Home Hii ndio saumu LEO KATIKA FUNGA-2

LEO KATIKA FUNGA-2

203
0

Allah  ﷻ Anasema:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}
Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. (2:183)

NDUGU ZANGU: AYA HII AMBAYO IMEKUJA KWA LENGO LA SISI KUFARADHISHIWA IBADA YA FUNGA, IMEKUJA KWA AINA FULANI YA  KUWAKHUSISHA WATU WENYE IMANI TU,

JE KWANINI IMEWAHUSU WAUMINI PEKEE?

 يا أيها الذين آمنوا، لم يقُل: يا أيُّها الناس، ولم يقل: يا عبادي كتب عليكم الصيام.

ALLAH MTUKUFU AMESEMA: ENYI MLIYO AMINI, NA HAKUSEMA: ENYI WATU, PIA HAKUSEMA: ENYI WAJA WANGU, MMEFARADHISHIWA JUU YENU KUFUNGA.

 إنما خاطب المؤمنين بالذات.
KWA HAKIKA WALA SI VINGINEVYO, ALLAH MTUKUFU AMEWALINGANIA WAUMINI KWA DHATI KABISA.

✅ JAWABU NI KWAMBA:

 لأنَّ الذي يستجيب لأمر الله هو المؤمن، عندما يسمع الله ينادي عليه يقول: لبَّيك ربي.
KWA SABABU, HAKIKA YULE AMBAE HUITIKIA AMRI YA ALLAH MTUKUFU NI MUUMINI, PALE AMSIKIAPO ALLAH AKIMLINGANIA KATIKA KUTEKELEZA AMRI ZAKE,  YEYE HUSEMA NIMEITIKIA EWE MOLA WANGU MLEZI.

NAHAPA NDIPO UTAKAPOJIFUNZA NA PENGINE KUPATA JAWABU LAKO LA SUALA AMBALO, HUENDA MUDA MREFU UMEKUA UKIJIULIZA: KWANINI BAADHI YA WAISILAMU HAWAFUNGI TENA BILA UDHURU WOWOTE KATIKA NYUDHURU ZA KISHERIA?. HAWAFUNGI KWA SABABU YA KUKOSA IMANI.

MAANA SIO SIFA YA MUUMINI KUTO ITIKIA WITO AU AMRI ZAKE ALLAH MTUKUFU AU HUKMU ZAKE, YEYE HUSEMA AMESIKIA NA AMETII.

Allah  ﷻ Anasema:

{إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَنْ يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ}

Haiwi kauli ya Waumini wanapo itwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila ni kusema: Tumesikia, na tumet’ii! Na hao ndio wenye kufanikiwa.

-Sura An-Nur, Ayah 51

MUUMIN HANA KHIYARI KATIKA UTEKELEZAJI WA AMRI ZAKE ALLAH KAMA ILIVYOKUJA KUBAINISHWA NDANI YA QUR AN TUKUFU.

Allah  ﷻ Anasema:

{وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا}
Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.
(33:36)

HII NDIO HEKIMA YA ALLAH MTUKUFU KUWAITA WAUMINI KATIKA AYA HII YA FUNGA.

LAKINI PIA HAPA KUNA SUALA LA SISI KUJIULIZA JUU YA HEKIMA YA QUR AN KUIJALIA FUNGA KUWEPO BAINA YA IMANI NA TAQ’WA.

 فلماذا جاء الصيام بين الإيمان والتقوى؟
JE, KWANINI IMEKUJA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA?

 الإيمان أوَّلاً، والصيام ثانيًا، والتقوى ثالثا
1- KWANZA IMANI.
2- PILI FUNGA.
3- TATU TAQWA.

JE IPI HASA HEKIMA YAKE?

IN SHA ALLAH TUTAANGALIA KATIKA DARSA YETU SEHEMU YA TATU (3).

ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here