Home KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE : 1

KUSAHAU NA HUKUMU ZAKE : 1

273
0

Nini hukumu ya sujudu ya sahau na sujudu ya tilawa (kusoma aya ya yenye sijda) ?Hukumu ya sujudu ya sahau ni wajibu, kwa kuwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- aliisujudu aliposahau. Na kitendo kama hichi kutoka kwake –rehma za Allah na amani zimshukie- kinachukuliwa kuwa wajibu, kwasababu kinabainisha yaliyokuja kwa ujumla katika Qur’ani, na kila ambacho kinabainisha fardhi hukumu yake ni sawa na hukumu ya fardhi. Hili linapata nguvu kwa kauli ya Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- “Salini kama munionavo nikisali”. Halikadhalika hukumu ya sujudu ya tilawa kwa vile Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- aliidumisha, hata katika sala ya fardhi, kama ilivotolewa na Abu Daud A’Tayaalisi toka kwa Ibnu Abbaas –Allah awaridhie- kwamba Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- alisoma katika sala ya alfajiri surat A’Sajdah akasujudu katika sala. Linatosha hilo kuwa dalili juu ya kuwajibika kwa sujudu ya tilawa, na linapewa nguvu na kwamba Allah Subhaana Wataala amewagomba wale ambao hawasujudu kwa kauli Yake:ﭽ ﯢ ﯣ ﯤ ﯥ ﯦ ﯧ ﭼ الانشقاق: ٢١{Na wanapo somewa Qur’ani hawasujudu}Na Allah anajua zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here