Sh. Kahlan Al-Kharusi Naibu Mufti mkuu wa Omani.
Suali:
Katika ulimwengu huu uliyijaa matatizo,fazaa na fitina katika wakati kama huu wa eidulfitri; kuna walionyimika kupata furaha katika siku kama hii miongoni mwa watoto na wengineo tunahitaji kutoka kwako Sheikh nasaha kwa dola zenye maafa hayo na kwa waislamu kwa jumla ?.
Jawabu:
Kwanza bila shaka watu wanahuzunika kwa yanayotokea leo katika ulimwengu wa kiislamu, lakini lazima ukweli usemwe…
Na hapa nina baadhi ya nasaha ninazodhani zikipata nyoyo zenye kufahamu huenda mambo yakabadilika…
Kwanza nawaambia wenye elimu ya sheria, walinganizi na wenye kutoa mawaidha,’sitisheni fatwa za (umwagaji) damu… kwasababu harufu zake zimekuwa mbovu, zimetia pua mafua’.
Wanavyuoni wakubwa walikuwa na uoga wakuzungumzia mambo ya umwagaji damu na leo tunawaona wanaojidhania kuwa miongoni mwa wenye elimu nao si miongoni mwao na hawalijali jambo hili la umwagaji damu!
Wanajitokeza mpaka kwenye satellite channels wakitoa fatwa za kuhalalisha damu, na kuua roho kwa ujumla na bila khofu wala kufikiria matokeo yake..!!
Kwahiyo hatua ya kwanza ni kujiwaidhi nafsi yangu na ndugu zangu, na ni ombi kwa mashekhe wetu na wanavyuoni wetu na walinganizi.
‘Tunasema Allah abariki juhudi zenu, lakini sitisheni fatwa za umwagaji damu mnazohalilishia damu za waso na hatia… kwa visababu na taswira ambazo hazina uzito wowote kwa Allah na mtahesabiwa juu ya kila tone la damu..’ zisitisheni kwa kuhofia hasira za Allah na kwa kutaka radhi zake..!
Nasaha ya pili:
Ni kwa mahakimu na wenye uamuzi… sitisheneni hukumu za kuua watu kwani zinaleta hasira na kutaka kulipa kisasi, kwasababu hukmu zinatolewa kwa kushuku tu.. na kukosea katika kusamehe ni bora kuliko kukosea katika kuadhibu na rekebisheni matatizo ya jamii zenu kwa hikma, na uangalifu na kuona mbali, na kuwaongoza walio hadaika katika haya matukio ya kisasa katika vijana, na muwahudhurishe kwenye mambo ya ushikamano na kufahamu ufahamu wa sawa wa waliokita kwenye elimu, na mwache nafasi ya uhuru wa haki za watu,
Ama kubaki hali hivi ilivyo; bila shaka kutazidi kumwagika damu na utumiaji nguvu na hamna atakaye faidika kwa hali kama hizi..!
Na ninawaambia ndugu zangu ambao ni watu wa kawaida (sio katika viongozi), ‘msijiingize kwenye msiyo yajua.. kwani Allah (swt) anasema:
وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا
سورة الإسراء:36
(Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo, hakika masikio, na macho, na nyoyo- vyote hivyo vitasailiwa) suratul Israa : 36
Na amesema (swt):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ
{سورة الحجرات: 6}
(Enyi mlio amini akikujieni mpotovu na khabari yoyote ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua…) suratul Hujuraat: 6
Tuna haja sana ya kuthibitisha khabari! Ni haja ilioje tuliyo nayo ya kuwa wasaidizi wa kuzima fitna na sio kuiwasha!!
Leo ikija khabari tu utaona watu wote na hasa wajinga kabla ya walio elimika kila mmoja wao anafanya bidii kuwasha fitna na kuzidisha majeraha maumivu, pamoja na kuwa kunyamaza kwao ni bora bali ni wajibu! Kwasababu wanayoyatoa ima ni kwa kuwa yamewafikia kwa njia za mawasiliano au matangazo, au khabari ziso aminika, au haikuwafikia sura kamili ya tukio,mara wanakua wenye kuwasha kamba za madhehebu, makundi na ubaguzi,kwa maoni yao na kushiriki kwao kwa maandishi au maneno. kwahiyo wajibu wao nao ni kusimama kwenye mipaka yao na wasizidishe moto wa fitna bali wafanye juhudi kuuzima moto huo.
pia kwa mnasaba huu.. ni hili jambo la kuhubiri madhehebu,jambo ambalo linasababisha uadui na kuzusha bughdha, na kwanini yote haya??!!!
Kwani yatabadilika madhehebu baada ya karne zote hizi? Au itabadilisha nini wasipoingia mamia ya watu kwenye madhehebu fulani?? Haya ni mambo ya ulimwengu ni siku zinakuja kwa zamu… Allah (swt) amesema:
وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ
سورة آل عمران:140
(Na siku namna hizi tunawaletea watu..) suratu Aali Imran : 140
Ni wajibu tuyaache haya ya mivutano ya madhehebu na tushike ya kuleta umoja wa umma huu, na tukumbuke kuwa Allah amesema:
وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ
سورة فصلت : 33
(Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema na akasema Hakika mimi ni katika Waislamu?
{Suratu Fussilat:33}
Tuachane na yanayoleta fitna na ubaguzi na mivutano tutizame yenye kutuunganisha,, na tuyapalilie na kuyapanda katika wanaokua miongoni mwetu.
Sio leo utakuta mtu hata hakushika dini wala hajishuhulishi na lolote katika dini lakini inapofika kwenye mivutano ya kimadhehebu utaona wao ndio wa kwanza wanao ng’ang’ania jambo hilo…
Na tunawaambia hawa wenye kuzungumzia madhehebu haipasi kuwa hivi kwani madhehebu ni sababu ya kuleta rehma na wasaa na sio sababu ya kuleta uovu na uhasama… unaozalisha baada ya hapo kuitana mafasiki, makafiri n.k. katika kadhiya zenye wasaa kwenye dini na haya baadaye yanapelekea kuhalalisha damu na ulipuzi.
Pia tusimame kwenye kauli ya Allah (swt): 《 Na mbebaji habebi mzigo wa mwengine..》 suratu faatir :18
Dhambi ya mtu asibebeshwe mwengine, vipi auliwe asiyekuwa na hatia kwa sababu watu katika jamii yake wameua au wamefanya jinaya flani basi afanyiwe yeye ??!!
Tuamke waislamu na yote wanayo tutakia maadui wa uislamu na waislamu na maadui wa amani!
Imetaarishwa na: Rashid alshukery.
Mkono kwa mkono hadi