Home Jawabu Kwa Mawahabi 3. FATAWA ZA MASHEIKH WETU – 3

3. FATAWA ZA MASHEIKH WETU – 3

284
0

Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad na Masahaba wake na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya malipo.

Tukiwa tumo katika kuwajibu Masalafi kuhusu tuhuma zao batili dhidi ya Ibadhi ambazo wanazisambaza huku na huko.

Tunaingia katika suala la KARAMA ZA MASHAIKH

Amesema Sheikh wa Kisalafi katika maandiko yake akitoa tarjuma ya maneno ya Sheikh Al-haarithii (r.a):

ولما توفي هذا الشيخ رضي الله عنه- وضع نعشه منحرفا عن القبلة قبل أن يصلى عليه فاستدار إلى القبلة كرامة له.”

((Kisha akasema Al-Haarithiy: Alipofariki huyu Sheikh –radhiya llaahu an`hu- kabla ya kusaliwa, jeneza lake waliliweka kinyume na kibala (waliuelekeza uso wake upande usiokuwa wa kibala) akajigeuza mwenyewe kuelekea kibala kwa sababu ya karama”!!!)) Mwisho wa kunukuu uk. Ole wake kila mzushi 125-126

JAWABU:

Namuambia, kwanza tulitaraji utoe tarajuma nzuri, na sio tarajuma ya kupotosha, kwani tarjuma yako inatuonesha kuwa Sheiikh Raiiis Jaaid Al-haruusi -Allah awe radhi naye- alijigeuza yeye mwenyewe; kwani uso wake ulielekezwa upande usiokuwa wa Kibla, na lililo sahihi ni kuwa Jeneza ndilo lililogeuka likajiweka sawa upande wa kibla bila ya Sheikh kutikisika.

Tunasema kuwambia hawa Masalafi: Sasa kuna ajabu gani katika hilo? Sheikh Al-Imam amekirimiwa kwa kuwekwa sawa jeneza lake, ni nani waliohusika na uwekaji sawa huo? Sisi hatujui, Allah ndiye anayejua, lakini hilo ni jambo linalowezekana, na kwa sababu sio jambo la kuzoeleka ndio likasemwa kuwa ni Karama.

Kisha tunawambia hawa Masalafi kuwa sisi Ibadhi hatukatai karama za Masheikh Wachamungu kwani hayo ni katika yanayowezekana kiakili, lakini hatuzifanyi Karama za Masheikh kuwa ni Hoja katika Dini, nasi tunaitakidi kuwa karama kubwa zaidi ni Mja kufa akiwa mchamungu, hakuna karama inayoshinda hiyo katika mafundisho ya Kiibadhi, na neno la Maulamaa wetu ni maarufu katika hilo:

الكرامة هي الموت على الاستقامة

Halafu tunawambia hawa Masalafi kuwa kama hamujui kuwa Maimamu wenu wamedaiwa pia kuwa walikuwa na Makarama basi angalieni haya:

Ibn Qayyim Al-jauziyyah munayemlakib kwa (Shamsudiiin) na ambaye ni mwanafunzi wa Sheikh Al-Islamu wenu Ibn Taimiyah Al-harraani, anaelezea haya:

لَقَدْ شَاهَدْتُ مِنْ فِرَاسَةِ شَيْخِ الْإِسْلَامِ ابْنِ تَيْمِيَّةَرَحِمَهُ اللَّهُ – أُمُورًا عَجِيبَةً. وَمَا لَمْ أُشَاهِدْهُ مِنْهَا أَعْظَمُ وَأَعْظَمُ. وَوَقَائِعُ فِرَاسَتِهِ تَسْتَدْعِي سِفْرًا ضَخْمًا. أَخْبَرَ أَصْحَابَهُ بِدُخُولِ التَّتَارِ الشَّامَ سَنَةَ تِسْعٍ وَتِسْعِينَ وَسِتِّمِائَةٍ، وَأَنَّ جُيُوشَ الْمُسْلِمِينَ تُكْسَرُ، وَأَنَّ دِمَشْقَ لَا يَكُونُ بِهَا قَتْلٌ عَامٌّ وَلَا سَبْيٌ عَامٌّ، وَأَنَّ كَلَبَ الْجَيْشِ وَحِدَّتَهُ فِي الْأَمْوَالِ. وَهَذَا قَبْلَ أَنْ يَهُمَّ التَّتَارُ بِالْحَرَكَةِ. ثُمَّ أَخْبَرَ النَّاسَ وَالْأُمَرَاءَ سَنَةَ اثْنَتَيْنِ وَسَبْعِمِائَةٍ لَمَّا تَحَرَّكَ التَّتَارُ وَقَصَدُوا الشَّامَ: أَنَّ الدَّائِرَةَ وَالْهَزِيمَةَ عَلَيْهِمْ. وَأَنَّ الظَّفَرَ وَالنَّصْرَ لِلْمُسْلِمِينَ. وَأَقْسَمَ عَلَى ذَلِكَ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ يَمِينًا. فَيُقَالُ لَهُ: قُلْ إِنْ شَاءَ اللَّهُ. فَيَقُولُ: إِنْ شَاءَ اللَّهُ تَحْقِيقًا لَا تَعْلِيقًا. وَسَمِعْتُهُ يَقُولُ ذَلِكَ. قَالَ: فَلَمَّا أَكْثَرُوا عَلَيَّ. قُلْتُ: لَا تُكْثِرُوا. كَتَبَ اللَّهُ تَعَالَى فِي اللَّوْحِ الْمَحْفُوظِ. أَنَّهُمْ مَهْزُومُونَ فِي هَذِهِ الْكَرَّةِ. وَأَنَّ النَّصْرَ لِجُيُوشِ الْإِسْلَامِ.

(Kwa hakika nimeshuhudia katika uoni wa ndani wa Sheikh wa Uislamu Ibnu Taymiyah –amrehemu Allah- mambo ya ajabu, na ambayo sikuyashuhudia katika hayo ni makubwa zaidi na makuu zaidi, na matokeo ya uoni wake wa ndani yanataka kitabu kikubwa:

  1. Aliwambia watu wake kuingia kwa Matatari katika Shaam katika mwaka wa mia sita na tisiini na tisa (696 Hj), na kuwa majeshi ya Waislamu yatavunjwa, na kuwa Demeshqi hakutakuwa na kupigana mwaka mzima wala sabyu (utekaji wa watoto na wanawake kwa sababu ya vita) muda wa mwaka, na kuwa makali ya jeshi na ujasiri wake utakuwa katika mali, na haya ni kabla ya kuazimia Matatari kufanya harakati.
  2. Kisha akawambia watu na viongozi katika mwaka wa mia saba na mbili (702) wakati Matatari walipoikusudia Shaam: Kwa hakika njama na kushindwa ni dhidi yao, na kuwa kufanikiwa na ushindi ni kwa Waislamu, na akaapa juu ya hilo zaidi ya viapo sabiini, basi iliambiwa: Sema Akitaka Allah. Basi akawa anasema: Akitaka Allah kwa kuhakikisha na si kwa kuegemeza. Na nimeyasikia hayo. Amesema: Basi walipozidisha kwangu nikasema: Musizidishe ameshaandika Allah mtukufu katika Lauhi Al-Mahfuudhi ya kuwa wao ni wenye kushindwa katika duru hii, na kuwa ushindi ni kwa majeshi ya Uislamu. Alisema: Basi nikawaonjesha baadhi ya viongozi na majeshi utamu wa ushindi kabla ya kutoka kwao kwa kukutana na adui.) [Ibnu Qayyim – Madariju Saalikina 2/458]

Sasa sijui ni lipi kubwa zaidi kati ya haya mawili?!

  1. Kueleza Sheikh wa Uislamu wa Kisalafi mambo ya Ghaibu tena kwa viapo zaidi ya sabiini
  2. Kukirimiwa Mwanachuoni mwanahaki wa Kiibadhi kwa kusawazishwa jeneza lake muelekeo wa Kibla.

Mbona Sheikh wa Kisalafi (Muwahabi) anakicheka Kabanzi kilichoko kwenye jicho la mwenzake anasahau kuwa katika Jicho lake kuna Jiti la Mkarambati!!!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here