Home All TIBA YA KIISLAMU

TIBA YA KIISLAMU

508
0
Accordion Content

Published By Said Al Habsy

TIBA YA KIISLAMU: SEHEMU YA KWANZA-UTANGULIZI
TIBA YA KIISLAMU.

Baada ya Kumshukuru Allah kwa utukufu wake. Sala na Salamu zimshukie Mtume S.A.W. Pamoja na Ahli zake na Sahaba zake Kiramu na matabiina wote na wenye kuufuata Uislamu kwa wema mpaka siku ya malipo. Baada ya hayo: Tunapenda kuandika nakala za fani ya tiba ambazo zitasaidia kielimu na maarifa juu ya mtu anapokuwa kapatwa na mtihani wa maradhi ili aweze kujisaidia na baadhi ya maarifa ya kitiba ambayo yanayo tokana na mafunzo ya Qur-an na Mtume S.A.W na wanazuoni khususan walozama na fani hii ya tiba.

Tunamuomba Allah atupe taufik katika kazi hii na najuwa wapo Maulamaa wengi wanaofahamu elimu hii, Ila mimi nitaeleza kile kichache nikijuwacho ili iwe sadaka yangu na wazee wangu ili kiwafae ndugu zangu kwa mashakili tulokuwa nayo ya Mitihani ya Maradhi na Shida za Kidunia. Leo nitasimama hapa In-Sha Allah nitaendelea pole pole mpaka tutapofika.

Ndugu yenu Nassor Haroub Nassor Al-Jabri.

Published By Said Al Habsy

TIBA YA KIISLAMU: SEHEMU YA PILI
TIBA YA KIISLAMU.


Tukiendelea na maelezo ya tiba ya kiislamu. Hapana budi kujuwa aina za Maradhi. Aina za Maradhi zipo aina mbili.

(1) Maradhi ya Nyoyo.
(2) Maradhi ya Mwili.

Ama maradhi ya moyo nayo yapo aina mbili.

Aina ya kwanza (1). Maradhi ya Shaka na Matamanio na mfano kama hayo yanompelekea mtu kuwa mbaya. Kama alivyosema Allah katika Qur-an Suratul Al-baqara Aya (10).

فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ فَزَادَهُمْ اللَّهُ مَرَضًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ

Tafsiri Ya Aya.
( Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo)

Ama Maradhi ya Matamanio (2) kama Allah alivyosema katika Suratul Al-Ahzab aya (32)
يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

Tafsiri Ya Aya:
Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema.

Ama Sehemu ya pili ya Maradhi ni Kimwili (2). Nayo yapo aina Mbili

Aina ya kwanza (1) Aliyojaalia Allah kimaumbile kwa kila mtu kama njaa au kiu au joto au baridi au tabu dawa yake ni kuondoka kwa kujisaidia mwenyewe au na mtu haitakikani mganga maalum.

Aina ya pili ya Maradhi ya Kimwili (2) Yaliyomo ndani mwilini kama, cancer au kidney failure na mfano wa hayo.

Ama aina ya pili ya maradhi ya mwili, ni ya nje ya mwili kama kupooza viungo vya mwili au majaraha au kuvunjika kiungo.Maradhi aina hii inahitajika twabibu anaelewa kuyatibu maradhi hayo kwa kutumia elimu na maarifa alonayo pamoja na dawa zitazokuwa muwafaka na maradhi ya mgonjwa na zana zitazosaidia wepesi wa tiba.

Kwa leo nasimama hapa Inshaallahu tutaendelea Sehemu ya tatu Mara nyengine. Wallahu Aalamu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here