Allah ﷻ Anasema:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}
Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. (2:183)
BAADA YA KUFAHAMAU NINI IMANI NA WAPI MAHALA PAKE, LEO KWA UWEZO WAKE ALLAH MTUKUFU TUFAHAMU PIA NINI TAQWA NA WAPI MAHALA PAKE.
فما هي التقوى؟
TAQWA NI NINI?
“التقوى: هي الخوف من الجليل، والعمل بالتنزيل، والرضا بالقليل، والاستعداد ليوم الرحيل”
TAQWA NI – KUMKHOFU ALLAH, NAKUTENDA KWA MUJIBU WA QUR’ANI, NAKURIDHIA KIDOGO CHA HALALI, PIA KUJIANDAA NA SAFARI (MAUTI)
HII NDIO MAANA YA TAQWA KWA UFUPI SANA.
محل التقوى- القلب.
MAHALA PA TAQWA NI MOYONI.
الإيمان تصديق بالقلب، والتقوى محلُّها القلب.
KUMBUKA: IMANI NI KUSADIKI KWA MOYO (MAHALA PAKE NI MOYONI) TAQWA PIA MAHALA PAKE NI MOYONI.
أشار النبي – صلَّى الله عليه وسلَّم – إلى صدره وقال: ((التقوى هاهنها))
ALIASHIRIA MTUME (ﷺ) KIFUANI NA AKASEMA: TAQWA IPO HAPA (NDANI YA KIFUA YANI MOYONI)
SASA TAZAMA HAPA.
الإيمان محلُّه القلب، والتقوى محلها القلب والإيمان في القلب، وكذلك الصيام سر بينك وبين ربِّك لا يعلمه إلاَّ هو.
IMANI MAHALA PAKE NI MOYONI, TAQWA PIA MAHALA PAKE NI MOYONI, KADHALIKA FUNGA NI SIRI BAINA YAKO NA MOLA WAKO MLEZI, HAKUNA ANAE IJUA FUNGA YAKO ILA ALLAH PEKEE.
إذا تستطيع أن تأكل وتشرب بعيد عن عيون الناس وتدعى أنك صائم.
HIVO BASI, WAWEZA KULA NA UKANYWA MBALI NA MACHO YA WATU, KISHA UKADAI UMEFUNGA.
LAKINI KWA SABABU FUNGA NI IBADA YA SIRI, BILA SHAKA SIRI HIYO AIJUA ALLAH MTUKUFU NA YEYE KWAKE HAKIFICHIKI KITU.
فإذا كان الإيمان أمرًا سريًّا، وكانت التقوى أمرًا سريًّا، وكان الصيام أمرًا سريًّا.
SASA BASI, IKIWA IMANI NI JAMBO LA SIRI. NA PIA TAQWA IKAWA NI JAMBO LA SIRI. NA HATA FUNGA NAYO IKAWA NI JAMBO LA SIRI.
فناسب ذلك أن يأتي الصيام بين الإيمان والتقوى.
NDIO IKAWA SABABU YA MNASABA KWA HILO KUJA IBADA YA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA.
لأنَّ الثلاثة أمورٌ سرّيَّة لا يطَّلع عليها إلا علام الغيوب.
KWA SABABU HAYA MAMBO MATATU NI MAMBO YA SIRI AMBAYO HAKUNA WA KUYAONA ILA MJUZI WA YALIYO JIFICHA (ALLAH MTUKUFU)
ولذلك اسمع إلى قول مولانا في الحديث القدسي يؤكد سرّيَّة الصيام، فيقول:
KWA AJILI HIYO, SIKILIZA KAULI YA ALLAH MTUKUFU KATIKA HADITHIL QUDSIY ATILIA NGUVU SIRI YA IBADA YA FUNGA KWA KUSEMA
“ﻛُﻞُّ ﻋَﻤَﻞِ ﺍﺑْﻦِ ﺁﺩَﻡَ ﻳُﻀَﺎﻋَﻒُ ﺍﻟْﺤَﺴَﻨَﺔُ ﻋَﺸْﺮُ ﺃَﻣْﺜَﺎﻟِﻬَﺎ ﺇِﻟَﻰ ﺳَﺒْﻌﻤِﺎﺋَﺔ ﺿِﻌْﻒٍ ﻗَﺎﻝَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﺰَّ ﻭَﺟَﻞَّ ﺇِﻟَّﺎ ﺍﻟﺼَّﻮْﻡَ ﻓَﺈِﻧَّﻪُ ﻟِﻲ ﻭَﺃَﻧَﺎ ﺃَﺟْﺰِﻱ ﺑِﻪِ ﻳَﺪَﻉُ ﺷَﻬْﻮَﺗَﻪُ ﻭَﻃَﻌَﺎﻣَﻪُ ﻣِﻦْ ﺃَﺟْﻠِﻲ ﻟِﻠﺼَّﺎﺋِﻢِ ﻓَﺮْﺣَﺘَﺎﻥِ ﻓَﺮْﺣَﺔٌ ﻋِﻨْﺪَ ﻓِﻄْﺮِﻩِ ﻭَﻓَﺮْﺣَﺔٌ ﻋِﻨْﺪَ ﻟِﻘَﺎﺀِ ﺭَﺑِّﻪِ ﻭَﻟَﺨُﻠُﻮﻑُ ﻓِﻴﻪِ ﺃَﻃْﻴَﺐُ ﻋِﻨْﺪَ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﻣِﻦْ ﺭِﻳﺢِ ﺍﻟْﻤِﺴْﻚِ” متفق عليه.
MAANA YAKE:
“Kila amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba. Na Allah ﷻ Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga swawm atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Mola wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk”
HII NDIO HEKIMA YA KUJA IBADA YA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA, KWA SABABU HIVYO VITU VITATU VYOOTE NI VITU VYA SIRI NA NDIO MAANA VIMEAMBATANA.
والله أعلم
ALLAH MTUKUFU: TWAKUOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.