Home Hii ndio saumu SAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 007

SAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 007

42
0

Anasema الله ﷻ katika Qur-an;

{شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ}

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa katika mji katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.

-Sura Al-Baqarah, Ayah 185

LEO TENA BI IDHINLLA TUNAANGALIA JAMBO LA TATU (3) KATIKA MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIWA NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI AMBAO NI MWEZI UNAOTUHITAJIA KUJIFUNGA SAWASAWA KWA KUFANYA KILA YALIYO YA KHERI,  JAMBO HILO NI.

3 – KUKITHIRISHA KUSOMA QUR-AAN.

Kwa nini kukithirisha kuisoma Qur an?  Kwa sababu Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi wa Qur-an, ni mwezi ambao   ndani yake ndio hasa kimeteremshwa kitabu huki kitukufu (Qur-aan),

Anasema الله ﷻ katika Qur-an;

{شَهْرُرَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَان}

Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe Hidaaya kwa watu na hoja bayana za Hidaaya na Al-Furqaan (Upambanuzi).

[Al-Baqarah: 185]

Ni vyema kwa kila  muislamu kuzidisha jitihada zake katika kukisoma  kitabu hiki kitukufu (Qur-aan) angalau kila muislamu aweze kukihitimisha japo mara moja katika mwezi huu. Bila shaka kabisa kwa zama hizi watu wengi wameshuulishwa na dunia na hasa kiasi ambacho laiti leo tungezikamata na kushinda nazo kama ambavyo tunazishika simu zetu na kushinda nazo tukisoma mambo mbalimbali, kwa hakika dunia na miji yetu ingejaa baraka tele.

Lakini kwa kweli Qur an tumeitelekeza sana ila tu kwa wachache sana miongoni mwetu,  sasa angalau basi ndani ya mwezi wa Qur an tukithirishe kuisoma kwa kuizingatia huenda ikapatikana kheri tukaikamata na kusoma hata baada ya Ramadhan.

Aidha hali ya kuisoma Qur an,  ndiyo iliyokua desturi ya maswahaba waongofu kushindana katika kukisoma kitabu cha Allah Mtukufu ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akihitimisha Qur-aan kila siku moja yani kwa siku juzuu 30, kadhalika na maswahaba wengine ambao walikua wakishindana na kuoneana wivu juu ya usomaji wa Qur an khususan ndani ya mwezi wa Ramadhan.

MWEZI WA RAMADHAN SIO MWEZI WA KUVUMBUWA KILA AINA YA MICHEZO NA KUPOTEZA MUDA,  BALI NI MWEZI WA KUCHUMA KWA KUKITHIRISHA KUISOMA QUR AN AMBAYO MALIPO YAKE YATAKUA MARA DUFU ZAIDI NA ZAIDI NA ZAIDI.

Previous articleSAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 008
Next articleSAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 006

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here