Home vitendo vya sunna katika sala 4. Takbiratul wakati wa Kurukuu na Kusujudu.

4. Takbiratul wakati wa Kurukuu na Kusujudu.

245
0

Kupiga Takbira yaani kusema “Allahu Akbar” wakati wa kurukuu na kusujudu ni sunna iliyotiliwa nguvu katika sehemu zote, isipokuwa tu wakati wa kuinuka kutoka katika rukuu. Kasema Abu Huraira R.A.A., [1]“

كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاةِ يُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْكَعُ ثُمَّ يَقُولُ سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ حِينَ يَرْفَعُ صُلْبَهُ مِنْ الرَّكْعَةِ ثُمَّ يَقُولُ وَهُوَ قَائِمٌ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَهْوِي سَاجِدًا ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ رَأْسَهُ ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَسْجُدُ ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ رَأَسَهُ ثُمَّ يَفْعَلُ ذَلِكَ فِي الصَّلاةِ كُلِّهَا حَتَّى يَقْضِيَهَا وَيُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ مِنْ الثِّنْتَيْنِ بَعْدَ الْجُلُوسِ.

Maana yake, “Alikuwa Mtume S.A.W. anakabir wakati anaposimama katika Salaa na anakabiri anaporukuu halafu anasema, “SAMIA LLAHU LIMAN HAMIDA.” anapoinua mgongo wake kutoka kwenye rukuu. Na anaposimama wima kabla hajasujudu anasema, “RABANA WALAKAL HAMD,” Na anaposujudu anasema, “ALLAHU AKBAR.” na pia anakabir anapoinua kichwa chake, kutoka kwenye sujudi, na anakabir anapoinuka kutoka kwenye kikao, na anafanya hivyo katika kila rakaa mpaka anapomaliza Salaa.” Pia Kasema Abdillah Ibn Masoud R.A.A., [2]“

رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكَبِّرُ فِي كُلِّ رَفْعٍ وَوَضْعٍ وَقِيَامٍ وَقُعُودٍ.

Maana yake, “Nimemuona Mtume S.A.W. akikabir kila anapoinuka, na anapokwenda chini, na anaposimama, na anapokaa (kwa tahiyatu)”

Ikiwa mtu atasahau kuitamka Takbira wakati wa kurukuu na kusujudu wakati Salaa, Salaa yake haiharibiki, akimaliza Salaa basi itanbidi asujudu sijdat sahau. Wamekhitilafiana wanavyuoni ikiwa atakuwa amesahau Takbira nyingi: baadhi yao wanasema airudie Salaa yake. Na Mwenyezi Mungu ndie mjuzi zaidi.

 

[1] Nnasaai 4/361 (1138).

[2] Ahmad 8/84 (3549)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here