Home fatawa za samahaat Sh. Ahmed Al-Khalili-Muft Wa Oman KUANDAMISHWA MWEZI WA HIJA

KUANDAMISHWA MWEZI WA HIJA

315
0

Msitahiwa Sheikh wetu Mwanachuoni Ahmad Hamad Al-Khalili    Allah mtukufu akupeni taufiki yake.

Mufti Mkuu wa Oman.

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Maudhui: Kutaka Fatwa kuhusu watu kulinganiwa kwenda katika misala ya Iddi siku ya Jumapili na wakatae kuisali siku ya Jumamosi.

Msitahiwa Mufti munajua vizuri yaliyotokeza kuhusiana na suala la muandamo wa mwezi wa Hijja hapa kwetu katika kufanyia kazi kalenda ya Ummu Al-Quraa (Saudia) pamoja na kuwa vielelezo vya elimu ya falaki vinatilia mkazo kutowezekana kuonekana muandamo katika sehemu zote za Oman, lakini baadhi ya Makhatibu na watu wema ameanza kuita watu katika miji na vijiji ili watoke kwa kusali sala ya Iddi ya Udh-hiyah katika misala na misikiti.

Ni ipi rai yenu ewe Msitahiwa kuhusu ulinganio huu?

Jee! Munaona kuwa zuri zaidi kulazimika kila mtu na hali yake binafsi na watu wake?

JAWABU:

Amesema Allah mtukufu: Na wanakuuliza kuhusu miandamo. Sema hiyo ni nyakati kwa watu na Hija..” Na maana yake ni kuwa nyakati za ibada zote zimefungwa kwa kuonekana muandamo na kuthibiti muandamo. Na iwapo haitawezekana kuonekana (Muandamo) kwa mujibu wa elimu ya falaki -ambayo imekua ni uhakika wa yakini katika kuainisha kwake kuthibiti ushahidi na kutothibiti kwake- kisha wakashuhudia mashahidi kuwa wao wameuona muandamo, ushahidi wao utarejeshwa na hautategemewa hata kama watakua ni zaidi ya kumi.

Na kwa hilo, hakika sisi hatukubaliani na hatua ya kuitanguliza Iddi kabla ya wakati wake wa kisheria, lakini hatuungi mkono zogo na fujo, basi hatukubaliani na hizo ilani za kuasi amri za serikali, pamoja na hayo, pia hatuoni njia ya kuwafuatilia wenye kuichunga dini yao kwa kusali sala Iddi wenyewe katika nyumba zao au katika sehemu zao binafsi kwa mujibu wa wakati wake wa kisheria, nao wakatekeleza ibada ya kuchinja katika siku ambayo wao wanaiona ndiyo hasa siku ya Udhhiyah ambayo ndani yake imekubalika kisheria, kwani hakika katika kuwafuatilia kuna uzuiaji baina yao na utekelezaji wa ibada hizi katika nyakati zake.

Na Allah ndiye anayejua zaidi.

TANBIHI

Fatwa hii ilikua katika mwezi wa Hijja mwaka 1435 Hijira iliokua katika mwaka 2014 Miladi.

FATWA ASILI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here