Home VITABU WATU WA OMANI

WATU WA OMANI

485
0

MAELEZO MAFUPI KUHUSU HADITHI HII:

Mtume ﷺ alikua akiwatuma Masahaba wake kwa kuwapa barua kuelekea pande mbali mbali za ulimwengu; ili wafikishie vijiji na makabila mbali mbali wito wa tauhidi. Wafikishiwa hao wapo kati yao waliokua wakiitikia wito wake na kuingia katika Uisalmu, na miongoni mwao wapo waliokua wakikataa na kubakia katika Ukafiri wao huku wakiwa ni wenye kuishi kwa amani na Waisalmu, na miongoni mwao pia walikuepo waliokua wakikataa wito pamoja na kuupiga vita Uislamu.

Katika hadithi hii anasimulia Abu Barza – Allah amridhie – kua Mtume ﷺ alimtuma mtu miongoni mwa Masahaba wake kuelekea katika kijiji kimoja kati ya vijiji vya Waarabu; ili awalinganie kuingia katika dini ya Uislamu. Sahaba huyo alipata matusi, kipigo, pamoja na maudhi mengine kutoka kwa watu wa kijiji hicho, naye akarudi na kumsimulia Mtume ﷺ yaliyo mkuta, hapo Mtume ﷺ akasema kumwambia yeye: «Lau ungeliwaendea watu wa Omani, wasinge kutusi wala wasinge kupiga», yaani: lau wewe ungelikwenda kwa watu wa mji huo wa Omani kwaajili ya kuwalingania na kuwaita katika dini ya haki basi wasinge kutukana wala  wasenge kupiga, wala watu wake wasinge kutendea kama yale waliokutendea watu wa kijiji hicho ulichokwenda.

Maneno hayo yanamaanisha kua watu wa Omani ni watu wenye sifa ya elimu, utulivu, usafi wa nyoyo na tabia njema.

Na hadithi hii imejaa maana pana yenye kuonyesha sifa njema kutoka kwa Mtume ﷺ juu ya watu wa nchi hiyo, na maneno yake yanabainisha ubora wao, na kwamba wao ni watu wanao waheshimu anaewajia, wala hataona kwao isipokua kheri tupu.

Kama kwamba ndani ya hadithi hii pia kuna ubainisho wa ubora wa tabia za mtu ambae Waislamu wanasalimika kutokana na maudhi yake, na pia inaonyesha uvumilivu wa Masahaba katika kueneza Uislamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here