Home KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE : 9

KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE : 9

130
0

Aliyetoa salamu baada ya rakaa mbili katika sala ya adhuhuri, akakumbuka baada ya kusujudu sijda mbili baada ya salamu, je asali tena upya ama aendeleze sala alipofika ?Ama angalitoa salamu na hakusujudu sijda mbili ingalimjuzia kuinuka na kuendeleza sala alipofika. Dalili juu ya hilo ni hadithi ya Dhul-yadaini, kwani katika hadithi hiyo Mtume wa Allah –rehma za Allah na amani zimshukie- alitoa salamu baada ya rakaa mbili akaambiwa : Ewe Mtume wa Allah ! je umesahau ama sala imepuguzwa ? Akasema –rehma za Allah na amani zimshukie : « Yote hayo hayakuwa ». Dhul-yadaini akamwambia : Bali yamekuwa ewe Mtume wa Allah. Akasema –rehma za Allah na amani zimshukie- « Je ni kama asemavo Dhul-yadaini ? ». Akaambiwa : Ndiyo. Akaelekea kibla –rehma za Allah na amani zimshukie- akatimiza sala. Na Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- alizungumza katika sala hiyo kwa ajili ya udhuru huo na ili aulize kukhusu asemayo Dhul-yadaini. Watu wetu katika suala hili wanaona kuwa kuzungumza kwake huko Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- kulikuwa katika wakati ambao mazungumzo katika sala bado hayajaharamika. Ama kuzungumza baada ya kuharamishwa mazungumzo katika sala na baada ya kupokewa kutoka kwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- kauli yake : « Hakika sala yetu hii haifai ndani yake cho chote katika maneno ya kibinaadamu », mazungumzo hayo kwa hiyo ni yenye kutengua sala, na inawajibika sala isaliwe tena upya.Ama zile sijda mbili baada ya salamu hizo hazimo katika sala, na kwa hiyo kuzisujudu ni tendo la nje ya sala, ambalo sala hubatilika kwalo, na kuwajibika isaliwe tena upya. Na Allah anajua zaidi.

Previous articleKUSAHAU NA HUKUMU ZAKE : 10
Next articleKUSAHAU NA HUKUMU ZAKE : 8

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here