Home MAPISHI Mzinga Wa Nyuki (khaliyat Nakhal)

Mzinga Wa Nyuki (khaliyat Nakhal)

196
0

VINAVYOHITAJIKA NA      –       VIPIMO VYAKE

1. UNGA                                             VIKOMBE 3

2. SUKARI                                          VIJIKO 2 VYA SUPU

3. MAZIWA                                         KIKOMBE KIMOJA NA NUSU

4. YAI                                                MOJA

5. CHUMVI                                          KIASI

6. HAMIRA                                          KIJIKO CHA CHAI KIMOJA

7. MAFUTA                                          1/2 KIKOMBE

8. CHEESE                                          KIASI YA KUTOSHA YA KUWEKA NDANI YA VIDUARA.

9. ILIKI KIASI

10. MAJI KIASI

JINSI YA KUCHANGANYA NA KUANZA KUPIKA.

Chukua bakuli changanyana hamira,sukari na maji acha kwa muda wa dakika 5, ikianza kuumuka chukua unga mimina hamira na changanya na mafuta huku unachanganganya weka na yai halafu anza kuchanganya na maziwa huku unaponda.

Ukiwa tayari ufunike uumuke, Ukishaumuka chukua tray ya kuziweka, anza kutengeneza viduara vidogo vidogo ndani yake weka cheese mpaka umalize na kuwa na duara kubwa kama unavyoona katika picha hapo juu.

Choma kwa moto wa kiasi kwa juu na chini yake.

NZURI KWA JIONI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here