Nini kauli yenu kama mtu ameghafilika katika sala yake na hakujua rakaa ngapi amesali, bali ametanabahi yumo katika tashahudi ya mwisho, je sala yake inakuwa sahihi kwa hali hii ?Kwa vile hakuwa anajua alichosali, wala nini amefanya katika sala yake na nini hakufanya basi naarudie sala yake tangu mwanzo, kwani ibada inapasa zitekelezwe kwa yakini siyo kwa shaka, na yakini haipo katika hali kama hii. Na Allah anajua zaidi.