Home KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE : 2

KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE : 2

310
0

Wakati gani huwa sijda ya sahau, je ni kabla ya salamu ama baada yake? Na nini kauli yenu kukhusu mtu aliyesali akatoka katika sala yake kwa kutoa salamu, kisha akakumbuka kuwa sala yake haikutimia, je akimu sala mara nyengine ama atimize kilichobaki katika sala yake, ama nini afanye?Katika sujudu ya sahau kuna khilafu: ipo kauli kuwa ni kabla ya salamu na ipo kauli baada ya salamu, na kuna kauli ikiwa ni kwa ajili ya kupunguza basi ni kabla ya salamu na ikiwa ni kwa ajili ya kuzidisha basi ni baada ya salamu, na hii ndiyo kauli bora inayojumuisha baina ya riwaya tafauti. Na mwenye kusahau kabla hajatimiza sala yake akatoa salamu atimize sala yake na asujudu kwa ajili ya sahau yake. Na Allah anajua zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here