Home All Mikono Katika Sala

Mikono Katika Sala

784
0

Published By Said Al Habsy

Assalaamu alaykum warahmatullahi taala wabarakaatuhu ndugu zangu, baada ya salamu rehma na amani zimfikie Bwana wetu mpenzi Nabii Muhammad na Swahaba zake watukufu na wote waliofuata nyayo zao hadi siku ya kiama.

Sina budi kumshukuru Allah mtukufu kwa kuniwafikisha katika moja ya mambo ya kheri nikaweza kukifanyia tarjuma kijitabu hiki.

Baada ya kukisoma kitabu hiki ambacho kimeandikwa na Sheikh Ahmad bin Soud Assiyaabiy na kuona kilichomo ndani yake na faida zilizomo, nikaonelea ipo haja ya kukifanyia tarjuma kwa lugha ya Kiswahili ili na wengine wasioelewa lugha ya kiarabu na wao wapate kufaidika, hasa Maibadhi wapate kujua kwa nini wao hawainui na hawafungi mikono na vile vile ndugu zetu wasio Maibadhi wajue angalau kwa ufupi sababu zilizowafanya ndugu zao Maibadhi wasiinue na wasifunge mikono wakati wa kusali.

Pamoja na kuwa kitabu chenyewe ni kidogo kwa kurasa kama alivyosema mwenyewe mtunzi wa kitabu hicho, lakini faida iliyomo ni kubwa sana, kwani uzuri wa kitabu hautizamwi wingi wa kurasa bali hutizamwa faida iliyomo ndani yake.

Kazi niliyoifanya ni :

1- kutarjumu kitabu chote (Teremsha Kitabu Kamili Kwa PDF)

2- kuhakikisha usahihi wa maneno aliyonukuu Sheikh kwa kurudia na kuangalia kwenye asli ya vitabu alivyovitaja

3- kuna baadhi ya maneno yamerukwa ima ameyawacha makusudi au yamesahauliwa wakati wa kuchapishwa kitabu, kutokana na umuhimu wake mimi nimeyaingiza ingawa ni machache mno na nimeyaweka ndani ya mabano [ … ] na kuelezea na atakaeangalia kitabu cha kiarabu na tarjuma hii anaweza kuona jambo hilo kwa hivyo namuomba radhi Sheikh wangu juu ya hilo na nataraji amenisamehe

4- kufanyia takhriji ya kauli hizo kwa kutaja kitabu, jina la Mtunzi Mujallad, juzuu na ukurasa

5- kufanya takhriji ya wapokezi wa hadithi aliowataja Sheikh ambao wamesababisha hadithi walizozipokea kuwa dhaifu au kuwa na illa kwa kutaja jina la kitabu, Mujallad au Juzuu na ukurasa

6- Takhriji nyingi nimetumia disc ya Almaktabatu-shshamilah na nyengine nimerudia katika vitabu vyenyewe na kutaja kimechapishwa na nani, mwaka kilochapishwa n.k.

Natarajia kuwa tarjuma yangu hii itaeleweka kirahisi kwa hivyo kama nimepatia basi hiyo ni tawfiki kutoka kwa Allah na kama nimekosea makosa hayo yatakuwa yametokea kwangu.

Tunamuomba Allah atuwafikishe katika kila jambo analoliridhia na analolipenda.

 

Published By Said Al Habsy

Zimekhitilafiana madhehebu za Kiislamu juu ya sifa na namna ya kuisali swala .. na khilafu kubwa iliyomo na yenye mjadala baina ya madhehebu hayo ni mambo mawili kuinua na kufunga, yaani kuinua mikono na kuifunga ndani ya swala, na kufunga maana yake ni kuweka mkono wa kulia juu ya kushoto ndani ya swala, na huenda ikawa wamedanganyika au wanahadaika baadhi ya watu katika Maibadhi kutokana na hadithi zilizopokewa kuhusu mambo hayo mawili, ikawa wao wanafuata madhehebu nyengine ambazo zinainua na kufunga mikono, na haikupelekea wao kufuata hivyo isipokuwa kutokujua kwao kuwa hadithi zilizopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.w.a) zipo zilo sahihi, na miongoni mwao ni dhaifu na nyengine ni za kutungwa, na wala hawakujipa taabu nafsi zao katika kuzichunguza hadithi zilizopokewa kuhusu kuinua na kufunga mikono ndani ya swala, ili iwabainikie udhaifu wake, bali jambo hilo halihitaji kazi kubwa kwani asli – ya vitabu- na marejeo yapo, tena yamejaa na elimu ya hadithi ina nguzo na misingi, kwayo hujulikana hadithi sahihi na hadithi dhaifu na ya kutungwa, na kuinasibisha hadithi iliyotungwa kwa Bwana Mtume (s.w.a) ni katika kupitilia mipaka na kwa hakika wanavyuoni wa elimu ya hadithi wameweka istilahi juu ya hayo.

Na hakika wameniomba baadhi ya ndugu zangu wema na kunitaka niandike kitabu, nichambue ndani yake hadithi zilizopokewa kuhusu kuinua na kufunga (mikono katika swala), hivyo ninaweka kitabu hiki ni kidogo kwa kurasa na ni ufupisho katika maana na mjengo, ndani yake kuna milango miwili na hitimisho:

 

Published By Said Al Habsy

MLANGO WA KWANZA:

Rai ya Maibadhi kuhusu suala la kuinua na kufunga mikono katika swala, na nimebainisha rai ya Maibadhi na dalili zao juu ya kutofaa kufanya hayo ndani ya swala.

 

 

MLANGO WA PILI:

Umegawika sehemu mbili:

– Sehemu ya kwanza: uchambuzi wa hadithi za kuinua (mikono)

– Sehemu ya pili : uchambuzi wa hadithi za kufunga (mikono)

Hitimisho:


Nimebainisha ndani yake jinsi Maibadhi walivyoshikamana na sunna sahihi, na kuziwacha ziso sahihi.

Na nimejilazimisha kuzichambua hadithi zilizomo katika kitabu cha “منتقى الأخبار” ambacho amekisherehesha mwanachuoni Ashshawkaniy na kukiita “نيل الأوطار ” na kitabu .. “بلوغ المرام” ambacho amekisherehesha mwanachuoni Asswan-a’niy na kukiita “سبل السلام”.

Na kwa hakika hadithi hizi –yaani ziliomo ndani ya vitabu viwili hivyo- ndizo zinazotegemewa na wale wanaosema kuinua na kufunga (mikono) basi zikiporomoka udalili wake baada ya kuzichambua, hapana shaka yoyote hadithi nyingine zitaporomoka kuzitolea dalili katika mambo hayo mawili.

Published By Said Al Habsy

RAI YA MAIBADHI KATIKA KUNYANYUA NA KUFUNGA MIKONO

Maibadhi wanaona kuinua na kufunga mikono katika swala hakusihi kwa sababu hivyo ni vitendo vilivyozidi katika swala, na wakahesabu kufanya hivyo ni mchezo katika swala na hoja zao juu ya hayo ni:-

KWANZA

Hadithi iliyopokewa na Imam Arrabii katika Musnad yake kutoka kwa Abi Ubayda kutoka kwa Jabir bin zayd kutoka kwa Ibnu Abbas (r.a) kutoka kwa Bwana Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) amesema:

“كَأَنِّي بِقَوْمٍ يَأْتُوْنَ مِنْ بَعْدِي يَرْفَعُوْنَ أَيْدِيَهُمْ فِي الصَّلاَةِ كَأَنَّهَا أَذْنَابُ خَيْلٍ شُمُسٍ” .

TAFSIRI:

(Kama kwamba kuna watu watakuja baada yangu wanainua mikono yao katika swala kama mikia ya farasi walioasi). 1

Kwa hivyo hadithi hii inaonyesha kuwa suala la kuinua mikono limezuka baada ya kufa Bwana Mtume (s.a.w). Kutokana na maneno yake (Kama kwamba kuna watu watakuja baada yangu).

Kwa maana hiyo Maibadhi wanasema kuwa hadithi za kufunga mikono zitakuwa ni dhaifu au zimetugwa, amesema Al-Imam Alqutb Muhammad bni Yussuf Atfayyish: “Na jambo lilokuwa wazi na lilonidhihirikia mimi kuwa madhehebu nyengine –wenye madhehebu manne – wameweka hadithi za kuitikia amin na kuinua mikono na (kudai) kuwa Bwana Mtume (s.a.w) alifanya hivyo hadi kufa kwake na wakawaekea maswahaba baada yake katika njia inayokubalika kwao wao”.

Na mimi ninasema kuwa hata kwao wao hadithi hizo haziwezi kukubalika lau kama zitafanyiwa uchambuzi wa kina wa kielimu kwa kutumia misingi ya elimu ya hadithi ambayo imewekwa kwa ajili ya kuzitambua hadithi zilizo sahihi na dhaifu.

______________________

1 – الجامع الصحيح مسند الإمام الربيع بن حبيب ابن عمر الأزدي البصري ، إعداد سعود بن عبدالله الوهيبي ، مكتبة مسقط ،1414هـ 1994م، ج1/58 ،الحديث 213

Published By Said Al Habsy

PILI

Hadithi ya yule mtu aliyekosea kusali, na imepokewa katika njia mbili:

1-Kwa njia ya Abi Hurayrah (r.a) ambayo imekuja kwa ujumla, na hii ndiyo naswi ya hadithi yenyewe ambayo ameipokea Imam Muslim:

عَنْ أَبِى هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ -صلى الله عليه وسلم- دَخَلَ الْمَسْجِدَ فَدَخَلَ رَجُلٌ فَصَلَّى ثُمَّ جَاءَ فَسَلَّمَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ -صلى الله عليه وسلم- فَرَدَّ رَسُولُ اللَّهِ -صلى الله عليه وسلم- السَّلاَمَ قَالَ « ارْجِعْ فَصَلِّ فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ ». فَرَجَعَ الرَّجُلُ فَصَلَّى كَمَا كَانَ صَلَّى ثُمَّ جَاءَ إِلَى النَّبِىِّ -صلى الله عليه وسلم- فَسَلَّمَ عَلَيْهِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ -صلى الله عليه وسلم- « وَعَلَيْكَ السَّلاَمُ » . ثُمَّ قَالَ

« ارْجِعْ فَصَلِّ فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ ». حَتَّى فَعَلَ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ ، فَقَالَ الرَّجُلُ وَالَّذِى بَعَثَكَ بِالْحَقِّ مَا أُحْسِنُ غَيْرَ هَذَا عَلِّمْنِى. قَالَ « إِذَا قُمْتَ إِلَى الصَّلاَةِ فَكَبِّرْ ثُمَّ اقْرَأْ مَا تَيَسَّرَ مَعَكَ مِنَ الْقُرْآنِ ثُمَّ ارْكَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ رَاكِعًا ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَعْتَدِلَ قَائِمًا ثُمَّ اسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا ثُمَّ افْعَلْ ذَلِكَ فِى صَلاَتِكَ كُلِّهَا »2.

___________________________

2-صحيح مسلم شرح الإمام النووي ـ المجلد 2/ج4 /ص107 ـ 106 ـ دار الفكري للطباعة والنشر والتوزيع ـ 1401 هـ / 1981

_________________________

TAFSIRI:

Kutoka kwa Abi Hurayrah (r.a)

kuwa: “Hakika Mjumbe wa Allah (s.a.w) aliingia msikitini, na punde akaingia mtu akaja akasali kisha (alipomaliza) akaja kumsalimia Bwana Mtume (s.a.w), na Bwana Mtume akamrudishia salamu na akamwambia rudi ukasali kwa hakika wewe hukusali, yule mtu akarudia kusali kama alivyosali mwanzo, kisha akaja kwa Bwana Mtume (s.a.w) kumsalimia, Bwana Mtume akamjibu salam yake, na akamwambia rudi ukasali kwani wewe hujasali, mpaka akafanya hivyo mara tatu, yule mtu akasema kumwambia Bwana Mtume (s.a.w): “Naapa kwa yule ambaye amekutuma wewe kwa haki, hakika siwezi kusali vizuri zaidi ya hivi nilivyofanya, (basi) nielimishe”, akasema (s.a.w) “Utaposimama kwa ajili ya swala piga takbira, kisha soma chochote kidogo katika Qur-ani, kisha utarukuu hadi utulie katika rukuu, kisha utainuka hadi usimame sawa sawa, kisha utasujudu hadi utulie sawa sawa katika sijda, kisha utainuka hadi utulie katika kukaa kwako, utafanya hivyo katika swala yako yote”.

2-Kwa njia ya Rifaa bnu Raafi-i na katika hadithi hii imekuja kwa ufafanuzi zaidi na hii ndio hadithi yenyewe ameipokea Abu Daud:

“Kuna mtu aliingia msikitini akaelezea kama alivyoelezea Abu Hurayrah … akasema Mjumbe wa Allah (s.a.w): “Kwa hakika haitimii swala ya mtu yeyote mpaka atawadhe inavyotakikana, kisha alete takbira amshukuru Allah mtukufu na amsifu, kisha asome chochote anachokitaka katika Qur-ani, kisha aseme Allahu akbar, halafu arukuu hadi viungo vyake vitulie, kisha atasema samiallahu liman hamidah, mpaka asimame sawa sawa kisha atasema Allahu akbar, kisha atasujudu hadi viungo vyake vitulie, kisha atasema Allahu akbar, kisha atainuka na kukaa sawa sawa, kisha atasema Allahu akbar, kisha atasujudu mpaka viungo vyake vitulie, kisha atainua kichwa chake na kupiga takbira, basi ikiwa atafanya hivyo swala yake itatimia”.3

Na katika riwaya nyengine katika upokezi wa Abi Daud mwisho wake amesema: “Atakaa sawa sawa kwa kukalia makalio yake na kuweka sawa mgongo wake, -akaielezea swala namna hiyo katika rakaa zote nne hadi kumaliza-, na kusema: Haitimii swala ya mmoja wenu mpaka afanye kama hivyo”.4

Amesema mwanachuoni Assubkiy kwenye sherhe ya sunan Abi Daud: “Kauli yake akaielezea swala namna hiyo …hadi mwisho” yaani amesema Rifaa akaielezea Bwana Mtume (s.a.w) namna hiyo iliyotajwa, mpaka akaelezea rakaa zote nne hadi mwisho wa swala, na Bwana Mtume (s.a.w) baada ya kumaliza kuielezea hiyo swala akasema haitimii swala ya mmoja wenu mpaka afanye kama nilivyoelezea.

Kwa hakika hadithi hii imeweka wazi lililo wajib na sunna na imekusanya namna ya kuisali swala yenyewe, na wala hamkutajwa ndani yake kuinua mikono wala kuifunga, kutokana na hayo ndiyo washereheshaji wa hadithi hii wamesema: “Yaliyotajwa katika hadithi hii ndiyo yaliyo ya wajibu na yasiyotajwa si wajibu”, na hivi ndivyo alivyosema mtunzi wa kitabu cha Subulu ssalaam:

” وَاعْلَمْ ” أَنَّ هَذَا حَدِيثٌ جَلِيلٌ تَكَرَّرَ مِنَ العُلَمَاءِ الاِسْتِدْلاَل بِهِ عَلَى وُجُوبِ كُلِّ مَا ذُكِرَ فِيهِ وَعَدَمِ وُجُوبِ كُلِّ مَا لَمْ يُذْكَرْ فِيهِ أَمَّا الاِسْتِدْلاَلُ عَلَى أَنَّ كُلَّ مَا ذُكِرَ فِيهِ وَاجِبٌ ]فَلأَنَّهُ سَاقَهُ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِلَفْظِ الأَمْرِ بَعْدَ قَوْلِهِ : ” لَنْ تَتِمَّ الصَّلاَةُ إِلاَّ بِمَا ذُكِرَ فِيهِ ” وَأَمَّا الاِسْتِدْلاَلُ بِأَنَّ كُلَّ مَا لَمْ يُذْكَرْ فِيهِ لاَ يَجِبُ[[5 فَلأَنَّ الْمَقَامَ مَقَامُ تَعْلِيمِ الْوَاجِبَاتِ فِي الصَّلاَةِ فَلَوْ تُرِكَ ذِكْرُ بَعْضِ مَا يَجِبُ لَكَانَ فِيهِ تَأْخِيرُ الْبَيَانِ عَنْ وَقْتِ الْحَاجَةِ وَهُوَ لاَ يَجُوزُ بِالإِجْمَاعِ “.
_____________________________________________________

[3] -Abu Daud Hadithi nambari:857 – juzuu 1/ 288 المكتبة الشاملة ط 3 –

[4]-Abu Daud Hadithi nambari: – 858 juzuu 1/ 288 المكتبة الشاملة ط 3 –

[5] – Maneno niliyoyatia katika mabano [… ] Shekh ameyasahau kuyanukuu.

_____________________________________

TAFSIRI:

“Na elewa ya kuwa hadithi hii ni tukufu sana wameirudiarudia sana wanavyuoni katika kuitolea dalili juu ya kuwajibika kila kilichotajwa, na kutowajibika kila kisichotajwa ndani yake.

Ama udalili wa kuwajibika kila kilichotajwa ni kwa sababu Bwana Mtume (s.a.w) ameielezea kwa lafdhi ya kuamrisha baada ya kauli yake ” لَنْ تَتِمَّ الصَّلاَةُ إلاَّ بِمَا ذُكِرَ فِيهِ “. Ama udalili wa kuwa kila kisichotajwa ndani yake si wajibu kwa sababu pahala hapo ni pakufundisha mambo ya wajibu katika swala, na lau kama ingaliwachwa kuelezewa baadhi ya mambo yaliyo ya wajibu ingalipatikana kucheleweshwa kubainisha mambo wakati unaohitajika, na kufanya hivyo haijuzu kwa kauli ya ijmaa”.6

Na wewe unaona ya kuwa hadithi hii tukufu haijagusia lolote juu ya suala la kuinua na kufunga mikono, na akitokea msemaji akasema: “Kwa hakika kuinua na kufunga mikono ni vitendo viwili maarufu katika swala wala havihitajii kuelezewa katika hadithi hiyo”.

Jawabu juu hilo ni:

Wale wanaokubalisha kuinua na kufunga mikono wamepokea kutoka kwa Ibni Masoud (r.a) kuwa aliweka mkono wake wa kushoto juu ya kulia (katika swala), Bwana Mtume (s.a.w) alipomuona akauchukua mkono wake wa kulia na kuuweka juu ya kushoto, basi ikiwa Ibnu Masoud (r.a) naye ni miongoni mwa maswahaba wakubwa na mwanachuoni wao ambaye Mjumbe wa Allah amemsifu kwa kusema (amejaa elimu tokea juu ya utosi wake hadi chini ya nyayo zake) naye amekosea kuweka mikono yake kwa mujibu ya walivyopokea, basi vipi kwa huyu bedui ambaye hakuweza kuisali swala kwa usahihi kwa mara nyingi, jee? Hahitajii kuwekewa wazi suala la kufunga na kuinua mikono katika swala kama ingalikuwa jambo hili lina usahihi ?.

 

Published By Said Al Habsy

MLANGO WA KWANZA – 3.Na simamisheni swala

Tatu


Hakika swala Allah ametuamrisha kwa ujumla katika kitabu chake kitukufu amesema: 7{… وَأَقِيمُوْا الصَّلاَةَ }.

Tafsiri yake: {Na simamisheni swala}.

Na zimekuja baadhi ya aya zinazoashiria nyakati za swala kama kauli yake Allah aliposema:

8{ أَقِمِ الصَّلاَةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَى غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا }

Tafsiri yake:

{Na simamisha swala jua linapopinduka (likenda magharibi) mpaka giza la usiku; na (msiache) Qur-ani ya (swala) ya alfajiri. Hakika (kusoma) Qur-ani katika (kusali swala ya) alfajiri kunahudhuriwa (na Malaika)}

_______________________

6- Subula ssalaam -J2/70 .المكتبة الشاملة ط 3

7- البقرة – 43

8- ا إسراء – 78

_____________________

Ama uchambuzi wa swala yenyewe na namna ya kuisali pamoja na takbira na tahlili na tahmidi na tasbihi na rukuu na sijda na kisimamo na kikao na idadi ya rakaa na kuweka wakati wa swala na swala ya safari kutokana na swala ya hadhari, yote hayo yamefafanuliwa na sunna tukufu, basi kwa nini wakhitilafiane waislamu katika suala la kuinua na kufunga mikono, wala wasikhitilafiane katika mambo mengine yaliyotajwa, pamoja na kuwa kufunga na kuinua mikono ni vitendo vilivyokuwa wazi wazi katika swala, na mjumbe wa Allah na maswahaba zake walikuwa ni wenye kusali sana, juu ya yote hayo hao wanaokubalisha kuinua na kufunga mikono wamesema wazi wazi ya kuwa mwenye kusali bila ya kuinua au kufunga mikono swala yake itakuwa imetimia, basi kutokana na hayo Maibadhi wamefuata ile kauli waliyokubaliana umma (muttafaq) na wakaiacha ile yenye khilafu ndani yake, amesema Imam Annawawiy katika sherhe ya Imam Muslim:

(وأجمعوا على أنه لا يجب شيء من الرفع )

Tafsiri yake:

“Wamekubaliana ya kwamba hakuna wajibu wowote katika kuinua (mikono)”.

Published By Said Al Habsy

MLANGO WA KWANZA – 4.Salini kama mnavyoniona ninasali

Nne:-

Amepokea Imam Ahmad na Albukhary kwa njia ya Malik bnul Huwayrith (r.a) kuwa Mjumbe wa allah rehma na amani ziwe juu yake amesema: ” Salini kama mnavyoniona ninasali”.

Na amri hii inatoka kwake Mjumbe wa Allah na ni ya wajib madamu hakuna dalili ya kuondosha uwajibu huo, na lau kama ingalikuwa kuinua na kufunga mikono ilikuwemo katika swala yake Bwana Mtume (s.a.w) bila shaka yangalikuwa mambo hayo ni wajibu, hivyo kwa nini wanaokubalisha jambo hilo wanasema (kuinua na kufunga mikono) ni sunna na wengine wanasema inapandelewa tu, jee ? Hii si dalili ya kuonyesha kutokusihi jambo hilo.

_____________________________________

[9] – (mujallad ya 2 juuzuu 4/95 chapa ya Daarul-fikriy 1981/1401- )

-Na akasema tena katika ukurasa huo huo : ( أجمعت الأمة على استحباب رفع اليدين عند تكبيرة الاحرام واختلفوا فيما سواها)

Tafsiri yake: “Umma umekubaliana katika kupendelea kuinua mikono wakati wa kupiga takbiratil-ihram na wakakhitilafiana kwenye takbira nyengine”.

Published By Said Al Habsy

MLANGO WA KWANZA – 5.Dhehebu la kiibadhi ni tokea karne ya kwanza ya Hijria

TANO

Kwa hakika mwanzo wa kuwepo Dhehebu la Kiibadhi ijulikanavyo kimaarufu au kiistilahi ni katika karne ya mwanzo Hijria ama kuanza kwake kihakika ni kwa Bwana Mtume (s.a.w), na tumesema ijulikanavyo kimaarufu au kiistilahi ni kwa sababu ya vipimo vya makisio vilivyowekwa katika kupatikana madhehebu za kiislamu. Na kuanza kwa Dhehebu la kiibadhi ni tokea karne ya kwanza ya Hijria – karne ya maswahaba – yaani Dhehebu hili limeanza kwa kusikia na kuona kutoka kwa maswahaba na wakati huo Dhehebu hilo lilikuwa na wanachuoni wengi tu miongoni mwao Suhar bni L-Abbas Al-abdy, Jabir bin Zayd, Jaafar bni Simaak, Al-hattaat bni Kaatib, Abdillahi bni Abbaadh, Abu Nuuh Saleh Ddahaan na kiongozi wao wote hao ni Tabii mkubwa kabisa Al-imam Jabir bin Zayd Al-azdy mtu wa Omani ambaye umma wa kiislamu umekubaliana juu ya uadilifu wake wala hakuna aliyemtia doa hata mmoja, na amepata elimu kutoka kwa maswahaba wengi kama kina Abi Said Alkhudry, Anas bni Malik, Abdillahi bni Umar, Abi Hurayrah, Abdillahi bni Abbaas radhi za Allah ziwe juu yao, vile vile amepokea kutoka kwa mamama wa waislamu –wakeze Bwana Mtume (s.a.w)-. Na hakika amesifiwa sana na Maswahaba sifa ambazo hakuzipata ila yeye tu, amesema Abdullahi bnu Abbaas (r.a) mwanachuoni wa umma na mtarjumani wa Qur-ani kuhusu Imam Jabir: “Lau kama watu wa Basra wangalifuata kauli ya Jabir bin Zayd ingeliwatosheleza elimu –aliyonayo- ya kitabu cha Allah” 10. Na akasema vile vile kuhusu yeye: “Muulizeni Jabir bin Zaid lau kama watu wa Mashariki na Magharibi wangalimuuliza basi ingaliwatosheleza elimu yake” na akasema pale baadhi ya watu wa Basra walipomuuliza “Vipi mnaniuliza mimi na mnaye –yupo kwenu- Jabir bin Zayd”11.

Na akasema Abdillah bin Umar (r.a) hakika yeye –Jabir bin Zayd- ni katika wanachuoni mashuhuri Basra.Na alipokufa Imam Jabir bin Zayd Alisema mtumishi wa Bwana Mtume (s.a.w) Anas bin Malik (r.a): “Leo amekufa yule aliye mjuzi wa elimu aliyekuwepo katika mgongo wa ardhi”. Pia alishuhudiwa kwa kusifiwa na wenzake kwa wingi wa elimu, utukufu na ubora wa tabia na kushika dini, kama Ibnu Siyriin, Alhassan Albaswariy, Qataadah na Iyaas bin Muawiyah. Na amesifiwa Imam Jabir bin Zayd sifa nyingi kutoka kwa wanachuoni wote wa kiislamu kwani

__________________________________

10 -Imam Albukhary katika kitabu chake Attaarikhul kabiir/ mujallad ththaaniy qismu ththaaniy juzuu 1/204 chapa ya Daarul-fikriy: mtu wa : 2202.

11 -AngaliaTahdhiibu TTahdhibcha IbnuHajar aliyekufa 852 H, chapa Daaru Ihyaai tturaathiL-Arabiy chapa ya 2 mwaka 1413HR/1993AD – JZ1/347-8.

_________________________________

historia ameandika kuwepo kwake –kwenye uwanja wa elimu- angalia tarjuma ya Imam Jabir bin Zayd katika vitabu vifuatavyo:

التاريخ الكبير للبخاري ، وحلية الأولياء لأبي نعيم ، وتذكرة الحفاظ للذهبي ، وطبقات ابن سعد ،

وتهذيب التهذيب لابن حجر، وطبقات المشايخ للدرجيني ، والسير للشماخي.

Basi kutokana na hayo lau ingalikuwa Bwana Mtume (s.a.w) aliinua na kufunga mikono hapana shaka maswahaba zake nao wangalifanya na wao kama wangalifanya vile vile Imam Jabir nae angalifanya, na ingalikuwa Imam Jabir amefanya hivyo hakuna wasi wasi na wafuasi wake nao wangalifanya, lakini Imam Jabir hakuwaona maswahaba wakiinua wala wakifunga mikono yao, bali wala hakupokea chochote kuhusu jambo hilo kutoka kwao, na jee? Inampelekea Imam Jabir aiwache sunna ambayo ameifanya Bwana Mtume (s.a.w) na wakaifanya maswahaba zake lau ingalikuwa sunna hii ni sahihi, kwani angaliiwacha sunna hiyo maswahaba wangalihesabu kuiwacha kwake ni kwenda kinyume na sunna kwa hivyo wasingalimsifu kwa sifa kubwa kubwa walizomsifia wala kumshuhudia kuwa na elimu na ubora, kwani hakika baadhi ya hadithi za kuinua mikono zimepokewa na Abdillahi bni Umar (r.a) ambaye amemshuhudia Imam Jabir kwa wingi wa elimu alionao na ubora mkubwa, kama tulivyoelezea huko nyuma jinsi walivyomsifia na tumeona namna gani ukubwa wa maingiliano aliyokuwa nayo baina yake na maswahaba hao, basi Imam Jabir awakhalif mashehe zake? Naye alikuwa mwenye pupa na hamu kubwa ya kupokea sunna za Bwana Mtume (s.a.w) katika kila kubwa lake na dogo lake, ikafika hadi kumuuliza mama wa waumini Aisha (r.a) kuhusu Bwana Mtume (s.a.w) alikuwa akianza vipi wakati wa jimai.

Published By Said Al Habsy

MLANGO WA KWANZA – 6.Hakika kila amali (zitalipwa) kutokana na nia na bila shaka kila mtu atalipwa kwa kile alichokinuia

Sita

Kwa hakika suala la kufunga na kuinua mikono hukumu yake haivuki zaidi ya kuwa ni mustahabbu (jambo linalopendelewa) kwa hao wanaojuzisha jambo hilo, hivi inaingia akilini kuwepo hadithi zote hizo zinazozungumzia jambo hilo? Wakati kuna misingi mikuu ya uislamu haikuja katika suala hilo isipokuwa hadithi moja au mbili tu, tuchukulie mfano wa nia, ambayo amali zote za uislamu zinasimamia hiyo, kwani matendo ya kiislamu yanategemea nia ili yaweze kuwa sahihi au kufisidika, imepokewa hadithi moja tu kuhusu jambo hilo nayo ni:

( إِنَّمَا الأَعْمَالُ بِالنِّيَاتِ وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِىءٍ مَا نَوَى)

Tafsiri:

(Hakika kila amali (zitalipwa) kutokana na nia na bila shaka kila mtu atalipwa kwa kile alichokinuia).

Wala hadithi hii haikuja isipokuwa kwa njia mbili tu:

1- Amepokea Imam Arrabii katika Musnad yake kwa njia ya Ibnu Abbas (r.a).

2- Wamepokea Maimamu wengine kwa njia ya Umar bnil Khattwab (r.a).

Basi sikiliza waliyoyasema Wanavyuoni juu ya shani ya hadithi hii tukufu, amesema Al-imam Nuruddin Ssaalimiy katika sherhe ya Musnad Arrabii: “Na hapo ndipo walipoitukuza hadithi hii wakasema ni nguzo miongoni mwa nguzo za uislam, hata ikasemwa hadithi hiyo ni theluthi ya elimu na kauli nyengine ni robo, na wengine wakasema ni khumus 1/5”.

Na amesema mwanachuoni Ibnu Hajar Al-asqalaaniy katika Fat-hul Baariy: “Yamepokewa mapokezi mengi kutoka kwa Maimamu juu ya kutukuza kiwango cha hadithi hii, amesema Abu Abdillahi hakuna kitu chochote katika mapokezi ya Bwana Mtume (s.a.w) yaliyokusanya na kutosholeza na yaliyo na faida nyingi kama hadithi hii”, Na imepokewa kutoka kwa wanavyuoni wengi sana kuhusu hadithi hii kuwa ni theluthi ya Uislamu na ikasemwa ni robo yake. Basi ikiwa nia ambayo ina sehemu kubwa katika dini imekuja hadithi moja tu inayoielezea, kwa hakika mtu anastaajabu sana kutokana na wingi wa hadithi zilizopo juu ya suala la kufunga na kuinua mikono hadi kukaribia kiwango cha tawaatur maanawiy lau zingalikuwa hadithi hizo ni sahihi, kutokana na wingi wa hidithi zenyewe na wingi wa njia zake .

Published By Said Al Habsy

Saba – Mwisho


Wakati wa kuzichambua hadithi zilizokuja katika kuinua na kufunga mikono itadhirika ya kuwa hadithi zote hizo ni dhaifu au za kuzuliwa, na wala hamna ndani yake hadithi sahihi, na inajulikana wazi ya kuwa haijuzu kufanya amali yoyote kwa kutumia hadithi dhaifu, na baadhi ya wanavyuoni wa elimu ya hadithi wa wakati wetu huu wanaonelea ya kuwa haifai kutumia hadithi dhaifu hata katika masuala ya kuraghibisha au kuhofisha – pamoja na kuwa wanachuoni wa zamani waliruhusu jambo hilo – yote kwa kukhofia mtu asije akaingia katika makemeo ya Bwana Mtume (s.a.w) aliposema:

“Mwenye kunizulia mimi kwa makusudi basi ajichagulie makao yake motoni”.14

Kwa hakika hadithi sahihi zilizopo zinatosha, kama ilivyokuwa swala ni ibada ambayo ni tawqifii (yaani hukumu zake zinaletwa kwa wahyi) basi haijuzu kwa muislamu yeyote yule kuzidisha au kupunguza kitu chochote kile ndani ya swala hiyo kwa kutumia hadithi dhaifu zilizo nyepesi kama

____________________________

12 -شرح الجامع الصحيح مسند الإمام الربيع بن حبيب ابن عمر الأزدي البصري، ج1 /11
فتح الباري شرح صحيح البخاري ج1/17، ط1، 1404هـ – 1986م- دار الريان للتراث – القاهرة – 13

14- فتح الباري شرح صحيح البخاري ج1/244 الحديث:110 ، ط1، 1404هـ – 1986م- دار الريان للتراث – القاهرة

_________________________________________________

uzi wa buibui, kwani kuzidisha kitu ndani yake ni sawa sawa na kupunguza, hivyo kutokana na dalili hizi Maibadhi wameonelea kutokujuzu kuinua au kufunga mikono katika swala.

Na huenda msemaji akasema hakuna dalili ya kuzuia kuinua na kufunga mikono katika swala, basi jawabu lake ni hili:-

1- Hadithi ya yule aliyekosea sala yake -wakati wa Bwana Mtume (s.a.w)- nayo ni hoja inayoonyesha namna ya kusali kwa itifaqi ya umma.

2- Kutoinua na kutofunga mikono ni asli ya mtu [akisimama], na jambo la asli halihitaji kuthibitishwa kwa dalili, bali dalili inakuwa juu ya jambo lilozidi juu ya asli.

3- Hakika kauli ya kuwacha kuinua na kufunga mikono ni istis-haab hali ya asli, na istis-haab hali ya asili ni miongoni mwa dalili za kiusuli ambazo hupitishwa hukumu kwayo.

4- Ameelezea mwanachuoni Ash-shawkaaniy katika kitabu chake Naylul-awtaar hadithi ambayo imepokewa na Abu Hurayrah (r.a) ambayo ni marfuu isemayo

“Mwenye kunyanyua mikono yake katika swala basi mtu huyo hana swala” na akasema: “Hakika Ibnul-jawziy ameiweka hadithi hii miongoni mwa hadithi maudhui (hadithi maudhui ni ile iliyotungwa)”. Na imesemwa ya kuwa Ibnul-Jawziy anafanya haraka katika kuzipa hadithi hukumu ya maudhui, ndio wakasema wanachuoni hakuzingatiwi moja kwa moja juu ya hukumu ya hidithi alizosema ni maudhui, kuwa hukumu yake ni ya kutungwa.

5- Hakika khushuu ni roho ya swala, wala haipatikani isipokuwa mtu abaki katika umbile la kiasili, na hapana shaka kuinua na kufunga mikono ni vitendo vinavyopatikana nje ya umbile la asili na kila kinachopingana na umbile la kiasili bila ya kuwepo dalili sahihi, vitu hivyo huzingatiwa kuwa vinakwenda kinyume na khushuu.

6- Amesema swahaba mtukufu bahrul-ilmu na mturujumani wa Qur-ani Abdillahi bni Abaas (r.a) katika kufasiri kauli ya Allah :

{ قَدْ أَفْلَحَ المُؤْمِنُوْنَ oالذِّينَ هُمْ فِي صَلاَتِهِمْ خَاشِعُوْنَ }

Tafsiri yake:

{Wamefaulu waumini wale ambao huleta khushuu katika swala zao} Akasema: ni wale wenye kunyenyekea ambao hawageuki kulia wala kushoto wala hawainui mikono yao katika swala.

7-Ukizingatia utagundua ya kuwa kuinua na kufunga mikono kumeshikiliwa zaidi na madhehebu yaliyokuja mwisho kuliko yaliyotangulia.

_______________________________________

15-Naylul Awtwaar Mujallad 1/ j2/183, Chapa 1 mwaka 1415H / 1995M. Daarul-Kutubil-ilmiyyah , Beirut-Lebnon
16-Almuuminuun Aya 1-2.
17- نتوير المقياس من تفسير ابن عباس- لأبي طاهر محمد بن يعقوب الفيروزابادي ، ص: 212
دار الحيل بيروت لبنان.

18-Madhehebu yaliyotangulia ni yale yalioanza mwanzo kabla ya mengine nayo ni Maibadhi – Mashia –Mahanafi na Malik.

Published By Said Al Habsy

UCHAMBUZI KUHUSU HADITHI ZA KUINUA NA KUFUNGA MIKONO

SEHEMU YA KWANZA:

HADITHI ZA KUINUA MIKONO

1-عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : ” كَانَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ رَفَعَ يَدَيْهِ مُدًّا ” .

رواه الخمسة إلا ابن ماجة ، ويقصد بالخمسة إلا ابن ماجة ، أحمد- أبو داود-الترمذي و النسائي[19]

TAFSIRI

(1)Kutoka kwa Abi Hurayrah (r.a) amesema: “Mjumbe wa Allah rehma na amani ziwe juu yake alikuwa akisimama kusali huinua mikono yakejuu”.

Wamepokea wapokezi watano isipokuwa Ibnu Maajah, na inakusudiwa watano isipokuwa Ibnu Maajah, ni Ahmad, Abu Daud, Attirmidhy na Annasaaiy, kwa istilahi ya mtunzi wa kitabu Muntaqaa Al-akhbaar.

[19]- Ahmad 2/375 hadithi ya : 8862. (مكتبة الشاملة)

– Abu Daud 1/255 hadithi ya: 738 . (مكتبة الشاملة)

-Attirmidhiy 2/5-6 hadithi ya: 239 : (مكتبة الشاملة)

239 – حدثنا قتيبة و أبو سعيد الأشج قالا حدثنا يحيى بن اليمان عن ابن أبي ذئب عن سعيد بن سمعان عن أبي هريرة قال : كان رسول الله صلى الله عليه و سلم إذا كبر نشر أصابعه

قال أبو عيسى حديث أبي هريرة [ حسن ]

[ و ] قد روى غير واحد هذا الحديث عن ابن أبي ذئب عن سعيد بن سمعان عن أبي هريرة أن النبي صلى اله عليه وسلم كان إذا دخل في الصلاة رفع يديه مدا

وهذا أصح من رواية يحيى بن اليمان وأخطأ يحيى بن اليمان في هذا الحديث

قال الشيخ الألباني : ضعيف.

240 -[ قال و ] حدثنا عبد الله بن عبد الرحمن أخبرنا عبيد الله بن عبد المجيد الحنفي حدثنا ابن أبي ذئب عن سعيد بن سمعان قال سمعت أبا هريرة يقول : كان رسول الله صلى الله عيه وسلم إذا قام إلى الصلاة رفع يديه مدا

قال [ [ أبو عيسى قال ] عبد الله [ بن عبد الرحمن ] وهذا أصح من حديث يحيى ابن اليمان وحديث يحيى بن اليمان خطأ

قال الشيخ الألباني : صحيح . (مكتبة الشاملة)

-Vipi iwe sahihi na ndani yake yumo Said bnu Sam’aan na Ubaydullah Alhanafiy nao wote wana udhaifu, angalia katika uchambuzi wa hadithi hii utaona.

-Annasaaiy 1/124 hadithi ya:883.(مكتبة الشاملة)

UCHAMBUZI WA HADITHI:

Na kasema Ashshawkaaniy katika kitabu cha Naylul-Awtwaar[20] :“Na ameipokea Addaaramiy kwa njia ya Ibni Abi dhi’ib kutoka kwa Muhammad bni Umar bni A’twaai kutoka kwa Muhammad bni Abdurrahman bni Thuwban kutoka kwa Abi Hurayrah”.[21]Hadithi hii katika sanad ya upokezi wa Ahmad na Abi Daud na Attirmidhiy na Annasaaiy yumo Said bni Sam-a’an, amesema Al-hafidh Adhdhahabiy kuhusu mtu huyo kwenye kitabu chake kiitwacho Miizanul-I-itidal: “Kuna ujahala juu ya mtu huyo, na Al-Azdiy amemdhoofisha”.[22]

Na kwenyeupokezi wa Addaaramiy[23] katika sanadi yake yumo Ubaydillahi bni Abdulmajiid Alhanafiy, amepokea Adhdhahabiy kutoka kwa Uthman bni Said kutoka kwaYahya kwamba mtu huyo si chochote si lolote (katika upokezi wa hadithi[24].(na misingi ya sheria katikahadithi inasema (إن الجرح مقدّم على التعديل)

Tafsiri yake: hakika illa au tuhuma hutangulizwa juu ya uadilifu.[25]

Hayo yote ni kwa ajili ya kuzilinda sunna tukufu za Bwana Mtume (s.a.w) kutokana na mchezo wa wachezaji na utunzi wa watungaji (yaani hadithi za uongo), kwa sababu hiyo hakika hadithi hii ni dhaifu.

2-وعن وائل بن حجر ( أَنَّهُ رَأَى رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَرْفَعُ يَدَيْهِ مَعَ التَّكْبِيرَةِ)
رواه أحمد – وأبو داود، قال الشوكاني وأخرجه البيهقي أيضا :


TAFSIRI:


(2) Imepokewa kutoka kwa Wail bnu Hujri (amemuona Mjumbe wa Allah rehma na amani ziwe juu yake huinua mokono yake miwili pamoja na takbira(.

Ameipokea Ahmad – Abu Daud, amesema Imam Ashshawkaniy ameielezea hadithi hii AlBayhaqiy vilevile. [26]

UCHAMBUZI WA HADITHI:

Na hadithi hii ni dhaifu kwa njia mbili:

a-Ameipokea Ahmad na Abu Daud kwa njia ya Abduljabbaar bni Wail, amesema ( yaani Abduljabbaar ): “Wamenihadithia watu wa nyumbani kwangu kutoka kwa baba yangu kwamba amemuona Mjumbe wa Allah rehma na amani ziwe juu yake anainua mikono pamoja na takbira”. Amesema Ashshawkaniy: “Amesema Almandhiry kuwa Abduljabbaar hakusikia hadithi hiyo kutoka kwa baba yake na watu wa nyumbani kwake hawatambuliki ni kina nani[27],kwa hivyo sanadi yake imekatika, na kukatika kwa sanadi katika hadithi ni daliliyaudhaifuwake” .

b-Kwenye upokezi wa Al-bayhaqiy katika sanadi yake yumo Abul-Bukhtury Said bni Fayruz Attwaiy, na amenukuu Adhdhahabiy kutoka kwa Salamata bnu Suhayl amesema kuhusu Abul-Bukhtury “kuwa ni mwenye kukithirisha na hadithi zake ni mursalna hupokea kutoka kwa maswahaba, na wala hakupokea kutoka kwa hata mmoja katika maswahaba wakubwa, na katika hadithi zake zilizopokewakwa kusikia (سماعا)basi hizo ni katika hadithi hasan((حسن nazilizokuja kwa upokeziwa(عن) hizo ni hadithi dhaifu, na katikaupokezi wa Al-Bayhaqiy imekuja kwa njia ya ( عن) kwa maana hiyo hadithi hii ni dhaifu.

3-Imepokewa kutoka kwa Ibni Umar ya kuwa:

3-((كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ رَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّى يَكُوْنَا بِحَذْوِ مَنْكِبَيْهِ ثُمَّ يُكَبِّرُ , فَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَرْكَعَ رَفَعَهُمَا مِثْل ذَلِكَ , وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرُّكُوْعِ رَفَعَهُمَا كَذَلِكَ أَيْضًا , وَقَالَ سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ)) متفق عليه ,

قال الشوكاني أخرجه البيهقي بزيادة؛ ” فَمَا زَالَتْ تِلْكَ صَلاَتُهُ حَتَّى لَقِيَ اللهَ تَعَالَى “

TAFSIRI:

3-“Alikuwa mjumbe wa Allah rehma na amani ziwe juu yake akisimama kwa ajili ya kusali huinua mikono yake mpaka inakuwa karibu na mabega kisha huleta takbira, na akitaka kurukuu huinua mikono hiyo vile vile,na akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu huinua vile vile nahusema“سمع الله لمن حمده ربنا ولك الحمد” muttafaqun-alayhi.

Amesema Ashshawkaniy hadithi hii ameitoa Al-Bayhaqiy mna ziada ndani yake “Haikuacha kuwa hiyo ndiyo swala yake hadi kufa kwake”.

[20]–Naylul Awtwaar Mujallad 1/ j2/181, Chapa 1 mwaka 1415H / 1995M. Daarul-Kutubil-ilmiyyah , Beirut-Lebnon

[21] – Sunani Addaaramiy 1/308 hadithi ya : 1237.

[22]-3206 – سعيد بن سمعان [ د، س، ت ].

عن أبى هريرة. فيه جهالة. ضعفه الازدي، وقواه غيره. وقال النسائي: ثقة . 2/143 (مكتبة الشاملة).

[23] –1237 – أخبرنا عبيد الله بن عبد المجيد الحنفي ثنا بن أبي ذئب عن محمد بن عمرو بن عطاء عن محمد بن عبد الرحمن بن ثوبان عن أبي هريرة : أن رسول الله صلى الله عليه و سلم لم يكن يقوم إلى الصلاة إلا رفع يديه مدا .(1/308)

قال حسين سليم أسد : إسناده صحيح.(مكتبة الشاملة)

[24]- 5381 – عبيد الله بن عبدالمجيد [ ع ]، أبو على الحنفي.عن قرة بن خالد، وطبقته وعنه الدارمي، والذهلى، وخلق. قال أبو حاتم، وغيره: ليس به بأس وروى عثمان بن سعيد، عن يحيى: ليس بشئ . – ميزان الإعتدال3/ 13

(مكتبة الشاملة).

[25] – Maana yake ni kuwa akitokea mtu katika wapokezi wa hadithi akawa anasifiwa kwa sifa aina mbili tofauti za uadilifu na udhaifu basi hutangulizwa sifa mbaya na zile nzuri hutupwa wala hazitizamwi, yote hayo ni kwa sababu ya kuzilinda hadithi tukufu na mikono ya wenyekuzichezea hadithi hizo au wenye kuzua hadithi za uongo, kwa hivyo hadithi hii ni dhaifu.

[26] – Nimeangalia musnad ya Imam Ahmad sijaiona hadithi hiyo.

– Sunanu Abu Daud 1/250 hadithi ya 725 (مكتبة الشاملة)

– Sunanul kubra lilBayhaqiy: 2/26 hadithi ya 2144.. (مكتبة الشاملة)

[27]-Naylul Awtwaar Mujallad 1/ j2/184, Chapa 1 mwaka 1415H / 1995M. Daarul-Kutubil-ilmiyyah , Beirut-Lebnon.

UCHAMBUZI WA HADITHI:

a-Hadithi hii katika sanadi yake kwenye upokezi wa Al-Bukhariy na Muslim kuna mtu anaitwa Muhammad bnu Muslim bnu Shihab Azzuhriy.

Amesema Alhafidh Adhdhahabiy (amekufa 748 H) kuhusu mtu huyo kwenye kitabu chake cha (mizaanul-iitidaal) “Kwa hakika alikuwa anafanya tadliis”.[28]

Na ametiwa aibu Azzuhriy kwa sababu ya kuchanganyika kwake na wafalme madhalimu katika Baniy Umayya, na akafungua mlango wa kuingia kwa wafalme hao “Wakamfanya (yaani Azzuhriy) ndiye mwega mkubwa wa kupitishia batili zao, na daraja la kuvukia katika kufikia balaa zao, wanawaingizia shaka maulamaa wengine na nyoyo za majahil zinafuata” kama alivyomuandikia juu ya hilo mmoja wa ndugu zake katika dini na kwa kweli jambo hilo ni katika mambo yanayoshusha na kuangusha cheo na heshima ya wanachuoni hasa kwa wapokezi wa sunna na maulamaa wa hadithi, amesema Imam Abu Ya-aquub Alwarjilaaniy kwenye kitabu chake Addaliil walburhaan “Na wakamuandikia yeye (yaani Azzuhriy) mafaqihi wapatao 120 wakimsimanga na kumtia aibu juu ya alilolifanya, miongoni mwa hao ni Jabir bni Zayd na Wahbu bni Munabbih na Abu Hazimil-faqiih, mwanachuoni wa Madina na mfano wa hao na kwa hakika nimeziona barua za hao watatu walizompelekea yeye”, na vile vile amenukuu Ibnu Qutaybah katika kitabu chakeAl-imamatu wassiyaasatu maneno ya Abi Haazimil mwanachuoni wa Madina aliyomwambia Azzuhriy mbele ya Sulayman bni Abdulmalik.

b-Vile vile hadithi hiyo kwenye sanadi yake katika upokezi wa Muslim na Albayhaqiy yumo Abdulmalik bni Abdul-aziz bni Jurayj, na Abdurrazzaaq bni Himam, ama Ibnu Jurayj amesema Adhdhahabiy kuwa alikuwa anadallis يُدَلِّسُ, na imenukuliwa kutoka kwa Abdillahi bni Ahmad bni Hanbal “ Amesema baba yangu baadhi ya hadithi hizi ambazo Ibnu Jurayj akiziunganisha (hadi kwa Bwana Mtume) ni hadithi zilizozuliwa”[29], na ama Abdurrazzaaq bni Himam wamemzungumza maulamaa wa hadithi baina ya kumkubali na kumdhoofisha[30] na kanuni za elimu ya hadithi zinasema ((أََنَّ الجَرْحَ مُقَدَّمٌ عَلَى التَّعْدِيلِ )) .

c-Vile vile katika hadithi hii kuna makosa ya kilugha kwenye lafdhi zake kwani kimekuja kitendo katika sigha (mfumo) wa sifa ya kiume na ambayo inatakiwa iwe ya kike[31], hadithi inasema ( حَتَى يَكُوْنَا ) na inavyotakikana iwe (حََى تَكُوْنَا) kwa sababu inayozungumzwa hapo ni mikono na maulamaa wanakataza kuwepo makosa ya kilugha katika hadithi, anasema Dr Subhi Ssaalih kwenye kitabu chake:“علوم الحديث ومصطلحه” Anashurutiza mpokezi wa hadithi awe “mwenye uwezo wa kuifikisha hadithi ufikishaji ambao hautakuwa na makosa ya kilugha”, na tuyatizame hayo maneno amenasibishiwa nani? Amenasibishiwa Abdillahi bni Umar na yeye anajulikana ni nani, ni Sahaba tena katika wenye elimu, naye ni miongoni mwa Maquraysh wenye akili sana na mwenye fasaha na ujuzi wa kuzungumza, tena Qur-ani imeteremshwa kwa lugha yao, na kwa kweli iko mbali sana kuwa Abdillahi bni Umar aweke lafdhi ya kiume kwenye lafdhi ya kike, tena bila ya sababu yoyote ya kimsingi inayohitaji kufanya hivyo na hapa haikupokewa hadithi hii kwa njia ya maana رِوَايَةُ الحَدِيْثِ بِالمَعْنَى, kwani riwaya za namna hizo ni kuwekwa neno badala ya neno tena liwe na maana hiyo hiyo bila ya kutoka nje ya kanuni za lugha ya kiarabu, na hao walioruhusu riwaya za aina hizo wameshurutisha mpokezi wa hadithi awe ni mjuzi wa misingi ya lugha ya kiarabu kama Sarfu –Nahaw na mfano wake, basi kutokana na vipimo hivi inamdhihirikia wazi msomaji kuwa hadithi hii ni dhaifu na udalili wake unaporomoka.

4-Imepokewa kutoka kwa Nafi-i :

4-أَنَّ ابنَ عُمَرَ كَانَ إِذاَ دَخَلَ فِي الصَّلاَةِ كَبَّرَ وَرَفَعَ يَدَيْهِ ، وَإِذَا رَكَعَ رَفَعَ يَدَيْهِ، وَإِذَا قَالَ سَمِعَ اللّهُ لِمَنْ حَمِدَه رَفَعَ يَدَيْهِ ، وَإِذَا قَامَ مِنَ الرَّكعَتَيْنِ رَفَعَ يَدَيْهِ ،وَرَفَعَ ذَالِكَ ابن عمر إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم . رواه البخاري والنَّسَائي وأبو داود.

TAFSIRI:

Kutoka kwa Nafi’i:

“Alikuwa Ibnu Umar akiingia ndani ya swala husoma takbira na kuinua mikono yake, na akirukuu huinua mikono yake, na akisemaسَمِعَ اللّهُ لِمَنْ حَمِدَه huinua mikono yake, na akiinuka kutoka kwenye rakaaya pili huinua mikono yake, na Ibnu Umar akaiinua hadithi hii hadi kwa Bwana Mtume (s.a.w).

Ameipokea Albukhariy –Annasaaiy- Abu Daud.

UCHAMBUZI WA HADITHI

Hadithi hii ni dhaifu kwa sababu mbili zifuatazo:-

)1(-Hadithi hii imetiwa illa kwa sababu ya ikhtilafu iliyopo katika kuiinua hadi kwa Bwana Mtume (s.a.w) na kutokuiinua, amesema mwanachuoni Ashshawkaniy katika kitabu chake Naylul-Awtwaar:[32]

“Na ameelezea Addaaraqutniy katika Al-ilal -العلل-ikhtilafu katika kuifikisha kwa Bwana Mtume (s.a.w) na kutoifikisha”[33].

Na hadithi iliyo sahihi ni ile iliyosalimika na shudhuudh na illa (شُذُوْذٌ وَ عِلَّةٌ ) .

)2(-Na katika sanadi yake kwenye upokezi wa Albukhary na Abi Daud, yumo Abdul-A-ala bin Abdul-A-ala Ashshamiy, amesema Ibnu Sa-ad mtu huyo hakuwa na uzito katika hadithi, na akasema Imam Ahmad alikuwa na aqida ya Alqadriyya, na amesema Bundaar ninaapa kwa jina la Allah alikuwa haujui mguu wake upi mrefu, tizama mizaanul-I-iitidaal cha Adhdhahabiy[34], na wala sikuiona hadithi hii kwa lafdhi hii kutoka kwa Naafii kwenye upokezi wa Annasaaiy, bali amepokea Annasaaiy hadithi za Anaafii kutoka kwa Ibnu Umar (r.a) kwa njia ya Salim bni Abdillahi. Na huenda ikawa imo katika kitabu cha Almujtabaa cha Annasaaiy. Na Almujtabaa ni kitabu kilichozikusanya hadithi zilizo sahihi kwa rai ya Annasaaiy kutoka katika kitabu chake cha Assunan. Na Allah ndie mjuzi zaidi kwa hilo.

5- Imepokewa kutoka kwa Imaam Aliy (k.w):

5-” عَنْرسول الله صلى الله عليه وسلم أَنَّهُإِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ الْمَكْتُوْبَةِ كَبَّرَ وَرَفَعَ يَدَيْهِ حَذْوَ الْمَنْكِبَيْهِ ، وَيَصْنَعُ مِثْلَ ذَلِكَ إِذَا قَضَى قِرَاءَتَهُ وَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَرْكَعَ، وَيَصْنَعُهُ إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرُّكُوْعِ ، وَلاَ يَرْفَعُ فِي شَيْءٍ مِنْ صَلاَتِهِ وَهُوَ قَاعِدٌ ، وَإِذَا قَامَ مِنَ السَّجْدَتَيْنِ رَفَعَ يَدَيْهِ كَذَلِكَ وَكَبَّرَ”

رواه أحمد وأبو داود والترمذي وصححه ، قال الشوكاني وأخرجه أيضا النسائي وابن ماجة.

TAFSIRI:

5-Amesema Imaam Aliy (k.w) kuwa: “Bwana Mtume (s.a.w.) alipokuwa akisimama kusali swala za Fardhi huleta takbiira na hunyanyua mikono yake kukaribia (sawa na) mabega yake, na hufanya hivyo akimaliza kisomo chake na pindi akitaka kurukuu, na huinyanyua pindi akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu, na wala hainui kitu katika swala ikiwa amekaa, na anapoinuka kutoka kwenye sijda mbili huinua mikono yake vilevile na huleta takbiira”. Imepokewa na Ahmad na Abu Daud na Attirmidhiy na kuisahihisha, na kasema Ashshawkaaniy (hadithi hii) vilevile ameipokea Annasaaiy na Ibnu Maajah.

UCHAMBUZI WA HADITHI

1-Hadithi hii kwenye upokezi wa Abu Daud na Ibnu Maajah katika sanadi zao yumo Mussa bni U’qbah, amesema Imaam Adhdhahabiy katika kitabu cha Almiizaan:( Na hakika mara nyengine amesema Ibnu Mai’in kuwa mtu huyo ana baadhi ya udhaifu[35], na ndani yake vile vile yumo Abdurrahman bniAbi Zzinaad, na amepokea Alhaafidh Ibnu Hajar katika kitabu cha Attahdhiib[36]udhaifu wa mtu huyo kutoka kwa wanavyuoni wengi miongoni mwao Ibni Mai’in na Aliy bni Mudiiniy na Saleh bni Muhammad na Ya’aquub bni Shaybah na A’mru bni Aliy na Annasaaiy na Abi Zar’a na Assaajiy na vile vile Malik naye kamzungumza na akaashiria kuhusu hadithi ya Attirmidhiy pale aliposema ( na katika mlango huu .. kutoka .. Aliy) na sikuiona katika Sunani- Nnasaaiy.

6-عن أبي قلابة (( أَنَّهُ رَأَى مَالِكَ بنَ الْحُوَيْرِثِ إِذَا صَلَّى كَبَّرَ وَرَفَعَ يَدَيْهِ وَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَرْكَعَ رَفَعَ يَدَيْهِ ، وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ رَفَعَ يَدَيْهِ ، وَحَدَّثَ أَنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَنَعَ هَكَذَا )) متفق عليه وعند أحمدومسلم(( أَنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، كَانَ إِذَا كَبَّرَ رَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّى يُحَاذِي بِهِمَا أُذُنَيْهِ، وَإِذَا رَكَعَ رَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّىيُحَاذِي بِهِمَا أُذُنَيْهِ، وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرُّكُوْعِ فَقَالَ سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ فَعَلَ مِثْلَ ذَلِكَ ))

TAFSIRI

6-Kutoka kwa Abi Qilaabah yeye ((Amemuona Malik bnal Huwayrith anaposali husoma takbira na kuinua mikono na anapotaka kurukuu huinua mikono yake, na akiinua kichwa chake huinua mikono yake, na akaelezea kuwa Bwana Mtume (s.a.w) alifanya hivi)) muttafaqun alayhi na katika upokezi wa Ahmad na Muslim (( kuwa Bwana Mtume (s.a.w) alikuwa akisoma takbira huinua mikono yake hadi kukaribia masikio yake, na akirukuu huinua mikono yake hadi kuwa sawa na masikio, na anapoinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu na kusema: سمع الله من حمدهhufanya kama hivyo)).

UCHAMBUZI WA HADITHI

1-Hadithi hii imepokewa kwa njia ya Abi Qilaabah nae ni dhaifu, kasema Ibnu Hajar katika kitabu cha Attah-dhiib[37]amemdhoofisha Ibnu Ttiin katika sherhe yake ya Albukhariy, وقال إنه معدود في البلهyaani yeye ni katika wanaohesabiwa kwa kuwa ni mwenye kupitilia mpaka katika kughafilikana kasema Adhdhahabiy katika Almizaan[38]((anajiamini nafsi yake isipokuwa anadallis kwa wale aliokutana nao na wale asiowahi kukutana nao, na alikuwa na suhuf (kurasa) akihadithia hadithi ndani yake na anadallis)).

8- وعن أَبِي حُمَيْدٍ السَّاعدِيِّ (( أَنَّهُ قَالَ وَهُوَ فِي عَشَرَةِ مِنْ أَصْحَابِ رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَحَدُهُمْ أَبُوْ قَتَادَةِ ، أَنَا أَعْلَمُكُمْ بِصَلاَةِ رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، قَالُوْا مَا كُنْتَ أَقْدَمَ مِنَّا لَهُ صُحْبَةً ، وَلاَ أَكْثَرَنَا لَهُ إِتْيَانًا ، قَالَ بَلَى، قَالُوْا فَاعْرِضْ , فَقَالَ كَانَ رَسُوْلُ اللهِ صَلىَّ اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ اعْتَدَلَ قَاِئمًا وَرَفَعَ يَدَيْهِ حَتَّى يُحَاذِي بِهِمَا مَنْكِبَيْهِ ثُمَّ يُكَبِّرْ .. إلى آخر الحديث)) رواه الخمسة إلا النسائي ورواه البخاري مختصرا .

TAFSIRI

7-Kutoka kwa Abi Humayd Assa’adiy amesema ((Naye yu pamoja na Masahaba 10 wa Bwana Mtume (s.a.w) mmoja wapo akiwa ni Abu Qataadah): “Mimi ninaijua zaidi swala ya Bwana Mtume (s.a.w) kuliko nyinyi” , wakwambia: “Wewe hujatutangulia sisi kwa usuhuba naye, wala kuwa naye zaidi kuliko sisi, akasema: Ndio, wakasema haya tuonyeshe (tuelezee), Akasema: Alikuwa Bwana Mtume (s.a.w) akitaka kusali husimama sawa sawa hali amenyooka na huinua mikono yake juu hadi kufikia mabega yake kisha huleta takbira … hadi mwisho wa hadithi”.

Wamepokea wapokezi watano isipokuwa Annasaaiy na ameipokea Albukhariy kwa ufupi.

UCHAMBUZI WA HADITHI

Hadithi hii inayo ya kuzungumziwa katika matni na sanad:

1-Kuhusu matni inaonyesha lugha yake ni nyepesi mno kupita kiasi katika maana yake, na wepesi wa maana ya kilugha unahisabiwa ni alama za hadithi ya kutungwa, kwa maana vipi wakhitilafiane 10 miongoni mwa maswahaba wakubwa ndani yake akiwemo Abu Humayd na Abu Qataadah, Abu Usayd na Abu Hurayrah juu ya usahihi wa namna ya kuisali swala? Hali wao walikuwa daima wapo na Bwana Mtume (s.a.w) wakati wote takriban, na walikuwa wakisali naye swala zote, basi inayumkinika kufichika swala ya Bwana Mtume (s.a.w) juu yao? Au inawezekana Bwana Mtume wa Allah awaache Maswahaba zake bila ya kuwafundisha swala! -Hasha haiwezekani kabisa- Bwana Mtume ambaye alikuwa akiwafundisha attahiyyatu kama alivyokuwa akiwafundisha sura miongoni mwa Qur-ani, na mwisho wa hadithi hiyo wakasema: “Umesema kweli hivi ndivyo alivyokuwa akisali Mjumbe wa Allah rehma na amani iwe juu yake na ali zake”.

Jee hivi inaingia akilini wakubali kirahisi kama hivyo na hali walikuwa wanakumbushana swala ya Bwana Mtume (s.a.w) huku wakiwa wamekhitilafiana namna ya kuisali, pamoja na hayo hadithi hii haikutaja kufunga mikono ndani yake na hao wanaojuzisha kufunga mikono wanaling’ang’ania sana jambo hilo kupita kiasi.

Na ninasema: Maneno kama haya hayawezi kutoka kwa Maswahaba, hayo maneno yote ni ya kutunga tu.

2-Ama kwa upande wa sanad katika upokezi wa Abu Daud na Ibnu Maajah yumo Muhammad bnu Amru bnu A’twa na vile vile Abdul-Humayd bnu Jaafar:

)a(-Wakakhitilafiana kuhusu Muhammad bnu Amru bnu A’twaa khitilafu kubwa sana wapo waliosema hakumdiriki Aba Qataadah wengine wamesema amemdiriki, wengine wakasema alifariki katika utawala wa Alwaliid bnu Yazid, baadhi yao wakasema kifo chake kilitokea katika utawala wa Hisham, pamoja na kuwa wengi miongoni mwa wachambuzi wa hadithi wanasema alifariki baada ya mwaka 120 Hijria, na amesema mwanachuoni Mahmoud Muhammad Khatwaab Assubkiy kwenye kitabu المنهل العذب المورود شرح سنن أبي داود “ Na imesemwa kuwa amefariki mwaka wa 154 Hijria”.

Vile vile wamekhitilafiana katika umri wake alipofariki, wapo waliosema amefariki akiwa na umri wa miaka 80 na ziada, wengine wakasema amefariki akiwa na miaka 90, kwa maana hiyo kwa tarehe aliyoitaja Assubkiy itakuwa hakumdiriki Aba Qataadah wala Aba Humayd, kwani Aba Qataadah inasemekana amefariki mwaka 54 Hijria na kauli nyengine amefariki katika ukhalifa wa Sayyidna Ali (k.w), na ama Abu Humayd amefariki mwaka 60 Hijria, kwa hivyo hakuwadiriki na Yahya amemdhoofisha katika baadhi ya riwaya zake.[39]

)b(- Na kuhusu Abdul-Humayd bnu Jaafar amesema Adhdhahabiy kwenye kitabu chake Almiizaan[40]: “Amesema Abu-Haatim si mtu wa kujengea hoja, na imesemwa kuwa alikuwa na rai ya Qadria, amesema Ali bnul-Mudiiniy alikuwa anaongelea imani ya Alqadria na alikuwa kwetu ni Thiqah na akasema alikuwa Sufiyan akimdhoofisha” .

Na amesema Assubkiy katika sherhe ya Sunani Abi Daud: “Amemdhoofisha Yahya bnu Said na Aththawriy na kasema Ibnu Hibban huenda ikawa mwenye kukosea”.

(c)- Na ameipokea Abu Daud kwa njia ya Abbaas bnu Suhl, lakini katika sanadi yake yumo Issa bni Abdillahi bni Malik amesema Assubkiy: “Amesema Ali bnul-Mudiiniy kuhusu (Issa bnu Abdillah) kuwa ni majhuul na wala hakuna mwengine aliyepokea hadithi kwake isipokuwa Muhammad bnu Is-haaq.[41]

(d)-Vile vile ameipokea Ibnu Maajah kwa ufupi na Attirmidhiy kwa njia ya Abbaas bnu Suhl, isipokuwa katika sanadi yake yumo Fulayh bnu Sulayman.

Amesema Adhdhahabiy:“Na hakika amesema Ibnu Mai’in na Abu Haatim na Annasaaiy huyo (Fulayh) si madhubuti, na kasema Abu Haatim nimemsikia Muawiya bnu Salih nimemsikia Yahya bnu Maiin amesema Fulayh bnu Sulayman si thiqah na wala mtoto wake si thiqah, na amepokea Abbaas bnu Yahya kuwa Fulayh si mtu wa kutolewa hoja, na amesema Abdullah bnu Ahmad nimemsikia Ibnu Mai’in anasema watu watatu wanaepukwa hadithi zao, Muhammad bnu Twalha bnu Musraf – Ayub bnu U’tba na Fulayh bnu Sulayman. Na amesema Abu Daud haitolewi hoja kwa njia ya Fulayh”.[42]

Na amenukuu Assubkiy katika sherhe yake ya Abi Daud kutoka kwa Alhakim kuwa amemdhoofisha, na amenukuu Alhafidh Ibnu Hajar Al-Asqalaaniy katika Attahdhiib kudhoofishwa kwake na idadi yawanavyuoni kati yao ni Ali bnu Mudiiniy.[43]

(e)-Na Albukhariy vile vile ameipokea hadithi hii kwa ufupi na bila ya sanadi.

Kwa hivyo hapana shaka yoyote kuwa hadithi hii ipo mbali na usahihi, na ina udhaifu katika matni na sanad, na kusimamisha hoja kwa hadithi yenye sifa kama hizi ni jambo lisilokubalika, na katika kitabu cha Subulu-ssalaam zimetajwa hadithi 4 zinazohusiana na kuinua mikono katika swala:

1-Hadithi ya Abu Humaiyd Assaadiy.

2-Hadithi ya Ibnu Umar kuwa Bwana Mtume (s.a.w) alikuwa anainua mikono yake ….

3-Hadithi ya Malik bnu Huwayrith.

4-Hadithi ya Wail bnu Hujr.

Na hadithi hizo tumeshazielezea na kubainisha udhaifu wake kwa namna yenye kutosheleza in shaa Allah, na zimekuja hadithi nyengine katika suala la kuinua mikono katika swala lakini ni dhaifu kama alivyoweka wazi Ibnu Hajar katika Fat-hul-Baary pale aliposema: “Na katika mlango huu –yaani wa kuinua mikono- zimepokewa hadithi nyingi kutoka kwa Maswahaba lakini zote hazikosi na ya kusemwa (upungufu na illa)”.[44]

[28] – محمد بن مسلم الزهري الحافظ الحجة-رقم: 8171- كان يدلس في النادر.( ميزان الإعتدال 4/40)

-Tadliis maana yake ni kumficha mpokezi usimtaje kabisa au ukamtaja kwa kun-ya au kabila ili asijulikane nani, kutokana na illa mbaya aliyonayo huyo aliyefichwa au kumtaja mtu kuwa kapokea kwake na hali hajapokea hadithi hiyo kutoka kwa huyo mtu .

[29]-ميزان الإعتدال2/659 mtu wa: 5227. Vile vile angalia Attahdhiib 3/476-8. (مكتبة الشاملة)

[30] -Angalia ميزان الإعتدال 2/ 609-14 , katajwa katika nambari 5044. (مكتبة الشاملة)

[31]- Kwani viungo vyote vilivyokuwa viwili viwili katika mwili wa mwanaadamu vinahesabiwa vina sifa ya kike.

[32] -Naylul Awtwaar Mujallad 1/ j2/188, Chapa 1 mwaka 1415H / 1995M. Daarul-Kutubil-ilmiyyah , Beirut-Lebnon.

– Vile vile amesema katika ukurasa huo: “Amesema Abu Daud:Ameipokea Aththaqafiy yaani Abdulwahhaab kutoka kwa Ubaydillah yaani Ibnu Umar ibn Hafswi wala hakuifikisha kwa Bwana Mtume (s.a.w) na hiyo ndio sahihi. Na vile vile ameipokea Allayth bni Saa’d na Ibnu Jurayj na Malik yaani Hawakuifikisha kwa Bwana mtume (s.a.w) –Mawquuf-.

[33]-Yaani hayo ayafanyayo ni kutoka kwa Mtume (s.a.w) au yanatokana na yeye mwenyewe Ibnu Umar (r.a)?

[34]-Juzuu 2/531 mtu wa 4728 المكتبة الشاملة .

– Vile vile Angalia Attahdhiib 10/321-2. Mtu wa:638 المكتبة الشاملة.

[35]-Miizaanul-i-itidaal 2/214, mtu wa :8897.المكتبة الشاملة

[36]-Attahdhiib 6/155 mtu : 356 .المكتبة الشاملة

-Angalia hadithi hiyo Imam Ali (k.w) anasema katika swala za fardhi kwa hivyo ina maana kwenye swala za sunna alikuwa hainui mikono.

[37] – Attahdhiib 5/197-8. Mtu wa:388 المكتبة الشاملة.

[38] -Mizaanul- i-itidaal 2/425-6 mtu wa: 4334. المكتبة الشاملة

[39] – Attahdhiib 9/332. Mtu wa :618 المكتبة الشاملة.

[40] – Miizanul-I-itidaal 2/539 mtu wa : 4767.المكتبة الشاملة.

[41]- Attahdhiib 8/194. Mtu wa :402. المكتبة الشاملة.

[42]-Miizanul –I-itidaal 3/365 Mtu wa : 6782.المكتبة الشاملة.

[43] – Attahdhiib 8/272. Mtu wa :553 المكتبة الشاملة.

[44] – J2/261- Chapa 1407H/1986ADدار الريان للتراث- القاهرة –

* Amesema Sh Assiyabiy:Na labda baadhi ya watu wamemevutiwa na kuathirika na kitabu –صفة صلاة النبي صلى الله عليه وسلم – cha Sheikh Albaaniy, ambaye ameweka ndani yake vipande vipande miongoni mwa hadithi hizi na hadithi nyengine, na katika jambo la kushangaza ni kuwa Sheikh Albaaniy ambaye anajulikana katika ufatiliaji wa kukosoa hadithi (zisizo sahihi) utamwona anajikalifisha – analazimisha – kwenye hadithi za kuinua na kufunga (mikono katika swala) kuzitafutia usahihi.

 

Published By Said Al Habsy

SEHEMU YA PILI:

HADITHI ZA KUFUNGA MIKONO

1- عَنْ وَائِل بن حُجْر(( أَنَّهُ رَأَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَفَعَ يَدَيْهِ حِيْنَ دَخَلَ فِي الصَّلاَةِ ، وَكَبَّرَ ثُمَّ الْتَحَفَ بِثَوْبِهِ ثُمَّ وَضَعَ الْيُمْنَى عَلَى الْيُسْرَى ، فَلَمَّا أَرَادَ أَنْ يَرْكَعَ أَخْرَجَ يَدَيْهِ ثُمَّ رَفَعَهُمَا وَكَبّرَ فَرَكَعَ ، فَلَمَّا قَالَ: سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ رَفَعَ يَدَيْهِ فَلَمَّا سَجَدَ ، سَجَدَ بَيْنَ كَفَّيْهِ)) رواه أحمد – مسلم وفي رواية لأحمد وأبي داود (( ثُمَّ وَضَعَ يَدَهُ الْيُمْنَى عَلَى كَفِّهِ الْيُسْرَى وَالرُّسْغِ وَالسَّاعِدِ )) قال الشوكاني الحديث أخرجه النسائي وابن حبان وابن خزيمة.

TAFSIRI :

1- Kutoka kwa Wail bnu Hujr yeye “Amemuona Mjumbe wa Allah ameinua mikono yake alipoingia ndani ya swala (alipoanza kuswali), na akaleta takbira (ihram), kisha akajizungushia nguo zake na kuweka mkono wa kulia juu ya kushoto, na alipotaka kurukuu aliitoa mikono yake (ndani ya nguo)kisha akaiinua na kukabir halafu akarukuu, na aliposemaسَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُakainua mikono yakena aliposujudu kasujudu baina ya viganja vyake viwili”.

Ameipokea Ahmad – Muslim. Na katika upokezi wa Ahmad na Abi Daud “Kisha akaweka mkono wake wa kulia juu ya kiganja chake cha kushoto na rasgh na said”.[45]

Amesema Imam Ashshawkaniy hadithi hii ameipokea Annasaiy na Ibnu Hibban na Ibnu Khuzaymah.

UCHAMBUZI

Hadithi hii ni dhaifu kwa sababu nyingi:

(1)-Mgongano wa matni yake, kwani baadhi yao wamepokea kwa kutaja kuinua mikono baada ya kuinua kichwa kutoka kwenye sijda, na wengine hawakutaja hivyo baada ya sijda na migongano katika hadithi ni dalili za udhaifu wake.

(2)-Mgongano katika kuifikisha hadithi kwa Bwana Mtume (s.a.w) na kwa Swahaba kwani mara imepokelewa musnad mara mursal [46].

(3)-Kuna mgongano juu ya jina la mpokezi wa hadithi hii kutoka kwa Wail bnu Hujr, kwani wamekhitilafiana juu yake inasemwa Alqamah bnu Wail na inasemwa Wail bnu Alqamah.

(4)-Amesema Ibnu Hajar katika Attahdhiib: “Alqamah hakusikia kutoka kwa baba yake) ”.[47]

(5)-Na katika sanadi yake yumo Hammam bnu Yahya, amesema Sheikh Mohammad bnu A’abid katika kitabu chake Alqawlul-Faaswil:[48]

“Ama wapokezi wengine wa hadithi hii hakuna anayetaka kuulizwa hali yake, ila Hammam bnu Yahya kwani juu yake kuna maneno, amesema Abu Haatim (huyo Hammam) ni thiqah lakini katika hifdhi yake kuna walakin, na amesema Ibnu Hanbal sijapata kumuona Yahya bnu Said ana rai mbaya juu ya yeyote yule kuliko juu ya Hajjaj na Ibnu Is-haaq na Hammam na hakuna anayeweza kumrudisha kwenye rai hiyo juu ya watu hao, na amesema Amru bnu Ali kwa hakika Yahya alikuwa haridhii hata kidogo juu ya hifdhi aliyokuwa nayo (Hammam) wala katika kitabu chake wala hakuwa akielezea hadithi zitokazo kwa Hammam” .[49]

Jee inabakia hadithi hii kuwa sahihi? Baada ya kuona aina za udhaifu ndani yake.

 -2وعن أبي حازم عن سهل بن سعد قال:” كَانَ النَّاسُ يُؤْمَرُوْنَ أَنْ يَضَعَ الرَّجُلُ الْيَدَ اليُمْنَى عَلَىذِرَاعِهِ الْيُسْرَى فِي الصَّلاَةِ “. قَالَ أَبُوْ حَازِمٍ ، وَلاَ أَعْلَمُهُ إِلاَّ يُنْمَى ذَلِكَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، رواه أحمد والبخاري.

TAFSIRI:

2-Kutoka kwa Abi Hazim kutoka kwa Sahlu bnu Sa’ad amesema: “Watu walikuwa wakiamrishwa aweke mtu mkono wa kulia juu ya dhiraa yake ya kushoto kwenye swala”. Amesema Abu Hazim: Wala sidhani amri hiyo isipokuwa inaashiria kuwa inatoka kwa Bwana Mtume (s.a.w).

Ameipokea Ahmad na Albukhariy.

UCHAMBUZI WA HADITHI

1-Amesema Sheikh Muhammad bnu A’abid: “Kwa hakika Addaaniy

amesema katika Almuwatwaa, hadithi hii ina illa, kwani hiyo ni dhana kutoka kwa Abi Hazim pale aliposema -لا أعلمه- , na amejibu Ibnu Hajar kwa kusema: “Kwa hakika lau ingalikuwa Aba Hazim hakusema – لا أعلمه – basi hadithi hiyo ingalikuwa na hukmu- المرفوع – , na kauli hiiinakamatana na kauli yake katika kitabu chake Alfat-h kuwa hukmu ya hadithi hiyo ni -الرفع-, kwani swahaba akisema tulikuwa tukiamrishwa, hapo inadhihirisha kuwa kauli hiyo inamrudia yule mwenye amri naye ni Bwana Mtume (s.a.w)”.

Na vile vile akasema: “Na amesema Abulhassan Addaaraqutniy na Alkhatwiib na Al-imam Abubakri Al-ismailiy na wengine haiwezi kuwa hukmu yake niMarfuubali ni Mawquufwala haizidi hapo, na wamesema Umma wa wanavyuoni wa hadithi na Mafuqahaa na wajuzi wa elimu ya usuli, ikiwa hajaunganisha maneno yake na wakati wa Bwana Mtume (s.a.w) basi hadithi hiyo si Marfuu, na akiunganisha akasema tulikuwa tunafanya katika uhai wa Bwana Mtume (s.a.w) au katika zama zake au mbele yake na mfano wa hayo basi hadithi hiyo itakuwa hukmu yake niMarfuu, na hii ndio kauli sahihi amesema Imam Annawawiy kwenye sherhe ya Imam Muslim.

Na kutokana na kauli hiyo hadithi hii haiwi Marfuu[50],hata kama asingalikuwa na shaka Abu Hazim seuze alikuwa na shaka, na ndio maana akasema Alhafidh Abu Amru bni Abdulbar katika kitabu التقصىkuwa: “Athari hii ni Mawquuf[51]kwa Sahl wala haizidi hapo”.

Na akasema: “Hakika mpokezi wa hadithi akisema kinyume na kile alichopokea hiyo inajulisha juu ya kufutwa (hukumu hiyo) kwani hakuna sababu ya kumfanya asifuate alichopokea isipokuwa ni hiyo (yaani kufutwa hukumu hiyo), na hapa miongoni mwa mfano huo ni hadithi ya kufunga mikono -katika swala- yaani imepokelewa kutoka kwa Sahl ameipokea Imam (Malik) kwenye Muwattwaa na baada yake wakaipokea Albukhariy na Muslim, pamoja na hayo akasema (Imam Malik) katika kitabu chake Almudawwanah kuwa kufunga mikono ni makruhi na kupendelea kuiachia (wakati wa kusali) na kitabu cha Almudawwanah kimekuja baada ya Almuwattwaa katika kutungwa”.

Hivyo basi tunaona jinsi zilivyojengeka sababu za udhaifu juu ya hadithi hii, hadi ikawa haiwezekani kutolewa hoja, wala dalili haitimii kwa kutumia hadithi hiyo, basi vipi itolewe dalili kwa hadithi iliyozungukwa na udhaifu? Tena katika amali ya Ibada nayo ni swala ambayo kila mtu huchunga ili aitekeleze itakiwavyo katika njia ya usahihi.

3-وعن ابن مسعود :(( أَنَّهُ كَانَ يُصَلِّي فَوَضَعَ يَدَهُ الْيُسْرَى عَلَى الْيُمْنَى ، فَرَءَاهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم فَوَضَعَ يَدَهُ اليُمْنَى عَلَى اليُسْرَى)) رواه أبوداود والنسائي وابن ماجة.

TAFSIRI :

3-Kutoka kwa Ibnu Masoud yeye ((Alikuwa anasali akaweka mkono wake wakushoto juu ya kulia, Bwana Mtume (s.a.w) akamuona akauweka mkono wake wakulia juu ya kushoto)) Ameipokea Abu Daud na Annasaaiy na Ibnu Majah.

UCHAMBUZI WA HADITHI

Amesema Imam Ashshawkaniy katika mlango huu imepokewa kutoka kwa Jabir kwa njia ya Ahmad na Addaaraqutniy na vile vile kwenye upokezi wa Addaaraqutniy ipo hadithi ya Ibnu Masoud.

Na hadithi zote hizo zimepitia katika njia ya Alhajjaj bnu Abi Zaynab, amesema Alhafidh Adhdhahabiy katika Almiizaan: “Amesema Ahmad ninakhofia kuwa dhaifu wa hadithi, na amesema Ibnu Mudiiniy ni dhaifu, na amesema Annasaaiy: Alhajjaj si mtu madhubuti (katika hadithi), na kasema Addaaraqutniy: yeye (yaani alhajjaj) si mtu madhubuti wala mwenye hifdhi”.[52]

Na katika upokezi wa Ahmad na Addaaraqutniy yumo Abdulrahman bnu Is-haaq Alwaasitwiy Alkuufiy amesema Imam Annawawiy kwenye sherhe ya Imam Muslim: Mtu huyo ni dhaifu kwa Ittifaaq[53] (makubaliano ya wanavyuoni wa elimu ya hadithi), na kasema Adhdhahabiy katika Almiizaan:“Wengi wamemdhoofisha, amesema Abu Twalib nilimuuliza Ahmad bnu Hanbal kuhusu mtu huyo akasema hana lolote ana hadithi za kuchukiza ( kupingwa), na amepokea Abdullahi bnu Ahmad bnu Hanbal kutoka kwa baba yake amesema huyo (Abdulrahman bnu Is-haaq Alwaasitwiy Alkuufiy) ana hadithi za kupingwa (kuchukiza) wala hastahiki kitu katika upokezi wa hadithi, na amepokea Abbaas kutoka kwa Yahya kuwa ni dhaifu na mara nyengine kasema ni mwenye kuachwa, na amepokea Muawiya bnu Salih kutoka kwa Yahya Alkuufiy kuwa huyo ni dhaifu, na kasema Albukhariy فيه نظر kuwa mtu huyo anahitaji uchunguzi, na amesema Annasaaiy na wengine kuwa ni dhaifu”[54].

Amesema Sheikh Muhammad bnu A’abid katika kitabu القول الفصلkuhusu kauli ya Albukhariy aliposema فيه نظرyaani anahitajia uchunguzi: “Wamekubaliana ya kuwa Albukhariy hasemi neno hilo isipokuwa kwa yule aliye dhaifu kwa watu wote”.

Hizi ndizo kauli za wanavyuoni wa hadithi juu ya hadithi hii, inatosha wao kuwa ni hoja ya kuidhoofisha hadithi hii.

4-وعن علي رضي الله عنه قال :(( إِنَّ مِنَ السُّـنَةِ فِي الصَّلاَةِ وَضْعَ اْلأَكُفِّ عَلَى اْلأَكُفِّ تَحْتَ السُّرَّةِ )) رواه أحمد – أبو داود – وأخرجه البيهقي والدارقطني وفي سنده عبدالرحمن بن إسحاق الواسطي وقد تقدم القول فيه أنه ضعيف باتفاق.

TAFSIRI :

4-Kutoka kwa Ali (r.a) amesema:

“Hakika katika sunna kwenye swala ni kuweka kiganja juu ya kiganja chini ya kitovu”. Ameipokea Ahmad – Abu Daud – vile vile Albayhaqiy na Addaaraqutniy.

UCHAMBUZI WA HADITHI

Katika sanadi ya hadithi hii yumo Abdulrahman bnu Is-haaq Alwaasitwiy na tumetangulia kumuelezea udhaifu wake kwa makubaliano ya wanachuoni wa hadithi.

Na mtunzi wa kitabu cha Albuluughul-maraam hakutaja hadithi inayozungumzia kufunga mikono isipokuwa hadithi moja tu nayo ni ya Waail bnu Hujr ambayo tumeitaja na tumeielezea huko nyuma .. na katika mlango huu zipo hadithi nyengine zinasemwa kuwa zinafika ishirini zimepokewa kwa njia ya masahaba kumi na nane, na amezichambua Sheikh mwanachuoni Muhammad A’abid ndani ya kitabu chake madhubuti [ القول الفصل ] na kubainisha udhaifu wake na kutofaa kwake kuzitendea kazi au kuzitolea dalili ..[55]


[45] -Rasgh (ni maungio baina ya kiganja na mkono) na Saaid (baada ya maungio hadi kufikia kisugudi).

[46] -Musnad: Ni hadithi iliyoungana upokezi wake hadi kwa Bwana Mtume (s.a.w), na kauli nyengine ni hadithi iliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w) ikiwa imeungana au imekatika. – Mursal: Ni hadithi aliyoielezea Tabii na kuiunganisha hadi kwa Bwana Mtume (s.a.w) bila ya kumtaja Sahaba aliyemsikia.

[47] – Attahdhiib 7/247. Mtu wa: 488. المكتبة الشاملة.

[48] – Uk :5

[49] -Angalia Attahdhiib 11/60-61. Mtu wa: 108. المكتبة الشاملة.

[50]- Marfuu: Ni hadithi aliyoilezea Sahaba kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w).

[51] -Mawquuf: Ni kauli au kitendo kilichomalizia kwa Sahaba, mfano: aseme: “Tulikuwa tunafanya” bila ya kusema tunafanya wakati wa Bwana Mtume (s.a.w), au: “katika sunna ni hivi” au “tuliamrishwa” au “Tulikuwa tunaamrishwa” au “Tulikatazwa” au Tuliruhusiwa”. Na mfano wa hayo. –

[52]-Miizaanul I-itidaal 1/462 Mtu wa : 1736 المكتبة الشاملة.

-Vile vile anagalia Tahdhiib 2/177 Mtu wa: 372. المكتبة الشاملة

[53] – Sahihu Muslim Sherhe ya Imam Annawawiy Mujallad 2 juzuu 4/115

دار الفكر للطباعة والنشر والتوزيع 1401 هـ /1981 م

[54] -Miizaanul I-itidaal 2/548 mtu wa : 4812.المكتبة الشاملة

[55]-Anasema Sh Assiyaabiy: Na nimeangalia taaliq ya Muhammad Nasiruddiin Albaniy katika kitabuchake alichokiita kwa madai na uongo [صفة صلاة النبي صلى الله عليه وسلم] anakipinga kijitabu hiki akitolea hoja ya kuwa hadithi hizi- za kufunga na kuinua mikono katika swala- zimepokewa ndani ya sahihi Albukhariy na Muslim. Na hoja hiyo ni nyepesi kuliko hata uzi wa buibui, kwani Albaniy yeye mwenyewe amedhoofisha hadithi ziliomo ndani ya sahihi Albukhariy na Muslim, na jambo hilo kwake ni katika migongano (ya kauli ) yake ambayo anazingatiwa kuwa ni hodari na maarufu katika hilo, vile vile amepinga yale niliyoyanukuu kutoka kwa Adhdhahabiy kwenye kumsifia Azzuhriy kuwa ana sifa ya kudallis na katika hilo kuwa sikunukuu kauli ya Adhdhahabiy aliyosema في النادر, na amepitikiwa Albaniykwani mimisikukusudia kuleta tarjuma ya Azzuhriy bali nilitaka kuthibitisha ya tadlis tu si vyengine, na kusifika na kitu kunathibiti (kwa sifa hiyo) ikiwa ni chache au nyingi, na hakika waarabu wameweka sifa ya kupitilia mpaka (صيغة المبالغة ) ili kuonyesha wingi kutokana na uchache, ingalikuwa ni hivyo basi yule anayedanganya kidogo asingehesabiwa kuwa ni muongo na sema mfano kama huu katika vitu vyengine vyingi.

Na ikawa kazi yake kuwashambulia Maibadhi na hilo si geni kwake kwani kaishi maisha yake yote katika kutukana na kushambulia, na ufupisho wa maneno ni kuwa hiyo taaliiq aliyoweka ni ya kipuuzi inapelekea kicheko kutokana na yaliyomo ndani yake ambayo yanatokana na silka, sifa na tabia zao Alhashwiyyah.

 

Published By Said Al Habsy

HITIMISHO

Na kwa hivyo unaona ndugu msomaji, pupa ya Maibadhi ya kufanya amali kwa kufuata hadithi sahihi, na kuziacha kwao hadithi dhaifu, yote hayo kwa kuogopa kuingia katika onyo la Bwana Mtume (s.w.a) –aliposema- “Mwenye kunizulia kwa makusudi basi ajichagulie mwenyewe makazi yake motoni”[56], na wala haiwezekani wakakhalifu sunna za Bwana Mtume (s.a.w) kwani hakika Dhehebu la Ibadhi limeanza katika karne ya mwanzo Hijriya na viongozi wake wameishi wakati wa masahaba watukufu, kwa hivyo inaelekea zaidi kuwa wapo kwenye haki na usahihi.

Na inatakikana juu ya kila muislamu awache kufanya amali kwa kutumia hadithi dhaifu, na awe na pupa katika kufanya ibada zake kwa kutumia hadithi sahihi, kwani lengo la kufanya ibada si jengine isipokuwa kujilazimisha katika kufuata amri za Allah mtukufu, hivyo basi kuzidisha –chochote – ndani ya ibada ni sawa na kupunguza.

Na kuzidisha vitendo ndani ya swala kama kuinua na kufunga mikono na kusema Amin na kutikisa kidole –kwenye tahiyyatu- na vitendo vyengine, kwa lengo la kujikurubisha kwa Allah Mtukufu kwa kutegemea hadithi dhaifu, kufanya hivyo si lolote isipokuwa kama mfano wa mwenye kusema: “Ametaka faida akapoteza rasli mali”.

Shukrani zote ni za Allah juu ya tawfiiq.

{Ewe Mola wetu tumeamini kile ulichokiteremsha na tumemfuata Mjumbe basi tujaaliye na sisi tuwe pamoja na wenye kushuhudia}.

Na rehma za Allah na amani ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad na watu wa nyumba yake na masahaba.

___________________________

Ndugu yenu katika uislamu
Nassor Mohammed Majid Al-ismailiy
Dar-es-salaam Tanzania.

___________________________

MAREJEO YA VITABU:

1-الجامع الصحيح مسند الإمام الربيع بن حبيب ابن عمر الأزدي البصري ، إعداد سعود بن عبدالله الوهيبي ، مكتبة مسقط 1414هـ 1994م، ج1

2-صحيح مسلم شرح الإمام النووي ـ المجلد 2/ج4 / ـ دار الفكري للطباعة والنشر والتوزيع ـ 1401 هـ / 1981 م

3-Sunani Abi Daud – juzuu 1/المكتبة الشاملة ط 3 –

4- Subula ssalaam -J2/ .المكتبة الشاملة ط 3 –

5-Attaarikhul kabiir cha Imam Albukhary / Mujallad 2 qismu ththaaniy juzuu 1/ chapa ya Daarul-fikriy.

6- Tahdhiibu TTahdhib cha Ibnu Hajar aliyekufa 852 H, chapa Daaru Ihyaai tturaathil-Arabiy chapa ya 2 mwaka 1413HR/1993AD –JUZUU ya 1-3-5-6-9-10.

7 -شرح الجامع الصحيح مسند الإمام الربيع بن حبيب ابن عمر الأزدي البصري، ج1، المطابع الذهبية – روي ، مسقط، عمان

8-فتح الباري شرح صحيح البخاري ج1-ج2، ط1، 1404هـ – 1986م- دار الريان للتراث – القاهرة-

9-Naylul Awtwaar Mujallad 1/ j2, Chapa 1 mwaka 1415H / 1995M. Daarul-Kutubil-ilmiyyah, Beirut-Lebnon

10- – نتوير المقياس من تفسير ابن عباس- لأبي طاهر محمد بن يعقوب الفيروزابادي ، دار الحيل بيروت لبنان.

11 -Musnad Imam Ahmad, Juzuu ya 2. (مكتبة الشاملة)

12-Sunanu Attirmidhiy, Juzuu ya 2. (مكتبة الشاملة)

13-Sunanu Annasaaiy, Juzuu ya 1.(مكتبة الشاملة)

14- Sunanu Addaaramiy, Juzuu ya 1.. (مكتبة الشاملة)

15- ميزان الإعتدال، للذهبي، ج1- ج2-ج3 -ج4،(مكتبة الشاملة)

16- Sunanul kubra lilBayhaqiy: J2.. (مكتبة الشاملة)

25-Mizaanul- i-itidaal 2/425-6 mtu wa: 4334. المكتبة الشاملة .

26-Attahdhiib Juzuu-2-3-5-6-7-8-9-10-11.المكتبة الشاملة.

30-Sheikh Mohammad bnu A’abid katika kitabu chake Alqawlul-Faaswil.

__________________________

[56] -فتح الباري شح صحيح البخاري ج1/244 الحديث:110 ، ط1، 1404هـ – 1986م- دار الريان للتراث – القاهرة

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here