Home MADHEHEBU YA UISLAM YA MWANZO MISINGI YA ASILI

MISINGI YA ASILI

280
0

Misingi ya kisheria kwa Ibadhi ni Qur an na Sunnah na Makubaliano ya wanachuoni mujtahidiina (Waliozamia katika ilmu na uchamungu), na si jambo geni kwa Waibadhi kuchukua kwao na kutolea dalili hadithi zilothibiti kutoka katika Musnad mbili za Bukhari na Muslim, na vitabu vingine vya hadithi na Fiqh vya madhehebu zingine, huku tukijua kuwa Kitabu cha Musnad Imaam Rabii bin Habiib Alfaraahidi – Allah amrehem – ndio kitabu cha mwanzo sahihi katika hadithi na sunnah za Mtume –Sallallahu alayhi wasallam-Na kitabu hicho ndio tegemezi lao la kwanza baada ya Qur an tukufu, na kitabu hicho kina sifa ya pekee ya kuwa na Mfuatano wa wapokezi kama dhahabu –kwa thamani na usafi-, Amesema Mwanachuoni bingwa wa hadithi Sheikh Said Alqannubi –Allah mtukufu amhifadhi- “Nacho –Kitabu cha Musnad Imaam Rabii- ni kitabu sahihi zaidi cha hadithi na cha kale zaidi, na riwaya zake nyingi ni kupitia njia ya Imaam Abii Ubaidah kutoka kwa Jabir bin Zaid kutoka kwa masahaba wa Mtume –Sallallahu alayhi wasallam- na inayofuatia kwa usahihi ni kitabu cha Imaam Albukhari”

Na kwa hakika Mwanachuoni Addarqutni Amemsifia Imaam Arraabi kwa kauli yake ” Amma Rabii bin Habiib Albasri si wa kuachwa”

Na anasema mwanachuoni Msuria Izzuddin Alttanuukhi katika maelezo yake kuhusu kitabu cha Aljaamii Alswahiih: ” Na katika bahati nzuri ilotokea katika elimu ya hadithi ni kuwa Marabii wawili – Rabii bin Subeih na Rabii bin Habiib walikuwa ni katika wa mwanzo miongoni mwa wakusanyajji wa hadithi na watunzi wake, na katika rehma za Allah mtukufu ametubakishia Kitabu cha Musnad Rabii bin Habiib… muaminifu, mwenye kuhifadhi, na mkweli zaidi katika watu”

Na azingatie mwenye uadilifu vitabu na utungaji wa kiibadhi wa kifiqh kama mkusanyiko wa kifqh wa KITAABU NNIL WA SHIFAA UL ALIIL cha mtungaji wake Qutbul aimmah (Kiongozi wa Maimam) Muhammad bin Yousuf Atfeish, pia kama Sharh ya Musnad Imaam Rabii cha mtunzi wake Imaam Saalimi – Rehma za Allah ziwe juu yao – na vitabu vingine, atakuta ndani yake asiyoyakuta katika vitabu vingine kwa nguvu ya hoja, ushujaa na kutokimbia uhakika, na hayo ni kwa kuzitaja qauli na rai za maimam na wanachuoni wa madhehebu zingine kwa heshima zote.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here