Home Hii ndio saumu SAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 001

SAUMU YAKO DHAMANA YAKO: 001

248
0

SAUMU YAKO DHAMANA YAKO

Anasema الله ﷻ katika Qur-an;

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ}

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu.

-Sura Aal-E-Imran, Ayah 102

*Zikiwa zimesalia siku chache kabisa kuelekea katika Mwezi wa Ramadhani,  Mwezi wenye uliyo barikiwa,  mwezi wenye fadhila nyingi,  mwezi wenye kheri nyingi kabisa,  mwezi wa Qur an.*

JE VIPI TUUPOKEE MWEZI HUO ?

*Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya waisilamu kufanya maasi wakiita (Vunja jungu)  yani maasi hayo huyafanya siku chache kabla ya kuingia Mwezi wa Ramadhani,  hali ambayo Ramadhani inawakuta wakiwa wachafu kwa maasi waliyo yafanya wakidai watajisafisha ndani ya ramadhani.*

*Haya ni mambo miongoni mwa mambo ya kijahili kabisa ambayo hayapaswi muisilamu kuwa nayo,  kwani haiwezekani mtu ametoka kazini kwake na tope miguuni kisha akaingia kulisafisha tope hilo sebuleni au chumbani kwake,  bila shaka mtu huyo ataonekana maj nuun wa kutupa.*

*Kadhalika Ramadhani yatupasa itukute tukiwa wasafi kabisa kutokana na madhambi,  muda huu ni muda wa kufanya istigh’faar kwa wingi wala sio muda wa kufanya maasi.*

*Lakini pia tukumbuke kwamba: Sisi hatuna dhamana na kifo,  waonaje siku hiyo ambayo pengine ndio umepanga kwenda kufanya maasi na mauti yanakukuta katika hali hiyo, nini utakwenda kumjibu Allah mtukufu?*

*Bila shaka mfano wa hicho ni kifo kibaya na Allah atunusuru sisi na waisilamu wenzetu,  kwani popoye tuwapo na tuendapo tu atembea na mauti,  hivyo muda woote twahitajika kujipanga kwa kuyaepuka maasi na kufanya yaliyo mema.*

Anasema الله ﷻ katika Qur-an;

{أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِكْكُمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنْتُمْ فِي بُرُوجٍ مُشَيَّدَةٍ ۗ وَإِنْ تُصِبْهُمْ حَسَنَةٌ يَقُولُوا هَٰذِهِ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ ۖ وَإِنْ تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَقُولُوا هَٰذِهِ مِنْ عِنْدِكَ ۚ قُلْ كُلٌّ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ ۖ فَمَالِ هَٰؤُلَاءِ الْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا}

Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu. Na likiwafikilia jema wanasema: Hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu. Na likiwafikilia ovu wanasema: Hili limetoka kwako wewe. Sema: Yote yanatokana na Mwenyezi Mungu. Basi wana nini watu hawa hata hawakaribii kufahamu maneno?

-Sura An-Nisa’, Ayah 78

JE VIPI TUIPOKEE RAMADHANI ?

FUATILIA MAKALA YAENDELEYAO.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here