Home MADHEHEBU YA UISLAM YA MWANZO PILI:KUBAKIA MOTONI MILELE-2.UOMBEZI

PILI:KUBAKIA MOTONI MILELE-2.UOMBEZI

228
0

2. UOMBEZI

Kwa ajili ya hayo yaliyopita Itikadi ya haki kwa ahlulhaqq wal Istiqaama ni kuwa Uombezi siku ya Qiyama ni kwa waislam peke yao, waliompwekesha Allah mtukufu, waliotubia -kabla ya kufa kwao-ambao Allah mtukufu anawaridhia, amesema Allah mtukufu:

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يَشْفَعُونَ إِلاَّ لِمَنْ ارْتَضَى وَهُمْ مِنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ (الأنبياء: 28)
“Wala hawatawaombea isipokuwa wale walioridhiwa na Allah mtukufu” Anbiyaa:28

Amma wale wang’anga’nizi, wabishi, waliodhulumu nafsi zao, inawatosha qauli ya Allah mtukufu:
وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الآزِفَةِ إِذِ الْقُلُوبُ لَدَى الْحَنَاجِرِ كَاظِمِينَ مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلاَ شَفِيعٍ يُطَاعُ (غافر: 18)
“Hawana madhalimu rafiki wala muombezi yoyote atakayetiiwa” Ghaafir:18

Na malaika katika dua zao hawawaombei msamaha ispokuwa wenye kutubia tu, huwaombea waumini kwa kusema:
الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ (غافر: 7).
“Mola wetu, umekienea kila kitu kwa rehma na elimu, wasamehe wale waliotubu na wakafuata njia yako, na uwakinge na adhabu ya moto”  Ghafir:7

Na haingii akilini, wala haikuthibiti dalili yoyote, Si katika Quran wala sunnah walaw moja tu, inayoonyesha eti wezi, wazinifu, waasi wa wazazi wao, na wengineo katika watu wa madhambi makubwa watakuja kwa Mtume –Sallallahu alayhi wasallam- ili awaombee kwa Allah mtukufu, ati na Allah mtukufu awasamehe na kuwaingiza peponi. Wametakasika na mambo hayo Allah mtukufu na Mtume wake –Sallallahu alayhi wasallam-”
Na vipi yatokee hayo, hali ya kuwa Mtume –Sallallahu alayhi wasallam- anamwambia binti yake na shangazi yake “Ewe Fatima mtoto wa Muhammad –Sallallahu alayhi wasallam- Ewe Safiyyah Shangazi (Amoo) wa Muhammad–Sallallahu alayhi wasallam-, ziokoeni nafsi zenu kutokana na moto, mimi sitokufaeni kitu kwa Allah mtukufu”
Natija ya hayo ni kuwa ITIKADI YA HAKI KWA AHLUL HAQ WAL ISTIQAMA NI KUBAKIA MILELE NDANI YA MOTO KWA WENYE MADHAMBI MAKUBWA KATIKA WAISLAM WAKIFA BILA KUTUBIA, hawatopata Muombezi, wala muokoaji.
Hakika Allah mtukufu amewagawa watu siku ya qiyama katika makundi mawili hakuna la tatu yake, kundi la Peponi na kundi la motoni, wala hakusema kuwa kuwa kuna kundi la tatu litakalotoka motoni kwenda peponi, vile vile Allah mtukufu amewagawa watu siku ya qiyama katika makundi mawili, wema na waovu hakuna la tatu yake, amesema Allah mtukufu:
إِنَّ الأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ (الإنفطار: 13)
وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ (الإنفطار: 14)
يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ (الإنفطار: 15)
وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ (الإنفطار: 16)
“Hakika wema watakuwa peponi, na hakika waovu watakua motoni, watauingia siku ya Qiyama, humo motoni hawatakosekanwa” Infitaar: 13 – 16

Na maana yake: hawato ondoka motoni wala hawatotoka, na hakuna mwenye akili anayesema mwenye kuacha sala, mlevi, mzinifu, kwamba wao ni wema, ispokuwa kama watatubia wakaamini, wakatenda wema. Na kama si hivyo vipi yatakubaliwa matendo ya muislam naye  hasali “na ikiharibika sala, yanakuwa yameharibika matendo yote”, haya ni kwa Yule aliyeharibikiwa na sala yake, basi vipi mtu asiyesali kabisa? na vipi ataingia peponi kwa kumpwekesha Allah mtukufu kwa uzushi wa yule anayedai ati yeye ndio kundi lenye kushinda, au pote lilio okoka ? Amesema Allah mtukufu:
فَخَلَفَ مِنْ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلاَةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا (مريم: 59)
إِلاَّ مَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُوْلَئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلاَ يُظْلَمُونَ شَيْئًا (مريم: 60)
“Wakafuatia baada yao wafuasi wabaya, wamepoteza sala na wamefuata matamanio, watakutana na adhabu kali, ispokuwa watakaotubia…” Mar yam 59 – 60

Na vipi ataingia peponi mwenye kula riba, ambaye Allah mtukufu amemtangazia vita kwa kusema:
وَمَنْ عَادَ فَأُوْلَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (البقرة: 275)
“Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watabakia milele” Baqarah:275

Ewe mola wetu, turuzuku touba ya kweli.
Ewe ndugu yangu mwenye kumpwekesha Allah mtukufu: Jua kuwa Itikadi ya kutolewa waasi motoni,  -imezaliwa na- kukulia kwa mayahudi -kisha kuenea kwa wengine-, anasema Allah mtukufu:
وَقَالُوا لَنْ تَمَسَّنَا النَّارُ إِلاَّ أَيَّامًا مَعْدُودَةً قُلْ أَاتَّخَذْتُمْ عِنْدَ اللَّهِ عَهْدًا فَلَنْ يُخْلِفَ اللَّهُ عَهْدَهُ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ مَا لاَ تَعْلَمُونَ (البقرة: 80)
“Na –mayahudi- walisema: Hautatugusa Moto ila kwa siku chache tu. Sema: JE Mmechukua ahadi kwa Allah mtukufu kuwa Allah mtukufu hatokwenda kinyume na ahadi yake? Au mnamsemea Allah mtukufu mambo msiyo yajua?” Baqarah:80
Na amesema Allah mtukufu kuhusu wao:
 يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَذَا الأَدْنَى وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا (الأعراف: 169)
“Wakashika anasa za haya maisha duni, na wakasema: Tutasamehewa!” Aaraf:169
Hiyo –iliyotajwa katika mambo ya uombezi- ndiyo itikadi ya Ahlil haqq wal istiqama, kwa dalili zake zenye nguvu na za wazi kutoka katika Quran, zenye kuonyesha usafi wa madhehebu hiyo, yenye kutiliwa mkazo na Sunnah ya Mtume –Sallallahu alayhi wasallam- iliyo sahihi, Amepokea Imam Bukhari kutoka kwa Nabii wa Rehma na uongofu –Sallallahu alayhi wasallam – kuwa amesema:  “Hakuna mja yoyote ambaye Allah mtukufu atamtawalisha kwa raia wake, kisha akawa hakuufanyia kazi –utawala huo -kwa nasaha za mola wake, ispokuwa hatopata hata harufu ya pepo”

Na amepokea Albazzar, Ahmad, Alnasaai, na Alhaakim kutoka kwa Ibn Umar – Allah mtukufu amridhie.- kuwa hakika Mtume –Sallallahu alayhi wasallam- amesema “Haingii peponi mwenye kuwaasi wazazi wake, wala mwenye kudumu katika ulevi”  na katika riwaya “Watu watatu Allah mtukufu amewaharamishia pepo, mwenye kudumu katika ulevi, mwenye kuwaasi wazazi wake wawili, na Duyyuth”  Duyyuuth ni Yule anayaona mabaya katika familia yake na wala hayakemei. Na imepokea na Imam Muslim  “Watu wa Makundi mawili katika watu wa motoni sijawaona bado, -kundi la kwanza ni la – watu wamekamata mijeledi kama mikia ya ng’ombe wakiwapiga watu, na –kundi la pili ni la – wanawake wamevaa wakienda uchi, wamepotoka na wanapotosha, vichwa vyao –wamevirefusha au kuvinyanyua- kama nundu la ngamia, hawataingia peponi, na wala hawatoipata harufu yake, japokuwa harufu yake yapatikana kwa mwendo wa kadha kadha”

Na hizi hadithi hata kama zimepokewa kwa njia pweke (( Aahadiyyah)), lakini kwa mkusanyiko wake inafikia Maana yake kuwa ni MUTAWAATIR.

Kwa hiyo Itikadi ya Ahlul haq wal istiqama ni kuwa pepo ni ya wachamungu tu, na dalili zao ni kutoka katika kitabu cha Allah mtukufu, Amesema :
تِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَنْ كَانَ تَقِيًّا (مريم: 63)
“Hiyo ndiyo Pepo tutayo warithisha katika waja wetu walio kuwa wachamungu” Maryam:63
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا (النبأ: 31)

“Hakika wachamungu wanastahiki kufuzu” Nabaa:31
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِنْدَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ (القلم: 34)

“Hakika wachamungu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi” Qalam:34
تِلْكَ الدَّارُ الآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لاَ يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الأَرْضِ وَلاَ فَسَادًا وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ (القصص: 83)
“Hayo ndiyo makaazi ya Akhera, tutawekea  wale wasio taka kujitukuza wala ufisadi duniani. Na mwisho mwema ni wa wachamungu” Qasas:83

Ewe Allah mtukufu, tujaalie kuwa wachamungu, wema.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here