Home tohara 5. Nini hukumu ya maji ya wadi, tahiri au si tahiri ikiwa...

5. Nini hukumu ya maji ya wadi, tahiri au si tahiri ikiwa yamebadilika moja kati ya sifa zake, nayo ni rangi kwa sababu ya udongo yanaoukumba?

219
0

Nini hukumu ya maji ya wadi, tahiri au si tahiri ikiwa yamebadilika moja kati ya sifa zake, nayo ni rangi kwa sababu ya udongo yanaoukumba?

Maji hayanajisiwi ila na kitakacho yaenea kikabadili rangi yake au ladha yake au harufu yake, kwa sharti hicho kitakacho yaenea kiwe ni najsi; ama mchanga si najsi bali unashirikiana na maji katika sifa zake mbili nazo ni utohara na utoharishi, na kwa hiyo udongo hauyanyang’anyi maji mojawapo ya sifa mbili hizo. Na Allah anajua zaidi.

__________________________________________________________________

Wadi = bonde kama mto lipitalo maji ya mvua.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here