Home Mujtahiduna SHEIKH ALALLAMAH SAEED MABRUUK AL-QANNUBI ALLAH AMUHIFADHI

SHEIKH ALALLAMAH SAEED MABRUUK AL-QANNUBI ALLAH AMUHIFADHI

272
0

21/02/2022
create new demo(same design)

Gravity Forms(google captcha ke liye)

websopcx
https://igrsup.gov.in/igrsup/newPropertySearchAction

AL2004071999602

317710067033

https://mnregaweb2.nic.in/netnrega/IndexFrame.aspx

intely
$P$BUPWWT94

rpukhraj
JN%R&UJ24^F43

hexalogixsystems@gmail.com
Il2=\GqG1ir7

Ni Sheikh Al-Allaamah Al-Muhaqiq Al-Muhaddith Saeed Mabrook Hamoud Al-Qannubi Allah amuhifadhi.

 

Amezaliwa mwaka 1384 Hijiria – 1964 Miladi katika kijiji cha Shaariq, Wilaya ya Mudhaibi, Mkoa wa Sharqiyah, nchini Oman.

Alianza masomo yake ya awali katika kijiji cha Al-Aflaaji kilicho karibu na kijiji alichozaliwa ndani yake, na kipaji chake cha ufahamu wa hali ya juu sana kilianza kuwachukua walimu wake tokea mwaka wake wa mwanzo alioanza masomo yake ya shule.

Baada ya hapo Sheikh Al-Qannubi -Allah amuhifadhi- alikutana na Mwanachuoni Mlezi Al-Allamah Sheikh Humoud Humaid Al-Sawafi -Allah amuhifadhi- huko Snaw, na hapo kikawa kikawa ndio kituo cha kuanza kuchukua elimu za Uislamu, alimlazimu Sheikh huyo, naye kwa upande wake alikua ni chemchemu ya hekima na busara na malezi bora na fani nyingi za elimu ya Dini yetu na Fasaha na tabia njema, pia Sheikh Al-Qannubi wakati wa kuwepo kwake kwa Sheikh Al-Sawafi aliweza kupata nafasi ya kusoma vitabu vingi; kwani Allah alimpa uwezo mkubwa sana wa kusoma vitabu na kuhifadhi yaliyomo ndani yake, vitabu ambavyo alivipata moja kwa moja katika maktaba ya Sheikh Humoud Al-Sawafi -Allah amuhifadhi-; kwani kipindi hicho Sheikh Al-Qannubi hakua akilimiliki isipokua vitabu vitatu tu navo ni Talqiinu Sibyaani na Tuhfatu Al-Aayaani na Riyaadhu Saalihina, navo ni miongoni mwa vitabu ambavyo Sheikh Al-Qannubi anavipenda sana hadi leo hii kwa sababu ndivo vilivokua mwanzo wa kupanda kwake daraja ya kielimu hadi kufikia daraja ya Mujtahid wa kutegemewa rasmi katika Fatawa na fani mbali mbali za elimu za Kiislamu.

Sheikh Al-Qannubi alisoma Maahad Al-Qadhaa wal- Waadh wal- Irshaadi, nacho ndicho chuo cha juu kabisa katika elimu za Dini na Ukadhi (Ujaji) ndani ya Oman, na hapo Sheikh Al-Qannubi alifanikiwa kupata fursa ya kukutana na wanavyuoni mbali mbali na kuchukua waliyonayo katika elimu, miongoni mwa Mashekhe hao ni Al-Allaamah Ahmad Hamad Al-Khalili Mufti mkuu wa Oman Allah amuhifadhi na atufae kwa elimu yake.

Alijulikana Sheikh Al-Qannubi kwa nguvu kubwa sana ya kuhifadhi, na ufahamu wa ndani na wa hali ya juu sana, na uhodari ulio nadra sana, na jitihada isiyo ya kawaida katika kutafuta elimu na kufuatilia masuala yake, na safari zake katika kutafuta vitabu na kuviulizia, na kwa sababu hiyo, leo hii Sheikh Al-Qannubi anamiliki maktaba yenye vitabu vya fani mbalimbali ambayo ni shida kupata mfano wake katika Omani, pia maktaba yake inakusanya vitabu mama vya sheria ya Kiislamu na fani mbalimbali za lugha ya Kiarabu.

Sheikh Al-Qannubi amekua wa juu sana katika elimu ya Hadithi na Usuli na Fiqhi naye ni bahari ya elimu katika fani hizo.

Sheikh Al-Qannubi ameandika vitabu na risala na jawabu nyingi miongoni mwa hizo ziko zilizochapishwa na nyengine bado hazijachapishwa.

Vitabu mashuhuri vya Sheikh Al-Qannubi ambavo vimeshapishwa ni:

Al-Imamu Rabii bin Habiib Makaanatuhu wa Musnaduhu.
Qurratu Al-Ainayni.
Arraayu Al-Muutabar.
Assaiful-Haadd.
Attuufaanul-Jaarif.
Hivi sasa Sheikh Al-Qannubi Allah amuhifadhi ni mshauri wa kielimu katika Wizara ya Wakfu na Mambo ya Kidini Oman, pia tunapata kutoka kwake vikao vingi vya darsa mbalimbali na kujibu masuali.

Ujumla wa maneno tunamalizia kuhusu Al-Allaamah Al-Qannubi Allah amuhifadhi kwa ushahidi wa Samaahatu Sheikh Al-Allaamah Ahmad Hamed Al-Khalili Allah amuhifadhi na atufae kwa elimu zao, amesema:

وعليه في عصرنا إمام المعقول والمنقول القنوبي حفظه الله.

“Na huu vile vile katika zama zetu hizi ndio msimamo wa Imamu wa Elimu za Akili na Kunakili Al-Qannubi Allah amuhifadhi.”

ويلمح من كلام الحافظ الحجة العلامة القنوبي حفظه الله.

“Na inaashiriwa katika maelezo ya Al-Haafidhu Al-Hujjatu Al-Allaamah Al-Qannubi Allah amuhifadhi.

وقد تولى مناقشة أكثرها في وقتنا هذا العلامة المحدث الكبير الحافظ الحجة الشيخ القنوبي جزاه الله تعالى خيرا وأطال في عمره.

“Na Al-Allaamah Al-Muhaddithu Mkuu Al-Haafidhu Al-Hujjah Sheikh Al-Qannubi ameshughulika vizuri kufafanua mengi yao katika zama zetu hizi, Allah mtukufu amlipe kheri na arefushe katika umri wake.”

فقد طلبت الإجابة عليها من علامتنا النحرير الشيخ سعيد بن مبروك القنوبي وهو شاب فتح الله بصيرته وأفاض عليه من مواهبه فبلغ في علوم الشريعة مرتبة لا يزاحمه فيها مزاحم.

“Nami nimetaka jawabu ya suala hili kutoka kwa Mwanaelimu wetu Mhakiki Sheikh Saeed Mabruuk Al-Qannubi nae ni kijana ambaye Allah amemfungulia mapeo yake basi amefikia katika elimu za sheria daraja ambayo hawi mweza naye mwengine”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here