Home saumu yako dhamana yako SAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 008

SAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 008

92
0

Anasema الله ﷻ katika Qur-an;

{شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ}

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa katika mji katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.

-Sura Al-Baqarah, Ayah 185

*NAAM NDUGU WAPENDWA KATIKA IMANI,  TUNAENDELEA KUELEZEA MAMBO MUHIMU MIONGONI MWA MAMBO AMBAYO TUNA PASWA KUYASHIKA KATIKA MWEZI HUU WA RAMADHANI,  MWEZI ULIYOBARIKIWA,  KATIKA MAMBO MUHIMU NI PAMOJA NA.

4 – QIYAAMUL-LAYL (KISIMAMO CHA  USIKU)

Bila shaka visimamo katika sala za usiku zinafaida nyingi sana,  hasa ukizingatia mtu ambae atasimama ndani ya mwezi ambao fadhila na malipo yake huwa makubwa zaidi.

Visimamo katika sala za usiku humkurubisha zaidi mja kwa Mola wake mlezi, pia humuweka kua katika daraja la waja wema wa Allah ambao amewaelezea ndani ya Qur an tukufu.

Anasema الله ﷻ katika Qur-an;

{وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا}

Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama.

-Sura Al-Furqan, Ayah 64

Lakini pamoja na hayo yoote;

Mtume (ﷺ) anasema:

(من قام رمضان إيماناً واحتساباً، غفر له ما تقدم من ذنبه)
أخرجه البخاري ومسلم

Atakayesimama [kwa Swalah ya usiku] kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)

Basi tusiwe wavivu juu ya kusimama katika sala za usiku,  wala tusipumbazwe na michezo mbalimbali katina simu, TV zetu, maana zama hizi wapo watu kazi yao ni kushinda au kukesha katika mitandao wakifuatilia tamthilia na mambo ya kipuuzi yasiyo na faida tena yenye khasara.

Kwa hakika huko ni kupoteza muda na wakati kiasi ambacho tutakuja jua thamani ya wakati katika kipindi ambacho kujua kwetu hakutokua na faida kabisa bali tutabakia na majuto yasiyo na manufaa.

TUKITHIRISHE SANA KUSIMAMA USIKU KWA AJILI YA IBADA ILI TUWE KARIBU ZAIDI NA ALLAH MTUKUFU WALA TUSIFANYE UVIVU JUU YA AMALI NA NAFASI HII AMBAYO HUENDA NDIO IKAWA YA MWISHO.

Previous articleSAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 002
Next articleSAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 007

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here