Home All Jawabu Kwa Makadiani

Jawabu Kwa Makadiani

684
2
Accordion Content

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

بسم الله الرحمن الرحيم

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu mwenye kuongoza, na rehma na amani ziwe kwa Mtume wake wa mwisho naye ni Mtume wetu Muhammad, ziwe kwake pamoja na Aali wake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Kwa hakika miongoni mwa Fitna kubwa sana ni fitna za upotevu wa kiitikadi, na kila upotevu wa kiitikadi unavyokuwa mbaya zaidi ndivo fitna yake inakuwa mbaya zaidi, na miongoni mwa fitna kubwa za Kiitikadi ni fitna ya kudai unabii na utume baada ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w), kwani hilo linakuwa ni rajibio la kuiharibu dini na kuivuruga.

Kwa hakika Madajjali Wadai unabii walitokezea katika zama za Nabii wetu Muhammad (s.a.w), na waliendelea kutokeza baada ya Nabii Muhammad (s.a.w), basi Waislamu hawakutofautiana -kuanzia zama za Masahaba (r.a)- katika ulazima wa kuwapiga vita Wadaiunabii hao wa uongo, basi walihukumiwa kuwa wao ni Washirikina.

Mtume wetu Muhammad (s.a.w) amesema kwa uwazi kabisa:

سيكون في أمتي كذابون ثلاثون ، كلهم يزعم أنه نبي ، و أنا خاتم النبيين ، لا نبي بعدي ، و لا تزال طائفة من أمتي على الحق ظاهرين ، لا يضرهم من خالفهم ، حتى يأتي أمر الله

((Kutakuwa katika umma wangu majiongo thalathini, kila mmoja wao atadai kuwa yeye ni nabii, na mimi ndiye khitimisho la Manabii, hakuna nabii yoyote baada yangu, na halitoacha kundi katika umma wangu kuwepo katika haki wako wazi, hawadhuriwi na wenye kutafautina nao mpaka itafika amri ya Allah))

[Tirmidhi 2219, Ahmed 22395, Ibn Maajah 3952, Abu Daudi 4252]

Kwa hiyo Wadaiunabii waongo walitokezea, basi kutokezea mdaiunabii muongo sio jambo geni katika tarehe ya waislamu.

Imepokewa kuwa katika kipindi cha Mfalme Maamuni [218 Hijiria – 833 Miladiyah], aliletewa mwanamke aliyedai unabii, basi Mfalme Maamuni alimuuliza mwanamke huyo. Ni nani wewe? Akajibu: Mimi ni Fatima Nabii. Akamuambia: Jee! Unayaamini aliyokuja nayo Muhammad (s.a.w)?. Akasema: Ndio, hakika yote aliyokuja nayo -hayo- ni haki. Hapo Mfalme Maamuni akamuambia: Kwa hakika Muhammad (s.a.w) amesema: ((Hakuna nabii baada yangu)). Hapo yule Mdaiunabii wa kike akasema: Amesema kweli (s.a.w), Jee! Amesema: Hakuna nabii wa kike baada yangu?!!. Hapo Mfalme Maamuni akawambia waliokuwepo: Ama mimi nimeshamaliza, basi yoyote mwenye hoja na ailete, kisha akacheka mpaka ukakunjuka uso wake.

Na katika miaka isiyokuwa ya mbali sana alitokeza Mdaiunabii muongo katika nchi ya India naye ni Mirza Ghulam Ahmed wa Kadiani aliyekufa mwaka wa 1326 Hijiria sawa na 1908 Miladiyah, Mdaiunabii huyu alitokezea katika kipindi ambacho Waislamu huko India walikuwa wametawaliwa kimabavu na Walowezi wa Kiengereza, na bila ya shaka Mdaiunabii huyu alikuwa ni tunda la njama za Mkoloni dhidi ya Waislamu; kwa hiyo mpaka hivi leo kundi lake linapata hifadhi na usaidizi kamili kupitia kwa Maadui wa Uislamu.

Na katika aliyoandika huyo Mdaiunabii Mirza Ghulam Ahmed kwa Serikali ya Uengereza ambayo yanatupa picha kamili jinsi gani walivyotumiliwa kikamilifu na Walowezi hao wa Kizungu ni maandiko yake haya:

“Kwa hakika zimenifikia habari zilizofuatana kuwa baadhi ya mahasidi wenye kunifanyia uadui mimi na marafiki zangu kwa sababu ya kutofautiana katika Itikadi au kwa sababu nyengine yoyote, ni kuwa wanawafikishia viongozi wa serikali wakarimu mambo yaliyo dhidi yangu, mambo ambayo hayahusiani na uhakika uhusiano wowote, basi ninaogopea kuja ukawavaa viongozi wa serikali uongo wao mwingi na uchochezi wao wa kila siku, basi wakaja wakaweka dhana mbaya kwetu, na hapo zikaja zikapotea juhudi zetu zote za kujitolea, basi kwa hayo natarajia kwa Serikali kuendelea kufanya kazi pamoja na familia hii na ijaribu mapenzi yake upande wake na utendaji wake kwa ajili yake kwa muda wa miaka 50 yenye kufuatana, utendaji ambao wamekiri wafanyakazi wa serikali wakarimu katika barua zao kwake kukiri kuliko wazi kuwa ni ukoo wenye kutimiza vizuri majukumu yake na uko safi sana katika kuipenda Serikali kwa muda mrefu, basi nataraji kutoka kwa Serikali ishirkiane na chipuo hili ambalo imelipalilia kwa mkono wake tena ifanye hivyo kwa kila ukali na kuchukua hadhari na kuhakikisha hifadhi na baada ya kuhakikisha”

[Kitabu Bariyyah Hazainu Ruuhiyah 13/349-350]

Kundi hili la Mdaiunabii Mkadiani Mirza Ghalam Ahmed linajitangaza kwa kila njia, nalo linajiita kwa jina la Jamaatu Ahmadiyah Islaamiyah kwa kiswahili ni Kundi la Waislamu wa Kiahmadia, na maarufu kuwa wao ni Makadiani.

Ni haki kuliita kwa jina la Makadiani; kwa kuzingatia kuwa baada ya kufa Mdaiunabii wao wafuasi wake waligawika makundi mawili kila moja likadai kuwa ndilo lililo sawa katika mafundisho yake na kupelekea kuingizana katika upotofu wao kwa wao, tena tofauti yao ni katika asili ya msingi wao wa kiitikadi, na makundi hayo ni:

 1. Laahuuriyah (Malahori) hili limesema kuwa Mirza ni msafishaji tu wa dini.
 2. Qaadiyaniyah (Makadiani) hili limeshikilia madai batili ya Mdaiunabii, basi limeitakidi kuwa Mirza ni Mahadii na Masihi na Nabii na Mtume hasa.

Kwa hakika makundi haya yote mawili ni makundi ya Kishirikina kwani yanaogelea katika uongo na udajjali wa Mdaiunabii wa Kikadiani Mizra Ghulam Ahmed.

  Amesema Allah mtukufu kwenye Kitabu chake:

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللّهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوْحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنَزلَ اللّهُ

((Na nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah uongo au akasema: “Nimepewa Wahayi” hali ya kuwa hajapewa wahayi wa chochote, na mwenye kusema nitateremsha mfano wa aliyoteremsha Allah…))

[Al-Anaam 93.]

Kwa hakika Mdaiunabii Mrza Ghulam Ahmed ni mmoja katika ya madhalimu hao wakubwa wenye kumzulia Allah uongo na kusema kuwa wamepewa wahayi hali ya kuwa hawajapewa wahayi wa chochote, tena ni Mdaiunabii huyu amedai wazi wazi kuwa yeye ameleta mfano wa aliyoyaleta Allah kwa Mtume wake Muhammad (s.a.w).

Na kwa hakika Mtume wetu Muhammad (s.a.w) amesema wazi wazi:

لاَ نَبِيَّ بَعْدِيْ

((Hakuna Nabii yoyote baada yangu))

[Bukhari 3455, 3532 Muslim 1842, 2404 Tirmidhi 2219, 3730, 3731 Abu Daudi 4252 Ibnu Maajah 121 Ahmed 7960, 11272]

Basi kama tulivyotangulia kubainisha kuwa Umma huu haujakubaliana makubaliano yenye nguvu zaidi kuliko makubaliano la kufungika kwa mlango wa Unabii baada ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w), kwa hakika makubaliano hayo yalianza tokea wakati wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na baada yake katika kila karne mpaka hivi leo na Allah mtukufu amesema kwenye Kitabu chake:

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءتْ مَصِيرًا

((Na yoyote atakayejipinza na Mtume (Muhammad) baada ya kubainikiwa yeye na uongofu na akafuata isiyokuwa njia ya waumini basi tutamuelekeza huko alikoelekea na tutamfikisha Jahannamu, nayo ni mafikio mabaya yalioje))

[Nisaa 115]

Basi bila shaka Mdaiunabii Mirza Ghulam Ahmed ni mwenye kujipinza na Mtume Muhammad (s.a.w) baada ya kubainikiwa na uongofu, tena amefuata njia isiyokuwa ya Waumini tokea zama za Mtume Muhammad (s.a.w) mpaka hivi leo, basi yeye ni mwenye kuelekea na kundi lake katika shimo la Jahannamu.

Baada ya kupata uhakika huo tulioufafanua kuhusu kundi hili la Mdaiunabii Mizra Ghulam Ahmed, tunasema pia kuwa Allah mtukufu kwenye Kitabu chake ametubainishia ujanza wa wapotevu wote kwa kumuambia Mtume wetu Muhammad (s.a.w):

هُوَ الَّذِيَ أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ في قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاء الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاء تَأْوِيلِهِ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلاَّ اللّهُ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلاَّ أُوْلُواْ الألْبَابِ

((Yeye ndiye alikuteremshia Kitabu, sehemu yake ni aya za kuhukumishwa hizo ndizo mama wa kitabu (tegemeo) na nyengine ni za kubabaisha, basi wale ambao katika nyoyo zao kuna upotofu wao huzikimbilia zile zenye kubabaisha katika hicho (Kitabu) kwa kutaka kufitinisha na kutaka uhakika wake, na hajui uhakika wake isipokuwa Allah. Na waliozamia katika elimu wanasema tumekiamini chote zote zinatoka kwa Mola wetu. Na hawakumbuki isipokuwa wenye kufahamu vizuri))

[Aala Imraan 7]

Kwa hiyo kundi hili pia nimejaribu kutegemea Aya zenye kubabaisha katika Qur-aani kwa lengo la kuhakikisha majaribio ya kuthibitisha madai yao ya uongo, basi tutaingia katika kufuatilia majaribio yao hayo kama yalivyotufikia kupitia ndimi zao wenyewe na kutoa jawabu yakinifu ili iwe sababu ya kuongoka mwenye kutaka uongofu, na kurejea kwa aliyokokotwa na wimbi ya Mdaiunabii huyu na wafuasi wake, tutayafanya hayo kwa idhini ya Allah mtukufu.

Wabillahi Taufiiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

2. NEEMA YA UNABII KWA UMA HUU.
Ameanza mlinganiaji wa Kiahmadyah kwa kusema kuwa Utume ni neema na sio laana na kuwa umati huu wa Mtume Muhammad (s.a.w) umesifiwa na Allah mtukufu kuwa ni umati bora kabisa, kwa hiyo umati ulio bora kabisa haiwezekani ukakosa daraja yenye neema, kisha mlinganiaji wa Kiamadiyah akaleta Aya inayosema:

وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلهمْ أَكْثَر الْأَوَّلِينَ وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِمْ مُنْذَرِينَ

((Na kwa hakika walipotea kabla yao wengi wa mwanzo * na kwa hakika tulitumia kwao wao waonyaji))

[Saafat 37/71-72]

Yeye Aya hii ameipa tarjuma isemayo:

((Hapo kabla wingi wa watu walipo potea * Tukaleta waonyaji kati yao))

Tarjuma ambayo haikubaliani na maneno ya Aya husika.

Kisha akasema kuwa wako Mitume wa aina mbili:

1. Wako Mitume walioleta sheria mpya.

2. Wako Mitume ambao hawakuleta sheria mpya, bali walikuja kuwarudisha watu waliotoka nje ya Sheria.

Akasema kuwa hao wote ni neema, kwa maana hiyo daraja ya Unabii ni neema na hilo linathibitishwa na neno la Mussa alipowambia kaumu yake:

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنْبِيَاءَ وَجَعَلَكُمْ مُلُوكًا وَآتَاكُمْ مَا لَمْ يُؤْتِ أَحَدًا مِنَ الْعَالَمِينَ

((Na aliposema Mussa kuwambia kaumu yake, enyi kaumu yangu kumbukeni neema ya Allah kwenu kwa kujaalia kwenu Manabii na kukujaalieni Wafalme na amekupeni ambayo hajapewa yoyote katika walimwengu))

[Maaidah 20]

Na namna hivi Mlinganiaji wa Kiahamadiya alivyojaribu kutetea madai yao ya kuendelea kupatikana Mitume baada ya Mtume Muhammad (s.a.w) kwa kutegemea sababu ya kuwa Unabii ni neema ya Allah na umati huu ndio umati bora kabisa kwa hiyo haiwezekani kukosekana ndani yake neema hii.

JAWABU:

Kwa hakika unabii ni neema miongoni mwa neema za Allah mtukufu hili hakuna anayelipinga, kama ilivyokua umati huu wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ndio umati bora kabisa baina ya umati zilizopita, hili pia halina shaka na hakuna anayelipinga.

Ama suala la neema ya kuendelea Unabii katika umati huu ulio bora zaidi kuliko umati zote zilizopita, suala hili linalo maana mbili moja inakubalika nayo siyo waliyoishikilia hawa Waahmadiyah, na maana hiyo ni kuendelea Unabii wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) mpaka kumalizika kwa Dunia; kwa hakika sisi hatuna shaka kuwa Unabii wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ni Unabii wenye kuendelea katika umma huu bila ya kumalizika, na kuendelea kwa Unabii huu bila ya shaka ni neema kubwa zaidi; kwa sababu yeye ndiye Mtume bora zaidi katika ya Mitume ya Allah mtukufu aliyoileta kwa waja wake, na suala la ubora wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) kuliko Manabii wote ni suala wanalolikubali Waahmadiyah, basi tunasema: Kwa hakika kuendelea kwa Unabii wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ni kuendelea kwa mafundisho yake na Kitabu chake na kubakia wafuasi wa haki wenye kuendelea na mafundisho ya Unabii huo mpaka kusimama kwa Kiama, na hili ni moja ya sifa za Unabii wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na umati wake.

Amesema Allah mtukufu katika Kitabu chake kumwambia Mtume wetu Muhammad (s.a.w):

قُلْ هَٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

((Sema: Hii ndiyo njia yangu ninaita kwa Allah kwa uoni wa ndani mimi na mwenye kunifuata, na ametakasika Allah na mimi si katika washirkina))

[Youssuf 108]

Kwa hiyo Mtume wetu Muhammad (s.a.w) amefariki, na kwa kufariki kwake kumekatika kuteremka Wahayi lakini Utume wake na Unabii wake nao ndio nuru ya uongofu aliyokuja nayo ni yenye kuendelea na kubakia mpaka siku ya kiama, na bila ya shaka kama ilivyokuwa Unabii ni neema, na umati huu ndio umati bora zaidi, basi Allah mtukufu amejaalia kubakia kwa bora ya neema za Unabii katika umati huu, nao ni Unabii wa mbora wa Manabii naye ni Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na neema hiyo ni yenye kubakia katika umati wake mpaka kusimama kwa kiama.

Na uhakika huu anaueleza Mtume wetu Muhammad (s.a.w) pale aliyaposema yanayohusiana na neema hii ya Unabii na kutofautisha baina yetu na waliopita kabla yetu katika neema hii:

كانت بنو إسرائيل تَسُوسُهُمُ الأنبياء، كُلما هلك نبي خلفهُ نبيٌّ، وإنهُ لا نبيَّ بعدي

((Walikuwa Bani Israili wanaingozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii, na hakika mambo yalivyo hakuna nabii yoyote baada yangu))

[Bukhari 3455 Muslim 1842 Ibnu Maajah 2871]

Kwa hiyo neema ya kuendelea kwa Unabii katika umati huu ulio bora kuliko umati zilizopita kabla yake inatafautiana kinamna baina yake na umati zilizotangulia, wala hakuna ulazima wa kuwa sawa sawa kinamna; kwa sababu Allah mtukufu anafanya katika mamlaka yake anavyotaka, wala hafanyi anayofanya kwa njia ya kulazimika kuyafanya bali anafanya anayofanya kwa njia ya khiyari katika aliyotaka kuyafanya, kwa maana hiyo neno la kulazimisha katika vitendo vya Allah mtukufu ni neno batili.

Na sisi tunaposoma Kitabu cha Allah mtukufu mwanzo kabisa tunakutia ishara nzito ya hili tulilolieleza; kwani Allah mtukufu ametuambia:

الم ﴿1﴾ ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِلْمُتَّقِينَ ﴿2﴾ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ ﴿3﴾ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿4﴾ أُولَٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِنْ رَبِّهِمْ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿5﴾

((Alif laaam miiim * hiki ni kitabu hakina shaka ndani yake ni uongofu kwa wachamungu * ambao wanaamini ya yaliyofichika (ghaibu) na wanasimamisha sala na katika tuliyowaruzuku wanatoa * ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako na kwa akhera wao ni wenye yakini * hao ndio walio katika uongofu utokao kwa Mola wao, na hao ndio waliofanikiwa))

[Baqarah 2/1-5]

Katika Aya ya nne katika sura hiyo ya pili Allah mtukufu anafafanua yale yanayolazimika kuyaamini kuwa hayo ndiyo yaliyotoka kwake nayo ni:-

Yale aliyoteremshwa kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w).
Yale yaliyoteremshwa kabla yake Mtume wetu Muhammad (s.a.w).
Na haya yote yanakusanya aliyoyateremsha kwa Manabii wote, wala hakututajia Allah mtukufu habari ya kuamini yatakayoteremshwa baada ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w), kwa hakika katika hili kuna Ishara ya wazi kuwa hakuna Mtume wala Nabii baada ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w); kwani hakuna uteremsho wa Wahayi utakaofuata baada ya kuondoka Mtume wetu Muhammad (s.a.w), na lau kuwa kuna uteremsho mwengine wa Wahayi basi isingetosha kupatikana uongofu na mafanikio kwa kuamini yaliyoteremshwa na Allah mtukufu kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na yaliyoteremshwa kabla yake tu, kama ilivyo katika Aya hizi tukufu.

Kwa maana hiyo, tunawambia Waahamadiyah kuwa: Neema ya Unabii uliobora zaidi nao ni mafundisho ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w), hiyo ni neema iliyopatikana kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) nayo ni kwa ajili ya umati wake, neema hii imeendelea kuwepo na itaendelea kuwepo mpaka kusimama kwa Kiama.

Ama maana ya pili ya kuendelea kwa Unabii nayo ndiyo maana wanayoikusudia Waahamdiyah, nayo ni maana ya kuendelea kupatikana wahayi mpya kwa kupatikana Manabii wengine baada ya Mtume Muhammad (s.a.w), hili ndilo kusudio lao Waahmadiyah katika kuelezea wanayoamini kuwa ni hoja yao, na hilo ndilo walilolikusudia kuwa ndiyo neema ya Unabii, yaani neema ya kuendelea kupatika Manabii bila ya kumalizika mpaka kusimama Kiama.

Mbali na ishara za wazi za kuonesha kubatilika kusudio lao hilo katika tuliyoeleza hapa katika maana ya mwanzo, lakini pia tutaingia kulizungumzia hilo katika sehemu ijayo ya jawabu yetu hii kwa Idhini ya Allah mtukufu.

Asante sana.

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

3. NJIA YA WALIONEEMESHWA.
Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu mwenye kuongoza, na rehma na amani ziwe kwa Mtume wake aliye mwisho wa Manabii naye ni Mtume wetu Muhammad, ziwe kwake pamoja na Aali wake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Ndugu zangu tukiwa tumo katika kuzijibu shubuhati za Kikadiani (Ahmadiyah) kama tulivyoahidi katika sehemu ya pili ya jawabu yetu hii, kuwa tutazungumzia kusudio lao hawa Kadiani kuhusiana na kuendelea neema ya Unabii na kuonesha ubatilifu wa shubuha yao hiyo katika sehemu hii.

Kama alivyokariri mlinganiaji wao kwa kusema zaidi ya mara moja kuwa: ‘Waislamu tunamuomba Allah katika kila rakaa ya sala kuwa atuongoze katika njia ya wale alowaneemesha na sio njia ya wale waliokasirikiwa wala ya wale waliopotea, na alowaneemesha Allah mtukufu amewataja kwenye Kitabu chake katika Suraati Nisaa pale aliposema:

((وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَئِكَ رَفِيقًا))

((Na mwenye kumtii Allah na Mtume, basi hao ni pamoja na ambao amewaneemesha Allah katika Manabii na Wasadikishaji na Mashahidi na Wema, na uzuri mkubwa kuwa pamoja nao))

[Nisaa 69]’

Naye akasema kuwa katika Aya hii kumetajwa makundi ya aliowaneemesha Allah mtukufu nayo ni:

Manabii.
Wasadikishaji.
Mashahidi.
Wema.
Akasema kuwa neema hizi ni lazima zote zipatikane katika Umma huu, kwa hiyo ni lazima wapatikane Manabii baada ya Muhammad (s.a.w) kama ilivyokuwa ni lazima wapatikane Wasadikishaji na Mashahidi na Wema.

Kisha baada ya hapo mlinganiaji wa Ukadiani akasema kuwa wenye kukataa neema ya kupatikana Manabii baada ya Muhammad hao ni sawa na watu wa Mtume Youssuf (a.s) ambao Allah ametupa habari yao:

((وَلَقَدْ جَاءَكُمْ يُوسُفُ مِنْ قَبْلُ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا زِلْتُمْ فِي شَكٍّ مِمَّا جَاءَكُمْ بِهِ حَتَّى إِذَا هَلَكَ قُلْتُمْ لَنْ يَبْعَثَ اللَّهُ مِنْ بَعْدِهِ رَسُولًا كَذَلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ مُرْتَابٌ))

((Kwa hakika alikujeni Youssuf hapo kabla kwa mabainisho basi hakuacha kuwa katika shaka kwa aliyokujeni nayo, mpaka alipokufa mukasema: Hatotuma Allah baada yake Mtume yoyote, namna hivo anampoteza Allah yule aliyepinduka mipaka wenye wasi wasi (shaka)))

[Ghaafir 34]

JAWABU:
Sisi tunamshukuru Allah mtukufu kwa neema zake, na kama tulivyotangulia kusema kuwa Unabii ni miongoni mwa neema kubwa kabisa, na kwa sababu huu tuliomo ndani yake ndio uma ulio bora kabisa basi Allah mtukufu ameuhusisha kwa Unabii ulio bora kabisa, nao ni Unabii wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ambaye ndiye mbora wa Mitume na Manabii, kwa hiyo Unabii ni neema hili halina mzozo ndani yake, basi tunasema kuwa: ‘Neema hii ya Unabii bado inaendelea katika Umma huu kwa kuendela Unabii wa Mtume Muhammad (s.a.w) mapka kitasimama Kiama.’

Ama kuhusu Dua tunayomuomba Allah mtukufu katika kila rakaa ya Sala, kwa hakika sisi tunachomuomba Allah mtukufu ni kutuongoza katika njia ya wale aliowaneemesha Allah mtukufu na hili liko wazi halihitaji ufafanuzi sana, na njia hiyo ambayo tunamuomba Allah atujaalie kuwemo ndani yake ni njia ya wote aliowataja Allah mtukufu katika Aya ya Suratu Nisaa, basi ni njia ipi hiyo? Hiyo ni njia ya Manabii na Mashahidi na Maswiddiki na Wema, nayo ndiyo njia ya kila mchamungu.

Kwa hiyo sisi hatujamuomba Allah mtukufu tuwe Manabii, wala tuwe Mashahidi, wala tuwe Maswiddiki, wala tuwe Wema kama anavyofikiria huyu Mkadiani na wapotoshaji wa kundi lake, tunasema kuwa sisi tunachomuomba Allah mtukufu katika kila rakaa ya sala ni kutuongoza katika njia yao hao wema aliowataja.

Sasa njia hiyo tunayomuomba Allah mtukufu atuongoze ndani yake ni njia ipi?

Hili ndilo suali ambalo Mkadiani hakulijua au kalikwepa kimakusudi kwa lengo la kupotosha makusudio ya Aya tukufu.

Basi sisi tunamwambia kuwa: Kwa bahati nzuri jawabu ya suali hili limebainishwa na Allah mtukufu katika Aya hiyo hiyo ya Surati Nisaa; kwani Allah mtukufu ametuambia humo kuwa ((Na mwenye kumtii Allah na Mtume …..)) kwa maana hiyo njia yao hao waliotajwa na ambayo tunamuomba Allah mtukufu atuongoze katika njia hiyo ni njia ya kumtii Allah na Mtume wake, nayo ni njia ya Wachamungu wote.

Kwa maana hiyo, madai ya kudai kuwa sisi tunaomba tuwe ima Manabii au Mashahidi au Maswiddiki au Wema, hayo ni madaihewa na batili, tena ni madai yasiyokuwa na hoja ya kuyasimamisha wala ya kuyathibitisha.

Tuangalie ndugu zangu maombi tunamuomba Allah mtukufu katika kila Rakaa:

((6. Tuongoe njia iliyo nyooka. 7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.))

Kwa hiyo sisi tunachomuomba Allah ni kutupa uongofu wa kuwa katika njia ya aliowaneemesha, na njia yao ni njia ya kumtii yeye Allah mtukufu katika hii Dunia, nayo ndiyo njia ya hao waliotajwa katika Surati Nisaa, wala hakuna khilafu katika hili aslan.

Na ubainisho wa kuwa pamoja nao, ni kuwa pamoja nao katika Pepo na Maridhio ya Mola mtukufu, kama tutakavyokuwa pamoja nao katika njia yao ya kumtii Allah mtukufu, na haya ndiyo yaliyobainishwa katika sababu hasa ya kuteremka kwa Aya hiyo ya Surati Nisaa.

Anatuambia Imamu Qutub Al-Aimah (r.a) katika Tafsiri yake akibainisha sababu ya kuteremka Aya hii:

((قال رجل : يا رسول الله لقد أحببتك حبا ما أحببته شيئا قط ، ولأنت أحب الى من والدى والناس اجمعين ، فكيف لى برؤيتك ، إن أنا دخلت الجنةن ولم يرد اليه شيئا ، فأنزل الله : { وَمَن يُطِعِ اللهَ وَالرَّسُولَ } الآية فدعاه رسول الله صلى الله عليه وسلم فتلاها عليه .))

“Alisema mtu: Ewe Mjumbe wa Allah, kwa hakika nimekupenda mapenzi ambayo sijawahipo kukipenda kitu (mfano wake), kwa hakika wewe unapendeza zaidi kwangu kuliko baba yangu na watu wote, basi vipi nitakuona ikiwa mimi nitaingia Peponi? Basi hakumjibu kitu. Akateremsha Allah mtukufu ((Na mwenye kumtii Allah na Mtume..)) Aya. Basi Mtume wa Allah (s.a.w) akamwita yule kijana na akamsomea hiyo Aya.”

Ama kuhusu Aya iliyoko katika Suraatu Ghaafir inayohusiana na Mtume Youssuf (a.s), tunafahamu sote kuwa maneno ya Aya hiyo yanawahusu watu maalumu katika zama maalumu, na watu hao ni Firauni (l.a) na watu wake wala sio watu wa Mtume Youssuf A.S kama alinyodai Mkadiani, kwani hayo ni Maneno ya Muumini katika watu wa Firauna akiyaelekeza kwa Mdai Uungu Firauna L.A na kaumu yake, basi kipindi cha maneno hayo kilikuwa ni zama za Mtume Mussa (a.s), kwa hiyo maneno hayo kwanza walielekezewa wasiokuwa waislamu asalan; kwani walielekezewa watu wanao itakidi kuwa Firauna ndiye mungu wao, kwa hiyo sio hoja kwa Waislamu wa wakati ule ambao wamo katika Imani sahihi ya kuamini kuja kwa Mitume baada ya Mtume Youssuf (a.s) bali na kuamini kwao kuja kwa Mitume na Manabii baada ya Mtume Mussa (a.s), na kwa neema hiyo aliwakumbusha Mussa (a.s) watu wake. Na inafahamika kuwa kila umma una mahusisho yake; ikiwa Wana wa Israili walihusishwa kwa neema ya kupatikana Manabii wa kuendelea, basi Umma wa Mtume Muhammad (s.a.w) umehusishwa kwa kuhifadhika kwa Unabii wa Muhammad (s.a.w) bila kukatika, na kwa hilo Allah mtukufu akauhifadhia Umma huu mafundisho ya Mtume wake (s.a.w) kwa kuyahifadhi katika asili yake. Kwa hakika Allah ameuneemesha Umma huu kwa kuhifadhika Kitabu chake na lugha ya Mtume wake, tena kwa kupokezana hayo kizazi kwa kizazi, neema ambayo hawakupata waliopita kabla.

Kwa hiyo Aya iliyoko katika Suratu Ghaafir sio hoja kwa watu wa Umma huu kwani inawaelekea Firauni na watu wake, nao hawakuwa wasilamu aslan, achilia mbali kuwa ni watu wa Mtume Issa A.S. au Mtume Muhammad aliye khitimisho la Manabii wote S.A.W.

Wabbilahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

3. NJIA YA WALIONEEMESHWA.
Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu mwenye kuongoza, na rehma na amani ziwe kwa Mtume wake aliye mwisho wa Manabii naye ni Mtume wetu Muhammad, ziwe kwake pamoja na Aali wake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Ndugu zangu tukiwa tumo katika kuzijibu shubuhati za Kikadiani (Ahmadiyah) kama tulivyoahidi katika sehemu ya pili ya jawabu yetu hii, kuwa tutazungumzia kusudio lao hawa Kadiani kuhusiana na kuendelea neema ya Unabii na kuonesha ubatilifu wa shubuha yao hiyo katika sehemu hii.

Kama alivyokariri mlinganiaji wao kwa kusema zaidi ya mara moja kuwa: ‘Waislamu tunamuomba Allah katika kila rakaa ya sala kuwa atuongoze katika njia ya wale alowaneemesha na sio njia ya wale waliokasirikiwa wala ya wale waliopotea, na alowaneemesha Allah mtukufu amewataja kwenye Kitabu chake katika Suraati Nisaa pale aliposema:

((وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَئِكَ رَفِيقًا))

((Na mwenye kumtii Allah na Mtume, basi hao ni pamoja na ambao amewaneemesha Allah katika Manabii na Wasadikishaji na Mashahidi na Wema, na uzuri mkubwa kuwa pamoja nao))

[Nisaa 69]’

Naye akasema kuwa katika Aya hii kumetajwa makundi ya aliowaneemesha Allah mtukufu nayo ni:

Manabii.
Wasadikishaji.
Mashahidi.
Wema.
Akasema kuwa neema hizi ni lazima zote zipatikane katika Umma huu, kwa hiyo ni lazima wapatikane Manabii baada ya Muhammad (s.a.w) kama ilivyokuwa ni lazima wapatikane Wasadikishaji na Mashahidi na Wema.

Kisha baada ya hapo mlinganiaji wa Ukadiani akasema kuwa wenye kukataa neema ya kupatikana Manabii baada ya Muhammad hao ni sawa na watu wa Mtume Youssuf (a.s) ambao Allah ametupa habari yao:

((وَلَقَدْ جَاءَكُمْ يُوسُفُ مِنْ قَبْلُ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا زِلْتُمْ فِي شَكٍّ مِمَّا جَاءَكُمْ بِهِ حَتَّى إِذَا هَلَكَ قُلْتُمْ لَنْ يَبْعَثَ اللَّهُ مِنْ بَعْدِهِ رَسُولًا كَذَلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ مُرْتَابٌ))

((Kwa hakika alikujeni Youssuf hapo kabla kwa mabainisho basi hakuacha kuwa katika shaka kwa aliyokujeni nayo, mpaka alipokufa mukasema: Hatotuma Allah baada yake Mtume yoyote, namna hivo anampoteza Allah yule aliyepinduka mipaka wenye wasi wasi (shaka)))

[Ghaafir 34]

JAWABU:
Sisi tunamshukuru Allah mtukufu kwa neema zake, na kama tulivyotangulia kusema kuwa Unabii ni miongoni mwa neema kubwa kabisa, na kwa sababu huu tuliomo ndani yake ndio uma ulio bora kabisa basi Allah mtukufu ameuhusisha kwa Unabii ulio bora kabisa, nao ni Unabii wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ambaye ndiye mbora wa Mitume na Manabii, kwa hiyo Unabii ni neema hili halina mzozo ndani yake, basi tunasema kuwa: ‘Neema hii ya Unabii bado inaendelea katika Umma huu kwa kuendela Unabii wa Mtume Muhammad (s.a.w) mapka kitasimama Kiama.’

Ama kuhusu Dua tunayomuomba Allah mtukufu katika kila rakaa ya Sala, kwa hakika sisi tunachomuomba Allah mtukufu ni kutuongoza katika njia ya wale aliowaneemesha Allah mtukufu na hili liko wazi halihitaji ufafanuzi sana, na njia hiyo ambayo tunamuomba Allah atujaalie kuwemo ndani yake ni njia ya wote aliowataja Allah mtukufu katika Aya ya Suratu Nisaa, basi ni njia ipi hiyo? Hiyo ni njia ya Manabii na Mashahidi na Maswiddiki na Wema, nayo ndiyo njia ya kila mchamungu.

Kwa hiyo sisi hatujamuomba Allah mtukufu tuwe Manabii, wala tuwe Mashahidi, wala tuwe Maswiddiki, wala tuwe Wema kama anavyofikiria huyu Mkadiani na wapotoshaji wa kundi lake, tunasema kuwa sisi tunachomuomba Allah mtukufu katika kila rakaa ya sala ni kutuongoza katika njia yao hao wema aliowataja.

Sasa njia hiyo tunayomuomba Allah mtukufu atuongoze ndani yake ni njia ipi?

Hili ndilo suali ambalo Mkadiani hakulijua au kalikwepa kimakusudi kwa lengo la kupotosha makusudio ya Aya tukufu.

Basi sisi tunamwambia kuwa: Kwa bahati nzuri jawabu ya suali hili limebainishwa na Allah mtukufu katika Aya hiyo hiyo ya Surati Nisaa; kwani Allah mtukufu ametuambia humo kuwa ((Na mwenye kumtii Allah na Mtume …..)) kwa maana hiyo njia yao hao waliotajwa na ambayo tunamuomba Allah mtukufu atuongoze katika njia hiyo ni njia ya kumtii Allah na Mtume wake, nayo ni njia ya Wachamungu wote.

Kwa maana hiyo, madai ya kudai kuwa sisi tunaomba tuwe ima Manabii au Mashahidi au Maswiddiki au Wema, hayo ni madaihewa na batili, tena ni madai yasiyokuwa na hoja ya kuyasimamisha wala ya kuyathibitisha.

Tuangalie ndugu zangu maombi tunamuomba Allah mtukufu katika kila Rakaa:

((6. Tuongoe njia iliyo nyooka. 7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.))

Kwa hiyo sisi tunachomuomba Allah ni kutupa uongofu wa kuwa katika njia ya aliowaneemesha, na njia yao ni njia ya kumtii yeye Allah mtukufu katika hii Dunia, nayo ndiyo njia ya hao waliotajwa katika Surati Nisaa, wala hakuna khilafu katika hili aslan.

Na ubainisho wa kuwa pamoja nao, ni kuwa pamoja nao katika Pepo na Maridhio ya Mola mtukufu, kama tutakavyokuwa pamoja nao katika njia yao ya kumtii Allah mtukufu, na haya ndiyo yaliyobainishwa katika sababu hasa ya kuteremka kwa Aya hiyo ya Surati Nisaa.

Anatuambia Imamu Qutub Al-Aimah (r.a) katika Tafsiri yake akibainisha sababu ya kuteremka Aya hii:

((قال رجل : يا رسول الله لقد أحببتك حبا ما أحببته شيئا قط ، ولأنت أحب الى من والدى والناس اجمعين ، فكيف لى برؤيتك ، إن أنا دخلت الجنةن ولم يرد اليه شيئا ، فأنزل الله : { وَمَن يُطِعِ اللهَ وَالرَّسُولَ } الآية فدعاه رسول الله صلى الله عليه وسلم فتلاها عليه .))

“Alisema mtu: Ewe Mjumbe wa Allah, kwa hakika nimekupenda mapenzi ambayo sijawahipo kukipenda kitu (mfano wake), kwa hakika wewe unapendeza zaidi kwangu kuliko baba yangu na watu wote, basi vipi nitakuona ikiwa mimi nitaingia Peponi? Basi hakumjibu kitu. Akateremsha Allah mtukufu ((Na mwenye kumtii Allah na Mtume..)) Aya. Basi Mtume wa Allah (s.a.w) akamwita yule kijana na akamsomea hiyo Aya.”

Ama kuhusu Aya iliyoko katika Suraatu Ghaafir inayohusiana na Mtume Youssuf (a.s), tunafahamu sote kuwa maneno ya Aya hiyo yanawahusu watu maalumu katika zama maalumu, na watu hao ni Firauni (l.a) na watu wake wala sio watu wa Mtume Youssuf A.S kama alinyodai Mkadiani, kwani hayo ni Maneno ya Muumini katika watu wa Firauna akiyaelekeza kwa Mdai Uungu Firauna L.A na kaumu yake, basi kipindi cha maneno hayo kilikuwa ni zama za Mtume Mussa (a.s), kwa hiyo maneno hayo kwanza walielekezewa wasiokuwa waislamu asalan; kwani walielekezewa watu wanao itakidi kuwa Firauna ndiye mungu wao, kwa hiyo sio hoja kwa Waislamu wa wakati ule ambao wamo katika Imani sahihi ya kuamini kuja kwa Mitume baada ya Mtume Youssuf (a.s) bali na kuamini kwao kuja kwa Mitume na Manabii baada ya Mtume Mussa (a.s), na kwa neema hiyo aliwakumbusha Mussa (a.s) watu wake. Na inafahamika kuwa kila umma una mahusisho yake; ikiwa Wana wa Israili walihusishwa kwa neema ya kupatikana Manabii wa kuendelea, basi Umma wa Mtume Muhammad (s.a.w) umehusishwa kwa kuhifadhika kwa Unabii wa Muhammad (s.a.w) bila kukatika, na kwa hilo Allah mtukufu akauhifadhia Umma huu mafundisho ya Mtume wake (s.a.w) kwa kuyahifadhi katika asili yake. Kwa hakika Allah ameuneemesha Umma huu kwa kuhifadhika Kitabu chake na lugha ya Mtume wake, tena kwa kupokezana hayo kizazi kwa kizazi, neema ambayo hawakupata waliopita kabla.

Kwa hiyo Aya iliyoko katika Suratu Ghaafir sio hoja kwa watu wa Umma huu kwani inawaelekea Firauni na watu wake, nao hawakuwa wasilamu aslan, achilia mbali kuwa ni watu wa Mtume Issa A.S. au Mtume Muhammad aliye khitimisho la Manabii wote S.A.W.

Wabbilahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

4. MITUME KWA WANA WA ADAM.
Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu mwenye kuongoza, na rehma na amani ziwe kwa Muhammad aliye khitimisho la Manabii pamoja na Aali wake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Ama baad,,,

Kwa hakika kundi pofu la Kiahmadia (Kadiani) likiwa katika rajibio la kuthibitisha madai yao batili ya kuendelea kutumwa Mitume na Manabii baada ya Mtume Muhammad S.A.W amejaribu kuipotosha Aya ya 35 ya Suuratu Al-Aarafi isemayo:

يَا بَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي فَمَنِ اتَّقَى وَأَصْلَحَ فَلاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ

((Enyi wana wa Adamu pindi wakikujieni Mitume miongoni mwenu wanaokuelezeni Aya zangu, basi yule ambaye ataepuka maovu na akatengenea, hao hakutakuwa na khofu kwao nao hawatahuzunika))

Kwanza: Wao wameipa Aya hiyo tafsiri isiyo kuwa sahihi nayo ni ((Enyi Wanadamu, bila shaka watakufikieni Mitume kutoka miongoni mwenu watawaelezeni Aya Zangu…)).

Pili: Makadiani wamesema kuwa Allah mtukufu amewaambia maneno hayo walio hai na sio waliokwisha kufa, kwa hiyo wakusudiwa ni watu wa zama za Mtume Muhammad S.A.W na watakaofuata baada yake, na kwa sababu Muhammad S.A.W alikuwa Mtume aliyeteremshiwa aya hii basi yeye siye mkusudiwa wa hao Mitume waliotajwa, bali wakusudiwa ni Mitume wataofuata baada yake, kwa maana hiyo mlango wa kutumwa Mitume na Mnabii haukufungwa kama inavyodaiwa, bali uko wazi Allah anatuma Mitume yake wakati wowote akitaka, na miongoni mwa Mitume hiyo ni Mkadiani Mirza Ghulamu Ahmed.. hayo ndiyo maneno yao.

JAWABU:
Bila shaka inajulikana kuwa Quraani tukufu haijipinzi nayo inatupa habari za matokeo ya zama tafauti, basi kama ilivyokua hatuwezi kusema kuwa neno la Allah:

يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَى لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا

((Ewe Zakariyah, Hakika sisi tunakubashiria kijana jina lake ni Yahya, hatukumjaalia kuwa na somo hapo kabla))

[Maryam 2]

Na neno la Allah mtukufu kuhusu mtoto huyo mwema:

وَسَلَامٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا

((Na amani iko juu yake siku aliyozaliwa na siku atayokufa na siku atayofufuliwa hai))

[Maryam 15]

kuwa maneno hayo aliambiwa mfu aliyekweisha kufa ambaye hayupo katika zama za Mtume Muhammad S.A.W., na kuwa mtoto huyo ambaye ni Nabii Yahya bado hajafa kama ilivyokua bado hajafufuliwa kwani haikusemwa siku aliyokufa bali imesemwa siku atakayokufa, vile vile hatuwezi kusema kuwa ((Enyi Wana wa Adam pindi wakikujieni Mitume miongoni mwenu…)) kuwa waliambiwa wafu kama wanavokejeli Maahmadia.

Kwa hakika lau kuwa uhakika ni kama wanavosema Makadiani kuhusu Aya hiyo basi ingalisema ((Enyi Watu ….)) au ((Enyi Mulioamini….)) kama ilivyo katika Aya nyingi, wala isingalisema ((Enyi Wana wa Adamu…..)).

Kutokana na hapo utafahamu kuwa madai ya Makadiani kuhusu Aya hiyo ni madai hewa yaliyojengwa juu ya msingi wa kupotosha andiko.

Kwa hakika Aya hiyo tukufu ni uchambuzi wa neno lake Allah mtukufu wakati Baba yetu Adamu na Mama yetu Hawa -alaihima salaamu- wanatolewa Peponi na kujaaliwa maisha ya kutahiniwa wao na kizazi chao katika Ardhi kama alivyotuambia Allah mtukufu kaatika Kitabu chake:

قُلْنَا اهْبِطُواْ مِنْهَا جَمِيعاً فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ

((Tukasema: Shukeni humo nyote, na pindi ukikujieni uongofu kutoka kwangu basi yule ambaye atafuata uongofu wangu hakuta kuwa na khofu kwao na hao hawatozunika))

[Baqarah 38].

Basi tunafahamu wazi wazi kuwa hayo wanayojishika nayo kibubusa hao Makadiani ni maneno yaliyoelekezwa kwa Watoto wa Adamu (Wana wa Adamu) tokea wakati huo wa Adamu na Hawa na kuendelea mapka siku ya kiama, kwa hiyo kila alipokuja Mtume yoyote alikumbusha agizo hilo na alitoa bishara ya Mtume anayefuata baada yake, naye anapokuja anapewa alama ya kusadikisha ujio wake ambayo ni kitambulisho cha kuhakikisha kuwa yeye ndiye mkusudiwa nayo huwa ni muujiza yakinifu, na sote unafahamu kuwa hakuna Nabii bila ya kuteremshiwa wahayi utokao kwa Allah mtukufu, na Allah mtukufu katika Kitabu chake Quraani tukufu anasema kuhusiana na waja wake waumini wachamungu waliofanikiwa kuwa wao ni:

والَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ

((Na ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako (Muhammad) na yaliyoteremshwa kabla yako (Mitume waliokua kabla ya Muhammad), nao wana yakini na Akhera))

[Baqarah 4]

Kwa hakika lau kuwa kuna mengine atakayoyateremsha Allah baada ya Mtume Muhammad S.A.W bila shaka isingalithibitishwa imani ya waumini na kufanikiwa kwao bila ya kuyaamini hayo kama ilivyokua imani yao haikuthibitishwa bila ya kuyaamini yaliyoteremshwa hapo kabla, na kutokana na hilo lingalikuja katika Aya hiyo neno ((Na ambayo tutateremsha baada yako)) na neno hilo halimo kabisa, si katika Aya hiyo wala nyengine yoyote katika Quraani tukufu, lakini Makadiani kama kawaida yao kuitungia Quraani maana isiyokuwa yake, basi wamelipa tamko (Al-Aakhirati) maana ya ((Yale yatayokuja baadae)) nayo ni maana inayosutwa na Quraani yenyewe, pia inasutwa na lugha ya Kiarabu, kama inavyosutwa maana hiyo na mjengeko wa Aya yenyewe; kwani Quraani haipinzani nayo imelazimisha imani ya kuamini Akhera na kuwa haiwezekani kufanikiwa kwa imani bila ya kuamini Akhera, nayo ndiyo iliyotajwa katika Aya tukufu, na juu ya yote hayo ufafanuzi wa Aya hiyo umekuja katika Aya mbili za Quraani tukufu nazo ni:

((Semeni Tumemuamini Allah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismaili na Is-haaka na Yaaqubu na Asbaati na waliyopewa Musaa na Issa, na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao, hatufarikishi baina ya yoyote kati yao na sisi ni wenye kusilamisha kwake (Waislamu) * Basi Wakiamini kama mulivyo yaamini watakuwa wameongoka, na wakikengeuka kwa hakika hao watakuwa katika kujimegua….)) [Baqarah 136-137].
((Sema: Tumeamini Allah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismaili na Is-haaka na Yaaqubu na Asbaati na waliyopewa Mussa na Issa na Manabii kutoka kwa Mola wao, hatutafautishi baina ya yoyote kati yao na sisi ni wenye kujisalimisha kwake (Waislamu) * Na wenye kutaka dini isiyokuwa ya Uislamu haitokubaliwa kwake, naye katika Akhera ni miongoni mwa waliokhasirika)) [Aala Imraani 84-85]
Aya hizo zote hazikutaja yatakayoteremshwa wala watakayopewa, bali zimetaja yaliyoteremshwa na waliyopewa kwani taayari yalishatokea; kwa hiyo hakuna chochote kitakachoteremshwa kwa yoyote baada ya Mtume Muhammad S.A.W, mpaka kitasimama Kiama.

BASI HAKUNA NABII BAADA YA MUHAMMAD S.A.W. WALA MTUME.

Vile vile katika Aya hizo kuna dalili ya wazi kuwa yoyote ayakayejivisha itikadi ya kuamini kuwepo uteremsho wa Wahyi baada ya Muhammad basi huyo anafuata dini isiyokuwa ya Uislamu na huyo amejimegua na kujiondosha katika safu ya Mtume Muhammad S.A.W. naye anaelekea motoni pamoja na Nabii wake wa Uongo akiwa ni Mkadiani Mirza Ghulamu Ahmed au mwengine yoyote, basi tujihadhari ya upofu na upotoshaji wa Makadiani.

Mtume wetu Muhammad (s.a.w) amesema kwa uwazi kabisa:

سيكون في أمتي كذابون ثلاثون ، كلهم يزعم أنه نبي ، و أنا خاتم النبيين ، لا نبي بعدي ، و لا تزال طائفة من أمتي على الحق ظاهرين ، لا يضرهم من خالفهم ، حتى يأتي أمر الله

((Kutakuwa katika umma wangu majiongo thalathini, kila mmoja wao atadai kuwa yeye ni nabii, na mimi ndiye khitimisho la Manabii, hakuna nabii yoyote baada yangu, na halitoacha kundi katika umma wangu kuwepo katika haki wako wazi, hawadhuriwi na wenye kutafautina nao mpaka itafika amri ya Allah))

[Tirmidhi 2219, Ahmed 22395, Ibn Maajah 3952, Abu Daudi 4252]

Wabillahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

5. AYA ZA AHADI (MIITHAAQ) YA MANABII (A.S.W).
Shukurani ni kwa Allah mtukufu mwenye kuongoza, na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad aliye mwisho wa Manabii pamoja na Aali wake na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Ama baad,,,

Tumewakuta Maahmadiyah (Makadiani) wanatumia pia Aya ya Miithaaq iliyoko katika Suuratu Aala Imraana na kuifanya kuwa kishikio chao katika madai yao hewa, na Aya hiyo inasema:

وَإِذْ أَخَذَ اللّهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّيْنَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَى ذَلِكُمْ إِصْرِي قَالُواْ أَقْرَرْنَا قَالَ فَاشْهَدُواْ وَأَنَاْ مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ

((Na alipochukua Allah ahadi nzito (Miithaaq) ya Manabii, ya kuwa nitapokupeni kitabu chochote na hekima yoyote kisha akakujieni Mtume mweye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi, ya kuwa mutamuamini na mutamnusuru (mutamsaidia). Akasema: Jee! Mumekubali na mumechukua juu ya hilo ahadi yangu? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni na mimi ni pamoja na nyinyi katika Mashahidi))

[3-Aala Imraan 81]

Makadiani husema kuwa Ahadi hii ni ile iliyotajwa katika Suuratu Al-Ahzaabi Aya ya 7 inayosema:

وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا

((Na tulipochukua kutoka kwa Manabii ahadi yao nzito (Miithaaq), na kutoka kwako (Muhammad), na kutoka kwa Nuuhu na Ibarahimu na Mussa na Issa mwana wa Mariyamu, na tukachukua kutoka kwao ahadi nzito sana))

[33-Al-Ahzaabi 07].

Maahamadiyah (Maqadiani) husema kuwa Manabii wote wamechukua Agano zito (MIITHAAQI) hilo akiwemo Mtume Muhammad S.A.W kwa kutajwa hasa, nalo ni agano ililowalazimu Manabii wote na mafuasi wao wote, na Mtume huyo ambaye limechukuliwa agano hilo kwa ajili yake bila shaka atakuja baada ya Mtume Muhammad S.A.W, na hakuna mwengine isipokuwa huyo wanaemuitakidi Maahmadiyah (Makadiani) nae ni Mkadiani Mirza Ahmad.

JAWABU:
Kwa mujibu wa ufafanuzi wa Kiahamadiyah (Kikadiani) inalazimika kuwa huyo wanayemuitakidi wao kuwa ni Mtume mwenye kuhusika na agano hilo zito ambaye ni huyo Mkadiani wao Mirza Ahmad hayumo katika Ahadi ya Manabii aliyoichukua Allah mtukufu kwa Manabii wote ambayo imetajwa katika Suuratu Al-Ahzaabi Aya ya Saba iliyotangulia, na kwa mujibu wa Aya hiyo ni kuwa Allah mtukufu alichukua ahadi hiyo nzito kwa Manabii wote na kutajwa hao watano (Muhammad na Nuuhu na Ibarahimu na Mussa na Issa mwana wa Mariamu) ni kwa sababu ya cheo chao kikubwa katika mkusanyo wa Manabii wote; kwani hao ni Uulu Al-Azmi. Basi kwa hakika hilo la kutokuwemo Mkadiani Mirza Ahmad wao katika Ahadi hiyo nzito (Miithaaq) linalazimisha kuwa yeye si Nabii; kwani Allah mtukufu alichukua agano hilo zito kwa Manabii wote, basi asiyekuwemo katika agano hilo zito huyo hatakuwa Nabii; kwani hakupata agano la Manabii, na kwa maana hiyo watakuwa Maahmadiyaah (Makadiaani) wameingia katika lazimisho la kushuhudia wenyewe kuwa Mirza wao si Nabii, bali ni Mjipachika Unabii.

Na Maahmadiyah (Makadiani) hawana budi waunganishe Aya ya 7 ya Suuratu Al-Ahzaabi na Aya ya 81 ya Suuratu Aala Imraana ili waweze kuthibitisha madai yao batili, lakini kama tunavyoona kuwa Aya ya MIITHAAQ ya Suuratu Al-Ahzaabi italazimisha kumkana asiyekuwemo katika Agano hilo, hata wakikaidika kutokuwemo katika Agano la Aya ya 81 ya Suuratu Aala Imraana.

Tukirudia tena katika Aya ya 81 ya Suuratu Aala Imraana, tunasema kuwa Aya hiyo inalazimisha kuwa Manabii wote wamehusika na Ahadi Nzito ya kumuamini na kumnusuru Mtume mmoja tu, na hilo linalazimisha kuwa Mtume huyo mwenye kuhusika na Agano hilo awe ni Mtume wa Mwisho, na hili litalazimisha mambo mawili kwa Maahamadiyah nayo ni:-

Kulazimika kuingia katika Itikadi wanayowatia Aibu nayo Wasilamu, nayo ni kuitakidi kuwa Muhammad S.A.W ndiye Mtume wa mwisho; kwani Maahmadiyah wamefikia kuwasema vibaya kuwa wanaitakidi itikadi ya watu wa Mtume Youssuf (A.S) waliotajwa katika Suuratu Al-Muumini (Ghaafir) aya ya 34. [40/34].
Kuporomoka utoleaji dalili wa Aya ya Suuratu Al-Aaarafi ianyosema: ((Enyi wana wa Adamu pindi wakikujieni Mitume miongoni mwenu wanaokuelezeni Aya zangu…)); kwani -kwa mujibu wa utoleaji dalili wao- ni kuwa watapaatikana Mitume baada ya Muhammad S.A.W na sio Mtume mmoja tu, na hawi Mtume ila awe Nabii, sasa Manabii hao watapata nafasi gani katika Aya za Miithaaq nazo ni Aya ya 7 ya Suuratu Al-Ahzaabi na Aya ya 81 ya Suuratu Aala Imraana?!. Suali ambalo haliwezi kupata Jawabu.
Kutokana na hayo mawili, inabainika wazi wazi ubatilifu wa Itikadi ya Maahmadiyah (Makadiani) na utoleaji wao wa Dalili; kwani Quraani tukufu haijipinzi wala haijifunji na kujibatilisha wenyewe kwa wenyewe.

MAANA SAHIHI YA AYA ZA MIITHAQI.
Hizi Aya -kama tulivyoona- ziko mbili, moja iko katika Suuratu Al-Ahzaabi nayo ni Aya ya 7, na nyengine iko katika Suuratu Aala Imraana nayo ni Aya ya 81.

Tukisema kuwa: Ahadi iliyotajwa katika Aya ya Suuratu Al-Ahzaabi imehusu kusimamisha dini vizuri na ufikishaji wa malinganio ya Allah mtukufu hakuta kuwa na nafasi kabisa kwa Maahmadiyah (Makadiani) ya kujishika na Aya ya Miithaq ya 81 Suuratu Aala Imraana, na kujishika na ahadi ya ufikishaji na kushimamisha dini ipasavyo kumeashiriwa na Aya ya 13 ya Suuratu Shuuraa:

شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّى بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ اللَّهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَن يَشَاء وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ

((Amekuekeeni katika Dini yale aliyomuusia kwayo Nuuhu, na ambayo tumekufunulia wewe (Muhammad), na ambayo tulimuusia kwayo Ibrahimu na Mussa na Issa, ya kuwa simamisheni Dini wala musifarikiane ndani yake, limekua kubwa sana kwa Washirikina lile munalowaita kulishika, Allah humchagua kwake anayemtaka na humuongoza kwake mwenye kunyenyekea))

[40-Shuura 13].

Tukisema kuwa: Ahadi iliyotajwa katika Aya ya 7 ya Suuratu Al-Ahzaabi ndiyo ile ile iliyotajwa katika aya ya 81 ya Suuratu Aala Imraaana, basi Ahadi hiyo itakuwa wamehusika nayo Manabii wote, na uhakika wake ni Ahadi ya kuendelea kwa Utume tokea kuanza kwake mpaka kumalizika kwake kwa kuzingatia awamu zake tafauti utakaopita ndani yake, nako kutakamatana vizuri na Aya ya Suuratu Al-Araafi inayosema: ((Ewe wana wa Adamu pindi itakapokufikieni Mitume miongoni mwenu wanaokuelezeni aya zangu…)) [7-Al-Aarafi 35], kwani Mitume ilitumwa kwa zama tafauti kuanzia Mtume wa Mwanzo naye ni Baba yetu Adamu A.S.W mpaka Mtume wa wisho naye ni Mtume wetu Muhammad S.A.W, basi Aya tukufu itakua inatupa uhakika wa Ahadi hiyo kuwa ni: kila Nabii na wafuasi wake wanalaziika kumuamini na kumnusuru Mtume anayefuata ambaye atasadikisha ya Mtume aliyemtangulia kabla, na namna hiyo inandelea mpaka kufikia Mtume wa mwisho ambaye ametajwa katika Aya tukufu, na kupatikana Mtume wa mwisho ni yakini na uhakika usiopingika; kwani Kiama ni chenye kusimama kwa hiyo kila kitu katika maisha haya kina mwisho wake, basi na utumaji wa Manabii una mwisho wake, na kwa hakika Nabii wa mwisho ni Mtume wetu Muhammad S.A.W naye ndiye mkusudiwa katika Aya tukufu basi yeye ndiye Mtume ambaye Manabii wote (Muhammad na wenzake) wamechukua ahadi ya kumnusuru na kumuamini atayekua wa mwisho miongoni mwao, na kwa uteuzi wa Allah nafasi hiyo ikawa kwa Mtume wetu Muhammad S.A.W.

Basi zinduka ewe ndugu yangu ikiwa umo katika safu za Mdai Unabii Mkadiani Mirza Ahmad jiwahi mapema kabla ya kufikiwa na kifo, na kama humo usije ukapotezwa katika njia yake; kwani hakika huyo ni Muongo na Dajjaali anaongoza wenye kumfuata wakiwa pamoja naye katika shimo la Jahannamu.

Allah atulinde na Adhabu yake.

Wabillahi Taufiiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Assalamu alaykum wa rahamatullahi wa barakatuhu.

Ndugu yangu Muislamu.

Kwa hakika kuna umuhimu mkubwa sana wa kumiliki ngao ya kumlazimisha hoja Muahamadia (Mkadiani) yoyote, nalo bila shaka ni jambo muhimu sana, basi zingatia haya tunayokupa hapa ili uwe katika njia ya kusimamisha hoja ya wazi juu ya Mkadiani yoyote pindi ikitokezea umefikiwa na Mkadiani kwa njia moja au nyengine.

Muulize mkadiani: Jee!! Allah mtukufu amesimamisha kutuma Manabii baada ya Muhammad S.A.W na kuwa yeye ndiye Nabii wa mwisho?

Atakujibu: Kutumwa Mitume kunaendelea baada ya Muhammad S.A.W.; kwani akijibu kinyume na hivo atakua amebatilisha Itikadi yake.

Hapo mtake dalili kutoka katika Quraani tukufu au Sunna ya Mtume Muhammad S.A.W.

Atakuletea Aya inayosema: ((Enyi Wana wa Adamu watakapokufikieni Mitume miongoni mwenu wanaokuelezeni Aya zangu……)) [Aaraf 35], na atakuambia: Maneno haya wanaambiwa Wanadamu walio hai, wala hawaambiwi wafu waliopita, kwa hiyo Mitume bila shaka inaendelea kutumwa baada ya Muhammad S.A.W.

Muulize: Bila shaka wewe unaamini kuwa Mirza Ghulaamu Ahmad ni Mtume baada ya Muhammad S.A.W. Jee!! Baina ya Mtume Muhammad S.A.W na huyo Mirza Ghlaam Ahmad kuna Mitume wangapi iliyotumwa?

Atakuambia: Hakuna Mtume yoyote baina ya Mtume Muhammad S.A.W na huyo Mirza Ghulaamu Ahmad anayemuamini yeye kuwa ni Mtume baada ya Mtume Muhammad S.A.W.

Hapo muulize: Jee!! Baada ya Mirza Ghulaamu Ahmad wataendelea kuja Mitume wengine?

Akisema: Hakuna Mtume mwengine baada yake atakua ameingia katika Itikadi ya kumalizika kutumwa Manabii, na wao wanawatia doa Waislamu kwa Itikadi hiyo na kuwambia kuwa wanaitakidi itikadi ya watu wa Mtume Youssuf A.S.W.
Vile vile atakua amekwenda kinyume na Aya aliyoitolea dalili ya kuendelea kutumwa Mitume baada ya Muhammad S.A.W; kwani Aya hiyo imesema Mitume wengi wala haikusema Mtume mmoja.

Ikiwa atasema: Bado itaendelea kutumwa Mitume mengine baada ya huyo Mirza wake ili aweze kusimama katika hoja yake ya Aya tukufu aliyoitegemea na aipukane na anayoyaona kuwa ni aibu ya watu wa Mtume Youssuf A.S.W ya kuamini kumalizika kuja kwa Manabii.

Muulize: Jee! Mitume hao na Manabii hao wana nafasi gani katika Aya ya 81 Ahadi ya Manabii iliyoko katika Suuratu Aala Imraana isemayo: ((Na Allah alipochukua ahadi nzito ya Manabii: Nitakapokupeni kitabu na hekima kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi ya kuwa mutamuamini Mtume huyo na kumnusuru..))??

Ukifika naye katika Aya hii zinduka vizuri sana; kwani atagota na kujaribu kukimbia hoja, mlazimishe, naye hatakua na nafasi ya kukujibu; kwani Aya hii kwa mujibu wa MANTIKI YA KIKADIANI Mtume ambaye Manabii wote wamechukua ahadi ya kumuamini na kumnusuru ni huyo wanayemuamini wao, naye ni Mkadiani Mirza Ghulam Ahmad ambaye kwa mujibu wa Itikadi yao ndiye Nabii pekee asiyekuwemo katika ahadi ya Manabii iliyomo katika Aya hiyo ya Suuratu Aala Imaraana wala ile iliyoko katika Aya ya 7 ya Suraati Al-Ahzaabi.

Na fahamu ndugu yangu kuwa uhakika ahadi hiyo imetimia kwa Manabii wote, asiyekuemo si Nabii.

Kwa hiyo:

Ima alazimike na neno alilolikimbia kabla, la kutokuja Mitume baada ya huyo Mirza, nalo linapekea kubatilika utoleaji wake wa dalili ya kuendelea kutumwa Mitume baada ya Muhammad S.A.W. wa Aya iliyotangulia: ((Enyi Wana wa Adamu……..)) ya Suratu Al-Aarafi, pia atakua ameingia katika aibu ya Itikadi ya Watu wa Youssuf A.S ya kumalizika ujio wa Manabii kwa mujibu wa neno lao wenyewe.
Au awatafutie nafasi katika Aya ya ahadi ya Manabii ya Suuratu Aala Imraana, na nafasi hiyo haipo kwa sababu Aya imesema Mtume wala haikusema Mitume.
Au akubali ubatili wa Itikadi yake yenye lazimisho la kupinzana kwa Aya za Quraani tukufu kama ulivyoona katika mada yetu hii..
Na tamu lao katika hayo ndilo chungu lao kwao.

Wabillahi Atufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

7. BISHARA YA MTUME AHMAD (S.A.W).
Baada ya kumshukuru Allah mtukufu na kumtakia wingi wa rehma na amani aliye khitimisho la Manabii Mtume wetu Ahmad aliyebashiriwa katika Taurati na Injili aliyeteremshiwa Quraani yeye pamoja na Aaali zake na Sahaba wake na kila mwenye kuongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya Malipo.

Wafuasi wa Mdai Unabii Mkadiani Mirza Ghulaam Ahamad wamekuja na madai hewa ya kudai kuwa huyo wanaemuamini wao kuwa ni Mtume baada ya Mtume Muhammad S.A.W ndiye mkusudiwa katika bishara aliyoitoa Mtume Issa bin Marayam (A.S.W) nayo ni bishara ya jina lake hasa ambalo ni Ahmad, nao wamedai kuwa Muhammad si Ahmad kwani hayo ni majina mawili tafauti.

JAWABU:
Aya tukufu inasema:

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ فَلَمَّا جَاءهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ

((Na aliposema Issa mwana wa Mariyamu: ”Enyi Wana wa Israili, hakika mimi ni Mtume wa Allah kwenu ni mwenye kusadikisha yaliyo mbele yangu katika Taurati na mwenye kubashiria Mtume atayekuja baada yangu jina lake ni Ahmad.” Basi alipowajia kwa mabainisho wakasema Huu ni uchawi wa wazi))

[61-Saff 7]

Katika Aya hii tukufu imekuja ndani yake bishara ya wazi kwa ulimi wa Mtume Issa A.S aliyetumwa kwa Wana wa Israili, bishara hiyo inahusu Mtume atayekuja baada yake na Mtume huyo jina lake ni Ahmad.

Ili tuweze kufahamu vizuri Aya hii tukufu tuzingatie haya yafuatayo:

Baada ya bishara hiyo tukufu, Allah mtukufu amebainisha kuwa Mtume huyo aitwae Ahmad ameshawajia hao Wana wa Israili nao wamesema kuwa huo ni uchawi ulio wazi, wala hakusema kuwa atakapowajia watasema…, kutokana na hapo Aya tukufu inatueleza bishara ambayo tayari imeshatokezea zama za kuretemka Aya tukufu nazo ni zama za Mtume wetu Muhammad S.A.W, kwa hiyo Aya tukufu inavunja uwezekano wa wakati unaofuata baada ya Muhammad S.A.W kuwa ndio wakati wa Mtume huyo, lakini inaleta yakini ya wazi kuwa wakati wa Mtume huyo Mbashiriwa aitwae Ahmad ni baada ya Mtume Issa A.S mpaka wakati ule ilioteremshwa ndani yake Aya hiyo tukufu; kwa hiyo haiwezekani Aya hii ikawa ni ubashirio wa Mtume baada ya Muhammad S.A.W.
Makubaliano ya wote ni kuwa hakuna Mtume yoyote aliyetokezea baada ya Issa A.S mpaka kuja kwa Mtume Muhammad S.A.W, na katika hili amesema Mtume Muhammad S.A.W alipokua akimueleza Mtume Issa A.S aliyetoa Bishara hii: ”Hakuna baina yangu na baina yake Nabii yoyote”.
Quraani tukufu inatueleza wazi wazi kuwa katika Taurati na Injili kuna bishara ya Mtume wetu Muhammad S.A.W kwa sifa zake [7-Al-Aarafi 157-158], na sisi mpaka wakati huu hatujaona Aya yenye kubainisha kuwa katika Taurati na Injili kuna bishara ya kuja Mtume na jina lake ni Muhammad, kwa maana hiyo inabainika kuwa Mtume Issa A.S alibashiria Mtume aliyebashiriwa katika Taurati na Injili kwa sifa zake naye ni Mtume wetu Muhammad S.A.W, na bishara ya jina la sifa ina nguvu zaidi kuliko bishara ya jina alama, kwani jina alama inawezekana kuitwa mwengine lakini jina sifa haiwezekani kuhusika nalo mwengine, amesema Mfasiri Qurtubi: ”Na maana ya Ahmad yaani mwenye kumhimidi Mola wake kuliko wote wenye kuhimidi. Na Manabii wote -rehema za Allah ziwe kwao- ni wenye kumhimidi Allah mtukufu, na Nabii wetu Ahmad ni mwingi wao kwa kuhimidi.”
Allah mtukufu amebainisha katika Quraani tukufu kuwa Mtume wetu Muhammad S.A.W ametumwa kwa watu wote, na Wana wa Israil ni miongoni mwao basi ametumwa kwao pia.
Allah mtukufu amemteua Mtume wetu Muhammad S.A.W kwa kubainisha yaliyoteremshwa kwake kama ilivyoelezwa katika [16-Nahal 64] naye amebainisha kuwa yeye ndiye mkusudiwa wa bishara hiyo pale aliposema: ((Mimi nina majina matano: Mimi ni Muhammad na Ahmad na Almaahii (Mfutaji) ambaye Allah anafuta kwa mimi ukafiri, na mimi ni Alhaashiru (Mkusanyaji) ambaye watu watakusanywa katika miguu yangu, na mimi ni Alaaqibu (Kimalizio yaani mwisho wa Manabii).)) [Bukhari – Sahihi 3532. Malik – Muwatta 3676. Nasaaii – Sunanu Alkubraa 11526].
Uma wa kiislamu wote umekubaliana kuwa mkusudiwa katika bishara hiyo aliyoitoa Mtume Issa A.S. katika Aya hiyo tukufu si mwengine asiyekuwa Mtume wetu Muhammad kwa jina la sifa yake nalo ni Ahmad.
Lau kuwa Aya hiyo inabashiria kuja kwa Mtume Ahmad baada ya Mtume Muhammad S.A.W lingekuwa mashuhuri hilo katika safu za Waislamu lakini haijulikani katika safu zao wote juu ya kutafautiana kwao kuwa kuna kauli ya kumsubiria Mtume mwengine baada ya Muhammad S.A.W jina lake ni Ahmad.
Kwa hakika kila mwenye kuzingatia Aya tukufu na hayo ya uhakika tuliyoyaeleza atafahamu wazi wazi kuwa Mtume Ahmad aliyebashiriwa na Mtume Issa A.S si mwengine bali ni Mtume wetu Muhammad S.A.W; kwani yeye:

Ndiye Mtume aliyekuja baada ya Mtume Issa A.S.
Ni Mtume mwenye majina mingi moja wapo ni Ahmad.
Ndiye Mtume aliyebashiriwa katika Taurati na Injili; kwa hiyo Mtume Issa A.S alielezea bishara hiyo.
Ndiye mwisho wa Manabii, basi mlango wa unabii na utume umefungwa kwa ujio wake S.A.W.
Na kwa haya yanaporomoka madai yote batili ya wafuasi Mdai Unabii Dajjali Mkadiani Mirza Ghulaamu Ahmad, na kubainika kuwa wao ni wenye kuita katika milango ya Jahannamu waliyoridhia kwa nafsi zao baada ya hoja ya wazi.

Wabillahi taufiqi.

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

8. MADAI YA MAAHMADIA KUGONGANA BAADHI YA AYA – 1.
Baada ya kumshukuru Allah mtukufu na kumtakia wingi wa rehma na amani kipenzi chetu aliye mwisho wa Manabii Muhammad na Aali zake na Masahaba wake na kila mfuataji wa njia yake mpaka siku ya malipo.

Umetufikia ujumbe kutoka kwa Maahamadiyah (Makadiani) wenye kudai kuwepo uwezekano wa kugongana katika Aya za Qur-aani, nao wamefanya hivo baada ya kushindwa hoja katika suala majibu yetu no 6 yaliyomo katika kiunganishi husika Hapa

Basi wakaleta baadhi ya Aya na kutaka ufumbuzi wetu katika Aya hizo, na sisi tunasema: ‘Ajabu ya Maahmadiyah katika suala lao hili ni kuwaona wanajisaidia kwa Ahalu Al-Kitaabi (Mayahudi na Manasara), nalo ni jambo linalofichua uhakika wao kuwa wao wanapata ubabaishaji wao kutoka kwa Mayahudi na Manasara, basi hizi hapa maudhui zao na jawabu yake

1. Amesema Allah mtukufu

(وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنْتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَٰكِنْ جَعَلْنَاهُ نُورًا نَهْدِي بِهِ مَنْ نَشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ)

[Surat Ash-Shura 52]

{Tafsiri za aya zote tuliandika kutoka mashafu ya Sheikh Salih Alfarisi }

Tafsiri: ((Na namna hivi Tumekufunulia wahyi kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini wala imani; lakini tumefanya kitabu hiki (Quran) ni nuru, ambayo kwa (nuru) hiyo unamuongoza Tumtakaye katika waja wetu. Na kwa yakini wewe unaongoza katika njia iliyonyooka))

(42:52)

وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ)

((Na kwa yakini wewe unaongoza katika njia iliyonyooka))

Halafu upande mwingine alisema:

(إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَٰكِنَّ اللَّهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ)

Tafsiri: ((Kwa hakika, wewe huwezi kumuongoa umpendaye, Naye anawajua waongokao.

[Surat Al-Qasas 56]

JAWABU:
Uongofu uko aina mbili:

uongofu wa kubainisha
na uongofu wa kuwafikishwa (kuwezeshwa)
Basi uongofu wa kubainisha huo umewekwa kwa Mtume Muhammad S.A.W, kwa hiyo hapo ndipo anapoongoza Mtume S.A.W kwa ujibu wa ufunuo wa Wahyi anaoupata kutoka kwa Allah mtukufu, ama uongofu wa kuwezeshwa huo haumiliki isipokuwa Allah mtukufu, nao ndio alioambiwa Mtume S.A.W kuwa yeye hamuongoi anayempenda lakini Allah humuongoa amtakae.

2 Amesema Allah mtukufu

قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنْتُ بَصِيرًا

[Surat Ta-Ha 125]

TAFSIRI. ((aseme ewe mola wangu mbona umenifufua kipofu na hali nilikuwa nikiona.))

Halafu upande mwingine alisema:

(لَقَدْ كُنْتَ فِي غَفْلَةٍ مِنْ هَٰذَا فَكَشَفْنَا عَنْكَ غِطَاءَكَ فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ)

[Surat Qaf 22]

Tafsiri: ((Aambiwe kwa hakika ulikuwa umo katika ghafla na jambo hili Basi tumekuondolea leo pazia yako kuona kwako leo kumekuwa kukali.))

JAWABU: Neno lililotumika katika Aya ya suuratu Twaaha ni (Baswiiran) na neno hili linamaanisha uoni wa moyo (kujua na kuwa na hoja ya kushika) na sio uoni wa macho, na hilo linakabiliana na upofu uliotajwa katika Aya hizo tukufu; kwa hiyo huo ni upofu (wa kukosa mashiko ya kujitetea na hoja ya kushika) na hayo yanaelezwa na Aya zilizopita katika suuratu Twaha (Na mwenye kuukwepwa ukumbusho wangu kwa hakika yeye atapata maisha ya dhiki na tutamfufua siku ya kiama akiwa kipofu (Yaani hana hoja ya kujishika)…

Ama Aya ya Suuratu Qaaf hiyo inaelezea uoni wa jicho hasa kuwa utakuwa wa kuona vizuri sana.

 

Kwa hiyo hakuna kugongana kwa Aya za Quraani isipkuwa kwa vipofu wasiofahamu Quraani na lugha yake.

Leo tumalizie hapa mpaka mara nyengine kwa Taufiki ya Allah mtukufu katika kumaliza mtititriko wa suali lao.

Wabillahi taufiqi.

Asanteni sana.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

9. MADAI YA MAAHMADIA KUGONGANA BAADHI YA AYA – 2.
Baada ya kumshukuru Allah mtukufu aliyekitakasa Kitabu chake na kuwana migongano, na baada ya kumtakia wingi wa rehma na amani kipenzi chetu aliye mwisho wa Manabii Muhammad na Aali zake na Masahaba wake na kila mfuataji wa njia yake mpaka siku ya malipo.

Tukiwa tumo katika sehemu ya pili ya kuwajibu Maahamadiyah (Makadiani) wenye kudai kuwepo uwezekano wa kugongana katika Aya za Qur-aani, nao wamefanya hivo baada ya kushindwa hoja katika suala majibu yetu no 6 yaliyomo katika kiunganishi husika Hapa.

Awamesema:

3 Amesema Allah mtukufu:

(إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ)

[Surat Al-Anfal 2]

Tafsiri:

((Hakika waumini ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa hofu na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wakamtegemea mola wao tu.))

Basi Allah mtukufu amesema:

الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ

((ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa hofu.))

Halafu upande mwingine alisema:

(الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُمْ بِذِكْرِ اللَّهِ ۗ أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ)

[Surat Ar-Ra’d 28]

((Nao ni wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah, sikilizeni kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia)).

JAWABU:
Kwa hakika madai yao katika sehemu hii ya tatu yanonesha wazi kuishiwa hawa Maahmadia (Makadiani) Allah mtukufu awatoe katika kiza ya Ushirikina waliomo ndani yake na awalete katika nuru ya Uislamu wa Mtume wa mwisho Muhammad S.A.W.

Kwa hakika sisi tumejaribu kutafuta pa kuweza kujishika katika madai yao katika sehemu hii ya tatu lakini hatujapaona kabisa, lakini huenda makusudio yao ni kuwa Allah anapotajwa wao hujaa khofu na wanamkumbuka Allah mtukugu nyoyo zao hutulia, masikini hawa Makadiani kama wao hawajui kuwa Waumini wa kweli wanaishi baina ya kukhofu na kutaraji, Waumini wa kweli wanakhofu na adahabu ya Allah mtukufu na wanataraji maridhi ya Allah, khofu yao inawakimbiza katika maasi na matarijio yao yanawaingiza katika kumtii. Na hili liko wazi kwa mwenye kuutaka ukweli.

4. Amesema Allah mtukufu:

(وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِنْدَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُلْ لَهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُلْ لَهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا)

[Surat Al-Isra’ 23]

Tafsiri:

((Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila yeye tu na ameagiza kuwafanya wema wazazi kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe au wote wawili basi usiwaambie hata Ah! wala usiwakemee na useme nao kwa msemo wa heshima.))

Halafu upande mwingine anafafanua kwamba alikuwa Yatiima:

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ

[Surat Ad-Dhuhaa 6 ]

Tafsiri:

((Je!! hakukukuta yatima akakupa makazi (mazuri ya kukaa))).

JAWABU:
Kwa kweli inaonesha kuishiwa kwa Maahmadia (Makadiani) kabisa kabisa, yaani wanashindwa wao kutafautisha baina ya mafundisho ya waumini na maelezo ahususi ya Mtume wa mweisho Muhammad S.A.W. Hivi hawa watu hawaoni kule Musimuabudu isipokua yeye peke yake (yaani Allah mtukufu) na kuwafanyia wema wazazi wawili, kuwa hapo wanaambiwa waumini wote kwa ujumla, na huku anaelezwa Mtume S.A.W hali yake mahususi kuwa alikutwa na Allah mtukufu akiwa ni yatima naye Allah mtukufu akamuhifadhi. Na hili liko wazi halihitaji maelezo ya ziada.

5. Amesema Allah mtukufu

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ

[Surat Ad-Dhuhaa 6 ]

Tafsiri:

((Na akakukuta hujui kuongoza njia akakuongoza?))

Ukiangalia Tafsiri ya Sheikh Salih alfarisi ktk juzuu amm (kitabu pekee si mashaf )

Utapata Tafsiri ifuatao

((Na akakukukuta umepotea naye akakuongoza.))

Halafu upande mwingine alisema.

(مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ)

[Surat An-Najm 2]

((Hajapotea mtu wenu (Huyu Nabii Muhammad) wala hakukosa))

JAWABU:
Na huku kuishiwa kwengine kwa Maahmadia (Makadiani) wanakuja na Tarjama mbili za Sheikh Abdalla Saleh Al-Farsi za Allah ya 6 ya Suuratu Dhuhaa nazo ni:

Na amekukuta umepotea naye akakuongoza.
Na akakukutia hujui kuongoza njia naye akakuongoza
Halafu eti hiyo iko kinyume na neno lake ((Hajapotea mwenzenu wala hajakosea)).

Tunawambia Aya ya 6 ya Suuratu Dhuhaa inaelezea hali ya Mtume S.A.W kabla ya kupata Wahyi wala Sheria na taarjama zote mbili zinaelezea hali hiyo, ama Aya ya pili ya Suuratu Najmi inaelezea hali yake baada ya kupata Wahyi na Sheria kutoka kwa Allah mtukufu.

Wabillahi taufiki

Lakini sisi bado tunawalazimisha na mada yaetu husika watoe jawabu kama wao ni wakweli kwani Quraani Allah mtukufu ameihifadhi na kujipinza, kwa hiyo fuata mada iliyowaumiza kwa kubofya hapa.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Shukurani zote ziwe kwa Allah mtukufu aliyetumeesha kwa neema ya Uislamu, na rehma na amani ziwe kwa aliye khitimisho la Manabii Mtume wetu Muhammad naye ndiye Ahmad aliyebashiriwa na Mtume Issa S.A.W pamoja na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Aba baada ya hayo.

Kwa hakika Maahamadia katika majaribio yao ya kutaka kuyavika madai yao batili ubabaishaji wa kulaghali na kudanganya huwa wanakuja na madai ya kusema eti wema waliopita katika Umma huu hawakufahamu kuwa Khaatamu Al-Anbiyaai kwa maana ya mwisho wa Manabii, na kujikakamua kwao kote katika kuthibitisha madai yao hayo husema: Hadhratu Aisha Mke wa Mtume S.A.W -Allah awe radhi naye- pia Hadharatu Mughiira bin Shuubah R.A walisema: ((Musiseme hakuna nabii baada ya Muhammad, bali semeni kuwa yeye ni Khaatamu Al-Anbiyaai; kwani imekuja kuwa Issa bin Mariyam S.A atashuka kwenu, basi ikiwa atashuka atakua yeye ni Nabii kabla yake na baada yake)).

Na jawabu, ni kuwa hayo yaliyoegemezwa kwa Bibi Aisha R.A na Mughiira bin Shuubah hayakuthibiti kutoka kwao kwa riwaya sahihi, pia imethibiti kutoka kwa Mtume S.A.W kuwa kasema zaidi ya mara moja: ((Hakuna Nabii baada yangu)), basi vipi tusadiki kuwa Masahaba R.A wakataze watu kuyasema ambayo Mtume S.A.W kayasema, hivi nani kati yao anaweza kumtovukia abadu Mtume S.A.W kwa kumkataza na kumwambia: “Usiseme hakuna Nabii baada yako”?. Kutokana na hapo inabainika kuwa hayo wanayayodai hayakuthibiti kutoka kwa Sahaba yoyote.

Na katika ubabaishaji wa Maahamadia husema kuwa Hakiim Tirmidhi (Ni mmoja wa watawa wa kisufi) amesema katika Kitabu chake kiitwacho Khatmu Al-Auliyaai: “Taawili ya Khaatamu Nabiiyina kuwa ni mwisho wa Manabii ni taawili ya wajinga wasiofahamu”.

Tunasema kuwa Hakiimu Tirmidhi yeye ana uoni wa ndani katika suala la Khatmu Nubuwah, nao ni uoni unaokusanya maana ya mwisho, kwa hiyo aliyokataa Hakiim Tirmidhi ni kuhusisha maana ya mwisho peke yake bila kuzingatia maana ya ndani iliyokusanywa katika neno KHAATAMU.

Na sio sisi wala nyinyi Maahamadia wa kumsemea Hakiim Tirmidhi hali ya kuwa maandiko yake yapo. 

Anasema Hakiim Tirmidhi katika Kitabu chake husika Khatmu Al-Auliyaai mwisho wa Kitabu ukurasa wa 446: “Na shukurani zote ni kwa Allah, na rehma za Allah ziwe KWA YULE AMBAE HAKUNA NABII YOYOTE BAADA YAKE (NAYE NI) MUHAMMAD KHAATAMU AL-ANBIYAAI aliyehusishwa kwa makaamu ya kuhimidiwa peke yake na kwa Aaali wake na Masahaba wake na amani nyingi…”.

Tunapata hapo kuwa Hakiim Tirmidhi anaitakidi kuwa Mtume wetu Muhammad S.A.W ndiye Nabii ambaye hakuna Nabii yoyote baada yake, na hilo linalazimisha kuwa yeye ni mwenye kuitakidi kuwa Mtume Muhammad S.A.W ni Nabii wa mwisho.

Hakiim Tirmidhi katika Kitabu chake hicho hicho uku 436 anasema:

((Jee! Si atakua katika wakati wa mwisho yule mwenye KHATMU YA WALAAYAH?!! Basi huyo ndiye hoja ya Allah juu ya Mawalii wote siku ya Kisimamo (Kiama). Kama alivokua Muhammad S.A.W ni mwisho wa Manabii wote ndio akapewa KHATMU YA UNABII naye ndiye hoja ya Allah mtukufu juu ya Manabii wote, basi vile vile atakua HUYU WALII AMBAYE YEYE NDIYE MWISHO WA MAWALII WOTE KATIKA MWISHO WA WAKATI)). 

Inaonekana wazi kuwa Hakiimu Tirmidhii anaitakidi kuwa sifa ya KHATMU haistahiki isipokua mwenye cheo kikubwa zaidi mbele ya Allah nacho ni cheo cha Hoja ya Allah mtukufu siku ya Kiama, cheo ambacho ulazima wake ni kuwa wa mwisho katika MAWALII NA MANABII, basi Nabii mwenye cheo cha KHATMU ni lazima atakua ndiye NABII WA MWISHO, na WALII mwenye cheo cha KHATMU ni lazima atakua ndiye WALII WA MWISHO.

Twabaan huo ni mtazamo wa Kisufi aliokua nao Hakiim Tirmidhi, kwa hiyo alichokataa Hakiim Tirmidhi ni kuhusisha KHAATAMU NABIYIINA kwa maana ya MWISHO WA MANABII peke yake; kwani yeye anaona katika hilo ni kuzingatia sifa ndogo YA UMWISHO ambayo imedhaminiwa na sifa kubwa ya UBORA WA KUWA HOJA YA ALLAH SIKU YA KIAMA KWA MANABII WOTE.

Kwa kuona kurasa husika za Kitabu KHATMU AL-AULIYAA unaweza kubofya kiunganishi husika HAPA.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

11. MADAI YA MFANO WA ISSA A.S.W.
Kila sifa njema ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa aliye khitimisho la Manabii aliyesema ((Na mimi ndiye KHAATAMU NABIYIINA HAKUNA NABII YOYOTE BAADA YANGU)) Nabii wetu Muhammad pamoja na Aali wake na Masahaba wake na kila mwenye kuongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Ama baadu.

Wanadai Maahmadia kuwa Mirza wao ni Mwana wa Mariam aliyepigiwa mfano katika neno lake Allah mtukufu: ((Na alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupigia ukelele)) [Zukhruf 57].

Wanadai Maahmadia kuwa hayo ni maelezo yanayomuhusu Mirza wao, kwani yeye ndiye mfano wa Issa mwana wa Mariamu katika Umma huu, mfano wake ni kama Issa Mwana wa Mariamu wa Bani Israili A.S.W. kwa hiyo kupiga makelele ya wapinzani wao ni uhakikisho wa yale yaliyoelezwa katika Aya hii tukufu.

JAWABU:
Kila mwenye kuisoma Aya hii tukufu anafahamu kuwa anayezungumziwa hapo ni ISSA MWANA WA MARIAMU S.A.W MTUME ALIYETUMWA KWA BANI ISRAILA si mwengine yoyote, Aya haijasema watakapoletewa mfano wa MWANA WA MARIAMU kama wanavodai Waumini wa Dini ya Kiahmadia, inawezekana wana makengekeza hawaoni vizuri; kwani Aya tukufu inasema ((NA ALIPO PIGWA MFANO MWANA WA MARIAMU)) ni jambo tayari limeshatokea na sio litatokea kama wanavodai wao, lakini wafuasi wa Mdai unabii muongo masikio yao na nyoyo zao vyote vimefungwa haviwezi kuifahamu Quraani.

Aya inayofuata inabainisha nani aliyepigiwa huo mfano, na lipi neno lao. Inasema:

((Na wakasema: MIUNGU YETU KWANI SI BORA KULIKO HUYO? HAWAJAKUPIGIA MFANO HUO ISIPOKUA NI UBISHI TU, BALI WAO NI WATU WAGOMVI)) [Zukhruf 58]

Aya tukufu inatubainishia kuwa Washirikina walijadiliana na Mtume S.A.W. kwa mfano wa Issa Mwana wa Mariamu A.S.W. kwa kusema kwao kuwa MIUNGU YAO NI BORA KULIKO ISSA MWANA WA MARIAMU.

Ni Mfano gani na vipi walijadiliana naye S.A.W?

Tunajua sote kua Quraani tukufu imemueleza Mtume Issa Mwana wa Mariamu A.S.W kua ameumbwa bila ya Baba na kuneemeshwa kwa Unabii na Utume, na kua Manasara wamemfanya Issa mwana wa Mariamu A.S.W kua ni Mungu wao.

1. Wakasema: Muhammad anataka tumuabudu Issa Mwana wa Mariamu kama anavoabudiwa na Manasara, sasa ni yupi bora Miungu yetu na huyo Issa bin Mariamu?!!.

2. Wakasema: Muhammad anatuambia kuwa wenye kuabudia pasina Allah wao na wanavoviabudu ni kuni za Motoni humo watasalia milele, sasa Manasara wanamuabudu Issa Mwana wa Mariamu kwa hiyo yeye huyo Mwana wa Mariamu na Miungu yetu ni nani bora zaidi ikiwa wote watakua Motoni na wenye kuwaabudu?!!

3. Walisema: “Muhammad anataka kujifanya kama Issa mwana wa Mariamu, watu wamuabudu kama anavoabudiwa Issa mwana wa Mariamu”

Kisha ndio wakasema: Kuwa Miungu yao ni bora kuliko Mwana wa Mariamu kwa kuwaenzi Mababu na Ibada zao, kwa hiyo kuabudia hayo Masanamu ni bora kuliko kuja kumuabudu Muhammad ambaye ni mmoja katika wao.

Kila mmoja azierejee hizo Aya tukufu katika Quraani tukufu anaona wazi wazi haya tuliyoyabainisha.

Juu ya yote haya tunawambia hawa waumini wa Dini ya Kiahmadia: Nyinyi munadai kuwa Mirza wenu katajwa kwa jina lake hasa katika Bishara ya Mtume Issa Mwana wa Mariamu A.S.W ya Mtume Ahmad atayekuja baada yake, sasa vipi tena munarudi na kumpachika huyu Mirza wenu kilemba ukoka eti yeye ni Issa bin Mariamu?!!! Hivi hamuoni jinsi Dini yenu inavolegelega mara Issa bin Mariamu, mara Ahmad, mara Masihi, mara Mahadi?!!!!

Wabillahi taufiiq.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

12. NA YEYE NI ELIMU YA KIAMA.

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa aliye sema: ((Mimi ni khitimisho la Manabii hakuna nabii yoyote baada yangu) Mtume wetu Muhammad pamoja na Masahaba wake na kila aliyeongoka katika njia yake mpaka siku ya Malipo.

Ama baadu.

Umetufikia ujumbe unaohusiana na mada iliyopia (11. MADAI YA MFANO WA ISSA A.S.W) ujumbe huo unadai kuwa ((Walamma dhuriba)) haifidishi wakati uliopita bali mfano wake ni kama ((Fallamaa rauhu zulfatan)) iliyoko katika aya ya 26 ya Suratu Al-Mulki kwa hiyo maana yake itakua ni ((Na atakapopigwa Mwana wa mariamu mfano..)) na kaumu yake ni Umati wake, na kusema kwao: ((Hivi miungu yetu si bora zaidi kuliko yeye huyo)) kuwa miungu hapo ni Wanavyuoni wa Madhehebu tafauti kwa kuwafanya miungu pasina Allah kama walivofanya hayo Wana Wa Israili, na kuwa Aya zinazofuata zinabaisha kuwa yeye atakuja na kuwa ni ELIMU YA KIAMA..

JAWABU:

Quraani iko wazi katika Aya zake haina haja ya kupewa maana zinazoiondoshea nuru yake kama hizo wanazotoa hao wenye kujidanganya wafuasi wa Dini ya Kiahmadia.

Ama kusema kwao kuwa ((Walamma dhuriba)) inafidisha wakati ujao kama ((Falamma Rarauhu)) iliyoko katika Suuratu Al-Muliki, ni kujisemea bila dalili wala hoja ya msingi, kwa sababu hii ya Suuratu Zukhrufi imeanza kwa (Wau) na haikuanza kwa (Fau) kama ya Suuratu Al-Mulik, mfano wake ni Aya 250 ya Suuratu Al-Baqarah ((Na walipotoka kupambana na Jaluti na majeshi yake)) imekuja ((Walamma barazuu)) sasa waseme basi na watakapotoka na sio na walipotoka. Inaosesha hawajui miundo ya maneno ya Kiarabu fasihi hao.

Ama kusema kwao kuwa Wanavyuoni wa Uma huu ni Miungu ya wafuasi wao kwa kuwafanya kwao hao ni Arbaabun min Duunillahi Miungu pasina Allah mtukufu, kwa hakika hilo linabeba Ukafiri wa wazi kabisa kwa mwenye kulisema kwa njia nne:

 1. Ulazima wa kuzikanusha Aya tukufu zenye kutuambia tuwaulize wenye elimu ikiwa hatujui (Nahal 43) na (Al-Anbiyaa 7), sasa wao hawa wafuasi wa Dini ya Kiahmadia wanajua zaidi cheo cha Maulamaa wa Uma huu kuliko Allah mtukufu na Mtume wake (S.A.W).
 2. Ulazima wa kuitakidi kwao kuwa Waislamu wote kuanzia Masahaba, Matabiina mpaka hivi leo ni Washirikina wanaabudu Maulamaa wao, kwa hiyo karne zote 13 hizo hakuna Waislamu. 
 3. Ulazima wa kuwa na wao ni wenye kumuitakidi huyo Mirza wao kuwa ni mungu wa ulinganisho uliomo katika Aya tukufu (Hivi miungu yetu si bora zaidi kuliko huyo (Issa mwana wa Mariamu)?!! Yaani kuliko mungu huyo.
 4. Ulazima wa kuwa na wao ni Washirikina au wakatae kufuata wanawaona wao kuwa ni Maulamaa katika Dini yao ya Kiahmadia.

Kwa hakika bidhaa yao hawa imedoda mbele ya kila mwenye kufikiri na mwenye akili, ametuambia Mtume wetu Muhammad S.A.W: ((WANAICHUKUA HII ELIMU KATIKA KILE MWENYE KUFUATIA WAADILIFU WAKE, WANAIONDOSHEA UHARIBIFU WA WENYE KUPINDUKIA MIPAKA, NA WALIYOJIPANGIA WABATILIFU, NA TAFSIRI ZA WAJINGA)) wala hakutuambia kama wanavosema Wafuasi wa Dini ya Kikadiani (Maahmadia), na kama wao ni wakweli watuletee hao WAADILIFU WAO WALIOPOKEZANA ELIMU ALIYOKUJA NAYO MUHAMMAD S.A.W KUPITIA KILA KIZAZI MPAKA HIVI LEO.

Kwa kuona Waadilifu wa Kiibadhi fuata kiunganishi hapa.

Allah anatuambia ((HAKUA YEYE (ISSA MWAN WA MARIAMU) ILA NI MJA TULIYEMNEEMESHA NA KUMFANYA NI RUWAZA KWA BANI ISRAILI)) [Al Zukhruf 59] eti “Ooooo Bani Israila ni huu Umati wa Muhammad” wamepata wapi wao kuwa Umati wa Muhammad ndio Bani Israili?!!!! Wazushi wakubwa.

Na sijui watasema nini kuhusu neno la Allah ((Maa dharabuuhu laka)) Na Hawakukupigia wewe mfano huo. 

Ama kuhusu Aya ya 61 isimayo ((Wainnahuu lailmun lissaa-a…)) tuchukue kwa maana ya (Na hakika yeye ni elimu ya kiama) na kuwa mkusudiwa wa neno YEYE ni Issa mwana wa Mariamu A.S.W, basi pia hakuna dalili ndani yake kuwa Mwana wa Mariamu A.S.W atakuja katika Uma huu kabla ya kusimama kiama, hayo ni kwa kukosekana ainisho la maana hiyo katika Aya tukufu, kwani Aya tukufu inatueleza kuwa YEYE NI ELIMU YA KIAMA na hilo ni haki; kwani kila Nabii ni elimu ya kukaribia Kiama, kwa hakika Manabii ni vituo vya zama tafauti, basi kila Nabii anapokuja ni elimu ya kujua kuwa Kiama kinakaribia, na katika kubashiria Mtume Issa Mwana wa Mariamu A.S.W ujio wa Mtume wa mwisho aliyetajwa katika Taurati na Injili na kuwa ujio wake utafuatia baada yake ni elimu ya wazi ya kujua ukaribu wa kufikia Kiama kwa kufika bishara hiyo wakati wake kwa kuja muhusika wake naye ni Mtume wetu Muhammad S.A.W; basi yeye S.A.W ndiye kituo cha mwisho kama alivosema S.A.W: ((Hakuna Nabii baada yangu, wala hakuna Uma baada yenu)) na amesema: ((Nimetumwa mimi na kiama kama hivi viwili -akiashiria kidole cha kati na cha kuashiria- na kilikaribia kunitangulia)).

Kwa hiyo Mtume ISSA MWANA WA MARIAMU A.S.W ameshafariki na hatarudi tena mpaka kiama kitasimama, kwa kujua hilo fuata kiunganishi husika hapa.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

13. USHUHUDA WA HAKI WA MIRZA GHULAM AHMED MKADIANI.
Baada ya kumshukuru Allah mtukufu na kumtakia rehema na amani kipenzi chetu Mtume wetu Muhammad naye ndiye Ahmad aliye khitimisho la Manabii aliyesema kwa bayana ya wazi kabisa (Mimi ndiye khitimisho la Manabii hakuna Nabii yoyote baada yangu), rehema na amani ziwe kwake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu tunakuleteeni ushuhuda wa Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani mdai unabii kiburuza na kivuli, na ushahidi huu ni wa haki, Allah mtukufu kwa hekima zake ameupitisha kwa Mirza mwenyewe ili uwe ni hoja kwa kila mwenye akili kuwa Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani hakua Mahdii wala Masihi wala Nabii wala Mtume, bali hukumu yake ni kama tutakavoona alivojihukumu mwenyewe.

Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani mara moja alidai kupata ufunuo wa kuwa yeye atamuoa Bintimwari wa Ahmed Beg aitwae Muhammadee Beijuum, basi Mirza alisema kuhusu ufunuo wake huo: “Na wajue wapinzani wetu kuwa hakuna kipimo kilicho bora zaidi na kifaacho zaidi cha kupima ukweli wetu na uongo wetu kuliko ufunuo huu (yaani wa kumuoa Bintimwari huyo aitwae Muhammadee Beijuum)” [Mir-aatu Kamaalatil- Islaam 288].

Ifahamike kuwa Baba wa Binti Ahmed Beg alikua ni katika jamaa wa Mirza Ghulaam Ahmed, naye alikua ni mtu mwenye haja, basi mara moja alikwenda kwa Mirza Ghulaam Ahmed kutaka kusaidiwa haja zake ndipo akamuambia: ((Nitakusaidia kwa shuruti ya kuniozesha Binti yako Muhammadee Beijuum)) wakati huo umri wa Mirza ulikua ni Miaka 50 na kitu kwa mujibu wa madai ya Maahmadia kuwa Mirza kazaliwa mwaka 1835 A.D na usahihi ni kuwa Mirza alizaliwa mwaka 1839 A.D na tokeo hili lilianza mwaka 1886 A.D.

Baba wa Binti alikataa sharti ya ukwe huo, na hapo Mirza vilipanda vitu vyake na kusema kuwa kapata ufunuo usemao: ((Hakika Allah amenidhihirishia sura ya ufunuo kuwa hakika Binti Mkubwa wa Ahmad Beg atakua mke wangu pamoja na kuwa jamaa zake wanapinga hilo na hawalitaki, lakini Allah ataniozesha mimi na ataondosha vizuizi vyote, na ahataweza yoyote kuzuia kupatikana jambo hilo)) [Izaalatu Auhaamu 396] na akasema: ((Hakika kumuoa Binti huyo ni jambo lililokwisha pitishwa na mimi ninaapa kwa Mola wangu kuwa huu ni ukweli na hamutaweza kulizuia hilo lisitokee, na kwa hakika ameshasema Allah mtukufu: Tumeshakuozesha huyo Binti sisi wenyewe na hataweza yoyote kubadilisha maneno yangu)) [Hikamu Samaawiyah uk. 40], pia akatoa ilani isemayo: ((Hakika ufunuo husika nao ni mimi kumuoa mwanamke huyu ni makadirio yaliyopitishwa, na makadirio hayatenguki kwa hali yoyote; kwa sababu nimepata katika ilihamu maneno haya ((Hakuna kubadilika kwa maneno ya Allah)) na maana yake ni kuwa ufunuo wangu huu hauna budi kutimia kwani kutotimia kwake ni kubatilisha maneno ya Allah)) [Ish-tiharu Ghulaam 16/10/1894].

Pia Mirza akatoa ilani nyengie nzito sana kuhusiana na Ufunuo huo wa kumuoa Binti huyo na kusema: ((Ikiwa ufunuo huu haukutimia basi mimi ni muovu kuliko waovu, enyi wehu huu sio uzushi wa mtu wala mchezo wa muovu mzushi, bali hii ni ahadi ya Allah ya kweli, Mungu ambae maneno yake hayabadiliki na Mungu ambaye hakuna wa kuzuia matakwa yake)) [Samiimatu Anjaam Aathaam uk. 54]

Majaribio ya Mirza yaliingia uwanjani na kumuandikia Bamkwe mtarajiwa Ahmed Beg ikiwa ni jaribio la kufanikisha ndoa tarajiwa: ((Ewe ndugu yangu mkarimu, Allah akuhifadhi, hivi sasa nimemaliza kufuatilia basi nikapatwa na usingizi nami nimeona (ndoto) Allah mtukufu ananiamrisha kukuonesha kwa sharti ya kuniozesha Bintibikra wako Mkubwa ili ustahiki kupata kheri nyingi za Allah na baraka zake na maneemesho yake na ukarimu wake, na akuondoshee matatizo na majanga, na kama hukunipa binti wako basi utakua ni mafikio ya lawama na adhabu, nami nimeshakufikishia aliyoniamrisha Allah ili upate maneemesho yake na ukarimu wake na akufungulie hazina za neema… vile vile mimi niko tayari kutia saini mkataba uliokuja naao kwangu, na juu ya hapo pia vyote ninavomiliki ni vyako na Allah, vile vile mimi niko tayari kumsaidia mtoto wako Azizi Beg ili apate ajira Polisi, pia nitamuozesha Binti wa Tajiri mkubwa katika wafuasi wangu) [Risalatu Ghulaam kwa Ahmed Beg kutoka Naushat Gheb uk. 100.]

Pia akamuandikia barua nyengine: ((Ukinipa Binti wako na ukaniozesha yeye nitakupa sehemu kubwa ya milki yangu ya ardhi na shamba langu, na nitampa Binti wako thuluthi 33% ya ninavomiliki, na mimi ni mkweli kwa ninayosema, na nitakupa kila utachotaka na kukitaka, na hutapata mtu bora wa kuunganisha udugu mfano wangu)) [Mir-aatu Kamaalatil- Islaam 573].

Basi Mirza alipoona vitisho na mali havijafanikiwa akaingia katika kujidhalilisha na kutaka kuhurumiwa mbele ya Bwamkwe mtarajiwa Ahmed Beg akamuandikia barua imekuja ndani yake: ((Mimi ninataraji kwenu kwa kila adabu na unyonge munikubalie kuoana mimi na Binti wenu, kwa sababu ndoa hii itahakikisha baraka nyingi na itafungua kwenu milango ya rehema ambayo hamuifikirii kabisa.. na nyinyi munajua kuwa ufunuo wangu huu umekua mashuhuri kwa maelfu ya watu bali kwa Malaki ya watu, na ulimwengu unasubiria kutimia kwa ufunuo huu, na maelfu ya viongozi wa dini ya kikiristo wanatamai kutotimia ufunuo huu ili watucheke, lakini Allah atawadhalilisha na ataninusuru… kutokana na hapo ninataraji munisaidie katika kuhakikisha ufunuo huu) [Barua ya Ghulam Mirza kwa Ahmed Beg 17/2/1892 kutoka “Kalimatu Fadhl Rahamaani” uk. 123.

Kisha Mirza aliwaandikia wanawe Ahmed na Fadhli ya kuwa wamsaidie katika suala hilo, kwa sababu Bwamkwe mtarajiwa Ahmed Beg alikua ni mjomba wa mke wa Fadhli, na Sultani yeye kulikua na uhusiano wa kifamilia kupitia mama yake, pia Mirza alimuandika mkewe ambaye ni Mama wa Sultani na Fadhli ya kuwa naye pia afanye juhudi ya kuhakikisha kuwa uke weza huo unatimia, basi aliandika haya: ((Iwapo Binti wa Ahmed Beg ataowana na mwengine asiyekua mimi, basi katika siku hiyo hiyo atakua Sultan Ahmed ni mwenye kuzuiliwa mrathi yangu na hatakua na fungamanao lolote na mimi, vile vile mama yake atakua ameachika, ama mwanangu Fadhli yeye pia atazuiliwa mirathi yangu ikiwa hakumuacha mke wake ambaye ni Binti wa dada wa Ahmed Beg, na hatakua na fungamano lolote na mimi atakua mfano wa ndugu yake Sultani) [Ilani ya Ghulam Ahmed 2/5/1891 kutoka kitabu Tabliigh Risaalah 2/9]

Lakini Allah mtukufu anafanya anayotaka, basi Binti wa Ahmed Beg Muhammadee Beujuum akaolewa na kijana aitwae Sultan Beg, lilikua ni pigo kubwa sana kwa wote na hasa hasa kwa Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani, afanye nini hali kitanzi alichojiwekea kimemkaa shingoni?

Lakini Mirza Ghulaam Ahmed hakuacha ujanja wake, wala hakuukata ukaidi wake basi aliendelea kwa vyovyote na iwe lakini Muhammadee Beijuum atakua ni mkewe tu; kwa sababu yeye ameozeshwa binti huyo Mbinguni, basi watu walipomzonga akasema: ((Hili ni sahihi kuwa Muhammadee Beijuum hakuoana na mimi, lakini bila ya shaka yoyote yeye ataoana na mimi kama ufunuo ulivosema, na hakika watu wananifanyia shere kwa sababu ya kutotimia ufunuo huu, ufunuo ambao sijaueleza kutokana na nafsi yangu bali nemuelezea baada ya kupata wahyi kutoka kwa Allah, na mimi ninasema ukweli ya kuwa itakuja siku vichwa vya hawa wanaofanya shere vitainama kwa majuto, kwani hakika mwanamke bado yuko hai na ataendelea hivo paka arejee kwangu na kuona na mimi, na mimi ninaamini hilo Imani ya yakini kwa sababu ahadi ya Allah haivunjiki). Ilani Ghulam Ahmed [Mandhuuri Ilaahii uk. 244 cha AlMandhuur Mkadiani.]

Na Mirza akaandika: ((Mimi nimenyenyekea mbele ya Allah na kuomba sana, basi nimepewa ilhamu isemayo: Mimi nitawaonesha ishara zangu kuwa huyu Mwanamke atabakia, na mume wake atakufa na wazazi wake watakufa ndani ya kipindi cha miaka mitatu, kisha mwanamke huyu atarejea kwangu, wala hakutakuwa na yoyote atakayeweza kuzuia)) Ilham Ghulaam kutoka Naushan Gheib.

Basi muda ukarefuka Mume wa Muhammadee Beijuum hakufa na Mwanamke huyo hakuoana na Mdaiunabiikivuli Mirza Ghulam Ahmed Mkadiani, na majiribio yake hayakukatika kwa muda wa miaka 22 (1886-1908) mpaka kufa kwake.

Ama Mke mtarajiwa Muhammadee Beijuum yeye alikufa mwaka 1966, ama mume wake Sultan Beg yeye aliendelea kuishi wala hakufa katika miaka mitatu kwani kifo chake kilitokea baada ya kufa Mirza Ghulaam Ahmed kwa mika 40 alifariki 1948.

Fikiria mwanamke huyu baada ya kifo cha Mumewe mwaka 1948 aliishi mpaka mwaka 1966 alikua wapi Mirza aliyefariki mwaka 1908 ili ahakikishe nyonzi zake?!!

Na namna hivi Allah mtukufu alivomdhalilisha Mirza Ghullam Ahmed Mkadiani kwa maneno yake mwenyewe aliposema kuwa kutofanikiwa kumuoa mwanamke huyo ni dalili yakinifu hasa ya uongo wake, bali ni dalili ya kuwa yeye ni muovu kuliko waovu.

Asili ya Mada hii ni Makala ya Kiarabu iliyoandikwa na Mchambuzi Mohamed Rashad Waziir.

Asanteni sana.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Bismillahi walhmadulillahi wa Salaatu wa Salaamu alaa Rasuulillahi Muhammad.

Wabaad.

Ndugu zangu kwa hakika Allah mtukufu amemfadhehesha Mdaiunabii Mirza Ghullamu Ahmad Mkadiani pia amewafedhehesha wafuasi wake Maahmadia wazi wazi, hayo ni kwa sababu Mirza Ghulaam Ahmad Mkadiani alidai kuwa yeye kapata ufunuo kuhusu umri wake kuwa ataishi miaka 80 na ikiongozeka basi ni 6 na ikipungua basi ni 6, yaani umri wake utakua baina ya miaka 74 mpaka 86, kwa maana hiyo ikibainika kuwa Mirza Ghulaam Ahmad Mkadiani aliishi umri chini ya miaka 74 au zaidi ya miaka 86 yatakua madai yake ya kupata ufunuo kutoka kwa Allah ni madai ya uongo kwani Allah mtukufu ni mkweli wala hakuna mkweli zaidi kuliko yeye.

Ust. Hani Tahir ambaye katubia na kulihama kundi la Dini ya Kiahmadia baada ya kugundua uhakika wa udanganyifu na ufichaji wa uhakika na kuwa Mirza mwenyewe anafedhehesha ubabaishaji wa Maahmadia. Ust. Huyu ana machache ya kutueleza kuhusiana na uhakika wa uzao wa Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani.

Anasema Ust. Hani Tahir: “Wafuasi wa mwenye uhodari wa kuharibu uhakika ni lazima watapata sehemu yao katika tabia za Mkuu wao Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani, na mimi hapa ninakutajieni mfano mmoja, nao ni kuwa wao wamekusudia hasa kuchafua tarehe ya uzao wa Mirza Ghulaam Ahmad Mkadiani, wamefanya hivo kwa makusudi ili wafanye jaribio la kuthibitisha ufunuo wa wahayi wa miaka 80.

Lakini la kushitua ni kuwa Mirza mwenyewe amebainisha tarehe ya kuzaliwa kwake tena kwa uwazi kabisa, ameutaja uzawa wake alipokua akielezea sera yake na hali zake, na akaufafanua uzawa wake kwa mambo ambayo haiwezekani kusahauliwa wala kuharibiwa, amesema: “Ama hali zangu binafsi nazo ni kuwa mimi nimezaliwa mwishoni mwa siku za Seikh katika mwaka  1839 au 1840 na mimi nilikua katika mwaka 1857 nina umri wa miaka 16 au 17 na ilikua bado sijaota ndevu wala sharubu.” [Kitaabu Al-Bariyyah alichoandika 1898].

Basi ikiwa Mirza Ghulaam Ahmad katika mwaka 1857 hajaota ndevu wala sharubu inabainika kuwa haiwezekani kuwa kazaliwa mwaka 1835 kama wanavozua Maahmadia; kwa sababu hilo litaweka madai ya kuwa Mirza alifikia umri wa miaka 22 bado hajaota ndevu wala sharubu, na hilo halikubaliki kiuhakikisho, hayo ni kwa mujibu wa jamii za India na ukoo wake, hasa hasa tukizingatia kwa kuwepo andiko lake mwenyewe akijieleza katika mwaka 1898 kuwa mwaka wa 1857 alikua na umri wa miaka 16 au 17 jambo ambalo uhakika uko karibu nalo zaidi, na hilo linatilia mkazo kuwa karibu zaidi na uhakika ni kuwa Mirza Ghulaam Ahmed alizaliwa mwaka 1840.” 

Likithibiti hili tunafahamu vipi Allah mtukufu alivomsuta Mirza Ghulaam Ahmed na kumfedhehesha na kukata mshipa wa shingo wa madai yake hewa, kwani umri wake aliokufia ulikua ni miaka 68 au tuseme 69 kinyume na ufunuo wa umri wake aliodai kuwa kaupata kutoka kwa Allah mtukufu kuwa umri wake ni baina ya miaka 74 mpaka 86.

Basi wale waliohadaika na udanganyifu wa Dini ya Kiahamadia tunawanasihi warudi katika safu za Uislamu, pia wahakikishe wenyewe haya tuliyoeleza kupitia marejeo tegemewa ya Mirza wenyewe.

Wabillahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Imetufikia jawabu kutoka kwa Maahmadia kuhusiana na umri wa Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani, nao wamedai kuwa wakati wa kuzaliwa Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani hakukua na utaratibu wa kudhibiti kumbukumbu za tarehe ya kuzaliwa kwa hiyo kujua tarahe hiyo ni kwa njia ya uhakikisho wa kufuatilia vigezo tafauti.

Maahmadia katika jawabu yao wamethibitisha uhakika kuwa Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani alisema kuwa kapata Wahyi kuhusu umri wake ni miaka 80 au karibu yake na kuwa ufafanuzi wake kuhusu Wahyi huo ni kati ya miaka 74 mpaka 80.

Suali jee Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani alifika huo umri wa miaka 74? Kwani ikiwa hakufikia itabainika wazi wazi kuwa ni muongo hakupata Wahyi wowote; kwani Allah mtukufu si muongo wala hakuna mkweli zaidi kuliko yeye.

Tukija katika tarehe ya kufa kwake kwa makubaliano ni 25/5/1908 AD iliyo sawa na 24/4/1326 HJ. kwa hiyo ili Wahyi wake uwe sahihi kuwa umri wake ni miaka 74 hadi 80 ni lazime awe Mirza Ghulaam Ahmed amezaliwa kati ya tarahe (25/4/1246 HJ na 25/4/1252 HJ) sawa na (21/10/1927 na 17/8/1933 AD). Na hili ni kwa kutegemea Idadi ya miaka kwa mujibu wa Kalenda ya Kiislamu; kwani ndio tegemeo la msingi katika Dini yetu, sasa tujiulize. Jee! Tarehe wanayotoa Maahmadia kwa mujibu wa uhakiki wao inakualiana na haya? Jawabu hapana, kwa hiyo bado Mirza Ghulaam Ahmed ni muongo.

Lakini uhakika waliokuja nao Maahmadia si sahihi kabisa, bali unawasuta hivi hivi kwa kutuonesha kuwa ni jaribiohewa la kuwazuga wasiofahamu, kwa nini?

Kwa sababu Mirza Ghulaam Ahmed mwenye amehakikisha mwaka wa kuzaliwa kwake kwa kusema: 

“Kuzaliwa kwangu kulitokea mnamo mwaka 1839 au 1840 katika zama za mwisho za Masingasinga na mnamo mwaka 1857 umri wangu ulikuwa ni wa miaka 16 au 17 hivi.” (Kitabul Bariyya, Ruhani Khazaain, jal 13 uk. 177, Haashiya (footnote) uk 34).

Kwa hiyo ima Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani awe ni mkweli katika maneno yake haya yasiyokua na chembe ya doa, au awe ni muongo na wao hawa ndio wakweli na tamu lao kwao ndio changu lao, kwani yeye mwenyewe anasema kuzaliwa kwake ilikua ima 1839 au 1840, yaani kwa makadirio ya mbali ni katika mwaka 1839 na makadirio ya karibu ni 1840, na kabainisha bayana safi kabisa kuwa Umri wake katika mwaka 1857 ulikua ima 16 au 17 inafahamika na wote kuwa 16 ikiwa ni mzawa wa mwaka 1840 na 17 ikiwa ni mzawa wa mwaka 1839. Na tunafahamu sote kuwa mtu aliyena akili zake timamu anajijua vizuri kuliko wengine achilia mbali mtu ambaye wao wanmuitakidi kuwa ni Mtume na Nabii na Masihi aliyeahidiwa, cheo ambacho lau kuwa ni cha kweli basi haiwezekani kuachwa katika kosa lau angalikua amekosea.

Na ajabu Maahmadia wameleta andiko hili nao hawakulimaliza kuwa yeye wakati huo alikua bado hajaota ndevu wala sharubu, nacho ni kielelezo safi cha uhakika wa makadirio ya umri wake kuwa ni sawa kabisa.

Maamadia katika jawabu yao wametupa andiko la Mirza lisemalo:

“Makadirio hasa ya umri wangu ni Mungu tu Mwenyewe Ndiye Ajuaye, lakini kutokana na ufahamu wangu ni kwamba hadi sasa kwenye mwaka huu wa 1323 Hijriya, umri wangu wakaribia miaka 70, na Allah Ndiye Ajuaye zaidi.” (Zamima Barahine Ahmadiyya sehemu ya 5 Ruhani Khazain jalada la 21 uk 365).

Tunafahamu sote kuwa Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani kafariki mwaka 1326, yaani aliposema maneno haya alikua bado hajafika umri wa miaka 70 bali anakaribia, na kukaribia maana yake ameshavuuka 65, na hili linakadhibisha madai ya kuwa yeye amefariki akiwa na umri wa zaidi ya miaka 74, kwa sababu hata tukadirie kuwa aliposema hayo alikua na umri wa miaka 69 ukiongeza 3 itakua ni 72 uko wapi Wahyi wa miaka 74 hadi 80? Uongo pia; kwani ikiwa kazaliwa 13/2/1835 AD nayo ni sawa 14/10/1250 HJ kwa mujibu wa madai yao, 1323-1250=73, yaani Mirza katika mwaka 1323 alikua na umri wa miaka 73 yaani ni muongo kuwa yeye anakaribia miaka 70 kwani hajafika hata 70 bado.

Lakini tuchukue kuwa kweli akazaliwa mwak 1839 au 1840, ambayo ni sawa na 1254 au 1255, tunakutia ima 1323-1255=68 au 1323-1254=69 ni kweli 100% kuwa katika mwaka 1323 umri wake unakaribia miaka 70 kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu, na tukija kwa mujibu wa kalenda ya Miladi 1323 = 1905. Itakua 1905-1839=66 au 1905-1840=65 bado ni kweli jamaa anakaribia 70.

Kwa hiyo uhakikisho wote kupitia maandiko ya Mirza mwenyewe ni kuwa kazaliwa mwaka 1839 au 1840 na kuwa alifariki bila ya kufikia umri wa miaka 74 kwa makadirio ya kalenda zote ya Kiislamu na ya Kimiladi.

Bali hajafikia umri wa miaka 74 hata kwa Terehe waliyotoka Maahamdia wenyewe ingawa si tarehe sahihi kiuhakikisho kama tulivoona.

Asanteni 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Nakumbuka nipotembelea kituo kikuu cha Maahmadia kilichopo katika jiji la London Uingezera, kituo walichokipa jina la Baitu Futuuh, na sisi tuliamua kufanya ziara hiyo fupi kwa lengo la kuwafahamu hawa Maahmadia kupitia wao wenyewe, pia kuwasikiliza jawabu yao kuhusu nafasi ya Mirza Ghulaamu Ahmed Mkadiani katika Ahadi ya Manabii lililotajwa katika Quraani tukufu katika Aya ya 81 ya Suratu Aala Imraan, na Aya ya 7 ya Suratu Al-Ahzaab, pia neno lao kuhusu Hadithi Sahihi ya Mtume S.A.W ((Haujabakia baada yangu katika Unabii isipokua mabashirio. Akaulizwa: Ni yapi hayo Mabashirio ewe Mtume wa Allah? Akasema: Ni ndoto njema anayoiona mja mwema)).

Walitupokea vizuri na kututembeza katika sehemu yao hiyo nikiwa mimi na mwenyeji wangu Sh. Seif Al-Miskiri Allah amuhifadhi, kisha walitufikisha naweza kusema ni Makataba, na hapo tulikutana na Maustadhi wawili Waarabu, mmoja wao ni Mmisri na mwengine ni Msyria au Mjordan, na baada ya maamkizi Ust. Mmisri ndiye aliyekua mzungumzaji, basi alileta suala la kukatika kwa adhabu ya moto siku ya kiama akidai kuwa kudumu adhabu milele kuko nje ya hekima, na sisi tukamjibu kuwa kutosadikisha hukumu ya Allah muweza wa kila kitu ndiko kuliko nje ya hekima, kisha tukamuingiza katika suala la Ahadi ya Manabii na kumlazimisha kwa malazimisho yake, basi tulipombana akasema: “Kama ni hivo basi ahadi hiyo halina maana yoyote,” na kwa neno lake hilo lenye madhumuni ya kutoheshimu mapitisho ya Allah nikaufunga mlango huo kwa jawabu yake hiyo ya kutupatupa yenye ishara ya kufilisika kihoja na dalili na hata mantiki, basi baada ya hapo wakaleta suala la kuwepo NASKH katika Quraani, na hapo walishadidia sana wakidai kuwa hakuna NASKH katika Quraani, nikawambia ni rai imesemwa na baadhi ya Wanavyuoni lakini uhakika ni kuwepo kwa NASKH katika Quraani, basi nikajua kuwa kundi hili la Maahmadia wanapiga vita fikra ya kuwepo NASKH katika Quraani.

Huenda mtu akauliza NASKH ni kitu gani tena?  

NASKH ni kufutwa hukumu au kisomo, yaani Aya imetereshwa ikiwa na hukumu ndani yake, kisha Aya ikafutwa kisomo chake au hukumu yake.

Kwa upande wa Quraani ziko aina tatu za NASKH:

 1. Kufutwa kisomo na kubakia hukumu, yaani Aya husika haimo katika Quraani lakini hukumu yake ipo, hukumu hiyo inajulikana kuwa kuthibiti kwake ni kwa Aya iliyofutwa kisomo chake. Zinduo: Aina hii ya NASKH kwetu sisi Ibadhi haikubaliki.
 2. Kufutwa hukumu na kubakia kisomo, hii inalazimisha kuwepo Aya katika Quraani lakini hukumu yake haifanyiwi kazi tena kwa kukaliwa na hukumu nyengine. Zinduo: Hii inakubalika kwetu sisi Ibadhi.
 3. Kufutwa hukumu na kisomo pamoja, hii maana yake Aya iliteremka kisha kisomo na hukumu vyote vikafutwa. Zinduo: Hii kwetu sisi Ibadhi haipo.

La kushangaza baada ya hayo yote ni sisi kukutia kuwa Mirza Ghulaamu Ahmed Mkadiani mwenyewe anathibitisha aina zote tatu za NASKH, sasa vipi Maahmadia wamefikia daraja hiyo ya kupingana na yule wanaemuitakidi wao kuwa ni Mtume na Nabii na Masihi Mauudi?!!!

Kwa hakika hili ni lenye kushangaza sana, na kuwaona wazi wazi kuwa wao ni kundi la upotoshaji wa kukusudia.

1. KUFUTWA KWA KISOMO:

Anasema Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani:

“لقد تلقيت صباح اليوم إلهاما وكنت أنوي أن أسجله ولكن لم أفعل ذلك معتمدا على الذاكرة ثم نسيته تماما ولم أذكره مع أني حاولت كثيرا. والحق أنه: {مَا نَنْسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنْسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِنْهَا أَوْ مِثْلِهَا}”.

“Kwa hakika nimepata asubuhi ya leo ilhamu nami nilikua nimewaka nia ya kuiandika, lakini sikufanya hilo kwa kutegemea kumbukumbu ya kuhifadhi basi nimeisahau kabisa, na sikuikumbuka pamoja na kujaribu kwangu sana, na HAKI ILIVYO NI KUWA ((HATUFUTI AYA YOYOTE AU KUISAHAULISHA ISIPOKUA HULETA ILIYO BORA ZAIDI YA HIYO AU MFANO WAKE)) [Badru J2. no. 7, idadi 6/3/1903 uk. 50]

“إن إلهنا قادر على كل شيء، وله القدرة كلها: {يَمْحُوا اللهُ مَا يَشَاءُ}. ونحن نؤمن أنه عزّ وجلّ ليس كالمنجّمين. إذا أصدر حكما صباحا فهو قادر على أن يستبدل به غيره مساء، والآية “مَا نَنْسَخْ مِنْ آيَةٍ” تشهد على ذلك”.

“Hakika Mungu wetu ni muweza wa kila kitu, yeye anao uwezo wote: ((Anafuta Allah anayotaka)) na sisi tunaamini kuwa yeye Allah mtukufu si kama waaguzi, basi akitoa hukumu asubuhi yeye ni muweza wa kuibadilisha kwa hukumu nyengine jioni, na Aya ((Hatufuti Aya yoyote)) inashuhudia hilo.” [Badru J7. no. 19-20, idadi 14/5/1903 uk. 4]

2. KUFUTWA KWA KISOMO NA KUBAKIA HUKUMU:

Anasema Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani:

“أنت إلى الآن تجهل عقيدة المسلمين، ألا تفهم أنه لو كان الإنسان مجبرا مكرها عند القرآن الكريم لما أمر القرآن صراحة بقطع يد السارق ورجم الزاني، ولم يرجم أحد، لقد ذكر القرآن الكريم خيار وحرية الإنسان لا في آية واحدة أو آيتين بل في مئات الآيات”. (الحرب المقدسة، ص 170، الخزائن الروحانية المجلد السادس ص 252)

“Wewe mpaka hivi sasa ni mjinga wa itikadi ya Waislamu, hivi hufahamu kuwa lau Mtu angalikua ni mtezwanguvu mlazimishwa asiyekua na hiari katika Quraani basi isingeliamrisha Quraani wazi wazi KUKATWA MKONO WA MWIZI NA KURUJUMIWA MZINIFU (kupigwa mawe hadi kufa), na kusingekua na yoyote wa kupiga mawe mzinfu. Kwa hakika Quraani tukufu imetaja hiari na uhuru wa Mtu si katika Aya moja au mbili bali katika mamia ya Aya.” [Harbu Muqaddasa uk. 170, Khazainu Ruuhania J6 uk.252].

Watuoneshe Maahmadia hukumu ya kurujumiwa Mzinifu ndani ya Quraani kama alivotueleza Mkadiani wao Mirza Ghulamu Ahmad, kwa hakika ima Mirza atakua ni muongo kwa kuinasibishia Quraani yasiyokuwemo ndani yake, au atakua anathibitisha kufutwa kwake kisomo na kubakia kwake hukumu, tamu lao kati ya hayo mawili ndio chungu lao kwa hawa Maahmadia.

3. KUFUTWA HUKUMU NA KUBAKIA KISOMO.

Anasema Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani:

: “يقول القرآن الكريم: {مَا نَنْسَخْ مِنْ آَيَةٍ أَوْ نُنْسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِنْهَا أَوْ مِثْلِهَا}. فقد قال القرآن في هذه الآية بوضوح تام بأنه لا يمكن نسخ آية إلا بآية فقط. لذا وعد أنه لا بد أن تنـزل آية مكانَ الآية المنسوخة”.

“Inasema Quraani tukufu: ((Hatufuti Aya yoyote au kuisahaulisha isipokua huleta iliyo bora daidi yake au mfano wake)) Kwa hakika Quraani imesema katika Aya hii kwa uwazi kamilifu, ya kuwa haiwezekani kufutwa Aya yoyote isipokua kwa Aya nyengine tu, na kwa hilo ameahidi kuteremshwa Aya sehemu ya Aya iliyofutwa”. [Alhaq Lidahyaani uk. 90-91].

: “فهل يُعقل أن تكون أوامر الله تعالى غير ناضجة وغير ثابتة ومليئة بالتعارضات إلى هذا الحد؛ بحيث يفرض خمسين صلاة أولا……ثم يخلف وعده مرات عديدة ويَنسخ آيات القرآن الكريم مرة بعد أخرى، وذلك دون أن تنـزل آية ناسخة بحسب منطوق الآية: {نَأْتِ بِخَيْرٍ مِنْهَا أَوْ مِثْلِهَا}”. (إزالة الأوهام)

“Basi inaingia akilini ziwe amri za Allah hazijapevuka na hazijathibiti na zijae migongano kiasi hiki, hata kufikia kulazimishwa mwanzo sala 50… kisha aende kinyume na ahadi yake mara nyingi na afute Aya za Quraani tukufu mara baada ya mara nyengine, na hayo bila kuteremka Aya iliyofuta kwa mujibu wa maelezo ya kuthibitisha ya Aya ((Tunaleta iliyo bora zaidi yake au mfano wake)).” [Izaalatu Auhaami).

Darsa hii ya Naskh asili yake ni ufafanuzi wa Ust. Hani Tahiri, naye alikua Muahmadia mtetezi hasa, lakini baada ya kuona uhakika wa kundi hilo na ubabishaji wa wazi wa Muanzilishi wake Mirza Ghulaam Ahmed Mkadiani, na jinsi alivofedheheshwa na Allah mtukufu kupitia ulimi wake na kalamu yake mwenyewe.

Ust. Hani Tahir aliamua kutubia na kuachana na kundi hilo na kubainisha kwa waja uhakika wa kundi hilo na maajabu ya Muanzilishi wake Mirza Ghulaam Ahmad Mkadiani.

Wabillahi Taufiiq.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Shukurani zote ziwe kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa aliye khitimisho la Manabii Mtume wetu Muhammad pamoja na Aali zake na Masahaba wake mpaka siku ya mwisho.

Baada ya kuona uhakika wa umri wa Mkadiani Mirza Ghulam Ahmed kuhusu umri wake kutoka katika maandiko yake mweyewe ambayo Maahmadia wamekubali usahihi wake kuwa -kwa mujibu wa neno lake- alizaliwa mwaka 1839 au 1840 na katika mwaka 1857 umri wake ulikua ni miaka 16 au 17 tena ni kijana mdogo hajaota ndevu wala sharubu, tukumbuke maneno hayo yamo katika kitabu alichoandika Mirza mwenyewe mwaka 1898.

Bila shaka Mirza alikua akikumbuka vizuri ujana wake kiasi cha kukumbuka kuwa mwaka 1857 alikua bado hajaota ndevu wala sharubu, na Mirza ni kijana wa jamii ya Kihindi, na uotaji wa ndevu na sharubu hauchelewi sana kwao na ndio maana akaeleza kuwa alikua hajaota ndevu wala sharubu ili kuhakikisha kuwa bado alikua ni mvulana mdogo wa miaka 16 au 17 kama alivojieleza, lakini tukija kwa mujibu wa tarehe ya Jamaa ya Kiahmadia isemayo kuwa Mirza alizaliwa mwaka 1835 A.D itakua Mirza ambaye kijana wa kihindi mwenye umri wa miaka 22 lakini bado hajaota ndevu wala sharubu; kwa hakika inafaa watutafutie mafano wake au wadai kuwa huo ulikua ni muujiza wa kuthibitisha wanayomdaia kwa sababu ni jambo lililo kinyume na mazoea kiasi cha kufikia kuwa ni nadra sana katika jamii ya Wahindi.

Lakini kama inavojulikana kuwa kundi hili la Kiahmadia limetopea katika ubabaishaji na udanganyifu, basi ili kun`gan`gania batili yao wamekuja na baadhi ya walioziita hakikishaji zao ili wazidanganye kwazo nafsi zao, wamesema kuwa: “Mirza Ghulam Ahmad Mkadiani hakua akijua umri wake wala akifahamu hasa tarehe yake ya kuzaliwa.”

Bila shaka wameyasema hayo ili wamnyamazishe Mirza na wamwabie wee nyamaza hujui hata umri wako, vipi unatuambia kuwa ulizaliwa mwaka 1839 au 1840 na kuwa katika mwaka 1857 ulikua bado hujaota ndevu wala sharubu kwa sababu ulikua mdogo kijana wa miaka 16 au 17, vipi unasema haya hali ya kuwa umri wako ulikua mwaka huo wa 1857 ni miaka 22; kwani ulizaliwa mwaka 1835, yaani Waumini wanajua zaidi na wakweli zaidi kuliko huyo wanaemuamini kuwa na cheo cha Umasihi na Umahadi na Unabii na Utume.

DALILI YA MAAHMADIA

Wamesema kuwa Mirza Ghulam Ahmed amesema: “Umri wangu ulipofikia miaka 40 basi Mwenyezi Mungu akanipa heshima ya kunifunulia Ilhaam na maneno yake” [Taryaaqul Quluub, Ruhaani Khazaain jal 15 uk 283]

Wakasema kuwa hayo pia aliyasema katika kitabu chake Barahine Ahmadiyayya sehemu ya tano, Ruhani Khazain jal 21 uk 135.
Na kuwa Mirza Ghalam Ahmed Mkadiani pia amesema:
“Hili ni jambo la ajabu, nami nalifahamu jambo hilo kuwa ni ishara fulani ya Mwenyezi Mungu kwamba mnamo mwaka 1290 Hijiria nilikuwa nimeshapata heshima kutoka kwa Allah ya kuongea naye (kwa ufunuo).” [Haqiqatul Wahi Ruhani Khazaain jal 22 uk 208].

Maahmadia kutokana na kauli mbili hizo wakaunganisha na kukokotoa ili wajipatie matokeo yao 1290 – 40 = 1250 Hijiria ambayo ni sawa na 1835 AD.

JAWABU:

La ajabu ni kuwa sehemu hii Mirza kirahisi kauli zake zimekua sahihi na alikua akiijua vizuri miaka yake, ama kule alikua haijui miaka akilengalenga tu, na sisi tukichukua hali ya kimaumbile kwa binadamu ni kuwa maneno haya yaliyomo katika Haqiqatu Al-Wahyi ni maneno aliyoyasema akiwa uzeeni karibu na kufa kwake; kwa hiyo kama Mirza hakua akifahamu hasa tarehe ya kuzaliwa kwake na alikua na tabia ya kukosea kumbukumbu kama walivomsifu Maahmadia wenyewe, basi athari za hayo zitakua karibu zaidi kupatikana katika umri kubwa kwa sababu ya udhaifu na uzee, hasa hasa tukizingatia kuwa maneno hayo ameyasema kabla ya mwaka tu wa kifo chake, na wao wanadai kuwa amekufa akiwa na umri wa miaka 75.

Juu ya yote hayo tujue kuwa Mirza Ghulam Ahmed Mkadiani atakua amejeruhiwa na wafuasi wake mwenyewe, tena kwa jeraha la kuwa hakua madhubuti katika kudhibiti habari na matokeo; kwa hiyo anakua dhaifu katika maelezo yake, -tunasema- lau kuwa Mirza ni mmoja wa wapokezi wa Hadithi basi Hadithi zilizopita kwake zingeachwa kwa sababu zingalihukumiwa kuwa zimepita kwa mpokezi aliyekua na udhaifu wa kumbukumbu na kuchanganyikiwa.

Ust. Hani Tahiri ambaye anafahamu vizuri sana mambo ya ndani ya Jumuia hii ya Kiahmadia anatumbia haya yafuatayo katika kujibu hakikisha waliyokuja nayo Maahmadia:

“Ninasema: Huo ni udanganyifu uliozidi udanganyifu, na hayo ni kwa sababu neno la Mirza kuwa kapata Wahyi katika mwaka 1290 Hijiria si zaidi ya kuwa ni uongo aliousema mwaka 1907 katika kitabu chake Haqiqatu Al-Wahyi, na hayo aliyafanya baada ya kuona andiko la Taurati, basi hapo ndipo alipopindisha tarehe ya mwanzo ya kupata Wahyi ili ikubaliane na Wahyi wa Taurati, kwani amesema: “Na imetajwa katika ufunuo wa Nabii Daniali kuhusu kudhihiri kwa Masihi aliyeahidiwa, nao ndio wakati wenyewe hasa alionipeleka Allah mtukufu ndani yake, kwani hakika imekuja ndani yake: “Wengi watajisafisha na watan`garishwa na watatahiniwa, ama waovu wao pia watafanya uovu wala hatafahamu yoyote kati ya waovu, lakini wenye kufahamu watafahamu, na kutoka wakati wa kuondosha maunguzo ya kudumu na kusimamisha uchafu wa uharibifu ni siku elfu moja na mia mbili na tisiini (1290), basi ni ubora ulioje kwa mwenye kusubiria na akafikia mpaka siku elfu na mia tatu na hamsini (1350)” Basi katika Wahyi huu alielezwa Masihi Mauudi ambaye atadhihiri katika zama za mwisho. Basi kwa hakika ametaja Nabii Daniali alama yake ya kuwa Mayahudi wataacha sadaka za kuunguzwa katika zama hizo na atadhihiri Masihi Muahidiwa baada ya kupita miaka 1290. Basi wakati huu ndio wakati wa kudhihiri Mja mwenye kujidogosha, kwa sababu Kitabu changu “Baraahinu Al-Ahmadiyah” kimetolewa baada ya kutumwa kwangu kwa miaka michache tu. Na jambo geni -na mimi nalizingatia kuwa ni aya kutoka kwa Allah- ni kuwa mimi nilipata heshima ya kusemezwa na mazungumzo ya kiungu katika mwaka 1290 Hijiria (1873 AD). [Haqiqatu Al-Wahyi]

Uhakika ni kuwa Mirza hakusema kweli pale alipodai kuwa yeye kapata heshima ya kusemezwa na mazungumzo ya Kiungu katika mwaka 1290 Hijiria, na hayo ni kwa sababu zifuatazo:

1. Mtoto wake Mirza Mahmoud anasema: “Alikua (Mirza) amefikia umri wa miaka arubiani (40) takriban wakati alipokufa Baba yake mzazi. Na siku hiyo ilikua ndio siku ya mwanzo iliyofunguliwa kwake milango ya Mbingu na akasemezwa na Mola wa Mbingu na Ardhi” [Tuhfatu Amiiri Weilaz]. Na katika yenye kujulikana kuwa Baba yake alifariki tarehe 3/6/1876 [Tadhkirah], na tarehe hiyo inakubaliana na mwaka 1293 na sio 1290.

2. Ikiwa neno lililopita hatutalikubali basi Mirza mwenyewe anasema katika mwaka 1883: “Nimepata katika mwaka 1868 A.D au 1869 A.D ilhamu ya ajabu sana… Kwa hakika amekuridhia Mola wako kwa haya uliyofanya, na atakubariki kwa baraka nyingi mpaka Wafalme watajipatia baraka kwa nguo zako.” [Baraahinu Raabii], na mwaka huo unakubaliana na mwaka 1286 Hijiria na sio mwaka 1290 Hijiria.

3. Na ikiwa pia hatutakubali hayo yaliyopita basi Mirza anasema kuwa yeye kapata Wayhi usemao “Miaka thamanini” kabla ya miaka 35 kutokea mwaka 1900 [Kitabu Al-Arbaina] yaani katika mwaka 1865 ambao unakubaliana na mwaka 1282 Hijiria, na pamoja na haya hii nambari ni ya ukaribu haitolewi hoja lakini inafaa katika mlangi wa kulazimishana tu, kwani uhakika ni kuwa sisi hatumsadiki mtu huyu kwa chochote alichokisema.
Na ajabu zaidi ni kuwa Muahmadia aliyekuja na dalili yake hiyo ya kupanga kupitia neno la Mirza amemzidi Mirza mwenyewe kwa uongo; kwa sababu Mirza mwenyewe baada ya ukurasa mmoja tu wa hayo aliyotolea hoja huyu Muahmadia ameandika: “Na umri wangu katika wakati huu unakaribia miaka 68” [Haqiqatu Al-Wahyi].

Basi ikiwa Mirza mwenyewe anataja kuwa umri wake unakaribia miaka 68 katika mwaka 1907 ambao ameandika maelezo hayo ni dhahiri kuwa bado anakumbuka kuwa kazaliwa mwaka 1839 kwa makadirio ya mbali zaidi, basi vipi huyu Muahmadia alivoghafilika kwa sababu ya mapendwa moyo yake hadi kufikia kuleta hikaya ya mwaka 1290 Hijiria kuwa ndio hoja?!!!
Mirza aliendelea kutolea hoja Wahyi wa Daniali kwa kusema: “Kisha Nabii Daniali anataja kipindi cha mwisho cha kudhihiri Masihi Muahidiwa yaani mwaka 1335. Na hii imekua ni Ilahaamu kutoka kwa Allah nimepatiwa kuhusu umri wangu. [Haqiqatu Al-Wahyi]

Nalo ni neno ambalo liko wazi kuwa Mirza alikua akiashiria kuwa yeye atakufa katika mwaka 1335 Hijiria kama alivo katika Wahyi wa miaka 80 aliodai kuupata, lakini hilo halikupaatikana, kwani Mirza alikufa baada ya mwaka mmoja takriban baada ya kuandika andiko hilo.. alikufa katika mwaka 1326 Hijiria yaani kabla ya miaka 9 ya nambari aliyoitaja Daniali, na kwa hilo ukabatilika Wahyi wa Daniali tokea mizizi yake. Na ikiwa atajipumbaza Muahamadia na kujaribu kupiga chenga kwa kusema pengine mwaka 1335 alikua akihadithia Baia ya Mirza Mahmoud. Tutamwambia: Hakika mwaka huo 1335 Hijiria unaambatana na mwaka 1917 A.D na sio 1914 A.D ambao Mahmaoud alipewa Baia ndani yake.

Wabillahi taufiki

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa Rahmatullahi wa barakatuh.

Anasema Mdaiunabii kiburuza Mirza Ghulamu Ahmed Mkadiani: “Katika sifa za Dajjali aliyeahidiwa ni kuwa yeye atadai unabii.” Tunafahamu sote kuwa Udajjali ni jinasifa lenye kubeba lazimisho la uongo na khiyana, basi Dajjali bila shaka atakua ni mwingi na uongo, ubabaishaji na kulaghai watu, na sisi tukichunguza na kuhakikisha tunakutia kuwa sifa za uongo na ubabaishaji na udanganyifu na ulaghai zimemlazimu Mdaiunabii kiburuza Mkadiani Mirza Ghulamu Ahmed, kiasi cha kuwa hakuna wahyi hata moja aliyodai kuwa kaipokea kutoka kwa Allah mtukufu isipokua Allah mtukufu alimkadhibisha katika madai yake.

Ust. Hani Tahiri ambae ni mmoja wa Maahamadia waliotubia baada ya kuitumikia Dini hiyo ya Kiahmadia kwa miaka mingi ana mengi ya kutueleza kuhusu Udajjali wa Mirza Ghulamu Ahmed, nayo ndiyo sababu hasa iliyomtoa katika kiza cha Dini hiyo mpya ya Kiahmadia na kurudi katika Uislamu.

Anatuambia Ust. Hani Tahiri:

Mirza ilimuuma sana pale Dr. Abdulhakiim Khaan alipojitoa katika safu zake na kuamua kumtangazia uhakika wake, bali hakumalizia hapo tu kwani naye pia alidai anapata Wahyi mahususi kuhusu Mirza, jambo ambalo Mirza lilimkera sana hadi kufikia kuandika haya yafuatayo:

“Inawezekana wengi wa watu wanajua kuwa Dr. Abdulhakiim Khaan aliyekua mmoja wa wafuasi wangu kwa muda wa miaka ishirini takriban ameritadi tokea siku chache na kuwa adui mkali sana, kwa hakika ameniita mimi kuwa ni muongo, mlaghai, shetani, dajjali, muovu na mlaji haramu, pia amenihesabu kuwa ni khaini mwenye tamaa, pupa, na mzushi mwenye kumzulia uongo Allah mtukufu, na hayo yamo katika kitabu chake ((Masihu Dajjali)), na hakuna aibu yoyote isipokua amenilenga nayo kama kwamba tokea kuumbwa kwa Dunia hakuna wa kupigiwa mfano wa maovu hayo yote isipokua mimi, na hakutosheka na hayo, bali alizunguka katika miji mikuu ya Punjabi na kutoa mihadhara ya kubainisha aibu zangu na kunilengea aina nyingi za maovu katika mikutano ya halaiki katika Lahore na Amritsar na Bitiyalah na mihadhara mengine katika miji tafauti, naye amenidhihirisha mimi kuwa ni hatari katika Ulimwengu na mbaya zaidi ya Shetani na kunifanyia shere katika mihadhara yake yote.

Kwa ufupi nimepata kutoka kwake maudhi ambayo haina haja kuyaeleza, na Miyaan Abdulhakiim hakutosheka kwa hayo tu, bali ameeneza katika kila muhadhara wake Wahyi zake kwa mamia ya watu, imekuja ndani yake: Hakika Allah amenipa ilhamu kuwa mtu huyu (yaani Mirza) ataangamia katika kipindi cha miaka sita, na yatamalizika maisha yake; kwa sababu yeye ni muongo mzushi”.

Nimesubiria katika Wahayi zake, lakini leo hii ya tarehe 14/8/1906 A.D imefika barua yake kwa ndugu yetu Mwema Mkuu Al-Muulawi Nurudini ameandika ndani yake -baada ya kueleza  kuhusu mimi aina nyingi za aibu na matusi mengi-: Hakika Allah mtukufu ameniambia katika tarehe 12/7/1906 A.D kuhusu maangamizi ya huyu mtu (Mirza). Na kuwa hakika ataangamia ndani ya miaka mitatu tokea tarehe ya leo.

Na kwa vile jambo hili hivi sasa limeshafikia upeo huu, basi hapana budi na mimi bila kuona usumbufu wowote nieneze yale aliyoniwekea wazi Allah mtukufu kuhusu yeye (yaani Dr. Abdulhakim Khaan).

Na kwa haki, katika haya kuna kheri kwa hawa watu; kwa sababu lau kuwa mimi kweli ni muongo mbele ya Allah, ninamzulia yeye usiku mchana tokea miaka 25 nimo tu katika namuongopea yeye bila kujali ukuu wake na utukufu wake, nami nimo katika kuwafanyia viumbe wake ulaghai wa kula mali zao kwa ukhaini na kwa njia za haramu na kuwaudhi wake kwa tabia zangu chafu na chuki za nafsi yangu, basi mimi ningalikua katika hali hiyo ninastahiki kupata adhabu kubwa na nzito kuliko mtu yoyote muovu ili watu wasalimike na fitina zangu, ama ikiwa mimi siko kama anavozua Miyan Abdulhakim, basi ninataraji kutoka kwa Allah ya kuwa hatanifisha kifo cha udhalilifu, kifo cha kujaalia mbale yangu laana na nyuma yangu laana. Kwa hakika sijafichika mbele ya jicho la Allah, hanijui isipokua yeye tu.

Na kwa kila hali ninaleta katika yanayofuata Wahayi zote mbili, yaani Wahayi ya Miyan Abdulhakim kuhusu mimi, na yale ambayo Allah mtukufu alimeniwekea wazi kutokana na Wahayi huo (wa Dr. Abdulhakiim Khaan), nami ninawacha hukumu kwa Allah muweza.

1. Wahyi wa Miyaan Abdulhakim Daktarimpasuaji Msaidizi katika Bitiyalah kuhusu mimi ambao kauandika katika barua yake aliyoituma kwa Ndugu yangu Mwema Al-Mulawi Nurudini unasema kama ifuatavyo: ((Nimepata katika tarehe 12/7/1906 A.D ilhamu zifuatazo kuhusu Mirza: Mirza ni mchupa mipaka, jiongo, laghai. Muovu ataangamia mbele ya mkweli. Na nimeambiwa kuwa ahadi ya kutimia hilo ni ndani ya miaka mitatu.))

Wahayi ambao nimeupata kutoka kwa Allah mtukufu wa kuelekeana na Wahayi huo uliotoka kwa Miyaan Abdulhakim Khaan Daktarimpasuaji Msaidizi katika Bitiyalah na tarajama yake ni kama ifuatavyo:

((Inapatikana kwa waliokubaliwa mbele ya Allah mifano ya kukubaliwa na alama zake. Hakika wao wanaitwa viongozi wa amani, wala hakuna nafasi ya yoyote kuwashinda hao, hakika upanga wa Malaika uliochomolewa mbele yako lakini wewe hujadiriki wakati na hujaona na hujajua. “Ewe Mola pambanua baina ya mkweli na muongo, wewe unamuona kila mwema na mkweli.)) 

Mtangazaji: Mirza Ghulam Ahmed Mkadiani.

16/8/1906 A.D sawa na 24/Jumaada 2/ 1324 HJ. [Jal. 2 la ilani na haqiqatu Al-Wahyi]

Ndugu zangu wasomaji, inajulikana wazi kuwa Dr. Abdulhakim Khaan amesema kuwa kipindi cha uhai wa Mirza hakivuuki miaka 3 kuanzia tarahe 12/7/1906 yaani hatafika tarehe 12/7/1909 A.D, na inafahamika kwa yakini kuwa Mirza alifariki kwa maradhi ya kipindupindu ambacho alidai kuwa alipata Wahayi wa kumbashiria kuwa hakitampata na hakitaingia nyumbani kwake kama tutakavoona, kwani Allah mtukufu akamkadhibisha akamsalitishia kipindupindu na kufa katika tarehe 26/5/1908 A.D.

Na ya ajabu ni kuwa Dr. Abdulhakiim Khaan alisema kuwa Ilhamu aliyoipata ilisema kuwa muongo kati yake na Mirza atafariki katika uhai wa mkweli, yaani lau kuwa Mirza ni mkweli katika madai yake basi Dr. Abdulhakim Khaan atafariki kabla ya kufa Mirza, na kama Mirza ni muongo katika madai yake basi atafariki kabla ya kufa Dr. Abdulhakiim Khaan, na Mirza kama tulivoona katika Wahayi wake kuna hiyo dua aliyoomba inayoashiria kukubali sharti ya Dr. Abdulhakiim Khaan ya kufa muongo katika uhai wa mkweli, lakini ndio hivo tena kama tunavojua Mirza ni muongo, Wahayi zake mara zote zinakua kinyumenyume; kwa hiyo akafariki katika uhai wa Dr. Abdulhakiim Khaan na kubainika kuwa Mirza ni muongo. 

Lakini cha ajabu ni kuwa Mirza Ghulamu Ahmed kabla ya kifo chake kwa miezi sita alidai kuwa kapata Wahayi unaosema: ((Vile vile Nitaongeza katika umri wako.)) Kwa maana: Nitamkadhibisha adui anayesema kuwa haujabakia katika umri wako isipokua miezi 14 kuanzia mwezi wa 7 mwaka wa 1907 A.D, pia (nitawakadhibisha) wengineo katika maadui wako ambao wanatabiri, nitawakadhibisha wote hao na nitaongeza katika umri wako ili watu wajue kuwa mimi ndiye Mungu, na kuwa kila jambo limo mikononi mwangu….. na nakuongezea wahayi mwengine unaosema ((Tauni kali sana ambayo haijawahi kutokea mfano wake itaenea katika nchi hii na nchi nyengine, na tauni hiyo itawafanya watu kuwa wehu.)) Sijui ikiwa tauni hiyo itaenea mwaka huu au ujao, lakini hakika Allah amenambia na kusema: “Nitakuokoa na kila atakayeingia nyumba yako, kama kwamba nyumba hii itakua ni jahazi la Nuhu, basi atakayeingia ataokoka.” [Ilani 5/11/1907, Al-hakam 10/11/1907 Uk. 6]

Na inafahamika kuwa Mirza alifariki Tarehe 26/5/1908 A.D tena kwa Tauni ya Kipindupindu ambayo alidai kuwa kapata Wahayi kuwa haitampata wala haitaingia nyumbani mwake.

Na sio hivo tu bali Mirza kabla ya kufa kwake kwa wiki chache aliandika: Walisimama mbele yangu maadui wengine wengi katika Waislamu na waliangamia na haijabakia kwao athari yoyote, ama hivi sasa amechangamka adui wa mwisho anayeitwa Abdulhakim Khaan, naye ni Daktari anaishi katika Wilaya ya Bitiyalah, naye anadai akiniashiria mimi, kuwa mimi -yaani mimi mja dhaifu- nitakufa ndani ya uhai wake yeye, na miadi ya hayo sitafika tarehe 4/9/1908 A.D na hilo litakua ni dalili ya ukweli wake. Mtu huyu adai kuwa anapata Ilahamu na ananiona mimi kuwa ni Dajjali Kafir Muongo… lakini Allah ameniambia kuhusu utabiri wake huo kuwa yeye atamchukua huyo kwa adhabu na atamuangamiza, na mimi nitaokolewa na shari yake, basi jambo hili liko katika mkono wa Allah mtukufu, na hakuna shaka kuwa hilo ni sahihi kiukamilifu, na hakika Allah atamnusuru aliye mkweli katika uoni wake”. [Yanbuu Al-Maarifah 1908].

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa batakatuhu.

Naama ndugu wasomaji tufahamu kuwa Mdaiunabiikiburuza Mkadiani Mirza Ghulaam Ahmed alikua ni mwoga sana wa mijadala anapokutana na wenye elimu, na leo tunakuletea mkasa wake wa kukimbia kufanya mjadala na Sheikh Thanaullahi kama tutakavoona katika maelezo yanayofuata.

Tufahamu kuwa Nabii yoyote hawi mwoga, na Allah mtukufu huwathibitisha kihoja mbele ya wapinzani wao na hawakimbii mijadala, hata Mtume wetu Muhammad S.A.W aliambiwa: ((Na jadiliana nao kwa yaliyo bora zaidi)) [Nahal 125].

Mnamo tarehe 10/1/1903 Mirza Ghulaamu Ahmad alijua kuwa Sheikh Thanaaullahi Al-Amritsiri yupo katika mji wa Kadiani kwa lengo la kupeana hoja za kielimu na yeye, basi hakuweza kusema chochote kuhusu jambo hilo ila neno lake: Wanakuja hapa maelfu ya watu kama wapita njia, hilo halitushughulishi sisi”… Kisha alipokuja kwa ajili ya sala ya Isha alisema: Zimenifikia kutoka kwa Sheikh Thanaaullahi barua mbili zenye kubeba kusudio moja … akapewa barua Sayyid Sarwar Shaah ili aisome mbele ya watu (Na hawakutaja hata herufi moja iliyomo katika barua hiyo katika malfudhaati yao). Kisha Mirza akasema: Mimi niko tayari, lakini itamlazimu asikilize maneno yetu kwa utulivu kwa muda wa wiki au siku kumi, ama ikiwa kusudio lake ni kujadiliana basi hilo ni kosa lake; kwa sababu sisi tumesimamisha kufanya mijadala tokea kitambo, ama ikiwa ni mwenye kutafuta haki basi inamlazimu aitafute katika kuondosha kosa lake kwa upole na utulivu. [Malfudhaatu Jal 1 No. 12. Idadi 16/1/1903]

Na katika siku ya 11/1/1903 Mirza aliandika jawabu refu akibainisha kukataa kwake mjadala na kukimbia kufanya mjadala na Sheikh Thanaullahi, jawabu hiyo ni dalili tosha kuwa Mirza alijawa na woga na khofu ya kuelekeana na Sheikh Thanaullahi, kama yalivo wazi hayo ndani ya jawabu hiyo, na sisi tunachukua katika jawabu yake baadhi ya vipande.

Amesema:

Sharti ya pili: “Hakika yalivo hasa ni kuwa hutakubaliwa kuzungumza kwa sauti, bali utaniandika msitari mmoja au miwili kwa kufupisha na utaleta ndani yake upinzani wako, na mimi nitakujibu kwa ufafanuzi katika kikao husika, hakuna haja ya kuandika upinzani kwa urefu bali itoshe msitari mmoja au miwili”

Sharti ya Tatu: Ulete upinzani mmoja tu katika siku nzima kwa sababu hukutuambia kabla kuwa unakuja bali umekuja kama wezi, na mimi siwezi kutoa katika siku hizi zaidi ya masaa matatu kwa sababu ya ufinyu wa wakati kwangu na mashughuliko yangu yaliyofungamana na uchapishaji wa kitabu, na ijulikane ya kuwa hutakubaliwa kabisa kuwa uanze majibizano na mimi kama watoa mawaidha mbele ya watu wa kawaida kama wanyama, bali italazimika ulazimike na ukimya kikamilifu uwe mfano wa kiziwi bubu, na hayo yote ili mazungumzo yasije yakageuka na kuwa majibizano ya mjadala, na itakulazimu kuleta suali kuhusu ufunuo mmoja tu na nipewe nafasi ya kujibu hadi masaa matatu, na utaambiwa baada ya kila saa ya kuwa ikiwa kujakinaika unayo haki ya kuleta kitu chengine kimaandishi, na hutapata nafsi ya kuyasoma kwa sauti kubwa bali mimi mwenyewe ndiye nitakaeyasoma, na italazimika maelezo yako yasizidi mistari mitatu ….

Kisha barua hiyo aliyojibu Mirza ikafikishwa kwa Sheikh Thanaaullahi, na baada ya muda mfupi ikaja kutoka kwa Sheikh Thanaullahi jawabu ya jawabu ya Mirza. [Marejeo yaliyopita].

Baada ya hayo wafuasi wa Mirza waliandika katika jarida la Badr: “Hakika Mirza aliumia sana kwa kusikia kwake jawabu isiyokubalika kiakili na iliyo mbali sana na maudhui yenyewe”

La ajabu wafuasi wa Mirza walishindwa kueleza kwa kutaleta yaliyoandikwa katika barua ya Sheikh Thanaullahi si ya kwanza wala ya pili.

Basi yaliyo wazi mbele ya kila mwenye akili timamu katika maelezo hayo ni haya yafuatayo:

1. Sheikh Thanaullahi alitoka Amrtisar na kwenda Kadiani kwa lengo la kupeana hoja kimjadala na Mirza katika mji wake mwenyewe, lakini Mirza alishindwa kuelekeana nae.

2. Mirza alikataa kufanya mjadala kwa kisingizio kuwa ameahidi hilo, na dharura yake hiyo ni mbaya zaidi kuliko kosa lake la kukataa kufanya mjadala huo. Kwa sababu kuna sababu gani hasa ya kuahidi kutofanya mijadala?!!! Ikiwa kwa hoja ya kuogopea watu na fujo lao, si huyo hapo mtu amekufikia ndani ya nyumba yako, kwa nini unampiga chenga ewe Mirza kama si woga na khofu ni nini?!!!.

3. Mirza anataka kumfanya Sheikh Thanaullahi kama ni Muahmadia mwenye utata wa kupita mara moja ambao unaotafuta jawabu.

4. Mirza anamshurutisha Sheikh Thanaullahi alazimike na kunyamaza kikamilifu mfano wa kiziwi bubu.

5. Mirza anamshurutisha Sheikh Thanaullahi asije akamuandikia zaidi ya upinzani mmoja kwa siku.

Kwa hakika Masihi Mirza ni Masihi mwoga aliyefilisika kihoja na dalili, anaita watu katika mijadala na kuwapa ushindani, kisha yeye ndiye wa mwanzo kukimbia mijadala, kisha tunawakuta walioleweshwa na danganya zake katika safu yake wanasadiki uongo wake vovote atakavowambia.

N.B: ASILI YA MADA HII NI UFAFANUZI WA UST. HANI TAHIRI 24/4/2017

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

بسم الله الرحمن الرحمن الرحيم
Baada ya usomaji wangu baadhi ya vitabu vya Mkadiani Mirza Ghulaamu Ahmad aliyefariki mwaka 1908 Miladi navo ni: 
1. Hakikatu Al-Wahyi.
2. Hamaamtu Al-Bushraa.
3. Khutbatu Al-Ilhaamiyah
4. Izaalatu Khataa.
Kwa ukweli nasema kuwa Mirza alikua ni mwenye kulaghai watu kwa elimu za kisufi na sio jengine lolote, na hakuna shaka katika hili, na kupitia njia hiyo akadai kuwa yeye ni Mahadii Msubiriwa na kuwa yeye ndiye Masihi Muahidiwa na kuwa yeye ndiye Issa bin Marayam A.S, bali sio hapo tu, kwani Mkadiani huyo alifikia kudai kuwa yeye ndiye Mtume Muhammad S.A.W pale aliposema: 
“فنبوتي ورسالتي هي بسبب كوني محمدا وأحمد”
“Basi unabii wangu na utume wangu ni kwa sababu nimekua mimi ndiye Muhammad na Ahmad” [Izaalatu Khataa uk. 4]
La kushangaza ni kukutia kwangu kuwa Mirza anasema katika Izaalatu Khataa huku akizungumzia kuhusu Aya inaosema:
(ولكن رسول الله وخاتم النبيين)
(Lakini ni Mtume wa Allah na khitimisho la Manabii)
Amesema maneno haya: 
“وفي هذه الآية نبوءة لا يعلمها خصومنا، وهي أن الله تعالى قد بين في هذه الآية أن أبواب النبوات بعد النبي صلى الله عليه وسلم قد أغلقت إلى يوم القيامة …. لقد أغلقت كل أبواب النبوة الكاملة لكن بابا واحدا مفتوح وهو باب سيرة الصديقية”
“Na katika Aya hii kuna unabii wasioujua wapinzani wetu, nao ni kuwa Allah mtukufu amebainisha katika Aya hii kuwa milango yote ya unabii imeshatimia, lakini mlango mmoja umefunguliwa nao ni mlango wa sira ya usadikishaji (Siiratu Siddiiqiyah)” [Izaalatu Khataa uk. 3]
Limenisitisha hili neno Usadikishaji (Siddiiqiyah), nikasema katika nafsi yangu: “Hakika neno hili ni la kisufi limeibiwa bila ya shaka yoyote.” 
 
UHAKIKISHO:
Ninasema kuwa Mirza Mkadiani bila ya shaka yoyote alitumia kitabu Khatmu Al-Walaayah cha Msufi Hakiimu Tirmidhi katika kudanganya watu na kuleta ulaghai wake huu, na baya zaidi ni kuwa Mirza hakufahamu makusudio ya Msufi Hakiimu Tirmidhii.
Anasema Msufi Hakiimu Tirmidhii:
“فالمحدث له الحديث والفراسة والالهام والصديقية. والنبي له ذلك كله والتنبؤ. والرسول له ذلك كله والرسالة. ومن دونهم من الأولياء لهم الفراسة والالهام والصديقية”
 “Basi msemeshwa anapata kusemeshwa na uzinduo na ilhamu na usadikishaji (Siddiiqiyah). Na Nabii anapata yote hayo na unabii. Na Mtume anapata yote hayo na utume. Na walio chini ya hapo katika Mawalii wanapata uzinduo na ilhamu na usadikishaji (Siddiiqiyah)” [Hakiimu Tirmidhii uk. 357-358]
Ninasema: Hakika Mdaiunabii Mkadiani Mirza Ghulamu Ahmed alipoona utajo wa unabii upo baada ya usadikishaji (Siddiiqiyah) alifikiria kuwa usadikishaji (Siddiiqiyah) ndio ulio karibu na unabii, basi akaufanya ndio mlango wake, akauita mlango wa sira ya uasdikishaji (Siddiiqiyah) ili alaghai watu wasiojua kwa kudai kuwa huo ndio mlango wa unabii wake, wala Mirza Mkadiani hakufahamu aliyoyasema Msufi Hakiimu Tirmidhi.
Angalieni ndugu zangu vipenzi, daraja za juu za Mawalii kwa mujibu wa Hakimu Tirmidhi ni kama ifuatavo:
1. Utume: Nayo ni maalumu kwa Mitume ya Allah tu, haipati mwengine yoyote asiyekua Mtume.
2. Unabii: Nayo ni maalumu kwa Manabii, na Mitume ni miongoni mwao, haipati mwengine asiyekua wao.
3. Kusemeshwa: Nayo ni maalumu kwa wanaosemeshwa tu na walio juu ya hapo kidaraja katika Manabii na Mitume, na haipati mwengine asiyekua wao.
Basi njia za kupata elimu ya ndani kwa mujibu wa Hakiimu Tirmidhi ni sita tu: Kusemeshwa, uzinduo, ilhamu, usadikishaji, unabii, na utume.
Mitume ni zao zote.
Manabii ni zao zote isipokua utume.
Wasemeshwaji ni zao zote isipokua unabii na utume.
Ama wasiokua katika hao katika Mawalii, hao wataogelea katika uzinduo na ilhamu na usadikishaji (Siddiiqiyah), na ndio akasema: 
“ومن دونهم من الأولياء لهم الفراسة والالهام والصديقية”
“Na walio chini ya hao katika Mawalii yao ni uzinduo na ilhamu na usadikishaji”.
Na hili maana yake Mkadiani hakufahamu aliyoyakusudia Msufi Hakiimu Tirmidhi, basi akajikatalia mwenyewe kupata utume na unabii na usemeshwaji, na maana ya hayo ni kuwa yeye si mtume wala nabii wala msemeshwaji.
Zindukeni enyi muliohadaiwa kwa Uahamdia hakika nyinyi muko katika njia isiyokua njia ya Waumini.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

SUALI KUTOKA KWA MAAHMADIA
Allah mtukufu katika Aya ya 81 ya Suuratu Aala Imraan amechukua ahadi ya Manabii wote ya kuwa watanamuamini na kumnusuru Mtume Msadikishaji, na Aya iwewasifu Manabii hao waliochukua ahadi hiyo kuwa ni wapewa Kitabu na Hekima, na bila shaka wasifu huu upo kwa Mtume Muhammad S.A.W kama ilivyoelezwa katika Aya 113 ya Suuratu Nisaa; kwa hiyo Muhammad S.A.W yumo katika wasifu wa Manabii waliopewa Kitabu na Hekima.
SUALI
Ni Mtume gani msadikishaji wa Mtume Muhammad S.A.W ikiwa si Masihi Al-Mauudi Mirza Ghulamu Ahmed Mkadiani a.s?
JAWABU
Kwanza: Mirza Ghulamu Ahmed Mkadiani hana haki hata ya kupata wasifu wa uchamungu achilia mbali wasifu wa Utume au Unabii au Umahdi au Umasihi; hayo ni kwa sababu ya kudhihiri udanganyifu wake katika funuo zake alizodai kuwa kazipata kutoka kwa Allah mtukufu, kwa mfano funuo zake za kumuoa Muhammadee Beijuum binti wa Ahmed Beg.
Pili: Aya tukufu ya Miithaaqi ya Manabii (81 Aala Imraana) haijasema kuwa Mtume Msadikishaji hatapewa Kitabu na Hekima, bali imetaja wasifu zake kama zifuatazo:
 1. Atakuja baada ya Manabii wote na hili linadhamini kuwa yeye ni Nabii wa Mwisho wao.
 2. Atakuwa ni mwenye kusadikisha Manabii waliopita kabla yake.
 3. Atakua ni Mtume na hili linadhamini kuwa atakuwa na Sheria ya mwisho.
Na sifa zote hizi zipo kwa Mtume wetu Muhammad S.A.W. kwa sababu Allah mtukufu amemsifu Mtume Muhammad S.A.W kuwa ni Khaatamu Nabiyyiina, yaani Mwisho wa Manabii kama ilivo katika Suuratu Al-Ahzaabi Aya ya 40, na Mtume S.A.W amesema akifafanua: ((Na mimi ni Khaatamu Nabiyyiina hakuna Nabii yoyote baada yangu)) [Tirmidhi 2219 Abu Daudi 4252]
 
Ama kuwa kwake S.A.W. ndiye Mtume Msadikishaji, hayo hayana shaka katika Uislamu, pia yameandikwa na Ghulamu Ahmed Mkadiani:-
 1. Allah mtukufu amemsifu Mtume Muhammad S.A.W kwa neno lake: ((Amekuteremshia Kitabu kwa Haki kinachosadikisha yaliyokua kabla yake na aliteremsha Taurati na Injili)) [Aala Imraana 3].
 2. Ama kuwa Nabii Muhammad S.A.W ni Mtume aliyeteuliwa kwa Sheria iliyokalia Sheria za Mitume waliomtangulia hili halina shaka ndani yake na Allah mtukufu amelisema wazi wazi katika Aya ya 48 ya Suuratu Al Maaidah: ((Na amekuteremshia Kitabu kwa haki chenye kusadikisha yaliyokua kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Allah na usifuate mapendwamoyo yao ukaacha haki iliyokujia…)).
 3. Ghulam Ahmed Mkadiani mwenyewe anasema kuwa Mtume Msadikishaji ni Khaatamu Nabiyyina ambaye ni Mtume wetu Muhammad S.A.W. Amesema: “Kutokana na hapo kwa hakika Quraani Tukufu imesema ya kuwa imechukuliwa ahadi kwa kila umma kupitia nabii wake ya kuwa watamuamini KHAATAMA NABIYYINA S.A.W. atakapotumwa na  kuwa watamnusuru.” [Rf. Haqiiqatu Al-Wahyi uk. 162].
Kwa hiyo inabainika wazi wazi kuwa Mtume Msadikishaji aliyetajwa katika Aya ya Miithaqi ni Mtume Muhammad S.A.W, na kuwa yeye ndiye Nabii wa mwisho, ama kuhusu wasifu wa kupewa Kitabu na Hekima huo ni wasifu wa Mitume wote akiwemo Mtume Msadikishaji ambae ni Muhammad S.A.W.
Wabillahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

SUALI KUTOKA KWA MAAHMADIA
Amesema Allah mtukufu 
(مَا كَانَ اللَّهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنْتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ وَلَٰكِنَّ اللَّهَ يَجْتَبِي مِنْ رُسُلِهِ مَنْ يَشَاءُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ ۚ وَإِنْ تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا فَلَكُمْ أَجْرٌ عَظِيمٌ)
[Surat Aal-E-Imran 179]
Pia Allah mtukufu amesema:
(اللَّهُ يَصْطَفِي مِنَ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا وَمِنَ النَّاسِ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ)
Katika Aya hizi tukufu kuna maneno haya
يَجْتَبِي na  يَصْطَفِي
Na zote hizi ni:
 فعل مضارع الفعل المضارع هو الفعل الذي يدل على حدث وقع في زمن يقبل الحال والاستقبال. ولا بد لكل فعل من فاعل أكان ظاهرا أم مستترا.
 
Kwa hiyo neno la mwanzo maana yake halisi ni anachagua , atachagua au huchagua
Na Neno la pili maana yake ni anachagua na atachagua na hakusema:
الله اصطفى من الملائكة رسلا ومن الناس
Jee hayo hayaoneshi wazi wazi kuwa uteuzi wa Mitume utaendelea baada ya Muhammad S.A.W.
 
JAWABU:
Allah mtukufu ameijaalia Quraani kuwa ya kiarabu, na kwa Waarabu iliteremshwa kuanzia Mtume wetu Muhammad S.A.W na Masahaba waliokua pamoja nae na Wanavyuoni wakubwa waliopokezana mafundisho ya Dini hii kizazi kwa kizazi mpaka hivi leo, na hakuna katika hao wote waliosema kuwa Aya hizo mbili ni dalili ya kuendelea kutumwa Mitume baada ya Mtume Muhammad S.A.W; kwa sababu wote walijua maana ya neno la Allah mtukufu pale aliposema:
((مَا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِنْ رِجَالِكُمْ وَلَكِنْ رَسُولَ اللَّهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ))
((Hakua Muhammad baba wa yoyote katika wanaume wenu lakini ni Mtume wa Allah na mwisho wa Manabii,))
[Al-Ahzaabu 40]
 
Pia walifahamu pale Mtume S.A.W alipobainisha kwa neno lake:

((أَنَا خَاتَمُ النَّبِيِّينَ ، لَا نَبِيَّ بَعْدِي))

((Mimi ni mwisho wa Manabii hakuna nabii yoyote baada yangu))
 
Na alipoeleza kwa njia ya mfano kuwa: ((Allah mtukufu amelitimiza jengo la Manabii na kubakia tufali moja tu ambalo kila anayeingia katika jingo hilo husema lau sehemu hii lilitimizwa tufali lake, basi mimi ndiye hilo tufali la mwisho))
 
Ama kuhusu Aya tukufu ambazo Maahamadia wamekuja nazo tunawambia kuwa hakuna ndani yake dalili ya madai yao.
 
Aya ya mwanzo inasema:
((Haiwi kwa Allah kuwaacha Waumini katika hali muliyonayo mpaka apambanue wabaya na wema, na haiwi kwa Allah kukujulisheni yaliyofichika, lakini Allah huchagua katika Mitume yake amtakae, basi aminini Allah na Mitume yake, na mukiamini na mukamcha mutapata ujira mkuu)) [Aala Imaraana 179]
Na Aya ya pili inasema:
((Allah huteua wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa Watu. Hakika Allah ni mzikivu muoni)) [Al-Hajji 75]
 
Tunawambia Maahmadia hata Tarjama yao ya Quraani katika maneno hayo yote mawili wameyapa maana ya ((huchagua)) kwa sababu yanafidisha hali iliyopo wakati wa uteremsho; kwani uhakika wake ni kumueleza Nabii wa mwisho ambae ni Mtume Msadikishaji Muhammad S.A.W, basi inafahamika kuwa maana kusudiwa ni kuwa Allah mtukufu huchagua katika Mitume yake amtakae kwa kumfunulia mambo ya ghaibu naye amemchagua Muhammad miongoni mwao na kumjaalia kuwa Nabii wa mwisho wa kumfungulia mambo ya Ghaibu, vile vile Allah mtukufu huchagua Mitume katika safu za Malaika na Watu basi amemchagua Muhammad na kumfanya kuwa Khitimisho la Manabii basi hakuna nabii yoyote baada yake, na amemchagua Jibrilu A.S kwa amana ya Wahayi wake. 
 
Tunawambia Maahmadia hata Mirza Ghulamu Ahmed Mkadiani analijua hilo kuwa Muhammad S.A.W ndiye Mtume wa Mwisho amesema kuhusu Mitume A.S:
“أولهم آدم وآخرهم أحمد فمبارك من استطاع أن يرى الأخير، إن الأنبياء كلهم يملكون فطرة منيرة ولكن أحمد صلى الله عليه وسلم أكثرهم نورا”
“Wa mwanzo wao ni Adamu na wa mwisho wao ni Ahmad, basi amebarikiwa aliyeweza kumuona wa Mwisho, hakika Manabii wote wanamiliki fitra moja, lakini Ahmad S.A.W ndiye mwingi wao kwa nuru”. [Al Baraahinu Al-Ahmadiyah 1/23]
 
Pia amesema kuhusu Aya tukufu ya Khitimisho la Manabii:
“Na ikiwa hapa itasemwa kuwa Bwana wetu Muhammad S.A.W ndiye Khaatamu Nabiyiina (Mwisho wa Manabii), basi vipi iwezekane kuja Nabii baada yake? Basi jawabu yake: Katika yasiyokua na shaka ndani yake ni ukahika wa kuwa hatakuja Nabii yoyote si wa zamani wala mpya kwa njia wanayoiwaza watu kuhusu uteremsho wa Issa A.S katika zama za mwisho; kwani wao wanaitakidi kuwa yeye atakua Nabii, bali wanaitakidi kuwa atafikiwa na ufunuo wa unabii kwa muda wa miaka arubaini, nao ni muda mrefu zaidi kuliko muda wa ufunuo wa Bwana wetu Muhammad S.A.W. itkadi hiyo bila shaka ni kosa. Na hakika Aya ((Lakini ni Mtume wa Allah na KHAATAMU NABIYIINA (MWISHO WA MANABII))) na Hadithi: ((Hakuna Nabii baada yangu)) mawili hayo yanashuhudia ushahidi wa wazi juu ya ubatilifu wa itikadi hiyo. Hakika mimi ninapinga vikali sana mfano wa itikadi hizo, na ninaiamini Imani ya kweli na kamilifu Aya hii inayosema ((Lakini ni Mtume wa Allah na KHAATAMU NABIYIINA)). Na katika Aya hii kuna unabii wasioujua wapinzani wetu, nao ni kuwa Allah mtukufu amebainisha katika Aya hii kuwa milango yote ya Unabii baada ya Nabii S.A.W imefungwa mpaka siku ya Kiama, kwa hiyo hivi sasa hakuna nafasi kwa Muhindusi yoyote wala Myahudi yoyote wala Mkiristo yoyote wala Muislamu yoyote wa kawaida ya kujithibitishia nafsi yake neno la Unabii. Kwa hakika imeshafungwa milango yote ya unabii.” [Izaalatu Khataa uk. 2-3].
 
Kwa hiyo ni wazi kuwa hata Mirza Ghulamu Ahmed Mkadiani alikua akiitakidi kuwa Mtume Muhammad S.A.W ndiye Nabii wa mwisho kupitia Aya tukufu ya Suuratu Al-Ahzaabi ya khitimisho la manabii pia kupitia Hadithi ya Mtume S.A.W: “Hakuna nabii yoyote baada yangu.”.
Ama kuhusu madai Mirza Ghulaamu Ahmed Mkadiani kuwa katika Aya hiyo (Wakhaatamu Nabiyiina) kuna malango mmoja wa Unabii haujafungwa, bila shaka hayo ni madai hewa tutayaeleza mara ijayo kwa idhini ya Allah mtukufu.  
Wabillahi Taufiiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

MKASA WA MUHAMMADEE BEGAM KWA KALAMU YA MIRZA GHULAMU AHMED MKADIANI (10)
UFAFANUZI MDOGO:

Mirza Ghulamu Ahmed Mkadiani alipata funuo ya kumuoa Binti mkubwa wa Ahmed Beg aitwae Muhammadee Begam, alipeleka posa mnamo mwaka 1887 na kuahidi kutoa mali nyingi sana, lakini posa yake haikufanikiwa, basi hapo akapokea funuo maalumu kuhusu Baba na Binti na Mume wa Binti iwapo atakuwa mwengine asiyekua yeye akasema: ((Hakika Allah amenifunulia ya kuwa kumuozesha kwako huyu Binti mume mwengine hakutabarikiwa kwako wala kwake, na kuwa utapatwa na misiba mingi na mwisho wa misiba hiyo ni kifo chako ambacho hakitavuuka miaka mitatu tokea siku ya kuolewa huyo Binti, bali kifo chako ni karibu, ama mume wa Binti atakayemuoa yeye atakufa ndani ya miaka miwili na nusu tokea siku ya ndoa))

Binti huyu aliolewa katika mwezi wa 4 mwaka 1892.

Kwa hiyo ili Mirza Ghulamu Ahmed Mkadiani awe mkweli katika funuo yake ilibidi Mume wa Binti huyu asimalize mwezi wa 10 wa mwaka 1894 ila awe ameshakufa, lakini mambo hayakuwa hivo; kwani Mume hakufa katika muda ulioainishwa katika funuo ya Ghulamu Ahmed Mkadiani.

Sasa endelea kusoma nakala kutoka kwa Ust. Hani Tahir.

MKASA HUU NI KUTOKA KITABU (MAKTOOB AHMAD) MWANZONI MWA MWAKA 1897.

Anasema Mirza Ghulamu Ahmed Mkadiani kwa lugha ya kiarabu.

Trj. ((Kisha Wanavyuoni wamenimiminia matusi na wameniumiza kwa lawama katika suala la Mkwe wa Ahmed (Mume wa Muhammadee Begam), na wamesema: “Hakika yeye hakufa katika wakati.”

Ama jawabu: Ujuwe kuwa ilhamu hii ilikusanya vifungu viwili, kifungu cha kifo cha Ahmed (Bamkwe)… na kifungu cha pili kinacho kamatana na Mkwe wake na kifo chake, basi kuchelewa kifo chake kusikuchome katika kifua chako.

Hakika Allah amenikhutubia kuhusu jamaa zangu wa karibu wenye kufanya uadui, basi amesema: ((Wamekadhibisha ishara zangu na wamekua wenye kuzifanyia shere, basi Allah atakutosheleza hao, na atamrejesha kwako, hakuna kubadilika kwa maneno ya Allah, hakika Mola wako ni mwenye kufanya anayotaka)).

Basi ameashiria katika tamko ((Basi Allah atakutosheleza hao)), ya kuwa Binti wa Ahmed Beg atarejeshwa tu kwangu baada ya kuangamia wazuiaji wote….

Kisha mimi sikukwambieni kuwa jambo hili limetimia kwa kiwango hicho… bali uhakika ni kuwa jambo hili limesimama katika hali yake, wala hakuna yoyote atakaye lirejesha kwa ujanja wake, basi jambo hili limeshapitishwa na Mola Mkuu, na utafika wakati wake kwa fadhila za Allah mkarimu. Naapa kwa yule aliyemtuma Muhammad mteuliwa na kumjaalia kuwa mbora wa Mitume na mbora wa waj, hakika hii ni haki na karibuni utaona. Hakika mimi ninaifanya habari hii kuwa ni kipimo cha ukweli wangu na uongo wangu, na mimi sijasema isipokua baada ya kapata ufunuo kutoka kwa Mola wangu. Hakika Jamaa zangu wa karibu watarejea kwa mara nyengine katika uharibifu, na wataongezeka katika ubaya na ukaidi, basi siku hiyo litateremka jambo lililokadiriwa kutoka kwa Mola wa waja, hakuna wa kurejesha kwa aliyopitisha, wala hakuna wa kuzuia kwa aliyotoa. Na hakika mimi ninawaona kuwa wao wameinamia katika mwendo wao wa mwanzo, na zimekua ngumu nyoyo zao kama ilivyo kawaida ya naukaa, wamesahau siku za fazaa na wamerejea katika kukadhibisha na kuvuka mipaka, basi itateremka amri ya Allah atakapoona kuwa wao ni wenye kuongezeka, na hakuwa yeye wa kuadhibu watu hali ya kuwa wanaogopa…

UFUPISHO WA ANDIKO:

1. Neno ((Allah Atakutosheleza wao) linatilia mkazo pitisho la ndoa yake baada ya kufa wazuiaji wote wa ndoa hiyo.
Basi ndoa ndio lengo hasa, na kuangamia kwao ni kwa sababu ya kukataa kwao kumuozesha, na baada ya kuangamia kwao wote atamuoa huyo mwanamke.

2. Mirza Ghulamu Ahmed ameifanya ndoa hii kuwa ni kipimo cha kujulikana kuwa yeye ni mkweli au muongo, na hakulisema hilo ila baada ya kupata ufunuo kutoka kwa Mola wake.

3. Familia ya Muhammadee Begam imerejea katika kukadhibisha na kupindukia mipaka, hili ikiwa kweli waliogopa kwa kufa baba wa Muhammadee kama alivodai Mirza. Na inalazimika kutoka na hili kufa mume wa Muhammadee mara moja, kwa sababu kifo chake kimecheleweshwa kwa sababu ya kuogopa kwake na kuogopa kwao kama alivodai Mirza, lakini kuogopa kwao huko kumeondoka sasa, na juu ya yote hayo mume wa Binti hakufa, wala Binti huyo hakurejeshwa kwa Mirza Ghulamu Ahmed kwa kumuoa.

Ifahamike kuwa funuo ya kifo cha Mume wa Muhammadee Begam muda wake unamalizika katika mwezi wa 10 wa mwaka 1894.

Kutokana na hayo utakua muda wa funuo hiyo umeshapita kwa miaka miwili na miezi miwili wakati wa kuandikwa maneno haya.

Hani Tahir 8/9/2017

Tr. Abu Hamed Hafidh Al-Sawafi 8/9/2017.

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

24. KHAATAMU NABIYYIINA
Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Takriban zaidi ya siku tatu hivi sasa Maahmadia wametujia na suala la maana ya neno KHAATAMU NABIYYIINA lililokuja katika Suuratu Al-Ahzaabi Aya ya 40, nao kama kawaida yao wamekuja na maneno mengi ambayo lengo lake ni kufikia katika maana wanayoitaka wao ya kudai kuwa makusudio yake ni MBORA WA MANBII, na sio MWISHO WA MANABII.

Na sisi upande wetu tumewataka Maahmadia wathibitishe masimamo wao huo kupitia maelezo ya muasisi wa Dini yao ya Kiahmadia Ghulamu Ahmed Mkadiani ambae kwa mujibu wa Itikadi yao -Mkadiani huyo- ni Mtume na Nabii na Masihi Mauudi, nasi tumewaambia wazi wazi kuwa kwenda kinyume na yeye katika ufahamu wa Aya husika au nyengineo ni kuhakikisha upinzani baina yao na Mkadiani wao huyo, na kupelekea hilo kuingia mmoja wao -ima wao au yeye- au wote wawili katika hukumu aliyoisema Ghulamu Ahmed Mkadiani katika kitabu chake NUZUULU AL-MASIIHI uk. 35:

“وإن استنتاج معنى مخالفا للقرآن الكريم إنما هو التحريف والإلحاد والدجل بعينه”

“Na kwa hakika kujiletea maana yoyote iliyo kinyume na Quraani Tukufu huko kutakua ni upotoshaji na upingajimungu (Il-haadi) na udajali wenyewe”

Tumewambia Maahmadia kuwa Allah mtukufu ametuambia kwenye Kitabu chake:

(وَأَنْزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ)

“Na tumeteremsha kwako ukumbusho (Quraani) ili ubainishie kwa watu yale yaliyoteremshwa kwao..” [Nahl 44]

Kwa hiyo ni wajibu wetu kukubali bayana aliyoitoa Mtume wetu S.A.W. kuhusu makusudio ya maneno KHAATAMA NABIYYIINA na sio kukaidika mbele yake S.A.W.. Na yeye S.A.W. amesema wazi wazi:

“وإنه سيكون من أمتي كذابون ثلاثون، كلهم يزعم أنه نبي، وأنا خاتم النبيين، ولا نبي بعدي”

“Hakika watakuwepo katika umati wangu waongo thalathini kila mmoja wao atadai kuwa yeye ni nabii, na mimi ndiye KHAATAMU NABIYYIINA HAKUNA NABII YOYOTE BAADA YANGU” [Tirmidhi 2219 Abu Daudi 4252 Ahmed bin Hambal 22395]

Kwa hiyo Mtume S.A.W. ambae ameteremshiwa Quraani tukufu ameshabainisha kuwa maana ya KHAATAMU NABIYYIINA ni “Hakuna nabii yoyote baada yake S.A.W.” tena bayana yake hii imedhamini hukumu ya kuwa kila atakayedai unabii baada yake S.A.W. kuwa huyo ni muongo ni lazima kujitenga naye, na Waislamu wa uhakika hawajatafautiana katika hili tokea zama za Masahaba -Allah awaridhie- mpaka hivi leo na mpaka siku ya Kiama.

Sasa enyi Maahmadia tuleteeni neno la huyu Mkadiani wenu kuhusu maana ya KHAATAMU NABIYYIINA ili tulione.

Jee! Mumechukua kutoka kwake au laa?

Tunajua kuwa neno hili ni zito sana kwao, na kwa sababu hiyo wakapiga chenga na sarakasi, na badala yake wakatuletea neno la Msufi Hakiimu Tirmidhi: “Wale wote wenye kusema Khaatama Nabiyyiina ni mwisho wa Manabii hao ni wehu na wajinga….” masikini mbali ya kuwa Hakiimu Tirmidhi ameeleza wazi kuwa Muhuri wa Unabii unalazimisha kuupata Nabii wa Mwisho ambae ni Mtume Muhammad S.A.W. kama ilivyo wazi katika Kitabu chake Khatmu Al Auliyaa uk. 436:

كما أن محمدا صلى الله عليه وسلم آخر الأنبياء فأعطي ختم النبوة فهو حجة الله تعالى على جميع الأنبياء

“Kama ilivyokua Muhammad S.A.W. ndiye mwisho wa Manabii ndio akapewa muhuri wa Unbii basi yeye ndiye hoja ya Allah amtukufu kwa Manabii wote”

Maahmadia hawajijui kumbe wanamponda kwa sifa hizo za wehu na ujinga huyo Ghulamu Ahmed Mkadiani wao; kwani Khaatama Nabiyyiina kwa mujibu wa maandiko yake haina maana isipokua ni mwisho wa Manabii tu kama tutakavoona in shaa Allah.

Kutokana na hapo tukaona ni wajibu wetu kuwasaidia Maahmadia kwa kuwaletea neno la Ghulamu Ahmed Mkadiani kuhusiana na Aya hii tukufu.

Asemema Ghulamu Ahmed Mkadiani katika Kitabu chake Hamaamatu Al-Bushraa uk. 49-50:

أما ذكر نزول عيسى بن مريم فما كان لمؤمن أن يحمل هذا الاسم المذكور في الأحاديث على ظاهر معناه لأنه يخالف قول الله عز وجل ((ما كان محمد أبا أحد من رجالكم ولكن رسول الله وخاتم النبيين)) ألا تعلم أن الرب الرحيم المتفضل سمى نبينا صلى الله عليه وسلم خاتم الأنبياء بغير استثناء وفسره نبينا في قوله لا نبي بعدي ببيان واضح للطالبين؟

“Ama utajo wa kushuka Issa mwana wa Mariyam, haikuwa kwa muumini yoyote kulichukua jina hilo lililotajwa katika hadithi nyingi kwa udhahiri wa maana yake; kwa sababu kufanya hivo ni kupingana na neno la Allah mtukufu: ((Hakua Muhammad baba wa yoyote katika wanaume wenu lakini ni Mtume wa Allah na KHAATAMA NABIYYIINA)), Hivi hujui kuwa Mola Mrehemevu Mneemeshaji amemwita Nabii wetu S.A.W. KHAATAMA NABIYYIINA bila kuvuliwa nabii yoyoye katika hukumu hiyo, nalo kalifasiri Nabii wetu katika neno lake: Hakuna Nabii yoyote baada yangu kwa ubainisho ulio wazi kwa wenye kutafuta ukweli?”

Bila shaka inaonekana wazi hapo kuwa Ghulamu Ahmed Mkadiani amepinga itikadi ya kuteremka Issa mwana wa Mariam A.S. kwa kuona kuwa itikadi hiyo inapingana na umwisho wa unabii kwa Mtume wetu Muhammad S.A.W. kwa maana hiyo alilifahamu neno KHAATAMA NABIYYIINA kuwa maana yake ni mwisho wa Manabii ambae hakuna nabii yoyote baada yake S.A.W.

Anaendelea Ghulamu Ahmed Mkadiani:

ولو جوزنا ظهور نبي بعد نبينا صلى الله عليه وسلم لجوزنا انفتاح باب وحي النبوة بعد تغليقها، وهذا خلف كما لا يخفى على المسلمين. وكيف يجيء نبي بعد رسولنا صلى الله عليه وسلم وقد انقطع الوحي بعد وفاته وختم الله به النبيين؟

“Na lau tutakubalisha kudhihiri nabii yoyote baada ya Nabii wetu S.A.W. basi tutakua tumekubalisha kufunguka mlango wa ufunuo wa unabii baada ya kufungwa kwake, na hilo litakua ni kuvunja hukumu isiyofichika mbele ya Waislamu. Na vipi aje nabii baada ya Mtume wetu S.A.W. hali ya kuwa wahyi umeshakatika baada ya kufa kwake, na kwa yeye huyo (S.A.W) Allah ameshatimiza Manabii?”

Ghulamu Ahmed Mkadiani akaendelea kusema akifafanua hasa kuwa KHAATAMA NABIYYIINA maana yake ni Mwisho wa Manabii:

أنعتقد بأن عيسى الذي أنزل عليه الإنجيل هو خاتم الأنبياء لا رسولنا؟

“Hivi sisi tuitakidi kuwa Issa ambaye ameteremshiwa Injili ndiye mwisho wa Manabii na sio Mtume wetu?”

Pia Ghulamu Ahmed Mkadiani katika kitabu chake Khutbatu Ilhaamiyah ambacho kwa mujibu wa mafundisho ya Dini yao ya Kiahmadia ni Ufunuo wa Allah na umethibitishwa katika Tadhkirah anasema:

أتزعمون أنه يرسل عيسى إلى الدنيا ويوحي إليه إلى أربعين سنة ويجعله خاتم الأنبياء وينسى قوله ((ولكن رسول الله وخاتم النبيين))؟ سبحانه عما تصفون

“Hivi munadai kuwa yeye (Allah) atamtuma Issa Duniani na atamfunulia kwa kipindi cha miaka 40 na atamfanya kuwa ndiye KHAATAMA (MWISHO) WA MANABII, na atasahau neno lake ((Lakini ni Mtume wa Allah na KHAATAMA (MWISHO) WA MANABII))? Ametakasika na hayo munayomsifu kwayo” [Rf. Khutbatu Ilhaamiyah uk. 89-90]

inafahamika vizuri sana kuwa hakuna Muislamu hata mmoja anayeitakidi kuwa Nabii Issa alaihi salaamu ni mbora zaidi kuliko Nabii wetu Muhammad alaihi salaamu, kama ilivyokua hakuna Muislamu hata mmoja aliyesema kuwa Mtume Issa A.S.W. akija atakua ndiye KHAATAMA NABIYYIINA, kutokana na hapo inabatilika kauli hiyo kuwa ndio kusudio la Mkadiani wao, na kudhihirika wazi wazi kuwa kusudio la Mkadiani ni KHAATAMA kwa maana ya MWISHO tu.

Pia imekuja katika Kitabu hicho hicho uk. 27 akimzungumzia Mtume Issa A.S.W. kwa kusema:

بعث الله رسوله عيسى بن مريم فيهم وجعله خاتم أنبيائهم

Allah kampeleka Mtume wake Issa bin Maryama kwao (yaani Bani Israaila) na akamfanya kuwa ndio KHAATAMA wa Manabii wao.

Ni wazi kuwa kusudio la KHAATAMA katika maneno ya Mkadiani wao hayo ni mwisho na haiwezekani kuwa maana yake ni mbora kwa sababu Mtume Mussa A.S.W. ndiye mbora wa Manabii wa Bani Israaila.

Na kama Muahmadia atapiga sarakasi zake na kudai kuwa neno ni KHAATIMA na sio KHAATAMA tunamwambia kuwa pia katika Aya tukufu katika visomo kumi kimoja tu cha Hafsi ndio KHAATAMA ama tisa vilivyobakia ni KHAATIMA.

Wassalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

OPEN ARTICLE

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

25. MUSTAKBALI WA DINI YA KIAHMADIA
Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh

Limetufikia suali kuhusiana na mustakbali wa Uahmadia jee unaweza ukachua nafasi ya kuwa na wafuasi wengi zaidi kuliko Waislamu duaniani katika karne zijazo?

Tunawambia kuwa Uahmadia hauna mustakbali katika safu za Waislamu kwa hiyo ni muhali kufikia hali ya kuwa ndio marejeo ya Uislamu duaniani, hayo ni kwa sababu tatu kuu.

1. Uislamu ni Dini aliyoichagulia Allah lugha ya Kiarabu fasaha kuwa ndiyo lugha yake, na uhakika wa maandiko ya muasisi wa Uahmadia Ghulamu Ahmed Mkadiani (1840-1908) katika lugha ya Kiarabu ni fedheha kubwa mbele ya wenye lugha hii tukufu; kwani maandiko yake ya Kiarabu yamemuanika kuwa yeye ni mjinga wa lugha ya Quraani, na uajemi wake wa Kiurdu katika maandiko yake ya Kiarabu uko wazi wazi hauna kificho chochote, pia wizi wake wa maandiko ya Al-Hariri na Al-Hamadhani uko wazi, na nususi za Kiurdu si tegemeo katika Sheria ya Kiislamu.

2. Fedheha nyingi za kitabia na kuongopea (uongoo) zimejaa katika maandiko yake; kwa mfano funuo zake ya kumuoa Binti Muhammadee Begam kabla ya kuolewa na baada ya kuwa mke wa watu, na funuo zake kuhusu kifo cha Kasisi Aat`ham, na hukumu yake ya mwisho iliyodhamini radi ya maapizo aliyoitoa kwa Sheikh Thanaaullahi kisha ikampiga mwenyewe, na mubaahala wake na Shekh Abdluhaqi Al-Ghaznawi, Mashekhe ambao waliendelea kuishi baada ya Ghulamu Ahmed Mkadiani, bila kusahau mkasa wake na Dr. Abdulhakiim Khaan.

3. Kupingana Uahmadia na Muasisi wao Ghulamu Ahmed Mkadiani katika masuala mengi sana ambayo wao wanawatia doa kwayo Waislamu, kiasi cha kuwa Muahmadia akitajiwa tu maandiko ya Ghulamu Ahmed Mkadiani anapiga chenga na sarakasi za ajabu.

Na juu ya yote hayo Jumuia yenyewe unadanganya sana, hususan katika idadi ya Maahmadia Duniani, katika mwaka 2004 ilitangaza kuwa Idadi ya Ahmadia duniani ni milioni mia nee 400,000,000 baada ya miaka 13 msemaji wao anatangaza kuwa Idadi yao bidhii malaayiin yaani baina ya milioni 3 mpaka milioni 7 hawavuuki hapo, na wazoefu wa Uahamadia wanawesema katika Idadi hiyo pia ni waongo.

Kutokana na hapo ni yakini isiyokua na shaka yoyote kuwa hakuna Mustakbali wa Uahmadia ulimwenguni isipokua wa kumalizika kwake tu na kufifia kila mawasiliano yanapoenea zaidi duani, kwani fedheha zake na za muasisi wake ni nyingi mno, nazo ni alama tosha kuwa Ghulamu Ahmed Mkadiani alikua Dajali miongoni mwa Madajali 30 alioeleza Mtume wetu Muhammad S.A.W. kutokeza kwao kabla ya kusimama Kiama, na kuwa kila mmoja wao atadai kuwa ni Nabii, Allah atuepushe na shari zao.

Wabillahi Taufiqi.

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

26. MIRZA NA DR. ABDULHAKIIM NO.2
KISA CHA DR. ABDULHAKIM KINAVUNJA UTI WA MONGO WA MIRZA KULIKO KINAVOUVUNJA KISA CHA THANAAULLAHI ALAMRATSARI

(SEHEMU YA PILI)

Nilieleza katika sehemu ya kwanza kuwa Mirza alitangaza ilani tarehe 16/08/1906 na ndani yake alisisitiza ubatilifu wa utabiri wa Abdulhakiim ulioeleza kuwa Mirza atakufa ndani ya kipindi cha miaka mitatu, basi Mirza alidai kuwa Allah mtukufu amempatia bishara ya kuwa: “Aliye muongo ndiye atakayekufa mwanzo.”

Kisha baada ya hapo Dr. Abdulhakiim aliandika katika ilani yake ya tarehe 01/07/1907:

“Mirza atatupwa katika shimo la Jahannamu kwa adhabu ya kifo ndani ya kipindi cha miezi 14 kuanzia leo.” [Rj. Tadhkirah nakala kutoka Ilani ya Haki na Kutimia hoja uk. 6].

Basi Mirza alijibu ilani hiyo ya Dr. Abdulhakiim kupitia Ilani yake ya tarehe 5/11/1907, yaani kabla ya kifo chake kwa nusu mwaka (Miezi 6) alisema ndani yake:

“Inalazimika kwa wafuasi wa jamaa yetu waitangaze funuo hii kwa kasi kubwa sana, na waichapishe wao wenyewe, na waitundike katika sehemu iliyo wazi ndani ya nyumba zao; ili iwe ni kumbukumbu.

Allah amenifunulia: “Mwambie adui yako ya kuwa Allah atakuchukua…” kisha Allah mtukufu akasema: “Nitarefusha umri wako, yaani nitathibitisha uongo wa Maadui wenye kusema kuwa umri wako haujabakia isipokua miezi 14 kuanzia July 1907 au yale waliyotabiri maadui wengine, nitathibitisha uongo wao wote na nitarefusha umri wako ili ijulikane ya kuwa hakika yangu mimi ndiye Allah muweza wa kila kitu.”

Funuo hii ni kuu, kwani Allah mtukufu amebainisha ndani yake ushindi wangu na kutokomezwa maadui, na utukufu wangu na udhalilifu wa maadui, na kustawi kwangu na kufifia kwa maadui, Allah mtukufu ameahidi makasiriko na adhabu kwa maadui, na ameeleza kuhusu mimi ya kuwa: “Jina lako litatukuzwa ulimwenguni na ushindi utakua ndio rafiki yako na ufunguzi, na kwamba yule adui mwenye kutamani kifo changu (anamkusudia Abdulhakiim) watateketezwa mbele ya macho yangu na kuangamizwa mfano wa watu wa tembo. Na Allah atadhihiri kwa makasiriko na atadhihirisha udhalilifu na mporomoko wa wale wasiojizuia na uongo na kujipa ushujaa nae atanidhalilishia ulimwengu na ataeneza jina langu ulimwenguni kwa utukufu na ukarimu.

Basi wafuasi wa jamaa yangu waangalie utimilivu wa funuo hii, na wadhihirishe ruwaza njema kwa uchamungu na utoharifu.

Vile vile kuna funuo nyengine iliyoshikamana na funuo hii ya kuwa tauni kumbakumba (janga ya maradhi ya maafa) imekaribia kuenea katika nchi hii na nchi nyengine, nayo haipati mfano wake kabla yake, na itawafanya watu kama wendawazimu, lakini mimi sijui ikiwa itaenea ndani ya mwaka huu au ndani ya mwaka ujao.” [Rf. Ilani ya 5/11/1907].

Baada ya ilani hiyo ya Mirza yenye wasia mzito sana kwa wafuasi wake, Dr. Abdulhakiim alitangaza ilani yake ya tarehe 16/2/1908 na akasema:

“Hakika Mirza ataagamia ndani ya kipindi mwisho wake ni tarehe 4/8/1908.” [Rf. Tadhkirah nakala kutoka Ilani ya Haki na kutimia hoja uk. 6].

Hapo Mirza akaandika kiambatanishi cha ilani hiyo kabla ya wiki chake za kifo chake akasema:

“Ama hivi sasa hakika amekuja juu adui mwengine jina lake ni Abdulhakiim Khaan, nae anadai huku akiniashiria mimi, ya kuwa nifakufa katika kipindi cha uhai wake (nitakufa kabla yake), sitavuuka tarehe 4/8/1908, na hilo litakua ni ishara ya ukweli wake.

Mtu huyu anadai kupata ilhaamu, nae ananiona mimi kuwa ni Dajali, Kafiri, Muongo sana…

hakika mtu huyu ameeleza utabiri unaonihusu mimi ya kuwa nitakufa ndani ya kipindi cha uhai wake, na muhula ni mpaka tarehe 4/8/1908, lakini Allah mtukufu amenieleza mkabala wa tabiri yake hiyo ya kuwa yeye huyo atachukuliwa kwa adhabu na kuwa Allah mtukufu atamuangamiza na mimi nitaokolewa na shari yake.

Basi jambo hilo limo mkononi mwa Allah mtukufu, wala hakuna shaka kuwa hilo ni sahihi kabisa, ya kuwa Allah atampa ushindi yule aliye mkweli katika uoni wake. [Rf. Yanbuu Almaarifa Khazaainu Rohaaniyah jalada la 23 ukurasa 337]

Na Mirza kabla ya kufa kwake kwa siku mbili aliandika akiashiria tabiri ya Abdulhakiim:

“Allah mtukufu atamuanika yule hasa aliye mkweli.” [Rf. Badr Jalada 7 Idadi 19-20 la terehe 24/5/1908 uk. 7]

Udanganyifu pekee alioweza kuufanya mwana wa Mirza katika mkasa huu ni neno lake: “Hakika Abdulhakiim alitangaza ilani katika tarehe 8/5/1908 akisema: (Mirza ataangamia kwa maradhi ya kuangamiza ndani ya tarehe 4/8/1908) kwa kugeuza kwake herufi yenye maana ya ndani ya muhula (mpaka) na kufanya badala yake herufi ya siku mahususi (ndani).

Na akasema: Allah mtukufu alipitisha kumuadhibu Abdulhakiim basi akapitisha kuwa Mirza afe ndani ya siku ya tarehe 26/5/1908 ili utabiri wa Abdulhakiim usitimie ambao ulisema kuwa takufa ndani ya siku ya tarehe 4/8/1908.

Kama kwamba Allah hawezi kuurefusha umri wa Mirza zaidi ya tarehe 4/8/1908 ili ushangiliwe ushindi na kufeli utabiri wa Abdulhakiim?

Au kama kwamba Allah hawezi kumuhukumu Mirza baada ya tarehe 4/8/1908 basi ikifika tu siku hiyo ndio atakufa mara moja, au abakie milele, basi kwa kuogopea uwezekano huu na ule Allah akapitisha kumuua Mirza kabla.”

Jee! Mumeshawahi kuona walio doda na waongo kuliko watu hawa?!

Hakika visa vya Mirza sio kuwa vinathibitisha uongo wake tu, bali vilevile vinathibitisha uongo wa wafuasi wake baada yake.

Hani Tahir 25/07/2017

Tarjama: Abu Hamed Hafidh Al-Sawafi

HAKI KWA DALILI.

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

27. MIRZA NA PADRI AT`HAM
Bismillahi walhamdulillahi wasalaatu wasalaamu alaa rasuulillahi Muhammad

Wa baad. Asalamu alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh.

Mungu hamfichi mnafiki, ni msemo tunaujua sana katika ulimi wa kiswahili, kwa kweli hiyo ndiyo hali ya Mirza Ghulam Ahmed Mkadiani ambae anaaminiwa na Maahmadia kuwa ni mteuliwa wa Allah kwa cheo cha unabii na utume na umasihi wa ahadi na umahdi… mpaka hapa neno letu linabakia kuwa ni tuhuma inayohitaji dalili za kulithibitisha.

Jee! Tunayo dalili yoyote katika hili?

Kwa kweli dalili za kuthibitisha uongo wa Ghulamu Ahmed Mkadiani ni nyingi sana; kwani uhakika unabakia kuwa kila funuo aliyodai Mkadiani huyu kuipata ilikadhibishwa na uhakika; kwani ilikua ni kinyumenyume na madai yake, na sisi hapa tutachukua moja ya funuo zake ambazo kazisajili kwa mkono wake mwenyewe na kubakia katika maandiko yake na kusambazwa na jumuia yake kupitia vyanzo vyao rasmi, ukiwa ni ushahidi tosha wa kuwa yeye ni muongo na mwenye kustahiki aina zote ya udhalilifu, funuo hiyo si nyengine ila ni ile ya kifo cha Padri Abdullahi At`ham ndani ya miezi kumi na tano, ifahamike kuwa Padri huyu alifanya mjadala na Mkadiani kwa muda wa siku kumi na tano, na yaliyojiri katika mjadala huo aliyasajili Mkadiani katika kitabu hicho.

Vizuri kuinakili funuo yenyewe kikamilifu kama ilivo katika sahifa tatu za mwisho za kitabu cha Mkadiani alichokiita Alharbu Almuqaddasah (Vita Vitakatifu).

Amesema Ghulamu Ahmed Mkadiani:

“Kwa vile Bwana At`ham anapinga miujiza ya Qurani tukufu kwa makusudi, na anapinga funuo zake pia, nami nimefanyiwa shere katika mkutano huu kwa kuletwa wagonjwa watatu na kusemwa: “ikiwa Uislamu ni dini ya kweli na wewe ni mwenye kupata ilhamu katika uhakika basi waponyeshe wagonjwa hawa watatu”, pamoja na kuwa mimi sijadai kabisa kuwa ni muweza wa kila kitu. Basi matakwa hayo hayakua kwa mujibu wa maelezo ya Qurani tukufu, bali yamehisabiwa hayo kuwa ni alama ya Imani ya Manasara katika Injili ya kuwa wao iwapo watakua waumini wakweli wataponyesha vilema na vipofu na viziwi bila shaka yoyote.

Lakini mimi nilendelea kuomba kwa ajili ya jambo hili, na ambayo yamefunuliwa kwangu usiku huu ni haya yafuatayo: Wakati nilipomuomba Allah mtukufu kwa unyenyekevu wote na matukuzo, nami nikamuomba ahukumu katika jambo hili, nikasema: “Hakika sisi si chochote ila ni waja madhaifu na bila ya hukumu yako hatuwezi kuhakikisha kitu chochote.” Hapo Mola wangu akanipa Aya hii ikiwa ni bishara kutoka kwake, nayo inasema: Upande ambao unachagua batili kwa makusudi katika mjadala huu baina ya pande mbili na ukaacha mungu wa haki na ukaabudu mtu dhaifu mafikio yake ni kutupwa katika maangamizo ndani ya miezi kumi na tano. Yaani kila mwezi unakabiliana na siku moja ya siku za mjadala, na kuwa yeye huyo atapata udhalilifu na unyongefu mkubwa sana, kwa sharti, iwapo hatarejea katika haki. Ama ambae yuko katika haki na anaamini Allah wa haki kwake utadhihiri ushindi na kukirimiwa, na utakapotimia ufunuo huu wataona baadhi ya vipofu, na watatembea baadhi ya vilema, na watasikia baadhi ya viziwi, kwa mujibu wa alivyotaka Allah mtukufu.

Basi shukurani zote ni kwa Allah na neema ni zake; kwani lau kuwa funuo hii haikudhihiri kutoka kwa Allah mtukufu siku zetu hizi kumi na tano zingalipotea bure. Na katika ada ya mtu dhalimu ya kuwa yeye haoni hali ya kuwa anatazama, wala hasikilizi hali ya kuwa anasikia, wala hazingatii hali ya kuwa anafahamu, na anaendelea katika ujasiri na uovu wala hajui kuwa Mungu yupo.

Hakika mimi ninajua vizuri, ya kuwa hivi sasa ndio wakati wa hukumu katika maudhui hii.

Nilikua nashangaa kwa nini mjadala huu umesadifu kuhudhuria kwangu mwenyewe, pamoja na kuwa kuna watu wengine wengi wanafanya mijadala ya kawaida?

Kwa kweli uhakika umeshabainika hivi sasa kuwa hayo yamekua ili kuidhihirisha Aya hii.

Basi mimi nanakubali katika makamu hii ya kuwa: lau utathibiti ubatilifu wa funuo hii, yaani lau kuwa upande ulio muongo katika uoni wa Allah haukuanguka katika maangamizo kwa adhabu ya kifo ndani ya miezi 15 kuanzia tarehe ya leo, basi mimi nitakua tayari kufikwa na aina yoyote ya adhabu, ni sawa kama nitadhalilishwa, au uso wangu utapakwa masizi, au nikafungwa kamba ya shingo, au nitauliwa kwa kunyongwa, nitakua tayari kwa chochote.

Ninasema nikiwa ninaapa kwa Allah mtukufu: “Kuwa Allah mtukufu atahakikisha niliyoyasema bila ya shaka yoyote, atahakikisha bila shaka yoyote, atahakikisha bila shaka yoyote. Inawezekana Ardhi na Mbingu zikaondoka lakini haiwezakani kuondoka maneno yake.”

Hivi sasa mimi namuuliza Mheshimiwa Abdullahi Aat`ham: Jee! Utaikubali Aya hii ikitimia ikiwa ni funuo kamilifu, ambayo ni funuo itokayo kwa Allah mtukufu ambayo imedhihiri kwa mujibu wa ulivotaka au laa?

Jee! si itakua hapo ni dalili iliyo ya nguvu ya kuwa Mtume wa Allah S.A.W. ambae umemsifu katika kitabu chako “Andaroonah Baible” kuwa ni Dajali ya kuwa uhakika wake ni mtume mkweli?

Ni lipi ninaloweza kusema zaidi ya hayo ikiwa Allah mtukufu mwenyewe ameshapitisha hukumu katika maudhui hii? Hii sio sehemu ya kufanyia shere bila ya haki.

Ikiwa mimi ni muongo basi nitayarishieni kitazi, na munione kuwa ni mlaaniwa zaidi ya Mashetani na Waovu na Walaaniwa wote…….. [Rf. Alharbu Almuqaddasah uk. 308-310]


Tarehe ya funuo hii ni 5/June/1893 kwa hiyo muhula wa kufa Padri Aat`hma au kutubia na kuwa Muahmadia ni mpaka tarehe 4/Sep/1894.

Tunajua sote kuwa funuo ya kifo kama hii ni funuo hewa kiuhakika; kwa sababu vifo vya watu ni ghaibu hakuna anevijua isipokua Allah mtukufu peke yake, basi kiasili uwezekano wa Padri na Mirza kufa mmoja wao katika kipindi hicho ni sawa, kama ilivokua kuendelea kubakia hai mmoja wai ni sawa pia, lakini sisi tunaweza kusema kuwa sehemu ambayo inawezekana ikahesabiwa kuwa itakua ni dalili ya usahihi wa madai ya Mkadiani kupitia funuo yake hii ni ile isemayo kuwa siku ya kutimia funuo hiyo kuna viziwi watasikia, na vipofu wataona, na vilema watatembea; kwa sababu hilo ni jambo liko nje ya mazoea, na kwa yakini halikutokeza, lakini juu ya yote hayo maandiko ya Maahmadia yanashuhudia kuwa Padri Aat`ham alipitisha miezi 15 bila ya kufariki wala kuingia katika Uahmadia wala kusilimu aslan, bali alibakia akiwa ni Padri Mkiristo hadi kufa kwake.

Anasema Mwana wa Mkadiani anayeitwa Bashirudini Mahmoud ambae ni Khalifa wake wa pili katika Dini ya Kiahmadia:

“Sitasahau tokeo ambalo nililiona wakati wa kufika siku ya mwisho ya muda uliowekwa wa kufa Padri Aat`ham katika funuo ya Masihi Mauudi … Ninakumbuka kuwa Maahmadia walijikusanya katika sehemu ambayo hivi leo lipo duka la Hakiim Muulawi Qutbudiin, nao walianza kumuomba Allah mtukufu kwa kilio na kelele wakisema: “Ewe Mola timiza funuo hii.” Na alikuwepo kati yao Muafghani mmoja jina lake Abdulaziz yeye alikua akijipiga kichwa chake na ukuta kwa nguvu sana huku anasema: “Ewe Mola usilifanye jua la leo kutua (kuchwa) mpaka umuangamize At`ham…” [Tafsiiru Al-Kabiir juzuu 9 ukurasa 594 toleo rasmi la Kiarabu].

Anasema Ust. Hani Tahir katika makala yake chini ya anuani: Funuo ya Abdullahi At`ham siku ya ujinga wa kiahmadia kisha siku za nuru ya uhakika.

Katika siku ya tarehe 5/June/1893 Mirza alitoa funuo kuwa Mtu huyo ya kuwa atakufa ndani ya kipindi cha miezi 15, lakini hakufa.

Hapo kabla nilikua nikisema: Hakika funuo hii inajulisha kujiamini sana kwa Mirza kwa upande wa Allah na nusra yake ya kumnusuru, hasa hasa pale Mirza alipotoa ushindani mbele ya Abdullahi At`ham ya kuwa atapata zawadi iwapo ataapa kiapo ya kuwa hakuiogopa funuo husika.

Baada ya kumaliza tarjama ya vitabu (vya Mirza) yakanibainikia haya yafuatayo:

1. Uhakika ni kuwa funuo hiyo ilikua janja ni kufunika kufeli kwake katika mjadala na kushindwa Mirza kuleta kitu chenye manufaa; kwani yeye mwenyewe amesema: “Lau kuwa funuo hii haikudhihiri kutoka kwa Allah mtukufu kwa hakika siku hizi kumi na tano ningalipotea bure.” [Ilani 115 ya 5/6/1893]

2. Ni jambo la kawaida sana kwa Mirza kutoa funuo, kwani yeye ni funuo nyingi, na kufunika kufeli kwake kwa njia ya funuo kuko tayari wakati wowote, na hapa ni kulikua ni kuogopa muhusika wa funuo. Na hata kama ataendelea kutangaza kuwa hakuogopa, basi Mirza angalishikilia tu kuwa aliogopa, na kuwa Allah amemuambia kuhusu hali ya nafsi yake.

3. Funuo isemayo: “Allah amejua huzuni ya Abdullahi At`ham na fazaa yake” haikuwepo kabla ya kumaliza muda wa miezi 15 kinyume na tulivokua tukifikiria, bali Mirza hakuwahi kudai kuwa aliipata isipokua baada ya kumaliza muda wa miezi 15, kisha ikabainika kuwa Mirza alibadilisha katika tarehe yake kwa kusogeza siku nne za kabla katika daftari la ilhamati zake, alifanya hivo ili azubaishe kuwa aliipata kabla ya kumaliza kipindi cha miezi 15.

4. Kuwa Aat`ham akuiogopa kabisa funuo hiyo ya Mirza, lakini hakuweza kuapa kwa sababu kuapa ni haramu katika Dini yake.

5. Tulikua tukifiria kuwa Mirza alitoa funuo katika ilani nyengine ya kuwa Aat`ham atakufa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, nae akafa baada ya miezi saba, na kwa hiyo funuo imetimia. Lakini uhakika ni kuwa hilo pia ni uongo usio na mashiko yoyote, kwani lililobainika wakati tuliposoma ilani zake (Mirza) ni kuwa ilani yake ilisema: “Iwapo Abdullahi At`ham ataapa basi atakufa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.” wala hakuzungumzia kabisa suala la iwapo hataapa. Na kwa sababu At`ham hakuapa, uhakika ukabainika kuwa hiyo pia ilikua ni funuo iliyofeli, na imekwisha pitisha uhakika wa kufeli kwake.

6. Ikabainika kuwa kila kitu kinakwenda kinyumenyume na yale anayoyasema Mirza, basi kifo cha At`ham haraka haraka baada ya Mirza kunyamaza kimnya hakina budi kuwa kinaonesha jambo muhimu, nalo ni kuwa Allah mtukufu anapitishia kwa Mirza kinyume na anavotamani Mirza. Basi kwa vile Mirza amenyamaza na afe sasa At`ham, na Mirza ajue kuwa ushindi si hadhi yake, bali kushindwa ndiko anakostahiki Mirza, si zaidi ya hapo.

7. Uongo wa Mirza kuhusiana na Abdullahi At`ham haukufungika kwa upande mmoja tu, bali ulienea, mara alikua anadai kuwa At`ham ni mtu mwenye haya na heshima sana, na mara nyengine anadai kwa At`ham anamtukana Mtume S.A.W. Anasema Mirza: “Alikua At`ham anamiliki haya sana na moyo wake ulikua umeathirika kwa ukweli wa kuogopa, wala hakua katika tabia mbaya, bali nasema ya ukweli na haki, kuwa mimi sijawahipo kumuona baina ya Manasara mpaka hivi sasa mtu mwenye tabia nzuri aliye mwingi wa haya mwenye majuto aliye wa sasa anaiogopa haki ndani ya moyo harakaharaka mfano wa Aat`ham.” [Ilani ya 22/3/1897] lakini Mirza huyo huyo baada ya miaka mitano anasema kuhusu A`tham: “Kwa hakika imetangulia kwake kumwita Nabii S.A.W. Dajali, na hilo ndilo lililokua sukumo la kufanya mjadala naye”. [Malfudhaat 4 Mwisho 1902] na huu ni uongo wa kipekee kwani hakumwita Dajali wala hilo alilolidai halikua sukumo la kufanya naye mjadala, bali sukumo la kumuingiza katika mjadala kuhakika lilikua ni wito uliotolewa na Dr. aliyekua mkiristo ndani ya mji na kuusikia mmoja wa wafuasi wa Mirza nae akapendekeza jina la Mirza.

8. Mirza hakuona haya yoyote kumzulia Abdullahi At`ham uongo kwa kuzua kuwa yeye ndiye alitaka apate funuo kutoka kwake. Alisema: “Kwa hakika nilisema kabla ya kuwa mimi sikuleta funuo kuhusu Lyak-hraam na Abdullahi Aat`ham lakini nilieleza funuo hizo baada ya wao wenyewe kushikilia kwao na baada ya kupata kukubali kulikoandikwa hasa na wao wenyewe” [Ilani ya 20/1/1899]. Lakini Mirza huyo huyo kabla ya hapo kwa miaka 6 anasema kuwa Allah amempa funuo kuhusu At`ham ikiwa ni bishara kutoka kwake. [Ilani 115 ya 5/6/1893] na hakueleza kabisa kuwa ni kwa sababu ya matakwa ya yoyote si Aat`ham wala mwengine.

Na namna hivi hali ya Mirza katika kila kisa kati ya visa vyake, ukifuatlia vizuri utakutia kuwa Mirza na Maahmadia baada yake wote wametopea katika uongo kwa namna ya ajabu sana.

Hani Tahir 20/Sep/2017.

 

Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi

WAFUASI: “ILIKUA YA KIROHO.”

MIRZA: “ILIMFELISHA KATIKA KUSUDIO LA DAAWA.”

Waislamu wote tunajua kuwa Mtume wa Allah Masihi Issa mwana wa Mariyam A.S. alihusishwa kwa miujiza ya kufinyanga ndege kwa udongo na kumpuliza na kuwa ndege anaruka kwa idhini ya Allah mtukufu, kuponyesha waliozaliwa vipofu hawaoni na wenye mabalanga na kuwapa watu uhakika wa walivokula na kulimbikiza majumbani mwao, yote hayo tumeyajua na kuyasadiki kupitia Quraani tukufu.

Katika kujadiliana kwetu na Mkadiani mmoja kutoka Tanzania aliyejitambulisha kwa jina la Abasi Ali aliyafanyia shere yale tunayoyaamini kuhusu miujiza aliyohusishwa nayo Mtume wa Allah Masihi Issa A.S. na kusema kuwa hayo hayakua ya kihisia bali ya kiroho, kama vile tulivoambiwa kuhusu makafiri kuwa ni viziwi vipofu mabubu na hawana akili hali ya kuwa wanasikia na wanaona na wanasema na wanafahamu, lakini makusudio yake ni viziwi kiroho na vipofu kiroho mabubu kiroho hawana akili kiroho, basi vile vile tuliyoelezwa kuhusu Miujiza ya Masihi A.S. yote si ya kihisia bali ni ya kiroho.

Kwetu sisi Maahmadia si wageni, tunazijua sarakasi na chenga zao vizuri sana; kwani sifa hiyo ilianza kwa muasisi wa jumuia yao Ghulam Ahmed Mkadiani, tatizo lao ni kupinzana kwao kila mmoja na sarakasi na chenga yake, matokeo yake ni kupinzana na muasisi wao katika aina ya chenga, na matokeo ni kupigana mweleka.

Kwa upande wa Ghulamu Ahmed Mkadiani, jambo hili la miujiza za Masihi Issa A.S. alilipiga sarakasi na chenga za ajabu sana lakini ni tafauti na sarakasi na chenga na Muumini wake aitwae Abasi Ali ambayo kaipata kupitia Jumuia yake, na hili la kupigana mweleka baina yao na Muasisi wao kwao si ajabu sana, hasa tukijua kuwa Muasisi kaeleza wazi wazi kwa herufi zisizokua na shaka kuwa kuzaliwa kwake kulikua katika mwaka 1839 au 1840 na katika mwaka 1857 alikua ni kijana chipukizi wa miaka 16 au 17 hajaanza kuota ndevu wala sharubu kama ilivo katika Rohani Khazaini 13/177, kisha Jumuia ikakusudia kudanganya kuhusu uzawa wake, kwa kusema ulikua katika mwaka 1835, ili kunusuru funuo yake hewa ya miaka 80.

Ama kuhusu sarakasi na chenga zake katika suala la Miujiza ya Masihi A.S. yeye hakukataa matokeo kama tunavyoyaamini bali alivumbua elimu aliyoiita Turbi ambayo wenye umahiri nayo wanaweza kufanya mambo ambayo kidhahiri ni ya ajabu lakini uhakika si ajabu yoyote, bali huwaathiri wahusika wake kiroho na kiakili wakati wanapoitumia, kutokana na hapo yeye haitaki elimu hiyo wala haitumii, kisha akasema kuwa Yeye: “Alimshuhudia mwenye umahiri wa elimu hiyo akiweka mkono wake juu ya ubao, basi mara ubao ule ukawa unatikisika na kutembea kama mnyama, na watu waliukalia na kuupanda juu yake kama farasi nao haukupunguza harakati zake wala mwendo wake.” [Izaalatu Auhaam 269] kwa hiyo kumbe aliyoyafanya Masihi Issa A.S. ni ya uhakika lakini si miujiza kama ilivotueleza Quraani tukufu, hii ndiyo tija ya sarakasi pigachenga ya Mirza kupitia jicho lake mwenyewe bila ya kuwepo mashahidi wa kuwauliza kuhusu tokeo husika na kuhakikisha.

Kisha Mirza aliendelea kuelezea, na kalamu hapa tumuachie mwenyewe sisi yetu ni tarjama tu.

Ghulamu Ahmed Mkadiani: “Kwa hali yoyote ile, Ifahamike kuwa hakika hizi kazi zilizofungamana na kazi ya (Elimu ya) Turbi ambazo Masihi A.S. alikua akizifanya zilikua kwa mujibu wa mapelekeo ya hali katika zama zile kwa mujibu wa hekima kusudiwa.

Lakini ijulikane kuwa kazi hii ya Turbi haipasi kupewa umuhimu mkubwa sana kama wanavozua watu wa kawaida.

Na lau si kuchukia kwangu na kukorogeka kwangu kinafsi kwa sababu yake (kazi hiyo) basi kungalikua na matarajio makubwa kwa fadhila za Allah na taufiki yake kupatikana hayo kwangu pia ili nisije nikawa katika daraja iliyo ya chini kuliko Masihi Ibnu Mariyam A.S. katika kuonesha maajabu hayo.

Lakini mimi ninapenda zaidi ile njia ya kiroho ambayo aliipita Nabii wetu S.A.W.

Ijulikane kuwa Masihi A.S. hakua akifanya mambo hayo ya hisia isipokua kwa idhini ya Allah na amri yake kwa kuangalia fikra za kihisia duni ambazo zilikua zimetawala katika tabia za Mayahudi, na lau kuwa si hivo kwa hakika Masihi A.S. hakua akiipenda kazi hiyo kabisa.

Na ili Ifahamike vizuri, ni kuwa kuna jambo baya sana katika kazi hizo za kihisia, nalo ni kuwa yule anayefanya kazi hizo huwa anatoa nguvu zake za kiakili na kiubongo ili aondoshe maradhi ya kimwili kwa kuendelea mara nyingi, kwa hakika yeye hudhoofika sana kiroho, bali taathira zake za kiroho za kuathiri katika roho na kuondosha maradhi ya kiroho huvunjika kidogo kidogo, na mara chache sana ndio hufanikiwa katika kuziongoa nafsi na kuzitoharisha, nalo ndilo lengo kuu la uhakika, na kwa sababu hii ndio Masihi A.S. akawa anaponyesha maradhi ya miili kupitia kazi hii (ya elimu ya Turbi) basi kiwango chake katika yale yanayohusiana na kuhakikisha uongofu na tauhidi na kunyooka vizuri kidini katika nyoyo za waja kwa sura kamilifu kilikua kimefifia sana hadi kufikia daraja iliyo karibu zaidi na kufeli kabisa..” [Rf. Izaalatu Al-Auhaami uk. 270]


Gallery is offline
Click to restore your gallery or contact us at support@cincopa.com

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here