Home Hii ndio saumu LEO KATIKA FUNGA-1

LEO KATIKA FUNGA-1

253
0

LEO KATIKA FUNGA (1)

Allah  Anasema:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}
Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. (2:183)

KWANZA KABISA HATUNA BUDI KUMSHUKURU ALLAH MTUKUFU KWA  KUTUJAALIA KUFIKIWA NA MWEZI HUU WA RAMADHANI TUKIWA WAZIMA WENYE AFYA ZA KUTOSHA KABISA, HII NI NEEMA MIONGONI MWA NEEMA KUBWA KABISA KUTOKA KWA MOLA WETU MLEZI,  KWANI WAPO WATU WENGI MIONGONI MWETU AMBAO HATUPO PAMOJA NAO TENA HAPA DUNIANI, NA HUENDA WENGI WETU TULIFUNGA NAO KATIKA MWAKA ULIYOPITA LAKINI SASA HAWAPO NA MAUTI WAMEWAONDOSHA KATIKA HII DUNIA, NA WENGINE WAPO LAKINI NI WAGONJWA NA HAWANA TENA SIHA YA KUWEZA KUTEKELEZA IBADA HII YA FUNGA, NDIO NIKAONA VEMA KWANZA NITANGULIZE KUWAKUMBUSHA JUU YA KUMSHUKURU ALLAH KWA KILA AMBAE AMEKUTWA AKIWA HAI TENA MWENYE SIHA YA KUTEKELEZA IBADA HII YA FUNGA.

PILI NAMUOMBA ALLAH AWASAMEHE NDUGU ZETU WALIYOTANGULIA MBELE YA HAQQI, NA AWAPONYE WAGONJWA WETU, PIA ATAQABBAL FUNGA ZETU. AAMIN YAA RABBAL AALAMIN.

TUINGIE KATIKA DARSA YETU FUPI KABISA INAYO HUSU FUNGA YA MWEZI WA RAMADHANI:

IBADA YA FUNGA NI IBADA ADHIMU KABISA MIONGONI MWA IBADA AMBAZO ALLAH MTUKUFU AMETUFARADHIAHIA SISI WAJA WAKE.

HIVO KUNA BAADHI YA MAMBO YATUPASA KWANZA TUYAFAHAMU.

1.KWANZA KABISA.

١- كم مرَّةً ذكر الصيام في القرآن الكريم؟
1- MARA NGAPI IMETAJWA FUNGA NDANI YA QUR’ANI?

JAWABU LAKE.

ذكر الله الصيام في القرآن الكريم أربع عشرة مرَّة، سبْع مرَّات في سورة البقرة وحدها، ومرَّة في سورة النِّساء، ومرَّتين في سورة المائدة، ومرَّة في سورة مريم، ومرَّتين في سورة الأحزاب، ومرَّة في سورة المجَادَلة.

ALLAH ATAKUAFU AMEITAJA IBADA YA FUNGA NDANI YA QUR’ANI MARA 14.

MARA SABA KATIKA SURATUL BAQARA PEKEE.

NA MARA MOJA KATIKA SURATU NISAA.

MARA MOJA KATIKA SURATUL MAAIDAH.

MARA MOJA TENA KATIKA SURATU MARYAM.

NA MARA MOJA KATIKA SURATUL MUJAADALAH AU MUJADILAH.

JUMLA UNAPATA KUFAHAMU KWAMBA IBADA YA FUNGA IMETAJWA NDANI YA QUR AN MARA KUMI NA NNE (14)

2. JAMABO LA PILI.

TUFAHAMU KWA UFUPI SANA NENO RAMADHANI.

(رمضان )
Neno Ramadhani limejengwa kwa herufi 5 ambazo ni hizi zifuatazo.

الراء ، والميم ، والضاد، واﻷلف، والنون.
1-Raau. 2-Miimu, 3- Dhadu, 4-Alifu,  5-Nuuni.

Baadhi ya wanachuni wamelitafsiri neno hili kwa tafsiri mbalimbali.

KWA UFUPI.

 ﻗﻴﻞ ﺇﻧﻤﺎ ﺳﻤﻲ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﻷﻧﻪ ﻳﺮﻣﺾ ﺍﻟﺬﻧﻮﺏ ﺃﻱ ﻳﺤﺮﻗﻬﺎ ﺑﺎﻷﻋﻤﺎﻝ ﺍﻟﺼﺎﻟﺤﺔ.
Yaelezewa kwamba: Hakika imeitwa Ramadhani kwa sababu huyayusha madhambi kwa maana huyaunguza kutokana na amali njema.

رمضان إسم من الرمض أى ﺷِﺪَّﺓُ الحرِّ
Ramadhan ni jina lililo tokana na ramdhi kwa maana joto kali (Lenye kuunguza)

Ramadhani huunguza madhambi, Pia vilevile huyayusha mafuta mwilini na hua sababu ya  kumkinga mfungaji juu ya vitu vyoote vyenye madhara.

Asema Mtume

  “الصَّوْمُ جُنَّةٌ، فَإِذَا كَانَ أَحَدُكُمْ صَائِمًا فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَجْهَلْ، وَإِنِ اِمْرُؤٌ قَاتَلَهُ أَوْ شَاتَمَهُ فَلْيَقُلْ: إِنِّي صَائِمٌ”.

MAANA YAKE.
“Funga ni kinga, ikiwa mmoja wenu atakuwa amefunga, basi asiseme maneno machafu, na wala asifanye mambo ya kijinga,  na akitokea mtu akagombana nae, au akamtukana, aseme, “Mimi nimefunga”.

FUNGA HUMZUIA MFUNGAJI KUTOFANYA MADHAMBI.

FUNGA HUMKINGA MFUNGAJI KUTOKANA NA MARADHI MBALIMBALI…

KADHALIKA HUONDOA SUMU MBALIMBALI KATIKA MWILI WA MWANAADAMU

HII NI MAANA FUPI YA NENO RAMADHANI.

Tazama Video fupi ifuatayo ili uone faida ya funga kwa afya yako kutokana na maelezo ya watafiti kupitia chuo cha Mtume Muhammad ﷺ.

ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here