Home All Msikiti Mkuu Wa Sultan Qaboos

Msikiti Mkuu Wa Sultan Qaboos

610
0

Msikiti wa Sultan Qaboos (Sultan Qaboos Grand Mosque) kama unavyojulikana ni msikiti mkubwa sana katika Oman na pia ni kituo cha uenezaji na mafunzo ya dini ya kiislam,fasihi na utamaduni. Maagizo ya ujenzi wa msikiti huu mkubwa katika Oman yalitolewa na mwenyewe mfalme Sultan Qaboos bin Said katika mwaka wa 1412 / 1992. Baada ya kuwa na mashindano ya kimataifa ya kuchagua mpango bora (best design) ya msikiti huu wa Sultan Qaboos katika mwaka wa 1413/1993,ujenzi ulichukua miaka sita na msikiti ulizinduliwa rasmi May,2001.

Msikiti Mkuu upo katika mji mkuu wa Muscat, Wilaya ya Baushar, Ghubra Kusini, kama km 10 kutoka Seeb International Airport. Kuba (dome) yake kubwa ya rangi ya dhahabu iliyopakwa au kuchovywa na ina mapambo kadhaa mashuhuri, Msikiti huo unaonekana katika barabara kuu na kuvutia wageni wake waumini kwa moyo wa Uislam kama dini,sayansi na ustaarabu. Msikiti huu mkuu unaonyesha jukumu lake na chanzo cha maarifa katika ulimwengu wa Kiislamu katika mambo ya kisayansi ktk dini.

Ukubwa wa ardhi hii ya msikiti huu mkuu ikiwa ni pamoja na maeneo yaliojengwa kikamilifu na sehemu nyenginezo kama za bustani na parking, eneo loote ni mita za mraba 416,000, ambayo mita za mraba 40,000 ni eneo la msikiti wenyewe, ukumbi wa msikiti una uwezo wa kuingiza waja 6,600 na ina kuba katikati ambayo imenyanyuliwa mita 50 juu ya sakafu. maeneo yoote ya kusalia yana uwezo ya zaidi ya waja 20,000. Ukumbi wa wanawake wa kusalia una uwezo wa zaidi ya 750 waja. Kwa sehemu za nje zilizowazi ina uwezo wakuingiza waja zaidi ya 8,000.

 

Kuna sehemu 8 za kutawadhia pembezoni ya msikiti. Nje ya msikiti kuna minara mitano mizuri ya kuvutia,mnara wa katikati ni mrefu zaidi ya mita 90. Minara mitano inawakilisha nguzo tano za Uislamu.

Njia kuu ya kuingilia msikitini ni kutoka kusini.Magharibi mwa Qibla ukuta unatambulika kwa inayojitokeza mihrab yake na kuna milango miwili rasmi. Kwa upande wa kaskazini, mlango wa Imamu unaelekea na kukuongoza moja kwa moja kwa mimbari na upande wa kusini ni mlango Mkuu wake Mfalme mwenyewe.

Msikiti pia una sehemu ya Information Center ya Kiislamu ambayo hutoa habari na mafundisho ya Uislamu na kwa lugha kadhaaKituo hicho kina hudumia wanaojiunga na Uislamu na kwa wasiokuwa Waislamu pia.

Kuta za ndani ya msikiti katika ukumbi mkuu ni mawe (marble) meupe na za rangi ya kijivu yaliopambwa kwa kazi ya kukata na kuchonga marble. holi la msikitini liko wazi kabisa na kuna nguzo nne kubwa zilizo beba au kuzuiya kuba (Dome) hiyo iliyo katikati baina ya nguzo hizo.

wakati milango mengine kubadilika paneli za viooo kusisitiza amani na umoja wa nafasi hiyo ya ukubwa uliouwekwa hasa kwa kusalia.

Yaliyoandikwa kwenye milango ni embellishments ya Kiislamu zipo aya za Qur’ani katika maandishi ya Thuluth, wakati milango mengine kubadilika paneli za viooo kusisitiza amani na umoja wa nafasi hiyo ya ukubwa uliouwekwa hasa kwa kusalia. Uteuzi wa mchoro katika ukumbi wa msikiti huonyesha mageuzi ya aina mbalimbali ya mapambo ya usanifu na utamaduni ambayo umetembea utajiri wake kutoka Hispania na Asia ya Kati.

Ukumbi wa Msikiti,sakafu yake imewekwa kipande kimoja tu cha zulia la Kiajemi linajumuisha mafundo milioni 1,700, limefunika eneo la mita za mraba 4,200, na zulia hilo lina uzito wa tani 21. Ilichukua miaka minne ya ktengeneza zulia hilo. Miezi kumi na tano ilitumika katika kukamilisha miundo (Finalising Design), kuandaa vifaa vya Weaving na warsha, miezi 27 katika ufumaji na miezi mitano ya kumaliza, usafishaji na kusawazishwa na kuunganisha vipande 58. hivi vipande viliunganishwa kisha na kuwekwa ndani ya ukumbi mkuu wa msikiti na wafumaji maalum. zulia hili ni zulia kubwa duniani.

Wasiokuwa Waislamu wanaruhusiwa kutembelea msikiti kila siku, isipokuwa siku ya Ijumaa, kutoka 08:30 hadi 11:00. Wageni huelezwa na kuvaa mavazi ya kujisitiri kabla kupita sehemu za ibada. Wanawake pia wanatakiwa kufunika nywele zao.

Gallery is offline
Click to restore your gallery or contact us at support@cincopa.com

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here