SWALI :
Jamani Eti kama wewe mwanaume umesafiri ukamuacha mkewako na mdogo wako wakiume ukakaa sana huko uliko kwenda kwa bahati mbaya mke wako akashkika akashindwa kujizuwiya na wewe madamu anakupenda akaamuwa asiende mbali akaona bora afanye mapenzi na ndugu yako kwa bahati mbaya amapata uja uzito na wewe uliporudi akaona asikufiche akwambiye ukweli.
Je ? Kama wewe ndio kaka utachukuwa uwamuzi gani ?
Utamuacha mke au utamfukuza nduguyako au utaficha siri ule maisha yako? Nahitaji jibu jamani lakueleweka!
JAWABU
➡Zinaa ni moja ya madhambi makubwa ambayo yana hukmu zake kutekelezewa duniani kabla ya akhera.
➡ Kutokana na hatari kubwa ya jambo hili:
Uisilamu umeweka mipaka maalumu ili kumkinga muisilamu asifikie kuwa mzinifu.
1. Kukatazwa mchanganyiko kati ya wanawake na wanaume, ambao kisheria wanaweza kuoana, japokuwa kujuzu huko ni kwa siku za baadae.
➡ watu wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mahram na ajnabiy katika Wanawake na wanaume.
➡ MAHRAM ni “Kila ambae anaharamika kuoana nae mpaka qiyaama “
Yaani haitotokea hali yoyote ikafaa kuoana nae.
Mfano :
* Baba hawezi kumuoa binti yake maisha.
* Kaka hawezi kumuoa dada yake maisha.
* Mtoto wa kiume hawezi kumuoa mama yake daima.
Na mfano wa hayo.
➡ Kuna wengine wanadhani kuwa :
Mke wa kaka yake anafaa kukaa nae faragha wao wawili tu, au kusafiri nae n.k
Au wanaume wengine wanadhani kuwa dada wa mkewe anafaa kuchanganyika nae katika faragha, na kugusana nae mikono n.k.
➡ Naam :
Uharamu wa kuoana kati ya hao upo, lakini ni wa muda maalumu ambao unaweza kumalizika kwa hali moja kati ya mbili :
1. Mume akimuacha mkewe talaka ambayo hawezi kumrejea tena, au talaka ya kuweza kumrejea, lakini akawa hakumrejea hata muda wa eda ukamaliza, hapo inajuzu kumposa dada wa aliekuwa mkewe. N.k
➡ Kwa hiyo shemeji kubakia na shemeji yake ni hatari kama kifo. Haifai.
2. Hali ya kutokea kifo cha mkewe.
Inajuzu kwa mume huyo kumuoa dada wa aliekuwa mumewe wakati wowote baada ya kifo hicho, kwa sababu mume hana eda ya kusubiri.
➡ Na mke wa mtu akizini na mwanaume zinaa ya hakika ya kuingiliana kwa tupu zao, kama yanavyokuwa maingiliano kati ya mke na mume; Mke huyo kuhusu ndoa yake kuna hali hizi :
1. ikiwa mumewe atamsadikisha katika hilo, Itakuwa ndoa yao imeharibika. ..NA wala haifai kwa mwanaume msafi wa tabia kuishi na mwanamke mchafu mzinifu.
➡ Na ikiwa madai yake yana aina ya kuwa hayana ukweli, basi haitokubalika mpaka akiri mara nne katika nyakati tofauti kuwa kweli amezini.
Akikiri mara hizo ni ikathibitishwa hilo, ndoa inavunjwa, na mwanamke huyo hatopata haki yoyote kwa mumewe.
Na ni kauli ya maulamaa wengi wa kiibaadhi allaah awahifadhi maulamaa wote wa kiisilaamu.
➡Tahadhari kubwa sana napenda kunabahisha
1. Kuna hatari kubwa katika kuchanganyika watoto wa kiume na wa kike hasa katika zao za kulala.
2.Pia kuchanganyika wafanyakazi wa ndani wa kiume na wa kike bila kuwa na mipaka maalumu ya kisheria.
3. Hatari ya ushemeji unaovuka mipaka ya dini ya kiisilaamu.
4. Hatari ya watoto wa kiume waliofikia umri wa kutambua mambo mbalimbali, kulala pamoja katika kitanda kimoja na kujifunika shuka moja.
Zimekuja hadithi mbalimbali za mtume s.a.w kutahadharisha mengi katika haya, na hata kwa wanawake kwa wanawake pia kuna mipaka yao maalumu.
Allaahu aalamu.
ELIMU KWA ELIMU HADI MAARIFA.
LIMEJIBIWA NA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY.
