SWALI :
Juzi nikiwa Dar es salaam na mmoja katika dada zetu kuwa :
Nini humu ya mwanamke anaevua nguo zake zote mbele ya wanawake wenzake?
JAWABU :
➡ Uisilamu ni dini ya usafi na kuhifadhi maumbile ya mwana adamu.
➡ Ni haramu kisheria kwa yoyote kufunua na kukashifu mwili wake mbele ya mwingine, ila ikiwa ni sehemu za mwili ambazo ni kawaida kuonekana, kama viganja vya mikono, na uso na sehemu za mwili mwingine ambazo si kati ya kitovu na magoti.
➡ mwanamke haifai kudhihirisha mapaja yake mbele ya wanawake wenzake.
➡ Na mwenye kufanya hivyo analaaniwa na allaah s.w yeye na kila mwenye kutazama kwa makusudi.
➡ Mtume s.a.w alimuusia swahabi wake Ally bin abii twaalib r.a kwa kumwambia :
“Ewe Ally;
“Usifunue paja lako kwa watu, na wala usitazame paja la aliekuwa hai wala aliekufa”
➡ Ni ajabu katika zama hizi kuona na kusikia wanawake Leo wanafanya haya yafuatayo :
1. Wanatoka majiani vichwa wazi na nywele zikionekana kwa watu.
2. Wengine wanavaa mashungi mafupi kiasi ambacho vifua vyao huonekana hata maumbile ya maziwa ya vifua vyao.
3. Na wengine wanakata nguo zao mpasuo sehemu ya kifua, na wanatembea hivyo mbele za wanaume wala hawajali.
4. Kuna wenye Kuvaa visketi vivupi na vya kubana na vya mpira, tena wanavaa viguo hivyo mbele za watu.
5. Na kuna mashule mengi yenye hostel za wanawake, hazina maadili ya kidini kabisa wala malezi.
➡ wanafunzi wanawake wakubwa wanakoga pamoja na kuvua nguo mbele za wenzao na kukoga pamoja.
Na hili ni kosa kubwa sana.
➡ wanavua nguo zote na Kuvaa nyingine mbele za wenzao hali ya kuwa wako miili mitupu haina kitu kinachiloifunika.
6. Wanachukuana picha wakiwa wamevaa nguo za ndani tu, na kutumiana katika simu kupitia mitandao ya kijamii, na wengine kuweka profile picha hizi.
7. Kupewa uhuru wa kutumia simu kwa uhuru bila nidhamu yoyote wala mipaka maalumu.
➡ je nini kinatarajiwa katika mazingira haya kwa wanawake hawa
➡ lini watapata tabia ya kuwa na haya
➡ lini watajifunza kuwa wema na wenye kuuhifadhi utu wao
➡ Ndugu zangu tukumbuke kuwa :
Watoto ni dhamana, na wazazi ni wadhamini.
Allaahu aalamu.
LIMEJIBIWA NA
SH. SHAABAN ALBATTAASHY.