VINAVYOHITAJIKA NA VIPIMO VYAKE.
1. UNGA WA NGANO VIKOMBE VYA CHAI 4.
2. MAYAI MATATU
3. SIAGI NUSU KIKOMBE CHA CHAI.
4. HAMIRA KIJIKO KIMOJA CHA SUPU.
5. SUKARI VIJIKO VIWILI VYA SUPU.
6. MAZIWA KIKOMBE KIMOJA CHA CHAI
7. CHUMVI ROBO KIJIKO CHA CHAI
8. MAJI KIKOMBE KIMOJA
9.MAFUTA YA KUKAAINGIA
10. SUKARI NA ILIKI (YA KUCHOVYA AU KUPAKA) KIKOMBE KIMOJA NA ILIKI KIJIKO KIMOJA CHA SUPU.
JINSI YA KUANZA KUCHANGANYA NA KUANZA KUPIKA
- UNACHUKUA UNGA NA CHUMVI NA SUKARI UNACHANGANYA PAMOJA.
- CHUKUA SIAGI ILIYOYAYUKA , MAYAI NA MAZIWA CHANGANYA PAMOJA. (WEKA KATIKA KIBAKULI TOFAUTI)
- CHUKUA MAJI NA TIA HAMIRA CHANGANYA NA UIACHE KWA MUDA WA DAKIKA 5 MPAKA IUMUKE.
- IKISHA UMUKA HAMIRA CHANGANYA NA MAZIWA ULIYOYATENGENEZA KATIKA UTARATIBU HAPO JUU KATIKA NAMBA 2. (STEP NO 2)
- ANZA KUTIA UNGA KIDOGO KIDOGO HUKU UNAPONDA KATIKA ULE MCHANGANYIKO WA MAZIWA ULIOUFANYA KATIKA TARATIBU YA 4 (STEP NO 4) UNAENDELEA MPAKA UNAMALIZA KIASI CHA UNGA WOOTE ULIOKUWA NAO NA VILE VILE UTAENDELEA KUPONDA MPAKA UHAKIKISHE UNGA UKO MLAINI KAMA WA MAANDAZI.
- UKIMALIZA KUPONDA UACHE UNGA HUWO MLAINI KWA MDA WA NUSU SAA ILI UPATE MDA WA KUUMUKA VIZURI.
- UNGA UKISHA UMUKA UGAWANJE MAFUNGU NANE KWA AJILI YA KUSUKUMA NA KUFANYA MADUARA YA DONATI.
- CHUKUA GLASI KWA AJILI YA KUKATA MADUARA NA UTUMIE KIFUNIKO CHA CHUPA YA MAJI KWA AJILI YA KUTOBOA DUARA LA KATIKATI – UTAENDELEA KUFANYA HIVYO MPAKA UMALIZE KIWANGO CHA UNGA WOOTE ULIOKUWA NAWO.
- CHUKUA KARAI LA MAFUTA NA ANZA KUZIKAANGA HIZO DONUTI – WEKA MOTO WA KIASI, ILI ZISIJE KUUNGUA – ENDELEA MPAKA UMALIZE ZOOTE , ZITOE NA USUBIRI ZIPOE.
- CHUKUA SUKARI NA ILIKI ISAGE PAMOJA MPAKA IWE LAINI SANA KAMA UNGA HALAFU CHONYA HIZO DONUTI KWENYE SUKARI HIYO YENYE ILIKI.
- TAYARI KWA KULA
NZURI KWA KAHAWA.