Home All JAWABU KWA MAWABABI

JAWABU KWA MAWABABI

514
0
Accordion Content

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

1. FATAWA ZA MASHEIKH WETU – 1
Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad pamoja na Aali zake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya Malipo.

Ama baada ya hayo.

Kwa hakika Allah anatutaka tuwe waadilifu kwa kila hali, na sisi Waislamu -hata kama tuko na tofauti kimadhehebu- tunatakiwa tusipindukie mipaka katika tofauti zetu; kwani tukija tukifanya hivyo tutajikuta tunafanyiana uadui na kuuana sisi kwa sisi baina ya safu zetu.

Ibadhi ni Madhehebu kama yalivyo Madhehebu mengine ya Kiislamu; kwa hiyo Ibadhi ina mafundisho ya kiitikadi (Aqidah) na kimatendo (Fiqhi) na kitabia (Akhlaaq), nayo ni mafundisho yaliyochukuliwa kupitia dalili sahihi za kisheria.

Maibadhi tumekinaika kidalili kuwa mafundisho yetu ni sahihi, nayo ndiyo haki aliyokuja nayo Mtume wa Allah Muhammad (s.a.w), na sote tunajuwa kuwa Allah mtukufu ametufafanulia wazi kwenye Kitabu chake kwa kutuambia:

((فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ فَأَنَّى تُصْرَفُونَ))

((Basi kuna nini baada ya haki isipokuwa upotevu?!!, basi vipi munageuzwa?!!))

[Younus 32]

Kwa maana hiyo ni Haki yetu -Ibadhi- kuitakidi kuwa yale yaliyotafautiana na mafundisho ya Ibadhi katika masaa-ilu diini (Itikadi) -kuwa hayo- hayatakuwa isipokuwa ni upotevu tu, -na aumie katika hilo yule atakayeumia- kwa sababu mafundisho yetu hayakujengwa katika msingi wa kuridhisha watu, bali yamejengwa katika msingi wa kuikusudia Haki aliyokuja nayo Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ili kufikia katika maridhio ya Allah mtukufu aliyetuumba; sisi hatuna shaka kuwa kila Madhehebu yanaitiakdi kuwa mafundisho yake ndiyo haki na yale yaliyotafautiana nayo ni batili, au ndio tuseme kuwa hao wanaojiita Masalafi -ambao ndio wanaochukua bendera ya kushambulia Ibadhi- wanaitakidi kuwa wasiokuwa na Itikadi yao wako katika haki?!!

Kwa hivyo kuitakidi Maimamu wa Kiibadhi na kutoa Fatwa za kuonesha uhaki wa mafundisho ya Ibadhi kiitikadi, na kuwa mafundisho yaliyotafautiana na mafundisho ya Ibadhi kiitikadi ni batili, kufanya hivyo ni haki yao wala sio doa aslan, wala hawawezi kulaumiwa katika hilo kama tutakavyoona baadae.

IBADHI HAWAACHI UADILIFU

Bila shaka msomaji anaefuatilia fatwa za Masheikh wa Kiibadhi kamwe hataweza kuona ndani yake uchochezi wa kuwafanyia uadui na ugaidi wale waliotafautiana na mafundisho ya Ibadhi, huwezi kukuta katika safu za Maimamu wa Kiibadhi fatawa chinjachinja za kuhimiza umwagaji damu na uuaji ovyo kwa sababu ya tofauti za kimisimamo au kimafundisho katika Dini yetu ya Uislamu, kutokana na hapo tunakutia fatwa zote walizotunakulia Masalafi hazivuuki mipaka ya kuitakidi, hazina ndani yake ugaidi wa kuua na kuwafanyia uadui wenye kutofautiana na Ibadhi katika masuala ya kiitikadi au Kifiqhi au mengineo, na huwezi kukuta katika Tarehe ya Maibadhi kuwa walipigana vita na kuua watu kwa misingi ya kutofautiana kimadhehebu.

Tunawaambia Waislamu wote kwa ujumla, hebu tutazame kidogo mafundisho ya Maimamu wa Kisalafi dhidi ya waislamu waliotafautiana na wao katika misimamo na mafundisho:-

1. Mohamed bin Is-haaq bin Khuzaimah (223 – 311 Hijiria):

Ndugu zangu huyu ni Imamu wa Maimamu wa Masalafi, anasema kuhusu wapinzani wake katika suala la Itikadi yao ya kumdhibiti Allah mtukufu kimipaka kama alivyotunakilia Ibnu Taimiyah Al-Harrani Al-Mujassim.

وَقَالَ مُحَمَّدُ بْنُ إسْحَاقَ بْنِ خُزَيْمَة إمَامُ الْأَئِمَّةِ: مَنْ لَمْ يَقُلْ إنَّ اللَّهَ فَوْقَ سَمَوَاتِهِ عَلَى عَرْشِهِ بَائِنٌ مِنْ خَلْقِهِ وَجَبَ أَنْ يُسْتَتَابَ فَإِنْ تَابَ وَإِلَّا ضُرِبَتْ عُنُقَهُ ثُمَّ أُلْقِيَ عَلَى مَزْبَلَةٍ لِئَلَّا يَتَأَذَّى بِرِيحِهِ أَهْلُ الْقِبْلَةِ وَلَا أَهْلُ الذِّمَّةِ ذَكَرَهُ عَنْهُ الْحَاكِمُ بِإِسْنَادِ صَحِيحٍ

Amesema Muhammad bin Is-haaq bin Khuzaimah Imamu wa Maimamu: ((Yoyote asiyekubali kusema kuwa Allah yuko juu ya mbingu zake, (amekaa kitako) juu ya Arshi yake, ameachana na viumbe wake (Yaani kuna masafa baina yake na viumbe wake), ni lazima atakiwe kutubia huyo, basi ima atubie, na kama hakutubia itakatwa shingo yake (chinjachinja) kisha atatupwa katika jaa la taka ili wasije wakaudhika kwa vundo (harufu mbaya) lake wana wa Kibla (Masalafi) na wana wa Dhima (Mayahudi na Manasara))). Ameitaja kutoka kwake Al-Hakim kwa sanadi sahihi.

Mwisho wa kunukuu Fatwa chinjachinja hii ya Imaamu wa Maimamu kwa Masalafi, Fatwa hii imefanywa nyimbo katika sehemu nyingi za vitabu vya Sheikh wa Uislamu wa Kisalafi Ibn Taymiyah. Rejea kitabu chake Majmuu Al-fatawa 5/52.

Sisi tunawapa ushindani hawa Masalafi wafanye upekuzi katika Ibadhi kisha watuletee fatwa uchochezi na chinjachinja kama hii kama wataipata.

2. Sheikh wa Uislamu wao Ibn Taimiyah Al-Harrani:

Huyu ni chinjachinja nambari moja anatuambia:

هذه الحشيشة الصلبة حرام سواء سكر منها أو لم يسكر والسكر منها حرام باتفاق المسلمين ومن استحل ذلك وزعم أنه حلال فإنه يستاتب فإن تاب وإلا قتل مرتدا لا يصلى عليه ولا يدفن في مقابر المسلمين

“Hakika hii tumbaku ngumu (ya kusokota) ni haramu, ni sawa inayolewesha au isiyolewesha, na kiliweshacho ni haramu kwa makubaliano ya Waislamu, na mwenye kuihalalisha hiyo (tumbaku) na akadai kuwa hiyo ni halali; kwa hakika huyo atatakiwa atubie, basi ima atubie na kama hakukubali kutubia atauliwa hali ya kuwa ameritadi, hasaliwi huyo wala hazikwi katika makaburi ya waislamu”.

Mwisho wa kunukuu Ibnu Taymiyah Fatawa Kubraa 3/423.

Ndugu zangu suala la kifiqhi la kula tumbaku, ikiwa hukukubaliana na Sheikh wa Uislamu wa Kisalafi basi ni kisu shingoni mwako.

Sheikh wa Uislamu wa Kisalafi Ibnu Taymiyah Al-Harrani Al-Mujassim anatunukulia kwa kuyakubali wazi wazi maneno haya:

من زعم أن الله لا يرى في الآخرة فقد كفر بالله وكذب بالقرآن ورد على الله أمره فيستتاب فإن تاب وإلا قتل

(Mwenye kuzua kuwa Allah haonekani Akhera basi huyo atakuwa amemkufuru Allah na ameikadhibisha Qur-aani na amemrudi Allah katika jambo lake, basi atatakiwa kutubia, ima atubie na kama akikataa atauliwa) [Bayaanu Talbiisi Jahamiyah 2/399, 4/457]

Na hii ndugu zangu ni mifano tu, lakini mafatwa chinjachinja kwa sababu za kutofautiana tu na wengine kwa hawa wanaojiita Masalafi ni kwa Makontena.

Na sisi katika sehemu hii -kwa yale yanayohusiana na Fatwa za Masheikh wetu ambazo wametunukulia hawa Masalafi- tunawambia: Hivi nyinyi itakudhuruni nini Itikadi ya Ibadhi huko Akhera ikiwa ni munaiitakidi kuwa ni itikadi batili?! Hivi munataka Imamu wa Kiibadhi aseme kuwa yeye yuko katika Batili?! Ajabu kubwa hii kutoka kwa hawa Masalafi.

MASALAFI NA UHARIBIFU WA MAANDIKO.

Ndugu zangu kuna kitu kinaitwa riwaya, yaani kuelezea kitu ikiwa ni tokeo au maneno, kuna riwaya kwa maana na kuna riwaya kwa kunakili kama ilivyo kwa muhusika wake, tunasoma vitabu vya Hadithi kama vile Sahihi Al-bukhari, Sahihi Muslaim, na Sunan Abu daudi, na Tirmidhi, na Nasaaii, na wengineo ambavyo ni vitabu mashuhuri sana kwa riwaya za hadithi za Mtume wetu Muhammad (s.a.w), navyo ni vitabu tegemewa katika madhehebu za Kisunni.

Na bila ya kurefusha, ni kuwa uhakika wa riwaya za vitabu hivyo ni mapokezi yaliyopita zaidi na daraja moja, yaani mwandishi wa Kitabu kasimulia aliyoyapata kutoka kwa fulani1, na huyu fulani1 pia anasimulia kutoka kwa fulani2, na mtiririko unakwenda namna hiyo mpaka kwa muhusika wa yaliyonukuliwa kutoka kwake ikiwa ni Mtume (s.a.w) au Sahaba au Tabiina, na asilimia kubwa ya riwaya hizo ni kwa njia ya kuelezea kimaana sio kunakili neno kwa neno.

Sasa hawa Masalafi -ambao hutegemea Dini ya Riwaya walizonakiliwa kutoka kwa waliopita- sisi huwashangaa sana tunapoona kutoka kwa kwao mwenendo wa kuvuruga riwaya, tabia ambayo haina daraja ya kuelezea kimaana aslan; kwani huwa wanatunukulia kutoka kitabuni kwa mujibu wa madai yao, lakini wao huwa wanakusudia kuvuruga kwa makusudi ili kufikia lengo lao, sasa vipi sisi tutaweza kukubali mapokezi ya Hadithi zao bila ya kuingiwa na shaka yoyote ya uwezekano wa kuchezewa asili ya riwaya hiyo?, au vipi tunaweza kukubali wanayotunakilia kutoka kwa wapinzani wao bila ya kuwa na shaka yoyote?!

Ikiwa hawa Masalafi wanatufikishia kimaandiko kutoka kwa Maibadhi kisha hawafanyi uadilifu wa riwaya yao ya kunakili, jambo ambalo wanalifanya kwa makusudi kwa lengo la kuuharibu uhakika, vipi isiwe haki kwetu kuchukua tahadhari kubwa sana katika riwaya zao zote?!!

Kwa hakika ni haki yetu kufanya hivyo kwani uhakika wao uko wazi kuwa amana ya kielimu hakuna kwao; kwa sababu tulitarajia kwa hawa Masalafi angalau wawe muadilifu wa kunakili maandiko ya Wanaelimu wetu kama yalivyo katika vitabu vyao lakini hilo pia limekuwa ni madaihewa kutoka kwao.

Kwa kweli wananikumbusha mara moja nilikuwa katika mjadala na mmoja wao, basi nikasema katika maneno yangu ((Usamehevu wa Allah ni haki ya kila mwenye kutubia, na asiyetubia mpaka yakamfika mauti hatakuwa na haki ya kusamehewa)) Basi yule Msalafi akasema: ((Hebu angalia vizuri ndugu haya ni maneno yako, mwenyewe unasema “Usamehevu wa Allah ni haki ya kila mwenye kutubia na asiyetubia” au kataa kama haya siyo maneno yako na hukuyasema)). Hapo nikashangaa sana kisha nikasema: Subhaana Allah, hivi kweli pana lengo dini kwa watu hawa au ni ushabiki tu? Kisha nikasema: Ikiwa hii ndiyo hali yao, basi vipi tutakuwa na yakini kuwa riwaya zilizopokewa na watangulizi wao hayakufanyika ndani yake haya haya na mfano wake kwa lengo la kunusuru batili yao?!!.

Huenda msomaji akasema kuwa hili ni tokeo la kawaida tu lililofanywa na wanafunzi wasiotegemewa katika uwanja wa kielimu kiuhakika, lakini uhakika sio hivyo na katika hili kuna ushahidi kwa kutosha.

Kuna Kitabu mashuhuri cha Hussein Bin Ghannaam naye Mwanafunzi wa Imamu wao hawa Masalafi Mohamed bin Abdilwahaab, Kitabu hichi kimeshapishwa chapa zaidi ya moja. Sasa tuangalie jinsi gani wanavyochezea maandiko ya vitabu, tuweze kujua uhakika wao hawa watu Allah awaongoe:

Chapaa ya kwanza ya Kitabu hichi ilichapishwa Misri mwaka 1368 Hijiria sawa na 1949 AD, na chapa hii iko juzuu mbili, Katika Juzuu ya pili ya chapa hii ukurasa wa 13 -14 kunaelezwa matokeo ya mwaka 1163 Hijiria, imekuja katika ukurasa wa 14 maneno haya:

فلما تحقق أهل الإسلام ما عزم عليه من ذلك المرام وأبرز الملك العلام لذوي الألباب من الأنام مصداق قوله (إن الله عزيز ذو انتقام) فتعاطى الأيمان على قتله من أهل التوحيد أناس أرادوا بذلك القربة وإراحة الناس وإزاحة ما عزم عليه من إيقاع النقمة والبأس ومن مشاهيرهم حمد بن راشد وإبراهيم بن زيد فأبطل الله بهم ذلك المكر والكيد، فلما انقضت صلاة الجمعة وخرج سرعان الناس مسرعين قتلوه في مسجده ومصلاه وأريح المسلمون من أذاهم

Sasa tukija katika chapa ya nne ya kitabu hichi hichi, nayo imechapishwaMisri na Lebanon mwaka 1415 Hijiria sawa na 1994 AD, nacho kiko Juzuu moja tu, tunalikutia tokeo hili hili limetajwa katika ukurasa wa 103 likielezwa hivi:

فلما تحقق أهل الإسلام ذلك تعاهد على قتله نفر منهم: حمد بن راشد، وإبراهيم بن زيد فلما انقضت صلاة الجمعة، قتلوه في مصلاه بالمسجد في رجب 1163 هـ

Nataraji hapa hapahitaji darubini la kupima sana, maandiko yako wazi kabisa, lau kuwa hii chapa ya nne ikaitwa ni Mukhtasari wa chapa ya kwanza ikawa ni kazi ya muwandishi mwengine ingekuwa kuna uadilifu nzuri, lakini sura hii tunayoiona, kwa hakika inatupa picha safi jinsi gani hawa Masalafi wanavyokusudia kugeuza maneno ya waandishi, na ikiwa hili ni kwa Kitabu hichi ambacho msomaji ikiwa atakisoma kwa chapa ya kwanza kisha akataka kukisoma tena kwa chapa ya nne bila shaka atajikuta yuko mbele ya kitabu chengine kabisa ambacho mfumo wa lugha baina yake na kile cha mwanzo ni tofauti kabisa. Na ikiwa hii ndiyo hali yao hawa Masalafi vipi Muislamu anapokea tu wanayoyaandika na kuyasema bila ya kuchukua hadhari kubwa kwa yanayotoka kwao?!!.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

2. FATAWA ZA MASHEIKH WETU – 2
Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Tukiwa tumo katika kuwajibu Masalafi kuhusu tuhuma zao batili dhidi ya Ibadhi ambazo wanazisambaza huku na huko.

Tunaingia katika fatawa walizotunukulia Masalafi kutoka kwa Wanavyuoni wetu wa Kiibadhi na kuzipa anuani ya fatawa mbovu za wanachuoni wa kiibadhi dhidi ya waislamu.

FAT`WA YA KWANZA:

Amesema Muandishi wa Kisalafi:

“Kwanza nitaanza na fat`wa ya Mwanachuoni wao aitwaye Jaad bin Khamis Al-Kharuusiy, iliyonukuliwa na Sheikh wa Kiibadhi Saalim Ibn Hamad Al-haarithiy katika kitabu chake “Al-Uquudu Al-Fidhiyyah fi Usuulil-Ibaadhiyyah” ukurasa wa 172. Sheikh Al-Haarithi anatunukulia swali aliloulizwa Sheikh Jaad na Jibu lake alilolitoa. Swali linasema hivi:

مسألة: سئل الشيخ جاعد بن خميس بن مبارك الخروصي – رحمه الله- عن ناشىء نشأ في طاعة الله تعالى، وهو من أهل الخلاف، إلا أنه لم يرتكب حرمة من محارم الله قط، وكان طول عمره زاهدا ناسكا، وفي ثواب الله راغبا، ولم يدع شيئا من أوامر الله تعالى إلا ائتمر به، ولا محجورا في دين الله إلا انتهى عنه، إلا أنه يدين بخلاف دين الإباضية قولا وعملا ونية واعتقادا ما حاله يكون إن مات على ذلك؟

“Aliulizwa Sheikh Jaaid Ibn Khamis Ibn Mubaraak Al-Kharuusiy kuhusu kijana aliyeinukia katika kumtii Allah, lakini msimamo wake ni kinyume (na msimamo wa Ibadhi) na kijana huyo hajawahi kufanya jambo lolote la haramu miongoni mwa aliyoyaharamisha Allah.

Umri wake wote alikuwa akifanya ibada, mwenye kuipa nyongo dunia, anatafuta malipo ya Akhera, hakuna amri katika amri za Allah ila ameitekeleza, wala hakuna makatazo ila ameyaacha, ISIPOKUWA KIJANA HUYO ANAFUATA DINI (MADHEHEBU) ILIYO KINYUME NA DINI YA KIIBADHI, KWA KAULI, VITENDO NA ITIKADI, JE, ITAKUWAJE HALI YAKE KAMA AKIFA KWENYE MSIMAMO HUO?)) Mwisho wa kunakili Ole wake….. uk. 125.

JAWABU YETU:

MOSI: Tunamuambia Sheikh huyu wa Kisalafi:

kwa hakika sisi tumerejea katika Kitabu husika ulichokitaja katika kitabu chako na katika ukurasa huo ulioutaja, lakini kwa bahati mbaya suali hilo ulilotunukulia hatukulikutia kwenye kitabu ulichotutajia.

Tufahamu ndugu zangu, kuwa mimi hapa ninabainisha kuwa amana ya kielimu kwa hawa watu haipo, na sisi tunasema wazi wazi kuwa Sheikh Saalim Al-haarithiy -Allah amridhie- hakutunakilia suali hilo kama alivodai muandishi wa Kisalafi -Allah amuongoe-. Tunamuambia muandishi wa Kitabu husika: Kwa hakika umemzulia Sheikh wetu Salim Al Harithi (r.a) kitu kisichokuwepo katika Kitabu chake “Al-Uquudu Al-Fidhiyyah fi Usuulil-Ibaadhiyyah”.

Ndugu zangu wasomaji, sisi hatukatai kuwa Sheikh Jaaid bin Khamis Al-kharuusi aliyefariki mwaka 1237 Hijiria -Allah awe radhi naye- aliulizwa suali hilo na jawabu akatoa, lakini hapa ninachokisema ni kuwa suali hilo hakulinakili Sheikh Al-haarithiy (r.a) katika Kitabu chake husika na katika ukurasa huo husika kama alivyodai muandishi wa Kisalafi, kwa hiyo nasema kuwa Sheikh wa Kisalafi amemnasibishia Sheikh Salim Al-haarithiy (r.a) yasiyohusika na Kitabu chake.

Na neno la Sheikh wa Kisalafi liko wazi kabisa katika hili halina doa amesema: ((Sheikh Al-Haarithi anatunukulia swali aliloulizwa Sheikh Jaaid na jibu lake alilolitoa.))

PILI: Ama kuhusu aliyoyaita Sheikh huyo wa Kisalafi kuwa ni Jawabu nayo ni:-

“قال العلامة الرباني المبارك جاعد بن خميس بن مبارك الخروصي : إني لأقسم بالله – قسم من بر في يمينه فلا حنث- أن من مات على الدين الإباضي الصحيح، غير ناكث لما عاهد الله عليه من قبل ولا مغير حقيقته، كلا ولا مبدل طريقته، أنه من السعداء، ومن أهل الجنة مع الأنبياء والأولياء، وإن مات على خلافه فليس له في الآخرة إلا النار وبئس المصير، لأنه الحق، وماذا بعد الحق إلا الضلال، فأنى تصرفون، على هذا – إن شاء الله – أحيا، وأموت عليه، وعليه ألقى الله رب العالمين. ولما توفي هذا الشيخ –رضي الله عنه- وضع نعشه منحرفا عن القبلة قبل أن يصلى عليه فاستدار إلى القبلة كرامة له.”

Amesema mwanachuoni mkubwa aliyebarikiwa, Jaaidu Ibn Khamis Ibn Mubarak Al-Kharusiy: “Mimi ninaapa kwa jina la Allah – kiapo cha mwenye kufanya wema kwenye kiapo chake bila ya kukivunja-:

Atakayekufa kwenye dini sahihi ya Uibadhi pasi na kuyachangua aliyomuahidi Allah kabla ya hapo, bila ya kubadili hakika yake wala kubadilisha njia yake, huyo ni katika watu wema, na ni katika watu wa peponi, na atakuwa pamoja na Manabii na Mawalii, NA KAMA (MTU HUYO) ATAKUFA KATIKA DINI NYINGINE ISIYOKUWA UIBADHI, BASI HATOPATA HUKO AKHERA ISIPOKUWA MOTO na marejeo mabaya kabisa ni huo moto, kwa sababu dini ya Uibadhi ndiyo dini ya haki. Na hakuna baada ya haki isipokuwa upotevu, basi wapi tena mnapogeuzwa! Inshaallah nitaishi juu ya msimamo huu na nitakufa nao, na msimamo huu ndio nitakutana na Mola wa walimwengu)). Mwisho wa kunukuu [Ole wake kila mzushi uk. 125-126]

JAWABU:

Tunasema: Maneno hayo kweli yamo katika kitabu hicho alichokitaja na katika ukurasa huo alioutaja, lakini hakuyaleta Sheikh wetu Salim Al-Harithi (r.a) kuwa ni jawabu ya suali kama anavyodai muandishi wa Kisalafi, nayo ni maneno aliyoyanukuu Sheikh Al-Harithi (r.a) katika kitabu chake hicho, na maneno hayo ni haki, wala hayana doa lolote, lakini tutamfanya nini Sheikh huyo wa Kisalafi?!

Hivi huyu Sheikh wa Kisalafi (Muwahabi) inaonesha hayajui waliyoandika Maulamaa wake kuhusiana na wale wasiokubaliana na Itikadi yao (Dini yao), kwa hiyo tunamuambia: Tukiongezea Fatwa za Imamu wa Maimamu wenu Ibnu Khuzaimah, tuangalie pia Fatwa zao kuhusiana na wasiokubali kuingia katika Usalafi (Uwahabi).

نشهد – ونحن علماء مكة، الواضعون خطوطنا، وأختامنا في هذا الرقيم – أن هذا الدين، الذي قام به الشيخ محمد بن عبد الوهاب، رحمه الله تعالى، ودعا إليه إمام المسلمين سعود بن عبد العزيز، من توحيد الله، ونفي الشرك، الذي ذكره في هذا الكتاب، أنه هو الحق الذي لا شك فيه ولا ريب، وأن ما وقع في مكة والمدينة، سابقا، ومصر والشام وغيرهما من البلاد إلى الآن، من أنواع الشرك المذكورة في هذا الكتاب، أنه: الكفر، المبيح للدم والمال والموجب للخلود في النار; ومن لم يدخل في هذا الدين، ويعمل به، ويوالي أهله، ويعادي أعداءه، فهو عندنا كافر بالله واليوم الآخر، وواجب على إمام المسلمين والمسلمين، جهاده وقتاله، حتى يتوب إلى الله مما هو عليه، ويعمل بهذا الدين.

((Tunashuhudia -na sisi ni Wanavyuoni wa Makka wenye kuweka maandishi yetu na mihuri yetu katika waraka huu- ya kuwa Dini hii ambayo amesimama nayo Sheikh Mohamed bin Abdilwahaabi -arehemewe na Allah mtukufu- na akailingania Imamu wa Waislamu Soud bin Abdilazizi, katika Tauhidi ya Allah na kukataa Ushirikina ambayo ameitaja katika kitabu hichi, ya kuwa hiyo ndiyo haki ambayo haina shaka ndani yake wala wasi wasi, na kuwa yote yaliyokuwa katika Makka na Madina hapo kabla na Misri na Shaam na nchi nyenginezo katika nchi zote mpaka hivi sasa katika aina za ushirkina zilizotajwa katika kitabu hichi yalivyo hasa (hayo yalikuwa) ni Ukafiri unaokubalisha kuua (Chinjachinja) na kuhodhi mali (Taifisha mali) na kulazimisha kubakia milele motoni, na yoyote asiyeingia katika Dini hii (Uwahabi) na kuifanyia kazi na kuwapenda watu wake na kuwachukia maadui zake basi huyo kwetu sisi ni mwenye kumkufuru Allah na siku ya mwisho na inalazimika kwa Imamu wa waislamu kumsimamishia jihadi mtu huyo na kupigana naye vita mpaka atubie kwa Allah mtukufu na afanyie kazi Dini hii)) [Duraru Saniyyah fi Ajiwabati Najjdiyah 1/314]

Jamani Fatawa zenye sura hiyo katika Kitabu hicho ni nyingi sana, yaani ima uwe muwahabi au wewe ni mshirkina tu, na maana yake utauliwa na mali yako itachukuliwa ngawira, na hayo wameyafanya, wameua watu kwa halaiki tena hadi Misikitini.

Kwa mfano:

Ameandika Sheikh Mwanafunzi wa Mohamed bin Abdilwahabi (Imamu wa Mawahabi) naye ni Hussein bin Ghannaam:-

لما تزايد شر عثمان بن معمر على أهل التوحيد (الوهابية السلفية) وظهر بغضه لهم وموالاته لأهل الباطل وتبين الشيخ محمد بن عبد الوهاب صدق ما كان يُرْوَى عنه

فلما تحقق أهل الإسلام ذلك تعاهد على قتله نفر منهم: حمد بن راشد، وإبراهيم بن زيد فلما انقضت صلاة الجمعة، قتلوه في مصلاه بالمسجد في رجب 1163 هـ

((Basi zilipoongezeka shari za Othman bin Mua bin Muammar kwa Wanatauhidi (Mawahabi Masalafi) na ikadhihiri chuki yake kwao na kuwapenda kwake Wanabatili (Waislamu wengine wasiokuwa Mawahabi) na ukabainika kwa Sheikh Mohamed bin Abdilwahabi ukweli wa yaliyokuwa yakielezwa kutoka kwake….

Basi Waislamu (Mawahabi Masalafi) walipolihakikisha hilo walipeana ahadi ya kumuua kundi katika wao: Hamed bin Rashid, na Ibrahim bin Zaid, basi ilipomaliza sala ya Ijumaa, walimuua katika msala wake Msikitini katika mwezi wa Rajab mwaka wa 1163 Hijiria)). [Taarikhu Najdi uk. 103].

Kwa hiyo hizo ni Fatawa tegemewa katika safu zao, zinatuambia ikiwa wewe hukuwa Msalafi basi wewe utakuwa umemkufuru Allah na Siku ya mwisho tena damu yako na mali yako ni halali kwao, tena ni lazima kwa kiongozi wa waislamu kukusimamishia jihadi na kupigana na wewe, na kuwa wewe ni kuni ya moto wa Jahannamu milele.

Na fatawa hazikutoshelezika hapo tu, bali zinatuambia kuwa kabla ya Ulinganio wa Mohamed bin Abdilwahabi hakukuwa na waislamu katika miji yote ya Waislamu, yaani watu wote walikuwa washirkina na kila asiyekubali dini yake basi huyo ni Mshirkina.

Tunamuambia Muandishi wa Kisalafi (Muwahabi):

Mbona anakicheka Kabanzi kilichoko kwenye jicho la mwenzake anasahau kuwa katika Jicho lake kuna Jiti la Mkarambati!!!

Kwa hiyo sisi Maibadhi tunamshukuru Allah mtukufu kwa taufiqi yake kuwa Masheikh wetu hawakufikia kuwatoa wafuasi wa Madhehebu nyengine nje ya Uislamu kwa sababu ya kutofautiana na Ibadhi katika mafundisho na misimamo, Fatawa za Masheikh wetu katika mlango huu hazikupindukia mipaka ya kuitakidi bila ya kuhalalisha damu na mali za wengine, na sisi tunaitakidi kuwa Ibadhi katika mafundisho yake na misimamo yake -katika yenye makubaliano katika safu zao- kuwa hayo ndiyo haki, tena hili haatuna shaka nalo hasa hasa katika yote yaliyoingiwa na tofauti za Kiitikadi, na Masheikh wetu wanaitakidi hivyo bila ya shaka yoyote, na hakuna baada ya haki isipokuwa upotevu kama alivyotuambia Allah mtukufu, na mimi nitawaongeza -hawa Masalafi- neno la Mwanaelimu wetu Mchamungu Sheikh Abu Muslim Salim bin Udaim Al-bahlaaniy (r.a) amesema akiwasifu Maamiri Al-muuminina wa Kiibadhi (r.a) waliohukumu Oman kwa mfumo wa Shuura kama Abu bakar Siddiqi (r.a) na Omar Al-faaruq (r.a), neema ambayo hatujaikuta kuwa nayo isipokuwa Ibadhi peke yao katika Historia nzima wa Waislamu.

لا يقبل الله دينا غير دينهم * ولا يصح الهدى إلا بما دانوا

((Haikubali Allah dini isiyokuwa dini yao * na hauwi sahihi uongofu isipokuwa kwa waliyoitakidi.))

Ikiwa linawaumiza hili liwaumize sana. Dini ya Ibadhi (Itikadi) ndiyo haki yakinifu katika Uislamu kwa mwenye kuutaka ukweli basi huu ndio ukweli.

ZINDUO MUHIMU SANA.

Ndugu zangu wasomaji, tunatakiwa tufahamu kuwa kila wahusika wa Madhehebu au fani ya elimu huwa na Istilahati zao, sasa mwenye kusoma vitabu vya Madhehebu fulani au fani fulani anatakiwa aziheshimu Istilihaati za Madhehebu au fani yenye kuhusika na maandiko anayoyasoma, kinyume na hivyo atajikuta anabeba ufahamu usiokusudiwa, na hili ni jambo muhimu sana la kumuepusha msomaji na kosa la kuyachukua maandiko ya Madhehebu yasiyokuwa yake kisha akayafahamu kwa Istihaati za Madhehebu yake anayoitakidi au Madhehebu mengine yoyote yasiyokuwa Madhehebu ya maandiko husika.

Kwa mafano:

Katika Ibadhi Shahaada ya kuingia katika Uislamu inaitwa Jumla, sasa ikiwa mtu hajui Istilahi hiyo kisha anachukua kitabu katika vitabu vya wanaelimu wa Kiibadhi anamkuta akilitaja neno hilo, kisha yeye analifahamu kwa maana ya Jumla ya Kinahau si utakuwa ni mtihani huo?!!
Katika Ibadhi neno kufru kiistilaahi ni kila kosa kubwa lolote, kwa hiyo anaweza mja akawa kafiri lakini asiwe mshirikina, hata kama mshirikina pia ni kafiri kwa kuzingatia kuwa yumo katika kosa la ushirikina ambalo ni miongoni mwa makosa makubwa. Sasa atakuja mtu anasoma kitabu anakuta Sheikh wa Kiibadhi kwa mfano anasema: “Atakayekunywa pombe amekufuru”. Kisha msomaji huyo akaruka akisema tizama Maibadhi hawa wanaitakidi kuwa mwenye kunywa pombe ni Mshirikina. Masikini hajijui kuwa anaharibu kusudio la andiko kwa sababu ya kulifahamu kwake neno -alilolisema Sheikh wa Kiibadhi- kwa ufahamu wa Istilahi ya Kisunni na Kikhawariji kuwa ukafiri ni ushirikina tu.
Sasa haya ni moja ya matatizo aliyonayo Sheikh wa Kisalafi aliyenukuu maandiko ya Maibadhi, hata akafikia kusema ((CHINI YA KIVULI CHA KUFURU NEEMA.)) neno linaloonyesha kujihukumia kwa watu kwa asiyoyafahamu kutoka kwao.

Tizameni ndugu zangu anayoyasema muandishi wa Kiwahabi angalieni niliyoyapigia msitari chini:
((ISIPOKUWA KIJANA HUYO ANAFUATA DINI (MADHEHEBU) ILIYO KINYUME NA DINI YA KIIBADHI, KWA KAULI, VITENDO NA ITIKADI, JE, ITAKUWAJE HALI YAKE KAMA AKIFA KWENYE MSIMAMO HUO?)) Mwisho wa kunakili uk. 125.

Muandishi wa Kisalafi amesema katika ufafanuzi wa hili:

((Pili: Tumeuona msimamo wa Ibadhi dhidi ya Waislamu wasiokuwa Ibadhi, maadamu wasi si Ibadhi, ni Mashafi, au Mahnbali n.k basi Akhera hawatapata Jazaa yoyote isipokuwa moto wa milele!)) mwisho wa kunukuu Uk. 126

JAWABU

Tunamuambia Muandishi wa Kisalafi: Ulikuwa ukubali kidogo kukaa darasani kwa Sheikh wa Kiibadhi kabla ya kusoma maandiko yao.

Kwani sisi Maibadhi katika mafundisho yetu tunaitakidi kuwa Masuala ya Uislamu yamegawika katika aina mbili kuu:-

1. Masuala ya Diini

2. Masuala ya Rai.

Na mafundisho yetu katika chuo cha Ibadhi yanatuambia kuwa:

لا يجوز الاختلاف في مسائل الدين

((Haifai kuwepo tofauti katika Masuala ya Dini))

Kwa hiyo huyu muandishi alikuwa asome japo kidogo ISTILAHAATI ZA KIIBADHI.

Tunasema: Wanaelimu wetu wa Kiibadhi wanapozungumza neno DINI YA UIBADHI huwa kusudio la neno hilo ni yale Masuala yasiyokubali kuingiwa na khilafu za kirai ndani yake, nayo yanajulikana kwetu kuwa hayo ni masuala yaliyothibiti kwa maandiko ya sheria kwa njia ya yakini (andiko safi la Aya ya Qur-ani, au Hadithi mutawatiri, au lazimisho la kiakili), na ili uweze kufahamu ndugu msomaji tazama kidogo anavyosema Imam Nuurudiini Asaalimiy (r.a) alipokuwa akifafanua moja ya masuala katika masuala ya kiitikadi yaliyoingiwa na khilafu ndani yake, nayo ni kama ilivyo katika kitabu chake Mashaaqi Al-Anwaar katika ufafanuzi wa suali.

((Jee! aliyeuliwa amekufa kwa ajali yake?))

Kuhusiana na suala hilo, ni maarufu kuwa Muutazila wanasema kuwa aliyeuliwa hakufa kwa ajali yake, bali atakuwa ima:

Amedhulumiwa umri wake uliobakia ikiwa ameuliwa kwa njia ya batili, au
Ametiwa adabu kama ni kwa njia ya haki itakuwa kama mtu kutozwa faini katika mali yake.
Baasi Sheikh Al-Imam Nurudiini Assaalimiy (r.a) baada ya kufafanua suala hilo akasema neno hili:

أقول وهذه المسألة وإن ظهر بطلان قول المعتزلة فيها لعدم الدليل الشاهد لدعواهم ليست من المسائل الدينية التي يفسق بها من خالف فيها

((Nasema: Na suala hili hata kama ubatili wa neno la Muutazila uko wazi ndani yake kwa kutokuwepo dalili yenye ushahidi wa madai yao, lakini si katika MASAAILU DIINIYAH ambayo huingizwa katika ufasiki yule atakaye kwenda kinyume nayo…..))

Tunawambia hawa Masalafi kuwa sisi Ibadhi katika mafundisho yetu tunasema kwa Madhehebu nne za Kisunni

1. Hanafi.

2. Maliki.

3. Shaafii.

4. Hanmbali.

Hizo ni katika Madhehebu za Fiqhi, na Madhehebu za Kifiqhi zote ni Madhehebu za Kirai.

Kwa hiyo tunawambia acheni kuchanganya madawa enyi Masalafi, kwani kufanya hivyo kunakuvunjieni uadilifu kwa wenye kufahamu, na kama mulikuwa humujui basi tumeshawaekeeni wazi.

Tuangalie tena hapa mfano mwengine wa wazi:

Katika Masaili Diini kwetu sisi Ibadhi, ni kuitakidi Al-Baraa-a kwa kila Fasiki ni sawa akiwa ni Muibadhi au si Muibadhi, akiwa ni Sahaba au si Sahaba.

Ikiwa Masalafi wanatukhalifu katika hili basi tunaitakidi kuwa wameikhalifu haki, kwa hiyo hili ni suala la Diini kwetu sisi Ibadhi.

Lakini tukija kwa mfano suala ya kuhusisha baadhi ya Masahaba (r.a) katika hukumu ya Baraa-a, suala ambalo Masalafi wanapenda sana kuwashambulia Ibadhi kidhulma kwa sababu yake:

Nalo ni suala la kumuweka Aliy au Othman au Muawiyah au Amru bin Al-aasi katika hukumu ya Baraa-a.

Suala hili kwetu sisi si katika Suala la Dini, kutokana na hapo hakulazimiki kwa Muibadhi kuitakidi Baraa-a kwa Sahaba yoyote katika hao, bali ni haramu kwake kumuweka yoyote katika hao au yoyote yule katika Al-baraa-a isipokuwa kama itambainikia bila ya shaka kuwa alikufa akiwa fasiki.

Nasema: Mimi ni Muibadhi lau kuwa itanibainikia kuwa Abu bakar Al-Siddiqi (r.a) alikufa akiwa ni fasiki basi hakutakuwa na nafasi kwangu isipokuwa kumuweka Sahaba huyo katika hukumu ya Baraa-a, kwani mafundisho ya Ibadhi yanatuambia kuwa mazingatio katika hukumu ya Walaa-aya ni Uchamungu sio nasabu wala usharifu, na mazingatio katika hukumu ya Baraa-a ni Ufasiki na sio jengine lolote.

Anasema mwanafikra wa Kiibadhi Khalid Al-Wehebi katika kitabu chake Ash-raatu Saati:

مسألة التفاضل بين الصحابة ليست من مسائل الدين على الإطلاق ولا يتعلق بها عمل ولا اعتقاد، وهي وليدة صراعات السياسة، وما ورد فيها من مرويات لا يمكن التحاكم إليها لكثرة التناقضات فيها ولوجود الشبهة الكبيرة في ضلوع السياسة في توظيفها

((Mas-ala ya kufadhilisha baina ya Masahaba si katika masaa-ilu diini hata mara moja, wala hayafungamani na tendo wala itikadi, nayo ni mazalio ya mivutano ya kisiasa, na yaliyopokewa ndani yake katika mapokezi haiwezekani kuyafanya kuwa ni suluhisho kwa sababu ya kupingana pingana kuliomo ndani yake, na kwa kuwepo utata mkubwa wa kuwa siasa imehusika katika uenezi wake)).

Kwa hiyo Shiekh Jaaidi Al-kharuusi (h.a) kiapo chake kinahusika na Masuala ya Dini (Itikadi) tu, na kila sehemu utakayosoma katika vitabu vya Ibadhi ukaona Diini ya Uibadhi unapaswa ujue kuwa inahusiana na Masuala ya Kiitikadi tu peke yake.

Na sisi tunasema wazi wazi, hivi itamfaa nini mwenye kuumaliza umri wake katika Ibada lakini kumbe itikadi yake ni batili, kwa mfano anaabudu Allah huku akimuitakidi kuwa anasifika kwa sifa kamili za mtu wa kinuru amezungukwa na sehemu tena anaitakidi kuwa yuko mbinguni?. Si tutasema tu kuwa uhakika wake mtu huyo anaabudu sanamu lililoko mbinguni kifikra, ikifika siku ya Kiama ataambiwa nenda ukachukue malipo yako kwa uliyekuwa ukimuabudu, huna malipo hapa leo.

Na lau kuwa ibada nyingi inafaa mbele ya Allah, basi Makhawariji watakuwa wa mwanzo kuingia Peponi au munasemaje enyi Masalafi? Au munapinga hadithi nyingi zinazoshuhudia kuwa wao ni wingi wa Ibada.

Halafu tunarudia tena kwa Masalafi na kuwaambia: Hivi nyinyi munadhurika nini kwa Itikadi isiyokuhukumuni kwa hukumu za chinjachinja na isiyokunyimeni uhuru wenu wa kuabudu na kuishi vizuri katika Jamii, ikiwa munaiona sio sahihi haitowadhuru kitu, au nyinyi munaitakidi kuwa huko Akhera Maibadhi ndiwo watakaokuwa mahakimu wa kuhukumu waja?!!!.

Lakini angalieni Fatawa Ugaidi za Maimamu wenu ambazo zinawataka Jihadi zenu ziwe dhibi ya Wanakibla wote waliotafautiana na nyinyi Kiitikadi, na matokeo yake mukawa ni rahisi kutumiliwa kwa maslaha ya Maadui wa Waislamu na Uislamu; kwani wao wakitaka sehemu yoyote kuichafua basi nyinyi ni kupewa Ishara tu, na hapo mutakuwa tayari kukata vichwa vya Masufi na Maash-ari na Maibadhi na Mashia na Mazaidiya na kila aliyetafautiana na nyinyi katika mlango wa Asmaau wa Sifaati kama alivyosema Ibn Khuzaimah, Allah amlipe kwa anayosathiki na walivyosema Maimamu wenu tegemewa kutokea Najidi kama tulivyonukuu.

Tazameni ndugu wasomaji Fat`wa ugaidi, fatwa chinjachinja hii, tena wanazo nyingi sana mfano wa fatwa hii ndugu zangu, lakini kila kitu kina wakati wake:

Amesema Muhammad bin Is-haaq bin Khuzaimah: ((Yule asiyesema (asiyeitakidi): Hakika Allah yuko juu ya mbingu zake juu ya Arshi yake ameachana na viumbe wake (Yaani kuna masafa baina yake na viumbe wake), ni lazima atakiwe kutubia, basi ima atubie na kama hakutubia itakatwa shingo yake kisha atatupwa katika jaa la taka ili wasije wakaudhika wana wa Kibla (Masalafi) na wana wa Dhima (Mayahudi na Manasara))).

Fatwa hii ameisimulia Ibn Taymiyah Rejea kitabu chake Majmuu Al-fatawa 5/52.

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Tukiwa tumo katika kuwajibu Masalafi kuhusu tuhuma zao batili dhidi ya Ibadhi ambazo wanazisambaza huku na huko.

Tunaingia katika suala la KARAMA ZA MASHAIKH

Amesema Sheikh wa Kisalafi katika maandiko yake akitoa tarjuma ya maneno ya Sheikh Al-haarithii (r.a):

ولما توفي هذا الشيخ رضي الله عنه- وضع نعشه منحرفا عن القبلة قبل أن يصلى عليه فاستدار إلى القبلة كرامة له.”

((Kisha akasema Al-Haarithiy: Alipofariki huyu Sheikh –radhiya llaahu an`hu- kabla ya kusaliwa, jeneza lake waliliweka kinyume na kibala (waliuelekeza uso wake upande usiokuwa wa kibala) akajigeuza mwenyewe kuelekea kibala kwa sababu ya karama”!!!)) Mwisho wa kunukuu uk. Ole wake kila mzushi 125-126

JAWABU:

Namuambia, kwanza tulitaraji utoe tarajuma nzuri, na sio tarajuma ya kupotosha, kwani tarjuma yako inatuonesha kuwa Sheiikh Raiiis Jaaid Al-haruusi -Allah awe radhi naye- alijigeuza yeye mwenyewe; kwani uso wake ulielekezwa upande usiokuwa wa Kibla, na lililo sahihi ni kuwa Jeneza ndilo lililogeuka likajiweka sawa upande wa kibla bila ya Sheikh kutikisika.

Tunasema kuwambia hawa Masalafi: Sasa kuna ajabu gani katika hilo? Sheikh Al-Imam amekirimiwa kwa kuwekwa sawa jeneza lake, ni nani waliohusika na uwekaji sawa huo? Sisi hatujui, Allah ndiye anayejua, lakini hilo ni jambo linalowezekana, na kwa sababu sio jambo la kuzoeleka ndio likasemwa kuwa ni Karama.

Kisha tunawambia hawa Masalafi kuwa sisi Ibadhi hatukatai karama za Masheikh Wachamungu kwani hayo ni katika yanayowezekana kiakili, lakini hatuzifanyi Karama za Masheikh kuwa ni Hoja katika Dini, nasi tunaitakidi kuwa karama kubwa zaidi ni Mja kufa akiwa mchamungu, hakuna karama inayoshinda hiyo katika mafundisho ya Kiibadhi, na neno la Maulamaa wetu ni maarufu katika hilo:

الكرامة هي الموت على الاستقامة

Halafu tunawambia hawa Masalafi kuwa kama hamujui kuwa Maimamu wenu wamedaiwa pia kuwa walikuwa na Makarama basi angalieni haya:

Ibn Qayyim Al-jauziyyah munayemlakib kwa (Shamsudiiin) na ambaye ni mwanafunzi wa Sheikh Al-Islamu wenu Ibn Taimiyah Al-harraani, anaelezea haya:

لَقَدْ شَاهَدْتُ مِنْ فِرَاسَةِ شَيْخِ الْإِسْلَامِ ابْنِ تَيْمِيَّةَ – رَحِمَهُ اللَّهُ – أُمُورًا عَجِيبَةً. وَمَا لَمْ أُشَاهِدْهُ مِنْهَا أَعْظَمُ وَأَعْظَمُ. وَوَقَائِعُ فِرَاسَتِهِ تَسْتَدْعِي سِفْرًا ضَخْمًا. أَخْبَرَ أَصْحَابَهُ بِدُخُولِ التَّتَارِ الشَّامَ سَنَةَ تِسْعٍ وَتِسْعِينَ وَسِتِّمِائَةٍ، وَأَنَّ جُيُوشَ الْمُسْلِمِينَ تُكْسَرُ، وَأَنَّ دِمَشْقَ لَا يَكُونُ بِهَا قَتْلٌ عَامٌّ وَلَا سَبْيٌ عَامٌّ، وَأَنَّ كَلَبَ الْجَيْشِ وَحِدَّتَهُ فِي الْأَمْوَالِ. وَهَذَا قَبْلَ أَنْ يَهُمَّ التَّتَارُ بِالْحَرَكَةِ. ثُمَّ أَخْبَرَ النَّاسَ وَالْأُمَرَاءَ سَنَةَ اثْنَتَيْنِ وَسَبْعِمِائَةٍ لَمَّا تَحَرَّكَ التَّتَارُ وَقَصَدُوا الشَّامَ: أَنَّ الدَّائِرَةَ وَالْهَزِيمَةَ عَلَيْهِمْ. وَأَنَّ الظَّفَرَ وَالنَّصْرَ لِلْمُسْلِمِينَ. وَأَقْسَمَ عَلَى ذَلِكَ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ يَمِينًا. فَيُقَالُ لَهُ: قُلْ إِنْ شَاءَ اللَّهُ. فَيَقُولُ: إِنْ شَاءَ اللَّهُ تَحْقِيقًا لَا تَعْلِيقًاوَسَمِعْتُهُ يَقُولُ ذَلِكَ. قَالَ: فَلَمَّا أَكْثَرُوا عَلَيَّقُلْتُ: لَا تُكْثِرُوا. كَتَبَ اللَّهُ تَعَالَى فِي اللَّوْحِ الْمَحْفُوظِ. أَنَّهُمْ مَهْزُومُونَ فِي هَذِهِ الْكَرَّةِ. وَأَنَّ النَّصْرَ لِجُيُوشِ الْإِسْلَامِ.

(Kwa hakika nimeshuhudia katika uoni wa ndani wa Sheikh wa Uislamu Ibnu Taymiyah –amrehemu Allah- mambo ya ajabu, na ambayo sikuyashuhudia katika hayo ni makubwa zaidi na makuu zaidi, na matokeo ya uoni wake wa ndani yanataka kitabu kikubwa:

 1. Aliwambia watu wake kuingia kwa Matatari katika Shaam katika mwaka wa mia sita na tisiini na tisa (696 Hj), na kuwa majeshi ya Waislamu yatavunjwa, na kuwa Demeshqi hakutakuwa na kupigana mwaka mzima wala sabyu (utekaji wa watoto na wanawake kwa sababu ya vita) muda wa mwaka, na kuwa makali ya jeshi na ujasiri wake utakuwa katika mali, na haya ni kabla ya kuazimia Matatari kufanya harakati.
 2. Kisha akawambia watu na viongozi katika mwaka wa mia saba na mbili (702) wakati Matatari walipoikusudia Shaam: Kwa hakika njama na kushindwa ni dhidi yao, na kuwa kufanikiwa na ushindi ni kwa Waislamu, na akaapa juu ya hilo zaidi ya viapo sabiini, basi iliambiwa: Sema Akitaka Allah. Basi akawa anasema: Akitaka Allah kwa kuhakikisha na si kwa kuegemeza. Na nimeyasikia hayo. Amesema: Basi walipozidisha kwangu nikasema: Musizidishe ameshaandika Allah mtukufu katika Lauhi Al-Mahfuudhi ya kuwa wao ni wenye kushindwa katika duru hii, na kuwa ushindi ni kwa majeshi ya Uislamu. Alisema: Basi nikawaonjesha baadhi ya viongozi na majeshi utamu wa ushindi kabla ya kutoka kwao kwa kukutana na adui.) [Ibnu Qayyim – Madariju Saalikina 2/458]

Sasa sijui ni lipi kubwa zaidi kati ya haya mawili?!

 1. Kueleza Sheikh wa Uislamu wa Kisalafi mambo ya Ghaibu tena kwa viapo zaidi ya sabiini
 2. Kukirimiwa Mwanachuoni mwanahaki wa Kiibadhi kwa kusawazishwa jeneza lake muelekeo wa Kibla.

Mbona Sheikh wa Kisalafi (Muwahabi) anakicheka Kabanzi kilichoko kwenye jicho la mwenzake anasahau kuwa katika Jicho lake kuna Jiti la Mkarambati!!!

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu, na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Tukiwa bado tumo katika kuwajibu Masalafi kuhusu tuhuma zao batili dhidi ya Ibadhi ambazo wanazisambaza huku na huko.

Tunaingia katika fatawa walizotunukulia Masalafi kutoka kwa Wanavyuoni wetu wa Kiibadhi na kuzipa anuani ya fatawa mbovu za wanachuoni wa kiibadhi dhidi ya waislamu.

FAT`WA YA PILI:

Muandishi wa Kisalafi akaendelea kuleta katika Kitabu chake (OLE WAKE…) Fatwa ya pili, nayo ni Fatwa ya Mwanachuoni wetu Sheikh Ahmad bin Maddaad Annaibi (r.a), huyu ni mwanachuoni aliyeishi Oman katika arne ya kumi Hirijia sawa na karna ya Kumi na saba Miladi.

Ameandika Muandishi wa Kisalafi akileta suali aliloulizwa Sheikh Ahmed (r.a):

“Sheikh unasaemaje kuhusu watu wa madhehebu nyingine ambao si Ibadhi? Je, itafaa kuwakosoa na kuwatia kwenye upotevu? Na je, itafaa kuwalaani? Na kama tutawalaani, je udhu wa mwenye kufanya hivyo utachanguka? Sheikh Ahmad bin Midaad akaajibu kwa kusema:

نعم جائز ذلك ، ولا ينتقض وضوء من فعل ذلك ، إذ هو قال الحق ، والصواب والصدق ، لأن جميع مخالفينا من المذاهب هم عندنا هالكون ، محدثون في الدين مبتدعون ، كافرون كفر نعمة ، منافقون ظالمون ، يشهد بذلك كتاب الله ، وسنة رسوله محمد – صلى الله عليه وسلم – وإجماع المسلمين. وندين لله تعالى ونعتقد أن دين الأباضي هو دين الله تعالى ، ودين رسوله ، وإن من خالف الدين الإباضي فهو في النار قطعا، بذلك نشهد وندين لله تعالى ، وإن من مات على الدين الأباضي فهو في الجنة قطعا بذلك ندين ، وأن من شك في الدين الأباضي وزعم أن الحق في غير الدين الأباضي فهو عندنا كافر كفر نعمة فاسق ، منافق مبتدع ، محدث في الدين… الخ”

“Naam, litafaa hilo (la kuwalaani) na hautachanguka udhu wa mwenye kufanya hivyo, kwa sababu atakuwa amesema haki, ukweli na sawa, KWA SABABU WATU WOTE WALIOTOFAUTIANA NA SISI KATIKA MADHEHEBU WAMEANGAMIA, WAMEZUSHA KATIKA DINI NA NI WATU WA BID`A NI MAKAFIRI WALIOKUFURU NEEMA NI WANAFIKI TENA MADHALIMU. Hilo linashuhudiwa na kitabu cha Allah na Sunna za Mtume wake Muhammad swalla llaahu alayhi wasallam na maafikiano ya Waislamu. Tunamuabudu Allah na kuitakidi kuwa dini ya kiibadhi ndiyo dini ya Allah na ndiyo dini ya Mtume wake swalla llahu alayhi wasallam. YOYOTE ATAKAYETOFAUTIANA NA IBADHI HAPANA SHAKA YOYOTE KUWA HUYO NI MTU WA MOTONI! sisi tunashuhudia kwamba atakayekufa akiwa kwenye dini ya Uibadhi huyo ni peponi bila ya shaka. NA ATAKAYEITILIA SHAKA DINI YA KIIBADHI, AKADAI KWAMBA HAKI IKO KWENYE DINI NYINGINE ISIYOKUWA YA KIIBADHI, HUYO KWETU NI KAFIRI ALIYEKUFURU NEEMA, TENA FASIKI, MNAFIKI, MZUSHI ALIYEZUA KATIKA DINI…”

Kisha baada ya hapo Muandishi wa Kisalafi akaingia katika kumfanyia shere Sheikh wetu Juma bin Mohamed Al-Mazrui Allah amuhifadhi kwa kusema:

“Ingelikuwa elimu ni kujibizana kihuni, na mimi ningesema: Enyi Makhawariji nyie, mbona vitabu vyenu vinanuka Tumbaku namna hii? Kama alivyosema Juma.” Nalaka zake [ Ole wake…. 128-129]

JAWABU YETU:

Kiasili Fatwa hii ni sahihi kutoka kwa Sheikh wetu Ahmad bin Maddaad (r.a), na usahihi wake hasa ni kwa kuzingatia haya yafuatayo.

Fatwa hii imenukuliwa na Sheikh Said bin Bashiir Asubhi (r.a) naye ni mwanachuoni wa karne ya kumi na mbili Hijiria -alifariki mwaka wa 1159 Hijiria- bila ya ziada isemayo:

“ومن خالف الدين الإباضي فقد خالف دين الله، وإن مات على غير الدين الإباضي فهو في النار قطعا بذلك نشهد وندين”

“Na mwenye kwenda kinyume na Dini (Itikadi) ya Kiibadhi basi huyo atakuwa amekwena kinyume na Dini (Itikadi) ya Allah, na atakayekufa katika isiyokuwa Dini (Itikadi) ya kiibadhi basi huyo ni katika moto bila shaka, kwa hilo tunashuhudia na tunaitakidi”

Pia Fatwa hiyo ya Sheikh Ahmed Bin Maddaad (r.a) imenukuliwa na Sheikh Muhanna Al-Busaidi (r.a) naye ni mwanachuoni wa karne ya kumi na tatu Hijiria -alifariki mwaka wa 1250 Hijiria- bila ya ziada isemayo:

((إن من خالف الدين الإباضي فهو في النار قطعا بذلك نشهد وندين لله تعالى. وإن من مات على الدين الأباضي فهو في الجنة قطعا بذلك ندين))

((Na atakaye kwenda kinyume na Dini (Itikadi) ya Kiibadhi basi huyo ni katika Moto bila ya shaka, kwa hilo tunashuhudia na tunaitakidi kwa ajili ya Allah mtukufu. Na kwa hakika atakayekufa akiwa kwenye Dini (Itikadi) ya Uibadhi huyo ni Peponi bila ya shaka, kwa hilo tunaitakidi.))

Kutokana na kuwepo tofauti hiyo tutainukuu Fatwa ya Sheikh Ahmed Maddaad (r.a) bila ya kuingiza maneno hayo waliyotofautiana Masheikh walioinukuu Fatwa hii, tunafanya hivo ili tuwemo katika mapokezi yenye makubaliano baina ya Masheikh wawili waliyotunukulia Fatwa hii, na kuacha waliyotafautiana ndani yake, kwa hiyo nitaweka Tarjuma sahihi ya Fatwa yenye makubaliano, kwa sababu ni wazi kuwa Muandishi wa Kiwahabi alikusudia:

 1. Upotoshaji wa kukusudia katika nakala yake kwa kuichomekea waliyotofautaina wale waliotunakilia Fatwa hii.
 2. Kutoa tafsiri ya kupotosha maana katika sehemu nyengine za Fatwa hii.

Basi sisi tutarekebisha mule alimokosea, pia tutaondosha ziada zenye tofauti ndani yake. kwa hiyo Fatwa hiyo ni kama hivi ifuatavyo:

“Naam, litafaa hilo (la kuwakosoa na kuwatia kwenye upotevu na kuwalaani) na hautachanguka udhu wa mwenye kufanya hivyo; kwa sababu atakuwa amesema haki, ukweli, na sawa.

KWA SABABU WOTE WALIOTOFAUTIANA NA SISI KATIKA MADHEHEBU NYENGINE HAO KWETU SISI WAMEANGAMIA, WAMEZUSHA KATIKA DINI, NI WATU WA BID`A, NI MAKAFIRI UKAFIRI WA NEEMA, NI WANAFIKI, NI MADHALIMU, Hilo linashuhudiwa na kitabu cha Allah na Sunna za Mtume wake Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- na maafikiano ya Waislamu.

Tunamuabudu Allah na kuitakidi kuwa Dini (Itikadi) ya Kiibadhi ndiyo dini (Itikadi) ya Allah na ndiyo dini (Itikadi) ya Mtume wake swalla llahu alayhi wasallam.

NA HAKIKA ATAKAYEITILIA SHAKA DINI (ITIKADI) YA KIIBADHI, AKADAI KWAMBA HAKI IKO KWENYE DINI (ITIKADI) NYINGINE ISIYOKUWA YA KIIBADHI, HUYO KWETU ATAKUWA NI KAFIRI UKAFIRI WA NEEMA, NI FASIKI, NI MNAFIKI, NI MZUSHI ALIYEZUA KATIKA DINI”. Mwisho wa Fatwa.

Ndugu msomaji, ukifuatilia haya na yale aliyoyaleta Muandishi wa Kisalafi utagundua kuwa katika maandiko yake:

 1. Kuna upotoshaji wa kukusudia wa malengwa ya Sheikh Ahmed bin Maddaad (r.a).
 2. Pia muandishi wa Kisalafi ameweka na kuchomekea ziada walizotofautiana ndani yake Masheikh waliotunukulia fatwa hii.

Tunarudia na kusema kuwa: Fatwa hii ni sahihi wala haina doa lolote, nayo ni fatwa inayokamatana na usahihi wa Itikadi ya Kiibadhi katika masuala yaliyoingiwa na tofauti za kiitikadi ndani yake baina ya makundi ya Waislamu; kwani masuala hayo ndiyo yaliyodhibitiwa kwa majina na kupelekea kukapatikana:-

 1. Itikadi ya Kiibadhi.
 2. Itikadi ya Kisalafi.
 3. Itikadi ya Kiash-ari.
 4. Itikadi ya Kimaturidi.
 5. Itikadi ya Kijahamia.
 6. Itikadi ya Kishia.
 7. Itikadi ya Kimuutazilah.
 8. Itikadi ya Kikhawariji.
 9. Itikadi ya Kijabria.
 10. Itikadi ya Kimurjia.

Na bila shaka yule ambaye ataitakidi itikadi isiyokuwa ya Kiibadhi basi huyo atakuwa amepotea ikiwa haki iko kwa Maibadhi, hili halina shaka yoyote ndani yake ilinashuhudiwa na Kitabu cha Allah:

فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ

((Na nini baada ya haki isipokuwa upotevu tu?!))

[Younus 32] 

na

وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

((Na wenye kufuata njia isiyokuwa ya Waumini basi tutamuelekeza alikoelekea na tutamfikisha Jahannamu nayo ni mafikio mabaya sana))

[Nisaa 115]

pia linashuhudiwa na Sunna ya Mtume (s.a.w):

((Umati wangu utagawika makundi sabiini na tatu yote ni motoni isipokuwa moja litaokoka)).

Kwa maana hiyo, ni haki kwa Sheikh wa Kiibadhi kumuingiza -Kiitikadi- yule aliye kinyume na Itikadi ya Kiibadhi katika hukumu ya udhalimu na ufasiki na ukafiri wa kufru neema nayo ni hukumu inayohusiana na unafiki, na katika hili kuna dalili ya wazi kuwa huyo aliyetafautiana na Dini ya Kiibadhi -kwa mujibu wa Dini ya Kiibadhi- ni Muislamu aliyemo katika Madhambi makubwa bila ya kumtoa nje ya Mila ya Kiislamu, na ikiwa hizo ndizo sifa zake basi kiuhakika atakuwa ni mwenye kustahiki laana Duniani na Akhera kwa mujibu wa Qur-ani na Sunna; kwani laana ni kwa Madhalimu na Mafasiki wote.

Sasa -ndugu zangu- katika hili hakuna la kushangaza hata kidogo; kwa sababu Fatwa ya Sheikh wetu haijafungua mlango wa kumfanyia uadui muislamu aliyetafautiana na Ibadhi kwa sababu ya tafauti yake tu.

Lakini -ndugu zangu- yenye kushangaza hasa ni yale yaliyomo katika fatwa potofu na chinjachinja za Maimamu wa Kiwahabi mfano wa hizi hapa chini:-

 1. Kutoka kwa Malik (Malik bin Anas Imamu wa Wamaliki) ya kuwa aliambiwa: Hakika wao wanasema kuwa Allah haonekani. Basi akasema: (Upanga upanga) [Ibnu Taymiyah Bayanu Talbiisi Jahamiyah 4/45] Inaonekana wazi -kwa mujibu wa Fatwa hii- ikiwa wewe hukukubali Itikadi ya Kisalafi ya Mungu wa kuonekana kwa macho basi hukumu yako ni kukatwa kichwa tu, tena kwa kuhimizwa haraka sana leteni upanga leteni uapanga tukate vichwa.
 2. Amesema Malik bin Anas (Imamu wa Wamaliki): (Mwenye kusema Qur-ani ni kiumbe atatakiwa kutubia, ima atubie na akikataa itakatwa shingo yake.) [Sharhu Usulu Itikadi Ahali Sunna 2/346 Hadithi no 495]. Na katika Hadithi no 496 ya Kitabu hicho hicho Malik bin Anas (Imamu wa Wamaliki) anamuambia Abullahi bin Nafii baada ya kumpa habari kuwa Iraqi kuna watu wanasema Qur-ani ni kiumbe: “Ewe Abdullahi bin Nafii umepata wapi maneno haya?! Umeingiza katika moyo wangu kitu nacho ni Ukafiri, mwenye kusema maneno haya auliwe wala asitakiwe kutubia”. Ndugu zangu, Malik bin Anas (Imamu wa Wamaliki) amepishana na Abu Hanifa (Imamu wa Mahanafi) kiumri kwa miaka 13 tu, Abu Hanifa alizaliwa mwaka wa 80 Hijiria na Malik alizaliwa mwaka wa 93 Hijiria. Abu Hanifa aliishi Iraqi na Malik aliishi Madina. Maliki hapa anatoa Fatwa ya kuuliwa mwenye kusema Qur-ani ni kiumbe, na maelezo ni kuwa watu hao wako Iraqi, na vitabu vya Mawahabi (Salafi) vinatueleza kwa riwaya nyingi sana kuwa mtu wa kwanza kusema Qur-ani ni kiumbe ni Abu Hanifa (Imamu wa Mahanafi).
 3. Tusomeni Fatwa yengine ya ajabu ya Imamu wao mkubwa anayejulikana kwa umaarufu kwa la Al-Barbahaari, naye ni Hassan bin Aliy bin Khalaf Al-Barbahari aliyefariki mwaka wa 329 Hijiria. Imamu huyu kasoma kwa wanafunzi wa Ahmed bin Hanmbal, Sheikh huyu anatupa fatwa za ajabu katika Kitabu chake (Sharhu Sunna), anasema kuhusu Kitabu chake hicho:

فرحم الله عبداً ورحم والديه قرأ هذا الكتاب وبثه وعمل به ودعا إليه واحتج به، فإنه دين الله ودين رسول الله صلى الله عليه وسلم، فإنه من استحل فأنه من انتحل شيئا خلاف ما في هذا الكتاب فإنه ليس يدين لله بدين ، وقد رده كله ، كما لو أن عبدا آمن بجميع ما قال الله تعالى إلا أنه شك في حرف فقد رد جميع ما قال الله تعالى وهو كافر

((Basi amrehemu Allah mja -na awarehemu wazazi wake wawili- kwa kukisoma Kitabu hichi na akakitangaza na akakifanyia kazi na akakilingania na akakitolea hoja, kwani hicho (Kitabu chake Sharhu Sunna) ndio Dini ya Allah na Dini ya Mtume wa Allah, na yalivyo hasa yoyote atakayeitakidi kitu kinyume na yaliyomo katika Kitabu hichi (Kitabu chake Sharhu Sunna) basi yeye huyo hamuabudu Allah kwa dini, naye atakuwa ameirejesha (dini) yote, kama ilivyokuwa mja ameyaamini yote aliyoyasema Allah mtukufu isipokuwa yeye ametia shaka katika herufi moja tu, basi atakuwa ameyarejesha yote aliyoyasema Allah mtukufu hali ya kuwa ni Kafiri)). [Sharhu Sunna 103]

Jamani hiyo ndio habari ya Masalafi (Mawahabi), kitabu hichi ni sawa sawa na Qur-ani tukufu kwa mujibu wa Fatwa hiyo, basi ukirejesha au ukitilia shaka herufi moja tu ya Kitabu cha Al Barbahari (Sharhu Sunna) basi wewe ni sawa na ulierejesha Qur-ani yote, tena isitoshe kitabu hicho ni maandiko ya kuyatangazwa na kuyafanyia kazi kutolea hoja hasa, yaani sawa na Qur-ani. (Astaghfirullahi).

Tena Al Barbahari kabla ya hapo amesema:

واعلموا رحمكم الله أن أصول البدع أربعة أبواب: انشعب من هذه الأربعة اثنان وسبعون هوى، ثم يصير كل واحد من البدع يتشعب، حتى تصير كلها إلى ألفين وثمانمائة مقالة، وكلها ضلالة، وكلها في النار إلا واحدة، وهو من آمن بما في هذا الكتاب، واعتقده من غير ريبة في قلبه ولا شكوك، فهو صاحب سنة، وهو الناجي إن شاء الله.

((Na mujue -Allah akurehemuni- ya kuwa misingi ya Bidaa ni minne, yametawanyika kutokana na hii minne mapendwamoyo sabiini na mbili, kisha kila moja miongoni mwa Bidaa ikagawika, mpaka zikafikia zote maneno elfu mbili na mia nane, na zote ni upotevu, na zote ni katika Moto isipokuwa moja tu, nalo ni mwenye kuamini yaliyomo katika Kitabu hichi (Sharhu Sunna) na akayaitakidi bila ya chembe ya wasi wasi katika moyo wake wala shaka yoyote, basi huyo ndiye mtu wa sunna, na yeye ndiye mwenye kuokoka apendapo Allah)) [Sharhu Sunna uk. 101-102]

Jamani Al Barabahari Imamu mkubwa wa Kiwahabi (Salafi) wa karne ya nne Hijiria kashamaliza mambo yote, kwani Kitabu chake ni kuliko Qur-ani kwa mujibu wa fatwa yake hiyo, na mimi hapa sina haja ya kutaja ya ajabu yaliyomo katika Kitabu chake hicho, basi nakutajieni hapa fatwa moja tu ya ajabu iliyomo katika Kitabu chake hicho, anatuambia.

واعلم أن من قال لفظي بالقرآن مخلوق فهو مبتدع ومن سكت فلم يقل مخلوق ولا غير مخلوق فهو جهمي هكذا قال أحمد بن حنبل

“Na ujue kuwa mwenye kusema matamko yangu ya Qur-ani ni kiumbe basi huyo ni mtu wa bidaa, na mwenye kunyamaza asiseme kuwa (Matamko yanayosomewa Qur-ani) ni kiumbe au sio kiumbe basi huyo ni Mjahamia, hamna hivi amesema Ahmed bin Hambal.” [Sharhu Sunna uk. 95]

Jamani tusisahau kuwa ukirejesha au ukitilia shaka herufi yoyote ya fatwa hiyo basi wewe kushakuwa Kafiri sawa na uliyerejesha herufi ya Qur-ani tukufu.

Fatwa inatuambia matamko ya waja wanaposoma Qur-ani sio kiumbe, na ukisema kinyume na hivo basi wewe ni mtu wa bidaa motoni, na ukinyamaza usiseme kitu basi wewe ni Mjahamia, na Mjahamia kwa mujibu wa kitabu chake hichi si Muislamu kabisa, na dalili yake ni kasema Ahmed bin Hambal, sasa sijui Ahmed bin Hambal alikuwa ni Mtume baada ya Muhammad (s.a.w) hata maneno yake yawe dalili?!!!.

Ndugu zangu, tujue kuwa Bukhari na Muslim imethibiti kuwa wao walikuwa wakisema matamko yao ya kusoma Qur-ani ni kiumbe, kwa hiyo kwa mujibu wa Muheshimiwa Msalafi Imamu Al-Barabahari mtunzi wa Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake atakuwa Bukhari na Muslim ni watu wa Bidaa, na kama tulivyoona kwa mujibu wa Fatwa ya Imamu Al-Barbahari kuwa watu wa Bidaa wote ni Motoni.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad pamoja na jamaa zake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Tumefikiwa na hujuma batili kutoka kwa Masalafi kudai kwao kuwa Ibadhi wanatukana Masahaba kwani baadhi ya Wanavyuoni wamefanya hivyo, la kama Maibadhi hawakubaliani na hilo itawalazimu wawakufurishe Wanavyuoni hao; kwani mwenye kutukana Sahaba ni Kafiri si Muislamu.

Tunawambia kuwa sisi tumebainisha kuhusu suala hili, basi tunaweza kurejea maudhui hii kwa kufuata kiunganishi hapa pia hapa.

Ama kuhusu lazimisho wanalojaribu kutulazimisha nalo, tunawambia kuwa sisi tunawataka kwanza walazimike nalo wao wenyewe, kwa sababu tunakutia katika Hadithi sahihi upande wao kuwa baadhi ya Masahaba wakitukana Masahaba wengine kwa mfano:

Katika Silsila ya Hadithi sahihi cha Mwanahadithi wao anayeitwa Al-Albani katika Juzuu ya 5 Ukurasa 18-19 aipokua akizungumzia riwaya ya 2008 inayosema ((Muuaji wa Ammaar na mporaji wake ni katika moto)) akasema: Na (hadithi hii) inayo njia yengine: Amesema Imam Ahmad (4/198) na Ibnu Saad katika “Twabaqaati” (3/260-261) na muweko ni kutoka kwake: Ametupa habari Othman bin Muslim amesema: Ametupa habari Hammaad bin Salamah amesema: Ametupa habari: Abu Hafsi na Kulthumu bin Jubair kutoka kwa Abu Ghaadiyah amesema: “Nilimsikia Ammaar bin Yaasir anamsema vibaya Othman anamtukana hapo Madina, akasema: Basi nikamuahidi kumuua nikasema: Akinimakisha Allah kwako kwa hakika nitalifanya, basi ilipokua siku ya Siffan akawa Ammaar anawapiga watu na hapo ikasemwa: Huyu Ammaar…..)) Ninasema (msemaji ni Albani): Na sanadi hii ni sahihi na watu wake ni waaminifu ni watu wa Muslim, na Abu Al-Ghaadiyah ni Al-Juhanii naye ni Sahaba kama walivolithibitisha hilo wengi……

Hayo ndiyo yaliyomo katika Kitabu hicho, kwa hiyo Masalafi walazimike na hukumu yao kwa Sahaba Ammaar bin Yaasir R.A au walizimike na Manhaj yao kuwa wanavyuoni hao walikua katika manhaj Salafu Saalihi ya Sahaba Ammaar bin Yassir R.A.

NA YOTE MAWILI HAYO TAMU LAO NDILO CHUNGU LAO KWAO.

kwani la mwanzo litawaingiza katika hukumu yao wenyewe, na la pili litavunja hukumu yao.

Wabillahi taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu aliyeumba kila kitu, na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad S.A.W pamoja na Aali zake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya Malipo.

Tumefikiwa na shubuhati -kutoka kwa Masalafi- kuhusiana na uwepo wa Allah mtukufu, na kupitia shubuhati hizo wamefikia kusema na kudai kuwa Ibadhi wanaabudu kisichokuepo.
Ni shubuhati gani hiyo? Na ipi jawabu yetu?.
SHUBUHATI:
Masalafi wanatuuliza:
Jee! Allah yupo? 
Ikiwa yupo.
Jee! Allah yupo ndani ya viumbe vyake au nje ya viumbe vyake? 
Jee! Yuko juu ya viumbe vyake au chini ya viumbe vyake? 
Jee! Yuko mbale ya viumbe vyake au nyuma ya viumbe vyake?! 
Jee! Yuko kuliani mwa viumbe vyake au kushotoni mwa viumbe vyake?!
JAWABU:
Tunawambia Masalafi kuwa kuwepo kwa Allah mtukufu hakuna shaka ndani yake katika Itikadi yetu, na dalili ya kuwepo kwake ni vitendo vyake ambavo athari zake ni viumbe vyake tunavoviona na tusivoviona, basi kila kiumbe ni dalili ya kuwepo Muuambaji ambaye ni Allah mtukufu, na kupitia vitendo vyake tunamtambulisha kama walivomtambulisha Mitume yake A.S.W.
Mtume Mussa A.S.W alipoulizwa na Mlaaniwa Firauni: “Ni nani Mola wenu ewe Mussa?” Alimjibu: “Mola wetu ni yule aliyekipa kila kitu umbile lake kisha akaongoza.” [Taaha 49-50].
Vile vile Mtume Ibarahim A.S.W alipopeana hoja na mja aliyeneemeshwa kwa neema ya Utawala: Mtume Ibrahim A.S.W alisema: Mola wangu ni yule anayehuisha na anayefisha. Yule Mja akasema: Na mimi nahuisha na nafisha. Hapo Mtume Ibrahim alimwambia: Hakika Allah analitoa jua upande wa Mashariki basi litoe wewe upande wa Magharibi. [Baqarah 258]
Pia Hud-hudi wa Mtume Sulleiman A.S aliwashangaa wale wenye kulisujudia jua na kuema: Hivi hawamsjudii Allah ambaye huyatoa yaliyofichika katika mbingu na ardhi na anayajua munayoyaficha na munayoyatangaza. Allah hakuna mungu isipokua yeye Mola wa Arshi Mkuu?!! [Naml 25 -26].
Basi tunawambia Masalafi:
Hebu zingatieni Quraani tukufu jinsi inavotuleleza namna Mtume Ibarahim A.S.W alivobatilisha uungu wa vitu vyenye harakati na mipaka ya kuhusika kwa uwepo wa sehemu bila ya sehemu nyengine. “Na namna hivo tulimuonesha Ibrahimu ufalme wa mbingu na ardhi ili awe miongoni mwa wenye yakini. Basi ulipomtanda Usiku aliona sayari. akasema: Huyu ndiye Mola wangu. na ilipotua alisema: Siwapendi wanaotua. Na alipouona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola wangu. Ulipotua alisema: Ikiwa hataniongoza Mola wangu kwa hakika nitakua katika watu waliopotea. Na alipoliona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola wangu huyu ndiye mkuu. basi lilipozama akasema: Enyi watu wangu hakika mimi najitenga na munayoyashirikisha. HAKIKA MIMI NAELEKEZA DHATI YANGU KWA YULE ALIYEUMBA MBINGU NA ARDHI KWA YEYE TU NA MIMI SI KATIKA WASHIRIKINA.” [Al-An-Aaam 75-79].
Basi sisi Ahalu Al-Haqi wal-Itiqaamah (Ibadhi) tunamthibitisha Allah mtukufu kama alivothibitishwa na Mitume yake mitukufu, kwa hakika aliye na mipaka ya kupatikana sehemu mbila ya sehemu na aliyena na harakati za kuondoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine huyo si Mungu wa haki kama alivotongoa hayo Mtume Ibrahimu A.S.W alipobatilisha Umola wa Sayari na Mwezi na Jua kwa sababu ya harakati zake za kupatikana na kukosekana, kwa hiyo Mola wa haki Allah mtukufu hasifiki kwa sifa hizo za harakati.
Na kwa hili la kupitia vitendo vyake vya kupatisha viumbe tunathibitisha uwepo wa Allah mtukufu, na kuwa uwepo wa Allah mtukufu ni wa lazima ambao ni tafauti na uwepo wa viumbe vyake vyote kwani uwepo wa viumbe ni wa kufaa na kutegemea muwekaji wake ambaye ni Allah mtukufu, na kwa sababu hii haiwezekani Allah mtukufu awemo katika uwepo kiumbe wa kutegemea kama ilivokua haiwezekani Allah mtukufu adhibitike kwa lazimisho lolote la uwepo kiumbe, kutokana na hapa tunasema kuwa kuwepo uwepo wa viumbe na kukosekana uwepo wa viumbe ni sawa mbele ya Allah mtukufu na kuwa uwepo wote wa viumbe ni sawa kwake yeye Allah mtukufu na ndio maana akatuambia kwenye kitabu chake: Popote mutapoelekea basi huko ndio upande wa Allah. [Baqarah 115] Na akatuambia: Na yeye (Allah mtukufu) yuko pamoja na nyinyi popote mulipo. [Al-hadidi 4] Na akatuambia: Hauwi mnon`gono wa watatu ila yeye (Allah mtukufu) ni wa nne wao, wala wa watano ila yeye huwa wa sita wao, wala wa chini ya hapo au zaidi isipokua yeye yu pamoja nao popote watakapo kuwepo. [Al-Mujaadilah 7].
Ama tukija kwa masuali yao yenye malazimisho ya mipaka tunawambia hayo masuali yote ni masuali ya kuuliziwa kiumbe si masuali ya kuuliziwa Muumba, tunasema hivi kwa sababu Allah mtukufu katuambia kuwa yeye ndiye Wamwanzo umwanzo wake ni wa kuwepo si wa kuanza, na Mtume wetu Muhammad S.A.W katuambia: “Alikua Allah wala hakukua na chochote kisichokua yeye” [Bukhari 3191] Na Allah katuambia kuwa Arshi na Maji vilikua kabla ya uumbaji wa Mbingu na Ardhi, na dalili zote zinaonesha kuwa maji ni kiumbe kinachohitaji sehemu ya kuwepo pia Arshi kwa sababu Allah mtukufu ametuambia kuwa Arshi imebebwa na imezungukwa. [Ghaafir 7], kwa sababu Allah mtukufu uwepo wake ni kabla ya uwepo kila kisichokua yeye basi hakuna kiichoshirkiana na yeye katika Uwanzo wake, kwa maana hiyo sehemu ni miongoni mwa viumbe vyake nayo imetangulia uumbwaji wa Arshi na Maji na Mbingu na Ardhi na hewa na nuru na giza kwa sababu vyote hivo vimo katika ulazima wa kuhitajia sehemu. Tukifahamu hili tutajua ubatilifu wa masuali waliouliza Masalafi kwa sababu ni masuala yaliyojengwa katika ulazima wa kuwemo wahusika wake katika mipaka ya sehemu, na hili linatuweka katika asili ya kutafautiana baina yetu na wao, nayo ni kuwa wao wanalazimisha uwepo wa sehemu katika hali zote kwa hiyo ulazima wa Itikadi yao ni kuwa sehemu haina mwanzo wa kuanza bali inashirkiana na Allah katika utangu, Allah kwa mujibu wa Itikadi yao ni mwenye kuhitajia sehemu ya kuwepo ndani yake kutokana na hapo wanalazimisha suala la kuulizia sehemu ya kuwepo Allah mtukufu utawasikia wanauliza: Allaha yuko wapi? Imewapita kuwa Allah uwepo wake hauhitajii sehemu ni uwepo wa kujitosheleza kwani yeye ni AL-GHANIYYU (Mkwasi asiyehitaji chengine).
Kinacholazimika kiitikadi ni kuwa Allah sio viumbe wake na kuwa viumbe wake sio Allah mtukufu na kuwa uwepo wa viumbe haujaathiri kitu chochote katika uwepo wa Allah mtukufu na kuwa uwepo wa Allah haujulikani kwa mipaka sita ya sehemu ya juu, chini, mbele, nyuma, kulia, na kushoto; kwa sababu hiyo yote ni miapaka viumbe na vinavyodhitiwa kwa mipaka hiyo vyote ni viumbe kutokana na hapo kuuliza Jee Allah yuko ndani ya viumbe au nje ya viumbe ni ulizo batili kwa sababu limejengeka ndani ya mipaka ya sehemu ambayo ni kiumbe, pia kuunganyika na viumbe au kuachana na viumbe ni ulizo batili kwa sababu limo katika mipaka ya sehemu, vile vile mbele au nyuma juu au chini kulia au kushoto yote hayo yamo katika mipaka ya sehemu ambayo ni kiumbe hauliziwi Allah mtukufu kwa masuali yaliyojengeka katika mipaka ya sehemu kwa sababu yeye hajadhibitiwa kwa mipaka ya sehemu kwani uwepo wake umetangulia uwepo wa sehemu yeye Allah mtukufu ndiye aliyeumba sehemu, basi kinacholazimika kujua kuwa sehemu sio yeye na yeye sio sehemu kama ilivokua viumbe sio yeye na yeye sio viumbe.
Tukilifahamu hili tutajua kuwa haiwezekani kwa akili ya binadamu kuogelea katika bahari iliyo nje ya mipaka ya sehemu ambayo ni kiumbe, kwa hiyo haina uwezo wa kifikiria isipokua kiumbe tu, kutokana na hapo ni wajibu wetu kumtakasa Allah na kila lenye lazimisho la kuhitajia sehemu kama kuwa na viungo au sura au namna fulani au kuonekana au umbo au harakati au kubadilika au kuhusika na sehemu ya kukita ndani yake na mfano wa hayo; kwani vyote hivo ni viumbe vinahitajia sehemu.
Ama kusema kwao kuwa sisi kwa itikadi hii tunaabudu kisichokuepo (Al-Adam) tunawambia sisi tunaabudu kisichokuwepo katika sehemu kwani Muumba wetu Allah mtukufu ndiye aliyeumba sehemu na vyote vyenye kuhitajia sehemu basi yeye ni Mkwasi (Al-Ghaniyyu) asiyehitajia sehemu wala kudhitiwa kwa sehemu, kwa hiyo ikiwa nyinyi munaabudia aliyemo ndani ya mipaka sehemu na kuwa huyo ndiye muanayemwita Allah, mujue kuwa sisi itikadi yetu ni kuwa Allah ametakasika na kuhitajia sehemu kwani ndiye aliyeumba sehemu na kwa sababu hiyo ndio tukaitakidi kuwa yeye hajafanana na chochote wala hakuna kilichofanana na yeye, na kuwa yeye ni Dhati Kamilifu.
Asanteni sana.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

SUALI:
Asalamu alaykum wa rahamatullahi wa barakatuh.
Tunafikishiwa ujumbe wa kuhadharishwa na Ibadhi unaosema kuwa Abdullaah ibnu Muslim Al-Mirwazi alisema: “Nilikuwa nikikaa na ibnu Siiriin; kisha nikaacha na nikakaa na maibadhi; basi nikaona -yaani: ndani ya ndoto- kama kuwa niko na watu wamebeba jeneza ya Nabii swalla llaahu aleihi wa sallam. Nikamjia Ibnu Siiriin nikamtajia (hiyo ndoto), akasema: Una nini mbona umekaa na watu wanataka kuyazika aliyokuja nayo Nabii swalla llaahu aleihi wa sallam!!” na kuwa hayo yamo katika Kitabu kinachoitwa [Siyar a’laami nnubalaa cha Mwanachuoni mkubwa anayeitwa Adh-dhahabi (4/617)]
Tunaomba ufafanuzi.
JAWABU:
Allah mtukufu kwenye kitabu chake ametuambia uhakika wa wale waliopita kabla ya Umma huu; ili iwe ni tahadhari kwa umma huu usije ukapatwa na maradhi yaliyowapata, akatuambia:
((Hayo ni kwa sababu wao walisema: “Hautatugusa moto isipokua siku chache”. Na yakawadanganya katika dini yao waliyokua wakiyazua.))
[Aaala Imraan 24].
Sasa gonjwa ni hilo hilo; kwani wao wamesema neno hilo hilo HAUTATUGUSA MOTO ISIPOKUA SIKU CHACHE, basi na njia yao ni hiyo hiyo ya  kujidanganya kwa waliyoyazua wenyewe katika Dini yao.
Basi huo ni uongo hauna kifuniko, wamejitungia ili kufurahisha nafsi zao kwa kuwapigia mafumbo batili wana wa HAKI KWA DALILI Ibadhi.
Ikiwa wameweza kumzulia Mtume S.A.W riwaya za uongo na kuziweka katika vitabu walivovivisha kilemba kikubwa cha ukoka eti hamuna la batili ndani yake, basi itakua ajabu kuzuliwa uongo wa ndoto za kuchekeshana za hadithi za Paukwa Pakawa dhidi ya Wana haki kwa dalili Ibadhi?!!!
Na tokea lini ndoto kuwa dalili katika umma huu?!!!
Kwa hakika kisa hicho ni ilani tosha kuwa wao wameshindwa na kufilisika kidalili mbele ya Ibadhi katika yaliyoingiwa na tafauti baina yetu.
Na la kushangaza zaidi, vipi hawa watu wanapiga debe usiku na mchana la kutegemea sanadi (mtiririko wa wapokezi) na kuhakikisha kisanadi ili maelezo yawe sahihi, kisha wakatujia na paukwa pakawa za kisa hicho cha kutunga barazani.
Kwa hiyo watuletee sanadi yake; kwani Dhahabi kafariki mwaka 748 Hijiria, na Ibnu Siirini kafariki mwaka 110 Hijiria baina yao kuna miaka 600 takriban, kwa hiyo watupatie sanadi yake. 
Na kwa hakika visa hivo vya paukwa pakawa ni kuhakikisha kwao kuwa uongo kwao ni fani yao katika dini.
Wallahu Al-Mustaanu.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Bismillahi wa Salatu wa Salamu alaa Rasuulillahi.

Wabaad.

Imetufikia tuhuma batili yenye kutoka kwa Maslafi, kwa kusema kwao kuwa Ibadhi ni Makhawariji wale waliotoka katika utawala wa Aliy na kumkufurisha Sahaba huyo, na wakaongeza kuwa Makhawariji pia wanamkufurisha Othman bin Affaan. Tuhuma hiyo ikaendelea kuleta suali uchochezi kwa kuuliza Jee! Ibadhi wanaitakidi nini juu ya Masahaba hawa wawili?!!

Baadae wanatuhuma batili hiyo wakaja na na kimalizio cha Aya kinachosema:

((وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذٰلِكَ فَأُوْلَـٰئِكَ هُمُ ٱلْفَاسِقُونَ))

((NA WATAKAO KUFURU BAADA YA HAYO BASI HAO NDIO WAOVU)) 
[Nuur 55]

Wakasema wanatuhuma batili hao kuwa Ibadhi wanaona aliyekusudiwa hapa ni Sahaba Othman.
Baada ya hapo wakasema:

KUTOKA KWENYE KITABU CHA TAFSIRI: HAMYAANU ZZAAD ILAA DAARIL-MA’AD.
(ni tafsiri ya qur’an ya maibaadhi.)

AMESEMA NDANI YA KITABU HIKI : 

” إن عثمان فرعون هذه الامة ” 

HAKIKA OTHMAN NI FIRAUN WA UMMA HUU .

Kisha wakasema: Subhaana Llaah Mashia wanasema maswahaba ni makafiri wote isipokua watu watatu au wanne , na ibaadhi wanasema Othman bin Affaan na Ally ni makafiri. !
Kisha wanatuhuma batili hao wa Kisalafi wakaendelea kusema:

AKASEMA TENA KWENYE KITABU HICHO :

وعن ابن مسعود: ما يوزن لعثمان يوم القيامة ذباب, فقال رجل: ذباب ! ,فقال: ولا جناح ذباب …

KUTOKA KWA IBN MASUUD: OTHMAN SIKU YA QIYAMA HATAKUA NA UZITO WA INZI , AKASEMA MTU MMOJA INZI ! AKASEMA WALA BAWA LA INZI ..

hii ni kumkufurisha swahaba mtukufu.

JAWABU:

Kwa hakika uongo ni kitu kibaya sana, na Allah mtukufu ametuambia kwenye kitabu chake na ya haki ametuambia Allah mtukufu:

((ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَنْ تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِمْ مَا كَانُوا يَفْتَرُونَ))

((Hayo ni kwa sababu wamesema hautatugusa moto isipokua siku chake. Na yakawahadaa katika Dini yao waliyokua wakiyazua))

[Aala Imraana 24]

Kwa hiyo, uzushi uzushi ndio dini yao hawa waliokumbwa na maradhi ya kiitikadi yanayoitwa HAUTATUGUSA MOTO ISIPOKUA KWA MUDA TU, bali hawa wamekumbwa na Maradhi mabaya zaidi ya Kiitikadi yanayoitwa TUTASAMEHEWA TU SISI kama alivoyaeleza Allah mtukufu katika Kitabu chake:

))فَخَلَفَ مِنْ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَذَا الْأَدْنَى وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا((

((Na kilifuatia baada yao kizazi kibaya waliorithi Kitabu wakawa wanachukua pato hili la chini na wanasema: TUTASAMEHEWA SISI))

[Al-Aarafi 169].

Si wanaamini Hadithi inayosema kuwa Allah mtukufu kasema:

وَمَنْ لَقِيَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطِيئَةً لَا يُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَقِيتُهُ بِمِثْلِهَا مَغْفِرَةً 

((Na atakayekutana nami akiwa na vyombo vyote vya Ardhini hali vimejaa madhambi, naye hanishirikishi na kitu basi nitakutana naye kwa mfano wa vyombo hivo vya usamehevu)) [Muslim 2687]

Ama kuhusu tuhuma yao tunawambia:

1. Maibadhi katika Itikadi yetu hatuna mafundisho ya kumchukia Sahaba yoyote wala kumtusi wala kumkufurisha, na yaliyoandikwa katika baadhi ya vitabu hayavuuki duara la kuwa ni rai ya wahusika wa waliyoyaandika kwa mujibu wa yalivodhihiri kwao na kwa misingi ya uadilifu bila ya upendeleo.

2. Maibadhi wanaposema fulani ni kafiri hawamaanishi kuwa fulani huyo ni mshirkina kama wanavomaanisha Masalafi na Makhawariji katika maneno yao, kwani inafahamika kwetu Ibadhi kuwa tukisema kafiri ni sawa na kusema dhalimu au fasiki, kutokana na hapo Wanavyuoni wetu wamesema ukafiri una daraja mbili, ukafiri unaokamatana na madhambi ya ushirkina huo ni ukafiri wa kishirikina, na ukafiri unaokamatana na madhambi yasiyokua ya kishirikina huo ni ukafiri wa neema mwenye nao ni fasiki mpaka atubie.

3. Maibadhi hawajasemapo kuwa Aya tukufu hiyo [Nuur 55] imemkusudia Othman bin Affaan kama wanavodai Masalafi.

4. Mwanachuoni Mfasiri Mohammad bin Youssuf Itfayyish Allah amrehemu, alifasiri Tafsiri yake hiyo aliyoipa jina la Hiimyaanu Zaadi ila Daar Al-Maadi, kisha baadae akakutia kuwemo ndani yake hadithi na athari nyingi zisizosihi basi akajidiriki mwenyewe kwa kutoa Tafsiri ya pili aliyoiita Taisiru Tafsiiri, sasa ikiwa kaleta hadithi au athari yoyote katika Tafsiri yake Himyaanu Zaadi kisha Hadithi hiyo hatukuikutia katika Tafsiri yake Taisiru Tafsiiri tunajua kuwa hadithi hiyo au athari hiyo ni katika alizoona ubatili wake.

5. Aliyoyasema Imamu Mfasiri Atfayyish Allah amrehemu hayavuuki kuwa ni rai yake kwa mujibu yalivofika kwake wakati alipokua akiandika Tafasiri yake hiyo, na hayo yako wazi katika maneno yake kama tutakavoona, kwa hiyo huwezi kuyalazimisha kwa Madhehebu yote.
Amesema katika tafsiri ya Aya hiyo:

{ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ } الانعام منهم والانعام يحصل بانجاز الوعد وحصول الخلافة والمراد بالكفر كفر النعمة وهو المسمى عندنا كفر النفاق أو المراد كفر الشرك بالارتداد * { فَأُوْلَئِكَ هُمُ الفَاسِقَونَ } الكاملون في النفاق أو الشرك وقيل : من كفر بعد هذا الذي نزلت فأولئك هم الفاسقون فسق شرك .

“{Na atakaye kufuru baada ya hayo} ya kuneeshwa kwao, na kuneemeshwa kunapatikana kwa kutimiziwa ahadi na kupatikana ukhalifa, na makusudio ya ukafiri ni ukafiri wa neema nao kwetu sisi unaitwa ukafiri wa kinafiki, au makusudio ni ukafiri wa Ushirikina kwa kuritadi * {Basi Hao ndio Mafasiki} Waliotimia katika unafiki au ushirkina, na imesemwa: Atakaekufuru baada ya haya ambayo yameteremka basi hao ndio Mafasiki ufasiki wa Kishirkina.”

Hiyo ndio Tafsiri yake kama ilivyo katika Hiimyaan Zaad cha Mwanachuoni Mohammad Atfayyish Allah amrehemu, wala hakuna hapo kuwa Aya hiyo amekusudiwa nayo Othmaan bin Affaan kama walivozua wazushi wabatilifu wa Kisalafi.

Ama kuhusu Othman bin Affan.

Sheikh ameeleza rai yake kwa yalivomdhihirikia yeye, amesema hivi:

وأقول والله أعلم بغيبه : أن أول من كفر تلك النعمة وجحد حقها عثمان بن عفان جعله المسلمون على أنفسهم وأموالهم ودينهم فخانهم في كل ذلك زاد في مسجد رسول الله صل الله عليه وسلم ووسعه وابتاع من قوم وأبى آخرون فغصبهم فصاحوا به فسيرهم للحبس وقال قد فعل بكم عمر هذا فلم تصيحوا به فكلمه فيهم عبد الله بن خالد بن أسيد فأطلقهم من السجن وقد جمع في ذلك غصب المال وقذف عمر رضي الله عنه وعزل سعد بن أبي وقاص عن الكوفة بلا حدث منه رضي الله عنه وساتعمل أخاه لأمه وهو الوليد بن عقبة ونزل { واتقوا فتنة } بحضرة أبي بكر وعمر رضي الله عنهما وعثمان وعلي فقال لعثمان بك تفتح وبك تنشب وقال لعلي : أنت إمامها وزمامها وقائدها تمشي فيها مشي البعير في قيده .

Nasema na Allah ndiye anayejua ghaibu yake: Hakika wa mwanzo aliyeikufuru neema hiyo na kuivunjia haki yake ni Othman bin Affaan, walimueka Waislamu juu ya nafsi zao na mali zao na dini yao naye akawakhini katika yote hayo, aliongeza katika Msikiti wa Mtume wa Allah S.A.W na kuutanua na akanunua kwa watu na wengine wakakataa, basi akawapokonya, nao wakamlalamikia, basi akawaingiza kifungoni, na akasema: “Hakika aliwafanyia Omari haya na nyinyi hamukumlaumu” Basi Abdullahi bin Khalid bin Asyad akamsemeza kuhusu watu hao naye akawatoa kifungoni, na kwa hakika amekusanya katika hayo unyan`ganyi wa mali na kumzulia Omar Allah amridhie. Na alitengua uongozi wa wilaya ya Kuufah kwa Saad bin Abi Waqqaas bila ya kufanya kosa lolote Allah amridhie kisha akamteua pahala pake Ndugu yake wa Mama mmoja Al-Waliidi bin Uqubah. Na imeteremka {Na iogopeni Fitna} wakiwepo Abu Bakar na Omar Allah awaridhie na Othman na Aliy, basi alimwambia Othman kwako wewe itafunguliwa na kwako itaripuka, na akamwambia Aliy: Wewe ndiye kiongozi wake na kufungo chake na muelekezaji wake unatembea ndani yake mwendo wa Ngamia katika kifungo chake”

Tuzinduke kuwa kosa alilozingumzia Al-Allaamah Itfayyish Allah amrehemu si kuongeza ukubwa wa Msikiti, bali ni kufanya hivo kwa kupokonya mali za watu ambazo utanuzi wa Msikiti ulizimeza mali hizo kidhulma katika eneo alilolitaka, na hii inamaanisha kuwa baadhi ya ardhi ya Msikiti wa Mtume uliopo Madina baada ya utanuzi huo ni ardhi ya kupokonya kwa kukataa wenyewe kuuza mali yao. Wallahu Al-Mustaan.

Jee!! Hayo aliyoeleza ni sahihi yalitokezea kweli au si sahihi hilo ni suala jengine.

La muhimu hapa ni kuwa Itfayyish Allah amrehemu ameeleza yaliyomfikia katika kipindi hicho alichoandika Tafsiri yake hii ambayo kama tulivoeleza kuwa aliirejea na kutoa Tafsiri nyengine ambayo aliiondoshea yasiyokua sahihi kwa kujidiriki mwenyewe.

Ama neno linalosema (Othaman ni Firauni wa Umma huu).

Sheikh Itfayyish amelileta hilo kwa njia ya riwaya amesema:

فقال فيه صلى الله عليه وسلم ((إن عثمان فرعون هذه الامة))

Basi akamsema Mtume S.A.W: ((Hakika Othman ni Firauni wa Umma huu))

Na Mwanachuoni akileta hadithi, ikiwa hadithi haikuthibiti haizingatiwi, na sisi hatujui mpaka saa hii kama kuna mwanachuoni yoyote wa Kiibadhi ameisema Hadithi hii isipokua Itfayyish peke yake, wala hatujui kuwepo mwanachuoni katika chuo cha Kiibadhi aliyeisahihisha hadithi hiyo, na sisi tunaikana hadithi hiyo, na tunasema kuwa hadithi hiyo haikusihi kutoka kwa Mtume S.A.W, na lau kuwa Mtume S.A.W kaisema basi Masahaba na Waislamu R.A wasingalimridhia kuwa Amiri wa Waumini baada ya Omar R.A, lakini ni kuwa Sheikh pengine aliikutia katika baadhi ya vitabu visivokua vya Kiibadhi nae akaichukua, kwani mwisho wa maelezo yake kuhusu Othman alisema maneno haya:

وما ذكر به ثابت عندنا وعند من تكلم في هذا النوع من المخالفين كالنوبي والقرطبي والابي وغيرهم .

Na yaliyotajwa kwake yamethibiti kwetu (yaani kwake yeye Sheikh Itfayyish) na kwa waliozungumzia katika aina hii katika wapinzani wetu kama vile Nuubii na Qurtubi na Al-Abiyi na wengineo..

Ama kuhusu neno lililoegemezwa kwa Ibnu Massoud R.A kuwa alisema Othman siku ya Kiama hana uzito wa nzi bali hata wa bawa la nzi.

Ni neno lililonasibishwa kwa Sahaba na Allah aalamu kuhusu usahihi wake; kwa sababu Masahaba kumsema vibaya Othman kumethibiti kwa riwaya za Masunni wenyewe na kuna malazimisho ya hayo kwa mujibu wa mantiki ya matokeo ya kitarehe, na miongoni mwa waliomsema vibaya Othman kwa kusahihishwa riwaya yake ni Ammaar bin Yaasir R.A.

Amesema Al-Albaani:

قال الإمام أحمد (4/197) وابن سعد في الطبقات (3/260-261) والسياق له: أخبرنا عثمان بن مسلم قال: أخبرنا حماد بن سلمة قال: أخبرنا أبو حفص وكلثوم بن جبير عن أبي غادية قال: “سمعت عمار بن ياسر يقع في عثمان يشتمه بالمدينة” قال قتوعدته بالقتل قلت: لئن أمكنني الله منك لأفعلن …….

قلت: وهذا إسناد صحيح رجاله ثقات رجال مسلم وأبو الغادية هو الجهني وهو صحابي كما أثبت ذلك جمع. اهـ المراد منه

“Amesema Imam Ahmad (4/197) na Ibnu Saad katika Twabaqaat (3/260-261) na maelezo ni yake: Ametuambia Othman bin Muslim amesema: Ametuambia Hammaad bin Salamah amesema: Ametuambia Abu Hafsi na Kulthumu bin Jubair kutoka kwa Abu Ghaadiyah amesema: Nilimsikia Ammaar bin Yaasir anamshambulia Othman, anamsema vibaya katika Mji wa Madina” Akasema: Nikamuahidi kumuua nikasema: Akinimakinisha Allah kwako kwa hakika nitalifanya..”

Ninasema: Na hii ni sanadi sahihi wapokezi wake ni waaminiwa ni wapokezi wa Muslim, na Abu Al-Ghaadiyah ni Al-Juhani naye ni Sahaba kama walivothibitisha hilo wengi” [Rej. Al-Albani – Silsilatu Ahaadithi Sahihah wa Shaiun min Fiqhiha wa Fawaaidiha 5/18-19].

Ikiwa hili limetokezea kwa Sahaba Ammaar bin Yaasir -Allah amridhie- basi si ajabu kutokezea kwa Sahaba Ibnu Massoud -Allah amridhie-, hasa hasa tukifahamu kuwa Khalifa wa tatu Othman bin Affaan alizingirwa katika makazi yake (Ikulu) kwa muda wa siku 40 akitakiwa kujiuzulu kwa kumuona kuwa amekosa sifa za Uongozi bora alizokua nazo kabla, na alipokataa ndipo walipomuua, na hao hao waliofanya hivo ndiwo waliompa Baia (Kiapo cha Utawala) Khalifa wa nne Ali bin Abi Twalib na wakawa chini ya Uongozi wake na miongoni mwao wakawa ni wakuu wa maradaka ya Miji na Jeshi, na sio hivo tu, bali Ali alipigana vita na kila aliyedai Kisasi cha kuuliwa Othman katika vita maarufu vya Jamal na Siffain na Masahaba wengi wakiwa pamoja na yeye, na Mtume S.A.W alisema:

ويح عمار تقتله الفئة الباغية يدعوهم إلى الجنة ويدعونه إلى النار

((Ajabu ilioje kwa Ammmaar atauliwa na kundi la waasi anawaita katika Pepo nao wanamuita katika Moto)) [Bukhari 447]

Na mwisho katika jawabu yetu hii fupi tunasema na katika Wanavyuoni waliowasema vibaya Masahaba R.A ni Sheikh wa Uislamu wa Masalafi Ibnu Taimia Al-Harraani anasema kuhusu Ali bin Abi Talib.

ثم يقال لهؤلاء الرافضة: لو قالت لكم النواصب: علي قد استحل دماء المسلمين وقاتلهم بغير أمر الله ورسوله على رياسته وقد قال النبي صلى الله عليه وسلم: سباب المسلم فسوق وقتاله كفر” وقال: “لا ترجعوا بعدي كفارا يضرب بعضكم رقاب بعض”فيكون علي كافرا لذلك لم تكن حجتكم أقوى من حجتهم لأن الأحاديث التي احتجوا بها صحيحة.

وأيضا قيقولون: قتل النفوس فساد، فمن قتل النفوس على طاعته كان مريدا للعلو في الأرض والفساد وهذا حال فرعون والله تعالى ((تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ)) سورة القصص فمن أراد العلو في الرض والفساد لم يكن من أهل السعادة في الآخرة.

Kisha wataambiwa hawa Marafidha (Mashia): lau wanakuambieni Nawasibu (Masunni wenye kumchukia Ali): Ali alihalalisha damu za Waislamu na akawapia vita bila ya amri ya Allah na Mtume wake kwa ajili ya utiifu wake, na Nabii S.A.W amesema: ((Kumtukana Muislamu ni ufasiki na kumpiga vita ni ukafiri)) na amesema: ((Musirejee baada yake mukawa Makafiri baadhi yenu wanapiga shingo (wanaua) za wengine)), basi Ali atakua ni kafiri kwa hayo, hoja yenu (enyi Marafidha) haitakua na nguvu zaidi kuliko hoja yao (Nawasib); kwa sababu Hadithi walizotolea hoja ni sahihi.

Na vile vile watasema: Kuua nafsi ni uharibifu, basi mwenye kuua nafsi kwa kutiiwa yeye anakua ni mwenye kutaka ukuu katika Ardhi na uharibifu, na hiyo ni hali ya Firauni, na Allah mtukufu anasema: ((Hiyo ni nyumba ya Akhera tunaijaalia kwa wasiotaka ukuu katika Ardhi wala uharibifu na mwisho mwema ni wa Wachamungu)) Suuratu Al-Qasas, basi mwenye kutaka ukuu na uharibifu katika Ardhi hatakua katika watu wa kufanikiwa katika Akhera” [Rej. Minhaaj Sunnati Nabawiyah 4/500-501]

Pia Ibnu Taimia Al-Harani amesema:

الرابع: أن الله قد أخبر أنه سيجعل للذين آمنوا وعملوا الصالحات ودا. وهذا وعد منه صادق. ومعلوم أن الله قد جعل للصحابة مودة في قلب كل مسلم لا سيما الخلفاء -رضي الله عنهم- لا سيما أبو بكر وعمر فإن عامة الصحابة والتابعين كانوا يودونهما وكانوا خير القرون. ولم يكن كذلك علي فإن كثيرا من الصحابة والتابعين كانوا يبغضونه ويسبونه ويقاتلونه اهـ

“La nne: Hakika Allah ameeleza kuwa yeye amejaalia kupata mapenzi kwa walioamini na kufanya mazuri, na hii ni ahadi ya kweli kutoka kwake, na inajulikana kuwa Allah amejaalia kupata Masahaba mapenzi katika moyo wa kila muislamu hasa hasa Makhalifa kati yao -Allah awaridhie- hasa hasa Abu Bakar na Omar; kwa hakika Masahaba wote na Matabiina walikua wakiwapenda wawili hao nao walikua ndio karne bora yao, na Ali hakua hivo kwani hakika wengi katika Masahaba na Matabiina walikua wakimchukia na wakimtukana na wakimpiga vita.” [Rej. Minhaaj Sunnati Nabawiyah 7/138].

Wabillahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Kuna msalafi mmoja huko Sudan ameshambulia Ibadhi kwa kusema: “Ama Itikadi ya kuwa Quraani ni kiumbe hiyo ni kumkufuru Allah kama alivoeleza hayo Ahmed bin Hambal,… Na anasema Abdullahi bin Ibadhi: Na yoyote anakampenda Othman bin Affaan na anayemuunga mkono, basi hakika sisi tunamshuhudisha Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume yake ya kuwa sisi tuko mbali nao hao, pia sisi maadui wao hao, kwa mikono yetu na ndimi zetu na nyoyo zetu, tunaishi katika hilo muda wa kuishi na tunakufa juu ya hilo tutakapo kufa na tutafufuliwa juu ya hilo tutakapofufuliwa, tunahesabiwa kwa hilo mbele ya Allah…”

Msalafi huyo akaendelea kusema: Hii ndiyo Itikadi ya Kiibadhi kuhusu Othman bin Affaan Allah amridhie, Dhu Nuuraini ambae Allah hakukusanya kwa yoyote mabinti wawili wa Nabii juu ya mgongo wa Ardhi isipokua kwa Othman bin Affaan Allah amridhie, .. na amesema Ibnu Ibadhi kuhusu Makhariji: Basi hii ndiyo khabari ya Makhawariji tunmashuhudisha Allah na Malaika wake ya kuwa sisi maadui kwa yoyote atakaewafanyia uadui, na kuwa sisi ni vipenzi kwa yoyote atayewapenda, kwa mikono yetu na ndimi zetu na nyoyo zetu, juu ya hilo tunaishi muda wa kuishi kwetu na juu yake tutakufa, na juu yake tutakutana na Allah” Maneno yote haya yamo katika Kitabu (Uquudu Al-Fidhiyah fi usuuli al-ibadhiyah uk. 121) na (Man`haju Daawa in`da Al-Ibadhiyah  uk 324-337). Nakala ya maneno ya Msalafi huyo.

Msalafi akaendelea kusema: Na Kitabu hichi kimesifiwa na Al-Khalili ambae ndiye Mufti wa Oman hivi sasa, naye ndiye Ibadhi mkubwa zaidi duniani katika zama hizi. Anawasifu Makhawariji hali ya kuwa Mtume Salla lwahu alaihi wa sallama kama ilivo katika Sunan Ibni Maajah amesema: Makhawariji ni mbwa wa motoni…..mpaka mwisho wa maneno ya Msalafi huyo Allah amuongoe. Mwisho wa kunakili.

JAWABU:

Kuhusu suala la kuwa Quraani ni kiumbe sisi hatuna shaka katika usahihi wa Itikadi hiyo, nayo ndiyo Itikadi sahihi kwa mujibu wa dalili, na Maibadhi wamekubaliana katika Itikadi ya kuwa Quraani ni kiumbe, kwa sababu Quraani ni kitu chengine kisichokua Allah mtukufu nacho kimeteremshwa nayo ni maneno ya Allah kwani ndiye aliyeyatokezesha na kuyajaalia, wala hatuna sisi Itikadi pofu ya kuitakidi kuwa sifa za Allah ni vitu vyengine visivokua dhati ya Allah, ama neno ya Ahmed bin Hambal kuwa hiyo ni Itikadi ya kumkufuru Allah tunasema hiyo ni fatwa chinjachinja pofu haina dalili na iliyofilisika kihoja, na neno la Ibnu Hambal si dalili ya kisheria, lakini juu ya yote hayo tunasema neno hilo la Ibnu Hambal lemesheheni vizuri roho ya Ukhawariji alioubainisha Mtume S.A.W. katika hadithi kadhaa na miongoni mwao ni hiyo aliyoipokea Ibnu Maajah isemayo: “Makhawariji ni mbwa wa motoni” Kwani wanautumikia kwa kuudhuru Uislamu na kuwapa matarajio hewa mafasiki na maovu.

Ama kuhusu suala la Barua ya Al-Imam Ibnu Ibadhi -Allah amridhie- tunasema kuwa mafundisho ya Kiitikadi katik Ibadhi ni kulazimika na mapenzi kwa vipenzi wote wa Allah nao ni Wachamungu, na kulazimika na uadui dhidi ya maadui wote wa Allah nao ni Mafasiki, boyfa hapa.

Kwa hiyo ikiwa Al-Imam Ibnu Ibadhi -Allah amridhie- imemdhihirikia yeye kuwa Othman bin Affaan amekufa hali ya kuwa ni fasiki basi si tatizo kwake kusema neno la haki katika hilo bila ya kuogopa lawama ya wenye kulaumu, ama kuwa Othman bin Affan alioa Mabinti wawili wa Mtume S.A.W. hiyo si sababu ya Walaayah wala hakuna sehemu katika Quraani wala Sunna iliyoandikwa kuwa kuoa binti wa Mtume ndio kufanikiwa mbele ya Allah na kupata pepo yake, lau kuwa Mtume S.A.W. alikua na mabinti 100 kisha Othman akaoa mmoja baada ya mwengine mpaka akamaliza wote 100 basi hilo la kuoa halitamsaidia kitu ikiwa atakufa katika ufasiki, achilia mbali mabinti wawili. Ama riwaya inayosema: “Halitamdhuru Othman atakalolifanya baada ya leo.” inaonesha wazi kuwa ni riwaya ya uzushi kwani Allah mtukufu hana upendeleo kuwa Othman akifanya dhambi na kufa fasiki basi hafikwi na hukumu ya Allah aliyoiandaa kwa Mafasiki.

Mtume S.A.W.: Amewadharisha Masahaba wake wote na -Othman ni miongoni mwao-:

لَا أُلْفِيَنَّ أَحَدَكُمْ يَجِيءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى رَقَبَتِهِ بَعِيرٌ لَهُ رُغَاءٌ ، يَقُولُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، أَغِثْنِي ، فَأَقُولُ : لَا أَمْلِكُ لَكَ شَيْئًا ، قَدْ أَبْلَغْتُكَ لَا أُلْفِيَنَّ أَحَدَكُمْ يَجِيءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى رَقَبَتِهِ فَرَسٌ لَهُ حَمْحَمَةٌ ، فَيَقُولُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، أَغِثْنِي ، فَأَقُولُ : لَا أَمْلِكُ لَكَ شَيْئًا ، قَدْ أَبْلَغْتُكَ لَا أُلْفِيَنَّ أَحَدَكُمْ يَجِيءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى رَقَبَتِهِ شَاةٌ لَهَا ثُغَاءٌ ، يَقُولُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، أَغِثْنِي ، فَأَقُولُ : لَا أَمْلِكُ لَكَ شَيْئًا ، قَدْ أَبْلَغْتُكَ لَا أُلْفِيَنَّ أَحَدَكُمْ يَجِيءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى رَقَبَتِهِ نَفْسٌ لَهَا صِيَاحٌ ، فَيَقُولُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، أَغِثْنِي ، فَأَقُولُ : لَا أَمْلِكُ لَكَ شَيْئًا ، قَدْ أَبْلَغْتُكَ لَا أُلْفِيَنَّ أَحَدَكُمْ يَجِيءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى رَقَبَتِهِ رِقَاعٌ تَخْفِقُ ، فَيَقُولُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، أَغِثْنِي ، فَأَقُولُ : لَا أَمْلِكُ لَكَ شَيْئًا ، قَدْ أَبْلَغْتُكَ لَا أُلْفِيَنَّ أَحَدَكُمْ يَجِيءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى رَقَبَتِهِ صَامِتٌ ، فَيَقُولُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، أَغِثْنِي ، فَأَقُولُ : لَا أَمْلِكُ لَكَ شَيْئًا ، قَدْ أَبْلَغْتُكَ “

Nisijemuona mmoja wenu anakuja siku ya Kiama hali ya kuwa amelazimikiwa na ngamia analia. Aseme: Ewe Mjumbe wa Allah niokoe.. Nitasema: Similiki kwao kitu leo kwa hakika nilikufikishia. Nisijemuona mmoja wenu anakuja siku ya Kiama hali ya kuwa amelazimikiwa na farasi analia. Aseme: Ewe Mjumbe wa Allah niokoe.. Nitasema: Similiki kwao kitu leo kwa hakika nilikufikishia. Nisijemuona mmoja wenu anakuja siku ya Kiama hali ya kuwa amelazimikiwa na mbuzi analia. Aseme: Ewe Mjumbe wa Allah niokoe.. Nitasema: Similiki kwao kitu leo kwa hakika nilikufikishia….. mpaka mwisho wa riwaya kama ilivyo katika Bukhari na Muslim na wengineo….

Bani Israili ni wana wa Yaaqoob mwana wa Is`haaq mwana wa Ibrahim lakini walipoasi na kufanya uadui walilaaniwa wala haukuwafaa kitu ukoo wao, basi lau kuwa tutakubali tu kimakadirio kuwa riwaya ni sahihi basi itakua imefungwa na sharti ya kuwa iwapo ataendelea katika hali yake hii aliyonayo hivi sasa ya uchamungu.

Tukija katika risala ya Al-Imam Ibnu Ibadhi R.A. inatulazimu kuiangalia kwa uadilifu, na sisi tukifanya hivo tunakutia sababu zilizopelekea kutoa hukumu ya Baraa-a kwa Othman bin Affaan. Jee! Mwenye kuzongwa na sababu hizo hiyo hatastahiki hayo aliyoyasema Al-Imam Ibnu Ibadhi Allah amridhie?!! Ikiwa atayastahiki kwa nini tumlaumu?!!!!!

Barua inasema: 

“Ama niliyoyataja kuhusu Othman, na niliyoyaweka wazi katika suala la viongozi, kwa hakika hakuna yoyote anayekataa ushahidi wa Allah katika Kitabu chake kwa alioteremsha kwa Mtume wake, kuwa [asiyehukumu kwa alioteremsha Allah, hao ndio Madhalimu], na [Makafiri] na[Mafasiki] 5/44-47.

Kisha mimi sikua nikutajie kitu chochote katika mambo ya Othman na viongozi isipokua Allah anajua kuwa hiyo ni haki, nami nakutajia ubainisho katika Kitabu cha Allah alichokiteremsha kwa Mtume wake katika hayo, na nitakuandikia katika niliyokutajia, na nitakupa habari za Othman na yale tuliyomtia makosani kwayo, ili nibainishe kwako jambo lake.

Kwa hakika alikuwa (Othman) ni miongoni mwa waliotangulia katika Uislamu na kuufanyia kazi vizuri, lakini Allah hakuwaondoshea waja mtihani.

 

Basi baada ya kifo chake ( yaani Omar R.A.), Waumini walishauriana, nao wakamkabidhi Othman uongozi, naye akafanya aliyotaka Allah ayafanye katika wanayoyajua Waislamu, akaendelea katika hilo mpaka ikakunjuliwa kwake dunia, na zikafunguliwa kwake hazina za ardhi kwa yale yote aliyotaka Allah mtukufu.

Kisha akaleta mambo mapya (Bidaa), mambo ambayo hayakufanywa na wenzake waliopita kabla yake, hali ya kuwa yale waliyoyazoea watu kwa Mtume wao bado ni mapya.

Basi Waumini walipoyaona aliyoyazua, walimwendea na wakamsemeza, nao wakamkumbusha kwa Kitabu cha Allah na Sunna za waliopita kabla yake katika Waumini, basi hayo yakawa ni mazito juu yake kukumbushwa kwa Aya za Kitabu cha Allah, na hapo aliwachukua kwa maguvu (ubabe), na akawapiga miongoni mwao aliyemtaka, na kuwafunga, na kuwahamisha.”

 

Sasa ikiwa kweli Othman aliyafanya hayo ndio Uislamu umuhami kwa sababu yeye ni Mkwe wa Mtume S.A.W. kaona Banati wake wawili?!!! Ajabu kubwa wallahi. Ikiwa unapinga kutokezea hayo kwa Othman kwa nini unalaumu yaliyomo katika Barua hali ya kuwa yamejengwa juu ya hayo?!!!

Sisi tunaingalia Barua ya Al-Imamu Abdullahi bin Ibadhi Al-Tamimi -Allah amridhie- kuwa ni Wathika wa kuhakikisha Uadilifu wa Uislamu katika chuo cha Madhehebu ya Kiibadhi, hakuna upendeleo katika hukumu za Allah.

Mtume S.A.W. amsema: “Hakika kuliwaangamiza waliopita kabla yenu vile kuwa wao anapoiba mkuu humuacha na anapoiba mnyonge humtia adabu, naapa Wallahi lau Faatima Bint Muhammad ameiba basi ningalikata kiganja chake” 

Huo ndio uadilifu unavotakiwa sio huyu ana ngao kwa sababu ni mkwe, ni mwana ni ami ni bina ami.

Kwa hiyo tunasema kuwa yakithibiti kwa muumini hayo ambayo Othamn bin Affaan ametiwa doa kwayo itamlazimikia kumuweka katika hukumu yake, na kama hayakuthibiti kwake basi asili ya kuridhiwa inabakia pale pale na kulazimika kusema Othman bin Affaan Allah amridhie.

Na ndio maana tukasema kuwa kumuweka Othman au Ali au Muawiyah au yoyote katika hukumu ya Baraa-a ni rai binafsi ya wahusika wake si fundisho katika milango ya Itikadi katika Ibadhi.

Ama suala la Makhawariji ambao Al-Imam Ibnu Ibadhi -Allah amridhie- ameeleza kuwaridhia, amefanya hiyo kwa njia ya mashaakala katika kujibu, anatuambia ikiwa hawa ambao wewe Abdulmalik unawaona ni Mkhawariji hiyo ndiyo hali yao basi Makhawariji hao hii ndiyo hali yao…….

Wabillahi taufiqi. 

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

MSALAFI:

Tanbihi: Ijulikane kuwa Katika uislamu kuna mambo ya kiitikadi ambayo alifundisha mtume “Swalla allahu alayh wasalam” na Itikadi hii waliiamini wanafunzi wake Masahaba ((Allah awawie radhi))

Ukiamini/Ukiitakidi kinyume na alichoacha Mtume we umezua katika Itikadi ya Uislamu UTAITWA MTU WA BID’A katika itikadi yako hiyo ambayo haina Asli katika uislamu.

JAWABU:

Kwanza: Sisi hatutafautiani katika kushikamana na mafundisho ya Mtume wetu Muhammad S.A.W. na ambayo aliwafundisha Masahaba wake R.A. ni sawa mafundisho hayo yakawa ni Itikadi au Fiqhi au Tabia njema.

pili: Tunaamini kuwa sababu ya upotevu wa kila aliyepotea ni:

 1. Kujitoa nje ya mafundisho ya Mtume wetu S.A.W.
 2. Kujitungia au kujipangia mafundisho kisha akayanasibisha kwa Mtume S.A.W.

Basi kwa sababu ya hii sababu ya pili zikaweza kupatikana hadithi uongo zilizonasibishwa kwa Mtume S.A.W. au Masahaba wake au kwa Maimamu waliopita.

Kwa sababu yote hayo yalitokezea basi Ibadhi tukakifanya Kitabu cha Allah mtukufu na Sunna yenye makubaliano, na malazimisho ya Kiakili kuwa ndiyo mizani kuu na dira ya kuujua upofu wa aliyepotea na uongofu wa aliyeokoka, kwani tunajua kuwa mafundisho ya Allah mtukufu na Mtume wake S.A.W.  yameelekezwa kwa wenye akili, na katu hayawezekani yapingane na Akili.

Basi Kitabu cha Allah ndio dira yetu, nacho amekisifu Allah mtukufu kwa neno lake:

((ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ))

((Hicho ni Kitabu hakuna shaka ndani yake, ni uongofu kwa wachamungu.))

Amesema Mtume S.A.W.:

«خَلَّفْتُ فِيكُمْ مَا إِنْ تَمَسَّكْتُمْ بِهِ لَنْ تَضِلُّوا أَبَدًا كِتَابَ اللَّه عَزَّ وَجَلَّ فَمَا لَمْ تَجِدُوهُ فِي كِتَابِ اللَّهِ فَفِي سُنَّتِي، فَمَا لَمْ تَجِدُوهُ فِي سُنَّتِي، فَإِلَى أُوْلِي الأَمْرِ مِنْكُمْ»

“Nimeacha kwenu yale ambayo mukijishika nayo hamutapotea baada yangu milele: Kitabu cha Allah, na ambacho hamutakipata katika Kitabu cha Allah basi ni katika Sunna yangu, na ambacho hamutakipata katika Sunna yangu basi ni kwa wenye mamlaka katika nyinyi (Viongozi waadilifu na Maulamaa wachamungu).” [Rabii 30]

Na hili pia limeelezwa na Allah mtukufu kwenye Kitabu chake:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا))

((Enyi mulioamini, mtiini Allah na mtiini Mtume na Viongozi katika nyinyi, na mukizozana katika kitu chochote basi kirejesheni kwa Allah na Mtume ikiwa nyinyi munamuamini Allah na siku ya mwisho, hilo ndilo bora na utatuzi ulio mzuri zaidi)) [Nisaa 59].

Kwa hiyo kujishika na Kitabu cha Allah na Sunna ya Mtume wetu S.A.W. ndio Dini yetu fuata kiunganishi husika ili uone Jumlatu Tauhidi hapa.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

MSALAFI:

لمن تنسب الإباضية :

Kwa nini wameitwa IBADHI?

مؤسسها الأول عبد الله بن إباض من بني مرة بن عبيد بن تميم ، ويرجع نسبه إلى إباض وهي قرية العارض باليمامة ، وعبد الله عاصر معاوية وتوفي في أواخر أيام عبد الملك بن مروان .

Jina hili linatokana na Muasisi wake anaitwa Abd’Allah Ibn Ibaadi kutoka kabila la Banu Murrah ibn Ubayd At’tamim

Alitokea katika kijiji cha Yamamah siku hizi panaitwa ((Aarid)) Abd’Allah alikuwa enzi za Muawiyah na kufariki mwishoni mwa Utawala wa Abdul maalik Ibn Marwan.

JAWABU:

Ni kujidanganya kuona kuwa Imam Abdullahi bin Ibadhi Al-Tamimi -Allah amridhie- ndie muasisi wa Madhehebu ya Ibadhi, kwa hakika sisi Maibadhi wenyewe hatulioni hilo wala halimo katika mafundisho yetu aslan, kwa hakika Ibadhi ni tokeo la kushikama na haki kwa mujibu wa dalili kila tafauti ilipotokezea katika umma huu wa Kiislamu, na ikiwa kuna mtu anadai kuwa Ibnu Ibadhi R.A. ni muasisi wa Madhehebu ya Ibadhi basi atulelee kauli zake katika vitabu vya Maibadhi, ni sawa kama ataweza kufanya hilo katika Itikadi yetu au Fiqhi yetu.

Tunachokijua sisi Maibadhi ni kuwa Imam Abdullahi Ibnu Ibadhi R.A. ni mmoja wa waliopata sharafu ya kukamatana na haki na kuibainisha mbele ya jamii katika zama zake akiwa ni mfuasi wa haki kwa dalili katika zama za Imam Jabir bin Zaid Al-Azdi Al-Omani aliyefariki mwaka 96 Hijiria -Allah amridhie- ambaye ndiye Imam wetu katika zama zake, na umaarufu wake ulipatikana kwa sababu za Kisiasa wakati huo.

Na hapa inafaa tueleze silsila yetu kama alivyoieleta Imam Ahmed bin Maddaad -Allah amrehemu- naye ni katika wanavyuoni wetu wa karne ya 10 Hijiria, ametueleza katika Sira yake kuwa yeye kachukua Dini yake kutoka kwa Abu Al-Mundhir Salama bin Muslim Al-Autabi Al-Sohari, naye kutoka kwa Sheikh Said bin Quraish, naye kutoka kwa Muhammad bin Al-Mukhtaar, naye kutoka kwa Sheikh Abu Al-Hassan Aliy bin Muhammad Al-Bisyaani Al-Asamm, naye kutoka kwa Sheikh Muhammad bin Abi Al-Hassan Anizwi, naye kutoka kwa Abdullahi bin Muhammad bin Barakah, naye kutoka kwa Abu Malik Ghassaan bin Muhammad Al-Sallaani, naye kutoka kwa Bashir na Abdullahi wana wa Muhammad bin Mahboub Al-Ruhaili Al-Quraishi, nao kutoka kwa Azzaan bin Saqri Al-Aqari Alnizwi, naye kutoka kwa Fadhlu bin Azzaan na Abu Al-Muuthir Saltu bin Khamis, nao kutoka kwa Muhammad bin Mahboub na Muhammad bin Ali na Al-Wadhaah, nao kutoka kwa Mussa bin Ali Al-Azkawi, naye kutoka kwa Hashim bin Ghailan Al-Siijani, naye kutoka kwa Mussa bin Abi Jabir Al-Azkawi, naye kutoka kwa Rabii bin Habib Al-Farahidi, naye kutoka kwa Abu Ubaida Muslim bin Abi Kariima Al-Tamimi, naye kutoka kwa Jabir bin Zaid Al-Azdi, naye kutoka kwa Abdullahi bin Abbaas na Aisha binti Abu Bakar na Abdullah bin Omar na wengineo katika Masahaba Allah awaridhie, nao kutoka kwa Nabii Muhammad S.A.W. naye kutoka kwa Jibrilu A.S. naye kutoka kwa Mola mtukufu Allah aliye mkuu.

Hii ni moja ya silsila ya mmoja wa Maimamu wetu Allah amrehemu, na silsila zote za Maimamu wa Ibadhi kituo chake ni Imam Abu Ubaidah Muslim bin Abi Karimah Al-Tamimi -Allah amrehemu- naye kupitia kwa Imam Jabir bin Zaid Al-Uzdi Al-Omani naye kupitia kwa Masahaba wa Mtume wetu Muhammad S.A.W.

Wala huwezi kupata silsila yoyote iliyopitia kwa Imam Abdullahi bin Ibadhi Al-Tamimi Allah amrehemu, na hii haina maana kumkataa -la haasha- bali ni kubainisha vituo vikuu ambavyo mafundisho yetu yalipitia humo tu, wala haina maana kuwa tuna kasumba pofu kuwa ikitufikia haki nje ya hawa ndio tena hatuikubali.

Anatuambia Imam Nurudini Assaalimi R.A.: “Na sisi hatuna madhehebu isipokuwa uislamu, basi tunaikubali haki kutoka kwa yoyote atakaye kuja nayo hata kama ni anachukiwa, na tunaikataa batili kwa yoyote atakaye kuja nayo hata kama ni kipenzi, tunawajuwa watu kwa haki, basi mkuu kwetu ni yule atakaye ikubali haki, na mdogo kwetu ni yule atakaye ikataa haki.

Na Mwana wa Ibadhi hajatupangia madhehebu, basi unasibisho wetu kwake yeye ni kwa dharura ya kuainisha wakati kila kundi lilipochukuwa njia yake”.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

MSALAFI:

TOFAUTI YAO NA AHLU SUNNAH IKO HAPA

ينكرون رؤية المؤمنين لله تعالى في الآخرة

Hawaamini kama Waumini watamuona ALLAH siku ya Qiyaama ((yaani Peponi))

[Ahlu sunnah Tunaamini kwa Dalili zilizokuja kuwa ALLAH ataonekana na WAUMINI AKHERA]

JAWABU:

Sisi tunamshukuru Allah mtukufu kwa taufiqi yake katika kushikamana na Itikadi sahihi kwa mujibu wa Kitabu chake na Sunna ya Mtume wake na ambayo haipingani na akili iliyosalimika, sisi tunaamini kuwa Allah mtukufu ndiye wa mwanzo (AL-AWWALU), basi uwepo wake umetangulia kila kisichokua yeye; kwa hiyo ni uwepo kamilifu usiohitaji sehemu wala wakati wala mbingu wala ardhi wala nuru wala giza; kwa sababu vyote hivo ni viumbe vyake Allah mtukufu amesema Mtume S.A.W.: (Alikua Allah wala hakukua na chengine kisichokua yeye) [Sahihi Bukhari 3020], basi ametakasika Allah na wanayomsifu wabatilifu wenye kumsifu kwa sifa za kuzingirwa na sehemu, akawa kwao ni mwili wa kuonekana kwa macho ya waja ametakasika Allah muumba na hilo utakaso kubwa kabisa; kwa hakika Allah amejisifu kwa ((Yeye hadirikiwi na vyenye kuona)) si macho, wala akili, wala moyo, wala chochote kile, hakika Allah mtukufu anaona waka haonekani, ikiwa wanaojiiya Ahalu Sunna wanaamini kuwa watamuona Allah siku ya kiama na peponi shauri yao, sisi hilo tunaliona ni muhali haliwezekani, si kwa udhaifu wetu bali kwa ukamilifu na ukwasi wa Allah mtukufu amesema Mtume S.A.W. ((Na hakuna kwa watu wa Peponi kilichozuia  kumuona Mola wao isipokua Ukuu wake Allah mtukufu)) [Bukhari na Muslim  katika sahihi zao]. Anasema Al-Haafidh Ibnu Hajjar Al-Asqalani: ((Na maana ya hadithi ya mlango huu ni kuwa kwa mujibu wa utukufu wa Allah na kujitosheleza kwake asionekane na yoyote..)) kwa hiyo sisi tunajikinga na upofu wa kuitakidi jambo linalopingana na utukufu wa Allah na ukuu wake na ukwasi wake.

Na zaidi kuhusu dalili zetu na jawabu zetu katika suala hili fuata viunganishi vifuatavyo.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

MSALAFI:

? يحرفون بعض أمور الآخرة وينفون حقيقتها كالميزان والصراط .

Wanafanya Tafsiri mbadala (metaphorical Interpretation) katika mambo yatakayotokea Qiyaama mathalan Mizani na Siraat ((Njia ya kwenda Peponi))

[Ahlu sunnah hatufanyi Taawili wala tafsiri mbadala bali tunaamini na kuchukua kama ambavyo tumefundishwa na Mtume wetu عليه السلام

JAWABU:

Tunamuambia huyu Msalafi kuwa Itikadi sahihi haijipinzi wala haipingani na Quraani tukufu, na sisi mpaka hivi sasa hatujaona katika Quraani tukufu pahala ilipotajwa hiyo Siraati iliyotundikwa juu ya Jahannamu iliyo kali kuliko upanga na nyembamba kama unywele na kunyakuliwa watu chini yake ambayo Masalafi wanaiitakidi, Quraani iko wazi kabisa kuwa wataokaostahiki kuadhibiwa motoni watapelekwa kwenye Moto wa Jahannamu, na kuwa Moto una milango yake inayofunguliwa na kufungwa, na bila shaka milango ndiyo sehemu iliyotayarishwa kwa kuingia katika nyumba husika; kwa hiyo Jahannamu ina milango yake na Allah ametueleza mpaka idadi ya hiyo milango kuwa ni 7, wala haijatueleza kuwepo Siraati juu yake, na bila shaka wenye kuitakidi Siraati wametegemea mapokezi wanayoitakidi kuwa ni Sahihi, ama sisi hatuoni usahihi wa mapokezi hayo kwa sababu ya kupingana kwake na Quraani tukufu.

Ama kuhusu Aya ya Suuratu Maryam:

((وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا * ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا))

((Na hakuna yoyote kati yenu ila atauingia limekua hilo ni jambo lililokwishapitishwa, kisha tutawaokoa waliomchamungu na tutawaacha madhalimu humo wakiyayatika)) [Maryam 71-72]

Tutasema kuwa wakhutubiwa katika suala la kuuingia moto katika Aya hii ni wale waliozungumzwa kabla yake nao ni wenye kukanusha ufufuo wa siku ya Kiama wamekhutubiwa kwa njia ya kuelekewa (Iltifaatu), kwa hiyo hao ndio wenye kuambiwa kuwa hakuna yoyote kati yenu nyinyi wenye kukanusha ufufuo ila atauingia tu huo moto wa Jahnnamu, ama Wachamungu wao Allah mtukufu ameshatueleza kuwa siku hiyo watakua katika Amani kamilifu na wataepushwa na Jahannamu bali hata vishindo vyake hawatavisikia na huko ndiko kuokolewa kwao, amesema Allah katika Sura hiyo hiyo:

((يَوْمَ نَحْشُرُ الْمُتَّقِينَ إِلَى الرَّحْمَٰنِ وَفْدًا * وَنَسُوقُ الْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا))

((Siku tutakapo wakusanya Wachamungu wakiwa wageni wakirimiwa kwa Mwingi wa rehema. * Na tutakapo wakokota waovu kuiendea Jahannamu kwa kuiingia)) [Maryam 85-86]

Kwa maana hiyo Wuruudi (Kuiingia) ni kwa Waovu tu si kwa Wachamungu.

Na amesema Allah mtukufu:

((إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ * لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا ۖ وَهُمْ فِي مَا اشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَالِدُونَ * لَا يَحْزُنُهُمُ الْفَزَعُ الْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ هَٰذَا يَوْمُكُمُ الَّذِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ))

((Hakika wale waliotanguliwa na kupata wema kutoka kwetu hao wataekwa mbali na moto * hawatasikia ndirimo zake nao katika yanayotamaniwa na nafsi zao watabakia * hautawahuzunisha mshitiko mkuu na watakutana na Malaika: Hii ndio siku yenu ambayo mulioahidiwa)). [Al-Anbiyaa 103-105]

Ama kuhusu Suala la Mizani sisi Itikadi yetu ni uzani wa zile mizani zilizotajwa katika Quraani tukufu, wala hatuna Itikadi na Mizani ya vitangara viwili vya kushindanisha mema kwa maovu, na tunasema wazi wazi kuwa Mizani hiyo ya vitangara viwili haipo Akhera wala haina utajo katika Quraani tukufu.

Kwa hakika Quraani imetuambia kuwa:

((وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ * وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ ))

((Uzani siku hiyo ni haki, basi yule ambaye mizani zake -ni nyingi- zitakua nzito hao ndiwo waliofanikiwa na yule ambaye mzani zake -ni nyingi- zitakua nyepesi hao ndiwo ambao wamezikhasiri nafsi zao kwa walivokua wakidhulumu kwa Aya zetu)) [A-Aaraaf 8-9]

Na Allah mtukufu amesema:

((فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ * وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ))

(Atakayetenda uzito wa tembe ya vumbi ya jema lolote ataiona * na atakayetenda uzito wa tembe ya vumbi ya shari yoyote ataiona) [Al-zilzalah 7-8]

Mchamungu ataona mizani za mema yake yaliyokubaliwa zimekua nzito na kuwa maovu yake yamesitiriwa na kuepushwa nayo atazidi furaha kwa hayo, ama fasiki muovu kafiri -ni sawa ukiwa ukafiri wake ni wa kishirikina (Mshirikina) au wa kineema (Mnafiki muislamu asi mkaidi wa kutubia)- yeye huyo ataona mema yake yamekataliwa kwa sababu ya ufasiki wake kwani Allah amawakubalia Wachamungu ambao ndio aliowatayarishia Pepo, basi huyo mizani za mema yake zimefifia kwani amezongwa na maovu yake na jahannamu ndio mafiko yake adumu humo milele.

Sasa ikiwa wewe umeamua kijidanganya kwa riwaya za kutengezewa kwa ajili ya matarajio hewa na ukaridhika kujinasibisha na Usalafi ukaacha uongofu wa Quraani ulio wazi na usio na shaka yoyote, ukakubali kubebeshwa fikra inayopingana na Quraani tukufu kwa kupitia nyimbo ya Fahamu ya Salafu Saalih, na ukaogopa kuitwa Muatwila na Mkhawariji shauri yako, jiulize tu hivi kweli atakua Saalih iwapo atapingana na Quraani tukufu?!!!

Hivi hamujui kuwa amesifiwa katika Uislamu yule aliyesifiwa kwa sababu ya kujishika vizuri na mafundisho ya Allah mtukufu, na amelaumiwa katika Uislamu yule aliyelaumiwa kwa sababu ya kutoheshimu mafundisho ya Allah mtukufu?

Hivi muna shaka na Kitabu cha Allah mtukufu?

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

 MSALAFI:

صفات الله ليست زائدة على ذات الله ولكنها هي عين ذاته .

Wanakataa sifa za Allah alizojisia Mwenyewe katika Qur’an na Mapokezi kutoka kwa Mtume wetu kuwa SIO HALISI bali wanazifanyia Falsafa katika Tafsiri

[Ahlu sunnah tunaamini sifa na majina ya Allah alizojisifia kama Kuchukia, kutabasam, Kusikia, kuona

kuwa Allah ana macho,Mikono miwili, miguu miwili lakini pia Ahlu sunnah tunaishia hapo Hatumfananishi Allah na viumbe wake wala hatukatai sifa zake]

JAWABU:

Kwanza nitoe tarjama ya neno letu alilolileta, ingawa limekatwa lakini linatosha, kwani Msalafi ameshindwa hata kutoa tarjama yake:

((Sifa za Allah si nyongeza juu ya dhati lakini ni dhati yenyewe))

Itikadi yetu Maibadhi ni kuwa sifa za Allah sio vitu vyengine visivokua Allah mtukufu mwenyewe tafauti na wanavoitakidi masalafi wenye kuitakidi Allah viungo na harakati.

Tumeitakidi hivo kwa sababu lau kuwa Sifa za Allah mtukufu ni vitu vyengine visivokua yeye basi italazimu mabatilifu yafuatayo:

 1. Kupangika kwa Dhati kwa kuwa na vinyambuliko na vigawiko na viungo vinavotegemeana baadhi yake, na hiyo ni hali ya kiumbe, basi vipi itakua kwa Muumba ambaye hafanani na chochote?!!
 2. Kupatikana vyatangu (visivo kuwa na mwanzo) vingi; kwani kila sifa itakua ni kitu kisichokua na mwanzo pamoja na Dhati husika.
 3. Kuwepo ufakiri wa Dhati kwa kuhitajia sifa hali ya kuwa sifa hizo hazina haja na Dhati; kwani Dhati itategemea Sifa.

Kutokana na hapo haiwezekani kabisa kuwa sifa za Allah ni vitu vyengine visivokua Allah mwenyewe, na kwa hilo ikalazimika kuitakidi kuwa Sifa zake ni yeye mwenyewe Allah mtukufu, na maana yake ni kujulisha ukamilifu wa kidhati wa Allah mtukufu kwa mujibu wa maudhui husika, na sio kuelezea kitu chengine kisichokua Dhati yake Allah mtukufu, Allah anajua kwa dhati yake, anaweza kwa Dhati yake, ni hai kwa Dhati yake, anasikia kwa Dhati yake, anaona kwa Dhati yake, anasema kwa Dhati yake, na namna hivi katika kumsifu Allah mtukufu, ujuzi wake ni wa kidhati, uwezo wake ni wa kidhati, uhai wake ni wa kidhati, usikivu wake ni wa kidhati, uoni wake ni wa kidhati, usemaji wake ni wa kidhati…..

Ama kuhusu neno la Msalafi:

[Ahlu sunnah tunaamini sifa na majina ya Allah alizojisifia kama Kuchukia, kutabasam, Kusikia, kuona.

kuwa Allah ana macho, Mikono miwili, miguu miwili, lakini pia Ahlu sunnah tunaishia hapo Hatumfananishi Allah na viumbe wake wala hatukatai sifa zake]

Tunamuambia huyu Msalafi:

Ulikua ufupishe safari tu kwa kusema kuwa nyinyi munamuitakidi Allah kuwa yuko katika sura ya Kijana barobaro (hana ndevu wala sharubu) kakaa kitako juu ya Arshi iliyobebwa na Malaika wanne, mmoja ana sura ya Mtu wanamme, na mmoja ana sura ya n`gombe dume, na mmoja ana sura ya Saqri (Agle), na mmoja ana sura ya simba. [Rf. Ibnu Khuzaimah – Tauhidi. Riwaya no 261. Ibn Hambal – Sunna Riwaya no. 175].

Au hujui ewe Msalafi kuwa Imamu wenu Ahmed bin Hambali aliulizwa kuhusu hadithi yenu (UONGO) inayosema kuwa Mtume S.A.W. alimuona Allah naye yuko katika sura ya kijana barobaro, basi alijibu:

“هذا الحديث رواه الكبر عن الكبر عن الصحابة عن النبي صلى الله عليه وسلم فمن شك في ذلك أو في شيء منه فهو جهمي لا تقبل شهادته ولا يسلم عليه ولا يعاد في مرضه”

Hii hadithi wameipokea WAKUU kutoka kwa WAKUU kutoka kwa MASAHABA kutoka kwa NABII S.A.W. basi yoyote atakayekuwa na shaka katika hadithi hiyo au chochote cha hadithi hiyo huyo ni MJAHAMIA ushahidi wake haukubaliwi, wala hasalamiwi huyo, na akiumwa hatembelewi huyo. [Ibtwaalu Taawilaati uk. 173 athari no 148]

Na Sheikh wa Uislamu wenu Ibnu Taimia amesema:

كما في الحديث الصحيح المرفوع عن قتادة عن عكرمة عن ابن عباس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: رأيت ربي في صورة شاب أمرد له وفرة حعد قطط في روضة خضراء.

Kama ilivyo katika Hadithi Sahihi iliyorufaishwa kutoka kwa Qatadah naye kutoka kwa Iqrimah naye kutoka kwa Ibnu Abbaas amesema: Amesema Mtume wa Allah S.A.W.: “Nilimuona Mola wangu yuko katika sura ya kijana barobaro ana mwenye timtimu chooko ndani ya bustani kijani” [Rf. Bayaanu Talbiisi Al-Jahmiyah juzuu ya 7 ukurasa 290].

Na hadithi hii pia kaisahihisha Al-Albani katika “Dhillahi Al-Janna fii Taaliqi Sunna” Hadithi no 440 ukurasa 192.

Sasa ulikua ufupishe safari tu uwambie watu kuwa Itikadi yenu ni kuwa Allah na mtu ni sawa sawa ila Allah haoti ndevu wala sharubu wala hazeeki tu, lakini mara macho mwili amra miguu miwili mara mikono wiliwi….maara lakini si mfano wa mtu. ya nini chenga nyingi?!!!!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here