Home Sh.Shaabani Al Bataashi Eti kuna Hadith iliyosahihi inayosema kua mwanamke akimruhusu mumewe kwa hiari yake...

Eti kuna Hadith iliyosahihi inayosema kua mwanamke akimruhusu mumewe kwa hiari yake kuoa mke wa pili ni kwamba mwanamke huyo akifa ataingia peponi

296
0

 SWALI :

Assalam aleykum warahma tullahi wabarakatuh!! Sheikh kuna swali: Eti kuna Hadith iliyosahihi inayosema kua mwanamke akimruhusu mumewe kwa hiari yake kuoa mke wa pili ni kwamba  mwanamke hy akifa ataingia peponi moja kwa moja kwa kua kumruhusu Mume kuoa mke wa pili ni km kapigana jihad je ni Kweli sheikh? Naomba majibu ukijaaliwa in shaa Allah!

JAWABU :

➡ Hadithi hiyo ina uzushi mtupu na wala Hakuna kitabu chochote nilichokuta habari kama hii.

➡ Na hata maelezo yaliyomo ndani ya hiyo inayosemwa kuwa ni hadithi yanaonyesha uongo uliomo ndani yake.

➡ Na katika alama za kuwa Hadithi  ni ya kutungwa tu :

1.  Kutoa malipo makubwa sana kwa sababu ya amali ndogo sana.

➡ mume akiwa ana uwezo wa kutekeleza uadilifu kati wake zake,  inajuzu kwake kuoa hata bila ruhusa ya mkewe.

➡ Na Hakuna malipo maalumu kwa mwanamke mwenye kumruhusu mumewe kuoa kwa hiyari yake.

Ila atapata malipo ya kawaida tu kwa kuwa amefanya jambo la kheri,  na hakuwa na chuki na mwenzake,  na amesubiri katika jambo ambalo nafsi huwa ina uzito kulisubiria.

Allaahu aalamu.

LIMEJIBIWA NA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY.LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here