Home MAJIBU YA TUHUMA JUU YA IBADHI 13.WASIA WA IMAM JABIR BIN ZAID (R.A)

13.WASIA WA IMAM JABIR BIN ZAID (R.A)

141
0

“Nakuusia kumcha Allah Mola Mkuu ambaye anayajua kwako usiyoyajua katika nafsi yako, na ambaye anayaona yaliyofichwa na dhamiri yako na kufanyiwa khiyana na macho yako na unayoyadhihirisha na unayoyaficha katika nafsi yako, na yeye yuko karibu yako kuliko mshipa wa shingo yako, basi muangalie Mola huyu ambaye yuko na wewe kwa daraja hiyo na uwe mwenye kumuogopa zaidi na mwenye kumcha yeye zaidi kuliko chengine chochote, na ujue kuwa wewe utakapomtii yeye utakua pamoja na (maridhio) yake katika nyumba yake pamoja na Manabii na Wasadikishaji na Mashahidi na ubora ulioje kuwa pamoja na hao, na ikiwa wewe utamuasi yeye basi atakuingiza motoni ambao muwako wake ni kwa watu na mawe”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here