakati alipolisema Mtume (s.a.w) na kua litatokezea baada ya kuondoka kwake, kwa hivyo kunyanyua Mikono katika Sala ni bidaa kwa mujibu wa hadithi hii nayo ni Hadithi Sahihi kabisa kwa sababu imekuja kwa mapokezi hayo yenye nguvu wala hawajapokea mengine katika haya, na linalotilia nguvu zaidi kua ni Bidaa ni yale mapokezi aliyoyapokea Imam Mus-lim, Abu Daud na wengineo kua Mtume (s.a.w) mara moja alitoka akaenda Msikitini akawakuta watu wamo katika Sala nao wananyanyua mikono akasema hivi:

ما بال قوم يرفعون أيديهم في الصلاة كأنها أذناب خيل شمس أسكنوا في صلاتكم

Bado watu wanaendelea kunyanyua mikono yao katika Sala kama ni mikia ya Farasi washupavu, tulizaneni katika Sala zenu”

Basi hadithi hii inaonyesha kua watu walikua akinyanyua mikono katika Sala zao kabla ya hapo kisha Mtume (s.a.w) alikataza tendo hilo, kwa hivyo likawa hukumu yake ni yenye kufutwa, kwa hivyo sio ajabu kupatikana mapokezi kua Mtume (s.a.w) alikua akinyanyua mikono katika sala kwa sababu hayo yalitokezea kisha Mtume (s.a.w) aliyaacha na kuyakataza.Na inawezekana Kua Mtume (s.a.w) alinyanyua kwa Dharura mara Moja kama ilivyoelezwa kua alitaka kuwafedhehesha Wanafiki ambao walificha Visanamu vyao chini ya Makwapa yao, ikiwa watanyanyua mikono yao vitaanguka visanamu na vitaonekana na kufedheheka, na ikiwa hawakufanya watafedheheka vile vile kwa kwenda kinyume na matendo ya Mtume (s.a.w),  na hapa utaona jinsi gani Mtume (s.a.w) alivyosema yale maneno ya ile hadithi ya mwanzo, kwa sababu waliothibitisha kitendo hicho walitegemea mapokezi tu peke yake na ikafichika upande wao hukumu ya kufutwa kwake, lakini Maibadhi kwa sababu ndio walioshikilia uadilifu tokea mwanzo kwao halikufichika jambo hilo, kwa hivyo hayo ndio mafundisho sahihi aliyoyawacha Mtume (s.a.w).

Na huenda mtu akasema: Hayo muliyoeleza ni katika Kunyanyua mikono tu lakini Kufunga mikono jee? Na Hadithi zimepokewa tena mingoni mwa Hizo ni zile alizopokea Bukhari na Mus-lim, kama Ile Hadithi aliyoieleza Wail bin Hajar (r.a) na Hadithi ya Sahal bin Saad (r.a).

Tunasema kua Hadithi zote zilizopokewa katika Kufunga Mikono zimetiwa Udhaifu ndani yake, na haya hayakuonyeshwa na Wanavyuoni wa Kiibadhi tu bali hata wa Kisunni, na mimi hapa nitachukua maneno ya Sheikh wa Kisunni Muhammed khadhari Shankiity katika kitabu chake: إبرام النقض لما قيل من أرجحية القبض amesema Sheikh huyo katika kitabu chake hicho baada ya kuizungumzia Hadithi hiyo ya Bukhari:

وحيث إنه لم يرو غير حديث مالك مع تبحره وشدة اطلاعه على الحديث علم أنه لم يجد حديثا أقوى عنده منه. وهذا أدل دليل على ما قدمناه من أن القبض لم يوجد فيه حديث صحيح سالم من الطعن والله الموفق للصواب اهـ

Na kwa kua yeye (yaani Imam Bukhariy) hakupokea isipokua Hadithi ya Malik, pamoja na kuzamia kwake na wingi wa kujua kwake juu ya Hadithi; ikajulikana kua hakupata Hadithi yenye nguvu zaidi kwake kuliko hiyo. Na hii ya kuonyesha zaidi kidalili juu ya tuliyoyatanguliza kua hakika Kufunga Mikono haijapatikana ndani yake Hadithi Sahihi iliyosalimika na kutiwa Doa, na Alla ndio Mwenye kuwezesha katika Usahihi”

Hayo yalikua ni Maneno aliyoyasema Mmoja katika Wanavyuoni wa Kisunni, katika Suala hili, basi ikiwa mambo ni hivyo mimi ninaona nitoshelezeke na hoja zao ambazo wamezitegemea katika kuthibitisha maneno yao hayo ya kuonyesha Udhaifu wa hizo Hadithi za kufunga mikono pale walipozifika Hadithi hizo Ambazo ndio tegemeo kubwa la wanaofunga Mikono.

Hadithi ya kwanza:

Hadithi ya Wail bin Hajar kua yeye alimuona Mtume (s.a.w) amenyanyua mikono miwili wakati alipoingia katika Sala na akapiga Tak-bira “Alisifu Hamaam kua ni karibu na Masikio yake mawili” kisha akajifunga kwa nguo yake, kisha akaweka mkono wake wa Kulia juu ya mkono wa Kushoto, alipotaka kurukuu alitoa Mikono yake katika Nguo kisha akainyanyua kisha Akatoa takbira na Akarukuu, na aliposema Samia Llahu liman Hamidah alinyanyua Mikono yake, na aliposujudu alisujudu Baina ya Viganja vyake viwili” 54 (401) Mus-lim.

Hiyo ndio hadithi inayotegemewa katika kufunga Mikono, amesema Sheikh Shankiity:

Na Hadithi hii imetiwa magojwa matatu: Mawili katika Upokezi wake, na Moja katika Maelezo yake na unaofuata ni ubainisho wake:

1.      Upokezi wake umekatika, na ubainisho wa hayo; ni kua Hadithi hii ameipokea Abdul Jabbar mtoto wa Wail kutoka kwa Ndugu yake Alqamah na Muachwa Huru wao, na Mazingatio ni mapokezi na Alqamah, ama Muachwa Huru  yeye hajulikani basi hazingatiwi, na Alqamah bin Wail na Ndugu yake Abdul Jabbar kutoka kwa Baba yao ni Mursalah kwa sababu hawakumuwahi, na hivi ndivyo alivyosema katika “تهذيب التهذيب’ na ameweka wazi Abu Daud katika Sunna yake kua hakika Abdul Jabbar hakumdiriki Baba yake, na maelezo yake katika Mlango wa kunyanyua Mikono: Amenihadithia Muhammad bin Jahaadah amenihadithia Abdul Jabbar bin Wail bin Hajr akisema: Nilikua Kijana siifahamu Sala ya Baba yangu..” Kisha alihadithia kutoka kwake Abu Daud baada ya hapo kutoka kwa Baba yake, kama itakavyokuja baadae kidogo. Alisema Shankiity: Hakika alisema Almaariziy katika “شرح مسلم” Hakika Muslim amepokea katika “صحيح” Hadithi kumi na nne zilizokatika upokezi wake, kuenda hadithi hii ni miongoni mwa hizo, kwani yaliyosemwa ndani yake katika Ukatiko uchache wa Hadhi zake ni kuondosha Usahihi wake”

2.      Mgongano uliyokaa katika Upokezi wake: Na hayo ni kua Hadithi katika Muslim ameipokea Abdul Jabbar kutoka kwa Ndugu yake Alqamah na Muachwa Huru wao, kutoka kwa Baba yake kama ulivyoona, na Ameipokea Abu Daud katika Mlango wa Kunyanyua Mikono kutoka kwa Abdul Jabbar bin Wail akisema: Nilikua Mtoto siifahamu Sala ya Baba yangu akanihadithia mimi Wail bin Alqamah kutoka kwa Baba yake Wail bin Hajar akisema: Nilisali pamoja na Mjumbe wa Alla (s.a,w) …” na haya yanakwenda kinyume na yaliyopita kutoka kwa Muslim. Na Wail bin Alqamah amesema Dhahabiy katika “الميزان” Hajulikani”. Kisha akaipokea baada ya hayo kutoka kwa Abdul Jabbar kutoka kwa Baba yake: Hakika yeye alimuona Mtume (s.a.w) ananyanyua mikono yake pamoja na Tak-bira”. Basi angalia haya pamoja na yaliyopita karibu katika neno lake Abdul Jabbar: Nilikua kijana siijui sala ya Baba yangu” na hapa anahadithia kutoka kwa Baba yake bila ya kuwepo wa kuunganisha, kisha akaipokea baada ya hayo kutoka kwa Abdul Jabbar akisema: Wamenihadithia mimi watu wa nyumbani kwangu kutoka kwa Baba yangu kua yeye aliwahadithia…” kisha akaipokea baada ya hapo kutoka kwa Asim bin Kulaib kutoka kwa Baba yake kutoka kwa Wail bin Hajar alisema: Nilisema: Kwa hakika nitatizama Sala ya Mjumbe wa Alla (s.a,w)  vipi anasali…..” na Asim bin Kulaib huyu ni Mur-jia alimuaminisha Ibn Maiin, na alisema Ibn Lmadainiy: Hayatolewi Hoja kwa aliyokua nayo peke yake” Basi haya ndio yaliyokua na Mgongano ndani yake, nao ni mgongano mzito unaolazimisha Udhaifu mzito kama yalivyoandikwa katika vitabu vya Usuli L-hadith.

3.      Ama yaliyomo katika Maelezo yake: Ni kua Hakika Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Wail bin Hajar kwa Mapokezi yaliyopita bila ya kuwemo ongezeko linakalokuja, na ameipokea Abu Daud kutoka kwa Asim bin Kulaib ambaye yamepita Mapokezi kutoka kwake, na ndani yake: Kisha akachukua Kushoto wake kwa Wakulia wake”, na alisema katika mapokezi haya ya Mwisho: Kisha aliweka mkono wake wa kulia juu ya kiganja cha Kushoto na Kifundo na Mkono” na akasema ndani yake: Kisha nilikuja baada ya Hapo katika Wakati ndani yake kuna Baridi mzito nikaona Watu juu yao kuna Nguo zao inatikisika mikono yao chini ya Nguo”. Na katika Mapokezi ya Asim ya Mwanzo hakutaja: Kisha nikaja katika wakati ndani yake kuna Baridi mzito….” na wala hakuyataja mwengine katika waliopokea Hadithi hii kutoka kwa Wail bin Hajar, na akayataja Asim bin Kulaib katika Mapokezi haya, na ongezeko hili ima liwe lenye kukubalika au sio lenye kukubalika, ikiwa ni lenye kukubalika litakua ni lenye dalili ya uwazi juu ya Kufutwa yale aliyoyapokea katika Mara ya mwanzo katika Kufunga, kwa sababu neno lake: Inatikisika mikono yao chini ya nguo” liko wazi katika kuachilia Mikono, kwa sababu kutikisika mikono katika hali ya kuifunga haiwezekani bila ya kutikisika na Mwili pamoja, kama ilivyo dhahiri kwa kuonekana na majaribio kwa anaetia shaka katika hilo, na haya yanayojulisha kufutwa kwa kufunga Mikoni ndio hayo tunayosema sisi Makundi ya Maalikiyah, isipokua asiyehisabika katika sisi na akasema kufunga kama utakavyokuja Ubainisho wake Alla akitaka. Na neno lake “Kisha nikaja Baada ya Hapo” linaungana na neno lake: Kisha akaweka mkono wake wa Kulia juu ya ya mgongo wa mkono wake wa Kushoto” liko wazi kua yale aliyoyaona Mara ya Pili ni kinyume na yale aliyoyaona katika Mara ya kwanza, na kama sio hivyo asingalihitaji kuyataja hayo. Na ikiwa ongezeko hilo halikubaliki kwa sababu ya waliopokea wengi kutoka kwa Wail bin Hajar itakua ni ulazimisho wa kugongana kwa hadithi ya Asim bin Kulaib kutoka kwake. Na Alla ndie muwezeshaji wa uhakika.

Basi haya ndio Maradhi Matatu yanayopatikana katika Hadithi ya Mus-lim.” Amemaliza Shankiity. Na haya hakuyasema Sheikh Shankiity peke yake bali wako wengine mfano wake kwa mfano Sheikh Muhammad Aabid ambaye alikua ni Mufti wa Maalikiyah kule Makka, Sheikh huyu anayo maneno mazito aliyoyasema katika kitabu chake alichokiita “القول الفصل في تأييد سنة السدل” na maana ya maneno hayo “Neno la Uwazi katika kushikamana na Sunna ya Muacha Mikono”

Ama Hadithi ya aliyopokea Imam Bikhariy no: (740) nayo ni Hadithi ya Malik kutoka kwa Abiy Hazim kutoka kwa Sahl bin Saad alisema: Walikua watu wanaamrishwa aweke mtu Mono wa Kulia juu ya Dhiraa yake ya Mkono wa Kushoto katika Sala” alisema Abu Hazim: Sijui jengine isipokua anaegemeza hilo kwa Nabii (s.a.w)” alisema Ismail: Linaegemezwa hilo wala hakusema: Anaegemeza”

Amesema Sheikh Muhammed Shankiity kuhusu Hadithi hii katika kitabu chake “إبرام النقض لما قيل من أرجحيةالقبض”: Na hadithi ya Bukhariy hii ina magonjwa kwa njia mbili: La kwanza imejibiwa kwa jawabu zenye kutiwa madowa, na La pili halijajibiwa kabisa.

1.      Alisema Daaniy katika At-raaf l-muwataa: Hadithi hii imetiwa magonjwa, kwa sababu ni Dhana kutoka kwa Abiy Hazim….

2.      Na ile ambayo bado haijajibiwa katika zile njia mbili za Magonjwa ni kua lile neno la Bukhariy ililopita: Na alisema Is-mail: Linaegemezwa hilo, wala hakusema anaegemeza hilo” alikusudia kwa neno hilo, kubainisha kua Mapokezi ya Is-mail Ibn Abi Uwais[17] ya Hadithi hii kutoka kwa Shekhe wake na Mjomba wake na Mtoto wa Ami yake ambaye ni Imam Malik -Alla amrehemu- yanatupa faida kua Hadithi ni Mur-sali na sio Mutasil. Amemaliza Sheikh Shankiity.

Haya tuliyoyaweka Hapa ni ya kutegemea Masheikh wa Kisunni ambao ni Maimam wa Madhehebu ya Imam Malik bin Anas Ambaye katika Madhehebu yake Hakuna kufunga mikono.

Sasa pia kuana dalili nyengine ambayo inakusanya yote ya kunyanyua mikono na kuifunga na kunyoosha kidole hasa hasa kwa wale wanaokitikisa, na dalili yenyewe ni hii:

Amesema Alla mtukufu: والذين هم في صلاتهم خاشعون Na wale ambao katika Sala zao ni wanyenye kevu”

Dalili hapa ni kua Unyenyekevu unapatikana katika kutulizana ndani ya Sala na kuiweka Fikra yote katika Sala tu, kama ilivyokuja katika Hadithi kua Ihasani ni kumuabudu Alla kama wewe Unamuona na ikiwa haiwezekani kumuona basi yeye anakuona” sasa jambo hili haliwezi kupatikana katika ukamilifu wake ikiwa  Akili zetu tunazipa kazi zaidi ya moja, kwa sababu kunyanyua mikono na kuizuia katika kuifunga isije ikajiachia na kuanguka, ni jambo la kulidhibiti katika Akili na hili wanalihisi zaidi wale wanaosimama kisimamo kirefu sana cha sala, kwani sisi tumewaona wengine wakishindwa wenyewe na kuiacha mikono yao na kua kama wanavyosali Maibadhi, na kuishughulisha Akili na jambo hili kunakosekana katika sala kama wanavyoisali Maibadhi, na vile vile jambo hili linapatikana katika kunyoosha kidole, kwa hivyo kuyafanya matendo hayo kunapunguza Khushui ambayo Alla alewasifu waja wake Waumin kwa sifa ya Khushui ndani ya Sala kama alivyosema; basi ijuilikane kua Sala kama wanavyoisali Maibadhi inahakikisha Zaidi Khushui katika Moyo wa anayesali.

KUITIKIA  AAMIN  KATIKA SALA.

Shukurani zote ni kwa Alla anayemuongoza anayemtaka katika njia iliyonyooka, na Rehma na Amani ziwe kwa Mtume (s.a.w) pamoja na Aali zake na Sahaba wake na kila mfuataji wa Njia yake mpaka siku ya Malipo (Amin).

Kwa hakika kuitikia Aamin ni jambo lisilotakiwa kufanywa ndani ya Sala kwa mujibu wa mafundisho ya Kiibadhi, na mimi ninaona ni jambo zuri kumuachia Sheikh Ahmed L-khaliliy (h.a) katika kulielezea jambo hili, kwa sababu nimeona maandiko yake katika ufafanuzi wa suala hili ni yenye kuleta faida kubwa sana, tena kwa ubainisho usiochokesha, basi Sheikh Ahmed L-haliliy (h.a) anasema hivi:

Tambua kua Aamin haimo katika Qur-ani kwa makubaliano ya wote, kwa kukosekana kwake katika Msahafu wa Imam ambao wamekubaliana Maswahaba (r.a) kukusanya yaliyo baina ya Kava zake mbili yaliyokua ni Qur-ani, na kuwekwa mbali humo isiyokua Qur-ani, na zikaenezwa nuskha zake katika miji, na kuenea katika Umma, wala hakutokezea aliyepinga kitu ndani yake, na Huskha hiyo ndio iliyotegemewa katika kufikisha Qur-ani kizazi kwa kizazi mpaka hivi leo, na Wanavyuoni wa Fiqhi na Tafsiri wameweka wazi kua Aamin haimo katika matamshi ya Qur-ani, amesema Mfasiri Mashuhuri Abu Hayyaan katika Tafsiri yake Kubwa (البحر المحيط ): Na vile vile wamezungumzia kuhusu –yaani Wafasiri- yanayohusu Aamin na lugha zake, na Tofauti katika maana zake, na hukumu yake katika Sala, nayo sio katika Qur-ani, kutokana na hilo tukaacha maneno yaliyomengi juu yake” na amesema Aloosiy katika Tafsiri yake (روح المعاني)  : Na si katika Qur-ani kwa makubaliano –mpaka akasema-: mpaka amesema zaidi ya mmoja kua atakayesema kua Aamin ni katika Qur-ani atakua amekufuru”.

Na ikiwa Tamshi la Aamin sio Qur-ani, basi litakua ni katika maneno ya watu, na maneno ya watu imethibi ukatazo wake ndani ya Sala baada ya kua ni ruhsa kabla ya katazo hilo; kwani ameelezea Imam Bukhari na Muslim na Nasaaiy kutoka kwa Zaid bin Arqam (r.a) kua alisema: Tulikua tukizungumza katika Sala, anamzungumzisha Mtu mwenzake na yeye yupo ubavuni pake, mpaka ilipoteremshwa (وقوموا لله قانتين) Na simameni kwa Ajili ya Alla kwa Unyenyekevu” Tukaamrishwa kunyamaza na tukakatazwa kuzungumza” na haya yamekuja kwa matamko mengine karibu na haya kwa Abu Daud na mengine kwa Tir-midhiy.

Na amepokea Bukhari na Muslim na Abu Daud kutoka kwa Ibn Masoud (r.a) kua alisema: Na tulikua tunamsalimia Mtume (s.a.w) na yeye yumo katika Sala na akiturejeshea Salamu juu yetu, basi tuliporudi kutoka kwa Najashi tulimsalimia Mtume (s.a.w) na yeye yumo katika Sala na hakuirudisha Salamu juu yetu, tukasema: Ewe Mjumbe wa Alla tulikua tunatoa Salamu juu yako ndani ya sala na ukiturejeshea juu yetu? Akasema: Hakika katika Sala kuna Shughuli” na mfano wa haya kwa Nassaiy; Na katika Hadithi yake kua Mtume (s.a.w) alisema: Hakika Alla aliyetakasika na kutukuka ameleta jipya katika sala, kua musizungumze isipokua kwa utajo wa Alla na yale yanayotakiwa kwenu na musimame kwa ajili ya Alla hali ya kunyenyekea” na katika Hadithi ya Muawiya bin L-hakam Salmiy katika Muslim na Abi Daudi: Hakika Mtume (s.a.w) alisema kumwambia yeye: Hakika hii Sala haitakiwi ndani yake chochote katika maneno ya watu; hakika mambo yalivyo hiyo ni Tas-bihi na Tak-biri na kusoma Qur-ani” Na katika jambo lenye kujulikana kua Aamin haimo katika hayo aliyoyataja katika lolote lile, kutokana na hayo wamesema As-habu wetu (Maibadhi) na Zaidiyya: kua Aamin imeingia katika yale yaliyokatazwa katika maneno ya watu ndani ya Sala, na yaliyopokewa kuhusu Aamin  katika Hadithi hayo yanachukuliwa kua yalikua kabla ya Kufutwa, lakini haya yamefichika juu ya wanaoona kubakia hukumu yake, kama ilivyofichika juu ya kundi la watu kufutwa hukumu ya Qunuti katika Sala pamoja na kuweka wazi zaidi ya mmoja miongoni mwa  Maswahaba (r.a) kua Qunuti imefutwa.

Wala isipingwe juu yetu kubakia Tah-midi na Tashahudi (tahiyyaatu)  katika Sala, kwa sababu Tah-midi ni jinsi ya Tas-bihi, na Tashahudi –hata kama sio Qur-ani- hakika yote ni Tam-jidi kwa ajili ya Alla mtukufu, nayo ina muweko wake maalumu, kwa hakika Mtume (s.a.w) alikua akiifanyia juhudi yake maalumu, kama yalivyoekwa wazi na Neno la Ibn Masoud (r.a): Alikua Mjumbe wa Alla (s.a,w) anatufundisha Tashahudi kama anavyo tufundisha Sura katika Qur-ani” nayo yako wazi kua hukumu yake ni ya Qur-ani ndani ya Sala, na yakutosheleze Makubaliano ya Umma juu ya kutofutwa Tah-midi na Tashahudi katika Sala kua ni Hoja na Dalili ya kutoingia hayo mawili katika yaliyofutwa miongoni mwa Maneno, na haiwi yaliyokubalika na wote kua ni sawa na yaliyokua na khilafu ndani yake.

Haya na ujue kua Njia ya As-habu wetu (Maibadhi) katika sala ni kuchukua Hadhari kwa kutochukua isipokua yale mapokezi yasiyofikiwa na shaka yoyote katika mambo yaliyo na khilafu ndani yake, kwa sababu sala ni Nguzo ya pili mingoni mwa nguzo za Uislamu ambayo inakuja baada ya Itikadi moja kwa moja, na Wenye Kuhakikisha katika Wanavyuoni juu ya kutofautiana Madhebu zao hawaikubali Hadithi Ahadiy kama ni hoja katika mambo ya kiitikadi, kutokana na kukosekana Yakini ndani yake, basi ikawa hii sala ni Jirani wa Itikadi katika utaratibu ina haki zaidi kuichukua kwa hadhari; Juu ya kua miongoni mwa Wanavyuoni wamesema kua Sala ya As-hab wetu (Maibadhi) kwa hakika inathibiti kwa Makubaliano ya wote, kwa sababu yale waliyoyaacha katika Matendo ndani yake kuna khilafu kwa wasio kua wao, na aliyeyasema kufanyiwa kazi haoni kua kuachwa kwake kutapelekea kuharibika Sala, basi inatosha hii kua ni Dalili ya Usahihi wa Sala ya asiyeitikia Aamin.

Na ikiwa kuna anayetia Doa juu yetu kwa kuacha Aamin  basi jawabu yake kua: Ni bora zaidi kutia Doa juu ya wanaoacha Bisimillahi nayo ni Aya katika Kitabu cha Alla imethibitishwa katika Misahafu yote kwa Makubaliano, kuliko kutia Doa juu ya anayeacha Aamin  nayo siyo katika Qur-ani kwa Makubaliano.

Allah ndie anayejua Zaidi

QUNUTI KATIKA SALA

Naona pia uwanja huu tuuwache kwa Sheikh Ahmed L-haliliy (h.a), basi yeye aliulizwa hivi:

Nimeona jawabu yenu kwa mtu wa Hanafii anayesali nyuma ya Imam wa Kishafii, na mukamuamrisha arudie sala yake kwa sababu ya Qunuti ya Imam wa Kishafii. Jee!! maana yake Sala ya Imam wa Kishafii sio sahihi kwa sababu ya Qunuti?

Tunataraji kutoka kwenu Ukarimu kwa kufaidika.”

Na hapo Sheikh Ahmed L-haliliy (h.a) alimjibu hivi:

Sikugusia katika jawabu yangu Sala ya Mshafii wala asiyekua Mshafii kukubalika au kubatilika kwake, wala haiwi kwangu nihukumu kubatilika Sala ya yeyote anayeshikilia Madhebu ikiwa ataitekeleza Sala yake kwa mujibu wa mafundisho ya madhehebu hayo, kwa hakika Wanavyuoni wa Kiislamu wanazo jitihada na Rai katika Sala na mengineyo miongoni mwa Ibada, wala hazihesabiwi khilafu zao hizo kua ni mambo yanayopelekea katika Matatizo, kwa sababu ni khilafu ya matawi, inakua hata katika Dhehebu moja; lakini mimi nilibainisha Jawabu kwa mujibu yanavyopelea Madhehbu ya Muulizaji, kua kisimamo kirefu katika sala bila kazi kinapelekea kubatilika Sala, na yaliyoshikiliwa na Rai katika Madhehebu hayo kwa makubaliano kua hakika kuwepo kwa Qunuti  kumefutwa kwa Hadithi zinazo onyesha kufutwa huko, wala hakuna khilafu katika kukubalika kwake, hata kama kuna Khilafu katika kufutwa Qunuti  kutokana na Hadithi hizo, na kwa ufupi Dalili za kufutwa Qunuti  katika sala zimo katika mambo matatu.

La kwanza:

Kuharamishwa Maneno katika Sala kwa yasiyokua Qur-ani wala Tas-bihi wala Tak-biri, baada ya kua hakuna matatizo katika maneno hayo hapo mwanzo, nao ndio ule wakati ilipokua Qunuti inafanyiwa kazi, na hizi hapa Hadithi zinazofuta:

1)   Ameelezea Imam Bukhari na Muslim na Nasaaiy kutoka kwa Zaid bin Arqam (r.a) kua alisema: Tulikua tukizungumza katika Sala, anamzungumzisha Mtu mwenzake na yeye yupo ubavuni pake, mpaka ilipoteremshwa (وقوموا لله قانتين) Na simameni kwa Ajili ya Alla kwa Unyenyekevu” Tukaamrishwa kunyamaza na tukakatazwa kuzungumza” na haya yamekuja kwa matamko mengine karibu na haya kwa Abu Daud na mengine kwa Tir-midhiy.

2)   Na amepokea Bukhari na Muslim na Abu Daud kutoka kwa Ibn Masoud (r.a) kua alisema: Na tulikua tunamsalimia Mtume (s.a.w) nay eye yumo katika Sala na akiturejeshea Salamu juu yetu, basi tuliporudi kutoka kwa Najashi tulimsalimia Mtume (s.a.w) nay eye yumo katika Sala na hakuirudisha Salamu juu yetu, tukasema: Ewe Mjumbe wa Alla tulikua tunatoa Salamu juu yako ndani ya sala na ukiturejeshea juu yetu? Akasema: Hakika katika Sala kuna Shughuli” na mfano wa haya kwa Nassaiy; Na katika Hadithi yake kua Mtume (s.a.w) alisema: Hakika Alla aliyetakasika na kutukuka ameleta jipya katika sala kua musizungumze isipokua kwa utajo wa Alla na yale yanayotakiwa kwenu na musimame kwa ajili ya Alla hali ya kunynyekea”

3)   Na amepokea Muslim na Abi Daudi Hadithi ya Muawiya bin L-hakam Salmiy katika: Hakika Mtume (s.a.w) alisema kumwambia yeye: Hakika hii Sala haitakiwi ndani yake chochote katika maneno ya watu; hakika mambo yalivyo ni Tas-bihi na Tak-biri na kusoma Qur-ani”.

Na katika yaliyoko wazi kua Qunuti  iko nje ya aliyoyataja kama ilivyo kua inahesabiwa kua ni maneno ya Watu ambayo hadithi inaonyesha kukatazwa, wala hairejeshwi ketu kuhusu Tashahudi katika Sala, kwani hakika ya Tashahudi ina hukumu nyengine, kwa sababu hayo ni maneno ya kupokewa maalumu, na alikua Mtume (s.a.w) anayawekea mahimizo maalumu, mpaka alikua akiwafundisha Maswahaba (r.a) wake kama anavyowafundisha sura katika Qur-ani, kama yalivyokuja kutoka kwa Ibn Masoud (r.a) na Qunuti sio namana hii.

La pili:

Mapokezi yanayoonyesha kutobakia Qunuti, kama Hadithi ya Anas aliyoisimulia Ahmed: Hakika Mtume (s.a.w) alikunuti mwezi mmoja kisha akaacha” na katika mataamshi aliyoyapokea Ahmed na Muslim na Nasaaiy na Ibn Maajah: Alikunuti mwezi mmoja akiomba juu ya Miji katika Miji ya Waarabu” na Hadithi ya Abi Maalik L-ashjaii amesema: Nilimuambia Baba yangu: Ewe Baba yangu hakika ulisali nyuma ya Mjumbe wa Alla (s.a,w)  na Abi Bakar na Oth-man na Aliy hapa Quufah sio inakaribia Miaka mitano, Jee!! walikua wakiqunuti? Naye alisema: Ee!! motto wangu ni jambo jipya, kwa maana walikua hawafanyi”. Na amepokea Ahmed na Tirmidhiy na Ibn Maajah na akaisahihisha Tirmidhiy na pia kaipokea Nassaaiy kwa tamshi: Nimesali nyuma ya Mjumbe wa Alla (s.a,w)  hakuqunuti, na nimesali nyuma ya Abi Bakar hakuqunuti, na nimesali nyuma ya Omar hakuqunuti, na nimesali nyuma ya Oth-man hakuqunuti, na nimesali nyuma ya Aliy hakuqunuti, kisha akasema: Ee!! motto wangu ni Bidaa”.

Na yamepokewa mfano wa haya kutoka kwa Ibn Abbaas katika mapokezi ya Daar-qutniy na Bayhaqiy, na kutoka kwa Ibn Masoud (r.a) katika mapokezi ya Tabaraniy katika kitabu chake (الأوسط) na Bayhaqiy na Haakim, na yamepokewa kutoka kwa Umi Salamah katika mapokezi ya Ibn Maajah, na ameelezea Tirmidhiy kua kutokuwepo Qunuti  ndio Neno la wengi wa wanavyuoni.

La tatu:

Hakika mapokezi ya Qunuti  hayakuja kua ni katika Sala ya Al-fajiri peke yake, kwani imepokewa na Bukhari kutoka kwa Anas (r.a) kua amesema: Ilikua Qunuti  katika Magharibi na Al-fajiri” Na mfano wa haya kutokwa kwa Baraai bin Aazib katika mapokezi ya Muslim na Tirmidhiy, basi vipi ihusishwe Qunuti  kwa Al-fajiri peke yake lau kwamba haikufutwa, pamoja na kua mapokezi yamekuja kua ni katika Al-fajiri na Magharibi? Imma iwe imebakia hukumu yake katika Zote mbili au iwe imefutwa katika zote mbili, na Neno la kua imebakia katika Moja wapo na imefitwa katika nyengine ni kujihukumia tu.

Juu ya yote haya hakika mimi simkatazi kuqunuti yule anayejishikilia na Dalili katika Ibada zake kwa mujibu wa Madhehebu yanayoona kubakia Qunuti, lakini haitakiwi kushangaa  yeyote ikiwa nitamjibu mwenye kua Madhehebu yake ambayo anaabudu kwa mujibu wa mafundisho yake, yanaonyesha kutobakia Qunuti baada ya kufutwa kwake, kua arejee Sala yake ambayo ameisali nyuma ya aliyequnuti na yeye anayajua hayo kwa Imam huyo, hakika hayo ni katika njia ya kuchukua Hadhari na sio vyengine, hakika Hadhari katika mambo ya Ibada ni njia wameifuata wengi watika Wanavyuoni” Na Alla anajua Zaidi.

KUDIRIKI SALA

Na vile vile inafaa zaidi kuzindua juu ya kuduriki sala, kwa hakika katika namana ya kudiriki kusali ipo khilafu baina yetu sisi Maibadhi na wengine katika Waislamu, basi sisi maibadhi tunasema kua Muislamu anapodiriki sala ya Imam, yeye atalazimika kuenda sambamba na Imam katika Sala yake ile, kwa hivyo kile anachokisali pamoja na Imam kinakua ndio sehemu ya Mwisho was ala yake, kwa hivyo Imama anapotoa salamu yeye atalazimika kusimama bila Tak-bira na hapo ataanza yale ya Mwanzo Baada ya kutoa Tak-biratu l-ihraam na ataendelea na Sala yake mpaka afike pale alipomkutia Imama wake bila kupunguza kitu wala kuongeza. Na ili ifahamike vizuri inabidi hapa tuweke mifano.

1.    Nimekuja katika Sala ya Imam na nikamkutia Imam katika rakaa ya mwanzo, na mimi nikaingia katika Sala bila kuwahi Al-hamdu itakua vipi sala yangu?

Jawabu:

Mimi katika hali hiyo imenipita Al-hamdu sikuiwahi pamoja na Imam, kwa hivyo itanilazimikia kuilipa hiyo alihamdu, na jinsi ya kuilipa itakua kwa kusimama –baada ya Imam kutoa Salamu- bila Tak-bira, na nitasoma Al-hamdu iliyonipita tu, kisha nitakaa bila ya Tak-bira na Baada kutulizana katika Kitako nitatoa Salamu, na Sala imemalizika.

2.    Nimekuja na nikamkuta Imam yuko katika Tahiyatu ya kwanza, na nilipotaka kukaa Imam akasimama kwa Tak-bira kwa bahati sikuwahi kukaa kitako, vipi nitatimiza Sala yangu?

Jawabu:

Katika hali hiyoitalazimikakuyalipa yale yaliyonipita tu, kwa hivyo Imam akitoa Salamu mimi nitalazimika kusimama bila ya Tak-bira na nitaanza mwanzo kwa Kusoma Al-hamdu, kisha nitarukuu na nitasujudu, tena nitasujudu mara ya pili, na nitasimama kwa rakaa ya pili, nitasoma Al-hamdu kisha nitarukuu na kusujudu, na nitakaa kwa kusoma Tahiyatu ya Mwanzo kisha nitasimama kwa tak-bira, na hapa ndipo nilipomkuta Imam kwa hivyo siongezi kitu wala sipunguzi nitakaa kitako bila Tak-bira na nitatulizana katika kitako, kisha nitatoa Salamu, na Sala nimeitimiza.

3. Nimekuja nimemkutia Imam yuko katika sijida ya kwanza katika Rakaa ya tatu jee nifanye nini?

Jawabu:

Ima hutoingia katika Sala mpaka amalize Sijida ya pili na pale akinyanyuka wewe ndio unaingia katika Sala, kisa anapotoa Salamu Utaanza kuyalipa yale yote yaliyokupita mpaka pale ulipoingia katika Sala, kisha utakaa kitako na utatoa salamu na sala Imekwisha, Au utaingia katika Sala na hapo utaungana na Imam katika Sijida ya pili, kisha Atakapotoa Salamu, wewe utalipa mpaka ile sijida ya Pili na hutolipa kile kisimamo cha Rakaa ya Nne, kwani ulikiwahi, lakini utakaa na utatoa Salamu na Sala imekwisha.

Hivi ndivyo Maibadhi wanavyolipa kile kilichowapita pamoja na Imam, Jee!! Dalili gani wanatumia katika suala hili?

Jawabu:

Dalili ya haya yote ni Hadithi ya Mtume (s.a.w) inayosema :

إذا أتيتم الصلاة عليكم السكينة فما أدركتم فصلوا وما فاتكم فأتموا –ووفي رواية- فاقضوا”

Munapokwenda katika Sala ni juu yenu kuwa watulivu mutakachokiwahi kisalini na kilichokupiteni kitimizeni -na katika mapokezi-  kilipeni” Basi haya ni mapokezi mawili, Amesema Sheikh Ahmed L-haliliy (h.a) kua yote ni Sahihi” na sisi tunategemea katika riwaya iliyosema “Kilipeni” kwa hivyo sisi tunalipa kilichotupita na wala hatutimizi, hii ni njia ya kutolea Dalili katika Hadithi hii. Amesema Sheikh Ahmed L-haliliy (h.a): Na Imam Nuru Dini Saalimiy (r.a) anao uchambuzi katika maudhui hii, na ufupisho wake ni kua hakuna Dalili katika kila riwaya mbili kwa kutegemea neno “Kilipeni” au “Kitimizeni” lakini hasa Dalili inapatikana katika lile neno “Kilichokupiteni” hakiki elezo la kupitwa ni dalili ya kua atakachokisali Maamuma pamoja na Sala ya Imam kitakua ni cha mwisho wa sala yake” kwa hivyo kile atakachokisali baada ya kutoa Imam Salamu, kitakua ni cha mwanzo ikiwa kwa neno la Kukitimiza au Kukilipa, na ufafanuzi huu mimi naona kua ndio wenye nguvu za Hoja hususan kutokana na kua Hadithi hii ndio tegemeo la wote katika kuelezea kudiriki Sala.

Basi jishike vizuri katika dalili hii wala usibabaike, kwani Haki iko wazi ndani yake.

Na Allah ndie anayejua Zaidi.

MAAGANO MEMA

KWA HAYA MACHACHE TUNAMUOMBA ALLAH ATUWEZESHE KUIFUATA HAKI NA ATUONDOSHE KATIKA BATILI, NA ATUJAALIE KATIKA WAJA WAKE ALIOWARIDHIA HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA, NA REHMA NA AMANI ZIWE KWA MBORA WA VIUMBE MTUME WETU MUHAMMAD PAMOJA NA AALI ZAKE NA MASWAHABA WAKE NA KILA ANAYEFUATA UONGOFU WAKE MPAKA SIKU YA MALIPO (AMIN)

Asantesana mpaka mara nyengine Allah akitujaalia.

Ndugu yenu

Hafidh. H. Seif Sawafiy

Wassalaam

1424H

[1]:Mapendwa moyo yamefanya kazi kubwa, hata kutungwa kisa hichi kua ni mkasa ulioandaliwa na Abdullahi bin Sabai, na kua wao ni wafuasi wa Ibn Sabai na ndio waliokua Khawarij Baadae; Jee!! unawajua hao? Baadhi yao ni hawa:

1.       Malik bin Harithi maarufu kwa Ash-tar, amemtaja Ibn Hibaan kua ni wa kuaminiwa katika Matabiina, na amesema Imam Aliy: Amrehemu Allah Malik hakika alikua kwangu mimi kama nilivyokua kwa Mjumbe wa Allah”

2.       Thabit bin Qais bin Khatiim bin Uday; amemtaja Ibn Shaahin kua ni katika Masahaba, na huyu alijeruhiwa siku ya Uhud majeraha 12 na akaitwa tokea siku hiyo na Mtume (s.a.w) Haasir, na alimtawalisha Aliy kua ni Gavana wa Madain na yeye aliendelea mpaka akaondolewa na Mughira siku za Muawiyah.

3.       Jundub bin Zuhair Ghamidiy ni mmoja katika Masahaba wa Mtume (s.a.w)

4.       Jundub bin Kaab Uzudiy; huyu ni Jundub Khair aliyemuua Mchawi, na huyu ni katika Mashwaba.

5.       Hakim bin Jibilah Abadiy; ni katika Masahab vile vile.

6.       Hamrani bin Aban; amesema Yahaya bin Main: Hamran ni Tabii wa watu wa madina na Muhaddithi wao.

7.       Zaid bin Sauhan Abadiy; ni ndugu wa Swaa-swaah na Saihan, alisilimu wakati wa Mtume na alikua katika Masahaba.

8.       Swaa-swaah bin Sauhan; ni katika Masahaba wa Mtume (s.a.w)

2: Amesema Allah mtukufu:

وقيل لهم تعالوا قاتلوا في سبيل الله أو ادفعوا قالوا لو نعلم قتالا لاتبعناكم هم للكفر يومئذ أقرب منهم للإيمان

Na inasemwa kwao: Njooni mupigane katika njia ya Allah au muhami, wanasema: Lau tunajua kupigana tungeliwafuata nyinyi, wao kwa Ukafiri siku hiyo ni karibu zaidi kuliko Imani”

Basi Maswahaba wanaijua Amri hii, na wao hawakumuhami kiongozi kwa sababu uongozi wake ulitoka nje ya Mipaka, na ilikua hakuna Matarajio ya kurejea, kwa hivyo kumuhami ni kuihami Dhulma, kwa sababu inatendeka chini ya kivuli chake, na Allah amekataza kusaidiana katika Uadui na Makosa, kama ilivyo katika (5:2) basi wao hawakufanya makosa Allah awape Radhi zake.

[3]:Anasema Allah: فإن بغت إحداهما على الأخرى فقاتلوا التى تبغي حتى تفيء إلى أمر الله  Na kama moja wapo katika makundi mawili Litaasi (kwa kufanya uadui) juu ya mwenginge lipigeni vita hilo lililofanya Uadui mpaka lirejee katika Amri ya Allah (ya kuacha uadui)” basi hii ndio Amri ya Allah katika kulipiga Kundi lililoasi, ili iwe ni sababu ya kuvunja Uadui juu ya mwenye Haki.

[4]:Na hapa tunaona baadhi ya waandishi wanaomnusuru Imam Aliy katika Kosa hili wanamtetea kwa kukisia kukubali Mtume (s.a.w) kufuta Jina la Utume katika Sulhu ya Hudaibiya, basi kukisia huko ni batili kwa sababu zifuatazo:

1.       Ah-naf bin Qais alimwambia Aliy katika kitendo hicho: Hakika hamuna nyinyi aliyokua nayo Mjumbe wa Allah (s.a,w) ” Anamwambia: Hili ndio jina ulilochukulia Ahadi na Kuwapiga Maadui”

2.       Kitendo cha Mtume (s.a.w) kilikua kwa Wahyi uliotoka kwa Allah, kwa hivyo ni jambo lakemaalumu katika Siku ile na sio katika wakati mwengine, kwa sababu hakuandika (s.a.w) katika Maandiko ya Baadae kwa hivyo ni Jambo ambalo limefutwa Hukumu yake.

3.       Walio pamoja na Muawiyah ni Waislamu wanakubali Haki za uongozi na kulazimika Kutii, lakini Muawiyah aliwababaisha kua Aliy sio Kiongozi na wala sio Amiri L-muuminina, na amewahadaa wengi katika jambo hili, kwa hivyo ni kumsaidia na kumpa nguvu katika Uasi wake.

4.       Kuacha Jina la Uongozi sio kama Kuacha Jina la Utume kwa Washirikina, kwa sababu wao wote wanakataa Utume wa Mtume (s.a.w) bila kubabaika yeyote katika viongozi wao.

5.       Utume ni jambo la Kiungu haliwezi kuondoka kwa kufutwa katika Maandiko ya watu, lakini Uongozi ni Jambo la Kibinadamu kutokana na Khiyari ya Waislamu, nalo nitaondoka kwa kujiuzulu Imam kwa Dharura na Kumuondosha Waislamu kwa Makosa.

Anapiga mfano Sheikh Salimiy katika  hali mbili hizi kwa kusema: Mfano wa Utume ni mfano wa Mama wa Mtu haiwezi kuondoka kua ni Mama yake ikiwa atataja kua ni Mama yake au hakutaja, ni sawa kama atakataa mwengine au hakukataa, haki zake zimethibiti; na mfano wa Uongozi ni mafano wa Mke wa Mtu amekua Mke wake kwa Fungo sahihi na kuridhia Mwanamke na Idhini ya Walii, na itaondoka hukumu ya kua Mke kwa Talaka, au Khulugh (Kujivua mwanamke) na kwa njia zote za kuondosha hukumu hiyo”

[5]:Hakuna shaka kua watu hawa walipigwa Vita kidhalimu, kwa sababu Aliy hakua tena Imam kwa kulivua Jina hilo kabla ya Sulhu, na kuondolewa katika Uongozi na Msuluhishi wake, basi aliongoza kundi tu kwa kujilazimisha na cheo kisichokua chake.

[6] :Wengi wanasoma na kuambiwa kua waliomuua Imam Aliy ni miongoni mwa wale watu wa Nah-rawani, na kinaletwa kisa kizuri cha kukutana watatu katika wao nao ni Abdul-rahman bin Muljim na Burak bin Abdillah na Amru bin Bakr, na kua Abdul-rahman bin Muljim alikutana na mwanamke mzuri wa kupita kiasi anayeitwa Qatwaam na mwisho wa kisa ndio Abdul-rahman alimuua Imam Aliy; Tunasema kua Kisa hichi ni Battili kinanuka kwa sababu hakikuthibiti kwa mapokezi Sahihi, kisa hiki amekipokea Imam Twabariy na Twabaraniy na Ibn L-athir na Al-hakim na Baladhuriy; Basi katika mapokezi ya Kisa hiki yumo Otham bin Abdl-rahman Taraaifiy L-harraniy naye anaitwa Abu Abdl-rahman, amesema:

1.       Imam Bukhari: Anapokea kwa watu Madhaifu…

2.       Abu Uruubah: Ameniambia mimi Muhammad bin Yahya :Layyin”

3.       Saajiy: anayo Manakiir

4.       Abdullahi bin Ahmed bin Hanmbali: Ameniambia mimi Baba yangu kua: Simkubalii.

5.       Ibn Numair: Kadhaab (Muongo mkubwa)

6.       Ibn Hibban: Anapokea kutoka kwa watu Madhaifu Mambo kwa anayadallis haifai kutolea Hoja kwa huyo”

Na huyu yumo katika Mapokezi ya Twabariy na Twabaraniy, ama mapokezi ya Ibn L-athir ni mapokezi yaliyokatika kwa sababu Mpokezi wake Muhammed bin Saad alizaliwa mwaka 168H na Imam Aliy alikufa mwaka 40H basi amepata wapi? Na vile vile katika mapoezi hayo yumo Husain bin Fahm na yeye sio wa Kutegemewa ameyasema hayo Daar-qutniy.

Ama mapokezi ya Haakim yumo ndani yake Ismaili bin Abdl-ramhan Saddiy ambaye ndie mpokezi, na huyu hakushuhudia mauaji ya Imam Aliy kwa sababu yeye ni wanaohisabiwa kua ni wa Tabaka ya Nne, na pamoja na kukatika kwa mapokezi haya bwana huyu hajasalimika na Majeraha amesema:

1.       Muhammad bin Issa: Alisema alituhadithia sisi Omar bin Shabah akisema: Alituhadithia sisi Abu Bakar bin Khallaan akisema: Nilimsikia  Muutamar bin Sullaiman anasema: Hakika katika Kuufah pana Waongo wawili Kalbiy na Saddiy.

2.       Muhammad bin Issa: Alituhadithia sisi Abdullahi bin Ahmed akisema: Nilisema kumwambia Yahya bin Main: Ibrahim bin L-muhajir na Saddiy wanakaribiana katika udhaifu”

3.       Amru bin Aliy: Nimemsikia Yahya bin Main ikiwa wametajwa Ibrahim bin L-muhajir na Saddiy basi alisema: Walikua ni Madhaifu wawili na Wadhalilifu wawili”

Ama mapokezi ya Baladhuriy pia yamekatika kwa sababu Shaabiy hakuhudhuria makutano ya Ibn Muljim na wenzake wakati walipopanga mpango huo.

Basi kutokana na Haya vipi mapokezi hayo yakubaliwe na jambo hilo liwe ni la uhakika lisilokubali kurejeshwa?

Juu ya yote haya Amesema Sheikh Saabii: Hakika makubaliano yamepita kua Ibn Muljim ndie aliyemuua Imam Aliy” hwa hivyo hili halina shaka, ama kisa hakikubaliki.

[7]:Anajiuliza Ustadh Ahmed Sulleiman Maaruf akisema: Jee!! Upanga uliomuua Aliy ulikua ni upanga wa Kikhawariji kweli? Au ulikua ni upanga wa Kisasi cha kibinafsi cha baadhi ya waliouliwa wa Nah-rawan, wala hakuna mkono wa Khawariji wote ndani yake? Au ni Mjumbe wa kimapenzi wa Mwanamke wa Kikhawarij jina lakeQutwaam? Au pigo la kunyemelea na mipango ya kisiasa lilipitishwa kwa jina la Khawarij na Mkono kwa Mjanja wa Shaam na Mshauri wake hodari Amru bin L-aas?

Alisema Muhammad bin Mah-buub bin Ruhail Qurashiy –alikua ni katika Wanavyuoni wakubwa wa Kiibadhi katika mwisho wa karne ya pili ya hijiriya- alipoulizwa kuhusu Ibn Muljim: Sijamsikia yeyote akimsifu wala akimlaumu wala hakijanifikia chochote kuhusu yeye” Ikasemwa: Pengine hayo (mauaji) ni kwa Mipango? akasema: Hapana”

Anasema Ustadh Ahmed Siyabiy: Abdul-rahman bin Muljim ni mtu ameingizwa katika Muhakkima au Ahl Nahrawani uingizo, na  akachanganywa katikati yao mchanganyo, pamoja na kua yeye hajulikani katika Safu zao.. na Neno la Imama huyu: Sijamsikia yeyote akimsifu” ni kwa sababu hayumo katika wao wala hana fungamano nao; na neno lake: Wala akimlaumu” kwa sababu ya kujitakasa kwao na kujieka mbali na Matusi na Kulaani”

[8]:Anasema Ustadh Ahmed Siyabiy: Mambo yalivyo Ibn Muljim alitengenezwa kwa njia ya Ash-ath bin Qais, na ni jambo la kitabia kutimia hayo kwa msukumo wa Muawiyah au kujua kwake”

Basi maneno haya yana mtazamo wake kwa sababu tuangalie matokeo ya kitarekhe ya Bwana huyu anayeitwa Ash-ath bin Qais:

1.       Aliritadi pamoja na walioritadi katika Utawala wa Abu baker Siddiq kisha akarejea katika Uislamu.

2.       Alijuta Abu baker Siddiq juu ya kua hakumuua Ash-ath na kusema: Ninatamani siku niliyoletewa Ash-ath bin Qais ningaliipiga shingo yake, kwa hakika inanijia mimi kua yeye haoni la Shari isipokua analikimbilia na kusaidia ndani yake”

3.       Aliandikiwa na Imam Aliy kwa kumuondosha katika Ugavana wa Azarbajaan aliotawalishwa na Oth-man bin Affaan: Hakika yamekudanganya katika Nafsi yako mafunguo ya Allah kwako, basi huachi kula Rizki yake na kujineemesha kwa neema zake na kuondoka mazuri yako katika siku za maisha yako, basi nijie mimi na uchukue yote uliyonayo katika Posho wala usifanye juu ya nafsi yako njia”

4.       Alishikilia kusimamisha Vita Siffain.

5.       Alishikilia kuchaguliwa Abu Mussa L-ashariy.

6.       Kuonesha waraka wa Tah-kiim kwa Makabila katika Jeshi la Aliy.

7.       Kumshikilia Aliy avunje Ahadi yake na Watu wa Hairuraa kua asimpeleke Abu Mussa.

8.       Kumshikilia Aliy walipokua Nakhiilah kuwaelekea Wa Nah-rawaan na kuwaacha Wa Shaam na hayo baada ya kupatikana matokeo ya Tah-kiim.

9.       Kuwavunja Moyo watu wa Aliy baada ya Nah-rawaan katika kumnusuru Aliy katika kupigana na Wa Shaam.

10.    Imepokewa kua Ash-ath aliingia kwa Aliy na Aliy akampa maneno makali, na hapo Ash-ath akamueka wazi kua atamuua. Akasema Imam Aliy kumjibu: Kwa Mauti unanitisha mimi? Naapa sijali ikiwa nitakaa juu ya mauti au Mauti yatakaa juu yangu.

11.    Imepokewa kua Ibn Muljim Alilala usiku ule kwa Ash-ath bin Qais akizungumza naye kwa Siri mpaka ikachomoza Alfajiri akamuambia: Inakufedhehesha Asubuhi” kisha Ash-ath akamtuma Mwanawe akimwambia: Ee kitoto changu kaangalie vili amekua Amir L-muuminina?

12.    Inapokewa kua Ndugu yake na pia Hijr bin Udai na Ami yake kila mmoja katika hao alisikia Ash-ath akimwambia Ibn Muljim: Inakufedhehesha Asubuhi” na baada ya tokeo kila mmoja katika hawa alimwambia Ash-ath: Ewe chongo wewe ndie uliemuua” au mfano wa haya.

Na ndio akasema Ibn Abi L-hadiid: Kila Uharibifu katika Utawala wa Aliy – Alaihi Salaam- na kila mvurugiko uliotokeza asili yake ni Ash-ath” na Shaharistaani anamzungumzia Ash-ath kwa kusema: Ni katika waliotoka sana kwa kumpiga vita (yaani Imam Aliy) na waliotoka katika Dini”

Na kwa hakika suala hili halihitaji utafuto mkubwa, kwa sababu uhakika ni kuondosha upinzani katika Uwanja wa siasa na ukiangalia Siasa ya Dola hii tokea mwanzo wake mpaka mwisho wake –isipokua Omar bin Abdulazizi (r.a)- utaliona  jambo hili liko wazi kama jua:

1.       Kukusanya Panga za watu wa Shaam dhidi ya Aliy.

2.       Ash-tar  Nakhaii alitiliwa Sumu katika kinywaji cha Asali kwa Amri ya Muawiyah.

3.       Muhammed bin Abi Bakar Siddiiq alitumiwa jeshi lililoongozwa na Amru bin L-aas na aliuliwa kinyama sana, kwani alinyimwa Maji mpaka alipofikia juhudi alikatwa katwa kisha alitupwa katika Mzoga wa Punda na kuchomwa Moto.

4.       Anasema Muawiyah: Hakika ilikua kwa Aliy bin Abiy Twaalib Mikono miwili yenye nguvu, niliukata Mmoja siku ya Siffain –yaan Ammaar bin Yaasir- na nimeukata mwengine leo –yaani Ash-tar”

5.       Hassan bin Aliy aliuliwa kwa kutiliwa sumu na Mke wake Jaadah bint Ash-ath bin Qais

Basi ni katika Tabia tukaona katika watu wa Aliy aneyemtuhumu Muawiyah anasema Abu L-aswad Dualiy:

ألا أبلغ معاوية بن حرب * فلا قرت عيون الشامتين

أفي شهر الصيام فجعتمونا * بخير الناس طرا أجمعين

Ee mfikishie Muawiya bin Harb * Hayajatulizana Macho ya wanaotukana

Jee!! katika mwezi wa Funga mumetuvamia * Kwa mbora wa Watu wote.

Juu ya yote hayo tulioleza kuhusu khabari hizi, ifahamike kua hata kama ni kweli mashirikiano hayo yalitokezea na yalifanywa na Ibn Muljim na wenzake na wao ni miongoni mwa watu wa Nah-rawani, basi kitendo hicho kinawarejea wenyewe, kwa sababu hakikufanywa kwa makubaliano wala hukumu iliyotoka kwao, na ndio akasema Mas-udiy: Na wengi katika Khawarij wanajitenga na Ibn Muljim kwa kumuua Imam Aliy kificho” Basi hili lifahamike vizuri.

9: Hili ni Jambo linalobabaisha wengi, na mapendwa moyo katika sehemu hii yanafanya kazi, kwa sababu wengi waliopandikiziwa yasiyokua ya ukweli wanawakusanya Maibadhi na Khawarij, katika hukumu Moja, hili bila Shaka ni kosa, tena ni kosa lisilokua na shaka, na kosa hili linapatikana hasa hasa kwa Sababu mbili:

1.       Kuhukumia Majina.

2.       Uchukivu wa kinafsi dhidi ya Maibadhi.

Ama sababu ya mwanzo inapatikana kwa kua hawa waliotoka katika  Utiifu wa Imam Aliy, baada ya kua wao ni sehemu ya Jeshi lake, basi kwa vile walijitoa ndio wakaitwa Khawarij na sio kwa Sababu nyengine, na hukumu hii kwa Maana hii haiwakamati wao tu, kwa sababu hata Twalha na Zubeir nao walifanya hivyo, kwa hivyo nao ni Khawarij, kwa hivyo jina hilo likitumika kwa Maana hii tu hakuna tatizo, lakini Baadae yakatokezea Makundi hayo matatu ambayo Waislamu wote walikubaliana kuwaita kwa jina la Khawarij, lakini jina hili mara hii lilibeba maana nyengine sio ile ya mwanzo, Mara hii lilibeba sura ya kutoka katika Dini, kama yalivyobashiria mafundisho ya Mtume (s.a.w), na kutoka huku ni kwa sababu ya kuhukumu hukumu ambazo zinakwenda kinyume na Mafundisho sahihi ya Uislamu yanayojulikana kidharura, na kwa makubaliano; basi kutokana na kufanana majina haya mawili; wasiojua  uhakika wakachanganya Mambo, na hapo ikapatikana fursa kwa wale wenye kubeba sababu ya pili, nao wakaanza kuchanganya hukumu za hawa na kuwapa wale, na kuzidi uchafuzi wa uhakika, na haya ndio yaliyomo katika maandiko ya wengi tokea kuanza utunzi, lakini uhakika vyovyote utakavyo fichwa hauachi kujitokeza, hili lifahamike; na kutokana na uhakika huu ndio akasema Sheikh Saalimiy (r.a): Na ujue kua jina la Khawarij lilikua katika wakati wa Mwanzo ni Sifa mzuri, kwa sababu ni mkusanyo wa waliotoka, nalo ni Kundi ambalo limetoka kwa Kupigana katika Njia ya Allah mtukufu, amesema Allah aliyetukuka: Na Wangali taka Kutoka wangalitayarisha kwa Ajili yake Silaha”; Kisha likawa ni Sifa Mbaya kwa wingi wa Tafsiri za walioko kinyume katika kuzifasiri Hadithi za Sifa mbaya zitakazo sifika nazo katika mwisho wa Wakati, kisha likazidi Jina hilo kua Baya walipolitumia Azaariqah na Suf-riyah, basi hilo ni katika Majina yaliyofichika Sababu yake na kuharibika kwa Mengine, kutokana na hayo unaona Ashabu wetu (Maibadhi) hawajiiti kwa jina hilo na wanajiita Ahli l-istiqamah kutokana na Istiqamah waliyonayo katika Dini” Basi hii ndio sababu kubwa inayowafanya Maibadhi kulikataa jina hilo, kutokana na ufahamu mbaya unaochukuliwa sifa zake mbaya, kwa sababu jina sio muhimu lakini maana inayobebwa na lile jina ndio muhimu, basi Maibadhi kwa maana hizo za upotofu sio Khawarij, na wala hatuwezi kuwaita Khawarij kwa sababu ya kuenea maana hizo zilizoenezwa kwa waliobeba jina hilo. Kwa hivyo Ibadhi sio Khawarij.

10: Wako wanaosema kua Maibadhi wanajibandika tu kwa Imam Jabir, na hali ya kua yeye anajitenga nao, wanayasema hayo wakitegemea yale yaliyomo katika kitabu cha Ibn Saad (طبقات), lakini ifahamike kua hayo mapokezi ya Inb Saad ni mapokezi baatil, kwa sababu tunamuona Imam Yahya bin Main anaeka wazi Ubatili wa mapokezi hayo, kwani yeye alipotajiwa mapokezi ya Abu Hilal kutoka kwa Imam Jabir kua alisema: Hakika yeye alikua akijitenga na Rai za Khawarij” Basi Ibn Main akasema: Na hii ni Batili” (tarekhe: Ibn main: J3:106) kisha baada ya hapo tunamuona Ibn Hajar anachukua neno la Ibn Main kua akisema: Alikua Jabir ni Ibadhi” (Tah-dhib: J2:38) kutokana na Haya hatuwezi kukubali mapokezi ya Abu Hilal, na tukaacha Maneno ya mwanachuoni huyu ambayo yanakubaliana na yale yaliyomo katika Madhehebu yenyewe ya Ibadhi. Na Allah ndie muwezeshaji wa Haki.

11: Mimi ninaona Khawarij wanaweza kupatikana wakati wowote ule, na kua Khawarij ni wale aliozitaja Sifa zao Mtume (s.a.w) katika Hadithi yake aliyoipokea Imam Rabii Bin Habib na Maimamu wengine wa Hadithi nayo inasema hivi: Kutoka kwa Abi Saidi Khud-riy kutoka kwa Mtume (s.a.w) kua alisema: Watatoka watu kwenu munaidharau Sala yenu mbele ya Sala yao, na Funga yenu mbele ya Funga yao, na Matendo yenu mbele ya matendo yao, wanasoma Qur-ani lakini haivuuki koo zao, wataihama dini kama Mshale unavyohama Upinde wake, utaangalia Kisu chake hutoona kitu, utaangalia mshale wake hutoona kitu, utaangalia unyoya wake hutoona kitu, na tayari unatembea katika Hewa na kwenda zake” basi kutokana na Hadithi tunaona kua Khawarij watakua na Sifa zifuatazo:

1.Watakua ni wingi wa Ibada kiasi cha kuidharau mmoja wetu Ibada yake mbele ya Ibada ya Khawarij.

2.Watakua ni wasomaji wa Qur-ani sana.

3.Qur-ani haivuuki katika Koo zao, kwa maana watakua mbali sana katika kuifahamu Qur-ani ndani fikra zao, maneno yao na hukumu zao.

4.Watakua mbali na Dini kama Mshale unavyokua mbali na Upinde wake. Kwa Maana Hawatakua na sehemu katika Dini isipokua Kujinasibisha tu.

Basi tuangalie katika Mizani hii ni nai Khawarij? Ni wale waliokubaliana na Qur-ani au ni wale wanaopingana na Qur-ani, na hii ndio Mizani ya Uadilifu, na Allah ndie anayejua zaidi.

10: Hadithi hii inagongana na Qur-ani, basi tunaona kua ni Dhaifu kwa sababu inatueleza kua Moto hautojaa siku ya kiama mpaka Allah aweke ndani yake Mguu wake ndio utasema hivyo utakavyosema, na Allah mtukufu anatuambia kua: Kwa hakika tutaijaza Jahannam kutokana na Majini na Watu wote” kwa hivyo Moto utasema Jee!! lipo la kuongeza? ikiwa bado tu hawajamaliza kuingia humo hao wa Motoni, na katika Aya hiyo isije ikafahamika kua Watu na Majini wote wataingia Motoni, la sio hivyo lakini ni wale watakao kua wa Motoni, na hayo maneno yamekuja hivyo kuonyesha kua Wengi ni wa motoni, na Wachache ndio wa Peponi basi kutokana na uchache wao kama kwamba sio chochote ukilinganisha na wale wa Motoni, Allah atuweke mbali na Adhabu ya Moto kwa sababu atakayeingia humo hana njia ya kutoka (Amin).

11: Hapa mapendwa Moyo yanafanya kazi yake, kwa sababu yalipofika katika Hadithi hii na kuona kua haiwezekani kumona Allah kutokana na Dalili iliyomo ndani yake, kwa hivyo ikawa hayapatikani yale inayotamani, yakaona kua hakuna njia isipokua, ni kuleta maana ya kuondoka Sifa ya Dhati ya Allah mtukufu ambayo ni Kib-riyai, na kutokana na hayo wako waliosema kua, sifa hiyo itaondoka kwa Fadhila zake Allah juu ya Waumini, na wako walisema: Kua atafanya pamoja nao kinyume na Sifa yake hiyo, na mengi yamesemwa ambayo ukitasoma au kuambiwa Mwili hisisimkwa kutokana na Kujihukumia kwao katika Dhati ya Muumba kama kwamba nayo ni Kiumbe inabadilika katika Hali na kwenda katika Hali nyengine, Hakika Allah ametakasika na wanayoyasema Mtakaso mkubwa kabisa.

[14] Namna ya kulipa Sala mtu alizoziacha, kuna khilafu ndani yake, na sisi tunaona kua kutarejea kwanza katika Nia ya Mwenye kutubia, kisha ataweza kupanga jinsi ya Kuzilipa, kwa kujibu wa wepesi wa kuzilipa, na kama hazijui sala zake alizoziacha atalazimika kukisia kwa itakapo tumania Nafsi yake kua hapa ni sawa sawa, na sio kufanya Hadaa na kwa Allah hakifichiki kitu.

[15]Namna ya kufunga itakua kama Namna ya Kusali katika Maelezo yaliyopita.

[16]Hili ni katika Mambo yenye Khilafu ndani yake, kwa sababu imethibiti, kua Mtume Muhammad (s.a.w) ndie Mtume wa mwisho, kwa ubainisho wa Allah, na vile vile yeye mwenyewe (s.a.w) amesema: Hakuna Nabii baada yangu” sasa ikiwa Masihi Issa mwana wa Mariyam (a.s) atakuja haitoacha kua katika moja ya hali tatu:

Ima atakua Mfuataji wa Sheria ya Muhammad (s.a.w), nalo ni jambo zito kwa sababu yeye kapewa Sheria na kitabu Injili, na hili linawezekana na kua ni njia ya Kumfadhilisha Mtume Muhammad (s.a.w).
Ima Atafuata Sheria yake yeye Peke yake, na kua Umma wa Muhammad (s.a.w) wataendelea na Sheria yao. Na kubainisha Uahribifu wa Sheria yake.
Au atakua ni Mtume na Nabii walioko Ardhini watalazimika kumfuata, kwa kuthibiti Utume wake, na yeye ni njia ya Uongofu na ubainishaji kwa waliopotea katika Umma huu, na hili lina Khatari yake kwa sababu ni kuthibitisha Utume baada ya Muhammad (s.a.w).
Mimi upande wangu suala hili ninasimama katika neno: Allah ndie anayejua wala sisemi kitu, kwa sababu sijaona Dalili isiyoingiwa na Shaka ya kuthibitisha Itikadi hii, kwa Hivyo ninasimama kwa kuiegemeza Elimu yake kwa Allah mtukufu, na wala sipingi kuja kwa Mtume Issa Mwana wa mar-yam (a.s) kwa maana ya Kwanza na Ya pili, bali naona kua hilo liko Karibu, zaidi kutokana na Mafundisho ya Qur-ani, kwa sababu katika Aya ya 81 ya sura ya 3, inatuonyesha kua Manabii wote alichukua Ahadi ya kumkubali Mtume atakayekuja baada yao na kumnusuru, na kufuata uongofu wake, na pia imepokewa kua Mtume wetu Muhammad alisema: Lau kua Ndugu yangu Mussa yuko hai asingelipata nafasi isipokua ya kunifuata mimi” na tukiangalia katika Aya ya 159 ya sura ya 4 tunaona kua Allah anahakikisha kua Kila Ahlil-kitabu atamuamini Mtume Issa kabla ya kufa kwake na huko kutakua kabla ya kusimama Kiama, na katika yanayojulikana kua Umri wa Mtume Issa ni kama wa Waja wengine, na imethibiti kua hakuuliwa na kua alipandishwa, kwa hivyo kuja kwake kuko karibu zaidi katika ukweli na haki kuliko kulipinga suala hili, na mimi ndio Itikadi yangu, na Ghaibu iko kwa Allah, yeye ndie anajua zaidi.

17: Imam Bukhari katika Hadithi hii anao Masheikh wawili, na wote wanaleta mapokezi hayo hayo nao ni: Abdullahi bin Maslamah, na Is-mail bin Abi Uwais; sasa hawa Masheikh wawili wametofautiana katika Abi Hazim jee! alisema: Anaegemeza hayo au yanaegemezwa hayo, ikiwa ni neno la mwanzo itakua aliyeegemeza ni Yule sahaba naye ni Sahl bin Saad (r.a), na ikiwa ni neno la pili itakua hajulikani aliyeegemeza hayo na Hadithi itakua Dhaifu kwa kukatika Upokezi au kwa kua ni Mursali. Na haya mawili yanafanya mapokezi haya ya Hadithi yagongane, na kugongana kwa mapokezi ya Hadithi ni dalili ya Udhaifu wake, wanayajua haya wanaojishughulisha na Elimu ya Hadithi (Wallahu aalamu).

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here