Home All Nizwa Mji Mkuu Wa Kiislamu Kwa Utamaduni Wake – 2015

Nizwa Mji Mkuu Wa Kiislamu Kwa Utamaduni Wake – 2015

430
0

Nizwa: Wilaya ya Nizwa katika Mkoa wa Al Dakhiliyah nchini Oman ni moja ya vituo au mji maarufu sana na unajulikana kwa umuhimu wake kwa ajili ya sayansi na wasomi (science and scholars) katika Oman.

Misikiti yake ni maarufu na imetoa wanavyuoni wengi au wasomi mbali mbali waliokuwa wamemaliza elimu katika fani tofauti tofauti kama vile wanafikra, waandishi na wanasheria (Fuqaha’a).

Wasomi hawo walichukua majukumu makubwa katika kuuendeleza Uislamu na maarifa katika nchi mbalimbali duniani.

Mji huu wa Nizwa, hapo zamani ulipewa jina jengine na kuitwa “Baydat AL Islamu” kwa sababu wengi wa wanasayansi na wanavyuoni walisomea hapo na kumaliza masomo yao ya daraja za juu, kama vile Imamu Imamu Jabir Bin Zaid (R.A) ambaye alizaliwa,Farq katika mji huwo wa Nizwa.

Pia, AL Bashir AL Nizwani ambaye aliechukua jukumu la kuendeleza na kuleta maarifa kutoka Al-Basra katika Iraq na Oman na wanasayansi wengineo walio andika vitabu vingi katika utamaduni wa Kiislamu na masomo mengineyo.

Nizwa pia imechangia jukumu muhimu katika mafanikio ya harakati za kisayansi  na kujenga ustaarabu mzuri wa Kiislamu katika Oman. Katika historia ya Oman, Nizwa, ambayo ilikuwa mji mkuu wa Oman katika nyakati za zamani na makao makuu ya serikali kwa kipindi cha zaidi ya miaka 1,000.

Ngome ya Nizwa katika (picha juu) ni moja ya vivutio vya utalii maarufu katika Oman kutokana na ukweli kwamba ni mfano wa ajabu wa kale usanifu wa Oman ambayo inatoa kielelezo cha namna ya watu wa Oman walivyoishi katika nyakati za zamani.

Nizwa ngome ni ya kipekee miongoni mwa ngome nyingine katika Oman kutokana na sura yake ya mviringo wa minara yake kuu ambayo pia hutokea kwa kuwa kubwa kwa mnara katika ngome nyenginezo katika Oman. Nizwa ngome ina visima saba, idadi ya magereza, na upande wa mashtaka chini.

Mji wa Nizwa ulichaguliwa kama vile Mji mkuu wa Utamaduni wa Islamic mwaka huu 2015 na chama cha Educational, Scientific and Cultural Organisation (ISECO) kwa nguvu ya kihistoria yake kwa miaka mingi iliyopita.

 

Video hapo chini ni Msikiti mkuu wa Sultan Qaboos Bin Said, uliofunguliwa hivi karibuni katika mji wa Nizwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here